Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KUFANIKISHA MBIO ZA "MBEYA TULIA MARATHON 2018"

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo, Mbio hizo Zimeshirikisha wanariadha mbalimbali wakiwemo wakenya na watanzania pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa mkoa wa Mbeya , kumekuwepo na washiriki wa mbio mbalimbali zikiwemo za Kilomita 41, kilomita 21, Kilomita 5, Kilomita 2, Mita 100, Mita 400 na Mita 800.

Dk. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge amewashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamewezesha kufanyika kwa mbio hizo kwa mafanikio makubwa mbali ya changamoto ndogondogo ambazo zitaendelea kuboreshwa katika maandalizi ya mbio zingine zitakazofanyika mwakani jijini Mbeya.
SE4
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akihojiwa na Mtangazaji wa Kituo Cha Luninga cha Clouds TV Hassan Ngoma kuhusu mafanikio ya mbio hizo za Mbeya Tulia Marathon 2018.
SE5
Mmoja wa wananchi waliohudhuria ili kushuhudia mbio hizo akisoma kipeperushi cha Bahati nasibu ya Mzuka huku akifurahia jambo katika kipeperushi hicho.
1
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akianzisha Mbio za mita 100 katika mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizowahusisha viongozi wa serikali , Wabunge na Madiwani kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo,
2
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku pamoja na baadhi ya wabunge wakishiriki mbio za mita 100 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 jijini Mbeya.
3
Watoto wakishiriki mbio za mita 1500.
4
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio hayo.
5
Washiriki wa mbio za Baiskeli Kilomita 150 wakiingia uwanja wa Sokoine mara baada ya kumaliza mbio hizo.
7
Wananchi wakifuatilia matukio.
SE1
Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi wa Tatu Mzuka na maofisa wa Tatu Mzuka Kulia ni Barbara Hassan Matangazaji wa Clouds Radio na Mwanamuziki wa Bongo Fleva Fid Q.
8
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akicheza Muziki wa Kwaito pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wa Serikali.
9
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akikabidhi king'amuzi na Dishi kwa washindi mbio za Kilomita 21. wanawake.
12
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akizungumza kwenye uwanja wa Sokoine mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.
13
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akifurahia jambo wakati Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza kwenye uwanja wa Sokoine mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.
14
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akisikiliza wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania RT Mh. Anthony Mtaka akizungumza .
15
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala akielezea jambo wakati alipokuwa akisifu umakini wa Naibu Spika Tulia Akson na kazi kubwa anayoifanya kusaidia jamii kupitia mfuko wa Dk. Tulia Trust.
16
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala na Naibu Spika Dk.Tulia Akson wakipiga picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilomita 21.
17
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande akiwavisha medali washindi wa mbio za kilomita 41.
18
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania Bw. Maharage Chande na Naibu Spika Dk. Tulia Akson pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala wakipiga picha ya pamoja na washindi mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
19
Baadhi ya washindi wa mbio hizo wakipiga picha huku wakiwa wameshika zawadi zao za ving'amuzi.

WAINGEREZA WAVUTIWA KUWEKEZA SELOUS, DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUWEKWA MAKUBALIANO YA AWALI (MOU)

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (hayuko pichani) kushirikiana na wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuandaa mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwenye Pori la Akiba Selous, ofisini kwake Jijini Dodoma juzi. Wawekezaji hao pichani ni Eva Sanchez na Nicholas Negre.

Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
..............................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza uandaliwe mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Mkataba huo wa makubaliano utahusisha wawekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na  utakapokamilika utasainiwa na pande zote mbili.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwake na wawekezaji hao, Eva Sanchez na Nicholas Negre.

Akiwasilisha maombi hayo, Sanchez amesema mradi huo utakuwa wa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ambao ndio wasimamizi wakuu wa Pori la Akiba Selous utakapoanzishwa mradi huo. 

Amesema pamoja na mambo mengine mradi huo wa utalii wa picha pia utasaidia kupiga vita ujangili na kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka pori hilo.

Dk. Kigwangalla amewataka wawekezaji hao kuwasilisha andiko la mradi huo, kufanya utafiti wa kina na tathmini ya athari za kimazingira zitakazoweza kujitokeza kutokana na uanzishwaji wa mradi huo.

Amesema kwa sasa Serikali inafanya marekebisho ya Sheria mbalimbali zitakazoiwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kutekelezaji majukumu yake ipasavyo ikiwemo uwekezaji wa aina hiyo kwenye sekta ya Utalii wa Picha na Uwindaji wa Kitalii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara amesema mamlaka hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji hao ili kutimiza azma ya Serikali ya kushirikisha wadau, watu binafsi na wawekezaji katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Pori la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na muwekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza, Eva Sanchez ofisini kwake Jijini Dodoma juzi alipowasilisha ombi lake la kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (kulia) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji huo.
 Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi (aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji huo.
 Waziri Kigwangalla akisisitiza jambo katika kikao hicho.
 Waziri Kigwangalla akitoa maelekezo katika kikao hicho.
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na muwekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza, Eva Sanchez ofisini kwake Jijini Dodoma juzi baada ya kupokea ombi lake la kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla,  Wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous Eva Sanchez na Nicholas Negre, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (kushoto) na Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi (kulia).

TTCL YAENDELEA KUTOA LINE BURE MTWARA

$
0
0

JOSEPH MPANGALA , MTWARA

Kampuni ya Mtandao wa sim TTCL Cooperation Imeendelea Kutoa na Kusajili line za sim Bure ili kuwawezesha wateja wake wapya kuweza kuwasilina kwa bei nafuu pamoja na kujiunga na vifurushi vya Internet.

Akiongea katika Kiwanja Cha mashujaa kilichopo mkoa wa mtwara katika Promosheni ya NYAKA NDINGA inayoendeshwa na kituo cha Radio cha EFM/TVE Meneja wa Mkoa Mhandisi Rumishael f. Temba anasema TTCL imeanzisha Bando kwa ajili ya internet ambayo wateja wengi wamekuwa wakiyapenda na Kuyatumia kwa wingi.

“Katika Upande wa mabando kwa TTCL ambayo wateja wake wanayapenda zaidi ni Boom Pack kwa ajili ya wanachuo,Serereka Bando la Kijanja ambalo kila mwananchii anaweza kulipata kwa bei nafuu pamoja na bando la Toboa”

Aidha TTCL imetambulisha Huduma ya T-pesa kwa mtandao ambapo unaweza kutumia kulipia Huduma ya LUKU bila ya kuwa na gharama za ziada.
 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akiongea na Wananchii kuhusina na Huduma Zinazotolewa na kampuni Hiyo wananchii waliokuja katika Promosheni ya Nyaka Ndinga Inayoendesha na EFM na TVE.
 Baadhi ya wateja wakiwa wamezunguka Banda la TTCL kwa ajili ya kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo.
 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akitoa zawadi kwa Washiriki Kumi watakaokwenda Dar es Salaam kwa ajili ya shindano kubwa la promosheni ya Nyaka Ndinga.

Je, ni salama kusafiri kwa ndege kipindi cha mvua?

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, usafiri wa ndege ndio njia salama zaidi ya usafiri kuliko zote duniani ukilinganisha na nyinginezo kama vile gari, reli, pikipiki na maji. Tafiti zimezingatia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya abiria vinavyosababishwa na njia ya usafiri husika.

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (IATA) lilitoa ripoti yake ya tathmini ya mwaka 2017. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa sekta ya usafiri wa anga imeboresha masuala ya usalama kwa asilimia 54 ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita. Kiwango cha ajali kwa mwaka 2016 kilikuwa ni 1.61 kwa safari milioni moja za ndege, ukilinganisha na kiwango cha 3.53 karibuni muongo mmoja uliopita, yaani mwaka 2007, na kupungua kwa zaidi ya asilimia 10 mwaka 2015. Mwaka 2016, abiria zaidi ya bilioni 3.7 walisafiri salama kwenye safari za kibiashara zaidi ya milioni 40.1.

Pamoja na takwimu hizo bado kwa baadhi ya abiria inakuwa ni changamoto kuutumia usafiri huo hususani kwenye kipindi cha mvua kubwa kama tunavyoshuhudia sasa katika maeneo mengi nchini Tanzania. Jumia Travel imekukusanyia mambo yafuatayo ya kufahamu na kufuata ili kukutoa hofu pindi utakapoamua kusafiri kwa ndege.

MAMBO UNAYOTAKIWA KUYAFAHAMU

Ni salama kusafiri kipindi mvua inanyesha. Kwa sababu umekutana na changamoto mbalimbali ukiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege haimaanishi hali itakuwa hivyo hivyo angani. Mashirika mbalimbali ya ndege duniani huendesha shughuli zao kipindi cha mvua. Huwa kunakuwa na sheria na taratibu zinazofuatwa ipasavyo kufanya hivyo, waongoza ndege hawawezi kuruhusu ndege kuondoka endapo hali ya hewa ni mbaya. Hivyo basi ondoa shaka kwamba ukiona ndege inapaa uwanjani, ujue safari yako ipo salama.

Tegemea mitikisiko ya kiasi. Kama ilivyo njia ya barabara au bahari kuna wakati unakutana na miinuko na kona za hapa na pale au mawimbi, vivyo hivyo na angani pia. Kusafiri kipindi cha mvua kubwa au upepo mkali kunaendana na mitikisiko kiasi ya ndege angani. Fahamu kuwa hali hiyo ni ya kawaida. Mitikisiko hiyo haimaanishi kwamba itaharibu chombo cha usafiri au kuhatarisha usalama wa abiria wake.

Radi haiwezi kudondosha ndege. Wataalamu wanabaisha kuwa ni hali ya kawaida ndege kukutana na radi mara kadhaa kwenye safari zake ndani ya mwaka. Na hata kama ikitokea, haimaanishi kwamba itaunguza ndege au abiria wake. Ndege nyingi zimeundwa kukabiliana na hali hiyo kwa kutumia vifaa maalum kwa teknolojia ya hali ya juu. Rubani anaweza kuamua kutua ndege kwa tahadhari zaidi.

Ndege zimeundwa kukabiliana na changamoto tofauti. Hali mbaya ya hewa haiwezi kuharibu ndege. Kila kifaa kwenye ndege kimeundwa madhubuti kukabiliana ipasavyo na changamoto za angani. Mabawa yake yameundwa kukabiliana na hali ngumu kama ilivyo sehemu ya kukaa abiria. Tofauti na unavyofikiri, ndege inaweza kubadilika na kukabiliana na hali tofauti hususani linapokuja suala la usalama wa abiria wake.

Marubani na wahudumu wamefundishwa kukabiliana na misukosuko ya angani. Si jambo la kushangaza kwa abiria waoga kusafiri angani kustaajabu ni kwa namna gani marubani na wahudumu wa ndege wanakuwa kwenye hali gani kipindi cha msukosuko angani. Wao pia kama binadamu wanakuwa na hofu hiyo. Lakini cha muhimu kufahamu ni kwamba watu hao ni wabobezi na wamefundwa ipasavyo kuhakikisha unasafiri na kufika salama.  

MAMBO UNAYOTAKIWA KUYAFUATA

Kama hauiamini hali ya hewa, ziamini takwimu. Ni hali ya kawaida kuwa na wasiwasi kusafiri kipindi ambacho hali ya hewa ni hatarishi. Inashauriwa kama hauiamini hali ya hewa basi amini takwimu zilizofanyika kabla. Takwimu na tafiti kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kuaminika duniani zimeonyesha kuwa usafiri wa anga ndio njia salama zaidi ya usafiri kuliko zote. Ni mara chache kusikia ndege imeanguka ukilinganisha na ajali za gari au pikipiki.   

Epuka tafiti nyingi kupita kiasi. Kuna msemo maarufu wa Kiswahili unaosema kwamba, ‘ukimchunguza s
ana bata hautomla.’ Uoga wa kusafiri angani unaweza kukupeleka kufanya tafiti kutosha. Ili kujua usalama wake, tahadhari za kuchukua na pengine namna ya kujiokoa. Kumbuka kwamba wewe sio mtaalamu kwenye sekta hiyo, iamini timu nzima ya marubani na wahudumu wake katika kukusafirisha salama. Chumba na chombo wanachokitumia marubani na timu yao kwenye ndege ndicho kinachopokea taarifa halisi juu ya hali iliyopo mbele yao na namna bora ya kuendesha chombo walichopewa dhamana.  

Watazame wahudumu wa ndege. Kama ni mara ya kwanza na una hofu kubwa pindi ndege itakapopaa na kuwa angani, unashauriwa kuwatazama wahudumu wa ndege namna wanavyofanya shughuli zao bila ya wasiwasi wowote. Kwa kufanya hivyo kutakupunguzia na kukuondelea wasiwasi kama abiria ukiwa kwenye ndege.

Tii maagizo. Hiki ni kipengele muhimu cha kuzingatia. Kwa kiasi kikubwa hofu na ghasia ndizo husababisha majeraha ndani ya ndege. Na mara nyingi huwa ni abiria au watumishi wengine ndani ya ndege ambao hawakufunga mikanda yao. Unaweza kuona ni sahihi kupuuza ishara za kukutaka kufunga mkanda ndani ya ndege kwa kuwa mambo ni shwari. Zingatia kuwa hizo ishara zimewekwa kwa makusudi maalum. Hakikisha kuwa unafuata maagizo na miongozo yote kutoka kwa wahudumu wa ndege hususani mafundisho ya alama za usalama yanayotolewa ndani ya ndege.

Usafiri wa ndege nchini Tanzania unakua kwa kasi na kuwa kiungo muhimu katika nyanja tofauti hususani za kiuchumi kama vile ajira, biashara na utalii. Ni rahisi kusafiri kupitia Jumia Travel ambapo imekukushanyia huduma za mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi sehemu moja mtandaoni.

Wabunge wa Afrika Mashariki watembelea Balozi Chikawe - Tokyo

$
0
0
 Wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chapter ya Tanzania wamezuru Ubalozi wa Tanzania Tokyo.  Wako ziara ya wiki moja nchini Japan. Pichani kushoto ni Ndugu Charles Mchome ambaye ni Mtanzania anayeishi Japan na ni Mdau wa globu ya Jamii.
Pichani kushoto ni Dkt Abdullah Hasnuu Makame,Balozi Mathias Chikawe,Mheshimiwa Josephine Lemoyan pamoja na Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa wakiwa katika picha ya pamoja.

WADAU WA HABARI DODOMA WAPEWA SOMO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Habel Chidawali akifungua Mkutano wa wadau wa habari mkoani Dodoma.
Wajumbe wa mkutano
 Mwanahabari Mkongwe Edna Ndejembi akizungumza katika mkutano wa wadau mkoani Dodoma.
 Mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC) Daniel Msangya akichangia katika mkutano wa wadau wa habari wa mkoa huo.
 Mwanahabari Idd Maalim akichangia kwenye mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
.....................................................
WADAU wa habari mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutumia wanahabari katika kuchochea mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye ngazi zote za utawala ili kuhabarisha umma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoa wa Dodoma ambao ulilenga kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusino baina yao na wanahabari na upatikanaji habari zinahusu maendeleo ya mkoa huo.
Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) ambao hufanyika kila mwaka.
Akichangia majadiliano kwenye mkutano huo, Masasi alisema tasnia ya habari ni muhimu kwa ustawi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na kuwahakikishia wanahabari kuwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa sasa zina mipango na shughuli nyingi za maendeleo hivyo zinahitaji wanahabari kufikisha taarif
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Habel Chidawali akifungua Mkutano wa wadau wa habari mkoani Dodoma.
Wajumbe wa mkutano
Mwanahabari Mkongwe Edna Ndejembi akizungumza katika mkutano wa wadau mkoani Dodoma.
Mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC) Daniel Msangya akichangia katika mkutano wa wadau wa habari wa mkoa huo.
Mwanahabari Idd Maalim akichangia kwenye mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Dodoma.


WADAU wa habari mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutumia wanahabari katika kuchochea mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye ngazi zote za utawala ili kuhabarisha umma.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoa wa Dodoma ambao ulilenga kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusino baina yao na wanahabari na upatikanaji habari zinahusu maendeleo ya mkoa huo.

Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) ambao hufanyika kila mwaka.Akichangia majadiliano kwenye mkutano huo, Masasi alisema tasnia ya habari ni muhimu kwa ustawi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na kuwahakikishia wanahabari kuwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa sasa zina mipango na shughuli nyingi za maendeleo hivyo zinahitaji wanahabari kufikisha taarifa hizo kwa wananchi.

Aidha aliwaomba wanahabari kuwasiliana na mamlaka za serikali hasa pale wanapopata taarifa za tatizo lolote ili kujua juhudi za serikali za kupambana nalo.Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC), Habel Chidawali aliwataka waandishi kuondokana na uandishi wa mazoea ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha aliwaomba wadau katika mkoa wa Dodoma kuvitumia vyombo vya habari katika kutangaza fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuwa vina uwezo wa kufikia kundi kubwa la wananchi.Naye, Mwandishi mkongwe nchini, Edna Ndejembi alisema kuwa ili Mkoa wa Dodoma uweze kufikia maendeleo yake hauna budi kuvitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo utatoa fursa kubwa kwa wadau kujitokeza na kuwekeza mkoani hapa.

Alisema mkoa wa Dodoma una fursa nyingi kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo cha zabibu ambazo zinahitaji kutangazwa ili kupata wawekezaji na kuwezesha mji huo kukua hasa ikizingatiwa tayari umepewa hadhi ya kuwa Jiji.Pamoja na hayo, Mlezi wa CPC Daniel msangya alisisitiza waandishi kujiendeleza kielimu na kujisoma vitabu na sheria mbalimbali ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
a hizo kwa wananchi.
Aidha aliwaomba wanahabari kuwasiliana na mamlaka za serikali hasa pale wanapopata taarifa za tatizo lolote ili kujua juhudi za serikali za kupambana nalo.
Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC), Habel Chidawali aliwataka waandishi kuondokana na uandishi wa mazoea ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Aidha aliwaomba wadau katika mkoa wa Dodoma kuvitumia vyombo vya habari katika kutangaza fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuwa vina uwezo wa kufikia kundi kubwa la wananchi.

Naye, Mwandishi mkongwe nchini, Edna Ndejembi alisema kuwa ili Mkoa wa Dodoma uweze kufikia maendeleo yake hauna budi kuvitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo utatoa fursa kubwa kwa wadau kujitokeza na kuwekeza mkoani hapa.
Alisema mkoa wa Dodoma una fursa nyingi kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo cha zabibu ambazo zinahitaji kutangazwa ili kupata wawekezaji na kuwezesha mji huo kukua hasa ikizingatiwa tayari umepewa hadhi ya kuwa Jiji.
Pamoja na hayo, Mlezi wa CPC Daniel msangya alisisitiza waandishi kujiendeleza kielimu na kujisoma vitabu na sheria mbalimbali ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Kamati za mashindano Handeni Kwetu Cup zaaswa kutimiza wajibu wao

$
0
0
VIONGOZI wa mpira wa miguu katika kata mbalimbali wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao wa kuratibu na kuyasimamia mashindano ya Ligi ya Handeni Kwetu Cup kwenye Kata zao ili mashindano hayo yawe na tija na kupatikana washindi kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Ushauri huo umetolewa na muasisi wa mashindano hayo, Kambi Mbwana, alipokuwa akizungumza na gazeti hili wilayani hapa, akisema kuwa kuna baadhi ya Kata zimekuwa zikisua sua kutokana na viongozi waliochaguliwa kutojua umuhimu wa uwajibikaji na kutimiza wajibu kwa maslahi mapana ya mpira wa miguu kwa kupitia mashindano hayo yanayodhaminiwa na bahati nasibu ya Biko 'ijue nguvu ya buku' na Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF).

Akizungumzia suala hilo, Mbwana alisema kabla ya kuanza mashindano hayo, Chama cha Mpira wa miguu wilayani Handeni mkoani Tanga (HDFA), kilichagua viongozi wake kila kata ili pamoja na kuyaratibu mashindano ya Handeni Kwetu kwenye Kata zao kwa ajili ya kutafuta washindi wawili wa kwenda ngazi ya tarafa, pia viongozi hao wangekuwa na majukumu ya kusimamia na kuendeza mpira kwenye kata zao, viongozi ambao upatikanaji wao ulilazimika kutumika kwa gharama ya muda na fedha.

"Kila mdau wa michezo anapaswa kujua kwenye kata yake kuna viongozi wa mpira waliochaguliwa ili kusimamia ligi hii, hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao ili mashindano yetu yaende vizuri kwa ajili ya kutoka kwenye kata na kuingia kwenye tarafa na baadae ngazi ya wilaya kama matarajio yetu.

" Kumekuwa na ucheleweshaji mkubwa kwa mashindano yetu kwa baadhi ya kata zetu jambo linaloweza kuathiri mfumo mzima wa ligi yetu tuliyoamua kuanzisha kwa minajiri ya kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika wilaya ya Handeni, hivyo nawaomba sana viongozi hawa watimize wajibu wao,"Alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, baadhi ya kata ambazo zimechelewa kuanza mashindano hayo ni pamoja na Segera, Sindeni, Kwachaga, Kwamsisi, Kiva, Kwaluguru, Kitumbi, Komkonga na Kwedizinga, wakati kata nyingine zilizosalia zikiwemo za Halmashauri ya Handeni mjini zenyewe zikiwa zinaelekea mwishoni, wakati zipo zile zilizomaliza kupata washindi wa kuelekea kwenye ngazi ya tarafa itakayoanza baada ya kumalizika katika hatua ya kata.

Mashindano ya Handeni Kwetu Cup yalizinduliwa mwezi Machi mwaka huu katika uwanja wa Mabatini, Mkata na kuhudhuliwa na watu mbalimbali kwa hisani ya Biko na NSSF huku waratibu wa mashindano hayo yatakayomalizika mwezi Novemba mwaka huu wakifungua milango kwa wadhamini wengine ili kuwezesha ligi hiyo ya aina yake ifanyike kwa mafanikio makubwa.

MKURUGENZI MTENDAJI TIC:UKUAJI WA KASI WA UCHUMI WA TANZANIA KIVUTIO KWA WAWEKEZAJI

$
0
0
*Azungumzia miradi mipya 109 waliyoisajili kwa kipindi cha miezi minne,fursa za ajira

Na Said Mwishehe,Globu

MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe ametoa hakikisho kwa wawekezaji na Watanzania kwa ujumla kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa na kwa sasa nchi yetu inashika nafasi ya tano kati ya mataifa 10 duniani ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Amesema kuimarika kwa uchumi huo wa Tanzania na kukuwa kwa kasi, maana yake inatoa usalama kwa anayetaka kuwekeza nchini kuwa na uhakika wa mtaji wake huku akielezea mafanikio ya TIC katika kuhamasisha uwekezaji nchini ambapo kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu wamefanikisha kuandikisha miradi mipya 109 inayotarajia kutoa fursa ya ajira 18,172.

Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anatoa mafanikio ya TIC kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu ambapo amefafanua kutokana na matokeo hayo ya haraka ya ukuaji wa uchumi yametokana na jitihada za Serikali  chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kupambana na rushwa , kuondoa urasimu kwa kutengeneza mazingira wezeshi ya usajili wa biashara na leseni kwa wawekezaji wa nfani na nje.

Akifafanua zaidi mambo mengine ambayo yamefanyika katika kuwahudumia wawekezaji kwa haraka ni pamoja na kuboresha mfumo wa huduma mahala pamoja ndani ya TIC ambapo kwa sasa kuna maofisa zaidi  10 wanaotoka kwenye wizara,idara na taasisi za Serikali kwa ajili ya kutoa huduma za kusajili kampuni.

Pia usaidizi wa kupata ardhi ya uwekezaji ,leseni mbalimbali ,kusajili VAT ,TIN na ushauri wa kitaalam kuhusu kodi,vivutio vya uwekezaji , vibali vya kazi na kutathimini masuala ya mazingira.Mwambe amesema kituo kimefanikisha uanzishaji wa kamati ya Taifa ya huduma kwa wawekezaji  ili kujadili mikakati ya kutatua changamoto za uwekezaji kabla na baada ya uwekezaji.

Kuhusu maeneo ambayo uwekezaji unafanyika zaidi ni sekta ya ujenzi, uzalishaji viwandani , usafirishaji wa mizigo, kilimo na miundombinu na kati ya miradi  mipya 109 , miradi 28 ambayo sawa na asilimia 34.86 inamilikiwa na wageni , miradi mitatu  ni ya ubia na miradi 68 inamilikiwa na Watanzania.

Akizungumzia uchumi wa Tanzania , Mwambe amesema  kituo kinawajibika kuishauri Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ambapo kulingana na na takwimu za Benki ya Rand Merchant (RMB) zilizotolewa  mwaka 2015 ,Tanzania inashika nafasi ya 9 kati ya nchi 10 za  Afrika zenye ushawishi wa kumvutia mwekezaji .

Pia amesema kwa ujumla uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa ambapo kwa sasa nchi inashika nafasi hiyo ya tano  na kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti ya the Centre for International Development (CID) ya Chuo Kikuu cha Havard ni kwamba Tanzania inatarajia kuwa nchi ya nne duniani na ya tatu kwa Afrika katika ukuaji wa uchumi wake.Mwambe amesema katika kipindi cha mwaka 2016 Tanzania iliendelea kubaki nafasi ya 9 kabla ya kupanda hasi nafasi ya saba mwaka 2017 kati ya nchi 10 za Afrika zenye ushawishi wa kumvutia mwekezaji  kuwekeza.

"Kwa kiasi kikubwa matokeo ya ukuaji wa kasi ya uchumi imekuwa sababu kubwa ya kuvutia wawekezaji kuwekeza.Amani na utulivu wa nchi yetu nayo imekuwa chachu ya nchi yetu kuwa kimbilio la uwekezaji na jukumu letu TIC ni kuhamasisha uwekezaji, hivyo tutaendelea kuifanya kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake,"amefafanua Mwambe.

Pia amesema katika kufanikisha mambo yake TIC imetumia njia mbalimbali kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi kama sehemu bora ya kuwekeza.Ametaja njia hizo ni pamoja na kushiriki makongamano ya biashara nje na kupokea ujumbe wa wafanyabishara na wawakilishi wa Serikali kutoka nje.

Mwambe ametoa shukrani kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za wilaya mpaka Taifa kwa juhudi zinazofanyika katika kufanikisha uwekezaji nchini huku akitoa mwito kwa wakuu wa mikoa ,wilaya na watendaji wa taasisi  zote za Serikali  kuongeza kasi za uboreshaji  wa huduma zao kwa wawekezaji.

"Juhudi hizi  zikifanyika kwa nguvu na kasi kubwa kwa pamoja basi Tazania chini ya Rais Magufuli  itaendelea kupaa, kuvutia uwekezaji , kuibua fursa za ajira kwa vijana, kupanua wigo wa walipa kodi na hatimaye kuongeza uzalishaji  na kufikia uchumi wa kati,"amesema Mwambe.

MWALIMU WA SEKONDARI ALIYEMPA MIMBA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ACHUKULIWE HATUA-RC MNDEME

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameagiza mwalimu wa sekondari aliyempa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.

Bei mpya za mafuta yatangazwa zanzibar

$
0
0
Na Mwashungi Tahir Maelezo 7-5-2018.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma, Nishati na Maji Zanzibar ZURA imetoa taarifa juu ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia kesho siku ya Jumanne ya tarehe 8-5-2018.

Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara Kaimu Mkuu kitengo cha uhusiano Khuzaimat Bakar Kheir alisema ZURA ina kawaida ya kupanga bei kwa kuzingatia mambo yafuatayo.Alisema wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ) katika mwezi wa Machi , 2018 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Mei ,2018.

Pia alisema gharama za uingizaji na uhifadhi wa Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar .Vile vile gharama za Usafiri , Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar .Thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola , kodi ya Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejereja.Kaimu huyo alisema Bei za mafuta kwa mwezi Mei 2018 zimeshuka ikilinganishwa na bei za Mwezi wa April 2018 , sababu za kushuka kwa bei ni .

Kushuka wastani wa mwendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ).Kushuka kwa Gharama za uingizaji na uhifadhi katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za kuyasafirisha tena hadi Zanzibar , hasa “Demurrage charges ambapo mafuta ya Petrol yameshuka kwa Tsh . 5 kwa lita kutoka Tsh. 18.96 hadi Tsh 13.98,mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh. 6 kutoka Tsh 21.08 kwa lita hadi Tsh. 15.53 na mafuta ta Taa haijabadilika kwa mwezi wa Mei, 2018.

Kushuka kwa gharama za usafirishaji , Bima na faida ya muagizaji (Premium) ambapo mafuta ya Petrol yameshuka kwa Tsh . 49 sawa Asilimia 60% , mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh 8 sawa na Asilimia 20% na Jet A-1(mafuta ya taa) haijabadilika.

Khuzaimat aliendelea kusema Bei ya reja reja ya mafuta ya petrol kwa mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh 89 kwa lita kutoka Tsh 2, 344 ya Mwezi wa April ,2018 hadi Tsh hadi Tsh 2, 255 kwa lita katika mwezi wa Mei , 2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.

Bei ya reja reja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh. 64 kwa lita kutoka Tsh 2, 314 ya Mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 2, 250 sawa na Asilimia 2%.Pia alisema bei ya reja reja mafuta ya taa kwa Mwezi wa Mei. 2018 haijabadilika ni Tsh 1.740 kwa lita.

Bei ya reja reja ya Mafuta ya Banka kwa Mwezi wa Mei , 2018 imeshuka kwa Tsh 78 kwa lita kutoka Tsh . 2,156 kwa lita katika Mwezi wa April, 2018 hadi Tsh, 2,078 katika mwezi wa Mei, 2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.

Na bei ya reja reja ya mafuta ya Ndege kwa Mwezi wa Mei imeshuka kwa Tsh 2.5 kwa lita kutoka Tsh. 1,812.63 kwa lita katika mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 1,810.21 katika Mwezi wa Mei, 2018 sawa na asilimia 0.13%.
Kaimu Mkuu kitengo cha uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti waHuduma, Nishati na Maji Zanzibar( ZURA) Khuzaimat Bakar Kheir akizubgumza na waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya bei za mafuta Zanzibar (Picha na Kijakazi Abdalla -Maelezo Zanzibar.).

AWESO CUP 2018 YAZINDULIWA KWA KISHINDO, SIMBA WAILIZA YANGA PANGANI

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizindua mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga. Pembeni ni Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja (mwenye traki suti bluu), Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza na msemaji wa Simba, Haji Manara na Jerry Muro.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza na Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja mara baada ya kumaliza kuzindua mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga.
Picha ya pamoja.
Wachezaji wa Simba tawi la Pangani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Wachezaji wa Yanga tawi la Pangani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Wachezaji wa Yanga tawi la Pangani wakiwapasha.
Wachezaji wa Simba tawi la Pangani wakiwapasha.
Wasanii wanaunda kundi la Uzalendo Kwanza wakifuatilia mtanange huo.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na waamuzi wa mtangane. Akisalimiana na wachezaji wa Simba tawi la Pangani.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana nawachezaji wa Yanga.
 Tambo za watani wa Jadi, Jerry Muro akitoa yake.
 Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo akimpa sapoti Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati akionyesha vitu vyake. Pembeni ni Mwakibinga.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah Issa akipatiwa hela na Msemaji wa Simba Haji Manara.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akisalimiana na Msemaji wa Simba Haji Manara.
Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
Ilikuwa ni vuta ni kuvute...
Wachezaji wakionyesha umwamba. Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza na  Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (mwenye kofia nyeusi) wakifuatilia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga. Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akiwa na Mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa wakifuatilia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Aweso (AWESO CUP 2018) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iyopita mjini Pangani, Tanga.
Asha Boko na Tausi wakionyeshana umwamba huku Msanii Nuh Mziwanda akitoa burudani.
Umatu wa watu waliohudhuria.
Mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa akiongea na wanachi wa Pangani wakati wa zoezi la kugawa zawadi.
mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa 
 Zawadi ya Jezi zikitolewa.
Wachezaji wa Yanga na Simba wakiwa wamebeba zawadi ya Maziwa ya Asas.
Picha/Habari na Cathbert Kajuna na Oscar Assenga- Pangani.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amefungua mashindano ya kombe la Aweso katika uwanja Kumba wilaya Pangani na kuwataka viongozi wa halmashauri ya Pangani kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya kuchezea. Katika kufanikisha ufunguzi wa kombe la Aweso wasanii wa filamu wanaunda kundi la Uzalendo Kwanza walishiriki ili kuhamasisha vijana kupenda michezo na sanaa.

 Akifungua mashindano hayo Naibu Waziri Juliana Shonza akatoa agizo kwa viongozi wa halmashauri kukarabati viwanja huku mkuu wa wilaya wa Pangani, Zainab Abdallah Issa amesema kuanzisha kwa kombe la Aweso kuanarudisha ari ya michezo wilayani humo. Kwa upande wake Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ambaye ndiye mwaandaaji wa kombe hilo amesema katika mashindano hayo watapatika vijana wenye vipaji. Nae mwenyekiti wa uzalendo kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema ushiriki wao unasaidia vijana kupenda michezo na sanaa. 

 "Tumekuja kuwaamsha vijana wenzetu ili watambue umuhimu wa kuwa Wazalendo na kujikwamua na watambue vipaji vyao, maana vijana wengi wamepoteza matumaini ya kuishi kutokana na kujiona wametengwa na jamii" amesema. Jumla ya timu 20 zinashiriki michuano ya kombe la uweso ambapo timu shiriki zikabidhiwa vifaa vya michezo na naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo. 

Katika ufunguzi wa kombe hilo uchezwa mchezo wa mashabiki Simba na Yanga ambapo timu ya Simba ikiongozwa na Msemaji Haji Manara waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga na wakapata maziwa ya Asas na fedha laki tano huku Yanga wakipata laki tatu na maziwa ya Asas. Huku zikishuhudiwa na Naibu Waziri wa Habari Michezo, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mkuu wa wilaya Pangani, Zainabu Issa, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE MOROGORO

$
0
0

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Magezera mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa magereza Mwandamizi (SACP) Mzee ramadhani Nyamka alipowasili Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo leo Mei 7, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Magezera mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa magereza Mwandamizi (SACP) Mzee ramadhani Nyamka alipowasili Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo leo Mei 7, 2018 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho leo Mei 7, 2018 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribisha maswali, maoni na ushauri toka kwa  jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho leo Mei 7, 2018. Wengine toka kulia ni Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa SUA Profesa  Raphael Tihelwa Chibunda,  Waziri wa elimu,sayansi,na teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe stephen Kebwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa taarifa nzuri Makamu Mkuu wa  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihelwa Chibunda alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho leo Mei 7, 2018.
 Sehemu ya wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Mrorogoro wakimsilikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofika na kukutana nao chuo hapo leo Mei 7, 2018


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Makamu Mkuu wa  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihelwa Chibunda alipofika na kukutana na wafanyakazi na wanafunzi pamoja na wadau wa chuo hicho leo Mei 7, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungiana mikono na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa   Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya kukutana nao leo Mei 7, 2018.  


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na baadhi ya  wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa   Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya kukutana nao leo Mei 7, 2018.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa alipotembelea   Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kukutana na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa chuo hicho leo meo7, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Tandari baada ya kukutana na  kuongea na wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wadau wa   Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada leo Mei 7, 2018.  Wengine ni  Waziri wa elimu,sayansi,na teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe stephen Kebwe.

Picha na IKULU

Biteko apiga marufuku bei holela madini ya ujenzi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amepiga marufuku tabia ya wachimbaji wa madini ya ujenzi ya kushusha bei ya madini hayo kwa ajili ya kuuza kwa wingi, badala ya kufuata bei elekezi iliyowekwa na Serikali  huku wakiwalipa  vibarua kiasi kidogo cha fedha kisichoendana na kazi ngumu wanazofanya.

Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo  mapema leo alipofanya ziara katika machimbo ya madini ya ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Amboni mkoani Tanga lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kuzungumza na wananchi.

Biteko alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa leseni kuuza madini aina ya kokoto kwa bei  ya chini na kupata faida huku wakiwalipa kiasi kidogo vibarua wanaofanya kazi ngumu ya kuponda kokoto kwa kutumia vifaa duni.

Akijibu kero mbalimbali zilizowasilishwa na wachimbaji madini ya kokoto Biteko alisema kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni hukakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha watanzania na kuwataka kuunda vikundi ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa na ruzuku kutoka Serikalini.

Alisema Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Usimamizi  Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imepanga mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupitia ruzuku na ununuzi wa vifaa vya uchimbaji ili waweze kufanya kazi katika mzaingira rafiki na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa  Sekta ya Madini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Tanga (kulia) Thobias Mwilapwa akielezea Sekta ya Madini katika Wilaya yake kwa watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vyombo vya Habari (hawapo pichani) kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika eneo linalotumika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi aina ya kokoto  lililopo katika eneo la Amboni Wilayani Tanga mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akizungumza na mponda kokoto, Helena  Joackim (aliyekaa chini) kwenye machimbo ya kokoto yanayomilikiwa na Swalehe  Khama yaliyopo katika eneo la Amboni Wilayani  Tanga mkoani Tanga.
 Mchimbaji mdogo wa madini ya kokoto Swalehe Khama akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye ziara hiyo.
 Mponda kokoto, Husna Bakari akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo kwa wachimbaji madini ya ujenzi aina ya kokoto kwenye ziara hiyo.


JAN INTERNATIONAL YACHEZESHA BAHATI NASIBU KWA WATEJA WAKE,MSHINDI AJISHINDIA GARI.

$
0
0

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Jan International Sheikh Muhmmad akisoma moja ya tiketi ya mshindi wa Bahati Nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo mbele ya wateja wao mapema mwisho mwa wiki Namanga,jijini Dar,ambapo mshindi alijinyakulia gari,kulia kwake ni Meneja wa Kampuni hiyo Mohamed Shebu Omari akishuhudia
  Murugenzi wa Kampuni ya Jan International Sheikh Muhmmad akiwaonesha  wateja wao (hawapo pichani) moja ya tiketi ya mshindi wa Bahati Nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo kwa Wateja wao mapema mwisho mwa wiki,Namanga Jijini Dar,ambapo mshindi alijinyakulia gari.
  Picha kulia ni baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Jan International wakimkabidhi Mshindi wa Bahati Nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo,mfano wa ufunguo kwa mshindi wa tatu kulia aliyejulikana kwa jina la Young Gwang Yu
Mshindi wa Gari Young Gwang Yu akiwa na mfano wa funguo mara baada ya kutajwa kuwa mshindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa na kampuni ya Jan International mbele ya Wateja wake mbalimbali (hawapo pichani),mapema mwisho mwa wiki. Jan International ni wauzaji wa magari yaliyotumika,ambapo kwa sasa inafanya kazi katika nchi 18 Duniani ikiwemo Tanzania

WATAKAO HUJUMU MIRADI YA ELIMU KUKIONA CHA MOTO.RC RUVUMA

$
0
0
Wilaya ya TUNDURU imefanikisha kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 600 kutoka kwa wakulima wa zao korosho,ambapo fedha hizo zitatumika katika kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuboresha kiwango cha cha ufahuru kwa wanafunzi na kupunga msongamoto wa wanafunzi katika madarasa.

kutokana na hutua hiyo mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME akawaonya viongozi wote watakaokwenda kinyume na utaratibu katika mtumizi ya fedha hizo. 

MASHINDANO YA SIRRO CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KIBITI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi mpira mmoja wa Viongozi wa timu zinazoshiriki mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti wakati wa uzinduzi wa michezo hiyo uliofanyika jana. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Migomba kutoka Wilayani Rufiji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasalimu wakazi wa Kibiti wakati wa Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Msanii Malima Ndolela (Mzee wa Ndolela) akitumbuiza wakati wa Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Msanii Man Prince akitumbuiza wakati wa Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

RC Makalla awataka wananchi kufanya mazoezi

$
0
0
Taasisi ya Mo Dewji imekuwa miongoni mwa wadhamini ambao kwa kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust wamewezesha kufanyika Tulia Marathon 2018, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo baada ya mbio za mwaka jana ambazo zilikuwa na mafanikio makubwa.

Akizungumza katika mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema watu wengi hawana utaratibu wa kufanya mazoezi jambo ambalo sio zuri kiafya na hivyo kuwataka wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Aidha Makalla alimpongeza Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zinasaidia sana mkoa huo kuboresha sekta ya afya na elimu. 

“Michezo ni muhimu sana kwa afya zetu … tujifunze na sisi tuanze kufanya mazoezi sababu ni muhimu sana kwa afya zetu. Mimi hapa nilipo sijawahi kuumwa maralia tangu nikiwa kidato cha kwanza lakini sababu nafanya mazoezi. Ukiwa unafanya mazoezi magonjwa haya ya pressure unaachana nayo,” alisema na kuongeza.

“Niseme tunafaidika sana kupitia Trulia Trust kwa mambo ambayo anayafanya, anaupenda mkoa wetu ameboresha miundombinu katika elimu na afya. Alianza kwenye ngoma na sasa anafanya Tulia Marathon na kutokana na marathon hii anakwenda kusaidia afya na elimu.”

Naye Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula alisema wameamua kushirikiana na Tulia Trust ili kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za afya.

“Tunatambua kwamba maisha ya mwanadamu yanaanza mimba inapotungwa hivyo ni muhimu sisi kama sehemu Watanzania tuliojengwa katika misingi ya upendo kuona ni muhimu kushirikiana na serikali na wadau wengine kama Tulia Trust kuweka mazingira bora ya wodi za uzazi ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini,

“Tunapongeza hatua ambazo zinachukuliwa na serikali za kukarabati vituo vya afya katika Halmashauri mbalimbali nchini kwa kujenga na kukarabati majengo ya upasuaji, wodi za wazazi na watoto pamoja na maabara. Tunaamini jitihada hizi zitasaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto nchini,” alisema Chengula.

Awali akizungumza kuhusu Tulia Marathon 2018, Dkt. Tulia alisema fedha ambazo zimepatikana katika mbio za mwaka huu zitatumika kusaidia kuboresha sekta ya elimu na afya kama ilivyokuwa mwaka jana na lengo lao ni kushirikiana na serikali ili kuwezesha wananchi wapate huduma bora za kiafya na elimu bora.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson akiongoza wanariadha waliojitokeza kukimbia katika Tulia Marathon 2018 zilizofanyika Jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dkt. Tulia Ackson akielezea mafanikio ambayo Tulia Marathon iliyapata kwa mwaka uliopita na mipango ya mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza namna Tulia Marathon inawasaidia kuboresha sekta ya afya na elimu na kutoa pongezi kwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

TANZANIA YATAJWA KUWA BUSTANI YA EDEN NA CHIMBUKO LA MWANADAMU WA KALE DUNIANI

$
0
0

Hatimaye utata uliokuwa ukiendelea duniani kwa watafiti wa mambo ya kale kuhusiana na mahali mwanadamu wa kwanza alipotokea umemalizika baada ya jopo la wataalam liloundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia ushahidi wa vinasaba kubaini kuwa binadamu huyo alitokea barani Afrika huku ikidaiwa kuwa ni Tanzania eneo la Olduvai Gorge.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki aloiutisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Amesema  utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani na kuwa kumalizika kwake kutaiwezesha sekta ya utalii nchini kukua kwa kasi sambamba na kuongeza pato la taifa.

MICHUZI TV: MZEE MAJUTO AFIKA SALAMA NCHINI INDIA, MWANAE AELEZEA WALIVYOPOKELEWA

MICHUZI TV: MZEE MAJUTO AFIKA SALAMA NCHINI INDIA, MWANAE AELEZEA WALIVYOPOKELEWA

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images