Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Waziri Ummy amjulia hali Mzee Majuto Muhimbili

$
0
0
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza jambo na Mchekeshaji mkongwe almaarufu kwa jina la Mzee Majuto mapema jana,alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,anakopatiwa matibabu


COCA-COLA BONITE YAZIDI KUWANEEMESHA MAELFU KWA ZAWADI ZA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA NA COKA'

$
0
0
Washindi wa wiki ya nne katika picha ya pamoja
Washindi wa pikipiki wakifurahi baada ya kukabidhiwazawadi zao.
Baadhi ya washindi wakisubiri kupokea zawadi katika hafla hiyo. Wakati promosheni ya mzuka wa Soka na Coka imeingia katika wiki ya 4 tangu izinduliwe ,zaidi ya wakazi 32 wa mikoa ya, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida wamejishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa za pikipiki,Luninga bapa za kisasa na fedha taslimu shilingi 100,000/- 

 Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kubwa kwa washindi wa wiki ya nne,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Bonite Bottlers, Chris Loiruk,alisema kumekuwa na ongezeko la washindi katika wiki ya nne tangu kuanza kwa promosheni hiyo,na kampuni inayo furaha kuona wateja wake wanaendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali. 

 “Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5,000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”,Alisema Loiruk. Washindi wapatao 18 ambao walikabidhiwa zawadi zao za Pikipiki,Luninga na Fedha taslimu katika hafla hiyo iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite mwishoni mwa wiki waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kiuchumi. 

Akiongea kwa niaba ya washindi waliokabidhiwa luninga, Denis Stanslaus mkazi wa Rau Madukani, Manispaa ya Moshi,alisema wamefurahi kupata zawadi za luninga za kisasa hususani katika kipindi hiki kuelekea mashindano ya kombe la dunia kwa kuwa wataburudika na mashindano hayo na familia zao na kupata habari kupitia luninga bapa za kisasa. 

Akiongea kwa niaba ya washindi wa pikipiki, Jackline Emmanuel, mkazi wa Kijenge Juu Mkoa wa Arusha ,alisema kuwa wanayo furaha kubwa kwa zawadi waliyojishindia na chombo hicho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha usafiri sambamba na matumizi ya biashara kwa ajili ya kuongeza pato la familia. Kwa upande wake, Elinaisha Nasari , Mkazi wa Tengeru Mkoa wa Arusha , akiongea kwa niaba ya washindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-alisema kuwa fedha walizojishindia zitawawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiwakabili sambamba na kuongeza mitaji yao ya biashara.

MADIWANI WATATU WA CHADEMA MONDULI WAACHIA NGAZI,WAJIUNGA CCM

$
0
0
 
Madiwani watatu wa CHADEMA wilayani Monduli wamejiuzuru nafasi zao na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM) mapema jana tarehe 29.04.2018 Madiwani hao kuanzia pichani kulia ni Bariki Sumuni Libilibi wa kata ya Monduli Juu,Einoti N. Leringa wa viti maalum kata ya Monduli Juu pamoja na Dominic Mawalla Kadogoo diwani wa kata ya Migungani.Wote kwa pamoja walikabidhi barua za kujiuzulu kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli
  Einoti N. Leringa wa viti maalum kata ya Monduli Juu akikabidhi barua yake ya kujiuzuru kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli
Benedict Mawalla kata ya Migungani akikabidhi barua yake ya kujiuzuru kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI KWENYE UZINDUZI WA BARABARA DODOMA-BABATII

JE WAJUA ATHARI ZA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO

$
0
0
Watu wengi huchukuliaTatizo la Maumivu ya Mgongo kama jambo la kawaida na hawafahamu kuwa linaweza kupelekea matatizo makubwa katika mwili.

Tatizo la mgongo likiachwa kwa muda mrefu linaweza kupelekea:

1.Ulemavu: Mtu anakuwa hana tena uwezo wa kusimama sawasawa na hivyo akitembea huelemea mbele. Hali hii humpa changamoto katika kuziendea shughuli za kila siku.

2.Kuwa tegemezi: Kwa watu wazima tatizo la mgongo la muda mrefu linawea kupelekea kushindwa kutembea mwenyewe hadi atumie fimbo. Hivyo mtu huwa tegemezi kwa fimbo katika kutembea kwake.

3.Kukosa usingizi. Kutokana na maumivu makali ya mgongo.

4.Ganzi ya mgongo na kusababisha matatizo ya mfumo wa fahamu.Maumivu ya mgongo pia hupelekea ganzi na kupoteza uwezo wa kuhisi vichocheo (joto,baridi, mguso) kwani katika pingili za mgongo katikati hupita neva za fahamu ambazo zinatoa mawasiliano kati ubongo na viungo vya mwili.

5. Inapunguza ufanisi katika tendo la ndoa: Utafiti uliofanywa na SpineUniversemwaka 2008 ulibaini kwamba Maumivu makali ya mgongo hupelekea Ufanisi mdogo wa kushiriki tendo la ndoa, kutoridhika katika tendo la ndoa, na ugumu katika mahusiano.

6. Maumivu makali ya mgongo yanaweza kupelekea msongo wa mawazo ambao pia hupelekea matatizo katika mahusiano na kushindwa kushiriki katika shughi za kiuchumi.

Happiness Massage ndio suluhisho pekee la maumivu makali ya mgongo

Tembelea ofisi zetu zilizopo Lamada Hotel, Ilala, Apartment no. 27.

Fanya Booking sasa kwa 
SMS +255 787 343 161

Tupigie simu
+255 715 343 161
+255 756 343 161

KWA MAELEZO ZAIDI NA KUJIFUNZA BOFYA HAPA

MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , FRANK LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI YA AKINA AVEVA YA UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Sports Club, Zacharias Hans Pope na Mkandarasi wa uwanja wa club hiyo, Frank Peter Lauwo waka matwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu.
 
Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa mahakama hiyo baada ya Swai kudai amewatafuta washtakiwa hao toka Machi mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani

Kutokana na mabadiliko hayo washtakiwa wamesomewa upya hati ya mashtaka na wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 10 tofauti na hati ya mashtaka ya zamani iliyokuwa na mashtaka matano.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania(Takukuru) Leornad Swai ameda kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali lakini ameomba kufanyia madaliko hati ya mashtaka.Katika mashtaka hayo washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria.

Akisoma mashataka hayo, Swai amedai, kwenye shtaka la kwanza, Aveva na Nyange, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka vibaya, pia wanadaiwa kati ya Machi 10 na 16 jijini Dar es Salaam, walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa fomu ya maombi ya Machi 15/2016 na kuhamisha dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyopo CRDB tawi la Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Barclays kwa madhumuni ya kujipatia faida.

Katika tarehe hizo hizo wakiwa Dar es Salaam kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionyesha simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.

Aidha wote kwa pamoja waliwasilisha nyaraka ya kughushi, inadaiwa kuwa Aveva Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya CRDB aliwasilisha nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa dola 300,000.Katika shtaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, imedaiwa Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola 187,817 wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Pia katika shitaka la sita la imedaiwa Nyange alimsaidia Aveva kujipapatia dola 187,817 kotoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushiKatika na shtaka la saba la kughushi, linaloqakabili mstakiwa wa Aveva, Nyange na Poppe.

Imedaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pomoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28/ 2016 wakionesha nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya USD 40,577 huku wakijua kwamba sio kweli.Katika shtaka la nane imedaiwa, , Aveva aliwasilisha hati ya madai (commercial invoice), ya uongo kwa Levison Kasulwa ya Mei 28/ 2016 kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola 40,577

Katika Shtaka la tisa Aveva, Nyange na Zacharia Machi 10 mwaka 2016 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577.Katika shtaka la mwisho imedaiwa, kati ya Machi na Septemba 2016 Lauwo aliendesha biashara kama mkandarasi kwa kujenga uwanja wa Simba uliopo Bunju jijini Dar es Salaam wakati akiwa hajasajiliwa

Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka hayo yote na wamepelekwa rumande kwa sababu shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili halina dhamana.Kesi hiyo imahirishwa hadi Mei,14 mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia kama washtakiwa hao wawili watakuwa wamekamatwa.

TCCIA KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WAZINDUA TYM

$
0
0

Naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Dar es salaam, Pro. Cuthbert Kimambo akiongea na TYM wakati wa kusain makubaliano na TCCIA.

Katika kuhakikisha Taifa letu la Tanzania linakuwa imara kiuchumi na kuwa na nguvu kazi kubwa ya Taifa, Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture ‘TCCIA’ imeingia makubaliano maalumu pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo TCCIA imetiliana saini katika makubaliano hayo ‘Memorundum of Understanding’ .

Makubaliano haya yanatoa nafasi kubwa kwa vijana kupitia TCCIA Youth Members, kitengo maalumu kwa vijana hasa waliopo vyuoni kuweza kutumia rasilmali zilizopo TCCIA kuweza kujijenga zaidi katika kazi zao pindi wanapokuwa bado wapo shule na hata baada ya kumaliza shule.

Akizungumza na TYM Makamu wa Rais wa TCCI Bw. Octavian Mshiu alisema TCCIA imeingia makubaliano haya na chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuhakikisha inatoa fursa kwa vijana wengi kuweza kupata nafasi za kuonesha kazi zao, kupata nafasi ya kuwa na watu ambao watawawezesha kuweza kutimiza ndoto zao ‘Mentorship’, kutoa nafasi ya wenye makampuni na biashara kuwatumia vijana wa ndani ambao sio tu ni wabunifu bali pia wenye uthubutu wa kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yetu, katika kuongeezea hilo prof. Cuthbert Kimambo lisema, makubaliano haya hayataishia tu kwa chuo cha UDSM bali wataendelea na kwenye vyuo vyote nchini
Makamu WA Rais wa TCCIA Octavian Mshiu, wakibadilishana makubaliano Na naibu makamu Mkuu WA chuo kikuu prof Cuthbert Kimambo baada ya kutia sain kuhusu ushiriki wawezekaji vijana wa Chama hicho TYM.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti UDSM Dr. Amelia Buriyo katika hotuba yake kwenda kwa wanafunzi baada ya uzinduzi huu alionesha kufurahishwa na jambo hili ambapo alitoa shime kwa vijana kuanza kuamka na kuchangamkia fursa hii adhimu kwao kwani sio kwamba itawakutanisha na watu ambao watawafanya ndoto zao katika miradi wanayoibuni kuwa kweli bali pia kuwezesha kupata nyezo za kufanyia kazi hasa upatikanaji wa mikopo.

Moja ya vijana ambao wamefanikiwa kupitia kujiajiri katika sekta ya ubunifu wa mavazi Bw.Jeff Jersey (Speshoz) alikuwepo kwenye halfa hii ambapo pamoja na mambo mengi aliyoyagusia alisisitiza sana kuhusiana na kuongeza thamani kwenye kila kitu ambacho wanakifanya kwani dunia ya sasa ni dunia ya ushindani na ushindani huhitaji sana ubunifu na kuongeza thamni katika kila kitu ambacho tunakifanya. Bw. Speshoz ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Speshoz aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita.
Jeff Jersey "Speshoz" akizungumza na TYM wakati wa kusain makubaliano kati ya TCCIA na UDSM.TCCIA Youth Members ‘TYM’ sasa imefunguliwa rasmi ambapo kila kijana anaweza kwenda kujisajili bila malipo yoyote.

DK. KIGWANGALLA ATOA OFA YA MAPUMZIKO YA FUNGATE YA ALI KIBA KATIKA HIFADHI ZA WANYAMAPORI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa ofa maalum kwa Mwanamuziki, Ally Kiba, mke wake na wasaidizi wake ambao ni mdogo wake Abdu Kiba na mkewe kupumzika katika Hifadhi ya Taifa atakayoichagua wakati wa fungate yake ili aweze kufurahi vivutio vya utalii vilivyopo na hivyo kuhamasisha utalii wa ndani. Ametoa ofa hiyo jana wakati wa harusi ya msanii huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa sherehe hiyo na Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Mgaya.
 Picha ya pamoja katika sherehe hiyo iliyojumuisha Bwana Harusi, Ali Kiba, mke wake na wapambe wake na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimum, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James.
Picha ya pamoja ya maharusi na viongozi wa chama na Serikali pamoja na Gvana wa Jiji la Mombasa, Rashid Bedzima (wa pili kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na  Wanamuziki, Ommy Dimpoz na Hamisi Mwanjuma MwanaFA.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa sherehe hiyo.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA ULIVYADHIMISHA SIKU YA MUUNGANO

$
0
0

Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akimpokea Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania iliyofanyika jijini New Delhi tarehe 26 Aprili 2018.
Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akiwa katika mazungumzo na Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Luvanda akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanzania

Balozi Luvanda akigongesheana glasi na Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India ikiwa ni ishara ya kuutakia mema Muungano wa Tanzania uweze kudumu milele.
Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India (katikati) akionesha jarida kuhusu miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa rasmi katika hafla hiyo.
Hafla ikiendelea
Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akimkabidhi zawadi ya kinyago Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India.

Picha ya pamoja.

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WILAYANI MUFINDI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Maofisa wa Polisi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi na kuzungumza na Maofisa na askari wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa vyeo mbalimbali wilayani Mufindi mkoani Iringa leo, wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi pamoja na kuona changamoto walizonazo askari wa Jeshi hilo na kuwataka kufanyakazi kwa kuzingatia sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, mhe. Jamhuri William (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo mkoani Iringa leo. Picha na Jeshi la Polisi.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KIWANDA CHA ASASI KILICHOPO MKOANI IRINGA

$
0
0
MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo.
MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Fuad Abri akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza na Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha ASAS wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo katikati ni .MNEC wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiendelea na ziara yake kiwandani hapo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Bw. Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS wakati akitoa maelezo alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo mjini Iringa katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.
Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha Asas akitoa maelezo wa kwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo Mjini Iringa , Ahmed Salim mmoja wa wakurugenzi wa ASAS na Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.
ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi.
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akitembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akionyeshwa moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha ASAS wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo wa pili kutoka kushoto ni MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa na anayefuatia ni Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa ASAS.
MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akizungumza na Spika wa Bunge ofisini kwake wakati Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai alipotembelea kiwanda cha Maziwa cha ASAS leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza jambo huku MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akimsikiliza wakati alipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS mkoani Iringa leo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha ASAS Bw. Fuad Abri wakati akitoa ripoti ya kiwanda hicho wakati alipokitembelea na kukagua uzalishaji.

PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Wananchi wa Kata ya Madege wakikatiza barabara kubwa ya Taragwe iliyojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha; kuelekea kwenye vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwenye Kijiji cha Sanganjelu wilani Gairo.

Wananchi wa kijiji cha Iyogwe wakisikiliza maelekezo ya utaratibu wa kusajiliwa kutoka kwa Msimamizi wa kituo ambaye hayupo pichani.

Ndg. Juma Ally mkazi wa Kata ya Iyogwe Wilaya ya Gairo – Morogoro akipigwa picha na kuchukuliwa alama zake za kibaiolojia wakati zoezi la Usajili likiendelea.

Wananchi wakazi wa kijiji cha Kilama wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakisikiliza kwa makini majina yao yakisomwa kuelekea kwenye chumba cha Usajili ikihusisha hatua ya kupigwa picha, kuweka alama za vidole na saini kileketroniki kwa kutumia mashine maalumu za kukusanya taarifa.
Afisa Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga akizungumza na wananchi wakati wa kukagua maendeleo ya shughuli za Usajili kwenye kijiji cha Ngayaki kata ya Leshata.

………………..



Usajili wa Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro umeendelea kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kusajili pamoja na changamoto kubwa ya mvua ambayo imeharibu miundombinu na kufanya baadhi ya maeneo kutofikika kwa kirahisi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sanganjelu Kata ya Madege wilayani humo Afisa Usajili Wilaya ya Gairo Ndg. Godwill Mwamanga amewahimiza wananchi wanaoshiri zoezi hilo kuwa makini wanapojaza taarifa zao kwa kuhakikisha wanajaza taarifa sahihi naza kweli ili kuepukana na usumbufu hapo baadae.

‘Nawasihi sana muwe wakweli kwenye taarifa zinazohusu umri, makazi na uraia wenu ili taarifa zitakazo kusanywa zikajenge mfumo madhubuti wa Utambuzi wa Taifa wenye taarifa sahihi za watu” alisisitiza

Kwa sasa zoezi la Usajili linaendelea katika Kata ya Madege na Lesha ambapo Kata zingine za Msingisi, Rubeho, Chanjale, Iyogwe, Italagwe na Mkalama zimekamilisha zoezi. Kata za Nongwe, Gairo, Chagongwe, Chakwale, Kibedya, Idibo, Nongwe, Mandege, Chagongwe, Ukwamani, Magoweko na Ngiloli zitaendelea na zoezi kwa kuzingatia ratiba ya usajili iliyotangazwa na Mamlaka.

Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa 21 inayoendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye kulenga kuwapatia wananchi Vitambulisho vya Taifa.

FAO NA USAID TANZANIA WAIPIGA TAFU SERIKALI KUKINGA KICHAA CHA MBWA

$
0
0

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Fred Kafeero (katikati) na Mwakilishi Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Dk. Patrick Swai wkati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo kwa Wilaya ya Moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, ambayo imeripotiwa kuwa na tatizo hilo hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika wizarani hapoleo Aprili 30 2018 jijini Dar es Salaam. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Kiongozi wa Timu wa FAO, Florunso Fesina akitoa mada kuhusu utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa madhara yasababiswayo na mifugo kutopewa chanjo hasa mbwa na paka wakati wa hafla ya shirika hilo kukabidhi msaada wa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa wizara ya Mifugo na uvuvi jjini Dar es Salaam leo.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na kilimo Duniani (FAO) Fred Kafeero (wa tatu kulia) na Mwakilishi shirika la Misaada la Marekani (USAID), Dk. Patrick Swai (wa pili kulia) wakionesha moja ya bango litakalotumika wakati wa tiba na na chanjo katika hafla ya kukabidhi msaada wa chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa tatu kushoto) kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo kwa Wilaya ya Moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, ambayo imeripotiwa kuwa na tatizo hilo hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni watendaji waandamizi wa wizara

Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia mada.

Kiongozi wa Timu wa FAO, Florunso Fesina akitoa mada kuhusu utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa madhara yasababiswayo na mifugo kutopewa chanjo hasa mbwa na paka wakati wa hafla ya shirika hilo kukabidhi msaada wa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa wizara ya Mifugo na Uvuvi jjini Dar es Salaam leo. 

WANANCHI WAHAMASISHWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

SERIKALI mkoani Kigoma imewataka viongozi mbalimbali kuwa mfano katika zoezi la kuhamasisha wananchi kuleta watoto wao wenye umri chini ya miaka 14 kwenye chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Akizungumza jana Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kimkoa iliyofanyika wilayana hapa,alisema njia ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kupata chanjo, kutokufanya ngono katika umri mdogo, kubeba ujauzito katika umri mdogo pamoja na kuwa na wanaume zaidi moja.

"Njia ya pili ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za awali ili kupata matibabu mapema,"alisema .Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mlindoko alisema katika wilaya yake kuna jumla ya watoto 1325 wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14.

Alisema katika wilaya yake inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 4974 na kwamba kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wametoa chanjo kwa watoto hao kwa asilimia 100.

Diwani wa kata ya Kazuramimba Nuru Kashakali, alisema amejitolea kuzunguka katika shule zote za msingi zilizopo kata yake ili kuwahamasisha watoto hao kujitokeza katika zoezi la kupatiwa chanjo.

Nao baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Uvinza Agustina Nzobanya mkazi wa Kazuramimba alisema yeye atahakikisha Watoto wake wote wanapatiwa Chanjo na kuendelea kuhimiza wananchi kuwaleta watoto wao ili kuepuka gharama zinazoweza kujitokezapindi wapatapo Ugonjwa huo.
Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, akizindua chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi mapema jana wilayani humo.
 Brigedia Jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, akizungumza jambo mbele ya wananchi (hawapo pichani),mapema jana wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi

BALOZI MASILINGI AMVALISHA CHEO BRIGEDIA JENERALI AP MUTTA MWAMBATA WA JESHI UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta (hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuvikwa cheo cha Brigedia Jenerali iliyofanyika siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington, DC.Balozi Wilson Masilingi alimwagia sifa kwa kazi nzuri anayofanya kwa nidhamu ya hali ya juu, kujituma kwake na kushirikiana ndio chachu ya mafanikio yake. 

Wambata wengine waliovikwa vyeo vya Brigedia Jenerali ni Brig Gen AS Nwamy- Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brig Gen AM Alphonce Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brig Gen JJ Mwaseba- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Brig Gen RC Ng'umbi- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akitoa hotuba fupi ya kumpongeza Brigedia Jenerali Adolph Mutta kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akiondoa cheo cha Colonel na kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbu wa mkutano a Nyerere hall uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimvua kofia ya cheo cha Colonel na kumvisha kofia ya cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa Nyerere Hall.uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta 
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akipongzwa na mkewe Agnes Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akitoa shukurani kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkuu wa majeshi Tanzania Luteni Jenerali Venance Mabeyo. Katika hotuba yake ya shukurani alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha pale alipo na kushukuru familia yake hasa mke wake. Brigedia Jenerali AP Mutta aliwashukuri Balozi mstaafu Mhe. Liberata Mulamula na Mhe. Balozi Wilson Masilingi wakiwemo Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ushirikiano wanaompa na akaahidi ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi yetu nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi (watatu toka kushoto) na wengine toka kushoto ni EdgarMutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta), Bi. Agnes Mutta (Mke wa Birigedia Jenerali Mutta),Bi Marystela Masilingi (mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi) na kulia ni Judy Mutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta)
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilibgi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilingi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na familia yake kutoka kushoto ni Edgar Mutta, mkewe Bi. Agnes Mutta na kulia ni Judy Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na mkewe Bi. Agnes Mutta.

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Wafanyakazi mbalimbali wakipita kwa maandamano katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Sehemu ya Wafanyakazi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wasanii wa kizazi kipya kutoka mkoani Iringa waliotumbuiza katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Sehemu ya Walimu waliohudhuria katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa wakipiga makofi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiwa na Chifu wa Wahehe, Mtwa Adam Mkwawa II ambaye alihudhuria katika katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiondoka katika uwanja wa CCM wa Samora mkoani Iringa mara baada ya kuhutubia katika shere za Mei Mosi. 

PICHA NA IKULU

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akikata keki ya sherehe ya Muungano na Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail.

Ubalozi wa Tanzania nchini uliadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzania mjini Riyadh kwa sherehe iliyojumuisha jumuiya wa wanadiplomasia, Watanzania na Wanadiaspora waishio nchini Saudi Arabia.
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza(kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail wakati wa sherehe ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
 Baadhi ya Watanzania waishio Saudi Arabia wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
 Picha ya pamoja na madaktari wa hisani wanaotoa huduma za afya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Baadhi ya wake wa Mabalozi wa Afrika waliohudhuria sherehe hizo kutoka kushoto Gabon, Gambia, Eritrea, Burkina Fasso, Tanzania, Cameroon, Ghana na Nigeria.  
Baadhi ya wageni na waalikwa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.

WAAJIRI ACHENI KUWEKA ZAWADI HEWA KWA WAFANYAKAZI WENU RC DODOMA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkta Bilinith Mahenge akizungumza na wafanyakazi katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zinazofanyika duniani kote kila Tarehe 1 ya mwezi wa 5 zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kitaifa mwaka huu zinafanyika mkoani Iringa
Sehemu ya wafanyakazi wa mkoani hapa wakifuatilia Hotuba ya mkuu wa mkoa hayupo piachani) kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi zenye kauli mbiu ya  kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Leo picha na Mahmoud ahmad Dodoma




MKUU wa mkoa Dodoma,Dk.Binilithi Mahenge amepiga marufuku waajiri wote kutoa ahadi hewa kwa wafanyakazi wanaotangazwa kuwa wafanyakazi bora na badala yake wafanyakazi hao wanatakiwa kupewa zawadi zao na vyeti kadri ilivyopangwa na halmashauri husika au mwajiri.
Mkuu huyo wa mkoa alisema imekuwa desturi waajiri wamekuwa wakitafuta sifa ya kutangaza dau kubwa au zawadi kubwa kwa wafanyakazi waliotangazwa kuwa bora lakini kinyume chake wafanyakazi hao wamekuwa wakiambulia vyeti huku pesa hawapewi na linakuwa deni sugu.
Dk.Mahenge alitoa kalipio hilo baada ya wafanyakazi bora wa jiji la Dodoma pamoja na wafanyakazi bora wa Wilaya ya Chemba kupewa vyeti tu huku wakiahidiwa kupewa fedha baadaye badala ya kupewa fedha muda huo huo.
Akizungumza na wafanyakazi wakati wa utoaji wa vyeti, zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiongozi huyo wa mkoa aliagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Godwin Kunambi pamoja na uongozi wa halmashauri ya Chemba kuhakikisha wanawapatia fedha zao wale wote waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na si vinginevyo.
Alisema imekuwa tabia ya halmashauri nyngi kutangaza wafanyakazi bora na kutangaza kuwapatia vyeti na fedha taslimu lakini hawafanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakizurumiwa au kupewa hundi feki jambo ambalo alisema ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi wanaojibidisha kufanya kazi kwa bidii.
“Haiwezekani wewe mkurugenzi au ofisa utumishi mkaatumia vigezo vyote vya kumpata mtumishi bora mkaandaa vyeti,lakini mkashindwa kuandaa fedha ya huyo mtumishi mnakuja hapa mnatoa ahadi jambo hili siwezi kukubaliana nalo sasa naagiza, mkurugenzi wa Jiji huko wapi?, hata kama hayupo naagiza wafanyakazi wote wanaotakiwa kupatiwa fedha zao wapatiwe le oleo (jana) au kesho kabla ya saa tatu (Leo).
“Imekuwa ni utamaduni wakuwadanganya wafanyakazi kwa kuwaandalia vyeti na kuwatajia zawadi ambazo hawapatiwi hili jambo kwa uongozi wa awamu ya tano hauwezi kukubalika lakini pia kwa sasa Dodoma ni makao makuu hatuwezi kufnya mambo ya aina hiyo hilo ni jambo ambalo haliwezi kukubalika kabisa kila mtu apatiwe haki yake.
DODOMA JIJI/MAKAO MAKUU.
Lcha ya mkoa wa Dodoma kupatiwa adhi ya kuwa makao makuu na manispaa kupandishwa adhi na kuwa Jiji lakini imekuwa tofauti katika sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) kwani hapakuwepo na kiongozi yoyote wa kitaifa.
Katika sherehe hizo zilizopambwa na maandamano mbalimbali hapakuwepo na mkurugenzi wa Jiji, Meya wa Jiji wala waziri yoyote au Naubu waziri na hata mbunge yoyote wa jimbo katika mkoa wa Dodoma.
RISALA YA WAFANYAKAZI
Kwa upande wa wafanyakazi wameitaka serikali kuona uwezekano wa kupandisha mishahara kwa watumishi ili waweze kuendana na hali ya maisha ya sasa kutokana na bidhaa mbalimbali hususani chakula kupanda bei.
Akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Sostenes Ndish, alisema kuwa wafanyakazi wanakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na mishahara midogo ambayo wakati mwingine wafanyakazi wanashindwa kufikia malengo.
Jambo lingine ambalo alilitaja ni pamoja na mafao ya wastaafu kucheleweshwa jambo ambalo alisema seriali inatakiwa kuangalia kwa upya ili inapokaribia mtumishi kustaafu apate fidia yake kwa wakati badala ya kukaa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Ndish alisema kuwa serikali inatakiwa kuwawajibisha waajiri ambao wamekuwa na tabia ya kuchelewesha makato ya watumishi au kutolipa kabisa katika mifuko ya jamii jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa malalamiko kati ya mfuko, mwajiri na mwajiliwa.
Kuhusu sekta binafsi alisema zimekuwa na tabia ya kuwafanyisha kazi watumishi wake lakini wamekuwa hawatoi mikataba wala ajira na kusababisha wafanyakazi wengi kutokuwa na fedha katika mifuko ya jamii jambo ambalo ni hatari kwa utumishi wao.
MAHOJIANO.
MMOJA wa wafanyakazi waliopatiwa zawadi kwa utumishi bara ni pamoja na Dereva wa Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Frank Malecella maarufu kwa jina la Muboss alisema kuwa siri kubwa ya yeye kupatiwa zawadi ya ufanyakazi bora ni pamoja na  kufanya kazi kwa utii pamojana kusikiliza mkuu wake wa kaza anasema nini.
“Ili uweze kufanya kazi vizuri ni lazima uwe na heshima kazini, kujali muda wa kazi, kuhusu masuala ya mishahara alisema yeye anakubaliana na kiwango ambacho kimepangwa na serikali huku akiwa na akili ya kujiongeza kwa lengo la kufanya kazi nyngine za kumuongezea kipato” alisema.
Naye Olipa Mwankemwa ambaye ni Ofisa rasilimali watu katika kiwanda cha machinjio ya kisasa ya nyama kilichopo Kizota, alisema kuwa serikali inatakiwa kusimamia zaidi changamoto ambazo wafanyakazi wanakumbana nazo.
Alisema kwamba wafanyakazi wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na mishahara kiduchu,kutokuwepo na usalama wa kutosha katika sehemu za kazi huku akisema kuwa waajiri wengi hawapeleki pesa ya makato katika mifuko ya jamii kwa wakati.
Olipa alisema zipo pia kampuni nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanyisha watu kazi lakini wamekuwa hawapo tayari kuwapatia mikataba ya kazi wala kuwapatia ajira jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kazi.
Kwa upande wake Salum Mkuya ambaye ni mtumishi wa TAMISEMI ,Elimu  alisema katatika sherehe za wafanyakazi Mei Mosi kwa wale ambao wanachaguliwa kuwa wafanyakazi bora wanatakiwa kupewa vifaa ambavyo vitawawezesha kufanya mambo ya kimaendeleo.
Alisema yafaa watumishi hao ambao wanachaguliwa kuwa wafanyakazi bora kupatiwa vifaa kama vile vya ujenzi au vifaa vya usafiri kulingana na zawadi ambayo muhusika amekuwa amepangiwa badala ya kuwapatia zawadi kama tv.
Muhsin Mulokozi ambaye ni Ofisa tarafa ya Mlali wilaya ya Kongwa alisema kuwa sherehe za wafanyakazi ni kuwafanya wafanyakazi hao kujitambua na kujitathimini kujua wamefanya kazi kwa kiwango gani kwa mwaka.
Hata hivyo alisema siri kubwa ya kufanya kazi kwa mafanikio ni kuhakikisha mfanyakazi anafanya kazi kwa malengo ya kuwahudumia wananchi pamoja na kujenga uhaminifu kwa serikali na jamii kwa ujumla.

KILELE CHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI WETE PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono juu wakati wakiimba wimbo maaluma wa mshikamano katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wakinyanyua mikono juu wakati wakiimba wimbo maaluma wa mshikamano katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wakiwa katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Wananchi wakiwa wamejifunika Mvua wakati walipokuwa wakiingika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)

Wafanyakazi mbali mbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Wafanyakazi mbali mbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.Picha na Ikulu

UTT AMIS PLC YASHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushiriki kushiriki maandamano ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani.
 Baadhi ya wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushiriki kushiriki maandamano ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani.
  Baadhi ya wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiwa katika picha ya pamoja.
 Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiongoza maandamno kuingia kwenye Uwanja wa Uhuru katika sherehe za Mei Mosi.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiingia Uwanja wa Uhuru kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa UTT Amis PLC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Gari la UTT AMIS PLC likipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa UTT AMIS PLC  wakiingia kwa maandamno kwenye Uwanja wa Uhuru.




Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images