Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

WALEMAVU KISARAWE KUPATIWA BIMA YA CHF ILIYOBORESHWA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kisarawe.
baadhi ya watu wenye ulemavu waliokabidhiwa vifaa wezeshi.
Baskeli za watu wenye ulemavu walizokabidhiwa.
Baadhi ya wananchi wa Kisarawe walio hudhuria mkutano wa ugawaji wa vifaa wezeshi vya walemavu.


Wilaya ya Kisarawe huenda ikawa wilaya ya mfano hapa nchini kwa wananchi wake wote wenye ulemavu kupatiwa bima ya afya iliyoboreshwa. 

Neema hiyo kwa walemavu imetokea leo wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu vilivyo tolewa na shirikisho la watu wenye ulemavu nchini(SHIVYAWATA).

Katika hafla hiyo ya ugawaji vifaa saidizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ambaye pia ni mbunge wa wilaya hiyo ya Kisarawe ametangaza neema hiyo kwa walemavu hao kwa kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe kufanya utaratibu wa kupata Sh.milioni 6 kutoka mapato ya ndani ili kuwalipia CHF iliyo boreshwa kwa vikundi 207 vya walemavu.

Amesema lengo ni walemavu wote wa wilaya hiyo wawe na uhakika wa kupata huduma ya afya ambapo kwasasa wilaya ya Kisarawe ina jumla ya watu wenye ulemavu wapatao 1608. Waziri Jafo ametoa msisitizo kwamba kwa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe haiwezi kushindwa kupata sh.milioni 6 ili kuwalipia walemavu.

Baada ya maelekezo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mussa Gama amethibitisha Waziri Jafo kuwa watahakikisha wanatekeleza agizo hilo kabla mwezi Juni 2018. Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Ndikilo amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Zuberi Samataba awaandikie wawekezaji wote wa viwanda wa mkoa wa Pwani waone namna watakavyoweza kuchangia vifaa saidizi cha walemavu ili walemavu wengine waliobaki waweze kusaidiwa vifaa hivyo wezeshi. 

Naye, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Happiness Seneda ameitaka jamii kushirikiana ili kuwasaidia watu wenye ulemavu wilayani Kisarawe.

UBA Restates Commitment to Growing Infrastructure, Deepens Financial Inclusion in Tanzania

0
0
UBA Tanzania, a subsidiary of the UBA Group, a pan African financial institution with presence in 20 African countries, Monday restated its commitment to support the Tanzanian government’s initiative to grow the country’s infrastructure, while also affirming the bank’s obligation to deepen the retail banking space in the country.
The assurance was given during a press conference addressed by the Bank’s Chief Operating Officer, Chris Byaruhanga in Dar Es Salaam, noting that as a member of UBA Group with asset of over $13 billion, the Tanzanian franchise has the capacity to finance any project irrespective of amount or size. “UBA Tanzania, relying on the strength of our group has capacity to finance any transactions irrespective of its size in either private or public sector. As a pan African with presence in key international markets of the world, we are positioned to provide the necessesary financial intermediation critical to the development of Tanzania,” says Byaruhanga.
Byaruhanga further informed the journalists of the key projects that have been financed by the Bank in Tanzania in recent times, including the provision of over $25 million facility for the construction of Kigogo Road in Dar Es Salaam and TZS15BN/- support Tanzania Electricity Supply Company (TANESCO), among other interventions. “Apart from these involvements, UBA Tanzania, a bank with strong retail base has come up with many innovations, especially in digital space to provide financial solutions to the needs of the banking consumers in this market,” the COO said while explaining the Bank’s strategy, claiming further that UBA Tanzania prioritises businesses whether they are small and medium scale enterprises (SMEs) or large corporates.
Speaking on the roles being played by UBA Group in the support of the economic development of the African continent, Nasir Ramon, Head, External Relations of UBA Plc, said UBA Group has continuously played big in the continent’s financial sector, saying that the UBA has committed over $5 billion into various projects on the continent in recent times.
United Bank for Africa is one of Africa’s leading financial institutions, with operations in 20 countries and 3 global financial centers: London, Paris and New York. From a single country operation in Nigeria, Africa’s largest economy, UBA has evolved into a pan-African provider of banking and related financial services through diverse channels globally.
UBA Tanzania is a subsidiary of UBA Plc and licensed by the Bank of Tanzania.  The Bank has been in Tanzania since 2009 and has continued to play a critical role in the Tanzania banking industry. UBA Tanzania offers a full range of banking products catering for large local corporates, public sector clients and multinational corporations that include trade finance lines, working capital facilities, collection solutions and robust payment platforms.

WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA

0
0
Na Rachel Mkundai, Morogoro

Jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 17,601 waliokuwa katika sekta isiyo rasmi mkoani Morogoro wametambuliwa na hivyo watapatiwa vitambulisho maalumu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu zoezi la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho maalumu wafanyabiashara wadogo wadogo walio katika sekta isiyo rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Masika mjini Morogoro.

Mwandumbya amesema zoezi la utambuzi linafanyika kwa kupitia vikundi vya wafanyabiashara ambapo katika mkoa wa Morogoro vikundi 1851 vyenye jumla ya wanachama 17,601 wametambuliwa na watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye jina na mahali wanapofanyia biashara zao ambavyo watadumu nabyo kwa miaka mitatu.

Ameongeza kuwa kati ya hivyo 1,851, vikundi 473 vimeshapatiwa mafunzo ya umuhimu wa kutambuliwa, kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya TRA, na kati ya hivyo vikundi 143 vyenye jumla ya wanachama 2,324 wameshasajiliwa ili waweze kufanya biashara zao bila usumbufu.“Lengo ni kuhakikisha kuwa tunawatambua wafanyabiashara wadogo wadogo kwa idadi yao kwa ajili ya serikali kupanga mipango mizuri ya kuboresha biashara zao ziweze kuendelea na vile vile serikali iweze kuweka mipango mizuri ya kuwapatia huduma mbalimbali”, alisema Bw. Mwandumbya.

Akizindua zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe, amesema ulipaji wa kodi ni jambo zuri sana na mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa inayofaidi matunda ya ulipaji kodi kwa kuwa na stendi nzuri ya kisasa ya mabasi ya abiria, stendi ya Msamvu.“Nitoe rai kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kutumia fursa hii ya kujisajili na kupatiwa vitambulisho vya TRA ili mkoa uweze kuwapatia huduma muhimu kama vile maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo ndani ya stendi ya Msamvu”, ametoa rai.
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakishangilia kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa vitambulisho maalum vinavyorasimisha rasmi shughuli zao za biashara mkoani hapo wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (Imeandaliwa Robert Okanda Blogs)

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Masika mkoani hapo wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa usajili na utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao zoezi ambalo linafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali uliofanyika 21 Mei, 2018 mkoani hapo.
(Juu na chini) Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi pamoja na viongozi wa ngazi ya juu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao 21 Mei, 2018 mkoani hapo.

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo.

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo.

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo.
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (PICHA ZOTE NA TRA)

WABUNGE WA CUF WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI

0
0

*Wasifu kasi yake na Waziri Mkuu ya uletaji maendeleo 
*Wasema maendeleo ya Kusini kwanza, vyama baadaye

WABUNGE watatu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) mikoa ya Lindi na Mtwara wamepongeza kasi ya utendaji kazi ya Rais John Pombe Magufuli katika kutatua kero za wananchi wa mikoa hiyo.

Wabunge hao Bw. Selemani Said Bungara (Kilwa Kusini), Bw. Zuberi Mohammed Kuchauka (Liwale) na Bw. Maftaha Abdallah Nachuma (Mtwara Mjini) walitoa pongezi hizo jana, (Jumatatu, Mei 21, 2018) wakati walipopewa nafasi ya kusalimia wananchi kwenye mikutano ya hadhara ambayo Waziri Mkuu alihutubia.

Akiwa wilayani Lindi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kituo cha kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa katika kijiji cha Mahumbika, aliwapa fursa wabunge wote alioambatana nao katika ziara hiyo maalum kwa ajili ya uzinduzi wa miundombinu ya nishati kwa mikoa ya Kusini.

Akizungumza na wananchi na viongozi wa taasisi mbalimbali mkoani humo waliohudhuria uzinduzi huo, Mbunge wa Kilwa Kusini, Bw. Bungara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Lindi alisema analishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuisimamia vizuri Serikali ya CCM. 

“Faida ya demokrasia ya vyama vingi ni kwamba CCM bila CUF, CCM hakuna na CUF bila CCM, kama ambavyo hakuna Simba bila Yanga wala hakuna Yanga bila Simba. Tuwe kitu kimoja tu, Kusini kwanza, vyama baadaye!” alisisitiza.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa juhudi zake za kuwaunganisha wabunge wa mikoa ya Kusini bila kuwabagua au kujali itikadi zao.

Naye Mbunge wa Liwale, Bw. Kuchauka alisema: “Niwapongeze wewe Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa yale ambayo mnayasimamia na mnaamini kwamba yataleta ukombozi kwa wananchi wa Tanzania. Lazima nikiri kwamba wakati mnazindua sera ya uchumi wa viwanda, nilikuwa siamini katika hiyo sera yenu kwa sababu niliona ni moja ya mbinu zenu za kututenga sisi watu wa mikoa ya Kusini.”

“Niliona hivyo kwa sababu nilijiuliza unawezaje kuwa na uchumi wa viwanda wakati huna nishati ya uhakika ya umeme? Sasa nimeona mwanga kwamba mikoa ya Kusini nayo inaweza kushiriki kwenye uchumi wa viwanda,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema hivi sasa hakuna asiyeona mambo yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwani dunia yote imekuwa kama kijiji na lolote linalofanywa na Mhe. Rais au Waziri Mkuu hakuna asiyejua. “Lolote analolifanya Mheshimiwa Rais au wewe Waziri Mkuu Watanzania wote watalijua, hakuna asiyeliona. Hivi sasa hakuna haja ya kubishana nani kafanya nini, jambo kubwa ni kuungana na tuangalie Tanzania yetu. Vyama vyote baadaye, Kusini kwanza,” alisisitiza. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Bw. Maftaha alisema mwaka 2006 baada ya kuhitimu kidato cha sita, alipangiwa afanye mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya sekondari Mingoyo, eneo la Mnazi Mmoja lakini alitafuta nyumba ya kuishi yenye umeme hakupata.

“Wakati ule nyumba zenye umeme zilikuwa hazizidi hata 10, na kulikuwa na simba na wadudu wa kila aina. Leo nafarijika kuona kwa kasi ya ajabu, ninyi viongozi tuliowapa dhamana, mnatumia rasilmali za nchi hii, mnasambaza umeme kwa wananchi wa mikoa ya Kusini, na pale Mnazi Mmoja leo hii, umeme siyo tatizo tena.” 

Wabunge wengine waliofuatana na Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bibi Hawa Ghasia; Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Bi. Hamida Mohammed Abdallah (Viti Maalum). Mbunge wa Nachingwea, Bw. Hassan Elias Masala, Mbunge wa Nanyamba, Bw. Abdallah Dadi Chikota.

Waziri Mkuu alizuru pia mkoa wa Mtwara na kukagua ujenzi wa bandari, ukarabati wa mabomba ya kupokelea mafuta, matenki ya kuhifadhi mafuta, kuzindua upanuzi wa kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa bandari.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 22, 2018.

TPB Plc YAWATOA HUFU WATEJA WOTE WALIOKUWA BENKI YA TWIGA BANCORP

0
0
OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi amewatoa hofu wateja wote waliokuwa kwenye Benki ya Twiga Bancorp huku akiwahakikishia kuwa wapo katika mikono salama na wataendelea kupata huduma kama hapo awali. 

Moshingi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana jioni baada ya kuandaa hafla fupi ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuwakaribisha wateja na wafanyakazi waliokuwa kwenye benki ya Twiga Bancorp. Amekumbusha kuwa benki ya TPB na Twiga Bancorp zimeunganishwa Mei 17 mwaka huu baada ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kutoa tamko rasmi. 

"Hakuna kilichobadilika, huduma zitabaki pale pale, wateja wote mtaendelea kuhudumiwa katika matawi ya iliyokuwa benki ya Twiga Bancorp mpaka kipindi cha mpito kikimalizika."Kipindi cha mpito tulichopewa na BoT ni miezi mitatu, ambayo itatupa nafasi kuweka mitandao ya benki hizi pamoja na kurahisisha katika kutoa huduma za kibenki,"amesema Moshingi. 

Kwa upande wake aliyekuwa Meneja Msimamizi wa iliyokuwa Benki ya Twiga Bancorp, Nkanwa Magina kutoka Benki Kuu ya Tanzania, amewataka wateja waliokuwa Benki ya Twiga Bancorp kutokuwa na wasiwasi, kwa kuwa kuunganishwa kwa benki hizo mbili kumeongeza nguvu katika utendaji wa kutoa huduma za kibenki. Pia amesema wafanyakazi waliokuwa katika benki ya Twiga Bancorp, waendelee na moyo ule ule waliotoka nao kwenye benki yao na kuonesha ushirikiano wa dhati wa wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya TPB.

Wakati huo huo waliokuwa wateja wa benki ya Twiga Bancorp, wametoa shukrani zao kwa uamuzi uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuunganisha benki hizo mbili, kwani ni faraja kwao na kusisitiza watapata huduma kwa ufanisi zaidi. "Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Serikali ya Awamu ya tano kwa uamuzi huu waliouchukuwa wakuunganisha benki hizi mbili kwani umetuondolea wasiwasi sisi tuliokuwa wateja wa Twiga Bancorp,"amesema mteja aliyefahamika kwa jina la Janet Mmari. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi akizungumza na wafanyakazi waliokuwa Twiga Bancorp pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati anawakaribisha rasmi kutokana na Benki Kuu ya Tanzania(BoT),kuziunganisha benki hizo.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Windhoek Tanzania Simon Salatiel ambaye ni moja ya wateja wa iliyokuwa benki ya Twiga Bancorp akitoa shukrani zake jijini Dar es Salaam baada ya benki hiyo kuunganishwa na benki ya TPB Plc.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Windhoek Tanzania Simon Salatiel ambaye ni moja ya wateja wa iliyokuwa benki ya Twiga Bancorp akitoa shukrani zake jijini Dar es Salaam baada ya benki hiyo kuunganishwa na benki ya TPB Plc.
Moja ya wateja wakubwa wa Benki ya Twiga Bancorp (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya TPB Plc jijini Dar es Saalaam baada ya kufanyika hafla iliyoandaliwa na benki ya TPB kuwakarabisha wateja na wafanyakazi wa Twiga kutokana na uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)kuziunganisha benki hizo.Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi.

ULEGA AFUNGUA MSIKITI, AZUNGUMZIA UMEME KUANZA KUSAMBAZWA VITONGOJI VYA MKURANGA

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua msikiti kwa kisasa  ujulikanao kama Maajid Habresh katika kijiji cha Tengelea huko Mkuranga.

Uzinduzi huu umefanyika leo ambapo ulienda sambamba na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika jimbo lake na kusikiliza maoni na kujibu maswali kutoka kwa wananchi.

Ulega amesema ni jukumu lao kusimamia maendeleo ya wananchi hasa katika elimu na amehaidi kusaidia katika kujenga madarasa na hawatachoka kumuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na wananchi kwa ujumla.Aidha ameeleza wananchi wa kijiji cha Kazole wajiandae kupata huduma ya umeme ikiwa na mkakati wa kuwapa huduma bora.

Katika ziara hiyo Ulega ametoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Kazole, na ametoa kiasi cha shilingi laki tatu kwa kikundi cha wajasiriamali kwa wanawake cha Thirty family vicoba  sambamba na kuwasalimu wananchi wa Mkuranga na kuwaomba wananchi wasizuie miradi ya maendeleo na kuitunza miradi hiyo.
 Muonekano wa msikiti aliuzindua Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdullah  uliopo katika kijiji cha  Tengelea Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. (Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah ulega akikabidhi mifuko ya saruji mia moja kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kazole.
 Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akishiriki shughuli ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Kazole  ambapo akimkabidhi mifuko mia moja ya Saruji.
 Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akigawa tende kwa waumini wa Msikiti huo  mara baada uliopo k katika kijiji cha Tengelea mkoa wa Pwani.
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi na mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na waumini wa msikiti wa Habresh mara baada ya kuzindua msikiti huo uliopo katika kijiji cha Tengelea mkoa wa Pwani.

BANK OF AFRICA ORGANISES AN IFTAR DINNER FOR CUSTOMERS IN DAR ES SALAAM

0
0
The Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Wasia Mushi delivers his welcoming remarks at the bank’s IFTAR Dinner at the Serena Hotel in Dar es salaam.The Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Wasia Mushi in a jovial moment as he welcomes some of the esteemed clients of the bank who attended the bank’s IFTAR Dinner at the Serena Hotel on 18th May 2018.The CEO and Managing Director of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Mr. Ammish OWUSU-AMOAH, deliver his speech during the bank’s IFTAR Dinner at Serena Hotel. The event brought together the CEO of the GROUP BANK OF AFRICA, Mr. Amine BOUABID, senior officials from BANK OF AFRICA GROUP, representatives from BOA KENYA, BOA UGANDA, BOA RWANDA and BOA GHANA, leaders from the Muslim fraternity and clients of bank.The Board Chairperson of BANK OF AFRICA- TANZANIA, Ambassador Mwanaidi .S. Maajar deliver his speech during the bank’s IFTAR Dinner at Serena Hotel. The event brought together the CEO of the GROUP BANK OF AFRICA, Mr. Amine BOUABID, senior officials from BANK OF AFRICA GROUP, representatives from BOA KENYA, BOA UGANDA, BOA RWANDA and BOA GHANA, leaders from the Muslim fraternity and clients of bank.Staff of BANK OF AFRICA and clients saving themselves with different assortments of food at the at the bank’s IFTAR Dinner at Serena Hotel, Friday 18th May 2018. Staff of BANK OF AFRICA and clients saving themselves with different assortments of food at the at the bank’s IFTAR Dinner at Serena Hotel, Friday 18th May 2018.

WABUNGE WA MIKOA YA KUSINI WAIMWAGIA SIFA SERIKALI NA TANESCO KWA KUMALIZA KERO YA UMEME MTWARA NA LINDI

0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, (wane kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi, na Mkuriugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, wakati alipowasili kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018. Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akitoka eneo la mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme wa Megawati 4 kila mmoja baada ya kuizindua, kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi Mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Wabunge wa Mikoa ya Kusini, wakiwa na mwenyekiti wao, Mhe. Selemani Bungara(wapili kushoto) 



WABUNGE wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wameimwagia sifa Serikali hususan Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme TANESCO kufuatia kumaliza adha ya umeme iliyodumu kwa takriban miaka 10 kwenye mikoa hiyo.

Pongezi hizo wamezitoa mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, baada ya kuzindua Kituo cha Kuzalisha umeme wa gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018.

Wa kwanza kutoa pongezi hizo alikuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia chama cha Wananchi CUF, Mhe Maftah Nachuma ambaye yeye alienda mbali zaidi na kufikia kusema atamuandalia Mhe. Waziri Mkuu mkutano mkubwa wa hadhara ili kuwaeleza wananchi wa jimbo lake, mafanikio yaliyoletwa na serikali.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, leo ninayofuraha kubwa sana, kwani kilio cha muda mrefu cha wana Mtwara, cha kukosa umeme wa uhakika, hatimaye kimepatiwa ufumbuzi na kwetu sisi hii ni sherehe kubwa, ningetamani mkutano huu ungewaalika na viongozi wengine wa vyama vya siasa, na mimi binafsi nitakuandalia mkutano mkubwa wa hadhara ili uje uwaeleze wananchi maendeleo haya yaliyoletwa na serikali.” Alisema Mhe. Nachuma.

Naye Mwenyekiti wa wabunge kutoka Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, alisema maendeleo haya ambayo serikali inawafikishia wananchi ni kwa sababu bunge linaisimamia vema serikali.“Siku zote tunasema Kusini kwanza mambo mengine baadaye, na mimi niwaambie, tutaendelea kupiga kelele hadi kero zote zitatuliwe, na niishukuru serikali kwa kumaliza hii kero ya umeme iliyudumu kwa muda mrefu.” Alisema Mhe. Bungara

Naye Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia, yeye pia aliipongeza serikali kwa kumaliza kero ya umeme Mkoani Mtwara, kwani sasa Mkoa wa Mtwara umekamilika kwa kila eneo katika Nyanja ya uwekezaji.

“Mikoa yetu ya Kusini tuna kila kitu, Gesi iko hapa, Bandari tunayo, Ardhi ambayo wala haihitaji fidia nayo ipo, na sasa tunao umeme wa uhakika unaopatikana masaa 24, hii ni fursa nzuri kwetu sisi tunaotoka mikoa ya Kusini.” Alisema Mhe. Hawa Ghasia.

Akitoa taarifa fupi ya kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema. Kituo cha kufua umeme kwa Gesi Asilia cha Mtwara kilianza rasmi kufanya kazi mwaka 2007, kwa sasa kituo hiki kinazaidi ya miaka kumi(10) na kina uwezo wa kuzalisha Megawati 18 za umeme na ndio chanzo pekee cha Nishati ya umeme kwa eneo lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara, isipokuwa kwa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kilwa na Liwale ambayo yanapata umeme kutoka kwenye vituo vyao vidogo.

“Mahitaji ya juu ya Nishati ya Umeme kwa eneo lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara ni takribani Megawati 16.5” Alisema Dkt. Mwinuka.

Alisema, Katika kukabiliana na changamoto ya kukua kwa mahitaji ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, serikali kupitia TANESCO ilifanya maamuzi ya upanuzi wa kituo hiki cha kuzalisha umeme ili kukiongezea uwezo wake. Hatua hii inahusisha usimikaji wa Mitambo miwili ya kufua umeme kila mmoja ukiwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2, na hivyo kufanya ongezeko la jumla la Megawati nne (4)

Hatua hii itaongeza uwezo wa kituo kuwa ni Megawati ishirini na mbili (22) ambao utatosheleza mahitaji ya sasa ya eneo hili na kuwa na ziada.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema, Hatua hii ni ya awali katika mpango endelevu unaolenga katika kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kiasi cha Megawati nyingine nne (4) zitafuatia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019, pia upo mpango mkubwa wa ujenzi wa mtambo wa Megawati 300 kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Japani JICA, unaotarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2020.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, aliwapa changamoto wakazi wa Mkoa wa Mtwara kutumia umeme huo kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwani sasa umeme ni bora na wa uhakika.

“Nitoe wito kwa vijana, sasa mnaweza kufanya shughuli za kunyoa(saloon), kuchomelea vyuma, kuranda mbao, kuuza juice, na hata wengine kuchaji simu na kuweka miziki kwenye simu kwa kutumia computer, mnayo fursa kubwa ya kufanya shughuli zenu ndogo ndogo za kiuchumi kupitia umeme huu ambao sasa unawaka masaa 24.” Alisema.

Waziri Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, kwa kuchangamkia haraka uwepo wa umeme wa kutosha kwa kuanza kuweka taa za barabarani na hivyo kuufanya mji wa Mtwara kung’aa majira ya usiku.
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe.Maftah Nachuma, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake.
Waziri Mkuu akipitia hotuba yake kabla ya kuhutubia.
Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Gesi Mkoani Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji ya Kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (katikati), Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (kulia) na viongozi wengine wa Mkoa wa Mtwara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi na viongozi wa juu wa Wizara ya Nishati na Shirika hilo, wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi cha Mtwara Mei 21, 2018.
Wananchi wakishangilia
Mama akiwa ma mwanaye huku akifurahi 
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughulikia uzalishaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia) na Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba.
Dkt. Kalemani akimnong'oneza kitu Meneja wa Kanda ya Kusini wa TANESCO, Mhandisi Aziz Salum.
Wafanyakazi wa TANESCO Mtwara
Waziri Mkuu Majaliwa na viongozi wengine wakifurahia burudani ya kwaya
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, wakiwa wenye furaha wakati vikundi vya burudani vikitoa burudani
Picha ya pamoja

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AMTEMBELEA MWANARIADHA ANAYEHESHIMIKA DUNIANI MZEE JOHN STEVEN AKHWARI NYUMBANI KWAKE MBULU MKOANI MANYARA

0
0



Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sani mjini Mbulu mkoani Manyara jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Mexco City mwaka 1968

John Steven Akwari aliyekuwa wa mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008 katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye, Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya 75 walioanza.

Mshindi wa mashindano hayo Mamo Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya saa moja baadaye yaani alitumia saa 3:25:27 kukiwa na watazamaji wachache uwanjani na jua lilikwisha kuzama. Awali wakati anaanza mbio hizo, Akwari alianguka na kupata majeraha kwenye goti ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa ya Amerika ya kati kuwa tofauti na nyumbani. Wanariadha wenzake walimpita moja baada ya mwingine na hivyo kukatiza ndoto yake ya kuiletea Tanzania medali ya kwanza kabisa ya Olimpiki, lakini hakukata tamaa bali alinuia kumaliza hayo mashindano.

Akiwa amefungwa bandeji mguuni huku akitokwa na damu, Akhwari alitokeza uwanjani saa moja baada ya mshindi kutangazwa, na kukiwa na watazamaji wachache na waandishi wa habari na giza likianza kuingia, uwanja ulizizima kuona Akhwari anachechemea akiwa na maumivu kuelekea mstari wa kumaliza mbio, wengi waliguswa baada ya kushuhudia tukio hilo. Alipoulizwa na waandishi kwa nini aliendelea na mashindano baada ya kuumia, aliwajibu kwa utulivu jibu rahisi ``Nchi yangu haikunituma maili zaidi ya 5000 kuanza mbio, bali kuzimaliza``
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akisalimiana na MZee John Steven Akhwari wakati alipoongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyemtembelea mzee huyo nyumbani kwake eneo la Sani mjini Mbulu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza jambo na Mzee John Steven Akhwari.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mee John Steven Akhwari alipokuwa aktoa maelezo kwake kuhusu mbambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya katika masuala ya mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakiangalia tuzo mbalimbali ambazo Mzee John Steven Akhwari kulia aliwahi kutumikiwa. 
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakionyeshwa mwenge wa Olimpiki ambao Mzee John Steven Akhwari kulia kutumikiwa jijini Beijing China baada ya kuukimbiza akiwa Balozi wa Mashindano hayo mwaka 2008. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa moja ya tuzo ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa nchini Uswisi .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyesswa Nisahani ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi 
Hapa wakionyeshwa vyeti mbalimbali ambavyo Mzee John Steven Akhwari aliwahi kutunikiwa kutambua mchango wake katika mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee John Steven Akhwari mara baada ya mazungumza yao.

FUATILIA MAJUMUISHO YA BAJETI 2018/2019: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

0
0

DAWA ZAVUSHWA KUPITIA MTO WENYE MAMBA MKOANI RUVUMA

0
0

Wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na wafanyakazi wa Bobari ya Dawa (MSD), wakisaidia kushusha maboksi yenye dawa na kuyaingiza kwenye mtumbwi baada ya kupelekewa na MSD Kanda ya Iringa leo na baadae kuyapeleka katika Zahanati ya Kijiji cha Mitomoni.
Maboksi ya dawa yakiingizwa kwenye mtumbwi.
Wakazi wa Kijiji cha Mitomoni wakisubiri mtumbwi ili kuwavusha upande wa pili wa mto Ruvuma.
Dawa zikipelekwa Zahanati ya Mitomoni
Maboksi ya dawa kutoka MSD yakishushwa
Wananchi wakishusha maboksi hayo kutoka katika mtumbwi.
Mkazi wa Kijiji cha Mitomoni Khadija Salum, akizungumzia upatikanaji wa dawa kutoka MSD.
Mkazi wa kijiji hicho, Mbwana Koloma, akizungumzia changamoto ya miundombinu ya barabara na jinsi wanavyopokea dawa kutoka MSD.
Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa Kijiji cha Mitomoni Omar Hassan akizungumza wakati wa kupokea dawa hizo.
Mmoja wa viongozi wa Kijiji cha Nakawale, Ima Komba akisaini fomu maalumu ya kupokelea dawa kutoka MSD.






Na Dotto Mwaibale, Ruvuma

WANANCHI wanaoishi katika Vijiji vya Mkenda na Mitomoni vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamesema changamoto kubwa waliyonayo ni mazingira magumu ya miundo mbinu ambayo inasababisha ugumu wa ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

Wakazi hao wamesema kuwa, mazingira ya kufikisha dawa kwenye vijiji hivyo hutegemea zaidi usafiri wa kuvuka mto Ruvuma ambapo hulazimika kutumia boti,ambapo hata hivyo maisha yao yanakuwa na mashaka ndani ya mtumbwi hiyo ambayo iko wazi kutokana na mto huo kuwa na mamba wengi.

"Changamoto yetu kubwa ni usafishaji wa dawa kuja hapa kijijini kutokana na kutegemea zaidi mto huu ambao una mamba wengi, hata mwaka huu mwanzoni mtumbwi huu mnaouona ulipinduka na watu wakiwapo wauza mitumba waliuawa na mamba; lakini tunashukuru Bohari ya Dawa (MSD) kwani wao wanaweza kutuletea dawa kwa wakati" alisema Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa kijiji cha Mitomoni Omar Hassan.

Alisema ili kuondoa changamoto hiyo, wanaiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara, ili dawa hizo zisafirishwe kwa njia ya barabara badala ya kutegemea mto huo. Alisema yeye na kamati yake wamekuwa wakipokea dawa mara nne kwa mwaka kutoka MSD na kuzihakiki kwa ajili ya matumizi.

"Pamoja na changamoto ya miundombinu lakini tumekuwa tukihakikisha dawa zinazoletwa na MSD zinafika kituoni na kutumika ipasavyo,"alisema.Alisema kutoka Songea mjini hadi Kijiji cha Mitomoni, Songea vijijini, katika kituo hicho cha afya ni km 135 na MSD imekuwa ikihakikisha dawa hizo zinafika.

Alisema changamoto zinakuwa kubwa zaidi kipindi cha mvua kwa kuwa miundombinu ya barabara hadi kufika kivukoni ni tatizo na kuna wakati dawa zinafika usiku na zinatakiwa kuvushwa usiku huo huo.Hassan alisema changamoto hiyo ya mamba katika mto huo anaijua vizuri kwani mtoto wake Sanifu Omar (27), alipoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakati alipokuwa akisafirisha abiria kwa kutumia mtumbwi.

Mkazi wa Kijiji cha Mitomoni Khadija Salum alisema wamekuwa wakipata dawa zote muhimu katika kituoni hicho ikiwemo za mama mjamzito na mtoto bila ya ubaguzi na kwa wakati."Mimi nina watoto watano kuanzia ujauzito wa kwanza sijawahi kukosa dawa hapa pamoja na ugumu wa miundombinu lakini dawa zinafika hivyo serikali ione haja ya kuboresha barabara zetu," alisema.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mitomoni, Ivo Hekela, alisema kijiji hicho kinahudumia agonjwa 12,000 kutoka vijiji vitano ambavyo ni Mitomoni, Mipotopoto,Konganywita,Mkenda,Uhuru na Mozambique. Meneja wa MSD Kanda ya Iringa, John Sipendi, alisema wamekuwa katika changamoto ya kufikia vituo hivyo vya pembezoni ikiwa ni pamoja na kutumia muda mrefu kufikisha dawa na wakati wa mvua kukwama kwa magari njiani na gharama za usafirishaji kuogezeka.

Madereva wa MSD Kanda ya Iringa wamesema wamekuwa wakishindwa kushusha dawa wakati wa mvua za masika kutokana na mto huo kujaa maji hivyo hulazimika kulala kijijini hapo kwa siku mbili hadi tatu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KUENDELEZA UHUSIANO NA MSHIKAMANO WAKE KWA VYAMA RAFIKI

0
0
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akimkabidhi Rais wa Chama Cha Ukumbozi wa Afrika Kusini (ANC) Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa barua maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg, jana. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu Mkuu wa ANC Ace Magashule Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Rais wa ANC Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa ANC Gwede Mantashe, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa ANC, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Katika ziara hiyo ambao Kinana ameambatana na Wenyeviti wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi, ikiwa na lengo la kuendeleza uhusiano na mshikamano uliopo baina ya Vyama hivyo.

Mtanzania Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Mazingira

0
0
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Bi.Joyce Msuya kutoka Tanzania kuwa naibu katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia program ya mazingira yenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa mataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 22 Mei, Bi Msuya anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw.Ibrahim Thiaw wa Mauritania aliyemaliza muda wake ambaye katibu Mkuu wa umoja wa mataifa amemuelezea kuwa na utumishi uliotukuka katika kipindi chake cha uongozi.

Bi.Joyce Msuya amekua akifanya kazi kama mshauri wa makamu wa rais wa benki ya dunia anayeshughulikia nchi za Asia Mashariki pamoja na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2017, makao makuu ya benki ya Dunia Washington D.C Marekani.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Msuya atatumia muzoefu wake wa miaka 20 katika benki ya Dunia, pamoja na uzoefu wake katika masuala ya maendeleo ya kimataifa katika kazi yake mpya na anaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa katika umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bi.Msuya amewahi kufanya kazi kama mwakilishi maalum wa benki ya Dunia na mkuu wa kundi la benki ya dunia nchini Korea ya kusini,pamoja na mratibu wa taasisi ya benki ya dunia katika Asia Mashariki na ukanda wa Pasifiki ofisi iliyoko China, na ameahi kuwa na nafasi mbalimbali za juu katika benki ya dunia na washirika wake.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa Bi.Joyce Msuya ana Shahada ya uzamili ya Maikrobailojia na kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada pamoja na shahada ya Baiokemia kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde,Scotland.

Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira ni mpango wa kidunia wa mazingira unaolenga kutoa mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa mazingira, na kuwashauri wadau na nchi wanachama kwa ujumla njia sahihi za kutunza na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira inafanya kazi na serikali,mashirika na asasi za kimataifa duniani kote. 

Riadha Tanzania wampongeza Mkurugenzi mpya MultiChoice

0
0
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limempongeza Mkurugenzi wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa MultiChoice Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Mei 20 mwaka huu, Kampuni ya MultiChoice Africa Limited, ilithibitisha uteuzi wa Wakurugenzi wawili, ambako Mtanzania Maharage Chande ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, anakuwa Mkurugenzi mpya wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Uteuzi huo uliotangazwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, unabainisha kuwa Maharage anachukua nafasi ya Stephen Isaboke aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki ambaye sasa anakuwa Mkuu wa Mamlaka (Group Executive Head of Regulatory). Uteuzi ambao unaanza Juni Mosi mwaka huu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, amesema uteuzi wa Maharage umezingatia uwezo na upeo wake mkubwa aliyouonyesha katika kipindi alipoiongoza MultiChoice Tanzania tangu alipojiunga nayo Juni 2016.

Rais wa RT, Anthony Mtaka, amesema familia ya Riadha Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi huo wa Maharage, hasa ukizingatia katika uongozi wake, MultiChoice Tanzania kupitia DStv, imekuwa mshirika mkubwa katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa Riadha hapa nchini.

“Sisi kama Riadha Tanzania, tumepokea kwa faraja kubwa kupanda kwa cheo kwa Mtanzania mwenzetu Maharage Chande, hakika tutamkumbuka kwa mengi katika kusapoti maendeleo ya Riadha hapa nchini….Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya na bila shaka mapenzi yake katika mchezo wa Riadha atayaendeleza,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Mtaka, alibainisha baadhi ya mchango wa MultiChoice Tanzania chini ya Maharage katika Riadha Tanzania, ni kutayarisha timu na wachezaji wa Riadha katika mashindano mbalimbali.

“Ni uthubutu wa Mkurugenzi Mtendaji Maharage Chande aliamua kumdhamini Mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya mashindano ya Olimpiki Rio de Jeneiro Brazil alipoibuka namba 5 na hatimaye kuja akiwa namba 3 katika mashindano makubwa ya Dunia huko London 2017.

“Maharage akiwa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Tanzania, ameendelea kuunga mkono Timu ya Riadha Tanzania ambapo mwaka huu kampuni yake ilitoa fedha za maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola,” alisema Mtaka na kuongeza.

Na hivi majuzi Maharage amempa udhamini mchezaji mwingine wa Riadha ili aweze kufanya maandalizi ya mashindano ya Dunia yatakayofanyika nchini Qatar 2019.

“Ukiacha hilo, MultiChoice Tanzania pia ilikuwa bega kwa bega na RT katika kuimarisha ushirikiano wa wanafamilia ya Riadha na Wadau wake wakiwamo waandaaji wa matukio mbalimbali ya mchezo wa Riadha,” alisema Mtaka na kuongeza.

Sisi kama Riadha Tanzania tunampongeza na kumtakia heri katika majukumu yake tukiamini heshima ya nchi yetu Tanzania katika kampuni hii kubwa duniani itaendelea kuaminika na kuheshimika, na zaidi sisi kama familia ya Riadha tunaahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa MultiChoice Tanzania.

TAASISI YA UHUSIANO WA UMMA TANZANIA (PRST) KUADHIMISHA WIKI YA MAWASILIANO AFRIKA MEI 25, 2018 JIJINI DAR

0
0
Katibu wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Ndege Makura, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 22, 2018 jijini Dar es Salaam wakati akielezea maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika inayotarajiwa kufanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta. Pembeni yake ni Rais wa PRST, Loth Makuza.
Rais wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST), Loth Makuza akitoa msisitizo kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika inayotarajiwa kufanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta. Kushoto ni Katibu wa PRST, Ndege Makura. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania, (PRST) inatarajia kufanya maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika, iliyoanza tokea Mei 21 na kilele chake kinatarajiwa kuwa Mei 25, 2018 na Tanzania watafanyia kwenye Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Chama hicho hapa Tanzania, Ndege Makura, amesema ili kufanikisha siku hiyo wameamua kuweka mezani maada inayoendana na agenda kuu ya siku hiyo Kitataifa ya Uchumi wa pamoja barani Afrika, wao wamekuja na Tanzania ya Viwanda. 

 Amesema takribani ya Mataifa yote yamekua katika kusherekea siku hiyo ya mawasiliano ambapo jumla ya miji 60 Barani Afrika wanasherekea ikiwemo na Tanzania. Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo, yapo malengo bainishwa Kimataifa huku Bara la Afrika wakijadili uchumi wa pamoja lakini kwa Tanzania watajadili suala la mchango wa Maafisa Uhusiano wa Umma ni kwa jinsi gani wanaweza kuchangia kuleta maendeleo ya uchumi hususani katika suala zima la kutangaza sera ya Tanzania ya Viwanda. 

 "Hii ni siku muhimu kwetu watu wa Uhusiano wa Umma , kwani tutajadili vitu vingi vinavyotokana na Sera za maendeleo ya Taifa, wapo watu wengi hawaelewi nini maana ya Viwanda, dhumuni lake na njia za kufikia ndoto hiyo ya Rais wetu, hata Bungeni tumeona Wabunge wakikinzana kuhusu viwanda, tunaleta mjadala huu ili kujadili kwa kina na wataalamu wetu , Wizara ya Viwanda, Afisa uhusiano wa umma kutoka Serikalini na Taasisi binafsi, waandishi wa habari, ili kusaidia ndoto ya Taifa letu kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025" amesema Makura. 

 Nae Rais wa PRST, Loth Makuza amesema kuwa umefika wakati wa kwenda kumkwamua afisa habari wa taasisi au shirika binafsi ili aweze kujitambua na kutambua malengo ya serikali yake kwa kujua umuhimu wa kazi yake. "Kuna Maofisa Habari wengi hawajitambui hasa kwa kuwa nyuma kabisa kwa vile wengine hawajui hata malengo ya serikali au mashirika yao, matokeo yake wao huishia kuandika taarifa za kuambiwa badala ya kuwa wao wawe miongoni mwa watu wanaoweza kuzitokea ufafanuzi zaidi na kwa kina," amesema Makuza.

 Ameongeza kuwa changamoto nyingi za kutokukamilika kwa Sera mbali mbali za maendeleo hapa nchini kutofikia lengo ni kutokana na kutoshirikishwa hivyo watu wamekuwa wakichelewa kupata taarifa na kujua kwa kina juu ya utungwaji wa Sera hizo. , Amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi ili kuchangia mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa letu pamoja na uchumi wa pamoja katika Bara letu la Afrika. 

 Barani Afrika Makao Makuu ya Taasisi ya Uhusiano wa Umma yapo mjini Lagos Nigeria na duniani hapo uingereza Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania, (PRST) ilizinduliwa rasmi mwaka jana Novemba 2, mwaka 2017, Jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania, huku ikitimiza zaidi ya wanachama 200, ambapo miongoni mwao wametokea kwenye Taasisi binafsi walizo ajiriwa na wengine kutoka Vyuoni.

TULIA TRUST YAWAPELEKA BUJORA DANCE GROUP KUWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DANCE INDIA

0
0
Na Zainab Nyamka, Blogu ya jamii

WASHINDI wa Tulia Traditiona Dance Festistal 2017 chini ya Taaisisi ya Tulia Trust Bujora Dance Group la Mkoa Mwanza jana  wameelekea nchini India kushiriki mashindano ya ngoma ya asili yatakayofanyika tarehe 25 na 26 wiki hii.

Akizungumza na vyombo vya habari mmoja wa wanakikundi hao Deogratius Willium ameeleza kuwa walishinda katika mashindano ya Tulia dance mwaka jana na kwa sasa wanaelekea India katika mashindano hayo ya ngoma za asili.

Aidha ameeleza kuwa wana uzoefu na wamejiandaa na wanajiamini, na kuwaomba watanzania wawaombee ili waweze kurudi na ushindi.Pia Veronika Sombi mshiriki wa kikundi hicho ameeleza kuwa ameeleza kuwa walishinda kwa kishindo Mbeya kwa kuibuka nafasi ya kwanza kati ya vikundi 81, hivyo ushindi lazima urudi nyumbani.

Pia wamemshukuru Dk. Tulia kwa kuanzisha mashindano hayo kwani kama vijana wamepata fursa ya kutangaza utamaduni wa mtanzania sambamba na kutembea katika nchi nyingi duniani kama Sweden na Korea.

Mashindano haya ya kulinda utamaduni yalianza mapema mwaka 2016 huko Tukuyu Mkoani Mbeya chini ya Dkt. Tulia Ackson ambaye ni naibu spika wa Bunge la Jamuhuri wa muungano wa Tanzania, pia ni muasisi wa mashindano hayo. 

Washindi wa mashindano hayo hunufaika kwa namna mbalimbali kama vile kueneza utamaduni nje ya nchi na kupata mafunzo katika vyuo vya sanaa hasa Bagamoyo ambapo washindi wa mwaka 2016 waliendeleza ujuzi katika chuo hicho cha sanaa.
Mwanakikundi wa Bujora Deogratius Willium akizungumza kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini India kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kucheza baada ya kuibuka washindi katika mashindano ya Tulia Traditional Dance Festival mwaka jana yaliyo chini ya Naibu Spika Dkt Tulia Ackson.

Rukwa watolewa mashaka kuhusu Ebola.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatoa mashaka wanarukwa juu ya kutokuwepo kwa ugonjwa wa Ebola katika Mkoa na kutahadharisha yeyote anaejaribu kuleta hofu ya ugonjwa huo katika Mkoa na kuwataka wananchi wasijengewe hofu bali waendelee kuchukua hatua za tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema kuwa Mkoa unaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha ufuatiliaji na kutekeleza mikakati ya udhibiti ikiwemo kutoa taarifa na elimu kwa jamii kwa kadiri itakavyohitajika ili ugonjwa huo usiingie katika mkoa.

“Katika kipindi hiki ambacho tunatakiwa kuchukua tahadhari kubwa, wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa ni lazima tuwe na mshikamano, umoja na tahadhari kubwa sana na hasa maeneo yale ya Ziwa Tanganyika ambako kuna muingiliano wa watu kutoka Zambia, DRC, Rwanda na Burundi. Lakini pia wanaotokea maeneo mengine ya nchi, la muhimu ni kuchukua tahadhari kubwa sana,” Alisema

Ameongeza kuwa wenyeviti wa vijiji wajizatiti katika kuboresha taarifa za wakazi wao kwenye madaftari yao na kuwa makini na wageni wanaoingia kwenye maeneo yao pamoja na kuitaka idara ya uhamiaji kuhakikisha wageni wote wanaingia katika njia zilizo rasmi.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa afya Mkoa kilichoitishwa na Mganga Mkuu wa mkoa ili kutoa elimu kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo waandishi wa habari juu kusambaza ujumbe huo wa kujihadhari na ugonjwa huu hatari wa Ebola.

Mmoja wa wadau hao akiwakilisha kundi la wazee, Zeno Nkoswe amesema kuwa serikali ya Mkoa haina budi kuhakikisha elimu hiyo inafikishwa kwa viongozi wote wa dini kwani wao wanauwezo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwa muda ufupi na ujumbe hatimae kutimiza malengo ya kufisha ujumbe huo kwa wananchi.

Akichangia mjadala huo mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila amesema kuwa serikali haina budi kutumia redio zilizopo Mkoani Rukwa ili kufikisha ujumbe huo kwa watu wote na maeneo yote ya Mkoa na mikoa ya jirani ili watu waweze kujikinga na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola upo katika nchi ya jirani ya Jamhuriya watu wa Kongo katika mji wa Biroko, jimbo la Equator na kwa taarifa za shirika la afya duniani, hadi kufikia tarehe 17 Mei, 2018 watu 44 walikuwa wamebainika kuwa na ugonjwa huo na watu 23 kufariki.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo

Ilala Yaahidi Kudumishia Miradi ya Dar – Urban

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imeahidi kuendeleza na kudumisha miradi iliyoachwa na shirika la Plan International katika maeneo ya Buguruni na Vingunguti.

Ahadi hiyo imetolewa leo jijini humo na Katibu Tawala wa Halmashauri hiyo, Edward Mpogolo alipokuwa akifunga programu ijulikanayo kama Dar – Urban iliyoanzishwa na shirika hilo ambayo imedumu katika maeneo hayo kwa miaka 26.

Mpogolo amesema kuwa shirika hilo limefanya kazi nzuri tangu kuanzishwa kwa program hiyo kwani imeleta mapinduzi makubwa katika kuimarisha huduma muhimu kwa wananchi kwa kuboresha sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya na ujenzi wa miundo mbinu.

“Toka mwaka 1992 wamekuwa na sisi wakitusaidia kutuboreshea huduma mbalimbali na katika kipindi chote hicho wameweza kutujengea shule mbili za msingi, kutujengea kituo cha Afya cha Buguruni, kuwaelimisha na kuwainua vijana hivyo tunawaahidi kuisimamia na kuidumisha miradi yote waliotuachia”, alisema Mpogolo.

Mpogolo amefafanua kuwa baada ya shirika hilo kujenga shule mbili za msingi za Vingunguti na Buguruni Moto Mpya mnamo mwaka 2016 ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 49 mpaka asilimia 98 pia tangu walipojenga kituo cha afya mnamo mwaka 2002 wagonjwa walikuwa 40 mpaka 50 kwa siku lakini kwa sasa kituo kinapokea wagonjwa kati ya 500 mpaka 600.

Vile vile katika kuelimisha vijana, Mpogolo amesema kuwa shirika hilo linajitahidi kuendana na Sera ya Serikali nchini ya kuwasaidia vijana ambapo wameweza kuelimisha vijana zaidi ya 2,000 na vijana hao wametumika kuwaelimisha wenzao zaidi ya 29,000 walioweza kujianzishia shughuli zao binafsi kwa ajili ya kujikimu. 

Aidha, Mpogolo ametoa rai kwa shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu ambazo zitasaidia kupunguza utegemezi kati yao na kuwafanya waweze kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Meneja Miradi ya Dar – Urban kutoka shirika la Plan International, Nicodemus Gachu amesema kuwa progamu hiyo inafungwa baada ya kuhitimisha utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo watahamia katika maeneo mengine yenye uhitaji.

“Kwa miaka 26 mradi huu umetumia zaidi ya bilioni 15 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya afya, elimu, ulinzi wa mtoto, ushirikishwaji, elimu ya afya ya uzazi na uwezeshaji vijana kiuchumi”, alisema Gachu.

Mradi huo utahamishiwa katika wilaya ya Nkasi iliyopo mkoani Rukwa kwa lengo kubwa la kumuwezesha mtoto wa kike kupata fursa mbalimbali katika jamii pamoja na kusaidia maeneo yenye uhitaji katika wilaya hiyo.

KWANDIKWA, MAVUNDE WAWAPA MATUMAINI WANANCHI WA MSALATO WALIOPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE

0
0

Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji (hawapo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni wakimsikiliza kwa makini Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.


 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi wake wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa wananchi wake wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji alipokuwa akiwasilisha malalamiko yake kuhusu kuchelewa kulipwa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Mpamaa Kata ya Miyuji akizungumza mbele ya viongozi kuhusu ucheleweshwaji wa fidia ya wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.

...............................................................................................................
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akiwa na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde leo wamekutana wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato Dodoma na kuwatoa hofu kuwa serikali itawalipa fidia zao.

Wananchi hao ni kutoka Mpamaa, Msalato, Makutupora, Miyuji na Nzughuni.


Akizungumza na wananchi hao, Kwandikwa amesema serikali inatambua madai yao na kwamba fidia zao zitalipwa kwa kuzingatia sheria za utwaaji ardhi. Amefafanua anaelewa wapo wananchi 1,470 ambao mwaka 2007/8 wamelipwa kiasi cha sh.bilioni 1.6.


Aidha amesema mwaka 2013 wananchi 980 walitathiminiwa ambapo kiasi cha sh.Bilioni 3 kilihitajika kwa ajili ya kuwalipa fidia. “Ndugu zanguni ni takribani miaka 5 sasa imepita, muda huo ni mrefu niwatoe hofu tu sheria zipo tutazizingatia,"amesisitiza


Kwandikwa amesema katika kuhakikisha wanalifanyia kazi hilo kwa haraka watashirikiana na wadau wote wanaohusika ili taratibu za ulipaji wa fidia zianze kwa mapema. Kwandikwa amesema wataangalia kama kuna sehemu watu wamechelewesha mchakato huo kwa uzembe hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.


Awali, akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, amesema wananchi hao tangu mwaka 2009 maeneo yao yalichukuliwa lakini hadi sasa hawajalipwa fidia.


 "Suala hili wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu niliahidi kulifuatilia hili,nilikueleza suala hili nashukuru umekuwa msumbufu kwangu wa kutaka kujua lini unakuja kuzungumza na wananchi hawa, nikushukuru sana wewe na meneja wa Tanroads mkoa, kwa kuwa sehemu ya msaada kwangu,"amesema mbunge huyo.


 Mavunde amempongeza Rais John Magufuli kwa kulijenga jiji la Dodoma kwa miundombinu mbalimbali na kusema hatua hiyo inaipa hadhi zaidi jiji hilo.


 Kwa upande wao, wananchi wameiomba serikali kuiangalia upya fidia watakayoilipa ili iendane na hali ya maisha ilivyo sasa kwa kuwa ni muda mrefu tangu wafanyiwe tathimini.

Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza kuendelea kuboresha uhusiano wa kibiashara

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akizungumza na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dokta Charles Kimei leo amekutana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa ili kuangalia njia bora zaidi za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote mbili. Akizungumza katika mkutano huo ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi kutoka Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza, Dokta Kimei alilishukuru Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo, akaunti za mishahara za askari na SACCOSS ya Magereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa huduma kwa askari Magereza.

“Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa biashara ambayo limekuwa likitupatia, niipongeze SACCOSS ya Magereza kwa uamuzi wa kuwa Wakala wa FahariHuduma, hii si tu itawaongezea kipato kupitia kamisheni za uwakala, pia itasogeza huduma za kibenki karibu na Maaskari Magereza”, alisema Dokta Kimei.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya CRDB, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei. 


Akielezea juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wafanyakazi Dokta Kimei alisema hivi karibuni Benki imeshusha riba inayo toza katika mikopo binafsi toka 20% mpaka 17%, muda wa marejesho umeongezwa toka miezi 72 hadi miezi 84, wakati kiwango cha kukopa kimeongezwa kutoka shilingi milioni 50 mpaka kufikia Shilingi Milioni 100 hivyo kuwapa wateja wigo mpana zaidi wa kukopa ili kufikia malengo.
Dokta Kimei pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha askari wa Jeshi la Magereza kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo huku akibainisha ya kuwa Benki ya CRDB imeanzisha utaratibu maalum wa kununua madeni na mikopo ya askari kutoka katika Taasisi zingine za Kifedha. Hivyo kutoa fursa kwa askari wenye mikopo Benki nyingine, kukopa toka Benki yao pendwa ya CRDB. Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Aprili 2018 tayari Benki ya CRDB ilikuwa imeshakopesha zaidi ya maofisa 5,415 wa Jeshi la Magereza ambapo jumla ya shilingi 29.4 bilioni zilikuwa zimekopeshwa kwao.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, wakati alipomtembelea ofisini kwake, Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Mkutano huo ulikuwa na lengo kudumisha uhusiano wa kibiashara baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini. 


Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa alimshukuru Dokta Kimei kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya CRDB kwa maboresho hayo katika huduma zake, huku akiisifu zaidi huduma ya Salary Advance ambayo alisema kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya askari. Dokta Malewa alisema katika maboresho hayo yanayoendelea Jeshi la Magereza lingependa kutumia mfumo wa kibenki katika kukusanya mapato yake katika miradi na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

“Nikuombe Dokta Kimei na uongozi mzima wa Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuweka huduma za kibenki kama ATM na Matawi kwenye maeneo ya Magereza yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo”, aliongezea Dokta Malewa. Dokta Malewa pia aliiomba Benki ya CRDB kushiriki katika miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Jeshi hilo ikiwamo ujenzi wa hospitali ya Jeshi la Magereza Ukonga, miradi ya Kilimo cha kisasa na chenye tija, mradi wa kokoto Msalato pamoja na uwekezaji katika miradi ya viwanda vidogo vidogo.
Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, wakiongozwa na Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Kamishna Festo Sanga (wa kwanza kulia) wakati wa kikao maalum na uongozi wa Benki ya CRDB, uliotembelea Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es salaam leo.
“Ningependa kuona pia Benki ya CRDB kuwa mteja wa bidhaa na huduma zinazotolewa na Jeshi la Magereza mfano Benki kutumia samani za ofisi na Magereza kupewa Kandarasi za ujenzi wa miradi ya Benki inayodhaminiwa au kumilikiwa na Benki”, aliongezea Dokta Malewa akionyesha fursa ya kibiashara iliyopo baina ya Benki na Jeshi la Magereza.

Dokta Kimei alimhakikishia Mkuu wa Jeshi la Magereza kuwa Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Jeshi hilo katika miradi mbalimbali ambayo wamepanga kuitekeleza, huku akihaahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Benki ya CRDB kufanya upembuzi yakinifu juu ya kuweka ATM na kufungua vito vya kutolea huduma katika maeneo ya Jeshi la Magereza ilikufikisha huduma kwa akari kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akieleza jambo kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Juma Malewa (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es salaam leo.

“Matarajio yangu ni kuona uhusiano baina yetu ukikua zaidi, naihidi kuwa kupitia Wakurugenzi na Mameneja wetu wa matawi tutaweka utaratibu wa kutembelea ofisi za Magereza nchi nzima ili kuhakikisha haya tuliyokubaliana hapa yanatekelezwa”, alisema Dokta Kimei.

Mkutano huo ulimalizika kwa Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza kutengeneza kikosi kazi cha kufuatilia utekelezaji wa maazimio ambapo Kamishna Gaston Sanga Mkurugenzi wa Utawala, fedha na Rasimali watu wa Jeshi la Magereza alichaguliwa kuwa Mwenyekiti akisaidiwa na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Bi. Jesica Nyachiro. Dokta Kimei pia alimuomba Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB Bi. Tully Mwambapa kuona namna ambavyo Benki ya CRDB itaweza kuunganisha shughuli zake za misaada kwa jamii na Jeshi la Magereza.


Katika mkutano huo Benki ya CRDB iliahidi kutoa msaada wa kompyuta na vitendea kazi vingine kwa Jeshi la Magereza ili kuongeza ufanisi wa Jeshi hilo. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi April 2018, Benki ilikuwa pia imeshafungua zaidi ya Akaunti elfu tatu (3,000) za mishahara kwa askari wa Jeshi la Magereza.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza.
Baadhi ya Maafisa wa Benki ya CRDB, wakiwa kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, wakati alipomtembelea ofisini kwake, Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Mkutano huo ulikuwa na lengo kudumisha uhusiano wa kibiashara baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini.
Picha ya pamoja.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images