Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1583 | 1584 | (Page 1585) | 1586 | 1587 | .... | 1898 | newer

  0 0

  NA   JOSEPH MPANGALA- MTWARA.

  Wamiliki wa Viwanja na mashamba waliopo kanda ya kusini,Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara wametakiwa kulipa Kodi ya Ardhi pamoja na malimbikizo ya Yamadeni kwa mwaka wa fedha 20017/2018ili kuepuka usumbufu wakupelekwa mahakamani,Kunadiwa malizao au kufutiwa miliki ya ardhi zao. 

  Kodi hii inatakiwa kulipwa kila tarehe 1Julai hadi mwezi disemba kila mwaka na ifikapo januari mosi ya kila mwaka kodi hii hulipwa pamoja na adhabu ambayo ni asilimi1 kwa kila mwezi wa kodi husika. 

  Akiongea na waandishi wa habari ofisin za kanda ya kusini mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa ardhi Kanda ya Kusini Gasper Luanda amesema wananchii woote wanaomiliki Viwanja na Mashamba kwenda ofisi za Halmashauri za Wilaya,Miji,manispaa pamoja na Ofisi za kanda kwa ajili ya kupata Makadirio ya Ankara za malipo. 

  “Tangazo hili linamuhusu mtu yeyote mwenye kiwanja na aliyemilikishwa lakini hata Yule aliyemilikishwa na amejenga kwa hiyo kama una jengo lako kwenye kiwanja ulichopewa inamana utalipa kodi mbili,Utalipa kodi ya ardhi kwenye wizara ya ardhi lakini kwa kupitia mawakala wetu ambao ni Halmashauri lakini sasa hivi tunamawakala kupitia banki za NMB na CRDB lakini ya kodi ya pango la ardhi unakwenda kulipiwa TRA kwa hiyo wananchii wasichanganye hizi kodi mbili kila moja inasimamiwa na Sheria zake. 

  Aidha Luanda ameongeza kuwa muitikio wa ulipaji kodi ya majengo,Vianja na mashamba katika kanda ya kusini umekuwa mkubwa kutokana na Makadirio waliopewa ya ukusanyaji kuendelea kuongezeka kila mwezi. 

  “Muitikio ni Mzuri kama mnavyojua makusanyo ya kodi yanakwenda na malengo sisi kama kanda Tulipewa jukumu la kukusanya Kodi ya Billion7.86 kanda kwa maana mikoa yote ya Mtwara Lindi na Ruvuma sasa watu wamelipa na Tunakaribia sasa Billion saba na Kitu lakini sasa kuna pengo la million mia sita/mia saba hivi halijakusanywa ndio maana tupo hapa kuwahimiza wale wachache ambao wamebaki basi nao watimize wajibu wao kwa sasabu kulipa kodi ni Lazima sio Hiari” 

  Kwa sasa Miggogoro katika Mkoa ya kanda ya kusini imeonekana kupingua kutokana na Kuweka Dawati la Migogo ambalo linasikiliza Migogoro ambapo kwa sasa wanaokuja kulalamika wamepunua kwa kiasi kikubwa. 
  Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda akongea na waandishi wa habari kuhusiana na Uahamisishaji wa Ulipaji wa kodi kwa wamiliki wa Viwanja na mashamba katika kanda ya Kusini Mikoa ya Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara.
  Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda wakifurahi jambo na Afisa Mipango miji Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkono Werema wakati wa kipindi cha Maswali na majibu na waandishi wa habari juu ya kodi kwa wamiliki wa Viawanja na mashamba Mkoani Mtwara

  0 0


  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imewaruhusu Maria na Consolata waliokuwa wamelezwa katika hispotali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na afya zao kuimarika.

  Pacha hao walikuwa wakipatiwa matibabu na madaktari bingwa wa Muhimbili na leo wamepelekwa Iringa ambako watapokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema pacha hao wamesindikizwa na madaktari wa Muhimbili haid Iringa na kwamba wakiwa huo wataendelea kupatiwa matibabu.

   “Consolata na Maria tumewaruhusu leo. Hii ni baada ya madaktari kujiridhisha kwamba afya  zao zimeimarika. Wataalamu wetu wamewafanyia vipimo mbalimbali na pia tumewasiliana na wenzetu wa nje na tukakubaliana tuwaruhusu sasa,” amesema Prof. Museru.

  Prof. Museru amesema kwamba pacha hao wamepatiwa machine ya CPAP & Oxygen ambayo itawasaidia kuwapatia tiba endapo watahitaji wakati wakiwa Iringa.

  Wakizungungumza kwa nyakati tofauti, Consolata amesema kwamba Muhimbili imewapatia huduma nzuri na wanawashukuru wataalamu mbalimbali waliokuwa wakiwapatia matibabu tangu walipolazwa.

  Naye Maria akizungumza kwa furaha amesema hivi sasa anajisikia vizuri tofauli na awali-kabla ya kupelekwa katika hispotali hiyo kwa ajili ya matibabu. Pia, amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili kwa kuwapatia huduma bora za matibabu.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Maria na Consolata leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai na wengine ni wataalamu waliokuwa wakiwapatia matibabu pacha hao.
   Kulia ni machine ya CPAP & Oxygen ambayo Maria na Consolata wamepewa endapo watahitaji matibabu yanayotolewa kwa kutumia mashine hiyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwaaga Maria na Consolata leo.
  Maria na Consolata wakisaidiwa kuingizwa kwenye gari ikiwa ni safari ya kuelekea Iringa leo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  0 0

  Michuano ya Kurugenzi Cup 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga imeendelea kutimua vumbi kwa timu ya Airport SC kuifunga Makulusa FC mabao 3-0.

  Katika mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom, hadi mapumziko timu ya Airport SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Abubakary Maina dakika ya nne kwa njia ya penati.

  Kipindi cha pili timu ya Airport SC ilipata mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Emmanuel Mallo kwenye dakika ya 50 na ya 55.

  Kwenye mchezo mwingine timu ya Stand United timu ya Mlimani FC iliifunga bao 1-0 na kuiondoa kwenye michuano hiyo.

  Fainali ya mashindano hayo iliyoshirikisha timu 10 inatarajiwa kufanyika jumapili ya wiki hii kwenye viwanja hivyo vya Haydom.

  Katibu wa chama cha soka wilaya ya Mbulu (MBFA) Joseph Nicodemus alisema michuano hiyo itakuwa chachu kwa vipaji vipya vya wilaya hiyo kupiga hatua kwenye mchezo huo.

  Nicodemus alisema anatarajia timu zitakazoshiriki michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya wilaya zitapata wachezaji kwenye michuano hiyo ya Kurugenzi Cup 2018.
  Waamuzi wa mashindano ya Kurugenzi CUP 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga wakishuhudia manahodha wa timu ya Makulusa FC Regi Gisimoy (kulia) na Samwel wa timu ya Airport FC wakitakiana heri ya mchezo ambapo walifungwa mabao 3-0.
  Wachezaji wa akiba wa timu ya Airport FC wakiwa benchi la ufundi huku wakiendelea furahi mchezo ambapo waliifungwa Makulusa Fc mabao 3-0.
   Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
  Baadhi ya wachezaji wakiushuhudia mpambano wa soka ukiwa unaendelea kwa kasi baina ya timu za Airtport FC dhidi ya Makulusa FC hazipo pichani.
  Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
  Mmoja wa wachezaji akigangwa na madaktari baada ya kuumia mguu katika mchezo huo.

  0 0


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga joelson kulia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo wakiwa kwenye  bango la uzinduzi wa Operesheni Zagamba 2018. Operesheni hiyo  ni maalum kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nchini, ambapo kitaifa ilizinduliwa Namanga kwenye Wilaya ya Longido. Picha na John Mapepele


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga joelson kulia akitoa maelezo ya maana ya Operesheni Nzagamba2018 kwenye  bango la uzinduzi wa Operesheni Zagamba 2018. Operesheni hiyo  ni maalum kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo na mazao yake nchini, ambapo kitaifa ilizinduliwa Namanga kwenye Wilaya ya Longido. Picha na John Mapepele


  *Atangaza operesheni ‘nzagamba’ kuwasaka wahujumu sekta ya mifugo  Na John Mapepele, Arusha

  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Serikali kila mwaka inapoteza jumla ya sh bilioni 263 kila mwaka kufuatia kushamiri kwa utoroshaji wa mifugo nje ya nchi na uingizaji wa mazao ya mifugo usiozingatia sheria na taratibu za nchi hali inayochangia ushindani usio wa haki kwa wazalishaji wa ndani ya nchi.

  Akizungumza jana kwenye mnada wa mifugo wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa operesheni maalum ya kitaifa ya kudhibiti upotevu wa mapato na usimamizi wa biashara ya mifugo na mazao yake iliyopewa jina la ‘Operesheni Nzagamba 2018’ Waziri Mpina alisema operesheni hiyo itamfikia kila mtu anayejishughulisha na tasnia nzima ya mifugo.

  Alisema operesheni hiyo itafika kwenye minada ya mifugo, bandarini, viwanja vya ndege, mipakani, kwenye masoko na maduka,supermarket, na machinjioni ili kujiridhisha na uhalali wa biashara hiyo.

  Pia Waziri Mpina alisema operesheni hiyo imefanikiwa kubaini kuwepo kwa ubabaishaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kufanya udanganyifu katika biashara ya dawa za mifugo,upotevu mkubwa wa mapato na uingizaji holela wa mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi ikiwemo nyama na maziwa kupitia njia za panya.

  Akitolea mfano eneo la Namanga zaidi ya mbuzi 22,000 zilikamatwa zikitoroshwa kwenda nchini Kenya huku makusanyo yakiongezeka na kufikia sh milioni 200 kwa muda wa mwezi mmoja tangu kuanza operesheni hiyo ambapo kwa upande wa Mwanza makusanyo yameongezeka kutoka sh milioni 17 kwa mwezi na kufikia Sh. Milioni 532.

  Waziri Mpina alisema tathimini ya awali iliyofanywa na wizara yake imebaini kuwa wastani wa ng’ombe milioni 1.6 hutoroshwa kila mwaka kwenda kuuzwa nchi za jirani ambapo Serikali hupoteza sh bilioni 56.4 kwa mwaka huku upande wa ngozi Serikali ikipoteza sh. Bilioni 87.6 kwa mwaka ambapo kwa upande wa nyama na maziwa Serikali hupoteza zaidi ya sh bilioni 120 kila mwaka

  Aidha alionya kuwa mifugo itakayokamatwa ikitoroshwa kwenda nchi jirani kinyume cha sheria Serikali itafanya maamuzi magumu ya kutoza faini kubwa ili kuhakikisha watu wote wanafuata sheria ili mifugo hiyo iweze kunufaisha watanzania wote kupitia mfumo wa ushuru na kodi.

  Kuhusu tozo ya mifugo inayokwenda nchi za nje, Waziri Mpina alisema msimamo wa Serikali unabaki pale pale ambapo kila ng’ombe atatakiwa kulipiwa sh 20,000 na Mbuzi sh. 5,000 huku akiruhusu vibali vya biashara za mifugo vinavyotolewa na halmashauri viendelee kutumika hadi pale Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakapoamua vinginevyo.

  Pia Waziri Mpina alipongeza uamuzi wa kujengwa kwa mnada wa kisasa wa mifugo katika eneo hilo la uliofadhiliwa na Mradi wa MIVARF na kugharimu sh. Milioni 782 na kusisitiza kuwa mnada huo utakuwa mkombozi mkubwa kwa wafugaji kupata soko la uhakika la mifugo yao.

  Kaimu Katibu Mkuu Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Lovince Assimwe alisema operesheni hiyo imewezesha kubaini mianya ya upotevu ya mapato yatokanayo na sekta ya mifugo na kusisitiza kuwa itakuwa endelevu hadi pale wadau wa sekta hiyo watakapofuata sheria za nchi.

  Dk Assimwe Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kusimamia sekta ya mifugo ili iweze kutoa mchango unaostahili kwa maendeleo ya Taifa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo alimshukuru Waziri Mpina kwa juhudi kubwa anazofanya za kudhibiti utoroshaji wa mifugo na kumhakikishia kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo itaendelea kushirikiana na wizara kuhakikisha mifugo haiendi nje ya nchi kwa njia za panya.

  Alisema maagizo yote yaliyotolewa na Waziri Mpina atatumia uwezo wake wote kuhakikisha yanasimamiwa kikamilifu ili kuweza kupata matokeo mazuri yanatoyarajiwa.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wakifunua pazia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembela kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
  .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kutembelea kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bidhaa za kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua utengenezaji wa maji ya kunywa  katika kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. 
   Maji ya kunywa ya UHURU PEAK yanayotengenezwa katika kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji  yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji  yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. PICHA NA IKULU

  0 0

  Aliyewahi kuwa Mbunge wa Monduli na Mkuu wa wilaya Mstaafu Luteni Mstaafu Lepilal Ole Molloimet aliyefariki Dunia Jumapili iliyopita,anatarajiwa kuzikwa kesho Ijumaa mjini Longido.Kwa mujibu wa msemaji wa familia Mh. Christopher Ole Sendeka, Luten Molloimet amefariki dunia kwa ugonjwa wa shinikizo la damu

  0 0

  Mchezaji Godfrey Ernest wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom Manyara akimtoka mchezaji wa timu ya Rambo FC pia ya Haydom katika mchezo wao uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom katika Mashindano ya  kombe la Kurugenzi Cup 2018 yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo timu ya Rema 1000 FC imeibuka na ushindi wa Magoli 5-3 dhindi ya Rambo FC.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-HAYDOM- MANYARA)
   Wachezaji wa timu ya Rema 100 FC ya Haydom wakishingilia  mara baada ya mchezaji Raurenc Marco kuifungia timu yake ya Rema 1000 FC goli lao la tano katika mchezo huo uliokuwa mkali dakika zote za mchezo.
   Kikosi cha timu ya Rema 1000 FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
   Kikosi cha timu ya Rambo FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
   Wachezaji wa timu ya Rambo FC na timu ya Rema 1000 FC wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Haydom.

   Mchezaji Ngaja Junior wa timu ya Rambo FC  bukta ya bluu na Masoud Juma wa Rema 1000 FC wakizungumza na waamuzi kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo huo uiofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom.
   Baadhi ya watoto wakigawiwa maputo kwenye benchi la ufundi la timu ya Rema 1000 FC.
   Kocha wa Rema 1000 FC Jared Ochieng akitoa maelekezo kwa wachezaji wake huku mmiliki wa timu hiyo Bw.Samson Madawa Bora ambaye pia ni Daktari katika Hospitali ya Haydom akimsikiliza wakati wa mapumziko ya mchezo huo.
   Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo huo.
   Bw. Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na Mawasiliano Halmashauri ya wilaya ya Mbulu akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kuangalia mchezo huo kuhusu huduma ya upasuaji kwa watu walioungua kwa moto inayotolewa na daktari wa kujitolea Joost Binmerts kutoka Uholanzi akishirikiana na madaktai wa Hospitali ya Haydom.
   Bw. Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na Mawasiliano Halmashauri ya wilaya ya Mbulu akizungumza na daktari wa kujitolea Joost Binmerts kutoka Uholanzi anayefanya kazi katika  Hospitali ya Haydom.
   Baadhi ya mashabiki wa mpira waliojitokeza kushuhudia mchezo huo wakifuatilia wakati ulipokuwa ukiendelea.

  Baadhi ya mashabiki wakifurahiamoja ya goli lililofungwa katika mchezo huo.
  .......................................................................................
  Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingi
  Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa
  kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.

  Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho,
  upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi,
  kwenye mashindano hayo  yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
  Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.

  Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na winga
  machachari wao Shafii Said wenye dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza
  cha mchezo huo.

  Mshambuliaji hatari wa timu ya Rema 1000 FC Masudi Juma aliipatia timu
  yake bao la pili kwenye dakika ya 29 mara baada ya kuwachambua pasipo
  na huruma walinzi watatu wa timu pinzani na kupachika kimiani bao la
  kiufundi, hadi mapumziko timu ya Lambo haikuona nyavu ya timu pinzani.

  Kipindi cha pili timu ya Lambo FC kupitia kocha wake ilifanya
  mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wawili na kuingiza nguvu mpya
  ambayo ilibadilisha sura ya mcheo na kuleta maajabu kwenye viwanja
  hivyo kwa kurudisha mabao mawili na kuongeza la tatu.

  Katika dakika ya 53  mshambuliaji wa timu ya Lambo FC Lazaro Zebedayo,
  aliyeingia kipindi cha pili alirejesha matumaini kwa kupachika bao
  safi la kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mkabaji
  Patrick Zacharia.

  Mnamo dakika ya 60 winga machachari wa timu ya Lambo FC Salvatory
  Zelote aliachia shuti kali umbali wa mita 23 na kutinga kimiani na
  kumuacha kipa ameduwaa hivyo kufunga bao la pili na kusawazisha na
  kuwanyanyua mashabiki kwa vifijo na nderemo katika viwanja hivyo.

  Timu ya Lambo FC iliamka usingizini baada ya kupata mabao hayo na
  kuishambulia kama nyuki timu ya Rema 1000 na kufanikiwa kuandika bao
  la tatu kupitia mshambuliaji wao machachari Lazaro Zebedayo ambaye
  ndiye mfungaji wa bao la kwanza.

  Benchi la ufundi kupitia kocha mkuu wa timu ya Rema 1000 Jerad Ochieng
  alifanya mabadiliko ya haraka kwa kumtoa kiungo mmoja na washambuliaji
  wawili na kubadilisha sura ya mchezo kwa muda  mfupi.

  Baada ya mabadiliko hayo, dakika ya 79 kulitokea piga nikupige katika
  lango la timu ya Lambo FC na hatimaye mshambuliaji wa timu ya Rema
  1000 FC Laurence Marco alizamisha nyavuni mpira uliokuwa ukiambaa
  pembeni mwa goli hilo.

  Bao la nne la timu ya Rema 1000 FC liliwekwa kimiani na nahodha wa
  timu hiyo Shafii Said baada ya kutokea faulu upande wa kushoto na
  kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango, kwa mara nyingine tena
  dakika mbili baada ya bao la nne kutinga kimiani, mshambuliaji
  Lawrence Marco alihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga bao la kichwa
  baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Masudi
  Juma.

  Mara baada ya mchezo kumalizika Mkurugenzi wa timu Rema 1000 Samson
  Madawabora hakusita kuonyesha furaha yake katika viwanja hivyo kwa
  kuwazawadia kila mchezaji wa timu hiyo shilingi elfu 10,000 papo hapo
  uwanjani.

  “Timu yetu ipo vizuri kocha wetu Jerad Ochieng ameshawapa maelezo ya
  kutosha wachezaji wetu hivi sasa ije timu yeyote tuu sisi sawa
  tutawafunga tuu kwani tupo vizuri,” alisema Madawabora.

  Wakizungumza mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa timu ya Lambo FC
  Paulo Modest alisema kwenye mchezo kuna matokeo matatu kushinda,
  kushindwa na kutoka sare hivyo anakubaliana na matokeo hayo huku kocha
  wa timu ya Rema 1000 FC Jerad Ochieng akisema wamejiandaa ipasavyo kwa
  mpambano ujao.

  0 0

  Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba, Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar), wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambapo pia walikuwepo wawakilishi na viongozi kutoka TFF pamoja na viongozi wa timu za Simba, Yanga na Singida United Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas alisema “michuano hii kuleta chachu na kumpata bingwa kwa upande wa Africa Mashariki”
  Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwaka mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanania zisifanye vibaya zaidi ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu.Kutakuwa na jumla ya timu nane za Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na moja kati ya timu iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton.

  Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.Napenda kuwatakia kila la kheri timu zetu tatu zinazokwenda kutuwakilisha jijini Nairobi, natumaini zitatutoa kimasomaso kwa kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, wataiwakilisha nchi yetu vilivyo kwa kucheza kwa uweledi na nidhamu” alimaliza Ndugu Tarimba

  Kwa upande wa timu ya Simba Ndugu Said Tulliy alisema “Napenda kuchukua nafasii hii kuwataarifu wanasimba kuwa tunakwenda kushiriki mashindano kama timu shindani na si timu shiriki na tunajua mwaka jana tulipata nafasi kama hii lakini tuliipoteza na tusingependa kitu kama hicho kijirudie. 

  Tumeona faida yake kutokana na jinsi wenzetu waliopita ni jinsi gani walivyofaidikakupitia mashindano hayo.Kama timu tumejiandaa na tuko tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba Sports Club na heshima ya Tanzania, tunakwenda na kikosi kamili ili kuhakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kushindana na timu iliyopangwa.
  Tunathibitisha kuwa tutashiriki mashindano haya kwa sababu ni mashindano muhimu, tuko tayari kwa ajili ya mashindano na timu yetu nzima na tuko tayari ya kushinda” alimaliza Ndugu Said Tulliy.
  “Changamoto ya mashindano iko pale pale lakini kwa mwaka huu nia yetu kuu ni kuchukua ubingwa ili kuleta heshima kimataifa” Charles Boniface Mkwasa Yanga
  “Kwanza napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu wamefanya timu yetu kujulikana kwenye kila kona ya nchi, moja kati ya wadhamini wetu wa nguvu ambao tunajivunia sana kutoka kampuni hii. Jambo kubwa tutakaloenda kulifanya kwenye michuano hii kimsingi kwa mwaka huu tumeweza kushirikishwa mapema ili tuweze kujipanga sisi kama timu lakini kikubwa zaidi ikumbukwe kuwa Singida United ni timu pekee iliyofanikiwa kufika nusu fainali kwa hapa Tanzania na mwaka huu tunaamini tutachukua kombe
  Kwa watanzania na watu wa Africa mashariki tunaombawatuunge mkono timu yetu. Ningependa kuwaomba SportPesa kuhakikisha kanuni na sheria za mpira wa miguu zinafatwa ili michuano hii iweze kumalizika vizuri”–Shabani Mande Singida United
  Tunapenda kuwashukuru SportPesa kwa kututambua na kutupa nafasi ya kushiriki katika michuano hii na napenda kuwaahidi hatutawaangusha ingawa hii itakuw mara ya kwanza kushiriki.” Maalim Masoud, Katibu wa klabu, JKU.  0 0

   Majengo ya Kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara yaliyojengwa kwa shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi wakikagua kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akieleza kazi iliyofanyika katika Kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara kwa  Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi kwa kutumia shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
  Baadhi ya wananchi wa Sunya , Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipotembelea Kituo cha afya cha Sunya kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
  ..................................................
  Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wameipongeza Serikali  ya awamu ya Tano kwa kuhakikisha miundombinu ya afya inaboreshwa na kupunguza malalamiko ya kukosekana kwa huduma ya afya kwa jamii.

  Wameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipotembelea  kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.

  Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema Serikali imeweza kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya  208 kwa  lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya  kwa wakati na karibu na   maeneo wanaoishi.

  Wanasema kuwa awali miundombinu mingi ya afya ilikuwa duni, kukosekana kwa vifaa tiba na umbali wa vituo vya afya ilikuwa ni changamoto kubwa kwa jamii hali ambayo ilipelekea wananchi wengi hasa wamama wajawazito kujifungulia nyumbani.

  Bw. Muhamed Ally mmoja wa wananchi anaesema awali wanawake walikuwa wakitembea muda mrefu kutafuta huduma za afya na kusababisha vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5, hivyo tunaishukuru serikali kwa kujenga miundombinu ya vituo vya afya nchini.

  Wakati huohuo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kusimamia Mradi wa Ujenzi wa mindombinu ya Kituo cha Afya cha Sunya.

  Pongezi hizo amezitoa jana wakati alipotembelea kituoni hapo kuona maendeleo ya Miundombinu iliyojengwa kupitia fedha za serikali shilingi milioni 400 kwa ajili ya chumba cha upasuaji, nyumba ya mtumishi, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti na maabara.

  Aidha Mhe.Jafo amesema kwa sasa Serikali imeanza kununua vifaa tiba kwa vituo vyote 208 vilivyokarabatiwa na kujengwa, hivyo amewaomba wananchi wa Sunya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

  0 0


   WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga
   Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto  ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi akizungumza wakati wa halfa hiyo
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akifungua mlango mara baada ya kuzindua  madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akingia ndani ya madarasa mara baada ya kuyazindua kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
   Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kabla ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia akifurahia jambo na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa Selebosi mara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya msingi Bombo
   Sehemu ya wananchi na viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia matukio mbalimbali


   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha akiwa amekalia madawati mara baada ya kufanya uzinduzi huo
  Kundi la Wasanii la Tanga Kwanza likitumbuiza kwenye uzinduzi huo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua madarasa hayo kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kulia mwenye suti ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimukatika akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Bombo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wanaounda kundi la Tanga Kwanza


  WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi  ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.

  Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje  ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.

  Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.

  Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi  cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.

  “Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.

  “Lakini pia kadri tunavyoacha kwenda Marekani na Ulaya ndivyo fedha hizo zinasaidia kutumika kwenye harakati za kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu kwa kuwapa watoto wetu elimu bora “Alisema.

  Awali akizungumza katika ufunguzi huo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyotumia zaidi ya milooni 279 zilitokana na mapato ya ndani ya halmashauri na kuongezewa na serikali.

  Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu kuweka msukumo wao ambapo alihaidia kuzungumza na Waziri wa Wizara hiyo kuweka mradi wa matokeo kwanza ndio wakapata na kupokea kiasi cha milioni 136.6.

  “Katika suala hili naomba nikupongeze sana Mh Waziri Ummy kwa kulipigania Jiji la Tanga ndani na nje kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hivyo nisema tutaendelea kushirikiana”Alisema.

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bombo Denis Mushi aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati ili wananfunzi waweze kuendelea na masomo.

  “Tunaishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi huu lakini Mh Waziri Ummy kwa  msukumo mkubwa uliouweka kwenye jambo hilo kwani shule waliokuwa wamehamia ya Mkwakwani walikuwa na msongamano mkubwa na kusababisha kutokupata matokeo mazuri “Alisema (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha )

  0 0

   
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.


   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema jana jijini Dar,wakati wa kumtambulisha mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.
   Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku akifafanua zaidi kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda kitita hicho cha TatuMzuka,aidha kufuatia ushindi huo Shakila pia  'alimbust' Mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.

  Mchezo wa namba unaongoza nchini Tanzania wa Tatu Mzuka leo umemtangaza na kumtambulisha mbele ya vyombo vya habari mama aliyejinyakulia kitita cha milioni 140 na wakati huo ‘kumbusti’ mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake.

  Shakila Amri Nyani, ambaye ni mkazi wa Newala, Mtwara na mama wa watoto 3 alisherehekea siku ya mama duniani kwa kumpa mama yake milioni 30 kama ishara ya kutambua mchango wake katika siku hiyo muhimu.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Bwana Sebastian Maganga alikuwepo kuwakab
  idhi hundi Bi Nyani pamoja na mama yake. “Mama zetu ni hazina na hakuna kiwango chochote cha pesa kinachoweza kutosha kulipa upendo, msaada na kazi kubwa walioifanya katika kutulea. Kwa ushindi huu Tatu Mzuka tunaamini Bi Nyani na mama yake watafurahia na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao” alisema Maganga

  Bi Nyani, mwenye miaka 38 alikuwepo kuelezea furaha yake na namna ambavyo alicheza mpaka akapata ushindi huo mnono wa milioni 140.“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda mrefu sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama naweza kupata nafasi kama hii. Mimi ni mjasiriamali na ninapanga kutumia pesa nilizoshinda kuongeza mtaji wa biashara yangu” alisema Bi Nyani

  Bi Fatuma Bakari ambaye ni mama mzazi wa Nyani aliishukuru Tatu Mzuka kwa kuja na kampeni ya ‘Wiki Maalumu ya mama’ ambayo imemfanya akabustiwa kwa pesa nyingi baada ya mtoto wake kushinda.“Mimi pia nitatumia pesa nilizobustiwa kuwabusti ndugu wengine na kufanya shughuli za maendeleo ili kuboresha hali ya maisha ya familia yangu.” Alisema Bi Fatuma

  Maganga alimalizia shughuli kwa kutoa dondoo ya kampeni mpya ilioanza leo – Mzukapaswedi. “Na hapa kinachohitajika ni namba zako 3 tu!! Za Bahati, ambazo zitakufanya ufikie mafanikio yako,iwe ni kuongeza elimu,kununua gari,kujenga frame za maduka, kuwekeza kwenye kilimo, nk, fanikisha matunda ya mzuka-paswedi yako kwa ushindi wa laki 1 hadi millioni 6 kila saa.
  Ushindi wa millioni 10 katika mzuka deile leo saa tatu na nusu usiku, na ushindi wa millioni 60, jumapili hii kuanzia saa 3 na nusu usiku, tuma 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na neno mzukapaswedi kutoka 3mzuka, ukishinda Tanzania inashinda...

  0 0

  Balozi wa Tanzania Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. Pamoja na Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.
  Kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatikani, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.
  Mabalozi wengine waliowasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi Retšelisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,  na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia. 
  Baada ya uwasilishaji hati, pia Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuia ya Watanzania wa Vatican. Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

   Balozi Dkt. Possi akikabidhi hati za utambulisho kama Balozi wa Tanzania Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis.
   Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
   Balozi Dkt. Possi katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Wengine ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdul Mhinte, na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana.
  Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Picha kwa hisani ya Vatican

  0 0


  Meza Kuu wakiimba wimbo wa taifa.

  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, ambao ndio wadhamini wakuu wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akiwasalimia washiriki wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam.

  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akitoa mada wakati wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika (African Women in The 4 Industrial Revolution in Tanzania) lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akitoa mada katika Kongamano hilo.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

  Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akitoa mada katika Kongamano hilo.

  Baadhi ya washiriki.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akimpongeza mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' baada ya kutoa mada katika kongamano hilo.

  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba sambaba na Ally Kiba.

  Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba sambaba na msanii wa Bongo Fleva Ally Kiba 'King Kiba'.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada katika kongamano hilo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, akitoa mada katika kongamano hilo.
  Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Azania Bank, Jackson Lohay (katikati), akifuatilia kongamano hilo pamoja na maofisa wa benki hiyo.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudensia Kabaka (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba yake wakati wa kongamano hilo.
  Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Amina Salum Ali, akisoma hotuba yake.

  Mmoja wa washiriki wa Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyati (katikati), alipotembelea banda la benki hiyo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa benki hiyo, Diana Balyati (kulia) alipotembelea banda la benki hiyo katika kongamano la 'Africa Reconnected Forum'.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Modester Maziba (kushoto), na kulia ni Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyati, kabla ya kuanza Kongamano la Kuwainua Wanawake Kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na benki hiyo.

  BENKI ya Azania imesema imedhamiria kuwasaidia wanawake katika kipindi hiki cha mapinduzi ya uchumi wa viwanda kwa kuwapatia mikopo mikubwa, ya kati na midogo kwa riba naafuu.

  Akizungumza jijini Dar es salaam katika kongamano la kuwainua wanawake kuelekea katika Mapinduzi ya nne ya viwanda barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' Mkurugenzi Mtendaji wa Azania ambao ndio wadhamini wakuu wa kongamano hilo Charles Itembe alisema wanawake ni kundi muhimu katika kufikia uchumi wa viwanda.

  Alisema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na kukabiliana na hali ya soko ilivyo wameshusha riba za mikopo kwa wafanyabiashara hao.

  "Benki nyingi sio sisi tu zimeshusha riba za mikopo hii ni kutokana na hali ya soko, na huenda zikaendelea kushuka hadi pale itakapoonekana imekuwa sawa kulingana na Benki yenyewe" alisema Itembe.

  Aidha alisema Benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake wanaojihusiha na kilimo kwani kilimo ndio kinategemewa katika kuzalisha malighafi za viwandani na kuongeza kuwa kikitumiwa vizuri uchumi wa kati utafikiwa kwa wakati.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Blogu ya jamiii

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Afrika Mashariki ya kuhifadhi Koraan yanayotarajia kufanyika Uwanja wa  Sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa leo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakati anazungumzia uwepo wa mashindano manne ya kuhifadhi Koraan ambayo yatafanyika kwa nyakati tofauti katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Sheikh Alhad amefafanua katika kipindi hiki cha Ramadhan katika Mkoa wa Dar es Salaam kutakuwa na mashindano manne ya kuhifadhi Koraan na kueleza Mei 20 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kuhifadhi Koraan kwa Afrika Mashariki na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa.

  Mbali ya Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi pia anatarajiwa kuwepo Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Al-Manahilul Islamic Centre.

  Pia Mei 26 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Koraan yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Suluhu Foundation yanayotarajia kufanyika Mnazi Mmoja jijini.Mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi pamoja na viongozi wengine kadhaa.
  Sheikh Alhad ameongeza Mei 27 mwaka huu yatafanyika mashindano yatakayohusisha Bara zima la Afrika na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Alhakim Foundation wakati Juni 3 mwaka huu yatafanyika mashindano mengine ya kimataifa yaliyoandaliwa na taasisi hiyo na mgeni rasmi bado haijafahamika atakuwa nani.

  Amefafanua mashindano hayo yanafanyika mwezi wa Ramadhan ni kutokana na ubora wa mwezi huo kwani ndio Koraan Tukufu iliteremshwa na kufafanua kijana wa Kiislamu anayehifadhi Koraan husaidia kuishi kwenye misingi ya maadili mema kwani atakuwa anajua nzuri na baya.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Duka jipya na la kisasa la Halotel lililoko Kinondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni, ambalo litawawezesha wateja wa Mtandao huo walioko maeneo ya Mikocheni, Msasani na maeneo jirani na hayo kupata huduma mbalimbali kama kusajili laini mpya, huduma za kifedha,kurejesha namba iliyopotea,vifaa vya mawasiliano na huduma nyingine nyingi kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

  002: Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Duka jipya na la kisasa la Halotel lililoko Kionondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni, ambalo litawawezesha wateja wa Mtandao huo walioko maeneo ya Mikocheni, Msasani na maeneo jirani na hayo kupata huduma mbalimbali kama kusajili laini mpya, huduma za kifedha,kurejesha namba iliyopotea,vifaa vya mawasiliano na huduma nyingine nyingi kwa urahisi na kwa gharama nafuu
  Burudani ikitolewa mara baada ya uzinduzi wa duka hilo jipya na la kisasa la Halotel lililopo Kionondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni,jijini Dar

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi Mdogo wa ofisi ya Mkoa.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akiitoa katika uzinduzi rasmi wa kamati hiyo.
  Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour akizungumza wakati wa kikao hicho.
  Wakuu wa wilaya za Siha,Onesmo Buswelu(kushoto)  ,Wilaya ya Same Rosemery Senyamule(katikati)  na Aron Mbogho wa wilaya ya Mwanga wakiwa katika kikao hicho ambao wao pia ni wajumbe  
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa huo.
  Mkuu wa wilaya ya Siha,Onesmo Buswelu akichangia jambo wakati wa kikao hicho cha uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa wa Kilimanjaro.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro iliyozinduliwa rasmi .

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
   

  serikali mkoani Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za kisekta za serikali za mitaa.  Mbali na majukumu hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za mkoa kwa kushirikiana na wakala.  Akizindua kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na kuwajibika ipasavyo.  “Sheria hii inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa “alisema Mghwira.  Mghwira alitoa maelekzo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kamati za maafa za wilaya ,kata na vijiji zinaundwa na kusimamiwa ili zitekeleze majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa sheria hiyo huku akiwaagiza wakulurugenzi kuwawezesha wakuu wa wilaya kuandaa utaratibu wa kutoa maelekezo kwa kamati a wilaya ,kata na vijiji .  “Hakuna haja ya kusubiri maafa yatokee ndiyo tufanye maandalizi ,tuanze sasa,kwa taarifa nilizonazo mvua bado zinaendelea ,twendeni katika maeneo yanayotuzunguka kutoa tahadhari za awali kwa wananchi wote wanaooonekana kupata madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha”alisema Mghwira.

                                              

  Mwisho.

  0 0

   Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Gladys Mtandila kutoka Makumbusho, Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha leo ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promoshen hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00#
   Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Ramadhan Ali  Ngolozi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha leo ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .
   Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Sakina Kassanga, askari polisi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha leo ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# 
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni iliyoisha leo ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo ilitoa simu janja 1,080 kwa wateja wake, pamoja na bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wote walionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .

  0 0


  0 0

    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea kabla ya kukabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. Wanaomsikilia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widson Mandarasi Mwanangwe. Msaada huo ni pamoja na tani 4.8 za mchele, tani 4.8 za Unga wa mahindi, tani 2.8 za sukari pamoja na tende
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. wanaoshuhudia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widson Mandarasi Mwanangwe. 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsikiliza Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga akishukuru baada ya kumkabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. wanaoshuhudia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widsob Mandarasi Mwanangwe. 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga na askari wengine waliofika kupokea vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. 
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana  na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga baada ya kukabidhi  vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. 


  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na  Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widsob Mandarasi Mwanangwe,  baada ya kumkabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018.  
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na asklari wanawake waliofika kupokea vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018.  
  Picha na IKULU 

older | 1 | .... | 1583 | 1584 | (Page 1585) | 1586 | 1587 | .... | 1898 | newer