Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 156 | 157 | (Page 158) | 159 | 160 | .... | 1903 | newer

  0 0

   TAMASHA LA FILAMU LA DAR FILAMU FESTIVAL (DFF 2013) KUFANYIKA 24TH– 26TH SEPTEMBER 2013 VIWANJA VYA CoICT- UDSM- POSTA KIJITONYAMA,  DAR ES SALAAM. 

  Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa www.filamucentral.co.tz  inapenda kutambulisha kwenu Tamasha la filamu linaloitwa Dar Filamu Festival (DFF) 2013 litalofanyika katika uwanja wa CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama,  kuanzia tarehe 24- hadi 26, September,2013 Tamasha litaambatana utoaji wa  Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure kwa siku tatu.Kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.


  Tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa ya ajili kwa vijana na jamii husika kwa ujumla, filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na hapa nchini katika kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya filamucentral kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu Ulimwenguni.


  Kwa tamasha hili la awali tutaonyesha filamu za hapa Tanzania pekee ikiwa ni utambulisho wa Dar Filamu Festival kwa mara ya kwanza kwenu wanahabari, miaka ijayo Tamasha litahakikisha linashirikisha filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha ya Kiswahili  kutoka popote Ulimwenguni.


  Akiongea na Waandishi wa Habari mratibu wa Tamasha hilo Staford Kihore pia amesema kuwa katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu siku tatu hizo kila siku imepewa jina kwa filamu zitakazoonyeshwa Tarehe 24th September, 2013 siku ya Jumanne ambayo ndio siku ya ufunguzi utakuwa ni usiku wa Bongo Movie Classics, 25th September, 2013 ni usiku wa Quality Nights.


  Na ile siku ya mwisho tarehe 26th September, 2013 itakuwa ni Stars Nights siku ambayo kutakuwa na wasanii wetu mbalimbali ambao wanajenga soko hilo la Bongo movie filamu, Tamasha hili linapambwa na wasanii wote wakiwakilishwa na wasanii wenzao wawili ambao ni Vincent Kigosi ‘Ray’ kama Official Producer and Director  for DFF 2013 na Elizabeth Michael ‘Lulu’ kama Official Actress for DFF 2013.


  Pia tamasha litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu kwa asubuhi ambapo madarasa  yataendeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa tarehe 24 September, 2013 masomo ya Uandishi wa Muswada, Uigizaji na  Uongozaji wa filamu yatafundishwa kwa washiriki, 25th September 2013 Siku nzima Makapuni ya Utengenezaji filamu yataonyesha na kutangaza kazi zao kwa wadau mbaliambali.


  Tarehe 26thSeptember 2013 ni siku muhimu sana kwani Taasisi kama vile TRA, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza, Wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine watakutana katika jukwaa la majadiliano kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu, pia filamu kadhaa zitaonyeshwa na kujadiliwa na wadau watakaokuwepo matukio yote ya asubuhi yatafanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa.


  Pia tunatoa shukrani kwa taasisi za Serikali kutuunga mkono katika ufanikishaji wa tamasha hilli la Dar Filamu Festival (DFF) 2013, taasisi kama Bodi ya Filamu na ukaguzi wa michezo ya kuigiza Tanzania, Tanzania Film Federation (TAFF), MFDI, Swahiliwood na makapuni ya usambazaji wa filamu Steps Entertainment Ltd, Leo Media na kampuni mpya ya usambazaji ya Proin Promotion ambayo imeanza hivi karibuni na kuonyesha dhamira ya kusaidia tasnia ya filamu, pia leo tunazindua mtandao wa www.dff.or.tz


  Kwa kutambua mchango wako kama mwanahabari tunaamini utaungana nasi katika kuhakikisha DFF inakuwa ni chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania, huku tukisema kuwa Dar Filamu Festival2013 kwa kauli mbiuya ‘Ubora wa Filamu Zetu’ ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja na kuwa jukwaa linalojenga tasnia ya filamu inayokua kila siku. Pia tunaomba ushiriki wako katika kufanikisha hili.


  Mratibu wa Tamasha la DFF 2013


  Staford Kihore.
  0 0

  ???????????????????????????????Balozi mpya wa vijana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania Bi.Tamara Bertha Itanisa. ???????????????????????????????Mabalozi wapya wa vijana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania Bi.Tamara Bertha Itanisa na kushoto ni naibu wake Alice Mseti.Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Snura 'Mama wa Manjanga' akiwapa ujumbe wa Tupo Wangapi??? Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond 'Sukari ya Warembo' akiwapa ujumbe wa Tupo Wangapi??? Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, H.Baba 'Mkali wa Mauno' akitoa burudani kwa Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia nyaraka za aina kumbukumbu mbalimbali kwenye maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya kumbukumbu za Kitaifa za Oman Dk.t Hemed Mohammed Al-Dhawyani kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa maonesho ya kumbukumbu za nyaraka ya kitaifa za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0     Kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga.
  ====  =====  ======
   Mwaka huu yadhamini tena uchapishaji wa stika za usalama barabarani pamoja na wiki ya usalama barabarani .
  Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa moja kati ya makampuni ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali kwa

  dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za barabarani.


  Akithibitisha madai hayo, Kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel imeweza kutoa mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa ikitoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na

  kikosi cha usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha ajali za mbarabarani.


  "Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani,  kwa miaka mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia imedhamini vipindi

  vya elimu ya usalama barabarani katika TV - kumekucha na Jambo Tanzania (ITV na TBC 1) na Radio one.


  Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na jeshi la polisi usalama barabarani  imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu =,Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati

  wakiendesha magari, vile vile  mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (Bodaboda) yaliyokuwa na lengo

  la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki ," alisema DCP Mpinga.


  Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania Bi Beatrice Singano Mallya, akizungumza juu ya suala hilo, amesema "Airtel imeamua kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani.


  Idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua  kujikita katika kuokoa maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujuma. Tunapenda kuwakumbusha watanzania

  kuwa swala la kupunguza ajali za barabarani ni wajibu wa kila mwananchi  hivyo tutii sheria bila shuruti"


   Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha lengo letu la kupunguza ajali linafanikiwa, tumeanza kuona mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabarani zinapungua kulinganisha na miaka iliyopita," alisema Beatrice.


  Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu wiki ya nenda kwa usalama barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza kupungua kwa kiasi kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana nao

  katika programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea mwaka 1995 ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000 na 4,000. Lakini Mwaka 2010 ukilinganisha na  2011 ajali zilipungua kwa 3% na 2011 na 2012 ajali zilipungua kwa 2%.


   Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini wiki hii ambapo kwa mwaka huu imejitolea kuchapisha tena stika za usalama barabarani pamoja na kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha bodaboda yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono juhudi za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote ili kuepusha ajali.


  0 0

    Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Kufuata Kanuni za Kiislamu (Islamic Banking), wa Benki ya NBC Tanzania, Yassir Masoud (katikati) akizungumza katika droo ya awamu ya pili  kupata washindi wawili waliojishindia safari wao na wenza wao inayolipiwa kila kitu na NBC kushiriki ibada ya Hija mjini Makka nchini Saudi Arabia baadae Mwezi ujao. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
    Meneja Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Eddie Mhina akipiga simu kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Islamic Banking ya benki hiyo ambayo washindi wawili na wenzao wao watalipiwa gharama zote kwenda Makka nchini Saudi Arabia kushiriki ibada ya Hijja baadae mwezi ujao. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo, Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
  Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein (katikati) akihakiki majina ya washindi wa kampeni hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo. 
  Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akifurahi pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati baadhi ya washindi wakielezea furaha yao baada ya kupigiwa simu na kujulishwa kujishindia safari ya kwenda hijja itakayolipiwa kila kitu na NBC. Kutoka kushoto ni Ofisa katika Idara ya Operesheni, Edesia Kahyarara, Meneja Masoko, Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano, Eddie Mhina na  Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein. 

  0 0
 • 09/09/13--08:18: JIFUNZE SAYANSI YA KIAFRIKA


 • UNGO AFRIKA ni taasisi inayo jihusisha na masuala ya utamaduni,mila na desturi za kiafrika . Tunapenda kuwatangazia watu wote kuwa tunatoa kozi maalumu ya kujifunza kozi iitwayo “ SAYANSI YA AFRIKA”. Katika kozi hii utajifunza namna ya kutumia NGUVU YA SAYANSI YA KIAFRIKA katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayo zunguka maisha ya kila siku ya mwanadamu kama vile (mapenzi/mahusiano, ndoa), biashara, kazi, ulinzi na magonjwa.  Tunapatikana jijini Dar Es salaam, na tunao wataalamu walio bobea katika sayansi ya kiafrika kutoka katika makabila yote ya Tanzania bara na visiwani. Wataalamu wetu wana ujuzi na uzoefu wa SAYANSI YA KIAFRIKA kutoka katika mataifa yote ya kiafrika,Arabuni na India.
  Tupo jijini Dar Es salaam.  Masomo kuanza, tarehe 01 OKTOBA 2013
  Kujiandikisha, tuandikie kupitia barua yetu :ungoafrika@gmail.com

  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 SEPTEMBA 2013.
  WAZUNGU WANAITA UCHAWI, LAKINI SISI TUNAITA, “ SAYANSI YA KIAFRIKA”

  KWA PAMOJA TUUNGANE KATIKA KULINDA NA KUENDELEZA, MILA,DESTURI NA TAMADUNI ZA MWAFRIKA.
  Kwa updates kuhusu taasisi yetu na shughuli zetu, endelea kutembelea:

  0 0

   Menina akifanya yake

   Vanessa jukwaani akiimba Closer

   Snura Majanga akitoa burudani

  Walter Chillambo akiimba
    Mashabiki waliojitokeza wakishangilia 

   Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki
  Wasanii wa Marco Chali Foundation wakiwa katika picha ya pamoja.

  ========  ===========  =========
  MSANII wa muziki wa kileo kutoka nchini Ghana Fuse ODG, Azonto amezikonga nyoyo za wapenzi wa burudani baada ya kuchanganya staili yake ya uchezaji Azonto pamoja na ile ya Kiduku ya hapa nchini.


  Fuse ODG ambae anajulikana zaidi kama Azonto alipanda jukwanii majira ya saa tisa kasoro usiku baada ya wasanii wengine wengi kumaliza kutoa burudani. Ilikuwa ni baada ya kupanda kwa kundi la Tip Top Connection huku likiongozwa na msanii Madee pamoja na msanii Chid Benz ambae aliimba nao kama msanii rafiki.

  Baada ya kumalizika kwa shoo hiyo kwa wasanii hao wa hapa nyumbani ndipo alipopanda msanii Azonto ambae alisikika akihamaisha kwa kutajan maneno ya kiswahili kama vile, Nawapenda, Mambo vip na piga kelele.


  Msanii huyo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwaweka karibu zaidi wapenzi wake wa burudani hasa pale alipowapandisha jukwaani vijana wawili kucheza nao Azonto na Kiduku.


  Alianza kwa kuwachezesha Azonto na kisha muda huo huo aliwabadilishia muziki na kucheza nao kiduku huku mwenyewe akiahidi kuiendeleza zaidi staili hiyo.


  Akizungumza baada ya onesho hilo alisema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo wasanii na watu wa Dar es salaam walivyompokea na kuahidi kuwa ataiendeleza staili ya kiduku nakuitangaza zaidi.


  "Mimi kwanza niliwahi kuja Tanzania na kufikia kule Arusha kwa mapumziko na kwa sasa nimekuja kwa kazi na nipo tayari kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kwani mwisho wa siku sisi ni waafrika ambao tunatakiwa kusaidiana na kuendelezana" alisema Azonto.


  Wasanii kama vile Madee, Tunda Man, Water Chilambo, Menina Atik, kundi la Navy Kenzo, B Heats, Mabeste, Eskide, Mapacha na wengineo wengi pia walitoa burudani safi siku hiyo. 

  0 0

  18Pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza zikiwa tayari kwa ajili ya kukabidhiwa.19 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha moja ya pikipiki kbaada ya kuzikabidhi kwa viongozi wa Kata 9 za Wilaya ya Nzega,20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki kwa Hanifa Musa Kutoka kata ya Isanzu huku Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala katikati akishuhudia tukio hilo.21 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk. Khamis Kigwangala mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa kikundi cha wazee wa Nzega mjini humo.22Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye akizunumza na wana Nzega.23Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizunumza na wananchi wakati alipowaambia hakuna haja ya kubadilisha mbunge mara kwa mara katika uchagzi kama mbuge aliyepo anafaa na anawatumikia wananchi vizuri kama vile Dk. Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala

  1Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye ukiwasili katika mji wa Nzega Katika wilaya hiyo Tayari kwa kuanza Ziara ya Siku 18 katikia mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara kesho ambapo ziara hiyo itaanza katika mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu huyo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo, Kinana leo amezungumza na wananchi wa Nzega na kukutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ambapo pia amepokea Pikipiki tisa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Dk. Khamis Kigwangala ambazo ambazo amezikabidhi kwa viongozi wa kata 9 kati ya 21 zilizopo katika Wilaya hiyo, ambapo pia amekabidhi mashine ya kutotolea vifaranga vya kuku kwa kikundi cha wazee wa Nzega , Pikipiki hizo zimekabidhiwa katika kata za Budushi, Ndala, Puge, Nkininziwa,Mbogwe, Lusu, ,Ijaniga, Utwigu na Isanzu baadae pikipiki 7 zitafutaiwa na kisha kata tano za mwisho. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NZEGA 2Vijana waendesha pikipiki na baiskeli wakiongoza msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 3 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu mara baada ya kuwasili wilayani Nzega leo 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita katikati ya vijana wa Greenguard wa CCM huku wakitoa heshima zao mble ya mgeni huyo mara baada ya kuwasili wilayani Nzega leo. 5Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali. 6 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama mbalimbali na wananchi mara baada ya kuwasili wilayani Nzega. 7Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi 8 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisamewa risala wakati alipozindua mradi wa ujenzi wa vibanda vya biashara vya mradi wa Chama cha Mapinduzi Wilayani10Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akizungumza na wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza. 11Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa Ndugu Nape Mosses Nnauye huku katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga makofi 12 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi huku Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza. 13Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo 14Wananchi wa Nzega wakiimba kwa furaha mara baada ya kumpokea katika mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana. 15Umati wa wanavikundi wakiwa katika mkutano huo17Mbunge wa Jimbo la Nzega Khamis Kigwangala akimsikiliza akiongea na wananchi 

  0 0

  Chifu wa Wasukuma Wilaya ya Kwimba Shimbi Martin Morgan akimabidhi silaha za jadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za kumtawaza kuwa Mtemi wa Sungusungu Kitaifa, zilizofanyika kijiji Ngudu, Wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza. 
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0
 • 09/09/13--14:01: --none--


 • 0 0

   Watoto yatima waliopo kwenye kituo cha Fema Matamba.
   Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akiongea na watoto na walezi wa kituo cha watoto yatima FEMA Matamba.
   Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akisalimiana na watoto yatima wa kituo cha Fema Matamba.
   Katibu akimpa mlezi wa watoto hao misaada hiyo
   Sehemu ya misaada iliyotolewa na chama hicho
  Muonekano wa kituo cha watoto yatima FEMA Matamba.
  ==========
  Jamii nchini imetakiwa kujenga desturi ya kusaidia wasiojiweza hasa watoto waishio katika mazingira hatarishi na wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima kwa kuwa hawakupenda kuishi maisha wanayoishi ya kukosa wazazi

  Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu wakati akikabidhi vitu mbalimbali vilivyotolewa na chama hicho vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 60,000 kwa ajili ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha FEMA Matamba kilichopo chini ya KKKT kilichopo kata ya Matamba wilaya ya Makete mkoani Njombe

  Mtaturu amesema wao kama chama wameguswa na namna watoto hao wanavyoishi katika kituo hicho kuwa wanahitaji misaada ya kila namna kutoka kwa wanamakete na ndio maana wamefikia hatua hiyo ambayo wanaimani itaungwa mkono na watu wengine

  "hawa watoto ni wetu na hakuna anayeweza kuja kutusaidia kuwalea kwa uchungu kama sisi wenyewe, sisi kama chama cha mapinduzi wilaya ya makete tumeonesha mfano kwa hiki kidogo tulichokileta tunaomba na wengine wawasaidie watoto hawa" alisema Mtaturu

  Kwa upande wake askofu Job Mbwilo ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na CCM wilaya ya Makete na kusema anaimani kuwa wapo wengine watakaojitokeza kuwaunga mkono hasa ukizingatia kituo hicho hakina mradi unaokiwezesha kupata fedha zaidi ya kutegemea misaada kwa wajerumani pamoja na wadau wengie wanaoguswa kuwasaidia kutoka ndani na nje ya nchi
   
  Chama hicho kimetoa sukari, sabuni pamoja na biskuti kwa ajili ya watoto hao 

  0 0

   The Bank of Tanzania (BoT) Deputy Governor Economic and Financial Policies Dr. Natu Mwamba (left)   receives a 10m/- dummy cheque from the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (second right) in fulfillment to the bank’s pledge to support  BoT’s Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund. 
   The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (right) explains a point to the Bank of Tanzania (BoT) Deputy Governor Economic and Financial Policies Dr. Natu Mwamba (left)   shortly before handing over a 10m/- cheque in fulfillment to the bank’s pledge to support  BoT’s Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund.
  The Exim Bank Tanzania Assistant Marketing Manager Anita Goshashy (right) clarifies a point during the event. Looking on at the left is the Photo by Staff Photographer. The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant. 
  =======  ======  =======
  EXIM bank Tanzania has handed over ten million shillings to support Bank of Tanzania’s (BoT) Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund, as Exim Bank’s commitment to supporting the education sector.

  BoT earlier last month announced that it was to sponsor six undergraduate and post graduate students pursuing maths, science and technology studies under the Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund.

  Speaking during a handover event held at the BoT headquarters in Dar es Salaam at the weekend, the Bank of Tanzania (BoT) Deputy Governor Economic and Financial Policies Dr. Natu Mwamba said the Fund is dedicated to the sponsorship of undergraduate female students pursuing maths, science and technology studies in the country’s varsities this year.

  “The fund will sponsor both male and female Tanzanians pursuing undergraduate degrees in economics, information technology, accounting and finance as well as students intending to pursue master’s programmes in those fields. “The scholarship will be granted on academic merit and be based on a rigorous selection process, it said, adding that successful applicants will be granted full scholarship including a lap top, ” she said.

  Dr Mwamba said the scholarship will cover all direct university costs -- tuition and registration and all direct student costs-- meals, accommodation, books and stationery besides field practical training, special faculty requirements and other related costs as specified in the respective Institutions’ cost structure. The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant during the occasion said, “Our institution appreciates the importance of supporting the education of promising youth for the future of the nation.”

  The bank’s Assistant Marketing Manager at Exim Bank, Anita Goshashy, added, “As part of our Corporate Social Responsibility (CSR), the bank has already supported a number of initiatives in education.”

  The Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund was formally launched in Arusha last year by H.E. President Jakaya Kikwete with an objective of promoting interest and excellence in maths, science and technology courses among female students.

  Every year the Fund intends to sponsor at least 25 eligible students and beneficiaries of the scholarship will include top female best performers in math or science subjects and admitted at a Tanzanian university to pursue undergraduate studies on a full-time basis.

  0 0

   Zuberi Mussa  katika muonekano wa picha tofauti 
  tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.

  Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira mkoani Tanga, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.

  Na Dotto Mwaibale, Tanga

  Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.

  Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili na ya tatu wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamshi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha  kama mtu aliyechanganyikiwa.

  Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa jadi.

  Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.

  Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

  Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.

  Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja na mke wake kipenzi  Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.

  Ndugu wanahabari wenzangu  na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote, Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali na vyama vya michezo  hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi wanayopata kwa waganga wa kienyeji badala yake wapelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.

  0 0

  Afisa Mwandamizi wa manunuzi Bodi ya michezo ya kubahatisha, Sadick Kasuhya kulia akimkabidhi mmoja ya madawati 100 yaliyotolewa kwa ufadhili wa Bodi ya michezo ya kubahatisha kwa Mbunge wa Viti maaluma kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Lita Kabati tukio lililofanyika katika shule ya msingi Sabasaba mkoani Iringa.
  ======  =====  ======
  Na Denis Mlowe,Iringa   .
    

  MBUNGE  wa Viti Maalum  Mkoa wa Iringa(CCM) Lita Kabati  ametoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 6.3  kwa shule za msingi  zilizoko mkoani hapa.


  Kabati akizungumza wakati akikabidhiwa madawati hayo kwa ufadhili wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania mwishoni mwa wiki, alisema shule nyingi mkoani hapa zina upungufu mkubwa wa madawati hivyo ni jukumu la kiongozi kuweza kusaidia kuondokana na hali hii na kuwashukuru bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania

  .

  “Nimefanya ziara katika shule za msingi nyingi za mkoani kwangu kuna matatizo mengi kama ukosefu wa madawati na vitabu ndipo nikawaomba wenzetu wa bodi ya michezo kubahatisha wanisaidie madawati kwa shule hizi hakika ninawashukuru sana hakika haitamaliza tatizo lakini itasaidia kupunguza japo kwa uchache” alisema Kabati


  Alisema kuwa elimu bora kwa wanafunzi wa shule za msingi unaendana na vifaa wanavyotumia katika kupata elimu ya msingi ikiwemo kakaa katika madawati bora kunachangia maendeleo ya taifa letu katika kukuza elimu.


  Kabati aliwataka viongozi wengine kuondokana na tabia ya kufikiria kuwa katika kuleta maendeleo ya mkoa ni mojawapo ya kampeni bali ni kuungana na kuweza kupambana katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaowawakilisha.


  Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Afisa Mwandamizi wa manunuzi Bodi ya michezo ya kubahatisha, Sadick Kasuhya alisema moja ya majukumu ya bodi kuweza kusaidia jamii katika sekta ya elimu na wataendelea kusaidia shule mbalimbali nchini. 


  Alisema kuwa kwa msaada huu wa madawati  100 yenye thamani ya shilingi milioni 6, 3 kutasaidia kupunguza tatizo la madawati kwa baadhi ya shule zitakazokabidhiwa msaada huo.
  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akizindua rasmi uwanja wa ndani wa michezo kwa kukata utepe. Walioshika utepe huo kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Malya Ndugu Allen Alex, Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamadunu na Michezo, Ndugu Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve na wa mwisho ni Mbunge wa Kwimba.
  Mkuu wa Chuo cha Michezo cha Malya Ndugu Allen Alex akimwelezea rais Jakaya Kikwete ramani ya eneo lote la chuo mara tu baada ya uzinduzi wa uwanja wa ndani wa michezo.
  Rais Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na hoihoi wakati alipowasili kwenye Chuo cha Michezo Malya kilichoko wilayani Kwimba tarehe 9.9.2013. 
  Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kituo cha polisi cha wilaya ya Kwimba mjini Ngudu tarehe 9.9.2013.


  0 0


   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo akitoa hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi baada ya ufungua rasmi Kikao cha siku mbili cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Elisante Ole Gabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Bw. Suleiman Ling’ande akitoa maneno machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ole Sante Grabriel katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.

   Mshauri Mwelekezi Bw. Ernest Omalla (aliyesimama) akitoa maelezo machache kabla kumkaribisha Mshauri Mwelekezi mwenzie Bw. Martin Cuff (kushoto) kwa ajili ya kutoa somo kwa washiriki katika ukumbi wa TCRA leo jijini Dar es Salaam.

   Mshauri Mwelekezi Bw. Ernest Omalla akitoa somo fupi juu ya Kikao cha siku mbili cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu uliofunguliwa jana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi Joyce Fissoo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Grabriel katika ukumbi wa TCRA  jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo (kulia) akimsomea maelezo muhimu Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia) mara baada ya kukamilisha kutoa hotuba fupi ya mgeni rasmi ambaye alimwakilisha. 

   Baadhi ya Washiriki waliohudhuria uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Filamu wakifuatilia somo toka kwa wadau mbalimbali wa TAFF pamoja na Washauri Waelekezi wakati wa uzinduzi Kikao cha siku mbiloi cha Wadau wa Filamu kuhusu Mjadala wa Sera ya Filamu kilichofanyika jana katika ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO. 


  0 0

  Shamo Towers & Shopping Centre sasa unaweza kupata  huduma mbalimbali  Kama;

  - huduma  za ki Benki
  - Huduma za afya na pharmacy  Aga Khan Medical centre.
  - Boutique ya kisasa 
  - Baby shop & Gift Shops
  - Electronics shop
  - Coffee Shop & fast food restaurant.
  - stationaries Shop.
  - Furniture centre.
  - village Supermarket, Voda Shop & Bureau de change. Kufunguliwa karibuni.

  Mbezi towers ipo Mbezi Beach, karibu na tangi bovu. 

  DUKA LA GALINA - FUN ZONE GIFT SHOP

  COFFEE SHOP- BOOGIE WOOGIE 

  DUKA LA KIAFRICA -WAQWETU.

  0 0


  Kamishna wa Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa akizihesabu kete 43 za dawa za kulevya aina ya Heroin jana, zilizokamatwa katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, juzi usiku ambapo zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Japan. Picha na Michael Jamson 

  • Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
  Dar es Salaam. Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.

  Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo. Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.

  Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni). Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.

  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
  Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu. Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
  Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.

  “Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.

  “Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda. “Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.

  “Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.” Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi.

  “Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.

  Shelukindo alisema wachezaji hao wapo mahabusu kwenye Kituo cha Polisi cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (Federal Police Crime Investigation) na hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa wamevaa. Watanzania wengine kuachiwa leo

  Shelukindo alisema kuna Watanzania wanne wanaotazamiwa kuachia leo baada ya kumaliza vifungo vyao baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya. “Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya nyuma wao walikuwa wamemeza wakapasuliwa dawa zikatolewa na baadhi yao walifariki. Hata hivyo, wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka minne wanaweza kurudishwa Tanzania,” alisema Shelukindo.SOURCE BOFYA HAPA.

  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Mgogoro wa ardhi katika tarafa za loliondo na sala zilizopo wilayani
  ngongoro  umeendelea kuchukuwa sura mpya kutokana na serekali
  kusimamia hoja zake za kutaka kuwaondoa  wafugaji kutoka katika maeneo
  ya vijiji vyao.

  Pia Mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu
  na haki za ardhi wamelalamikia kitendo cha serekali kusitisha mpango
  ulinzishwa hivi karibuni wa kupima vijiji vya loliliondo na sale
  ambavyo vimekuwa vimekuwa vikikabiliwa na mgogoro wa ardhi kwa zaidi
  ya miaka 20 .

  Mkakati huo ambao unatajwa kuwa ulianza mwaka 2009  baada ya serekali
  kufanya operesheni ya kuwaondoa wafugaji hao kwa nguvu kutokana na
  sababu  mbalimbali zilizodaiwa ikiwemo ya uharibufu wa mazingira
  ,ongezeko la watu hususa ni kutoka katika nchi jirani ya kenya
  ,kulinda vyanzo vya maji pamoja na ikolojia ya hifadhi ya serengeti.

  Aidha mashirika ya kiraia yanayojihusisha na utetezi wa haki za
  binadamu na haki za aridhi walibanisha kuwa sababu hizi zote sio za
  kweli na kwamba zilikuwa ni hila za kutaka kuwanyang'anya wananchi
  ardhi yao ya asili na katika hayo serekali katika kuhalalisha  mpango
  wa kuwapokonya wananchi wa loliondo ardhi yao walitengeneza mpango  wa
  matumizi bora ya ardhi mwaka 2010 mpango ambao ulikataliwa na wananchi
  kutokana na kuto shirikishwa.

  Akiongea na waandishi wa habari  mkurugenzi wa Lashehabingo Charles
  Ndangoya  alisea kuwa tatizo hili limekuwa la muda mrefu sasa na
  katika mwaka wa 2012 serekali iliitisha vyeti vya baadhi ya vijiji vya
  loliondo vilivyokuwa vimepimwa kwa madai kuwa vilikuwa na migogoro na
  vijiji jirani jambo ambalo sio la kweli  huku akibinisha kuwa vijiji
  vilivyotajwa kuwa vinamgogoro ambavyo ni ololosokwan na engaresero
  vilikataa kurejesha vyeti vyao kutokana na sababu iliotolewa kuwa
  hawaoni ukweli wa serekali wenye msingi.

  Aliongeza kuwa aikuishia hapo mwaka 2013 serekali ilitaka tena
  kuwapokonya wananchi hao eneo hilo la wafugaji wa loliondo kw amanufaa
  ya mwekezaji wa kampuni ya uwindaji ya OBC jaribio ambalo wananchi
  waliweza kulizuia kwa kutumia nguvu zao wenyewe na wakidai kuwa
  ugawaji huo ungeweza kuleta mathara makubwa sana kwa jamii na vizazi
  vijavyo ambapo walilazimika kwenda hadi kwa  waziri mkuu kupeleka
  malalamiko yao  ambapo waziri alitoa agizo kwa mkuu wa mkoa kuangalia
  namna ya kutatua tatizo hilo ambapo ndipo serekali ilituma tume ya
  watu nane kwa ajili ya upimaji ramani  wa vijiji vyote   vya wilaya ya
  loliondo ambavyo havijawai kupimwa  ambapo pamoja zoezi hilo lilikuwa
  zuri lakini bado walikuwa wanawasisi wasi na pale lilipoanza
  kutekelezwa wananchi hao walifurahi wakijua mgogoro wa mda mrefu
  umeisha.

  Naye mkurugenzi mungine ambaye ametoka katika mashirika hayo  ya
  utetezi wa haki za binadamu  Ambaye ametoka shirika la pingos Forum
  Emanuel Siringe yeye alidai kuwa wananchi walifurahia sana swali
  wakijua kuwa kile walichokuwa wanatafuta kwa muda mrefu kimepata
  umbuzi lakini matumaini hayo yameanza kwisha na kwa sasa hawajui hatma
  ya maisha yao kutkana na kile kilichodaiwa mpango wa serekali juu ya
  aridhi yao kwani mpango huo ulisitishwa ghafla kwa amri ya waziri wa
  ardhi na maendeleo ya makazi bila kueleza sababu ya msingi za
  kusitishwa mpango huo wa upimaji.

  Aidha alisema kuwa wananchi wamefanya kila juhudi katika kutafuta
  ardhi yao na wametumia vyombo mbalimbali kupatza sauti zao ili
  serekali isikie lakini haijachukua hatua yeyote na watu zaidi ya
  milioni 1.7 wamesini  kampeni ilioendeshwa na shirika la kimataifa la
  Acaaz kupinga hatua ya rais kikwete kuwaondoa wafugaji wa kimasa
  kutoka katika ardhi yao ya asili  lakini hawajafanikiwa.

  Naye mkurugenzi wa shirika la Ngonet Samwel Nangiria aliomba serekali
  kuandaa mpango shirikishi wa kupima vijiji vyote vya loliondo na sale
  kama ilivyokusudiwa kufanya hapo awali na kufanya mpango wa matumizi
  bora ya ardhi ambayo wananchi ndio wanaamini kuwa ndiyo suluhisho la
  mgogoro  huu uliodumu kwa uda mrefu,huku akiitaka serekali kuanglia
  maslahi ya wananchi zaidi kuliko ya wawekezaji ili kuepuka migogoro
  isiyo kuwa  na msingi wowote .

  "napenda pia kuitaka serekali iache  kabisa mpango wake wa kutenga
  eneo la kilometa za mraba 1500 kwa maslahi binafsi ya mwekezaji kwani
  eneo hilo ni muhimu kwa maisha ya wafugaji wanaoishi loliondo kwa
  kizazi cha sasa na kijacho  na pia izingatie sana sheria za ardhi za
  vijiji katika kushughulikia mgogoro wa loliondo badala ya kuzingatia
  sheria za mazingira na wanaya pori pekee"Alisema Nangiria

older | 1 | .... | 156 | 157 | (Page 158) | 159 | 160 | .... | 1903 | newer