Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Hasunga atembelea pori la akiba Mkungunero

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akitoa maelekezo kwa Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la la akiba la Mkungunero alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Maafisa hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo ya namna bora ya usimamizi wa hifadhi za wanyamapori alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa kikao na Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa. Wakwanza kulia kwake ni Meneja wa pori la akiba la Mkungunero Bw. Emmanuel M. Birasso na Meneja wa pori la akiba la Swaga Swaga Bw. Alfred Choya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata wakati wa kikao na Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akitizama sehemu ya ng’ombe waliokamatwa na Maafisa wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero kwa kuingia katika hifadhi hiyo wakati alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori la Mkungunero jana Wilayani Kondoa, ambapo zaidi ya ng’ombe 250 wanashikiliwa. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi – Usimamiziwa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata na kulia kwake ni Kaimu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kondoa Bw. Juma Solomon Nyamwakirya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Bumbuta Bw. Bashiru Mtoro (kulia) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kulia) akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa Bi. Hija Suru (kushoto) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa pori la akiba la Mkungunero Bw. Emmanuel M. Birasso (kushoto) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akimsikiliza Bw. Yohana Bilo ambaye ng’ombe wake wanashikiliwa na Maafisa Hifadhi wa pori la Mkungunero kwa kuingia katika pori hilo alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafugaji wa vijiji vinavyozunguka pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.

PICHA ZOTE NA: OCTAVIAN KIMARIO- MAELEZO.

VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI

0
0
 Daraja la Kivule likiendelea kujengwa katika Mto Kizinga eneo la Sirali,Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipita kwenye daraja la muda baada lile la awali kubomolewa kupisha ujenzi wa daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi ujao. 

Na Richard Mwaikenda, Kivule, Dar

Viongozi wa Kata ya Kivule, Ukonga Dar, wameunganisha nguvu kuwasaka vipaka wanaowapora watu wanaopita wakati wa usiku katika Daraja linalojengwa katika MTO Kizinga.

Uamuzi huo umefanywa baada hivi karibuni Majira ya SAA 5 usiku ambapo mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika Daraja la muda kuporwa na vibaka Simu na vitu vingine.

Tukio hili aliliripoti kituo kidogo cha POLISI cha Kitunda, na kwa viongozi wa Kata ya Kivule, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule, Amos Angaya na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim.

Mwandishi wa Habari hii alishuhudia viongozi hao wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, Kijana Jaffari aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji huo akishirikiana na wenzie.

Viongozi hao walimnasa 'Kibaka' huyo kwa ushirikiano Mkubwa na waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogondogo wanaoendesha shughuli zao darajani hapo.

Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.

Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.

Kwa umoja wao, viongozi hao waliapa kutokomeza vitendo vya uovu vilivyoanza kuota mizizi katika eneo hilo la Daraja ambalo limekata mawasiliano ya usafiri Kati ya Kivule Mwembeni na Silari baada Daraja bovu kuvunjwa na kuanza kujenga jipya.

Kwa.mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim, Ujenzi wa Daraja hilo unatarajiwa kukamilika Mei, Mwaka huu.

Hivi sasa daladala kutoka Banana zinaishia upande wa Mwembeni na zinazotoka Frem kumi zinaishia Silari. Magari mengine yanapitia Daraja la Bombambili.

VERTIV YAJA NA VIFAA VYA KISASA VYA KUKABILIANA NA MAJANGA YA UMEME

0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Vertiv imefanya maboresho ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vinavyotumika katika ujenzi, viwandani na maofisini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao wamiliki wa viwanda na kampuni mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza jana Dar es Salaam, katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk alisema kuwa wamefanya maboresho ya bidhaa zao ili kusaidia wateja wao kujua endapo vifaa vyao vimepata hitilafu au la.

Amesema bidhaa wanazozizalisha ni pamoja na vifaa vya kudhibiti nguvu ya umeme, Ac zinazotumika kwenye viwanda, UPS na ambazo zimewekewa uwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji kama kifaa anachotumia kimeshindwa kufanya kazi kwa sababu gani.

‘’Tumefanya maboresho kwa bidhaa zetu ambapo wenye vituo vya data kama vile kampuni za simu, ofisi za serikali na kampuni binafsi watapata taarifa kuonesha kuwa kama UPS au AC za viwandani hazifanyi kazi kwa sababu ya umeme mdogo au kuna tatizo lingine ambalo linapaswa kufanyiwa marekebisho,’’ amefafanua Wyk.

Amesisitiza kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hizo ambazo zinatumika katika nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki (EAC) na Ulaya kwa kuwa wanaamini ukuaji wa teknolojia unasaidia katika kuleta maendeleo chanya kwa kila nchi.

Naye mshirika wa kibiashara na Mtaalamu wa masula ya mawasiliano, Mihayo Wilmore amesema kuwa uboreshaji wa vifaa hivyo utasaidia maeneo mengi ikiwemo hospitalini na maofisini ambako matumizi makubwa ya teknolojia hufanyika.

Amesema kuwa watu wanaotumia mitambo mbalimbali katika shughuli zao, ni muhimu kujua ni muda gani vifaa vyao vimeweza kuzimika kwa sababu ya kuisha kwa umeme, hutupata ujumbe mfupi wa maandishi kuelezea tatizo lililotokea.

‘’Ni muhimu kwa hospitali kujua UPS wanayotumia inaweza kuzimika kwa muda gani na sababu gani zinazosababisha jenereta kuzimika hii itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma haraka. Pia wameonesha uwezo wa kutengeneza vituo vya data katika simu au kompyuta ili kutoa taarifa kwa haraka kwa wateja wao,’’ ameeleza Wilmore.
Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake katika soko la Tanzania Chini ya usambazaji wa kampuni ya Elcom Solution 
Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, Johan Terblanche akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake juu ya umuhimu wa UPS kutoka Vertiv katika Data Centre. 
Mkurugenzi wa huduma wa Vertiv Mashariki ya Kati , Pascal Bodin akieleza namna kampuni hiyo ilivyoweza kunufaisha Viwanda vya ukanda huo.
Mshirika wa kibiashara wa Elcom Solution ambao wamewakaribisha Vertiv nchini, Mihayo Wilmore akieleza Waandishi wa Habari umuhimu wa mitambo ya Vertiv katika sekta ya Afya nchini.
Wakurugenzi wa EL- COM Solutions , Deen Nathwani, Jimy Apson na Amin Valji wakizungumza jambo wakati wa Warsha wa kutambuslisha bidhaa za Vertiv nchini.
Wafanyakazi wa Vertiv wakiwa katika picha ya pamoja na Washirika wao El-com Solution na washirika wengine kutoka nchini Kenya mara baada ya kumaliza warsha ya kutambulisha bidhaa zao Tanzania

MEI MOSI KITAIFA IRINGA ,RAIS JPM KWA MARA YA KWANZA KUTUA IRINGA

0
0

Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoa wa Iringa kuelezea maandalizi ya Mei Mosi kitaifa yatakayofanyika mkoani Iringa
Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya (kushoto ) akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Tukusuga Mwaisumbe na Ester Malibiche pamoja na waandishi wengine walioshiriki kikao cha maandalizi ya Mei Mosi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kulia akiwapongeza viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi
Wajumbe wa TUCTA wakiimba wimbo wa wafanyakazi leo
Wimbo wa kuwaunganisha wafanyakazi

Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya kulia akiwa na wajumbe wenzake .



.................................................................

Na MatukiodaimaBlog.

SHIRIKISHO la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao ni waandaaji wa sherehe za wafanyakazi kitaifa (MEI MOSI) wamempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kukubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa .

Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya alisema leo kuwa katika sherehe hizo za wafanyakazi duniani kwa Tanzania zitafanyika katika mkoa wa Iringa kwenye uwanja wa Samora na kuwa tayari Rais Dkt Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi .

Hivyo aliwataka wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe hizo na kuwa kupitia sherehe hizo watapata fursa ya kujua mikakati ya serikali dhidi ya wafanyakazi nchini japo hadi sasa wanapongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya kuwarejesha kazini wafanyakazi waliokuwa wamesimamishwa kazi kutokana na elimu yao ya darasa la saba.

Rais huyo alisema kuwa TUCTA imefanya jitihada kubwa za kukutana na serikali kuwapigania wafanyakazi hao walioondolewa kazini kutokana na elimu yao na serikali imesikiliza na imewarejesha kazini .

Alisema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa kuongeza ajira pamoja na kusikiliza kero mbali mbali za wafanyakazi na kuzipatia majibu .

Akielezea juu ya maandalizi ya sherehe za mei mosi mkoani Iringa alisema kwa sehemu kubwa maandalizi yanakwenda vizuri na wamepata ratibu ya kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Iringa kutoa elimu pamoja na kututana na wafanyakazi ili kujua changamoto zao.

" TUCTA inapenda kuishukuru serikali ya mkoa wa Iringa kwa kukubali kupokea maadhimisho haya ya Mei mosi 2018 TUCTA kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Amina Masenza pamoja na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge ,kazi ,vijana , ajira na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama tumefanya maandalizi ya kutosha"

Alisema kabla ya Mei mosi mambo yakayofanyika Iringa ni pamoja na makongamano mawili ya kimkoa na moja la kitaifa na kuwakongamano la kwanza litafanyika April 23 katika wilaya ya Mufindi ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam wakati kongamano la pili litafanyika wilaya ya Kilolo April 25 na mgeni rasmi ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah huku April 27 litafanyika kongamano la kitaifa litakalohusu Tanzania ya uchumi wa viwanda kwenye ukumbi wa Kichangani ambalo viongozi mbali mbali wa kitaifa watashiriki .

Aidha alisema kutakuwa na michezo ya Mei mosi ya fani mbali mbali itakayoanza April 16 hadi April 30 katika uwanja wa Samora kuwa kwa ajili ya kuwafanya wafanyabiashara na wajasilia mali kutumia fursa ya mei mosi Iringa maonyesho ya bidhaa mbali mbali yatafanyika .

WAZIRI MWAKYEMBE: TATUENI KERO ZA WADAU KWA HARAKA NA UFANISI

0
0
 Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Makoye Alex Nkenyenge akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (Hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kikao cha13 cha  Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika leo Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi za Waziri Mkuu
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa kufarijiana Bw. Mussa Varisanga akiwasilisha taarifa kuhusu mfuko huo wakati wa kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,kilichofanyika leo Mkoani Dodoma.
 Afisa Ushirika kutoka Manispaa ya Dodoma Bw.Greyson Masawe akiwasilisha mada kuhusu uanzishaji wa Chama cha Kuweka na Kukopa Akiba (SACCOSS) katika  kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kilichofanyika leo Mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali wkatika kikao cha 13 cha Baraza hilo.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali katika kikao cha 13 cha Baraza hilo.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo baada ya kufungua rasmi kikao cha 13 cha  Baraza la Wafanyakazi lkilichofanyika leo Mkoani Dodoma, (Picha na Lorietha Laurence, Dodoma).
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha  Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu leo Mkoani Dodoma.
 

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dodoma.


Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kuwahudumia wananchi kwa kujibu hoja na kutatua kero zao kwa haraka na ufanisi.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma na Waziri Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akifungua kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo, ambacho hufanyika mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za watumishi.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa kazi zetu” amesema Dkt. Mwakyembe. Aidha Dkt. Mwakyembe ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao ili kuimarisha utendaji wa kazi.

“Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha taratibu za kiutendaji zinafuatwa na kuzingatiwa” amesema Dkt. Mwakyembe. Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia kikao hicho ambacho kipo kwa mujibu wa sheria, na kuwasisitiza watumishi kuyafanyia kazi yale yote waliyoelezwa.

“Nawaomba watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira” amesema Bibi.Susan.

Naye Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw.Makoye Alex Nkenyenge alimshukuru mgeni rasmi kwa niaba ya wajumbe wote na kuhaidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

0
0
KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imepanga kutumia vyema mageuzi yanayoendelea katika sekta ya anga nchini kwa kuboresha zaidi huduma zake ili ziandane na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza, kwasasa kampuni hiyo inaandaa mikakati itayoiwezesha kujitanua ili kunufaika zaidi na ongezeko la idadi ya ndege za kitaifa na kimataifa linalotarajiwa kufuatia mageuzi hayo.

“Tunachokifanya Puma Energy ni kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya anga’’ alisema Tungaraza katika mahojiano yake na waandishi wa habari hivi karibuni katika Mkutano wa wadau wa sekta ya anga barani Afrika ulioandaliwa na Umoja Wa Mashirika ya Ndege barani Afrika (AFRAA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege nchini (ATCl) uliofanyika visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Alitolea mfano wa maboresho yaliyofanywa na kampuni hiyo katika mfumo wake wa huduma ya mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuwezesha kampuni hiyo kukidhi mahitaji ya usambazaji wa nishati hiyo ambayo yanayotarajiwa kuongezeka mara tu baada ya kukamilika kwa upanuzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three).

Alisema lengo la kampuni hiyo katika sekta ya anga ni kutoa huduma ya mafuta kwa bei ya ushindani kwa wateja wake huku pia ikizingatia kutoa huduma hizo kwa kukidhi mahitaji ya viwango usalama na ubora wa kimataifa.

"Linapokuja suala la usambazi wa mafuta ya ndege huwa tunajitahidi sana kuhakikisha tunawapa urahisi zaidi wateja wetu kwa kuhakikisha tunaratibu kila kitu sisi kuanzia uagizaji, utunzaji, uhifadhi na usafiri hadi kwenye vituo vyetu vilivyopo kwenye viwanja vya ndege kwa kutumia rasilimali watu wenye weledi zaidi katika suala hilo,’’ .

“Ni wazi tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’ alitaja.

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA YA USAFIRI YA WATU 7 JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


Kampuni ya Taxify inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika katika utoaji wa huduma zake za usafiri kwa njia ya mtandao, imetambulisha huduma nyingine mpya inayopatikana kwenye 'App' yake itakayofahamika kama 'Taxify XL'.


Kipengele hicho kipya kwenye app ya Taxify kimelenga kurahisisha usafiri katika maeneo mengi zaidi jijini Dar es Salaam.

Taxify XL (kubwa zaidi) ni kipengele ambacho kinawahusu wasafiri wanaokuwa kwenye kundi la takribani watu saba (7). Dhumuni la Taxify kuleta aina ya magari yanayochukua watu wengi, imetokana na matakwa ya wateja ambao wengi wa huduma ya usafiri wa magari makubwa.

"Kipengele cha XL ni mojawapo ya huduma mahususi kwa wale wanaosafiri katika makundi makubwa. Tayari tunatoa huduma kuanzia kundi la watu wanne kwa huduma ya Taxi za kawaida, Watu watatu katika kipengele cha bajaji. Na sasa huduma hii mpya ya XL itawapa watu fursa ya kusafiri hadi watu 7, " alisema Shivachi Muleji, ambaye ni Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini, Remmy Eseka alisema Taxify ni kampuni ya kwanza ya masuala ya usafiri ambayo inatoa huduma hiyo hapa jijini Dar es salaam.Aliongeza kuwa ni huduma kwa kila mtu lakini hasa inakusudia kundi fulani la watu wanaosafiri kuelekea sehemu fulani kwa pamoja.

"Magari kama Toyota Alphard, Toyota Noah, Toyota Wish, Probox ni miongoni mwa magari ambayo wateja wetu watarajie kuyatumia kwenye huduma hii ya Taxify XL," alisema Eseka.Eseka pia aliongeza kwamba madereva ya magari ya jumuiya ya XL, watatakiwa kupitia mafunzo kama ilivyo kwa madereva wanaotoa huduma zingine za Taxify.

Pia wanatakiwa kuwa na kadi za usajili wa magari, stika halali za bima pamoja na leseni za udereva.Katika uzinduzi wa huduma ya Taxify XL kampuni hiyo imetoa punguzo la asilimia 20 kwenye usafiri huo. Gharama ya kuanza safari ikiwa ni Sh1,000, Sh 140 kwa dakika, Sh500 kwa kilometa, na Sh3,000 kama nauli ya kiwango cha chini. Taxify itawapa madereva malipo ya ziada kwa kila huduma kufidia punguzo hilo.

Taxify inachukua kamisheni ya asilimia 15 pekee kutoka kwa madereva wake, ambayo ni karibu nusu ya kiwango kinachochukuliwa na kampuni zingine zinazotoa huduma kama hiyo.Hii inaiwezesha Taxify kutoa bei nafuu kwa wateja wake, huku ikitoa malipo mazuri kwa madereva hao.

Kwa jiji la Dar es Salaam, Taxify sasa inatoa huduma kwenye makundi matatu ambayo ni pamoja na Taxi:- (Gari za abiria wanne), Bajaji (iliyozinduliwa hivi karibuni) na sasa XL, ikiwa ni sehemu ya kampuni kuendeleza ubunifu na kuwa mbele katika ushindani.

TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

0
0
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita James Jilala (kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Geita. Katikati ni Afisa wa Kodi Mwandamizi wa TRA Makao Makuu Maternus Mallya.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwasajili wafanyabiashara wapya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lameck Ndida akitoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kwa wafanyabiashara wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.


Na Veronica Kazimoto, Geita,

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesajili jumla ya wafanyabiashara wapya 600 katika kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyofanyika mkoani Geita ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Menenja wa TRA mkoani hapa James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa kufika mkoani Geita hususani katika maeneo ambayo hakuna ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi ndani ya wiki moja.

“Nianze kwa kuishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa hatua ambayo mmeifanya ya kufika katika Mkoa wetu wa Geita hasa maeneo ambayo hatuna ofisi ya TRA na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi kwa muda mfupi kitu ambacho kimekuwa historia kwetu,” alisema Jilala.

Jilala alisema kuwa, baadhi ya wafanyabiashara walishindwa kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa wakati, kwasababu walitakiwa kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda Geita mjini kwa ajili ya kupata huduma hiyo. Hivyo, zoezi hili limewarahisishia wafayabiashara kusajiliwa na kupatiwa TIN.

Naye Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi alisema kuwa , pamoja na usajili wa wafanyabiashara hao, shughuli mbalimbali zimefanyika katika kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kupitia semina na kuwatembelea katika sehemu zao za biashara.

“Katika zoezi hili tumefanya shughuli nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wafanyabiashara mahali wanapofanyia biashara zao, tumesajili wafanyabiashara wapya na tumetoa semina mbalimbali ambazo tunaamini kabisa zitakuwa zimebadilisha mtizamo, utendaji na mwenendo mzima wa ulipaji kodi katika Mkoa huu wa Geita,” alieleza Mwangosi.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi ni moja ya mikakati ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania imejiwekea katika kuhakikisha kuwa inasajili wafanyabiashara 1,000,000 katika mwaka huu wa Fedha wa 2017/18.

TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO KUNUSURU KAYA MASKINI-PSSN.

0
0

Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge(aliyesisima) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo na Serikali ulioanza leo mjini Dar es salaam . 



Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Mohamed Muderis (aliyesimama) akitoa maelezo kwenye Mkutano wa Wadau wa Maendeleo,Serikali na TASAF unaojadili maendeleo ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


Baadhi ya Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa TASAFna Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa TASAFna Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
 
 
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF- na wadau wa Maendeleo wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia pamoja na mambo mengine utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ------PSSN- unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF. 

Pamoja na Mkutano huo ulioanza leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam , wadau hao wa Maendeleo,maafisa wa serikali na wenyeji TASAF watatembelea mkoa wa Kagera,Shinyanga,Manyara,Unguja,Pemba na Tanga ambako watakutana na viongozi wa serikali na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kujionea namna Mpango huo unavyoendelea kuchangia uboreshwaji wa Kaya za Walengwa. 

Utaratibu wa serikali kupitia TASAF kukutana na Wadau wa Maendeleo hufanyika kila baada ya miezi sita kwa lengo la kutathimini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza kutekelezwa mwaka 2012 Tanzania Bara, Unguja na Pemba. 

Hadi sasa takribani Kaya za Wanufaika Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa kwenye Mpango ambapo licha ya kupata ruzuku inayotolewa kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili, walengwa hao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli za kujiongezea kipato kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda, Mpango wa kuweka akiba na kukopeshana kupitia vikundi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi. 

Aidha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unatekelezwa kupitia Kaya Maskini ambazo zilibainishwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao kwa sasa unatekelezwa katika asilimia 70 ya vijiji nchini kote wakati jitihada za kutafuta fedha ili kukamilisha asilimia 30 ya vijiji viliyosalia zinaendelea. 

Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa kwenye mkutano huo zinaonyesha kuwapo kwa mafanikio makubwa kwa walengwa ambao wengi wao wameanza kujiwekea rasilimali ambapo mifano ya uboresha makazi,kupata uwezo wa kuhudumia kaya zao,elimu na afya zimebainishwa kupatikana kwa kaya za walengwa . 

Zifuatazo ni picha za wadau wa Maendeleo na maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wao ulioanza leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge(aliyesisima) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo na Serikali ulioanza leo mjini Dar es salaam .
 

MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI

0
0
*Ashauri wanafunzi wasiende shule kwa siku mbili, waliokuwa majumbani nao wakae huko huko

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MVUA zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam imesababisha vifo vya watu nane katika Jiji hilo huku miundimbinu ya barabara nayo ikiharibiwa.

Akizungumza kuhusu athari za mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema taarifa ambazo anazo ni kwamba kuna watu 8 wamekufa kutokana na mvua hizo.Amefafanua taarifa rasmi itatolewa kwani kinachoendelea sasa ameagiza kata zote kufanya tathimini ya athari za mvua hizo.

Ameongeza vifo hivyo vimetokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameeleza ipo haja ya wakazi wa Jiji hilo kuhakikisha wanakuwa makini katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

"Mvua hizi zimesababisha maafa ambako taarifa ambazo ninazo kuna watu 8 wamefariki dunia kwasababu ya hizi mvua.Tutatoa taarifa rasmi baadae.Pia mvua zimesababisha kuharibika kwa miundombinu na barabara nyingi kutopitika,"amesema Makonda wakati anazungumzia athari za mvua akiwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salam ambako eneo hilo maji yamejaa.

Pia Makonda amesema athari za mvua hizo zingeweza kuwa kubwa zaidi iwapo watu wangetoka majumbani kwao, na hivyo ameshauri ni vema Walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakatoa ruhusa kwa siku mbili ili wanafunzi wasiende shule ili kuepuka maafa kwani baadhi ya magari yamekuwa yakitumbukia mtoni.

"Nito rai kwa walimu wakuu na hasa kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa taarifa walimu wa shule zote kuwa kwa siku mbili hizi yaani Jumanne na Jumatano wanafunzi wasiende shuleni.

"Hii itasaidia kupunguza maafa ambayo yanaweza kutokea kwa kuruhusu watoto waende shule huku tukijiua miundombini yetu haiko salama.Kwa wale ambao wako mabodeni nishauri waondoke huko kwani wanaweza kupata athari zaidi na kwamba hakuna sababu ya kupanda juu ya paa la nyumba kulinda bati,"amefafanua Makonda.

Makonda ameitumia siku ya leo kufanya ziara ya kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambako ameshuhudia namna ambavyo mvua hiyo imeleta madhara katika maeneo mbalimbali ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha hawajengi kwenye njia za maji na kubwa zaidi kutunza mazingira.

SERIKALI KULINDA THAMANI YA SHILINGI KWA KUONGEZA THAMANI YA BIDHAA ZA NDANI

0
0
Na: WFM

Serikali imeeleza kuwa inalinda thamani ya Shilingi kwa kudhibiti mfumuko wa bei ya huduma na bidhaa, kuhamasisha usafirishaji na uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani nje ya nchi kupitia program ya “Export Credit Guarantee Scheme” na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za Kigeni.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Devotha Mathew Minja aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kulinda thamani ya Shilingi kwa kuwa wapo wamiliki wa majengo ambao wanapangisha majengo kwa kutumia fedha za kigeni kama vile Dola ya Kimarekani badala ya fedha ya Kitanzania hivyo kusababisha kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa matumizi ya fedha za kigeni sambamba na Shilingi ya Tanzania hapa nchini yanasimamiwa na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 (The Foreign Exchange Act, 1992), Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya Mwaka 2006 na Tamko la Serikali la mwaka 2007 kuhusu matumizi ya fedha za kigeni kulipia bidhaa na huduma katika soko la ndani.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa mwezi Desemba 2017, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alitoa tamko kwa umma kuwa kuanzia Januari Mosi, 2018 bei zote hapa nchini zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania zikijumuisha kodi ya nyumba za kuishi na ofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei ya vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

“Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, ambapo zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, visa kwa wageni na gharama za viwanja vya ndege na hoteli, hata hivyo wageni hao wanapaswa kutambuliwa kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa Kampuni”. Alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha aliongeza kuwa viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka bei hizo katika sarafu vinatakiwa kuwekwa wazi na visizidi vile vya soko, vilevile ni benki na maduka ya fedha za kigeni pekee ndiyo yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

Katika maswali ya nyongeza ya Mbunge huyo alitaka kujua sababu zinazofanya baadhi ya Taasisi kuendelea kupata na kutoa huduma kwa Dola, pia alihoji Serikali itapitia lini upya Sheria zake ili kuwa na sheria itakayozuia matumizi ya fedha za Kigeni kama ilivyo kwa nchi ya Afrika Kusini.

Dkt. Kijaji alisema kwa kuwa wajibu wa marekebisho na kupitisha Sheria ni wa Bunge hivyo basi, iwapo sheria iliyopo ina upungufu ni vema kukafanyika maboresho kupitia Bunge.“Ikumbukwe kuwa katika misingi ya Uchumi mambo yanayosababisha kushuka au kudorora kwa thamani ya fedha yeyote duniani ni pamoja na Nakisi ya Urari wa Biashara ambapo kwa Serikali ya Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini” alisema Dkt. Kijaji.

Alibainisha kuwa Mfumuko wa bei na tofauti ya Msimu huchangia kushuka kwa thamani ya fedha ambapo Tanzania inaendelea kudhibiti mfumuko huo na Serikali tayari imefunga zaidi ya maduka 92 ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yameshindwa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kudhibiti maduka hayo kuwa kichaka cha kusafirisha fedha za Tanzania isivyo halali mambo ambayo yanaonesha juhudi za Serikali kuimarisha kwa kiwango kikubwa thamani ya shilingi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA JIJINI LONDON

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amkutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza  Mhe. Penny Mordaunt .
Makamu wa Rais ambaye amewasili nchini Uingereza leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mkutano wake na Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.
Makamu wa Rais pia alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.
Mwisho Makamu wa Rais alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara nchini.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za kijamii, alisema nchi yake ipo tayari kusaidia katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt(kushoto) jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahige jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akipokelewa na  Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro alipowasili jijini London.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mbele ya Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BRAZIL

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (hayupo pichani) walipokutana kwa Majadiliano ya Kisiasa yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Aprili, 2018. Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili ya Mhe. Balozi Fernando hapa nchini. Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu namna ya kuboresha mashirikiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili hususan katika eneo la biashara na uwekezaji. 

Pia Naibu Mawaziri hao walijadili namna ya kutekeleza kikamilifu Mradi wa Pamba kwenye eneo la Ziwa Victoria na matokeo ya kusainiwa kwa mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Brazil pia lilijadiliwa. Aidha, Brazil wameahidi kushirikiana na Tanzania kwenye sekta ya afya hususan katika kupambana na maradhi ya Selimundu (Sircle-cell) na kwa upande wa Zanzibar watashirikiana katika afya ya mama na mtoto hususan kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (katikati) nae akizungumza wakati wa majadiliano ya kisiasa kati yake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (hayupo pichani). Wengine kwenye picha ni Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente (kushoto) na Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Kaskazini na Mashariki mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil, Bw. Paulo Cypriano. 
Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimsikiliza kwa makini Mhe. Fernando de Abreu (hayupo pichani), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil wakati wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) 
Mhe. Dkt. Kolimba na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo hayo 
Mhe. Fernando de Abreu na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo
Mhe. Dtk. Kolimba kwa pamoja na Mhe. Balozi Fernando wakishuhudia uwekwaji saini wa Hati ya Makubaliano kuhusu kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil uliokuwa ukisainiwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente. 
Hati ikisainiwa. Pembeni ya Balozi Nchimbi ni Bw. Mustafa M. Ussi, Afisa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria .
Mhe. Balozi Nchimbi na Mhe. Balozi Puente wakibadilishana Hati hiyo mara baada ya kusaini huku Naibu Mawaziri wakishuhudia 
Mhe. Dkt. Susan akiwa na Mhe. Balozi Fernando mara baada ya kukamilisha majadiliano 
Mhe. Dkt. Kolimba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Fernando (wa nne kushoto). Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, mhe. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia), Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Iglesias Puente (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Kilimo, Dkt. Everina Lukonge (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga 
Picha ya pamoja kati ya Naibu Mawaziri na wajumbe wote wa Tanzania na Brazil

Dkt Mwakyembe aeleza misingi ya kisheria Mawaziri kueleza Utekelezaji

0
0

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BIL 12.97/-KIGOMA

0
0
Editha Karlo,Blog ya jamii(Kigoma)

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga ameupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2018 leo kutoka kwa Mkuu wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu katika kijiji cha Nyamtukuza Eilayani Kakonko ambapo mwenye huo utatembela miradi 50 yenye thamani ya Sh.bilioni 12.97.

Mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Kigoma na kati ya miradi hiyo miradi 24 itazinduliwa, miradi 11 itafunguliwa, miradi 11 itawekewa mawe ya msingi na miradi 2 itakaguliwa. 

Pia miradi 2 itakuwa ya uwezesho wa vikundi vya wajasiriamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Mwenge wa mwaka huu umebeba ujumbe wa kauli mbiu"Elimu ni ufungo wa maisha wekeza sasa kwa maedeleo ya Taifa letu".

Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu kitaifa ni Charles Kabeho(Dar es salaam)akishirikiana na Issa Abasi(Kusini Pemba)Agusta Safari(Geita)Ipyana Mlilo(Tanga)Dominick Njunwa(Kigoma)na Riziki Hassa(kusini Unguja).

Aprili 24 mwaka huu Mwenge huo utahitimisha mbio zake mkoani humo na kukabidhiwa mkoani Tabora kwa ajili ya kuendelea na mbio zake.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akisoma taarifa ya Mkoa ya miradi ya mwenge kwa kiongozi mwenge 2018 Charles Kabeho.
Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi mwenge wa uhuru 2018 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagalu kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA, KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mjema akimpa pole mmoja wa akina mama aliyevuka katika daraja la hilo  la muda linalohatarisha usalama wa wananchi wanaopita hapo.
 Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.

 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
 Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.
 Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake.Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya watu.
 Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Diwani wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.
 Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa
serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.
 Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.
 Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja
 la Ulongoni A.

 Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati  baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja  la Ulongoni A.
Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao. RC Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.
Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo RC Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa. Aidha RC Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro.
Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga RC Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao. 
Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini pamoja na vyombo vya habari.

VETA SHINYANGA YAFUNGUA FURSA KWA KUENDELEZA MAFUNZO SEKTA YA MADINI, UJENZI,KILIMO,MISUTU

0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Shinyanga

CHUO cha Ufundi Stadi (VETA)Mkoa wa Shinyanga kimeanzisha na kuendeleza mafunzo ya kozi yenye kulenga kuzalisha nguvukazi yenye ujuzi wa kusaidia sekta za madini, ujenzi, kilimo na misitu. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Afridon Mkhomoi wakati anazungumza na waandishi habari waliotembelea katika chuo hicho leo.Amezitaja kozi zilizoanzishwa katika mwelekeo wa kusaidia sekta hizo ni ukataji na ung’arishaji madini ya vito, ufundi wa mitambo mikubwa,uendeshaji wa mitambo mikubwa na upasuaji miamba.

Amesema chuo cha VETA Shinyanga kina kozi ambazo zina uwigo mkubwa wa ajira katika uchimbaji wa madini, ujenzi, kilimo na misitu, lakini bado idadi ya vijana wanaojiunga ni ndogo.

Aidha amesema mwitikio wa wananchi wenyeji wa Mkoa wa Shinyanga kusoma katika chuo ni mdogo zaidi, hivyo kufanya chuo hicho kudahili zaidi wanafunzi kutoka mikoa mingine.Hata hivyo, kozi ya uendeshaji wa mitambo mikubwa imeonekana kuvutia vijana wengi wakiwemo wasichana na kwa mwaka huu, kozi hiyo ina jumla ya wanafunzi 149.

Ambapo wapo wa mafunzo ya muda mrefu wa miaka miwili na muda mfupi wa miezi miwili. Kati ya wanafunzi hao, 11 ni wasichana.Mmoja wanafunzi wa kozi hiyo, Happiness Mposola amesema amevutiwa na kozi hiyo na kuamua kujiunga nayo licha ya mtazamo uliokuwepo kwa muda mrefu kuwa hiyo ni kozi kwa ajili ya wanaume.

Amesema sasa ni wakati wa wanawake kuamka katika kuchangamkia fursa mbalimbali kwani hakuna kazi alizopangiwa mwanaume au mwanamke pekee, bali kazi zote zinaweza kufanywa na wanaume na wanawake.

Kwa upande wa Mratibu wa Mafunzo wa Chuo hicho, Magu Mabelele amesema, kozi hiyo imevutia hata vijana kutoka nchi zingine za Afrika."Katika kipindi cha miaka miwili tumekupokea wanafunzi kutoka nchi za Rwanda, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi," amefafanua.
 Mkuu wa Chuo cha VETA  Shinyanga, Afridon Mkhomoi akizungumza na waandishi habari walipotembelea chuo hicho kuhusiana na fursa ambazo zinapatikana katika chuo.

02.Mwanafunzi wa Uendeshaji wa Mitambo, Happiness Mposola akizungumza kuhusiana na kozi uendeshaji matambo alivyojipanga.

03.Mwanafunzi wa Veta Shinyanga katika kozi ya Uendeshaji na  Mitambo, Happiness Mposola akiendesha Escaveter ikiwa sehemu ya kozi hiyo.

04.Mwanafunzi wa kozi ya Ukataji na Ungalishaji wa Madini ya Vital, Jeta Giga akingalisha madini ya vital katika mitambo.
.Wanafunzi wa Chuo cha VETA wa wakionesha ujuzi katika kufungua Injini nza mitambo.
Mkufunzi wa Kozi ya Salon na Mapambo, Juddy Marcus akizungumza kuhusiana na kozi ya salon na mwitikio kwa vijana kujifunza kozi hiyo.

MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA

0
0
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake baada ya kupanda moja ya mche wa mti wa asili ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika hilo
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Fokas Bundala(wa kushoto) akipanda mche wa mti wa asili aina ya mninga ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kulia) ni diwani kata ya Visiga Mbegu Kambi Legeza.Picha na Mwamvua Mwinyi


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

JAMII imehimizwa kupanda miti hasa ya asili ambayo ipo hatarini kutoweka pamoja na kulinda mazingira kwa faida na manufaa ya kizazi kijacho.

Aidha wananchi wameaswa kuacha kukata miti na misitu ovyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuondoa uoto wa asili.

Rai hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la – SAHO-linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti na kuhimiza kutunza mazingira , Emmanuel Luamba wakati wa uzinduzi wao wa kampeni ya upandaji miti kata ya Visiga ,Kibaha Mkoani Pwani.

Alisema wananchi wanahimizwa kupanda miti lakini isisahaulike miti ya asili ikiwemo mninga,mkwaju,mkongo ambayo ina faida zake katika kukuza uchumi ,kuleta hewa safi na kuwa na nchi ya kijani.

Luamba alieleza wameotesha miche ya miti ya asili ipatayo 10,000 ambayo wanaisambaza iweze kupandwa taasisi za umma ikiwemo mashuleni ,kwa wananchi kata ya Visiga, kisha ngazi ya halmashauri na baadae Mkoa.

“Tumeanzia taasisi za umma ikiwemo shule mbalimbali na jamii ili kuwa na uelewa wa kujua faida za miti hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vinavyokuja” alielezea Luamba.Akizungumzia ujio wa shirika hilo ,mwenyekiti huyo alibainisha wanatarajia kuwa na matawi nchi nzima .

Luamba alielezea kwamba lengo lao ni kurejesha miti asili kwa kiasi kikubwa kwamaana imekuwa ikivunwa kwa kasi na kuwa na hatari ya kutoweka .Nae diwani wa kata ya Visiga Mbegu Kambi Legeza aliwataka wananchi kushirikiana na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kupanda miti na kuitunza.

“Ni jukumu letu sote kuunga mkono kampeni hii ili kuwa na maeneo na nchi ya kijani pamoja na hewa safi ” alisema Legeza.Legeza alikemea ukataji miti kiholela na kuchoma moto miti kwa ajili ya mkaa kusiko kwa utaratibu maalumu hali inayosababisha kupoteza miti .

Aliishukuru SAHO kwa kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kunarejeshwa uoto wa asili na kutunza na kupanda miti kwenye mazingira yanayotuzunguka.Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ,makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Fokas Bundala aliwataka wananchi kuilinda miche ya miti wanayopewa kupanda badala ya kuitelekeza .

Kwa upande wake ,mwanafunzi wa shule ya msingi Visiga ,anaesoma darasa la saba ,Abdul Faraji alieleza wamepanda miche ya miti shuleni hapo na alilishukuru Shirika hilo kwa kuona umuhimu kuanza na kampeni hiyo katika shule mabalimbali ili kupata ufahamu wa miti hiyo.

Alisema wamekuwa wakisikia miti ya asili bila kujua ni ipi na faida zake lakini sasa atakuwa balozi mzuri kuwaelimisha watoto wengine juu ya suala hilo .

SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI MATUKIO YA UVUVI HARAMU NCHINI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katikati akipanda moja kati ya mikoko ya miche 140,000 iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga kulia ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn MworiaWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katikati akipanda moja kati ya mikoko ya miche 140,000 iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga kulia ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wa tatu kutoka kulia akiwa na Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia kushoto wakitembela kwenye ufukwe wa bahari ya hindi mara baada ya kupanda moja kati ya mikoko iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katika akizungumza mara baada ya kupanda miti hiyo ya mikoko kushoto ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn MworiaWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba kulia akimsikiliza kwa umakini Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia katikati aliyekuwa akieleza dhamira yao ya kusaidia upandaji wa miti hiyo ya mikokoSehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakipiga selfie na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji wa miti ya mikokoWafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba mara baada ya kumalzika kwa zoezi la upandaji wa miti ya mikoko


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema serikali imefanikiwa kudhibiti matukio ya uvuvi haramu kwa zaidi ya asilimia 80 katika maeneo ya bahari na maziwa baada ya kuimarisha doria na ukaguzi wa samaki wanaovuliwa.

Aliyasema hayo wakati wa upandaji wa mikoko katika Pwani ya Bahari ya Hindi ambayo ilipandwa eneo la Mwambani Jijini Tanga chini ya Udhamini wa Mfuko wa Vodacom (Vodacom Faundation).

Alisema kuimarika kwa doria hizo kumesaidia wananachi kuwa na uelewa mpana kuhusu madhara ya uvuvi haramu na hivyo kuanz kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo ikiwemo ulinzi wa mazingira ya bahari ya hindi na rasilimali zake.

Waziri huyo alisema pamoja na jitihada za wizara katika kudhibiti fukwe za bahari zinasiendelee kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi lakini bado kuna maeneo mengi ambayo yanahitaji kuhifadhiwa kwa kupandwa miti ya mikoko.

Pamoja na hayo Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Vodacom Foundation kwa kuja na kampeni ya upandaji wa mikoko ili kuhifadhi mazingira ya bahari kwa kile alichosema kuwa kutasaidia kuboresha mazingira hayo.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na chama cha skauti Tanzania waliamua kuja na kampeni hiyo upandaji wa mikoko ili kuhifadhi mazingira ya Fukwe.

Alisema kwamba kwa kuanzia kampeni hiyo wameanzia kwa mkoa wa Tanga na wanatarajia kuipeleka nchi nzima ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images