Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Taarifa kuhusu ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mhe. Heiko Maas anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini tarehe 03 na 04 Mei, 2018. 

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano. Waziri huyo atakuja nchini kwa ndege binafsi akiambatana na ujumbe wa watu hamsini (50). 

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri huyo nchini Tanzania na Barani Afrika tangu ateuliwe tarehe 14 Machi, 2018 kwenye wadhifa wa sasa kutoka kwenye wadhifa aliokuwa nao awali wa Waziri wa Sheria. Kwenye ziara yake hii ya awali Barani Afrika, atatembelea nchi mbili tu ambazo ni Tanzania na Ethiopia ambayo ni Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (Afican Union). Hii inadhihirisha dhamira ya Ujerumani na hasa Waziri huyo mpya wa Mambo ya Nje kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Tanzania.

Wakati wa ziara hiyo nchini, Mhe. Maas ataonana kwa mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na baadaye kwa pamoja watakutana na vyombo vya habari kuelezea madhumuni ya ziara ya Waziri huyo nchini.

Aidha, tarehe o4 Mei, 2018, Mhe. Waziri Maas anatarajiwa kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Askari (Askari Monument) Jijini Dar es Salaam pamoja na kutembelea Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chang’ombe. 

Siku hiyo hiyo, Mhe. Maas ataondoka Dar es Salaam kuelekea Arusha. Akiwa Arusha Mhe. Waziri Maas atakutana na viongozi wa Mahakama ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (United Nations Mechanism for International Criminal Tribiunals-MICT) na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (African Court on Human and Peoples’ Rights). Pamoja na kutembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa kunufaika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwenye nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tangu kuanza kwa mahusiano kati ya nchi hizi mbili, Ujerumani imekuwa ikiisadia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, elimu, miundombinu, nishati mbadala, mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili na uwindaji haramu.

Mhe. Maas ataondoka nchini tarehe 04 Mei, 2018 kurejea Ujerumani.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 02 Mei, 2018

UBA Shareholders Hail Performance, Higher Dividend Payout

$
0
0
Shareholders of United Bank for Africa (UBA) Plc on Monday hailed the board and management of the bank for the impressive performance recorded in 2017 and were highly pleased with the remarkable contributions of its African subsidiaries that accounted for over 45 percent of the group’s income.

The shareholders gave the commendation at the 56th annual general meeting in Lagos. UBA posted profit after tax (PAT) of USD237 million for the 2017 financial year and recommended a total dividend of 0.3 USD cents per share, which was ratified at the AGM. Speaking at the meeting, the Chairman, Progressive Shareholders Association of Nigeria, Mr. Boniface Okezie: “I want to specially commend the Board and Management of UBA, especially the Chairman, Tony Elumelu and Group Managing Director/CEO, Kennedy Uzoka, whose leadership, has brought tremendous progress to this great institution in the past two years. 

We, the shareholders, are impressed with results that you have recorded so far and the achievements that the bank has recorded under your leadership, especially the sterling contributions of our subsidiaries in Africa. We are impressed with the continuous penetration of the Group’s franchise and market share gain across Africa. UBA has further demonstrated that Africa can nurture great companies and great things can be originated from Africa. UBA has showcased a high level of ingenuity in the banking space, and we are glad with the attendant value creation for shareholders and the broader stakeholders.”

Another shareholder, Mr. Timothy Adesiyan, commended the Management for being the African bank to pioneer Artificial Intelligence technology, with the launch of UBA’s Virtual Banking Robot, named “Leo”, a Chatbot which enhances lifestyle banking, as it enables customers to carry out all forms of basic banking transaction through Facebook chat. Also, speaking at the General Meeting of Shareholders of the Group, Nonah Awoh, who commended the bank for the performance, equally tasked the management to do more to ensure that all the African subsidiaries contribute at least 50 per cent to the bottom-line of the Group in the near future.

In his address to shareholders, Elumelu, said the bank recorded strong growth in both top and bottom lines in 2017.

He said: “Overall, our bank grew profit before tax by 16.1 per cent to USD318 million. More importantly, the bank remains financially strong, with BASEL II capital adequacy ratio of 20% well ahead of the 15% regulatory requirement in Nigeria and the Group’s capital adequacy ratio of 25% ranks one of the highest amongst Sub-Sahara African banking groups. More importantly, the Group remains very liquid, reinforcing the strength of our balance sheet. We recently opened for business in Mali, as we see the economy of Mali to be very viable, with strong growth prospects for us and other corporates in that market. 

Mali is a strategic fit for our Group and this time and the corporates and SMEs in Mali will benefit from our expertise and banking capacity in varying sectors of the economy, in addition to our value proposition to the retail customers, who can efficiently leverage our digital banking offerings to facilitate their banking transactions with ease. Hence, we see us adding a lot of value to the Malian economy and we expect positive profit contribution to our Group from this new subsidiary, going forward.  

On his part, Uzoka, the Group Managing Director/CEO said: “UBA has built a great brand that is recognised all over the world, and because of this, we have decided to be customer centric. This means our focus is on putting our customers first in all we do by making sure that we do things from the customers’ standpoint.”
Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa(UBA) Plc, Mr. Kennedy Uzoka, Group Chairman, UBA Plc, Mr. Tony Elumelu; Company Secretary, Mr. Bili Odum; and Group Deputy Managing Director, Mr. Victor Osadolor, at the 56th Annual General Meeting of the Bank held in Lagos
 Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa(UBA) Plc, Mr. Kennedy Uzoka; Group Chairman, UBA Plc, Mr. Tony Elumelu; Company Secretary, Mr. Bili Odum; Group Deputy Managing Director, Mr. Victor Osadolor; and Director, Ambassador Adekunle Olumide, at the 56th Annual General Meeting of UBA Plc  held in Lagos on Monday

WANAHABARI KIGOMA WAHIMIZWA KUZINGATIA WELEDI, KUONGEZA UBUNIFU ILI KUCHOCHEA MAENDELEO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WANAHABARI mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuongeza ubunifu katika kazi zao ili kuchochea maendeleo ya mkoa huo.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo amesema uandishi wa habari za matukio umepitwa na wakati kama waandishi wenye taaaluma wanatakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari zenye ubunifu na weledi mkubwa kwa kutafuta undani wa habari wanazo ziandika. 
Aidha amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuwashawishi vijana wadogo kuipenda fani ya uandishi wa habari, kwa kuwatembelea wanafunzi shuleni na kutoa elimu kuhusu fani hiyo ili kuepukana na fani hiyo kuonekana wanaoingia huko ni wale wanaoshindwa kutimiza ndoto zao kwakuwa fani hiyo ni sawa na Fani zingine.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma (KGPC)Adela Madyane amesema chama cha waandishi wa habari kina mpango wa kuwaunganisha waandishi wa habari wote mkoani Kigoma ili kuhakikisha wanakuwa na maadili na kuzingatia misingi ya uandishi wa habari.

Amesema Chama hicho kinaendelea kusimamia misingi na taratibu za kitaaluma zilizowekwa kisheria ilikuondoa migogoro baina ya Wanahabari na wadau wa maendeleo, na wanachama wenye vigezo ili kuepuka waandishi wasio na taaluma .
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma Fadhili Abdallah amesema kama waandishi wa habari watahakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi kuhakikisha wanaripoti habari zenye tija na maendeleo kwa ajili ya kuuinua mkoa wa Kigoma.

Amesema changamoto wanazokutana nazo kama Waandishi wa habari ni pamoja na baadhi ya viongozi na wadau kuzuia baadhi ya taarifa na kuwanyima ushirikiano Waaandishi pindi wanapo hitaji taarifa na kuomba Viongozi wote kutoa ushirikiano kwakuwa Waandishi wa habari wana mchango Mkubwa wa Kuinua maendeleo hasa katika mikoa ambayo bado iko nyuma.
Pica ya pamoja

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

$
0
0
TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba, imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo. 

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao. 

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa. Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine. 

Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi. 

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL Corporation inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko sambamba na kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao zinazotolewa na Shirika letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA. 

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa. Nia yetu ni kuwa sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo hayo. T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania. 

Imetolewa na; 
Ofisi ya Uhusiano, 
TTCL Makao Makuu, 
Dar Es Salaam. 
3 Machi, 2018

TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Wanaume ya Men At Work imeendesha mchakato wa kuchangia damu kwa lengo la kutaka itumike kuwasaidia akina kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi.Pia damu hiyo itawasaidia majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell  Stanslaus amesema leo mkoani hapa wameamua kuchangia damu  kama mchango wa wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jamii kwani wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.Stanslaus amewataka wanaume wote nchini 
kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii .

"Kwa sasa  tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu,"amesema Stanslaus .Ameongeza taasisi hiyo ina kazi ya kuwahasisha wanaume wanawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi  familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.

Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson amesema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu  ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.Kwa upande wa Melayeki  amesema kwake ni mara yake ya kwanza kutoa damu, hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu.
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu
 Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson   wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid(picha na Woinde Shizza,Arusha )

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus  akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.

Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Viongozi Kutoa Chanjo Kuzuia Saratani Ya Mlango wa Kizazi

RAIS DKT MAGUFULI AHANI MSIBA WA MKUU WA MKOA MSTAAFU MAREHEMU MZEE ABBAS KANDORO MJINI IRINGA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa pole kwa wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitambulishwa kwa watoto wa marehemu walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiomba dua pamoja na wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018. Picha na IKULU  

TANZIA:DAKTARI BINGWA WA USINGIZI KWA WATOTO NA WAGONJWA MAHUTUTI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi anasikitika kutangaza kifo cha Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa kilichotokea jana jioni tarehe 02/05/2018.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kusafirishwa kesho tarehe 04/05/2018 kwenda katika kijiji cha Nzihi kilichopo  Iringa vijijini kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 05/05/2018.

Heshima za mwisho zitatolewa kesho tarehe 4/5/2018 katika ukumbi wa kufundishia uliopo chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili kuanzia saa 2 asubuhi hadi  saa 3  na baadaye nyumbani kwa kaka wa Marehemu kuanzia saa 6 mchana.

Kwa namna ya kipekee Prof. Janabi anatoa  pole kwa familia ya Marehemu, Wafanyakazi  wote, ndugu,  jamaa, marafiki  pamoja na wote walioguswa na msiba huu.

Msiba uko nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndugu Lumumba Mhewa mtaa wa Mivumoni Madale.
  
“Bwana Ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”.
  
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
03/05/2018

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA BARABARA NA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAKULA CHA KUKU NA VIFARANGA

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Msenza alipowasili eneo la Ihema kuzindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na kulia kwa Rais ni Mama Janeth Magufuli.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen wenye sherehe za uzinduzi wa barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.  
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen na viongozi wengine wakizindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.  
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na uongozi wa kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa kabla ya kukizindua rasmi leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga alipowasili katika kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa kabla ya kukizindua rasmi leo Alhamisi Mei 3, 2018
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga alipowasili katika kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa kabla ya kukizindua rasmi leo Alhamisi Mei 3, 2018 

Picha na IKULU

Uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali - Mwakyembe

$
0
0
Na Mwandishi wetu.

VYOMBO vya habari nchini vimekumbushwa kwamba uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali, bali kujiangalia  wenyewe na pia vyombo vyao vya habari.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akihutubia hadhira ya waandishi wa habari katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, sherehe zilizofanyika kitaifa katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.

Katika hotuba yake baada ya kusikiliza hoja kadha kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari nchini na hisia kwamba vinaminywa Waziri huyo alisema kwamba ipo haja ya tasnia kujiangalia yenyewe kama inatenda haki na weledi kwa taifa hili.
“Kalamu ya mwanahabari ina nguvu sana, ina nguvu sawa na ya silaha, ikitumiwa vizuri ni mlinzi na ikitumiwa vibaya ni maafa” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema katika mazingira ya sasa ambako kuna walimu wengi kuna baadhi ya watu wanapiga kelele kuhusu kufuatwa kwa sheria wakisema sio demokrasia, huku wakifahamu fika kwamba hata katika nchi zao hicho wanachoimba demokrasia hakipo.Akihutubia kama mgeni rasmi alisema kwamba ingawa dirisha lipo wazi kwa majadiliano, serikali haitarudi nyuma kutokana na haja mahsusi ya udhibiti wa yanayoendelea katika mitandao kwa manufaa ya taifa hili leo na kesho.

 “Kuhusu Kanuni za Maudhui Mtandaoni, hili tunaweza kukaa na kujadili lakini kama Serikali hatutarudi nyuma katika hili. “Kupitia mtandao, bila kuweka udhibiti kuna mambo mengi yanapita ambayo hatuwezi kukubaliana nayo”  alisema Dk Mwakyembe.

Akiwasilisha salamu za Jukwaa la wahariri nchini TEF, Kaimu Mwenyekiti Deodatus Balile alisema kwamba ipo haja ya kuendesha mdahalo wa kitaifa kuhusu mustakabali wa uhuru wa habari nchini Tanzania ambao hatima yake ni amani na maridhiano.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison  Mwakyembe akizungumza kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Audrey Azoulay wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart akitoa salamu za Umoja huo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Musokwa akitoa salamu za TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akitoa salamu za taasisi hiyo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
  Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa  salamu za Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akitoa salamu za UTPC wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika  Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akimkabidhi Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe nakala ya ripoti inayohusu uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa Kujitegemea, Rose Haji Mwalimu wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mkuu wa wilaya ya Kongwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deogratius Ndejembi akizungumza na washiriki wakati akifunga kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakongwe (Veterans) mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika  Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

KAMPUNI YA GOAN CABLE CO.LTD YA KOREA KUSINI KUJENGA KIWANDA CHA NYAYA NCHINI

$
0
0
*Rais wa kampuni hiyo atua nchini, afanya mazungumzo ya kina na TIC

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC)kimefanya mazungumzo ya kina na Kampuni ya Goan Cable Co.LTD ambayo inataka kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza nyaya nchini.

Mazungumzo kati ya TIC yamefanyika Mei 2 mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ujumbe wa watu wanne wanaokiongozwa na Rais wa Kampuni Jael In Yoon kufika nchini na kujadiliana na kituo hicho katika masuala ya uwekezaji katika eneo hilo. 

Taarifa ya TIC kwa vyombo vya habari ambayo imetolewa leo jijini Dar es Salaam imesema Kampuni ya Gaon Cable Co. Ltd ni kongwe na imebobea katika utengenezaji wa nyaya za umeme mkubwa na wa kati huko Korea ya Kusini. 

Na kwamba kampuni hiyo pia imehusika katika kutengeneza miundombinu ya kusambaza umeme Korea ya Kusini kwa zaidi ya miaka 60.TIC imefafanua ujio wa wafanyabiashara hao umefanyika kutokana na kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Korea Kusini lililoandaliwa na kituo hicho kwa kushirikiana na na Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

"Kongamano hilo la kibaishara kati ya Tanzania na Korea Kusini lilifanyika Januari 31 mwaka huu katika mji wa Seoul,"imeeleza.Imefafanuliwa lengo la ziara ya ujumbe wa kampuni hiyo ni kuangalia fursa za uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya nishati hasa kufungua kiwanda cha kutengeneza nyaya nchini.

Pia ujumbe huo umekuja nchini ili kuonana na taasisi husika katika sekta ya nishati ili kufanya mazungumzo na kupata miongozo ya kuanzisha kiwanda hicho."TIC imefanya mkutano na wafanyabiashara hao na kuwapa taarifa zote muhimu.Pia kuwahakikishia utayari wa kuwasidia katika hatua zote za uanzishaji mradi huo.

"Ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja. Huduma hizo ni pamoja na usaidizi wa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji, kuandikisha Kampuni, kujisajili na VAT, TIN, Kupata Leseni ya biashara na vivutio vya uwekezaji.

"Pia kibali cha kazi daraja A na C, hati za ukazi daraja A na B, kusajiliwa kwa ajili ya kupata viwango vya ubora (TBS),cheti cha uwezekaji, kutathmini masuala yahusuyo mazingira (NEMC), kusaidiwa kupata vibali vya usalama mahala pa kazi (OSHA) na Kusaidiwa upatikanaji wa vibali kwa uwekezaji unaohusisha chakula na dawa (TFDA),"imesema TIC katika taarifa yake.

Wakiwa nchini, wageni hao pia walifanya mikutano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka yaUkanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa majadiliano na miongozo zaidi ya kuwekeza katika sekta ya umeme pamoja na kupata eneo la kuweka mradi huo. 

TIC imesisitiza uanzishwaji wa kiwanda hicho nchini utakuwa na mchango mkubwa si tu katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kupunguza uagizaji wa nyaya bali pia kuimarisha njia za usambazaji wa umeme nchini pamoja na nchi jirani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe (kushoto) akiwa  na Rais wa Kampuni ya Gaon Cable Jael Yoon baada ya kufanya mazungumzo kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dar es Salaam.

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO SASA NI T PESA

$
0
0
TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba, imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo. 

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao. 

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa. Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine. 

Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi. 

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL Corporation inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko sambamba na kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao zinazotolewa na Shirika letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA. 

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa. Nia yetu ni kuwa sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo hayo. T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania. 

Imetolewa na; 
Ofisi ya Uhusiano, 
TTCL Makao Makuu, 
Dar Es Salaam. 
3 Machi, 2018
Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), imebadili nembo na jina la iliyokuwa TTCL Pesa na sasa kujulikana kama T Pesa baada ya Uzinduzi uliofanyika jijini Dodoma leo. (Picha:Mroki Mroki-Daily News Digital)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION), Waziri Kindamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo ya na jina lipya la TTCL Pesa.
Meza Kuu ikifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo.
Meza Kuu ikifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL Corp, Omar Nundu akizungumza.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilaino (Sekta ya Mawasiliano), Atashasta Nditiye akizungumza wakati wa usimduzi huo. 
Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akitoa neno wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imemchagua, Naghenjwa Kaboyoka(Picha:Mroki Mroki-Daily News Digital)
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilaino (Sekta ya Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa amezindua Nembo mpya ya T Pesa.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilaino (Sekta ya Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa amezindua Nembo mpya ya T Pesa.


picha mbalimbali za pamoja zikipigwa kwa makundi mbalimbali tofauti(Picha:Mroki Mroki-Daily News Digital)
Wananchi wakijisajili na huduma ya T Pesa.

MCHUNGAJI MSIGWA AVUNJA MWIKO, AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO BILA UPENDELEO,KUJALI VYAMA

$
0
0


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MBUNGE wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)MchungaMchungaji Peter Msigwa ameamua kutema nyongo na kuweka wazi namna ambavyo anafurahishwa na utendaji kazi wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli.

Mchungaji Msigwa amevunja ukimya na kuamua kumsifu Rais jana akiwa mkoani Iringa ambapo alipata nafasi ya kualikwa kwenye chakula kilichoandaliwa na Rais kwa wazee wa Mkoa huo ambapo mbunge huyo alikuwa miongoni mwa walioalikwa na waliopata nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais.

Akizungumza jana mkoani Iringa Mchungaji Msigwa amesema Rais Dk.Magufuli amekuwa akisisitiza kwenye hotuba zake kuwa yeye hajali mambo ya vyama na hilo limedhihirika kuwa ni kweli hajali vyama.

"Umesaidia sana , fedha za kutoka kwako zimekuja nyingi, kama alivyosema Waziri Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Sh.bilioni 3.5.

"Tuna stendi nzuri ipo Ipogoro ya karibu Sh.bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli mheshimiwa Rais hupendelei.Fedha zinakuja hata sisi ambao ni wa Chadema unaleta fedha, kwa hiyo tunakupongeza sana kutokana na juhudi zako za kuleta maendeleo ,"amesema Mchungaji Msigwa.

Wakati anazungumza hayo kulikuwa kimya huku baadhi ya wageni waalikwa kwenye chakula hicho wakifurahia kwa chini chini.Hata hivyo baadhi ya wadau wa siasa nchini wamesema kilichofanywa na mbunge huyo ni katika kuthibitisha kutoka kwenye moyo wake kuwa kuna mambo mengi mazuri ambayo Rais anafanya bila upendeleo.

Hata hivyo ni wazi Mchungaji Msigwa sasa anaingia kwenye orodha ya wabunge ambao wamefurashwa na utendaji kazi wa Rais .Historia ya Mchungaji inaonesha hajawahi kusifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano lakini hatimaye amekubali kuwa kazi inafanyika kwa maendeleo ya Watanzania wote.

TAARIFA KWA UMMA

RC GAMBO: WAAJIRI ACHENI KUWATISHA WAFANYAKAZI

$
0
0
Na. Vero, Ignatus, Arusha

Mkuu wa mkoa mrisho Gambo amewataka waajiri kupokea changamoto za wafanyakazi na kuzitatua sambamba na wafanyakazi kuwa huru kusema   changamoto wanazokumbana nazo.

Gambo  amekemea kitendo cha baadhi ya waajiri wanaowatisha wafanyakazi,amesema kuwa jambo hilo halikubaliki ,atakapobainihatua stahiki zitachukuliwa."Nimepata taarifa kuna maeneo ambayo wafanyakazi waliweza kutoa kero zao na maoni yao na baadhi ya waajiri waliwatisha ,jambo hilo halikubaliki na atakapobainika sheria stahiki zitachukuliwa dhidi yake" alisema Gambo
Ameyazungumza hayo katika sherehe za mei mosi Jijiji Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi  na kutilia mkazo kuwa yapo malalamiko ya watumishi wa serikali kukamatwa na kuwekwa ndani kwa makosa ambayo ni ya kiutumishi,amewataka viongozi kufanya kazi kwa weledi,kwakuzingatia sheria na taratibu. "Kama mfanyakazi amefanya kosa la kiuhalifu,ashughulikiwe kama mhalifu,bali kama kosa ni la kiutumishi,zipo sheria na kanuni za kitumishi ni vyema zikazingatiwa" 

Amesema wafanyakazi wanatakiwa kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwani viongozi pekee wa mkoa hawawezi kusukuma gurudumu la maendeleo bila ya kushirikuana na wafanyakazi ambao ni wadau muhimu katika nchi.

Akijibu risala ya wafanyakazi Jijini Arusha iliyosomwa na Katibu wa Tughe  Samweli Magero amesema kuwa changamoto ya uhaba wa majaji tayari mhe.Rais alifanya uteuzi wa majaji kadhaa ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kwenda kuziba mapengo yaliyokuwepo.

Mwisho aliwapongeza wananchi kwa ujumla pamoja na wafanyakazi kuwa wameweza kuonyesha uzalendo kwa mkoa kwani Arusha imebadilika kwa kuithamini amani kuliko chochote
Wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambae ni mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi ,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,,Katibu tawala wa Jiji la Arusha Charles Kwitega na Karibu wa Tughe Jijini hapo Samweli Magero.Picha Vero Ignatus Boog.
Meza kuu wakiwa wanafurahia jambo wakati wakati Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanjani .
Baadhi ya wafanyakazi kutoka kiwanda cha A-Z wakiwa wanapita mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za meimosi katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.
Pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha Jijini Arusha katika uwanja wa  Shekh Amri Abaid bado wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali waliendelea kusalia uwanjani bila kuondoka katika sherehe za Mei Mosi mkani hapo. Picha na Vero Ignatus Blog. 
Fedy Sanga( kulia)akikabidhiwa cheti na Hundi ya Sh, milioni 1 baada ya kuteuliwa kuwa mfanyakazi bora Kwa wafanyakazi wa Jiji la Arusha. Picha na Vero Ignatus Blog.

MAHAKAMA KUU YAZUIA MATUMIZI YA KANUNI ZA MTANDAO (ONLINE CONTENT REGULATION 2018) KWA MUDA

$
0
0
 Hakama Kuu Kanda ya Mtwara leo imetoa  zuio la muda ( temporary injuction) linalozuia matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018.

Mahakama imetoa zuio hilo baada ya taasisi sita kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzia matumizi ya Kanuni hizo April 30, mwaka huu.

Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Legal and Human Rights Cente (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Media Council of Tanzania (MCT), Jamii Media, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Tanzania Editors Forum (TEF).

Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (judicial review) zimewashitaki  Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba:-

i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake ( Ultra vires)

ii) Zinakiuka kanuni za usawa (natural justice)

iii) Kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza ( Freedom of exepression) haki ya kusikilizwa( rights to be heard) , na haki ya usiri ( Privacy rights)

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 may 2018.

CALL TO PARTICIPATE IN THE FIRST NATIONAL SKILLS DEVELOPMENT WORKSHOP AT JNICC DAR ES SALAAM 10th MAY 2018

WAZIRI MWIJAGE AKABIDHI TUZO ZA RAIS ZA VIWANDANI (PMAYA)

$
0
0
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,  akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa pili wawakilishi wa Kampuni ya PLASCO Ltd, kutoka (kushoto) Unguu Sulay, Edith James na Alimiya Osman, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania, James Alva, wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya utoaji Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa jumla Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Group, Roberto Jarrin, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika Makampuni matatu makubwa (TOP 3) Meneja wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Helene Weesie, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo Meneja Rasilimali watu  wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Daphne Kakonge, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais za Viwandani. 
Afisa Masoko wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmasy, akipokea cheti cha shukrani wakati wa hafla hiyo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wa udhamini mwakilishi wa Kampuni ya IPP, Paul Urio, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Cheti cha kutambua mchango wa udhamini Mwenyekiti wa Kampuni ya Montage, Nestory Mapunda, wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Na Muhidin Sufiani, Dar
WAZIRI wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa azma ya kukua kwa uchumi unategemea sekta ya viwanda na hakuna budi kuhakikisha wanatimiza vigezo vya uchumi ili ukue kwa asilimia 12 kwa mwaka, pato la taifa lisipungue chini ya asilimia 15 na ajira kuongeza kwa asilimia 40 ya ajira zote.
Mwijage amesema hayo wakati wautoaji tuzo za Rais za Viwandani (PMAYA) kwa mwaka 2017 zilizofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuwataka Shirikisho la Viwanda (CTI) kuwa wabunifu na kuzitangaza bidhaa zao ili kuweza kuingiza mapato ya asilimia 25 ya fedha za kigeni.
Akizungumza wakati wa utoaji tuzo hizo, Mwijage amesema kuwa serikali ya awamu ya tano toka iingie madarakani imeweza kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
"Mpaka sasa toka Desemba 2015 tayari tumewahamasisha wawekezaji wa ndani na wa kujenga viwanda vipya 3,306 na tunawapongeza wawekezaji wa ndani nannje kwa kuchagua kuwekeza Tanzania na kuunga mkono serikali yetu ya kukuza uchumi wa viwanda kufikia 2025, " amesema Mwijage.
" Natambua kuwa baadhi yenu mna madai mbalimbali ya kurejeshewa malipo yenu yakiwemo ya ushuru wa forodha ya 15% ya ziafa kwenye uaguzaji wa sukari kwa ajili ya matumizi ya viwanda na malipo ya marejesho ya ongezeko la thamani," 
Mwijage amesema zipo changamoto zinazotokana na wenye viwanda wenyewe ikiwemo udhaifu wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ya Tanzania unasababisha bidhaa za ndani kutokufahamika vizuti miongoni mwa watanzania na watuamiaji wa nje.
Mwijage amesema kupitia baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) itahakikisha watanzania wote wanashiriki katika ujenzi wa uchumi. Serikali kupitia baraza la uwezeshaji lina miradi ya kimkakati ya kusaidia viwanda vyetu na watanzania kwa ujumla kupata fursa mbalimbali zilizopo. 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CTI Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru serikali kwa kuweka mijadala ya kuwasaidia watanzania wafanyabiashara hasa wenye viwanda  na baada ya serikali ya awamu ya tano kuja na sera ya ujenzi wa viwanda watanzania wengi wamejitokeza kuanzisha viwanda mbalimbali kwa azma ya kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.
Aidha ameeleza kuwa katika maadhimisho ya miaka 13 katika utoaji wa tuzo mwaka 2016 mheshimiwa Rais alipendekeza kuhusisha sekta zote na wasio wanachama  wahusishwe na tuzo ya matumizi bora nishati viwandani ilianzishwa.
Mashindano hayo yataleta ushindani mkubwa katika sekta ya viwanda hali itakayopelekea kukuwa kwa uchumi  na kuongeza pato la taifa.
Katika tuzo za mwaka 2017  kampuni ya bia ya Tanzania Breweries (TBL)  iliweza kupata ushindi wa jumla katika viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa mbalimbali wakifuatiwa na Zenufa na mshindi wa tatu ni Plasco  Ltd

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA




 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo, CEO wa Kampuni ya Jambo Plastics Ltd, Rupa Suchack.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi cheti Mshirika wa Taasisi ya Kaizen Tanzania, James Alva na msidizi wake Beatrice Kithinji, wakati wa hafla hiyo.
 Wasnii wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre wakitoa burudani

WAZIRI MAHIGA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI WAKUTANA KWA MAZUNGUMZO RASMI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa ameongozana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kufanya mazungumzo rasmi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani. Mhe. Waziri Maas yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 03 hadi 04 Mei, 2018 
Mhe. Waziri Mahiga akimkaribisha rasmi nchini Mhe. Waziri Maas 
Mhe. Waziri Maas akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili JNICC huku Waziri Mahiga akishuhudia 
Mhe. Waziri Mahiga akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Ujerumani. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Zanzibar, Mhe. Issa Haji Gavu, kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas akiongoza ujumbe wa Ujerumani kwenye mazungumzo kati ya nchi hiyo na Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Detlef Waechter 
Mazunguzmo rasmi kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Maas yakiendelea 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Heiko Maas wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akitoa utaratibu kuhusu mkutano kati ya Mawaziri hao na Waandishi wa Habari (Joint Press Conference) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) kuhusu madhumuni ya ziara ya Waziri Maas nchini 
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Waziri Maas wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yao ambayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo pamoja na kuboresha maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na uwekezaji, biashara, kupambana na rushwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya na usafirishaji binadamu pamoja na kupambana na ujangili wa wanyamapori. 
Sehemu ya Waandishi wa Habari na Viongozi kutoka Serikalini wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Maas ambao hawapo pichani. 
Mhe. Waziri Maas pia alipata fursa ya kutembelea Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chnag'ombe ambayo ni miongoni mwa shule chache nchini zinazofundisha Lugha ya Kijerumani. Pichani akiwa na wanafunzi wanaojifunza lugha hiyo shuleni hapo 
Mmoja wa wanafunzi shuleni hapo akimzawadia Mhe. Maas picha ya kuchora ya Hifandhi ya Mlima Kilimanjaro 
Mhe. Maas akiwa na mmoja wa walimu (mwenye kitambulisho) wanaofundisha Lugha ya Kijerumani katika Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chang'ombe

JWTZ WAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NA NMB KWA AJILI YA MASHINDANO YA MKUU WA MAJESHII

$
0
0
Mlezi wa timu za Jeshi, Luten Kanal, David Mziray akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa NMB, Mahususi kwa wateja, Gibson  Mlaseko kwa ajili ya michezo ya Mkuu wa Majeshi itakayofanyika jijini Dar es Salaam

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENK ya NMB imetoa vifaa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 10 kwa timu za Majeshi ambazo zinajiandaa na mashindano ya Majeshi yanayotarajia kuanza Mei 8 hadi 20, mwaka huu kwenye viwanja vya Uhuru na Twalipo Jijini Dar es Salaam.
Michezo mbali mbali ikiwemo soka,netiboll, riadha, ngumi, kulenga shaba na mpira wa mikono inatarajiwa kuwepo na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.

Akizungumza kwenye Hafla ya kukabidhia vifaa hivyo Makao Makuu ya Meneja Mwandamizi na Mahusiano kwa Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko alisema kuwa sababu ya kutoa msaada huo ni kutokana na mahusiano mazuri waliyokuwa nayo na JWTZ, katika mambo ya michezo.
“Nashukuru kwa mahusiano mazuri kati yet una JWTZ kwani hii ni mara ya tatu tunasaidiana nao katika maswala mbalimbali ya michezo, pia lengo la msaada huu ni kutambua umuhimu wa michezo kuwa ni kuibua vipaji kujenga Afya na ajira hivyo tunamani wenzetu watavitumia vifaa hivi vizuri na kufikia malengo,” alisema Mlaseko.

Kwaupande wake Luteni Kanali David Mziray, aliishukuru NMB, kwa msaada huo na kusema watahakikisha wanavitumia vizuri ili kutimiza malengo ambayo wamejiwekea katika mashindano hayo.
“Tunawashukuru NMB kwa msaada huu vifaa hivi vitaongeza chachu ya mashindano yetu ambayo hufanyika kila mwaka tunaomba na makampuni mengine yaige mfano wao ili kuinua michezo nchini,” alisema Mziray.

Vifaa vilivyo tolewa ni pamoja na mipira ya michezo yote, Jezi za michezo yote michezo mingine ambayo itashindaniwa katika michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Mlezi wa timu za Jeshi, Luten Kanal, David Mziray akipokea vifaa vua michezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa NMB, Mahususi kwa wateja, Gibson  Mlaseko kwa ajili ya michezo ya Mkuu wa Majeshi itakayofanyika jijini Dar es Salaam

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images