Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TCRA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDO NCHINI

$
0
0
Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.

Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema  kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu
“Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.

Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao.

Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.

“Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA  kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima kwa ujumla.” Alisema Melo.

Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia  namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni.

“Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu.

Aliongeza “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.

“Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.



Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe
Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela
Vijana na mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA walioudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makini







Mtaalamu na Mshauri wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
  Mtendaji Mkuu wa tzNIC  Abibu Ntahigiye katika mjadala wa nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.

Waziri wa Afya azindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu Kigoma

$
0
0
*Vyandarua Bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka Matangazo katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na Matibu ya Malaria ni bure na Wananchi hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia gharama hizo. 

Maagizo hayo aliyatoa jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati akizindua ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa Wakina Mama wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha kwaajili ya Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure. 

Waziri Mwalimu alisema Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la JohnsHopkins Center for Communication na Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti malaria Na kuratibiwa na Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP kwa hiyo vyandarua hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie. 

Aidha alisema ofisi ya takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia 10% kutokana na Mikakati iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria. 

Alisema mikakati ya Serikali ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT) Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea vya malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili kujikinga kuumwa na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu wakati wa ujauzito ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria. 

"Niendelee Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii kulipia, wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria liishe , Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe Malalamiko yao ilikuweza kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa Malaria", alisema Mwalimu. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na waliopo ni watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa. 

Wakitoa Malalamiko yao Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo mbele ya Mh Waziri, Lydia Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi 2500/= kwaajili ya Kipimo cha Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili ya Matibabu . 

Alisema pamoja na kuwa na Kadi ya bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba Waziri kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo elekeza. 

Hata hivyo Wananchi hao Shukuru Issa aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja na kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa maelekezo kwa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa kituo hicho kwakuwa kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo cha Afya.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy akizungumza leo kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga mapema leo,mkoani Kigoma.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la 
 Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work  chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 

KIVULINI YAKUTANA NA WANA MABADILIKO NA WADAU WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Shirika la Kivulini limeendesha vikao vya tathmini na mipango mikakati ya utekelezaji wa mradi wa Usawa wa Kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini na Kishapu mkoani Shinyanga.
Vikao hivyo vilivyofanyika Aprili 23,2018 na Aprili 24,2018 katika ukumbi wa Katemi Hotel Mjini Shinyanga vimewaleta pamoja wadau wakuu katika kupinga ukatili wa kijinsia na wana mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii kutoka vijiji vya Nyida, Nsalala, Welezo, Nduguti na Nyida kwa wilaya ya Shinyanga vijijini.
Akizungumza wakati wa vikao hivyo, Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Muhoja alisema tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwezi Septemba mwaka 2017 kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika jamii kwani sasa wananchi wana elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia.
“Suala la ukatili haliwezi kuisha leo,tunapaswa kushirikiana wadau wote,tutoe taarifa za matukio ya ukatili na tuendelee kutoa elimu kwani jamii ikipata elimu matukio haya yatapungua”,aliongeza Muhoja.
Aidha alisema bado halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inakabiliwa na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake ambapo wanawake wamekuwa wakikatwa mapanga hivyo kuomba wadau kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ukatili huo.
Awali akizungumza, Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa wakiwa ukumbini alisema lengo la vikao hivyo ni kufanya tathmini ya shughuli na matokeo ya mradi huo mwaka 2017 na kupanga mikakati ya shughuli za mradi huo kwa mwaka 2018 ambao unatekelezwa na shirika la Kivulini kwa kushirikiana na Shirika la OXFAM.
Alisema katika kutekeleza mradi huo mwaka 2017 wamefanikiwa kuwafikia watu 14,988 kati yao wanawake ni 7652 na wanaume 7336 ambapo walitoa elimu ya mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa njia ya mafunzo,midahalo jamii na sinema.
Nao washiriki wa vikao hivyo walisema kutokana na jitihada zinazofanywa na shirika la Kivulini walisema kumekuwepo na ongezeko la uelewa kwa jamii na makundi maalum kuhusiana na sheria,sera na mifumo iliyopo inayohusiana na ukatili wa kijinsia na matumizi ya mifumo inayowasaidia wahanga wa ukatili.
Naye Afisa kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher alisema hivi sasa jamii ina mwitikio mkubwa kwa sababu wengi wamekuwa wakifika katika dawati la jinsia na watoto kutoa taarifa za matukio ya ukatili.
“Jamii imebadilika,mfano mwaka 2017 tulipokea matukio 52 ya ukatili wa kijinsia lakini mwaka huu tumepokea matukio 82,hii ni hatua kubwa,tunachosisitiza sasa ni wahanga wa matukio ya ubakaji wawe wanatoa taarifa ndani ya saa 72 (siku tatu) na kuepuka kumaliza kesi kifamilia”,alieleza.
Kwa upande wake,Afisa Mtendaji wa kata ya Nyida Daudi Lazaro alisema jamii inaendelea kubadilika na kuachana na mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke na wamekuwa wakitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia katika vikao na mikutano mbalimbali.
 
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Muhoja akizungumza wakati wa kikao cha tathmini na mipango mikakati ya utekelezaji wa mradi wa Usawa wa Kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana uliohudhuriwa na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wakiwemo viongozi wa serikali za vijiji,kata,maafisa maendeleo,dawati la jinsia na watoto katika ukumbi wa Katemi Hotel mjini Shinyanga Aprili 23,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Muhoja akizungumza wakati wa kikao cha tathmini na mipango mikakati ya utekelezaji wa mradi wa Usawa wa Kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa ukumbini 
Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa akielezea lengo la kufanya lengo la vikao hivyo ni kufanya tathmini ya shughuli na matokeo ya mradi huo mwaka 2017 na kupanga mikakati ya shughuli za mradi huo kwa mwaka 2018. 
Marzia Nzota kutoka shirika la RUDI akizungumza wakati wa kikao hicho. Shirika hilo linashirikiana na shirika la Kivulini kutekeleza mradi wa Usawa wa Kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana 
Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa akiangalia kazi inayofanywa na kikundi
Afisa kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu mwamko wa jamii kutoa taarifa juu ya matukio ya kikatili dhidi ya watoto na wanawake
Mwenyekiti wa kijiji cha Welezo Janeth Mabula akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Kikao kinaendelea..
Mdau akiandika dondoo muhimu
Wadau wakiwa ukumbini
Aprili 24,2018 ; Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa akizungumza na wana mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii kutoka vijiji vya Nyida, Nsalala, Welezo, Nduguti na Nyida kwa wilaya ya Shinyanga vijijini.
Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa akizungumza na wana mabadiliko.
Wana mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii wakiwa ukumbini
Wana mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii wakiwa ukumbini
Wana mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii wakifanya kazi ya kikundi
Afisa Mwandamizi Msaidizi wa mradi huo,Vaileth Elisa akielezea jambo wakati wa kazi za vikundi
Mwana mabadiliko Lucia James  kutoka kijiji cha Nduguti akiwasilisha kazi ya kundi lake
Wana Mabadiliko wakiwa ukumbini
Mwana mabadiliko Aron Marco kutoka kijiji cha Butini akiwasilisha kazi ya kundi lake
Picha ya pamoja wana mabadiliko
Picha ya pamoja wana mabadiliko.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RAIS DKT.MAGUFULI ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO UHURU WA HABARI NCHINI

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Mgufuli  kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu ikiwa ndio kilele chake na kauli mbiu inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.

Ambapo  wageni  zaidi ya 300 wanatajiriwa kuhudhuria  hafla hiyo wakiwepo wadau , wanahabari  ,wabunge na taasisi mbalimbali ambapo kimataifa Afrika  inafanyika Nchini Ghana Accra zaidi ya nchi 100  zitawakilisha katika hafla hiyo.

Akizungumza  jjjini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi  ya vyombo vya habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Salome Kitomari amesema katika siku hizo watazungumzia umuhimu wa  uhuru wa habari, utawala bora kwa waandishi wa habari na  wanasheria kama Mahakama kuwa na uhuru  wa kusimamia kesi za jinai za kuwa na uwazi kwa wanahabari vilevile na kukumbusha kutekeleza majukumu katika  uandikaji wa habari kuwa sahihi.

Aidha Makamo wa Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Jane Mihanji amesema wao wamekuwa na jukumu la kuwaweka pamoja waandishi wa  habari  na kuwapa mafunzo na  kuwapatia  vitendea kazi.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya uhuru wa habari  Nchini ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma  Mei 2 hadi 3  mwaka huu na kauli mbiu inasema  ni wajibu wa Serikali vyombo vya habari haki na utawala wa sheria.
Makamu wa Rais wa  Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mahanji akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyokwenda begakwabega na waandishi kwa kuto semina ili kutoa habari zenye faida kwa Taifa.
Mkurugenzi wa  Tanzania Media Foundation (TMF) Fausta Musokwa akizungumza na waandishi wa habari wanavyochangia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari kwa kutoa pesa ili vyombo hivyo vijiendeshe.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari kuhusuumoja wa Mataifa unavyodhamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

TPDC KUWANUFAISHA WANANCHI KWA GESI ASILIA MAJUMBANI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akieleza kwa kina Mradi Mpya wa Kuunganisha gesi asilia kutoka bomba kubwa hadi kwenye bomba dogo la Ubungo Mikocheni mradi ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi miwili. Piv
Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA, Lu Xiaoqiang akielza kwa waandishi wa habari namna watakaovyotekeleza ujenzi wa Miundombinu hiyo kwa ufanisi na wakati kadiri ya masharti ya mkataba. Pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ubungo Tanesco, Sophia Fitina akielezea jinsi walivyoupokea mradi huo tokea umeingia katika eneo lao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (wa tatu toka kushoto) akiwa na  Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA ndugu Lu Xiaoqiang (anayemfuatia Kushoto) pamoja na wafanyakazi wanaotekeleza mradi huo.



Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi mradi wa uunganishaji wa gesi asilia kutoka katika bomba kubwa la gesi asilia linalomilikiwa na TPDC kwenda kwenye bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kutoka Ubungo hadi Mikocheni ambalo nalo linamilikiwa na TPDC ili kuongeza kiasi cha gesi asilia katika bomba hilo kwa lengo la kuwafikia watumiaji wengi zaidi.

 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akikabidhi jukumu la ujenzi wa mradi wa uunganishwaji wa gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam katika eneo la Valvu namba 15 (Block Valve Station-BVS) ambapo ndipo bomba hilo litarajiwa kujengwa hadi eneo la Ubungo Maziwa litakapounganishwa na bomba dogo la usambazaji wa gesi asilia kuelekea Mikocheni Dar es Salaam. 

 “Leo ni siku kubwa sana kwetu kama Kampuni ya Mafuta ya Taifa tunapokabidhi rasmi jukumu la ujenzi wa miundombinu ya kutoa gesi asilia kutoka kwenye bomba letu kubwa kwenda kwenye bomba letu dogo la usambazaji wa gesi asilia kazi ambayo itafanywa na kampuni ya SINOMA ambayo faida yake kubwa ni kulipa uwezo wa kubeba na kusambaza gesi nyingi zaidi itakayoruhusu uunganishwaji zaidi wa gesi asilia kwa watumiaji wapya katika maeneo yote ambayo bomba hilo linapita yaani Ubungo, Sinza, Chuo Kikuu, Survey, Mwenge na Mikocheni” alifafanua Kaimu Mkurugenzi.

 Akizungumzia wanufaika wa mradi huo pindi utakapokamilika, ndugu Musomba amesema kuwa, pamoja na kuendelea kusambaza kwa watumiaji wa zamani ambao ni MM I, MM II, MM III, TanPack na Iron and Steel wateja wapya watakaonufaika ambao tayari wameshakubaliana ni Coca Cola kwanza Limited na BIDCO na nyumba 70 katika awamu ya kwanza na kwamba wanatarajia kuunganisha kwa viwanda zaidi vitakavyokuwa tayari kwa muda wowote. 

Aidha akieleza kuhusu utaratibu wa uunganishwaji wa gesi asilia kwa watumiaji Mhandisi Musomba ameeleza kuwa, “Utaratibu ni wa kawaida sana kikubwa mteja tarajiwa anatakiwa kuwasilisha barua ya maombi ya gesi asilia kisha wataalam kufanya utafiti wa namna ya kumuunganishia mteja gesi hiyo na kwa upande wa watumiaji wa majumbani tunashauri pia nyumba kadhaa kuungana pamoja na kuleta barua kisha taratibu za kiutalamu za namna ya kuwafikishia gesi asilia zifanyike.” 

Kwa upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa SINOMA, Lu Xiaoqiang ambao ndio Wakandarasi walioshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo amesema kuwa, “Leo ni siku ya furaha kwa kuwa tumeweza kupata nafasi ya kutekeleza mradi wa TPDC wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka eneo la Ubungo bomba ambalo tunaamini litasaidia kukuza uchumi wa nchi nzuri ya Tanzania kwa kusambaza nishati viwandani na majumbani.” 

 Akizungumzia gharama za matumizi ya gesi asilia majumbani Mhandisi Musomba amefafanua kuwa, “Matumizi ya gesi asilia ni ya gharama nafuu kulinganisha na mkaa na gesi za mitungi-LPG ambapo kwa mtumiaji wa gesi za mitungi mfano wa Kilo 15 ambayo itatumika kwa mwezi mmoja kama akitumia gesi asilia atatumia hadi miezi miwili na hivyo kuokoa karibu nusu ya gharama ya matumizi ya nishati majumbani lakini pia gesi asilia ni nyepesi kuliko hewa na hivyo kuwa salama zaidi kwa matumizi hata pale inapovuja kwa kuwa hupotea hewani.” 

Jukumu la kusambaza gesi asilia ni la msingi kwa maeneo ya uchumi imara wa viwanda na hivyo TPDC inaendelea kufanya tafiti za kitaalamu za usambazaji wa gesi asilia katika maeneo mengine ya nchi yakiwemo Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga na Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KATIKA UKUMBI WA MSEKWA MKOANI DODOMA

$
0
0


Na Lilian Lundo - MAELEZO,Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wanaafrika Mashariki kujiamini kuwa wanaweza kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea mataifa mengine.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa  akihutubia Bunge la Nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika mkoani humo kwa mara kwanza  tangu kuanza kwa Bunge hilo.
“Ninazungumza hili si kwamba hatuhitaji msaada au hatuhitaji ushirikiano, lakini ni lazima tuliweke hili wazi, kwamba tukiamua tunaweza na mifano ipo mingi ikiwemo Tanzania”. Alisisitiza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.
“Tanzania tunajenga reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 700.26 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa thamani ya shilingi Trilioni 7.6, tumeweza kununua ndege sita na pia tumejenga meli kubwa katika Ziwa Victoria bila kuomba mkopo popote,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameongeza kuwa wabunge wa Afrika Mashariki wanaowajibu wa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na Jumuiya hiyo Rais Magufuli amesema kuwa kabla ya kuanza kwa umoja wa forodha mwaka 2005 biashara kati ya nchi wanachama ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.8 lakini baada ya kuanzishwa kwa umoja wa forodha imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5.
Mbali na hayo Rais,  Magufuli ameshukuru uamuzi wa bunge hilo kufanyika mjini Dodoma ambapo kwa sasa Serikali imehamishia shughuli zake zote katika mkoa huo, na tayari watumishi wa serikali zaidi ya 3000 wameshahamia huku Rais Magufuli akitarajiwa kuhamia muda wowote mwaka huu.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Martin Ngoga amesema Bunge hilo linasubiri marekebisho ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ili  lugha ya Kiswahili ianze kutumika kama lugha rasmi katika vikao vya bunge hilo na katika jumuiya hiyo kwa kuzingatia azimio lililokwishapitishwa.
“Hatuoni sababu ya kutumia lugha za wageni wakati kuna lugha yetu ambayo tunazungumza ambayo ni kiswahili,” alisema Dkt. Ngoga.
Bunge la Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mkoani Dodoma katika ukumbi mdogo wa Bunge wa Pius Msekwa. Bunge hilo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa kwa ajili ya kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa wimbo wa taifa uliokuwa ukipigwa ndani ya ukumbi wa Bunge wa  Msekwa ambapo alihutubia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mkoni Dodoma.
 Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Martin Ngoga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki (EALA).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linalofanyika mkoni Dodoma.
  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuhutubia Bunge la EALA mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa tatu kutoka kulia, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga wa nne kutoka kulia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuwahutubia mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) Martin Ngoga mara baada ya kuhutubia Bunge hilo la Afrika Mashariki linalofanyika mkoani Dodoma. Picha na IKULU.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WA NYANDA ZA JUU KUSINI

MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

$
0
0
 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari. Msanii nguli wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours. Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.

 Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla. “Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond 

 Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza. 

 Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. “Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”

PUMA YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI

$
0
0


 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande, Dar es Salaam, Nasri Mustafa akumuonesha Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia) picha aliyoichora na kushinda tuzo  ya usalama barabarani 2017, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Puma wa  mafunzo ya ya usalama barabarani kwa wanafunzi, jana katika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania.Wa pili kushoto ni SajentiHussein Ramadhan Mwalimu wa Trafiki Makao Makao Makuu ya Usalama Barabarani.Imeandaliwa na Richard Mwaikenda.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini. 

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.

AKizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu,  alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.

Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria,  bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.

"Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;

"Hivyo kwa kuwafundisha usalama barabarani tunawapa ufahamu wa kuwajenga katika matumizi salama ya barabara...hiki ndicho kipaumbele chetu."

Alifafanua kwamba baada ya mafunzo  wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchora michoro ya usalama barabarani na mshindi pamoja na shule anayotoka wanazawadiwa.

Corsaletti alisema kampuni hiyo ilianzisha mafunzo hayo mwaka 2013 na imeendelea kufanya hivyo hadi sasa kwa kufikia shule 47 na kuwafundisha wanafunzi 60,000 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Geita.

Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa kiwango cha ajali katika shule zilizopatiwa mafunzo kimepungua.


Corsaletti, alisema kampuni hiyo itaendelea na kampeni ya usalama barabarani na kuahidi kufanyakazi pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani, maofisa kutoka manispaa au wilaya zinakotoka shule  zilizochaguliwa ili kuhakikisha lengo linatimia.



 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia), akimshukuru Mbunja kwa kuzindua mpango huo.
 Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania, akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango huo.



Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange  akiiweka sawa picha iliyochorwa na Mwanafunzi Nasri Mustafa na kushinda tuzo ya Usalama barabarani 2027
 Shemu ya wadau wa usalama barabarani
 Baadhi ya walimu na wanafunzi waliohudhuria uzinduzi huo
 Wanahabari wakiwa kazini
 Sehemu ya wadau wa usalama barabarani
 Mwanafunzi Nasri Mustafa akionesha picha aliyoichora ya usalama barabarani. Picha hiyo ilishinda tuzo ya kwanza 2017

 Wadau wa usalama barabrani wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi a mpango huo
 Mgeni rasmi, Mbunja na Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti wakiwa na furaha
  Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti, Akisalimiana na wadau baada ya uzinduzi
 Wakiwa katika picha ya pamoja


BENKI YA ACCESS YATOA MSAADA WA KOMPYUTA 10 MEZA PAMOJA NA VITI KWA SHULE YA SEKONDARI TURIANI KINONDONI

$
0
0
Meneja Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Bw. Simon Sijaona akikabidhi moja ya kompyuta 10 kwa Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam zilizotolewa na benki ya Access kwa shule hiyo Baadhi ya vitu vingine vilivyotolewa na benki ya Access kwa shule hiyo ni pamoja na viti 10na meza za kompyuta 10 wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Mwanafunzi Amina Ibony wa kidato cha IV na Nasib Masenga Kidato cha IV.
2
Meneja Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Bw. Simon Sijaona akiwa na Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam mara baada ya kukabidhi kompyuta hizo kutoka kulia ni Benedig Mfoi Meneja Uendeshaji Camara Education Foundation Tanzania.
3
Meneja Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Bw. Simon Sijaona akizungumza mara baada ya kukabidhi kompyuta hizo kulia ni Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam
4
Meneja Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Bw. Simon Sijaona akimsikiliza Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akisoma risala ya shule mara baada ya kupokea kompyuta 10 kutoka Benki ya Access ya jijini Dar es salaam.
5
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Turiani wilaya ya Kinondoni wakitumia kompyuta mara baada ya kukabidhiwa na benki ya Access leo jijini Dar es salaam.
6
Meneja Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Bw. Simon Sijaona na Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakiwaelekeza namna ya kutumia kompyuta hizo mara baada ya kukabidhiwa shuleni hapo leo.
7
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakifurahia wakati walipopewa taarifa ya kuletewa kompyuta hizo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Izungo Angalo kutoka Benki ya Access ya jijini Dar es salaam.
8
Bw. Izungo Angalo Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Turiani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akitoa taarifa ya kupokelewa kwa kompyuta 10 kutoka Benki ya Access.

MSAJILI WA NGOs AMEZITAKA NGOs KUJIHAKIKI KAMA HUWATOHIKIKI NGOs ZAO WATOTAMBULIKA NA SERIKALI

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AHUDHURIA MKUTANO WA SADC TROIKA EXTRA JIJINI LUANDA, ANGOLA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018. 

Mkutano huu umeitishwa baada ya mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC Mkutano huu umetanguliwa na kikao cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018. 

Mkutano huu ulihusisha nchi wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria, Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka; Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. 
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho  Mhe. Edgar Lungu, Rais wa ZambiaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati IIIMfalme wa Swaziland  Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço  Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),   Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini Luanda Angola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KIWANDA KIKUBWA CHA UTENGENEZAJI KEMIKALI KUJENGWA MLANDIZI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
  
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage leo ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa w aujeniz wa kiwanda Mama cha dawa kilichogharimu Bilioni 256 katika eneo la Msufini  Mlandizi mkoa wa Pwani.
  


Akizungumza leo Mlandizi Mkoani Pwani Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage akimwakilisha makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa anawapongeza JUNACO kwa uthubutu wao ambao kiwanda hicho kitanufaisha taifa na wananchi kwa ujumla na kuwataka kuviendeleza viwanda hivyo.


Mwijage amehaidi   kujenga viwanda vingi na kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 na ameeleza kuwezesha viwanda hivyo katika miundombinu na kuwashauri wawekezaji hao kutoa nafasi za uwakala kwa nchi mbalimbali.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asumta Mshama ameeleza kuwa wapo tayari kupokea viwanda na wanamuhaidi mheshimiwa Rais wataendeleza kazi.


Mkurugenzi wa JUNACO Tanzania   Justine Lumbert ameeleza kuwa mradi huu una wawekezaji wawili ambao ni JUNACO Tanzania kampuni kutoka Tanzania na SERBA Dynamic International ya nchini Malaysia na mradi huu utagharimu shilingi bilioni 256 na kuufanya kuwa mradi mkubwa Afrika.


Aidha ameeleza kuwa katika kutekeleza mradi huu ni mwitikio wa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda ambapo wataokoa fedha nyingi zinazotumika kununua dawa nje na kuingiza fedha za kigeni. na kuhusu utengenezaji wa dawa wameona ni muhimu kutokana na uhitaji wa dawa kwa kiasi kikubwa na kilimo hasa katika utakatishaji maji ili kuweza kufikia malengo ya upatikanaji wa maji kwa asilimia 90 mwaka 2025.


Pia ameeleza kuwa kiwanda hiki kitakamilika baada ya miezi 23 na zaidi ya ajira rasmi  700 zitatolewa.Pia ameeleza uzalishaji wa kiwanda hivyo bidhaa zitauzwa nchini kwa asilimia 20 na asilimia 80 zitauzwa nje ya Afrika na nje ya Afrika.


Naye Mkurugenzi wa SERBA dynamic international amehaidi kufanya mapinduzi katika mradi huu kwa teknolojia ya hali ya juu kama walivyofanya katika nchi za India, Malaysia na Marekani.


 Waziri wa  Viwanda,Biashara na uwekezaji Charles Mwijage kushoto akipiaga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Kiwanda cha Dawa cha Msufini kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu. kulia ni Viongozi mbalimbali wa bunge na mkoa wa pwani.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwa niaba ya makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
 Mkurugenzi wa JUNACO Tanzania   Justine Lumbert akieleza uwekezaji wake katika ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa katika eneo la Msufini mkoani Pwani.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson akizungumza juu ya umuhimu wa kiwanda cha Dawa cha Msufini kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani  
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba akizungumzia umuhimu wa utunzaji wa Mazingira katika maendeleo ya Viwanda wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha Msufini.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji , Mhandisi Isac Kamwele akieleza umuhimu wa Maji katika maendeleo ya Viwanda. 
 Mkuu w amkoa wa Pwani Mhandisi, Evarist Ndikilo akizungumzia malighafi zitakazopatikana katika mkoa wa pwani katika kuendesha kiwanda hicho.  
  Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba  akiteta jambo na Mbunge wa Kibaha Vijijini , Amouhd Jumaa  katika viwanja vya msufini
 Baadhi ya Wageni wa alikwa katika uzinduzi wa kiwanda cha dawa wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi. 

BENKI YA CBA YAKUTANA NA WATEJA WAKE JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Commerial Bank of Africa (CBA) Tanzania, Gift Shoko akizungumza na wadau wa benki hiyo katika hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha, huku akiwajulisha hatua mbalimbali za kibenki zilizoboreshwa kwa wateja wao (Habari picha na Pamela Mollel Arusha)
Wadau wa benki ya Commerial Bank of Africa,CBA wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Arusha kwa lengo la kuwajulisha hatua mbalimbali walizozifikia huku wateja wao wakipata wasaa wa kueleza changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi Mkuu Mendaji wa Be Gift Shoko kushoto akizungumza na mmoja wa wadau wa benki hiyo jijini Arusha
Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki ya CBA, Julius Konyani akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni na wadau wa benki hiyo jijini Arusha kwa lengo la kuwajulisha hatua mbalimbali walizozifikia huku wateja wao wakipata wasaa wa kueleza changamoto zinazowakabili.

Wadau wa benki hiyo wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni jijini Arusha


Na Pamela Mollel,Arusha

UKATA wa fedha katika uwekezaji na kukuza biashara ya utalii mkoani hapa umepata tiba baada ya Commerial Bank of Africa, kusema itashirikiana na wafanyabiashara kuwapa mikopo hadi kufikia dola za Marekani milioni 50 kwa atakayetaka.

Mkuu wa Idara ya Masoko wa benki hiyo, Julius Konyani, alisema wafanyabiashara 500 katika sekta ya utalii mkoani hapa kila mmoja anaweza kukopeshwa dola za Marekani milioni 50.Alisema hayo katika ya katika chakula cha jioni walichoandaa kwa ajili ya kubadilishana nao mawazo na wateja wao.

“Mteja mmoja anaweza kukopeshwa dola za Marekani milioni 50, tunaweza kuwakopesha wateja 500 hapa Arusha kila mmoja kiasi hicho cha mkopo hapa,” alisema.Alisema benki yake imefanya utafiti kwa mikoa mbalimbali kuangalia fursa zilizopo kama vile kilimo na utalii, na hivyo, imejipanga kuwawezesha wateja hao kukopa kiasi wanachohitaji ili kuendeleza na kukuza uwekezaji katika mkoa yao.

Hata hivyo, alisema vigezo na masharti ya ukopaji yatakazingatiwa kabla ya kutoa mkopo kwa mteja.Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya CBA TanzaniaGift Shoko akizungumzia suala la riba na wateja hao, alisema, benki yao haina tofauti na benki zingine na kwamba wamechukua hatua ya kupunguza.

Alisema baadhi ya wateja wao tayari wameshapata barua za kuwajulisha kuhusu punguzo hilo.Akizungumzia kuhusu madai ya kufungwa kwa matawi yao mikoani, Shoko alisema, walichofunga siyo matawi isipokuwa huduma zilizokuwa zikitolelwa na mawakala.

Alisema huduma za mawakala zilizokuwa zikitolewa Tunduma, Mtwara na Moshi ndizo zilifungwa, lakini hata hivyo, alisema wateja wao wanaendelea kupata huduma kupitia huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 22 YA KIFO CHA DR. FRANCIS MW. MSELLEMU

$
0
0
DR. FRANCIS MW. MSELLEMU 1941- 1996 Baba, Ni Miaka 22 sasa tangu uondoke hata bila ya kutuambia neno la KWAHERI! Maisha yetu hayajawahi kuwa rahisi bila uwepo wako, Baba. Japo watu wanatuona tukicheka , hawajui ni kiasi gani mioyo yetu inahuzunika kwa kukukosa malezi, mapenzi na uwepo wako wewe. Hata hivyo tunamshukuru MUNGU kwa kuendelea kutulinda, kututunza na kutubariki. Ameedelea kuwa kweli kwetu Mume wa Mjane na Baba wa Yatima.

 Tunakuombea Pumziko la Milele, na tukiamini kwamba siku moja tutakutana na tutaimba Halleluya pamoja na wewe mbinguni. Unakumbukwa daima na Mke wako Mpendwa Kodawa Mikaline Msellemu - ‘Mama K’ kama ulivyo kuwa umezoea kumuita, Watoto, Wakwe zako, pamoja na Wajukuu. Ndugu , Jamaa na Marafiki nao hawajakusahau. ‘Mamillioni Wanaitegemea’-Pumzika kwa Amani DAD!

MALARIA YAPUNGUA MPAKA ASILIMIA 7. 3 NCHINI.

$
0
0
Na Ripota wetu Kasulu, Kigoma 

MAAMBUKIZI ya viashiria vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yame pungua kwa Watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017 hii ni kuzigatia harakati zinazo fanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la WHO kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa huo. 

Akizindua takwimu zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu , alisema Siku ya leo kupitia maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Kigoma, atazindua rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017. 

Kwa Mujibu wa Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa alithibitisha Matokeo ya sasa ya utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa Zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3. Hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha utambuzi wa vimelea (mRDT). 

Waziri Ummy alisema utafiti huo unaonesha Mikoa yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja. 

"Takwimu hizi, zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na hii ni habari njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu ipo tayari kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae tuweze kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa, tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja katika kufikia malengo tuliyojiwekea ili jamii, hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito ambao ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa malaria waweze kuepukana na ugonjwa huu", alisema Waziri Mwalimu. Alisema Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, lakini bado kuna changamoto, ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya kutokomeza malaria nchini. 

Changamoto hizo ni pamoja na Wanajamii kutotumia vyandarua ipasavyo katika kujikinga na ugonjwa wa malaria, kuwepo kwa mitazamo potofu juu afua za kupambana na malaria; mfano dhana ya kuwa viuatilifu-ukoko za kunyunyizia ukutani zinaleta kunguni na viroboto na kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume ni dhana potofu ambazo hazina ukweli wowote. Vilevile, Jamii kutoshiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuharibu mazaliaya Mbu. 

Kwa upande wake Mkurugenzi mwakilishi wa shirika la misaada na Maendeleo la Marekani USAID Andy Karas alisema kwa zaidi ya miaka 12 USAID imekuwa ikifanya kazi pamoja na serikali kupitia Wizara ya Afya kwaajili ya Kupambana na Malaria. 

Alisema watoto wengi walio hai leo ni kwa juhudi za serikali, kwa kushirikiana na Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria kwa Muda wote wameweza kusambaza vyandarua zaidi ya milioni 10 na kununua viuwadudu zaidi ya milioni 20 na kupuliza dawa ya Mbu kwenye maeneo hatarishi vile vile wameweza kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kufanya takwimu mbalimbali juu ya kupungua kwa ugonjwa wa Malaria. 

Nae Balozi wa Usizwi Florence Tinguell aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa juhudi kubwa walizo zifanya katika kuhakikisha wanatokomeza Malaria ,imeweza kubuni mbinu. Kwa zaidi ya miaka 50 Ubalozi wa Uswizi umekuwa ukifadhili tafiti za malaria ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi ya Ifakara Health Institute. 

Hata hivyo mjumbe wa kamati ya bunge ya kupambana na Malaria ( TAPAMA) na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve alisema wao kama wabunge wanatoa wito kwa Wananchi wote kuwa jukumu la kupambana na Malaria na mapambano dhidi ya Malaria ni la Wananchi na wasiiachie serikali peke yake na kuomba nguvu kubwa ielekezwe kwenye kinga na wahudumu wa Afya na wakina mama kufika hospitali kwa wakati ilikuweza kupatiwa kinga ya Malaria.

Kilele cha Maadhmisho ya Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akionyesha rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako – kwanza kulia, Balozi wa Uswizi ha Tanzania Florence Tinguell na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni– kwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania – NBS Albina Chuwa.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na viongozi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu kushoto akipokea ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopungua kwa malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Malaria Duniani Mkoani Kigoma,pichani kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Afisa Mradi JOHNS HOPKINS  VectorWorks  Jacqueline Madundo akitoa maelezo mafupi kuhusu mfumo unaosimia uwajibikaji katika maswala ya vyandarua nchini kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa  kilele cha Maadhmisho ya Malaria yaliyofanyika leo katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Kundi la muziki wa Bongo fleva la WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa Malaria ambayo imehadhimishwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Kundi la wananchi lililojitokeza katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ili kusikiliza ujumbe kuhusu Malaria, mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (MB).

Kikundi cha ngoma kutoka Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kikiburudisha Viongozi na wananchi waliofika katika viwanja vya Umoja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AKUNWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (katikati) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakiingia kwenye jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya Rais huyo kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mjini Dodoma 
Sehemu ya ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukiwa katika chumba cha wageni Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (hayupo pichani) aliyewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. 
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) akisisitiza jambo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango. 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakigonga “tano” wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. 



Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, DKT. AKINUMWI ADESINA, ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili ijayo,

Dkt. Adesina ameyasema hayo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

“Tunajivunia uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza miongoni mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.6” alisema Dkt. Adesina

Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

“Katika miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha usafirishaji wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji wa uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Adesina.

Dkt. Adesina ameutaja mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400 wenye njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda wa Kusini na Kusini Magharibi mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.

“Miradi hii pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji inayotarajiwa kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi wake mahili, wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu” aliongeza Dkt. Adesina.

Alisema Tanzania imepiga hatua katika viwango vya wananchi kupata huduma ya umeme ambapo awali ilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa kiwango hicho kimepanda hadi kufikia asilimia 38 na kwamba lengo la benki hiyo ni kutaka kiwango hicho kifikie asilimia 82 katika miaka michache ijayo.

Alisema ili kufikia hatua hiyo Benki yake ina mpango wa kuboresha Shirika la Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO ili liongeze uzalishaji wa umeme wenye gharama nafuu, kuongeza ufanisi na kutengeneza faida ili kuchochea maendeleo ya viwanda.

Aidha, Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, ameeleza kuwa benki yake inasiadia kuendeleza kilimo nchini kupitia Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, kwa kukuza masoko na uongezaji thamani ya mazao ya wakulima yanayozalishwa kupitia mradi huo.

Akizungumzia miradi ya kikanda, Dkt. Adesina alisema kuwa benki yake imewekeza katika miradi ya nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ili kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Kenya ili kurahisisha biashara na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika nchi hizo.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nyanja mbalimbali.

Alisema kuwa AfDB, licha ya kusaidia kwa kiasi kikubwa kufadhili miradi ya ujenzi wa barabara, nishati na mingine mingi na mfuko mkuu wa Serikali, mwaja jana ilitoa pia mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kukuza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, zinazotumika kukopesha wakulima.

Dkt. Mpango amesema kuwa Rais huyo akiwa hapa nchini atatembelea mradi wa kituo cha kupooza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma na ataungana na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua barabara ya Dodoma-Babati hadi Arusha, iliyofadhiliwa na Benki hiyo na washirika wake.

QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

$
0
0
Qatar Airways yapeleka waandishi kutoka vituo mbalimbali vya habari na utangazaji  vya Africa kwa ajili ya matembezi mjini Doha. Katika matembezi hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali kama Makumbusho ya Sanaa ya kiislamu (museum of Islamic art) haya ni makumbusho yaliyopo katika mji mkuu wa Qatar, Doha. Pia walitembelea Kijiji cha kitamaduni cha Katara, Katara ni kijiji kitamaduni huko Doha, Qatar. 

Iko katika pwani ya mashariki kati ya West Bay na Lulu ambayo Ilifunguliwa mnamo Oktoba 2010. Walitembelea The Grand Mosque, Msikiti wa Kitaifa Qatar. Huu ni mojawapo ya misikiti mikubwa ya kihistoria nchini Qatar, Msikiti huu uko katika wilaya ya Jubailat Doha. Wanahabari hao pia walipata nafasi ya kutembelea maeneo kama Souq waqif, Falcon souq, na Gold souq ambapo waliweza kujionea vitu vingi kama mapambo na vito vya thamani vilivyotengenezwa kwa dhahabu na madini ya aina mbalimbali.

Katika ziara yao mjini Doha waandishi wa habari walitembelea Qatar foundation, Al Shaqab sehemu ambayo hutumika kuwapa mafunzo farasi katika jamii za kiarabu, the Pearl na Khalifa International Stadium; ambayo inajulikana kama Uwanja wa Taifa, ni uwanja unaotumika kwa shughuli mbalimbali huko Qatar ambao pia ni kama sehemu ya eneo la Doha Sports City, ambalo linajumuisha Aspire Academy, Kituo cha Hamad Aquatic, na Aspire Tower park. Uwanja ulipewa jina hilo baada ya Khalifa bin Hamad Al Thani, ambaye zamani alikuwa kiongozi wa dini ya kiislamu (Emir) nchini Qatar. Mbali na maeneo hayo wanahabari walitembelea Regency sealine camp, Desert Safari, pia kituo cha utangazaji cha Al Jazeera.

Qatar Airways ina Zaidi ya miaka 20 katika kutoa huduma za anga, Ni shirika la ndege ambalo limejishindia tuzo mbalimbali ambapo kwa mwaka 2017 Qatar airways ilipata tuzo nyingi Zaidi ya tano na mwaka huu  imeshinda tuzo mbalimbali zikiwemo Crystal cabin award, Skytrax world airport award 2018, 2018 TripAdvisor travelers’ choice awards na Apex passenger choice award 2018. Qatar Airways imeshinda tuzo za Skytrax airline of the year mara nne (4) mfululizo katika miaka ya 2011, 2012, 2015 na 2017.

                                       “QATAR AIRWAYS, GOING PLACES TOGETHER.” 
    
 Wanahabari kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja walipokwenda kutembelea Makumbusho ya sanaa ya kiislamu mjini Doha.
 Waandishi na wadau wa habari wakiwa wamepumzika baada ya kuwasili Hamad International Airport mjini Doha, Qatar.  
Waandishi na wadau wa habari kutoka nchi mbalimbali za Africa i.e Tanzania, Uganda wakiwa katika picha ya pamoja walipokuwa Doha.

WAKALA WA VIPIMO YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA WA PAMBA

$
0
0
Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa Wakulima wa pamba kuhusu Mizani sahihi zinazotakiwa kutumika wakati wa msimu wa ununuzi wa pamba, elimu hii ya vipimo ni ya muhimu kwa Wakulima wakiwa katika maandalizi ya kuelekea katika msimu wa ununuzi wa pamba . 

Mpaka sasa Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora imetoa elimu kwa Wakulima wa pamba katika wilaya mbili (2) ambazo ni Nzega na Igunga, na takribani kata 20 zimefikiwa na kupata elimu hiyo ambapo zoezi bado linaendelea. 

Wakulima wa pamba wameipokea kwa furaha elimu ya utambuzi wa mizani sahihi iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo, kwani itawasaidia kuwabaini kwa urahisi wale wanaotumia mizani ambazo hazija hakikiwa wakiwa na lengo la kutaka kuwaibia pamba yao. 

Pia, elimu ya utambuzi wa mizani sahihi zilizohakikiwa na WMA itawasaidia Wakulima kuuza pamba safi, kwani apo awali walikuwa wanajihusisha na uchafuzi wa pamba kwa kuweka michanga, kokoto, mafuta ya kenge pamoja na maji ili waweze kuongeza uzito katika pamba pindi waendapo kuiuza.

Wakala wa Vipimo inatoa wito kwa wadau wote wa zao la pamba kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yeyote haswa uchakachuaji wa mizani wakati wa ununuzi wa pamba, kwani kwa yeyote atakaye kamatwa kwa makosa hayo atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura na. 340.

Pia, WMA ina namba maalumu kwa ajili ya wananchi kupiga na kupata msaada pindi wakutanapo na changamoto za kivipimo, namba hiyo ni 0800 110097 namba hii ni bure kabisa.
 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakioneshwa sehemu ya kuweka lakili (seal) na kubandika stika ya WMA mara baada ya mizani kuhakikiwa.
 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakielekezwa na afisa vipimo namna ya kutambua mizani ya saa (salter) iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo.
Afisa Vipimo akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyo hakikiwa kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Igunga kijiji cha mwabakina kata ya mbutu mkoani Tabora.

SEHEMU YA PILI YA HISTORIA YA VITA YA MAJI MAJI

$
0
0
Waanzilishi wa mwanzo wa Vita ya Maji Maji walikuwa ni Machifu na mganga wa jadi kutoka jamii za Wangindo na wamatumbi na baadaye vuguvugu hilo lilienea kama moto kwenya jamii nyingi ikijumuisha jamii za Wamatumbi,Wamwera,Wangindo,Wangoni,wapogoro,Wandendeule,Wabena,Wasangu na nyingine nyingi. Kwa undani wa Historia hii ya Vita ya Maji Maji tizama sehemu ya pili ya Historia ya Vita hivyo.
KAMA ULIPITWA NA SEHEMU YA KWANZA YA HISTORIA YA VITA YA MAJI MAJI HII HAPA CHINI.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images