Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1586 | 1587 | (Page 1588) | 1589 | 1590 | .... | 1897 | newer

  0 0

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.

  Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa EBOLA kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.

  “Napenda kuwatoa hofu watanzania kwamba hakuna ugonjwa wa EBOLA na wala hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo, hivyo tuendelee na shughuli za kujenga Taifa ila tunatakiwa tuchukue tahadhari za kujikinga juu ya ugonjwa huu” alisema Dkt. Ndugulile. 

  Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa EBOLA usiingie nchini Serikali imeweka vifaa vya kupima joto la mwili (themo scaner) pia wapo wataalamu wa Afya ambao wanauliza hali ya wageni wanaoingia katika mipaka yote inayoizunguka nchi yetu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia. 

  Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa, Serikali haijafunga mipaka ya nchi kwa sababu ya kujikinga na EBOLA."Tanzania hatujafunga mipaka na hatuwezi kufunga biashara za mipakani ila tumeimarisha ufuatiliaji wa watu wanaoingia nchini hususani maeneo ya viwanja vya ndege na mipaka mingine yote." 

  Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameitaka mikoa yote iliyo mipakani kudhibiti watu wote wanaoingia nchini kwa njia za panya ili kuepusha uingizaji wa ugonjwa huo kwa wananchi huku akiwataka wafanyabiashara wa mipakani kutoa ushirikiano ili kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini. 

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani ambaye pia ni Afisa wa kushughulikia magonjwa ya kuambukiza Dkt. Grace Saguti amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kupata elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo. 

  “Elimu inahitajika ya kutosha kwa wananchi wote hasa katika kufichua wagonjwa wa Ebola kama watagundulika hasa wanaotoka nje ya nchi ili kupata msaada kutoka kwa watoa huduma za afya walio yao juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa Wizara na wawakilishi wa WHO wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa Habari kutoika vyombo mbali mbali wakifuatilia kwa makini tamko kuhusu gonjwa wa Ebola alilotoa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0


  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  WANAWAKE wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.

  “Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.

  Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

  Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.
  Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.

  Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.
  “Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.

  Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Shirika la Amref Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
  akizunguza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kulia kwake ni Mgeni rasmi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA wameshiriki kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha ubunifu kwa vijana na kuonesha jinsi kijana anavyoweza kusoma kwa kujitengemea kwa kutumia ubunifu wa  aplikesheni ya VSOMO inayotoa  elimu kwa mtandao.

  Kwa miaka miwili sasa, VETA kupitia applikesheni ya VSOMO imekuwa ikitoa elimu kupitia mtandao kwa wanafunzi ambao wanataka kupata elimu ya ufundi stadi kwa udhamini wa Airtel Tanzania.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamani hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kampuni ya Airtel iliamua kuwa mmoja wa wadau wa teknolojia hii ya kutoa elimu ya VSOMO ikiwa ni moja wa mkakati wake wa kurudisha sehemu ya faida yake katika kusaidia Jamii. Kwa kuweza kutambua umuhimu wa Jamii inayotuzunguka, tuna miradi ya kusaidia vijana kujikwamua yenye lengo ya kuwapa vijana ujuzi ili wajiajiri au wapate ajira kwenye sekta mbali mbali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga uchumi wa viwanda.

  Airtel Tanzania inayo furaha kuona kuwa matumizi ya smartphone yakiwa ni darasa au ikiwa ni moja ya njia ya kutumika kupata elimu ya ufundi. Hii haiukuwa rahisi kufanya peke yetu ndio sababu tuliamua kushirikiana na VETA kama taasisi ya serikali yenye mamlaka ya kutumia elimu ya ufundi hapa nchini huku DTBi wakiwa ndio waliombuni applikesheni ya VSOMO, alisema Singano.

  Airtel na washirika wake VETA na DTBi kwa sasa wana utaratibu mpya wa malipo kwa awamu ili kuwezesha wanafunzi wanaotaka kupata elimu ya ufundi stadi kufanya bila kupata changamoto za kulipa karo, aliongeza Singano.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.
   Godfrey Magila kutoka taasisi ya DTBi akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi
   Mratibu wa VSOMO kutoka Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA Charles Mapuli  akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.


  0 0

  Na Agnes Francis Blogu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30 katika kuelekea mwisho wa Ligi  kuu  ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.

  Ndimbo amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora kwa msimu huu.

  Amewataja wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce  Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na Adam Salamba(Lipuli).

  Wengine ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya (Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud Ambokile(Mbeya City).

  Pia Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga), Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
  Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).

  "Mchakato wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua

  Pia amesema licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika uboreshaji

  "Tuzo iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala ya kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi,"amesema Ndimbo

  Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi wa Tatu,Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.

  Ndimbo amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

  "Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.

  "Wachezaji  ambao  walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba). 

  "Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa  Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.

  Ambapo wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  KAMPENI ya ujenzi wa Choo cha Mtoto wa kike katika Halmashauri ya Manispaa jijini Dar es Salaam inakwenda vizuri kutokana na wadau walioahidi kuchangia kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo hicho kuendelea kutimiza ahadi zao zikiwamo za fedha ambapo Mratibu wa kampeni hiyo Tabu Shaibu amekabidhiwa Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo.

  Akizungumza leo baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Shaibu ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini amesema ahadi zilizotolewa na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema zimeendelea kutekelezwa kwani wameendelea kupokea michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kwa nyakati tofauti.Amesema kampeni hiyo imetokana na uamuzi wa Watumishi Wanawake wa Manispaa hiyo kuanzisha ujenzi wa choo hicho katika hivyo vitakavyojengwa kwenye shule za msingi na Shaibu amefafanua choo cha mfano kinajengwa Shule ya Msingi Chanika.Ujenzi umefikia hatua ya linta na kilichobaki ni kupaua.

  "Tunashukuru kwa namna wadau mbalimbali wanavyoendelea kutimiza ahadi zao kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike.Tuendelee kusisitiza wale ambao bado hawajatimiza ahadi aidha ya fedha au vifaa vya ujenzi basi kuitekeleza."Lengo letu ni kutimiza lengo la kampeni hii ambayo tunakwenda kumkoamboa mtoto wa kike wa Manispaa ya Ilala ambaye leo yupo shuleni na siku zijazo atakuwa mtumishi wa manispaa yetu,"amesema Shaibu.Kuhusu mchango wa Sh.milioni moja uliotolewa na Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa manispaa hiyo, Shaibu amesema anamshukuru kwa kutekeleza ahadi yake na hakika ameonesha dhamira njema ya kufanikisha ujenzi huo na kusisitiza amekuwa akipokea michango kwa nyakati tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali.

  Kwa upande wa Mwaikambo amesema kikubwa ni kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike katika manispaa ya Ilala huku akisisitiza walioahidi watekeleze na kwamba ataendelea kushirikiana na watumishi wanawake na wadau wa maendeleo ili kampeni ifanikiwe."Niliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa choo hicho ambacho ni maalumu kwa mtoto wa kike.Hivyo nitaendelea kushirikiana na wadau wote kwa lengo la kufanikisha malengo yetu na wale ambao wameahidi niwaombe waendelee kutimiza ahadi zao,"amefafanua.

  Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mjema alisema ipo haja ya kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike na akifafanua vyoo kufafanua vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa na ndani kutakuwa na mahitaji yote muhimu. 
   Mratibu wa Kampeni ya Ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati anapokea fedha Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo hicho.Kushoto ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala.
   Mratibu wa Kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(kushoto) akipokea fedha Sh.milioni moja leo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia).Anayeshuhudia ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale a.k.a Babu Tale,  kurudishwa Mahabusu ya polisi mpaka Msajili wa Mahakama hiyo atakaporudi kutoka Dodoma.

  Amri hiyo imetolewa leo na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Lucy Massam baada ya Babu Tale na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kushindwa kufikia makubaliano licha ya msajili kuwapa muda wa dakika 10 pande zote wajadiliane namna ya kulimaliza suala hilo.

  Babu Tale ambaye pia ni Meneja wa mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond Platnumz', amefikishwa mahakamani hapo leo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kusikiliza kesi inayomkabili.

  Babu Tale, amekamatwa kutokana na amri iliyotolewa Februari 16 mwaka huu na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Wilbard Mashauri iliyoamuru mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale wakamatwe.

  Amri hiyo pia, ilielekeza watuhimiwa hao wakikamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo Mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine.Hata hivyo, mtuhumiwa Babu Tale baada ya kufikishwa mahakamani hapo jana kesi yake ilishindikana kusikilizwa kwa kuwa Msajili Mashauri yuko Dodoma kikazi.

  Kutokana na kushindwa kufikia muafaka baada ya dakika hizo kumi kuisha, Msajili Massam ameamuru babu Tale arudishwe mahabusu ya polisi mpaka Msajili Mashauri atakaporudi kwa ajili ya maelekezo mengine.

  Hata hivyo kipindi chote cha majadiliano Babu Tale alikuwa katika mahabusu ya mahakama hiyo wakati ndugu zake wanajadiliana na mdai wake kabla ya kuieleza mahakama muafaka watakaofikia na kisha mahakama kutoa maelekezo.

  Awali Mahakama hiyo iliwaamuru watuhumiwa hao kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh.milioni 250 baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

  Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde alikuwa akidai kuwa aliingia mkataba na kampuni ya kina Babu Tale (Tiptop Connection) ili wamrekodi mahubiri yake kisha wayauze na kugawana mapato.Hata hivyo baada ya kurekodi masomo saba, walimkatia mawasiliano na alipowatafuta na kukutana nao wakamweleza kuwa wameamua kuachana na mpango huo.

  Sheikh Mbonde alidai kuwa akiwa kwenye mahubiri Dodoma ndipo akakutana na mikanda ya video katika mfumo wa DVD yenye mahubiri yake huku kukiwa na namba za simu za viongozi hao wa Tiptop.

  Sheikh Mbonde alidai baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa DVD hizo zilikuwa zikiuzwa katika mikoa mbalimbali, ndipo akawafungulia kesi ya madai ya fidia kutokana ukiukwaji wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni ofisini kwake Jijini Dodoma leo ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye tafiti za binadamu wa kale katika eneo la Olduvai, kuboresha utoaji wa elimu hususan ya mapishi ya vyakula vya Kiitaliano katika Chuo cha Taifa cha Utalii na Utangazaji wa vivutio vya utalii nchini. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma leo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiagana na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma leo. (Picha na Hamza Temba-WMU)

  0 0


  0 0


     
  Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. 

  Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu.

  Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. 
  Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba. 
  Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma .
  Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 
  Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma 
  Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. 
  Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. 
  Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara 
  Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma

  HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA (MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019
  ORODHA YA VIFUPISHO

  AF

  Adaptation Fund

  AfDB

  African Development Bank

  AfCFTA

  African Continental Free Trade Area

  AGOA

  African Growth and Opportunity Act

  AICC

  Arusha International Conference Centre

  AMISOM

  African Union Mission to Somalia

  APRM

  African Peer Review Mechanism

  BBC

  British Broadcasting Corporation

  CGTN

  China Global Television Network

  COMESA

  Common Market for Eastern and


  Southern Africa

  COP

  Conference of Parties

  DW

  Deutsche Welle

  EAC

  East African Community

  EPA

  Economic Partnership Agreement

  FAO

  Food and Agriculture Organization


  FIB

  Force Intervention Brigade


  FOCAC

  Forum on China-Africa Cooperation


  ii
  GCF

  Green Climate Fund

  GEF

  Global Environment Facility

  GIZ

  The Deutsche Gesellschaft für

  Internationale Zusammenarbeit GmbH


  GPEDC

  Global Partnership for Effective


  Development Cooperation

  IAEA

  International Atomic Energy Agency

  IGAD

  Intergovernmental Authority on


  Development

  ILO

  International Labour Organization

  IMF

  International Monetary Fund

  IOM

  International Organization for Migration

  IORA

  Indian Ocean Rim Association

  JNICC

  Julius Nyerere International Convention


  Centre

  KCB

  Kenya Commercial Bank

  KOICA

  Korea International Cooperation Agency

  LDCF

  Least Developed Countries Fund


  iii  MINUSCA                   United Nations Multidimensional Integrated


  Stabilisation Mission in the Central African Republic


  MK-ICC                       Mt. Kilimanjaro International Convention


  Centre


  MONUSCO               United Nations Organisation Stabilisation


  Mission in the Democratic Republic of the Congo


  NPT                                 Non – Proliferation Treaty


  PSPF                             Public Sector Pension Fund


  RFI                                  Radio France International


  RMB                               Renminbi


  SADC                            Southern African Development


  Community


  SDGs                             Sustainable Development


  Goals


  TAZARA                     Tanzania-Zambia Railway Authority


  TBC                                Tanzania Broadcasting Corporation


  TEHAMA                   Teknolojia ya Habari na Mawasiliano


  TIC                                  Tanzania Investment Centre


  TMEA                           Trademark East Africa


  UKIMWI                      Upungufu wa Kinga Mwilini


  iv  UNAMID  United Nations African Union Mission in Darfur
  UNDP  United Nations Development Progamme

  UNDAP
  United Nations Development Assistance Plan
  UNEP  United Nations Environment Progamme


  UNESCO  United Nations Educational Scientific and Cultural Organization
  UNFPA  United Nations Population Fund
  UN-HABITAT  United Nations Human Settlement Programme
  UNHCR  United Nations High Commission for Refugees
  UNICEF  United Nations Children’s Emergency Fund
  UN-ICTR  United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda
  UNIDO  United Nations Industrial Development Organization
  UNIFIL  United Nations Interim Force in Lebanon
  UNISFA  United Nations Interim Security Force for Abyei

  v  UNMISS                       United Nations Mission in the Republic


  of South Sudan


  UTT                                 Unit Trust of Tanzania


  VoA                                 Voice of America


  WHO                              World Health Organization  WTO                               World Trade Organization


  WWF                              World Wildlife Fund  vi  UTANGULIZI


  1.   Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.


  2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu.


  3.   Mheshimiwa Spika, naungana na wenzanguwalionitangulia kuwashukuru na kuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwa hakika hotuba zao sio tu zimezungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira katika mustakabali wa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa, kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu ya Wizara yangu.
  1  4.   Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hiikutoa shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya uongozi wa Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi Rehani (Mb). Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimili muhimu katika kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.


  5.   Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombanitumie nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine Mkenda, Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu; mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu wa Idara na Vitengo; watumishi wa Wizara; na taasisi zilizo chini ya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaa Bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2018/19.
  6.   Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa,naungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa


  Jimbo la Songea Mjini kwa kifo cha Mhe. Leonidas Gama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kilichotokea mwezi Novemba 2017. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.
  2  7.   Mheshimiwa Spika, nawapongeza wabunge wotewaliochaguliwa na kuteuliwa kisha kuapishwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha. Kuchaguliwa na kuteuliwa kwao ni kielelezo cha kuaminiwa na wananchi ili kuwawakilisha ipasavyo katika Bunge hili.


  8.   Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhilakama sitamshukuru kwa dhati mke wangu mpendwa Elizabeth Mahiga pamoja na watoto kwa kunivumilia, kuniunga mkono na kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili niweze kutekeleza majukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais katika kujenga na kutetea maslahi ya taifa letu.


  HALI YA MAHUSIANO NA NCHI NYINGINE


  9.   Mheshimiwa Spika, mahusiano ya Tanzania na nchi namashirika mbalimbali ya kikanda na kimataifa yameendelea kushamiri kwa manufaa ya pande zote zinazohusika. Tanzania tuna mahusiano mazuri na majirani zetu wote. Kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Tanzania ina makubaliano ya kuondoa vikwazo vya biashara na nchi zote jirani, yaani Msumbiji, Malawi, Zambia, Kongo DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya. Kwa kuzingatia misingi ya Sera yetu ya Mambo ya Nje, tumeendelea kuchukua kila hatua kudumisha ujirani mwema na nchi jirani. Tunazo ofisi za ubalozi katika nchi zote ambazo ni majirani zetu kwenye nchi kavu na pia katika visiwa vya Komoros. Tumeendelea na jitihada za kujenga ujirani mwema kwa jamii zinazoishi mipakani na jamii za nchi jirani.
  3  Katika kuimarisha mahusiano hayo, viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali wameendelea kufanya ziara hapa nchini. Mathalan, kwa mwaka wa fedha 2017/18, Tanzania ilipokea Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Uganda, Misri, Burundi, Msumbiji na Rwanda. Aidha, Mawaziri na Naibu Mawaziri kutoka nchi za Ujerumani, Israel, Uingereza, Norway, Oman, Burundi, Misri, Poland, Shelisheli, Maldves, China na Brazil walitembelea Tanzania katika kipindi hicho. Pia, Tanzania ilipokea wajumbe maalum wa wakuu wa nchi na serikali kutoka nchi za Uganda, Rwanda,Misri, Poland, Burundi, Morocco, Mjumbe Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Palestina. Aidha, Ethiopia ipo katika hatua za mwisho za kufungua ubalozi hapa nchini na Belarus nao wametuma timu ya uangalizi mwezi Desemba 2017 na kuahidi kufungua ubalozi wao mwezi Juni 2018.


  10.           Mheshimiwa Spika, nchi yetu ilitembelewa piana Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yakiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO); Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Chakula na Kilimo (FAO); Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS); na Jumuiya ya Madola. Aidha, viongozi wengine na wataalam kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Shirika la Maendeleo la Japan (JICA); Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA) na Aga Khan walitembelea Tanzania.

  4  11.           Mheshimiwa Spika, Viongozi wetu Wakuu wa Kitaifayaani Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar nao walifanya ziara za kiserikali na kushiriki mikutano katika nchi mbalimbali.  12.           Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kuwa namahusiano mazuri ya kidiplomasia na nchi mbalimbali duniani. Hadi sasa jumla ya nchi 62 zina mabalozi wakaazi hapa nchini. Kati ya hizo, nchi za China, Oman, Msumbiji na India zinaendesha pia ofisi ndogo za ubalozi (konseli kuu) Zanzibar. Kadhalika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na kuwa na ubalozi Dar es Salaam, ina Konseli Kuu mjini Kigoma. Aidha, nchi 39 zinawakilishwa nchini na mabalozi wasio wakaazi ambao ofisi zao zipo nje ya Tanzania.Vilevile, wapo makonseli wa heshima 24 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na yapo mashirika 23 ya kimataifa yenye hadhi ya kidiplomasia yanayofanya kazi nchini.


  13.           Mheshimiwa Spika, Tanzania ina jumla ya balozi 41zinazotuwakilisha nje ya nchi. Pamoja na balozi hizo nchi yetu ina ofisi 3 za Konseli Kuu katika miji ya Mombasa,


  Jeddah na Dubai. Kadhalika Tanzania ina jumla ya makonseli wa heshima 35 wanaotuwakilisha katika miji mbalimbali duniani.

  5  14.           Mheshimiwa Spika,katika hotuba yangu ya bajetimwaka jana nilieleza kuhusu Serikali kufungua balozi mpya sita katika nchi za Algeria, Israel, Uturuki, Sudan, Qatar na Korea Kusini. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba tayari tumepeleka mabalozi kwenye vituo hivyo.
  MISINGI YA NCHI KATIKA MAHUSIANO YA KIMATAIFA


  15.           Mheshimiwa Spika, taifa lolote duniani huongozwana misingi ambayo lengo lake kuu ni kudumisha amani, ulinzi, usalama na mshikamano wa wananchi wake na taifa kwa ujumla. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu mara baada ya uhuru. Misingi hiyo ni pamoja na kulinda uhuru wetu; kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa; kulinda mipaka ya nchi yetu; kulinda haki; kuimarisha ujirani mwema; na kuunga mkono Sera ya Kutofungamana na Upande wowote kama dira na msimamo wetu katika mahusiano na nchi nyingine katika Jumuiya ya Kimataifa.


  16.           Mheshimiwa Spika,misingi hiyo ndiyo inayotufanyaleo tujivunie Taifa lenye amani, ulinzi imara na usalama duniani; taifa ambalo limekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, haki na uhuru; kutafuta amani na kutatua migogoro ya nchi mbalimbali kwa gharama kubwa ya rasilimali watu na fedha; Taifa linalojitolea wanajeshi wake kwenye ulinzi wa amani, na kuwa tegemeo la mataifa katika misheni za kulinda amani; Taifa ambalo limekuwa kimbilio
  6  kubwa kwa wananchi wa mataifa mengine yenye migogoro na ambao wanalazimika kukimbilia nchi nyingine kuokoa maisha yao na kupewa hifadhi nchini mwetu.  17.           Mheshimiwa Spika, Tanzania inaheshimu misingiya mahusiano na mataifa mengine duniani ambayo tuna mahusiano ya kidiplomasia na yale ambayo bado hatuna mahusiano ya kidiplomasia. Ni kwa misingi hiyo, mataifa mengine nayo yanawajibika kuheshimu misingi ya Tanzania kama ilivyoainishwa hapo juu. Nataka kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Tanzania italinda misingi hiyo daima. Aidha, napenda ieleweke wazi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na mataifa yote duniani na kushiriki kikamilifu katika mijadala na majukwaa ya kimataifa katika kutetea uhuru, haki za binadamu na usawa kwa kuzingatia mahusiano yaliyopo kwa kila nchi kwa ajili ya maslahi mapana ya uchumi, jamii na maendeleo ya nchi yetu.  Ni kwa mantiki hiyo, Tanzania itaendelea kutekeleza Sera ya Kutofungamana na Upande wowote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote. Tanzania haitarajii nchi nyingine yoyote kuiamulia mambo yake, kushinikizwa, kutishwa au kuingiliwa na nchi yoyote katika mambo yetu ya ndani. Marafiki wetu ni lazima waheshimu msimamo wetu kwamba hatutachaguliwa nani awe rafiki yetu na nani awe adui wetu. Maslahi ya nchi yetu na imani yetu ya haki na usawa wa binadamu ndio dira ya msimamo wetu kimataifa.
  7  MSIMAMO WA TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KIMATAIFA


  18.           Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikulieleza Bunge lako Tukufu kuwa msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Palestina na Israel haujabadilika. Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya kuwa na mataifa mawili yaani Palestina huru na Israel salama. Tunaendelea kuunga mkono kufanyika kwa majadiliano yatakayosaidia kumalizika kwa mgogoro huo uliodumu muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Ni kweli kwamba mahusiano yetu na Israel yanaongezeka na tutahakikisha yanashamiri kwa manufaa na maendeleo ya Taifa letu. Tanzania inatambua kuwa Israel ina haki ya kuishi kama Taifa huru na salama na hivyo ndivyo iwe kwa Wapalestina ambao ni majirani zao. Tutashiriki katika mijadala yote kimataifa katika kutafuta suluhu ya mashariki ya kati.  19.           Mheshimiwa Spika, Tanzania pia inaendeleakuunga mkono juhudi za usuluhishi wa mgogoro wa Sahara Magharibi, katika mchakato wa maelewano unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa na kuungwa mkono na Umoja wa Afrika. Tuna imani kuwa kurejea kwa Morocco katika Umoja wa Afrika kutatoa fursa kwa Umoja huo kutoa mchango wake katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao kwa muda mrefu umekuwa ukishughulikiwa na Umoja wa Mataifa. POLISARIO ni chama cha ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali na uanachama wa
  8  Umoja wa Afrika tangu mwaka 1982. Suala hili limeanza kuleta utata wa kisheria katika Umoja wa Afrika na katika duru za kimataifa. Morocco imeanzisha Ubalozi hapa nchini. Mfalme Mohamed VI alitembelea hapa nchini mwishoni mwa mwaka 2016 na kutiliana saini mikataba 21 ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Tanzania iliunga mkono Morocco kurudi katika Umoja wa Afrika na kuingia katika Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika. Tanzania itaendelea kushiriki katika vikao mbalimbali vya kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Tunatarajia uhusiano wetu na nchi ya Morocco utaendelea kukua hasa katika sekta mbalimbali.


  UTEKELEZAJI WA SERA YA MAMBO YA NJE Kulinda Amani


  20.           Mheshimiwa Spika, hali ya usalama dunianiimeendelea kuimarika pamoja na kwamba changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasa inayoendelea katika nchi mbalimbali duniani, matukio ya kigaidi na kuongezeka makundi yenye itikadi kali pamoja na athari za kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Tishio jingine kimataifa ni biashara haramu kama vile za madawa ya kulevya, usafirishaji wa binadamu na utakatishaji wa fedha ambayo haina mipaka. Katika kukabiliana na changamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkono jitihada za kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarisha amani na usalama duniani.
  9  21.           Mheshimiwa Spika, katika kuunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa zinazolenga kuimarisha amani na usalama duniani, nchi yetu imeendelea kutoa mchango wa askari wake kwenye misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Mchango huu ni muhimu na umeiletea nchi yetu sifa kubwa kimataifa kwa askari kuwa na nidhamu na kujitoa katika kuifanya dunia kuwa salama. Ushiriki wa askari wetu katika misheni hizo umewaongezea weledi na ujuzi katika masuala ya medani za kijeshi na usalama wa kimataifa.  22.           Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyaliyopatikana, tumekuwa tukipata changamoto za kupoteza baadhi ya askari wetu katika misheni hizo. Kwa mfano, shambulio la tarehe 8 Desemba 2017 lililosababisha askari wetu 15 kupoteza maisha na wengine 43 kujeruhiwa nchini DRC, linabaki kuwa moja ya shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea kwenye misheni za kulinda amani duniani kwa takribani miaka 25 iliyopita.


  23.           Mheshimiwa Spika, tunaushukuru Umoja waMataifa kwa kuunda timu ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo iliyojumuisha maafisa wawili wa ngazi ya juu kutoka


  Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Timu hiyo imeshakamilisha uchunguzi wake kuhusu chanzo cha tukio hilo na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kuzuia matukio kama hayo yasitokee tena. Serikali inaendelea kuwasiliana na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utekelezaji wa taarifa hiyo ambayo itasaidia pia Umoja wa Mataifa kuboresha utendaji 

  wake na ulinzi wa askari kwenye misheni za kulinda amani.  10
  24.           Mheshimiwa Spika, naomba ifahamike kwamba,pamoja na shambulio hilo kubwa na la kusikitisha, kamwe hatutarudi nyuma wala kukatishwa tamaa. Tunaamini kwenye misingi yetu ya kusimamia haki na kulinda amani kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu na kuweka mazingira mazuri ya ustawi wa jamii. Tanzania itaendelea kusimamia misingi hiyo na kuimarisha ushiriki wetu katika misheni za kulinda amani duniani.  MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18


  25.           Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumuya Wizara kwa mwaka 2017/18, Wizara yangu ilitengewa kiasi cha Shilingi 157,980,248,704. Kati ya fedha hizo, Shilingi 149,980,248,704 ilikuwa kwa ajili ya Matumiziya Kawaida na Shilingi 8,000,000,000 ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. Katika fedha zilizotengwa kwa Matumizi ya Kawaida, Shilingi 140,496,296,704ilikuwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi 9,483,952,000 ilikuwa kwa ajili ya mishahara.  26.           Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2017/18, Wizara ilitarajia kukusanya maduhuli kiasi cha Shilingi 25,773,882,820. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili


  2018, Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi22,198,966,840, sawa na asilimia 86 ya makisio ya
  11  makusanyo yote ya maduhuli. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018, balozi zetu nje zimerejesha katika Mfuko Mkuu wa Serikali kiasi cha Shilingi 13,025,539,374. Wizara yangu itaendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa kiasi chote cha maduhuli kitakachokusanywa kwa mwaka wa fedha 2017/18 kinarejeshwa katika Mfuko Mkuu kama ilivyoelekezwa na Serikali.  27.           Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 30 Aprili


  2018, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 114,185,986,274, sawa na asilimia 72 ya bajeti iliyopitishwa na Bunge. Kati ya fedha hizo, Shilingi 104,538,835,394ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya Matumizi Mengineyo; Shilingi 6,226,955,225 ilikuwa kwa ajili ya mishahara; na Shilingi 3,420,195,655 ilikuwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.


  Miradi ya Maendeleo ya Wizara  28.           Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2017/18, Wizara ilipangiwa bajeti ya maendeleo kiasi cha Shilingi 8,000,000,000. Hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi Mei 2018, Wizara ilipokea kutoka Hazina mgao wa fedha za bajeti ya maendeleo kiasi cha Shilingi3,420,195,655, sawa na asilimia 42.7 ya fedha za bajetiya maendeleo iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi1,815,527,215 zimepangwa kutumika kufanya ukarabatiwa jengo la ofisi na makazi ya watumishi kwenye ubalozi wa Tanzania Kampala; Shilingi 315,425,000 ni kwa ajili ya ukarabati wa makazi ya balozi Kinshasa; Shilingi
  12  593,300,000 kutumika kukarabati nyumba za ubalozi wa Tanzania Lilongwe; Shilingi 195,943,440 kukarabati makazi ya balozi wa Tanzania Brussels; na shilingi500,000,000 kwa ajili ya kukarabati miundombinu yaChuo cha Diplomasia.  29.           Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kufuatiliaWizara ya Fedha na Mipango upatikanaji wa fedha za maendeleo kiasi cha Shilingi 4,579,804,345 sawa na asilimia 57.3 ambazo hazijatolewa ili kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2017/18.  30.           Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuzingatiasheria, kanuni, taratibu na miongozo ya fedha za umma katika kudhibiti mapato na matumizi ya Serikali. Kwa kudhihirisha hilo, Wizara pamoja na balozi zake 39 zimepata hati safi isipokuwa balozi mbili zimepata hati zenye shaka katika ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/17. Nachukua fursa hii kuwashukuru watendaji wa Wizara na kuwahimiza waendelee kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za umma na ununuzi wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.


  31.           Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa taarifa yamapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18, naomba sasa nitumie fursa hii kueleza kwa kifupi baadhi ya mafanikio ya Wizara katika kipindi hicho.


  13  DIPLOMASIA YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA


  32.           Mheshimiwa Spika, katika malengo ya Seraya Mambo ya Nje kuna malengo ambayo ni ya kudumu yanayoiwezesha nchi kuwa katika nafasi ya jumuiya ya mataifa kama Taifa huru lenye umoja, usalama na lenye hadhi na siha nzuri. Hii hasa ni diplomasia ya siasa. Pia kuna malengo ambayo yanaendana na wakati huo wa uongozi na vipaumbele vya Serikali na Taifa kwa ujumla. Katika miaka ya sitini hadi themanini malengo ya ziada katika Sera ya Tanzania yalikuwa ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwa ukoloni na ubaguzi wa rangi. Baada ya kukamilisha hayo Tanzania iliona umuhimu wa kuwa na Sera ya Mambo ya Nje yenye msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukuma maendeleo ya Taifa letu.  33.           Mheshimiwa Spika, Diplomasia ya uchumi nimsisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo, mbinu na maarifa yanayoelekeza taifa kupata na kuvuna rasilimali na utaalam kutoka jumuiya ya mataifa ili kuleta na kuchochea maendeleo ya taifa husika. Mwaka 2001 Tanzania ilipitisha sera inayosisitiza diplomasia ya uchumi ili kuendeleza maendeleo hasa katika sekta ya uchumi. Katika Awamu hii ya tano, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alitangaza mapema kuwa Tanzania iwe ni nchi ya viwanda ili kusukuma zaidi maendeleo ya uchumi na ajira kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka

  2025. Azma hii inamaanisha kuwa diplomasia ya uchumi
  14  lazima iongeze mkakati wa Diplomasia wa Viwanda ili kutekeleza maono na mawazo ya Mheshimiwa Rais kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vilivyojikita kwenye kilimo. Diplomasia ya uchumi wa viwanda lazima itoe vipaumbele katika uwekezaji, miundombinu ikiwa ni pamoja na nishati, biashara na masoko ya bidhaa kutoka viwandani. Sambamba na mkakati huo, dhana ya diplomasia ya uchumi lazima iendelee kulenga sekta nyingine kama kilimo, utalii na madini ambayo kwa namna moja au nyingine zinashabihiana na viwanda.


  Viwanda, Biashara na Uwekezaji


  34.           Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza diplomasiaya uchumi, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine ndani ya Serikali na kutoka sekta binafsi inaratibu upatikanaji wa masoko, mitaji, na teknolojia kwa ajili ya kukuza biashara na uwekezaji nchini. Miongoni mwa juhudi zilizofanywa na Wizara yangu ni kushawishi wawekezaji kupitia ziara za viongozi, balozi zetu nje ya nchi, na makongamano ya biashara na uwekezaji yaliyofanyika ndani na nje ya nchi. Kupitia juhudi hizo, tumeweza kufanikisha kuleta ujumbe wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Hispania, Misri, China, India, Falme za Kiarabu, Oman na Israel. Baadhi ya wawekezaji hao tayari wameingia ubia na kampuni za Tanzania na wengine wameanza hatua mbalimbali za uwekezaji nchini.


  15  Moja ya hatua hizo ni uamuzi uliofanywa na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani mwezi Aprili 2018 wa kufungua ofisi maalum ya biashara ya nchi hiyo inayoitwa AHK kwa lengo la kuratibu kwa ukaribu zaidi uwekezaji na biashara zinazofanywa na zitakazofanywa na Ujerumani hapa nchini. Aidha, Ufaransa imefungua ofisi ya biashara kupitia kampuni ya BASF kwa lengo la kuratibu shughuli za kibiashara zitakazokuwa zikifanywa na kampuni hiyo na wabia wake hususan katika masuala ya uzalishaji wa kemikali za viwandani.  35.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu pia iliratibuushiriki wa Tanzania kwenye makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji yaliyoandaliwa nje ya nchi. Makongamano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika nchini Kenya, Hispania, Uturuki, Uholanzi, Indonesia, Korea Kusini, China, Vietnam, Ujerumani na Umoja wa Falme za Kiarabu. Aidha, viongozi wetu wanapopata fursa ya kufanya ziara mbalimbali nje ya nchi wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuzungumza na kuwashawishi wawekezaji kuwekeza nchini, binafsi nimekuwa nikifanya hivyo na viongozi wenzangu pia wamekuwa wakifanya hivyo. Kwa mfano, mwezi Aprili 2018 Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alitembelea Falme za Kiarabu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipofanya ziara ya kikazi nchini China walitumia fursa hiyo kushawishi wawekezaji katika sekta za uvuvi, viwanda, kilimo na utalii na hatimaye kuingia nao makubaliano ya kuanza hatua za uwekezaji kwenye
  16  sekta hizo.  36.           Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018, Wizaraikishirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania; na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kupitia ubalozi wetu nchini Kenya iliandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania, yaliyofanyika Nairobi. Haya yalikuwa ni maonesho ya kipekee kuwahi kufanywa na nchi yetu. Jumla ya kampuni 27 zinazozalisha bidhaa za viwandani kutoka Tanzania zilishiriki ili kutangaza bidhaa zao na kuvutia utalii. Maonesho hayo yalitoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutafuta masoko ya bidhaa zetu nchini Kenya.


  37.           Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa maonesho hayo yamefungua soko zaidi kwa bidhaa za Tanzania nchini Kenya na kuimarisha mahusiano kati ya nchi zetu mbili na wafanyabiashara. Natoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya masoko ya bidhaa za Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi zetu nyingine pia zimekuwa zikiendesha makongamano na shughuli nyingine mbalimbali za kukuza utalii, kuvutia wawekezaji na kutafuta masoko.


  38.           Mheshimiwa Spika, juhudi hizi zinazofanywa naWizara yangu pamoja na wadau wengine ndani na nje ya Serikali zinatoa nafasi kwa wafanyabiashara na wawekezaji kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara, masoko, teknolojia na upatikanaji wa mitaji. Hivyo, ninatoa rai

  17  kwa wadau wote wanaosimamia masuala ya biashara na uwekezaji kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza nchini. Nitumie fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wetu kutumia fursa hizo kikamilifu.  39.           Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha biasharakati ya Tanzania na Misri, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau husika iliratibu majadiliano ya kuondoleana ushuru wa forodha na Misri. Majadiliano hayo yamekamilika mwezi Machi 2018 kwa pande zote kukubaliana kuwa, Misri iondoe ushuru kwa kiwango cha asilimia 100, na Tanzania iondoe kwa kiwango cha asilimia 96.89. Kiwango kilichosalia kwa Tanzania kitaondolewa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.  40.           Mheshimiwa Spika, mwezi Febuari, 2018 nilifanyaziara ya kikazi nchini Korea Kusini ambapo nilifungua kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi hiyo. Kufuatia kongamano hilo viongozi wa kampuni ya Hyundai walifika nchini kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kwa lengo kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vipuli vya magari. Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji itaendelea kufuatilia mazungumzo hayo.Halikadhalika, nilipotembelea China mwishoni mwa mwaka jana nilikutana na wawekezaji katika viwanda vya magari ambao wameahidi kuja kuona uwezekano wa kuwekeza hapa nchini.

  18  Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Umwagiliaji


  41.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibuupatikanaji wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 55 kutoka Serikali ya Poland ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maghala na vihenge vya kuhifadhia nafaka katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa, Songwe, Dodoma, Shinyanga, Manyara, na Katavi. Kukamilika kwa mradi huo kutapunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno (post-harvest loss). Wizara yangu pia imeratibu upatikanaji wa ufadhili wa mradi wa kituo kikubwa cha ujenzi wa kuzalisha samaki cha Zanzibar unaodhaminiwa kwa ushirika kati ya Korea Kusini kupitia Shirika lake la maendeleo la KOICA pamoja na Shirika la Chakula Duniani (FAO) wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3.2.


  42.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikianana wadau wengine imefanikisha kupatikana ufadhili wa miradi ya umwagiliaji ya Muhongo-Kagera na bonde la Luiche-Kigoma kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait. Baada ya kukamilika kwa tathmini ya miradi hiyo mwezi Machi 2018, rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 15.3 ilisainiwa. Aidha, ushirikiano wa Tanzania na China kupitia jukwaa la FOCAC umeendelea kuchangia sekta ya maji ambapo katika kipindi hiki, Zanzibar imefadhiliwa mradi wa kujenga kituo kipya cha kutibu maji katika eneo la Donge Mbiji, wilaya ya Kaskazini Unguja wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 5.5.
  19  Ujenzi na Miundombinu


  43.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakujenga mahusiano mazuri na nchi marafiki na mashirika ya kimataifa ambao ni washirika wetu wa maendeleo. Uhusiano huo mzuri umewezesha Serikali kupata ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Miongoni mwa ufadhili huo ni ule uliotoka Umoja wa Ulaya, Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la maendeleo la USAID, Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la maendeleo la DFID, Serikali ya Japan kupitia shirika lake la maendeleo la JICA, Serikali ya Korea Kusini kupitia shirika lake la maendeleo la KOICA, Serikali ya Ujerumani kupitia GIZ, Serikali ya Denmark kupitia DANIDA, Serikali ya Canada kupitia CIDA, Serikali ya Ufaransa kupitia shirika lake la AFD, Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Abudhabi, Serikali ya Saudi Arabia kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Saudia, pamoja na Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa maendeleo wa Kuwait. Serikali ya Oman pia imekubali kusaidia kufadhili uboreshaji wa baadhi ya miundombinu katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jiji la Dodoma.  44.           Mheshimiwa Spika, halikadhalika, Chinaimezikaribisha nchi za Afrika kujiunga na mpango wake wa One Belt One Road Initiative ambao unatoa manufaa mapana katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati, reli, barabara, bandari na viwanja vya ndege. Kutokana na hatua hiyo, nilipofanya ziara yangu nchini China, niliwasilisha
  20  maombi ya Tanzania kujiunga na mpango huo. Napenda kulifahamisha Bunge lako kuwa, mwezi Aprili 2018 Serikali ya China ilikubali ombi hilo na taratibu za kujiunga na mpango huo zinaendelea.


  Afya na Ustawi wa Jamii


  45.           Mheshimiwa Spika, sekta ya afya ni miongoni mwasekta zinazonufaika na ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka nchi wahisani pamoja na washirika wetu wa maendeleo. Serikali ya Marekani mwezi Mei 2018 iliahidi kutoa Dola za Marekani milioni 512 kufadhili Mpango wa Kupambana na Virusi vya Ukimwi nchini chini ya program yake ijulikanayo kama President’s Emergency Plan forAIDS Relief (PEPFAR). Serikali ya Kuwait pia imezinduampango maalum wa kusaidia sekta ya afya hapa nchini wenye thamani ya Dola za Marekani 500,000. Mpango huo ujulikanao kama Half-Million Dollar Program umewezesha upatikanaji wa vifaatiba kwa watu wenye mahitaji maalum katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mifupa ya MOI, pamoja na Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma. Aidha, Kuwait imetoa Dola za Marekani milioni 13.6 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Zanzibar; na Serikali ya China pia imesaidia ukarabati wa Hospitali ya Abdulla Mzee, Pemba kama moja ya miradi yake ya afya hapa nchini. Serikali ya Israel itaongeza misaada yake ya wataalam, mafunzo na vifaa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete.
  21  46.           Mheshimiwa Spika, Tanzania pia imenufaika naMfuko wa Afya duniani ujulikanao kama Global Fund unaotoa ufadhili wa programu mbalimbali za kukabiliana na maradhi ya Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi. Tangu mfuko huo uanzishwe hapa nchini mwaka 2013, tayari Tanzania imenufaika na Dola za Marekani takriban bilioni 2 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazonufaika zaidi na ufadhili wa mfuko huo barani Afrika. Aidha, mwezi Aprili 2018 Serikali ilisaini makubaliano na mfuko huo ya kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni 700 kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya afya katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Wadau wengine wanaosaidia sekta ya afya ni mashirika ya maendeleo ya kimataifa pamoja na nchi marafiki kama vile Uingereza, Denmark, Canada,


  Ireland, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu, Cuba, Misri, Israel, Ujerumani, na Brazil.


  Nishati na Madini


  47.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kutambuaumuhimu wa sekta hii katika maendeleo ya uchumi wa nchi imeendelea kuitafutia washirika kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa katika miradi yake mbalimbali. Miongoni mwa wafadhili wakubwa ni Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia. Aidha, kupitia ziara iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway hapa nchini mwezi Juni 2017, Serikali ya nchi hiyo imezindua awamu ya pili ya program itakayodumu hadi mwaka 2020, kwa ajili ya kuendeleza sekta ya mafuta nchini. Kupitia programu hiyo, Norway itatoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 5.9


  22  kwa ajili ya kuendeleza sekta ya mafuta hapa nchini, na kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni 10.5 kwa ajili ya kuendeleza mfumo wa ukusanyaji kodi. Nchi nyingine zinazofadhili miradi kwenye sekta hii kwa kupitia Wizara yangu ni pamoja na Ujerumani, Sweden, Finland na India.


  Elimu na Mafunzo ya Ufundi


  48.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakuratibu upatikanaji wa fursa za masomo na mafunzo ya ufundi kutoka nchi marafiki. Ufadhili huo ni katika mafunzo ya muda mfupi, shahada ya kwanza, uzamili, uzamivu, uboreshaji mafunzo ya ualimu, uboreshaji mitaala na miundombinu ya kufundishia katika vyuo vyetu vya ufundi na teknolojia; vitabu; pamoja na ujenzi wa maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nachukua fursa hii kuzishukuru nchi zote zinazofadhili miradi katika sekta ya elimu na mafunzo ikiwa ni pamoja na China, Italia, Hungary, Poland, Uholanzi, Australia, India, Malta, Misri, Korea, Malaysia, Indonesia, Vietnam, Japan, New Zealand, Algeria, Uingereza, Ujerumani, Uswisi, Brunei, Oman, Cuba, Israel, Palestina na Saudi Arabia. Natoa wito kwa Watanzania watumie fursa hizi ipasavyo.


  Utalii


  49.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Balozizetu nje imeendelea kushirikiana na wadau wengine wa Serikali kutangaza vivutio vya utalii na kuratibu ujio wa watalii nchini. Nafurahi kutambua ripoti iliyotolewa mwezi
  23  Mei 2018 na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na ripoti za balozi zetu zikiainisha kwamba idadi ya watalii nchini sio tu imeongezeka lakini pia pato litokanalo na sekta hiyo limeongezeka. Aidha, ripoti hizo zimebainisha kwamba tofauti na ilivyozoeleka huko nyuma kwa watalii wengi walikuwa wakitoka nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania, hivi sasa kuna ongezeko kubwa pia la watalii kutoka nchi za China, Australia, Uholanzi, Uswisi, India na Israel. Ongezeko hilo la idadi ya watalii ni matokeo ya kasi ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini inayofanywa na mamlaka za ndani pamoja na balozi zetu nje ya nchi. Wizara yangu kupitia balozi zetu itaendeleza juhudi hizi kwa kasi zaidi hasa katika Balozi zetu mpya za Korea Kusini, Uturuki, Qatar na Israel.


  50.           Mheshimiwa Spika, katika kutangaza vivutio vyautalii vya Tanzania katika nchi zenye watalii wengi, ubalozi wa Tanzania Beijing umeendelea kutumia nafasi yake ya kimkakati kwa kutangaza utalii wetu kupitia mitandao ya kijamii ya China kama QQ na WeChat kwa kuweka matangazo ya vivutio kwa lugha za kichina. Aidha, ubalozi kwa kushirikiana na mamlaka za utalii nchini ziliandaa ziara za waigizaji mashuhuri kutoka China ambapo waliandaa makala za kutangaza utalii wa Kisiwapanza -Pemba, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mbuga ya Selou na Ziwa Eyasi. Makala hizo zilizoandaliwa zimelenga kutangazwa katika runinga zinazoangaliwa na watu wengi zaidi nchini China. Soko la watalii kutoka China ni kubwa kuliko yote kama tukijitangaza vizuri
  24  51.           Mheshimiwa Spika, kufuatia ziara ya meli ya Sultanwa Oman mwezi Oktoba 2017, Serikali ya Oman imeahidi kukarabati na kuhifadhi Jumba la Maajabu (Beit el Ajab) Zanzibar. Aidha, mwezi Aprili 2018 Tanzania na Oman zilisaini makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya kumbukumbu na nyaraka ili kukuza utalii unaotokana na historia kati ya Oman na Zanzibar.


  Msamaha wa madeni ya nje


  52.           Mheshimiwa Spika, moja ya hatua inayofanywana Wizara yangu kwa kushirikiana na wizara nyingine ni kushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza au kuweka masharti nafuu ya kuyalipa. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa nilipofanya ziara nchini Iran mwezi Oktoba 2017, Serikali ya nchi hiyo iliridhia na kutangaza kusamehe riba ya deni lililokopwa mwaka 1984 ambayo kwa sasa imefikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 150.


  Aidha, mwezi Septemba 2017, Serikali ya Brazil pia ilitoa msamaha wa thamani ya Dola za Marekani milioni 203.6 ambayo ni asilimia 86 ya deni lote tunalodaiwa na nchi hiyo. Misamaha hiyo ni wazi itaipa nafuu nchi yetu katika kulipa madeni. Naomba kutumia nafasi hii kuzishukuru Serikali za Iran na Brazil kwa misamaha hiyo.  53.           Mheshimiwa Spika, pamoja na wajibu wa Serikalikulipa madeni yake nje, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine ndani ya Serikali itaendelea na juhudi za kuomba kusamehewa au kupata nafuu ya aina yoyote


  katika kulipa madeni ya Serikali. 25  MIKUTANO YA TUME ZA PAMOJA ZA KUDUMU ZA USHIRIKIANO


  54.           Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha,Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliratibu na kushiriki katika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Misri uliofanyika Cairo, mwezi Januari 2018. Mimi binafsi niliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambapo nchi zetu mbili zilikubaliana kushirikiana katika sekta za viwanda, biashara na uwekezaji; maji; kilimo, mifugo na uvuvi; ujenzi, uchukuzi na mawasiliano; afya, nishati, maliasili na utalii; elimu, mambo ya ndani ya nchi na habari. Majadiliano ya utekelezaji wa maazimio mbalimbali yameshaanza na tayari uongozi wa Shirika la ndege la Misri umeshatembelea nchini na kukutana na wataalam wa Idara na Taasisi za Serikali.  USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA JUMUIYA ZA KIKANDA NA KIMATAIFA


  Jumuiya za Kikanda Jumuiya ya Afrika Mashariki


  Uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Forodha  55.           Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibukamati ya kitaifa ya kufuatilia uondoaji wa vikwazo vya kibiashara visivyo vya forodha pamoja na mikutano
  26  ya kikanda kwa ajili ya kujadili vikwazo mbalimbali vinavyojitokeza. Kwa kipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Machi 2018, jumla ya vikwazo sita vilivyodumu kwa muda mrefu vimeondolewa na hivyo kufikia jumla ya vikwazo 122 vilivyoondolewa tangu mwaka 2009. Majadiliano ya kuviondoa vikwazo vingine 33 bado yanaendelea. Miongoni mwa vikwazo vilivyoondolewa vinavyoihusu Tanzania ni kupunguzwa kwa vizuizi barabarani katika njia kuu ya kati na kaskazini; kuwianisha muda wa kufanya kazi baina ya mamlaka za mapato za Tanzania na Kenya kwenye ukaguzi wa mizigo katika bandari kavu mjini Nairobi; kuondoa kodi ya ongezeko la thamani katika huduma za bandari kwa mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi; tozo ya Dola za Marekani 152 kwa mabasi yanayotoka Rwanda na zuio la kuuza bidhaa za chakula kwenda Uganda, pamoja na kurekebisha sheria na kuainisha ubora wa bidhaa mbalimbali tunazouziana.  Mapitio ya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha  56.           Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana nawadau wengine imeendelea kuratibu na kusimamia mapitio ya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha. Kwa sasa nchi za Jumuiya zimeendelea kufanya tafiti katika ngazi ya nchi na kanda kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi ya namna ya kupanga viwango vya ushuru wa forodha katika Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha wa Jumuiya. Majumuisho ya awali ya matokeo ya tafiti kutoka kila nchi mwanachama wa Jumuiya yanapendekeza mabadiliko ya viwango vya
  27  ushuru wa forodha yazingatie ukuzaji wa viwanda kwa nchi wanachama; kupunguza gharama za uzalishaji; kuongeza biashara miongoni mwa nchi wanachama; na kuwalinda walaji.  Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki  57.           Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18, Wizara iliratibu majadiliano ya mapitio ya Jedwali la Biashara ya Huduma katika Itifaki ya Soko la Pamoja. Lengo la kufanya mapitio hayo ni kuondoa changamoto zilizokuwa zikikwaza utekelezaji wa Itifaki hiyo katika eneo la huduma. Tayari nchi zote wanachama zimewasilisha maboresho ya jedwali la huduma katika Itifaki ya Soko la Pamoja ambapo changamoto zilizoainishwa zimepatiwa ufumbuzi.  58.           Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutoaji wa elimu kwa umma mijini na vijijini ili kuwawezesha wananchi na hasa vijana kushiriki katika kuchangamkia fursa zilizoko kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wizara kwa kushirikiana na asasi za kiraia pamoja na vyombo vya habari kupitia makongamano mbalimbali iliendesha programu maalum ya kuhamasisha vijana wa Kitanzania kuzitambua na kuzitumia ipasavyo fursa zitokanazo na Mtangamano wa Afrika Mashariki. Programu hiyo ilipewa jina la Kampeni ya Msafara wa Vijana ya Biashara ya Kuvuka Mpaka. Kampeni hiyo ilifanyika katika

  28  mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Manyara na Arusha. Wizara pia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ilitoa elimu kwa umma kwa vijana wa vyuo vikuu juu ya kuchangamkia fursa katika mtangamano.  Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha ya Afrika Mashariki  59.           Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2017/18 Wizara yangu imeendelea kuratibu na kushiriki katika uandaaji wa sera, sheria, kanuni na taratibu za kuendeleza sekta ya fedha katika eneo la usimamizi wa bima, huduma ndogo za kifedha (microfinance), pensheni na benki. Aidha, Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2018/19 itaendelea kuratibu na kushiriki majadiliano ya maeneo tajwa hapo juu hadi yatakapokamilika.  60.           Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa, Bunge la Afrika Mashariki lililokaa Dodoma mwezi Aprili 2018, lilipokea na kujadili miswada miwili inayohusiana na utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Miswada hiyo ni ya kuanzisha Taasisi ya Fedha na Taasisi ya Takwimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Muswada wa Kuanzisha Taasisi ya Fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipitishwa na Bunge hilo na hatua inayofuata ni kuidhinishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama.


  29  Ushirikiano Baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanda Nyingine  61.           Mheshimiwa Spika, Viongozi Wakuu wa Nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wao wa 18 uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2017 pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuwa Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda na mwenyekiti wa Jumuiya, akutane na Rais wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Jean-Claude Juncker ili kujadili changamoto za Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi (EPA) baina ya Jumuiya hizo. Kufuatia maamuzi hayo, Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika ziara hiyo iliyofanyika Brussels, Ubelgiji mwezi Septemba 2017. Mwenyekiti aliwasilisha rasmi hoja za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu changamoto za EPA na mwezi Desemba 2017, Rais wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Jean-Claude Juncker aliwasilisha majibu ya hoja hizo.


  62.           Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 19 waViongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Kampala mwezi Februari 2018 Rais wa Uganda na Mwenyekiti wa Jumuiya aliwasilisha majibu ya Umoja wa Ulaya kwa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya. Viongozi Wakuu hao hawakuridhishwa na majibu yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya hivyo, walimpa mamlaka Mwenyekiti wa Jumuiya kuendelea kuwasiliana na Umoja wa Ulaya kwa lengo la kupata majibu yanayoendana na hoja zilizowasilishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  30  63.           Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka2017/18, Wizara iliendelea kuratibu majadiliano ya maeneo yaliyosalia katika kuanzisha Eneo Huru la Biashara la Utatu wa COMESA-EAC-SADC pamoja na kuweka katika lugha ya kiuandishi viambatisho vya Mkataba huo. Majadiliano yamekamilika katika Kiambatisho Na. II kinachohusu Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara, Kiambatisho Na. IV kinachohusu Sheria ya Utambuzi wa Uasilia wa Bidhaa na Kiambatisho Na. X kinachohusu Utatuzi wa Migogoro. Majadiliano yanaendelea baina ya nchi wanachama kwenye kanuni za utambuzi wa uasilia wa bidhaa pamoja na uondoaji wa ushuru wa forodha.


  Sekta za Uzalishaji  64.           Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeratibu maandalizi na ushiriki wa Tanzania katika mikutano ya kuandaa sera na mikakati ya kukuza viwanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan katika maeneo yaliyoainishwa na Wakuu wa Nchi kuwa ya vipaumbele hasa utengenezaji wa magari, uzalishaji wa dawa na bidhaa za nguo na ngozi. Wizara ilihakikisha vipaumbele vya nchi vinajumuishwa katika sera na mikakati iliyoandaliwa ikiwemo Mkakati wa Tano wa Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2016/17-2020/21. Ni mategemeo yetu kuwa sera hizi za mtangamano zitasaidia kukuza viwanda na hivyo kuchangia kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
  31  Uendelezaji wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii  65.           Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutekelezaji wa programu na miradi ya kikanda ya uendelezaji wa miundombinu ya uchumi na huduma za jamii kama ifuatavyo:  Maendeleo ya Miundombinu ya Uchukuzi, Nishati na Uwekezaji katika Sekta ya Afya  66.           Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushirikikatika Mkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliojadili maendeleo ya sekta ya miundombinu ya uchukuzi, nishati, na uwekezaji katika sekta ya afya uliofanyika Kampala mwezi Februari 2018. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kubaini kiasi cha fedha kinachohitajika kutekeleza miradi hiyo ambapo imeelezwa kuwa katika miaka 10 ijayo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 78 zitahitajika kutekeleza miradi ya miundombinu ya uchukuzi na nishati. Hivyo, miradi 17 ya kipaumbele cha juu ilipitishwa ambapo miradi 10 kati ya hiyo itatekelezwa Tanzania.  67.           Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha sekta yaafya, Wakuu wa Nchi walipitisha vipaumbele tisa. Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kupanua wigo wa huduma za tiba za ubingwa kwa kuimarisha miundombinu, vifaatiba


  na wataalam; na kupambana na magonjwa ya mlipuko 32  na dharura za kiafya zinazotokana na mwingiliano wa kimataifa. Vilevile, vipaumbele hivyo vimeelekezwa katika kujenga uwezo wa taasisi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya afya kwa kuwianisha mitaala ya mafunzo, viwango na miongozo katika sekta ya afya ili kuwa na wataalam wa kutosha na wenye weledi; kupanua wigo wa matumizi na huduma za bima ya afya na hifadhi ya afya ya jamii; na kuendeleza utafiti katika sekta ya afya.  68.           Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu kuwaWizara za kisekta kwa kadri hali ya bajeti itakavyoruhusu, zitaendelea kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kipaumbele.


  Usimamizi wa Mazingira Bonde la Ziwa Victoria  69.           Mheshimiwa Spika, wakati wa kikao kilichopita chabajeti cha 2017/18, nililiarifu Bunge lako Tukufu kuhusu Awamu ya Pili ya Mradi wa Usimamizi wa Mazingira katika Ziwa Victoria. Naomba kuliarifu Bunge lako kuwa mradi huo umekamilika mwezi Desemba 2017 ambapo faida zilizopatikana ni pamoja na kupunguza magugu maji na kuwapatia maji safi na salama wananchi wanaoishi maeneo ya mradi. Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wengine inaratibu majadiliano ya Awamu ya Tatu ya Mradi huo.  70.           Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu upatikanajiwa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kikanda


  33  cha Uratibu wa Usalama na Uokozi (Maritime Rescue Coordination Centre - MRCC) katika Ziwa Victoria jijini Mwanza. Tanzania imewasilisha Hati ya Umiliki wa Kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 13,287 kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ujenzi wa kituo hicho utakuwa na manufaa ya kurahisisha usafirishaji katika Ziwa Victoria na udhibiti, uokozi na usalama.


  Masuala ya Siasa  71.           Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarishademokrasia, utawala bora, na kulinda haki za binadamu kwa kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa kuzingatia hilo, Wizara iliratibu na kushiriki kwenye kongamano la Utawala Bora la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika Arusha mwezi Oktoba 2017. Pamoja na mambo mengine, kongamano hilo liliazimia kwamba Tume za Haki za Binadamu za nchi wanachama zitoe mafunzo kwa vyombo vya usalama. Aidha, nchi wanachama zilitakiwa kuimarisha uwezo wa Tume za Uchaguzi ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa usawa na kwa kuzingatia maadili.


  Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya na Rwanda  72.           Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza demokrasiana kulinda amani katika Jumuiya, Tanzania ilikuwa sehemu ya timu ya waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika chaguzi zilizofanyika nchini Rwanda


  34  na Kenya mwaka 2017. Katika chaguzi hizo, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kutoka muungano wa Jubilee alichaguliwa kuwa Rais Kenya na Mheshimiwa Paul Kagame kutoka chama cha RPF alichaguliwa kuwa Rais Rwanda. Ripoti za usimamizi katika chaguzi hizo zimeeleza kuwa chaguzi zilikuwa huru na haki. Nachukua nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wananchi wa Kenya na Rwanda kwa kufanya chaguzi kwa amani.  Fungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki  73.           Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 35 wa dharura waBaraza la Mawaziri wa Jumuiya uliofanyika Kampala, mwezi Februari 2018 ulipitisha Rasimu ya Andiko, Hadidu za Rejea, na Mpangokazi wa kuanzisha Fungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki. Aidha, maandalizi ya rasimu ya Katiba ya Fungamano yanaendelea kwa mujibu wa mpangokazi ulioidhinishwa na zoezi hili linatarajiwa kukamilika mwaka 2022.


  Hati Mpya ya Kusafiria ya Kielektroniki ya Afrika Mashariki  74.           Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Nchi Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wao wa 17 uliofanyika Arusha mwezi Februari 2016 walizindua rasmi hati ya kusafiria ya kielektroniki ya Jumuiya ya Afrika


  Mashariki na kukubaliana kuwa kila nchi mwanachama ianze kuzitumia ifikapo mwezi Januari 2018.
  35  75.           Mheshimiwa Spika, napenda kulieleza Bunge lakoTukufu kuwa mwezi Januari 2018, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Mugufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi hati hiyo kwa wananchi wa Tanzania. Wananchi wa Tanzania wataruhusiwa kuendelea kutumia hati walizonazo kwa kipindi cha miaka miwili hadi ifikapo mwezi Desemba 2019. Utoaji wa hati hizi unasimamiwa na mamlaka husika katika kila nchi mwanachama kulingana na sheria za nchi yake.


  Mapambano Dhidi ya Ugaidi na Uharamia  76.           Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Afrika Masharikiinaandaa mpango wa utekelezaji wa mkakati wa kupambana na ugaidi. Mkutano wa wadau uliofanyika Mwanza, mwezi Oktoba 2017 uliandaa mfumo utakaowezesha vyombo vinavyohusika na mapambano dhidi ya ugaidi kufanya kazi kwa pamoja katika kutekeleza mkakati huo.


  77.           Mheshimiwa Spika, katika kupambana na uharamiakwenye Bahari ya Hindi, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa Kikanda wa kupambana na uharamia kwa kuratibu makubaliano maalum ya namna ya kubadilishana taarifa za wahalifu. Kufikiwa kwa makubaliano hayo kutasaidia nchi wanachama kubadilishana uzoefu na kubaini mbinu zinazotumiwa na maharamia ili kuimarisha mapambano dhidi ya uharamia katika Bahari ya Hindi. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
  36  Taifa iliratibu zoezi la pamoja la kijeshi la kamandi za kijeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo kama ‘EAC CPX USHIRIKIANO IMARA 2017’ lililofanyika Dar es Salaam mwezi Desemba 2017. Lengo la zoezi hilo lilikuwa ni kujenga uwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kuendesha operesheni za kulinda amani; kupambana na ugaidi; kupambana na uharamia; na kukabiliana na majanga.  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)


  78.           Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 37 wa Wakuu waNchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ulifanyika Pretoria mwezi Agosti 2017. Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimwakilisha Mheshimiwa Rais.  79.           Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na usalama kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017. Taarifa hiyo ilieleza kwa kina tathmini ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda hususan katika Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Madagascar na Falme ya Lesotho. Tanzania ilipongezwa kwa kusimamia vizuri majukumu ya Asasi hiyo.

  37  80.           Mheshimiwa Spika, Mkutano huo, pamoja namambo mengine, ulimteua Dkt Stergomena L. Tax, kuendelea na wadhifa wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha pili na cha mwisho; uliazimia kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufanya uchaguzi tarehe 23 Desemba 2018; na kuridhia ombi la Serikali ya Visiwa vya Comoro kuwa mwanachama wa 16 wa Jumuiya hiyo.  81.           Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Tanzania ilikabidhi rasmi uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Jamhuri ya Angola.


  Ushirikiano kati ya SADC na Umoja wa Ulaya  82.           Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Maendeleo Kusinimwa Afrika na Umoja wa Ulaya ziliingia makubaliano ya mpango wa ushirikiano wa miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. Katika Mpango huo, Umoja wa Ulaya, pamoja na mambo mengine, uliridhia kutoa kiasi cha Euro milioni 31.6 kupitia Awamu ya 11 ya Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya, kuzisaidia nchi wanachama wa SADC kutekeleza Itifaki ya Biashara. Tayari Tanzania imenufaika na mpango huo kwa kupokea kiasi cha Euro 420,000 kati ya Euro milioni 1.4 zilizoahidiwa. Kiasi hicho cha fedha kitatumika kufanya mapitio ya Sera ya viwanda ya Tanzania, kuhamasisha biashara na kuondoa vikwazo vya


  kibiashara visivyo vya kiushuru. 38  Jumuiya ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi


  83.           Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibarkwa kushirikiana na IORA ilifanya warsha ya kuandaa Mkakati wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Uvuvi katika Ukanda wa Bahari ya Hindi mwezi Oktoba 2017.  84.           Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania imeanzakunufaika na mtandao wa kupeana taarifa za biashara (IORA Trade Repository) ikiwemo mfumo wa kodi, uasili wa bidhaa, taratibu za forodha na upatikanaji wa leseni za uingizaji wa bidhaa kwa kila nchi iliyo ndani ya Jumuiya uliozinduliwa rasmi mwezi Agosti 2017.


  Umoja wa Afrika


  85.           Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu ushiriki waTanzania kwenye Mkutano wa 30 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mwezi Januari 2018. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alimuwakilisha Mheshimiwa Rais ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulijadili taarifa ya Mheshimiwa Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuhuisha Mifumo ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika. Mkutano huo uliazimia nchi wanachama ziendelee na majadiliano ya namna bora ya kutekeleza mapendekezo ya mabadiliko ya kuhuisha


  Mifumo ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika ili kufikia muafaka 39  kwa nchi zote. Aidha, mkutano huo ulizindua soko moja la usafiri wa anga Afrika. Hadi sasa nchi wanachama 21 zimesaini Mkataba wa soko hilo unaotarajiwa kuchochea utalii na kuongeza ajira.  86.           Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 29 waWakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mwezi Julai 2017, Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wanne wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu Masuala ya Rushwa ambapo Bi. Sabina Seja anaiwakilisha Tanzania. Wajumbe wengine kwenye Bodi hiyo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Algeria na Misri.


  87.           Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji iliratibu na kushiriki katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Kigali mwezi Machi 2018. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa kupitia mkataba na itifaki tatu za uanzishwaji wa eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA). Hatua hiyo ni utekelezaji wa maazimio ya Wakuu wa Nchi na Serikali yaliyofikiwa mwaka 2012 kutaka kuanzisha Eneo Huru la Biashara Afrika ambapo majadiliano yake yalizinduliwa rasmi mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2017. Katika mkutano huo nchi wanachama 44 zilitia saini mkataba huo na hatua inayofuata ni nchi kuridhia ili utekelezaji wake uanze rasmi.

  40  88.           Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba huoutazisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi kwa kushiriki kwenye soko la pamoja ambalo lina watu zaidi ya bilioni moja na pato ghafi linalokadiriwa kuwa na jumla ya zaidi ya Dola za Marekani trilioni 3.4. Ni muhimu kwa Tanzania kuongeza uzalishaji na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa mitaji ili kutumia vyema fursa ya soko hilo.  Mkutano wa Masuala ya Mipaka ya Nchi za Umoja wa Afrika


  89.           Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maazimioya Umoja wa Afrika yaliyofikiwa Addis Ababa mwezi Juni


  2007, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuhakiki na kuimarisha mipaka yake na nchi tunazopakana nazo na tayari tumeanza kuhakiki mipaka kati ya Tanzania na nchi za Kenya na Uganda.  90.           Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa mbali na utekelezaji wa azimio hilo, zoezi la uhakiki wa mipaka ya nchi yetu ni endelevu, na linalenga kuweka usimamizi mzuri wa maeneo ya mipaka; kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu; kurahisisha ukusanyaji wa mapato mipakani; kudhibiti uhalifu katika maeneo ya mipaka; kuweka mipango ya maendeleo na utoaji wa huduma za msingi za jamii; na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo baina ya jamii za mipakani.

  41  Ushirikiano wa Kimataifa


  Umoja wa Mataifa


  91.           Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu lakela kuratibu masuala ya kimataifa, Wizara yangu iliratibu na kushiriki mikutano mbalimbali. Baadhi ya Mikutano hiyo ni pamoja na: Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa; UN-HABITAT; UNIDO; Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake; Mikutano ya Kimataifa inayohusu wakimbizi na uhamiaji; Baraza la Haki za Binadamu; Shirika la Chakula Duniani (FAO); na Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola.  92.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibu nakushiriki katika Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2017. Nilipata fursa ya kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vikao vya ngazi ya juu vilivyokutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Masuala muhimu yaliyojadiliwa wakati wa vikao hivyo yalihusu uhusiano wa kidiplomasia, ajenda ya uendelezaji wa viwanda, biashara, uwekezaji, hali ya usalama na amani duniani na mapambano dhidi ya ugaidi.


  93.           Mheshimiwa Spika, pamoja na masuala mengine,Tanzania ilitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za Serikali


  42  ya Awamu ya Tano ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa na Mashirika yake. Vilevile, Tanzania ilieleza hali ya utekelezaji wa ajenda ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 (Malengo ya Maendeleo Endelevu) na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaletea maendeleo watu wake ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa; dawa za kulevya; uwindaji haramu; kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuziba mianya ya ukwepaji kodi; na kusimamia uwajibikaji na nidhamu ya utumishi wa umma. Aidha, Tanzania ilitumia fursa hiyo kuomba mashirika ya kimataifa na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kutoa misaada ya fedha, teknolojia na utaalam ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo endelevu na kuondoa umaskini nchini.


  94.           Mheshimiwa Spika, Tanzania kama zilivyo nchiwanachama wengine wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ilishiriki katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Shirika hilo uliofanyika Paris mwezi Oktoba 2017. Ajenda kuu ya Tanzania katika Mkutano huo ilikuwa kuwasilisha uamuzi wake wa kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Stigler’s Gorge. Katika kutekeleza azma hii, ujumbe wa Tanzania uliungana na wajumbe wengine wa nchi zinazoendelea kusisitiza umuhimu wa Shirika hilo kuweka uwiano kati ya uhifadhi wa maeneo ya urithi wa dunia na kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo husika. Aidha, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zilitumia mkutano huo kuomba msaada wa kuimarisha miundombinu katika
  43  maeneo hayo.  95.           Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendeleakushirikiana na wadau wengine kusukuma ajenda ya kitaifa ya kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Katika kutekeleza azma ya kukuza viwanda, Wizara iliratibu ujio wa Dkt. Li Yong, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) mwezi Machi 2018. Moja ya manufaa ya ziara hiyo ilikuwa ni kusainiwa kwa tamko la kusudio la kuiingiza Tanzania katika mpango maalum wa ushirikiano wa kuendeleza viwanda unaojulikana kama Program for Country Partnership. Kwa kuwa mpango huu umefanyika kwa mafanikio katika nchi za Ethiopia, Senegal na Peru, Tanzania inaendelea na majadiliano ya karibu na UNIDO ili nayo iingizwe katika mpango huo wenye fursa kubwa katika kusukuma maendeleo ya viwanda ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanda.  96.           Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo Shirika laUNIDO lilitoa msaada wa vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Dola za Marekani 80,000 kwa wakulima wa zao la mwani Zanzibar. Vifaa hivyo vitatumika kwa ajili ya shughuli za kilimo, usafirishaji na usindikaji wa mwani jambo ambalo litasaidia kuongeza thamani ya zao hilo katika soko la dunia.  97.           Mheshimiwa Spika, mwaka jana nililijulisha Bungelako Tukufu kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za

  44  kuridhia Mkataba wa Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi ambao Bunge lako Tukufu liliridhia mwezi Aprili 2018. Napenda kulishukuru Bunge lako Tukufu kwa hatua hiyo na tayari Mheshimiwa Rais alisaini hati ya kuridhia na hivyo kuwezesha nchi yetu kutambuliwa rasmi kama mwanachama wa makubaliano hayo. Naomba kutumia fursa hii kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika, kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine wote ndani na nje ya Serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kuwezesha suala hili kufanikiwa. Ni dhahiri kwamba makubaliano haya yana manufaa kwa nchi yetu na dunia nzima.


  Kushughulikia Masuala ya Wakimbizi  98.           Mheshimiwa Spika, moja ya nguzo za Sera yaMambo ya Nje ya Tanzania ni kulinda utaifa wetu, mipaka ya nchi na uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kusimamia nguzo hii muhimu, mwezi Januari 2018, Serikali ilifanya uamuzi wa kujitoa kwenye mpango maalum wa majaribio wa kuhudumia Wakimbizi ujulikanao kama Comprehensive Refugees Response Framework (CRRF). Mpango huo unalenga kuwanufaisha wakimbizi kwa kupanua wigo wa hifadhi yao na kuwawezesha kujitegemea kwa Serikali kuwapatia ardhi, uhuru wa kutembea mahali popote na vibali vya kufanya kazi popote nchini.


  99.           Mheshimiwa Spika, uamuzi wa Serikali kujitoakwenye Mpango huo umezingatia maslahi mapana ya


  45  Taifa letu hususan masuala ya usalama. Nitumie fursa hii kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa pamoja na nia yetu nzuri ya kuwasaidia wakimbizi; usalama, amani na ulinzi wa Taifa letu ndivyo vipaumbele namba moja vya Taifa letu.  100.       Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kutokuafikimpango huo bado Tanzania itaendelea kupokea na kuhifadhi wakimbizi pale inapolazimika kwa kuzingatia sheria za nchi na mikataba ya kikanda na kimataifa. Aidha, tunaendelea kutoa wito kwa wakimbizi kurudi makwao kwa hiari pale ambapo hali ya usalama kwenye nchi zao inapotengemaa.


  Jumuiya ya Madola


  101.       Mheshimiwa Spika, Makamu wa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alimwakilisha Rais kwenye mkutano wa 25 wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika London mwezi Aprili 2018. Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulipitisha maazimio matano yanayosisitiza kuifanya dunia kuwa mahali penye ustawi na salama zaidi ili kuchochea maendeleo, kuleta usawa, utunzaji wa mazingira, amani, haki za binadamu na demokrasia. Maazimio hayo pia yameweka msisitizo kwenye mapambano dhidi ya ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, utumwa, makundi yenye misimamo mikali na uhalifu mwingine wa kimataifa.

  46  102.       Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Serikali kwa kaulimoja walikubaliana kufanya kila liwezekanalo kuongeza biashara na uwekezaji miongoni mwa nchi wanachama. Tanzania ilifanikiwa kuingiza ajenda ya viwanda, nishati ya uhakika na kukuza uchumi kuwa sehemu ya majadiliano na hatimaye kuingia kwenye tamko la mwisho la mkutano huo.  103.       Mheshimiwa Spika, wakati wa mkutano huo,Mheshimiwa Makamu wa Rais alifanya mazungumzo na viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo Rais wa Uganda, Waziri Mkuu wa Australia, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza na Mjukuu wa Malkia, Prince William. Katika mikutano hiyo, viongozi hao waliahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali yakiwemo ya elimu, biashara na uwekezaji na mapambano dhidi ya ujangili na biashara haramu ya wanyamapori. Prince William ni mmoja kati ya viongozi wanaounga mkono jitihada za Tanzania katika mapambano dhidi ya ujangili na uwindaji haramu.  104.       Mheshimiwa Spika, akiwa London, MheshimiwaMakamu wa Rais alikutana na viongozi wa makampuni sita yanayowekeza na yenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania. Kwenye mikutano hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwathibitishia na kuwahakikishia kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji nchini na kukaribisha wawekezaji wengine.

  47  KUSIMAMIA MIKATABA NA MAKUBALIANO YA KIMATAIFA


  105.       Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18 Wizara iliratibu na kusimamia kusainiwa kwa mikataba, hati za makubaliano na kumbukumbu za mazungumzo baina ya Tanzania na nchi mbalimbali. Mikataba na makubaliano hayo ni kiashiria kikubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi yetu na nchi nyingine, mashirika ya Kikanda na Kimataifa katika kuongeza kasi ya kuvutia uwekezaji, kukuza biashara na kutangaza utalii. Wizara inaendelea kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi yetu. Orodha ya mikataba na hati za makubaliano zilizosainiwa katika kipindi hicho ni kama inavyooneshwa kwenye Kiambatisho.  KURATIBU NA KUSIMAMIA MASUALA YA WATANZANIA WAISHIO UGHAIBUNI


  106.         Mheshimiwa Spika, kwa kutambua Watanzaniawanaoishi ughaibuni kama wadau muhimu wa maendeleo, Wizara yangu imeendelea kubuni mbinu mbalimbali za kuwashirikisha katika kuchangia maendeleo ya nchi. Moja ya mbinu hizo ni kuandaa makongamano ndani na nje ya nchi ambapo mwezi Agosti 2017, Wizara yangu kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliandaa Kongamano la Nne la Diaspora lililowakutanisha Watanzania zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali na wadau
  48  wa maendeleo hapa nchini. Kupitia kongamano hilo, Diaspora walihimizwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu kwa kuhamasisha uwekezaji wa mitaji kutoka nje.  107.       Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018 lilifanyikakongamano lingine lililoandaliwa na Diaspora jijini Dallas Marekani, ambalo pamoja na masuala mengine, lililenga kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kuhamasisha wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo utalii.


  108.                Mheshimiwa Spika, mchango wa Diasporakatika maendeleo ya nchi unajidhihirisha katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Yafuatayo ni baadhi ya maeneo hayo:  i.              Diaspora imenunua nyumba zenye thamani ya Shilingi bilioni 29.7 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya biashara na viwanja mbalimbali kati ya mwaka 2011 hadi 2017.  ii.            Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 2013-2017, Diaspora kwa ujumla wao walituma nchini kiasi kisichopungua Dola za Marekani bilioni 2.3.


  49  iii.         Timu ya madaktari wa kitanzania waishio Marekani kupitia taasisi ya afya, elimu na maendeleo (Head Inc.) ilitoa huduma ya afya bila malipo na vifaatiba katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja;  iv.         Jumuiya ya Watanzania nchini Marekani (DICOTA) iliandaa jukwaa la afya mwezi Novemba 2017 ambalo lilihudhuriwa na wataalam wa afya zaidi ya 130 kutoka Tanzania na Marekani ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutathmini njia madhubuti za kuendeleza sekta ya afya nchini Tanzania. Juhudi hizi ziliwezesha kupatikana kwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi na wafanyakazi zaidi ya 60 kutoka vyuo vikuu na hospitali nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Tiba KCMC, Hubert Kairuki, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na hospitali ya Bugando.  v.           Aidha, Dkt. Frank Minja mtanzania mtaalam wa Radiolojia wa Chuo Kikuu cha Yale Marekani amesaidia kuimarisha mfumo wa teknolojia ya kisasa ya radiolojia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.  109.       Mheshimiwa Spika, wakati ambapo kipaumbelecha kitaifa ni viwanda, tunahitaji kufikiria ujuzi maalum


  50  walionao Watanzania wanaoishi katika Diaspora, na vile vile mchango wa kifedha ambao wanaweza kuchangia kutoka kwenye vyanzo vyao binafsi au kwa kushirikiana na raia wa nje, mabenki na taasisi nyingine za nje. Ili kuwezesha viwanda vyetu kuuza nje, tunahitaji kutambua, kupima na kupenya katika masoko mbalimbali ya kigeni. Watanzania walioishi nchi za kigeni na watoto wao wanaweza kuchangia zaidi kutokana na ujuzi wao kwa kupata masoko kwa kutumia ujuzi wao wa lugha za kigeni.


  110.       Mheshimiwa Spika, watanzania wengi walioDiaspora wanachangia sana maendeleo ya kijamii na uchumi wa familia zao na Tanzania kwa ujumla, na wako tayari kushiriki katika jukumu kubwa la kujenga uchumi wa Taifa hili. Pengine tunahitaji kuwa na mfumo wa kisheria na sera ya kutoa huduma hiyo kwa uhalali na uhakika.
  TATHMINI YA HALI YA DUNIA Hali ya usalama


  111.       Mheshimiwa Spika, hali ya usalama dunianiimeendelea kuimarika pamoja na kwamba changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo. Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasa katika baadhi ya nchi, matukio ya kigaidi na kuongezeka makundi yenye itikadi kali na athari za kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Katika kukabiliana na changamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkono
  51  jitihada za kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarisha amani na usalama duniani.  112.       Mheshimiwa Spika, kuhusu migogoro yakisiasa katika baadhi ya nchi, naomba nitumie fursa hii kuizungumzia kama ifuatavyo:


  Lesotho


  113.       Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi na usalamanchini Lesotho bado hairidhishi. SADC ilituma misheni maalum ya ulinzi wa amani ili kusaidia nchi hiyo kutekeleza maazimio ya kurejesha amani. Naomba niliarifu Bunge lako Tukufu kuwa misheni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe

  2 Desemba 2017 na ina jumla ya maafisa 269. Serikali ya Lesotho imetakiwa kutekeleza maazimio yanayohusu maboresho ya mifumo ya Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja.


  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo


  114.       Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalamanchini DRC hairidhishi. Hivi sasa Serikali ya nchi hiyo inaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 23 Desemba 2018. Maandalizi ya uchaguzi huu yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa zoezi la kuandikisha wapiga kura na kupitisha sheria mpya ya uchaguzi. Natoa rai kwa wadau wa ndani na nje kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu kama ulivyopangwa. Hata hivyo, DRC inahitaji kusaidiwa kwa hali na mali katika kuandaa uchaguzi huo
  52  hususan ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote Barani Afrika.


  Madagascar


  115.       Mheshimiwa Spika, hali ya siasa nchini Madagascarhairidhishi na SADC imetuma ujumbe wa Baraza la ushauri la masuala ya uchaguzi nchini humo ili kufanya tathmini ya utayari wa nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu Novemba 2018. Aidha, SADC ilimtuma Mheshimiwa Joaquim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji na mjumbe maalum wa SADC tarehe 8 hadi 13 Mei 2018 kwa lengo la kusaidia kuweka mazingira ya amani kabla ya uchaguzi mkuu.


  Sudan Kusini  116.       Mheshimiwa Spika, hali ya usalama nchini SudanKusini imeendelea kuwa ya wasiwasi kutokana na uhasama kati ya Serikali na upinzani. Aidha, hatua ya waliokuwa viongozi wa juu wa jeshi la nchi hiyo kuamua kuunda vikundi vya uasi imezidi kuchochea mgogoro huo. Hadi sasa mgogoro huo umesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukimbilia nchi jirani na wengine zaidi ya 230,000 kulazimika kuyakimbia makazi yao na kuhifadhiwa kwenye makambi ya Umoja wa Mataifa nchini humo.


  117.       Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba wamwezi Agosti 2015 wa kugawana madaraka umeendelea kusuasua licha ya jitihada za Jumuiya ya Maendeleo ya IGAD za mwaka 2017 za kufufua utekelezaji wa makubaliano
  53  hayo. Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zinaendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. Tanzania inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa kutafuta suluhu ya kudumu nchini humo.


  Somalia  118.       Mheshimiwa Spika, hali ya usalama na siasa nchiniSomalia inaendelea kuimarika baada ya kuwa na Katiba mpya na uchaguzi wa Bunge kufanyika. Kwa kupitia jitihada kubwa za Jeshi la Serikali ya Somalia kwa kushirikiana na AMISOM, Serikali imerejesha zaidi ya asilimia 80 ya maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab. Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo kikundi hicho kimeendelea kuwa ni kikwazo cha kuleta amani nchini humo.  119.       Mheshimiwa Spika, kwa upande mwinginemajeshi ya AMISOM yameanza kuondoa askari wake na kuhamasisha Jeshi la Somalia kuanza kuchukua jukumu la kulinda usalama wa nchi yake. Katika kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba 2017, jumla ya askari 1,000 wa AMISOM waliondolewa na kurudishwa katika nchi zao. Tanzania inaitakia Serikali ya Somalia na watu wake mafanikio katika mipango ya kurejesha na kuimarisha amani na usalama nchini humo.

  54  Libya  120.       Mheshimiwa Spika, hali ya amani na usalamanchini Libya ni tete. Hali hiyo imechangiwa na Dola kukosa udhibiti wa nchi, kuongezeka kwa makundi yanayokinzana na kukwama kwa mazungumzo ya amani. Tanzania inaunga mkono juhudi za kimataifa zinazoendelea kupitia Umoja wa Afrika za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.


  121.       Mheshimiwa Spika, siku za hivi karibuni,imeripotiwa kuibuka kwa biashara haramu ya binadamu na utumwa katika baadhi ya maeneo nchini Libya. Tanzania inalaani kwa nguvu zote kuwepo kwa biashara hiyo na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua stahiki kwa wale waliohusika.


  Burundi  122.       Mheshimiwa Spika, kuhusu mgogoro wa kisiasanchini Burundi napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba jitihada kubwa zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya usuluhishi wa Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda akisaidiwa na Mwezeshaji Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimesaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Burundi tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 mgogoro huo ulipoibuka. 


  55  123.       Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushirikikatika mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi uliofanyika Arusha, mwezi Novemba 2017. Mazungumzo hayo yalijumuisha Serikali ya Jamhuri ya Burundi na makundi yanayohusika na mgogoro huo wakiwemo wanasiasa, Marais wastaafu, viongozi wa dini, vyama vya siasa na vyama vya kiraia.


  Syria  124.       Mheshimiwa Spika, mgogoro wa Syria badounaendelea kuwa moja kati ya ajenda muhimu kwenye jumuiya ya kimataifa. Mgogoro huo unazidi kuwa mgumu kutokana na mvutano wa mataifa makubwa. Tunayasihi mataifa yanayohusika na mgogoro huo kushirikiana ili kurejesha amani nchini humo kwa njia ya mazungumzo. Hii inatokana na ukweli kwamba vita vinavyoendelea baina ya makundi mbalimbali yanayoungwa mkono na nchi za kigeni huzidisha uhasama na kusababisha hasara kubwa kwa maisha ya binadamu wasio na hatia pamoja na uharibifu wa miundombinu ya nchi hiyo.


  Yemen  125.       Mheshimiwa Spika, Tanzania ina imani kwambawananchi wa Yemen wana haki ya kujiamulia mustakabali wa nchi yao. Kutokana na mgogoro huo idadi ya vifo, raia wanaokimbia nchi yao na wanaopoteza makazi inazidi kuongezeka. Tanzania inaamini kuwa mgogoro huu
  56  unaweza kupatiwa suluhu kwa pande zinazohasimiana kukaa pamoja na inaunga mkono juhudi za usuluhisho wa mgogoro huo, kupitia jumuiya za kimataifa.  Iran  126.       Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 nchi wanachamawa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani ziliingia makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia ili kuondolewa vikwazo vya kiuchumi. Mkataba huo ulitoa matumaini ya ushirikiano wa kimataifa katika juhudi za kuondokana na silaha za nyuklia. Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi Mei 2018, mmojawapo wa wadau wakuu ametangaza kujitoa katika mkataba huo. Tanzania inazisihi pande zote zinazohusika kuendelea kuheshimu mkataba huo na kama kuna dosari katika mkataba huo zitatuliwe kwa njia ya mazungumzo.


  Rasi ya Korea  127.       Mheshimiwa Spika, Rasi ya Korea ni miongonimwa maeneo yenye historia ya mgogoro wa muda mrefu na kutishia hali ya amani na usalama duniani. Hata hivyo, hali hiyo imeanza kubadilika kufuatia tukio la kihistoria lililoshuhudiwa mwezi Aprili 2018 wakati Marais wa Korea Kaskazini na Korea Kusini walipokutana katika eneo la mpaka wa nchi hizo (Demilitarized Zone) baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhasama. Marais hao walikutana kujadili namna ya kumaliza tofauti zao na kushirikiana. Aidha,
  57  mkutano huo umefanyika baada ya miaka 10 tangu viongozi watangulizi wa nchi hizo mbili, Rais Kim Jong Il na Rais Roh Moo-hyun kukutana mwaka 2007.  128.       Mheshimiwa Spika, baada ya Rais wa Jamhuri yaKorea Moon Jae-in kuingia madarakani mwaka 2017, moja ya agenda za serikali yake ilikuwa ni kukaa katika meza ya majadiliano na Korea ya Kaskazini ili kutafuta suhuhu. Nia hiyo njema ya kiongozi huyo iliimarishwa na hotuba ya Rais wa Korea Kaskazini ya mwaka mpya 2018, ambapo alimtakia heri na mafanikio Rais wa Korea Kusini katika kuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi ya Februari 2018. Baada ya salamu hizo Rais wa Korea Kusini alimwalika mwenzake kushiriki ufunguzi pamoja na kutuma timu kushiriki katika mashindano hayo. Mwanzo huo mzuri ulizaa matunda na dunia iliendelea kushuhudia mazungumzo mbalimbali katika ngazi za juu za Maofisa wa usalama wa nchi hizo mbili na hatimaye mkutano huu wa kihistoria.  129.       Mheshimiwa Spika, Tanzania kama nchimwanachama wa Umoja wa Mataifa, ambayo imekuwa ikichangia sana katika harakati za kuimarisha amani na usalama duniani, na kusimamia suluhu ya migogoro kupitia mazungumzo inapongeza kwa dhati hatua hii ambayo imeonesha umuhimu wa diplomasia katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo. Dunia inasubiri kwa hamu matokeo ya mazungumzo kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na rais Kim Jong-un wa Korea ya Kaskazini


  58  yatakayofanyika baadae mwaka huu.
  Bahari ya Kusini ya China (South China Sea)


  130.       Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa ikifuatiliakwa makini hali ya usalama katika Bahari ya Kusini ya China na visiwa vyake. Tunaunga mkono msimamo wa China unaotaka pawe na mazungumzo baina ya nchi zinazohusika katika kutatua mgogoro na kuondoa tofauti zilizopo kati ya nchi hizo kwa mazungumzo ili kufikia suluhu kwa njia ya amani.


  Nchi za Ghuba  131.       Mheshimiwa Spika, Tanzania inafuatilia kwamakini mwelekeo wa siasa na tofauti zilizopo katika nchi za ghuba, hususan Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri kwa upande moja na Qatar kwa upande mwingine, nchi zote hizi zina uhusiano mzuri na Tanzania. Nchi hizi zina rasilimali kubwa ya mafuta na gesi ambayo ni muhimu kwa uchumi wao na dunia kwa ujumla. Tanzania inazisihi nchi hizi ambazo ni muhimu kwa amani na uchumi wa dunia kuzungumza na kufikia muafaka wa tofauti zao kwa amani.
  59  Hali ya Uchumi  132.       Mheshimiwa Spika, uchumi wa dunia umeendeleakuimarika ambapo kwa sasa unakadiriwa kukua kwa asilimia 3 ikilinganishwa na asilimia 2.4 mwaka 2016. Ukuaji huo umechangiwa zaidi na kuimarika kwa uchumi wa mataifa yaliyoendelea, uwekezaji wa mitaji kwenye nchi zinazoibukia kiuchumi, pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa. Hali hii inatoa matumaini ya kuimarika kwa biashara ya bidhaa hususan kutoka nchi zinazoendelea.  133.       Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Afrika,shughuli za kiuchumi zimeendelea kuimarika zikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa uchumi wa mataifa yaliyoendelea pamoja na masoko yanayoibukia. Uchumi wa Afrika unakadiriwa kukua kwa asilimia 3.1 mwaka 2018 kutoka asilimia 1.5 mwaka 2016. Ukuaji huu unatarajiwa kuendelea kutokana na kuimarika kwa hali ya soko la fedha la nje (external financial market conditions). Hali hii itasaidia kuongezeka kwa uwekezaji katika miundombinu ya kimkakati kama vile reli, bandari na barabara. Hata hivyo, ukuaji wa uchumi katika Afrika unatarajiwa kuwa na viwango tofauti ambapo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kuendelea kuimarika zaidi. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuendelea kuwa kinara katika ukuaji wa uchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na hata katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.


  60  134.       Mheshimiwa Spika, hali hii nzuri ya ukuajikiuchumi kwa ujumla wake, unaweza kuathiriwa na baadhi ya matatizo ya kimfumo hususan kwenye sekta ya fedha na kodi. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuweka mfumo mahsusi wa ushirikiano wa masuala ya kodi kwa ajili ya kuondoa ushindani wa kukusanya kodi na kuyalazimisha makampuni ya kimataifa kulipa kodi stahiki kwenye nchi yanapowekeza. Aidha, Tanzania inahamasisha ushirikiano madhubuti wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na uhamishwaji haramu wa fedha ili kupambana na vitendo vya rushwa vya kimataifa. Kwa sasa thamani ya fedha zinazohamishwa kutoka nchi zinazoendelea kwenda nchi tajiri ni kubwa kuliko thamani ya misaada ya maendeleo inayotolewa kwa nchi zinazoendelea hivyo ni muhimu kuwa na mkakati wa pamoja kudhibiti uhalifu huu unaokwamisha jitihada za maendeleo Afrika na kwingineko. Changamoto hizi zinahitaji ushirikiano wa kimataifa kuzitatua na kuimarisha mifumo ya kisiasa na kiusalama ili kuweka mazingira mazuri ya kujenga uchumi imara kwa watu wote.


  135.       Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwakeShirika la Biashara Duniani (WTO), limekuwa muhimili mkubwa katika kuhakikisha biashara duniani zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizojadiliwa na kukubalika na nchi zote wanachama. Kama leo hii pasingekuwepo na WTO ili kusimamia uendeshaji wa biashara na hasa kulinda maslahi ya nchi zinazoendelea kama Tanzania, dunia ingekuwa siyo mahali salama pakufanya biashara. Migogoro na mivutano ya
  61  kibiashara ingekuwa mingi na ingezorotesha maendeleo.  136.       Mheshimiwa Spika, hivi sasa Shirika hili linapitiachangamoto zinazotishia uwepo wake na ustawi wa biashara duniani tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 20 iliyopita. Hali hii inasababishwa na kuongezeka kwa maamuzi ya nchi moja moja (unilateralism) badala ya kuzingatia misingi ya kuamua kwa pamoja (multilateralism) iliyojengwa na WTO. Nchi zinazoendelea zikiruhusu hili, zitakuwa za kwanza kuangamia. Natoa wito kwa nchi zote hususan zilizoendelea kuheshimu na kulinda misingi ya ushirikiano wa kimataifa katika kufanya maamuzi ya biashara duniani. Pale panapotokea sintofahamu, ni vizuri kufuata taratibu za usuluhishi za kimataifa zinazokubalika.


  137.       Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Tanzania itaendelea kusimamia na kutetea misingi ya ushirikiano wa kimataifa katika kufikia maamuzi yanayohusu mustakabali wa dunia kwenye nyanja zote.


  TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA


  138.       Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia taasisitatu ambazo ni Chuo cha Diplomasia, Taasisi ya Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, ambacho pia kinasimamia Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Dar es Salaam. Naomba nichukue fursa hii kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kama ifuatavyo:
  62  Chuo cha Diplomasia


  139.       Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendelea kutekelezamajukumu ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kushauri


  Wizara katika masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yamejikita zaidi katika programu ya diplomasia ya uchumi ili kwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya mageuzi ya uchumi wa Tanzania kuwa wa viwanda.


  140.       Mheshimiwa Spika, katika kujiimarisha, Chuokinatekeleza mradi wa upanuzi na uboreshaji wa miundombinu yake ili kuongeza udahili wa wanafunzi. Madhumuni ya hatua hizi ni kutoa nafasi zaidi ya elimu kwa umma na kukiongezea chuo mapato na hatimaye kupunguza utegemezi wa fedha za uendeshaji kutoka Serikalini. Katika kufanikisha hilo, Wizara inaendelea kutenga fedha zaidi kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho.


  Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha


  141.       Mheshimiwa Spika, Kituo cha Kimataifa chaMikutano Arusha (AICC) kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia ya mikutano hapa nchini na kuchangia katika kukuza uchumi. Hadi kufikia mwezi Machi 2018 Kituo kilikuwa mwenyeji wa mikutano 257 ambapo kati ya hiyo, mikutano 57 ni ya kimataifa na 200 ya kitaifa ambayo imeingiza jumla ya Shilingi 2,036,218,423.

  63  142.       Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwakawa fedha 2018/19, Kituo kimepanga kuingiza mapato ya Shilingi 16,743,620,893. Kati ya fedha hizo, Shilingi 15,587,877,637 ni kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani; na Shilingi 1,155,743,256 zitatokana na mkopo. Aidha, Kituocha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kinategemewa kuingiza kiasi cha Shilingi 3,338,800,000.


  143.       Mheshimiwa Spika, Kituo cha AICC kinategemeakukopa Shilingi 1,155,000,000 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Hospitali ya AICC. Aidha, kituo kinaendelea kufanya taratibu za kuwezesha ujenzi wa kituo mahsusi cha mikutano kitakachoitwa Mt. Kilimanjaro International Convention Centre (MK-ICC). Kituo hicho ndicho kitakachokuwa suluhisho la utekelezaji wa diplomasia ya mikutano ya kimataifa na maonesho hapa nchini. Vilevile, Kituo kimeiomba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mikutano jijini Dodoma.


  Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika (APRM)


  144.       Mheshimiwa Spika, APRM ni mpango wa nchi zaAfrika wa kujitathmini katika masuala ya utawala bora. Tanzania ilijiunga na Mpango huo mwaka 2004, na uliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005. Lengo la APRM ni kuziwezesha nchi za Afrika kuimarisha utawala bora kwa kushirikisha wananchi wake kubainisha changamoto na kuzigeuza kuwa fursa za


  64  maendeleo ili kubaini mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.  145.       Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18, kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, APRM Tanzania iliendelea kutekeleza shughuli zilizopangwa kwenye mpangokazi kama ifuatavyo:


  (i)     Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa APRM kwa ufadhili wa jumla ya Dola za Marekani 100,000 kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania;
  (ii)   Kusimamia uzinduzi wa Ripoti ya nchi uliofanywa tarehe 19 Julai 2017 na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;


  (iii)Kufanya warsha ya kuwajengea uwezo watendajiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuunganisha mipango ya maendeleo ya nchi pamoja na mpangokazi wa APRM;


  (iv)Kushiriki mikutano ya APRM kulingana na Mkataba wa Makubaliano wa kujiunga na APRM; na


  65  (v)   Kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa shughuli za APRM.  146.       Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimuwa misingi ya utawala bora, Wizara yangu itaendelea kuiwezesha APRM kutekeleza majukumu yake.
  UTAWALA NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU


  147.       Mheshimiwa Spika, Wizara ina jumla ya watumishi456 wa kada mbalimbali. Kati ya hao, 347 wapo Makao Makuu ya Wizara na 109 wapo katika Balozi zetu nje ya nchi.


  Ajira Mpya  148.            Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka2017/18, Wizara ilipata kibali cha kuajiri watumishi 10 wa kada mbalimbali ambapo hadi sasa watumishi 5 tayari wameripoti kazini na watumishi 5 taratibu za ajira zao zinaendelea.  Upandishaji vyeo watumishi  149.       Mheshimiwa  Spika,  katika  kipindi  cha  mwaka


  2017/18, Wizara imepata kibali kutoka Ofisi ya Rais,


  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora cha kuwapandishavyeowatumishi97.Taratibuzakuwapandisha
  66  vyeo watumishi hao zinaendelea kukamilishwa.  Uteuzi  150.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya uteuzi wa mabalozi watano ambapo kati yao watatu wamepangiwa vituo na wawili taratibu za kuwapangia vituo zinaendelea.


  Mafunzo  151.       Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwajengeauwezo Watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ndani na nje ya nchi. Watumishi 31 walihudhuria mafunzo ya muda mfupi na watumishi 9 wanaendelea na mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili. Aidha, Wizara ilipokea nafasi 5,220 za mafunzo kutoka nchi 27 wahisani na marafiki. Kati ya nafasi hizo mafunzo ya muda mfupi ni 4,650 na ya muda mrefu ni 570. Wizara iliratibu fursa hizo kwa kuzitangaza kwa umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari, tovuti ya wizara, mitandao ya kijamii na nyingine ziliwasilishwa moja kwa moja kwenye Wizara na Idara za kisekta ili watanzania wenye sifa waweze kuomba nafasi hizo.


  152.       Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa SeminaElekezi kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la


  Afrika                                     Mashariki iliyofanyika mwezi Januari, 2018, 67  Jijini Dar es Salaam. Lengo la Semina hiyo lilikuwa ni kuwajengea uelewa Waheshimiwa Wabunge hao katika masuala yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao, wakihakikisha kuwa wanawasilisha na kutetea hoja zenye manufaa na maslahi mapana kwa ustawi wa nchi yetu wakati wa mijadala ndani ya Bunge hilo.  153.       Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18 Wizara yangu imekabiliana na changamoto mbalimbali za kimfumo wa dunia, pamoja na zile za kiutendaji. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi mkubwa kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wote wa ndani na nje kuhakikisha kwamba malengo ya Serikali kwenye ushirikiano wa kimataifa yanatimia bila kujali uwepo wa changamoto hizo. Napenda kutumia fursa hii kuhimiza wadau kuendelea kushirikiana na Wizara yangu ili kwa pamoja tuweze kutimiza azma ya Serikali ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wote.  SHUKRANI  154.       Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombakuchukua fursa hii kuwashukuru Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kupitia nchi na mashirika yao kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
  68  155.       Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tanoimeendelea kupata mafanikio makubwa kutokana na mchango wa wadau na washirika wa maendeleo kutoka nchi na asasi mbalimbali za kitaifa, kikanda, kimataifa pamoja na sekta binafsi. Naomba nitumie fursa hii kuzishukuru nchi za Afrika Kusini, Algeria, Australia, Austria, Brazil, Canada, China, Cuba, Denmark, Finland, Hungary, India, Italia, Ireland, Israel, Iran, Japan, Korea Kusini, Kuwait, Malaysia, Marekani, Malta, Misri, Morocco, New Zealand, Norway, Oman, Pakistan, Palestina, Poland, Qatar, Saudi Arabia, Sweden, Singapore, Sri-Lanka, Thailand, Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ureno, Urusi, Uswisi, Uturuki na Vietnam kwa kuchangia mafanikio hayo muhimu kwa Taifa.
  156.       Mheshimiwa Spika, shukrani ziwaendee pia Umojawa Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, African CapacityBuilding Facility, Benki ya Dunia, IAEA, Shirika la FedhaDuniani (IMF), Investment Climate Facility for Africa, UNDP na Mashirika mengine yote ya Umoja wa Mataifa, TradeMark East Africa, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo yaKiuchumi ya Afrika (BADEA), The Association of EuropeanParliamentarians with Africa, WWF, The Belinda and Bill gates Foundation, Global Fund, International Committee of the Red Cross, International Federation of the Red Cross and Red Crescent Societies, Medecins Sans Frontieres pamojana Mifuko na Mashirika mbalimbali ya Misaada. Ni dhahiri kuwa mafanikio tuliyoyapata yamechangiwa kwa misaada
  69  na ushirikiano wenu.


  MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19


  157.       Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari miongoni mwamalengo yaliyopangwa kutekelezwa na Wizara yangu katika mwaka wa Fedha 2018/19 ni pamoja na:  i.        Kuendelea kulinda na kutetea misingi ya Taifa;  ii.      Kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ikiweka msisitizo kwenye diplomasia ya uchumi kuelekea Tanzania ya viwanda;  iii.    Kuendelea kuvutia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali, biashara pamoja na kutangaza vivutio vya utalii;  iv.    Kuratibu Tume za Pamoja za Kudumu za Ushirikiano (JPC);  v.      Kufuatilia mwelekeo wa siasa na uchumi duniani na kutathmini matokeo yake kwa siasa ya mambo ya nje ya Tanzania;  vi.    Kuendelea kuratibu utekelezaji wa makubaliano ya kikanda na kimataifa ikiwemo agenda ya
  70  Umoja wa Afrika ya 2063; na agenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030;  vii.  Kufuatilia fursa mbalimbali zinazotokana na ushiriki wa Tanzania katika mtangamano wa kikanda na mashirika ya kimataifa;  viii.Kuendelea kuongeza uwakilishi wa Tanzania nje kwa kufungua Balozi mpya, Konseli Kuu, kutumia Konseli za Heshima sambamba na kuongeza umiliki wa nyumba za makazi ya watumishi na ofisi balozini;  ix.        Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa;  x.      Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mikataba mbalimbali iliyosainiwa kati ya nchi yetu na nchi nyingine na kufuatilia ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa nchi yetu na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa;  xi.    Kuongeza mshikamano na jumuiya za watanzania wanaoishi ughaibuni na kuweka utaratibu madhubuti utakaowawezesha kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa;  xii.  Kuendelea kushirikiana na Wizara, Taasisi za
  71  Serikali, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari katika kuelimisha umma juu ya fursa mbalimbali zitokanazo na ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya za kikanda na kimataifa;


  xiii.Kuendelea kutafuta nafasi za masomo, misaada na kushawishi nchi na mashirika kutufutia madeni; na


  xiv. Kuendelea kujenga uwezo wa watumishi Wizarani.


  MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19


  158.       Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha2018/19, Wizara yangu imetengewa bajeti ya kiasi cha Shilingi 177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi 154,810,812,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, Shilingi 11,795,420,000 ni kwa ajili ya mishahara na Shilingi 10,400,000,000 ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.


  159.       Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya matumizimengineyo, Shilingi 116,010,729,689 ni kwa ajili ya matumizi ya vifungu vya Balozini, Shilingi 35,324,806,566 ni kwa ajili ya vifungu vya makao makuu ya Wizara, Shilingi1,077,362,234 ni kwa ajili ya Mpango wa KujitathminiKiutawala bora Tanzania, Shilingi 1,000,000,000 ni kwa ajili ya fedha za matumizi mengineyo ya Chuo cha Diplomasia, Shilingi 1,239,633,751 ni kwa ajili ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na
  72  Shilingi 158,279,760 ni kwa ajili ya Bodi ya Ushauri waMasuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika.


  160. Mheshimiwa Spika,katika fedha za bajetiya maendeleo, kiasi cha Shillingi 10,400,000,000 zilizopangwa kwa mwaka wa fedha 2018/19, kiasi cha Shilingi 6,180,676,000 zitatumika kwa ajili ya ujenziwa jengo la ofisi ya ubalozi wa Tanzania Muscat, Oman; Shilingi 1,819,324,000 ni kwa ajili ya ukarabati wamajengo ya ofisi na makazi yaliyopo ubalozi wa Tanzania Khartoum, Sudan; na Shilingi 2,400,000,000 ni kwa ajili ya upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ya chuo cha diplomasia.  161.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2018/19, Wizara kupitia balozi zake, inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 28,564,158,100 ikiwa ni maduhuli ya Serikali.


  HITIMISHO


  162.       Mheshimiwa Spika, ili kuweza kutekelezakikamilifu majukumu ya Wizara, kwa mwaka wa fedha 2018/2019, naomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi166,606,232,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaidana Shilingi 10,400,000,000 ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.


  73  163.       Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hiikukushukuru wewe binafsi na waheshimiwa wabunge kwa kunisikiliza.  164.       Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.  74  KIAMBATISHO


  ORODHA YA MIKATABA ILIYORATIBIWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018.


  Katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2017/2018, Wizara ilisimamia na kuratibu uwekaji saini wa Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa kama ifuatavyo:-


  Mikataba Baina ya Tanzania na Nchi Nyingine (Bilateral Agreements)


  (a)                Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu ushirikiano wa Sekta ya Nishati kusaidia eneo la Nangoma lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda, iliyowekwa saini Julai, 2017, Bukoba, Tanzania.


  (b)               Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya elimu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Hungary kupitia Wizara zenye dhamana na masuala ya Elimu, uliowekwa saini tarehe 27 Septemba, 2017, Hungary.


  (c)                Hati ya Makubalino kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Jimbo la Hanan ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Elimu, iliyowekwa saini tarehe 25 Septemba, 2017, China.


  (d)               Hati ya Makubalino kati ya Shirika la Habari la Utangazaji la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Habari la Utangazaji la Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu masuala ya utangazaji iliyowekwa saini tarehe
  75  10 Novemba, 2017, Msaka, Uganda .


  (e)                Mkataba wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Saudi


  Arabia kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga, uliowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017-Colombo, Sri Lanka.


  (f)                Mkataba wa Ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na New


  Zealand kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga uliowekwa saini tarehe tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (g)               Hati ya Makubalino baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uswisi kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (h)               Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jordan kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (i)                 Hati ya Makubalino kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya


  Marekani kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga iliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017-Colombo, Sri Lanka.


  (j)                 Kumbukumbu ya Mazungumzo (Records of Discussions) kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Japan kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (k)               Kumbukumbu ya Mazungumzo (Agreed Minutes) kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini
  76  tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (l)                 Kumbukumbu ya Mazungumzo (Records of Discussions) kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uturuki kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (m)             Kumbukumbu ya Mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na


  Oman kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017-Colombo, Sri Lanka.


  (n)               Kumbukumbu ya Mazungumzo (Agreed Minutes) kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sri Lanka kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga yaliyowekwa saini tarehe 7 Desemba, 2017- Colombo, Sri Lanka.


  (o)               Hati ya Makubalino kati ya Wizara ya Maliasili na Utali ya Wizara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Utalii Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuhusu ushirikiano katika masuala ya utalii, iliyowekwa saini tarehe 10 Januari, 2018, Misri.


  (p)

  Hati  ya  Makubaliano

  kati

  ya  Serikali

  ya


  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali


  ya  Jamhuri  ya  Kiarabu  ya  Misri  kuhusu


  ushirikiano katika nyanja ya kilimo, iliyowekwa


  saini tarehe 10 Januari, 2018, Misri.


  (q)

  Hati  ya  Makubaliano

  kati

  ya  Chuo

  cha


  Diplomasia  cha

  Serikali  ya  Jamhuri

  ya


  Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Mafunzo


  ya Kidiplomasia ya

  Jamhuri ya Kiarabu ya


  Misri  kuhusu

  ushirikiano

  katika  masuala


  ya diplomasia,

  iliyowekwa saini tarehe

  10

  Januari, 2018, Misri.
  77  (r)                 Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Maendeleo la Taifa la Israel (Mashav- Israel Agency for International Developement Cooperation kuhusu kuboresha huduma za afya, iliyowekwa saini tarehe 22 Januari, 2018 Dar es Salaam, Tanzania.


  (s)                Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Serikali ya Palestine kuhusu ushirikiano katika masuala ya afya, iliyowekwa saini tarehe 5 Machi, 2018, Dar es Salaam, Tanzania.


  (t)           Mkataba wa Ushirikiano     kati ya Serikali ya


  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali

  ya Jamhuri Rwanda kuhusu mradi wa pamoja

  wa  ujenzi wa reli ya kisasa  (Standard Gauge

  Railway-SGR), uliowekwa saini tarehe 9 Machi,

  2018, Kigali, Rwanda.


  (u)               Itifaki kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inayohusu Madaktari kutoka China kuja kufanya kazi Tanzania, iliyowekwa saini tarehe 4 Aprili, 2018, Dar es Salaam, Tanzania.


  (v)               Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Brazil


  kuhusu ushirikiano katika nyanja ya Siasa, iliyowekwa saini tarehe 16 Aprili, 2018, Dar es Salaam, Tanzania.


  78  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Karagwe.

  WAZAZI na walezi Mkoani Kagera katika kuelekea msimu wa sikukuu wametakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao zawadi ya kuwaingiza kwenye mpango wa Toto afya kadi ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.

  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Kadi za toto afya pamoja na upimaji wa afya bure kwa wananchi wa magonjwa yasiyoambukiza zoezi lililofanyika katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.

  Mheruka alisema kuwa mzazi au mlezi kumpatia mtoto zawadi ya kadi ya toto afya ni muhimu badala ya kumpatia zawadi ya nguo ambazo atazivaa na zitaisha."Ndugu zangu wazazi wenzangu baada ya kumaliza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zawadi nzuri ya kuwapatia watoto wetu ni kuwaingiza katika mpango huu wa toto afya kadi kwani utamuwezesha mtoto kuwa na uhakika wa matibabu anapougua kwa kipindi cha mwaka mmoja"alisema Mkuu wa Wilaya

  Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa wataendelea kuhimiza wananchi waweze kuingiza watoto wao katika mpango huo.Meneja wa Mfuko wa bima ya Taifa ya afya(NHIF)Elias Odhiambo alisema kuwa wiki hii NHIF wanafanya zoezi la upimaji wa afya wananchi bure na kutoa toto afya kadi katika maeneo ya Omurushaka na Kayanga Wilayani Karagwe.

  Alisema kuwa magonjwa wanayopima wananchi ni uwiano wa uzito na refu(BMI)Kisukari,shinikizo la damu(BP)pamoja na kutoa ushauri.Odhiambo amewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe kutumia fursa hiyo kujua hali za afya zao sambamba na kupata elimu ya kujikinga na maradhi lakini pia kujiunga na mfuko huo."Nawaomba wananchi wote wafike maeneo ambayo tumeweka vituo kwaajili ya tutoa huduma ili waweze kupata huduma kwani huduma hizi tunatoa bure"alisema

  Alisema huduma ya toto afya kadi inahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 8,ambapoatatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi.Alisema mwanachama wa toto afya kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa NHIF ambazo anapata na ambazo zimeorodheshwa katika huduma.Baadhi ya wananchi waliofika katika uzinduzi huo wameupongeza mfuko wa bima ya afya kwa jitihada zake za kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

  "Mfuko huu umetusaidia kutuletea hii huduma ya upimaji wa afya kwani inatusaidia kujua afya zetu lakini pia tunapata fursa ya kuujua vizuri mfuko na huduma zake ambazo ndo mkombozi wa maisha ya kila mwananchi,tunaomba huduma kama hizi ziwe endelevu"alisema Edson Kamugisha.
  Meneja wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambona wananchi(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza na utoaji wa toto afya kadi katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka akimkabithi kadi ya toto afya kadi mmoja wa watoto waliopatiwa kadi katika zoezi la uzinduzi wa kupima afya bure na utoaji wa toto afya kadi kwenye stand ya magari ya omurushaka Wilayani Karagwe
  Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya Taifa Mkoa wa Kagera Adam Kanza akiongea na wananchi katika stand ya magari ya Omurushaka juu ya umuhimu wa kuwakatia watoto wao toto afya kadi
  Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.

  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Shirika la ndege la Precision Air limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya MaxMalipo ikiwa ni katika kuboresha huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya kieletroniki.

  Kupitia makubaliano hayo Precision Air itatumia mfumo wa malipo wa MaxMalipo kuwezesha wateja wake kulipia tiketi tiketi zao kwa njia ya malipo ya mitandao ya simu, Benko na Mawakala wa MaxMalipo.

  Akizungumza baada ya kuwekeana saini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Sauda Rajab utakuwa na faida kwa wateja wa Precision Air kulipia tiketi zao kwa urahisi zaidi ambapo watalipa kwa njia ya simu kupitia mitandao yote ya simu za mkononi, malipo kupitia akauntibza benki zinazokubali malipo kupitia mfumo wa MaxMalipo na mawakala wote nchini takribani elfu thelathini (30,000).

  Sauda amesema kuwa, makubaliano haya ni kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Juni 2017 hadi Juni 2020 na kukiwa na mkakati wa ongezeko la abiria kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza mkataba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Precision Air Sauda Rajab (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakitia saini makubaliano ya kimkataba ya huduma za ulipaji tiketi kwa njia ya kieletroniki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia nakubaliano na kampuni ya MaxMalipo, kulia ni Makurugenzi Mkazi MaxMalipo Tanzania Charles Natal.

  "Mkataba wetu na MaxMalipo ambapo ni wa miaka mitatu umewekewa makubaliano ya ongezeko la abiria ambapo kwa mwaka tunachukua takribani wateja laki nne (400,000) ila mkakati uliowekwa zaidi ni kufikia malengo ya kuongeza wateja kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza,"amesema Sauda.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo nchini Tanzania Charles Natal amesema kuwa ubia huu baina ya MaxMalipo na Precision Air unawezesha wateja wote kufanya malipo ya tiketi za usafiri wa ndege kwa urahisi zaidi na kwa haraka.

  Amesema kwa sasa MaxMalipo ipo katika nchi tano za Afrika na ikiwemo Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia na tayari nchini Kenya wataanza huduma zao hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uwekaji saini makubaliano na Shirika la Ndege la Precisio Air kwa ajilo ya huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya Kieletroniki, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab na Menena Masoko na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi

  "Tumejizatiti zaidi kutoa huduma za malipo ya tiketi kwa njia ya kieletroniki badala ya kufanya booking online au kupitia kwenye ofisi za Precision Air na kupatiwa nambari ya malipo (booking reference number),"amesema Natal.
  Mkataba huo umesainiwa mbele ya waandishi na wahabari na ubadilishana hati za makubaliano hayo kuonyesha kuanza kazi mara moja.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakipeaa mikono baada ya kubalishana hati za makubaliano baina yao. 
  Picha ya pamoja baina ya uongozi wa Precision Air na MaxMalipo Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab, Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal. Meneja Masoko Na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Deogratius Lazaro.Picha na Emmanuel Masaka.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua Kituo cha Polisi cha Kiluvya wilayani Ubungo Mei 24, 2018. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi, Hamad masauni na wanne kukhoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Siro, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa a Dar es salaam na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva. (Picha na Ofiosi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Siro baada ya kufungua Kituo cha Polisi cha Mbweni Wilayani Kawe, Mei 24, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza bungeni alipokuwa akijibu hoja wa wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma juzi.

  ............................................................

  Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kuanza mchakato wa kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa.

  Mchakato huo tayari umeungwa mkono na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  Hayo yameelezwa juzi bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akihitimisha mjadala wa bajeti wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

  “Mheshimiwa Spika, ninaomba kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa  Mhe. Rais ameridhia ombi letu la kupandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Chief Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa, kipekee namshukuru sana Mhe. Rais kwa kuridhia ombi letu hilo” amesema Dkt. Kigwangalla.

  Amesema kufuatia hatua hiyo, wizara yake inaanzisha mchakato rasmi wa kukamilisha taratibu  za kupandisha hadhi mapori hayo ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika kanda ya Kaskazini Magharibi na hivyo kufikia azma ya Serikali kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 8 na mapato ya dola za kimarekani bilioni 16 katika kipindi cha miaka 7 ijayo.

  Inaelezwa kuwa mchakato huo utapitia hatua mbalimbali ikiwemo kuwashirikisha wadau husika kupata maoni yao, mapendekezo kuwasilishwa baraza la mawaziri kabla ya kujadiliwa bungeni na hatimaye kuwasilishwa kwa Mhe. Rais kwa ajili ya kuidhinishwa kuwa Sheria kamili ya kupandisha hadhi mapori hayo.

  Akizungumzia mikakati mingine mipya ya kuboresha sekta ya maliasili na utalii itakayotekelezwa, Dkt. Kigwangalla amesema ni pamoja na kuanzisha mamlaka ya usimamizi na uendelezaji wa utalii wa fukwe nchini, kuhuisha maeneo ya vivutio vya Mambo ya Kale na kuviunganisha katika 'package' moja ya utalii na vivutio vya wanyamapori.

  Mikakati mingine ni kuunda mfumo mmoja funganishi wa TEHAMA uitwao "MNRT Portal" kwa ajili ya kutoa leseni na vibali, ukusanyaji wa takwimu na mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya sekta ya maliasili na utalii, ambapo utaunganishwa na mifumo mingine ya Serikali iliwemo GePG, NIDA, TIRA, BRELA, TRA na NBS.

  Amesema mikakati mingine ni kuanzisha Jeshi Usu, Utambulisho wa Utalii wa Tanzania Kimataifa ujulikanao kama "Tanzania, Unforgettable", kufungua utalii wa kanda ya kusini, kuanzisha mwezi wa maadhimisho ya Urithi wa Mtanzania "Urithi Festival"  (Septemba), kuhuisha sheria za TANAPA, TAWA na TFS, pamoja na kuunda kanuni mpya za kusimamia vizuri sekta hizo.

  Pori la Akiba Burigi lina ukubwa wa kilomita za mraba 2,941 katika wilaya za Karagwe, Muleba na Ngara mkoani Kagera, wakati Pori la Kimisi likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,030 katika wilaya za Ngara na Karagwe mkoani humo.

  Pori la Akiba Biharamulo lina ukubwa wa kilomita za mraba 731 katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera na wilaya ya Chato mkoani Geita, huku Pori la Akiba Ibanda likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 200 na Pori la Akiba Rumanyika kilomita za mraba 800 katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.

  Mapori haya yapo katika ukanda muhimu wa kuunganisha watalii kutoka ikolojia za Magharibi na Mashariki ambapo uwanja wa ndege wa Chato utakuwa muhimu katika kutoa mawasiliano.

  Mapori hayo ambayo yanasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA sasa yatakuwa chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania - TANAPA punde baada ya mchakato wa kuyapandisha hadhi kukamilika. 

  Bunge limeidhinisha Sh. bilioni 115.794 kwa ajili ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Sh. bilioni 85.816 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. bilioni 29,978 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 
    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza bungeni alipokuwa akijibu hoja wa wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma juzi.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakipongezwa na wabunge mbalimbali baada ya bajeti ya wizara yao kupitishwa na Bunge juzi jioni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa - TANAPA na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali George Waitara (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania - TAWA, Meja  Jenerali (Mstaafu) Hamis Rajabu SEMFUKO wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitishwa na Bunge.
   Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Katibu Mkuu, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki, Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo baada ya bajeti ya wizara yao kupitishwa na Bunge juzi jioni. 

  0 0


  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeutaka uongozi wa Kambi ya Wazee na watu wasiojiweza Nunge kuwakamata wahusika wanaouza viwanja katika eneo la kambi hiyo .

  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu kero za  Wazee wa Nunge alipotembelea kambi hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

  Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisimamisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi wan je na kambi hiyo uliokuwa unaendelea katika eneo hilo ambalo inadaiwa sio muhusika wa eneo la kambi ya wazee ya Nunge na kusema aliyeuziwa katika eneo hilo Serikali haitamtambua. “Marufuku kwa mtu yeyote kuuza,kununua wala kujenga pamoja na kuchimba mchanga katika eneo la kambi hii na mtu atakayebainika anajihusisha na vitendo hivyo basi hatua za sharia zitafuata zidi yake “ alisisitiza Dkt. Ndugulile.

  Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa misaada inayokuja katika kambi hiyo iwe inawekwa kwenye utaratibu maalumu ili kila mmoja aweze kupata mahitaji anayostahili kwa wakati husika na viorodheshwe kwenye daftari la kambi hiyo kama kumbukumbu ili kuondoa changamoto ya kurumbana kuhusu mahitaji kwa wazee hao.

  Mbali na hayo Dkt. ametoa muda wa wiki mbili tatizo la usafiri kwa wazee wa kambi hiyo liwe limeshughukulikiwa kwa kutengeneza bajaji iliyotolewa na Serikali kwa manufaa ya Wazee wa kambi hiyo na si vinginevyo.

  Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha kambi ya wazee Nunge Dkt. Dismas Chihwalo wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hiko amesema kuwa ili uwepo utaratibu mzuri wa kuhudumia walengwa katika kambi hiyo ni lazima kuwepo na makualiano maalumu kwa kutia saini baina ya wanaoletwa kwa mahitaji maalum na viongozi wa kambi hiyo.

  “Serikali inatakiwa kuhakikisha wanaoletwa kwa ajili ya huduma maalum na kwa muda maalum wanatia saini mkataba wa makubaliano ili kuweza kuepusha migogoro ya kutoa huduma katika kambi hiyo kwa wanaostahili” alisema Dkt. Chihwalo.Kambi ya Wazee na wasiojiweza Nunge ilianzishwa mwaka 1936 kwa makusudi ya kuwahudumia Wazee na wasiojiweza pamoja na wenye ukoma ili wasipate shida za mahittaji muhimu na huduma za afya kwa wakati sahihi. 
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua chakula wanachopikiwa wazee wa kambi ya Nunge iliyopo Kigamboni wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja ya binti wa Mhitaji anaeishi katika kambi hiyo ya Nunge iliyopo Wilaya ya Kigamboni, huku lengo la ziara hiyo likiwa kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo.
   Baadhi ya Wazee waliojitokeza katika ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee wa Nunge ili kupata fursa ya kuzungumza na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara kituoni hapo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wake wa jimbo la Kigamboni Wilayani Kigamboni pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa kituo cha kulelea wazee cha Nunge na wazee waliojitokeza kumsikiliza pindi alipofanya ziara kituoni hapo.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja,Nlanla Gumede kutoka Afrika Kusini na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa. 
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja akizungumza kabla ya kukaribisha mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma..Kulia kwake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama Nlanla Gumede kutoka Afrika Kusini na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Uongozi  Prof Joseph Semboja wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.
   Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa Akizungumzia umuhimu wa mkakati wa ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda uliofanyika leo Jijini Dodoma.
   Wadau wa mdahalo wa kitaifa wa kujadili ushirikishwaji wa jamii katika uwekezaji  ndani ya nchi ili kuchangia ajenda ya viwanda  wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akizindua mdahalo huo leo Jijini Dodoma.
  Picha zote na Daudi Manongi,Dodoma.  0 0

  Na Ramadhan Ali - Maelezo
  Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imegundua udanganyifu uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara Ujudi Abass wa kubadilisha utambulisho (brand) wa mafuta ya kula ya TURKEY na kuweka utambulisho wa  OKI kinyume na sheria.
  Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Khamis Ali amesema udanganyifu huo uliokuwa ukifanywa ndani ya Tawi la CCM Makadsara ulibainika baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
  Alisema utambulisho wa OKI uliokuwa ukitumiwa  kinyume na sheria na mfanyabiashara huyo ulikuwa wa kughushi na lengo lake kubwa ni kutafuta soka na bei ya juu katika masoko ya Dar e salaam ambako  hivi sasa kunaupungufu wa mafuta hayo.
  Dkt. Khamis alisema kuwa mafuta hayo, zaidi ya galoni 747, yanatoka nchini Indonesia na yalizalishwa mwezi Mei mwaka 2017 na muda  wa mwisho wa matimizi ni mwezi Mei mwaka 2019 hivyo yapo salama kwa ajili ya matumizi na kosa la mfanyabiashara huyo ni kubadilisha utambulisho halali wa TURKEY na kuweka utambulisho wa Kampuni nyengine
  Alisema mfanyabiashara Ujudi Abss hivi sasa anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na  anatarajiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria wakati wowote kujibu tuhuma za udanganyifu.
  Mwakilishi wa Kampuni ya Sahara ambao ni wakala wa OKI ameeleza kusikitishwa na kitendo cha  udanganyifu wa  uliofanywa na mfanyabiashara huyo kutumia stika za kampuni hiyo kwa lengo la kutafuta kipato kwa vile mafuta ya OKI ni maarufu na yanasoko.
  Alisema kitendo cha kutumia stika ya kampuni kwa biashara nyengine kwa njia  udanganyifu kinaweza kushusha hadhi ya biashara ya halisi na  kupoteza imani kwa watumiaji. 
   KAIMU Mkurugenzi Huduma za  Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Abdulaziz Shaib Moh’d akibandua stika ya kughushi ya OKI iliyowekwa kwenye mageleni ya mafuta ya kula ya kampuni ya TURKEY  katika eneo la Shaurimoyo Mjini Zanzibar.
   BAADHI ya madumu ya  mafuata ya kula kutoka Indonesia yenye stika ya  TURKEY yakiwa  yamepandishiwa  stika ya OKI  kwa njia za udanganyifu bila ya idhini ya wamiliki wa kampuni hiyo.
   VIFAA vilivyotumika kubadilishia Stika za mafuta ya TURKEY kutoka Indonesia na kuwekwa stika ya OKI juu kwa njia za udanganyifu bila ya idhini ya wamiliki wa kampuni hiyo.
   MADUMU ya mafuta ya kula yakiwa  yameshabadiliswa stika ya asili ya TURKEY na kuwekwa ya OKI yakisubiri kuingizwa Sokoni.
    KAIMU Mkurugenzi  Mtendaji Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar akionyesha stika zilizotumika kufanyia udanganyifu  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Makadara Mjini Zanzibar.
  MWAKILISHI wa Kampuni ya Sahara ambao ni Wakala wa Mafuta ya OKI Salum Moh’d akizungumza na Waandishi wa Habari jinsi ya kampuni hiyo ilivyosikitishwa na udanganyifu wa kutumika stika ya kampuni hiyo bila idhini yao.
  Na Abdalla Omar / Maelezo Zanzibar

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa maagizo kwa Mkandarasi SUMA JKT baada ya kukagua ujenzi wa madarasa manne LEO yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akikagua ujenzi wa sakafu wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hombolo leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne katika shule hiyo. 
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Hombolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Suma JKT kuhakikisha madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo Jijini Dodoma yanawekewa madawati kwa gharama ya shilingi milioni 20 .

  Ameyasema hayo wakati alipokagua shule hiyo leo kuona maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne yaliyojengwa kwa kutumia “FORCE ACCOUNT “ambapo alibaini uduni mkubwa katika ujenzi wa madarasa hayo.

  Mhe. Jafo amesema inashangaza kuona maeneo mengine wametumia fedha zilizotolewa na Serikali kujenga madarasa pamoja na kuweka madarasa tofauti na Jiji la Dodoma hivyo ameagiza kuhakikisha wanatumia fedha zilizobaki milioni 20 kwa ajili ya kuweka madawati.“Naagiza, uongozi wa Jiji la Dodoma na SUMA JKT kuhakikisha madarasa yote manne yaliyojengwa kwa fedha za Serikali yamewekwa madawati kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na kuwa na mazingira mazuri ya kuapata elimu.” Anasema jafo

  Mhe. Jafo amefafanua kuwa SUMA JKT wameenda kinyume na matakwa ya Serikali ya kujenga madarasa na kuweka maruru kitendo ambacho kinarudisha nyuma uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kurudisha maendeleo katika jiji la Dodoma.Mhe. Jafo amesema kuwa amekerwa na uhafifu wa zege lililotumika katika ujenzi wa sakafu ya madarasa hayo ambapo mpaka sasa yameanza kuvunjika kabla ya kutumika.Aidha amewataka kurekebisha sakafu hiyo mapema.

  “Ninawaagisa kuvunja sakafu ya madarasa na kujenga nyingine, na msinipe mashaka na kuanza kukagua ubora wa majengo yaliyojengwa na kukuta yako chini ya kiwango, nataka madarasa ambayo sakafu yake ni imara na ya kudumu” amesema Jafo.Akifafanua kuhusu matatizo ya maji Mhe. Jafo amesema Serikali imejipanga kutatua kero ya maji nchini na itachimba kisima kitakachotoa maji kwa shule hiyo.

  Aidha amewaka wanafuzi hao kunzingatia masomo kwa kusoma kwa bidii na kuwa na kampeni maalum ya kuondoa ziro ili kuondokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne na cha Sita.

older | 1 | .... | 1586 | 1587 | (Page 1588) | 1589 | 1590 | .... | 1897 | newer