Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

SPORTPESA YATIMIZA NDOTO ZA WATANZANIA 20 KUPITIA PROMOSHENI YA KUSHINDA BAJAJI


WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO CALVIN GWABARA

$
0
0
Na: Amina Hezron, Morogoro

Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika wamebaka au kuwapa mimba wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nchini.
Baadhi ya wadau wa Elimu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa elimu wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wakati wa mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania TEN /MET ili kupeana mrejesho wa namna ya kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.

Katika mkutano huo wa wadau wamebaini ushiriki wa karibu wa wazazi na watoto wao haupo kwa kiasi kikubwa jambo linaloelekea kuendelea kuwepo kwa changamoto hiyo.

Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo Bi. Maajabu Nkamyemka amesema kwa wilaya ya mvomero takwimu zinaonesha hadi April 6 mwaka huu takribani mimba 90 zimebainika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo miongoni mwa hizo mimba 13 ni kutoka shule za msingi.

Aidha Bi. Nkamyemka amesema kuwa ni jukumu la wazazi na walimu kwa kushirikiana na wanafunzi kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao ni wahusika bila kuwafumbia macho ili sekta husika kupambana nao ili kutokomeza janga hilo.

"kwa kuwa binti akipewa ujauzito huwa tunahangaika tu na aliyempa ujauzito, na yule mwenye ujauzito tunamuacha sasa bhas sasa kwa kuwa wazazi hawataki kuleta ushirikiano tutamfungulia kesi mwanafunzi mwenye mimba pamoja na wazazi ili wazaz wawachunge watoto wao ipasavyo "Alisema Nkamyemka.
Wadau hao wa elimu wakiwa ndani ya mkutano huo 

Naye mratibu elimu wa kata za mhonda na Kweuma bwn, Heriamini Mariki amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya mimba hasa kwa wanafunzi, wa sekondari jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wazazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo huku akitaja sababu zinazochangia kuwa ni pamoja na uelewa finyu wa wazazi na wakati mwingine umaskini kwa baadhi ya kaya nyingi wilayani humo.

“Sisi kama wadau wajibu wetu mkubwa ni kuwapatia elimu wazazi juu ya athari za kutokaa karibu na watoto wao na kuwa wawazi juu ya madhara ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo" alisema Mariki

Naye diwani wa kata ya mhonda Bw. Abdallah Hassani Khalifa ametoa rai kwa Serikali kujenga hosteli kwa shule za kata ili kuondokana na tatizo la mimba za utotoni linaloikumba nchi nzima kwa kiasi kikubwa, huku akiwataka wazazi na walimu wanawapa watoto wanafunzi ushirikiano wa kutosha na ulinzi kwani ndiyo haki pekee wanaotakiwa kuzipata ili kufanya vyema katika masomo yao.

TANZANIA KUUNGANA NCHI WANACHAMA UMOJA WA MATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA MARALIA DUNIANI 2018

COCA-COLA BONITE YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA NA COKA'

$
0
0
 Mmoja wa washindi wa pokipiki akikabidhiwa zawadi yake.
 Baadhi ya washindi wa luninga katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Washindi wa pikipiki wakijaribu kuendesha pikipiki zao baada ya kukabidhiwa wakiwa na Meneja Mauzo wa Bonite, Boniface Mwassi.
Wshindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-baada ya kukaidhiwa zawadi zao na Afisa Mwandamizi wa Mauzo wa Bonite, Godfrey Imani.
Baadhi ya washindi wakisubiri kukabidhiwa zawadi zao Wakazi 25 wa miji ya Moshi na Arusha wameimaliza wiki kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao walizojishindia kupitia promosheni ya kiwanda cha Coca-Cola cha Bonite kilichopo mjini Moshi inayojulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka”Zawadi walizojishindia wananchi hao ni pamoja na pikipiki 3,televisheni 7,na 15 pesa taslimu shilingi 100,000/- Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Bonite Bottlers, Chris Loiruk,alisema kampuni inayo furaha kuona wateja wake wataendelea kushiriki katika promosheni hii na kuweza kujishindia zawadi mbalimbali. 

Alisema Promosheni hii iliyozinduliwa mapema mwezi huu itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida .

”Zipo zawadi nyingi zimeandaliwa kwa ajili ya wateja wetu zikiwemo pikipiki,luninga bapa za kisasa,fedha taslimu kuanzia 5000 hadi 100,000/-na soda za bure, tunatoa wito waendelee kushiriki waweze kujishindia”.Alisisitiza Loiruk. Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kuandaa promosheni zenye mwelekeo wa kuwakwamua wateja wake kimaisha sambamba na kuleta furaha kwa familia kupitia kuangalia luninga za kisasa. 

Akiongea kwa niaba ya washindi wa pikipiki, Elisha Nanyaro Mkazi wa Tengeru, mkoani Arusha,alisema kuwa wanayo furaha kubwa kwa zawadi waliyojishindia na chombo hicho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha usafiri sambamba na matumizi ya biashara kwa ajili ya kuongeza pato la familia.

 Naye mmoja wa washindi Fransisca Mtuy,akiongea kwa niaba ya washindi wa luninga,alisema kuwa ushindi wa zawadi zao umekuja kwa wakati mwafaka ambapo mashindano ya soka ya kombe la Dunia yanakaribia,hivyo wataweza kuyaangalia pamoja na familia zao kwa kutumia luninga nzuri pia wataweza kufurahia habari na vipindi mbalimbali . 

 Kwa upande wake,Hawa Abrahamani,mjasiriamali na mkazi wa Arusha, akiongea kwa niaba ya washindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-alisema kuwa fedha walizojishindia zitawawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiwakabili sambamba na kuongeza mitaji yao ya biashara.

UJENZI WA JENGO LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI DODOMA, TBA YATAKIWA KUONGEZA KASI

$
0
0
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wamefanya ziara ya kutembelea eneo la mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume eneo la Njedengwa mkoani Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo.

Ujenzi huo unafanywa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) na Kusimamiwa na Chuo Kikuu Ardhi.

Kufuatia ziara hiyo Wajumbe wa NEC wameonesha kutoridhishwa na Kasi ya ujenzi ya Mkandarasi anayejenga ofisi hizo (TBA) na kutoa wito kwa mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) na Wajumbe wa Tume wakiangalia eneo la linapojengwa jengwa la Utawala la Tume ya Taifa ya Uchaguzi enero la Njedengwa mkoani Dodoma. Wajumbe wa NEC wametembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Ofisi za NEC mkoani Dodoma
 Hili ni Eneo la Maghala ya kuhifadhia vifaa vya Uchaguzi likiwa katika hatua za Ujenzi.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mradi kutoka TBA, Arch. Steven Simba.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) na Wajumbe wa Tume wakielekea katika eneo la ujenzi wa Ofisi za Tume mkoani Dodoma. Wengine alioambatana nao ni Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume kutoka Chuo Kikuu Ardhi QS Godwin Maro (kushoto) na Mhandisi Yohana Mashauri - Mhandisi wa Mradi huo kutoka TBA

WAANDISHI WA HABARI NI KUNDI MUHIMU KATIKA KUFIKISHA UJUMBE KWA JAMII.DC SONGEA

$
0
0
Vyombo vya habari,mitandao ya kijamii imeonekana kuwa na mchango mkubwa katika jamii kutokana na uwezo wa kufikisha ujumbe kwa haraka ukilinganisha makundi mengine.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya SONGEA POLOLET MGEMA wakati wa mafunzo kwa wataalamu watakaoenda kutoa chanzo kwa ajili ya kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wa watoto wa kike mwenye umri wa miaka 9 hadi 14 ambayo hufanyika leo mkoani Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.

WANANCHI KIJIJI LUMWAGO MAFINGA MJINI WASHANGILIA KUWAKA UMEME

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam,Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi wakiwa nafungua na kuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Lumwago kata ya Upendo Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa.NA FREDY MGUNDA,IRINGA. 

Airtel kuviwezesha vikundi vya kinamama kujiendesha kidigitali

$
0
0
· Zaidi ya vikundi vya wajasiriamali 100 kunufaika na huduma ya Timiza Vikoba na Mafunzo ya Tehama

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeviasa vikundi vya kina mama wajasiriamali kutumia fursa wanazozitoa kupitia bidhaa na huduma mbalimbali za kibunifu ikiwemo Timiza Vikoba ili kujiendesha kidigital na kukuza biashara zao. 
 
Hayo yalisemwa na meneja miradi wa Airtel Bi Jane Matinde wakati wa mkutano wa viongozi wa vikundi vya kina mama wajasiriamali jijini Dar uliondaliwa na Star Women group.

Akitoa ufafanuzi wa kina Matinde alisema “Timiza vikoba ni huduma inayowawezesha vikundi kuweka na kuchukua mikopo kupitia simu zao za mkononi kwa kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayotolewa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Maendeleo.

Timiza Vikoba inaviwezesha vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50 kujisaji na kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu”.

Matinde aliwashauri wanawake hao wajarisiamali kutumia njia za teknologia ya kisasa katika kufanya miamala ya kifedha kwa usalama, uhakika na urahisi zaidi kupitia huduma ya Timiza Vikoba “ huduma hii itawarahisishia sana kutuma pesa za michango na marejesho kupitia simu, itaokoa muda wa kukutana na kuweka uwazi kwani kila mwana kikundi anapoweka pesa fedha au kuomba mkopo kila moja anapata taarifa hapohapo nakuridhia, nawahimiza mchangamkie fursa hii.

Pamoja na huduma ya Timiza pia tunawawezesha kupata mafunzo ya Tehama kupitia maabara ya kompyuta ya Airtel fursa iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama. Tayari tunao wajasiriamali ambao wanaendelea kunufaika na masomo haya hivvo hii pia ni fursa kwenu kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi. Mafunzo haya ya Tehama yatawawezesha kutunza rekodi na mahesabu ya biashara vizuri zaidi, kutumia aplikesheni mbalimbali kuendesha biashara zenu kwa ufanusi na kukuza mitaji alisisitiza Matinde

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Star Women group na mwandaji wa mkutano huo, Bi Queen Cuthbert Sendiga aliwashukuru sana Airtel kwa kuwapatia wakinamama hao wajasiriamali fursa kupitia huduma na bidhaa zao na kuwaomba waendelea kushirikiana nao katika kutoa fursa hizi zitakazowainua wakina mama kwani ndio muhimili wa familia na kichochoe kikubwa katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla. Aidha aliahidi kuwahamasisha kina mama wengi kujiunga na masomo ya Tehama kwani uelewa bado ni Mdogo na pia kutumia technologia ya kisasa katika kuweka na kukopa kupitia huduma ya Timiza Vikoba.

Tangu kuzinduliwa kwa huduma ya Timiza Vikoba wachama zaidi ya 261,673 na vikundi 26,158 vimeshajiandikisha huku mikopo zaidi ya 774 yenye thamani ya shilingi milioni 49 kutolewa kwa vikundi hivyo

SEHEMU YA KWANZA YA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI.

$
0
0
Jina la vita vya Maji Maji lilitokana na imani ya matumizi ya “Dawa” iliyochanganywa na maji ,punje za mahindi na mtama zilizosadikika kuwa zitampa mpiganaji kinga ya kutodhurika kwa shambulio la risasi za Wajerumani .Kwa undani wa Historia hii ya Vita vya Maji Maji tizama sehemu ya Kwanza ya Historia ya Vita hivyo.

Benki ya Barclays Tanzania yasaidia kambi ya upasuaji watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi,yakabidhi kadi za bima ya afya (NHIF) 200 kwa watoto hao.

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy (wa tatu kushoto,) akikabidhi vifaa vya kusaidia upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa (wa pili kushoto), katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wengine ni watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.

Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy(kulia), akikabidhi kadi ya bima ya afya (NHIF) kwa mmoja wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi , Joy Jacob katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto (mstari wa nyuma) ni kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa, watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays. Madaktari wa upasuaji wa MOI wakifanya upasuaji mwa mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na tatizo la kichwa kikubwa katika kambi ya upasuaji iliyodhaminiwa na Barclays katika hospitali hiyo jana. Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji wa Mikopo Isiyolipwa wa Barclays Khatibu Mohammedy (nyuma katikati), wakishuhudia.

Baadhi ya watoto 200 waliopewa msaada wa kadi za bima ya afya (NHIF) na benki ya Barclays Tanzania wakionyesha kadi zao katika hafla hiyo katika hafla ambayo benki hiyo pia ilidhamini kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.

$
0
0

NA. Estom Sanga-

Wadau wa Maendeleo wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia kwa ufanisi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Mpango ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya umaskini kwa Walengwa wake.

Wadau hao wa Maendeleo ambao wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na Walengwa na kushuhudia namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa, wamejionea namna Walengwa wanavyoendelea kuboresha maisha yao kwa kutumia fursa ya kujumuishwa kwenye shughuli za Mpango zilizoanza takribani miaka mitano iliyopita.

Katika maeneo walikotembelea ikiwemo, Zanzibar, Korogwe,Shinyanga,Kagera, na Manyara,wadau hao wa Maendeleo walioambatana na Maafisa wa serikali na wale wa TASAF wameshuhudia mafanikio makubwa katika sekta za elimu, afya,ujenzi wa nyumba ,kilimo ,ufugaji na miradi ya uchimbaji wa malambo ya maji na jitihada mpya za kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana miongoni mwa Walengwa ili kukuza zaidi uwezo wao kiuchumi.

Wadau hao wa Maendeleo pia wamevutiwa zaidi na namna Walengwa wa TASAF walivyoamua kwa hiari yao kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF-na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote wa mwaka katika kaya husika, huku katika maeneo mengi mahudhurio ya watoto wanaotoka kwenye Kaya za Walengwa yamekuwa mazuri ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa shughuli za Mpango.

Kutokana na mabadiliko chanya kwa Walengwa, Kumekuwa na mahitaji makubwa ya Wataalamu hususani wa Ugani ambao wanahitajika kusaidia jitihada za Walengwa hao wa TASAF kutekeleza miradi ya kiuchumi wanayoianzisha ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi, ng’ombe,nguruwe,bata, na kilimo kulingana na maeneo yao.

Aidha imebainika kuwa idadi kubwa ya Wananchi ambao hawakupata fursa ya kuorodheshwa kwenye shughuli za Mpango ,wangelipenda kupata fursa hiyo ili waweze pia kunufaika na huduma zitolewazo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.Hata hivyo kwa nyakati tofauti Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amezungumzia dhamira njema ya serikali ya kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanaostahili kunufaika na shughuli za Mpango wanafanya hivyo nchini kote. Amesema serikali itafanya hivyo pindi fedha zitakapapatikana.

Hii leo Wadau hao wa maendeleo kutoka taasisi zinazochangia utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA zilizoko katika vijiji zaidi ya ELFU TISA sawa na asilimia 70 ya vijiji vyote nchini, wanaendelea na Mkutano wao kwenye Ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF .
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaoendela kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.

Mmoja wa Maafisa wa TASAF ,Peter Lwanda aliyeshika kipaza sauti, akiwasilisha taarifa ya ziara ya wadau waliotembelea mkoa wa Shinyanga kuona utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wakifuatilia taarifa inayowasilishwa na mmoja wa Maafisa waliotemebelea maeneo ya utekelezwaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akijadiliana jambo na Kiongozi wa Shughuli za TASAF Benki ya Dunia Mohammed Muderis kwenye Mkutano wa Wadau.

SPIKA EALA AIPONGEZA TANZANIA KWA MAENDELEO

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Martin Ngoga (watatu kushoto) baada ya mazungumzo, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. Wengine pichani ni Wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, kutoka kushoto ni Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Martin Ngoga, Bungeni mjini Dodoma Aprili 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe.Martin Ngoga kabla ya mazungumzo yao, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018.
 
SPIKA wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dkt. Martin Ngoga ameishukuru na kuipongeza Serikari ya Tanzania kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa reli kwa sababu inaleta manufaa hata kwa nchi jirani.

"Miradi hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa kwa kasi si kwamba inachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, bali hata wa nchi nyingi za jirani kwa kuwa nazo zitanufaika na miradi hiyo kwani si nchi zote zina bandari".

Dkt. Ngoga ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 23, 2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Bungeni mjini Dodoma.Amesema tayari wamejadili ripoti iliyotokana na ziara iliyofanywa na wabunge hao katika upande wa korido ya kuishi na korido ya kaskazini ambapo wametoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na baraza la mawaziri.

"Tayari tumeshajadili miswada miwili inayohusu Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na mswada wa Takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2017."Pia Spika huyo amesema wamefurahia uwepo wao nchini, ambapo mbali na shughuli zao za kibunge pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wameshiriki kampeni ya kukijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1,000 kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema amefarijika na uamuzi wa Bunge la EALA kufanya vikao vyake katika nchi wanachama kwa sababu unatoa fursa ya kujua mazingira ya nchi hizo pamoja na maendeleo yake.Amesema nchi wanachama wanamatumaini makubwa na bunge hilo katika kuimarisha na kuboresha maendeleo ya mataifa yao, hivyo amewatakia mjadala mwema.

Katika hata nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wabunge hao na marafiki zao kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanja, utalii, kilimo na madini.Kwa mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) vinafanyika Dodoma katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa ulipo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vilianza Aprili 17, 2018 na vinatarajiwa kumalizika Aprili 29, 2018.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,41193 - 
DODOMA.
JUMATATU, 
APRILI 23, 2018.

Water as an immediate energy solution for Tanzania

$
0
0
It is common knowledge that water sustains alllife on Earth and that nothing can be grown or survivewithout it. When used effectively, water can also provideclean electricityfor millions of people. In this review, we will discuss how it can be done without affecting the environment and why it is so important to us in Tanzania. 
Tanzania has abundant energy sources, most of which remain unexploited. Hydro has traditionally played a significant role, with an installed capacity of 562 MW, which accounts for roughly one-third of the total installed power capacity. With a hydro potential of 4.7 GW, the country plans to further development this source, but views weak transmission infrastructure as a significant short-term barrier.

Only 41% of the population currently has access to electricity. Low population density and expensive transmission costs have led to the government adopting targeted policies to develop off-grid schemes in order to increase the current levels of rural electricity access.


Power where it is needed

Minihydro power planttechnology available today may serve as an important alternative to traditional large scale hydro power generationinTanzania, because the resources of minor water streamsare practically omnipresent. Mini hydro power plantsare quick, cost effective and simple to installand maintain, and supplyecologically clean and affordableelectricity.Hungarian companyGANZ EEM, a subsidiary of state owned Russian nuclear corporation Rosatomrecently presented an innovative portable mini hydro power plant for the African market. The containerisedunits are easy to transport and are great forelectricity generation in remote areas.

Rosatom Central and Southern Africa regional vice-president Dmitry Shornikov notes that, “Rosatom offer numerous energy solutions for African countries and one of the most promising is our innovative containerized mini-hydropower plant, with a design capacity of up to 2 MW. A single facility is capable of providing electricity to between 250 and 400 houses for roughly 40 years”.

The mini hydro plants which have a life span of roughly 40 years and a warranty of 12 years can be monitored and operated remotely from anywhere in the world. The plantswhich operate at a 93% capacity factor requireminimalhead, and do not require dam construction and therefore cause no environmental harm to river and other reservoir ecology.

Mini Hydro plantsare able to meet electricity requirements for residential, retail and corporate consumers in remoteareas where central supplies are not available or where transmission lines aredifficultor costly to install.

Mini Hydro plants are also an excellent alternative to inefficient, costly and ecologically unfriendly diesel generators. The units can be installed inline of existing pipelines and are therefore also perfect for the mining and manufacturing sectors, particularly those that use a great deal of water. The plants dramatically reduce electricity costs and ultimately reduce production costs, making local products more cost effective on the global market.

WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO.

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo, Kwa Mawaziri walipokutana kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dodoma Aprili 23, 2018.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

………………………………………………………………

Na.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.

Ametoa kauli hiyo leo (Aprili 23, 2018) alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.

Waziri Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.

“Namtaka Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri Mhagama

Aidha amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache mara moja kwa mujibu wa sheria.

Waziri Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi

Pamoja na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista ya mali za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.

“Msajili wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kuwa na regista ya mali zake ndani ya wiki tatu kuanzia leo kwani kukosa daftari la mali za kudumu ni kinyume na kifungu Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya mwaka 1992.”alisisitiza Waziri.

Sambamba na hilo Waziri alimtaka Msajili wa Vyama vya siasa kuhakikisha vyama vyote vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili kuondokana na mapungufu ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama vitatu kati ya tisa vina nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.

“Msajili wa vyama ahakikishe vyama vya siasa vinatekeleza miongozo yote kihasibu pamoja na kanuni za fedha, ambazo zinaelekeza nyaraka ziwe na viambatisho sahihi kwani ripoti ilibainisha vyama vitatu vilikuwa na malipo yenye nyaraka pungufu zenye thamani ya shilingi 735,978,559 ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa uhalali wa malipo hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.

Awali kifungu cha 14(1)(a) na (b)(i) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kinaelekeza kuwa, kila chama cha siasa kinapaswa kutunza taarifa za mapato na matumizi, ikiwamo taarifa za mali zake. Vile vile, kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, taarifa ya hesabu zake zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja taarifa ya mali zake.

Hivyo, Kifungu hicho kinampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa hesabu za kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Katika mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2017, CAG amefanya ukaguzi wa hesabu za Vyama vya Siasa kumi ikiwemo; CCM, CHADEMA, NLD, TLP, Demokrasia Makini (MAKINI), TLP, DP, SAU, AFP, CCK na ADC kati ya vyama vya siasa kumi na tisa vyenye usajili wa kudumu. Vyama vya Siasa tisa (9) havikuwasilisha hesabu zake kwake kwa wakati kwa ajili ya ukaguzi, hivyo hakukaguliwa.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA JENGO LA PSPF PLAZA NA TAWI LA BENKI YA NMB MJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na viongozi mbalimbali baada ya kufunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini Dodoma leo April 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi mbalimbali akiakata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini  Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage mijini Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na viongozi wengine kukata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kitengo cha huduma kwa wateja akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kuzindua rasmi Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Jengo la PSPF Plaza na Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018. Picha na IKULU

TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA),imeingia makubaliano ya miaka mitatu na Shirika la Viwango nchini (TBS) katika kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha wajasiriamali na wafanyabiashara wanahudumiwa katika kukuza kazi zao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Agness Kejo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa pamoja kati ya watendaji wa TFDA na TBS,ambapo amesema amesema kuwa changamoto za wafanyabishara na wajasiriamali ni vema zikapatiwa ufumbuzi wake ili watimize malego yao kwa maslahi ya Taifa.

Amefafanua kwenye ujenzi wa viwanda nchini kunategemea mashirika ya TBS na TFDA katika kuviwezesha viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na hatimaye kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ya nchi.

Amesisitiza hakuna sababu ya mjasiriamali au mfanyabishara kutumia muda mwingi kupata huduma kutoka TBS au TFDA , hivyo ni vema wakashirikiana katika kuondoa changamoto ambazo zipo na huenda zinakwaza wadau hao muhimu katika maendeleo ya nchi

Kejo ameongeza watendaji katika pande mbili hizo ni lazima waendane na azma ya Serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda kuwasaidia afanyabiashara na wajasiriamali kupata elimu kuhusu bidhaa watazozalisha kwa kuzingatia ubora.Aidha amesema ushirikiano huo umefanyika na shirika la Viwango 
Zanzibar ikiwa ni kujenga Tanzania kwa pamoja katika kufikia uchumi wa kati watanzania.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kati watendaji wa TFDA na TBS katika vituo vya kanda na ipakani kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na taasisi hizo,  jijini Dar es Salaam.
 aimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula  (TFDA), Justin Makisi akizungumza kuhusiana na ufunguzi na mada zitakazojadiliwa katika kufanya kazi kama timu, jijini Dar es Salaam.
03. Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa TFDA na TBS

Wakazi Dar, Mtwara kuanza kunufaika na Huduma ya Usambazaji Gesi yenye Punguzo ya bei ya Asilimia 40

Serikali kuanza kutoa hati za viwanja kwa njia ya kielektroniki

WANAWAKE WA GAIRO WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KATIKA KUANZISHA VIWANDA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akipongezwa na mchungaji Canon Chamwenye wa kanisa Anglikana Msingisi mara baada ya kumaliza kuongea na akina mama juu ya kuanzisha kiwanda ili waweze kujikwamua katika maisha yao.
Mmoja ya akinamama akitoa shukrani ya kuku kwa mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe afanikisha ushawishi wa ujenzi wa viwanda kwa kuanzia na wanawake kanisa la Anglikana Dinari ya Rubeho Gairo. Ushawishi huo ulianza mwezi wa sita mwaka 2017 ambapo Mhe. Mchembe alihudhuria mkutano wa wanawake wa kanisa hilo akiwa Mgeni Rasmi. 

 Katika mkutano huo Mhe. Mchembe aliwashawishi akinamama hao kupitia umoja wao waanzishe kiwanda ili kiwainue kiuchumi. Aidha wapate mahali pa kuuza mbegu za alizeti ambazo kwa sasa alizeti ni kati ya mazao makuu ya biashara wilayani Gairo. 

 Hatimaye mpango umekamilika na Mhe. Mchembe amechangia pesa za Kitanzania shilingi laki tano kuhamasisha ujenzi wa kiwanda. Jumla ya gharama ya mradi ni shilingi milioni kumi na tisa. Majengo yanaendelea kufunguliwa na mradi unategemewa kuanza mwishoni mwa mwaka 2018. Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wana Dinari hiyo iliyojumuisha Kata ya Rubeho na Msingisi. Wanawake ni nguzo ya Maendeleo na uchumi wa viwanda.

RAIS MAGUFULI AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA UWEKEZAJI WENYE TIJA DODOMA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
 Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la kitegauchumi mkoani Dodoma.

Kilichomfanya Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa 12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Aprili 23, 2018.

“Ninyi mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” 

Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 


Rais pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.“Nimefurahi kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania, ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira wakati wa ujenzi.” Alipongeza. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema, PSPF ndio Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii kuweka kitegauchumi cha jingo mkoani Dodoma na hivyo kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuhamia makao makuu ya Nchi, mjini Dodoma. 

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akielezea historia ya uwekezaji huo alisema, Mfuko ulipewa viwanja vya mradi huu na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mwaka 2012 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuendeshea shughuli za Mfuko pindi inapotokea dharura (business continuity) pamoja na kibiashara. Kazi ya usanifu na ujenzi wa jengo hili lilianza Julai 2015 na kukamilika Januari 2018 na kwa sasa jengo liko kwenye kipindi cha uangalizi (Defect Liability Period) ambacho kitaisha Januari 2019. Gharama tarajiwa za mradi yaani “contract sum” ni shilingi bilioni 37.02. Mpaka sasa Mfuko umeshalipa kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 30.56. 

Jengo hili lina minara miwili, mmoja ukiwa na ghorofa 11 na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60 pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara. 

“Hadi sasa jengo limepata wapangaji ambao kwa uchache ni kama ifuatavyo; NMB Bank, AZANIA Bank, TIB Corporate Bank, Benki ya Kilimo, GIZ, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TASAF, TANAPA, TBS, Gaming Board, PPRA, Makao Makuu ya TARURA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao hawa pamoja na wengine wanafanya jengo kuwa limepangishwa kwa asilimia 98. Na kufikia leo Mfuko umeshakusanya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 1.06 bilioni kutokana na malipo ya pango na tunatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka na kufikia miaka minane mradi utakua umerejesha fedha zote zilizowekezwa.”Alibainisha Bw. Mayingu. 
Rais akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Mhandisi Musa Iyombe, akitoa hotuba yake.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, (wakwanza kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Siro, wakati wa uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa PSPF
Mameneja wa PSPF
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Binilith Mahenge, (kushoto), akipokewa na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akiwasili kwenye eneo la tukio.
Rais, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wadhamini na wafanyakazi wa PSPF.
Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi.Costantina Martin, (kushoto), akibadilishana mawazo na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abass, (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Kikundi cha Sanaa kikitumbuiza kwenye hafla hiyo.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images