Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1560 | 1561 | (Page 1562) | 1563 | 1564 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  SHULE ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea jijini  Dar es Salaam imeshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.

  Wakati Shule ya Msingi Mtendeni imeshika nafasi ya kwanza kwa shule bora za Serikali ambapo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo imetoa tuzo kwa shule hizo pamoja na nyingine ambazo nazo zimefanya vizuri.

  Akizungumza Dar es Salaam leo baada ya kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema , Mwalimu Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate Julius Luge amesema shule yao imefanya vizuri kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya menejimenti, walimu, wanafunzi na wazazi.

  Amesema tuzo hiyo imewapa ari zaidi ya kuendelea kujikita kutoa elimu bura na sahihi kwa wanafunzi wa shuleni kwao na kufafanua mbali ya kufanya vizuri kitaaluma pia wanafunzi wao wamefanya vizuri katika eneo la vipaji,"Moja ya mikakati ya shule yetu ni kufanya vizuri katika eneo la taaluma ya elimu lakini pia tumejikita katika kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wetu .Hivyo tupo vizuri katika taaluma na kukuza vipaji na imani yetu tutaendelea kufanya vizuri zaidi ya hapa,"amesema Mwalimu Luge.

  Shule ya Fourtain Gate imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana namna ambavyo imejikita katika kutoa elimu bora na kuhakikisha wanashika nafasi za kwanza kwenye matokeo ya kitaifa na hiyo inatokana na kazi kubwa inayofanywa na walimu katika kuandaa wanafunzi wao kitaaluma.Awali Ofisa Elimu Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas akitaja shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mbali na Fourtain Gate kwa shule za binafsi nafasi ya pili ni Tusiime, ya tatu St.Joseph Millleniam, nafasi ya nne Genius King, nafasi ya tano Masedonian na sita Lusasaro.

  Nafasi ya saba imeshikiliwa na Shule ya Batvalley , nafasi ya nane Nyiwa, nafasi ya tisa Herritage na nafasi ya 10 ni Green Hill.Kwa upande wa shule bora za Serikali Thomas amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Shule ya Msingi Mtendeni,Shule ya Msingi Zanaki imeshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ni Shule ya Msingi Kiwalani.

  Ametaja nafasi ya nne ni shule ya msingi Olimpio, nafasi ya tano Shule ya Msimbazi Mseto, nafasi ya sita Shule ya Msingi Diamond, nafasi ya nane Shule ya Msingi Lumumba, nafasi ya tisa Shule ya Msingi Mkoani na nafasi ya 10 Shule ya Msingi Maktaba.Manispaa ya Ilala katika matokeo ya mtihani wa darasa
  la saba mwaka jana kimkoa imeshika nafasi ya pili na kitaifa imeshika nafasi ya nne.Hata hivyo shule hizo zimetakiwa kuongeza juhudi ili washike nafasi ya kwanza kwa matokeo ya mwaka huu kwa ngazi ya kitaifa na kimkoa.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema(mwenye kiremba) akiwa na Mwalim Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea Julius Luge leo baada ya kumkabidhi tuzo maalumu kutokana na shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 bora za binafsi katika matokeo ya mtihani wa darasa saba mwaka 2017 kwa shule zilizopo kwenye manispaa hiyo.
   Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza katika hafla za utoaji wa tuzo hizo leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na walimu,wanafunzi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa shule za msingi zilizofanya vizuri katika Manispaa ya Ilala leo jiji Dar as Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika kitabu cha maombolezo alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa mjane wa marehemu Mama Cesilia Kabula Fidelis alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho walipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa watoto wa marehemu Bw. Richard Lubala (kushoto kwake) na Charles Lubala (kulia kwake) alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
  Mama Janeth Magufuli akimpa maneno ya faraja Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, kwa kufiwa na baba yake mzazi Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, kwa kufiwa na baba yake mzazi Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifariji wafiwa walipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Jacek Czaputowicz mara baada ya kumkaribisha rasmi Wizarani tarehe 12 Aprili, 2018. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, kilimo, utalii, biashara na uwekezaji. Mhe. Czaputowicz yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atazindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
  Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Czaputowicz wakionesha Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Poland.

  Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin (kulia) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kushoto), Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha (wa pili kushoto) na Afisa Mawasiliano, Bi. Robi Bwiru (wa pili kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Czaputowicz (hawapo pichani).

  Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akiwa na Wajumbe wengine kutoka Poland wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe Czaputowicz (hawapo pichani)
  Picha ya pamoja.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao kushiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi  Aprili 12, 2018. Kulia ni mke mdogo, Bibi      Nekiteto Sokoine.
   Mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, akimvisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mgolole wa Kimasai ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani kwao, kijiji cha Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha Alhamisi Aprili 12, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo ya marehemu Edward M. Sokoine kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi  Aprili 12, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi wa mkoa wa Arusha na wa Serikali kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia baada ya kutoa salaam zake kwa wananchi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiomba dua baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Sokoine mara baada ya kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kuenzi fikra za hayati Edward Moringe Sokoine.  

  “Tutaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma kwa kuzingatia yale yote ambayo Mheshimiwa Sokoine aliyaanzisha,” amesema. 
   Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, Aprili 12, 2018 wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha Sokoine, iliyofanyika kijijini kwake Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha. 

  Ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu  Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha,  Mhashamu Josephat Lebulu, ilihudhuriwa na viongozi wa dini wa wilaya, viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Tate ole Nasha na baadhi ya wabunge.

   Waziri Mkuu amesema Mhe. Sokoine alikuwa adui wa wahujumu uchumi na alihakikisha uchumi wa nchi unakua kwa maslahi ya Watanzania wote. “Mungu alitupa hazina iliyong'ara na kuangaza. Sote tuendelee kuangaza kwa kutenda mema na kuendeleza yale yote aliyoyaanzisha mpendwa wetu,” alisema.  
  “Katika maisha yake,  hakuwa na ubinafsi, uroho, wala tamaa ya kujilimbikizia mali. Hili ni jambo la kuigwa na sisi viongozi wa umma. Nasi tulioko kwenye nafasi hizi za uongozi,  tumuombe Mungu atuwezeshe tutende yale aliyoyaanzisha,” alisisitiza.  

  Alitumia fursa hiyo kuwafikishia wanafamilia na wananchi waliohudhuria ibada hiyo, salaam za pole kutoka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.  
  Mapema, akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mst. Lebulu alimuelezea hayati Sokoine kuwa ni kiongozi aliyechapa kazi kwa bidii, mwenye uzalendo, aliyeongozwa na upendo na uwajibikaji kwa wananchi anaowaongoza.  

  “Ili tuweze kuwajibika na kuwa wazalendo kwelikweli, tunapaswa kuwa waaminifu na watu tunaomcha Mungu. Mtu awaye wa dini yoyote ile, kama hamchi Mungu, hawezi kuwa muwajibikaji.” Alisema kila mtu anapaswa kumheshimu mwenzake kwa dini na imani yake. “Tuheshimiane kila mmoja kwa dini na imani yake, kwa sababu sote tumeumbwa kwa sura na mfano wake. Siyo kwamba tuvumiliane, tunatakiwa tusidharauliane bali tuheshimiane,” alisisitiza.

  “Ni lazima tuwe waaminifu, tuache unafiki, tuache kuwa na maisha yenye hila na hiyana na badala yake, tuongozwe na dhamiri safi. Tuwe waaminifu kwa wenzetu, kwa dini na imani zetu na zaidi ya yote tuwe waaminifu kwa nchi yetu,” alisema. “Ni aibu kukuta Mtanzania anaitukana nchi yake. Tupende vijiji vyetu, tarafa zetu, mikoa yetu na nchi yetu. Tuipende, tuitunze na tuilinde ili iwe nchi bora. Tuwe mfano kwa watoto wetu na wazazi wetu katika kuijali nchi yetu,” alisisitiza. 

  Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi alipopewa nafasi awasalimie wananchi, alisema kuna watu wanakufa lakini bado wanaendelea kuwa hai na kwa hilo, wanafamilia wanapaswa kuendelea kumshukuru Mungu. 
  "Tangu alipofariki mwaka 1984, hakuna mtu aliyejua kwamba hadi sasa, ambapo ni miaka 34 imepita, Edward Moringe Sokoine ataendelea kuwa hai. Ninasema yu hai kwa sababu maneno na matendo yake, bado yanaishi,” alisema. 

  “Edward Moringe Sokoine amegoma kufa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere amekataa kufa. Na sisi wasaidizi wa Rais Magufuli, tunapaswa kujitoa kwa wananchi na Taifa; kujiongeza zaidi katika utumishi wetu na hasa kuwajibika kwa kulitumikia zaidi Taifa kuliko kudai mapato ili tutakapoitwa kwenye promosheni iliyo kuu, wanaosalia waone faida ya kuwepo kwetu hapa duniani,” alisema huku akishangiliwa.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya familia, msemaji wa familia ya marehemu Sokoine, Bw, Lembris Kivuyo alisema wanaishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa karibu sana na familia hiyo tangu Mhe. Sokoine alipofariki. 
  “Tunaishukuru sana Serikali na tunazidi kuwasihi Watanzania waendelee kumuombea Mheshimiwa Rais Magufuli ili aendelee kuongoza Taifa hili bila ajizi na sisi kama familia tutaendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika jitihada zake za kutetea rasilmali za Taifa,” alisema.


  0 0


  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuhusu mikakati wa bandari hiyo kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi MtambalikePRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huoMwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huoSehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga  MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa yaliyofanyika.

  Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji .

  Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo kusafirisha bidhaa zao.

  “Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama.

  Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika.

  “Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia shehena inayowasili “Alisema.

  Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika kufanya kazi hizo kwa wakati (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  0 0


  0 0


  Wahenga wanasema hujafa hujaumbika. Na ule msemo usemao kwamba maendeleo hayana vyama ni hakika na bayana. 

  Mwezi January mwaka huu nilikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa mahabusu kwa siku 8 kesi ya kisiasa , Hali hiyo ilimpelekea mke wangu Stellah ambaye alikuwa mjamzito kupata mshutuko na kuharibu mwenendo wa mimba yake. 

  Jana usiku mke wangu ninayempenda sana hakuweza kuendelea kumlea mtoto akiwa tumboni badala yake madakatari walihangaika kuokoa uhai wa mwanangu na mama yake na kazi hiyo walifanikisha kwa 100%.

  Lengo la ujumbe huu ni shukrani za dhati kwa ASAS FAMILY waliojenga jengo la kuokoa maisha ya watoto wachanga ASAS NEONATAL UNIT watoto ambao walikuwa wanapoteza maisha yao kila siku kutokana na vifaa tiba duni pamoja na ukosefu wa wodi yenyewe ya kutunza ninaoweza kuwaita "Malaika wa Mungu".

  Amenidokeza Nesi mmoja katika hosipitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa kuwa kwa juma moja kabla ya ASAS FAMILY kujenga jengo hilo kupitia Mkurugenzi wao SALIM ABRI ASAS wameweza kupunguza kiwango cha vifo kutoka 20 mpaka vifo vya wachanga 2.

  Nesi huyo ameendelea mbele na kunieleza kuwa ASAS haohao wamejenga Intesive Care Unit (ICU) ya kisasa ambayo imegharimu zaidi ya 300,000,000/= yenye uwezo wa kuhudumia mahutihuti 10 kwa mara moja ambayo bado haijazindiliwa. 

  Ninajua wana Iringa wengi watapata huduma hapo kama mwanangu mwenye 850gm anavyopata huduma leo. 

  I humbly acknowledge and pray for the blessings to the efforts made by this family to save hundreds of patients. 

  Leonce Marto , 

  Mkt BAVICHA IringaMjini.

  12.04,2018 .

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega walipokutana na Wadhamini na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya maonesho hayo (hawapo pichani) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25 - 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.
  Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Aprili 2018 katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kuambatana na hafla ya kukabidhi udhamini kwa ajili ya kufanikisha maonesho hayo maarufu kama ''Wiki ya Tanzania nchini Kenya'' ambayo yataenda sambamba na sherehe za miaka 54 za Muungano wa Tanzania. 
  Sehemu ya wadhamini na wajumbe wa kamati ya maandalizi wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiongozwa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) 
  Viongozi wa Kampuni ya NIDA TEXTILE MILLS (T) wakimkabidhi Mhe. Waziri Mahiga mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 22,700,000/- kwa ajili ya kudhamini maonesho ya didhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Muhammad Waseem. 
  Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru Mwakilishi wa Kampuni ya Mohamed Enterprises, Bi. Barbara Gonzale baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha shillingi millioni ishirini na tano (25,000,000) kwa ajili ya kudhamini maonesho hayo. 
  Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru mwakilishi kutoka kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd, Bw. Maleke Hans baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha Dola za Marekani 5,000 (sawa na shilingi milioni kumi na moja za Tanzania). 
  Mhe. Waziri Mahiga akisikiliza taarifa fupi ya udhamini na hatua ya maandalizi iliyofikiwa kutoka kwa Katibu wa Kamati, Balozi Mbega, pembeni ni baadhi ya Wadhamini na Wajumbe wa Kamati. 
  Sehemu nyingine ya wajumbe wa kamati wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Balozi Mbega kwa Mhe. Waziri Mahiga. 
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Jacek Czaputowicz wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa Poland hapa nchini. Ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo zilizopo Masaki, Jijini Dar es Salaam ulifanyika tarehe 12 Aprili, 2018. Ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Poland, nchi hiyo ilifungua tena Ubalozi wake hapa nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya uzinduzi wa ofisi hizi hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya. 
  Waziri Mahiga akimpongeza Waziri Czaputowicz kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kufungua Ofisi za Ubalozi hapa nchini. 
  Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Waziri Czaputowicz wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ufunguzi wa ofisi za Ubalozi wa Poland nchini.
  Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Czaputowicza na waandishi wa habari ukiendelea.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa baadhi ya viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea katika Ofisi yake Bungeni Dodoma Aprili 12, 2018.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kanisa la Baptist nchini.
  Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama kuzungumza masuala yao na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada za kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipata maelekezo ya hati ya pongezi (ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli) kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwashukuru viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)  Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendela kuliombea Taifa ili kudumisha Amani na Utulivu uliopo.

  Ametoa pongezi hizo hii leo alipokutana na Uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza Serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

  “Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo.”Alisema Waziri Mhagama

  Aliongezea kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wetu wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kufikia azma yake ya “Tanzania ya Viwanda”.

  “Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu Uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na Viongozi wote kwa ujumla wao ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo.”Alisisitiza Waziri Mhagama

  Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika Huduma za kijamii hususan kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na Shule, Vyuo na Zahanati zinazohudumia Wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.

  “Ni vyema sasa mkawa na mipango endelevu ya kuboresha Taasisi zenu ikiwemo Chuo cha Mount Meru na shule zenu ili kuendelea kutoa huduma za kielimu, afya ili kuwa na Watanzania wenye uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.”Alisisitiza Waziri.

  Aidha kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.

  “Binafsi ninaipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa juhudi zake pamoja na uongozi wote na tunaahidi kuendelea kuwaweka mikononi mwa Mungu ili kuwa na nchi yenye Amani, Upendo, Mshikamano na Utulivu.”Alisisitiza Askofu Manase.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe. 

  Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama inatekelezwa. 

  Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana. 

  "Miradi yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema Kamba 

  Aliongeza kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia makubaliano ya kuomba punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika kwenye ujenzi miradi. 

  Aidha Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa local fundi unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku thamani ya fedha ikionekana. Kamba aliwataka watumishi kuona anao wajibu na sehemu yake ya kufanya kazi na kuhudumia wnanchi ikiwa ni utekelezaji wa ilanai na kuhakikisha lengo lililowekwa linafikiwa kwa kiwango cha juu. 

  Kwa upande wake a Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa alisema kwamba yeye pamoja na Madiwani , Mkurugenzi na watendaji wake wanaimba wimbo mmoja , thamani ya fedha inayoonekana katika kila mradi ni matokeo ya usimamizi uliopo ambao wamepewa na mamalaka kusimamaia. 

  Ameongeza kuwa kigamboni inaweza kuwa ya kwanza kwa Halmashauri zinazotekeleza ujenzi wa makao makuu tangu kuanzishwa kwani ndani ya kipindi kifupi cha miaka 2 tangu kuanzishwa kwake na watumishi watakuwa tayari kwenye jengo lao la Utawala lenye ghorofa 3, hii imewezekana kutokana na mfumo mzuri wa matumizi ya fedha. 

  Aidha alisema kuwa mfumo unaotumika wa mafundi wenyeji unaokoa kiwango kikubwa cha fedha ambazo zilikuwa zinapotea bila sababu katika mfumo wa manunuzi. 

  "Nadhani tuendelee kuangali hizi sheria za manunuzi, zinazumiza sana Serikali na tuanze kufuata taratibu za kawaida, mfano mfuko wa misumari kwa mfumo wa manunuzi unaweza nunua hadi elfu 6000, wakati kawaida unanunua elfu3000 hadi elfu 3500"Alisema Mkuu wa Wilaya. 

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephene Katemba alisema kuwa anashukuru kutembelewa na viongozi wake na kuona namna gani Ilani  ya Chama inatekelezwa, 

  Amesema hadi sasa ameshapokea Bilion 2 kwaajili ya ujenzi wa jengo la utawala na taratibu zote zimezingatiwa za kupata mkandarasi , mradi unayobond ya kulinda( secured bond) na performance bond ( fedha zitekelezwe kwa kadri inavyotakiwa). 

  Mwisho alishukuru ujio wa viongozi wa Chama na kwamba kwake ni hamasa kubwa hivyo yeye kama kiongozi atajitahidi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kadri ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotaka. 

  Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa iliyoambatana na viongozi mbalimbali wa Chama walipata fursa ya kutembelea mradi wa ukarabati wa Zahanati ya Buyuni, Ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji, Ujenzi wa miundombinu ya Shule kwaajili ya kuanzisha kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Nguva, ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa uanzishwaji Sekondari eneo la Shule ya Msingi Kigamboni. 


  Imeandaliwa na: 
  Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano 
  Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni 

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.

  Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao
   

  jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta ​
  Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha ​
  muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti
  Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni akiwa ameongozana na viongozi nyingine kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kimbiji. ​
  ​ Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dk.Charles Mkombachepa akitoa maelekezo ndani ya jengo la maabara na upasuaji ​

  0 0

  *Ahimiza vijana kusaka maarifa kwa nguvu zote ili wawe viongozi bora
  *Ataka wazee kurithisha vijana yale yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere

  Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira katika Serikali ya Awamu ya Tano Januari Makamba amesema vijana wengi nchini kwa sasa wamejaa taarifa badala ya 
  maarifa.

  Hivyo amesema ili vijana wawe viongozi bora na wanzuri kwa Taifa letu ni vema wakafanya juhudi na kuhakikisha wanapata maarifa ambayo yatakuwa dira na muelekeo kwa nchi yetu.January amesema hayo leo wakati wa Kongamabo la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo imefanyika katika Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaa. 

  Mada kuu kwenye kongamano inasema Kuelekea uchumi wa kati mchango wa Mwalimu Nyerere kuhusu amani,umoja wa kitaifa na uwajibikaji.Amesema yeye kama viongozi kijana ametumia kongamano hilo muhimu kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere katika ujenzi wa taifa hili na kwa sehemu kubwa aliongoza kwa maarifa makubwa na yenye tija kwa nchi yetu.

  Hivyo amesema kwa vijana wote wa Tanzania hasa wanaotaka kuwa viongozi ni vema wakajikita kitafuta maarifa zaidi badala ya kujaza taarifa vichwani ambazo nyingine hazina tija.

  "Taarifa inakuwezesha tu kuwa mzuri kwenye mazungunzo katika vijiwe vya kahawa na katika kupiga soga.Lakini ukiwa na maarifa yatakufanya kijana kuwa kiongozi bora kwa nchi yetu.Nimebahatika kwenda Butiama na nilipofika nilifanikiwa kuingia maktaba yake Mwalimu, utaona namna ambavyo 
  amesoma vitabu vingi sana ili kuwa na maarifa mapana kwa ajili ya kuliongoza vema taifa letu,"amesema January.

  Ametoa mwito kwa vijana nchini kuhakikisha wanatumia muda mwingi kusaka maarifa badala ya taarifa na kuongeza Mwalimu Nyerere alifika Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 32 lakini kutokana na maarifa yake wazee walimuamini na akawa Rais wa Tanu.

  Amefafanua kwa bahati mbaya kwenye mitandao ya kijamii kwa sehemu kubwa vijana wanaangalia zaidi mambo ambayo hayana maana na kutoa mifano kwa kueleza wengi wanaangalia taarifa za wasanii."Nenda kwenye youtub kisha angalia hotuba za Mwalimu Nyerere ambayo zinazungumzia mambo mapana ya nchi yametazamwa na watu ngapi.

  Kisha angalia mambo yanayohusu wasanii yametazamwa 
  na watu wakangapi.Utaona taarifa za wasanii zinaangaliwa zaidi kuliko hotuba za Mwalimu ambazo ni muhimu kuangaliwa na kila kijana,"amesema.

  Pia amesema vijana waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere wametimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanajenga nchini na kuweka misingi imara ya umoja na mshikamano, hivyo swali ambalo vijana wa sasa wamepanga kufanya nini kwa ajili ya nchi yetu.Amefafanua Mwalimu Nyerere wakati wa uhai amewahi kutoa hutuba ambayo alizungumzia kuanza kuona nyufa,hivyo vijana waliopo leo lazima watafakari nyufa hizo bado zipo na nini wanafanya kiziziba.

  Kuhusu umuhimu wa kukumbukizi ya Mwalimu ,January amesema ni muhimu kuwa na kongamano hilo kwani linatoa nafasi kwa vijana kufahamu Mwalimu Nyerere alifanya nini kwa ajili ya Taifa letu.


  Baadhi ya wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere January Makamba(hayupo pichani) leo.
  Mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Janaary Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa na viongozi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere baada ya kufungua rasmi kongamano hilo ambalo lilikuwa na mada mbalimbali. kongamano hilo limefanyika leo chuoni hapo

  0 0  Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo Tanzania, Hussein Sayed (kushoto) akizungumza na waandishi kuhusu uthibitisho wa kimataifa wa huduma za fedha kwa njia ya simu ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’ ambao huduma ya kifedha ya Tigo Pesa imetunukiwa katika kongamano la Mobile 360 World Congress lililofanyika mjini Abidjan, Cote d'Ivoire jana. Uthibitisho huo unaifanya Tigo Pesa kuwa mojawapo ya huduma za kifedha kwa njia ya simu ya kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huo wa kimataifa. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kulia) akizungumza na waandishi kuhusu uthibitisho wa kimataifa wa huduma za fedha kwa njia ya simu ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’ ambao huduma ya kifedha ya Tigo Pesa imetunukiwa katika kongamano la Mobile 360 World Congress lililofanyika mjini Abidjan, Cote d'Ivoire jana. Uthibitisho huo unaifanya Tigo Pesa kuwa mojawapo ya huduma za kifedha kwa njia ya simu ya kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huo wa kimataifa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo Tanzania, Hussein Sayed .  Tigo Pesa, huduma ya kifedha kwa simu za mkononi inayoongoza nchini, imepokea uthibitisho wa kimataifa ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’.

  Uthibitisho huu unatambua uwezo mkubwa wa Tigo Pesa katika kutoa huduma salama, kwa uwazi, za kuaminika na thabiti zinazokuza haki za wateja na kuzuia miamala ya kihalifu. Tigo Pesa ni moja kati ya watoa huduma za kifedha kwa simu za mkononi wa kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huu kutoka GSMA.

  GSMA Mobile Money Certification’ ni mkakati wa kimataifa unaolenga kuleta huduma za kifedha salama, wazi na thabiti zaidi kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi duniani kote. Huku kukiwa na zaidi ya akaunti 690 milioni za fedha kwa simu za mkononi duniani, sekta ya simu za mkononi inaboresha maisha duniani na imewezesha mamilioni ya watu wasiokuwa na akaunti za benki kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo, Hussein Sayed alisema, “Tigo Pesa inajivunia mchango wake mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha nchini kwa kutoa fursa kwa mamilioni ya Watanzania wasio na huduma za kibenki kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kifedha.’

  Uthibitisho huu kutoka GSMA ni ishara tosha kuwa Tigo Pesa imepiga hatua kubwa kuhakikisha kuwa fedha za wateja wetu zipo salama, na kuwa haki zao zinalindwa. Kupitia taratibu zetu za kibiashara tunalenga kutoa huduma zenye viwango vya juu zaidi.

  GSMA imebainisha kuwa vigezo vinavyotumika kutoa uthibitisho huu vinazingatia viwango vya ubora wa kimataifa katika utoaji huduma za kifedha. Kabla ya kupokea uthibitisho huo, kila mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu za mkononi sharti afikie asilimia 100% ya vigezo vilivyowekwa. Watoa huduma wanaopokea uthibitisho huu ni wale tu waliofanikiwa kuonesha kuwa hatua za uendeshaji wa biashara zao ni miongoni mwa zile zilizo bora, zinazoaminika na kuwajibika zaidi katika mfumo mzima wa utoaji huduma za kifedha duniani.

  “Tigo Pesa inajivunia kufikia vigezo vilivyotuwezesha kupokea uthibitisho huu kutoka GSMA. Hii inaonesha ubora na uwajibikaji katika huduma zetu. Vile vile inathibitisha kuwa tunaongoza katika mageuzi ya kidigitali na utoaji wa huduma za kifedha ulimwenguni,’ Hussein aliongeza.

  Pamoja na azma ya Tigo kutoa huduma za kiwango cha kimatifa kwa wateja wetu, huduma yetu ya Tigo pesa imeboreshwa na kuwa mfumo kamili wa huduma za kifedha. Daima tupo mstari wa mbele katika ubunifu wa huduma katika soko hili; kwa mfano tulikuwa mtoa huduma wa kwanza duniani kuzindua huduma ya fedha kwa simu za mkononi iliyowezesha uhamishaji wa fedha kwenda mitandao mingine nchini. Pia tulianzisha huduma ya kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi kwa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika. Tigo pia ndio kampuni ya kwanza ya simu za mkononi kutoa gawio la faida kwa wateja wetu.

  ‘Uthibitisho huu wa GSMA unaashiria uendeshaji wa biashara yetu unazingatia mojawapo ya mifumo bora zaidi duniani. Tigo Pesa inaaminika na kuwajibika, hivyo ni mshirika bora wa kibiashara,’ Afisa huyo Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo alibainisha.

  ‘GSMA Mobile Money Certification’ unaonesha mwamko mkubwa kwa upande wa watoa huduma kuzuia utakatishaji wa fedha na ufadhili wa ugaidi; pamoja na kutoa huduma bora, za uhakika, salama na zisizokuwa na upendeleo kwa wateja na washirika wote wa kibiashara.


  0 0

   Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF), wakiendelea na zoezi la usajili wa watoto kwenye bima ya afya ambao wanalipiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda.  Mpango wa TOTO AFYA KADI unamnufaisha mtoto chini ya umri wa miaka 18.


  0 0

   Makamu wa Rais akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman leo ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   Makamu wa Rais akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshinda ofisini kwa  Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshinda ofisini kwa  Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) ​

  0 0

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), inaratibu ziara ya viongozi wa makampuni ya biashara zaidi ya 30 kutoka Ufaransa ambao ni wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Ufaransa (MEDEF) yenye mtandao wa makampuni zaidi ya 7100.

  Ziara hiyo itakayofanyika kuanzia tarehe 15 – 18 Aprili 2018, inalenga kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa; kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania; kushawishi makampuni makubwa ya Ufaransa kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo nishati, miundombinu, viwanda, maji n.k na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu na kuanzisha ushirikiano baina yao.

  Ukiwa nchini, ujumbe huo utapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa serikali na kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ufaransa litakalofanyika tarehe 18 Aprili 2018, jijini Dar es Salaam. 

  Aidha, baada ya kongamano hilo, Wizara kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) itafanya mkutano na wafanyabiashara Wakitanzania wenye nia ya kutafuta masoko nchini Ufaransa, tarehe 20 Aprili 2018. Ubalozi utaelezea fursa zilizopo nchini Ufaransa na mikakati ya kufanya bidhaa za Tanzania hususan za kilimo ziweze kuuzwa nchini humo.

  Wizara inatoa wito kwa Wafanyabishara wa Tanzania kushiriki kikamilifu na kuchangamkia fursa hii muhimu.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dar es Salaam
  13 Aprili, 2018

  0 0


  0 0

   Muonekano wa ubavuni wa jengo la bweni la wanafunzi  
    moja ya chumba cha wanafunzi ndani ya bweni 
   korido la moja ya bweni litakalotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano
   ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea
  moja ya jengo la maabara ya kisayansi
   baadhi ya vifaa vya majaribio ka vitendo vilivyopo ndani  ya maabara ya sayansi
   baadhi ya vifaa kwaajili ya mafunzo kwa vitendo

  Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kufungua kidato cha tano na sita Julai mwaka huu katika Shule ya Sekondari Nguva kwa kuwa na wanafunzi 160 wa kiume pekee ikiwa na michepuo ya PCM,PCB,HGE na EGM. 

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari yenye kidato cha tano na sita kwenye Halmashauri, na kutimiza maelekezo ya Serikali kwa kila Halmashauri kuwa na shule ya kidato cha tano na sita, Manispaa iliamua kuboresha miundombinu ya Shule ya Nguva ili iweze kukidhi mahitaji hayo. 

  Aidha amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa thamani ya shilingi 492,864,576 kwa kushirikiana na Serikali kuu, ambapo Serikali kuu imeweza kuchangia kiasi cha shilingi 259,000,000 na vyanzo vya ndani vya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ilichangia shilingi 233,864.576. 

  Mkurugenzi amesema kwamba ili kuhakikisha Shule ina hadhi ya kidato cha tano na sita kwa mujibu wa vigezo vya wizara, ujenzi wa mabweni mawili kwaajili ya wanafunzi, vyoo, ujenzi wa daharia ambao bado unaendelea, ujenzi wa madarasa manne na ununuzi wa madawati, ununuzi wa vitanda kwaajili ya mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa maabara ya sayansi na ujenzi wa jengo la utawala linalojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda vimefanyika . 

  Mkurugenzi amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha masomo ya kidato cha tano na sita yanatolewa kwa watoto wanaomaliza kidato cha nne kwa shule za sekondari za Kigamboni. 

  Kukamilika kwa mradi kutawezesha kuongeza idadi ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na sita,kuchochea maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kutoa fursa pana kwa wanafunzi kujiunga na elimu ya juu. 

  Ameongeza kuwa ujenzi wa bwalo la chakula litakalowawezesha wanafunzi kutumia kwaajili ya chakula linaendelea kujengwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. 

  Imeandaliwa na: 
  Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano 
  Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni 
  13/04/2018
   

older | 1 | .... | 1560 | 1561 | (Page 1562) | 1563 | 1564 | .... | 1897 | newer