Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live

MAAFISA UGANI WAKABIDHIWA PIKI PIKI GEITA TC

$
0
0
Na Joel Maduka,Geita.

Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa pikipiki nne(4) kwa Maafisa kilimo wa Kata ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuwatembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na wakulima katika maeneo yao.

Akikabidhi pikipiki hizo,mapema leo katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Halmashauri hiyo kupitia viongozi wake kwa kuona umuhimu wa kununua pikipiki hizo ili ziweze kuwasaidia wataalam wa kilimo kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kutoa huduma za ugani kwa wakulima.

Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka Maafisa ugani waliopatiwa pikipiki hizo wafanye kazi zao kwa weledi mkubwa katika kuwafikia wakulima wengi zaidi na kutoa huduma stahiki na tahmini ya kina ifanyike juu ya ufanisi wa Maafisa ugani wote wenye vyombo vua usafiri.

Mhandisi Robert Gabriel amefafanua kuwa Mkoa wa Geita umejipanga kuanzisha kilimo cha korosho ili kuongeza mazao ya biashara, hivyo ujio wa pikipiki hizo utasaidia sana kutembea na kubaini maeneo mbalimbali yanayofaa kwa kilimo cha zao la korosho.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ametumia fursa hiyo kuziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Geita kuiga mfano thabiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kufikisha lengo la asilimia 100 kwa kuwawezesha Maafisa Ugani wote nyenzo za usafiri ili wakasimamie shughuli za kilimo. Pia watenge asilimia 10 ya mapato yatokanayo na ushuru wa mauzo ya pamba ili fedha hizo zisaidie kutoa huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kununua pikipiki.

Kwa upande wao Maafisa Ugani wa Kata za Bung’wangoko na Mtakuja, Ndg. Allan Kisomeko na Jackline Otieno kwa niaba ya wenzao wameishukuru Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kuwapatia vyombo vya usafiri vitakavyowawezesha kufanya kazi kurahisi na kuwafikia wakulima wengi kwa muda mfupi, tofauti na awali walipokuwa wakitembea kwa miguu au kutumia usafiri wa baiskeli kuwafuata wakulia katika maeneo yao ndani ya Kata wanazozihudumia.

Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa pikipiki nne aina ya Honda ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi bilioni kumi na mbili na laki nane(12,800,000/= )kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Kassimu Majaliwa alipofanya kikao na Wakuu wa Mikoa kumi inayozalisha zao la pamba nchini mwezi Septemba 2017 mjini Dodoma, ambapo aliziagiza Halmashauri zote katika Mikoa hiyo kununua pikipiki kwa ajili ya Maafisa ugani wao ili waweze kuwafikia wakulima wengi kwa muda mfupi.
Halmashauri ya Mji Geita yatoa pikipiki 4 aina ya Honda zenye thamani ya Tsh. 12,800,000 kwa Maafisa ugani wa kata za Bung'wangoko, Kanyala,Nyanguku na Mtakuja. Pichani ni Bi. Jackline Otieno, Afisa Ugani wa kata ya Mtakuja akifurahi kukabidhiwa pikipiki na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel leo tarehe 5 aprili katika ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Geita. Halmashauri imefikia lengo la asilimia 100% kwa kuwawezesha Maafisa ugani wa kata zote 13 kupata pikipiki 

RAIS DKT. MAGUFULI AELEKEA MKOANI MANYARA Leo

$
0
0
Picha zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Marubani wa Ndege ya abiria ya ATCL wakati akielekea kupanda ndege hiyo kuelekea mkoani Kilimanjaro na badae mkoani Manyara kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kitaifa mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ndege hiyo ya abiria ya Shirika la Ndege la ATCL kuelekea mkoani Kilimanjaro na baadae mkoani Manyara.

PICHA NA IKULU

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA KILA KIJIJI KUTENGA ENEO LA UHIFADHI WA MISITU, ATOA SIKU 7 KWA TFS KUWASILISHA MPANGO WA UVUNAJI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Na Hamza Temba, WMU, Kishapu, Shinyanga
.......................................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga maeneo katika kila kijiji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ikiwa ni pamoja na vijiji hivyo kuunda kanuni na taratibu zao wenyewe za kusimamia maeneo hayo. 

Ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika mkoani humo kuanzia Aprili 03 mwaka huu.

Katika kufanikisha zoezi hilo ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuchagua mikoa 10 ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo ikiwemo mikoa ya Shinyanga na Tabora ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu.

Ameugiza pia we uongozi huo wa TFS kuweka mpango wa uhifadhi wa misitu ya asili katika maeneo hayo kwa kushirikiana na vijiji kupanga maeneo yanayostahili kuhifadhiwa sambamba na kuwapa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa maeneo hayo.

Wakati huo huo Dk. Kigwangalla ametoa siku saba kwa uongozi huo wa Wakala wa Huduma za Misitu kuwasilisha kwake mpango wa tathmini ya uvunaji wa mazao ya misitu wa nchi nzima kwa kuzingatia kiasi cha rasilimali misitu kilichopo na kiwango halisi kitakachotakiwa kuvunwa ambacho hakitazidi robo ya rasilimali iliyopo.

"Hatuwezi kuendelea tu kutoa vibali vya kuvuna misitu hatujui tunavuna wapi, tuna rasilimali kiasi gani, wavune kiasi gani, hapana, mnitengenezee mpango laa sivyo nitasitisha uvunaji, nikisema nasitisha uvunaji nitapeleka waraka kwa Wakuu wa Mikoa, na nina uhakika kwa nguvu walinayo hawashindwi kuzuia uvunaji. 

"Kwahiyo TFS nawapa siku saba mniletee mpango wa tathmini ya namna ambavyo tuna rasilimali kwenye kila mkoa, tujue mkoa flani una miti cubic mita kadhaa ya mbao kadhaa, ya kuni kadhaa, ya mkaa kadhaa na kwa mwaka huu tutaruhusu wavune kwenye msitu fulani  kiasi kadhaa, twende kisayansi, sio Meneja wa TFS anakaa Wilayani anatoa vibali watu wanaenda kuvuna,".

Dk. Kigwangalla amesema  takwimu za uharibifu wa misitu hapa nchini zinatisha jambo ambalo likiachwa liendelee bila kuchukua hatua nchi itageuka kuwa jangwa.

"Kwa mwaka tunakata miti kwa mahitaji mbalimbali kati ya ekari 800,000 na 1,200,000.
Ili kurejesha walau nusu ya miti tunayokata kwa mwaka tunahitaji kupanda miti 3,000,000 kwa mwaka mfululizo kwa miaka 17 ili kufidia kiasi cha uharibifu tunachofanya kwa nusu mwaka" alisema Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ezekiel Mwakalukwa ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alisema kumekuwepo na jitihada za kuandaa programu kubwa za kitaifa za uhifadhi wa mazingira katika maeneo mahususi yaliyoonekana kuzidiwa na tatizo la uharibifu wa mazingira. 

Alitaja Programu hizo kuwa ni Hifadhi Ardhi Dodoma (HADO), Hifadhi Ardhi Shinyanga (HASHI), na Hifadhi Mazingira Iringa (HIMA).

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alisema mkoa wake kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Tabora umeanza kuchukua hatua za kurejesha uoto wa asili katika maeneo yao ikiwemo kuanzisha utaratibu wa kugawa miche ya miti kwa kila kaya pamoja na kuimarisha kamati za uhifadhi wa mazingira.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Taboba, Aggrey Mwanri alisema ushirikiano huo ni muhimu kwani utawezesha kukabiliana na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo kwa kuweka mikakati ya pamoja wa kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiteta jambo wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiwasalimu wananchi wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
  Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ezekiel Mwakalukwa ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa maelezo kuhusu maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakielekea eneo la tukio la kupanda miti wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki kucheza ngoma wakati wa maadhimisho hayo.

TAFITI ZINAONESHA NI MUHIMU KUWEKEZA KATIKA UFUNDI STADI KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA-DKT MMARI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya REPOA Dk.Donald Mmari amesema kuna sababu ya kuwekeza zaidi katika kutoa elimu ya ufundi stadi nchini kwa lengo la kupika watalaamu wa fani mbalimbali ambao watashiriki kufanya kazi zenye tija na kuleta ushindani kimataifa.

Dk.Mmari ametoa kauli hiyo wakati akielezea changamoto ambazo wamezibaini kwenye warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na REPOA kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Amesema wadau walioko kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina mambo mengi kwa maslahi mapana ya nchi yetu na katika mjadala huo wamebaini bado kunachangamoto ambazo ni vema zikafanyiwa kazi ili kufikia malengo ya ujenzi wa viwanda na kuwa na bidhaa zenye ushindani katika soko la kimataifa.

Ametaja moja ya changamoto ambao wameijadili ni uhaba wa wataalam katika nyanja mbalimbali na hiyo inatokana na kutowekeza zaidi kwenye elimu ya Ufundi stadi ambayo inaandaa vijana kujiajiri na kuwa watalaamu wazuri."Tumekubaliana na kutoa mapendekezo kuwa ili tuingie kwenye ushindani ipo haja ya kuhakikisha watanzania wanaalindaliwa katika elimu na ujuzi unaohusu masuala ya ufundi.

"Ni vema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta za umma na binafsi kuwekeza zaidi katika kuwajengea uwezo wananchi ambao utawafanya washiriki kikamilifu katika kufanya kazi kwenye viwanda,"amesema Dk.Mmari.Amefafanua nchi nyingi ambazo zimeendelea na zenye uwezo wa kuhimili ushindani kwenye soko la kimataifa msingi wake mkubwa wamewekeza katika elimu, ujuzi na utalaam.

"Hivyo ili kushindana nao lazima Tanzania nayo ikawekeza katika elimu, ujuzi na utaalamu kwa kuandaaa vijana watakaokuwa na ujuzi.Tumekubaliana yale ambayo tumeyaona kama changamato tumeweka na mapendekezo yetu na tumekubaliana Serikali iyapate na ikiwezekana kuyafanyia kazi,"amesem Dk.Mmari.

Amesisitiza ni vema nchi ikawekeza zaidi kwenye kujenga vyuo vya VETA ambavyo jukumu litakuwa kuandaa watalaam na kwamba kuna wakati iliingia kasumba ya kuwa na vyuo vikuu vingi ili wanaohitimu wawe na Shahada lakini elimu hiyo haina ujuzi na matokeo yake kunaibuka changamoto ya uhaba wa watalaamu.

Kwa upande wa Mlkuregenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural 
Asspciation (TAHA) Jacqueline Mkindi amesema pamoja na kujadili mambo mengi kwenye warsha hiyo wamegundua ujuzi kwenye maeneo ya viwandani bado tatizo kubwa.Amesema ipo haja ya kuhakikisha wanaandaliwa watalaamu wenye ujuzi unaokubalika kimataifa kwa lengo la kuwa na bidhaa zenye ushindani na kufafanua jukumu ambalo TAHA wanafanya ni kuwaandaa vijana kujiajiri kwa kuwapatia mafunzo yenye ujuzi.

"TAHA tumebaini kuna tatizo la uhaba wa watalaam, kwa mfano kwetu inapofika kipindi cha kuchanganya mbegu maabara lazima utakuta wanaofanya kazi hiyo ni watalaamu kutoka nje."Sababu kubwa ni kwamba kwetu hawapo.Hivyo wakati nchi inajipanga kwenye ujenzi wa viwanda ni vema ikaenda sambamba na kuandaa watalaam ili kuondoa changamoto iliyopo,"amesema Mkindi.

Ameongeza cha msingi ni kuweka uratibu mzuri utakaosaidia vijana kuwajengea uwezo utakaosadia kuondoa changamoto ya uhaba wa watalaamu katika fani mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini, REPOA, Dk. Donald Mmari akizungumza wakati wa kufunga Warsha ya siku mbili kwa watafiti iliyoandaliwa na tasisi yake juu ya kwanini ushindani ni muhimu kuelekea uchumi wa Viwanda.
Mlkuregenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Asspciation (TAHA) Jacqueline Mkindi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo walipjadili nafasi ya kilimo katika uchumi wa Viwanda.
Mratibu na Mtafiti wa Warsha hiyo kutoka Repoa, Dk. Blandina Kilama akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo wakati alipokuwa akiongoza meza ya majadiliano.
Mtafiti Kutoka Repoa, Dk. Lucas Katera akizungumza jambo kaatika mjadala wa Nishati kuelekea Uchumi wa Viwanda wakati wa Warsha ya siku Mbili ya Watafiti iliyoandaliwa na Repoa.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya siku mbili kwa watafiti juu ya kwanini ushindani ni Muhimu kuelekea Uchumi wa Viwanda wakifatilia mada kwa makini.

Makazi ya Jebel Sifah nchini Oman ni fursa za kiuchumi kwa watu wote

$
0
0

Balozi Mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini wa nne kutoka kulia akiwa amesimama baada ya kumaliza kuzungumza kwenye maonyesho ya makazi ya Oman Visiwani Zanzibar yakiandaliwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman. Maonyesho hayo yamefanyika katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar. Wengine ni wadau wa ardhi na makazi waliohudhuria kwenye maonyesho hayo. Picha na Mpiga picha wetu.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HUKU maonyesho ya makazi ya Jebel Sifah yanayoonyeshwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman yakiendelea visiwani Zanzibar katika Hotel ya The Park Hyatt, baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara wa visiwani hapa wametakiwa kupanua wigo wao wa kibiashara kwa kununua makazi yao nchini Oman ili wajiwekee vitega uchumi kwa ajili ya maendeleo yao.

Ushauri huo umetolewa leo na Meneja Mauzo wa Muriya, Ghizlane El Gouchi, wakati wa kuelimisha wakazi na wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji kazi wao katika sekta ya ardhi na makazi waliyojikita nchini Oman, huku wakijivunia maendeleo makubwa kwenye sekta hiyo muhimu dunian kote.

Wadau wa ardhi na makazi nchini Tanzania, Ali Al Maskary kulia na Aflah Al Maskary kushoto wakifuatilia jambo na mdau wa ardhi kutoka Oman, Faisal Said Rashid Alzakwani katika maonyesho ya makazi yanayoendeshwa na kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman kwa ajili ya kununua makazi nchini humo. Tukio hilo linafanyika leo Aprili 6, katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni.
Faisal Said Rashid Alzakwani kushoto akipiga picha na aalozi mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini.
Alisema kwamba ni vyema Watanzania wote wakiwamo wafanyabiashara wakaelewa umuhimu wa kujitanua kibiashara kwa kuangalia uanIshwaji wa biashara nje ya mipaka yao, huku Kampuni yao ikifungua milango kwa kuwauzia makazi kwa utaratibu mzuri na rahisi katika maeneo yenye solo kama vile pembeni mwa bahari ambako wanaweza kuyatumia kama fursa za kiuchumi bila kusahau hati ya kuishi nchini Oman.

Muriya ni kampuni kubwa iliyojikita katika utoaji wa huduma za makazi na utalii nchini Oman, ambao kwa wiki moja sasa wanaendelea na maonyesho yao ya kibiashara wakianzia jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar kama njia ya kubadilishana mawazo na kuwajulisha Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla juu ya biashara zao.

“Umuhimu wa biashara ni kupanuka kutoka eneo dogo kwenda eneo kubwa, hivyo ni lazima wadau wa Zanzibar kutafuta fursa nyingine hususan za kuwekeza nchini Oman katika eneo la makazi ambayo tutawauzia na wao watalipa kwa awamu ndani ya kipindi cha miaka miwili, tukiamini kuwa kwa wale wenye malengo wanaweza kufanikiwa, ambapo asilimia 10 zitalipwa baada ya kujisajili, huku gharama zetu zikianzia Dola 98,000 tu,"Alisema.

Kwa mujibu wa El Gouchi, mradi wao wa Jebel Sifah ni mwendo wa dakika 40 tu kutoka Muscat, karibu na ufukweni ambayo yana ukubwa hadi wa square meter 365,000, ukiwa ni mradi mkubwa unaowahusu Watanzania wote na ni fursa nzuri za uwekezaji.

Maonyesho hayo ya kibiashara ya makazi yanayouzwa na Kampuni ya Muriya, yamefanyika jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa tangu Aprili 3 hadi 5, ambapo kwa wakazi wa Zanzibar wenyewe wamefanikiwa kufikiwa na maonyesho hayo jana Aprili 6 katika Hoteli ya The Park Hyatt kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na elimu juu ya umuhimu wa uwekezaji kwenye sekta ya makazi.


TIGO YAMWAGA SIMU JANJA ZA TEKNO R6 KWA WASHINDI WA DROO YA NYAKANYAKA BONUS

$
0
0
.  Mtaalam wa huduma na bidhaa wa mtandao wa tigo tanzania  baraka hamza akiongea na waandishi wa habari mkoani morogoro wakati  wa hafla ya kukabidhi simu aina za tekno r6 kwa washindi  wa promosheni ya tigo nyakanyaka bonas, ambapo wateja 672 wa tigo wamejishindia simu hizo zenye uwezo wa 4g.
Mmoja wa washindi wa nyakanyaka bonus mwl justina Mathew jaka akikabidhiwa  zawadi ya simu  na meneja wa tigo kanda ya kati-pwani patricia sempinge katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya tigo huduma kwa wateja mkoani morogoro. Wateja 672 wa tigo wamejishindia simu za tecno r6 zenye uwezo wa 4g.


Meneja Mauzo Tigo Mkoa Wa Morogoro Abbas Abdraman Akikabidhi Zawadi Ya Simu Ya Tecno R6 Kwa Samson Baada Ya Kuwa Mojawapo Ya Washindi 672 Katika Promosheni Ya Tigo Nyaka Nyaka Bonas.
Mojawapo Ya Washindi 672 Wa Droo Ya Nyakanyaka Bonas Farida Yussuph(Katikati)  Akipokea Zawadi Ya Simu Aina Ya Tecno R6 Kutoka Kwa Meneja Wa Tigo Kanda Ya Kati-Pwani Patricia Sempinge(Kushoto) Wakati Wa Hafla Iliyofanyika Katika Ofisi Ya Tigo Huduma Kwa Wateja Mkoani Morogoro.
Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza (Kulia) Na Abbas Abdraman Meneja Mauzo Tigo Mkoa Wa Morogoro (Kushoto)  Wakikabidhi Zawadi Ya Simu Tecno R6 Kwa Mojawapo Ya Washindi 672 Wa Promotion Ya Tigo Nyakanyaka Petrocia Makongera (Katikati) Katika Hafla Iliyofanyika Katika Ofisi Ya Tigo Huduma Kwa Wateja Mkoani Morogoro
. Meneja Wa Tigo Kanda Ya Kati-Pwani Patricia Sempinge Pamoja Na Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza (Kulia) Akikabidhi Zawadi Ya Simu Ya Tecno R6 Kwa Mojawapo Ya Washindi Wa Promosheni Ya Nyakanyaka Bonasi, Japhet Mbonea Mkoani Morogoro.
Mkazi Wa Morogoro Henry Msemwa Akipokea Zawadi Ya Simu Aina Ya Tekno R6 Kutoka Kwa Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza Mara Baada Ya Kuwa Moja Wa Washindi Wa Droo Ya Nyakanyaka Bonas

Baadhi ya washindi  wa promotion ya nyakanyaka bonus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tigo katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya tigo huduma kwa wateja mkoani morogoro. Wateja 672 wa tigo wamejishindia simu za tecno r6 zenye uwezo wa 4g.

TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM

$
0
0
Na Ropota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio vya Times FM na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema kuwa Radio ya Times FM walitangaza mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum.

Imeelezwa kwenye mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

"Times FM wamepewa onyo na kutakiwa kumuomba radhi Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya utangazaji,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kuhusu Radio ya Clouds FM ni kwamba imepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki  Ibrahim Musa a.k.a Roma mkatoliki na Naibu Waziri Shonza.

Makamu wa Rais aendelea na ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Katibu wa Chadema mkoa wa Kusini Unguja Bw. Ali Othman Shomari ambaye amejiunga na CCM leo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoa wa Kusini Unguja Bw. Ali Othman Shomari ambaye amejiunga na CCM leo,akizungumza jambo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja,ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan alimpokea . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY

$
0
0


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii


HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imekosa mashine ya X-RAY hali inayosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila.


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imekosa mashine ya X-RAY ,hali inayosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila.

Akizungumza na Michuzi blog, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ameeleza ujenzi wa hospitali ya Mkamba unaendelea vizuri hadi sasa nyumba ya mganga, chumba cha upasuaji, maabara na wodi ya wazazi zipo katika hatua nzuri na hii ni kwa msaada wa serikali.

Mwandambo ameeleza wanapokea akina zaidi ya 300 kwa ajili ya kujifungua, hivyo ujenzi wa hospitali ya Mkamba utapunguza adha hiyo.Aidha meeleza kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa mashine ya X-RAY tangu ilipoanzishwa na bado wanapambana na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ili kutatua changamoto hiyo.

Pia amefafanua kuwa rufaa za kokosa damu zimepungua kutoka asilimia 28 hadi asilimia 3 na bado wanaendelea kuelimisha wananchi kuhusu kulima na kula mboga za majani sambamba na matumizi ya dawa za kuongeza damu kwa wajawazito.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde ameeleza madaktari wapo ila hawana mashine ya X-RAY hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa hospitali nyingine.

Aidha Munde amesema madaktari wapo na chumba cha X-RAY kipo tayari kwa kutegemea mashine kutoka kwa Wizara husika lakini bado ni kitendawili.Pia Munde ameongeza mwaka jana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Ulega walikuwa na maongezi na aliyekuwa Balozi wa China nchini kuhusu kupatikana kwa mashine hiyo.

"Na maongezi hayo yana matumaini kidogo baada ya kufika muafaka wa balozi huyo kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo,"amesema.Amefafanua kama Halmashauri wanatakiwa kuchangia dola za Marekani 40,000 ambazo zinatakiwa zilipwe kwa wasambazaji ndipo dola  30,000 zitolewa na balozi wa China kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo.
 Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti  wa Afya  wa kituo cha Mkamba,Haji Abdallah Pepo mara baada ya kukagua mradi wa majengo ya Kituo cha Afya Mkamba,Mradi huo umefikia hatua ya mwisho za ujenzi wa miundombinu ambapo ujenzi huo umeelekezwa kwenye chumba cha upasuaji,wodi ya wazazi,Maabara na Nyumba ya Mganga.

 Muonekano wa majengo ya kituo cha Afya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Hosptal ya Wilaya kukosa mashine ya X-RAY,hali inayosabaisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Mhimbili na Mloganzila.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kukosekana kwa huduma ya mashine ya X-RAY ,hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa katika hospitali nyingine.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

Akizungumza na Michuzi blog, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ameeleza ujenzi wa hospitali ya Mkamba unaendelea vizuri hadi sasa nyumba ya mganga, chumba cha upasuaji, maabara na wodi ya wazazi zipo katika hatua nzuri na hii ni kwa msaada wa serikali.

Mwandambo ameeleza wanapokea akina zaidi ya 300 kwa ajili ya kujifungua, hivyo ujenzi wa hospitali ya Mkamba utapunguza adha hiyo.Aidha meeleza kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa mashine ya X-RAY tangu ilipoanzishwa na bado wanapambana na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ili kutatua changamoto hiyo.

Pia amefafanua kuwa rufaa za kokosa damu zimepungua kutoka asilimia 28 hadi asilimia 3 na bado wanaendelea kuelimisha wananchi kuhusu kulima na kula mboga za majani sambamba na matumizi ya dawa za kuongeza damu kwa wajawazito.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde ameeleza madaktari wapo ila hawana mashine ya X-RAY hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa hospitali nyingine.

Aidha Munde amesema madaktari wapo na chumba cha X-RAY kipo tayari kwa kutegemea mashine kutoka kwa Wizara husika lakini bado ni kitendawili.Pia Munde ameongeza mwaka jana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Ulega walikuwa na maongezi na aliyekuwa Balozi wa China nchini kuhusu kupatikana kwa mashine hiyo.

"Na maongezi hayo yana matumaini kidogo baada ya kufika muafaka wa balozi huyo kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo,"amesema.Amefafanua kama Halmashauri wanatakiwa kuchangia dola za Marekani 40,000 ambazo zinatakiwa zilipwe kwa wasambazaji ndipo dola 30,000 zitolewa na balozi wa China kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo.
 Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti  wa Afya  wa kituo cha Mkamba,Haji Abdallah Pepo mara baada ya kukagua mradi wa majengo ya Kituo cha Afya Mkamba  ukimefikia hatua ya mwisho za ujenzi wa miundombinu ambapo ujenzi huo umeelekezwa kwenye chumba cha upasuaji,wodi ya wazazi,Maabara na Nyumba ya Mganga.

 Muonekano wa majego ya kituo cha Afya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo akizungumza na Michuzi Blog juu ya Hosptal ya Wilaya ya  imekosa mashine ya X-RAY hali inayopelekea matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya taifa Mhimbili na Mloganzila.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog juu ya mashine ya X-RAY hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa katika hospitali nyingine.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

BALOZI WILBROAD SLAA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO KWA MFALME WA SWEDEN

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Wilbroad Slaa leo amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden.

ALICHOKISEMA DKT. ABBASI KWA WAANDISHI WA HABARI WA KAMPUNI YA GLOBALGROUP

KUMBUKUMBU YA MIAKA 46 YA SHEIKH ABEID AMANI KARUME

Ufanisi Katika Huduma za Afya Kuongezeka

$
0
0
 
Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Mifumo ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mradi wa Programu ya Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Desideri Wengaa akifafanua mada kuhusu Mfumo wa Uandaaji Taarifa za Kiuhasibu (FFARS) wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Edwin Chao akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Steven Kitinya (Mwezeshaji) akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Bi. Janeth Kibambo akizungumza wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bi. Catherine Usubisya na Mfamasia wa Mkoa wa Morogoro Bi. Martha Kikwale. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Mwakilishi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bi. Catherine Usubisya akielezea jambo wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Meneja Programu wa Mkoa wa Dodoma toka Taasisi ya Kuhamasisha Uimarishaji wa Mifumo ya Afya (HPSS) akielezea jambo wakati wa mafunzo kwa ajili ya wakufunzi wa mikoa kuhusu mifumo ya Upelekaji wa fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Afya (DHFF), Bima ya Afya ya Jamii(CHF) na Utaratibu wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa MSD (Jazia – Prime Vendor System) leo jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa makini. (Picha zote na: MAELEZO, Mbeya.)

NAIBU WAZIRI KWANDIKA AFUNGA BARAZA LA WAFANYAKAZI SEKTA YA UJENZI, MOROGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa, akihutubia viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati akifunga kikao cha pili cha baraza hilo kilichofanyika mkoani  Morogoro.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kushoto), akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kufunga kikao cha siku ya pili cha baraza hilo, mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kushoto), kabla ya kufunga baraza hilo lililokutana kwa siku mbili, mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), wakati akifunga kikao cha siku ya pili ya baraza la wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), akimsindikiza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), mara baada ya kufunga kikao cha siku  mbili cha baraza la wafanyakazi mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi mara baada ya kufunga kikao cha baraza hilo kilichofanyika mkoani Morogoro.

DC KIGAMBONI ATOA AMRI KWA WASIMAMIZI WA MRADI WA LAKE OIL KUFANYIWA MAHOJIANO MAALUM NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama leo wametembelea kata ya Pemba mnazi eneo la Yaleyale panu kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Alhamisi ya wiki iliyopita walipokuwa wakikagua majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe za bahari.
DSCN1118
Akiongea na vyombo vya habari katika matembezi hayo Mh.Hashim Mgandilwa amesema kuwa takribani wiki mbili zilizopita walikuwa wanatembelea maeneo ya fukwe za bahari ili kufanya ukaguzi kutokana na wilaya hiyo ya kigamboni kuwa lango la biashara haramu na wahamiaji halamu.
DSCN1114
Pia amesema kuwa katika ukaguzi huo waliofanya eneo linalomilikiwa na mwekezaji wa Lake oil lilikutwa na tatizo kwa kuwa na gati linaloweza kutumiwa na chombo chochote cha maji katika kushusha na kupakia mzigo wowote na kuagiza gati hilo kubomolewa ndani ya siku tano lakini maagizo hayo yamekiukwa ambapo utejelezaji umeanza kutekelezwa leo kinyume na barua waliyoituma halimashauri ikionyesha utekelezaji huo kutendeka.
DSCN1001
Hata hivyo mkuu wa wilaya akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ameagiza kukamatwa kwa wahusika hao ili kufanyiwa mhojiano zaidi kwa sababu za kiusalama sambamba na kufika na vibali vinavyowaruhusu kufuga swala pamoja na hati miliki zinazoonyesha umiliki halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo watanyang’anywa eneo hilo na kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
DSCN0930
Viongozi hao waliokamatwa ni kiongozi mkuu wa miradi kutoka lake oil Fahim Mohammed na Mkurugenzi msaidizi wa lake oil Halid Mohammed, hata hivyo viongozi hao wamekana kukaidi agizo la mkuu wa wilaya na kuomba kupewa angalau muda wa mwezi mmoja kwani shughuli ya ubomoaji waliyoagizwa kufanya ni ngumu na inahitaji vifaa maalumu.
DSCN0874
Kwa upande wake mwanasheria kutoka NEMC Manchale Heche amesema kuwa lake oil walipokea barua kutoka ofisi za NEMC ya kuwaruhusu kuendesha mradi pembezoni mwa bahari lakini hawakuruhusiwa kujenga nyumba za kudumu na walipewa masharti ambayo wameyakiuka.Hivyo Kufuatia ukiukwaji wa masharti hayo waliyopewa kutoka NEMC mwanasheria huyo amewafutia kibali cha kuendeleza mradi huo mpaka hapo watakapokutana na kufanya makubaliano ya kupata kibali kingine na kufuata masharti kama sheria inavyosema.

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAGERA (KCU) CHAFAFANUA KUHUSU MALIPO YA AWALI YA KAHAWA YA WAKULIMA

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK 

Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).

Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.

Amebainisha hayo wakati akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa  pamoja katika kuhudumia zao la  kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato  baada ya kufanya mauzo.

Alisema bei halisi ya mkulima kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo  wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.

Hivyo kwa vile mchakato wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi wao kupitia  Mkutano Mkuu, wanajadili malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.

Niyegila alibainisha kuwa mnamo tarehe 27/03/2018, Chama Kikuu cha Kagera kilifanya Mkutano wake Mkuu ambao pamoja na mambo mengine wanachama walijadili malipo ya awali ya mkulima (Advance Payments). Katika makisio hayo,  Menejimenti na Bodi ya KCU (1990) Ltd walipendekeza malipo ya awali yawe ni TZS 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda.

Alisema kuwa baada ya mjadala, wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa katika upande wa malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo ya awali. Aliongeza kuwa Kiwango kipya pendekezwa kitawasilishwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwa ajili ya kuidhinishwa.

Alisisitiza kuwa kile kilichojadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama si tangazo la bei bali ni malipo ya awali kwa mkulima ambapo Kwa mujibu wa sheria, bei elekezi ya zao la kahawa inatolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa utaratibu wa ushirika, bei halisi itajulikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika sokoni na si vinginevyo.

Niyegila aliongeza kuwa kwa utaratibu wa sasa wa Serikali, kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.

Kwa mantiki hiyo, hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika

KATIBU WA BUNGE, NDG. KAGAIGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMATI NDOGO YA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo tarehe 7 MachI, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma. Kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi.


Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia kikao kati yao na Katibu wa Bunge, pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge kikilenga kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. Kutoka kushoto ni Mhe. Leontine Nzeyimana, Mhe. Aden Abdikadir (wa pili kushoto), Mhe. Dkt. Anne Leonardo (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga (kulia)
 

Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) wakiwa katika kikao cha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge walioongozwa na Katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai (wa pili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. 

Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioongozwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SERIKALI YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO YA KIUCHUMI WA KUWAIT

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (wa tano kutoka kulia), na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akiongoza mazungumzo kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, akitia saini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na mmoja wa wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34.4, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, lenye ukubwa wa hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman na kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
 
“Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.
 
Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Kuwait zitatia saini mkataba rasmi wa mkopo huo wenye masharti nafuu ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili mradi huo uanze kutekelezwa ili kuongeza kipato cha wananchi na kuwa na uhakika wa chakula.Amesema Nchi ya Kuwait imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ukarabati wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
 
”Kwa upande wa Tanzania Bara wametoa mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami ambayo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha mikoa ya Magharibi mwa Tanzania” aliongeza Dkt. MpangoMiradi mingine ambayo nchi hiyo imeonesha nia ya kuisaidia nchi, ni pamoja na ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, uboreshaji wa barabara ya kutoka Morogoro hadi Dodoma na ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma ambazo zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango ameishukuru nchi ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, kwa nia yake njema na thabiti katika kusaidia nchi ya Tanzania kutekeleza kwa mafanikio miradi ya Maendeleo ya kiuchumi katika nia yake ya kupata maendeleo Stahiki.Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha na Mipango kwa ukarimu pamoja na Idara ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ushirikiano mzuri katika hatua za kufanikisha utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji wa Bonde la Luiche, Mkoani Kigoma.“Tumetembelea eneo la mradi kwa takribani wiki mbili tumejionea uzuri wa nchi hii na fursa zilizopo, hii ni nchi tajiri na inaweza kuwa tajiri kuliko Kuwait kwa kuwa kila kitu kinachoweza kufanya nchi hii iwe tajiri kipo”.Alieleza Dkt. Bahman.
 
Amesema mradi huo wa umwagiliaji hautakuwa wa mwisho kupewa fedha na mfuko huo bali utaendelea kusaidia kutekeleza miradi mingine mingi kama ilivyokuwa ikifanya, kutokana na ushirikiano mzuri, wa kihistoria, na wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

LAZIMA WAWEPO MADEREVA WAWILI KWA MABASI YAENDAYO MIKOANI-KAMANDA MWANGAMILO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni kimesema mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani lazima wawepo  madereva wawili na hilo haliepukiki.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Solomon Mwangamilo amesema ukaguzi wa mabasi na madeva wawili ni endelevu katika kuhakikisha abiria wanasafiri salama.

Mwangamilo amesema wamiliki mabasi wahakikishe wanazingatia usalama wa mabasi na abiria.Pia wahakikishe kunakuwa na madereva wawili ambao watapokeza kuendesha wakiwa safarini.Amesema basi likitoka katika kituo cha Ubungo lazima madereva wawili wasaini na mpaka wanafika katika kituo chao mwisho wanahakikiwa, hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya udanganyifu kutokana na mtando uliopo katika jeshi la Polisi.

Mwangamilo amesema wanaoingiza mabasi ambayo mabovu na kutegemea wataondoka na abiria kituo cha mabasi Ubungo wanajidanganya  na wataofanya hivyo watakwenda jela.“Kazi yetu ni kuhakikisha wananchi wanasafiri na mabasi yakiwa salama kutokana ukaguzi unaofanyika kila kukicha na hakuna basi litakaloachwa huku likiwa lina ubovu wa kuhatarisha watumiaji wa usafiri huo” amesema Mwangamilo.

Aidha amesema askari katika mkoa wa Kinondoni hasa kituo cha mabasi Ubungo kuwa kufanya kazi ya ukaguzi bila kikomo katika kuwalinda usalama wa abiria wanatumia mabasi ya mikoani na nchi jirani.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wakati wakifanya ukaguzi mabasi kutuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.
Abiria wakishuka katika Basi la Princess Line linalofanya safari zake Dar es Salaam ,Babati baada ya Basi hilo kuonekana na hitilafu takiribani ya masaa manne katika kituo cha Ubungo na kufanya kampuni kuwabadilishia basi lingine.
Askari wa Usalama Barabani katika kituo kikuu cha Ubungo, Koplo Rashid Abdallah akizungumza na abiria walio kaa zaidi ya masaa manne katika Basi la Princess Line, leo .jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabasi yalikutwa na kamera yetu katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA POLISI CHA UTALII NA DIPLOMASIA, NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI NA KUSHUHUDIA MAZOEZI YA MEDANI KATIKA SIKU YA KARUME JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na viongozi wengine pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro  wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa  na viongozi wengine akikata utepe  kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya familia za askari polisi baada ya kufungua  rasmi nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la askari polisi  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Gari maalumu la kunyunyizia maji ya kuwashawasha likionesha namna kikosi cha kutuliza ghasia cha Jeshi la Polisi kinavyoweza kupambana na waandamanaji  katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018.   Aprili 7, 2018. 
 Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna  kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018 


Viewing all 46339 articles
Browse latest View live




Latest Images