Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

KIGWANGALA ATUMIA NGORONGORO MARATHON KUWATUMIA SALAMU MAJANGILI

$
0
0
PICHANI: Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (fulana nyekundu) akiwa na uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) pamoja na baadhi ya washiriki wa mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika leo Aprili 21, 2018. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA Profesa Abiud Kaswamila (namba 002), Mhifadhi Mkuu wa NCAA Dkt. Fred Manongi (namba 003) na Meneja Mahusiano wa NCAA Joyce Mgaya (kulia waliosimama). (Picha na Yusuph Mussa Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, Karatu
Immamatukio Blog

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala ametuma salamu kwa majangilli wanaojihusisha na uwindaji haramu wa wanyama kwenye Hifadhi za Taifa ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Amesema Serikali na wadau wengine wamejipanga kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa kwa kudhibiti ujangili wa wanyama na viumbe hai vyote vinavyotokana na maliasili yetu ya asili kwenye hifadhi za Taifa.

Dkt. Kigwangala alituma salamu hizo kupitia Mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika leo Aprili 21, 2018 kwa kuanzia Lango Kuu la kuingilia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu mkoani Arusha.

Pamoja na kuwa mgeni rasmi kwenye mbio hizo, Dkt. Kigwangala pia alikimbia kilomita 21 kuanzia saa 3.30 asubuhi na kumaliza saa 6.20 mchana, na kusema hiyo ni ishara tosha ya kujipanga na kukabiliana na majangili. Dkt. Kigwangala alisema kwa kumaliza mbio hizo, sio tu anawatishia majangili kuwa yupo vizuri kukabiliana nao, bali anataka askari wote wa wanyama pole wawe wakakamavu na asimuone askari yeyote mwenye kitambi.

"Moja ya malengo ya mbio za Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu ni kupambana na ujangili na majangili. Na sikumaliza mbio hizi za kilomita 21 kwa bahati mbaya, bali ni kuwadhihirishia majangili na watu wote wenye nia mbaya na rasilimali zetu kuwa nipo fiti.

"Lakini sio kwa majangili, hata kwa askari wetu, nataka kuwaeleza kuwa kuanzia sasa sitaki kuona askari anakuwa na kitambi. Hatuwezi kupambana na majangili kama askari wetu wana vitambi na wapo legelege... Na nataka kuwaeleza askari kama wanataka twende nao pamoja kwenye hili basi wajipange" alisema Kigwangala.

Dkt. Kigwangala alisema nia nyingine ya NCAA kudhamini mbio hizo ni kutangaza shughuli za utalii ndani na nje ya nchi, kwani anaamini kupitia waandishi wa habari na washiriki wa mashindano hayo kutokea ndani na nje ya nchi, itawezesha kuongeza watalii na hifadhi hiyo kujulikana zaidi.

Naye Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka, alisema moja ya mambo yanayotushinda nchini ni kujitangaza, lakini hapo hapo kushindwa kupenda vya kwetu, kwani pamoja na kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, lakini matangazo yake mengi yapo Kenya.

Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alisema amefurahishwa na uongozi wa NCAA kudhamini mashindano hayo, kwani yatawezesha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kufahamika duniani kote.

"Kwenye Serikali ukiwa na mtu kama Dkt. Fred Manongi (Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) mambo yatakwenda vizuri. Tumempa taarifa wiki mbili kabla ya mashindano kumuomba atudhamini, lakini akawa amekubali na mambo yamekwenda vizuri.

"Hiki cha kukubali kudhamini mashindano haya ni kikubwa sana. Sasa anatufanya Watanzania tuanze kujitangaza na kupenda vya kwetu. Hili tatizo la kushindwa kujitangaza ni kubwa ndiyo maana kila siku kuna malalamiko kuwa Kenya wanajitangaza Mlima Kilimanjaro ni wa kwao. Sisi sasa tujitoe na kuonesha rasilimali hizi za utalii ni za kwetu" alisema Mtaka.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akionesha medali yake kwa waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mbio za Ngorongoro Marathon (kilomita 21). Alimaliza mbio hizo saa 6.20 mchana. Mbio hizo zilizoanza leo Aprili 21, 2018 saa 3.30 asubuhi kwenye lango kuu la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), zimehitimishwa kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu. NCAA ndiyo wadhamini wakuu wa mbio hizo. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akihutubia wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha mara baada ya kumalizika mbio za Ngorongoro Marathon leo Aprili 21, 2018 na kuhitimishwa kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu. Wa pili kulia ni Rais wa Chama cha Riadha (RT) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA Profesa Abiud Kaswamila. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Fred Manongi (kulia), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Jubilate Mnyenye (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Cecilia Pareso (katikati) wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (hayupo pichani) kwenye kilele cha mbio za Ngorongoro Marathon zilizohitimishwa kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu leo Aprili 21, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).


CHANJO YA KUKINGA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI HAIATHIRI UWEZO WA BINTI-HINCHA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

MRATIBU wa chanjo Mkoa wa Pwani, Abbas Hincha amesema, jumla ya watoto wa kike 18,823 waliopo shule na nje ya shule mkoani hapo wanatarajia kupatiwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu. Aidha ameitoa shaka jamii kuwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ni salama, haina madhara na haiathiri uwezo wa binti kupata watoto hapo baadae .

Akitolea ufafanuzi juu ya suala hilo, wakati wa semina kwa wanahabari kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, Kibaha, Hincha alisema tayari wameshapokea chanjo na wataanza kuzitoa katika vituo mbalimbali vya huduma.

Pamoja na hayo ,alivitaka vyombo vya habari kubaini uzushi ama uvumi kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya katika mamlaka husika na kutoa mrejesho kwenye jamii baada ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu.

Hincha alieleza chanjo hiyo haina madhara na badala yake ina viudhi vichache kama ilivyo kwenye chanjo nyingine ikiwemo kuweka wekundu ama kuweka uvimbe kiasi eneo alilochomwa mhusika mkono wa kushoto. Aliwataka wazazi na jamii kuacha kudanganyana na kuzusha mambo ambayo yatakwamisha juhudi za kutolewa chanjo hiyo .

Mratibu huyo ,alisisitiza serikali imethibitisha usalama wa umadhubuti wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ndiyo maana imeiongeza kwenye mpango wa Taifa wa chanjo ili iweze kusaidia kudhibiti tatizo hilo kwa akinamama.

Alisema mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi mbili.

"Dozi ya pili itatolewa miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza" alisema Hincha .

Hincha alisema chanjo ya HPV kwa wasichana huwakinga wasipate saratani ya mlango wa kizazi pindi wawapo watu wazima wakiwa na familia zao.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa huo ,Hussein Athumani  ambae pia anaesimamia masuala ya kinywa na meno Mkoani Pwani,alisema  saratani hiyo ina athari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote. Alisema inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea.

Athumani alisema saratani hiyo inashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake, nafasi ya kwanza inashikwa na saratani ya matiti .

"Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti " Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakinamam vitokanavyo na saratani"alibainisha Athumani.

Alifafanua chanjo hiyo inagharama kwani dozi moja ni dollar 15 ambapo dozi mbili ni dollar 30. Athumani alielezea ,wanawake 7,304 nchini wamegundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi kati ya hao 4,216 asilimia 18 walifariki kutokana na tatizo hilo .

Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika semina hiyo ,Gerald Manase kutoka TAMISEMI alisema ,wasichana na wanawake wanaohitaji huduma ya chanjo ambao sio walengwa wa uanzishwaji wa chanjo hiyo inayotolewa na mlango wa Taifa wa chanjo wanaweza kupata chanjo katika hospital binafsi zinazotoa chanjo hiyo .

Dalili za saratani hiyo ni maumivu ya mgongo,miguu  ,kiuno,kuchoka,kutokwa damu nyingi bila mpangilio baada ya kujamiiana,uchafu kwenye uke wa majimaji,kuvimba miguu na inasababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalamu kama human papilloma virus(HPV).

BENKI YA DUNIA YAONESHA NIA KUSHIRIKI UJENZI RELI YA ISAKA - KIGALI

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania (kulia) na ujumbe wa Benki ya Dunia (kushoto) wakiwa katika majadiliano ya miradi ya maendelea inayotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka ujao wa fedha.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop akitoa ufafanuzi wa miradi ambayo itatekelezwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bi. Mamta Murthi .
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akielezea miradi ambayo itatekelezwa kwa mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Prof. Florens Luoga.

Na. WFM- Washington DC

Benki ya Dunia imeonesha dhamira ya kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka kwenda Rusumo na baadae Kigali pamoja na miundombinu mingine ya usafirishaji  kama barabara ili kusaidia kuendeleza biashara na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati wa majadiliano na wataalamu wa Benki ya Dunia yaliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, kwenye mikutano ya mwaka ya kipupwe inayoendelea mjini Washington DC Marekani.

Dkt. Mpango amesema kuwa miradi ya Kikanda ambayo Benki hiyo imeonesha nia ya kuitekeleza ni ile ya uboreshaji wa mazingira na bandari katika ziwa Victoria zikiwemo za mikoa ya Mwanza, Musoma na Kigoma na Bandari zilizoko katika Ziwa Tanganyika ambazo zitarahisisha usafiri wa kwenda Burundi na Congo.

‘Miradi hii ya Kikanda na Kitaifa ambayo Benki ya Dunia imepanga kuitekeleza kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa mwaka ujao wa fedha itahakikisha kunakuwa na mazingira endelevu na tija kwa kuwa inagusa nchi zote zinazozunguka maziwa hayo mawili’, alieleza Dkt. Mpango.

Amesema kuwa ni lazima kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kadri iwezekanavyo ili kuendelea kufaidi rasilimali za maziwa hayo makubwa  kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na nchi jirani zinazozunguka maziwa hayo.

Aidha amebainisha kuwa mwakani, Benki ya Dunia imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya tekeleza mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji eneo la Ruhuji ambapo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 300.

‘Eneo hili la sekta ya umeme ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya viwanda kwa kuwa uchumi wa viwanda hauwezi kukua bila kuwepo umeme wa uhakika’ alifafanua Waziri Mpango.

Vilevile Benki ya Dunia (WB) imekubali kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo katika uchambuzi wa miradi mbalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania kutokuingia kwenye madeni makubwa zaidi ambayo hayawezi kulipika.

Waziri Mpango alieleza kuwa kutokuwa na ufanisi wa kutosha katika kuchambua miradi ambayo inagharamiwa na fedha za mikopo inasababisha nchi kubeba mzigo mkubwa wa madeni hivyo ni vyema Tanzania ikahakikisha kuwa miradi hasa ile inayogharamiwa kwa fedha za mikopo inachambuliwa vizuri ili mradi husika unapokamilika uweze kulipa deni.

Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali itakua na miradi mingi ya kutekeleza, miongoni mwa miradi hiyo ni kupambana na tatizo la utapiamlo hivyo ni vema kama nchi ikaangalia namna bora ambayo Benki ya Dunia inaweza kusaidia katika utekelezaji wake.

“Kitaalamu mpaka mwanadamu anapofikisha siku 1000 ni kipindi muhimu sana kinachoamua maisha ya mwanadamu atakapokuwa mtu mzima atakuwa na uwezo gani wa kufikiri, kutokana na hali hiyo mtu ambaye atakua na utapiamlo uwezo wake utakua ni mdogo zaidi kulinganisha na mtoto aliyepata lishe bora’” alifafanua Dkt. Mpango.

Katika kutekeleza mradi huo Serikali itafanya kazi na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi ya Chakula na Lishe ili kuhakikisha kwamba Taifa linapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la utapiamlo.

Mikutano hiyo ya mwaka ya kipupwe kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Wataalamu wa Benki ya Dunia imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa Tanzania itanufaika kutokana programu mbalimbali ambazo zitagharamiwa na Benki ya Dunia kwa mikopo nafuu.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA AZUNGUMZIA FURSA AMBAYO NCHI YETU IMEIPATA KWENYE MAONESHO YA UTALII

$
0
0
Na Ripota Wetu, China.

BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema zaidi watu 1,000 wamepata fursa ya kutembelea banda la Tanzania ambalo lilikuwepo kwenye maonesho ya utalii nchini humo.

Idadi hiyo ya watu ambao wametembelea banda la Tanzania imesaidia kuwapatia taarifa sahihi na za kutosha kuhusu utalii wetu na ni moja ya eneo ambalo limetumika vema kutangaza vivuto vilivyopo.

Balozi Kairuki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye maoesho ya utalii yaliyofanyika nchini China ambayo yamemalizika hivi karibuni.

Akifafanua zaidi kuhusu Maonyesho ya biashara ya Utalii (China Outboard Travel & Tourism Market COTTM) yaliyomalizika hivi karibuni jijini Beijing China Balozi Kairuki amesema maonesho hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa.

"Zaidi ya watu 1,000 wameweza kutembelea banda la Tanzania hatua ambayo imesadia watu wengi kupata taarifa za kutosha kuhusu fursa za Tanzania.Naipongeza bodi ya utalii na mamlaka zote za utalii Tanzania pamoja na mawakala wa utalii ambao walishiriki kwa lengo la kuchangamkia fursa hiyo,"amesema.

Ameogeza soko la China ni jipya na linalokua kwa kasi,hivyo matarajio yao hizo taasisi za bodi ya utalii, Hifadhi ya Ngorongoro ,TANAPA watapewa nguvu zaidi, watawezeshwa kibajeti ili wakushiriki maonyesho mengi zaidi hapa China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (Kushoto) akishiriki mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yaliongozwa na Bi. Mei Qing  mtangazaji maarufu wa Television hiyo.
 Afisa Utalii kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Piter Makutian (Kushoto) akizungumza jambo katika  mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yalifanyika wakati wa Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.
 Mahojiano yakiendelea  yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel"
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mahojiano kwenye kituo cha runinga  cha  "Chinese Satelite Travel" 
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) akipata maelezo kuhusu Maonyesho ya Utalii  kutoka kwa Afisa Utalii Mwandamizi - Hifadhi ya Taifa Tarangire Theodora Aloyce (katikati), Wa pili kushoto ni Afisa Utalii habari  - Bodi ya Utalii Tanzania, Irene  Mville, Afisa Utalii- Mamlaka ya Hifadhi  ya Eneo la Ngorongoro, Piter Makutian (wa pili kulia) na Afisa Kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China, Lusekelo Gwassa
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini China, Remidius Emmanuel(Kushoto)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Safari, Peter Larocque inayofanya kazi zake nchini Tanzania.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MJINI DODOMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6. Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota mjini Dodoma. Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula. Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mradi huo mkubwa na baada ya kukamilika utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, hivyo amewataka viongozi wa NFRA wahakikishe kwamba hakuna mahindi yatayoharibika katika maghala yao.

”Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha NFRA inakuwa na uwezo wa kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya dharula lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bila vikwazo”.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakuu wa Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanatimiza wajibu wao ili mradi ukamilike kwa wakati.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bibi Vumilia Zikankuba alisema mradi huo unatekelezwa katika maeneo manane ya Kanda za Wakala huo ambayo ni Dodoma (Dodoma), Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga (Shinyanga), Babati (Manyara).

Bibi Vumilia alisema katika Kanda ya Dodoma wanajenga vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na kufanya kanda hiyo kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,000 kutoka uwezo wa sasa wa tani 39,000. Alisema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

“Utekelezaji wa mikataba kati ya NFRA na wakandarasi ulianza Desemba 2017 ambapo muda wa utekelezaji ni miezi 18 tangu tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji wa mikataba ya wakandarasi, hivyo kabla ya 2020 utakuwa umekamilika”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama. Wengine ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Anthon Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Balozi wa Poland nchini Tanzania, Balozi Krzysztof Buzalski.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzystof Buzalski na kulia Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.
Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai akizungumza Katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018. Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wabunge na Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliopozungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.

MAKAMBA: MUUNGANO NI URITHI WETU, TU UTUNZE.

MAJIBU YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU HOJA ZA WABUNGE

UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI UMEIMARIKA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.

Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.

Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mradi huo mkubwa na baada ya kukamilika utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, hivyo amewataka viongozi wa NFRA wahakikishe kwamba hakuna mahindi yatayoharibika katika maghala yao.

”Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha NFRA inakuwa na uwezo wa kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya dharula lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bila vikwazo”.

Hata hivyp, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakuu wa Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanatimiza wajibu wao ili mradi ukamilike kwa wakati.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bibi Vumilia Zikankuba alisema mradi huo unatekelezwa katika maeneo manane ya Kanda za Wakala huo ambayo ni Dodoma (Dodoma), Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga (Shinyanga), Babati (Manyara).

Bibi Vumilia alisema katika Kanda ya Dodoma wanajenga vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na kufanya kanda hiyo kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,000 kutoka uwezo wa sasa wa tani 39,000.

Alisema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

“Utekelezaji wa mikataba kati ya NFRA na wakandarasi ulianza Desemba 2017 ambapo muda wa utekelezaji ni miezi 18 tangu tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji wa mikataba ya wakandarasi, hivyo kabla ya 2020 utakuwa umekamilika”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama.

Wengine ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Anthon Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya naBalozi wa Poland nchini Tanzania, Balozi Krzysztof Buzalski.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMAMOSI, APRILI 21, 2018.

WANANCHI WAPEWA TAHADHARI YA ONGEZEKO MARADHI YA MATUMBO YA KUHARISHA ZANZIBAR

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 

Jamii imetakiwa kuchukua tahadhari juu ya Ongezeko la Maradhi ya Matumbo ya kuharisha ambayo yameanza toka kuanza kwa msimu wa Mvua za masika katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Tahadhari hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi Kinga Zanzibar Dkt Mohamed Dahoma alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa Maradhi Zanzibar.

Amesema toka kuanza kwa msimu wa Mvua za masika Kituo cha ufuatiliaji wa mwenendo wa maradhi Zanzibar kimebaini zaidi ya Wagonjwa 700 wa Matumbo ya kuharisha.“Mpaka sasa hivi hakuna Mgonjwa wa Kipindupindu Zanzibar iliyokuwepo ni kuongezeka kwa Maradhi ya Matumbo ya kuharisha.

Ni wajibu wetu kuchukua tahadhari” Alisema Dkt Dahoma.Hata hivyo amesema hadi sasa hakuna Mgonjwa wowote aliyebaiwa kuugua Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar.Kutokana na hali hiyo Wizara ya Afya inatoa tahadhari ili Jamii iweze kujilinda ipasavyo dhidi ya maradhi hayo.

Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Taasisi zake mbali mbali inaendelea na juhudi zake kuhakikisha taaluma ya afya kwa wananchi inawafikia na kutoa huduma stahiki kwa wale wote walioahirika na maradhi ya matumbo katika Vituo vya afya.Dkt Dahoma ametoa Wito kwa jamii kuwapeleka katika Vituo vya matibabu wagonjwa wote watakaobainika kuharisha badala ya kuwatibia majumbani.Amesema Serikali imejipanga kwa Vifaa Dawa na Madaktari wa kutosha kuhakikisha kila anayeathirika na maradhi hayo anatibiwa ipasavyo.

Akielezea kuhusua maradhi ya Matumbo ya kuharisha Dkt Dahoma amefafanua kuwa Maradhi hayo hutokana na mrundikano wa uchafu na husambazwa kupitia kinyesi kuingia katika chakula au maji.Hivyo ni wajibu wa jamii kuhifadhi vyanzo vya maji na chakula dhidi ya maradhi hayo.

Aidha amesisitiza kunawa vyema kwa sabuni kabla na baada ya kula na kutumia maji yaliyochemshwa kwa ajili ya kunywa.Zanzibar hukabiliwa na Mvua za Masika kila ifikapo mwezi machi na hadi May ambazo licha ya kuwa Neema kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, huambata na mitihani ikiwemo maafa, maradhi ya kuharisha na kipindupindu.
KAIMU Mkurugenzi Kinga Dkt Moh’d Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ongezeko la maradhi ya kuharisha toka kuanza kwa msimu wa Masika-Picha na Abdalla Omar

MAKAMBA: MUUNGANO NI URITHI WETU, TU UTUNZE.

$
0
0
1


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua kongamano la vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo mkoani Dodoma. Jumla ya Vyuo sita vimeshiriki katika Kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Mipango, Dodoma na mada kuu ikiwa ni fursa zilizopo katika Muungano.

Sehemu ya wanafunzi kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kongamano hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma na kuhudhuriwa na wanafunzi kutoka Vyuo vya Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara, St. John, Chuo cha Mipango, Chuo cha Madini na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Waratibu wa kongamano hilo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Bi. Lupy Mwaikambo, Bw. Sifuni Msangi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.


Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018

$
0
0









Dar es Salaam, Tarehe 20 Aprili 2018.... Kampuni ya Uber imemtangaza msanii Idris Sultan kuwa balozi wake mpya nchini Tanzania mwaka 2018. Idris anakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuwa balozi wa Uber, programu ya usafiri yenye umaarufu mkubwa, nchini Tanzania.
Msanii huyu wa uchekeshaji, muigizaji wa tamthlia, na mtangazaji wa vipindi vya redio ametangazwa rasmi katika hafla ya kukata na shoka iliyokwenda kwa jina la #IdrisnaUber iliyohudhuriwa na wageni wachache na wanahabari wa humu inchini. Shughuli hiyo imefanyika katika mgahawa wa kifahari wa Akemi jijini Dar es Salaam.
Tangu mwanzoni mwa zoezi hili, tulifanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba tunampata balozi mwenye ufuasi mkubwa na atakayeiletea Uber ufanisi nchini Tanzania,amenukuliwa Bi.Elizabeth Njeri, Meneja wa Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki. Idris Sultan ni mcheshi na ni msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji,tamthlia, na utangazaji wa vipindi vya redio.

 Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu ni mzalendo kweli kweli - yeye ni kielelezo cha Utanzania na anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati. Hizi ndizo sifa tunazosistiza tunapotaka kuwa na mkataba na mabalozi wa kampuni yetu kwa sababu zinasaidia sana katika kuonesha kwamba tunajali maslahi ya wasafiri na madereva wanaotumia mfumo wetu nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Alfred Msemo; Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, alisema; “Kampuni ya Uber inajituma kutumia uwezo wake kupitia oparesheni zake kimataifa ili kuwa karibu na wateja wake humu nchini. Mchango wa Idris Sultan katika muziki wa Tanzania unaendana na dhamira yetu ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo wetu hapa nchini. Tutaendelea kuwahudumia wasafiri wetu sambamba na kutoa fursa za ajira kwa madereva wanaotumia mfumo wetu.
Idris alifurahi sana alipotangazwa kuwa Balozi wa Uber nchini Tanzania; “Nimefurahi sana na ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adimu ya kushirikiana na Uber,kwa sababu mimi nishabiki mkubwa wa mapinduzi yaliyoletwa katika sekta ya usafiri kupitia kwa mfumo wake kote duniani. Nimefurahi kuona jinsi Uber imepata umaarufu jijini Dar es Salaam, binafsi mara nyingi mimi hutumia usafiri wa uberX nikiwa na marafiki zangu kwenye mitoko yetu ya jioni na sasa wamaleta huduma nyingine ya bajaji; uberPOA ambayo nina hamu sana kuitumia - utaniona hivi karibuni. Uber inaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya madereva jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua usafiri wanaotaka. Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kampuni ambayo inajituma kuleta mabadiliko chanya katika maisha yetu.
Baadaye kwenye hafla hiyo, Idris alipanda jukwaani na kuwatumbuiza mashabiki, wanahabari,na wafanyakazi wa Uber kwa kionjo cha kazi yake ya uchekeshaji. Msanii huyo na mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother Africa alivunja mbavu za umati huo kwa vichekesho vyake.  
Tangazo hili linakuja siku chache tangu Uber ilipo tangaza kushirikiana na Tigo kwenye mpangoambao wateja wa Tigo wanapata bando za bure wanapotumia programu ya Uber. Ushirikianohuu wa kipekee nchini Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri na maderevawanaotumia Uber na umechochea wasafiri na madereva zaidi kujiandikisha kutumia programuya Uber nchini Tanzania.

MKOA WA DAR ES SALAAM KUTOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE WA MIAKA 14

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAFUNZO ya utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi (Human vaccine) yametolewa leo jijini Dar es salaam na kuwataka watu wa kada zote kuhimiza watoto kupata kinga hiyo ya saratani.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa chanjo hii itapunguza vifo vya wanawake wengi na ametoa rai kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na aturudie ili kukamilisha dozi kwa zoezi litakaloanza tarehe 23 mwezi huu.

Aidha amewataka wananchi kutumia fursa hii ya Serikali ya awamu ya tano kwa kujitokeza katika vituo 270 vilivyoorodheshwa na amewataka Wenyeviti wa Mitaa kuhamasisha akina Mama kupeleka watoto wao wakapate chanjo hii ili kuokoa maisha ya wanawake wengi pia ameeleza kuwa wana mpango wa kuendesha zoezi la kupima tezi dume nyumba kwa nyumba katika Mkoa wa Dar es salaam.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala bi. Sophia Mjema ameeleza kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na amewaomba akina baba kuwakumbusha akina Mama kuhusiana na chanjo hii.

Mratibu wa huduma za chanjo na uzazi Mkoa Bi. Ziada Sella ameeleza kuwa saratani ya shingo ya uzazi ni ya pili kwa madhara kwa mwanamke ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo huuwa wanawake wengi. Kuhusu dalili za awali la ugonjwa huo ameeleza kuwa kuvimba miguu, kutoka uchafu wa kahawia uliochanganyika na damu, maumivu ya miguu, mgongo na kiuno ni dalili za awali za saratani.

Kuhusiana na chanjo hii bi. Sella ameeleza kuwa watoto wa miaka 14 watapatiwa chanjo hii mara mbili kwa kurudia mara baada ya miezi 6 aidha watoto wenye maambukizi ya virusi ya Ukimwi (HIV) watapata chanjo tatu watakayorudia baada ya miezi 2 watakayochoma katika vituo vya afya na ya tatu watachoma na wenzao mashuleni baada ya miezi sita.

Aidha katika utoaji wa chanjo kuna vituo 270 ikiwa vituo 71 katika Manispaa ya Ilala, 48 Ubungo, 19 Kigamboni, 65 Kinondoni na 48 katika Manispaa ya Temeke.
Aidha amesisitiza wananchi kutokuwa na imani potofu kuhusu chanjo hizo kwani kinga ni bora kuliko tiba. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akizungumza leo katika uzinduziwa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, kabla ya uzinguzi wa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Salatani ya mlango wa Kizazi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akifafanua kuhusu zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.

MKURUGRNZI WA FADHAGET AUNGA MKONO KWA VITENDO KAULI MBIU YA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
*Aishukuru Serikali,SIDO kwa kutambua mchango wa kiwanda
chake cha virutubisho tiba

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki kiwanda cha Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science, Dkt Fadhili Emily ameishukuru Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO) pamoja na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaona vijana wa Tanzania kuwa wanao uwezo wa kumiliki viwanda.

Amesema kuwa kauli ya Rais Magufuli imewafanya vijana wajikwamue na umasikini uliokithiri na sasa wigo wa ajira unaendelea kuongezeka kutikana na viwanda vinavyoanzishwa kutokana na dhamira njema ya Serikali inavyohimiza ujenzi wa viwanda.

Amesema hayo wakati anazungumzia na Michuz Blog baada ya SIDO kumtunuku cheti cha kutambua kiwanda chake na mchango ambao anautoa katika kuelekea nchi ya viwanda ambapo cheti hicho amekabidhiwa jana."Sisi kama kiwanda cha kwanza Tanzania cha kuandaa virutubisho tiba vyenye uwezo wa kupambana na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa mwanadamu tunaahidi kuzalisha mara dufu ili kuhakikisha watu wanapatapa kilicho bora zaidi kutoka Fadhaget Nutrition Science,"amefafanua.

Akifafanua zaidi kuhusu Fadhaget Nutrion Science,Fadhili  amesema wamekuwa wakiandaa virutubisho tiba kwa njia za kisasa kabisa kwa kuzingatia kanuni za usalama wa vyakula na virutubisho duniani yaani HACCP(Hazard Analysis and Critical Control Point).Amesema furaha yao ni kuhakikisha watu wanatapa tiba salama isiyo na madhara ya baadae na wamefanikiwa baada ya kuandaa virutubisho kwa magonjwa karibia yote hasa yale ya virusi vya magonjwa ya muda mrefu.

Ametaja baadhi ya magonjwa hayo ni Ukimwi, vidonda vya tumbo, U.T.I sugu, malaria sugu ,upungufu wa nguvu za kiume, figo , ini, kifua kikuu , pumu (arthima), kisukari, matatizo ya uzazi pande zote yaani kutopatikana mtoto katika ndoa , uvimbe wa kizazi na kuziba kwa mirija ya kizazi ."Pia magonjwa ya zinaa na dalili nyngine nyingi za hatali kiafya kama vile miguu kufa ganzi , miguu kuwaka moto, miguu kuvimba na unapoibonyeza lina baki shimo kama unavyobonyeza ndizi mbivu.

"Kuwashwa ukeni kwa akina mama na kutokwa na uchafu mzito mweupe katika via vya uzazi au wa kahawia wenye harufu na unapopata mkojo unakuwa wa njano sana ikiwa ni pamoja na matatizo ya kukosekana kwa hamu ya tendo la ndoa,"amesema.Kuhusu cheti ambacho amepewa na SIDO cha kutambua kiwanda chake amesema kama kijana wa Kitanzania atahakikisha cheti hichi kinakumbusha kuwa analo jukumu la kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda na kwake na kuongeza itakuwa chache kwake kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa maslahi ya Watanzania wote.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki Kiwanda cha
Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science (kushoto),Fadhili Emily  akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO).Cheti hicho ni kwa ajili ya kutambuliwa kwa kiwanda chake ambacho amekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
 
Cheti ambacho amekabidhiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki Kiwanda cha Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science kutoka Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO).




SERIKALI INAFANYA TATHIMIN YA FIDIA ARIDHI NA MAENDELEZO YAKE MPAKA WA TANZANIA, KENYA

$
0
0


Na Rehema Isango, Tarime, Mara

SERIKALI inafanya tathmini kuhusu fidia ya ardhi na maendelezo yake katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya iwapo kutakuwa na utwaaji ardhi wakati wa zoezi la kuimarisha mpaka linaloendelea mkoani Mara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Doroth Mwanyika alisema hayo wakati alipokagua kazi ya uimarishaji mpaka katika eneo la upande wa pwani ya Ziwa Victoria mkoani Mara katika kijiji cha Kirongwe kata ya Bukura Wilayani Rorya hadi eneo la Sirari mkoani Tarime.

Amefafanua Serikali inafanya tahmini hiyo kwa lengo la kuona wananchi waliopo katika eneo huru (buffer zone) iwapo watatakiwa kupisha eneo hilo, itumike njia bora ya kujadiliana nao au namna mbadala ya kuwasaidia wananchi hao.

“Kwanza wananchi walioendeleza maeneo ya mipakani walipewa elimu wakati wa mchakati wa uhamasishaji lililofanywa na wataalam wetu kabla ya kuanza kwa kazi ya uimarishaji mpaka." Wengine wameelewa na kuchukua hatua ya kupisha wakati kazi ya uimarishaji mpaka inaendelea,” amesema Mwanyika.

Aidha Serikali imebainisha kuwa itahakikisha inatatua changamoto hizo zilizojitokeza katika zoezi hilo kwa njia ya amani na kwa kuzingatia haki. Mapema Machi mwaka huu, Serikali za pande zote mbili Tanzania na Kenya zilikubaliana kuanza kazi ya uimarishaji wa mpaka wa Kimataifa katika urefu wa kilomita 238 za nchi kavu kutoka ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natroni mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika ( wa tatu kutoka kushoto  aliyeinama) akigusa moja ya alama mpya zinazoongezwa kila baada ya urefu wa mita mia moja kwenye mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya. Bibi Mwanyika na Makatibu Wakuu wengine wanne walikagua mpaka huo wakati wa kazi ya uimarishaji iliyoanza Machi mwaka huu. Picha zote na Rehema Isango WANMM

MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020 NCHINI JAPAN KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA - DK. KIGWANGALLA

$
0
0



Na Hamza Temba-Ngorongoro, Arusha

Mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 yatatumika kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia timu ya Taifa ya riadha na banda la maonesho ya utalii.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilika kwa mashindano ya riadha ya Ngorongoro Marathon 2018 katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana.

Dkt. Kigwangalla alitoa kauli hiyo wakati akijibu ombi la Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye aliiomba wizara yake kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kusaidia maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo.

Mtaka pia aliomba Mamlaka hiyo itumie timu ya Taifa ya riadha Tanzania kama mabalozi wao wa kutangaza vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo ya Ngorongoro ndani na nje ya nchi.

Akijibu maombi hayo, Dk. Kigwangalla alisema kitaundwa kikosi kazi cha pamoja kati ya wizara yake kupitia taasisi zake hususan Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Chama cha Riadha Tanzania ili kuainisha mahitaji ya mashindano hayo na kuweka makubaliano yatakayonufaisha pande zote.

"Kama tunaweza kupata jukwaa la nchi zaidi ya 50 au 100 kwa kufadhili wanariadha 200 kwenda kushiriki, manake hilo jukwaa linatulipa, kwa sababu tunawekeza kidogo tunaonekana kwa kiasi kikubwa.

"Mwaka 2020 kwenye Olimpiki lazima tuwekeze, na sisi Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zetu tutapenda tuunde kikosi kazi cha pamoja ili tuangalie gharama zinazohusika, maandalizi yanayohitajika ili na sisi kama Wizara kupitia taasisi zetu kama Ngorongoro tuweze kuona nini mchango wetu, lakini sisi tutataka tujue faida yetu hasa itakuwa ni nini" alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema mashindano hayo yatatoa fursa pana kwa Taifa kutangaza vivutio vyake mbali na juhudi zinazofanywa hivi sasa kupitia maonesho ya kimataifa. "Kupitia mashindano hayo tutapeleka pia maombi kwenye ofisi ya balozi wetu nchini Japan ili tupewe banda la kunadi vivutio vyetu vya utalii" alisema.

Dk. Kigwangalla pia aliitaka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kukubali ombi la Chama cha Riadha Tanzania la kuanzisha kituo cha mafunzo ya riadha mjini Karatu ili kuimarisha mchezo huo na timu ya riadha Tanzania sambamba na kutumia kituo hicho kama fursa ya kutangaza utalii wa hifadhi hiyo.

Alisema kituo hicho pia kijengwe sanamu za wanariadha mashuhuri waliowahi kuiletea sifa Tanzania na kuweka rekodi mbalimbali ili kutoa motisha kwa wanariadha wengine wanaochipukia.

Alisema mbali na kuanzisha kituo hicho, timu hiyo ya Riadha Tanzania inaweza pia kupewa jina la Ngorongoro ili kuitangaza hifadhi hiyo yenye vivutio vya kipekee duniani ambavyo vimeifanya itambulike kama sehemu ya urithi wa dunia.

Mashindano ya Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu 2018 yamehusisha washikiri kutoka Tanzania na Kenya ambapo washindi wa kwanza wa mbio hizo za kilomita 21 upande wanaume na wanawake wametoka nchini Kenya. Kaulimbiu ya mashindano hayo imelenga kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimsalimia Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri Kigwangalla akiwa tayari kuzindua mashindano hayo katika umbali wa kilomita 21.
Washiriki wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya wakitimua mbio kuanza mashindano hayo ya Ngorongoro Marathon 2018 umbali wa Kilomita 21 mjini Karatu mkoani Arusha. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya watalii nao walitumia fursa hiyo kusaka medali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika harakati za kusaka medali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihitimisha mbio za kilomita 21 za mashindano ya Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Haikuwa kazi rahisi, washiriki wengine walilazimika kuvua viatu na kuvaa kandambili ili kurahisiha kazi yao ya kutafuta medali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akionesha medali aliyopewa pamoja na washiriki wengine wa mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani. 
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini Tanzania, Filbert Bayi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akitoa salamu zake katika hagla hiyo ambapo ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kufadhili mashindano hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Karatu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha mashindano hayo mjini Karatu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi cheti cha shukurani Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi kwa kufanikisha mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja mshindi wa kwanza wa kilomita 21  kwa wanawake, Monica Chemko kutoka Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja mshindi wa kwanza wa kilomita 21  kwa wananume, Joseph Patha kutoka Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wengine wa mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 yaliyifanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. 

MSANIFU MKONGWE AACHA URITHI WA MAARIFA CHUO KIKUU ARDHI DAR ES SALAAM

$
0
0


Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Livin Mosha akipokea sehemu ya vitabu vya usanifu majengo na ujenzi kutoka kwa Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida (wa pili kushoto) alivyokuwa akitumia enzi za kufanya kazi. Hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Aprili mwishoni mwa wiki 2018. Pamoja nao (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo wa ARU, Dkt. Ombeni Swai na Mkuu wa Idara ya Mazingira ya Ndani ya Nyumba wa ARU, Dkt. Shubira Kalugila. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida akimshirikisha jambo Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa ARU)Profesa Livin Mosha wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitabu hivyo.
Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU)Profesa Livin Mosha na Dkt. Kalugila wakiondoka na vitabu hivyo kwa ajili ya matumizi ya Chuo Kikuu Ardhi.
Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Livin Mosha akimshukuru Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida baada wakati wa hafla ya kupokea sehemu ya vitabu vya usanifu majengo na ujenzi alivyokuwa akitumia enzi za kufanya kazi. Hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Aprili 20 2018.  

MBUNGE MAULID MTULIA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO KATA ZA MSISIRI A, B, NA KAMBANGWA KINONDONI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo am bayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa 
ms1
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa , mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena akielezea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akifanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa

ms5
Muonekano wa maji yaliyozingira nyumba za wakazi wa Kata za Msisiri A na B na Kambangwa katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam.
ms6
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akipita kwa tabu wakati alipofanya ziara ya kukagua mae neo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms8
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akiangalia moja ya madimbwi yaliyojaa maji mtaani alipo fanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms9ms10
Mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia akimsikiliza Diwani Songoro Mnyonge wakati akitoa maelezo kwake kuhusu mafuriko ambayo yamewakumba wananchi wa maeneo hayo.
ms4
Mratibu wa Kanda ya Mashariki Japhary Chemgege akitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Abdallah Mtulia wakati wa ziara ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
......................................................................................

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Maulid Mtulia(CCM), ametembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko ya maji huku akitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi wa jimbo hilo ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua za masika huku akiishauri Halmashauri Manispaa ya Kinondoni kutafuta suluhu ya kudumu ili wananchi wabaki salama.

Pia amesema mbali ya kutoa pole atatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kunyonya maji pamoja na fedha ya kununua mafuta ili maji ambayo bado yapo kwenye makazi ya wananchi wake yaondolewe huku akitoa katazo la watu wasiendelee kujenga kwenye bwawa la Tengeza wala kutupa taka kwani athari zake ni kubwa kwa wananchi walio wengi.

Mbunge Mtulia amesema hayo jana jimboni kwake Kinondoni baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa ambapo pia ameshuhudia baadhi ya watu kujenga makazi kwenye bwawa la Tengeneza na matokeo yake maji kukosa pakwenda na hivyo kuharibu makazi ya watu.

Pia ametembelea baadhi ya nyumba za wananchi wa maeneo hayo ambapo zaidi ya asilimia 70 ya makazi ya watu yamekumbwa na mafuriko ambapo akatumia nafasi hiyo kuiomba Halmashauri ya Kinondoni kurekebisha mitaro iliyopo ili maji yapite kwa urahisi huku akitoa ombi la kuchimbwa kwa mitaro mikubwa ambayo itakuwa suluhu ya maji kutokwenda kwenye makazi ya watu kama ilivyo sasa.

Akizungumza zaidi kuhusu mafuriko hayo na athari ambazo wananchi wamezipata Mtulia amesema kwanza anatoa pole kwa wananchi hao lakini kikubwa ambacho anamini kitaisaidia wananchi hao kubaki salama ni kuangalia namna ambayo itasaidia maji hayo kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
“Nimefanya ziara ya kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko, nimeambatana na watalaam mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kwa maana ya mjumuiko wao ni sawa nipo kwenye ziara hii na wizara tatu.Kwa kuwa wao ni watalaamu watakuwa na njia nzuri na sahihi ya kuhakikisha unatafutwa ufumbuzi wa maji hayo kuondolewa na wananchi waendelee na maisha yao.

“Pia niombe wale ambao wanajaza taka kwenye bwawa Tengeneza waache mara moja kwani madhara yake ni maji kukosa pakwenda.Pia wale ambao wanaendelea na ujenzi nao waache ili kazi ibaki namna ya kuwasaidia waliopo wawe salama.

“Na ndio dhamira ya ziara yangu ya kwanza kuangalia athari za mvua , kutoa pole na namna ya kushirikisha watalaamu kuangalia namna ya kufanya kwa ajili ya wananchi wetu,”amesisitiza Mtulia.

Akizungumzia hatua ambazo ameamua kuzichukua hivi sasa ili kuwaondolewa wananchi hao adha ya maji ambayo bado yapo kwenye makazi yao, Mtulia amefafanua atatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kuvuta maji na pia atatoa fedha kwa ajili ya kununuliwa mafuta ili mashine hizo zifanye kazi.

“Kama mbunge nimeguswa na athari ambazo wananchi wamezipata lakini nitatumia fedha za mfuko wa jimbo kuhakikisha maji haya yanaondolewa kwenye makazi ya watu.Kikubwa nimeona hali ilivyo na kilichobaki sisi wanasiasa tukae na watalaam wa manispaa tutafute ufumbuzi wa muda na wa kudumu,”ameongeza Mtulia.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena amesema changamoto kubwa ya kujaa maji kwenye makazi ya watu inatokana na baadhi ya wananchi kujenga kwenye bwawa la Tengeneza na kufafanua ipo haja ya mbunge kushiririkiana a halmashauri kuangalia namna ya kuzuia watu wasiendelee kujenga.

Wakati huohuo Diwani Songoro Mnyonge amemwambia Mbunge kuwa ili kutafuta suluhu ya kudumi katika maeneo hayo ni kupatikana kwa mitaro mirefu ya kupitisha maji na wao walishatoa mapendekezo ya kuchimbwa mitaro mitano, hivyo mbunge asaidie katika kufanikisha hilo kwani ndio suluhu ya kudumu kwa wananchi.

“Gharama za uchimbaji wa mifereji hiyo ni kama Sh.milioni 6.5 na ukweli ni kwamba athari za mafuriko hayo ambazo wananchi wamezipata ni zaidi ya fedha hizo.Hivyo tushauri na kutoa ombi kwa mbunge wetu kutusaidia katika hili a tunaimani naye sana kuwa atatusaidiana hatimaye mitaro kuchimbwa,”amesisitiza Mnyonge.

Kwa upande wa Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la Mazingira Japhary Chemgege amesema matatizo yanayotokea sasa ya maeneo hayo kujaa maji inatokana na baadhi ya wananchi kujenga makazi kwenye bwawa hilo ambalo kitaalam linafahamika kama tindiga.

Amefafanua maeneo ya matindiga kiasili ni maeneo ambayo yapo kwa ajili ya kuhafidhi maji na hiyo ni asili ya uumbaji wa dunia , hivyo wananchi wanapogeuza maeneo hayo kuwa makazi maana yake changamoto ya maji kujaa katika makazi ya wati itaendelea.

Amesema kisheria hairuhusiwi watu kujenga nyumba katika maeneo ya matindiga na kimsingi wanatakiwa kuondoka ili wengine wabaki salama.

KAIMU MURUGENZI MKUU NIDA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA MAENDELEO YA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WATU

$
0
0






Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Kushoto ni Ndg. Andrew W. Massawe Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Ndg Albert Msovela na kushoto ni Ndg. Alphonce Malibiche Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho; na wa mwisho ni Ndg. Rose Joseph Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano.


Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Usajili vitambulisho vya Taifa kwa wananchi mkoani humo.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Usajili vitambulisho vya Taifa kwa wananchi mkoani humo.
Viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kikao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwasajili wananchi na kumaliza zoezi kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. ,Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, mara alipowasili kwenye ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Pembeni ni Katibu Tawala huo Ndg Albert Msovela
Wananchi wa Kijiji cha Usanda Kata ya Tinde mkoani Shinyanga walivyokutwa kwenye foleni ya Usajili Vitambulisho vya Taifa kwenye zoezi linaloendelea mkoani humo wakati wa ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliyoifanya hivi karibuni.
Bi. Magdalena E. Ngosha mkazi wa kijiji cha Usanda Kata ya Tinde akichukuliwa alama za vidole na Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea kijijini hapo.

…………………………………………………………………………..

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Ndg. Andrew W. Msssawe amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha Usajili wananchi mkoani humo mwezi Mei mwaka huu ili NIDA kupata muda wa kutosha kufanya uhakiki na mapingamizi kwa wale wote waliosajiliwa; na kuwezesha Mamlaka kuzalisha vitambulisho kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga kukagua maendeleo ya zoezi la Usajii na Utambuzi wa Watu linaloendelea; akiwa ameambatana na Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Ndg. Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami na Ndg. Steven Kapesa Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo; Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg. Albert Msovela amesema mkoa wa Shinyanga una changamoto kubwa ya wahamiaji haramu hususani Wilaya ya Kahama na kwamba wamejipanga Usajili katika eneo hilo kufanyika kwa uangalifu mkubwa kwa kuhusisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.

Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa Ndg.Bashiri Mang’enya amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa NIDA; Idara yake imejipanga vizuri kuhakikisha maafisa Uhamiaji wa kutosha wanakuwepo wakati wote wa zoezi na kwa kushirikiana na NIDA watu wote wenye sifa kuwa wanasajiliwa kwa kusimamia misingi na taratibu zote za Usajili kwa mujibu wa sheria.

Aidha; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg. Andrew W. Massawe ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa jitihada kubwa wanazozifanya kuhakikisha Usajili unafanyika pamoja na kuwepo changamoto nyingi; na kuahidi kuongeza vifaa kwa maana ya mashine za Usajili na watendaji ili kuongeza kasi ya Usajili.

Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa iliyoanza usajili mwezi Septemba mwaka jana; na hadi sasa Wilaya ambazo ziko kwenye hatua ya kukamilisha Usajili ni Shinyanga na Kishapu huku Wilaya ya Kahama ikitegemea kuongezewa nguvu kubwa ili zoezi hilo kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

Vijana Waaswa Kulinda na Kudumisha Muungano

$
0
0

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Vijana Nchini wametakiwa kulinda na kudumisha Muungano kwa Vitendo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho ikiwa ni sehemu ya kuonesha uzalendo.

Akizungumza wakati wa Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na kuudumisha.

“Vijana tunawategemea muwe watetezi na walinzi wa Muungano wetu kwa kuwa huu ni urithi wa Taifa tunawajibika kuulinda na kuudumisha kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Makamba. Akifafanua Makamba amesema kuwa vijna wanaowajibu wakuonesha uzalendo wao kwa kudumisha Muungano ambao unalitambulisha taifa nje ya mipaka yetu.

Mambo mengine yanayolitambulisha Taifa letu ni Lugha, Mipaka yetu, Historia, Utamaduni wa kisiasa na kijamii.“ Waasisi wa Taifa letu walikuwa na dhamira njema ndio maana waliasisi Muungano wetu na kuweka mipaka mipya ya Taifa letu tofauti na ile ya wakoloni hivyo hili ni jambo la kujivunia” Alisisitiza Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaobeza Muungano kwa kuwa hawalitakii mema taifa letu.Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe na Waziri (mstaafu) wa baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Kwanza mara baada ya Uhuru Balozi Job Lusinde akizungumza katika mahojiano maalum mjini Dodoma amewaasa vijana kudumisha Muungano kwa kujifunza historia ya Muungano ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuuenzi.

“Vijana wajitahidi wawe waadilifu kwa kulinda uhuru wetu, umoja wetu na muungano wetu kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Balozi Lusinde.

Akifafanua Balozi Lusinde amesema vijana wanapaswa kuepuka vitendo vya wizi na ufisadi ili kuchochea maendeleo.Mada zilizotolewa katika Kongamano hilo ni pamoja na Historia na faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kongamano kuhusu Muungano limefanyika Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya siku ya Muungano yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2018 mjini Dodoma, Kongamano hilo limewahusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Mipango, CBE, St. John, Chuo cha Madini na Chuo cha Maendeleo Vijijini Hombolo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba

SPORTPESA YATIMIZA NDOTO ZA WATANZANIA 20 KUPITIA PROMOSHENI YA KUSHINDA BAJAJI

$
0
0


Promosheni ya Jiongeze na M-Pesa, Shindana SportPesa imefikia tamati siku ya Alhamisi ya April 19 na kushuhudia watanzania 20 kutoka mikoa mbalimbali wakijishindia bajaji aina ya TVS KING.
Promosheni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa wakishirikiana na Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa ilizinduliwa rasmi siku ya Februari 9 mwaka huu kwenye viwanja vya Zakiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Katika promosheni hiyo iliyodumu kwa wiki kumi, washindi wawili walikuwa wakijinyakulia bajaji mpya kila wiki katika droo zilizokuwa zikichezeshwa siku za Jumatatu na Alhamisi zikisimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.
Kwa mara nyingine tena tumeshuhudia SportPesa wakiendelea kuwainua watanzania kiuchumi huku promosheni hii ikiwa ni muendelezo wa ile promosheni ya kwanza iliyodumu kwa siku mia moja ambayo ilikwenda kwa jina la ShindanaSportPesa.

WashindiJumla ya washindi 20 wamepatikana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo Bwana DaudiSima (36) kutoka Makete Njombe ndiye alifungua dimba kwenye drooya kwanza iliyofanyika Februari 12 na baada ya hapo washindi wengine walifuata ambao ni Edwin Victor (23), AggreyLauwo (19), Godfrey Magesa (37), Enock Sagwa (32), Yohana William (28), Richard Steven (23), ErastoFloridi (22), Joseph Nzary (32) na Gerald Christopher (25).

Wengineni Paschal Raphael (24), Mathayo Edward (27), Majaliwa Hassan (29), Yohana Msigala (22), JumaTwike (35), John Mawela (32). Karim Prosper (29), Adam Obura (34), Linda Mwandu (32) na AwadhHussein (28) ambaye ndiye amefunga dimba.

Mwanza yaburuza
Mkoa wa Mwanza umeongoza kwa kutoa washindi wengi (4) ukifuatiwa kwa ukaribu na mkoa wa Mara wenye jumla ya washindi watatu, kisha mikoa ya Dar es Salaam, Rukwa, Kagerana Iringa yenye washindi wawili kila mmoja na bila kusahau Mbeya, Ruvuma, Njombe, Shinyangana Kilimanjaro yenye mshindi mmoja mmoja.

NdotokuwakweliWakati wa kukabidhi bajaji ambazo zilikuwa zikipelekwa na SportPesa hadi nyumbani kwa washindi, washindi wote walieleza jinsi ambavyo bajaji hizo zitaweza kuwakwamua kiuchumi.Yohana William (28)kutoka Mwanza nimuuza kuku katika soko la Igoma nayeye kwa upande wake anaamini ataweza kutimiza ndoto zake kupitia ushindi huo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images