Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1571 | 1572 | (Page 1573) | 1574 | 1575 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John  Shibuda
  PMO_0845
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda, katika kakao kati yake na kamati hiyo, ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  …………….

   VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.

  Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.

  “Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”

  Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

  Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.

  0 0

  Na Mahmoud Ahmad Dodoma

  RAIS John Mguguli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawachukulia hatua kali watu wote waliohusika katika kufanya ubadhilifu wa zaidi y ash bilioni 1.5 ya mradi wa maji wa Ntomoko.

  Agizo hilo alilitoa jana wakati wa ufunguza wa barabara ya Dodoma Manyara yenye urefu wa kilometa 251 iliyozinduliwa katika eneo la Bicha wilayani kondoa mkoani hapa ambayo itaongeza fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi wa mikoa hiyo miwili.

  Akiwahutubia wananchi wa Kondoa na Manyara,muda mfupi baada ya kupatiwa taarifa ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Bilinithi Mahenge, kuelezea kuwa kuna ubadhirifu wa zaidi ya sh.bilioni moja na nusu zilizopotea katika mradi wa maji wa ntomoko na kuwakosesha huduma ya maji wananchi wa wilaya ya Kondoa na Chemba.

  Mradi huo wa kutandika mabomba ya kusambazia maji kuwafikia wananchi ambapo waliopewa dhamana hiyo badala ya kutandika mabomba ambayo yanauwezo mkubwa wa kufikisha maji wao wakaweka mabomba madogo ambayo hayana uwezo .“Kama ni kuchomoka basi wachomoke wale wote waliofanya ubadhirifu wa mradi huu kwani wanawapa shida wananchi wanyonge ambao walikuwa wapate huduma ya maji tokea mwaka 1980” alisisitiza Rais

  Aidha kwa upande mwingine Rais Magufuli akawataka viongozi wa wilaya hiyo kuacha migogoro ya wao kwa wao na kuwa migogoro inachangia kushindwa kuwapelekea wananchi huduma za maendeleo kwa wakati na yeye hakuwatuma kwenda kuibua migogoro hiyo. Kwa upande wake Rais wa Benki ya maendeleo ya Afrika Akinwim Adesina aiahidi neema kwa Jiji jipya la Dodoma na serikali kwa Ujumla kwamba atatoa ushirikiano kuahakikisha serikali na jiji hilo wanapata fedha za miradi.

  Amesema kuwa Bara bara hiyo itafungua milango ya kiuchumi kwa lango la Kaskazini mwa Afrika na kusini ambapo hiyo itakuwa fursa pana kwa wananchi wa mataifa nane barani humo ambayo barabara hiyo inapita kutoka Cape town hadi Cairo nchini Misri

  Nae waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa km.251 imejengwa kwa jumla ya tsh.bilon 378.4 kati ya hizo fedha za ndani blion107.6 na zilizobakia zimechangiwa na wafadhili Benki ya maendeleo ya Afrika(AFDB) na shirika la maendeleo la Japani(JICA).

  0 0  Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
  V25A4096
  Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
  V25A4092
  Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (katikati) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulie na kulia ni Mbunge wa Momba, Mhe. David Silinde
  V25A4179
  Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
  V25A4185
  Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (wa pili kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0

  Isabela Nchimbi Afisa Mradi Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akizungumza katika mkutano wa kutoa Mrejesho wa Matokeo ya Awamu ya Kwanza ya Mradi uliokuwa na lengo la Kuchangia Ongezeko la Uwakilishi na Ushiriki wa Wanawake katika Shughuli za Uongozi na Siasa uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam ikishirikisha wadau mbalimbali kutoka vyama vya siasa , Asasi za Kiraia, Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi, Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha Wanasheria wanwake TAWLA
  Isabela Nchimbi Afisa Mradi Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akionyesha kitabu chenye malengo ya Mrejesho wa Matokeo ya Awamu ya Kwanza ya Mradi uliokuwa lengo la Kuchangia Ongezeko la Uwakilishi na Ushiriki wa Wanawake katika Shughuli za Uongozi na Siasa katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya ya New Africa jijini Dar es salaam.
  Isabela Nchimbi Afisa Mradi Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akifafanua katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya ya New Africa jijini Dar es salaam
  Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA akichangia hoja katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jana jijini Dar es salaam 
  Rose Julius Afia Mradi wa Women Fund Tanzania akichangia hoja katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jana jijini Dar es salaam. 
  Catherine Vermand Mwanacha na Mwakilishi kutoka Chama cha Chadema akichangia hoja katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jana jijini Dar es salaam. 
  Baadhi ya wadau wa mkutano huo wakifuatilia mkutano huo.
   
  Jaquiline Moshi kushoto Afisa Sheria TAWLA na Debora Nyasibaa Mhasibu TAWLA wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
    
  Ofisa Kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
  Josephine Arnold Afisa Mradi TAWLA akifafanua baadhi ya hoja wakati wa mkutano huo.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Msimamizi wa Makampuni ya Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu ofisini kwake Jijini Dodoma jana ambapo walijadili uwekezaji wa kuimarisha sekta ya utalii na uhifadhi nchini. Umoja huo umeahidi kutoa ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia na Kuwait pamoja na Msimamizi wa Jumuiya ya Makampuni ya Albawardi inayoendesha hoteli mbalimbali za kitalii nchini ikiwemo Hyatt Regency na Four Season Serengeti ofisini kwake Jijini Dodoma jana.

  Mazungumzo hayo yaliyolenga kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha sekta ya uhifadhi na utalii kwa maslahi ya nchi hizo tatu. Mabalozi hao ni Bandar Abdulla wa Saudi Arabia, Mohammad Rashed Alamiri wa Kuwait na Fouad Mustafa Msimamizi wa Makampuni ya Albawardi ya Umoja wa Falme za Kirabu kwa upande wa Tanzania na Afrika ya Mashariki.

  Dk. Kigwangalla aliwaomba mabalozi hao kupitia jumuiya zao za uwekezaji kuwekeza katika miundombinu ya hoteli za kitalii Jijini Dodoma na kwenye Mapori ya Akiba katika Sakiti ya Kaskazini, Kusini na Magharibi hususan Pori la Akiba la Burigi.

  Naye Msimamizi wa Jumuiya ya Makampuni ya Albawardi, kwa upande wa Tanzania na Afrika ya Mashariki, Fouad Mustafa alisema jumuiya hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika ujenzi wa miundombinu ya barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

  Alisema mbali na uwekezaji uliopo hivi sasa jumuiya hiyo inajenga hoteli nyingine za kitalii tatu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro na katikati ya Jijini la Arusha ambapo ameiomba Serikali kuzifungua kupitia viongozi wake wa juu pale ujenzi wake utakapokamilika hususan Mhe. Rais.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Msimamizi wa Makampuni ya Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu ofisini kwake Jijini Dodoma jana ambapo walijadili uwekezaji wa kuimarisha sekta ya utalii na uhifadhi nchini. Umoja huo umeahidi kutoa ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mohammad Rashed Alamiri (kushoto) ofisini kwake Jijini Dodoma jana ambapo walijadili namna ya kuimarisha sekta ya utalii na uhifadhi nchini. Wa pili kulia ni Msimamizi wa Makampuni ya Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu ambao wameahidi kutoa ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Mazungumzo yakiwa yanaendelea.Waziri Kigwangalla akizungumza katika kikao hicho.Waziri Kigwangalla akiagana na msafara huo.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa Semina ya Waajiri kuhusu Sheria Mpya ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF.
   Baadhi ya waajiri katika semina hiyo.
  Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akisisitiza jambo wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF. Kulia ni Kaimu Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Ilala, Christine Kamuzora na Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed. 
  Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed, akizungumza wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF. 
   Kaimu Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. 
  Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akitoa mada wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. 
  Baadhi ya Waajiri wakiwa katika semina. 
  Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, James Oigo, akijibu maswali wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa na NSSF. Kushoto ni Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Kinondoni,Marko Mgheke na Kaimu Meneja wa Uendeshaji NSSF, Omary Mzia.


  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendesha semina kwa waajiri wa Mkoa wa Temeke katika jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na waajiri takrabani 200 waliopo katika mkoa wa Temeke kwa mgawanyo wa mipaka ya NSSF.

  Akifungua Semina hiyo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni, aliwaambia waajiri kwamba sheria mpya ya hifadhi ya jamii imeshasainiwa na Rais na sasa zimebakia taratibu za kiuendeshaji.

  ‘Semina hizo ambazo zimepangwa kuendelea nchi nzima zikiwa na lango la kuwahimiza waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuliwezesha Shirika kulipa mafao ya wanachama kwa ufanisi, kuzijua changamoto zinazowakumba waajiri na kujibu hoja nyingi walizokuwa nazo waajiri kuhusu uelekeo mpya baada ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuunganishwa na kubaki miwili yaani NSSF na PSSSF’, alisema Mmuni.

  Naye Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, James Oigo, akiwasilisha mada kwa waajiri hao alisema, Sheria mpya imefafanua kuwa Mfuko mpya wa waajiriwa wa sekta ya Umma (PSSSF) utakuwa unahudumia waajiriwa wote waliopo katika sekta ya umma wakati NSSF itahudumia waajiriwa wote wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

  Akifafanua kuhusu Sheria hiyo Oigo alisema kuwa, NSSF ni mfuko pekee utakaokuwa unahudumia wanachama Waajiriwa wote wa sekta binafsi, Waajiriwa wote wa Kigeni walioajiriwa Tanzania Bara, Waaajiriwa wote waliajiriwa katika taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara, Watu wote waliojiajiri wenyewe na wale wa sekta isiyo rasmi.

  Aidha amefafanua kuwa,waajiriwa wote ambao wataajiriwa baada ya sheria hii kuanza ndio watakuwa katika mfuko ama wa PSSSF endapo wanaajiriwa katika sekta ya umma na NSSF endapo wanaajiriwa katika sekta binafsi, Aidha kwa wale ambao walishaajiriwa wakati sheria hii inaanza ambapo walikuwa katika mifuko iliyounganishwa watakuwa wanachama wa mfuko wa PSSSF bila kujali wapo setka binafsi au ya umma na wale ambao walikuwa wanachama wa NSSF watabakia kuwa wanachama wa NSSF bila kujali sekta wanayotoka. Alizidi kufafanua kuwa kanuni ya ulipaji mafao na idadi ya mafao yatakuwa ya aina moja kwa mifuko yote miwili.

  Wakati huo huo, Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni, Marco Magheke, alisema, Shirika limejipanga kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama wake na kuwahakikishia waajiri kuwa NSSF itamaliza changamoto ndogondogo ambazo waajiri walizitaja wakati wa semina hiyo.

  0 0

  Afisa Maendeleo wa Mkoa Rukwa akitoa elimu ya namna ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa shule saba za mjini Sumbawanga mapema leo mjini humo. Kampeini ya Kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inatolewa Wizara ya Afya(Maendeleo ya Jamii). Picha zote na Wizara ya Afya. 
  Afisa Maendeleo Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Christopher Mushi akitoa elimu ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi kutoka shule saba za mji wa Sumbawanga leo mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa. 
  Wanafunzi kutoka shule saba za Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa wakifuatilia kwa makini kampeini ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mapema leo kufuatia juhudi za Wizara ya Afya(Maendeleo ya Jamii) kutokomeza mimba na ndoa za utotoni hapa Nchini. 
  Madereva bodaboda wa mji wa Sumbawanga wakiwasili Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kushiriki kampeini za kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mapema leo mjini sumbawanga.   Na Anthony Ishengoma-Wizara ya Afya. 

  Mkoa wa Rukwa kwasasa huna jumla ya kesi 256 zinazohusiana na mimba kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari na Msingi. 

  Akiongea katika Mkutano uliondaliwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na Ofisi ya Mkoa wa Rukwa kwa madereva bodaboda kuhusu mimba na ndoa za utotoni Kaimu KatibuTawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Abubakari Kunenge amesema idadi ya kesi hizi imepatikana kwa kipindi cha miezi tisa kwa mwaka 2017/18. 

  Aidha Bw. Kunenge amesema kuwa kwa baadhi ya baba wa familia mkoani Rukwa wanadhani wanadhani mimba za utotoni sio tatizo na linafanyika bila kujali madhara yake. ”Suala la mimba za utotoni ni suala la kosa kisheria na ukosefu wa haki ya mtoto ambalo lazima tulikomeshe Mkoani kwetu”.Alisisitiza Bw. Kunenge. 

  Kaimu Katibu tawala huyo pia amesema tatizo la mimba na ndoa za utotoni ni kikwazo kwa juhudi za serikali la kuwa na uwakilishi wa 50/50 katika nafasi mbalimbali za uongozi. Ameongeza kuwa suala la Mimba za utotoni pia linachangia ongezeko la watoto wa mitaani akiutaja mkoa wake kuwa pia uko juu kitakwimu kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wa mitaani. 

  Aidha Dereva boda boda Mkoani Rukwa Bw. Ezekia Kalinga akichangia mjadala wa mimba na za utotoni amesema mazingira ya kusomea wanafunzi sio mazuri kwa sababu baadhi ya mabinti wanasafili umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni. Aidha Bw. Kalinga amesema wanafunzi wasiokuwa wavumilivu kwasababu tu ya ukosefu wa chakula shuleni mwanafunzi anajikuta amejiingiza katika matendo yasiyofaa. 

  Kwa mjibu wa takwimu za jeshi la polisi mkoani Rukwa Wilaya ya Nkasi inaoongoza kwa kuwa na wanafunzi 106 ikifuatiwa na Wilaya za Sumbawanga vijijini 58,Sumbawanga mjini 56 na Wilaya ya Kalambo ni wanafunzi 36.

  0 0

   Pichani kulia ni Muendesha boda boda Magembe Daniel akiwa na Mama yake Mzazi Mama Magembe,wakiwa wameshika mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 140 baada ya kuibuka mshindi wa mchezo wa kubahatisha TatuMzuka hivi karibuni

   Magembe ambaye ni Mkazi wa Kibiti-Rufiji anamshukuru Mama yake Mzazi kwa kumlea vizuri,kama vile haitoshi anamshukuru zaidi kwa kumnunulia Piki piki na kuifanyia biashara,anasema na ndi maana mara baada ya kupata taarifa kuwa nimeshinda mchezo wa TatuMzuka,Mtu kwanza kabisa kumtaarifu alikuwa ni mama yake mzazi, kuwa ameshinda mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,anasema mama yake hakuamini lakini alimtia moyo yakuwa na subira zaidi ili kubaini kama ni kweli ama la.

  "Vijana wenzangu ninaofanya nao kazi wamenisihi nitulie,kwa sababu mara nyingi baada ya kuipata fedha nyingi, vijana hukengeuka,nilijiwekea nadhiri kuwa nikipata fedha nyingi ntafanya biashara zangu,lakini ndoto yangu kubwa ni kujenga nyumba kubwa ambayo ntaishi na familia yangu,ingawaje bado sijaoa",aliongeza kusema Magembe.
  Pichani kulia ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kijana mwendesha boda boda,Mageme Daniel  aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar

  Maganga alisema kuwa mpaka sasa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umevunja historia kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 20 za Kitanzania,ambazo zimekwenda kwa Washindi mbalimbali wa Mzuka Jackpot,Washindi wa Mzuka Daily na washindi mbalimbali,ambapo washindi milioni 58 wamejitokeza kujishindia mamilioni ya TatuMzuka.

  "Tatumzuka imeendelea kuwa fahari ya wachezaji wa mchezo wa kubahatisha kwa sababu ina uwezo wa kutoa washindi wengi,hivyo nawaomba Watanzania waendelee kucheza mchezo huu,na kwamba hamasa kubwa ni kuendelea kuwafikia washiriki wengi zaidi kila kona ya nchi yetu,kuhakikisha mchezo huu unakuwa fahari ya Watanzania,wenye kuwaletea tija ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali",alisema Maganga.
  Pichani kushoto ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa pamoja na  kijana mwendesha boda boda,Magembe Daniel  aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar.

  0 0  Marehemu Mzee Abbas Kandoro enzi za uhai wake


  0 0


  0 0

  Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesisitiza kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali za Tanzania na Kenya ili kuhakikisha bidhaa na mazao ya kilimo yanayozalishwa na wananchi yanapata soko la kuaminika katika ukanda wa Afrika Mashariki hususan Kenya.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda alipotembelea maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya, yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Mhe. Mwangi Kiunjuri tarehe 25 April, 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya. 

  Maonesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo imeambatana na maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Kongamano la biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa mataifa hayo ili waweza kufanya makubaliano ya kibiashara, kupeana uzoefu na kuwezesha bidhaa za viwanda vya Tanzania kupenyeza katika soko la Kenya kama ambavyo bidhaa na huduma za wakenya zilivyoingia katika soko la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

  Aidha, aliongeza ushirikiano huo utasaidia kukuza biashara na uwekezaji na hivyo kuongeza ajira, kuinua pato la taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla. ‘’ Tanzania itaendelea kushirikiana na mataifa yote na itaendelea kufata taratibu na kanuni za biashara zilizokubaliwa kimataifa” alisema Prof. Mkenda

  Vilevile Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji alipata fursa ya kutembelea maonesho hayo ya bidhaa ambapo alisisitiza umuhimu wa kuthamini bidhaa zetu na kwamba Serikali ya Tanzania na Kenya zitaendelea kuimarisha undugu na mshikamano uliopo kama ilivyokubaliwa na marais wa Tanzania na Kenya walipokutana Kampala, Uganda katika Mkutano wa 19 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwataka viongozi katika nchi zao kumaliza vikwazo vya kibiashara. “ Serikali itaendelea kuweka mazingira wezesha kwa wafanyabiashara hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wote kufuata taratibu na masharti katika kufanya biashara zao” alisema Prof. Ole Gabriel .

  Wiki ya Tanzania nchini Kenya imeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia ubalozi wake wa Nairobi, Kenya kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Bara), Wizara ya Viwanda na Biashara (Serikari ya Mapinduzi Zanzibar), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Tanzania ambao walijitoa kwa hali mali katika kudhamini ili kufanikisha Wiki ya Tanzania nchini Kenya.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiongea na wawakilishi kutoka kampuni ya Agricom Afrika Ltd walioshiriki maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya tarehe 27 Aprili 2018.
  Prof. Adolf Mkenda pamoja na maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakipata ufafanuzi wa biashara ya matunda na mboga mboga kutoka kampuni ya Agricom. 
  Prof. Mkenda akipata ufafanuzi wa ubora na matumizi ya mabomba yanayotengenezwa na kampuni ya kitanzania ya PLASCO LTD kutoka kwa Mhandisi Elisaria Aminiel. 
  Mmoja wa Mabalozi wanaowakilisha nchini Kenya akinunua mkanda kutoka banda la kampuni ya kitanzania inayozalisha bidhaa za ngozi WOISO Original Products, Pembeni ni mwakilishi kutoka kampuni hiyo, Bw. Justine Msigwa.

  0 0

  Programu ya Football for Friendship (F4F) 2018 inabadilisha ndoto ya kombe la Dunia la FIFA kuwa kweli kwa Zipora Mollel pamoja na Laigwanani Lomayani Mollel, vijana hao kutoka kabila la Maasai wamechaguliwa kwenda Russia kuiwakilisha Tanzania huku gharama zote zikibebwa na F4F. 

  F4F ni programu ya kimataifa ya watoto ya kila mwaka inayoratibiwa na kampuni ya kimataifa Gazprom ambayo inaunga mkono miradi ya kijamii ulimwenguni na kuweka viwango vipya kuhusiana na sera za kijamii.

  Inatarajiwa kufanyika Moscow, Russia kuanzia Juni 8-15, kuelekea michuano ya Kombe la Dunia, lengo la programu hii ni kutangaza maadili yanayohusiana na mpira wa miguu kwa vijana wadogo ikiwa ni pamoja na kuheshimu mila, utaifa na usawa.

  Laigwanani Mollel ataiwakilisha Tanzania akiwa mchezaji anayechipukia wakati Ziporah Mollel yeye atashiriki kama mwanahabari chipukizi, watakuwa wawakilishi wa nchi kwenye kombe la Dunia licha kwamba timu ya taifa imeshindwa kufuzu katika mashindano hayo. Wataungana na wachezaji wenye umri wa miaka 12 pamoja na waandishi kutoka mataifa 210 na kujumuika kushiriki programu ya siku nane (8).

  Mwaka 2018 mataifa mapya 147 na kanda zitashiriki programu ya F4F inayohusisha watu 3,700 wenye umri kati ya miaka 12 na 16 walioshiriki program hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.

  Laigwanani Mollel na Ziporah (miaka 12) wataambana na meneja wa uendeshaji kutoka Lengo Football Academy, Bw. Amani Mzava, kocha Bw. Alvin Girelisu. Lengo Football Academy inajivunia kushirikiana na Clouds FM na Clouds TV. Mwanahabari mashuhuri wa michezo Shaffih Dauda kutoka Clouds FM/TV ataongozana na msafara wa watanzania kwenda Russia kuiwakilisha Tanzania.

  Jumla ya timu 32 za kirafiki za kimataifa zitashindana katika mechi za kirafiki kucheza mpira wa miguu 'Friendship World Championship' Juni 12, 2018. Kuelekea mashindano hayo  kila mchezaji atafundishwa makocha watoto ambao ambao ni wachezaji wenye umri kati ya miaka 14 na 16 kutoka mataifa tofauti. 

  Zaidi ya vyombo vya habari 5,000 kutoka sehemu mbalimbali Duniani vitaripoti progamu  hiyo kitu ambacho kinatazamiwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni elimu ya kipekee. Vyombo vya habari vitashirikisha waandishi wa habari watoto wa F4F wenye umri wa miaka 12 kutoka nchi 211 wataripoti habari zao za F4F ambazo zitasambaa ulimwengu mzima.

  Fursa hii ni matokeo ya F4F (RUS) programu inayoendelea kwa kushirikiana na Lengo Football Academy (TZ) ambayo imeidhinishwa na TFF. Lengo Football Academy ni shirika la Tanzania na Australia linalosaidia vijana wa Arusha, Tanzania kwa kutumia nguvu ya mpira wa miguu kutengeneza njia kwa vijana kufikia ndoto zao kwenye maisha ndani na nje ya uwanja. Lengo Football Academy inashirikiana na Football for Friendship (F4F) kusaidia nchi 12 kuhudhuria programu ikijumuisha Tanzania, Australia, New Zealand pamoja na nchi 9 za visiwa vya Pasific.

  Emanuel Saakai, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lengo Football Academy amesema, "tunafurahi kushirikiana na Football for Friendship na kupata fursa ya kutoa vijana wawili kutoka kwenye Academy yetu ya Arusha kwenda kupata uzoefu. Tumepata upendeleo kuandaa programu hii kwa nchi nyingi Duniani kote, hakika tutaiweka Tanzania kwenye ramani ya Russia 2018.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akiwakaribisha wageni waalikwa katika ufunguzi wa siku ya Tanzania ambayo huadhimishwa tarehe 26 Aprili siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hafla ya maadhimisho hayo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Ababu Namwamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akihutubia wageni waalikwa waliohudhuria katika mchaparo ulioandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Kenya tarehe 26 April 2018. 
  Viongozi wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya na Mkuu wa Mabalozi nchini Kenya wakikata keki katika kusheherekea maadhimisho ya muungano huo. 
  Viongozi wa Serikali kutoka Kenya na Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa hafla hiyo, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Balozi Macharia Kamau, Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Mhe. Hassan Hafidh, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje, Mhe. Ababu Namwamba na Balozi mteule wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania, Mhe. Kazungu Kambi. 
  Viongozi pamoja na wageni waalikwa wakisherehekea kwa pamoja muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 
  Sehemu ya waheshimiwa mabalozi na Wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha nchini Kenya wakifatilia hafla hiyo. 
  Sehemu nyingine ya wawakilishi hao nchini Kenya wakifuatilia hafla. 
  Sehemu ya mabalozi wa Afrika wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 
  Mhe. Naibu Waziri Namwamba akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri Hafidh. 
  Sehemu ya wajumbe wa kamati ya maandalizi, viongozi na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Muungano. 
  Picha ya pamoja 
  Kikundi cha muziki wa taarabu cha Zanzibar Culture group kikitumbuiza. 
  Wahudumu wakihudumia vinywaji kutoka kampuni za kitanzania.

  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa RUVUMA imeokoa zaidi ya shilingi milioni 21 ikiwa ni marejesho yaliyolipwa kwa watumishi hewa kwenye Idara ya afya.Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa RUVUMA, OWEN JASSON amesema fedha hizo imeokolewa katika kipindi cha Januari mpaka Machi mwaka huu.

  0 0  Wanafunzi wa shahada ya uzamili wa fani za afya wakifuatilia warsha ya maadili ya kitaaluma iliyofanyika katika hospitali ya taaluma na tiba, MAMC
  Kutoka kulia, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, MAMC, Dkt Hendry Sawe, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud, Mkurugenzi wa mafunzo ya Uzamili, Dkt Emmanuel Balandya na Mkurugenzi wa Mafunzo Endelevu na Maendeleo ya Uweledi Dkt Doreen Mloka wakifuatilia ufunguzi wa warsha ya maadili ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili wa afya, MAMC.
  Mratibu wa warsha ya maadili ya kitaaluma ya wanafunzi wa shahada ya uzamili wa fani za afya, Dkt Francis Furia akiongoza kipindi majadiliano wakati wa warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano MAMC
  Mwanafunzi wa shahada ya uzamili, MUHAS akichangia hoja wakati wa kipindi cha majadiliano katika warsha ya maadili ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili wa afya ilitolewa na hospitali ya taaluma na tiba, MAMC iliyopo Mloganzila  Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MAMC iliyopo Mloganzila imefanya warsha ya mafunzo ya maadili ya taaluma kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili.

  Akizungumza katika warsha hii Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud amesema msingi wa huduma zinazotolewa na hospitali ya Taaluma na Tiba, MAMC umemlenga mgonjwa na hivyo kiwango cha hali ya juu cha maadili ya taaluma kinahitakiwa ili tuweze kufikia lengo hili. 
   
  Prof. Aboud amesisitiza kuwa wanafunzi wa shahada ya uzamili katika fani za afya ambao tayari ni madaktari, wafamasia, wauguzi n.k ni nguvu kazi muhimu sana katika hospitali kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wateja ambao ni wagonjwa na pia kuzingatia kutoa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati kwa mgonjwa au ndugu wa mgonjwa.

  Naye Mkurugenzi wa Mafunzo ya Uzamili, Dkt Emmanuel Balandya amekumbusha kuwa MUHAS inazingatia masuala ya maadili ya kitaaluma kwa umakini sana na ndio maana yamesisitizwa wakati walipoanza mafunzo na kufundishwa katika muhula wa kwanza wa masoma. 
   
  Na kwa kuwa mafunzo haya ni endelevu, Dkt Balandya ameeleza, imeonekana ni muhimu kuwa na warsha hii katika kipindi hichi cha mpito kutoka masomo ya sayansi za msingi (basic sciences) kwenda kwenye masomo ya sayansi za kliniki (clinical sciences). Dkt. Balandya amewasisitizia kuwa washiriki wa warsha hii kuwa namna wanavyomjali mgonjwa ni muhimu zaidi kuliko kile wanachokijua.

  "Tunaweza kushindwa kuhakikisha kuwa wagonjwa wote wanapona lakini tunaweza kubadilisha maisha yao kwa namna tunavyowahudumia kwa kuwajali", aliongeza. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MAMC, Dkt Hendry Sawe amesema warsha hii ya maadili ya kitaaluma kwa watu wa fani za afya (madaktari, wafamasia, wauguzi n.k) imelenga namna ya kufanya kazi kitaaluma kwa kuzingatia kanuni za ufanyaji kazi za taaluma husika. 
   
  Hii ni muhimu kwa sababu watoa huduma wa afya wanahusika moja kwa moja na maisha ya watu (wagonjwa). "Mafunzo haya yamejikita kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili kwa sababu wengi wao ni viongozi wajao katika fani mbalimbali za afya nchini", aliongeza Dkt Sawe.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umekabidhi vifaa mbalimbali viwakimo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation ambayo imekuwa ikijihusisha kutoa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu.

  Baadhi ya vifaa hivyo ni viti maalumu vya kusaidia wenye ulemavu ‘wheelchair’ 15, magongo 20, kofia za kujikinga na jua 40 na fimbo maalumu 30 kwa ajili ya watu  wasioona.

  Akizungumza wakati wa tukio hilo la taasisi hiyo kukabidhiwa vifaa hivyo, Katibu wa kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Mohammad Alamiri, amefafanua msaada huo umetokana na mapenzi mema ya ubalozi huo kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania na kuahidi kuendelea kutoa kwa wenye uhitaji.

  "Kwa kipindi cha miaka mitatu, Kuwait imekuwa na utaratibu wa kuzisaidia taasisi mbalimbali zilizopo katika mfumo wake, kwa kuzipatia misaada mbalimbali kwa ajili ya kupunguza changamoto zinazowapata watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu waliopo nchini,"amesema.

  Ameongeza ubalozi wao umekuwa na utaratibu huo unaolenga kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu, wakiwemo walemavu wa ngozi(Albino) watu wasioona na wengineo wenye matatizo ya kutembea wanafaidika na misaada ambapo tayari Sh.bilioni 1.1 
  zimetumika katika mpango huo.

  Amezitaka taasisi zote ambazo zinapata misaada kwa ajili ya kuwasaidia wenye mahitaji kuhakikisha wanafikisha kwa walengwa na kueleza makubaliano ya ubalozi huo na taasisi wanazozipatia misaada hiyo moja ni baada ya kujiridhisha wana moyo wa kusaidia jamii kama ambavyo wanaridhishwa na taasisi hiyo.

  Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania Mohammed Chanzi, ametumia nafasi hiyo kuzikumbusha taasisi kuhakikisha wanafikisa misaada kwa walegwa badala ya kupokea na kubaki nayo.

  Amesema kupokea msaada ni jambo moja lakini kuufikisha unakokwenda ni jambo la pili na hivyo ametoa rai kwa taasisi na mashiriki pindi yanapopewa misaada basi iwe inafika na kupongeza taasisi hiyo kwa uaminifu wao ambao umesababisha Ubalozi wa Kuwait kuwa karibu nao na kusaidia jamii ya Watanzania.

  Amesema kwa kufanya hivyo anaamini kutaendelea kuwavutia wadau mbalimbali, zikiwemo balozi zingine kujitokeza na kutoa misaada hiyo na hivyo kuwanufahisha walengwa kulingana na mahitaji yao.

  Naye Mkurugenzi Mwazilishi wa taasisi ya kuhudumia watoto wenye shida mbalimbali cha Humanity Actions for Children Foundation Rahma Abdallah pamoja na kuushukuru ubalozi wa Kuwait kwa misaada hiyo, amesema tayari ofisi yake imeweka utaratibu wa kuigawa misaada hiyo kwa walengwa wakati wowote kuanzia wiki ijayo.

  Amesema kuanzishwa kwa taasisi hiyo, zaidi kulilenga kuhakikisha mtoto na watu  wenye matatizo mbalimbali wakiwemo walemavu  wanapata huduma mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

  Mwenyekiti wa Humanity Actions for Children Foundation Rashid Mchujuiko  amelezea kufurahishwa na msaada huo wa Ubalozi wa Kuwait ambapo naye amesisitiza lazima vifaa hivyo vifike kwa walengwa na itakuwa ni tukio la wazi ili umma ujue.
   Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akikabidhi kiti  maalum cha walemavu kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation leo jijini Dar es Salaam .Kulia kwake ni Mkurugenzi Mwanzilishi wa taasisi hiyo Ramha Abdallah.
   Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akikabidhi 
  kofia kwa ajili ya kuzuia mwanga wa jua kwa Mkurugenzi Mwanzilishi wa taasisi hiyo Ramha Abdallah (kulia) leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha albino nchini Mohammed Chanzi.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania Mohammed Chanzi (aliyesimama) akizungumza kabla ya Ubalozi wa Kuiwat nchini Tanzania kutoa msaada wa vifaa kwa ajil ya watu wenye mahitaji maalum kwa Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Kwanza wa Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania Mohammad Alamiri(katikati) akisaini kitabu cha wageni baaada ya kuwasili  katika Taasisi ya Humanity Actions for Children Foundation kabla ya kukabidhi vifaa kwa taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.Wakwanza kulia Katibu Mkuu Chama cha Albino Mohammed Chanzi na kushoto Mkurugenzi Mwazilishi wa taasisi Rahma Abdallah.

  0 0

  Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli ndugu Edward Lenanu Laizer amejiuzulu rasmi nafasi yake ya udiwani kata ya Naalarami na kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM leo tarehe 28/04/2018.
   Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli ndugu Edward Lenanu Laizer  akiwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli na kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na chama cha CCM leo April 28, 2018

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Taasisi ya Tulia Trust imezindua Tulia Marathon itakayofanyika Mei 6 katika uwanja Sokoine jijini Mbeya.

  Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Tulia Marathon, Mratibu wa mashindano hayo na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema kuwa mashindano ya mbio hizo kwa fedha zitakazopatikana ni kwa ajili ya afya hususan afya ya mtoto kwa jamii ya Mbeya.

  Dk. Tulia amesema kuwa amekuwa anaungwa mkono na wadhamini katika kufanikisha taasisi hiyo kuendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali katika kuandaa michezo.Amesema kuwa mashindano ya mbio hizo yatakuwa na muonekano tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika nchini kutokana na kujumuisha kila kundi katika jamii.

  Aidha amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya kilomita 42 Full , Half Marathon 21 , wanafunzi kwa mbio za kilomita Tano , mbio za baiskeli kilomita 150 kwa wanaume na kilomita 75 kwa wanawake, Kilomita tano watakimbia watu kwa ajili ya kujifurahisga pamoja na watoto watakimbia kilomota mbili.

  Fomu kwa ajili ya maombi ya kushirikia mashindano ya Tulia Marathon zinapatikana katika tovuti yawww.tuliatrust.org

  Wadhamini wa mashindano ya Tulia Marathon hayo ni Mo Dewj Foundation, Mantra Tanzania, Tatu Muzuka pamoja na Derm Electrics T LTD.
  01.Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa Tulia Marathon itakayofanyika Mbeya, leo jijini Dar es Salaam.
  02. Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga akizungumza kuhusiana na kudhamini mashindano ya Tulia Marathon
  Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akimkabidhi tshirt, Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga kwa kutambua mchango wa Tatu Muzuka katika kudhamini mashindano hayo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya wagonjwa wawili; Suzana Athanas John (22) na Asha Atuman Kisabengo (28) kupandikizwa figo kila mmoja na kuruhusiwa kurejea nyumbani leo. Kutoka kushoto ni mtaalamu katika vyumba maalumu vya wagonjwa wa waliopandikizwa figo, Elizabeth Sephen, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Onesmo Kisanga na Dkt. Muhidini.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akitoa maelezo ya awali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu upandikizaji figo kwa wagonjwa wanne. Upandikizaji huo ulianza tarehe 16-18 Aprili, 2018.
  Asha Kisabengo (28) akiwashukuru madaktari na wataalamu wengine kwa mwezesha kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupandikizwa figo katika hospitali hiyo.
  Mtaalamu kwenye vyumba maalumu vya wagonjwa wa waliopandikizwa figo, Elizabeth Stephen akieleza jinsi walivyokuwa wakitoa huduma maalumu kwa ndugu waliotoa figo na kwa wagonjwa waliopandikizwa figo hadi kufanikiwa kuruhusiwa kurejea nyumbani leo.
  Asha Kisabengo akilia kwa furaha baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kupandikiza figo na kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi.
  utoka kulia ni Suzana Athanas John (22) na Asha Atuman Kisabengo(28) wakiwa katika picha ya pamoja.
  Wauguzi, ndugu waliotoa figo na waliopandikizwa figo wakiwa katika picha ya pamoja.  Dar es salaam, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeweka mipango ya muda mrefu na muda mfupi ili kuhakikisha huduma ya upandikizaji figo inakuwa endelevu, na imedhamiria kupandikiza figo kwa wagonjwa zaidi 200 kwa mwaka.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dare es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuruhusiwa wagonjwa wawili ambao wamepandikizwa figo Aprili mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Amesema katika mpango wa muda mfupi, kila mwezi hospitali hiyo itapandikiza figo wagonjwa watano, hivyo kwa mwaka itakuwa imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 60.

  “Mipango ya muda mrefu ni kuwa na sehemu maalum ya upandikizaji figo na hivi karibuni MNH itaanza ujenzi wa jengo jipya la ghorofa saba na katika jengo hilo tutatenga sehemu maalum ya upandikizaji figo , kila siku mgonjwa mmoja atapandikizwa figo, kwa wiki tutakuwa tumepandikiza figo wagonjwa watano, kwa mwezi wagonjwa 20 na kwa mwaka tutafanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 240,’’ amesema Aminiel.

  Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya Figo Muhimbili , Dkt. Jacqueline Shoo amesema tukio hilo ni la kihisoria kwani mwaka jana hospitali ilifanikiwa kupandikiza figo mgonjwa mmoja na Aprili mwaka huu hospitali hiyo imepandikiza figo wagonjwa wanne kwa mfululizo.

  Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo MNH, Dkt. Onesmo Kisanga amesema takribani wagonjwa 800 nchini wanasubiri huduma ya upandikizaji figo na kati ya hao 50 tayari wameandaliwa.

  Kwa upande wao wagonjwa waliopandikizwa figo na kuruhusiwa leo, Bi. Suzana John na Bi. Asha Athuman Kisebengo wameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbii pamoja na waaalam wake kwa kuwapatia matibabu ya ubingwa wa juu ambayo awali hayakuwepo nchini.

  0 0

  Kampuni ya nguo la Woolworths imefungua duka mpya la nguo lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, likiwa ni duka la tano la kampuni hiyo kwa hapa nchini.

  Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki alisema huo ni mwendelezo kampuni hiyo kufungua maduka ambayo yanauza nguo zenye viwango bora na hivyo kuwataka wananchi kutembelea maduka hayo ili kununua nguo.

  Alisema baada ya ufunguzi wa duka hilo wamejipanga kufunga duka lingin makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwasogezea bidhaa zao wateja wao na hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa serikali wamehamia mkoani humo.

  "Ni hatua nzuri kwenda mbele, uchumi kwa sasa ni mgumu, wakati wengine wafunga maduka sisi tunafungua kubwa nchini kuliko yote, tumeweza kudhibiti mdororo wa uchumi pamoja na kuwa tumeshindwa kufikia malengo yetu lakini tumekuwa imara,

  "Kuanzia mwaka kesho tutaanza kuangalia ujenzi wa duka Dodoma, Dodoma ni makao makuu ya nchi, wapo viongozi wa Serikali na hakuna huduma kama hizi. Tumeanza kuongea na wajenzi ili katika miaka miwili ijayo tufungue duka Dodoma," alisema Mafuruku.

  Aidha alizungumza kuhusu wafanyabiasha ambao wanakwepa kodi ambapo kuhusu kampuni yao alisema wamekuwa wakilipa kodi zote ambazo wanatakiwa kulipa na kutumia nafasi hiyo kuwataka wanaokwepa kulipa kodi waache tabia hiyo.

  "Mtu anayefanya biashara kwa kutokuwa mwaminfu ipo siku atapambana na serikali, ila sisi sitaki kusikia mfanyakazi anakuja kusema bosi hii pesa nimemhonga mtu wa TRA, sisi kila siku tunawafundisha wafanyakazi wetu walipe kodi zote, hata kama ni kubwa," alisema.
  Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akikata utepe kuashirikia ufunguzi wa duka duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Rabi Hume)
  Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akiingia katika duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 

older | 1 | .... | 1571 | 1572 | (Page 1573) | 1574 | 1575 | .... | 1898 | newer