Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Wafanyakazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wauaga Mwili Wa Mfanyakazi Mwenzao

$
0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 jijini Dar es Salaam. Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakielekea katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiimba wimbo wa maombolezo kabla ya kwenda katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 .
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao ni marafiki wa karibu wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Marehemu Onesmo Mhewa wakieleza jinsi walivyofanya kazi kwa ukaribu na marehemu wakati wa halfa fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa na sura za majonzi wakati wa hafla fupi ya kuuaga mwili wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili . Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini.

Picha na JKCI

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW

$
0
0

Na.WAMJW

Serikali inatarajia kupata dola ya kimarekani milioni 512 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani kupitia fungu la mradi wa dharura wa Rais wa kupambana na UKIMWI Duniani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa akipokea rasmi taarifa ya kutolewa fedha za UKIMWI kwenye hafla iliyofanyika kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa.

Dkt.Ndugulile alisema fedha hizo ambazo serikali itapatiwa zitatumika kwa ajili ya kununulia dawa za kufubaza makali ya Virus vya UKIMWI pia zitagawiwa kwa afua mbalimbali za kupambana na kuzuia maambukizi ya UKIMWI pamoja na uhamasishaji wa upimaji wa Virus vya UKIMWI nchini. 

Aidha ,alisema kiasi hicho cha fedha zinatakiwa kutumika ndani ya mwaka mmoja kwa kwa kujikita kwenye malengo ya Dunia ya tisini tatu(90,90,90) kwa kuhakikisha kwamba asilimia 90 ya watanzania wote wanaohisiwa kuwa na Virusi vya UKIMWi wanafikiwa,asilimia 90 ya wenye Virusi baada ya kupima wana pata tiba na asilimia 90 wanaopata tiba kuweza kufumbaza Virusi vya UKIMWI.

Alisema kama nchi imekuwa na changamoto kubwa sana na asilimia 90 ya kwanza ya upimaji kutokana na Takwimu za mwaka jana za hali ya maambukizi nchini zinaonyesha bado kuna changamoto kubwa hususan kwenye makundi ya vijana bado maambukizi yanaongezeka hasa kwa wasichana”vilevile kwa upande wa wanaume ambao ni wagumu kwenda kupima na wengine wanapima ila wanachelewa kuanza dawa na kutofuata misingi ya umezaji dawa na hivyo kufa zaidi”.

“Mkakati ambao tunautafakari na kuja nao ni ule wa mwananchi kuweza kujipima wenyewe kwa kutumia mate(Self-Test) hivyo kila mtu aweze kujijpima mwenyewe kwa kwenda kununua kipimo duka la dawa kama ilivyo kwa wanawake kujipima ujauzito”alisema Dkt.Ndugulile

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haitawapima wanaume kwa nguvu kwenye ma bar bali itatumika utaratibu ule ule katika makundi yao kwa kuwapatia ushauri nasaha na kupima kwa hiari “hatusemi wanaume watapimwa kwa nguvu hapana utaratibu utakua ule ule hivyo wananchi msipate hofu” alisema dkt.Ndugulile

Alitaja mikakati mingine ni kwenda kuwafikia makundi mahususi ambayo inaonekana yana maambukizi makubwa ikiwemo ya wavuvi pamoja na migodini hivyo alitoa rai kwa watanzania kujitokeza ili kuweza kufikia asilimia 90 kutoka 52 ya upimaji wa Virus vya UKIMWI.Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inm alisema nchi yake ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kujenga Tanzania yenye afya nzuri.

SERIKALI YAWAAGIZA MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI KOTE NCHINI KUWA CHACHU YA MABADILIKO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Tixon Nzunda akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu  na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.
 Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Beatrice Kimoleta akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Tixon Nzunda kufungua kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.

Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu  na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Elimu ( hayupo pichani ) wakati  akifungua kikao kazi cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa OR-TAMISEMI  jijini Dodoma leo.
............................................................
Na Angela Msimbira, OR Tamisemi.

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa maelekezo ya kimkakati kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango na Uratibu pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Serikali za Mitaa kote nchini kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko yenye kujenga ustawi wa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI  anayeshughulikia elimu Mhe. Tixon Nzunda katika  Kikao kazi  cha kujadili tathmini ya uandaaji wa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019 na miradi ya kimkakati kwa Makatibu Tawala Wasaidizi  wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala wa Serikali za Mitaa kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Akifungua kikao hicho Nzunda amesema kuwa ili kuleta mabadiliko yenye lengo la kujenga ustawi wa wananchi lazima kuwe na rasilimali watu wanaoamini mabadiliko,  hivyo Makatibu Tawala Wasidizi wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa  ndio viongozi wanaopaswa kuelimisha jamii kuhusu dira, dhima  na programu ambazo Serikali inataka kufikia katika malengo makuu ya kujenga Ustawi wa wananchi.

Amewataka kubadilika kwa fikra, mtizamo, mwelekeo  na mikakati  ili kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa Serikali  kwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na serikali katika kutoa huduma bora kwa jamii na kuleta maendeleo nchini.

“Ninyi ndio “engine” (gurumudu) ya kuleta maadiliko. Ndio kitovu cha kuleta Mabadiliko saidianeni na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi, msiogope kuwashauri, kuwakosoa, na kuwaelekeza ili kuleta maendeleo katika jamii mnazozihudumia” Amesema Nzunda 

Mhe. Nzunda  amesema kuwa Serikali imejipanga  kuona mabadiliko makubwa  ya kiutendaji kuanzia ngazi  za Serikali za Mitaa hivyo amewataka kutoa maelekezo ya Serikali yanazingatia Sera, sheria, kanuni  na programu za uendeshaji  kazi ndani ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“ Makatibu Tawala wa Mipango na Uratibu na Makatibu Tawala Wasidizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanapaswa kujua dira ya Serikali  na mipango ya Mikoa  na kuwa na dhana ya usimamiaji na ufuatiliaji mtakuwa mmesaidia kuleta mabadiliko makubwa kwenye Mikoa yenu” Amesema Nzunda

Katika suala ya matumizi wa fedha za miradi Mhe Nzunda amesema kuna tatizo linaloendelea la kubadilisha matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi, fedha kukaa muda mrefu kwenye akaunti bila kufanyiwa kazi kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuchelewa kukamilika kwa miradi.

Aidha amezitaja baadhi ya changamoto za uandaaji wa mpango zinazoikumba mamlaka ya serikali za mitaa kuwa ni kutozingatia mpango mkakati, kutozingatia vipaumbele vya serikali  pamoja na kushindwa kusimamia bajeti ipasavyo.

Katika hatua nyingine Nzunda ameoneshwa kukerwa na tabia za baadhi ya Wakurugenzi ambao hadi sasa hawajawalipa fedha za uhamisho walimu waliohamishwa kutoka shule za msingi kwenda kufundisha shule za sekondari wakati serikali ilishatoa fedha hizo, hivyo aliwataka suala hilo kusimamiwa kikamilifu.

Akizungumzia juu ya baadhi ya halmashauri kupata hati chafu na nyingine kutapa hati zisizoridhisha amesema kitendo hicho kinasababishwa na uzembe wa watu wengi na sio Mkurugenzi peke yake bali wahusika wote watawajibishwa ili kuhakikisha kuwa kila mtu anawajibika ipasavyo katika majukumu yake.

Awali akimkaribisha Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa  Bi. Beatrice Kimoleta amesema lengo la kikao hicho ni kujitathmini juu ya bajeti iliyomalizika sasa pamoja na kuandaa mipango na bajeti katika mwaka wa fedha 2018/2019.

DK RICHARD MASIKA ATEULIWA MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA(AUWSA)

$
0
0
Filbert Rweyemamu,Arusha.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Isack Kamwele amemteua Mhandisi Dk. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(AUWSA) kuanzia April 23 hadi April 22, 2021.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini,Athumani Shariff ilisema Dk Masika alikua Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha hadi alipostaafu Septemba 30,2017.

Pia Mhandisi Kamwele amewateua wajumbe tisa wa bodi ya AUWSA ambao ni Richard Kwitega(Katibu Tawala mkoa),Athumani Kihamia(Mkurugenzi wa Jiji),Francis Mbise(Diwani wa Kata ya Muriet,Vincent Lasway(Mfanyabiashara) na Elishilia Kaaya(Mkurugenzi Mtendaji-AICC).

Wajumbe wengine ni Jackiline Mkindi(Mkurugenzi wa (TAHA),Mhandisi Ruth Koya(Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA),Edward Mrosso(Wakili) na Agnela Nyoni(Mwakilishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji).

Katika uteuzi mpya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha kwa nafasi yake huingia moja kwa moja lakini wakati huu hakuteuliwa baada ya Bodi iliyopita kuvunjwa Januari 19,2018 na Waziri wa Maji kwasababu ya kutoridhishwa kiutendaji.Bodi iliyopita Mwenyekiti alikua Dk Job Laizer,Richard Kwitega,Athumani Kihamia,Kalist Lazaro,Agnela Nyoni,Charles Marunda,Thomas Mosso,Halima Mamuya,Mhandisi Felix Godfrey na Mhandisi Ruth Koya.

Pia Dk Masika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Michezo Malya katika uteuzi uliofanywa na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe April 4 mwaka huu.Akizungumza na Mwananchi jana,Dk Masika alisema bado ni mapema kuzungumzia mikakati ya Bodi mpya kwakua haijazinduliwa ila atajitahidi kuongeza tija,ufanisi na kutoa huduma bora zaidi.

"Bodi ikishazinduliwa na kuanza kazi tutajitahidi kutekeleza wajibu wetu kwa weledi,ubunifu,bidii na uaminifu kwaajili ya kuwahudumia wananchi wetu,"alisema Dk Masika.Serikali imetoa kiasi cha Sh 514 bilioni kwaajili ya kuhakikisha kero ya maji katika jiji la Arusha na viunga vyake linakua historia na utekelezaji wa mradi umeshaanza.
Mhandisi Dk Richard Masika 

RAIS DKT. MAGUFULI AONGEA NA WANANCHI MIKUMI, AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU –IFAKARA YENYE KM 66.9 NA DARAJA LA MTO RUAHA ENEO LA NYANDEO KIDATU

$
0
0
Wananchi wakimsikikliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli eneo Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Wananchi wakimsikikliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli eneo Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Wananchi wakimsikikliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli eneo Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Wananchi wakimsikikliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli eneo Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi eneo la Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi eneo la Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi eneo la Mikumi wakati akiwa njiani kuelekea kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuhusu matatizo ya mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya  Kidodi mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuhusu matatizo ya mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya  Kidodi mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtendaji wa eneo hilo akizungumza kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuhusu matatizo ya mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya  Kidodi mkoani Morogoro.
Bendi ya Uluguru Original ikitumbuiza
Wimbo wa Taifa
Sehemu ya wageni waalikwa 
Sehemu ya wageni waalikwa 
Wabunge na Sehemu ya wageni waalikwa 
Wabunge na sehemu ya wageni waalikwa 
Makandarasi wasimamizi
Kamati ya ulinzi na usalama
Sehemu ya wageni waalikwa 
Sehemu ya wageni wananchi
Sehemu ya wageni wananchi
Sehemu ya wageni wananchi na watendaji
Sehemu ya wageni wananchi
Sehemu ya wageni wananchi
Sehemu ya wageni wananchi
Sehemu ya Wanahabari wa Morogoro wakifuatilia kila kinachoendelea
 Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Morogoro Ndg. Innocent Kalogeris akisalimia wananchi

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe akisoma ripoti ya mkoa wake
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga akitambulisha wageni
Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer akitambulishwa

Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akisoma muhtasari wa mradi
Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy
Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer akiongea
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwaalika wabunge wa mkoa wa Morogoro kusalimia wananchi
Wabunge wa Morogoro wakiitikia wito
Mbunge wa Malinyi Mhe. Dkt. Haji Mponda akisalimia wananchi
Wabunge wa Morogoro wakisubiri zamu zao kusalimia wananchi
Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijualikali akisalimia wananchi
Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijualikali akisalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule "Profesa J" akisalimia wananchi
Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule "Profesa J" akisalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mbunge wa Mikumi Joseph Haule kutumbuiza katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.
Mbunge wa Mikumi Joseph Haule akitumbuiza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.
Mbunge wa Mvomero Mhe. Suleiman Saddiq akisalimia
Mbunge wa Mvomero Mhe. Suleiman Saddiq akisalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akisalimia
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akisalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Getrude Rwakatare akisalimia
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Getrude Rwakatare akisalimiana na Mama Janeth Magufuli 
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Getrude Rwakatare akisalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Mbunge wa Mlimba Mhe. Suzan Kiwanga akisalimia wananchi
Mbunge wa Mlimba Mhe. Suzan Kiwanga akifurahia jambo baada ya kusalimiana na Rais Dkt. Magufuli
Mbunge wa Kilosa Mhe. Mbaraka Salim Bawazir akisalimia
Mbunge wa Kilosa Mhe. Mbaraka Salim Bawazir akisalimiana na Rais Dkt Magufuli
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Dk Jasmin Tsekwa akisalimia wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Viti Maalum kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Dk Jasmin Tsekwa 
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Imary Mgumba akisalimia
Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Imary Mgumba akisalimiana na Rais Dkt Magufuli
Mbunge akisalimia
Mbunge akisalimiana na Rais Dkt Magufuli
Mbunge wa Morogoro mjini Mhe. Abdulazizi Mohamed Abood akisalimia
Mhe. Abood akisogea kusalimiana na Rais Dkt Magufuli
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge Mhe Moshi Selemani Kakoso(Mpanda Vijijini) akisalimia wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge Mhe Moshi Selemani Kakoso(Mpanda Vijijini) akisalimiana na Rais Dkt Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kidatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la kidatu lenye urefu wa mita 130.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea eneo la uwekaji wa jiwe la msingi akiwa na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya mradi toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akiwa na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria kuwekwa jiwe la msingi pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Ami Mpungwe aliyekuwepo kwenye hafla hio.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy kushoto  na Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer kulia kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kushoto pamoja viongozi mbalimbali na wabunge wa mkoa wa Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia baada ya kukata utepe pamoja Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy kushoto  na Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer kulia kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kushoto pamoja viongozi mbalimbali na wabunge wa mkoa wa Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja baada ya kuweka jiwe la msingi pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja baada ya kuweka jiwe la msingi pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro baada ya kuhitimisha hafla hio.

NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AJIFUA KUJIANDAA NA MBIO ZA MTM KESHO

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (katikati mbele) akiwaongoza baadhi ya wanamichezo Jijini Mbeya katika mazoezi ya kukimbia zaidi ya Kilomita 8 kutokea Uzunguni hadi kiwanja cha michezo Ruanda Nzovwe kujiandaa na Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zinazofanyika kesho jijini Mbeya kuanzia saa 12 asubuhi katika Uwanja wa Sokoine. 

Halmashauri ya Manispaa Kigamboni yapongezwa kwa kupata Hati safi

$
0
0
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni limeipongeza Manispaa kwa kupata Hati safi baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba kutoa taarifa ya kupokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG )inayoonesha Manispaa kuwa na hati safi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Pongezi hizo zimetolewa leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la kawaida la robo ya tatu ya mwaka (Jan-Mach 2018) lililofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Kisota .Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad amesema kuwa Hati safi imepatikana kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Wataalamu wa Manispaa na Madiwani na kwamba ni faraja kwa Manispaa nzima.

"Tumefarijika sana kupata matokeo haya, hati hii safi isingepatikana kama kungekuwepo na kutokuelewana baina ya wataalamu na madiwani, tunajivunia umoja wetu"Alisema Mh.Hoja .Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya amesema kuwa kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Baraza lina kila sababu ya kuipongeza Manispaa kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha pamoja na upya wake hati safi inapatikana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa tafsiri ya matokea haya ni ushirikiano uliopo kati ya watendaji , wasimamizi pamoja na Waheshimiwa Madiwani ndio uliopelekea kupatikana kwa Hati safi.

Ameongeza kuwa kuangalia nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali, kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba rasilimali watu ambao anawaongoza wapo katika kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa la wananchi kupata huduma zile zilizokusudiwa. Tunashukuru tumeweza kufikia malengo yaliyotarajiwa na tunaamini hata katika mwaka wa fedha unaokuja tutaendelea kufanya vizuri" Alisema Mkurugenzi.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepata hati safi ( Unqualified Report) kwenye sekta zote na miradi ya maendeleo ikiwemo ya Barabara na Maji inayotekelezwa na Manipsaa

Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
04/05/2018.
 Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifatilia taarifa za Kata kwa makini
 Baadhi ya Wataalamu walioshiriki kwenye kikao cha Baraza
 Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya akitoa pongezi kwa watendaji wa Manispaa kwaniaba ya Madiwani wote.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba akitoa taarifa ya kupokea  Hati safi kutoka CAG
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad akiwapongeza Wataalamna Madiwani  kwa ushirikiano uliopelekeakupatikana kwa Hati safi.
 

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI,AFUNGUA DARAJA KUBWA MTO KILOMBERO LILOLOPEWA JINA NA DARAJA LA MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
DCIM100MEDIADJI_0568.JPG
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Wabunge wa mkoa wa Morogoro na Viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali mara baada ya kufungua Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.PICHA NA IKULU




 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula kona katika Wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli lenye urefu wa M384) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiberege wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mang’ula Mrindoko Msangi mara baada ya kumkabidhi kiasi cha Shilingi milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule hiyo. Mwanafunzi huyo alielezea kwa ufasaha kero inayowakabili shuleni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanakijiji wa Sanje( hawapo pichani ) wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

SERIKALI YAELEZA FURSA YA UFUGAJI WA NYUKI HAPA NCHINI - NAIBU WAZIRI JAPHET HASUNGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo. Kushoto ni MKuu wa Kitengo cha Masoko, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mwanahamisi Mapolu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Deosdedit Bwoyo.

Na Hamza Temba - Dodoma
.............................................................

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa kubwa iliyopo hapa nchini ya ufugaji nyuki na uwepo wa masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao yake na kuyaongezea thamani ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo leo mbele ya wadau wa sekta ya ufugaji nyuki kutoka mikoa yote nchini katika mkutano aliouitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Amesema kwa sasa mchango wa sekta ya nyuki katika pato la taifa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo za ufugaji nyuki hapa nchini ambazo zikitumiwa ipasavyo zitasaidia kuinua pato la wananchi na taifa kwa ujumla.

Amesema mbali na kuongeza uzalishaji, mazao hayo pia yanatakiwa kuongezewa thamani na kuwekewa ngazi za ubora ili yaweze kuhimili masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, ili kuimarisha sekta hiyo Serikali itashirikiana na wadau kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kutafuta masoko, kuimarisha uwekezaji na kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta ambayo ina soko kubwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa wizara hiyo, Deosdedit Bwoyo amesema Tanzania ni moja kati ya nchi 50 duniani zenye utajiri mkubwa wa rasilimali za misitu ambazo zinatoa fursa pana ya ufugaji nyuki nchini.

Amesema eneo la misitu ni takriban hekta milioni 48.1 ambalo ni asilimia 54 ya ukubwa ardhi yote ya Tanzania ambayo ikitumiwa ipasavyo na wananchi itawawawezesha kujiajiri na kuongeza uzalisahaji wa mazao ya nyuki na mapato.

Amesema ili kulinda mazalia ya nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini, Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS, imeanzisha hifadhi za nyuki 11 huku Serikali za vijiji zikianzisha hifadhi za nyuki 14.

Wadau walioshiriki mkutano huo ambao ni wazalishaji, wachakataji na wasafirishaji wameishukuru Serikali kwa kuandaa mkutano huo na kuiomba kusaidia katika tafiti, elimu kwa wananachi wanaojihusisha na ufugaji nyuki hususan maeneo ya vijijini na utafutaji wa masoko ya uhakika.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deosdedit Bwoyo akiwasilisha hotuba yake kwa wadau hao.Mkurugenzi Msaidi wa Uendelezaji Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Allen Richard akitambulisha meza kuu katika mkutano huo.Wadau wa Misitu na Nyuki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani). Katikati ni Magdalena Muya wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Stephen Msemo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (kulia).Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano huo.Mmoja ya wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini akitoa maoni yake.Mmoja ya wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini akitoa maoni yake.Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini wakati wa kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo.Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini wakati wa kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo.

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AZINDUA MASHINDANO YA AWESO CUP,MURO NA MANARA WAYANOGESHA KUWAONGOZA MASHABIKI WA SIMBA VS YANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikagua wachezaji wa timu ya  Mashabiki wa Yanga muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya mashabiki wa Yanga na timu ya mashabiki wa Simba leo mjini Pangani.
PIC 02
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya  mashabiki wa Simba muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kushoto kwake ni Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso.
PIC 03
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akifurahia jambo na Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.
PIC 04
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na aliyewahi kuwa Msemaji wa Timu ya Yanga Bw. Jerry Muro wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.
PIC 05
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishin wa Habari muda mfupi kabala ya kuanza kwa  mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso ambaye ni mdhamini wa mashindano hayo.
PIC 06
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokea fedha taslimu shilingi milioni moja kutoka kwa Bw. Romanus Mkonda Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama mchango kwa ajili ya mashindano ya Aweso Cup.Kulia kwake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah wakishuhudia tukio hilo leo mjini Pangani.
PICHA ZOTE NA:OCTAVIAN Kimario
WHUSM

MBEYA PRESS CLUB WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KWA MJADALA MKUBWA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika akizungumza wakati akifungua mkutano wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3 waadishi wa Habari mkoa wa Mbeya wamadhimisha siku hiyo leo, Kutoka kulia ni Frank Leonard Mwenyekiti wa Press Club Iringa, Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club. KAULI MBIU ya maadhimisho hayo mkoa wa Mbeya ni "Uhuru wa Vyombo vya habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa Maendeleo ya Mkoa wa Mbeya" 


Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Frank Leonard Mwenyekiti wa Iringa Press Club wakati akizungumza katika mkutano huo kama mmoja wa wageni waalikwa, katikati ni Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club.


Frank Leonard Mwenyekiti wa Iringa Press Club akichangia mada katika mkutano huo.


Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Bi. Julieth Godrey Manech akichangia na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa upande wa Taaisis ya Kuzuia rushwa nchini TAKUKURU jinsi waandishiwa wanavyoweza kushirikiana na tasisi hiyo.


Mwanahabari Charles Mwakipesilepamoja na baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mjadala huo.


Mdau Joseph Mwaisango ni mmoja wa wanahabari walioshiriki katika maadhimisho hayo.


Wadau mbalimbali wakiwa wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo


Mwanahabari Naomi Malala akizungumza jambo na mwanahabari mwenzie Rachel Mwangosi huku Plaxeda Mbullu akiwasikiliza.

  

Keneth Simbaya Rais Mstaafu wa Vyama vya waandishi wa habari nchini UPC pamoja na washiriki wengine wakiwa katika mkutano huo.


Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari mara baada ya kufungua mkutano wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3

TIRA IKISHIRIKIANA NA TAASISI YA BIMA NCHINI IIT YAZINDUA MFUMO WA TIIP

$
0
0

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo A. Saqware akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo mara baada ya kuzindua mfumo wa kieletroniki ujulikanayo kama Tanzania Imports Insurance Portal(TIIP)utakao wezesha waagizaji bidhaa nje ya nchi kununua Bima toka kampuni za kitanzania,mfumo huo umeandaliwa na TIRA ikishirikiana na Taasisi ya Bima nchini (IIT)warsha iliyofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa Bima.(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Meneja wa kanda kaskazini wa usimamizi mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elieza Rweikiza akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha Juzi
Wadau wa Bima wakisikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo pamojana mambo mengine alisema kuwa Soko la bima Tanzania linaendeshwa na kampuni za bima zipatazo 31,madalali takribani 150 na wakala wa bima wapatao 413,Sekta ya bima husimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA)kwa mujibu wa sheria ya bima ya mwaka 2009
Rais wa Taasisi ya Bima Tanzania BoscoJames Bugali akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha

Meza mkuu
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru(kushoto)akiwa na Mkurugenzi wa sheria TIRA
Meneja wa kampuni ya Bima ya Britam Lois Yateru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo

SERIKALI KUTUMIA BILIONI 131.47 KUTEKELELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb).
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb) wakinyanyua vitabu vya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka, akinyanyua Kitabu cha Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa-TAMISEMI, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini mikataba ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushuhudia kutiwa saini mikataba ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Sekretarieti ya maandalizi ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkakati huo, Jijini Dodoma.

 Wadau kutoka Sekta mbalimbali wakiwemo wabunge, wakurugenzi wa TAMISEMI na viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliohudhuria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.


Na Benny Mwaipaja, WFM,  Dodoma
 Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Serikali imezindua Mkakati wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za     Mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea.

 Mkakati huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambapo amesema kiasi cha shilingi bilioni 131.47 kitatumika kutoa ruzuku ya utekelezaji wa miradi 22 kwa halmashari 17 zilizoko katika mikoa 10 nchini, katika mwaka wa fedha 2018/19.

 Ameitaja mikoa hiyo ambayo Halmashauri zake zimekidhi vigezo vya kunufaika na miradi ya kimkakati katika awamu ya kwanza ya mpango huo kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro, Mtwara, Pwani, Simiyu na Songwe.

 Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa Halmashuri zinajenga uwezo wa kujitegemea kwa takribani asilimia 80 hadi 100 ifikapo mwaka 2025, badala ya hali ya sasa ambapo halmashauri hizo zinategemea ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa zaidi ya asilimia 88.Amezitaka halmashuri zitakazopata fedha za miradi hiyo kuhakikisha fedha hizo zinawekezwa kwenye miradi yenye tija, inayokuza ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya halmashauri.

Ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kubuni miradi ya kibiashara kwa ajili ya wananchi wanaowaongoza kwa kutengeneza ajira kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Alionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji wanaosimamia miradi hiyo ikiwa watatumia fedha hizo kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa na kurejea kauli ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwamba kufuja fedha za Serikali katika kipindi hiki ni sawa na kunywa sumu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, amesema kuwa Serikali inazo fedha za kutosha kufanikisha mkakati huo na kutoa wito kwa viongozi wa Mikoa husika kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanisha miradi yenye tija ili ipatiwe fedha.

Alifafanua kuwa tayari Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wa Dar es Salaam katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kujenga Kituo cha Mabasi cha Mbezi Luis, Ujenzi wa Soko la Mburahati katika Manispaa ya Ubungo, Ujenzi wa Soko la Kisasa la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Selemani Jaffo (Mb) amesema kuwa Ofisi yake itaanza kufuatilia na kupima utendaji kazi wa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini ili kuona kama wanaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliwapongeza Wakurugenzi walioonesha mfano katika kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni miradi yenye tija na ya kimkakati iliyopewa Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango na kuwataka watendaji wengine waige mfano huo.

Baadhi ya miradi itakaotekelezwa na Halmashauri zilizokidhi vigezo ni pamoja na Ujenzi wa Masoko ya Kisasa, Ujenzi wa Maegesho ya Malori, Ujenzi wa stendi za kisasa, Maghala ya kuhifadhi mazao, Masoko ya Kisasa, Machinjio na Ujenzi wa Viwanda.

SIR ALEX FERGUSON AFANYIWA UPASUAJI KATIKA UBONGO WAKE, AWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUM

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson imebainika amefanyiwa Upasuaji katika Ubongo wake baada ya hapo awali kuripotiwa kuumwa ghafla.


Manchester United kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter imetoa taarifa ya kuumwa kwa Sir Ferguson kwa kusema kuwa "Tayari ameingia kufanyiwa upasuaji wa Ubongo wake na zoezi linaendelea vizuri lakini anahitaji kuwa katika Uangalizi maalum kwa msaada ili arudi katika hali yake ya kawaida".

Kabla yakuumwa, Sir Alex Ferguson hapo nyuma alinekana katika mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal, Old Trafford wakati wakumuaga Kocha wa Washika Mitutu wa London (Gunners), Arsene Wenger anayeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.


Sir Alex Furguson alishinda Mataji 13 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 26 alipokuwa akiifundisha Manchester United kabla yakustaafu mwaka 2013.

Chanzo: Goal. com
 

Kampuni ya utafiti wa madini ya CANACO yapewa siku saba kuwasilisha mkataba serikalini

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipa siku saba kampuni  inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited, kuwasilisha mikataba na nyaraka zote kati yake na kampuni ya Tanzania Gold Field Limited ili kubaini namna makubaliano  ya mkataba yalivyofanyika ikiwa ni pamoja na ulipaji kodi serikalini,
Biteko aliyasema hayo  alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo  wilayani Handeni mkoani Tanga mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania  Limited na kutoridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo.
Waziri  Biteko yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua shughuli za madini pamoja na kuzungumza na wananchi na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli za madini.
Alisema mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania Limited, amebaini kuwa kampuni hiyo mara baada ya kukamilisha shughuli zake za utafiti wa madini ya dhahabu, kampuni hiyo iliikaribisha kampuni nyingine ijulikanayo kama Tanzania Gold Field Limited ya Canada kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo la Magambasi wilayani Handeni mkoani Tanga pasipo kufuata taratibu za kisheria.
Aliendelea kusema kuwa, kampuni ya Tanzania Gold Field Limited iliwataka wachimbaji wadogo waliokuwa wanaendelea na shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo kuondoka ili waanze uchimbaji madini jambo ambalo lilitekelezwa.
Alieleza kuwa, kampuni ya Tanzania  Gold Field Limited ilianza shughuli zake bila kuwasilisha makubaliano ya kimaandishi kati yake na kampuni ya CANACO Tanzania Limited  Serikalini pamoja na kodi jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.
Biteko aliendelea kusema kuwa kampuni inayotambulika mpaka sasa kisheria ni ya  CANACO Tanzania Limited ambapo shughuli za madini katika eneo la Magambasi zimekuwa zikifanyika bila kufuata sheria na kanuni za mazingira.
“Haiwezekani wachimbaji wadogo ambao ndio wamiliki wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wakaondolewa halafu akapewa mwekezaji mkubwa ambaye mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuchejua mabaki wa udongo wenye dhahabu na kuuza na kuharibu mazingira huku wachimbaji wadogo  wenye uwezo wa kuchimba dhahabu wakihangaika na kuishi katika lindi la umaskini,” alisema Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika  eneo la kampuni inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.

 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wa pili kutoka kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni  inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.
 Sehemu wa wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo mbele ya wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe (kushoto) akielezea mchango wa sekta ya madini kwenye wilaya yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia).

MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA 2018/19 WAANZA RASMI

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Eng Charles Tizeba akizindua msimu wa ununuzi pamba mwaka 2018/19 wilayani Igunga. 

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ametangaza bei elekezi ya kununulia pamba msimu huu wa 2018/19 kuwa shilingi 1,100/= kwa kilo moja ya pamba mbegu. Akiongea katika siku ya ufunguzi wa msimu wa ununuzi wilayani Igunga tarehe 1/5/2018 Mhe. 

Tizeba amesema, “Msimu huu bei ya pamba itakuwa shilingi 1,100/= kwa kilo moja kutokana na bei katika soko la dunia kuwa haziridhishi, na kwamba bado pamba yetu nyingi inauzwa nje ikiwa ghafi hali inayotufanya tuwe tegemezi kwenye suala la bei, lakini Serikali iko katika mchakato wa kuhamasisha maendeleo ya Viwanda vya nguo nchini hali hii itaboresha bei ya pamba nchini” Aliongeza kusema kwamba, ili kumpunguzia mkulima mzigo wa madeni ya pembejeo na makali ya bei kushuka kwa shilingi mia kutoka ile ya msimu uliopita, Serikali imeamua kulibeba deni la zaidi ya shilini bilioni 30 la viuadudu ambavyo wakulima walikopeshwa msimu huu ili kuwafanya wakulima waweze kunufaika na kilimo chao. 

Aidha kuanzia msimu ujao wa kilimo, wakulima watapatiwa pembejeo zote ambazo ni mbegu za kupanda, kamba za kupandia na viuadudu bure bila kulipia gharama yoyote. Akifafanua kuhusu mchakato wa bei, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga alisema; bei elekezi ya pamba inasimamiwa kwa sheria ya Pamba Na.2 ya mwaka 2001, ambayo inaelekeza kwamba kabla ya msimu wa ununuzi wa pamba kuanza lazima wadau wa msingi wa zao la pamba wakutane na kukubaliana juu ya bei. Hili limewekwa ili kuwa na mazingira ya ushindani wa haki katika biashara ya pamba na kulinda maslahi ya wakulima.

 “Kwa mujibu wa sheria ya Pamba Na. 2 ya mwaka 2001, Bodi ya Pamba ambayo ndiyo msimamizi wa tasnia ya pamba inaitisha kikao cha kujadili na kukubaliana kuhusu bei elekezi ya kununulia pamba kabla ya kuanza kwa msimu. Wadau wa msingi katika kikao cha bei ni wakulima wanaowakilishwa na Vyama vya Ushirika, Wanunuzi wa Pamba, Wizara ya Kilimo, Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Pamba na Bodi ya Pamba inayosimamia mchakato mzima. Vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika mchakato wa kupata bei elekezi ni pamoja na bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia, gharama za ununuzi na uchambuaji wa pamba, ushuru wa Serikali na bei ya mbegu za kukamua mafuta”. 

Alisema Mtunga Pamoja na bei elekezi ya msimu huu kushuka kwa kiasi cha shilingi 100 ikilinganishwa na msimu uliopita, lakini ukweli ni kwamba msimu uliopita wafanyabiashara wengi walishindwa kufanyabiashara ya pamba kutokana na gharama kuwa kubwa hali ambayo ilifanya wakulima kukaa na pamba yao kwa muda mrefu sana bila kupata soko. Kwa makisio ya uzalishaji wa tani 600,000 msimu huu ambao ni ongezeko la zaidi ya asilimia 400 kutoka tani 132,000 za msimu uliopita, hatua za makusudi lazima ziangaliwe ili kuhakikisha mkulima hakosi soko; hii ni pamoja na kuwa na bei ambayo ni rafiki kwa pande zote za mnunuzi na mkulima.

 “kumekuwa na ongezeko kubwa sana la eno la uzalishaji wa pamba msimu huu kutoka ekari 650,000 msimu uliopita hadi ekari 3,000,000 msimu huu ambazo zimepandwa tani 26,500 za mbegu. Ongezeko hili linamaanisha onezeko pia la pato la mkulima mmoja mmoja” alisema Mtunga. Akifafanua kuhusu mfumo wa ununuzi wa pamba, Mtunga alisema, pamba yote ya wakulima itanunuliwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS). 

Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Vyama vya Ushirika na Mrajisi wa Ushirika wanawajibika kusimamia zoezi la ununuzi na kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati. Fedha za wakulima baada ya kuuza pamba zitalipwa kupitia akaunti za benki za wakulima ndani ya siku tatu baada ya mkulima kuuza pamba yake kwenye Chama cha Msingi. Wanunuzi wote wanawajika kununua pamba kutoka kwenye Vyama vya Msingi na siyo kwa wakulima.

 Aidha mnunuzi atalipa chama cha msingi asilimia tatu (3%) ya ushuru kama gharama ya ununuzi wa pamba. Mchakato wa kuanzisha vituo vya ununuzi chini ya AMCOS sanjari na kutoa elimu ya ushirika na matumizi sahihi ya mizani ya digiti unaendelea katika maeneo yote inakozalishwa pamba. Wakala wa Vipimo (WMA) watasimamia suala la mizani kuhakikisha inafanya kazi inavyostahili. 

 “Bodi ya Pamba itaendelea kusimamia ununuzi katika AMCOS kuhakikisha biashara inafanyika kwa uwazi na haki, wakulima wanalipwa kwa wakati na uzingatiaji wa sheria za ununuzi wa pamba pamoja na usafi na ubora wa pamba” alisema Mtunga na kuongeza kwamba; usafi na ubora wa pamba ni suala ambalo linapewa kipaumbele kikubwa kwa sababu uchafu kwenye pamba unaathiri ubora na sifa ya pamba katika soko la dunia. 

Wakulima na wanunuzi wanajibu wa kutunza ubora wa pamba. Utafiti unaonesha kwamba kuongezeka kwa tija katika kilimo cha pamba kutamuongezea mkulima kipato zaidi kuliko ongezeko la bei, hali ambayo iliifanya Bodi ya Pamba kuwekeza katika utoaji wa elimu ya Kanuni Kumi za Kilimo Bora cha Pamba hasa upandaji wa pamba kwa mistari. Msimu uliopita wilaya zaidi ya 13 zilipatiwa kamba za kupandia pamba zilizowekewa vipimo ambazo ziligawiwa bure kwa wakulima; msimu ujao Bodi ya Pamba inatarajia kugawa kamba katika maeneo yote yanayolimwa pamba. 

Katika msimu ujao wa kilimo 2018/19, wakulima wote watapanda mbegu aina ya UKM08 ambayo imeidhinishwa; mbegu hii kwa mujibu wa utafiti itamwongezea mkulima tija kwa zaidi ya asilimia 25 kwa sababu inaukinzani na magonjwa ya pamba ambayo ni Mnyauko Fuzari na Bakabakteria, pia ina uwiano mkubwa wa nyuzi ikilinganishwa na aina nyingine za mbegu hususan UK91. 

Ili kufikia uchumi wa kati na viwanda, Serikali inahamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda vya nguo nchini ili pamba yetu iwezekuongezewa thamani kabla ya kuuzwa nje ya nchi na kuongeza bei ya pamba kwa mkulima. Pamba inazalishwa katika mikoa 17 nchini ambayo ni Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Tabora, Singida, Kigoma, Katavi, Dodoma, Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Iringa.

“SIRRO CUP KIBITI ” KUFUNGULIWA JUMATATU

$
0
0


Na. Jeshi la Polisi.

Michezo ya kuwania kombe la Sirro Kibiti mwaka 2018 inatarajiwa kuzinduliwa jumatatu Mei 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro katika uwanja wa Samora Wilayani Kibiti.

Akizungumza wilayani Kibiti baada ya kukagua maandalizi hayo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema uzinduzi huo utahudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Pwani.

Mwakalukwa amesema lengo la michezo hiyo ni kuwaweka pamoja na kudumisha usalama kwa wakazi wa Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji baada ya matatizo yaliyowakumba kumalizika.

Ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia burudani mbalimbali pamoja na maneno ya viongozi mbalimbali yatakayotolewa katika ufunguzi wa michezo hiyo ambapo ratiba itaanza saa saa nne asubuhi.

Kwa upande wake Mratibu wa Kombe hilo, Koplo Ramadhan Tamimu amesema michezo hiyo itakapofikia tamati bingwa atajinyakulia kombe na fedha taslimu Milioni moja huku yakichagizwa na kauli mbiu ya “Kibiti Salama, Jamii Salama”

Naye Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibiti Rashid Mkinga amesema wamejiandaa vyema na anauhakika wa kombe hilo kubaki wilayani Kibiti kwa kuwa pamoja na kuwa na timu bora lakini pia wanatarajia kupata mashabiki wengi.

Ufunguzi huo utapambwa na burudani mbalimbali zikiongozwa na Bendi ya dansi ya Jeshi la Polisi, Msanii wa nyimbo za asili Ndolela, Man Prince na vikundi mbalimbali kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA KUANZA MITIHANI KIDATO CHA SITA,UALIMU

$
0
0

*Watakaofanya udanganyifu wa aina yoyote kukiona cha moto

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BARAZA la Mitihani la Tanzania(Necta) limetoa onyo kali kwa wamiliki wa shule,walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mitihani ya Kidato cha Sita na Kozi za ualimu inayoanza kesho Mei 7 hadi Mei 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa baraza hilo  ni kwamba jumla ya watahiniwa 87,643 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 77,222 na watahiniwa wa kujitegemea ni 10,421.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde ametangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.Akisisitiza Dk.Msonde amesema baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua yeyote atakayejihusisha kufanya udanganyifu katika mihitani kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi.

Amefafanua ikiwa panoja na kuwafutia matokeo yote watahiniwa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu."Wadadau wore wanaombwa kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini uwepo wa mtu au kikundi cha watu kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile," amesema Dk.Msonde.Pia amesema baraza linatoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa amani na utulivu .

"Wananchi wanaombwa kuheshimu eneo la mitihani na kuhakikisha asiyehusika  haingii maeneo ya shule,"amesema Dk.Msonde.Ameongeza wamiliki wa shule na vyuo wanatakiwa kutambua shule na vituo vya maalum vya mitihani  na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingiliwa majukumu ya usimamizi wa mitihani kwa kipindi chote hicho.

" Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake ubahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa,"amesema Dk.Msonde.Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taiga zinazingatiwa ipasavyo.

Kwa upande wa wawatahiniwa ,amesema baraza linaamini walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha elimu ya sekondari na kozi za mafunzo ya ualimu.Hivyo matarajio yao watahiniwa watafanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshwe uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi walioupata kipindi cha mafunzo yao.
 Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo alipokuwa akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA DAWA CHA M-PHARMACEUTICALS WILAYANI BAGAMOYO

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wapili kulia), akishirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu kulia) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wanne kulia) na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi (watano kulia) kuzindua uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu  unaoatarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za ukuzaji sekta ya viwanda nchini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kulia), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wapili kulia) ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo(wakwanza  kulia), Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi(wanne kulia) na viongozi wengine wakimsikiliza Mtaalamu wa michoro,Ruchir Sharma akielezea na kuonyesha ramani ya kiwanda cha dawa kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo baada ya Waziri Ummy kuweka jiwe la msingi wa ujenzi huo. Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa  za Binadamu kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya afya kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage   akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu  kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya viwanda na uwekezaji  kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi, akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo alishukuru ushirikiano aliopata kutoka serikalini wakati wa mchakato wa uanzishwaji kiwanda hicho .Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
 Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Bagamoyo,Muyengi Machumu,Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza,Malisa Emmanuel na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bagamoyo Adam Maro, wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu Kerege wilayani Bagamoyo.
Wasanii kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa Sherehe za Uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu unaoatajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Picha  na Abubakari Akida

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MABASI CHA KISASA MSAMVU, MOROGORO

$
0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali baada ya kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiapeana mikono na  wadau mbalimbali baada ya kufungua  rasmi  kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  na viongozi na wadau mbalimbali wakipata maelezo ya mradi kabla ya ya kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Abdulazizi Abood wakati wa sherehe za kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Prosper Mbena wakati wa sherehe za kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018 
 Muonekano wa kituo kipya na cha kisasa cha mabasi kilichopo eneo la Msamvu katika manisapaa ya Morogoro kilichofunguliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo Mei 6, 2018

Picha na IKULU
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images