Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1539 | 1540 | (Page 1541) | 1542 | 1543 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA baada ya kufika kwenye ofisi yake . 
  Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita, 
  Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda akimashukuru Mkuu wa Mkoa baada ya kutembelea miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwenye Wilaya za Bukombe pamoja na Chato. 
  Meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta ,Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya Tatu kwenye baadhi ya maeneo. 
  Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa REA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.


  Na, Joel Maduka,Geita

  Mkoa wa Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kutokana na vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499 ambazo zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.

  Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa kwanza utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo utafanya umeme kuongezeka kwa Asilimia 51 kwa wateja waliopo sasa.

  “Mategemeo yetu ni kwamba mzunguko wa pili ambao unatarajia kuanza mwaka 2019 na kumalizika mwaka 2020 na 2021 utafanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita kupata umeme kwa asilimia mia moja” Alisema Ruweta.

  Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kujua kuwa hakuna fidia ambazo watalipwa kutokana na mradi huo.

  “Wito kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Geita watoe ushirikiano Katika vijiji vyote ambako wataalamu wetu watapitia wajue kuwa hakuna fidia kwasababu mradi huu utakuja kwaajili ya kutupatia maendeleo na unapowasha umeme itasaidia kukua kwa uchumi wa eneo husika na Mkoa wetu” Alisema Luhumbi. 

  Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa REA Gedion Kaunda alisema hadi sasa hivi bado hawajaona tatizo lolote ambalo lipo kwenye mradi huo na kwamba wanaamini watafanikisha kwenye maeneo yote ambayo mradio huo umepangwa kufanyika.

  Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Mkoani Geita unatekelezwa na mkandarasi aitwaye White city Guangdong JV ambaye ni ubia wa Kampuni ya Kitanzania na Kampuni ya nje na unatarajia kugharimu zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 61 na fedha za Kimarekani Dola milioni 7.8.

  0 0

    TRA 8TRA2
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akisisitiza jambo wakati alipokutana na Makamu Kamishna wa Idara ya Huduma za Forodha Korea, Roh Suk-Hwan (kushoto) pamoja na ujumbe wake jijini Dar es Salaam ili kujadili maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Idara hiyo, ikiwemo Mfumo wa Uondoshaji Mizigo Bandarini (TANCIS) na dirisha moja (Single Window System). 

  0 0

  Na Ripota wetu, Same

  Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule ameagiza wa Kata ya Bombo awekwe ndani chini ya ulinzi mkali kwa saa 8 kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Bombo na kumtaka apewa siku 2 kuleta maelezo kwa nini asichukuliwe hatua.

  Dc Sinyamule, amefikia uamuzi huo mara baada ya wataalamu wa kutaka hela za kujenga bweni la Shule ya sekondari ya Bombo zihamishiwe shule nyingine kutokana na wananachi wa kata ya Bombo kutotoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa bweni hilo unakamilka.

  "Fedha za serikali ( P4R) zilipelekwa tangu mapema 2017 na mradi ulitakiwa kuisha Nov. 2017 na Ikitegemewa kuwa kuanzia hapo ujenzi wa bweni uanze na mpaka leo nimefika hapa March 2018 bado hata msingi haujakamilika kujengwa na kutoa sababu zisizo na tija.

  Mtendaji huyu ameshindw akusimamia Vizuri majukumu yake ya kuhamasisha watu kushiriki katika miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa bweni la shule hii ambayo serikali ilishatoa fedha kilichotakiwa ni nguvu ya wananchi.

  Amesema kuwa Wananchi wa eneo la Bombo hawajitokezi kwenye kusaidia kazi. na Mtendaji kama muhamasishaji hajitumi, hivyo nimeamuru awekwe chini ya ulinzi masaa 8 kwani hela za Serikali zakaa bila kazi kwa muda mrefu. Zaichafulia jina Wilaya yangu , Kwani tunaonekana wote ni wazembe.

  Dc Sinyamule amesema ni heri tushauri hela hizi zihamishiwe mahali ambako wananchi wako tayari kupokea maendeleo na kushiriki; kwani wanaohitaji fedha hizi ni wengi kwani Viongozi wa kisiasa hawatoi ushirikiano, na wanachangia kufanya kazi ichelewe.

  Amesema Serikali ya CCM ina dhamira njema na haina ubaguzi katika maendeleo. lakini wanaoletewa maendeleo wanaleta uzembe; nitamshauri Waziri hela hizi zipelekwe kumalizia shule ambazo wananchi wameshajitolea zinangoja umaliziaji. 

  DC Sinyamule ametaja kuwa shule hiyo ililetewa Tshs Milioni 245 kwa ajili ya kujenga madarasa 4, choo na mabweni 2. Ambapo tangu Aug. 2017 kazi ya ujenzi wa madarasa ilikuwa imekamilika. Lakini baada ya hapo hakuna kilichofanyika kwa miezi 7 sasa huu sio utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua Msingi wa Bweni la Shule ya Sekondari Bombo Wialayani hapo ambao umekwama tangu 2017 kutokana na Wananchi kushindw akujitokeza kuchangia ujenzi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akikagua, akiwa ameongozana na Wataalamu kutoka Wilayani kukagua Madarasa yaliyojengwa tangu 2017 bila kukamilika.

  0 0

  Wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya chumvi ya Gendabi Wilayani Hanang' wanatarajia kunufaika na rasilimali hiyo, baada ya Serikali kupata mwekezaji atakayejenga kiwanda cha chumvi eneo hilo.

  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza jana kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano wilayani humo alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa watakaokwamisha mradi huo. Mnyeti alisema wapo baadhi ya wanasiasa wanaotumia matatizo ya wananchi kuwa fursa hivyo hawezi kukubali wakwamishe mradi huo mkubwa wenye faida kwa jamii.

  "Nimesikia hapa kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia shida za watu kujinufaisha kisiasa, sasa nikimkuta anapinga hili nitamshughulikia bila kujali chama chake,," alisema Mnyeti. Alisema kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji hivyo wananchi wa eneo hilo wajiandae kunufaika kiuchumi kwa kuchimba chumvi kwa wingi na kuuza kiwandani hapo.

  "Haya ndiyo maendeleo tunayosema siyo siasa za maji taka kwani chumvi itakuwa na thamani kubwa tofauti na hivi sasa kwani kiwanda kitawanufaisha," alisema Mnyeti. Aliwataka wananchi wa eneo hilo kujiweka tayari na uwekezaji huo ili kuhakikisha uzalishaji unafanyika wa kutosha kwani soko la uhakiki litakuwepo kwa kadiri watakavyofanya uzalishaji.

  "Suala la miundombinu ya barabara watu wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (Tarura) wametuhakikishia kufanikisha hilo ili uwekezaji huo usikwame," alisema Mnyeti. Mkazi wa eneo hilo Paulo Baso alisema wanakabiliwa na baadhi ya changamoto kwenye machimbo ya chumvi ikiwemo miundombinu na soko la uhakiki la kuuza chumvi hiyo.

  Baso alisema pia vifaa vya kuchimbia chumvi hivyo ni tatizo kwani vyombo vya kutolea chumvi bado ni tatizo ila kupitia kiwanda hicho wanatarajia kuongeza kipato chao. Alisema hata bei ya chumvi hiyo inazidi kushuka kutokana na soko kwani gunia moja hununuliwa kwa sh1,000 badala ya sh5,000 iliyokuwepo awali.

  Mwenyekiti wa CCM wilayani Hanang, Mathew Darema alisema tatizo la ukosefu wa soko la chumvi linawakabili wachimbaji wengi wanaojishughulisha na shughuli hizo. "Tunamshukuru mkuu wetu wa mkoa kwa kufanikisha uwekezaji huu mzuri ambao kwa namna moja au nyingine utanufaisha jamii ya eneo hili kwa kuongeza ajira," alisema Darema. 
   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiangalia kiatu kilichotengenezwa na kikundi cha Datoga cha Wilayani Hanang kinachotengenezwa vifaa vinavyotokana usindikaji wa ngozi.
   Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akipokea heshima kutoka kwa skauti mara baada ya kuwasili Wilayani Hanang jana alipoanza ziara ya siku tano, ya kutembelea wilaya hiyo kwa kuzungumza na wananchi, kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero zao. 
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, (kushoto) akizungumza jana kwenye eneo la kuhifadhi dawa baada ya kukagua mazingira ya hospitali ya Wilaya ya Hanang kwenye ziara yake ya siku tano.  


  0 0


   Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto) wakizindua rasmi Tovuti ya MISA Tanzania inayopatikana hapa www.tanzania.misa.org
   Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto)pamoja na wadau mbalimbali ambao hawapo pichani wakipata maelezo kuhusiana na Tovuti ya MISA Tanzania kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa 
  Sengiyumva ambaye hayupo pichani.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva(kulia) kulia akiendelea kutoa maelezo mbali mbali na vitu ambavyo vinapatikana katika Tovuti ya MISA Tanzania 
   Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Tovuti ya MISA Tanzania Jijini Arusha.

  0 0

   Meneja wa Tawi la NBC mjini Moshi, Salma Yatera (kushoto), akikabidhi kadi ya usajili wa gari jipya aina ya Suzuki Carry kwa Lucina Massawe baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni. Anayeangalia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi. NBC imetoa zawadi ya magari sita katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu.
   Meneja Masoko wa NBC (kutoka kushoto), Meneja wa NBC Tawi la Moshi, Salma Yatera, mshindi wa zawadi ya gari jipya aina ya Suzuki Carry ya kameni ya akaunti ya Malengo, Lucina Massawe na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Flbert Mponzi, wakishangilia mara baada ya mshindi huyo kukabidhiwa gari lake mjini Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni. NBC imetoa zawadi ya magari sita katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu.
   Meneja wa Tawi la NBC mjini Moshi, Salma Yatera (kushoto), akikabidhi kadi ya usajili wa gari jipya aina ya Suzuki Carry kwa Lucina Massawe baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni. NBC imetoa zawadi ya magari sita katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu.
   Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (kushoto), akikabidhi kadi ya usajili wa gari jipya aina ya Suzuki Carry kwa Lucina Massawe baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni. NBC imetoa zawadi ya magari sita katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu.
  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (kushoto), akikabidhi kadi ya usajili wa gari jipya aina ya Suzuki Carry kwa Lucina Massawe baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni. NBC imetoa zawadi ya magari sita katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Kulia ni Meneja wa NBC Tawi la Moshi, Salma Yatera.

  0 0

  Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr, Rashid Mfaume (wa tatu kushoto) akifungua zoezi la uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno kwa watoto waliopo katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara . Kuanzia kushoto ni Kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Arnold Mtenga, Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana na kushoto kwa mgeni rasmi ni Daktari wa Meno Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr. Nuru Mpuya. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 
  Mlezi Jackson Leonard (kushoto) na Mlezi Flora Kankutebe wakifatilia jambo wakati watoto hao walipokuwa wakifanyiwa uchunguzi huku watoto wendine wakiwa katika msitari wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
  Dakt. Bingwa wa Magonjwa ya Kinywa na Meno kwa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr, Conrad Mselle akimpati uji mmoja wa watoto hao huku wengine wa kiwa katika msitari wakisubiri na wao kupatiwa uji
  Mwalimu msaidizi wa kituo hicho, Mohamed Makana akiwakaribisha wageni na kutoa utangulizi wa kituo hicho
  Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr, Rashid Mfaume (wa pili kulia) mstari wa mbele katika picha ya pamoja na madaktri hao 
  Dakt. Bingwa wa Magonjwa ya Kinywa na Meno kwa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr, Conrad Mselle akionyesha kwa mfano namna nzuri ya upigaji mswaki kwa Zephania Bahebe mmoja kati ya watoto wanaoishi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, Mkoani Shinyanga katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, Ambapo Kitaifa yatafanyika Machi 20, 2018,Tarime Mkoani Mara
  Kiongozi wa msafara ambaye pia ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Arnold Mtenga akimfanyi uchunguzi wa kinywa mmoj wa watoto hao waishio kituoni hapo, Peter Tito , kulia anaye andika ni Daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Habiba Madjapa
  Kiongozi wa msafara ambaye pia ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Arnold Mtenga akizungumza n waandishi wa habari 
  Daktari wa Meno Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr. Nuru Mpuya akizungumza na waandishi wa habari.

  0 0

  Je wajua yakuwa unaweza baadilisha maisha na mtandao wa simu? Hebu angalia video hii kujua wengine wamefanyaje?

  0 0

  Na John Nditi, Morogoro

  WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema ili kuleta  ufanisi mkubwa katika usimamizi  wa miradi ya maji safi na salama  vijijini, ipo haja ya kuwa na chombo cha kusimamia  huduma za maji vijijini utakaosimamiwa na wizara kwa lengo la kuleta uwajibikaji wa karibu kwa watumishi wanaosimamia sekta ya maji nchini.

  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso alisema hayo  kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali kikiwemo cha Dumila juu katika Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

  Kabla ya kuzungumza na wananchi  alipata fursa ya  kukagua ujenzi wa mradi wa maji Dumila  ambao ulianza kujengwa tangu Januari 24, 2014 na kukamilishwa Desemba 15, 2017 kwa gharama ya Sh milioni 800.5.

  Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya wiki moja  mkoani Morogoro  iliyomfikisha katika   halmashauri za wilaya sita  kati ya tisa ambazo ni  Malinyi, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Manispaa ya Morogoro na Kilosa .

  Alisema  kuwa,  miradi mingi ya maji safi na salama inayotekelezwa vijijini imekosa usimamizi wa karibu, ufanisi na mingi imejengwa chini ya viwango na baadhi katika maeneo ambayo vyanzo vyake vya maji si  vya kuaminika.
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuwapelekea mafundi wa ujenzi  kwa ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 katika mji wa Malinyi, ( kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda akichanganya saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi huo.
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuchanganya mchanga na saruji  kwa  ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 mjini Malinyi na ( kushoto kwake ) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda ,  na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.
  Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso,  akimsiliza Mzee Said Mazinge  wa  Kata ya Kibati, wilaya ya Mvomero , mkoa wa Morogoro  kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama  alipofanya ziara  wilayani Mvomero. .
   Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa mji wa Mlimba , wilaya ya Kilombero  juu ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa maji maeneo ya vijijini na mijini.
   Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso  akipambu maji katika moja ya kisima kirefu  mara baada ya kukizundia katika kijiji cha Chikuti, wilaya ya Ulanga kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa kijiji hicho .


  0 0

    Shirika la Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo. 

   Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.
  Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.

  "Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu waitumie.""Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier. 

  Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TaESA Boniface Chandaruba


  *Ni kwa ajili ya kupata kazi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta Tanzania-Uganda

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaESA) umetangaza kuanza kwa mchakato wa utambuzi wa Watanzania wenye taaluma na ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi ambapo mwisho wa usajili ni Machi 30 mwaka huu.

  Mchakato wa utambuzi huo ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga nchini.

  Akizungumza Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Boniface Chandaruba amesema kuwa ili kuhakikisha Watanzania wengi wananuifaka na fursa za ajira zitokanazo na mradi wa bomba la mafuta TaESA imepewa jukumu la kuhamasisha wote wenye taaluma na ujuzi nchini katika sekta ya mafuta na gesi wajitokeze.

  “Hivyo tunaomba Watanzania wenye sifa kuja kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye kanzidata ya Wakala kwa lengo la kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi wa ujenzi wa bomba hilo.

  “Usajili huu unafanyika bure ,hivyo tunasisitiza hakuna gharama yoyote itakayotozwa kwa Mtanzania yeyote atakayehitaji kusajiliwa.Maelezo ya kina kuhusu aina ya fursa za ajira zinazotegemewa kutolewa yanapatikana katika tovuti ya Wakala ya www.taesa.go.tz,”amesema .

  Chandaruba amesema mchakato wa usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana kupitia tovuti ya Wakala au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizopo Dar es Salaam,Arusha, Dodoma na Mwanza.Pia amesema fumu hizo zinapatikana kwa barua pepe eacop@taesa.go.tz na kwamba mchakato wa usajili unatarajia kumalizika Machi 30 mwaka huu.

  Ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania wote kuwa watumishi wa TaESA ni wanazingatia maadili ,hivyo hakuna rushwa ya aina yoyote kwa mtanzania ambaye anataka kujisajili.Kuhusu idadi ya ajira ambazo zitapatikana kwenye mradi huo, Chandaruba amesema unategemewa kuzalisha ajira 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1000 wakati wa uendeshaji wake.

  Amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba hilo la kusafirisha mafuta ni moja ya mradi mkubwa kutekelezwa hapa nchini na unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 3.5 sawa na Sh.trilioni 8.“Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba utafanyika nhini Tanzania.Jumla ya Wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa nane,”amesema.

  Ametaja mikoa hiyo ni Kagera, Geita, Shinyanga,Tabora,Singida,Dodoma,Manyara na Tanga.Amefafanua licha ya bomba kupita kwenye maeneo hayo lakini ajira zitatolewa kwa Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini.

  Alipoulizwa kama ndio wanatangaza sasa au walishatangaza siku za nyuma kuhusu watanzania kujisajili , amejibu kuwa ujenzi wa bomba hilo umekuwa ukizungumzwa kwa nyakati tofauti na hivyo kila eneo limekuwa likitangaza, lakini wao ambao ndio wakala wa ajira nao wanayo nafasi ya kuufahamisha umma.

  Hivyo siku 16 ambazo zimebaki zinatosha watu kujisajili hasa kwa kuzingatia teknolokia ya habari na mawasiliano imerahisisha na kufafanua tayari wananchi walishaanza kujaza fomu na kuzipeleka kwenye wilaya na mikoa na sasa wanaotuma maombi hayo watajua wenye jukumu hilo ni TaESA.

  Kuhusu TaESA amesema walianza kutoa huduma mwaka 2008 ambapo moja ya majukumu yake ni kukusanya,kuchambua na kusambaza taarifa za soko la ajira, pia kuendesha mafunzo kwa watafuta kazi ili kuwajengea uwezo na mbinu za kutafuta kazi na kuajirika.

  Amezungumzia changamoto ya soko la ajira duniani, na kutumia nafasi hiyo kuwashauri wasomi nchini kuwa kutumia elimu ambayo wameipata kujiajiri na hatimaye nao kutoa ajira kwa wengine na kuongeza jukumu la Serikali ni kuandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha Watanzania kujiajiri.

  Amesema kwa mwaka idadi ya wasomi wanaohitimi vyuo vikuu ni 600,000, hivyo kwa idadi hiyo unaweza kuona soko la ajira serikali halitoshi, hivyo ni vema jamii ikaanza kubadili fikra kwa kutambua badala ya kusubiri ajira serikalini wakatumia elimu wanayoipata kujiajiri.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amewashauri Wasimamizi na waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini( TASAF) kushirikiana na viongozi wa vijiji na wataalamu wa aridhi kuanzishisha miradi itakayokuwa endelevu ambayo itakawaondoa haraka wanufaika wa mfuko huo.

  Polepole ametoa kauli hiyo jana akiwa kwenye ziara yake ya mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea wanufaika wa TASAF katika Kijijji cha Nyabitaka wilayani Kibondo mkoani Kigoma.Alipata nafasi ya Shamba darasa lenye hekari mbili la kilimo cha mseto kinachosimamiwa na wanufaika hao.

  Polepole amewashauri waratibu wa TASAF kushirikiana na watalaamu wa aridhi na viongozi wa vijiji kutenga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya wanufaika badala ya kuwapatia Sh.40,000 kwa kila mwezi.

  "Wasikisimamiwa vema kwenye kilimo watapiga hatua za kimaendeleo haraka zaidi na baada ya mwaka mmoja wanafuika hao hawatakuwa masikini tena.Hivyo ni vema mkaangalia mbinu sahihi za kuwaondoa wanufaika hawa kwenye umasikini,"amesema Polepole.

  Amesema Serikali ya CCM imeandaa mpango huu wa maendeleo kwa ajili ya kunusuru kaya masikini na lengo ikiwa ni kuwainua watu watoke kwenye umasikini uliopitiliza na kufafanua mwaka 2025 mpango huo wa TASAF utakwisha endapo utamalizika na wananchi hawajapatiwa miradi ya kujikwamua na umasikini itakuwa haijasaidia chochote.

  Amewaahidi wananchi wilayani Kibondo kuwa Serikali ya Awamu ya tano ya CCM itatoa Sh.milioni 52 kwa ajili ya wananchi wakopeshwe kwa lengo la kuwaondoa kwenye umasikini na kuwaomba watendaji na wenyeviti wa vijiji kuandaa utaratibu bora wa kuwakopesha Wananchi hao kwa utaratibu mzuri.

  Kwa upande wa Mratibu wa TASAF mkoani Kigoma Jailos Pilla aMEsema utaratibu wa mfuko huo ni kuwa Wanufaika kubuni mradi wa maendeleo.Hivyo baada ya kubuni mradi na kuwezeshwa na TASAF baadae mradi unakuwa mali ya Serikali ya kijiji.

  Amesema kila mnufaika anatakiwa kujifunza kupitia miradi hiyo inayoanzishwa ili aweze kuanzisha nyumbani kwake ili ajikwamue katika umasikini.Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Lucia Mihayo amesema fedha alizozipata alizitumia kununa tofali na bati na mpaka sasa ameanza ujenzi wa nyumba ya bati ili aishi vizuri yeye na familia yake.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya umeme kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa,  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wabunge waliofika kwenye uzinduzi wa Reli hiyo ya Kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Reli hio ya Kisasa katika eneo la Ihumwa Stesheni mkoani Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru madereva wa magari yatakayofanya kazi ya ujenzi wa reli hiyo ya kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.
   Sehemu ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
    Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika eneo la Ihumwa Stesheni kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi.
  Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa Reli ya kisasa ya umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli PICHA NA IKULU

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akitia saini makubaliano ya Mashirikiano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuhusu uanzishwaji wa Kliniki ya utoaji matibabu kwa Wagonjwa wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (aliyesimama kulia) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdallah.
  Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Kippi Warioba na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini .

  NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .
  SEKTA ya Utalii nchini imepata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru .
  Changamoto hiyo inafika kikomo rasmi baada ya kampuni ya Kilimanjaro SAR kuzindua Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na muinuko wa juu pamoja na utumiaji wa Helkopta kwa ajili ya uokoaji katika Hifadhi za Mlima Kilimanjarona Mlima Meru.
  Mbali na uzinduzi huo Kilimanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi ,kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima hiyo.
  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni ya Kilimanjaro SAR na Hospitali ya St Joseph ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba aliyekuwa mgeni rasmi amesema hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro.
  Huduma hii ya kwanza kutolewa barani Afrika inaiweka Tanzania katika nafasi ya pili katika Ramani ya Dunia, kuwa  na kliniki ya kipekee katika utoaji wa huduma kwa wapanda Mlima na kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuongeza idadi ya Watalii. 
  Hata hivyo kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
  Ulbanie Lyimo ni mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph akaeleza faida itakayopatikana kutokana na kuingia makubaliano na kampuni hiyo ya Uokoaji ya Kilimanjaro SAR kuongeza maarifa katika utoaji wa matibabu kutoka kwa madaktari wa kigeni watakao hudumia wagonjwa wa Mlimani.
  Kuanza kwa kliniki hii ni msaada kwa maiha ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro na Meru ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.

  0 0  Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia wakati alipomtembelea ofisini kwake kufanya mazungumzo naye pia alitembelea Kituo cha kufufua umeme kwa njia ya Maji kilichopo Hale wilayani Korogwe

  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho
  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili kutoka kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia kitu wakati walipotembelea kituo hicho
  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakiangalia mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakati walipotembelea kituo hicho kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe,Rehema Bwasi
  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wa pili katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto wakitembelea mitambo iliyopo kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakati walipotembelea kituo hicho
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Meneja wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kulia ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kulia
  Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme kutoka Tanesco Makao Makuu Bakaya Mtamakaya akizungumza wakati ziara hiyo ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt kushoto kulia ni Meneja wa Uzalishaji wa Kituo cha Pangani Hydro Systems
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao cha pamoja mara baada ya Balozi huyo wa Sweden kutembelea kituo hicho cha Uzalishaji wa Umeme kulia Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt
  Meneja Uzalishaji wa Pangani Hydro Systems Mhandisi Stephen Mahenda kushoto akiteta jambo na na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt kushoto

  Balozi wa Sweden nchini Katarina Rangnitt akitembelea maeneo mbalimbali kwenye kituo hicho.


  SERIKALI ya Sweden imetoa kiasi cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na dola za Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani Tanga.

  Hayo yamebainishwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga. Amesema kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

  Amesema kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha katika kukarabati mgodi huo." Nishati ni jambo muhimu katika maendeleo ya viwanda na Tanzania tayari imeweka mikakati mizuri katika maendeleo ya viwanda hivyo,serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha kwa kukarabati mgodi huo "alisema.

  Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amemshukuru balozi huyo kwa serikali ya Sweden kufadhili mradi huo,pia amemkaribisha balozi huyo kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na uchumi." Nawashukuru serikali ya Sweden kwa kufadhili mradi huo na mheshimwa Rais ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji mkoani Tanga haswa katika sekta ya viwanda hivyo karibuni Tanga mje kuwekeza" alisema.

  Kwa upande wake Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Hale Mhandisi Steven Mahemba amesema kuwa mtambo huo umepunguza uzalishaji kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa mitambo.

  " Kituo hiki kimejengwa kuanzia mwaka 1962 na kumalizika mwaka 1964 na kina muda wa takribani miaka 52 hivyo pia kutokana na uchakavu wa miundombinu take imepunguza uzalishaji kutoka megawati 21 mpaka 4 hadi 8" alisema.

  Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka mitatu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina ambaye pia ni mwenyekiti wa Ka  mati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo akizungumza na wachimbaji wadogo wakati wa kikao cha kujadili soko la madini ya dhahabu kilichofanyika Mkoani Geita .
  Katibu msaidizi wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo,Bw Gregory Kibusi akijitambulisha na kuelezea lengo ambalo limewapeleka Mkoani Geita mbele ya Afisa madini wa Mkoa huo. 
  Afisa madini Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akizungumza na Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo ambao walikuwa wamewasili kwenye ofisi za madini Mkoani Humo. 
  Bw,Nuru Shabani ambaye ni mchimbaji mdogo akionesha kemikali ambayo amekuwa akiitumia kukamatia madini kwenye eneo la mgodi wake. 
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye pia ni mchimbaji ,Bw Leornad Kiganga Bugomola akiwakaribisha wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa madini. 
  Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale ambaye pia ni mchimbaji na Mjumbe kwenye kamati hiyo,Hussen Nassoro Kasu akiwataka wachimbaji kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kwenye shughuli zao. 
  Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa kwenye kikao hicho.


  Na Joel Maduka,Geita

  Serikali kupitia Shirika la Viwango nchini, TBS limetakiwa kuchunguza kemikali bandia zinazouzwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wachimbaji wadogo wa madini hali inayosababisha hasara kwa wachimbaji hao.

  Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini, (FEMATA) Bw John Bina amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha wachimbaji wadogo Mkoani Geita kwa lengo la kujadili namna Serikali inavyoweza kufanikisha ujenzi wa soko la madini kwa kanda ya ziwa.

  Alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza kemikali bandia kwa wachimbaji wadogo na hivyo kuwasababishia hasara.“Tunaomba serikali na TBS kuangalia sanaa haya madawa ambayo yanaingia nchini kuhakikisha wanachunguza kemikali hizi kwani kwa sasa uzalishaji unashuka kwa kiasi kikubwa wa madini ,na nyie wachimbaji niwaombe muwe mnachunguza kabla ya kununua kwani kweli mnaingia hasara kubwa sanaa”Alisisitiza Bina.

  Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Bw Nuru Shabani alisema kwa kuuziwa Kemikali hizo bandia amekuwa akiathirika katika shughuli zake.“Kiukweli tunaathirika sanaa na hili halina ubisha sasa hivi unaweza kununua tani moja ya kaboni unakuta inapitisha bila ya kushika mali inamaana hadi iwe na pipim kuanzia mia saba hadi mia nane ,Ila kwa sasa nashukuru walau serikali imetambua mchango wetu na imetuthamini mimi nilikuwa naomba kupitia Kitengo chetu tuwe na wasimamizi ambao watatusaidia kubaini kemikali hizi”Alisema Nuru.

  Bw John Bina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia kero za wachimbaji wadogo alisema pamoja na matatizo hayo lakini wachimbaji hao wamekubaliana kuanzishwa kwa soko la madini Mkoani Mwanza ili kudhibiti vitendo vya utoroshwaji wa madini.

  0 0

  Serikali imesema inajiandaa kuupokea mradi wa ‘Global Learning XPRIZE’ unaowawezesha watoto walio nje ya mfumo rasmi kujifunza stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kupitia Michezo iliyowekwa kwenye tableti, kutoka kwa wadau wanaoufadhili baada ya kumalizika muda wa majaribio. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali. 
  Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi akizungumza kuhusu maandalizi ya serikali kuupokea mradi wa Global Learning XPRIZE.

  “Kama serikali mradi unapomalizika tunaangalia namna ya kuuendeleza. Tutaendelea kushirikiana na halmashauri zetu zilizoko kwenye mradi wauone kama ni wa kwao na kwamba badala ya watoto kuzurura mitaani wanaendelea kujifunza,” amesema Mushi na kuongeza. “Tunaagiza wale wahusika, wadau wa elimu katika ngazi zote za kijiji hadi mkoa wa Tanga waone kama hiki kilicholetwa kwetu ni zawadi,na ni lazima kuuendeleza ili kupunguza watoto walioko nje ya mfumo rasmi; kwa maana hiyo inatakiwa tuwe na ushirikiano kuona changamoto baada ya huu mradi kumalizika ili kuzifanyia kazi.” 
  Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

  Akielezea utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza na ulipofikia, Afisa Msaidizi wa Mradi kutoka UNESCO, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 2000 kutoka vitongoji 141 katika wilaya 6 za mkoa wa Tanga wamenufaika na mradi huo. “Baada ya miezi 15 ya mradi kukamilika, mradi utakabidhiwa kwa serikali ili kuendelea kuusimamia, ambapo tumekutana leo Tarehe 13/3/2018 na wawakilishi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (BMT) , Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na TAMISEMI ili kuweza kuangalia ni jinsi gani watoto walio katika mradi wataingia katika mfumo rasmi katika ngazi husika,” amesema. 
   Wadau mbalimbali wakichangia katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.
     
  Washiriki wa mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

  0 0


  0 0


  Robert Butambele (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Sinza, Dar es salaam akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni kumi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Butembele aliibuka mshindi wa kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.
  Said Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini, Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.
  Baadhi ya mawakala mbali mbali walioshinda zawadi katika promosheni ya mawakala wa Tigo pesa iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo. Hii ilikuwa baada ya kupokea zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo.

  Wakala wawili (2) washinda TZS 10 millioni na TZS 5 millioni kila mmoja.
  Nane (8) wapata TZS 3 millioni na TZS 2 millioni kila mmoja, huku mamia wengine wakizoa zawadi na bonasi lukuki


  Dar es Salaam, 14 Machi, 2018.


  Kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.

  Wakala RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.

  Pamoja na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.

  Mojelwa Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.

  Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema kuwa lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni kuwadhamini na kuwashukuru mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini.

  “Ningependa kuwapongeza mawakala wetu kwa kazi kubw wanayofanya ya kuhakikisha kuwa huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’ alisema.Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.

  Kampuni ya Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.

  Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.

  0 0

  Na: Veronica Kazimoto

  Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wameombwa kuwa mabalozi wazuri katika sehemu zao za kazi na katika jamii wanayoishi kwa kuwaelimisha wananchi masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

  Akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Kodi kwenye Kikao Kazi cha Maafisa hao kinachoendelea  jijini Arusha , Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo, alisema elimu ya kodi itawafikia watu wengi zaidi kwa kuwa maafisa hao wana ushirikiano mkubwa katika kutoa habari sahihi kwa umma.

  "Kila mmoja wetu anachokifanya ni sauti kwa mwenzake mahali alipo, ndio maana hata katika mitandao mbalimbali tumekuwa tukisaidiana kwa kuwa, ukiona jambo baya linasemwa juu ya taasisi ya mwenzako au Serikali unamsaidia kutoa ufafanuzi, hivyo, mkielewa mada yangu hapa, najua mtanisaidia kuelimisha masuala ya kodi katika sehemu zenu za kazi na maeneo mengine", alisema Kayombo.

  Kayombo alisema kuwa, maafisa hao wana nafasi kubwa katika kuelimisha jamii na kusahihisha baadhi ya wananchi ambao wanakuwa na elimu isiyo sahihi kuhusu masuala yanayohusu kodi na ukusanyaji wa mapato kwa ujumla. 

  Aidha, pamoja na mambo mengine, Richard Kayombo aliwakumbusha Maafisa hao suala zima la kudai risiti kila wakati wanaponunua bidhaa ili kuchangia maendeleo ya nchi.
  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo, akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Kodi kwenye Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kinachoendelea jijini Arusha.  Kikao hicho kinatarajia kumalizika tarehe 16 Machi, mwaka huu. (Picha na Benedict Liwenga).


older | 1 | .... | 1539 | 1540 | (Page 1541) | 1542 | 1543 | .... | 1897 | newer