Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1551 | 1552 | (Page 1553) | 1554 | 1555 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wa Bima uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
  Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
  Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo.
  Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima yaliyohudhuria maonyesho hayo. 

   Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Kampuni za bima nchini zimeshauriwa kuwahudua wananchi kwa ukweli na uwazi na kutoa huduma za kiwango cha juu ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi. Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba wakati mkutano wa wadau bima ulioandaliwa African Insurance Digital Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa bima imeanzishwa kwa ajili ya kulinda biashara na mali hivyo wananchi wanatakiwa kuhudumiwa katika kulinda biashara na mali zao huku wakitoa elimu kwa uwazi. Aliongeza kuwa mtu mwenye bima katika biashara au mali likitokea janga haiwezi kuwa sifuri kutokana na kukata bima kwa ajili ya biashara na mali hizo.

   "Kampuni za Bima ili ziweze kufanya kazi ni lazima zisajiliwe katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi," alisema. Alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda sekta ya bima zina mchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi. Nae Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi. 

  Mtavangu alisema kuwa lengo lingine kuu la mkutano wa kuwakutanisha ni wadau ni pamoja na kujadili changamoto zinazowazunguka watoa huduma wa bima kuweza kujadili kwa nia ya kuboresha utoaji wa Bima kwa wananchi. Aidha Mwenyekiti huyo alisema mkutano huo wameuandaa katika kipindi mwafaka katika kwenda na dhamira ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo watoa huduma wa bima ndiyo fursa ya kufanya kazi na viwanda hivyo katika utoaji wa bima. 

  "Tutaendelea kufanya mikutano zaidi ili katika kuwaweka watoa huduma wa bima kuwa karibu na wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa maonesho ambapo wananchi wanaweza kupata huduma za bima," alisema. Mkutano huo wa pili wa masuala ya BIMA, ilisema kuenda pamoja na maoneshi ya Bima kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo. 

  Nchi zipatazo Tano zimewesha kushiriki katika mkutano huo ni Rwanda, Kenya, Afika Kusini, Nigeria na Tanzania ambao ndiyo wenyeji wa mkutano. Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Bima nchini, Sam Kamanga aliyaomba makampuni ya bima kuendelea kutoa bima kwa uaminifu na uwazi mkubwa ili kuweza kujijengea heshima katika jamii. "Nawaomba watoa huduma zote muwe wawazi, na huduma zenu ziwe za kiwango cha juu maana tumekuwa tukipata malalamiko mengi toka kwa wananchi juu ya uzembe mchache ambao umekuwa ukifanywa na kampuni ambazo si waaminifu, hivyo lazima tufuate sheria na kanuni tulizojiwekea," alisema. 

   Alisema kuwa uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya Bima hivyo wasipokuwa waaminifu watashindwa kuhudumia viwanda na taifa likatapa matokeo chanya.

  0 0

  WATETEZI wa Rasilimali Wasio na Mipaka(Warami)limesema limesikitishwa na kitendo cha Kamati kuu ya Chadema kuingilia uhuru wa Mahakama baada ya jana kuitisha mkutano kuzungumzia mambo yalipo mahakamani.

  Warami wameongeza kuwa si tu kuingilia uhuru wa mahakama pia chama hicho kimekwenda mbali zaidi kwa kutoa masharti yanayoashiria uvunjifu wa amani iwapo Mwenyekiti wa Freeman Mbowe na viongozi wengine watanyimwa dhamana leo.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugunzi wa Utafiti wa Warami Philipo Mwakibinga amesema jana baadhi ya viongozi wa Chadema kupitia mkutano wao wameonesha dhahiri kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kuanza kushinikisha maamuzi ya Mahakama.

  “Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, Profesa Abdallah Safari na wenzao wakiwa wanajua kuwa Mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya kuonesha kuwa viongozi hawatetendewi haki kama hawatapa dhamana leo.

  “Wanafanya hivyo wakijua wazi jambo hili limelenga kuishawishi , kushinikiza na kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo wao kwa kuacha misingi ya haki wajibu na maadili ya kimahakama,”amesema Mwakibinga.Amefafanua Watanzania ni mashahidi Mbowe na wenzake ambao wapo Mahakamani wamekamatwa kama matokeo ya matendo yao ya kushawishi na kuchochea chuki miongoni watanzania jambo ambalo si la kiutamaduni kwa Taifa.

  “Warami tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa sheria ni kama kaa la moto na unapovunja sharia lazima ujue umeamua kushika kaa la moto kwa hivyo lazima ujiandae kuungua.“Tunawakumbusha Chadema ,hasa wakina Lema na wenzao watii sheria , waache maneno ya kichochezi yasiyo ya kiuongozi na wasiendelee kuropoka ropoka, zama za kuwachekea waropokaji zimepitwa na wakati,”amesema.


  Mwakibinga amesema Lema kukamatwa kwa viongozi wa chama chake ni mkakati uliopangwa na Serikali kwa ajili ya kuwakomoa.


  Amesema Warami wanawapa changamoto Chadema , wamuulize Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ajitokeze hadharani wakati Augustino Mrema akiwa NCCR-Mageuzi na baadae TLP alivyokuwa anakamatwa na vyombo vya dola je alikuwa analazimisha vyombo vya dola vimkamate wakati Mrema hakuwa na makosa kwa wakati ule.

  “Chadema waache kuharibu sifa ya vyombo vyetu vya kiusalama hasa idara nyeti ya Usalama wa Taifa kwa kuwasingizia mambo ya ajabu ajabu kwa ajili ya kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama,”amesema Mwakibinga.

  Ameongeza Warami inawataka Chadema kuacha kukimbia kivuli chao na waswahili wanasema ‘ukilikoroga lazima ulinywe’ .“Hivyo Chadema walinywe kwa kadiri ya walivyorikoroga.Pia iache Mahakama itafisiri sheria na kwa kuwa wameweka wanasheria wanaowaamini, wawahimize wanasheria wao kuhakikisha wanashinda kesi zinazowakabili,”amesisitiza.


  KUHUSU MAASKOFU KUTUMIKA

  Mwakibinga amesema mara ya mwisho walihoji iwapo maaskofu wanatumika na vyama vya siasa hasa Chadema.

  “Nafikiri wote sasa tumejiridhisha kuwa maaskofu wetu wameamua kutumika kulipa fadhila za waliokuwa wanawapa fedha katika zama za kufanya harambee ya fedha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

  “Matukio ya Chadema kuunga mkono hadharani waraka wa maaskofu ,ACT Wazalendo kunifukuza uanachama kwa mimi kuwakosoa maaskofu na Maalim Seif kutangaza hadharani anaunga mkono madudu yale ya maaskofu,”amesema.

  Ameongeza hivyo ni vishiaria na kuthibitisha wazi maaskofu wameamua kutumika na kuyaacha maelekezo na mafunzo ya dini yanayotaka kilicho cha kaisari apewe kaisari na kilicho cha Mungu apewe Mungu.

  Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanasiasa, wanaharakati , wanahabari , viongozi wa dini , taasisi binafsi waanzishe utaratibu wa kuheshimu uhuru wa Mahakama na kutoa kauli za mashinikizo.
  Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga , akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuingia uhuru wa Mahakama.
  Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga, akiwaeleza jambo waandishi wa habari yaliyojiri katika mkutano mkuu wa Chadema.--

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma , Machi 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuongoza Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha Kupitia Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wapili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpamgo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) baada ya kuongoza Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo akitoa maelekezo kwa wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu wa mkoa huo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
  Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Arusha Bi. Irene Ngao akizungumza na Wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu yaliyofanyika leo jijini Arusha. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.
  Wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha wakifuatilia mafunzo ya uandaaji wa filamu yaliyofanyika leo jijini Arusha, mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania yamehusisha zaidi ya wasanii mia moja.
  Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Arusha Mjini Bw. Antony Mushi akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa Filamu wa Mkoa wa Arusha yaliyofanyika leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) akicheza ngoma na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mtikisiko Sanaa Group cha jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa filamu mkoani humo mapema hii leo. Zaidi ya wasanii mia moja wamepatiwa mafunzo hayo.PICHA ZOTE NA:OCTAVIAN KIMARIO,WHUSM

  0 0


  Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
  MSEMAJI wa Serikali Dkt. Abbas Hassan amesema utoaji taarifa na habari kwa sasa ni takwa la kisheria na si utashi wa ofisa habari na tayari wameelezwa hilo na wanaliambua.

  Dk.Abbas ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza kutoa matokeo ya utafiti mpya wa mwaka 2018.Utafiti huo umetolewa leo jijini.

  Amesema utafiti huo umeonesha namna ambavyo wananchi wametoa maoni yao katika suala la upatikanaji wa taarifa nchini na kufafanua kwa sasa suala la kutoa taarifa ni takwa la kisheria.

  "Tunayo sheria sasa ambayo inatoa ulazima wa taarifa kutolewa pale inapohijika.Kutoa taarifa ni hatua moja lakini pia lazima tuangalie sasa hiyo habari ikoje katika suala la usalama wa nchi.Kwa upande wetu wote ambao wanahusika na utoaji taarifa wanajua ni wajibu wao na lipo kisheria,"amesema Dk.Abbas.

  Amesema wananchi wengi wanaamini na kusikiliza au kupata habari kupitia redio na kwamba mchango wao kama Serikali wanao mchango wao na kwamba hadi jana inaonesha magezeti na majarida, machapisho ambayo yamesajiliwa ni 169 ambayo yamesajiliwa na redio 150 ambazo zimepewa leseni.

  Amefaanua wanatoa kipaumbele kwenye maendeleo ya redio na kwamba wamejikita katika kutoa mafunzo mbalimbali.Kuhusu maofisa habari amesema  dhana nzima ya utoaji habari na taarifa zi lazima uvae suti na kufafanua kwa sasa kwa ofisa habari kutoa habari si utashi binafsi bali ni takwa la kisheria

  Amepongeza utafiti wa Twaweza na kusisitiza uwe endelevu kwa kufanyika hata kila baada ya miezi sita.Pia sheria zifuatwe na kuhusu suala la uhuru wa habari ameeleza kuwa ni muhimu lakini uzingatie haki na wajibu wake.


  "Kikubwa tufahamu sisi wote ni wadau na hivyo tushirikiane na kwamba kikubwa ni kupigania haki ya kupata habari.Kuna taratibu za kufauata na hata pale unaposikia kuna haki ya kuishi lazima ufurukute ili uishi.Nashauri mambo mengi kuhusu masuala ya habari na hilo ndio kazi yangu,"amesema Dk.Abbas.

  Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT WAZALENDO) amesema kwa mujibu wa utafiti watu wengi wamesema hawajisii kumkosoa Rais, Makamu wa  Rais na Waziri Mkuu.

  Pia utafiti unaonesha wananchi wengi hawaamini taarifa mbalimbali ambazo zinatoka kwenye vyanzo mbalimbali na hivyo iko haja ya watoa taarifa hizo zitazamwe na kufafanua huenda jamii inaona habari zinazotoka hata kwenye vyombo vya habari si sahihi.

  Amesema utafiti unaonesha kuwa wananchi wengi sasa wanamini zaidi matamko ya Rais na Waziri Mkuu na kuomba Twaweza kuagalia mbunge wa Kigoma mjini amepongeza taasi hii na ameshauri kuwe na ulinganifu kwa kuangalia huko nyuma kulikuaje.

  "Tunapaswa kupata ulinganifu wa kimuda ambao haujafanyika kwenye utafiti na kwamba anamini huko mbele wataonesha na ulinganifu kati ya mwaka mmoja na mwingine kwa yale ambayo wanayafanyia utafiti,"amesema.

  Akizungumzia utafiti huo Mkurugenzi wa TWAWEZA Aidan Yakuze ameeleza utafiti huo kati ya mambo ya waliyoangalia ni uhuru wa kumkosoa Rais, makamu wa Rais na waziri mkuu ambapo matokeo yameonesha kuwa  wananchi hawajisikii huru kumkosoa Rais kwa asilimia 60, Makamu wa Rais asilimia 54 na Waziri mkuu asilimia 51.

  Pia utafiti huo unaonesha wananchi hawapo huru kuwakosoa Mawaziri kwa asilimia 47, wakuu wa mikoa asilimia 46, na Wakuu wa wilaya kwa asilimia 43.

  Aidha utafiti huo umeonesha kuwa wananchi wengi wana imani kubwa na taarifa zitolewazo na Rais kwa asilimia 70, na Waziri mkuu asilimia 64.

  Pia kwa upande wa wawakilishi wabunge wa Chama tawala kwa asilimia 26, wabunge wa upinzani  asilimia 12, viongozi wa serikali asilimia 22 huku idadi ndogo zaidi wanawaamini Wenyeviti wao wa vijiji kwa asilimia 30.

  Pia utafiti huo umeonesha kwamba uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari unaungwa mkono na wananchi walio wengi wao kwa asilimia 62 wameeleza kuwa gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuendelea kuchapisha.

  Aidha utafiti huu umeonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawafahamu sheria mpya zinazosimamia masuala ya taarifa hasa za kimtandao na zile za kitakwimu.
   Mbunge wa kigoma Mjini Zito Kabwe akizungumza na waandishi wa Habari akiwapongeza Taasisi ya Twaweza kwa kazi nzuri walioifanya,akiwataka wasiishie mjini tu waende na vijijini.
   Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa Habari Mara baada ya kupokea ripoti hizo kutoka kwa Twaweza,na akiwataka kufanya tafiti hizo kuwa endelevu kwa kila Baada ya miezi 6 Leo katika makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza Aidan Yakuze akizungumza wakati wa kutoa ripoti ya namna ya uwasilishwaji wa Taarifa na habari kwa Jamii leo makumbusho ya Taifa Jijini Dar ea Salaam.

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WANANCHI wengi wamesema wana imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais kwa asilimia 70  na Waziri Mkuu kwa asilimia 64 huku idadi ndogo zaidi wanamwamini mwenyekiti wao wa kijiji kwa asilimia 30, wabunge  wa chama tawala asilimia 26 na  wa upinzani asilimia 12 wakati viongozi wa Serikali kwa ujumla ya asilimia 22.

  Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze wakati anatoa matokeo ya Twaweza yalitokana na utafiti uliofanyika uliojukana kama muhtasari  uitwao Siyo kwa kiasi hicho? 

  Pia maoni ya wananchi kuhusu taarifa na mijadala ambapo Eyakuze anafafanua takwimu za muhtasari huo zinatokana na utafiti wa Sauti za Wananchi ambao huratibiwa na taasisi ya yao.Sauti za Wananchi ni utafiti wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

  "Matokeo ya utafiti unaonesha wananchi wengi kuwa na imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu,"amesisitiza.

  Pia amesema wananchi wanaendelea kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa ambapo  wananchi 7 kati ya 10 wanasema taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma ni mali ya umma ni asilimia 70 juu zaidi kutoka asilimia 60 mwaka 2015).

  "Na wananchi 9 kati ya 10 wanasema wananchi wa kawaida wapate taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma kwa asilimia 86  juu zaidi kutoka asilimia 77  mwaka 2015) na kwa kuwapa wananchi uwezo wa kupata taarifa kunaweza kupunguza rushwa asilimia 86 , juu zaidi kutoka asilimia 80 mwaka 2015.

  "Pamoja na kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa, wananchi 9 kati ya 10 hawajawahi kuomba taarifa kutoka katika ofisi za serikali kwa asilimia 95 , mamlaka za maji asilimia 93 , au vituo vya afya  asilimia 93,"amesema. 

  Ameongza utafiti unaonesha kuwa wananchi wameendelea kutumia vyanzo vile vile vya habari bila kuwa na mabadiliko makubwa isipokuwa kwa upande wa runinga ambapo mwaka 2013 runinga ilikuwa ni chanzo kikuu cha taarifa kwa asilimia 7 ya wananchi na mwaka 2017 ni asilimia 23 ya wananchi. 

  Eyakuze amesema hata hivyo imani kwa aina mbalimbali za vyanzo vya habari inashuka .Radio kutoka asilimia 80 mwaka 2016 hadi asilimia 64 mwaka 2017, runinga kutoka asilimia 73 mwaka 2016 hadi asilimia 69 mwaka 2017 na maneno ya kuambiwa kutoka asilimia 27 mwaka 2016 hadi asilimia 13 mwaka 2017.

   "Pamoja na kushuka kwa imani na vyombo vya habari, wananchi bado wanaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari kwani  wananchi wanasema gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuchapisha marekebisho ni asilimia 62 badala ya gazeti hilo kufungiwa ama kutozwa faini asilimia 38. 

  "Idadi kubwa ya wananchi pia wanasema kuwa Serikali ipate ridhaa ya mahakama katika kufanya maamuzi yoyote ya kuliadhibu gazeti kwa kutoa taarifa zenye  maudhui yasiofaa kwa asilimia 54.Japokuwa wananchi wana mtazamo thabiti kuhusu upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kuzungumza, ni wananchi wachache sana wanaofahamu sheria zinazohusiana na masuala ya habari,"amesema. 

  Kuhusu Sheria inayofahamika zaidi katika suala hilo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015), ambayo inafahamika na asilimia 10 ya wananchi huku asilimia 4 pekee ya wananchi wakifahamu Sheria ya Huduma za Habari (2016). 

  Pia wananchi wengi pia hawajaunganishwa kwenye mifumo ya uraia ambapo ni mwananchi 1 kati ya 4 au pungufu mwenye cheti cha kuzaliwa asilimia 25, kitambulisho cha uraia asilimia 21, leseni ya udereva asilimia 9 na hati ya kusafiria asilimia 5. Hata hivyo, karibu wananchi wote asilimia 98 wana vitambulisho vya mpiga kura

  Eyakuze, anamesema wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kujieleza lakini ukweli wa mambo ni kwamba hawaombi taarifa hizo, wana imani duni na vyanzo vyote vya taarifa ukiweka kando kauli zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu, na hawajioni kama wanaweza kuwakosoa viongozi wakuu wa serikali.

   “Kutokana na kwamba hivi karibuni serikali imepitisha kanuni za Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa tuna imani kuwa itakidhi kiu ya wananchi ya kupata taarifa kutoka serikalini. 

  "Tunaishauri Serikali kuweka wazi taarifa ili kuyafikia matarajio ya wananchi. Cha kusikitisha, wananchi wanakamatwa na serikari kwa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii. Ni vyema serikali ikatambua thamani ya mijadala huru ya umma na ukosoaji wenye lengo la kujenga katika mapambano dhidi ya rushwa na katika harakati za kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati,"amesema.

  Akifafanua kuhusu utafiti huo amesema uwakilishi wa Tanzania Bara pekee, Zanzibar haihusiki  na kwa  maelezo zaidi kuhusu mbinu za utafiti huu kwa anayetaka kujua zaidi atembelee www.twaweza.org/sauti. Takwimu za muhtasari huo zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,519 kutoka awamu ya 25 ya kundi la pili la Sauti za Wananchi, na zilikusanywa kati ya Novemba 7 na Novemba 27 mwaka 2017.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akiwasili katika viwanja vya Mahafali ya kiwatunuku Askari Polisi waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi. Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. 
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akitoa hotuba katika Mahafali ya kuwatunuku Askari Polisi waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi. Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Polisi.
  Baadhi ya wahitimu waliohitimu astashahada na stashahada za Sayansi ya Polisi na Upelelezi kutoka vyuo vya Polisi wakiwa kwenye  Sherehe zilifanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam


  0 0

   


  0 0


  0 0


  0 0

  Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeendesha kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi mkoani humo.
  Kikao hicho cha siku mbili kilichoandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC), kimefanyika Machi 27,2018 hadi Machi 28,2018 katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza.
  Miongoni mwa wadau waliohudhuria kikao hicho ni waratibu wa Ukimwi ngazi ya mkoa na wilaya,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri,waganga wakuu wa wilaya,waratibu wa afya ya uzazi na mtoto,waratibu wa kifua kikuu,mashirika,taasisi na wadau mbalimbali wanaofanya shughuli za kupambana na VVU na Ukimwi.
  Akifungua kikao hicho,Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella alisema mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi yatafanikiwa tu endapo kila mdau atashiriki 
  “Sisi kama mkoa wa Mwanza ni wa pili kwa idadi kubwa ya watu baada ya Dar es salaam,lakini pia tupo wa pili kwa shughuli za uchumi, takwimu za mwaka 2011/2012 zinaonesha kuwa tulikuwa na maambukizi ya asilimia 4.2 lakini mwaka 2016/2017 maambukizi yamepanda hadi kufikia asilimia 7.2”,alieleza.
  “Ili tushushe asilimia hizi kubwa za maambukizi lazima wadau wote tushirikiane katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuelekeza nguvu zaidi katika kundi la vijana ambalo linapata maambukizi ya VVU kwa kasi”,aliongeza Mongella.
  Aidha alisema teknolojia na utandawazi inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi kwani vijana wanatumia vibaya mitandao ya mawasiliano na kusababisha kujiingiza katika tabia hatarishi zinazochongia kuwepo kwa maambukizi.
  Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wadau wa afya mkoani humo likiwemo shirika la AGPAHI ambalo limekuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya nchini,kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mkoa huo una takribani watu 90,000 wanaokisiwa kuwa na maambukizi ya VVU na bado hawajafikiwa.
  Aliongeza kuwa shirika hilo lina mpango wa kuwafikia watu wapatao 37,900 kwa ajili ya kuwapatia huduma za tiba na matunzo watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na Ukimwi (kutokana na takwimu za utafiti wa Tanzania HIV Impact Survey (THIS) 2016 – 2017).
  ANGALIA PICHA WAKATI WA KIKAO
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akizungumza katika kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa. Kushoto ni Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Mwanza Dk. Sylas Wambura. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akiwasisitiza wadau wa afya kuungana katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akilishukuru shirika la AGPAHI na Watu wa Marekani kupitia CDC kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.
  Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Mwanza Dk. Sylas Wambura akizungumza wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
  Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza wakiwa ukumbini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa shirika hilo litaendelea kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.
  Mwakilishi wa Centres for Disease Control (CDC) nchini, Eva Matiko akizungumza katika kikao hicho.Wadau wa masuala ya VVU na Ukimwi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa kikao hicho.
  Wadau wakiwa ukumbini.
  Wafanyakazi wa shirika la AGPAHI mkoa wa Mwanza wakiwa ukumbini.
  Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Masele akizungumza katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Magu, Hadija Nyembu akichangia hoja wakati wa kikao hicho kuhusu namna ya kupambana na maambukizi ya VVU.
  Mratibu wa Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria kutoka TAMISEMI, Mbuuni akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
  Kikao kinaendelea...
  Wadau wakiwa ukumbini.Picha zote  na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Click here to Reply, Reply to all, or Forward 3.93 GB (26%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 51 minutes ago Details

  0 0  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akimkabidhi zawadi ya daftari mwanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya msingi Barazani Kata ya Maghang, Julieth John kutokana na utunzaji bora wa vyanzo vya maji na mazingira, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza na wananchi wa Kata ya Maghang juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.
  ………  Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, imepokea kutoka serikali kuu kiasi cha sh1 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Mji mdogo wa Haydom. Pia, kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 Halmashauri hiyo imetengewa sh. 2.3 bilioni za ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba za kuishi watumishi. 

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hudson Kamoga aliyasema hayo jana wakati akizungumza juu ya mikakati ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Haydom. Alisema baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo kupitisha uamuzi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kuwa Haydom, hivi sasa wapo kwenye mchakato wa utekelezaji. 

  “Hadi mwakani kipindi kama hiki tutakuwa tumeshahamia kwenye makao makuu mapya ya halmashauri yetu kule Haydom na kuondoka hapa Mbulu mjini,” alisema Kamoga. Alisema awali Mbulu iligawanywa mwaka 2015 na kuwa na halmashauri mbili ya mji na wilaya, hivyo huu ni wakati wa kujenga ofisi zao mpya kwa lengo la kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi. 

  “Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kutupatia fedha hizo za ujenzi wa makao makuu mapya ya halmashauri yetu ya wilaya,” alisema Kamoga. Mkazi wa mji mdogo wa Haydom, Paul John alishukuru uamuzi wa kujengwa makao makuu mapya kwenye eneo hilo tofauti na uamuzi wa awali wa kujenga Dongobesh. 

  “Huku kuna huduma mbalimbali za kijamii nyingi ikiwemo kituo kikubwa cha polisi, benki hospitali kubwa, tofauti na Dongobesh ambayo haina hata benki,” alisema John. Mkazi wa Dongobesh Aloyce Martin alisema kuenea kwa unywaji na biashara ya pombe haramu ya gongo kwenye eneo hilo kumewagharimu hadi kusababisha makao makuu mapya ya halmashauri hiyo yakahamishiwa Haydom.
  “Makosa ni ya kwetu sisi wenyewe kwani tulipata nafasi badala ya kuitumia ipasavyo sisi tukaichezea hadi ikawadondokea watu wa Haydom,” alisema Martin.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akikagua kituo cha uzalishaji umeme na kusambaza umeme mkoani Mtwara . wakati alipotembelea kituo hicho jana akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalaama Bw. Evod Mmanda.
  Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Hamisi Mgalu akipata maelezo katika kituo cha uzalishaji umeme na kusambaza umeme mkoani Mtwara wakati akipokea ripoti ya kituo hicho alipotembelea akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalaama Bw. Evod Mmanda.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mtwara Mh. Evod Mmanda metembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Mangopachanne Mtwara vijijini na kujionea ujenzi wa shule hiyo unavyendelea.Mh. Mmanda amemuaguza mkandarasi wa ujenzi wa shule hiyo kufanya kazi kwa bidii na kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ili shule hiyo ianze kutumika na kuwasaidia wanfunzi kutotembea umbali mrefu kwenda kupata elimu.
  boi2
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mtwara Mh. Evod Mmanda akitoa maagizo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo.
  boi3
  Diwani na wataalamu wa halmashauri nilioandamana na Mkuu wa wilaya huyo hayupo pichani mara baada ya kukagua ujenzi huo.

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea mpango mkakati wa Mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi ambaye sasa ndiye muendeshaji wa Mashindano hayo. Serikali imetoa baraka zake kwa uongozi wa The Look Company Limited kwa nia yake ya kurudisha heshima, hadhi na mvuto wa tasnia ya urembo hapa nchini kupitia Mashindano hayo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu wake, Juliana Shonza (kushoto) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi baada ya mazungumzo yao, jana katika ofisi za Ukombozi wa bara la Afrika, zilizopo Garden avenue, Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea mpango mkakati wa Mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi ambaye sasa ndiye muendeshaji wa Mashindano hayo. Serikali imetoa baraka zake kwa uongozi wa The Look Company Limited kwa nia yake ya kurudisha heshima, hadhi na mvuto wa tasnia ya urembo hapa nchini kupitia Mashindano hayo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu wake, Juliana Shonza (kushoto) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi baada ya mazungumzo yao, jana katika ofisi za Ukombozi wa bara la Afrika, zilizopo Garden avenue, Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi 

  Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inatarajia kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yatakayoanza Aprili 3,2018 hadi  Aprili 5,2018. 

  Katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambapo kauli mbiu ni ‘Tanzania ya Viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya Viwanda’. 

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack wakati akizungumza ofisini kwake ambapo amebainisha kuwa madhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali. Miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanyika ni pamoja na zoezi la upandaji miti na kuwa kila kaya itakabidhiwa miche kwa ajili ya kuipanda katika maeneo yao na kutakiwa kuitunza. 

  Mhe. Telack alisema kuwa lengo la zoezi hilo la upandaji wa miti ni kuifanya Wilaya ya Kishapu kuwa ya kijani kwa kuondoa hali ya jangwa inayoinyemelea. Sanjari na upandaji miti pia madhimisho hayo yataambatana na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi ili kujenga uelewa wa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. 

  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kutaja maeneo yatakayopandwa miti ni vijiji vya Mwatuju kata ya Shagigilu na Songwa. Alisema maadhimisho yataambatana pia na maonesho ya bidhaa za misitu pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ambapo vyote hivyo vinatarajiwa kuoneshwa katika viwanja vya Shirecu. 

  Mhe. Taraba alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao na kuitunza ili kuendelea kuhifadhi mazingira na kuepusha mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame. 

  Tayari Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kishapu wameanza uhamasishaji na utoaji elimu ya uhifadhi wa misitu umeanza kufanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo utoaji wa elimu kwa njia ya sinema.

  0 0  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

  KIWANDA cha kutengeneza nguzo za zege cha Hunnan Power ,mjini Kibaha Mkoani Pwani ,kimefungwa kutokana na kukosa tenda na soko , tangu uzalishaji uanze mwezi september mwaka jana.

  Kutokana na hali hiyo, kiwanda hicho kimebaki gofu na kupunguza ajira kutoka wafanyakazi 30 hadi wawili kwasasa.Hayo yalibainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,alipotembelea viwanda nane vilivyoanza uzalishaji na ambavyo vipo kwenye hatua za ujenzi mjini Kibaha.

  Alisema mkoa huo unadhamira ya kuwa ukanda wa Viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali lakini endapo soko litakuwa hakuna ,wawekezaji watakata tamaa.Alisema mkoa una viwanda vinavyotengeneza nguzo za zege viwili ikiwemo Hunnan Power /Kibaha na East Africa infrastructure engineering Ltd kilichopo Fukayosi /Bagamoyo ambavyo vinahofiwa kushindwa kuendelea kuzalisha kwasababu ya bidhaa zake kukosa wateja.

  "Katika ziara hii tumebaini changamoto ya kiwanda cha Hunnan Power kukosa masoko na tenda huko shirika la umeme (Tanesco ),hawajapata tenda mara tatu ,""Hali hiyo imesababisha kiwanda hicho kufungwa, hakizalishi ,mashine zimefungiwa ndani ,kiwanda kimezungukwa nyasi ,kimekuwa gofu na ajira hakuna" suala hili linaangusha juhudi za rais John Magufuli ,Mkoa na serikali"alisema mhandisi Ndikilo.

  Mhandisi Ndikilo alieleza, wawekezaji wanajitoa kuunga mkono na kuitikia wito wa serikali kujenga viwanda lakini baadhi vinakumbana na changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika.Aliahidi kuzungumza na waziri mwenye dhamana na mkoa utafuatilia ili waziri wa nishati aweze kusaidia suala hilo.

  Mkuu huyo wa mkoa aliitakaTanesco kuangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo na kuangalia namna ya kutoa tenda ili kuokoa kuinua viwanda hivyo.Mhandisi Ndikilo alitaja changamoto nyingine alizofikishiwa kwenye ziara hiyo,kuwa ni umeme,maji barabara na vibali kutoka TFDA.Aliwasihi viongozi wa wilaya ,halmashauri kuandika barua moja kwa moja kwa taasisi husika watatue matatizo hayo ili kuwavutia wawekezaji ."Official communication itasaidia kuliko kusumbua sana hawa wawekezaji ,,itakuwa rahisi kufanya ufuatiliaji na kuzibana taasisi husika na kuzisukuma zifanye utekelezaji " alisisitiza.

  Awali akitoa taarifa ya kiwanda cha Hunnan Power ,mkalimani wa kiwandani hapo, Suleiman Ramadhani alisema kiwanda kilianza ujenzi Jan 2017 na kuanza uzalishaji September 2017 na kimegharimu dollar milioni mbili na hakijawahi kuuza hata nguzo moja.Alisema kiwanda hakifanyi kazi tangu Jan mwaka huu kwakuwa kinategemea tenda na soko .

  Suleiman alielezea kuwa ,wenye viwanda wanahitaji kujenga kiwanda kingine katika eneo hilo lakini wanashindwa kwasasa hadi hapo watakapopata wateja .Mhandisi wa udhibiti wa mapato Tanesco mkoani Pwani ,Fabian Rukiko ,alisema hawajawahi kutumia nguzo za zege mkoani hapo hadi hapo itakapohitajika.

  Alikishauri kiwanda hicho kujitangaza kupitia kitengo cha mauzo na masoko kwani itasaidia kufanya ufuatiliaji na kushirikiana na wadau wakubwa watakaoweza kununua bidhaa hiyo muhimu ambayo inadumu kwa kipindi kirefu.Mwezi Novemba 2017, waziri wa Nishati Dk.Merdard Kalemani alitembelea kiwanda cha nguzo za zege kilichopo Fukayosi na alilitaka shirika la umeme Tanesco kutumia nguzo zinazozalishwa nchini kwenye ujenzi wa miradi mikubwa.

  Nanukuu":"baada ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa nguzo za umeme toka nchi za nje na kuruhusu wawekezaji kutengeneza nchini, sasa umefika wakati TANESCO ianze kutumia nguzo za zege kuanzia Desemba 2017 kwenye miradi mikubwa";alisema.
  Kiwanda cha Hunnan Power kinachotengeneza nguzo za zege mjini Kibaha, kikionekana kutoweza kuendelea na uzalishaji kutokana na kukosa soko na tenda ,na nguzo zikionekana kubaki chini bila mauzo ,wakati mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,alipofanya ziara yake ya siku moja kutembelea viwanda nane mjini hapo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
  Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,alipofanya ziara yake ya siku moja kutembelea viwanda nane mjini Kibaha ambavyo vingine vianza uzalishaji na vingine vikiwa hatua mbalimbali za ujenzi (picha na Mwamvua Mwinyi)

older | 1 | .... | 1551 | 1552 | (Page 1553) | 1554 | 1555 | .... | 1897 | newer