Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1570 | 1571 | (Page 1572) | 1573 | 1574 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (kulia) akionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu hiyo mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati).   Meneja wa Kitengo cha Ushirikiano wa Biashara wa TECNO Tanzania, Anuj Khosla (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto), Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati), Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya (wa pili kulia) pamoja na Meneja Msaidizi wa Masoko wa TECNO Tanzania, William Motta  wakionesha simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu mpya ya TECNO Camon X inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. .
  Mwandishi wa Habari, John Dande (wa pili kulia) akipokea kutoka kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Biashara wa Tigo, David Umoh (wa pili kushoto)  zawadi ya simu janja mpya aina ya TECNO Camon X aliyoshinda katika droo maalum iliyofanyika wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa simu hiyo mpya ya TECNO Camon X iliyofanyika katika ofisi za kampuni ya simu ya Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Simu janja za TECNO Camon X zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na kwenye duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00#. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na kushoto ni  Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania, Eric Mkomoya.  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania inaungana na kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kupanua wigo wa matumizi ya simu janja (smartphone) nchini pamoja na kuwapa wateja huduma bora zaidi za kidigitali, huku wakizundua simu mpya yenye uwezo wa 4G aina ya TECNO Camon X. 

  TECNO Camon X imejazwa of ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata fursa ya kufurahia  huduma za kipekee za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. 

  ‘Tigo ipo katika kilele cha mageuzi ya kidigitali na ndio mtandao wa kwanza na pekee wa simu za mkononi nchini ambapo wateja wataweza kujipatia simu janja, za kisasa zaidi, zenye uwezo wa 4G za TECNO Camon X kupitia maduka yetu yote ya Tigo. Pia wateja wetu wana fursa ya kununua simu hizi janja za TECNO Camon X kwa njia ya kulipia kwa awamu kutoka kwa duka la simu la Tigo kwa kupiga *147*00#,’ Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alibainisha.


  Meneja Uhusiano wa TECNO Tanzania Eric Mkomoya alisema ‘Tunafurahia ushirikiano huu utakaowezesha upatikanaji wa bidhaa murwa na ofa kabambe kwa Watanzania kupitia mtandao mkubwa, wa uhakika na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hii ni hatua kubwa ya ukuaji wa soko la simu nchini itakayowezesha wateja kupata simu janja ya kisasa zaidi ya TECNO Camon X kwa wakati ule ule ambapo simu hiyo inazinduliwa kote duniani”.

  Umoh aliongeza kuwa, ‘Tigo inalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya zimu janja za kisasa nchini, huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma bora zaidi za intaneti kupitia mtandao wetu mpana na uhakika zaidi nchini wa Tigo 4G. Ndio maana Tigo inatoa ofa ya 3GB intaneti bure kila mwezi kwa miezi sita kwa wateja wote watakaonunua simu janja ya TECNO Camon X.’

  Simu inayotumia kadi mbili ya TECNO Camon X ina kioo cha kikubwa cha inchi 6, uwezo wa 3GB RAM, memori ya 16GB, camera ya mbele yenye uwezo wa  20MegaPixel (MP) na camera ya nyuma yenye uwezo wa 16 MP pamoja na uwezo wa kutambua sura. Simu hiyo pia inakuja na garantii ya miezi 13. Vyote hivi vinaifanya simu hii kuwa bora kwa mtumiaji anayehitaji simu bora. Simu janja ya TECNO Camon X itapatikana kwa bei ya TSH 449,999/- na inapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini, katika duka la bidhaa la Tigo kwa kupiga namba *147*00# na kwenye duka la mtandao la www.jumia.co.tz/tigo-shop.


  0 0
 • 04/26/18--06:11: TCCIA YAZINDUA HUDUMA YA TYM
 • Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akizundua huduma mpya ya TMY leo, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda ​akifwatiwa na Patrick Emmunel Meneja Maendeleo ya Viwanda TCCIA, wa Mwisho kulia ni Helen Mangare Afisa Uhusiano Eag akifatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

  CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua huduma ya ‘TCCIA Youth Membership’ (TYM) ambayo ni uanachama wa vijana kwenye chama hicho.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais wa TCCIA, Octo Mshiu alisema mpango huo umekuja kufuatia chama hicho kutambua umuhimu wa Vijana na Wanawake ambapo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka ilipitisha mabadiliko ya katiba yake ambapo iliweza kuingiza uwakilishi wa wanawake na vijana kwenye TCCIA.Mshiu alisema Kutokana na kutambua umuhimu huo TCCIA kwa kushirikiana na washauri wake wa Biashara na Masoko tumeweza kuanzisha huduma hii muhimu ya Wanachama Vijana.
  Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa TYM, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

  “ Wote tunatambua kwamba ajira ni changamoto kubwa Duniani na Tanzania pia, hivyo kuwajenga na kuwaandaa vijana kujiajiri na kuboresha uelewa wao wa biashara ni jambo la muhimu sana, “alisema Mshiu.Aliongeza kuwa ili kujenga Taifa lenye tija, mafanikio na uwezo wa kutumia fursa zilizopo ndani ya Tanzania, kanda ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia ni kuwa na vijana waliondaliwa vyema kwenye ujasiriamali huku ujuzi likiwa ni jambo la msingi.

  Tunaamini kwa dhati kabisa kuwapa fursa Vijana ya kuwa wanachama wa TCCIA sio tu itawaongezea upeo wa kujua biashara bali pia kuwapa fursa ya kujifunza kutoka kwa wanachama waandaminizi wanaomiliki biashara na viwanda, ’’alisema..

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Gotfrid Muganda alisema TCCIA imedhamiria kuwa muhimili wa kusaidia akinamama na Vijana kufikia malengo yao ya kuwa wafanyabiashara wabobezi, kwani moja ya malengo ya kuanzishwa kwa TCCIA ni kukuza biashara.Kwa upande wa Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Masoko na Biashara wa TCCIA, Imani Kajula alisema lengo moja wapo kuu la TCCIA ni kujenga vizazi nyenye uwezo wa kufanya biashara, hivyo TYM ni huduma maalum ya kuvutia na kuongeza uwezo wa vijana sio tu kuwa wajasiriamali wazuri bali pia kuona Zaidi fursa na kuzitumia..Kajula alisema TYM itaendelea kufungua matawi kwenye vyuo, mikoa na maeneo mbalimbali Nchini ambapo wiki hii inatarajia kuzinduliwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baada ya hapo vyuo vingine vitafuata.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula. akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo mbele ya waandishi wa Habari kulia kwake ni Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu.Alisema TYM itawapa fursa vijana kujifunza kutoka kwa wanachama wazoefu, kubadilishana mawazo, kupata fursa ya mafunzo na pia mijadala ya biashara, kilimo na viwanda.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika jukwa kuu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Wananchi, Magereza na Polisi vikipita kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Kikosi cha Makomando wa (JWTZ) kikipita na kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


  0 0

  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  MKOA wa Dar ea Salaam umeadhimisha miaka 54 ya Muungano kwa kutoa misaada ya chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

  Akizungunza leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema misaada iliyotolewa ni pamoja na magodoro, chandarua, nashuka, mito, sukari, unga,mchele pamoja na mafuta ya kupika.

  Makonda amesema misaada hiyo itagawanywa kwa familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na mafuriko lengo likiwa ni kusaidia familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwa tabu baada ya mvua kuharibu vyakula na mali.

  Aidha amezishukuru taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.

  Pia amesema kuwa Mkoa umeandaa mkakati wa kukabiliana na mafuriko ya mara kwa mara ambapo hivi karibuni atahitisha mkutano na wananchi wote waishio mabondeni ili kuangalia namna bora kutatua suala hilo.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman wamesema wameamua kutumia siku ya muungano kuzikumbuka na kusaidia familia ambazo zimekumbwa na mafuriko na sasa zinaishi kwa tabu.

  Aidha wamempongeza Rais Dr. John Magufuli kwa kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akipokea msaada wa chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center,Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza leo katika hafla ya kupokea msaada.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwashukuru viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center leo.

  0 0

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.

   "Tumeona mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu ashindwe kuongea tuanze michango," alisema nyerere. "Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha," amesema Nyerere.

   Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC) Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza kutupa tiketi 2 za ndege. Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla. 

  Nyerere amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli. Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone. "Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango yote mje kunichukua," amesema. Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.
  Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akimsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiongea machache mara baada ya kumtembelea Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mzee Majuto akitoa shukrani zake mara baada ya kutembelewa na kuonyeshwa mwanga wa matibabu zaidi nchini India.
  Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.
  Kicheko kidogo...
  Mtoto wa Mzee Majuto, Hamza akitoa shukrani kwa wasanii waliofika kumsalimia baba yake.
  Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiteta jambo na Mzee Majuto.  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania


  Miongoni mwa mikoa maarufu nchini Tanzania ni pamoja na Tanga. Ukiachana na ukaribu wake na jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Tanga una utajiri wa utamaduni wa Waswahili wanaopatikana katika pwani ya bahari ya Hindi, makumbusho ya kihistoria, shughuli za uchumi na kibiashara, pamoja na wanasiasa na wanasanaa mbalimbali mashuhuri wanaolipeperusha vema jina la mkoa huu.   

  Hivi karibuni mkoa wa Tanga umekuwa ni eneo mojawapo la kitalii linalokua kwa kasi na kuwavutia watalii wengi ndani na nje ya Tanzania. Watalii wengi kupendelea kwenda Tanga kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa zikiwemo miongoni mwao tayari wamekwishatembelea sehemu zingine, kupata simulizi kutoka kwa watu wao wa karibu pamoja na vivutio vingine ambavyo havipatikani sehemu zingine isipokuwa Tanga.

  Jumia Travel imekukusanyia baadhi ya sababu ambazo zimepelekea watu wengi kupendelea kwenda kutalii mkoa wa Tanga:  

  Jiografia. Asilimia kubwa ya watalii hupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo katika jiji la Dar es Salaam. Umbali uliopo kati ya jiji hili na mkoa wa Tanga sio mkubwa, huchukua muda wa takribani masaa 6 kitu ambacho watalii wengi huweza kumudu. Hii imerahisisha shughuli za kitalii kwa urahisi kwa sababu watalii wanaweza kwenda na kurudi kwa urahisi. 

  Vivutio vya kitalii. Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali ambavyo haviwezi kupatikana sehemu nyingine. Tanga inazo mbuga kama vile Saadani, Mkomazi, na Jozani ambazo unaweza kujionea wanyama, ndege na mimea ya aina mbalimbali lakini pia ina maeneo kama vile mapango ya Amboni na makumbusho ya kale ambayo yamebeba historia na urithi wa mkoa huo tangu enzi za wakoloni.   

  Hali ya hewa. Miongoni mwa mji mashuhuri kwa shughuli za kitalii hivi sasa mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla ni Lushoto. Hali ya hewa nzuri, mandhari ya kuvutia na hoteli za kitalii katika eneo hili zimekuwa ni hamasa kubwa kwa wasafiri wengi. Eneo la Lushoto ambalo linapatikana kwenye safu ya milima ya Usambara limejizolea umaarufu kutokana na shughuli tofauti za kitalii kama vile matembezi na kupanda milima, shughuli za uvuvi, kuendesha baiskeli, kutembelea makumbusho ya kale, nakadhalika. Na kwa kuongezea eneo hili limewekezwa kwa hoteli za kisasa za kitalii.   

  Hoteli za kitalii. Kutokana na kuwepo kwa shughuli nyingi za kitalii, kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika huduma ya malazi. Miongoni mwa changamoto kubwa inayoikumba sekta ya utalii nchini na duniani kote ni huduma ya malazi. Malazi ni huduma ambayo huwa ghali ukilinganisha na huduma nyingine kama vile usafiri wa kwenda na kurudi, viingilio na makato mengineyo. 

  Mkoa wa Tanga umejitahidi kwa hilo, wafanyabiashara wengi wamejenga hoteli ili kuweza kukidhi haja ya kila aina ya mtalii. Si jambo la kushangaza kukuta hoteli za kitalii karibu na vivutio vya kitalii.        

  Gharama nafuu. Miundombinu kama vile barabara imewavutia watu wengi kwenda kwa urahisi kutalii vivutio vya mkoa wa Tanga kwani imerahisisha gharama za usafiri. Ukiachana na usafiri wa mabasi yanayokwenda na kurudi kila siku, watu wengi siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia usafiri wao binafsi. Unafuu pia upo kwenye huduma ya malazi ambayo kila mtu anaweza kumudu pamoja na gharama za kuishi kwenye jiji hilo kwa ujumla.  

  Ukarimu wa watu wake. Watu wa Tanga wanasifika kuwa na haiba ya ukarimu kama walivyo watanzania wengi nchini. Hiki nacho kimekuwa ni kivutio kingine kwa watalii wengi kutembelea eneo hilo. Ukarimu huwavuta watalii wengi, kuwajengea hali ya usalama na kujifunza mengi kutoka kwa wenyeji wao. Wakazi wa Tanga wanatoa mchango mkubwa katika kulitangaza jiji lao kitalii kwa kuwapokea wageni na kuwafunza mambo yanayopatikana mkoani mwao.  

  Kama ulikuwa unafikiria sehemu ya kwenda kutalii tofauti na sehemu ulizozizoea, Tanga itakuwa ni chaguo sahihi kwa hivi sasa. Ni miongoni mwa sehemu zinazofikika kwa urahisi na unaweza kufanya shughuli nyingi ndani ya muda mfupi na kurejea kwenye majukumu yako ya kawaida.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  KATIKA kuadhimisha Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kampuni ya simu ya Airtel Tanzania sambamba na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA), wamekuja na mbinu mpya ya kutoa mafunzo kupitia simu ya mkononi.

  Akizungumza na Michuzi blog Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde ameeleza leo jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na VETA wameamua kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kupitia apllication ya Vsomo inayopatika playstore bure kabisa ambayo baada ya kusoma ukifaulu kwa asilimia 40 atachaguliwa katika VETA iliyokaribu kuweza kuendelea na masomo.

  Aidha ameeleza zaidi ya kozi 11 zinapatikana, hivyo vijana wanatakiwa kupakuwa application hiyo ili kujifunza kozi mbalimbali kama vile umeme wa majumbani na malipo ya kozi hizi ni shilingi laki moja na ishirini pekee.Kwa upande wa Meneja mradi wa Vsomo kutoka VETA Charles Mapuli ameeleza hadi sasa waliopakua application hiyo wapo zaidi ya 3500, waliosajiliwa 10,800 na waliosoma na kufanya mitihani wapo 120.

  Pia masomo hayo ni ya muda mfupi kwa miaka miwili hadi mitatu na itawasaidia vijana wengi kufikia malengo yao na kufikia azma ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

  Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es salaam kuhusiana na fursa ya Vsomo ambaye inatoa fursa ya kusoma masomo ya ufundi kupitia simu ya mkononi.
  Katibu mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu akisikiliza maelezk kutoka kwa Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde kuhusiana na kusoma kupitia simu ya mkononi maarufu kama VSOMO.
  Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza meneja wa Vsomo,Charles Mapuli kutoka VETA katika maonesho ya siku ya kitaifa ya mtoto wa kike na Tehama leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
  Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

  Wanafunzi wa kidato cha sita wapatao 451 wa  shule ya wavulana Kibiti Boys  iliyopo wilaya  ya kibiti  Mkoani  wakisikiliza kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele alipotembelea shule hii mapema wiki katika kuwajengea uwezo katika maandalizi yao ya mitihani ya mwisho na pia kuwapa dondoo za mafanikio katika maisha kwa ujumla.

  Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa Mkurungezi wa KONCEPT  Krantz  Mwantepele  Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

  Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti wakionesha kuwa wamehamasika na nasaha zilizotolewa na Mkurungezi mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
  Mkuu wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys Dismas Njawa akifafanua jambo kabla ya kufunga kongamano hilo lililoendeshwa na Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele . Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
  Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT akifurahi jambo na Mkuu wa shule ya wavulana Kibiti Boys  Dismas Njawa mara baada ya kumaliza kongamano.Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

  Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
  Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katikaa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys mara baada ya Kongamano.Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.


  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,  Dkt. Akinumwi  Adesina, amesema Benki hiyo imeridhishwa na utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini kwani inachochea mageuzi katika maisha ya wananchi .
   Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma na kutembelea  kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa  benki hiyo inatambua na kupongeza juhudi za  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
  Dkt. Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la upatikanaji wa umeme katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo Burundi na Kenya.
  Alisema kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha na nchi jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75 kufanikisha mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.
  "Umeme ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa binadamu, ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa hiyo uchumi bila umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt. Adesina
  Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali ili mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa ajili ya kujenga mradi wa nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa nchi.
  "Vile vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi cha dola za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya kujenga mradi wa umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili kuboresha na kuwa na umeme wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya viwanda nchini" alisema Dkt. Adesina
  Alisema kuwa kwa ujumla Benki yake katika kipindi cha miaka miwili ijayo (2018/2019 na 2019/2020) Benki yake itatoa kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.5 katika sekta ya umeme na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo itawawezesha wazalishaji mali wadogo, wa kati na wakubwa kuzalisha bidhaa na mali mbalimbali na hivyo kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
  Kituo cha kupoza umeme zuzu ni sehemu ya mradi wa umeme unaonufaisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga ambapo vijiji zaidi ya 121 vimeshanufaika na maradi huo   wa uzalishaji na usambazaji wa umeme kwa mikoa husika.
  Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
  Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali ya Tanzania inashukuru kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na kusaidia Serikali katika uwekezaji mkubwa unaogusa  nyanja mbalimbali ikiwemo nishati na miundo mbinu mingine kama barabara.
  Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe.  Subira Mgalu amesema kuwa Benki hiyo ni mshirika wa kweli katika sekta ya nishati na imewezesha kufanikiwa kwa miradi mbalimbali ya umeme ukiwemo ule unaoinifaisha mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma, Shinyanga na Dodoma.
  Miradi inayotekelezwa hapa nchini kwa sasa  kupitia ufadhili wa Benki ya AfDB imefikia  zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
  Ushirikiano wa AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971 na mpaka sasa benki hiyo imeipatia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.6, karibu shilingi trilioni 8 za Tanzania.
   Rais wa AfDB  yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
   Naibu Waziri wa  Nishati Mhe. Subira Mgalu akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme  cha zuzu mkoani humo .
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip  Isdori  Mpango ( Mb)  akimuongoza   Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini  Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme  cha zuzu mkoani humo.
   Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina akisalimiana na Mhandisi  Peter  Kigadi mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme  cha Zuzu mkoani humo .
   Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina akisisisitiza jinsi Benki hiyo inavyoridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa nishati hali itakayochochea maendeleo.
   Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Mkoani Dodoma Bw. Joseph Mongi akitoa maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi wakati wa ziara ya Rais  wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina katika kituo hicho.
   Sehemu ya Miundombinu ya kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma kama inavyoonekana.
   Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati  Mhe. Subira Mgalu.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip  Isdori  Mpango (Mb)   na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu,  wakimuongoza    Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt.  Akinumwi Adesina kukagua miundombinu ya Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0


  0 0

  AMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imejivunia ufanisi wa huduma ya mafuta iliyotoa kwa ndege kubwa aina ya Airbus 380 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Emirates iliyotua kwa dharura Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza alisema hatua hiyo ni sehemu ya uthibitisho kuwa Tanzania kupitia kampuni ya Puma Energy ina uwezo wa kutosha kutoa huduma ya nishati hiyo hata kwa ndege kubwa zaidi duniani.

  “Uwezo wa kutoa huduma ya nishati ya mafuta kwa ndege kubwa kama hizi tena kwa ufanisi ni moja ya kivutio muhimu kwa mashirika mengine makubwa kuweza kuleta ndege zao hapa nchini hasa kipindi hiki ambapo Serikali imejipanga kuleta mageuzi katika sekta ya anga hivyo Puma Energy Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya kuwezesha mageuzi hayo,’’ alisema.

  Akizungumzia zoezi hilo lililofanyika mapema siku ya Jumatano kabla ndege hiyo haijaondoka hapa nchini kuelekea Mauritius, Meneja wa Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopo JNIA, Mohammed Ngayahika alisema lilifanyika kwa kasi na ufanisi mkubwa likihusisha jumla ya lita 98,709 za nishati hiyo.

  “Kwa hapa nchini Puma Energy ndio yenye uwezo pekee wa kujaza mafuta kwenye ndege kubwa kutokana na uwekezaji mkubwa iliyoufanya kwenye vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa ‘kupump’ mafuta kwa kasi kubwa kama tulivyofanya kwenye zoezi hili ambapo tulisukuma mafuta kwa kasi ya lita 2,800 kwa kila dakika moja na hivyo kufanya zoezi hili kuwa rahisi sana tena kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia taratibu zote za kiusalama,’’ alisema.

  Naye, Emmanuel Ngowi kutoka kampuni hiyo ambae ndiye aliyeendesha zoezi hilo alisema baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Shirika la Ndege la Emirates lilionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma hiyo hatua ambayo muhimu katika muendelezo wa biashara. “Kwa muda mrefu Puma Energy tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’. aliongeza

  Ndege hiyo iliyopaswa kutua nchini Mauritius , ilitua kwa dharura uwanjani hapo majira ya saa 7:15 mchana ikiwa na abiria 475 kufuatia hali mbaya ya hewa kwenye uwanja ilipotakiwa kutua nchini humo.
   Mtoa huduma ya Mafuta ya ndege wa kampuni ya Puma Energy katika Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopoUwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam BwEmmanuel Ngowi akisimamia ujazaji wa mafuta kwenye ndege kubwa aina ya Airbus 380 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Emirates iliyotua kwa dharura kwenye uwanja huo hivi karibuni.
   Zoezi la ujazaji mafuta likendelea…!
   Kisha taratibu zote za manunuzi zilifuatwa!


  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

  MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza Vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanzania, kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao.

  Pongezi hizo alizitoa jana Mara baada ya Mchezo huo uliofanyika katika Viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi, ambapo vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM waliibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya timu ya Vijana wa Bodaboda na kuwapatia kila timu mbuzi mmoja na mchele kilo 20 kwa ajili ya kudumisha na kuuenzi Muungano.

  Brigedia Gaguti alisema Vijana hao wameonesha Mfano mzuri wa kuigwa na wameienzi falsafa ya Muungano kwa kitendo walichokifanya na kuwataka Vijana hao kuendelea kudumisha umoja na mshikamano hata katika maendeleo ili kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unasonga mbele,kufanya kazi kwa bidii pamoja na Kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Nitoe pongezi kwa Vijana wa kigoma kwa Viongozi wa UVCCM na Boda boda kwa hili mlilolifanya la kudumisha Muungano na kuuenzi na kuudumisha , lakini kubwa zaidi mmetoa funzo kwa mchezo huu mlioufanyam, hili ni funzo hata kwa vijana wengine na Watanzania wote mnatakiwa kuishi kwa ushirikiano sio kwa michezo tu hata katika Mambo mengine ya maendeleo ili kuendeleza umoja, mshikamano na uzalendo kama Watanzania bila kujali itikadi za Vyama vyetu", alisema Mkuu huyo.

  Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kigoma Silvia Sigura alisema Wao kama Viongozi wa Vijana walibuni mchezo huo katika sikuku ya Muungano,lengo likiwa ni kuwaunganisha Vijana wa Mkoa wa kigoma kuwa wamoja na kuendeleza ushirikiano katika kuuinua Mkoa wa Kigoma.

  Alisema Michezo ni Afya,ni jambo linaloweza kuwaunganisha Vijana kwa umoja na kuendelea kushirikiana katika Mambo mbali mbali,na Kuwaomba Vijana kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri  ili kudumisha amani na mshikamano wa Taifa la Watanzania bila kuangalia Vyama vyao na kuendeleza umoja na mshikamano katika kazi na mambo mbali mbali ya Kijamii.

  Nao baadhi ya Vijana wa boda boda walioshiriki katika Mchezo huo January Exavery alisema wanaushukuru sana uongozi wa UVCCM mkoa wa Kigoma kwa Kuandaa mchezo huo wa kirafiki na kuomba ushirikiano huo waliouanzisha uendelee na kuwaasa vijana wengine waachane na ushabiki wa Vyama vya siasa kwa kufanya mambo yasiyo na msingi na wafanye kazi.

  Alisema Rais anafanya kazi kibwa kuhakikisha Wananchi wanapata hiduma bora na maendeleo na kuwaasa Vijana kiwa Wakati huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kushirikiana na sio wakati wa kukaa vijiweni na kuzungumzia siasa zisizo na Maendeleo na Wafanye kazi kwa bidii ilikuondokana na Umasikini.
  MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza wakati akiwapongeza Vijana wa Kigoma kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao kwa dhana ya kuuenzi Muungano wa Tanzania, .

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa upandaji miti, kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, kushoto ni Mhe. Ferdinand Wambali,Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akipanda mti wake.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipanda mti.
  Watumishi na Wadau mbalimbali nao walishiriki katika zoezi la kupanda miti.

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza jambo, ameipongea Mahakama kwa kupata eneo zuri kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
  Jaji Muumuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akitoa neno kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Kiwanja cha Mahakama itakapojengwa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania mkoani Dodoma.   Baadhi ya wafanyakazi wa Mahakama na wadau mbalimbali wakiwa katika tukio hilo.
  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Dodoma, Mhe. Mwanaisha Kwariko akizungumza katika Sherehe hizo.
  (Picha na Mary Gwera)

  0 0

  Balozi Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba yake.aliyelezea mambo mbalimbali ikiwemo kuitangaza Tanzania katika maswala ya utalii ikiwemo uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani. Katika hotuba hiyo Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliongelea jinsi ya nchi ya Tanzania ilivyokua na amani na salama kwa watalii kwenda Tanzania kwenda kujionea vivutio mbalimbali na katika kuimarisha utalii, Serikali ya awamu ya tano chini ya Rasi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amenunu ndege sita za usafiri zikiwemo tatu ambazo zimeshaanza kufanya kazi na zinginge tatu zitawasili ifikapo mwezi wa June mwaka huu ikiwemo ndege kubwaya Dreamline. Katika sherehe hiyo video ya vivutio mbalimbali zikiwemo mbuga zetu za hifadhi ya taifa zilikua zikionyeshwa.
   Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ) akisoma hotuba yake na kuelezea uhusiano wa Marekani na Tanzania tangia zaiara ya baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alivyotembelea Marekani mwaka 1963 enzi hizo ikiongozwa na Rais John Kennedy.
  Mshereheshaji Julia Nyerere akisisitiza jamabo na utaratibu wa kitu gani kinafuata
  Mapokezi wakihakikisha kila mgeni anapokelewa vizuri na kwa ukarimu kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production chini ya udhamini wa Kilimanjaro Studio.
  Kulia ni Balozi wa Tanzania nchiniMarekani Mhe. Wilson Masilingi akifuatiwa na mkewe Marystela Masilingi wakiwa pamoja nae Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakijiandaa kupokea wageni waalikwa kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani.
  Wageni wakiwasili huku wakisalimiana na Mhe. Balozi Wilson Masilingi, mkewe Marystela Masilingi,Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Muta na mkewe.
  Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Mkewe Marystela Masilingi, Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakipiga picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa waliokuwa wakiingia ukumbini..
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa na mgeni wao. Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi wakiwa wamesimama kwa nyimbo za Taifa Tanzania na Marekani.


  0 0

  Kampuni ya Coca-Cola Nyanza Bottlers ya Mwanza imemwaga zawadi kwa washindi wa promosheni ya Mzuka wa Soka na Coka inayoendelea.Wakazi 16 wa kanda ya ziwa wiki hii wameweza kukabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki 7,luninga bapa 7,na 2 fedha taslimu.
  Zawadi hizo zimekabidhiwa na Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo,Samwel Makenge,ambaye alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola iliwaweze kujishindia zawadi kwa kuwa bado ziko nyingi.
  Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
  Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza
  Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
  Washindi wa zawadi za Coca-Cola wakipokea zawadi zao kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola kanda ya ziwa,Samwel Makenge katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mkoani Mwanza.
  Baadhi ya washindi katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

  0 0


  Afisa Msajili Mkoa wa Morogoro Ndg. Sererya Wambura (kulia\0 akiwa pamoja na Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta wa NIDA Ndg. Rajabu Kabeya wakipitia ripoti za Usajili na Utambuzi wa watu za mkoa wa Morogoro.
  Ndg. Thabit Salum Likanyaga Mwenyekiti Serikali ya Mtaa wa Kilongo, Kata ya Mkundi akigawa fomu kwa wananchi wa mtaa wake kwa ajili ya zoezi la uchukuaji alama za kibaiolojia linaloendelea kwenye mtaa huo.

  Wananchi Kata ya Kihonda Kaskazini, Mtaa wa Yespa wakiwa kwenye harakati za kujaza fomu na wengine wakiwa katika hatia ya kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole.

  Maafisa Wasajili Wasaidizi Ndg. Alice Makarara aliyeketi na Ndg, Aziza Makoa wakitoa huduma kwa wateja waliofika ofisi ya wilaya ya NIDA ya Usajili Morogoro kuchukua vitambulisho vyao. Aliyeketi meza ya pembeni yao ni Ndg. Lucy Alphonce. Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA akichakata taarifa za waombaji Vitambulisho vya Taifa Morogoro.

  ………………


  Watendaji mkoani Morogoro wamekuwa hamasa kubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu linaloendelea kwasasa mkoani humo likihusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

  Zoezi hilo ambalo linahusisha wananchi wote waliosajiliwa awamu ya kwanza mwaka 2014-15 ambao walishiriki hatua ya kujaza fomu; hatua ya sasa inahusisha uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki na kusajili wananchi wapya ambao hawakufanya usajili wa awamu ya kwanza.

  Afisa Usajili mkoa wa Morogoro Ndg. Sererya Wambura amesema kwa jumla utekelezaji wa zoezi kwa mkoa wa Morogoro ni mzuri na mwitikio wa wananchi ni mkubwa huku akipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na watendaji wa Serikali ngazi zote, kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kusajiliwa.

  Amezitaja wilaya ambazo zinaendelea na zoezi la Usajili mkoani humo kuwa Morogoro Mjini, Mvomero, Gaieo, Kilosa,Malinyi na Ulanga.

  Ameshukuru Uongozi wa mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano mkubwa ikiwemo kuhamasisha na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa ili wajitokeze kusajiliwa.

  Mkoa wa Morogoro unakusudia kukamilisha zoezi la Usajili mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu kwa kusajili zaidi wa wananchi 900,000.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
    Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma-PICHA NA IKULU


  0 0

  Uongozi wa klabu ya Simba umesema unaamini kabisa waamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga Jumapili, watatenda haki.


  Klabu hiyo kupitia kwa Afisa habari wao, Haji Manara amesema hawatawalalamikia waamuzi kabla lakini wanaamini kikubwa ni haki na zaidi waamuzi wengi ni vijana na wanajua maana ya mchezo wa haki.

  “Waamuzi watakaocheza tunaamini watafuata sheria 17 za soka kwa ajili ya kufanya haki itendeke,” alisema.

  Manara amesema kuwa mpaka sasa kikosi chao hakina majeruhi hata mmoja kikosini kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Yanga utakaopigwa kwenye dimba la Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

  Simba wakiwa vinara wa ligi hiyo kwa pointi 59 kutokana na mechi 25, watakuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Yanga waliopo nafasi ya pili na pointi 48, huku wakiwa wameshuka dimbani mara 23.

  Simba inashuka dimbani Jumapili kuivaa Yanga katika mechi ambayo kama watashinda, basi watakuwa wamejihakikishia kubeba ubingwa kwa asilimia 95.

  Manara amesema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri baada ya kikosi cha timu hiyo kurejea wakitokea Morogoro walipoweka kambi ya siku tatu.

  Amesema taarifa kutoka benchi la ufundi kwamba kikosi hicho kinaendelea vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo huo kwa kuhakikisha wanapata pointi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya mbio za ubingwa.

  “Hadi leo hakuna majeruhi na timu inaendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko na kikubwa tunawaomba waamuzi kuzitendea haki kanuni na sheria za soka, waepuke kuingia na matokeo yao mfukoni,"alisema Manara.à

  Manara amesema anaiheshimu Yanga haswa kuelekea katika pambano hilo la watani wa jadi, hivyo huenda wasipate ushindi ila wanaenda kutafuta pointi muhimu katika mchezo huo.

  “Tuna imani ya timu yetu inaweza kuchukuwa ubingwa, lakini sio kama tutashinda mechi zote, mashabiki watambue kwamba kuna mechi tutapoteza, lakini kikubwa wachezaji wanapambana kuhakikisha tunafikia malengo yaliyokuwepo tangu awali,” amesema Manara.

  0 0


  *Dereva wa Noah naye afariki, askari JWTZ, Polisi wajeruhiwa

  Na Ripota Wetu,Morogoro 

  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitha kufariki dunia kwa watu wawili akiwamo mtoto wa miezi tisa Amina Hassan baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha gari ndogo aina ya noah pamoja na basi la Jeshi la Polisi.

  Akizungumza kwa njia ya simu na Michuzi Blog jioni hii kuhusu ajali hiyo Kamanda Matei amesema imetokea saa saba mchana eneo la Mikese Maseyu mkoani humo, ambapo Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo lilikuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam.

  Amefafanua mbali ya kufa kwa mtoto huyo dereva wa Noah hiyo iliyopata ajali ambaye amemtaja kwa jina la Zimbao Cornel huku akielezea kujeruhiwa kwa askari Polisi wanne na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) nao wanne na wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

  Alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa kwenye Noah amesema bado haijathibitika walikuwa wangapi lakini wanaendelea kufuatilia na kisha watatoa taarifa kamili.

  Kuhusu hali za majeruhi Kamanda Matei amesema wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika, hivyo kikubwa ni kuwaombea ili wapone haraka na kurejea kwenye ujenzi wa nchi.

  Kabla ya kuthibitishwa na kamanda kuhusu ajali hiyo, Ripota Wetu ameshuhudia gari hiyo ya Noah ikiwa imeharibika vibaya na baada ya ajali kutokea waliopoteza maisha na majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

  Kwa upande wa Muuguzi wa zamu kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoani Edwine Damas amekiri kupokea mwili wa mtoto huyo na majeruhi na wanaendelea kuwapatia matibabu.
   Pichani ni  gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro.
  Pichani ni  Baadhi ya Askari wa JWTZ na Jeshi la Polisi wakishiriki kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali ya gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro. 
   Baadhi ya Askari wa JWTZ wakitoa msaada kwa majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea

  0 0

  Brighton James – JKCI.

  Watanzania wameshauriwa kufanya mazoezi, kula vyakula bora, kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri kwa kufanya hivyo watajiepusha na magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yanaouwa watu wengi Duniani.

  Ushauri huo umetolewa leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani Mazen Albaghded wakati akiongea na waandishi wa habari katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

  Dkt. Albaghded alisema kuwa ulaji wa vyakula vyenye mafuta na bila kufanya mazoezi ambayo yangesaidia kuyeyusha mafuta hayo kunaweza kusababisha kupata kirahisi ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo. Wagonjwa wa kisukari na wenye shinikizo la juu la damu nao wanaweza kupata ugonjwa huo kirahisi.

  “Mishipa ya damu inapozungukwa na mafuta baadaye huweza kuziba na hivyo damu kushindwa kwenda katika misuli ya moyo (myocardium) na kusababisha mtu kupata shambulio la moyo”, alisema.Akizungumzia kuhusu kambi hiyo ya matibabu ya siku nne Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Tulizo Shemu alisema wagonjwa wanaotibiwa ni wale wanaohitaji matibabu ya kibingwa yenye uhitaji wa uchunguzi yakinifu.

  Dkt. Shemu alisema kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo kwa mgonjwa wanaangalia kama mishipa ya moyo imeziba na ikiwa imeziba wanaizibua kwa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum kinachojulikana kwa jina la “stent” ambacho kinasaidia mshipa wa damu usizibe tena.

  Katika kambi hiyo ambayo ilienda sambamba na mafunzo ya kubadilishana ujuzi wa kazi jumla ya wagonjwa 23 wamefanyiwa vipimo na matibabu ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
   
  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 23 wamezibuliwa mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani wakimzibua mgonjwa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 23 wamezibuliwa mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.Picha na Brighton James – JKCI

older | 1 | .... | 1570 | 1571 | (Page 1572) | 1573 | 1574 | .... | 1897 | newer