Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU

$
0
0
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Festo Kiswaga . 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa( TANAPA) Allan Kjazi akikabidhi Hundi ya Kiasi cha Sh Mil 50 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa huo ,wengine kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi ,Bw Festo Kiswaga . 
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za TAifa (TANAPA) Pascal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.



Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana .

Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za wasichana na wavulana.

Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.

Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.

KONGAMANO LA TANZANIA YA VIWANDA LAFANA MKOANI IRINGA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.
Baadhi ya wajumbe wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya kuifikia Siku ya Mei Mosi wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano, Mkoani Iringa.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akiongea umuhimu wa kuwa na Tanzania ya Viwanda wakati wa Kongamano la maandalizi ya Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.
Baadhi ya wajume wakifuatilia Kongamano la maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi walipokutana kujadili masuala ya Tanzania ya Viwanda Aprili 27, 2018.
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda (katikati) akifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018.
Katibu Mkuu TUCTA Dk Yahaya Msingwa akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akizungumza wakati wa Kongamano la kuelekea sikukuu ya wafanyakazi duniani lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Bw. Tumaini Nyamhokya akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista nje ya ukumbi wa Kichangani Iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista (wan ne kutoka kushoto) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (kulia kwake) wakiwa katika picha ya baadhi ya Watendaji wa Serikali walipohudhuria katika kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Iringa Aprili 27, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akisalimia wajumbe waliohudhuria katika Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akipokelewa na Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza alipowasili mkoani hapo kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi akiongozana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akisema jambo wakati wa kikao kifupi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya shughuli za Mei Mosi mkoani hapo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

UMISSETA YAZINDULIWA MTWARA

$
0
0


JOSEPH MPANGALA -Mtwara.

Mashindano ya Copa CocaCola Umisseta 2018 yamezinduliwa rasmi katka mkoa wa Mtwara.

Akizindua mashindano hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambaye ni mkuu wa wilaya, Evod Mmanda ametaka washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumiz ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.

Mmanda amesema michezo inajenga afya na kuboresha mwili na kusema mwanafunzi atakayejihusisha katika mapenzi na kumpa mwenzake ujauzito sheria zitachukuliwa kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine hivyo watumie muda huo kushiriki michezo.

“Hakuna muda wa ziada usiotumika vizuri wa kwenda kufanya mahusiano yaliyo nje ya utaratibu yanayopelekea mapenzi kwa watoto wa shule wote wa pande mbili,sheria iko pale pale atachukuliwa hatua kama mtu mwingine kwa watoto wa kike wakiwa kama waathirika wa kwanza na watoto wa kiume,ukamataji unakamata vile vile,”amesema Mmanda

Brand meneja wa Coca Cola Tanzania, Sialovise Shayo amesema kikubwa kinachofanyika ni kugawavifaa vya michezo kwa mpira wa miguu na mpira wa kikapu na kutoa viburudisho vinavyozalishwa na kampuni hiyo kwa wanafunzi. “Kama kampuni tunaamini vijana ili wawe imara kakili ni lazima wafanye michezo hivyo tunawapatia vifaa vya michezo,maji na Cocacola kwasababu vipaji haviboreshi tu elimu lakini pia wakiwa wachezaji bora wanaweza kucheza lgi za kimataifa kama anavyofanya Mbwana Samata,”amesema Shayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akipokea zawadi ya Mpira kutoka kwa Brand Meneja wa Cocacola Tanzania Sialovise Shayo katika uzinduzi wa Mashindano ya Copa cocacola Umisseta Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akimkabidhi Vifaa vya michezo Mwalim wa shule ya seminary ya Mtwara Sisters Philipo Milanzi
 Mkuu wa Wilaya Avod Mmanda akikagua moja ya Timu zinzoshiriki katika Mashindani ya copa cocacola Umisseta mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya Avod Mmanda akikagua moja ya Timu zinzoshiriki katika Mashindani ya copa cocacola Umisseta mkoani Mtwara.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA KANDORO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombelezo ya Marehemu Abbas Kandoro aliyefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimpa pole mke wa Marehemu Abbas Kandoro, Mariam Kandoro nyumbani kwa marehemu Mbweni jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

RMO,DMO TENGENI SIKU ZA UCHUNGUZI WA SARATANI-WAZIRI UMMY

$
0
0

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza leo Jijini Tanga wakati alipozindua kampeni ya chanjo ya
saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama
katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni
hiyo

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell akizungumza katika
uzinduzi huo ambapo alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa
kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza katika uzinduzi huo

Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon akizungumza wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akisalimiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO)Jairy Khanga mara
baada ya kuwasili kwenye kituo cha Afya cha Ngamiani alipokwenda
kuzindua chanjo hiyo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga wakiangalia ngoma ya Msanja wakati wa uzinduzi
huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo kabla ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Monica Kinala

Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati wa uzinduzi huo ksuhoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa Selebosi
katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni
Mkuu wa wilaya hiyo.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akifurahia jambo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo ya chanjo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akimpongeza mwanafunzi wa shule ya Sekondari mara baada ya kuchanjwa
chanjo hiyo kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa
ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga na katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji
la Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akitazama namna mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Masiwani Hanifa Juma
anavyopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi wake leo kushoto ni Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga
WAZIRI  wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akifurahia jambo mara baada ya kumaliza uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiangalia kadi walizopatiwa wanafunzi hao baada ya kupitiwa chanjo WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga na wanafunzi mbele waliopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi huo
Wanafunzi waliopatiwa chanjo wakionyesha kadi zao
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon kulia akiteta
jambo na Dkt Hamisi mara baada ya kufanyika uzinduzi huo

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kutenga siku moja kwa mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti
kwa wanawake na tezi dume.

Waziri huyo ametoa agizo hilo mkoani Tanga leo wakati akizindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Amesema kuwa hali ya saratani kwa nchi zinazoendelea haswa zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wagonjwa wa saratani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka. Amesema kuwa Tanzania kunakuwa na wagonjwa 50,000 waliogunduliwa na tatizo la saratani.

Amesema kuwa katika wagonjwa hao asilimia 33 wanakutwa na saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 12 wanagundulika na saratani ya matiti. Amebainisha
kuwa kila katika wagonjwa 100,wagonjwa 80 wanakuwa katika hatua za
mwisho za ugonjwa na kufanya matibabu kuwa magumu.

” Narudia kutoa agizo kuwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutenga siku moja kila mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani kwa wanawake na wanaume”
alisema.  Kuhusu chanjo amesema kuwa mwaka huu wamelenga kutoa
kwa wanawake laki sita na elfu kumi sita kwa mabinti wenye umri wa
miaka 14 kutokana na uchache wa chanjo.

” Kwa kuanzia mwaka huu tutatoa chanjo laki sita na elfu kumi na sita kutokana dozi ya chanjo,tuliyoipata ni laki sita na elfu ishirini” alisema. Aidha
alitoa wito chanjo itolewe kwa mabinti hali ya kuwa wazazi au walezi
wao wameridhia.

” Ninatoa wito kwa watoa huduma za afya hii chanjo mnapoitoa hakikisheni wazazi au walezi wameridhia” alisema  Awalikaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.

Kati ya hao 30,000 ni wanafunzi wa shule mbalimbali na 8,000 kutokana nyumbani watapatiwa katika hospitali na vituo vya Afya 18 vilivyoteuliwa.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

RUVUSHOOTING APAPASWA NA MAJI MAJI 3 – 1, MARCEL AONDOKA NA MPIRA

$
0
0
Mchezo kati ya Maji Maji na Ruvu shooting katika uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma umemalizika na Maji Maji kuibuka mbabe wa bao 3 – 1 Mabao yote matatu ya Maji Maji yamefungwa na Marcel Boniventure na baada ya mpira kumalizika amekabidhiwa Mpira baada ya kufunga magoli yote matatu.

Chuo cha Kodi Chapongezwa Kuwajengea Uwezo Wanafunzi Wake

$
0
0

Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. Kutoka kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi na Naibu Mkuuwa Chuo cha Kodi A
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi akizungumza wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouely akielezea namna anavyofurahishwa na jinsi Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya kodi wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Bi. Oliver Njunwa akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
Mwakilishi kutoka Taasisi ya Global Education Link (GEL), Bi. Happiness Agathon akimkabidhi kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi wa mwaka wa TATU WA Chuo cha Kodi (ITA), Bi. Nteghenjwa Kidika zawadi ya ushindi wa pili katika uwasilishaji wa mada wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. Wanafunzi hao waliwasilisha mada kuhusu hesabu za kodi na forodha. Kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja (hayupo pichani) ambaye alimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Bw. Wilberforce Benda( mwnye Kaunda suti) akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha wanafunzi walioibuka washindi wa kwanza katika uwasilishaji wa mada wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.Wanafunzi hao waliwasilisha mada kuhusu namna ya kuandaa mipango ya kodi. (Frank Shija – MAELEZO

AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma 

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kuahidi kuwa atahakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika Jiji la Dodoma na mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge. 

Akiwa katika uwanja wa ndege Jijini Dodoma, Dkt. Adesina amemmwagia sifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia ukuaji wa uchumi uliofikia wastani wa asilimia 7 kwa mwaka pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa, kuimarisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, kupiga vita matumizi mabaya ya rasilimali za umma ili kuwaondoa wananchi wake katika umasikini. 

Dkt. Adesina amesema kwa kutambua mchango huo pamoja na umahili wa Waziri wa Fedfha na mipango Dkt. Philip Mpango, wa kusimamia uchumi na sera ya bajeti na fedha, benki yake itaendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili nchi iweze kupiga hatua kubwa kupitia miundombinu mbalimbali inayotekelezwa kupitia benki yake na washirika wengine wa maendeleo. 

Miongoni mwa miradi ambayo Benki hiyo imepanga kusaidia ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa utakaojengwa katika eneo la Msalato, nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo kwa kuanzia benki hiyo itatoa zaidi ya shilingi bilioni 200. 

“Tumekuwa na majadiliano ya kina na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kuhusu mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge ambao utazalisha Kw 2100, Benki yetu itaangalia namna ya kutoa fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mradi huo mkubwa” alisema Dkt. Adesina. 

Alisema kuwa suala la mapinduzi ya viwanda haliwezi kufanikiwa bila kuwa na nishati ya umeme ya uhakika na kwamba benki yake itawekeza dola za Marekani bilioni 1.5 kwa ajili ya sekta ya nishati na itaongeza kiasi kingine cha dola milioni 950 kwa ajili ya kazi hiyo. 

“Mwaka huu tutatoa fedha kwa ajili ya kuboresha nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na tuna mpango pia wa kuboresha Shirika la Ugavi wa Umeme hapa nchini-TANESCO, ili liweze kuzalisha umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu kwa ajili ya kuendeleza mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda” aliongeza Dkt. Adesina 

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameelezea kufurahishwa na ujio wa Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, na kwamba ujio huo umeleta neema kwa nchi baada ya benki hiyo kuahidi kutoa shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato pamoja na kuahidi kutoa fedha kwa ajili ya kujenga barabara za mchepuko (mzunguko) Jijini Dodoma. 

Dkt. Mpango amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo na watembee kifua mbele kwa kuwa hivi sasa Tanzania imeshika nafasi ya pili katika Bara la Afrika kwa ukuaji wa uchumi kwa kasi ikitanguliwa na nchi ya Ethiopia, na Rais Adesina amelisemea vizuri jambo hilo. 

Ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971, ambapo mpaka sasa benki hiyo imewekeza kiasi cha dola bilioni 3.6, sawa na zaidi ya shilingi trilion 8, katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo umeme, barabara, maji na usafi wa mazingira, uboreshaji rasilimali watu pamoja na masuala ya utawala bora.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SIKU YA MWANAMKE WA MFANO TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizindua Siku ya Wanawake wa Mfano Tanzania iliyoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) katika ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam 
Mama Fatma Karume akionyesha juu tuzo ya Mwanamke wa Mfano Tanzania ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika harakati za Mapinduzi ambapo yeye alikuwa mke wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Abeid Aman Karume 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi tuzo ya Mwanamke wa Mfano mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete. 
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anna Makinda akionyesha juu Tuzo yake ya Mwanamke wa Mfano mara baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mama Fatma Karume mke wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akitoa nasaha zake mara baada ya kupokea tuzo ya Mwanamke wa Mfano iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT). 

Picha na Ofisi ya Makamu 

……………….. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika harakati za Uhuru wan chi hii. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Siku ya Mwanamke wa Mfano Tanzania iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) 

Makamu wa Rais alisema Ni dhahiri kuwa wanawake walikuwa na mchango mkubwa sana. Walifanya kazi kubwa katika uhamasishaji, malezi ya watoto na vijana na kusimama bega kwa bega na kuunga mkono wanaume waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano. Walifanya mengi nyuma ya pazia ambayo yalikuwa na mchango mkubwa katika Taifa letu. Mapenzi yao, subira yao na mchango wao wa hali na mali ndio uliowapa nafasi wanaume kufanikisha harakati za uhuru kwa kuwa wanawake waliwapa wepesi kwa kuwapunguzia mzigo mzito uliokuwa mabegani mwao. Haiyumkini, katika ngao yetu ya Taifa, ikatambua nafasi ya mwanamke kwa kuwekwa sambamba na mwanaume. 

Makamu wa Rais aliendelea kusema kutokana na kazi kubwa ya wanawake jasiri na mashujaa waliotutangulia, wanawake wa nchi yetu wameendelea kutoa mchango mkubwa katika Uongozi katika nchi yetu na nje ya mipaka yake. 

Makamu wa Rais alitoa wito kwa Wanawake na kusema Tuzo za “Mwanamke wa Mfano Tanzania” ziwe chachu yetu Wanawake katika kuchapa kazi, kuungana, kushikamana katika kuleta maendeleo miongoni mwetu na jamii nzima ya Watanzania. Sisi wanawake ni nusu ya watu wote nchini. Sisi tukijiongeza tukaendelea, kaya zetu zinaendelea na hatimaye nchi inaendelea. 

Makamu wa Rais aliwataka Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kuchukua jukumu lenu la kuwasemea, kuwatetea na kuwaunganisha wanawake wote wa Tanzania wana CCM, wasio wana CCM na wasio na vyama. Ndio wajibu wa UWT mliopewa na Katiba ya CCM. Katika nchi yetu, hamna chombo chochote kikubwa cha kuwaunganisha wanawake isipokuwa ninyi. Nawakumbusha kuwa nanyi mnatazamwa na wanawake wa nchi yetu. 

Jumla ya Tuzo 26 za Mwanamke wa Mfano zilitolewa .

WAZIRI WA NISHATI DKT KALEMANI AZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani sambamba na wabia wa kampuni ya Baobao Energy System akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda hicho.

Na Leandra Gabriel,  ya jamii

KATIKA kuelekea uchumi wa kati wa viwanda kampuni ya Baobao Energy Systems Tanzania (BEST) imefungua kiwanda cha kutengeneza mita za umeme za luku na hii ni kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati kufikia 2025.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye pia Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameeleza kufurahishwa  na kufarijika kwa kupata mwaliko wa kuzindua kiwanda hicho kwani mita za luku zinategemewa na wadau wengi nchini na amewapongeza na kuwataka TANESCO kujipanga katika kukabiliana changamoto za kukidhi mahitaji ya kutoa huduma za umeme kwa wananchi.

Aidha Dkt Kalemani ameeleza kuwa Julai mosi mwaka huu hakuna mita za luku zitakazoagizwa kutoka nje na hii ni baada ya kufanya tathimini kwa miezi mitatu na kujiridhisha na uzalishwaji wa mita hizo hapa nchini na kuanzia Mei mwaka huu mita za luku zitanunuliwa kutoka Baobab.

Pia Dkt Kalemani amewataka wamiliki wa kiwanda hiki kuzingatia uharaka wa utengenezaji, wingi wa mita hizo, ubora na upatikanaji wake kirahisi, Na ameeleza umuhimu wa mita hizi ikiwa pamoja na matengenezo pindi zinapoharibika, gharama nafuu na uharaka tofauti na zile zinazoagizwa nje na amewataka TANESCO kuunganisha umeme kwa siku zisizozidi 7.

Mwakilishi wa Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji Aristides Mbwasi amewapongeza wamiliki na kiwanda hicho na kuahidi ushirikiano pale watakapohitaji kwani kwa sasa taifa lipo katika malengo ya kuijenga Tanzania mpya kama Serikali ya awamu ya tano ilivyoazimia.

Naye Meneja mkuu wa kampuni ya Baobab Energy Systems Tanzania, Mhandisi Hashim Ibrahim amemshukuru waziri wa nishati kwa kuja kufungua kiwanda hicho na kueleza kuwa kampuni hiyo ni ya ubia baina ya kampuni ya Comfix Engineering Ltd ya Tanzania inayomiliki hisa kwa asilimia 51 na hii ni kwa kutoa mchango wa fedha, majengo, rasilimali watu na fedha na kampuni ya EDMI ya nchini Singapore inayomiliki hisa kwa asilimia 49 
na kuchangia mtaji kupitia mitambo na teknolojia kwa ujumla.

Hashim ameeleza kuwa hawaogopi ushindani na kampuni za nje ila tatizo lao ni pale kampuni hizo zinapopewa unafuu wa gharama na uzalishaji na ameiomba serikali kutoa ushirikiano ili kuweza kujenga Tanzania ya viwanda na ameeleza kuwa wana mpango wa kutengeneza mita za gesi na maji hapo baadaye.

Kuhusu uzalishaji wa mita katika kiwanda hicho Hashim ameeleza kuwa mita zitakazotengenezwa na kuuzwa nje na ndani ya nchi zitaliongezea taifa mapato yanayotarajiwa kufikia shilingi Bilioni 97 kwa mwaka.

Pia Mkurugenzi mkuu mauzo wa Kampuni ya EDMI ya nchini Singapore Lam Wee Chee ameeleza kuwa kwa miaka 10 kampuni ya EDMI imefanya kazi na Shirika la Umeme (TANESCO) hasa kwa kusambaza mita hizo na zaidi ya mita 100000 zimenunuliwa na TANESCO kutoka EDMI na kwa sasa watawapa mfumo utakaowasaidia kusoma taarifa zote na kudhibiti wizi wa umeme.

Aidha ameeleza juhudi zao katika kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano na kuahidi kutoa huduma bora kwa wateja wao kupitia TANESCO ambao ndio wasambazaji wa mita hizo.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na baadhi wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za kiserikali na wafanyakazi wa kiwanda cha Baobao Energy System Tanzania wakati wa kuzindua kiwanda hicho kinachojihusisha na utengenezaji wa mita la LUKU, tukio lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa  kampuni ya Baobao Energy System Mhandisi Hashim Ibrahim akizungumzia kiwanda hicho kitakachokuwa kinatengeneza mita za LUKU hapahapa nchini wakati wa uzinduzi kilichozindukiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.
 Mkurugenzi wa Mkuu wa Mauzo wa EDMI Lam Wee Chee akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Baobao Energy System jana Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Nishati akizindua kiwanda cha Baobao Energy System jana Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Baobao Energy System Hashim Ibrahim akimuelezea jambo Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipokua akikagua chumba kinachotumika kutengeneza mita za LUKU wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikagua mitambo inayotumika kwa ajili ya utengenezeaji wa mita za LUKU wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho namna wanavyoweza kutengeneza mita za LUKU zenye ubora.Picha zote na Zainab Nyamka.

IDADI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO YA MVUA KATIKA KATA YA MWARU YAFIKIA ZAIDI YA WAKAZI 700

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly IKUNGI 

IDADI ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilaya ya Ikungi waliokosa makazi kutokana na nyumba zao kuanguka kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa zimeongezeka kutoka kaya 22 zanye zaidi ya wakazi 154 hadi kufikia kaya 177 zenye zaidi ya wakazi 700 baada ya nyumba189 kuanguka.

Ongezeko la idadi hiyo ya wakazi linatokana na mvua kubwa iliyonyesha apr,16 hadi 18,mwaka huu na kusababisha mto kuacha njia yake na kulenga katika Kitongoji cha Mwasusu,na ndipo kaya 22 zenye zaidi ya wakazi 154 katika vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,Kata ya Mwaru kukosa makazi baada ya nyumba 34 kuanguka.u

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mwaru,Hamisi Malongo alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa za athari zilizotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa Mkoani Singida na kuongeza kwamba pamoja na nyumba hizo vile vile makanisa matatu ya FPCT na AIC yalianguka kufuatia mvua hizo.

“Na tuliloligundua sisi kama viongozi kama serikali upande wa kata kwamba vijiji vya Kaugeri na Mduguyu ni vijiji vya mpakani na Mkoa wa Tabora ambavyo ndiyo bonde la Mto Wembere unapita kwa hiyo mvua inaponyesha pande zote za dunia kwa hiyo wao ni rahisi sana kuathirika na mvua hizo.”alisisitiza Malongo.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugeri,Laurence Bomba Torokoko akizungumzia hasara zilizotokana na mvua hizo alizitaja kuwa ni pamoja na nyumba 105 zenye wakazi 412 walikosa makazi kabisa ya kuishi na hekari 92 za mazao mbali mbali.

Madhara mengine kwa mujibu wa Torokoko magunia 334 ya mpunga na mtama,kuku 20 na ng’ombe moja amba hatha hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwasaidia familia zilizoathirika kutokana na mvua hizo ambazo bado zinaendelea kunyesha.

Kwa upande wao baadhi ya waathirika wa mvua hizo,Mchungaji,Hosea Eliudi licha ya kuishukuru serikali kwa msaada wa awali lakini hakusita kueleza changamoto zinazowakabili kwenye kambi hiyo kuwa ni hatari ya kuugua ugonjwa wa malaria kutokana na kuwepo kwa mbu wengi huku wakiwa hawana vyandarua baada ya walivyokuwa wakitumia kuangukiwa na nyumba zao.

Misaada pamoja na changamoto zingine kwa mujibu wa mchungaji huyo ni mahema makubwa yatakayoimarisha kambi hiyo kufanana na zile za wakimbizi na kuzitaja changamoto zingine kuwa ni kushindwa kuvuna kwa kuwa hawana sehemu ya kuhifadhi mazao yao.

Mashiri Masunga mkazi wa ni mmoja waathirika wa mafuriko ya mvua hizo kwa upande wake anaelekeza shutuma zake kwa Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi,Elibariki Kingu kwamba licha ya kuwaahidi kuwapelekea kadi za CCM pamoja na maturubai tangu apr,23,mwaka huu lakini wamejikuta wakiende na matatizo ya kutokuwa na kifaa hicho muhimu kwa kujikinga na mvua.

Mmoja wa wananchi walioathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha akiwa kwenye makazi yake mapya yaliyopo kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri akihofia wingu lililotanda kama alivyokutwa na kamera ya kituo hiki(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilayani Ikungi wakihamisha baadhdi ya vitu vilivyosalia kwenye makazi yao ya zamani na kuhamia kwenye eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa sisku tatu mfululizo na hivyo kusababisha zaidi ya wakazi 700 kukosa mahali pa kuishi
Ni Miundombinu ya barabara ya kutoka Mlandala kwenda kwenye Kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafurriko ya mvua zilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Singida.

KUMEKUCHA MISS TABORA 2018

$
0
0

Kumekucha: Fomu za kushiriki mashindano ya Miss Tabora zitaanza kutolewa tarehe 02/05/2018 hadi tarehe 20/05/2018 katika ofisi zote za utamaduni za Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Tabora. 

Auditions kwa Wilaya zote zitaanza kufanyika tarehe 21.05.2018 hadi tarehe 04.06.2018.

Warembo wote 16 watakaokidhi vigezo wataingia kambini na kupata mafunzo mbalimbali na kushiriki kampeni na shughuli za kijamii wakisubiria fainali tarehe 07/07/2018.

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa habari zaidi za Miss Tabora 2018.

@genevieve.tz 
@genevieve_updates
@newmisstanzania
@genampangala

👑👑👑👑👑

#MissTabora2018 
#UremboNiMalengo
#UremboNaKaziKwaMaendeleoYaJamii

WAJASIRIA MALI Z'BAR WAPEWA MBINU MPYA.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

WANAWAKE visiwani Zanzibar wameshauriwa kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa lengo la kujiongezea kipato na kujiajiri wenyewe.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT) Pily Khamis Lapda, amesema wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya shughuli za ujasiriamali kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.

Amesema zipo njia mbali mbali za kuwakomboa wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda na kuamini shughuli za ujasiriamali kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.Amewashauri wanawake nchini kujiamini pindi wanapoanzisha biashara zao sambamba na kujiwekea malengo ya kudumu ya kibiashara yatakayowasaidia kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara. 

Mkurugenzi huyo Pily, akizungumzia malengo ya taasisi yake inayoendesha na kusimamia mafunzo ya kuyajengea uwezo wa kitaaluma makundi mbali mbali ya kijamii ili kupata uwezo wa kutumia ipasavyo fursa za ujasiriamali wenye maendeleo.“Wanawake tuwe mstari wa mbele kujifunza mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi, pia tujitume na kuwa wabunifu katika biashara zetu ili nasi tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.

Akitoa mada ya Uvumbuzi binafsi, mtaalamu wa Saikolojia na maendeleo ya vijana, Joseph Mrindo amesema wanawake waliopo katika sekta ya ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya ujasiriamali mdogo mdogo kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.

Ameeleza kuwa Zanzibar ni sehemu muhimu yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kujiongeza kibiashara.Mtaalamu huyo, amewasihi wajasiriamali kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za maendeleo ya kibiashara ili wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha kupewa mikopo kwa wakati na benki mbali mbali nchini.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiria mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi wa kufanya biashara zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na taasisi ya New vision consortium (NVCT)iliyopo Zanzibar na jumla ya washiriki 200 kutoka taasisi binafsi na za umma wanapewa ujuzi huo wa ujasiriamali.

Wadhamini wa mafunzo hayo ni pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na IQUITY BANK



MKURUGENZI wa New vision consortium Pily Khamis Lapda(aliyekaa katikati) akifungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar yaliyofanyika katika Skuli ya Haile-Sela-ssie.
BAADHI ya washiriki katika mafunzo hayo kutoka taasisi binafsi na za umma wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo, huko Skuli ya Haile-Sela-ssie.
MSHIRIKI wa mafunzo ambaye pia ni mjasiria mali kutoka U.WT. jimbo la Mwera Salama Mohamed Tahir akichangia mada ya uvumbuzi binafsi.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.


MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi. Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi. 

Aidha, akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao. 


Mfuko umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018. 
Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw. Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza

Usalama Mahala pa Kazi, TANESCO yaibuka Kidedea yakabidhiwa Ngao, IRINGA

$
0
0
Usalama Mahala pa Kazi, TANESCO yaibuka Kidedea yakabidhiwa Ngao, IRINGA  
Shirika la Umeme TANESCO, limeibuka Kidedea Kwa Kupata Ushindi Kwenye Shindano la Usalama Mahali pa Kazi lililoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya IRINGA.

TANESCO imepata Ushindi huo Kupitia Sekta ya Huduma, ambapo imekabidhiwa Ngao na Cheti ikiwa ni Heshima ya Kutambuliwa Kama Taasisi ambayo imefanya Vizuri Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.

Baada ya Shirika hilo la Umeme Kutangazwa Mshindi na Kukabidhiwa Ngao, Afisa Afya na Usalama Makao makuu NELSON MNYANYI amesema Elimu ya Afya na Usalama imekuwa Kichocheo Kikubwa katika Kupunguza Ajali kwa Wafanyakazi wa TANESCO pamoja na Wananchi kwa Ujumla.

Kwa Upande wake Afisa Afya na Usalama FRED KAYEGA akielezea Ushindi huo amesema licha ya Kupokelewa kwa Faraja, ni Motisha kwa TANESCO kuendelea Kufanya Vizuri zaidi Kwenye Sekta ya huduma Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.Katika Banda la TANESCO elimu mbalimbali kuhusu Afya na Usalama na Elimu Kuhusu Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme iliweza Kutolewa kwenye Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.
Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji CHARLES MWIJAGE akiangalia Baada la TANESCO mara Baada ya Kulitembelea Katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa, ambapo Shirika hilo limeibuka Mshindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano ya Usalama Mahala pa Kazi yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA.
Maaofisa wa Shirika la Umeme TANESCO, Kutoka Kushoto Sylvester Matiki ( Afisa Masoko ), Nelson Mnyanyi ( Afisa Usalama ), Fred Kayenga ( Afisa Muandamizi Usalama na Afya Mahali pa kazi ) pamoja na Hassan Athumani (Mwenyekiti wa majadiliano TUICO TANESCO) wakifurahia Ushindi wa Ngao na Cheti Baada ya Kukabidhiwa Kama Washindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.
Wananchi Mbalimbali Katika Manispaa ya Iringa Waliofika Katika Banda la TANESCO katika Viwanja vya Kichangani Wakipewa Elimu Kuhusu Afya na Usalama pamoja na Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme.
Afisa wa TANESCO, Kitengo cha Huduma kwa Wateja ENIDY ELSON akitoa Elimu ya matumizi Bora ya Umeme kwa Wanafunzi na Wananchi Waliofika Kwenye Banda la Shirika hilo Wakati wa Shindao la Usalama Mahala pa Kazi lilioendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA KATIKA SEHEMU YA IRINGA-MIGORI-FUFU KM 189 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia  wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika sherehe hizo za ufunguzi wa barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Isimani Mkoani Iringa
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa jukwaa kuu pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida, Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakifatilia sherehe za ufunguzi wa barabara ya ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa mjini waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa.
Mwananchi wa Iringa mjini akipuliza pembe ya ng’ombe  wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili Iringa mjini katika ziara ya kikazi. PICHA NA IKULU

PROFESA KABUDI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume Casmir Kyuki na kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Casmir Kyuki (Kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Khalist Luanda mara baada ya kufunguka mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume (Idara ya Mapitio) Angelah Bahati (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Sehemu ya Wajumbe Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.


Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.


………………


Na Munir Shemweta, Morogoro


Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha watumishi katika mipango ya uendeshaji Taasisi kwa kuwa suala hilo lipo kisheria.

Aidha, alisema kwa miaka yote Serikali imekuwa ikisisitiza Taasisi kujenga na kutekeleza utaratibu wa kushirikisha watumishi na hali hiyo inatokana na ukweli kuwa palipo na watumishi wengi pana mawazo mengi.Profesa Kabudi alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa kumi na tatu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.

‘’Ushirikishwaji watumishi kwenye mipango ya uendeshaji ofisi unasaidia kupata mawazo mengi na mapya yanayoweza kurahisisha uendeshaji wa ofisi na kutoa fursa ya kusikiliza kero na changamoto kwenye uendeshaji wa Taasisi na kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi’’ alisema profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa, kwa kushirikiana na watumishi ni dhahiri wanapata morari wa kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa mipango ya taasisi ambayo wao wenyewe walishiriki kuiandaa.Waziri huyo wa Katiba na Sheria alisema, ushirikishwaji unafanywa kupitia baraza la wafanyakazi kwa kuwa baraza ni chombo kinachowashirikisha wafanyakazi katika kupanga , kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali inayohusu shughuli za kazi za Taasisi kama zilivyoainishwa katika sheria za nchi.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, Mabaraza hutoa fursa kwa wafanyakazi kushiriki katika maamuzi mbalimbali na kuboresha uhusiano baina ya wafanyakazi na uongozi pamoja na mazingira ya utendaji hasa mahala pa kazi hivyo baraza ni chombo cha kuimarisha na kuboresha demokrasia mahala pa kazi.

Amewataka wajumbe wa baraza wa Tume ya Kurekebisha Sheria kuzingatia suala la nidhamu kazini, misingi ya kazi na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu. Aidha, alitaka uzembe kazini upigwe vita na suala la kufanya kazi kwa mazoea kukomeshwe na kubainisha kuwa,vipaumbele viwekwe katika kulinda rasilimali za Tume na kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na mali zake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria ambaye ni Katibu Mtendaji Tume Casmir Kyuki alisema katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018 Tume yake imeweza kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika bajeti.

Ameyataja majukumu hayo kuwa ni kufanya mapitio ya Mfumo wa Sheria Unaosimamia Haki Jinai, Sheria ya Ushahidi, Uchambuzi wa Kesi za Mahakama ya Rufaa, Mfumo wa Sheria Unaosimamia Huduma ya Ustawi wa Jamii, Mfumo wa Sheria za Ufilisi pamoja na kutoa elimu ya sheria kwa umma.

Ameishukuru serikali kwa mabadiliko makubwa iliyoyafanya katika sekta ya sheria kupitia tangazo la serikali namba 48,49 na 50 ambapo yameleta muundo mpya kwa kuanzishwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai na ile ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi.

WAZIRI MHAGAMA : SERIKALI HAITAPUUZA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI

$
0
0
Serikali imesema kamwe haitapuuza suala la Usalama na Afya mahali pa kazi hususani katika kipindi hiki ambacho msisitizo mkubwa ni katika kujenga uchumi wa viwanda.

Msimamo huo wa serikali umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Jenista Mhagama, alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa na wageni mbali mbali waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi Duniani.

Mh. Mhagama ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya siku hiyo ambayo huadhimishwa kila ifikapo Aprili 28, alisema katika kipindi hiki ambapo mwelekeo wa nchi ni kujenga uchumi wa viwanda, suala la usalama na afya za wafanyakazi ni lazima lizingatiwe.

“Ningependa kusisitiza kuwa, serikali ya awamu ya tano kamwe haitapuuza suala la usalama na afya mahala pa kazi hasa wakati huu tunapojenga uchumi wa viwanda ambao utaambatana na vihatarishi vingi vipya,” alisema Mh. Waziri na kuongeza: 
“Kwa hivyo, itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kupunguza au hata ikiwezekana kuondoa kabisa vifo, ajali, magonjwa na madhara yatokanayo na kazi”.

Kwahapa nchini, masuala ya Usalama na Afya katika sehemu za kazi, yapo chini ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ambao husimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Bunge ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
OSHA husajili sehemu zote za kazi nchini na kuzitembelea kwaajili ya kufanya kaguzi za kiusalama na afya ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi mbali mbali vitokanavyo na kazi wanazozifanya.
Na Eleuter Mbilinyi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akisalimiana na watumishi wa OSHA mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa ambako maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi Duniani yalifanyika. Aliombatana nao ni Katibu Mkuu katika Wizara yake, Eric Shitindi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akiwa katika banda la OSHA katika maonesho ya Usalama na Afya mahali pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa. Alioongozana nao ni Katibu Mkuu katika Wizara yake, Eric Shitindi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda. 
*****

IGP SIRRO AKUTANA NA KAMATI YA UKARABATI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa Kituo cha Polisi Mikumi mkoani Morogoro leo, wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi, ambapo aliwakumbusha askari wajibu wao wa kufanyakazi kwa kufuata sheria na taratibu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, wakati akizungumza na askari wa Kituo cha Polisi Mikumi mkoani Morogoro leo, ambapo aliwakumbusha askari wajibu wao wa kufanyakazi kwa kufuata sheria na taratibu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wadau welevu wa Jeshi hilo wanaojenga ofisi za kituo cha Polisi Usalama barabarani Mikumi mkoani Morogoro leo, wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi.Picha na Jeshi la Polisi.

IRINGA NA MAJIRANI TUCHANGAMKIE FURSA KWENYE UTALII - MBUNGE WA MAFINGA MHE COSATO CHUMI

$
0
0
Baada ya uzinduzi wa barabara ya Migori-Iringa ambayo ni sehemu ya Barabara ya Dodoma hadi Iringa, Mhe Rais alizungumzia nia yake ya kuhakikisha Utalii unanyanyuka Southern Circuit ambapo Mkoa wa Iringa ndio kitovu.

Kati ya mambo ambayo Serikali imedhamiria kuyafanya ni pamoja na kuufanya uwanja wa ndege wa Nduli kuwa mkubwa na wa kisasa, na kujenga barabara ya Iringa hadi geti la Ruaha National Park.

Hatua hizi ni wazi kuwa zitaifungua Iringa kifursa mbalimbali. Ni muhimu kuanza kujiweka sawa kuanzia mafunzo katika masuala ya Utalii.Ni wajibu wetu kuwa-encourage vijana wetu kujihusisha na masuala ya Utalii ikiwa ni pamoja na kujifunza lugha za nje kama Kispaniola, kifaransa, kijerumani nk

Ukienda Zanzibar kwa mfano, kuna vijana wengi sana wamejikita katika shughuli za utalii kama kuongoza watalii nk. Vijana hao wamefanikiwa kwa sababu waliona hiyo fursa na kuichangamkia japo kwa kupata basic courses za masuala ya Utalii.

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali, mpaka kufikia 2017, sekta ya utalii ndio ilikuwa inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni, kiasi cha zaidi ya 17%. Kwa hiyo kuna fursa katika Utalii. Iringa na maeneo/mikoa ya jirani tujiandae katika kuchangamkia fursa hii inayokuja mbele yetu.

Cosato Chumi
Mafinga Mjini
30 April, 2018
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mhe.Cosato Chumi mapema jana mara baada ya kuwasili mkoani Iringa
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images