Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1581 | 1582 | (Page 1583) | 1584 | 1585 | .... | 1898 | newer

  0 0  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu atatumia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli au kazi siziso na malipo kwa manufaa ya jamii.

  Lulu ambaye ameachiliwa Mei 12 mwaka huu (Jumamosi)anakwenda kutumia kifungo chake nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania na sababu za kutumia kifungo hicho nje kumetokana na kukidhi vigezo vya kisheria na kuonesha tabia njema akiwa gerezani.

  Taarifa ya Jeshi la Magereza iliyotolewa leo jijinni Dar es Salaam imeeleza Aprili  26 mwaka huu katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1) ya Katiba alitoa msamaha wa 1/4 ya adhabu kwa wafungwa wote waliokuwa na sifa za kunufaika na msamaha huo.

  "Kutokana na msamaha huo Lulu alinufaika na msamaha huo

  na Mei 12 mwaka huu ametolewa gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania,"imesema taarifa ya Jeshi la Magereza.

  Hata hivyo licha ya sheria kuelezea kuwa Lulu anatakiwa kufanya shughuli za kijamii bila malipo yeyote haijaweka wazi ni kazi gani ambayo atakwenda kuifanya baada ya kuwa nje.

  Lulu kabla kabla ya msamaha huo alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kupokelewa gerezani hapo Novemba 13 mwaka 2017.


  0 0

  Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) kwa mwaka fedha kuanzia 2015 hadi 2017.

  Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema halmashauri kupata hati ya mashaka kwa hoja zinazojibika na zinazojirudia kila mwaka ni uzembe wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.

  “Watumishi bado wapo wachache wanaofanya kazi kwa mazoea bila ya kufuata sheria na taratibu za kiutumishi”.Ameuwagiza uongozi wa halmashauri ya Longido kutoa barua za onyo kwa watumishi wote waliotajwa kwenye taarifa ya mkaguzi wa nje ili iwe fundisho kwa watumishi wote umma.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amesema ifike wakati sasa viongozi kutoonea huruma mtumishi yoyote anaebainika ana makosa, kwani hoja nyingi katika halmashuri hiyo zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka.Amesema hatua madhubuti ni lazima sasa zichukuliwe ili kudhibiti tabia hii ya mazoea ya hoja kujirudiarudia kila mala.

  Akisisitiza zaidi mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kazi ya viongozi ni kusimamia sheria na taratibu za kazi,hivyo ataendelea kusimamia sheria za utumishi wa umma katika halmshauri yake kwani mpaka sasa hali imeanza kubadilika kwa watumishi kuwa na nidhani.

  Aidha, amesema halmshauri ipo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa na kuhakikisha halmashauri yake haitapata tena hati ya mashaka kwa miaka inayokuja.Gambo yupo katika ziara ya siku 3 wilayani Longido ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa katika wilaya hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG.
  Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisoma baadhi ya hoja zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) katika kikao chake na watumishi wa halmashauri ya Longido.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Tabora na wilaya ya Nzega wakikagua eneo ambalo miundombinu ya barabara itapitishwa.
   Viongozi wakikagua eneo litakapojengwa daraja la Nhombola 
  Wananchi wakiwa upande wa pili wa mto katika eneo ambalo litajengwa daraja la Nhombola.
  ......................................................
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea wananchi wenye tabia mbaya ya kuiba vyuma vinavyo wekwa katika kingo za madaraja kwamba watakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

   Jafo ametoa onyo hilo alipokuwa wilayani Nzega mkoani Tabora alipokwenda kukagua aneo la Nhombola panapotarajiwa kujengwa daraja kubwa katika mwaka wa fedha 2018/2019.

  Daraja la Nhombola ni moja ya ahadi ya Rais John Magufuli ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga Sh.milioni 500 kupitia wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo.

  Akikagua eneo hilo, Waziri Jafo amesema baadhi ya watu wana tabia ya wizi wa vyuma ambavyo wanakwenda kuviuza kama vyuma chakavu. 

  Jafo amesisitiza kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hivyo wananchi wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo kwani inapo haribiwa wao ndio wanaotaabika. 

  Amemtaka kila mmoja awe mlinzi wa miundombinu inayogharamiwa na serikali yao.

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wa    Tanzania Health Summit wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa  hundi ya shilingi milioni moja fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa JKCI  kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni mama wa mtoto Asha Omary mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
  Rais wa  Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu. Kila mwaka  Tanzania Health Summit wanaandaa mashindano ya Heart Marathon lengo likiwa  ni kusaidia watoto wanaosumbuliwa na  magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.Picha na JKCI

  0 0

  Warsha hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga kwa ufadhili wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga imefanyika leo Jumatatu Mei 14,2018 katika chuo hicho mjini Shinyanga kwa kukutanisha walimu 100.Warsha hiyo ni sehemu ya Mpango Maalumu uliobuniwa na Chuo hicho kwa ajili ya kujenga uwezo watumishi wa umma hasa walimu juu ya masuala ya jinsia.

  Akifungua warsha hiyo,Matiro alisema mbinu stahiki za kupambana na ukatili wa kijinsia zitafanikiwa endapo dhana,aina,matokeo na sababu za ukatili zitaeleweka kuanzia ngazi ya msingi hususani shuleni ambapo watoto wanatumia muda mwingi wa maisha yao.“Niwapongeze sana kwa kuanzisha mpango huu wa kuwafikia walimu,warsha hii ni nyeti sana na huenda kuna walimu ambao walishawahi kushuhudia ama kutenda vitendo vya kibaguzi kwa watoto kwa kujua ama kutojua,kwa hali hii vitendo hivyo vina athari kubwa katika maendeleo ya kitaaluma kwa watoto”,alisema Matiro.

  Aidha alisema ni jukumu la walimu na shule kuweka kanuni na taratibu ambazo zitatoa ulinzi na kusaidia jamii nzima ya shule kuishi kwa amani na kuzingatia usawa.“Niwaombe msiishie kwa walimu pekee kutoa elimu hii,bali wafikieni pia watumishi wote wa umma kwani nao kwa sehemu yao wana mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii inayothamini usawa wa kijinsia”,aliongeza.

  Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa warsha hiyo.Kushoto ni Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho.Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo na kueleza kuwa kukosekana kwa usawa baina ya wasichana na na wavulana shuleni na katika jamii ni chanzo kikuu cha ukatili kitu kinachofanya ukatili kuwa suala la kijinsia.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyokutanisha walimu 100 kutoka shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
  Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho akizungumza wakati wa warsha hiyo ambapo alisema wameamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya masuala ya jinsia kwa walimu ili kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu kwa wanafunzi wao kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii.
  Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati akifungua mashindano ya Vijana ya Banda Cup kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo pia alitoa vifaa vya michezo kwa timu zote 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoa na viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na wachezai wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuizundua na kugawa vifaa vya michezo Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na wachezai wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuizundua na kugawa vifaa vya michezo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto akiingia kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipokwenda kuzindua mashindano ya Banda Cup na kugawa vifaa vya michezo kwa timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo kulia ni Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 ambazo zinashiriki michuano ya Banda Cup ikiwa ni mchango wake kusaidia mashindano hayo.

  Makabidhiano hayo yalifanywa kwa timu 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo wakati alipokwenda kuyafungua kwenye viwanja vya CCM mkwakwani mjini Tanga.Mashindano hayo yameanzishwa na Beki wa timu ya Baroka FC ya nchini Afrika kusini Abdi Banda akiwa na lengo la kusaidia kuinua vipaji vya soka na kuvikuza ili kuweza kuwa na hazina kubwa kwa siku zijazo.

  Akizungumza juzi wakati akikabidhi vifaa hivyo ambazo ni Jezi seti mojamoja kwa kila timu shiriki,Waziri Ummy alisema mchezo wa mpira wa miguu unaweza kuwasaidia vijana iwapo watazingatia na kujituma.Alisema pamoja na hayo lakini anampongeza muandaaji wake kwa kuona namna ya kuyaanzisha ili kuwasaidia kukuza vipaji vya wachezaji wachanga ambao baadae wataweza kusaidia kwenye soka letu.

  “Nimempongeza kwa moyo wake wa uzalendo na sio kwamba ana fedha nyingi sana lakini kile kidogo anachokipata ameona ashirikiana na watuwa Tanga hivyo nasi tutahakikisha tunashirikiana naye”Alisema.Hata hivyo Waziri huyo alisema licha ya kutoa vifaa hivyo lakini atatoa fedha kwa Mfungaji bora 100,000, mwamuzi bora 100,000, timu yenye nidhamu 200,000, mlinda mlango bora 100,000 huku mchezaji bora akitoka na 100,000.

  Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Ummy,Mratibu waMashindano Ibrahimu Kidiwa alisema katika mashindano hayoyanashirikisha timu 16 ambapo mshindi wa kwanza atapata.sh.500,000,mshindi wa pili atapata 250,000,mshindi wa tatu atapatash.100,000 na mipira miwili (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wananchi wa wilaya ya Mkalama iliyopo mkoani Singida kushikamana ili kuinua wilaya yao kimaendeleo.

  Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia umati wa wananchi wa wilayani hiyo katika shughuli za uzinduzi wa wiki ya elimu inayofanyika wilayani Mkalama.Jafo amebainisha kwamba wilaya ya Mkalama ilikuwa wilaya ya mwisho katika matokea ya darasa la saba ya mwaka 2017 hivyo wanapaswa kushikamana kuondoa aibu hiyo.

  Katika mkutano huo, amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo kwa kazi kubwa anayofanya ambayo imesaidia kusukuma maendeleo wilayani humo kwa kushirikiana vyema na serikali na kufanikisha miradi ya afya, maji, pamoja na elimu. Aidha amesema kwasasa serikali inaboresha kituo kimoja cha afya na pia anefanikisha  mpango kabambe wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo imepangwa kujengwa katika bajeti ya 2018/2019.

  Kadhalika, Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama kumwita mkandarasi aliyejenga jengo la halmashauri ambaye ni Kampuni ya Mzinga kurudi haraka ndani ya wiki ijayo ili arekebishe maeneo yenye dosari.Pamoja na hayo, Jafo amesisitiza watumishi wote kuwa waadilifu kwani Ofisi yake anayoiongoza haiwezi kuvumilia ufisadi, wizi, uzembe, na ubabaishaji kazini.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na viongozi na wananchi wa wilaya ya Mkalama.
  Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimtembeza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye vikundi mbalimbali vya burudani.
  Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimkaribisha Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kuzungumza katika uzinduzi wa wiki ya elimu.
  Jengo la Halmashauri ya Mkalama ambalo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameagiza lifanyiwe marekebisho.
  Baadhi ya vikundi vya burudani vikitumbuiza katika uzinduzi wa wiki ya elimu wilayani Mkalama

  0 0

  Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara Mhandisi MEDRAD MMOLE amesema kukosekana kwa vibarua kumepelekea kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo unaofanywa na kandarasi ya Suma JKT.

  0 0  0 0


  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii 

  KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua kifurushi kisichokuwa na ukomo wa muda kitakacho wawezesha wateja wa mtandao huo kuwasiliana bila kikomo kupitia kifurushi kabambe cha Super Halo.

  Wateja wa mtandao wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho wataweza kupiga simu au kutumia intaneti hadi pale vifurushi vitakapokwisha muda wa matumizi.

  Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda amesema kuwa, uzinduzi huo wa vifurushi vya Super Halo ni mapinduzi mengine makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuondoa ukomo wa muda katika vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti.

  Amesema kama kampuni wamedhamiria kuwafurahisha wateja Kwa huduma kabambe za mawasiliano bila ya kuwa na wasiwasi wa kuisha kwa muda wa matumizi ya mawasiliano. Pia ameeleza kuwa mteja wa Halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia shilingi 500 na kupata dakika 17 za kupiga Halotel bila kikomo cha muda na kwa shilingi 500 na kwa 500 hiyo hiyo mteja anaweza kujiunga na kupata MB 110 za intaneti za kutumia bila kikomo. 

  Ameeleza lengo kubwa la kifurushi hicho ni kumwezesha mteja kuona thamani ya pesa yake na kuweza kufurahia mawasiliano ya kupiga simu na kutumia MB za intaneti bila kikomo.
   Baadhi Wateja wa Mtandao wa Halotel  wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyo vinavyouzwa na kampuni ya simu ya  Halotel mara baada ya uzinduzi huo.
   Afisa Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala  akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Milimani City jijini Dar es  Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza katika uzinduzi wa kifurushi kisichokuwa na ukomo kilichopewa jina na Super halo katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar as Salaam.

  0 0


  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Asaad (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro (kulia)wakifurahia jambo wakati aliokuwa kimsindikiza mara baada Katibu Mkuu huyo kufungua mkuatano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya CAG uliofanyika mjini Dodoma leo.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika mjini Dodoma leo .

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
  Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Musa Asaad akitoa taarifa ya Ofisi yake wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya CAG lililofanyika leo jijini Dodoma .
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.

  wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Juma Assad amesema ofisi yake imefanikiwa kutoa taarifa kwa wakati, kila inapofika Machi 30 ya kila mwaka licha ya kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti.

  Profesa Assad ameeleza hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambao unalenga kupitisha bajeti ya mwaka na kujadili masuala ya kiutendaji ambayo yanawasilishwa na kuitishwa na wajumbe.

  Akizungumza katika mkutano huo, CAG amesema ufinyu huo unaosababisha shughuli za kiofisi kutofanyika pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya dharula yanayoibuka nje ya ukomo wao wa bajeti.“Baraza hii limekuwa na ufanisi mkubwa katika kusimamia majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba,”amesema Prof. Assad

  Amesema pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo ofisi hiyo imeyapata, bado zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili na zinahitaji utatuzi wa kina.Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kushindwa kukamilisha ujenzi kwa ajili ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa kutokana na kutotolewa kwa fedha za maendeleo kama ilivyopangwa na kwa wakati.

  Aidha amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2017/18 hadi kufikia Machi, 2018 Ofisi ilishindwa kuwajengea uwezo watumishi kulingana na viwango vya kimataifa vya ukaguzi kutokana na ufinyu wa bajeti.“Kuna changamoto ya mwenendo wa upatikanaji wa fedha za matumizi mengineyo na maendeleo kutoka mfumo mkuu wa serikali kutoendana na mahitaji halisi ya majukumu ya Taasisi hususani ukaguzi na mafunzo kwa watumishi,”amesema.

  Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro ameitaka ofisi ya Taifa ya ukaguzi kutekeleza agizo la serikali kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.Dk. Ndumbaro amesema tayari viongozi mbalimbali wa serikali walishahamia, hivyo ni mategemeo yake kuwa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi nayo pia ipo katika mkakati wa kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma kama ambavyo taasisi nyingine zimefanya.

  0 0


  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amepokea mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya Sh.milioni tatu kutoka Shirika la Bima la Taifa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.

  Akizungumza na Michuzi blog, Ulega ameeleza leo kuwa mifuko hiyo ya saruji itatumika itatumika katika ujenzi wa zahanati katika vijiji mbalimbali kama Kibamba, kazole, Yavayava na Mkanonge wilayani humo.

  Ulega amesema kuwa kazi hiyo ni ya wote katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli na kuifikisha Tanzania mbele zaidi na kusisitiza ujenzi wa miundombinu hasa ya madarasa na zahanati unaendelea katika vijiji mbalimbali na hiyo ni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi.

  Aidha Ulega amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia Wilaya ya Mkuranga kwa ujenzi wa shule na zahanati.

  Kwa upande wa Meneja Masoko wa Shirika la bima la taifa Elisante Maleko ameeleza utoaji wa mifuko hiyo ya saruji ni kutokana na uhusiano mzuri baina yao, hivyo wakaona faida wanayopata kutoka kwa wananchi hao ambao ni wateja wazuri ni kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa na zahanati katika vijiji mbalimbali vya Mkuranga.

  Mkurugenzi wa Shirika hilo tawi la Ubungo Segeja Mabulla amemshukuru mbunge na mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwakutanisha na kutoa elimu ya kuwasaidia wananchi kuhusu masuala ya bima.Pia amewapongeza wakazi wa Wilaya hiyo kwa kuwa wateja wazuri wa bima za halmashauri na bima za maisha.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea mifuko 200  saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima la Taifa,Elisante Maleko yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya zahanati na madarasa leo mkoani Pwani.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea kava la tairi la gari kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima Taifa,Elisante Maleko  leo mkoani Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na  Mbunge wa Mkuranga  Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

  0 0  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani umekaribia ambapo Waislamu wote nchini na duniani wanatarajiwa kuanza kufunga. Mwezi huu muhimu kiimani huchukuliwa kama kipindi cha toba ambapo waumini hufunga kwa kujinyima kula, kufanya ibada pamoja na kufanya matendo mema na ya huruma katika kipindi chote cha mfungo. 

  Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa Ramadhani, Jumia Travel imekukusanyia mambo yafuatayo ya kufanya ndani ya kipindi hiki ili kukurahisishia kufanikishia mfungo wako. 

  Kamilisha funga zako. Mafundisho yanawataka waumini wafunge kwa imani na kwa moyo wote ili kupata thawabu kutoka kwa Mungu, ikiwemo dhambi zao kusamehewa. Kuna faida kubwa za kufunga ambazo zinatarajiwa baada ya kuisha kwa mfungo. Kwa hiyo, endapo utafunga hakikisha unafunga kwa moyo wote na dhamira ya dhati moyoni ili uje ulipwe kwa matendo yako. 

  Fanya matendo yatakayompendeza Mungu. Lengo kuu la Ramadhani ni kurudisha imani kwa mwenyezi Mungu kwa kuachana na anasa za dunia. Mfungo, kiasilia, utakusaidia kuyafanikisha hayo lakini utafanikiwa zaidi kwa kuyachunga matendo yako hususani yale yasiyompendeza muumba wako. Ni vema katika kipindi hiki kuwa unajikumbusha mara kwa mara kipindi chote cha mfungo, kwa kufanya hivyo utaogopa kutenda au kufikiria maovu. 

  Soma Quran. Ramadhani ni mwezi wa Quran. Itakuwa haujaitendea haki na ni kazi bure kama hautokisoma kitabu hiki kitukufu. Hii hapa ni njia rahisi unayoweza kuifuata. Kwa kuwa utakuwa unafunga, maana yake utakuwa huru muda wa chakula cha mchana. Utumie muda huo kusoma. Kama hauna kitabu, mambo yamerahisishwa kupitia teknolojia siku hizi. Unaweza kupakua programu ya simu ya mkononi na kujisomea. Hii ni njia rahisi na inayowezekana ya kujisomea Quran. 

  Chunga ulimi wako. Njia mojawapo rahisi inayoweza kuharibu funga yako ni kwa kujihusisha na umbeya na maongezi yasiyompendeza Mungu. Mwenyezi Mungu hamuhitaji mtu ambaye hataki kuachana na mienendo yake miovu katika kipindi cha mfungo. Hivyo basi, kwa mwaka huu, jitahidi kwa kadri uwezavyo kukaa mbali au kujiepusha na maongezi ambayo yatakupelekea kumkosea muumba wako. 

  Toa msaada. Mtume Muhammad (SAW), alikuwa akijulikana kama mtu mwenye ukarimu wa hali ya juu, lakini kipindi cha mwezi wa Ramadhani ukarimu wake uliongezeka kupita kiwango. Ramadhani inakupatia fursa pekee ya kuongeza moyo wako wa kujitolea ili kujiongezea thawabu zaidi. Kwa kuongezea, utakuwa unafanya kama vile alivyofanya mtume wa Mungu. Kwa hiyo, hakikisha unawasaidia watu mbalimbali wasiojiweza na kuhitaji msaada katika kipindi hiki cha mfungo. 

  Ramadhani ni kipindi muhimu cha kujitafakari kiimani, kujiimarisha na kujitoa kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Jumia Travel ingependa kuwatakiwa Waislamu wote maandalizi ya mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuyazingatia mafundisho na yale yote yaliyoagizwa ili kumaliza salama.

  0 0

  Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (kushoto) akiwapokea wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Nchini Uganda waliotembela Wizara kuona ubora wa miradi ya Benki ya Dunia inavyotekelezwa.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu (kulia) akiwa na mjumbe wa Kamati hiyo toka Uganda wakifuatilia kikao na Naibu Waziri wa Tamisemi(hayupo pichani) Mhe. Joasephat Kandege.
  Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akifurahia jambo wakati wa kikao cha Mapokezi ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.
  Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP
  Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP

  …………….

  Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam.

  Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.

  Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka Benki ya Dunia;

  “Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.

  Akipokea ujumbe huo toka Bunge la Uganda Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema mradi huu umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwapunguzia kero wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.

  “Karibu mjifunze kwa kuona mtaona barabara zilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu, njia za bora waenda kwa miguu, mifereji yenye viwango ya kusafirishia maji ya mvua, masoko na ofisi za miradi pamoja na maabara za kisasa za kupima ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa “ alisema Kandege.

  Akielezea Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za Mkopo wa Benki ya Dunia Mratibu wa Miradi hiyo toka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Davis Shemangale amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na unalengo la kuboresha Jiji la Dar es salaam lizidi kuwa bora katika Sekta ya miundombinu, usafiri mjini pamoja na usalama

  Eng. Shemangale aliongeza kuwa mradi huo pia utaboresha makazi bora sambamba na kujenga uwezo wa Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza kumbukumbu na takwimu itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato.

  Naye mratibu wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP) Eng. Emmanuel Ndyamukama amesema Katika awamu ya kwanza ya mradi huu itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aidha Shirika la maendeleo la Nchi za Nordic litatoa ruzuku ya dola za kimarekani Mil. Tano kwa ajili ya kukabili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na huku Serikali ya Tanzania ikichangia takribani Dola za Kimarekani Mil. 25.3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi walioathirika na mradi.

  Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa iko katika ziara ya mafunzo kwa muda wa siku Tano na itatemebela miradi ya uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP), Mabasi yaendayo haraka (BRT) kasha kuelekea katika Manispaa ya Morogoro ambako watatembelea mradi wa uboreshaji na uimarishaji wa Mamlaka za Miji (ULGSP) kasha kumalizia na Jiji la Dodoma ambako watajione mradi wa Uboreshaji Miji Kimkakati (TSCP).

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira (katikati) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof, Faustine Bee ( mwenye tai) alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya tukio la Career Day ,tukio ambalo Mghwira alikuwa mgeni rasmi .
  Baadhi ya Wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria tukio la Career Day lililofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere ,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa tukio la Career Day alipoalikwa kuwa mgeni rasmi ,tukio hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) 
  Baadhi ya Wananfunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof,Faustine Bee akizungumza katika tukio hilo .
  Baadhi a wanafunzi wa MOCU
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala na Fedha wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MOCU) Prof Freddy Kilima akizungumza wakati wa tukio la Career Day .
  Baadhi ya Wageni walioalikwa kushiriki tukio la Career Day kutoka nchini Sweden .
  Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MOCU) Nalemuta Ngoitiko akizungumza katika tukio hilo.
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Taaluma Prof,Alfred Sife akitoa neno la shukrani wakati wa tukio la Career Day lililoandaliwa na serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
  Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alipata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma fani mbalimbali katika chuo kikuu cha Ushirika ,Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Pro Faustine Bee wakifurahia kazi ya Sanaa ya uchoraji iliyofanywa na mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa Shahada ya Sheria katika chuo hicho ,Omega Lyimo 
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Prof Faustine Bee ni kama aamini baada ya kuona picha yake iliyochorwa na Mwanafunzi Omega Lyimo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tukio la Career Day,Onesmo Mbisse akikabidhi zawadi ya T shirt zenye nembo ya chuo hicho kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira .
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tukio la Career Day,Onesmo Mbisse akikabidhi zawadi ya T shirt zenye nembo ya chuo hicho kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Prof Faustine Bee.  Na Dixon Busagaga,Moshi 

  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Prof, Faustine Bee ameshauri kuanzishwa kwa ujasiliamali wa Kiushirika utakao saidia wahitimu wa vyuo vikuu nchini kujipatia kipato na kuongeza kasi ya ukuzaji wa Uchumi kabla ya kupata ajira ya kudumu.

  Katika maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo ,Prof Bee alitolea mfano, moja ya changamoto zilizopo kwa baadhi ya vyama vya ushirika kwa kukosa wataalamu wa kuweka vizuri hesabu ya vitabu vyao.

  “Pamoja na juhudi hizi binafsi za kwenda kutengeneza ajira na kuanzisha ujasiliamali wa mtu mmoja mmoja ,ni vema sasa tuone namna ambavyo tutaanzisha ujasiliamali wa kiushirika kwa maana wahitimu wa chuo kikuu wanapo maliza waende kuanzisha vyama vya ushirka vya aina tofauti.”alisema Prof Bee.

  “Kuna vyama vina shida ya uandishi wa hesabu wa vitabu vyao ,tupate ambao watakuwa wakifanya kazi hiyo na watakuwa wakijipatia pesa,lakini pia wapo wengine ambao wangeweza kuanzisha vyama vya ushirika vya aina tofauti ,vya fedha, vya mazao ,vya uvuvi, ili mradi viongeze kasi ya ukuzaji wa uchumi wetu na pia kutengeneza ajaira kwa atu wengine .aliongeza Prof ,Bee.

  Maadhimisho ya siku hii yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo yalitanguliwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kuuzwa na wanafunzo wa chuo hicho pamoja na uwasilishaji wa mada ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akaikumbusha menejimenti ya chuo sehemu ya wajibu wa chuo.

  “Katika kujenga na kuimarisha fani ya ushirika ,Chuo Kikuu hiki cha ushirika ndicho kingekuwa kioo chetu ,kila siku tunasema tukitaka kuzungumza na wana ushirika twende Chuo Kikuu cha Ushirika ,tupate taarifa sahihi kutoka chuoni ,tupate taarifa za uchambuzi mzuri ,za tafiti mbalimbali kuhusiana na mazao mbalimbai yanayounda ushirika”alisema Mghwira .

  Katika tukio la “Career Day” linalofanyika chuo kikuu cha Ushirika Moshi kila mwaka huku likiwakutanisha wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao ya elimu ya Juu pamoja na waajiri kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wahitimu wakizilinganisha na masomo waliyojifunza.

  Tukio la Career Day huandaliwa na serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu mkuu wa chuo hicho ,utawala na fedha kwa lengo la kuwaonyesha waajiri shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi hao zikiambatana na masomo yao .

  0 0


  Na Editha Karlo wa blog ya Jamii,Kigoma

  WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za Taifa mbalimbali zilizopo nchini ili kuweza kujionea urithi na vivutio adimu vilivyopo kwenye hifadhi hizo.

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga aliyasema hayo leo wakati warsha ya siku moja ya wadau mbalimbali wa Mkoani Kigoma wa Hifadhi ya milima ya mahale kilichokuwa kinajadili mpango kabambe wa miaka kumi wa kuendeleza hifadhi ya Taifa ya mahale.

  Alisema katika Mkoa wa kigoma tumepata bahati ya kuwa na hifadhi mbili za Taifa ambazo ni hifadhi ya Taifa ya milima ya Mahale na Hifadhi ya Taifa ya gombe hivyo lazima juhudi za kutangaza hifadhi hizo ziongezeke.

  "Tunajua Hifadhi ya mahale inachangamoto ya usafiri wa kufika kule kwani ili kufika inakulazimu kusafiri kwa njia ya maji kwa muda mrefu kutumia boti za kawaida,tunaomba mtuwekee speed boti, ila TANAPA mnafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watalii wanaweze kufika Mahale kwa njia ya barabara"alisema Maganga

  Maganga alisema kuwa mtu mmoja anapotembelea hifadhi ni sawa na watu kumi wametembelea kwani akitoka huko anakuwa balozi wa wengine.Mkuu huyo wa Mkoa alisema pia kupitia sekta ya utalii lazima iendane na kauli mbiu ya serekali ya sasa ya Tanzania ya viwanda."Hawa watalii kutoka nchi mbalimbali wanaokuja kutembea vivutio vyetu pia huwa wanaangali wapi pa kuwekeza tutumie fursa hizo za kuwashawishi waje kuwekeza nchini"alisema

  Naye Ahmed Mbugi meneja wa ujirani mwema wa hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la hifadhi la Taifa(TANAPA)Allan Kijazi amesema kuwa ili mpango huo uweze kufanikiwa wamekusanya maoni mbalimbali ya wadau kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa na leo maoni hayo wanayawasilisha kwa wadau mbalimbali kupitia warsha hiyo.

  Mbugi alisema kuwa wao kama shirika wanajitahidi mahitaji yote muhimu yanapatikana kwa wageni wanaoenda kutembelea hifadhi.Alisema Hifadhi ya milima ya mahale inachangamoto ya usafiri ambapo miundombinu ya barabara ya kwenda huko haikuwa rafiki hapo awali lakini sasa hivi toka barabara itengenezwe watalii wameongezeka kwenda mahale.

  Alisema kupitia mpango huo kabambe wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale ambao umewashirikisha wadau wa ngazi zote baada ya miaka kumi hifadhi ya milima ya mahale ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba hifadhi hiyo.
   Picha ya pamoja baina ya wadau mbalimbali wa utalii wa Mkoa wa Kigoma na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga muda mfupi baada ya kuzindua warsha ya kujadili mpango kabambe wa miaka 10 wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa utalii wa Mkoa wa kigoma inayojadili mpango kabambe wa miaka 10 ya  kuendekeza hifadhi ya Milima ya Mahale
   Meneja wa ujirani wa hifadhi ya milima ya Mahale, Ahmed Mbugi akielezea hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwenye kikao cha wadau wa utalii wa kuendeleza hifadhi ya Mahale
   Wadau wa utalii wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika warsha ya siku moja ya kupitisha mipango kabambe ya miaka 10 ya kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale

  0 0

  .Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo amesikitishwa na gharama kubwa iliyotumika katika ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Endasak.

  Ameyasema hayo wakati akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak leo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.Amesema hajaridhishwa na gharama kubwa iliyotumika ya shilingi milioni 175.6 ya ujenzi wa Bweni moja wakati katika maeneo mengine fedha hizo hutumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni mawili.

  "Inasikitisha sana kuona dhamani ya jengo lililojengwa haliwndani na fedha Ilizotolewana Serikali" Anasema Jafo.Amewataka viongozi w halmashauri kusimamia miaradi ya maendeleo kwa weledi na umakini mkubwa ili iendane na dhamani ya fedha zinazotolewa na Serikali.

  Wakati huohuo, Mkuu wa Shule ya Endasak Mwl. Gisera Msofe amemueleza Mhe.Jafo kuwa Ujenzi wa bweni la wanafunzi wa shule hiyo umegharimu shilingi bilioni 170.6@ na mradi huo unatekelezwa kwa njia ya" Force Account"

  Aidha ameishukuru Serikali kwa utoaji wa elimu bila malipo na ujenzi wa bweni kwa kuwa wanafunzi wengi wanapata elimu bila kuchangia na kuongeza hamasa kwa wazazi kusomesha watoto.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akizungumza katika ukaguzi wa bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
  Bweni la shule ya sekondari Endasak
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Endasak

  0 0

  Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa siku ya Jumatano ya Mei 9, imetimiza mwaka mmoja tangu ilipoanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini.SportPesa ambayo imeanzia nchini Kenya mwaka 2014, iliingia Tanzania kwa kishindo ikiwa imejidhatiti katika kusaidia kukuza sekta ya michezo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.Katika kutimiza azma yake, SportPesa ilianza kwa kutoa mchango wa Shilingi Milioni 50 kusaidia maandalizi ya timu ya Serengeti Boys iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya vijana ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon mwaka jana.

  Baada ya hapo SportPesa iliendelea kuiteka sekta ya michezo nchini kwa kuingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na vilabu vikongwe vya Simba na Yanga pamoja na mkataba wa mwaka mmoja na Singida United.Udhamini huo ulishuhudia vilabu vya Simba, Yanga na Singida United vikishiriki michuano mipya ya SportPesa Super Cup ambayo ilikuwa na lengo na kumpata mshindi mmoja atakayechuana na klabu ya Everton.


  Kwa takribani wiki moja (kuanzia Juni 5-11), uwanja wa Uhuru ulifurika mashabiki lukuki waliokuja kushuhudia ladha ya michuano hiyo ambayo pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars kutoka Kenya sambamba na Jang’ómbe kutoka Zanzibar vikitoana jasho kuzisaka zaidi ya Shilingi Milioni 60.

  Ziara ya Everton
  Sote ni mashahidi jinsi SportPesa ilivyojitoa mhanga kuileta nchini klabu ya Everton ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya EPL kutembelea Tanzania na hivyo kuitangaza vyema nchi yetu kimataifa.Sahau kuhusu mashabiki waliofurika uwanja wa Taifa Julai 13 kumshuhudia Wayne Rooney akivaa uzi wa Everton kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya Gor Mahia, lakini sote ni mshahidi jinsi ziara ile ilivyoleta manufaa makubwa.
  Tunakumbuka jinsi sekta ya utalii ilivyonufaika ambapo Balozi wa Everton, Leon Osman alipata fursa ya kutembelea Kreta maarufu ya Ngorongoro bila kusahau jinsi uwanja wetu wa taifa ulivyoweza kurekebishwa kwenye sehemu ya kuchezea na vyumba vya kubadilishia nguo ili kufikia viwango vya kimataifa kwa Everton kuweza kuutumia.Lakini pia hatuwezei kuzisahau semina za uongozi wa Soka zilizotolewa na wataalam wa Everton kwa viongozi wetu wa soka bila kusahau kliniki za soka za vijana na misaada mbalimbali ya kijamii waliyotoa kwa wale wenye uhitaji.

  Bajaji 120 Achilia mbali sekta ya michezo, lakini SportPesa pia imefanya promosheni za aina yake zilizokuwa na lengo ka kuinua kipato cha mtanzania mmoja mmoja.Shinda na SportPesa” ilikuwa gumzo kwa zaidi ya siku 170 kuanzia Oktoba mwaka jana ambapo watanzania 120 waliweza kujishindia bajaji mpya aina ya TVS KING kila siku, kila wiki.Ama hakika familia 120 zina neno la shukrani kwa SportPesa kutokana na uwezeshaji ule ambao tumeshuhudia jinsi ulivyotoa ajira kwa vijana wa kitanzania.

  Sio rahisi kuilezea SportPesa kwa Makala moja kwani mambo ambayo wamefanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ni mengi na makubwa.Kwa niaba ya wapenda michezo wote nchini, tunapenda kuitakia kampuni ya SportPesa Heri ya maadhimisho ya mwaka mmoja na hakika hatutaweza kuisahau ziara ya Everton kwani ilimfumbua macho kila mmoja wetu na kuona kuwa kila jambo linawezekana kama tukiweka nia.

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kufunga mashine ya kisasa ya utasishaji taka ambayo itapunguza uchomaji wa taka za plastiki ambazo zina madhara kwa binadamu Mashine hiyo yenye thamani ya Dola Laki moja imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) hivyo Hospitali ya Taifa Muhimbili itakua hospitali ya kwanza ya Umma kuwa na mashine hiyo. 

   Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni kutoka UNDP ambao umekuja kwa lengo la kukagua utekelezwaji wa mradi wa mazingira , Mkuu wa Idara ya Mazingira MNH Muhandisi Veilla Matee amesema mashine hiyo itafungwa wiki hii na wiki ijayo itaanza kufanya kazi na kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuja kununua malighafi ambayo hutumika kutengeneza vifaa vya plastiki. 

   ‘’ Tumepokea mashine ya utasishaji kutoka UNDP na mara baada ya kufungwa mashine hiyo tutatoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo watendaji wetu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi, mbali na kupewa mashine hiyo ya kisasa pia UNDP wametupatia vitendea kazi mbalimbali vya kuhifadhi taka ambavyo vitatusaidia sana katika mradi huu ’’amefafanua Injinia Matee. 

  Hospitalia ya Taifa Muhimbili kwa siku huzalisha taka hatarishi kilo 800 kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa inayowahudumia . Mradi huo wa mazingira unasimamiwa na Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Kitengo cha Uhakiki na Ubora Muhimbili.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) ambao umekuja kuangalia utekelezwaji wa mradi wa mazingira . UNDP wametoa msaada wa mashine ya kisasa ya utasishaji ambayo itasaidia kupunguza uchomaji wa taka za plastiki.

  Taka 02: Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira ambao wameambatana na ujumbe kutoka UNDP .
  Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira ambao wameambatana na ujumbe kutoka UNDP .
  Wadau hao wakimsilikiza Muhandisi Matee  alipokua akifafanua jambo wakati wa tukio hilo.
  Mshauri wa masuala ya Mazingira kutoka UNDP Zambia Bi. Winnie Musonda akiuliza swali mara baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo mapema leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

older | 1 | .... | 1581 | 1582 | (Page 1583) | 1584 | 1585 | .... | 1898 | newer