Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1559 | 1560 | (Page 1561) | 1562 | 1563 | .... | 1896 | newer

  0 0


  0 0

  Na: Calvin Edward Gwabara, Morogoro.


  SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linaisaidia Tanzania kuwa na mfumo bora wa kukusanya na kuhifadhi taarifa za hewa ya ukaa nchini ili taarifa hizo ziweze kutumika katika mipango mbalimbali ya kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuwa na taarifa sahihi za mchango wan chi katika kukabiliana na tatizo hilo.
  Baadhi ya washiriki mafunzo hayo kutoka wizara mbalimbali na vyuo vikuu wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo.
  Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa wadau wakuu wa mpango huo na namna ya kutumia mfumo huo katika kukusanya taarifa hizo mtaalamu wa miradi inayohusu nishati na mabadiliko ya tabia nchi kutoka UNDP tawi la Tanzania Bwana Abbas Kitogo amesema mfumo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na takwimu sahihi za hali ya hewa ya ukaa na namna tunavyopambana katika kuipunguza .
  Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania hatuna taarifa sahihi na rasmi sana pale inapotakiwa kueleza mchango wetu kama taifa katika kutatua changamoto hiyo na hivyo kushindwa kujua kama nchi tufanye tuongeze nguvu wapi au tufanye nini katika kusaidia jitihada hizo za dunia.  Aidha amebainisha kuwa kupitia mradi huo wa kujenga uwezo wa serikali katika kujenga mifumo ya jinsi ya kuzia hewa ukaa Tanzania wameamua kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kama vile wizara na vyuo vikuu lengo likuwa ni kuwawezesha wataalamu wa serikali kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi  na kuzitolea taarifa kule zinakotakiwa.

  ‘’Tunatakiwa kutoa taarifa kwa umoja wa mataifa ule mpango maalumu wa hewa ukaa na mbadiliko ya tabia ya nchi tunazalisha hewa kiasi gani na mipango yetu ya kupunguza ni kiasi gani na namna ambavyo kama nchi tunaweza kupambana na tatizo hilo hivyo ni muhimu mfumo huu wa taarifa uwepo maana kwa sasa hatuna’’ Alisema Kitogo.


  Amesema kuwa Wataalamu wametungenezea mfumo GG inventory System  ambao utakuwa katika hali ya taarifa lakini pia kama tovuti maalumu ambayo itakuwa inasimamiwa ofisi ya makamu raisi lakini watakaokuwa wanaifanyia kazi ni kituo cha kitaifa cha kufuatilia kaboni kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo  SUA maana wao ndio wana utaalamu wa kufanya kazi hii.

  Ameongeza kuwa kwa kuweka mfumo huo SUA utawezesha wanafunzi pia wanaosoma hapo kuweza kujifunza na kuwa na uwezo kuutumia mfumo lakini pia kuona namna unavyofanya kazi pale ambapo watakutana nao.

  ‘’Tumepitisha mkataba wa Paris wa kuungamkono juhudi za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika hewa ya ukaa hivyo ni muhimu kuwa na mfumo huo ambao utatuwezesha Tanzania kujitathimini na kuona jitihada zinazofanyika pale tunapotakiwa kutoa taarifa ya nchi kwenye umoja wa mataifa’’ Aliongeza Kitogo.

  Amesema kupitia UNDP wameweza kutafuta wataalamu hao na kuwapa kazi ya kutengeneza mfumo huo na baada ya kuutengeneza sasa wameuleta na kuwafonyesha unavyofanya kazi na kuwafundisha namna ya kuutumia maana ni mfumo ambao unabadilika hivyo unahitaji kuboreshwa.


  Kwa upande wake mratibu wa kituo cha kitaifa cha kufuatilia hewa ya kaboni kilichopo SUA Prof. Zahabu Eliakimu amesema kuwa mwanzoni wakati walipoanzsha kituo hicho cha kitaifa walikuwa wamejikita kwenye kufuatilia hewa chafu zinazosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi walikuwa wanaiangalia zaidi hewa moja ya kabondayoksidi  lakini kupitia mfumo huu watahusisha hewa zote  saba zinazohusika katika kusababisha mabariliki ya tabia nchi.

  Amezitaja hewa hizo ambazo mfumo huu utahusika katika kuzifuatilia ukiachia mbali ile ya carbondioxide ya awali ambazo zitaangaliwa katika kila sekta  kuwa ni Green house,Methane,Chlorofluorcarbon,Hydrofluorcarbon,Nitrous Oxide,Walter Vapor pamoja na Ozone.

  ‘’Tunavyoenda na kuzingalia hewa zote hizi tunabaki kuona kuwa hewa ambayo ndio inaongoza zaidi katika kuchangaia mabadiliko hayo ya tabia ya nchi kuwa ni Carbondioxide lakini hizo nyingine zinachangia kwa kiasi kidogo lakini sekta inayohusika zaidi ni sekta ya matumizi ya ardhi kwenye mistu,kilimo makazi ya watu  ndiyo kupitia madaliko hayo’’ Alisema Prof. Eliakimu.

  Kwa upande wake Mataalamu mwandamizi wa mazingira kutoka  ofisi ya makamu wa rais Bi. Adelaida Tillya amesema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwa taifa kwani utaisaidia nchi kuweka mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwakuwa sayansi imeonyesha vitu vinavyoweza kuachangia mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana nayo kama nchi na mtu mmojammoja.

  ‘’Tanzania inaonekana haichangii kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi kama ambavyo zinachangia nchi zingine, lakini ni lazima kuangalia maendeleo ya nchi kama tunapunguza au tunaongeza uzalishaji wa hewa ukaa’’ Alisema Bi. Tillya.

  Ameongeza kuwa kwa nchi zinazoendelea zimejiwekea mikakati ya kitaifa katika  kuangalia malengo ambayo nchi imejiwekea kama imefikiwa au la na kuweza kutoa ripoti kwa mamlaka husika kila baada ya miaka miwili kama unavyotutaka Mkataba wa kimataifa  tuliousaini  wa kuungana na nchi zingine duniani katika kupunguza tatizo hili.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati alipofungua kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Ndg. Nyasilu Ndulu akiwasilisha Taarifa ya Utekelzaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo, katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Bw. Fariji Mishael mtaalamu wa ufuatiliaji wa tathmini kutoka Ofisi ya TASAF Makao makuu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi hao juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi akichangia jambo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donald Magesa akichangia jambo, katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akichangia jambo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
  Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.

  ………………….

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Kaya 6120 sawa na asilimia 52 ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu zimewezeshwa kulima pamba ekari 8712 katika Msimu wa mwaka 2017/2018 kwa kutumia fedha za uhawilishaji.

  Hayo yalibainishwa na Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Bw. Nyasilu Ndulu wakati wa kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi juu ya mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.

  Nyasilu amesema pamoja na kulima pamba walengwa wa mpango huo katika Wilaya ya Bariadi na wilaya nyingine Mkoani Simiyu, kupitia fedha za uhawilishaji (wanazopewa) wamefanikiwa kujenga nyumba, kufuga, kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

  Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uhawilishaji chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu mwaka 2015 hadi sasa, tayari awamu 17 za malipo zimekwisha fanyika kwa walengwa 37, 533 na jumla ya shilingi bilioni 28.9 zimelipwa kwa wahusika.

  Amesema fedha hizo zimejumuisha ruzuku za aina mbili ikiwa ni ruzuku ya msingi na ile itokanayo na utimizaji wa mashati ya Afya na Elimu ambapo watoto 39,068 sawa na asilimia 90.3 wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule na kukuhudhuria shuleni na watoto 51, 280 sawa na asilimia 93.1 wamepata mahitaji ya kliniki na kupelekwa kliniki.

  “Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeweza kuwasaidia walengwa kujikwamua kutoka kwenye umaskini, wapo walioanzisha biashara, wanaolima, wanaofuga, waliojenga nyumba bora; kwa kutumia fedha hizi wanazopewa wapo ambao watoto walikuwa hawahudhurii shuleni na kliniki lakini sasa hivi mahudhurio mazuri” Alisema.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka awali akifungua kikao amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata walengwa, wanufaika wote waliofanya mambo ya maendeleo ni vema wakawa mfano kwa wenzao huku akiwataka wale walioshindwa kuondolewa kwenye mpango huo.

  Aidha, Mtaka aliwataka walengwa wote wa mpango kuendana na malengo ya nchi ya kuelekea kwenye Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 badala ya kuwaza kuendelea kubaki katika mpango huo.

  “Mtazamo wangu mimi ni vizuri wanufaika wa TASAF waendane na Mpango wa Nchi, tunaposema tunataka kwenda kwenye Uchumi wa Kati kufikia mwaka 2025 wanufaika wa TASAF wanapaswa kujindaa kwenda kwenye uchumi wa kati, ili badala ya watu kutaka tu kuingia kwenye mpango, tupate watu wanaotaka kutoka baada ya kupiga hatua na kutoka kwenye umaskini waliokuwa nao mwanzo” alifafanua Mtaka

  Nae Bw. Fariji Mishael mtaalamu wa ufuatiliaji wa tathmini kutoka Ofisi ya TASAF Makao makuu aliupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza mpango huo vizuri na kuomba wataalamu kuwasaidia walengwa walio kwenye maeneo yao katika kuwashauri namna bora ya kuendesha miradi waliyoianzisha ili iwe endelevu na iweze kuwasaidia kiuchumi.

  0 0


   East African Court of Justice Nairobi, 12th April 2018:   The Court Plenary which is a court’s activity that takes place twice a year commenced yesterday in Nairobi, Kenya. 

  The President of the Court, Justice Dr Emmanuel Ugirashebuja congratulated the new Judge Justice Charles Nyachae from the Republic of Kenya, upon his appointment as Judge of the First Instance Division who will replace Justice Isaac Lenaola whose term will end in June 2018.

  His Lordship, the President also congratulated Justice Dr Faustin Ntezilyayo who was designated by the EAC Heads of State in February this year, as a Deputy Principal Judge the same position that Justice Lenaola is holding. The President paid tribute to Justice Lenaola for his dedicated service for the last seven years and to his contribution to the development of the jurisprudence of the Court.

  The Plenary received reports from two Divisions of the Court headed by the President and the Principal Judge and the Registrar on the progress, achievements, challenges and new developments of the Court.

  The Plenary considered the court’s contribution in training of the bar associations in the region on the rules and procedure of the Court, such as the Rwanda Bar Association and that the rest will also be trained upon their requests. The Court further recommended to strengthen the collaboration of the Court with the Bar Associations in order to engage them as legal fraternity to support the court in raising the quality of advocacy.

  Their Lordships during the Plenary, raised and deliberated on several concerns that affect the Court’s performance, including, the Court not holding sessions as scheduled due to budgetary constraints. The Plenary also recommended to the management to look for alternative funding and proposals to the Development Partners to fund the court’s activities. 

  In terms of enhancement of capacity of the court, it was recommended that, the Court utilizes its retired judges who are familiar with the East Africa Community Laws and practices of the Court for better knowledge and skills on handling issues pertaining to interpretation of the Treaty and Protocols for the Establishment of the East African Community.

  The Judges also pointed out that, the Court needs to engage in the regional level workshops such as the East African Magistrates and Judges Association (EAMJA), and the Commonwealth Magistrates and Judges Association (CMJA) to create more awareness of the Court to various stakeholders.

  The Plenary also recommended to the management of the Court, to improve its internal communication for ease of sharing information among all Judges and staff to create a sense of knowledge on the updates and new developments of the Court.

  Another important discussion was on proposed amendments to the Treaty particularly on Chapter eight (8). Several recommendations were made on amendments of the Treaty that would enhance the work of the Court. The Plenary will officially be closed by the Cabinet Secretary, Hon Peter Munya for East African Community and Northern Corridor Developments, Kenya.

  The court Plenary followed several workshops: The Validation of the EACJ Strategic Plan for the next five (5) years 2018-2023, which will be adopted and the Court begins the implementation process, the Rules Committee meeting which reviewed and proposed amendments of the rules of procedure of the Court to ease the litigants concerns and the Training of Judges and Registrars on arbitration practices, drafting and decision making in settling disputes. All the meetings took place in Nairobi and were earlier officiated by the Chief Justice of Kenya.

  The Plenary is being attended by the Judges, Registrars and other support staff of the Court.


  0 0

  Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame akitoa maelezo kuhusiana na Mkutano na kumkaribisha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa CUF kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo katikati akifafanua baadhi ya maswala mbalimbali ya Mwenendo na Migogoro ndani ya chama hicho kwa Waandishi wa Habari Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.kulia yake ni Kiongozi wa Ulinzi wa CUF Thney Juma na Kushoto ni Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO

  0 0

  Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame akitoa maelezo kuhusiana na Mkutano na kumkaribisha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa CUF kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo katikati akifafanua baadhi ya maswala mbalimbali ya Mwenendo na Migogoro ndani ya chama hicho kwa Waandishi wa Habari Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.kulia yake ni Kiongozi wa Ulinzi wa CUF Thney Juma na Kushoto ni Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO

  0 0


  0 0

  Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja na kutatua changamoto mbalimbali. 

  Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

  Kamishna Luoga alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.
  Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (kushoto) akielezea kazi za mita za kupimia mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kulia)
  Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati mbele) Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto mbele) na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya (kulia mbele) wakiendelea na ziara katika kituo hicho.
  Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akielekeza jambo katika sehemu ya kupokea mafuta aina ya petroli na dizeli katika kituo hicho.
  Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (mbele) akimwongoza Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya pamoja na wajumbe wengine katika ziara hiyo.
  Sehemu ya gati za kupokea mafuta katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati) akionesha sehemu ya mita za kupima mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) pamoja na wajumbe wengine (hawapo pichani) katika ziara hiyo.

  0 0

  PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay makes a presentation on Irrigation Financing during SUA Agriculture & Agribusiness Conference 2018.
  Acting Managing Director for TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (centre) laments on modus operandi of the proposed Irrigation Financing during SUA Agriculture & Agribusiness Conference 2018. Others in picture are FSDT’s Head of Agriculture and Rural Finance, Mr. Mwombeki Baregu (left) and PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay (right).
  FSDT’s Head of Agriculture and Rural Finance, Mr. Mwombeki Baregu (left) contributing during the meeting. Others in picture are PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay (right) and TADB Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha (centre)..
  The trio Irrigation Financing collaborators attentively taking contributions from the floor.


  By Our Reporter – Morogoro

  Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), The Private Agricultural Sector Support Trust (PASS) and Financial Sector Deepening Trust (FSDT) are in the process to find initial fund amounting TZS 100 billion to supporting irrigation infrastructure development in the country.

  Speaking during the meeting to discuss collaboration on irrigation financing, Acting Managing Director for TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha said lending for agriculture infrastructure is a challenge in Tanzania as a result has been retrograding sector growth in the country.

  He added that this is caused due to high cost of borrowing and limited payback period for the loans associated with the limited use of irrigation.

  “A consequence of this challenging lending environment to agricultural infrastructure, which requires long-term payback period, is limited investment in agriculture productivity, particularly in irrigation infrastructure,” he said.

  On his part, PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay said that the intervention in irrigation development has verified worldwide that it boosts crop production 3-4 times than that of rain fed agriculture.

  He added that the effective irrigation also needs to be combined with increased use of farm inputs (high quality seeds, fertilizers, agrochemicals etc) to reach maximum yield increase as well as improving productivity and reduce dependence on hoe / ox plough for land cultivation.

  According to Mr. Bohay the investment will stimulate investments and promote growth of commercial agriculture and agri-businesses in Tanzania due to its capacity in boosting crop production.

  “We all know with developed/improved irrigation infrastructure and water management, paddy yields on an average can increase from 1.8 tones per hectare to 5 tones per hectare,” Mr. Bohay said.

  Contributing during the meeting, FSDT’s Head of Agriculture and Rural Finance, Mr. Mwombeki Baregu mentioned that the need to have in place strong irrigation financing is associated with efforts made by the National Irrigation Commission and 2030 Water RG to assist the financial sector to develop a solution to financing the investment needs in agriculture infrastructure, particularly irrigation infrastructure.

  He added that the partnership facilitated studies on the demand for irrigation financing in Tanzania, engaged partners on the possible solutions, and developed a model that would be able to support a solution.

  According to Mr. Baregu this model will be implemented by TADB and PASS.

  Noting FSDT’s role, Mr. Baregu said, “FSDT seeks to facilitate “more and better financial services” to where a vast majority of Tanzanians are employed and located. This includes diagnosis of the barriers to agriculture and rural finance transactions and working with a broad range of partners to implement interventions that address the constraints and unlock access, usage, quality, and welfare of financial services.”

  History shows the modern irrigation was introduced in Tanganyika in 1930 through the establishment of the Tanganyika Planting Company Ltd and other commercial farms and estates. Since Independence a large potential for irrigation has been identified, partly as commercial irrigation schemes, partly for smallholders organized in water users associations.

  Only part of that potential has so far been realized. According to National irrigation Policy 2009 Tanzania has the identified irrigation potential area of 29.4 million hectares for sustainable irrigation development, of which 2.3 million ha are classified as high potential; 4.8 million ha as medium potential; and 22.3 million ha as low potential. Out of 2.3 million ha with high potential for irrigation development, only 461,326 hectares (1.6%) has been put under irrigation.

  0 0  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiasa jamii nchini kujiepusha  na migogoro kwa vile haina tija  na badala yake idumishe amani, upendo na uadilifu ili kumuezi mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu  Alhaj Ali Mtopa.

  Aliyasema hayo jana (Jumatano, Aprili 11, 2018) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika katika kijijini Nanjilinji wilayani Kilwa. Alhaji Mtopa alifariki Jumatatu Aprili 9 jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu alisema haitapendeza kusikia jamii, wanafamilia, watendaji au wanasiasa waliokuzwa au kufunzwa na marehemu Alhaj Mtopa wakifarakana  kwa sababu yoyote ile kwani  siku zote marehemu alikuwa kiongozi aliyejitahidi sana kuwawaunganisha watu na mpenda amani.

  “Tumepoteza kiongozi maarufu mwenye historia pana, amekuwa mtumishi ndani chama (CCM) na Serikali kwa muda mrefu. Alikuwa kiongozi mwema muadilifu, mtiifu na mchapakazi kwa miaka mingi”.“Marehemu Alhaj Mtopa hakua mbaguzi kwenye kuielimisha jamii namna ya kuendesha siasaza kistaarabu. Kifo chake kinatuacha na huzuni, kazi yetu kubwa ni kumuombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuilaza roho yake mahali pema”. Alisistiza Mheshimiwa Majaliwa.

  Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafamilia kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na baba ambaye alikuwa nguzo ya familia na jamii. Hivyo aliwaomba kutoruhusu mgawanyiko wa aina yoyote baina yao.“Katika kipindi hiki kigumu ambacho tumeondokewa na mzee wetu na mwalimu wetu wa siasa na uongozi wetu nawasihi sana wanafamilia kuwa watulivu kwani haitapendeza kusikia kuwa kuna mgogoro au mgawanyiko kati yenu”.

  Alisema yeye binafsi amepata msaada mkubwa kutoka kwa maremu Alhaj Mtopa katika masuala ya siasa na kijamii  kwa vile  mara nyingi akiwa katika ziara zake mkoani Lindi na katika jimbo lake la Ruangwa aliambatana na marehemu na kwa pamoja walishirikiana kutatua kero na kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
    
  Mbali na Waziri Mkuu viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo, ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mbunge wa Mtama, Napa Nnauye na  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

  Wengine ni Mke wa Rais wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Kuteuliwa Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na Pamoja na Waziri wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mbunge wa Kilwa Kusini,Selemani Ally Bungara na Mbunge mstaafu wa Mtama, Benard Membe.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.
  ALHAMISI, APRILI 12, 2018.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipowasili  kushiriki mazishi ya Mwanasiasa na Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waombolezaji wakishiriki katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM wa mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa kwenye kijiji cha Nanjilinji wialyani Kilwa Aprili 11, 20918. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj, Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Apili 11, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki katika sala ya kumwombea Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Lindi,   Alhaj Ali Mtopa wakati aposhiriki katika mazishi  ya Mwansiasa huyo yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nanjilinji  wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akishiriki katika mazishi ya Mwanasiasa na Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0


  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza majina ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Ramadhani Juma ,Ofisi ya Mkurugenzi

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma kupitia Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu imeendelea kuimarisha miundombinu ya usafi kwa kuongeza vifaa vya kutunza uchafu katika mitaa kadhaa ya Mji ili kuhakikisha Wananchi hawatupi taka ovyo.

  Akizungumza wakati wa uwekji wa vifaa hivyo, Mkuu wa Idara hiyo Dickson Kimaro alisema Manispaa inatarajia kuongeza ‘vitunza uchafu’ 11 katika mitaa mbalimbali ili kuweka mazingira rafiki ya kutunza uchafu kwa Wakazi wa Mji wanaokuwa katika shughuli zao za kila siku.

  “Hizi ni juhudi za makusudi ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa safi muda wote…natoa wito kwa Wakazi wa Manispaa yetu watumie vifaa hivi kuhifadhia uchafu mdogo wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku” alisema Kimaro.

  Alisema mbali na vifaa hivyo, tayari Manispaa ilishasambaza vifaa vikubwa vya kukusanyia taka za aina zote (Skip Bucket) 61 katika Kata mbalimbali zinazotumika kama vituo vya kukusanyia taka kabla ya kubebwa na Mitambo ya Manispaa na kupelekwa katika Dampo la Kisasa lililopo eneo la Chidaya Kata ya Matumbulu nje kidogo ya Mji.  Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu wa Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro akikagua moja ya vifaa vipya vilivyowekwa katika Mtaa wa Kuu kwa ajili kutunza uchafu ikiwa ni juhudi za Manispaa hiyo kuhakikisha Mji unakuwa safi wakati wote.

  Moja ya vifaa vya kutunzia taka (kulia) kilichopo mkabala na Viwanja vya Nyerere katikati ya Mji wa Dodoma

  0 0

  Na Baltazar Mashaka, Mwanza

  Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Bwiru la jijini Mwanza limemtunuku cheti Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibtain Meghjee kwa kutambua huduma za jamii zinazotolewa na taasisi hiyo katika sekta za afya,elimu na maji bila kujali itikadi za dini wala kubagua.

  Akizungumza kabla ya hafla hiyo Mchungaji Ephafra Zabron alisema taasisi ya TD & CF imefanya mambo mengi muhimu ya kusaidia jamii kwa kuhudumia watu wa dini na madhehebu mbalimbali bila ubaguzi katika masuala ya afya, elimu na maji lakini pia imejenga shule, nyumba za ibada (misikiti na makanisa) na kuchimba visima.

  “Tusipotoshwe na watu kuwa watu wa dini ya Kiislamu wana mitizamo tofauti na wapo watu wanapotosha na kuleta lugha za kufarakanisha watu kuwa ukimwona Muislamu ni adui yako si kweli.Waislamu wanatuzidi mambo mengi na wanatimiza maandiko kwa vitendo ambapo kila Ijumaa wanatoa misaada kwa jamii ya wahitaji,” alisema Mchungaji Ephafra. 

  Mchungaji huyo alieleza kuwa Kanisa la AICT Bwiru linatambua mchango mkubwa wa Sibtain Meghjee na taasisi yake kwa jamii kwani anafanya huduma aliyoifanya Yesu na kuwataka waumini wa kanisa hilo na wakazi wa eneo la Bwiru wajifunze kutokana na kazi zinazofanywa na The Desk & Chair.

  Akisoma risala ya kanisa hilo Paulo Sweya alisema kanisa hilo linatoa huduma za kiroho na kijamii kwa waumini na watu mbalimbali kulingana na mahitaji ya jamii inayowazunguka hasa wazee wasiojiweza, wajane, yatima, walemavu na wagonjwa bila kujali itikadi wala kabila lakini pia limendelea na huduma kuu ya kueneza neno la Mungu kwa jamii ya watanzania wote ili kudumisha amani na upendo bila kujali itikadi za dini.

  Aliongeza kuwa ili kumudu kuwahudumia wahitaji hao kanisa limebuni miradi mbalimbali ili kuweza kumudu kuwahudumia lakini kutokana na ukosefu wa fedha wameshindwa kuikamilisha na hivyo kutoa huduma duni zisizofikia kiwango cha ubora unaokusudiwa. 

  Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ukumbi wa mikutano na ufukwe, shule ya awali na huduma ya chakula kwa ajili ya kujiongezea kipato, kisima na matanki ya kuhifadhia maji, choo, mitambo ya umeme jua,nyumba ya mchungaji, ofisi za viongozi wa kanisa na usafiri, ili miradi hiyo ikamilike inahitaji kiasi cha shilingi milioni 28.5.

  “Ndugu Mgeni rasmi kuja kwako hapa kumetuthibitishia kuwa ni mtu wa pekee, mwenye moyo wa upendo, msikivu unayejali wahitaji katika jamiii mbalimbali na tumejifunza kwako somo la upendo pasipo ubaguzi wa aina yoyote na hivyo wewe ni mfano wa kuigwa kwenye jamii na tunamwomba Mungu akupe afya njema uendelee kumtumikia.Pia jamii iendelee kujifunza kwako na matendo yako mema yawe somo kwa jamii ujio wako ni fundisho kwa wote wanaomwabudu Mungu aliyewaumba,”alisema Sweya.

  Akijibu risala hiyo baada ya kutunukiwa cheti sambamba na Mkurugenzi wa Nitetee Foundation Meghjee aliahidi kusaidia ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo inayotekelezwa na Kanisa hilo la AICT Bwiru.

  “Sisi kama waislamu na taasisi ya The Desk & Chair Foundation tunashukuru kwa kutualika na kutushirikisha kwenye ibada na shughuli zenu za maendeleo.Tunaahidi kusaidia ujenzi wa miradi yenu na tutaana na hili la maji tutaanza nalo mara moja lakini misaada tutakayoitoa lazima ifanye kazi iliyokusudiwa,”alisema.
  Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja kutokana na kutambua mvhango wa taasisi hiyo wa kusaidia jamii.Hafla iliyofanyika kanisani hapo Jumalipili iliyopita.
  Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja (kushoto),akipokea kitabu cha Kuran tukufu kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee. Anayeshuhudia kushoto wa kwanza ni Mchungaji wa Kanisa la Bwiru, Ephafra zabron na kulia ni Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya ziwa Hashimu Ramadhan.
  Picha na Baltazar Mashaka
  ……………….

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

  HALMASHAURI 182 nchini ikiwemo saba za mkoani Pwani ,zinadaiwa kutumia vibaya mabilioni ya fedha yaliyotumika kuondoa zaidi ya lita 100,000 za dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech Products Limited,kilichopo Mji Wa Kibaha ,ikiwa ni agizo alilolitoa Rais Dkt.John Magufuli June 22 mwaka jana.

  Aidha halmashauri ambazo zinadaiwa kiasi cha sh.bil.1.8 walizochukulia dawa hiyo zimetakiwa kulipa fedha hiyo haraka ili kiwanda kiweze kujiendesha na kulipa watumishi wake mishahara.

  Akizungumza katika ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa ya viuadudu inayozalishwa katika kiwanda hicho ,meneja wa udhibiti wa ubora na viwango kiwandani hapo , Samwel Mziray , alisema ni halmashauri mbili pekee zilizochukua dawa hiyo kwa awamu ya pili.

  Alieleza halmashauri 184 zilichukua dawa kwa awamu ya kwanza na ya pili zaidi ya lita 200,000 ambazo wameziweka stoo bila kuzitumia wakidai hawana fedha ya kununulia pampu."Wanashindwa kuzitumia kutokana na kukosa pampu ya kupulizia ,hii ni aibu ,nimesikitishwa sana na hali hii, "

  "Ni ngumu na jambo la ajabu leo hii Rais atoke kuja kufuatilia agizo lake ama kuzifuatilia halmashauri hizo, serikali ina nia njema lakini watendaji tunashusha juhudi za Rais na serikali ""Ninawaomba wakuu wa mikoa mingine nchini kuiga mfano wa mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ya kuhamasisha kununua dawa hizo, ili kupambana na vita dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria." alieleza Mziray .

  Mziray alieleza baada ya agizo la Rais walianza na mikoa 14 katika halmashauri 96 na awamu ya pili waligawa kwenye halmashauri za mikoa 12 na kutimiza mikoa 26 na halmashauri 184 nchini .Hata hivyo baada ya mgao wa kwanza halmashauri ya Rufiji iliongeza Lita 540 na Kibaha Vijijini waliongeza lita 520 .

  Mziray alifafanua nchi ya Niger wameshawaunga mkono Kwa kununua dawa hiyo pamoja na Angola ambayo imeagiza lita 106,020 lakini cha kustaajabisha Tanzania na Kibaha Mjini bado hawajatambua umuhimu huo.Aliwataka wakurugenzi wa halmashauri na jamii kujitokeza kununua dawa ya viuadudu ili kuondokana na vifo vinavyotokana na malaria.

  Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alikitaka kiwanda hicho kijitangaze katika vyombo mbalimbali vya habari na kutoa elimu kwa jamii kuwa madawa hayo hayana madhara kwa matumizi ya binadamu .Alisema biashara bila matangazo haijiuzi hivyo ni wakati wa kujitangaza ili hali kuinua soko na kutambulika.

  Pia Ndikilo alieleza halmashauri zilizofungia dawa hizo ni aibu "sijui tumelongwa nini,malaria ipo dawa ipo hatununui ,hivi tunasubiri Rais aje tena atununulie tena dawa ,haiwezekani"

  "Nchi imetumia dollar milioni 22 ,wafanyakazi 127 wanakosa mishahara yao pale kiwandani,leo halmashauri hazioni hili ????ni lazima watumie dawa hizi na kupata matokeo" alisisitiza Ndikilo.

  Mkuu huyo wa mkoa alikemea tabia hiyo na kuwataka wachukue dawa na kuchukua nyingine pasipo kufungia stoo na kudai atakaerudia makosa aondoke kwenye nafasi yake mara moja.Ndikilo alisema hatomvumilia mkurugenzi anachezea mamilioni ya fedha wanayotenga kwa ajili ya kupambana na malaria ,na atakaejiona hatoshi aanze kuondoka katika nayadhifa yake kupisha wengine.

  Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, Yudas Ndungile ,alisema idara ya afya mkoa inahimiza matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu.

  Alibainisha ,mwaka 2017 vyandarua 59,494 viligawiwa mashuleni pia vyandarua 48,120 viligawiwa kwenye kliniki na mwaka 2016 vyandarua 877,297 viligawiwa katika ngazi ya kaya na familia .

  Ndungile alielezea wanakabiliana na malaria na kutoa elimu ya usafishaji wa mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu kwenye madimbwi ,suala lililosaidia vifo vinavyotokana na malaria kupungua na malaria kushuka kuwa ugonjwa wa pili kati ya magonjwa yanayoongoza kimkoa.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo alisema wameitikia wito uliotolewa na mkuu wa mkoa na wanakwenda kuagiza lita 720 ili kuua mazalia ya mbu wa malaria.

  Omolo alisema kuwa awali walichukua lita 520 ambazo walizitumia ,na wanaahidi kutoweka stoo . 
   Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (wa kulia) ,akimkabidhi dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze ,Edes Lukoa wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo ,Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
   Meneja wa udhibiti wa ubora na viwango katika kiwanda kinachozalisha dawa ya viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Mjini Kibaha akionyesha wananchi kuwa dawa hiyo haina madhara, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  Serikali itadumisha ushirikiano na sekta binafsi katika kutafuta fursa za kibiashara katika soko la pamoja la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani ili kujenga uchumi.
  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati akipokea michango ya wadau toka sekta binafsi kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya.
  "Ninawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na kuonyesha uthubutu wa kuingia katika soko la Kenya, ninyi ni mabalozi wa wafanyabiashara wengine katika kutafuta fursa za kibiashara nje ya Tanzania"alisema Balozi Mahiga.
  Balozi Mahiga alisema Tanzania inazobidhaa nyingi za viwanda ambazo nchi nyingine hawazijui bidhaa hizo, hivyo kinachofanywa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali jambo la kijivunia.
  Aidha, Balozi Mahiga alisema kuwa kufanya biashara nje ya nchi kunaimarisha uhusiano wa kisiasa baina ya Serikali ya Tanzania na nchi nyingine na kukuza diplomasia ya uchumi.Aliongeza kuwa hii ni fursa kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao ni msisitizo na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.
  Waliotoa michango yao ni Kampuni ya Konyagi ambao wamechangia shilingi milioni 11, Mohamed Enterprises, Shilingi milioni 25 na NIDA TEXTILE MILLS (T) LTD imetoa hundi ya shilingi milioni 22.
  Balozi Mahiga amewaomba wafanyabiashara wengine wajitokeze kuchangia na kushiriki katika fursa hiyo ya kutafuta masoko nje ya nchi hususan Kenya ambapo bidhaa za Tanzania zitaoneshwa huko kuanzia tarehe 25 hadi 28, Aprili, 2018.
  Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Rehema Mtingwa, amesema sekta binafsi iko tayari kushirikiana na Serikali katika kufanikisha upatikanaji wa fursa za kibiashara nchini Kenya na sehemu nyingine.
  Hii ni mara ya pili kwa wadau toka sekta binafsi kuchangia maandalizi hayo, kundi la kwanza ambalo lilijumuisha KNAUF Company LTD, IPP Media, Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Bravo Logistics na Lake Oil Company Limited, liliwasilisha michango yake juma lililopita.

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya jamii

  MKUU wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier ambapo kwa sehemu kubwa mazungumzo yao yamejikita kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika mapema jumatatu wiki ijayo.

  Akizungumza leo jijini Dar es salaam Makonda amemshukuru balozi na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.Kuhusu kongamano hilo Makonda amesema siku ya Jumatatu Kampuni 30 kutoka Ufaransa yatawasili nchini na kufanya mkutano wenye malengo ya kuufanya mji wa Dar es salaam kuwa kama miji mingine duniani katika masuala ya maji, afya, usafiri na masuala mengine ya kiteknolojia.

  Aidha ameeleza kampuni hizo zitaangalia fursa na vipaumbele vya Serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Jiji la Dar es salaam kuja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka ufarasa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.

  Kwa upande wa Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier amefurahi na kumshukuru Mkuu ya Mkoa Dar na kueleza kuwa Dar es Salaam  ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sambamba na dhamira ya Rais Dk.John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.Aidha amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizi mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.

  Kuhusu mchakato wa kusaidia watoto waliotelekezwa Makonda amewashukuru wanahabari kwa kuwa sehemu ya wapatanishi wa familia hizo aidha amewataka wananchi kuja kupata huduma katika viwanja vya ofisi yake na si katika simu na mitandao na amefafanua hadi sasa familia 178 wameelewana na kukubaliana kupeana fedha za matunzo na zaidi ya watu 1498 wameshapatiwa huduma.

  "Na Jumatatu wataitwa baba wa familia hizo licha ya baadhi yao kuanza kuripoti na ameeleza kuwa walio tayari kupima DNA wajitokeze watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya mdau moja kutoka Afrika Kusini ambaye ameahidi kuwasaidia watoto waliotelekezwa Toto Afya Card. (Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akiwa katika banda la Mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya (NHIF) akiangalia namna uandikishaji wa Toto Afya Card ukiendelea leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na jukumu la kuwasaidia wanawake ambao wamezalishwa watoto na kisha kutelekezwa na waume zao huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Sh.milioni 250 ndizo zitakazotumika katika kuwakatia bima ya afya watoto zaidi ya 1500 waliotelekezwa.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya umati mkubwa wa akina mama ambao wamefika ofisini kwake kupata msaada huo baada ya kuutangaza kuwasaidia wanawake wa mkoa wake ambao wametelekezwa, amesema anashukuru wadau mbalimbali wameendelea kujitokza na kusaidia watoto hao.

  Amefafanua kuwa katika suala la bima ya afya kwa watoto hao ni kwamba jumla ya Sh.milioni 250 zinatarajia kutumika kwa ajili ya kuwakatia bima hiyo ya afya ambayo itawezesha kupata tiba.

  "Kuna mdau mmoja kutoka Afrika Kusini ameahidi kuwasaidia watoto hao katika suala la afya hasa katika kupata bima ya afya na tayari mchakato huo umeanza leo hii na mdau huyo ameahidi kusaidia watoto zaidi ya 1500 ambao watagharimu kiasi hicho cha fedha,"amesema Makonda.

  Kuhusu sifa za watoto watakaopatiwa bima za afya bure ambayo ni ya mwaka mmoja,Makonda amesema lazima mtoto awe ametelekezwa, awe raia wa Tanzania na awe na umri usiozidi miaka 18.

  Kwa upande wa Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Wilaya ya Kinondoni Magreth Malangila ameeleza ili kukamilisha mchakato huo wazazi waje na picha (pasport) ya rangi ya bluu na cheti cha kuzaliwa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke, Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa nikuagana na Mheshimiwa Makamu wa Rais ambaye atamuakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM) utakao fanyika mjini London kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 20 Aprili mwaka huu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo  ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana  na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke (kulia) pamoja na Mkuu wa Masuala ya Kijamii na Siasa  Bw. Marc Thayre ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS uliofanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki na Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia).
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akihutubia baraza hilo.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akihutubia baraza hilo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania waliohitimu mafunzo ya Jeshi Usu hivi karibuni wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala huyo uliofanyika leo mjini Dodoma. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki muda mfupi baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo. 

older | 1 | .... | 1559 | 1560 | (Page 1561) | 1562 | 1563 | .... | 1896 | newer