Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

JUMIA YATOA SAMSUNG S9 NA S9+ KWA WATEJA WAKE

0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliyoinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mteja Happiness Keto akionesha simu hiyo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia aliyoinunua simu hiyo aina ya Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!
Mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia akionesha simu hiyo kwa wanahabari.


Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mteja Happiness Keto akizungumza kwenye mkutano huo.


JUMIA imekabidhi simu mbili za Samsung Galaxy S9 na S9+ kwa wateja wake wawili ambao waliibuka washindi kupitia zoezi la kusaka simu kwenye mtandao wao (Treasure Hunt) kupitia kampeni ya ‘Mobile Week.’

Katika zoezi hilo wateja waliofanikiwa kuzipata simu hizo zilizofichwa, walipewa ofa ya kuzinunua kwa bei ya chini kupindukia tofauti na gharama yake halisi. Baada ya kufanikiwa kufanikiwa kuipata simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu, wakati mwenzake Lumby Elia yeye aliinunua Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!

Bei halisi ya simu ya Samsung Galaxy S9 ni shilingi 2,049,000 ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,500,000 wakati Samsung Galaxy S9+ ni shilingi 2,315,000 nayo ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,800,000! Hivyo unaweza kujionea ni kwa namna gani wateja hawa walivyokuwa na bahati!

Simu hizi zilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu na kampuni ya Samsung duniani ambapo kwa hapa nchini Tanzania ilikuwa ikipatikana kwa malipo ya kabla kupitia kwenye mtandao wa Jumia pekee.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa simu yake ya Samsung Galaxy S9+, Lumby Elia amesema kuwa ana furaha sana hatimaye kuishika simu hiyo mkononi kwa mara ya kwanza kwani ni kama ndoto kuinunua kwa bei hiyo kwa sababu ni sawa na bure.

“Ni ndoto ya watu wengi kumiliki bidhaa ambayo ni toleo jipya hususani kama simu ambazo kila mwaka huwa zinakuja na matoleo na maboresho tofauti. Simu hii kwangu mimi ni kama ndoto kutokana na ubora na thamani yake pamoja na uwezo ilionao,” alisema na kumalizia Bi. Elia, “Naishukuru sana Jumia kwa zawadi hii lakini pia kwa fursa iliyoitoa kwa wateja wake kuweza kutumia bidhaa halisi na mpya kabisa iliyoingia kwa mara ya kwanza sokoni. Nawasihi wateja wengine wakiona fursa kama hizi wasizipuuzie, ni kweli kama hivi mnavyoona.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott ameongezea kuwa ni madhumuni ya kampuni yake kuona inabadili utamaduni wa Watanzania katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.

“Nafahamu kwamba bado Watanzania wengi wana hofu ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kwa sababu wengi wao wamejaribu kulaghaiwa mara kadhaa walipojaribu kufanya hivyo. Lakini ningependa kuwahakikishia mambo ni tofauti kwa Jumia. Jumia ni sehemu PEKEE inayokuhakikishia bidhaa halisi. Unaweza ukaagiza bidhaa, halafu ukalipia mara baada ya kukufikia, tena ukiwa umeridhika nayo. Hata baada ya kununua bidhaa, halafu ukabadili mawazo yako ndani ya siku 7, ikiwa bado haijafunguliwa wala kutumika, ikakurudishia pesa zako - hata gharama za kusafirisha! Hata namna ya kufikiwa na bidhaa yako ni haraka pia! Inachukua takribani muda wa siku 2 tu kwa bidhaa zinazoagizwa ndani ya jiji la Dar es Salaam,” alifafanua Prescott.

“Kuonesha kwamba tunawajali wateja wetu, Jumia leo inazindua rasmi kampeni nyingine ya ‘Mobile Week.’ Safari hii ikiwa imeboreshwa zaidi kwa ofa, mapunguzo ya bei na zawadi kemkem kwa wateja,” alisema Prescott na kuhitimisha kuwa, “kitu cha kusisimua zaidia, tunafahamu kuwa kwa mashabiki wengi wa mchezo wa mpira wa miguu macho na masikio yote wametega kuelekea kuanza kwa Kombe la Dunia. Jumia hatutowaacha watupu, tuna kampeni kubwa pia itakuja siku si chache pamoja na nyinginezo nyingi zitakazokuwa zikiendeshwa kila wiki.”

COASTAL UNION YAMKABIDHI TUZO YA HESHIMA WAZIRI UMMY WA KUISAIDIA KURUDI LIGI KUU

0
0
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akipokea tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake kwa kuipandisha timu ya Coastal Union kucheza Ligi kuu msimu ujao kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu hiyo Salimu Bawaziri mapema leo kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipofungua mashindano ya Ligi ya Banda Cup . Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akionyesha waandishi wa habari tuzo aliyokabidhiwa na klabu ya Coastal Union kwa kutoa mchango wake kuipandisha kucheza Ligi kuu msimu ujao kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (CCM) Azzah Hamadi Hilali  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)kushoto akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuisaidia timu hiyo kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao tuzo hiyo walikabidhiwa pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano January Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli(CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM),Asas ya Iringa na Mo Dewji. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

DK. KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA MAPITIO YA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA UTALII YA MWAKA 2018 LEO JIJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.

............................................

WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla amesema  Serikali itaendelea kutekeleza sera ya Taifa ya Utalii  kwa ushirikiano na wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za maliasili na utalii nchini.

Dk. Kigwangalla ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma leo wakati akifungua warsha ya kitaifa ya mapitio ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018.


Amesema mafanikio ya sekta ya utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali katika kutekeleza sera hiyo.


“Sera hiyo kwa ushirikiano na Wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji.


“Wote tunaelewa ya kuwa Utalii ni moja wapo ya sekta zinazokua kwa kasi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kupunguza umasikini wa kipato”.


Amesema ukuaji wa sekta hiyo, umedhihirika pale ambapo katika miaka ya hivi karibuni mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.2 mwaka 2017.


Amesema ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017.


Waziri Kigwangalla amesema sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).


Akizungumzia mambo yaliyowekewa mkazo katika rasimu hiyo amesema ni pamoja na Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wote wa utalii katika kuhifadhi rasilimali za utalii.


“Kuendeleza rasilimali watu, kuimairisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kuimarisha mnyororo wa thamani katika mazao ya utalii, kuongeza wigo wa mzao ya utalii kama vile kuendeleza utalii wa fukwe na utalii wa mikutano, kuweka mkazo katika kutangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii kimataifa.


“Napenda kusisitiza kuwa, Sera hii itakuwa na nyenzo nyingine muhimu za kuitekeleza ambazo ni Mkakati wa utekelezaji wa Sera na Progamu ya Maendeleo ya Utalii nchini.


“Tayari Wizara imeanza maandalizi ya awali ya kukamilisha nyenzo hizo na mtashirikishwa kikamilifu katika kuziandaa na kuitekeleza wake,”alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema sera ya Taifa ya Utalii iliyopo hivi sasa ilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka 18 iliyopita.


Amesema kwa kutambua hilo, Wizara iliona kuna umuhimu mkubwa kupitia upya Sera hiyo ili kuhakikisha ukuaji wa Sekta ya Utalii nchini unaenda sambamba na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani ikiwamo mabadiliko ya teknolojia, kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimazingira.


Aidha,alisema kwa kuzingatia kuwa msingi mkuu wa kuandaa Sera yeyote ni kuwashirikisha wadau ambao ndio watekelezaji wa Sera hiyo, mapitio ya Sera hii, yameshirikisha wadau wote muhimu tangu hatua za awali.


“Kazi hii ilipangwa kufanyika kwa awamu tano (5) ambazo ni kukusanya maoni ya wadau katika kanda saba za Tanzania Bara na Zanzibar, uchambuzi wa maoni na kuandaa rasimu ya Sera, kuwasilisha rasimu ya Sera kwenye warsha ya kitaifa ambayo inafanyika leo na hatimaye kuandaa rasimu ya mwisho ya Sera na Mkakati wa Utekelezaji,” alisema.


Warsha hiyo imejumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi wanaohusika maendeleo ya sekta ya utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika warsha hiyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii Deogracious Mdam akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ESRF, Deodatus Sagamiko akizumza katika warsha hiyo. ESRF ni moja ya wadau wakuu waliofadhili zoezi hilo la kuhuisha sera ya taifa ya utalii.
 Baadhi ya wadau katika wa warsha hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
 Meza kuu.
 Wadau. 
  
 Picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati) akifurahia jambo na Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deogracious Mdam wakati Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na mdau wa utalii, Dk. Leaky Abdallah wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 Jijini Dodoma leo.
Baadhi ya wadau wa utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

Wataalam Wawasilisha Usanifu Wa Awali Wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kimataifa Cha Msalato Dodoma

0
0
Wahandisi Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga.
Meneja Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga (wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga.
Mhandisi Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Bw. Said Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma.
Mwonekano wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.

Picha na Bahati Mollel wa TAA

Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliokuwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Anne Makinda akizungumza na Wadau wa Mfuko kutoka Wizara mbalimbali jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akieleza mikakati ya Mfuko katika kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda.


Na Grace Michael, Dodoma

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua ili kuepukana na usumbufu wa kutafuta au kutumia gharama kubwa za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), Anne Makinda wakati akizungumza na wadau kutoka Wizara zote Jijini Dodoma.

Amesema kuwa mwananchi anapokuwa na bima ya afya anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote bila kujali kama ana fedha ama hana ikilinganishwa na mwananchi ambaye hana bima ya afya ambapo akiugua ni lazima aanze kutafuta fedha za kujitibia.

“Ni lazima ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua, tunashuhudia namna wananchi wanavyopata shida wakati wakiwa wamefikwa na maradhi hali inayosababisha wengine hata kulazimisha kutumia njia za mkato au udanganyifu hivyo ili kuepukana na matatizo haya ni vyema tukawa na huu utamaduni wa kukata bima ya afya mapema,”alisema Mama Makinda.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya kwa kuhakikisha dawa, vifaa tiba na mahitaji yote katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ili mwananchi apate huduma kamilifu.

Kutokana na hayo, aliwataka wadau hao kushirikiana na Mfuko kwa karibu kwa kutoa maoni ama ushauri wao kwa uwazi ili kuleta mabadiliko chanya ya kihuduma kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hasa katika kipindi hiki cha kuelekea afya bora kwa wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema, Mfuko umejipanga katika uboreshaji wa huduma zake ikiwemo taratibu zinazowawezesha wananchi kujiunga na huduma zake.

Alisema kuwa, kwa sasa mfuko unaangalia uwezekano wa kumwezesha mwananchi mmoja mmoja kujiunga na mfuko lakini pia utaratibu wa kulipa fedha kidogo kidogo, taratibu ambao zitawawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma za mfuko.

“Tumejipanga na tumedhamiria kufikia mwaka 2020 ni lazima tuhudumie wananchi wengi zaidi na kwa sasa tunajipanga kuzindua huduma mbalimbali ambazo zinalenga kumnufaisha mwananchi wa kawaida kabisa,”alisema.

Akizungumzia suala la huduma bora, alisema mfuko umeweka mazingira rafiki kwa watoa huduma kupata mikopo rahisi kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao hususan vifaa tiba na uimarishaji wa miundombinu hatua ambayo imewezesha upatikanaji wa huduma nyingi na bora kupatikana nchini.

Alitumia mwanya huo pia kukemea tabia ya baadhi ya watoa huduma na wanachama wasio waaminifu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu ambapo alisema Mfuko hauko tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea na badala yake hatua kali zitachukuliwa kwa wanaofanya vitendo hivyo.

Kwa upande wa wadau ambao ni Maofisa Waandamizi kutoka wizara zote, waliupongeza mfuko kwa kazi kubwa ambayo umefanya ya utoaji wa huduma na uwekezaji katika sekta ya afya ambao umesaidia huduma nyingi za kitaalam ambazo awali hazikupatikana nchini kupatikana.

IGP SIRRO AWAPA SOMO WASTAAFU POLISI.

0
0
Na. Jeshi la Polisi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaasa Makamishna wastaafu wa Polisi kuendelea kukabiliana na uhalifu wawapo uraiani baada ya kustaafu utumishi wa Polisi kwa kuwa mapambano ya uhalifu hayana mipaka. 

IGP Sirro aliyasema hayo jana wakati wa hafla maalum ya kuwaaga waliokuwa Makamishna wa Polisi, Glodwing Mtweve na Elice Mapunda katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, hafla ambayo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa Polisi, Askari na familia za wastaafu hao. 

“Mmefanya kazi kubwa sana wakati mlipokuwa nasi na uzoefu wenu tutaendelea kuuhitaji na kuutumia lakini sasa mnaporudi uraiani haina mana kuwa hamruhusiwi kuendeleza mapambano ya uhalifu la hasha hii ni fursa sasa ya kuwasaidia wananchi kupata mbinu ili kwa pamoja mshirikiane na Jeshi la Polisi kuukabili uhalifu kwa kuwa mtakuwa karibu na jamii zaidi” Alisema IGP Sirro. 

Kwa upande wake Kamishna Mstaafu Clodwin Mtweve amewataka Maofisa na Askari Polisi kuendelea kufanya kazi zao kwa kujituma na weledi ili kuhakikisha kuwa uhalifu unaendelea kupungua kwa kuwa uhalifu sasa unafanywa kisayansi. 

Mtweve amesema wanaoendelea kulitumikia Jeshi la Polisi hawana budi kuyafuata yale mazuri yote waliyofanya na yale mabaya kuyaacha ili nao waweze kumaliza salama utumishi wao salama na kuagwa kama ilivyokuwa kwao. 

Naye Kamishna mstaafu Elice Mapunda ambaye alikuwa Mwanamke wa kwanza kufikia cheo cha kamishna wa Polisi tangu kupata uhuru aliwataka askari wa kike nchini kujituma ili kupata mafanikio kama ilivyo kwa wanaume kwa kuwa kupata vyeo ndani ya jeshi hilo hakuangalii jinsia bali ni utendaji wa kazi. 

Amesema askari wa kike hana tofauti na wa kiume kwa kuwa mafunzo wanayopitia ni ya aina moja hivyo wakijituma zaidi na kufanya kazi zao kwa ufanisi wataonekana na kupewa madaraka kwa mujibu wa taratibu na kanuni za Jeshi hilo. 

Dkt Kalemani azindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati

0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati na kutoa maagizo mbalimbali kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi ili Sekta ya Nishati iendelee kuwa injini katika ukuaji wa uchumi.

Dkt. Kalemani amezindua Baraza hilo tarehe 11 Mei, 2018 mkoani Dodoma ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye alimwakilisha Katibu wa TUGHE Taifa na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.

Akizungumza na Wajumbe wa Baraza, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wajumbe wa TUGHE, Tawi la Wizara ya Nishati, Dkt. Kalemani alisema kuwa, jukumu kuu la Wizara na Taasisi zake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya umeme ya kutosha hivyo wana jukumu la kutafakari namna ya kutekeleza suala hilo.

Dkt. Kalemani, aliwaagiza watendaji wa Wizara na Taaisi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na miundombinu ya kutosha ya kusafirisha umeme ili umeme unaozalishwa uweze kuwafikia wananchi kwani kuna sehemu ambazo umeme umekuwa ni mwingi kuliko matumizi ya nishati hiyo. Aidha, Dkt Kalemani aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa, wananchi waliolipia huduma ya umeme, wanaunganishwa na huduma hiyo ndani ya wakati ambao ni siku Saba.

Vilevile Dkt. Kalemani, alisema kuwa, kila mtendaji ana jukumu la kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kuhusu masuala yanayohusu Watumishi, Dkt Kalemani aliagiza kuwa watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu wathibitishwe katika nafasi hizo ili watumishi hao watekeleze majukumu yao kwa kujiamini na kuwa na ari.

Waziri wa Nishati pia aliagiza kuwa, watumishi wapandishwe madaraja kama inavyostahili ili kuwapa morali ya kufanya kazi, pia motisha na mafunzo sehemu ya kazi yaendelee kutolewa ili kuwajengea uelewa watumishi na hivyo kuleta ufanisi katika Sekta wanayoisimamia. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na kupongeza ushirikiano anaopata kutoka kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi katika majukumu yake ya kila siku, aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Nishati yanatekelezwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua alisema kuwa Baraza hilo la Wafanyakazi ni muhimu kwani pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Watumishi, pia litajadili utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Nishati kwa mwaka 2017/2018 na mipango ya maendeleo kwa mwaka 2018/2019. Vilevile alisema kuwa, Baraza hilo litajadili Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2017/18 na litapitia Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2018/19. 

 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (wa kwanza kulia),  Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (wa kwanza kushoto) na Katibu Mpya wa Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Nishati, Pascal Mduma (wa pili kulia) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (kulia) na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (kushoto) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.
 Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti (waliosimama) iliyoandaa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na kushoto kwake ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.
 Watendaji kutoka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu na Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA EAGT DKT. MWAKIPESILE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown  Mwakipesile, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

JAFO AAGIZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BWANGA UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ametoa mwezi mmoja kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Chato mkoani Geita kusimamia ipasavyo na kukamilisha Ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Bwanga ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kutoka serikali kuu. 

Waziri Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita katika ziara ya kukagua wa miradi ya maendeleo. Jafo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na ametoa siku 30 kazi zote ziwe zimekamilika.Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita ya Magufuli.

Shule hiyo imeimarishwa miundombinu yake ya vyumba vya madarasa, vyoo, bwalo la chakula, pamoja na mabweni. Akizungumza shuleni hapo, Jafo amewapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya Magufuli kwa kuwa miongoni mwa shule 25 bora nchini kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017.Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu kuweka jitihada zao kwenye masomo ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Magufuli wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya shule hiyo.
Majengo ya kituo cha afya Bwanga 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita kwenye ukaguzi wa ukarabati wa kituo cha Afya Bwanga.

WILAYA YA MADABA YAJA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUBORESHA KIWANGO CHA ELIMU.

0
0
Halimashauri ya wilaya ya MADABA mkoani Ruvuma imeadhimia kuandaa mikakati madhubuti ya kuboresha kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na makazi bora ya walimu katika shule husika. Hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani la robo tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018.

Hakutakuwa na Upungufu wa Sukari- Dkt Tizeba

0
0
Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni waziri  wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari  itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi  June mwaka 2018.

Aidha  Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini  kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara  kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine  tani 25,441.25 kipo Bandarini .Kwa kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba  nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.

Awali Dkt.Tizeba  alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.Hata hivyo mapitio yanaonesha kwamba  msimu wa mwaka 2017/18  viwanda vya ndani vilizalisha tani 306,226  za sukari kwa matumizi ya kawaida  ambapo mwisho wa msimu huu uzalishaji umefikia tani 307,481.76 aliongezea Dkt. Tizeba.

Akimalizia taarifa yake Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina yeyote ya sukari hapa nchini na ikizingatiwa  kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi mei ambapo ukarabati (services ) itakuwa imekamilika .
Waziri  wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba

TAXIFY YAWAWEZESHA MADEREVA-WASHIRIKA WA BAJAJI KWA KUWAPATIA SIMU ZA SMARTPHONE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Kampuni ya Taxify inayokuwa kwa kasi zaidi duniani katika utoaji wa huduma ya usafiri kidijitali, sasa inawawezesha madereva-washirika wake wa Bajaji kwa kuwapatia simu za kisasa aina ya Smartphone.

Mpango mkakati huo umelenga kuwasaidia madereva wa Bajaji kutumia huduma ya Taxify kwa urahisi, kuboresha biashara na kujiongezea kipato cha juu zaidi.

Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka alisema,"Mamia ya madereva wa Bajaji wanatamani sana kufanya kazi pamoja nasi lakini changamoto kubwa inayowakabili ni kutokuwa na simu za kisasa yaani ‘Smartphones’. Tunarahisisha kwa madereva kutumia huduma mbalimbali za Taxify kwa kuwapatia vitendea kazi hivi kwa mkopo.

Kupitia mapato watakayokuwa wanapata mara baada ya kuanza kufanya kazi na sisi wataweza kulipia mikopo yao kidogo kidogo na kwa awamu."

Kwa upande wake, dereva wa Bajaji ambaye ni mkazi wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, Steven Simon alisema, Taxify imeleta mabadiliko ya jinsi wanavyofanya biashara kwa sasa.

"Kupitia Taxify, sasa hatuna tena haja ya kusubiri kwa muda mrefu kusubiria wateja, tunaweza kupokea maombi ya wateja kutoka sehemu yoyote ya maeneo ya jijiji. Tumefanikiwa kupata kipato zaidi kuliko tulichokuwa tunapata hapo awali," aliongeza. 

Taxify imedhamiria kuwawezesha madereva wanaofanya nao kazi kujiongezea kipato. Kamisheni inayochukuliwa kwa kila safari ni asilimia 15 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 25 katika soko hilo la usafirishji kidijitali. Hii ina maanisha kwamba Taxify inatoza gharama ndogo za nauli kwa abiria wake huku madereva wakijipatia kipato kikubwa ukilinganisha na wadau wengine wanaotoa huduma ya usafiri kidijitali.

AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA

0
0
Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP) limeendesha kongamano kwa wanafunzi 120 kutoka shule nane zilizopo katika kata Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

Kongamano hilo lililoongozwa na mdahalo wenye mada "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?" limefanyika leo Jumapili Mei 13,2018 katika ukumbi wa Ibanza Hotel uliopo mjini Shinyanga.

Mbali na kuongozwa na mada hiyo,pia wanafunzi hao wameonesha michezo kadha wa kadha huku mada mbalimbali zikitolewa ikiwemo huduma rafiki kwa vijana,ukatili wa kijinsia na madhara yake,majukumu ya afisa ustawi wa jamii na mazingira rafiki shuleni pamoja na umuhimu wa michezo.

Awali akizungumza, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana unaotekelezwa na shirika la AGAPE kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Sida kutoka SWEDEN , Lucy Maganga alizitaja shule hizo kuwa ni shule za msingi Busanda,Nzagaluba,Manyada,Shingida,Shabuluba na shule za sekondari Usanda,Singita na Samuye.“Mdahalo huu umelenga kuwajengea uelewa wanafunzi kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate mimba wakiwa shuleni na magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi”,alieleza.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape, John Myola alisema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinasababisha ndoto za watoto kutotimia hivyo kuitaka jamii kuungana katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa.“Masuala ya ukatili yameumiza sana watoto,yamekatisha ndoto zao na wakati mwingine kusababisha madhara ya kudumu kwa watoto yakiwemo ya kimwili na kisaikolojia,lazima jamii ibadilike ili kuwalinda watoto hawa”,alisema Myola.

Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kutengeneza urafiki na watoto ili kujua matatizo wanayokutana nayo ikiwemo kufanyiwa ukatili na watu wa karibu waliopo katika jamii inayowazunguka.Naye Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery alisema ataendelea kuhamasisha walimu na viongozi mbalimnbali kutoa elimu juu ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana huku akiwataka wazazi,walezi na walimu kuangalia aina za adhabu kwa watoto na kuhakikisha wanawapatia muda wa kucheza.

Nao washiriki wa kongamano walikubaliana kuendelea kutoa elimu ya uzazi na masuala ya ukatili dhidi ya watoto kwa wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao.Nimekuwekea picha za matukio yaliyojiri wakati wa mdahalo huo,Angalia picha hapa chini
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo uliokutanisha pamoja wanafunzi 120 kutoka shule 8 zilizopo katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga leo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo akifungua mdahalo huo ambapo aliwataka wanafunzi hao kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wakatishe masomo yao mfano kupata mimba wakiwa shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akizungumza ukumbini. Kushoto ni Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery, kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta aliyehudhuria mdahalo huo kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola ukumbini.
Wanafunzi wakifurahia jambo ukumbini.
Wanafunzi wakiendelea kufuatilia matukio ukumbini.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akielezea malengo ya mdahalo huo wenye mada isemayo "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akitoa mwongozo wa kuchangia mada ya '"Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Shingita,Kashindye Shija akichangia mada ukumbini 
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Shabuluba, Philipo Jacob akichangia mada wakati wa mdahalo huo.
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Samuye, Veronica John akichangia mada wakati wa mdahalo huo.
Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Usanda,Philipo Malale akichangia mada ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akitoa mada kuhusu majukumu ya afisa ustawi wa jamii.Alisema miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto.
Kulia ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Samuye akimuuliza swali Atupokile Maseta kuhusu hatua zipi zinachukuliwa endapo mzazi atatekeleza familia yake.
Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery akitoa mada kuhusu Mazingira salama kwa wanafunzi shuleni na umuhimu wa michezo kwa wanafunzi.
Mwanafunzi akielezea umuhimu wa michezo kwa watoto.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Nzagaluba wakiimba wimbo kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya watoto.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Manyada wakiimba ngonjera.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Samuye wakiimba shairi.
Wananfunzi wakicheza muziki ukumbini.
Afisa ulaghabishi wa shirika la AGAPE, Dotto Wayala akicheza muziki na wanafunzi ukumbini.
Muziki umekolea: Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akikata viuno wakati wanafunzi wakicheza muziki ukumbini.
Kushoto ni Afisa Mradi wa Elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ,Lucy Maganga naye akionesha uwezo wa kucheza muziki.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Shingita wakifuatilia matukio ukumbini.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Usanda wakionesha mchezo wa igizo kuhusu nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.
Wanafunzi wa shule ya msingi Shingida wakicheza ukumbini
Walimu wakifurahia jambo ukumbini.
Walimu wakifuatilia matukio ukumbini.
Walimu wakiwa ukumbini.
Wafanyakazi wa shirika la AGAPE wakifurahia jambo ukumbini.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Samuye wakionesha mchezo wa igizo.
Wanafunzi wakicheza muziki.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Shingita wakcheza ukumbini
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akitoa mada kuhusu masuala ya ukatili.
Kijana Samson Mtesigwa akitoa burudani ya wimbo maalumu kuhusu umuhimu wa kupeleka watoto shule.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

JAFO AFURAHISHWA NA MRADI WA MACHINJIO JIJI LA MWANZA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa na jiji la Mwanza kwa kuboresha machinjio ya Kisasa ndani ya jiji hilo. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo alipotembelea mradi huo mkubwa ambao kukamilika kwake kutawezesha kuchinjwa ng'ombe 700 kwa siku.Aidha mradi huo utaongeza mapato ya jiji hilo ambapo yanatarajiwa kuongezeka kutoka Sh. milioni 30 kwa mwezi hadi Sh.milioni 120 kwa mwezi kwa chanzo hicho pekee. 

Akizungumza katika mradi huo, Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zingine nchini kuiga utekelezaji wa mradi huo.Aidha Waziri huyo Jafo amempongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mongela, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula, Mkuu wa wilaya, pamoja na Mkurugenzi wa jiji na baraza la madiwani kwa usimamizi wa miradi na utendaji kazi wao uliotukuka.

Mbali na kutembelea mradi wa machinjio , katika ziara hiyo pia Jafo amefanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa shule ya wasichana ya Ngaza, eneo linalo tarajiwa kujengwa maegesho ya magari ya mizigo, stendi ya Nyegezi inayotarajiwa kuboresha, miundombinu ya barabara za mawe na Hospitali ya Nyamagana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Mwanza wakikagua Miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipongeza ujenzi mzuri wa barabara za changarawe katika mitaa ya jiji la Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ngaza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ngaza.
Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya jiji hilo.
Machinjio inayoboreshwa katika jiji la Mwanza.

MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA

0
0
Na Jumbe Ismailly IRAMBA

WANAFUNZI 99 wa darasa la awali katika shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,tarafa ya Shelui,wilayani Iramba,Mkoani Singida wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti huku wakitumia magoti ya miguu yao kama meza wakati wakiandika kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati unaoikabili shule hiyo.

Kaimu Ofisa elimu Kata ya Mgongo,Lazaro Isaya Sakata alithibitisha kuwepo kwa upungufu huo wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati kwenye hafla fupi ya kupokea tani tano za mifuko ya saruji zilizotolewa na Kampuni ya kuchimba madini ya Mgongo Gold Mine kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

Alifafanua Ofisa huyo wa elimu kuwa wanafunzi wa awali katika shule ya msingi Kibululu wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti kwa sababu hakuna chumba cha darasa kinachoweza kuwamudu kuingia wote 99 na kuweza kumsikiliza mwalimu wao kikamilifu.

Kwa mujibu wa Sakata wanafunzi hao 99 wanatakiwa kuwa na vyumba vinne vya madarasa kutokana na kwamba uwiano wa mkondo mmoja ni wanafunzi 25,kitu ambacho kimekuwa kigumu na kulazimika kuwakusanya chini ya miti na kuendelea na masomo.

“Sasa namna ya kumudu kwamba niangalie kila mmoja anaumba vipi ile herufi au kile ninachokifundisha,inakuwa ni kazi kidogo mara kuna mvua mnatoka mnakimbia,mara jua kali inabidi msogee mahali Fulani na mara kuna upepo kwa wakati wote wanakuwa ni vurugu halafu mkiwa nje watoto hawajifunzi vizuri”alisisitiza Sakata.

Akikabidhi msaada huo wa tani tano za saruji,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Michael Sagati alitumia fursa hiyo kuyashawishi Makampuni yanayochimba madini katika Kijiji cha Kibululu kujitokeza na kuhakikisha wanawekeza kwenye sekta ya elimu.

Kwa mujibu Mkurugenzi huyo endapo wawekezaji hao watajikita zaidi katika sekta ya elimu watakuwa wamewapatia watoto urithi wa maisha kuliko hata urithi wa fedha,majengo na hata mali nyinginezo walizonazo na kwamba uwekezaji huo utakuwa wa kudumu na hautasahaulika hata mbinguni.

Naye mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya MGM,Gabrieli Issah alibainisha kuwa msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.8 ni utekelezaji wa ahadi waliyotoa ambayo pia ni sera ya nchi kwamba kila mwananchi anayejihusisha na uchimba,lazima maeneo yanayozunguka machimbo hayo yaweze kufaidika na uchimbaji huo.

Akipokea msaada huo,Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibululu,Mwanjaa Danieli Mkoma aliweka wazi kwamba katika mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi mwaka jana,asilimia 26 ya wanafunzi 78 waliofanya mitihani ndiyo waliofanya vizuri huku asilimia 74 walifanya vibaya.

Kata ya Mgongo ina shule za msingi tano zikiwepo nne shule nne za msingi na moja ya sekondari na kwamba hakuna shule ya msingi inayojitosheleza kwa vyumba vya madarasa pamoja na madawati wakati kwa shule ya msingi Kibululu ina upungufu wa nyumba za walimu 8 vyumba vya madarasa vinane.
Ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,wilayani Iramba wakionekana wakipanda juu ya gari dogo lililoleta saruji kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wanafunzi kusomea chini ili waweze kushusha mzigo huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Sagati akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo katika picha ya pamoja mara baada ya gari lililobeba saruji kuwasili shuleni hapo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

DC GAIRO AAGIZA WACHIMBAJI MADINI WASIO NA LESENI KUSIMAMISHA UCHIMBAJI MARA MOJA

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kutembelea sehemu ya migodi inayochibwa kinyemela na wachimbaji wasiokuwa na leseni.
Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni. Mhe. Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo wachimbaji wameweka mashine nzito na wanafanya kazi wakati hawana leseni. 

 Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kifungu cha 18 kimeweka bayana adhabu kwa mchimbaji haramu. Ikiwa ni mtu binafsi faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miaka mitatu au vyote pamoja. Kama ni kampuni basi ni faini isiyozidi shilingi milioni 50. Mheshimiwa Mchembe aliendelea mbali na kuelezea kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji namba 29 ambapo madini yaliyopatikana kupitia uchimbaji haramu yatataifishwa na Serikali chini ya Kamishna wa madini na kuuzwa kwa mnada. Mitambo yote pia inapaswa kutaifishwa. 

 Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Mchembe ametoa maagizo hayo na kumtaka Afisa Madini Mkoa na Kanda kufatilia jambo hilo kwa karibu. Pia amepiga marufuku raia wa kigeni kutembelea maeneo ya machimbo bila kibali. Aidha uzingatiwaji wa kanuni 3 (1) (2) ambapo mchimbaji anatakiwa kuwasilisha kwa Afisa Madini mkazi kanda taarifa ya tathmini na mpango wake wa utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza kuchimba madini. Wilaya ya Gairo ina madini aina mbalimbali na maeneo ya milimani yameachwa na mashimo makubwa.

WAZIRI KIGWANGALLA AMTEUA MISS JOURNALISM TANZANIA 2018 KUWA BALOZI WA UTALII WA PORI LA AKIBA SELOUS

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous. 

Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
.............................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji la Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.

Amefanya uteuzi huo mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma baada ya mazungumzo na mwanamitindo huyo aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kuandaa  mradi wa kijamii ambao ni sehemu ya shindano atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018 litakalofanyika Oktoba 27 Jijini Arusha.

Kufuatia uteuzi huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika barua ya uteuzi kwa balozi huyo mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi ili pamoja na mambo mengine aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.

Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa safari maalum ya balozi huyo mteule aweze kutembelea Pori la Akiba Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.

Sambamba na pori hilo atatembelea pia mapori mengine ikiwemo BBK (Burigi, Biharamulo na Kimisi) mkoani Kagera na Mpanga Kipengele mkoani Njombe ambapo  atatumia fursa hiyo kufanya mahojiano na wasichana wa vijiji jirani na hifadhi hizo kwa ajili ya mradi wa kijamii wa kuwainua ikiwa ni sehemu yenye alama muhimu kwenye shindano hilo la Dunia la Miss Journalism 2018.

Awali akiwasilisha ombi lake kwa Waziri Kigwangalla la ufadhili wa safari yake ya ushiriki wa mashindano hayo, Witness pia aliomba kupewa fursa ya kuwa balozi wa Tanzania kwenye moja ya sekta ikiwemo Misitu, Nyuki au Utalii.

Mbali na kushikilia taji la Miss Journalism Tanzania 2018, Witness amesema amewahi kushinda mataji mengine manne makubwa ya kimataifa ya ulimbwende nchini Afrika ya Kusini anakosomea urubani kwa sasa.

Anasema, "Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Garden Route 2017, ambalo ni taji la kitaifa la kuhamasisha na kukuza sekta ya Maliasili na Utalii nchini humo, licha ya kuwa ugenini nilitumia fursa hiyo kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania. 

"Mashindano haya yalihusisha washiriki 600 na wote walikuwa na asili ya kizungu, mimi peke yangu nilikuwa na asili ya kiafrika na niliibuka mshindi". 

Aliyataja mataji mengine kuwa ni Miss Bees Cape Town 2017 kwa ajili kuhamasisha uhifadhi wa sekta ya nyuki na mataji mawili ya kimkoa ambayo ni Miss Asla Capetown 2017 na Miss Carnival Mosselbay 2017.

Mataji mengine ya kitaifa aliyowahi kushinda Witness hapa nchini ni pamoja na Miss Arusha Higher Learning 2014 na Miss Northern Zone 2014.

Mashindano hayo ya Dunia ya Miss Journalism 2018 yanahusisha pia uhamasishaji wa maendeleo ya utalii, utamaduni wa amani, uandishi wa habari na kupiga vita ugonjwa wa ukimwi na Malaria.

Pori la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa taji la urembo la "Miss Garden Route South Africa 2017" ambalo ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha utalii nchini Afrika ya Kusini na Miss Journalism Tanzania 2018, Witness Teddy Kavumo (21) aliyeshinda taji hilo na mataji mengine matatu nchini humo mwaka jana, alipomtembelea ofisini kwake mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki kwenye mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma alipomtembelea mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa wa utalii wa Pori la Akiba Selous.

INVITATION TO ICT SHORT COURSES

0
0

KILIMANJARO BIA YA TANZANIA KINYWAJI RASMI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

0
0
 Meneja wa kiwanda cha Ilala, Calvin Martin na Meneja Masoko George Kavishe, wakiongoza wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa promosheni ya bia ya Kilimanjaro kufanya cheers
 Maofisa waandamizi wa ABinBev wakifuatilia matukio na shamrashamra wakati wa hafla ya uzinduzi
 Wageni waalikwa na wafanyakazi wa TBL wakiburudika wakati wa uzinduzi huo
 Shamrashamra mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi
 Shamrashamra mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi
Wageni mbalimbali wakifuatilia matukio na kupata burudani wakati wa uzinduzi. *Kuwazawadi wateja wake kushuhudia mechi za mashindano hayo Live Kampuni ya Tanzania Breweries Limited mwishoni mwa wiki imetangaza ushirikiano wake na shirika la Soka Duniani (FIFA), ambapo bia yake ya Kilimanjaro, imetangazwa kuwa bia rasmi ya Tanzania katika mashindano ya Kombe la Dunia 2018 yatakayofanyika nchini Urusi. 

 Kutangazwa huku kunaenda sambamba na kuzinduliwa kwa promosheni kubwa ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania itakayowazawadia wateja wa bia ya Kilimanjaro nafasi ya kujindia safari ya kushuhudia baadhi mechi za kombe la dunia nchini Urusi mubashara na pia kujishindia muda wa maongezi 2,500/= kila wanaponunua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara (sita) 6 kutuma number iliyopo chini ya kizibo kwenda 15451 fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/- Kila wiki kwa wiki Kumi. 

 Hafla kubwa ya uzinduzi iliyojumuisha wafanyakazi wa TBL,Waandishi wa habari,wasanii na wadau mbalimali wa kampuni ilifanyika katika kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi utaendelea kufanyika katika mikoa mingine Meneja Masoko, udhamini na program za wateja Afrika Masharariki wa kampuni ya TBL Group Bwana George Kavishe alisema “Tunayo furaha chapa yetu maarufu ya Kilimanjaro kutangazwa kuwa bia rasmi ya Tanzania katika msimu huu wa kombe la Dunia la FIFA 2018, kampuni inatangaza kuzindua kampeni maalumu ambayo itawawezesha wateja watakaobahatika kushinda kugharamiwa safari ya kwenda Urusi kuangalia mechi za kombe la Dunia mubashara sambamba na zawadi za fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni moja kila wiki, muda wa maongezi 2,500 kila unaposhiriki kutuma number iliyopo chini ya kizibo mara 6, pamoja na zawadi kem kem zitakazotolewa kwenye promosheni za kwenye mabaa zaidi ya mia tatu nchi nzima.

 Alisema washindi wapatao 10 watawezeshwa kugharamiwa kuona mashindano ya kombe la Dunia na washindi wengi wataweza kujishindia fedha taslimu, na muda wa maongezi. “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”

.Alisisitiza Ili kujishindia zawadi mteja anapaswa kutuma namba zilizopo kwenye chupa za bia ya Kilimanjaro kwenda namba 15451 ili kujipatia fedha taslimu na muda wa maongezi, Zawadi ya ticket ni kwa wale wataoshiriki kujibu maswali yatakayoendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya www.Kililager.com na kujipatia point za ushindi. Promosheni hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na litaendeshwa nchi nzima na matangazo yake yamezinduliwa rasmi pia kupitia televisheni, radio na mitandao ya kijamii.

COCA-COLA BONITE YAZIDI KULETA RAHA YA MZUKA WA SOKA NA COKA KANDA YA KASKAZINI

0
0

 Washindi wa luninga na pikipiki wakifurahia zawadi zao.
 Washindi wa luninga na pikipiki wakifurahia zawadi zao.
Mmoja wa washindi wa fedha taslimu akipokea zawadi yake Wakati mashindano ya kombe la Dunia 2018 yanakaribia, kampuni ya Coca-Cola Bonite Bottlers Limited ya mjini Moshi inazidi kumwaga zawadi za pikipiki,luninga za kisasa na fedha taslimu kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini kupitia promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka inayoendelea. Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi 16 wa wiki liyopita, Meneja Mauzo wa Bonite, mkoa wa Arusha Bw. Boniphace Mwasi, alisema zaidi ya wateja 50 wamejishindia zawadi na zawadi bado ziko nyingi. “Bado tunazo zawadi nyingi hivyo natoa wito kwa wakazi wote wa kanda ya kaskazini kuchangamkia kunywa soda za Coca-Cola, ili waweze kujishindia zawadi”. Wakiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuleta furaha kwa jamii hususani kwa kuwakwamua kiuchumi.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images