Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

Mkazi wa Zanzibar ajishindia bidhaa zenye thamani ya Tsh. milioni 1 kutoka Jumia

$
0
0
Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo amejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili. 

Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.

Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.

“Mimi ni mteja mzuri wa Jumia kwa sababu naitumia mara kwa mara kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikinifika mpaka ninakoishi Zanzibar. Baada ya kuliona hili shindano, niliona ni vema nimpendekeze mwenzangu ashinde. Ukizingatia tupo kwenye maandalizi ya ndoa yetu, suala la mahari pamoja na vyombo vya ndani ni gharama hivyo ushindi wake ungekuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli yetu,” alisema Bw. Juma ambaye ni mchumba wa mshindi wa kampeni hiyo, Bi. Patricia.

“Sikuwa na wasiwasi kwamba endapo angeshinda asingeweza kupatiwa zawadi zake. Kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mashindano kadhaa kama vile ‘Treasure Hunt’ kipindi cha Mobile Week, wateja walikuwa wanashinda simu na kukabidhiwa bila ya ubabaishaji wowote,” alimalizia Bw. Juma.

Akielezea furaha yake mara baada ya kutangazwa mshindi Bi. Patricia Philipo amesema kuwa, “kusema ukweli hapo mwanzo sikutarajia kama ningeweza kushinda kutokana na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wangu. Kuna wakati nilitaka kukata tamaa kwa sababu mwenzangu alikuwa ameniacha mbali, mashabiki wake walikuwa wanamuunga mkono na kuwashirikisha wengine kwa kiasi kikubwa.”

“Lakini niliongeza bidii na kumuomba Mungu ili niweze kufanikiwa. Na kweli ilifika mahala mpinzani wangu akakata tamaa. Hapo ndipo mimi nilipoongeza bidii zaidi na kufanikiwa kuibuka mshindi,” aliongezea Bi. Patricia na kuhitimisha, “nina furaha kubwa katika kipindi hiki kwani zawadi niliyoshinda ni kubwa. Vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja si jambo la kawaida. Jumia wameweka alama kubwa katika maisha yangu na nawaombea waendelee kuwajali wateja wao kwa bidhaa bora, ofa lukuki pamoja na kuwa waaminifu.”

Kampeni ya ‘Big Home Makeover’ kutoka Jumia ilyodumu kwa takribani mwezi mmoja, ilikuwa na dhamira ya kuwawezesha wateja wake kununua vyombo vya ndani kwa gharama nafuu. Lakini pia ilitoa fursa ya kumzawadia mteja mmoja aliyependekezwa na mtu wake wa karibu vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni mmoja. 

“Tunampongeza mshindi wetu Bi. Patricia kwa ushindi aliojipatia lakini pia tunawasihi wateja wetu kuchangamkia bidhaa mbalimbali kwenye mtandao wetu. Kupitia mtandao unaweza kuokoa muda na gharama pamoja na usumbufu wa kufuata bidhaa. Lakini cha muhimu ni njia salama na ya uhakika, Jumia inawapatia fursa wateja wake kufanya manunuzi na kisha kulipia baada ya kuridhika na mzigo aliofikishiwa,” alisema Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey.

“Hivi sasa kupitia mtandao wetu tunaendesha kampeni ya kutoa punguzo kubwa la bei ambalo hauwezi kupata sehemu yoyote. Kwa mfano, simu zinazouzwa Jumia ni pungufu ya shilingi 50,000 tofauti na ukienda kwenye maduka moja kwa moja, vivyo hivyo kwa bidhaa nyinginezo, kila bidhaa utakayoiona basi ujue imepunguzwa kiasi hicho! Tunawasihi watanzania wasicheze mbali na jumia ili kuweza kunufaika na mambo haya mazuri,” alihitimisha Geofrey. 
a.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni moja,Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo mara baada ya kujishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.

Bi. Patricia Philipo aliibuka mshindi baada ya mchumba wake Bw. Mwalim Juma Kumpendekeza ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.  
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akizungumza mapema leo jijini Dar kuhusu ushindi wa Mkazi wa visiwani Zanzibar, Bi. Patricia Philipo (hayupo pichani) aliyejishindia vyombo vya ndani vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka Jumia kupitia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ katika mwezi uliopita wa Aprili.Pichani kushoto ni Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma. 

Mshindi huyo alipatikana kupitia kampeni iliyoendeshwa kwa jina la ‘Big Home Makeover’ kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Wateja walitakiwa kupendekeza mtu wao wa karibu ambaye waliona anastahili nyumba yake kupendezeshwa na Jumia kwa kupatiwa ofa ya vyombo vya ndani.
 Afisa Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Hadija Natalia Tuwano pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey wakimsikiliza kwa makini Mchumba wa mshindi,Bw. Mwalim Juma  akitoa ushuhuda wa namna alivyompendekeza Mchumba wake na kujishindia vyombo vya ndani  mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,Mwalimu Juma  alimpendekeza mchumba wake Bi. Patricia Philipo ashinde zawadi ya vyombo hivyo ili kumrahishia asije kusumbuka kununua tena pindi watakapofunga ndoa.

NG'UMBI AVISHWA RASMI CHEO CHA BRIGEDIA JENERALI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa  Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi amemvisha  rasmi Kanali R.C Ng’umbi  cheo kipya cha  Brigedia Jenerali.

Brigedia Jenerali Ng’umbi  ambaye pia ni Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Tanzania  nchini China , ni miongoni mwa maofisa  27 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo  tarehe 12 Aprili mwaka ,2018 na Rais na Amiri Jeshi  Mkuu Dkt. John Magufuli.

 Akizungumza Mara baada ya kuvalishwa Cheo hicho jana Mei 7 , Brigedia Jenerali  alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu  Dk. Magufuli  pamoja na uongozi wa Makao Makuu ya Jeshi kwa kupandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.

Tukio hilo lilifanyika  katika ofisi za  ubalozi wa Tanzania nchini China  na kuhudhuriwa na maofisa  pamoja na watumishi  kutoka ofisi  za Ubalozi  pamoja na familia zao.
 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa  Kairuki kwa niaba ya Makao Makuu ya Jeshi akimvisha  rasmi Kanali R.C Ng’umbi  cheo kipya cha  Brigedia Jenerali katika hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China.
  Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa  Kairuki, Brigedia Jenerali, R.C Ng'umbi  wakiwa katika picha ya pamoja  na Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.
  Brigedia Jenerali R.C Ng'umbi akiwa katika  picha ya pamoja  na Balozi Mbelwa Kairuki, Maafisa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.

JAFO AAGIZA KUREKEBISHWA MAZINGIRA YA SOKO LA FERI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo  akikagua soko la samaki Feri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo  akiagana na viongozi mara baada ya kukagua soko la samaki Feri.
..............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Soko la samaki Feri pamoja na Manispaa ya Ilala kufanya marekebisho ya soko hilo ndani ya siku 45 ili wafanya biashara waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama.

Jafo ametoa maagizo hayo alipotembelea sokoni hapo leo hii na kukutana na baadhi ya mambo hayapo sawa ikiwemo ubovu wa mifumo ya maji taka, uchakavu wa meza za kuzuia samaki, kukosekana kwa mapanda ya kuuzia samaki kwa wavuvi wadogo, na kusitishwa kwa huduma ya mamalishe na babalishe kwa upande wa wavuvi wadogo.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo ameagiza kufanyike marekebisho ndani ya siku hizo 45 sambamba na kuwarejesha wafanyabiasha wa chakula katika eneo la wavuvi wadogo ili nao wajipatie mahitaji yao ya kimaisha kama ilivyokuwa hapo awali.

Aidha, Waziri Jafo amewataka wavuvi na wafanya biashara wa soko la feri kuzingatia sheria kwa kutoruhusu watu wanaojishughulisha na shughuli haramu za uuzaji wa madawa ya kulevya kujiingiza katika maeneo yao.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI APRIL WASHUKA

CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI

$
0
0
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Utawala na Fedha), Prof. Ernest Kihanga, akisoma hotuba yake kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Miaka Minne utakaotafiti na kuonyesha njia sahihi ya sekta isiyo rasmi kupata Huduma za Hifadhi za Jamii.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Washiri kutoka ndani na nje ya nchi.
Abbas Cothema Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF akiwa katika kongamano hilo.
 Meza Kuu.



Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.
Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.

Anne Kamau kutoka Institute Development Studies (IDS) Chuo Kikuu cha Nairobi akitoa mada kuhusu sekta isiyo rasmi katika Huduma za Hifadhi za Jamii.
Washiriki.
Washiriki.


Abbas Cothema Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF akitoa mada katika kongamano hilo.
Abbas Cothema Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF akitoa mada katika kongamano hilo.
Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Godbertha Kinyongo, akizungumza na wandishi wa habari.

NA MWANDISHI WETU
LICHA ya kuchangia asilimia 35 katika pato la taifa, bado sekta isiyo rasmi haijapewa uzito unaostahili kwa kutoshiriki ipasavyo kwenye hifadhi za jamii.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa miaka minne utakaotafiti na kuonesha njia sahihi ya Sekta isiyo rasmi kupata huduma za hifadhi za jamii.
“Tumeona tufanye utafiti ili kuona namna sahihi ya kusaidia waliojiajiri kwenye sekta isiyorasmi kwa kuwa ni kundi kubwa linalofanya biashara ndogondogo zinazochangia karibu asilimia 35 kwenye pato la taifa.
“Katika mradi huu tunaziangalia sekta za aina tatu zisizo rasmi kwanza ujenzi, usafirishaji na wajasiriamali ambao ndio kundi kubwa… kama bodaboda vijana wetu wengi wamejiajiri humu lakini hawana taarifa za kutosha kuhusu haki yao ya kuingia kwenye hifadhi za jamii.
“Hawa mama lishe wengi lakini jiulize wangapi wamejisajili na NSSF? Wangapi wanazo kadi za bima ya afya? Hawa madereva wa bodaboda kila leo wanapata ajali wangapi wanazo bima za matibabu?.
“Hao ndio tunaowazungumzia na tumewaalika kwenye warsha hii waje waseme changamoto zao na tutawaambia namna ya kutoka huko ili wafanye kazi zao kwa furaha na amani wajue kwamba mchango wao kwa taifa ni mkubwa,” alisema Dk. Kinyondo.
Kuhusu mradi huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Profesa Ernest Kihanga aliyemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, alisema mradi huo ulioanza mwaka 2017 hadi mwaka 2020 umeshirikisha wasomi kutoka nchi tatu tofauti kwa ufadhili wa Shirika la Msaada la watu wa Denmark (DANIDA).
Alivitaja vyuo vilivyoshiriki kwenye mradi huo wa utafiti kuwa ni Chuo Kikuu cha Roskile kutoka Denmark, Chuo Kikuu cha Nairobi cha Kenya na Mzumbe kutoka Tanzania.
Alisema utafiti uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2014 ulionesha kwamba watu wanane kati ya 10 waliopata kazi kwa mara ya kwanza walikuwa kwenye sekta isiyo rasmi.
“Ni ukweli usiopingika kwamba sekta isiyo rasmi inakuwa kwa kasi… sio tu hapa Tanzania ama Kenya, bali katika nchi nyingi zinazoendela ulimwenguni kote.
“Ninafahamu kwamba watafiti mbalimbali wamekwishafanya tafiti katika sekta hii kwa ujumla wake na hasa katika kuangalia jinsi gani shughuli za wafanyakazi katika sekta hii zinaweza kurasimishwa.
“…Umasikini wa mahitaji muhimu ambao inamaanisha uwezo wa mwananchi kushindwa kujipatia mahitaji muhimu ya maisha umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2006 mpaka asilimia 28.2 mwaka 2012.
“Katika kipindi hicho hicho, umasikini uliokithiri ulipungua kutoka asilimia 11.7 mpaka asilimia 9.7 ingawa kuna ukuaji unaowasaidia wananchi masikini, bado maandiko yanasema asilimia 70 ya watanzania wanaishi chini ya Dola mbili za Marekani kwa siku.
“Hakika, wengi walioko katika biashara hii ya bodaboda, ama wafanyabiashara ndogondogo ama mafundi ujenzi hawana aina yoyote ya ulinzi wa kijamii inayowalenga.
“Nilikua nasoma ripoti ya polisi ya usalama barabarani ya mwaka 2016 kwa bodaboda pekee na imeonyesha mfano mwaka 2014 kulikua na ajali 4,169 zilizosababisha vifo 928 na majeraha 3,884; mwaka 2015 kulikua na ajali 2,626, vifo 934 na majeraha 2,370.
“…Kwa robo mwaka pekee ya mwaka 2016 kulikua na ajali 663; vifo 200 na majeraha 559,” alisema Profesa Kihanga.

WAKULIMA NJOMBE WAFURAHIA MBEGU BORA YA MUHOGO WAWASHUKURU WATAFITI SERIKALI

$
0
0

Wakulima na wakazi wa kata ya Lupembe Mkoani Njombe wakifurahia mavuno makubwa ya mbegu za Muhogo zinazostawi kwenye maeneo ya baridi kali.

Na: Calvin Edward Gwabara
Njombe.

Wakulima Mkoani Njombe wamewashukuru watafiti na Serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa mbegu bora za muhogo ambazo zinauwezo wa kustawi kwenye maeneo ya baridi hasa nyanda za juu kusini baada ya utafiti  wa mwaka mmoja ulifanywa na watafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Mikocheni MARI na chuo kikuu cha Dar es salaam.

Wakiongea kwa furaha wakati wa zoezi la kuvuna mihogo hiyo ambayo ilipandwa mwaka mmoja uliopita wakulima hao wamesema sasa wamepata zao la biashara la uhakika baada ya zao la la chai kusumbua biashara yake .

Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake bwana Mapambano Luhongori Mkazi wa kijiji cha Lupembe wilaya ya njombe mkoani humo amesema kuwa Zao la Muhogo sasa litakuwa mkombozi kwa wakulima wengi ambao wamekuwa na shauku ya kulima zao hilo ili kuweza kunufaika na fursa kubwa ambazo wanazipata wakulima wa mikoa mingine kama vile Mara, Geita na Pwani.

‘’ Kutokana na uhitaji na soko kubwa la muhogo mkoani njombe nimejaribu mara kadhaa kulima zao la muhogo bila mafanikio lakini siamini macho yangu leo kuona katika eneo hilihili ambalo tulipanda mbegu hizi bora za watafiti kwenye shamba darasa imetoka mihogo mingi na mizuri kiasi hiki, ila nimegundua kuwa mbegu tulizokuwa tunatumia za kienyeji hazifai ukanda wetu’’ Alisema Luhongoli mkulima kutoka mkoa huo.
Mtafiti kiongozi wa Utafiti huo Dkt. Joseph Ndunguru akifafanua jambo kwa wakulima mara baada ya kuvuna baadhi ya mashina hayo kwenye kila aina 75 walizopanda eneo hilo.
Kwa upande wake Bi Rehema Malekela ambaye pia alishiriki kuanzia mwazo wa utafiti mpaka wakati huu wa kuvuna amesema kilimo cha zao hilo kilikuwa kidogo sana ambapo familia zimekuwa zikilima mashina machache kuzunguka nyumba kwaajili ya vitafunywa vya chai tu baada ya kuona zao hilo haliwezi kuwapatia tija kama wakulima wa maene mengine nchini.

Bi Malekela ameongeza kuwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani waislamu hupata shida sana kupata muhogo na hivyo kuwalazimu baadahi ya wafanyabiashara wengi kwenda kufuata mihogo kwenye mikoa mingine inayozalisha zao hilo kwa wingi na kuja kuiuza mkoani humo kwa bei kubwa.

“ Kwakweli ukifunua moyo wangu na moyo wa kila mtu unayemuona hapa aliyekuja kushiriki zoezi hili utaona furaha isiyo na kifani ndio maana unaona tumejitokeza kwa wingi watu kutoka Tarafa nzima kuja kushuhudia kupatikana kwa zao linguine la biashara kwenye eneo letu” Alisema Bi. Malekela kwa niaba ya wakina mama wengine.

Mamia ya wakulima na wakazi wa Kata ya Lupembe na maeneo mengine waliojitokeza kuangalia matokeo hayo ya utafiti kuona kama wanaweza kulima Muhogo kwenye ukanda huo wa baridi kali.

Aliongeza kuwa kingine kikubwa wanachowashukuru watafiti hao ni kuwaahidi kuwapelekea mbegu hizo kila mkulima kupitia vikundi vyao na kuwafundisha namna ya kuchakata muhogo na kupata bidhaa mbalimbali kama vile clips,Biskuti,Maandazi na aina zingine za vyakula ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Kwa upande wake mtafiti kiongozi wa utafiti huo kutoka Kituo cha utafiti wa Kilimo Mikocheni MARI Dkt. Joseph Ndunguru amesema kuwa kwa muda mrefu wakulima kwenye maeneo ya baridi wamekuwa hawalimi zao hili hali ambayo imekuwa ikiwakosesha fursa mbalimbali zitokanazo na zao hilo ambazo wakulima wa maeneo yenye joto wanazipata kwa kuzalisha muhogo.

Amesema katika utafiti huo wamepeleka mbegu aina 75 za muhigo katika maeneo matatu ya utafiti huo ambayo ni Mkoa wa  Njombe ambapo wanaangalia aina za muhogo kati ya hizo ambazo zitastawi na kuvumilia baridi hadi la nyuzijoto 16 -22C na eneo linguine ni mkoa wa Dodoma kuangalia aina ya mihogo itakayoweza kuvumilia ukame na Mkoa wa Pwani katika eneo la Chambezi ambapo wanaangalia changamoto ya joto na magonjwa.
Dkt. Joseph Ndunguru na Dkt. Gladness Temu wakiwa wamebeba moja ya mashina ya mbegu hizo yaliyovunnwa hivi karibuni katika eneo la Chambezi ambalo walikuwa wakiangalia mbegu zinazostawi kwenye eneo la Joto na magonjwa.
‘’ Kwakweli tumepata mafanikio makubwa sana kwa mfano kwa Mkoa wa Njombe kwenye baridi ,aina 47 kati ya aina 75 tulizopanda kwenye shamba hili kwenye eneo lenye bardi zaidi tum  eona zimefanya vizuri sana nah ii ni kutuonyesha kuwa sasa wakulima wa eneo hilo wanaweza kunufaika na kilimo hiki’’ Alisema Dkt. Ndunguru.

Mtafiti huyo ameongeza kuwa pamoja na kufanya vizuri kwa aina hizo 47 lakini wamegundua kuwa katika eneo hilo shina linatoa mihogo mingi sana lakini haiwezi kukomaa kwa muda wa mwaka mmoja kama ilivyo kwenye maeneo yenye joto na hivyo kuhitaji muda zaidi ya mwaka mmoja ili inenepe na kukomaa vizuri.

Kwa upande wake mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt. Gladness Temu ambaye ni mtafiti katika mradi huu amesema kuwa katika kipindi chote cha utafiti huo wamekuwa wakitembelea shamba hilo na kuchukua takwimu mbalimbali muhimu ambazo zitakuja mwishoni kusaidia katika hitimisho na mapendekezo kwa wakulima.
Dkt. Gladness Temu akiinua shina la Muhogo walilovuna huko Chambezi hivi karibuni.

Amesema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na kuangalia kama mbegu hizo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia magonjwa mabayo ni hataro sana kwa mihogo kwa sasa lakini hayakujitokeza kabisa kwenye shamba hilo hali ambayo inawafanya kuamini uzalishaji utakuwa mkubwa sana katika eneo hilo.

‘’ Katika kuhakikisha magonjwa hayo hayatokei kabisa tutawaletea mbegu bora na safi ili waanze kilimo hicho bila magonjwa nah ii itawasaidia sana sasa kuwa wazalishaji wa mbegu za muhogo wazuri maana eneo lao halina magonjwa hayo kwa sasa’’ Alisistizia  Dkt. Gladness.

Mradi huu wa utafiti unafanywa kwa kushirkiana na nchi Tatu za Tanzania,Kenya na Hispania kwa ufadhili wa shirikala la maenedeleo la umoja wa Ulaya kupitia kwa shirikala la chakula na kilimo duniani  FAO.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha utafiti wa Kilimo Mikocheni cha jijini Dar es salaam MARI wakifurahi wakati waliposhirikiana kuinua shina moja la Muhogo huko Chambezi Bagamoyo.


WAZIRI MAHIGA AFUNGUA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA, ISRAEL

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel Ufunguzi huo ulifanyika jijini Tel Aviv tarehe 08 Mei 2018. Wengine katika picha ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima.wakigongesheana glasi kwa ajili ya kuwatakia afya njema viongozi wa mataifa yao, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga wakisalimiana na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked walipowasili kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiweka saini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa ajili ya kuzifungua rasmi. Anayemwangalia ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked 
Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked akiweka saini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa ajili ya kushiriki ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akibadilishana mawazo na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked walipowasili kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwahutubia mamia ya watu hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. Pembeni yake ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet. 
Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked akiwahutubia mamia ya watu hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. Kushoto ni Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima. 
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akiwahutubia mamia ya watu hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. Waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi Israel. 
Bi. Kisa Doris Mwaseba (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Israel. 
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anaiwakilisha pia Tanzanaia nchini Uswisi, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Zurich. Dkt. Possi alikuja kumpokea na kumsindikiza Mhe. Waziri akiwa njiani kuelekea Israel. 




Dkt, Mahiga afungua Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Israel

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania. 

Ufunguzi wa ofisi hiyo ya ubalozi iliyopo katika mji wa Tel Aviv ulifanyika leo na ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked, Mabalozi wa nchi za Afrika na Watanzania wanaoishi nchini humo.

Katika hotuba yake, Dkt. Mahiga aliitaja Israel kama nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake lakini bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji, viwanda, matibabu, TEHAMA, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.

Kwa upande wa ulinzi na usalama, Waziri Mahiga alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi leo.


Dkt. Mahiga alieleza kuwa Israel ni nchi yenye mafanikio makubwa duniani ambapo imepelekea raia wake wengi kushinda tuzo za Nobel na hiyo imetokana na harakati zao kwa ajili ya wanadamu.Aliishukuru Israel kufuatia mawaziri wake wawili kufanya ziara za kikazi nchini Tanzania hivi karibuni. Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi, Mhe. Avigdor Liberman aliyetembelea Tanzania tarehe 20 hadi 22 Machi 2018 na Waziri wa Sheria, Mhe. Ayelet Shaked ambaye alikuwa nchini tarehe 23 na 24 Aprili 2018.

Katika ziara hizo masuala mbalimbali yaliafikiwa ikwemo Israel kuisaidia Tanzania kuanzisha chombo cha kutoa msaada wa kisheria kwa wasiojiweza ambacho kwa upande wa Israel kimeshaanzishwa na kina mafanikio makubwa.Dkt.Mahiga aliwakaribisha Waisrael kuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii kwa kuwa Tanzania ina vivutio lukuki vya utalii. Alisema zaidi ya watalii elf 50 wanakuja Tanzania kila mwaka lakini hawatoshi kutokana na uwingi wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wake, Mhe. Shaked alibainisha kuwa Israel ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo kusaidia teknolojia ya kisasa kwenye kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji.Aidha, Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima alishukuru wadau wote ikiwemo Serikali ya Israel kwa kumpa ushirikiano wa kutosha uliofanikisha upatikanaji wa ofisi hiyo na kufunguliwa rasmi tarehe 08 Mei 2018. Aliwahakikishia umma uliohudhuria hafla hiyo na wadau wengine kuwa wasisite kufika kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma watakazozihitaji. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Israel
09 Mei 2017

JAFO AAGIZA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI KATIKA VITUO VYOTE VYA AFYA 208 VINAVYOBORESHWA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa agizo la ufungwaji wa mifumo ya kielektroniki katika vituo vya afya vinavyojengwa nchin.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakati alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato katika vituo vyote vya Afya 208 vinavyoboreshwa hapa nchini. 

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo alipotembelea wilayani Chamwino mkoani Dodoma kukagua Ujenzi wa kituo cha Afya Chamwino ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amewapongeza watendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi vizuri wa miundombinu hiyo ambapo amejulishwa kuwa hadi sasa jengo la upasuaji, maabara, nyumba ya daktari, chumba cha kuhifadhi maiti, na wodi ya wazazi zipo hatua za mwisho. 

Kufuatia maendeleo hayo mazuri ya ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini, Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ili vituo hivyo vitakapokamilika viweze kukusanya mapato ipasavyo na kutoa huduma bora kwa wananchi.

WASHIRIKI WA WAZO LA UBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA MAPINDUZI YA KILIMO YA ABINBEV NA TBL GROUP WAPIGWA MSASA DAR

$
0
0
Washiriki wa wazo la ubunifu wa teknolojia ya mapinduzi ya kilimo ya ABINBEV na TBL Group wapigwa msasa Dar es Salaam Washiriki wa wazo la ubunifu la kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo watakaotangazwa katika mkutano mkubwa wa masuala ya ubunifu,matumizi ya teknolojia na ukuzaji wa sekta ya kilimo katika ustawishaji wa jamii unaojulikana kama ,The East Africa (EA) Innovation Event, utakaofanyika jijini Dar es Salaam . 

 Mkutano huu umeandaliwa na kampuni ya ukuzaji ubunifu wa kiteknolojia ya Bits & Bytes kwa kushirikiana na kampuni ya ABIn Bev Africa na Tanzania Breweries Limited,na umelenga kuonyesha ubunifu unavyoweza kuleta mabadiliko endelevu kwenye jamii, mojawapo ikiwa mradi wake kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo unaojulikana kama Smart Barley.

 Utakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wataalamu wa kilimo,wabunifu,wahandisi na jamii mbalimbali za wafugaji na utajikita zaidi kujadili ya kupambana na changamoto zinazowakabili wakulima wadogowadogo nchini na mikakati ya kuwawezesha kuongeza mavuno kutokana na shughuli zao za kilimo. 

 Meneja wa huduma za kilimo wa IBinBev Afrika Mashariki , Coetzee Theunis , alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited (NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mvua.

Kwa kuwawezesha kupata teknolojia za kisasa wataweza kuongeza mavuno zaidi na maisha yao kuwa bora zaidi. Kwa upande wake mwanzilishi wa kampuni ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah Zuweina Farah,amesema kuwa mkutano wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa kwa ushirikiano na kampuni ya ABIn Bev,utajadili changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.
 Baadhi ya washiriki wa shindano la wazo la ubunifu wakimsikiza Meneja wa sekta ya kilimo wa ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Coetzee Theunis
 Makamu wa Rais wa kampuni ya Solutions Africa Zone Lee Dowson wapili (kushoto) akifafanua jambo juu ya mashine ya kupandia nafaka iliyobuniwa na wanachama wa Better Planters Enterprise (BPE) toka Arusha
 Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
---

UZINDUZI WA COPA UMISSETA SINGIDA WAFANA

$
0
0
 Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Na Mwandishi Wetu- Singida. 

Mashindano ya Copa Umisseta ngazi ya mikoa yanaendelea ambapo yamezinduliwa mkoani Singida, katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi, aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo. Hafla ya uzinduzi huo wa michezo hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo, wadau wa michezo, walimu na wanafunzi wa shule za sekondari ambao walishiriki kucheza michezo mbalimbali. 

 Mkuu wa mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi katika hotuba yake ya ufunguzi,aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kutoa udhamini kwa michezo hiyo na amewaasa washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumizi ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.

 Alisema mashindano hayo ni jukwaa kubwa la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo na Ushahidi wa suala hili upo kwa kuwa kuna wanamichezo wengi wanaotokea mkoani Singida ambao vipaji vyao viliibuliwa na Umisseta vilevile mkoa huo katika mashindano ya mwaka jana ulifanya vizuri katika ngazi ya kitaifa kwa kushika nafasi ya tatu. 

Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa bidhaa za Coca-Cola mkoani Singida, Joseph Simplis ,amesema Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 na lengo kubwa ni kuhakikisha inawashirikisha wanafunzi wengi zaidi nchini sambamba na kuibua na kukuza vipaji vya michezo.Aliwaasa wanafunzi wa Mtwara kuchangamkia fursa hii. Katika kufanikisha michezo hii, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikitoa udhamini wa vifaa vya michezo ambapo imelenga kusambaza vifaa kwa shule za sekondari 4,000. 

Katika uzinduzi huo alikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni kwa wawakilishi wa shule mbalimbali mkoani humo. Uzinduzi wa Copa Umisseta mkoani Singida ni wa tano kufanyika baada ya kufanyika katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Mashindano hayo ngazi ya kitaifa yatafanyika mwezi Juni mwaka huu mkoani Mwanza.

Waziri Mwakyembe afungua Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

$
0
0
Na Genofeva Matemu- WHUSM

Timu za majeshi kupitia michezo mbalimbali zimetakiwa kuweka mikakati na kuibua wanamichezo wazuri ambao wataiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa na kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) katika uwanja wa uhuru jana Jijini Dar es Salaam

“Ni matarajio yangu kuwa uwepo wa michezo hii inaashiria azma na nia thabiti ya kurejesha enzi  za majeshi yetu kutoa uwakilishi ulio mzuri katika michezo ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo zamani” amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed amesema kuwa kufanyika kwa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi kila mwaka kunathibitisha azma ya JWTZ kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kuunda timu za JWTZ zitakazotumika kuimarisha timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ya Kimataifa. 
Jenerali Yakubu amesema kuwa uwepo wa michezo ya majeshi katika jumuiya ya Afrika Mashariki umekua nyenzo ya kudumisha amani baina ya nchi wanachama hivyo wachezaji watakaopata fursa kushiriki michuano hiyo washiriki vema na kuleta tija kupitia michezo hiyo. 

Mashindano ya Muula wa tano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) yenye kauli mbiu isemayo “Tushiriki Michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda   Afya zetu na kudumisha mshikamano” yataendana na uteuzi wa wanamichezo watakaoteuliwa kuunda timu za JWTZ zitakazoshiriki mashindano tarajiwa ya Majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko nchini Kenya mwaka 2019
 Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipokua akikagua timu hiyo wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Makao Makuu ya Jeshi wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

UMMY MWALIMU – SERIKALI IMETENGA BILION TATU (3) KWA AJILI YA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI

$
0
0


  Mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Bw. Richard Jordison, akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.

  Balozi wa GGM, Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge, iliyofanyika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyoko jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.

 Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communcations, Ms. Fatma Fernandes wa pili kutoka kulia, ambaye alinunua picha ya makamu wa Raisi Mheshimiwa Samia Suluhu katika mnada uliofanyika wakati wa uzinduzi wa Kili Challenge ili kukusanya fedha za kupambana na UKIMWI, jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100M) kwa watoto wa kituo cha moyo wa huruma kilichopo Geita ili kusaidia mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt.Leornard Maboko, Mkurugenzi wa GGM, Bw. Richard Jordison na kulia, Mkurugenzi wa kituo cha Moyo wa Huruma Sister Adalbera Mukure.
 Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge, katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyoko jijini Dar es salaam.
    Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu akishiriki katika harambe iliyofanyika kwenye uzinduzi wa Kilimanjaro Challenge ili kuchangia mfuko kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI nchini.
  Makamu raisi wa GGM, Bw. Simon Shayo akizungumza katika uzinduzi wa Kilimanjaro Challenge ya mwaka 2018, jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Dar es salaam: Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ilizindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kili Challenge 2018), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.  Shughuli hii ilifanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu, aliitikia wito wa kufika Dar es salaam, katika hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, ambapo alifanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na  kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro.

Kili Challenge ni mfuko unachangia juhudi za serikali  katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU). Kili Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulishirikisha Tume ya kuthibiti UKIMWI, Tanzania TACAIDS, na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja (1) zilikusanywa katika tukio hilo.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameitaka serikali kutumia mbinu mbalimbali na kuweka mikakati itayohakikisha fedha zinazotwengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI zinatumika kwa kusudi hilo, na hivyo kuondokana na kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo zinatakiwa zielekezwe moja kwa moja kwa wahusika na sio kutumika kama posho za vikao, huku zikionyesha jitihada zilizofanywa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, pia akiendelea kusema, fedha hizo zinatakiwa kuisaidia nchi katika kuzipa nguvu sekta ndogo ili kuthibiti maambukizi ya UKIMWI nchini.
Katika harambee iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa Kili Challenge Mheshimiwa Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, alisema harambee hiyo iliyoandaliwa ili kudhibiti UKIMWI, ni muhimu kwa lengo maalumu ili kuacha kuwa tegemezi wa misaada, huku akiendelea kusema serikali imetakiwa kuwa na ubunifu, kama kweli imedhamiria katika mapambano haya, na kusema moja ya mbinu ni kwa kushirikiana kwa ukaribu na sekta binafsi ili kutafuta namna ya kupambana na UKIMWI.
Aidha Mhe. Ummy Mwalimu aliwaomba wadau kuweka mbele moyo wa kujitolea na kuchangia mfuko wa Kili Challenge kwa manufaa ya wananchi. Alisema wahenga walisema  kutoa ni moyo na si utajiri. Kwa upande wa Serikali, tayari tumetenga fedha Bilioni tatu (3 bilioni) kwenye bajeti ya 2018/2019 ili iendelee kuchangia mfuko wa UKIMWI uliouanzishwa mwaka 2015.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu geita (GGM), Bw. Richard Jordison alisema GGM kwa ushirikiano na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania, (TACAIDS) na washiriki wengine imekusudia kuona jamii yenye afya na nguvu ya kuzalisha kama ambavyo ni malengo ya serikali kuifanya Tanzania ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Pia akitumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Tanzania kwa niaba ya wafanyakazi wa GGM, kwa ushirikiano walioutoa tangu kuanza kwa Kili Challenge mwaka 2002.
Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania, (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko, alisema kutokana na kuendelea kuwepo kwa VVU na UKIMWI, ushiriki wa wadau mbalimbali nchini, hususani sekta binafsi umekuwa siku zote ukipewa kipaumbele na serikali. Hivyo kuendelea kutekelezwa kwa mfuko huu wa Kili Challemge hapa nchini siyo tu kumeongeza huduma kwa walengwa bali imesaidia utekelezaji wa dhima ya “Kili Challenge” ya kushirikisha wadau kuchangia kwa hali na mali katika udhibiti wa UKIMWI.

Dkt. Leonard Maboko amesema pamoja na hatua zilizofikiwa kwenye mwitikio dhidi ya VVU na UKIMWI tangia ugunduliwe, UKIMWI bado ni tatizo kubwa kijamii na kiuchumi nchini. Kwa mfano, bado kuna maambukizi mapya yanayokadiriwa kufikia 81,000 kila mwaka, ambapo kiwango cha maambukizi ni 4.7 %. Aidha takribani watu milioni 1.4 wanaishi na VVU nchini Tanzania, huku akieleza zaidi kuwa wanawake wa rika zote bado wanaathirika zaidi na UKIMWI kuliko wanaume. 

Hali hii inaonesha kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa wanalemewa na mzigo wa ugonjwa wa UKIMWI. Katika jitihada za kujenga mwitikio kabambe wa kitaifa, Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imeendelea kushughulikia changamoto za unyanyapaa, usawa na Ukatili wa Kijinsia ili kulinda haki za watu walioathirika kwa njia moja au nyingine na janga la VVU na UKIMWI.

Mkurungenzi wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko, amesisitiza wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia mwitikio wa kitaifa dhidi ya UKIMWI ili mchango wa sekta binafsi uendelee kuongeza nguvu kwenye jitihada za serikali na kupunguza pengo linalotokana na mchango wa Serikali na Wahisani.

Vilevile, Mkurugenzi wa TACAIDS,  Dkt. Leonard Maboko, ameushukuru uongozi wa GGM kwa kushirikiana nao hadi kutimiza miaka 17 ya utekelezaji wa mfuko huu wa Kili Challenge huku akisema hiki ni kielelezo cha ushirikiano wa sekta binafsi katika udhibiti wa UKIMWI nchini.

Lakini pia mkurugenzi wa GGM, Bw. Richard Jordison alitoa shukrani zake kwa Balozi wa GGM Bw, Mrisho Mpoto kwa kazi nzuri anayoifanya, huku akisema, “Msanii huyu amekuwa Balozi mzuri kwenye masuala ya UKIMWI na hasa kuhamasisha uchangiaji wa fedha katika mfuklo wa Kili Challenge kwa kupanda au kuzunguka mlima wa Kilimanjaro kupitia baiskeli.”

Ili kushiriki GGM Kili Challenge, unaweza kuchangia mfuko huu kwa kujifadhili au kumfadhili mwingine kupanda au kuzunguka mlima Kilimanjaro. Kwa mawasiliano zaidi au kutoa mchango wasiliana nasi kupitia email: GGMkilichallenge@anglogoldashant.com, au tovuti www.geitakilichallenge.com.

Geita Gold Mine na TACAIDS tunatumia mwamvuli huu wa Kili Challenge katika kuelimisha jamii kuhusu janga hili la VVU/UKIMWI na tunatarajia siku moja Tanzania itatangaza kuisha kwa maambukizi ya VVU/Ukimwi kama takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 %  mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.geitakilichallenge.com

MAKAMANDA WA POLISI WAJINOA KUUKABILI UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Kamishna wa Polisi (Ushirikishwaji wa Jamii), Mussa Ali Mussa akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Baadhi ya Makamanda wa Polisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya IGP Simon Sirro (hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utu wa Mtoto, Mtengeti Koshuma (kushoto) na Mwakilishi wa UNFPA nchini Bi Christine Mwanukizi(kulia) baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).

MAKAMANDA WA POLISI WAJINOA KUUKABILI UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Kamishna wa Polisi (Ushirikishwaji wa Jamii), Mussa Ali Mussa akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Baadhi ya Makamanda wa Polisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya IGP Simon Sirro (hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utu wa Mtoto, Mtengeti Koshuma (kushoto) na Mwakilishi wa UNFPA nchini Bi Christine Mwanukizi(kulia) baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).

MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

$
0
0
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae  kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa  mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.
Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.

Dar es Salaam, 09 Mei 2018. Mashindano maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia kuwavutia mashabiki wengi  wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote wa mbio hizo.

Katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’ ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo. Baada ya majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.

Tofauti na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.

"Kimataifa, Rotary na vilabu vyake wana sifa ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa kupitia wanachama wake wa kujitolea, wakielekeza karibia asilimia mia ya fedha zote za miradi kwa walengwa”, alisema raisi wa sasa wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay, Anne Saels. “Tunaamini kwamba kupitia miradi ya elimu iliyopangwa tunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye maisha ya watu katika jamii na tunafuraha kuwa mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary yatakuwa na jukumu muhimu katika kukamilisha hili”.

Mwenyekiti wa bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah anaamini kuwa  mashindano hayo kwa mwaka huu hayatawaangusha mashabiki. “Kwa motto ya ‘Wakanda Goat Are You’,tukikumbuka muvi iliyofanya vizuri kwa mwaka huu ya ‘Black Panther’, tunatumai kuwavutia mashabiki wapya na wadau wa mbio za mbuzi vilevile”,aliongea mwenyekiti huyo.

Kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita, mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yamefanikiwa kuvutia wadhamini wakuu kama vile Toyota, Swiss International Airlines na Coca Cola. Tunashukuru kwa imani ya wadhamini wetu katika shirika letu na tunaamini kuwa mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yatakuwa ya burudani kwa kila mmoja”.

Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Rotary nane jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi , mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za  kwenye wilaya za kupanda miti. Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii.

Dkt, Mahiga atembelea taasisi ya Save the Children Haert ya Israel

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameshukuru Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuokoa maisha ya watu wengi nchini, hususan watoto.

Waziri Mahiga alitoa shukrani hizo leo alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu aliyoianza jana. "Zamani nilijua kuwa mtu akizaliwa na maradhi ya kurithi, mtu huyo hawezi kuishi lazima atakufa, lakini uwepo wa taasisi yenu kumenifanya niondoe itikadi hiyo" Dkt. Mahiga alisema.

Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart imeisifu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa ni moja ya Taasi bora kusini mwa Jangwa la Sahara na kwamba ina uwezo na wataalam wa kufanya upasuaji bila ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi. "Serikali inachotakiwa kufanya ni kuiboresha taasisi hiyo kwa kujenga majengo mapya na kuipatia vifaa zaidi na itakapofanya hivyo itaokoa maisha ya watu na fedha nyingi ambazo zingelitumika kugharamia matibabu nje ya nchi". Mkurugenzi wa taasisi hiyo alishauri.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo alimweleza Dkt. Mahiga kuwa taasisi ilianzishwa miaka ya 90 kwa madhumuni ya kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi ya moyo duniani kote, hususan katika nchi zinazoendelea. Hadi sasa imeshatoa matibabu kwa zaidi ya watoto 460,000 wenye maradhi ya moyo kutoka Afrika, Amerika, Asia na kwingineko.

Shughuli za taasisi hiyo inajumuisha kutibu wagonjwa, kutoa mafunzo kwa madaktari na wakufunzi na kusambaza madaktari katika nchi mbalimbali kuendesha upasuaji kwa kipindi maalum. Madaktari waliopewa mafunzo na taasisi hiyo wanaendelea kupata miongozo ya taasisi wanaporejea katika nchi zao kwa ajili ya kufanya matibabu.

Mhe. Waziri alipokuwa katika taasisi hiyo alipata fursa ya kuonana na Watanzania wanaosoma na wengine wanaopata matibabu ya maradhi ya moyo katika taasisi hiyo. Aidha, alioneshwa watoto wawili wanaougua maradhi ya moyo kutoka Nymmar na Romania ambao kwa mujibu wa Mkurugenzi alisema ndio wa kwanza kupokelewa kutoka nchi hizo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Israel
10 Mei 2017 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akiongea na wawakilishi wa Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo kujionea namna inavyoendesha shughuli zao. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimjulia hali mmoja wa watoto kutoka Tanzania anayepata tiba ya maradhi ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel 
Kutoka kulia, mtu wa kwanza na wa pili ni Watanzania wanaosomea fani za tiba za maradhi ya moyo katika taasisi ya Save the Children Haert wakiongea na Mhe. Waziri wakati alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel leo. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Save the Children Heart ya Israel akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri hayupo pichani namna taasisi hiyo inavyofanya kazi. 
Wanne kutoka kushoto ni wanafunzi kutoka Tanzania wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya Moyo wakimsikiliza Mkurugenzi wao hayupo pichani. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Save the Children Heart/ 
Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akibadilishana mawasiliano na wanafunzi wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya moyo kutoka Tanzania. 
Ulinzi wa Mpaka kwenye Ukanda wa Ghaza 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Afisa Usalama kutoka Kitengo cha Protection Unit alipowasili katika eneo la Netiv Haasara lililopo Ghaza ambapo ni mpakani na eneo la Palestina linalotawaliwa na Hamas. 
Mkazi wa eneo la Netiv Haasara, Ghaza, Bibi Hila Fenton akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri na wajumbe wengine kuhusu madhila wanayokutana nayo wananchi wa Israel wanaoishi karibu na mpaka wa Ghaza. 
Bibi Hila Fenton akionesha mabaki ya gruneti la kwanza kabisa kurushwa kutoka Palestina na kuangukia kwenye eneo wanaloishi mwaka 2001/ 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akipokea maelekezo alipowasili eneo la mpaka katika ukanda wa Ghaza lililojengwa ukuta/ 
Wageni wanaofika katika eneo la mpaka huu wanaombwa kuandika ujumbe wa matumaini katika mawe yaliyotengenezwa kwa sanaa ya aina yake na kuyabandika kwenye ukuta unaozuia maguruneti kupita. Hapo Mhe, Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima wakibandika vijiwe vyenye ujumbe wa kuleta matumaini kwenye ukanda wa Ghaza. 
Bi. Kisa Mwaseba naye akibandika ujumbe wake 
Sehemu ya ukuta wa sengenge unaotenganisha mpaka wa Israel na Palestina katika Ukanda wa Ghaza. 
Sehemu ya ukuta uliojengwa imara kuzuia vijiji vya Israel vilivyo mipakani visifikiwe na mashumbulizi ya magruneti. 

Eneo la Ukaguzi wa Malori ya mizigo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipata maeleozo kutoka kwa Meneja wa Usalama wa ukaguzi wa malori ya mizigo yanayokwenda Palestina kutoka Israel na kinyume chake. 
Meneja wa Usalama anatoa maelezo namna kazi ya kukagua malori ya mizigo inavyofanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia uwezekano wowote wa kupitisha vilipuzi au vifaa vya kuundia vilipuzi. 
Baadhi ya Malori ya mizigo
baadhi ya mizigo ambayo imekamilika kukaguliwa inasubiri kusafirishwa
Eneo la ukaguzi wa maslori ya mizigo ambalo pia limejengewa ukuta kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya maguruneti. 
Scanner inayotumika kukagua malori ya mizigo ambayo ina nguvu kubwa ya kubaini vifaa vilivyobebwa katika lori kimoja baada ya kingine. kutokana na nguvu ya scanner hiyo harusiwi mtu kukaa karibu inapofanya kazi. 
Waziri Mahiga akionesha moja ya mitambo iliyofungwa kwa ajili ya kuzuia bomu lisilipuke kabla halijasababisha madhara.

TAARIFA YA UAPISHO KUTOKA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA LEO

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mhe. Alphayo Kidata  aliyemuapisha kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora   wakila kiapo cha ahadi na uadilifu kwa viongozi wa umma kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza  baada ya kuwaapisha  Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.Wengine mbele Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na  Mhe. Alphayo Kidata aliyemuapisha kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Balozi wa Tanzania nchini  Canada aliyemaliza muda wake Mhe. Jack Zoka  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. 

Picha na IKULU

Waziri Dkt. Mahiga afanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akipeana mkono na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman walipokutana jijini Tel Aviv leo asubuhi kwa ajili ya kufanya mazungumzo 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na ujumbe wake (kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo ambapo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kushirikiana katika masuala ya ulinzi na usalama. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wa kwanza kulia na akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima na Afisa Dawati wa Israel, Bi Kisa Mwaseba wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Israel. 
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman wa kwanza kulia akisisitiza jambo kwenye mazungumzo hayo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi zawadi kwa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman walipokutana jijini Tel Aviv leo asubuhi. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga naye akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman jijini Tel Aviv leo asubuhi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israaele, Mhe. Avigdor Liberman. 
Waheshimiwa Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima wa kwanza kushoto na Balozi wa Israel nchini Kenya ambaye anawakilisha pia Tanzania.

Tatu Mzuka yatangaza ushirikiano wa kibiashara na Wema Sepetu

$
0
0
Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, leo imetangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu.

Ushirikiano huu ni mwendelezo wa mpango mkakakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania katika kuboresha maisha yao. Kusudi hasa la Tatu Mzuka kama ilivyoelezwa ni kusambaza fursa kwa watu wengi kadri inavyowezekana ili kubadilisha maisha yao.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alisema kwamba ushirikiano huu ni mmojawapo kati ya nyingi ambazo Tatu Mzuka wanajihusisha nazo.‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.‘Ninawashukuru sana Tatu Mzuka kwa ushirikiano huu, ambao hakika sio tu utanigusa mimi bali mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla wao katika kujitengenezea fursa za kuboresha maisha yao’ alisema Wema.

Wema alisema kwa kuanza, anaomba mashabiki zake wachangamkie fursa ya kucheza Tatu Mzuka, ambapo kama unatumia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, unaingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111 na baada ya hapo unaweka namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na jina langu WEMA na baada ya hapo ingiza kiasi unachotaka kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000.

‘Pamoja na kujiongezea nafasi za kushinda za kawaida za Tatu Mzuka kila saa hadi milioni 6, kila siku unaweza kushinda milioni 10 pamoja na zaidi ya milioni 140 kila Jumapili, utapata fursa zaidi ya zawadi mbalimbali kutoka kwa Wema’ alisema Wema. Pamoja na utambulisho wa Wema, Tatu Mzuka pia ilitangaza kwamba Jumapili hii ya tarehe 13 ambayo ni siku ya mama duniani kuna milioni 140 ambayo lazima itolewe kwa mtu mmoja pamoja na mama yake.

‘Hii ni fursa kwa kila mtanzania ambaye kwa namna moja ama nyingine angependa kumshukuru mama yake au mlezi wake kwa kazi kubwa aliyofanya, na hivyo ukicheza sasa, unaingia kwenye Mzuka Deile ambayo inafanyika kila siku Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo milioni 10 lazima itoke kwa mtanzania mmoja na yeye atamgawia mama yake milioni 3, wakati Jumapili hii kwenye Mzuka Jackpot yeyote atakayeshinda milioni 140 atambusti mama yake kwa milioni 30’ alihitimisha Maganga
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu pichani kushoto.

‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.

Bi Wema Sepetu akizungumza mbele ya waanidishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano nae wa kibiashara .

Wema Sepetu akifurahia jambo mara baada ya kutangazwa ushirikiano wake na kampuni ya The Netwek-ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live


Latest Images