Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1579 | 1580 | (Page 1581) | 1582 | 1583 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mbunge wa Songea Mjini Mhe Dkt  Damas Ndumbaro wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
   Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Bungeni leo Jijini Dodoma. 
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Nishati wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
   Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akionyesha kitabu chenye idadi ya Viwanda vyote nchini wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kitabu hicho kina kurasa mia tisa.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)  walipomtembelea leo Bungeni.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akimskiliza Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa Bungeni leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma, Mei 10, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Bungeni jijini Dodoma, Mei 10, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim,  Bungeni mjini Dodoma,  Mei 10, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bungeni mjini Dodoma, Mei 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akiwasilisha  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo, Bungeni mjini Dodoma, Mei 10, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulie (kulia), na wabunge wa Viti Maalum, Faida Bakari na Anna Lupembe (wapili kulia) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 10, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 10, 2018.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  *Yasema maitosita kumuondoa mwendeshaji wa sasa 

  SERIKALI imesema inakusudia kuongeza mtoa huduma mwingine katika uendeshaji wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambayeataingiza mabasi yake na kutathmini ufanisi wa mbia wa sasa ili kuimarisha huduma ya usafiri Jijini Dar es salaam 
  Amesema iwapo itabainika kwamba mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri, Serikali haitasita kumuondoa na kumpa mwendeshaji mwingine kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw.Maulid Mtulya katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

  Katika swali lake Bw. Mtulia alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya uboreshaji wa wa mradi wa UDART unaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria Jijini Dar Es Salaam ili kuweza kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri.

  “Tunatafuta mbia mwingine aweze kuingiza mabasi yake kwenye mradi huu ili aweze kuongeza ushindani na nasi tupate kupata huduma bora kwa maana ya ushindani utaongeza huduma bora zaidi,” amesisitiza.Waziri Mkuu ameongeza kuwawako wawekezaji wa ndani na nje ukiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar Es Salaam (UWADAR) ambao wameonyesha nia na uwezo wa kutoa huduma hiyo na kuufanya mradi huo kutoa huduma kwa ubora unaotakiwa.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.“Mheshimiwa Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.

  Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha maeneo na kukithiri kwa uchafu.

  Waziri Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.
  ALHAMISI, Mei 10, 2018.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa ameshika orodha ya wafanyabiashara wa soko la Magomeni akisisitiza wapewe kipaumbele baada ya soko kukamilika.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kinondoni.
  Wananchi wa Magomeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo(hayupo pichani).
  Muonekano wa soko la Kisasa linalojengwa Magomeni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kukamilisha ndani ya muda ujenzi wa soko Jipya la Kinondoni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara 693 waliopo hivi sasa.

  Jafo ametaka wafanyabiashara hao wawe wa kwanza kumpatia maeneo ya Biashara bila kunyanyaswa baada ya ujenzi wa soko hilo jipya la kisasa kukamilika.Akizungumza alipotembelea soko hilo leo, Waziri Jafo amesema kuna kasumba imejengeka ambapo masoko yanapojengwa wale waliokutwa sokoni kabla ya ujenzi huwa watatupwa nje na badala yake watu wengine wapya wenye fedha ndio hupatiwa.

  "Nataka hawa wananchi waliopo sasa hapa sokoni ndio wawe watu wa kwanza kukabidhiwa maeneo ya biashara baada ya ujenzi kukamilika," amesisitiza Jafo.Waziri Jafo amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia kwa kuwa ndiye aliyewasilisha kilio cha wanafanyabishara wa Magomeni na serikali imekisikia na kuamua kupeleka fedha.

  Pia amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kinondoni kwa mshikamano mkubwa chini ya Mkuu wa wilaya yao Ally Hapi na kwamba chini ya Mkuu huyo wilaya hiyo imetulia sana  na inasonga mbele na hakuna migogoro ya viongozi inayoweza kurudisha nyuma maendeleo.

  Aidha, Waziri Jafo amempongeza pia kwa kuanza utekelezaji wa utoaji wa mikopo kwa Vijana na wanawake bila Riba.Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni imepata Kiasi cha Sh.Bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo kutoka serikali kuu katika mpango wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

  0 0  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Kh. Shaaban kwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya India, Bw. David Resquinha wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania.
  Bi. Shaaban na Bw. Resquinha wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini

  Picha ya pamoja 

  Serikali ya India kupitia Benki ya Exim imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 500, sawa na shilingi Trilioni 1.14 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania.

  Hafla ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika leo tarehe 10 Mei, 2018 mjini New Delhi, India ambapo Bi. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango na Bw. David Resquinha, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim walisaini kwa niaba ya Serikali zao..

  Miji itakayonufaika na Fedha za mkopo huu ni Muheza, Makambako, Kayanga, Njombe, Manyoni, Songea, Sikonge, Chunya, Kasulu, Kilwa Masoko, Rujewa, Mugumu, Geita, Makonde, Wangingómbe, Handeni , Singida mjini, Kiomboi, Mpanda, Chemba, Mafinga, Urambo-Kaliua pamoja na miji ya Zanzibar.

  Akizungumza baada ya kusaini mkataba, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Kh. Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa sababu itawezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika miji husika hivyo kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na maji yasiyo salama. 

  Aidha, miradi itasaidia kufikiwa kwa malengo na mipango ya Taifa na Kimataifa ya Maendeleo ikiwemo: Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano awamu ya pili (FYDPII) , Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III) na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDG’s).

  Vilevile, amesema uamuzi wa Serikali wa kuboresha huduma za maji umelenga kuwapunguzia Wananchi husususan Wanawake adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, na hivyo kupata muda wa kutosha kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo.

  0 0

   TASAF stakeholders from World Bank, WFP, DFID, UNICEF, USAID and Government of Tanzania met with the Deputy Permanent Secretary of Ministry of Finance Mr. Khatibu Kazungu yesterday. The main agenda was to share a progress report of the project TASAF is implementing i.e. Production Social Safety Net (PSSN) I and Preparation of PSSN II.  This meeting follows a combined joint mission conducted recently with stakeholders from the Government, Donors and TASAF.

  In his remarks the Deputy Permanent Secretary commended TASAF for the achievements obtained so far.  He further highlighted the Government of Tanzania fully supports the initiative done by TASAF as it compliments efforts done by the President Dr. Magufuli to enhance economic activities that will eventually eradicate poverty in the Country and improve living condition of many Tanzanians.
  Mr. Muderis Abdallah (first right) from World Bank clarifying a point to the Deputy Permanent Secretary Mr. Kazungu, Listening carefully is Mr. Matteo Caravani from World Food Program
  Mr. Ladislaus Mwamanga, Executive director for TASAF (with spectacles), responding to the stakeholders during the meeting.
   Stakeholders listening to a presentation made by Mr. Muderis of the WB, indicating the progress report of what TASAF has done to date and the way forward.

  0 0

   Meneja Masoko na Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Nyanza, akiongea na waandishi wa habari.
   Washindi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi zao.
  Baadhi ya washindi wakifurahia zawadi walizojishindia. 

   Promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka ya kampuni ya Coca-Cola Nyanza Bottlers ya jijini Mwanza inazidi kuwezesha wateja wa soda kujishindia zawadi ambapo wiki hii wateja 11 wamekabidhiwa pikipiki na wengine 4 wamekabidhiwa luninga bapa za kisasa. 

  Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,Meneja Masoko na Mauzo wa Nyanza Bottlers,Samwel Makenge ,alisema kumekuwa na ongezeko la washindi ,na kampuni inayo furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali. 

  “Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”,Alisema Makenge. Washindi wapatao 15 ambao walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki naLuninga katika hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza, waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi.

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus akifafanua jambo mbele ya watumishi wa Idara hiyo walipokutana na ujumbe kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwa ajili ya kujengewa uelewa kuhusu huduma za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Afisa Mauzo wa TTCL, Bi. Rahel Mremi na Esther Killango. TTCL ni shirika la Serikali linalotoa huduma za mawasiliano likiwa na kauli mbiu "Rudi Nyumbani Kumenoga."
   Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Rahel Mremi akionyesha Line za TTCL mbele ya Watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus na Afisa Mauzo wa TTCL, Esther Killango(kushoto).

   Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Esther Killango akifafanua jambo mbele ya Watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Msaidizi wa Mauzo wa TTCL, Bi. Damiana Shemweta, Afisa Mauzo wa TTCL, Bi. Rahel Mremi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus(wapili kutoka kushoto). 
   Baadhi ya watumishi wa Idara ya Habari - MAELEZO, kituo cha Dar es Salaam wakifuatilia maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) walipotembelewa na maafisa mauzo kutoka shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Rahel Mremi akionyesha moja ya aina ya simu zinazotumika kwa ajili ya huduma ya sauti mbele ya watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus(katikati) na Afisa Mauzo wa TTCL, Esther Killango.
  Msaidizi wa mauzo toka Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Damiana Shemweta akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya huduma na bidhaa za shirika hilo kwa watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)

  0 0

  Na BMG
  Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.Antony Mtaka amelishukuru na kulipongeza shirika la Amref Health Africa kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha huduma za afya katika mkoa huo.

  Mhe.Mtaka ametoa pongezi hizo leo Mei 11, 2018 wakati akipokea gari la wagonjwa (Ambulance) lililotolewa na shirika la Amref kwa ajili ya hospitali teule ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa gari hilo.

  Mhe.Mtaka amesema shirika hilo kupitia mradi wake wa Uzazi Uzima limesaidia kuboresha huduma mbalimbali za afya mkoani Simiyu ikiwemo ujenzi na ukarabati Zahanati, Vituo vya Afya, wodi (Mama Ngojea) pamoja na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.

  Meneja Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr.Serafina Mkuwa amesema gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na kodi na kwamba limekabidhiwa kupitia mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.Shirika la Amref Health Africa linatekeleza miradi mbalimbai ya afya hapa nchini kupitia ufadhili ya serikali ya Canada.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka akipokea Ambulance iliyotolewa na shirika la Amref.
  Mkurugenzi wa Shirika la Amref Canada, Onome Ako akitoa salami sake wakati wa makabidhiano ya Ambulance hiyo.
  Meneja wa Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr. Serafina Mkuwa akizungumza wakati wa shughuli hiyo.

  0 0


  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

  Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amesema kuwepo kwa Taasisi ya kutibu maradhi ya mishapa ya fahamu na uti wa mgongo (Neuro) hapa Zanzibar ni heshma kubwa na amewashauri wananchi wanaokabiliwa na matitizo hayo kutumia fursa ya kuwepo taasisi hiyo kwenda kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu kwani kinauwezo mzuri wa kutibu maradhi hayo.

  Amesema Taasisi hiyo itasaidia kuwajengea uwezo wataalamu wachache waliopo Zanzibar wanaoshughulika na magonjwa hayo na imeipunguzia Serikali gharama ya kuwasafirisha wagonjwa nje ya Zanzibar.Waziri wa Afya ameeleza hayo katika Taasisi ya Neuro iliyopo Hospitali kuu ya Mnazimmoja, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka nchi za Afrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Amesema kuwepo Taasisi hiyo Zanzibar imeipunguzia Serikali kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mgonjwa mmoja kumsafirisha kwenda kufanyiwa matibabu nje ya Zanzibar na wagonjwa wengi wenyematatizo ya mishipa ya fahamu na uti wa mgongo wanatibiwa bila kutoa malipo.

  Waziri Hamad Rashid ameongeza kuwa taasisi hiyo inahitaji madaktari bingwa wazalendo sita na hivi sasa wapo watatu tu na utaratibu wa kuitumia taasisi hiyo kufanya warsha za Kimataifa itawasaidia madaktari wa Zanzibar kuwajengea uwezo zaidi.Amewashauri wananchi wa Zanzibar kujenga utaratibu wa kuvitumia vituo vya afya vya Wilaya na Mikoa kwa matatizo madogo ya kiafya ili Hospitali Kuu ya Mnazimmoja itumike kwa matatizo makubwa yaliyoshindikana kwani Serikali imevijengea uwezo vituo vya vijijini kwa vifaa tiba na dawa muhimu.

  Daktari bingwa wa maradhi ya ubongo na uti wa mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi Kenya Dkt. Mahmood Qureish ambae anaratibu mafunzo hayo amesema Taasisi ya Neuro ya Zanzibar imekuwa maarufu kwa nchi za Afrika Mashariki na wagonjwa kutoka mataifa hayo wanafika kwa ajili ya matibabu.

  Amesema mafunzo ya Taasisi ya Neuro ya Zanzibar ambayo ni ya kwanza kufanyika yataendeshwa darasani na vitendo katika vyumba vya upasuaji ili kuwajengea uwezo washiriki kufanya matibabu ya ubongo na uti wa mgongo watakaporejea nchini mwao.Mafunzo hayo yanawashirikisha madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka Kenya, Sudan, Afrika Kusini, Zimbabwe Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akifungua warsha ya siku tatu ya Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara inayofanyika Taasisi ya Neuro iliyopo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara waliohudhuria katika mkutano unaofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed katikat alievalia suti rangi ya krimu akipiga picha ya pamoja na Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara (Picha na Abdalla Omar 
  Daktari bingwa wa maradhi ya ubongo na uti wa mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi Kenya Dkt. Mahmood Qureish ambae anaratibu mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari (Picha na Abdalla Omar  Maelezo – Zanzibar).

  0 0

   Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwaaga Maofisa na Askari Polisi huku wakisukumwa katika gari maalumu wakati wa Gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.Gwaride hilo lilifanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).


   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na IGP Mstaafu Omar Mahita wakati hafla maalum ya kuwaaga  Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).
   Kamishna Mstaafu wa Polisi Clodwing Mtweve akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake wakati wa hafla maalum ya kumuaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam  (Picha na Jeshi la Polisi).
  Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla maalum ya kuwaaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia FFU wakitoa heshima wakati  wa gwaride maalam la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia jambo na Makamishna wastaafu Clodwing Mtweve (katikati) na Elice Mapunda (kushoto) wakati wa hafla maalum ya kuwaaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).


  0 0

   . Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati akiondoka akiwa katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Na Mahmoud Ahmad Dodoma

  Imeelezwa kuwa Ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini, umedhihirika mapato yatokanayo na utalii kuongezaka kutoka Dola bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola bilioni 2.2 mwaka 2017. 

  Ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017. Ambapo Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkta Hamis Kigwangala wakati akifungua kongamano la kupitia rasimu ya sera ya Taifa ya utalii ya mwaka1999 linalofanyika jijini hapa na kuwashirikisha wadau wa sekta ya utalii nchini kutoka sekta binafsi na za umma.

  Kigwangala amesema kuwa maboresho hayo yaende sambamba na mwendelezo wa mchakato wa kazi nzima ya kupitia Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ambayo ni muhimu kwa mstakabali wa sekta ya utalii hapa nchini ambayo Kama ilivyoelezwa hapo awali, mojawapo ya dhumuni la msingi la hatua hiyo linalenga kuwa na Sera inayoendana na mabadiliko ya kiuchumi, mazingira, tecknolojia, kijamii na kisiasa yanayotokea ndani na nje ya nchi yetu ambayo yanagusa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

  Amesema kuwa warsha imejumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Umma na Binafsi ambao kwa namna moja au nyingine huguswa au hushiriki katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Aidha, kama mnavyofahamu, utalii ni sekta mtambuka na ili kufanikisha ukuaji wake unahitajika ushirikiano thabiti baina ya wadau wote. Ushirikiano huu utaweza kuleta matokeo chanya iwapo kuna Sera madhubuti ambayo mchakato wake wa maandalizi umeshirikisha wadau kikamilifu.

  “ Vilevile, nawashukuru wadau wa Sekta Binafsi kupitia Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT) kwa kuchangia sehemu ya gharama ya kazi hii hususan, kuwezesha warsha ya kukusanya maoni Kanda ya Kaskazini iliyofanyika Jijini Arusha. Hakika ushirikiano wa namna hii ndio utawezesha kuendeleza sekta ya Utalii na hata kuwezesha nchi yetu kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati kama ilivyobainishwa kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2025”. Alisema Kigwangala

  Amesisitiza kuwa, Sera hii itakuwa ni nyenzo nyingine muhimu za kuitekeleza ambazo ni Mkakati wa utekelezaji wa Sera na Progamu ya Maendeleo ya Utalii nchini. Tayari Wizara imeanza maandalizi ya awali ya kukamilisha nyenzo hizo na kuwa watashirikishwa kikamilifu katika kuziandaa na kuitekeleza.

  Nae katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja jenerali Gaudence Milanzi akimkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa Mafanikio haya ya Sekta ya utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali kutekeleza Sera hiyo kwa ushirikiano na Wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji na kuibuka na maboresho kwa ajili ya rasimu hii ya Sera kwa mustakabali wa sekta ya Utalii nchini.

  Amesema kuwa lengo la kuhuisha rasimu ya será ya taifa ya utalii ni la wadau wote wa sekta hiyo hivyo será hiyo ilifanyiwa mabadiliko miaka 18 iliyopita na kuweza kuifikisha sekta hii hapa ilipo ni busara zetu sasa ziweze kutufikisha kufikia kwenye malengo tarajiwa kwa kuwashirikisha wadau wote katika mchakato mzima hili limepelekea leo kuja na rasimu hii.

  0 0

  Ni kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa Wataalamu mbalimbali walioudhuria kongamano la The East Africa (EA) Innovation Event la kampuni mama ya TBL Group ya ABInBev lenye lengo la kuleta mapinduzi ya kilimo kupitia sayansi na teknolojia lililoandaliwa na taasisi ya Bits&Bites Technology Convention na kufanyika jijini Dar es Salaam, wamedhihirisha kuwa mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini na barani Afrika kwa ujumla yanawezekana kupitia matumizi ya teknolojia za kisayansi. 

   Kongamano hilo ambalo lilijumuisha wataalamu wa fani ya kilimo,watafiti,wahandisi na wabunifu kutoka kanda ya Afrika Mashariki walijadili jinsi ya kupata ufumbuzi wa kuinua kilimo cha wakulima wadogo kupitia teknolojia za kisasa na za gharama nafuu ambapo pia walishiriki shindano la ubunifu wa nyenzo za kiteknolojia ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kazi zao walizogundua.

   Makampuni ya Imara Tech,Mobisol na Back Save Equipment yaliibuka na ushindi baada ya jopo la majaji waliokuwa wanasimamia shindano hilo kubainisha kuwa ugunduzi wao wa nyenzo za kiteknolojia unaweza kusaidia kuinua maisha ya wakulima wadogo.Kazi zilizowapatia ushindi washiriki zitaanza kufanyiwa majaribio kabla ya mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa ambao ni wakulima hususani wadogowadogo.

   Akiongea wakati wa kufunga kongamano hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Sembeye, alisema kuwa kongamano hili limefanyika kwa wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga kuingia katika uchumi wa viwanda ambao unaenda sambamba na kufanya mapinduzi ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda vitakavyoanzishwa,pia kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha.

   Sembeye, alisema njia pekee ya kuleta mapinduzi ya kilimo ni kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa na za gharama nafuu ambazo wakulima wengi wa hali ya chini wanaweza kumudu kuzinunua na kuzitumia kwa ajili ya kuwawezesha kupata tija na ufanisi katika kazi zao. 

   “Kutokana na taarifa za tafiti mbalimbali imebainishwa kuwa bara la Africa lina hekari 600 milioni ambazo hazitumiki ambazo zikitumika ipasavyo zitaweza kuzalisha chakula cha kulisha watu wapatao bilioni 9 hadi kufikia mwaka 2050 na ardhi hii haitanufaisha bara la Afrika tu bali dunia nzima, sekta ya kilimo inaonekana kuwa na fursa kubwa, kinachotakiwa ni kujipanga kuhakikisha inaenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolia yanayobadilika kila siku”Alisema Sembeye. 

   Sembeye aliipongeza kampuni ya TBL Group na ABInBev kwa kuanzisha mkakati wa kushirikiana na makampuni ya wasomi wabunifu kutafuta njia ya kuwawezesha wakulima wadogowadogo kuongeza uzalishaji kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa “Nawaasa mhakikikishe kazi za washindi wa leo na mawazo mazuri yaliyopatikana kwenye kongamano hilo yafanyiwe kazi kwa lengo lililokusudiwa la kuongeza uzalishaji kwa wakulima wadogo kupitia teknolojia za kisasa. 

   Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGGOT), Geoffrey Kirenga ,alisema kuwa wakati umefika sasa wa watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwenye kilimo badala ya kubaki nyuma kama watazamaji.

   Aliwataka pia wasomi wa kitanzania kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo sambamba na ubunifu wa nyenzo za kisasa na kuongeza kuwa vijana ambao ni wengi wasiogope kujiingiza huko kwa kuwa kuna fursa kubwa “Tunapoongelea kilimo cha kisasa na cha kisayansi hatupaswi kuwaacha vijana nyuma kwa kuwa ndio watumiaji wakubwa wa vifaa vya teknolojia za kisasa,wakivitumia kwa shughuli za kilimo wanaweza kunufaika na kuinua maisha yao” Alisema. 

   Mkurugenzi wa kitengo cha sheria na Masuala ya Ndani wa kiwanda cha bia cha Nile,nchini Uganda kilichopo chini ya kampuni ya ABINBEV,Onapito Okomoloit,, alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited (NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mvua,wakiwezeshwa kiteknolojia wataongeza uzalishaji na maisha yao kuwa bora. 

   Mwanzilishi wa taasisi ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah ,amesema kuwa kongamano la mwaka huu limepata mafanikio makubwa hususani kwa kutoka na maazimio ya kupambana na changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.
  Washindi wa shindano la ubunifu wa kiteknolojia katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

  0 0


   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali.

   Majengo mapya yaliyokarabatiwa katika shule ya msingi Ihembe.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Kagera.
  Baadhi ya wananchi wa Ihembe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kwenye uzinduzi wa madarasa yaliyokarabatiwa.

  ...................................................
  Wananchi wa kijiji cha Ihembe wilayani Karagwe Mkoani Kagera   wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukarabati miundombinu ya shule yao msingi ya Ihembe ambayo hapo awali ilikuwa katika hali mbaya.

  Awali wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wakisomea katika madarasa machakavu sana ambayo yalijengwa tangu mwaka 1948. 

  Kufuatia hali hiyo, Julai mwaka jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alifanya ziara shuleni hapo na kukutana na  hali hiyo ambayo ilimhuzunisha na kuamua kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.

  Kwasasa shule hiyo ina vyumba vitano vya madarasa, matundu ya vyoo nane, pamoja na stoo zimeboreshwa kisasa. 

  Katika uzinduzi huo, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa kwa ushirikiano mkubwa anaoufanya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI hadi kufanikiwa utekelezaji wa mradi huo pamoja na miradi mingine ya Afya, na barabara. 

  Jafo anaendelea na ziara yake mkoani Kagera ya uzinduzi wa miradi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali akiwa na Kamati ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
                                                                                              
    Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

  Hayo ya mesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

  Dkt. Mpoki amesema wamepata kibali hicho kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuongeza kwamba Wizara yake inalo jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya utumishi wa kada za afya chini ya Wizara ya Afya.

  Aidha, alisema kibali hicho chenye aina mbili za mwajiri ikiwepo nafasi 6,180 ambazo zimeenda Hospitali zilizo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Nafasi 1,820 zimeenda Hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara zingine na Taasisi za Umma pamoja na Hospitali ya Mlongazila na Benjamini Mkapa.

  Alitaja sifa za waombaji wa nafasi hizo kuwa, awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiri wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali na asiwe ameshawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi.Hata hivyo, Dkt. Mpoki amewakumbusha wataalam hasa wale wanaosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma kuambatanisha nakala za usajili au leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika wakati wa maombi hayo.

  Katibu Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na kueleza kuwa nafasi hizi 8,000 ni juhudi za Serikali za kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya. 

  Imetolewa na : 
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya 
  11/5/2018

  0 0

  Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young (wa pili kushoto) akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Kulia ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young (wa pili kushoto) alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Kulia ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania.
  Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young akimkabidhi zawadi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Wa kwanza kushoto ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania na wa kwanza kulia ni Bw. Said Athumani, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa TRA.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young wakipeana mikono baada ya kumaliza mazungumzo wakati Balozi huyo alipomtembelea Kamishna Mkuu ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Wa kwanza kulia ni Bw. Said Athumani, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa TRA. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Maruku katika Halmashauri ya  wilayani ya Bukoba
  Wananchi wa kijiji cha Maruku wakiwa katika mkutano wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye wodi ya wazazi.
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI na  Mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini  Jasson Rweikiza akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kwa uwekaji wa jiwe la msingi katika wodi ya wazazi Maruku.
  Mjumbe wa kamati ya Utawala na TAMISEMI Mhe. Khatib Said Haji akiwahimiza wananchi wa Maruku katika kuhusu kushiriki kwenye maendeleo.
  Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Angelina Malembeka akiongea na wananchi wa kijiji cha Maruku Bukoba vijijini.

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na wajumbe wa Kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.................................................................
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameimwagia sifa Kamati ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI kwa ushauri na usimamizi wake.


  Waziri Jafo aliyasema hayo alipokuwa amealikwa na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini kuweka jiwe la Msingi katika wodi ya wazazi ya zahanati ya Maruku ambayo inatarajiwa kuwa Kituo cha afya.Amesema anashukuru kamati hiyo kwa maelekezo, ushauri na usimamizi wake kwa wizara hiyo.

  Katika zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi, Waziri Jafo ameambatana na Kamati ya Bunge ya TAMISEMI ambayo ipo mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua miradi iliyo chini ya Ofisi ya TAMISEMI. 

  Naye, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini Mhe. Jasson Rweikiza alimshukuru Waziri Jafo  kwa uchapakazi na usikivu wake katika utekelezaji wa ushauri na  maelekezo ya kamati ya Bunge.

  Aidha, wajumbe wa kamati wamewataka wananchi wa Bukoba vijijini kushikamana kwa pamoja na mbunge wao katika ajenda ya kujiletea maendeleo.

  0 0


   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo  akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali.

   Majengo mapya yaliyokarabatiwa katika shule ya msingi Ihembe.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Kagera.
  Baadhi ya wananchi wa Ihembe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kwenye uzinduzi wa madarasa yaliyokarabatiwa.

  ...................................................
  Wananchi wa kijiji cha Ihembe wilayani Karagwe Mkoani Kagera   wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukarabati miundombinu ya shule yao msingi ya Ihembe ambayo hapo awali ilikuwa katika hali mbaya.

  Awali wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wakisomea katika madarasa machakavu sana ambayo yalijengwa tangu mwaka 1948. 

  Kufuatia hali hiyo, Julai mwaka jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alifanya ziara shuleni hapo na kukutana na  hali hiyo ambayo ilimhuzunisha na kuamua kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.

  Kwasasa shule hiyo ina vyumba vitano vya madarasa, matundu ya vyoo nane, pamoja na stoo zimeboreshwa kisasa. 

  Katika uzinduzi huo, Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa kwa ushirikiano mkubwa anaoufanya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI hadi kufanikiwa utekelezaji wa mradi huo pamoja na miradi mingine ya Afya, na barabara. 

  Jafo anaendelea na ziara yake mkoani Kagera ya uzinduzi wa miradi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali akiwa na Kamati ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI.

older | 1 | .... | 1579 | 1580 | (Page 1581) | 1582 | 1583 | .... | 1898 | newer