Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA UYOVU-BWANGA KM 45 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika eneo la Uyovu mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika eneo la Uyovu mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Uyovu mkoani Geita kabla ya kufungua rasmi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi wakati akitizama kwaya ya Baraka ilipokuwa ikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanakwaya ya Baraka wakati alipowasili Uyovu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyakayondwa Bangwa mkoani Geita wakati akielekea Uyovu kwa ajili ya ufunguzi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Uyovu mara baada ya kufungua Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. PICHA NA IKULU.

SOARING WOMEN INTERNATIONAL WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2018

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha. Hayo yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Amesema kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi au za ubunifu za kuweza Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale walioasisi. 
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soaring Women International, Luphurise Lema amesema kuwa wakati alipokuwa anafanya kazi aliona kuwa watu waliosoma nje ya ndio wana akili lakini alitambua kuwa sio hivyo tofauti yake ni kujiamini tu na kuamini kila kinachofanyika hata mwanamke anaweza. Luphurise amesema kuwa kila mwanamke asimame imara na kuamini kila anachofanya anaweza kuleta mabadiliko hata ya dunia. 
Nae mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ ambaye ni mchora katuni na mtangazaji wa Cloud Radio/Tv ja ya Watengeneza mjadala, Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ amesema kuwa wanawake ni watu muhimu na majukumu anayofanya mwanamke akipewa mwanaume hawezi kuyafanya isipokuwa alioanzisha kauli kuwa hawawezi ndio imewafikisha wanawake lakini wakaze buti wanaweza kuleta mabadiliko. Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soaring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soaring Women International, Luphurise Lema (kushoto).



Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto) na Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia).

Mchangiaji wa Shirika la AMREF, Dk. Florence Temu akichangia mada katika siku wanawake duniani.

Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko akichangia mada katika siku wanawake duniani.
Waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja.
Meneja wa Udhibiti wa Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta - Yambi akitoa shukrani zake kwa wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Soring Women International, Luphurise Lema akitoa shukrani za pekee kwa wadau waliojitokeza kumuunga mkono katika shughuli yake ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Dunia aliyoiandaa jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa Vikoba nchini Tanzania, Devota Likokola akichangia mada.

Akinamama waliohudhuria katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

JAFO AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo ameongoza zoezi la kufanya mazoezi kwa watumishi wa Wizara hiyo na Taasisi zake za Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mfuko wa Pension wa LAPF, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB), Wakala wa Barabara za Vijijini(TARURA) na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) huku akitoa wito kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.

Mazoezi hayo yamelenga kujenga afya kwa Watanzania na kujiondoa katika hatari ya magonjwa nyemelezi ambapo michezo ya Soka, Riadha, kutembea kwa kasi na Kuvuta kamba ilishindaniwa.

Mhe. Jafo ameambatana na Viongozi wengine wakiwemo Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Zainab Chaula, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deogratius Ndejembi na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Dodoma, pia baadhi yakazi wa Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa, Jafo alisema Watanzania wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuiweka miili yao vizuri na ametoa agizo kwa ofisi yake kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara moja ili kufahamiana pamoja na kujenga hamasa ya kufanya kazi.

“Haya mazoezi tunamuunga mkono Makamu wa Rais Mama Samia katika juhudi zake za kufanya mazoezi,mazoezi ni muhimu kwa afya sasa kila mwezi tutakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi ili kuongeza hamasa ya kufanya kazi,”alisema.Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda alitoa dua maalum ya kuombea wote waliohudhuria, Mhe. Rais John Magufuli na kumshukuru Mhe. Jafo kwa kuandaa bonanza hilo ambalo linaleta hamasa, upendo na mshikamano wa watumishi Umma na watanzania.

Naye Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Afya, Dk.Zainabu Chaula alimshukuru Jafo kwa kuandaa mazoezi hayo kwani yatawasaidia k kujenga afya pamoja na kupongeza hamasa ya kufanya kazi.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Mahenge alisema kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi ni lazima kuwe na viwanja bora vya Michezo.

“Mheshimiwa Rais ameanza ujenzi wa Uwanja wa michezo wa Kisasa katika eneo la Nzuguni lazima tumuunge mkono kwani tunataka Mkoa wa Dodoma uwe wa kuvutia hivyo ni lazima kuwe na viwanja vingi vya michezo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa wizara yake.

MNEC SALIM ASAS BADO ANAUMIZWA NA USHINDI WA MBUNGE MSIGWA WA MWAKA 2015

$
0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) MNEC Salim Asas  akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015
 Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi(CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.

Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa  ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na  chama cha mapinduzi zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.

“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.

“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo

Jongoo alimshukuru MNEC kwa kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.

“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo
kawaida:

RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA ISAKA-USHIROMBO, AZUIA WANANCHI KUHAMISHWA KUPISHA UJENZI WA CHUO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, Leo 10 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Sehemu ya mamia ya wananchi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli  wakati wa sherehe za uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, Leo 10 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Kahama-Geita 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Leo 10 Machi 2018 amezindua barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132 iliyojengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami.


Katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo katika Eneo la Nyasubi, Kahama Mjini Mhe Rais Magufuli amesema kuwa Barabara hiyo ni chachu ya ukuaji wa uchumi na kiungo cha Mikoa ya Shinyanga, Geita na Kagera pia ni sehemu ya kurahisisha na kuimarisha mahusiano chanya ya kibiashara baina ya nchi za Uganda, Rwanda na Burundi.


Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara nchini kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa kwani serikali inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 269 kununua dawa nje ya nchi hivyo endapo watajenga viwanda hivyo vya dawa serikali itawanufaisha wafanyabiashara wa ndani ya nchi kwa kununua bidhaa hizo.


Kama alivyojipambanua katika kuwatetea wanyonge Mhe Rais Magufuli ameagiza kutohamishwa wananchi waliovamia eneo la ardhi ya Wizara ya Elimu, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (MWAMVA), na kusema kuwa wananchi hao ndio waliompigia kura na hatimaye kuwa Rais wa nchi hivyo hawapaswi kunyanyaswa.


Aidha, aliwataka wananchi wengine kutoendelea na ujenzi wa nyumba za makazi katika Mtaa wa Igomelo, Kata ya Malunga ili eneo lililosalia la hekari 40 ndilo litumike kujenga chuo hicho.


Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewashukuru wabunge wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wabunge wengine wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 ambayo inataka kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi kupitia rasilimali zao.


Aidha, serikali imekuwa ikikusanya mapato mengi kupitia sekta ya madini ambapo mwaka 2014/2015 ilikusanya jumla ya shilingi Bilioni 168.09, mwaka 2015/2016 ilikusanya zaidi ya Bilioni 205, mwaka 2016/2017 ikikusanya jumla ya Shilingi Bilioni 213.365


Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Bugalama (CHADEMA), Katibu mwenezi Kanda ya ziwa  (CHADEMA) na wanachama wengine 50 wamejivua uanachama wa Chadema mbele ya Rais Magufuli na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi huku wakisema kuwa wameridhishwa na utendaji wake katika kuwatumikia watanzania.


Mradi wa ukarabati wa barabara hiyo ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132 iliyojengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami ni sehemu ya barabara kutoka Isaka hadi Lusumo yenye kilomita 1334 iliyokuwa imejengwa mwaka 1980 na mwanzoni mwaka 1990 hivyo imetumika kwa kipindi cha miaka 20 bila kufanyiwa marekebisho.


Dhifa ya uzinduzi wa barabara hiyo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack, Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mhe Elius John Kuandikwa (Mb), Naibu waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale, na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.

FAHAMU CHIMBUKO LA MATIMILA BENDI, NA MIKAKATI ILIYOPO KWA SASA

$
0
0
Kushoto ni Mtangazaji wa Ruvuma TV Nancy Mbogoro akimuuliza swali Mpenda Mvula ambaye ni mtoto wa marehemu Abrose Mvula aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Super Matimila.
..................................
Mtoto wa Mzee Abrose Mvula ambaye ndiye alikuwa mmiliki wa bendi ya Super Matimila aelezea chimbuko la  bendi hiyo , Historia ya bendi,kwa nini iliitwa matimila,ilikuwaje mzee wake akaanzisha bendi hiyo pamoja na historia  ya Remmy Ongala akiwa na bendi ya Matimila na mikakati iliyopo juu ya bandi hiyo kwa sasa.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ISAKA-USHIROMBO KM 132 KATIKA MJI WA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Kahama mara baada ya kufungua barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
 Sehemu ya Wananchi waliofika kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telak wakwanza kushoto, wabunge wa mkoa wa Shinyanga pamoja na Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi CCM waliohamia kutoka vyama vya Upinzani.
 Sehemu ya Barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Kahama mara baada ya kufungua barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Masumbwe Mbogwe mkoani Geita wakati akielekea Kahama mkoani Shinyanga. PICHA NA IKULU

HOTUBA YA MHE DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA BARABARA YA ISAKA USHIROMBO


‘OLE WENU WEZI WA MAJI’-NAIBU WAZIRI AWESO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ametoa onyo kali kwa wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji na kuwataka waache tabia hiyo mara moja kwa kuwa Serikali imechoka kuingia gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya maji na kuhujumiwa.
Hayo yamesemwa wakati alipotembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) wakati akizungumza na Bodi, menejimenti na watumishi wa mamlaka hiyo inayotoa huduma ya maji kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Aweso amesema wizara itaanzisha kampeni kabambe nchi nzima ya kubaini mtandao mzima na wale wote wanaoihujumu Serikali kwa wizi wa maji na miundombinu yake na kuziagiza mamlaka zote nchini kuweka mikakati mizuri ya kudhibiti tabia hiyo.
Amesema miradi ya maji imegharimu fedha nyingi sana ili kuwanufaisha wananchi wote kwa kufuata taratibu za kupata huduma hiyo kihalali na si kinyume na taratibu, akisisitiza kuwa ni haki ya mwananchi kupata maji lakini pia ana wajibu wa kuitunza miundombinu ya maji ili itoe huduma ya uhakika na endelevu.
‘‘Ninatangaza vita na wezi wa maji na wahujumu wa miundombinu ya maji, ole wenu wenye tabia hiyo maana tumechoka kwa kuwa inaturudisha sana nyuma kimaendeleo na nitalivalia njuga suala hili mpaka likome’’, amesisitiza Aweso.
Aidha, Naibu Waziri Aweso ametembelea mradi wa Hoza Salala uliopo Kijiji cha Kibati, wilayani Mvomero, mradi uliokuwa umegubikwa na tuhuma za ufisadi ambapo ameivunja Bodi ya Maji ya mradi huo na kuagiza iundwe mpya baada ya kugundua matumizi mabaya ya fedha kwa wajumbe wa kamati ya bodi.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, Mhandisi Nicholaus Angumbwike kwenye mtambo mpya wa kusafisha na kutibu maji wa Mambogo, Morogoro.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, Mhandisi Nicholaus Angumbwike alipotembelea Bwawa la Mindu, Morogoro.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Sadiq Morad wakiwa kwenye eneo la mradi wa Hoza Salala, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibati, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ZAUNGANISHA NGUVU KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU KATIKA ZIWA VICTORIA.

$
0
0
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe. Luhaga Joelson Mpina(Mb) mwenye miwani akimkabidhi uenyekiti  wa Baraza  la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi na Utunzaji wa Viumbe Kwenye Maji katika nchi za Afrika Mashariki(FASCoM)  Mhe. Ssempija Vicente Bamulangaki ambaye ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda hivi karibuni.
 Baraza  la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi na Utunzaji wa Viumbe Kwenye Maji katika nchi za Afrika Mashariki(FASCoM) linaliwajumuisha  Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi wa Tanzania, Uganda na Kenya, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi katika picha ya pamoja  baada ya kikao cha kwanza cha Baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni Entebbe nchini Uganda.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina(mwenye miwani) baada ya kikao cha kwanza cha Baraza  la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi na Utunzaji wa Viumbe Kwenye Maji katika nchi za Afrika Mashariki(FASCoM) kilichofanyika hivi karibuni Entebbe nchini Uganda.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt Yohana Budeba.
 Na Mwandishi Maalum, Entebbe
Zatenga  bilioni 4 za kufanya doria ya pamoja kunusuru kutoweka kwa Sangara. 
 
NCHI za Tanzania, Kenya na Uganda kwa pamoja zimeridhia kufanya operesheni ya pamoja ya kupambana na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria ili kuokoa samaki aina ya sangara walioko katika hatari kubwa ya kutoweka .
Uamuzi huo umefikiwa na Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria  ( LVFO) ambapo wameidhinisha Dola za Kimarekani 1,800,000 sawa na sh. Bilioni 4.1  za kitanzania kwa ajili ya kufanya operesheni hiyo katika Ziwa Victoria.
Hivyo nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kila moja itapata Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh. Bilioni 1.3 ili kufanikisha operesheni hiyo ya kuokoa samaki aina ya sangara walioko katika tishio la kutoweka katika Ziwa Victoria kutokana na kushamiri uvuvi haramu.
Kwa siku za karibuni kulikuwa na malalamiko kuwa operesheni hiyo inafanyika upande mmoja tu wa ziwa hilo kwa Tanzania huku shughuli za uvuvi haramu zikidaiwa kufanyika katika nchi za Kenya na Uganda hivyo uamuzi huo utasaidia kumaliza tatizo hilo lilidumu kwa miaka mingi sasa.
Akizungumza katika kikao kukabidhi madaraka kwa nchi ya Uganda mjini Entebbe juzi, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Baraza hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Luhaga Mpina alisema fedha hizo zitasaidia kuongeza kasi ya kupambana na uvuvi haramu ambapo kwa Tanzania ilishaanza operesheni hiyo mwanzoni mwa mwaka huu na kuleta mafanikio makubwa.
Mpina pia aliwaomba viongozi wa nchi wanachama wanaozunguka Ziwa Victoria kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotolewa na Taasisi za Utafiti za  KMFRI, TAFIRI na NaFIRRI ikiwemo kanuni ya urefu wa samaki aina ya sangara wanaoruhusiwa kuvuliwa (slot size regulations) kati ya sentimita 50 hadi 85, Kanuni hii licha ya kuagizwa na Kikao cha Baraza la Mawaziri 2016  kutumika kwa nchi zote lakini baadhi ya nchi hazijatekeleza sharti hili kikamilifu.
Aidha Waziri Mpina pia  aliwakumbusha viongozi wa nchi zinazotumia Ziwa Victoria kuwaeleza ukweli wananchi wao wanaojishughulisha na biashara ya uvuvi kuhusu Sheria za Uvuvi za nchi zingine ili kujiepusha na adha watakazokumbana nazo pindi nchi husika inapochukua hatua  kwa mujibu wa sheria zake na kwamba  Tanzania itaendelea kuheshimu sheria za nchi nyingine ili kulinda rasimali za ziwa hilo.
“Ni imani yangu kuwa itakuwa hivyo hivyo Kenya na  itakuwa hivyo hivyo Uganda kwani rasilimali hii ni mali yetu sote hivyo tunajukumu kubwa la kuilinda kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho”alisema.
Hivyo Waziri Mpina alisisitiza kuwa biashara ya uvuvi haramu itabaki historia katika nchi za Afrika Mashariki kama viongozi watakuwa na dhamira safi na kujitoa kwa moyo wote kulinda rasilimali hizo na kwamba vita hiyo haiwezi kufanikiwa kama viongozi hawatajitoa mhanga kufanikisha kazi hiyo.
Hata hivyo chini ya uenyekiti wake, Waziri Mpina alijivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana ikiwemo kuanzishwa vya vikosi kazi mtambuka vilivyoweza kongoza mapambano ya uvuvi haramu ikiwemo Inter-Agency Unit ya Kenya, Multi-Agency Task Team(MATT) ya Tanzania na Fisheries Protection Force(FPF) ya Uganda.
Alisema  Tanzania imepata mafanikio makubwa baada ya kuendeshwa kwa operesheni Sangara 2018 ambayo ililenga kupambana na uvuvi haramu kwa kuondoa zana zote haramu ndani ya ziwa, kudhibiti wazalishaji zana haramu pamoja na wachakataji wa samaki wasioruhusiwa.
Aidha Waziri Mpina alimweleza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda, Ssempijja Vicent Bamulaki kutambua kuwa kupewa fursa ya kuongoza watu ni kupewa  fursa ya kuleta  mageuzi na kwamba uongozi ni vitendo sio nafasi.
Waziri Mpina alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara ni mbaya katika Ziwa Victoria kwani kwa mujibu wa taarifa kutoka Taasisi za Utafiti za Afrika Mashariki zinaonyesha kuwa sangara wenye urefu wa sentimita 50 na kuendelea wamepungua na kubakia asilimia 5 tu, hivyo juhudi za haraka zisipochukuliwa samaki hao watatoweka na shughuli za uvuvi katika ziwa hilo zitakoma .
Aidha, Waziri alisema  katika kipindi cha uongozi wake kumekuwepo na changamoto mbalimbali zikiwemo uvuvi haramu,utoroshaji wa mazao ya uvuvi,usimamizi dhaifu wa sheria, uvunaji holela,nguvu kubwa ya uvuvi,ukwepaji wa mapato ya Serikali, nchi wanachama na nchi za nje kuingia katika mipaka ya nchi nyingine na kufanya biashara ya uvuvi bila vibali wala leseni.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa LVFO anayemaliza muda wake, Godfrey Monor alisema nafasi ya Katibu Mtendaji kwa kipindi hiki ni ya Tanzania na nafasi na Katibu Mtendaji Msaidizi ni ya nchi ya Uganda baada ya Sekretarieti iliyopo kumaliza muda wake Agosti mwaka huu kwa mujibu wa mkataba wa LVFO kifungu cha X hivyo nchi husika zifanye mchakato wa kujaza nafasi hizo kwa muda muafaka.
Monor alisema miongoni mwa maazimio ya kikao hicho ni pamoja na kuundwa kwa chombo kipya kitakachosimamia rasilimali za uvuvi katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Fisheries Organizatin – EAFO) ili kusimamia shughuli zote za uvuvi katika mito,maziwa na bahari badala ilivyokuwa awali kwa LVFO kusimamia Ziwa Victoria pekee.
Waziri Mpina alisema  miongoni  mwa ajenda za  kikao hicho cha Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria ( LVFO) ilikuwa ni kujadili utekelezaji wa  maagizo ya  kikao cha awali cha tisa cha Baraza hilo kilichofanyika Nairobi nchini Kenya Januari 29 mwaka 2016.
Baadhi maagizo yaliyowasilishwa ni pamoja  na kuwasilisha taarifa za tafiti za kisayansi kutoka katika taasisi zenye dhamana ya kufanya tafiti za uvuvi kwenye nchi wanachama ili kusaidia usimamizi wa pamoja wa Ziwa Victoria ambapo  taasisi hizo kwa upande wa Tanzania ni TAFIRI, Kenya ni KMFRI na  NaFIRRI kwa upande wa Uganda.
Mheshimiwa Mpina alisema kikao hiki kimekuwa ni kikao cha kwanza baada ya mabadiliko  makubwa yaliyofanywa katika kikao cha tisa cha Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria  ( LVFO) kilichofanyika Nairobi nchini Kenya Januari 29 mwaka 2016 ambacho kilifanya mabadiliko ambayo yanalifanya baraza hilo kuwa Baraza  la Mawaziri wa Sekta ya Uvuvi na Utunzaji wa Viumbe Kwenye Majikatika nchi za Afrika Mashariki(FASCoM)  badala ya (LVFO)

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA NA KUZALISHA MAFUTA YA ALIZETI CHA MOUNT MERU MILLERS KILICHOPO MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria ufunguzi wa  kiwanda kikubwa cha Kusindika na kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers kilichopo mkoani Singida. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu tisini za mafuta ya alizeti kwa mwaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda hicho kikubwa cha kusindika Alizeti cha Mount meru millers kilichopo mkoani Singida. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba, mmiliki wa Kiwanda hicho Atul Mittal mwenye nguo nyeupe na  Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenda kukagua shughuli mbalimbali za kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti kilichopo mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Atul Mittal mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti mkoani Singida. PICHA NA IKULU

KUBENEA AWASILISHA MUSWADA WA KUTAKA MABADILIKO YA KATIBA BUNGENI

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, amewasilisha bungeni hoja binafsi, kutaka kufanyika mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ili kuruhusu kuundwa kwa “Tume Huru ya Uchaguzi.


Kubenea ambaye leo amewaita Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuwaeleza kwanini ameamua kupeleka muswada huo katika bunge hili linaloanza tarehe moja april.

 Kubenea amesema, uchaguzi huru na haki, hauwezi kufanyika nchini bila kuwapo na chombo huru cha kusimamia na kuendesha chaguzi hizo.

“Hoja kwamba NEC siyo chombo huru, siyo maneno yangu pekee. Haya yameelezwa vizuri na wanazuoni mbalimbali, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali ambayo iliundwa na Rais wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mwaka 1991.tume hii ya Jaji Nyalali ndio iliyokuja kupendekeza kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi nchini,’’Amesema Kubenea.


 Aliongeza kuwa mwaka 1999, Tume iliyoundwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuratibu maoni ya wananchi kuhusu Katiba ilipigilia msumali mwingine kuhusu muundo wa sasa wa NEC iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga.

Kwenye ripoti ya Jaji Kisanga alisema “hatua ya wajumbe wa Tume kuteuliwa na Rais ambaye pia aweza kuwa kiongozi wa chama cha siasa kinachotawala, katika utendaji wao wa kazi ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watakuwa wanalipa fadhila 
 Mbunge wa Ubungo , Saed Kubenea akizungumza na Waandishi wa Habri juu ya Hoja yake aliyowasilisha bungeni kuundwe kwa tume ya huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 Mbunge wa Bukoba Mjini , Willfred Rwakatale, akivchangia jambo wakati Kubenea alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuwasilisha hoja ya kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi.
 Mbunge wa Mosho Vijini, Antony Komu , akichangia jambo mara baada ya Kubenea mara kuzungumza na Waandishi wa Habari juu kuwasilisha Hoja Binafsi.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioudhuria Mkutano huo 

WAZIRI KIGWANGALLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA KANDA - PORI LA AKIBA RUKWA KUPISHA UCHUNGUZI KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UJANGILI

ASANTE ALEX MSAMA TUKUTANE CCM KIRUMBA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu huku akiwatangaza baadhi ya waimbaji katika tamasha hilo kushoto ni mwimbaji Beatrice Mwaipaja na kulia ni Mwimbaji Paul Clement.
Beatrice Mwaipaja kushoto na Mwimbaji Paul Clement. wakizungumza na waandishiwa habari kuhusu maandalizia ya Tamasha la Pasaka.




Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

APRILI Moja katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza,macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa uwanjani hapo.Kwanini jibu ni moja tu kutakuwa na Tamasha la Pasaka.

Tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likiandaliwa na Msama Promotion kila mwaka na kufanyika siku ya Sikuu ya Pasaka.Ni tamasha ambalo limekuwa likiwaweka Watanzania pamoja.

Ni tamasha ambalo msingi wake mkubwa ni kudumisha upendo na mshikamano kwa Watanzania na kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusu tamasha hilo.Kwa kukumbusha tu kauli mbiu kwenye tamasha la Pasaka kwa mwaka jana ilikuwa inasema hivi "Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu" ...na lilifanyika jijini Dar es Salaam, Mwanza na mikoa mingine kwa siku tofauti .

Tamasha la Pasaka la mwaka huu ambalo sasa linafanyika Mwanza kwa mara ya kwanza kauli mbiu yake inasema “UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU” na sababu kubwa ni kwamba Msama Promotion inataka kuwahubiria injili ya Amani na Upendo wakazi wa Kanda ya Ziwana na Vitongoji vyake.

Ukweli ni kwamba msingi mkuu wa Tamasha la Pasaka ni kutumia tamasha hilo kwa ajili ya kuabudu na kumtukuza Mungu.Hivyo ni tamasha ambalo linahusisha zaidi waimbaji wa nyimbo za Injili huku waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi Maaskofu na wachungaji wakitoa jumbe nyingi za kuhumiza Upendo, Amani na Utulivu kwa watanzania.

Kampuni ya Msama Promotioni kupitia Mkurugenzi wake Alex Msama imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha wanaohudhuria tamasha hilo wanaburudika kutokana na aina ya waimbaji ambao hupata nafasi ya kutumbuiza kwa kuimba nyimbo za Injili katika tamasha hilo.

Waimbaji wengi maarufu wa muziki huo kutoka ndani na nje ya Tanzania wamekuwa wakishiriki kila mwaka kwenye Tamasha la Pasaka.Tamasha ambalo mwaka huu ni la 18 tangu kuanzishwa kwake

Kadri miaka inavyosonga mbele ndivyo ambavyo umaarufu wake unazidi kuongezeka.Kwanini? Jibu ni kwamba Watanzania wamekuwa wakisubiria kwa hamu tamasha hilo kila mwaka na limekuwa ni Baraka tosha kwa maisha yao na familia zao mbele ya Mungu.

Msama na Kampuni yake imefungua milango sahihi ya Watanzania kupata sehemu ya kwenda siku ya Pasaka na si kwingine bali ni kwenye tamasha la Pasaka.Hivyo jamii ya Watanzania na hasa yenye hofu ya Mungu imekuwa ikitamani kuona siku ya Tamasha la Pasaka inafika ili kujumuika na wenzao wengine kushuhudia uponyaji wa mungu kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za Injili.

Hongera Msama kwasababu umetambua katika maisha ya binadamu kuna njia nyingi za kumfanya kuwa karibu na Mungu wake hasa kwenye sikukuu ambazo kimsingi zinatokana na imani za dini.Sikukuu ya Pasaka huadhimishwa kila mwaka baada ya Wakristo duniani kote kumaliza Kwaresma kwa siku 40 ambayo huhitimishwa kwa sikukuu ya Pasaka.

Ukweli ni kwamba Tamasha la Pasaka limekuwa na historia ya aina yake nchini kwetu.Wakati linaanza lilionekana kama tamasha la kawaida lakini kama ambavyo nimeeleza hapo juu sasa kila mmoja wetu analichukulia kwa uzito wa aina yake.Zipo sababu nyingi lakini kubwa zaidi ni tamasha ambalo pamoja na kwamba limekuwa likitumika sehemu ya kutumbuiza wananchi wanaofika kwenye tamasha hilo kwa kupata nafasi ya kushuhudia waimbaji wa nyimbo za Injili.

Akizungumzia tamasha la Pasaka kwa mwaka huu Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama anasema ni la kipekee sana kwasababu ni kwa mara ya kwanza linafanyika Kanda ya Ziwa tangu kuanzishwa kwake miaka kadhaa iliyopita.

"Hii ni fursa pekee kwa watu wa Kanda ya Ziwa na vitongoji vyake katika burudani , kupata baraka za Mungu lakini kuwaunganisha Watanzania pamoja."Kwa kutumia tamasha la Pasaka mbali ya kutoa burudani inayoambana na ujumbe wenye kumpendeza Mungu, pia hutoa nafasi ya Watanzania kumkaribia Mungu zaidi na kubwa zaidi kufurahia sikukuu ya Pasaka tukiwa wamoja,"anasema Msama.

Msama anasema kila baada ya kumalizika kwa mTamasha la Pasaka kiasi cha fedha zinazopatikana zimekuwa zikitumika katika kulipia karo za baadhi ya watoto yatima katika vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu lakini pia zimekuwa zikisaidia kutoa misaada ya mahitaji maalum ikiwemo chakula katika vituo hivyo ili nao wajisikie ni miongoni mwa watu wanaoshiriki kikamilifu katika msima wa Tamasha la Pasaka

Anafafanua kuwa Aprili 1 mwaka huu Tamasha la Pasaka litafanyika Uwanja wa CCM Kirumba likitumbizwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka mataifa mbalimbali.

"Aprili 2 mwaka huu tamasha hilo lifanyika Bariadi mkoani Simiyu kwenye Uwanjwa wa Halmashauri.Hivyo kwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika huko Kanda ya Ziwa tofauti na miaka yote ambapo limekuwa likianzia katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine ikiwamo ya Mbeya, Iringa na Morogoro,"anasema Msama.

Kwa kuwakumbusha tu Watanzania kwa mwaka huu baadhi ya waimbaji wa muziki wa Injili watakaotumbuiza siku ya tamasha hilo ni Rose Mhando ambaye pia atatumia tamasha hilo kuzindua albamu yake.

Pia watakuwepo Upendo Nkone , Christopher Mwahangira, Beatrice Baraka, Matha Mwaipaja, Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia, Solomon Mkukubwa kutoka Kenya, Faraja Ntaboba kutoka DR Congo , Paul Crement, Jesca Honore, Angel Bernard, wengine wengi.

Kwa mazingira ya aina hiyo , hakuna sababu ya mkazi wa Kanda ya Ziwa kuanza kutafakari na kuumiza kichwa wapi pakwenda.Huna sababu kwani tayari Msama Promotion tayari amekurahisishia.Msama bado anasisitiza kuwa wakazi wa Mwanza na Simiyu kujiandaa kwa ajili ya kuhudhuria tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2018.

"Njooni kwenye tamasha la Pasaka mwaka , mje mpokee baraka.Tupo kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wanapata burudani ya muziki wa Injili na kila mwaka limekuwa na mvuto wa aina yeke.Karibuni nyote kwani ni tamasha ambalo hufanyika mara moja kila mwaka na sasa ni zamu ya Kanda ya Ziwa,"amesema Msama.

Binafsi naungana na Msama.Naomba niwe balozi wake wa kuzungumzia tamasha la Pasaka kwa kuwaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa uwepo wapo wao siku hiyo ni muhimu kama ambavyo Msama ameona umuhimu wa kulipeleka tamasha hilo huko.Najua mikoa mingine nako wanalisubiri na kwa kuwa limekuwa likifanyika kila mwaka huenda mwakani litakuwa mkoani kwako.

Nihitimishe kwa kusisitiza kuwa Aprili Moja mwaka huu wakazi wa Kanda ya Ziwa na hasa mikoa ya Mwanza na Simiyu tukutane CCM Kirumba na Uwanja wa Halmashauri Bariadi kwa ajili ya Tamasha la Pasaka

MAHUSIANO KAZINI YANAKUFANYA USIJIAMINI -ANNA MAKINDA

$
0
0
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,Anne Makinda akizungumza na wanawake wa Mfuo huo leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.


Imeelezwa kuwa mashirika mengi yamekuwa yakianguka na kukosa mweelekeo kwa sabababu ya washirika wake kuwa na mahusiano ya mapenzi wao kwa wao wawapo kazini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Wa bodi Wa mfuko wa Taifa Wa bima ya afya NHIF  Spika  wa bunge mstaafu Anne Makinda wakati Wa sherehe za kuadhimisha siku ya wanawake iliyofanywa na shirika hilo ofsini kwao jijini Dar es salaam.

Akizungumza na watumishi Wa NHIF Makinda amesema kuwa na mahusiano kazini yanakufanya usijiamini uwapo kazini.

"Ukiwa na mahusiano na bosi wako hata kama utafanya Kazi kwa juhudi na kupandishwa cheo itaonekana kama umepanda kwa sababu mahusiano mliyokuwa nayo,"alisema Makinda.

Makinda amewaasa wafanyakazi wa NHIF wafanye Kazi kwa uaminifu na waache makandokando.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa NHIFA Bernard Konga amesema shirika lao linasimamia suala zima la usawa wa kijinsia na watahakikisha wanawake wenye sifa wanapanda cheo.


Aidha Rose Gabriel ambae ni Mwenyekiti wa akina mama NHIF ametoa rai kwa wanawake kusherekea siku ya wanawake kwa kudumisha Umoja na mshikikamano

Amesema unapokuwa kazini masuala ya mahusiano uachane nayo na kufanya kazi kwa waminifu pamoja na kujituma kwa bidii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza machache katika leo jijin Dar es Salaam wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda akikata keki leo wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe,Anne Makinda akimlisha keki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
 Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu Anne Makinda akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.
 Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu,  Anne Makinda akimkabidhi zawadi wa kikombe Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Anne Makinda akilishwa keki na Mwenyekiti wa wanawake wa (NHIF)Rose Gabriel.
Baadhi ya wanawake wakiwa katika makoo makuu ya (NHIF) jijini Dar es Salaam wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 kila mwaka kwaajili ya kujua mchango wa mwanamke katika nafasi mbalimbali za ajira pamoja na kujua dhamani ya Mwanamke katika jamii.


Taarifa kwa Umma

Wafanyakazi wanawake TBL Group walivyoadhimisha siku yao

$
0
0
 Mtaalamu wa masuala ya ujasiriamali Ndinhesya Mallango kutoka taasisi ya Mbeya Research and Consultancy Firm (MRCF) akiwapiga msasa wafanyakazi wanawake wa TBL Mbeya.
...........................................................................
Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya TBL Group katika viwanda vya Dar es Salaam,Arusha,Mbeya,Mwanza na Kilimanjaro, walisherekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kupatiwa semina zinazohusiana na masuala ya maisha ya kazini,familia na kijamii, sambamba na kupata burudani za aina mbalimbali.
 Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifuatilia mada kuhusiana na urembo
 Wanawake Mwanza nao walipigwa msasa
 Wafanyakazi wa Arusha na Moshi wakiburudika kwa muziki
 Wafanyakazi wanawake wa Dar es Salaam wakifuatilia  mada mbalimbali
Wafanyakazi wa Arusha na Moshi wakiburudika kwa muziki

Dkt.Abbas apongeza utafiti uliofanywa na Misatan kwa kushirikiana na CPESA

$
0
0
Na.Vero Ignatus Arusha.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema Maafisa Mawasiliano serikalini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa mabosi wao, ikiwano wengine kutokutaka habari zao zisikike kwenye vyombo vya habari.

Dkt.Abbas aliyasema hayo jana mjini hapa wakati mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.

Alisema kupitia ripoti hiyo aliyoiunga mkono na kuisoma vyema atahakikisha maofisa mawasiliano zaidi ya 300 wanaokutana mjini Arusha wanapata utafiti huo."Nimesoma utafiti huu, kurasa zote upo vizuri, niwaombe muendelee kufanya tafiti kama hizi kwani ni chakula kwetu," alisema Dkt. Abbas.

Akizungumzia utafiti uliofanywa katika mikoa 7 na MISATAN Wakili wa mahakama kuu James Marenga amesema ofisi za halmashauri ya mikoa ya Arusha na kigoma ,walau ndiyo zimeonekana ndiyo wanafanaya vizuri katika kuwa wazi katika utoaji wa taarifa kuliko ofisi za mikoa.

Dodoma manispaa,halmashauri ya Jiji la mbeya,Kigoma ofisi ya mkuu Arusha, ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza hakukuwa na ushirikiano,vilevile mkoa wa Mtwara hakukuwa na ushirikiano ,Dar ni katika halmashari ya Jiji,Kwahiyo Utafiti huo ulikuwa umegawanya utoaji  wa taarifa kwa ofisi za mkuu wa mikoa na ofisi za halmashauri au za Majiji katika mikoa iliyochaguliwa.

Moja ya mapendekezo yaliyotolewa baada ya utafiti huo vitengo vya watoa taarifa vinaimarishwa kama inavyotakiwa  katika sheria ya haki  kupata taarifa ya mwaka 2016.Vilevile utafiti huo unasisitiza kuwepo na uwazi katika utoaji wa taarifa haswa kwenye taasisi za serikali.
Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja uliofanyika Jijini Arusha ,ulioandaliwa na MISATAN kwa kushorikiana na CIPESA.
Kaimu Mkurugenzi Gasirigwa Sengiyumva
Wakili wa Mahakama Kuu Janes Marenga akifafanua jambo katika mkutano wa siki moja uliaondalowa na Misatan na kufanyika Jiiini Arusha.
Mshiriki kutoka nchini Uganda akichangia jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau mbàlimbali pamoja na waandishi walioshiriki katika mkutano huo Jijini Arusha.
Mwandishi wa Gazeti la Habari leo Veronica Mheta akichangia mada katika mkutano huo
Mwenyekiti wa MISATAN Salome Kitomari akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Jijini Arusha
Mmoja wa washiriki kutoka CIPESSA akitoa mada katika mkutano huo
Msemaji wa TANAPA Paschal Shelutete akichangia jambo katika mkitano huo.
Kaimu mkurugenzi wa MISATAN nchini Gasirigwa Sengiyumva (wa kwanza kushoto)akiwa na mmiliki wa Wazalendo Blog,Gadiola Emmanuel (mwenye skafu nyekundu shingoni)
 Mafunzo yakiendelea katika Hotel ya Impala Jijini Arusha.

KUWAIT YAZINDUA KISIMA CHA 61 KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI

$
0
0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akizindua kisima cha maji katika shule Gezaulole. akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (wa tatu kulia), na Sheikh Kaporo ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa kisima wa kwanza kushoto 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem akihutubia baada ya uzinduzi wa kisima, kulia kwake ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu Waryam Shabani.
Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi akizungumza jmbo mara baad ya Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem kuzindua kisima 
Wanafunzi wakiwa wamebeba vifaa maalumu vya kuhifadhi maji vilivyotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait Nchini
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapati mdftari na mikoba
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh.Jasem Al-Najem katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem ajumuika na wanafunzi darasani na kukagua madftri yao
Wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kumkaribisha mgeni rasmi Mh, Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem.


Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe, Jasem Al-Najem azindua kisima cha 61 katika shule ya msingi ya Gezaulole, Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam machi 7, 2018, Ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa ''Kisima cha Maji katika kila Shule''.

Ulio anzishwa na Ubalozi wa Kuwati mwishoni mwa mwaka 2016, Hafla ya uzinduzi wa kisim hicho kilihudhuliw na Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Maziku Luhemeg, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Gezaulole, Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shabani pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hiyo,kilicho zindiuliwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem.

Ambapo kitanufaisha shule ya Msingi ya Gezaulole iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na shule jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushyyenye wanafunzi 250 iliyo anzishwa mwaka 2007.

Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh. Jasem Al-Najem katika hotuba yake baada ya uzinduzi huo amesema kuwa Ubalozi wa nchini mwake umeanzisha mradi wa "Kisima cha Maji" ilikuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa Tanzania, Mh. Jonh Magufuli ya kutoa Elimu bure .Balozi Mhe, Jasem Al-Najem ameeleza kuwa kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo katika kutatua changamoto zitakazo kabiliana na shule hiyo,

Aidha aliahidi kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo, madaftari , , mikoba na vifaa vya kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao kujihimu katika masomo yao ili wawe mdaktari, wanahabari, walimu.

Diwani Sumangila kwa upande wake Francis Chichi ameishukuru Kuwait kwa kuwachimbia kisima cha maji katika shule hiyo huku akimuomba Balozi, Jasem Al-Najem kusaidia Kata yake gari la kubebea wagonjwa ili kuwaondolea akina mama wajawzito na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika Hospitali na katika vituo vya Afya ambapo baadhi yao wakati mwingine hulazimika kukodi Pikipiki ili kufika huko, jambo ambalo linahatarisha uhai wao.

MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Picha zote na Elisa Shunda
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Mlao (kulia) wakielekea kupanda ndege kuanza safari kuelekea wilayani Mafia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao (kulia) wakiwa ndani ya ndege safarini kuelekea wilayani Mafia kwa ziara ya kutembelea umoja wa vijana.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Mlao wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mafia tayari kuanza kwa ziara yao.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akilakiwa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mafia tayari kuanza kwa ziara yake.

Wenyeji wakiwaongoza wageni kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Mafia.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia,Gilbert Sandagula akitoa ufafanuzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa ujumla jinsi inavyosaidia vijana wa wilaya hiyo kunufaika na mikopo na miradi mbalimbali inayotolewa na ofisi hizo kwa vijana. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akiulizia mambo mbalimbali yahusuyo vijana wa Wilaya ya Mafia kwa uongozi wa wilaya hiyo ofisini hapo. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango,akizungumza wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao walipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia kupokea taarifa ya usaidizi wa ofisi hiyo katika kuwasaidia vijana wa wilaya hiyo kwenye mikopo ya asilimia 4%.
Katibu wa Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani,Fakh Seif akizungumza na akielezea masuala mbalimbali yanayofanywa na mbunge wa jimbo hilo katika kuwasaidia vijana wa wilaya ya Mafia.


Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki akizungumza katika mkutano huo na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa chama hicho.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo. Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM), Ally Omary Hassan akikabidhi risala ya umoja huo kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (Kulia) katika mkutano na wajumbe wa baraza UVCCM la wilaya ya Mafia. Anayeshuhudia Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Mlao akiwasisitiza wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Mafia kwa kushirikiana na viongozi wao katika kuhakikisha wanaimarisha chama hicho ili kishinde kwa kishindo uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ambao ndiyo sahihi ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki (kushoto) vitabu vya kanuni 100 na kadi za umoja wa vijana 200 kama zawadi kwa ajili ya jumuiya hiyo ya vijana ya Wilaya ya Mafia. Wanaoshuhudia kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (aliyejifunika kitambaa rangi ya njano) na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,,Ramadhan Mlao (kushoto kwake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia. Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia,Mohamed Faki (kushoto) baada ya kumalizika kwa shughuli za mkutano na wajumbe wa baraza la vijana la UVCCM la Wilaya ya Mafia. jumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia,Mohamed Faki (kushoto) baada ya kumalizika kwa shughuli za mkutano na wajumbe wa baraza la vijana la UVCCM la Wilaya ya Mafia.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (aliyejifunika kitambaa rangi ya njano) na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,,Ramadhan Mlao (kushoto kwake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia.





Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro.




Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akibarizi na kujionea uzuri wa fukwe za bahari katika Kisiwa cha Mafia.




NA ELISA SHUNDA,MAFIA .

VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya ziara wilayani humo leo ambapo katika kuhakikisha vijana wa wilaya hiyo wananufaika na serikali ya Dk.John Pombe Magufuli amepata fursa ya kutembelea ofisi ya wilaya na halmashauri ambapo amekutana na uongozi na kupewa maelezo ya mnufaiko wa vijana wa Mafia katika asilimia 4% ya mikopo na miradi inayotolewa na uongozi huo kwa vijana hao.

Mwenyekiti Makwiro amewaeleza vijana hao kuwa wao ndiyo nguvu ya chama na kuwataka kusimama ngangari kama viongozi na vijana wa CCM kwa kutumia nguvu,mali,akili na rasilimali zao zote katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambapo ndiyo msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na urais hivyo ni jukumu lao vijana kukipigania chama katika maandalizi ya uchaguzi huo.

“nimefarijika siku ya leo kukutana na viongozi na vijana wa CCM wa Wilaya hii ya Mafia napenda kuwausia na kuwakumbusha vijana wenzangu mmeomba nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu hivyo basi unapoomba nafasi katika chama hiki usitarajie labda kuna hela utapata au uwe kibaraka wa kiongozi Fulani ili maisha yako yaendelee hapana umeomba nafasi ya uongozi kwa ajili ya kuwatumikia vijana wenzako ni jukumu lako kama kiongozi sasa kutumia nguvu zako,akili,mali na rasilimali katika kukitumikia chama hiki;

“Kupitia nyie vijana wa Chama Cha Mapinduzi ambao leo hii ni viongozi wa UVCCM kuanzia ngazi ya wilaya,kata na mitaa kuhakikisha mnakisaidia chama hiki kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa 2019 wa serikali za mitaa ambapo ushindi wa kishindo wa CCM ndiyo utakaowezesha maandalizi ya ushindi wa kishindo wa uchaguzi mkuu wa 2020 hivyo jitoeni kwa hali na mali mkisaidie chama hiki,msikubali kuwa watumwa wa watu katika kuwachagulia viongozi tumieni akili zenu katika kujitafutia kipato halali ili muwe na jeuri kwa watu wanaotaka kuwaweka mifukoni” Alisema Makwiro

Aidha Mwenyekiti huyo amewasihi vijana hao kuwa na uvumilivu kusameheana kuondoa tofauti baina yao zilizopo ambazo zimetokana na uchaguzi wa ngazi mbalimbali za vijana wilayani humo kuwaomba waungane wakijenge chama kwa pamoja na kukivusha salama katika chaguzi zijazo za serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hata hivyo Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa PwaniRamadhan Mlao amewakumbusha vijana wa mafia kushirikiana katika ngazi zote kuhakikisha wanaijenga jumuiya ya vijana kwa kushirikiana kwa pamoja kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya ili wakisaidie chama katika chaguzi zijazo.

Akizungumza kwa niaba ya vijana hao,Mwenyekiti waUVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki,alisema kuwa wamepokea maelekezo kutoka kwa viongozi hao yeye akishirikiana na wajumbe wa baraza la vijana wa wilaya hiyo kuhakikisha wanaitisha mkutano ili kuondoa tofauti zilizopo ambazo zilisababishwa kwenye kipindi cha uchaguzi.

Lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha kila mabaraza ya wilaya wanaelewa CBO kwa kina na ifanyiwe kazi kwa vijana kujiunga katika vikundi na kunufaika na fedha za vijana zinazotolewa na halmashauri husika ili kuinua uchumi wa vijana.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images