Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

ZIMAMOTO YAWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MOTO WA SOKO MBAGALA

$
0
0
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage, akiwapa pole Waathirika wa moto ulioteketeza vibanda vya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
 Kamaishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akimfariji kwa kumpa pole Mama lishe Bi. Fatma Hassan aliyeunguliwa na vitendea kazi vyake kufuatia tukio la kuungua kwa moto kwa soko la nguo Mbagala.  Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akikagua eneo la Soko la Nguo Mbagala lililoteketea kwa moto juzi. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
Sehemu ya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam walioathirika na moto ulioteketeza vibanda vya wafanyabiashara hao juzi. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)


TAMASHA LA PASAKA WASHIRIKI WAZIDI KUMIMINIKA KANDA YA ZIWA, UPENDO NKONE NA JOSHUA MLELWA NDANI

$
0
0

Mmoja wa Waandaaji wa Tamasha la Pasaka 2018, Ufoo Saro akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Tamsha hili ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha waimbaji wengine waliweza kuungana kuleta utamu zaidi ndani ya Kanda ya Ziwa na vitongoji vyake. Waimbaji waliotangazwa ni Joshua Mlelwa (Kushoto) na Mwanamama Upendo Nkone (kulia).
Ufoo Saro amesema kuwa suala la Usalam limezingatiwa vyema hivyo wajitokeze kwa wingi bila kukosa.

Katika Tamasha hilo, Mwimbaji Rose Muhando anatarajia kuzindua albamu yake ambayo amejiandaa kwa muda mrefu.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joseph Mlelwa (kushoto) akitoa kiburudisho cha wimbo wake wa Yesu Anaweza aliouimba mwaka 2016. Mlelwa amesema kuwa amejiandaa vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa ngumu ili kuweza kufanikisha zaidi tamasha hilo. Tamasha la Pasaka Mwaka 2018 litafanyika Kanda ya Ziwa ambapo Aprili 1 itakuwa ndani ya Uwanja wa CCM - Kilumba na Aprili 2, 2018 ndani ya Uwanja wa Halmashauri, Simiyu. Mwimbaji Joseph Mlelwa ni mmoja ya waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group ambapo kwa sasa amekuwa akifanya kazi zake peke yake.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone amethibitisha rasmi kushiriki Tamasha la Pasaka 2018 kwa kuwatoa hofu wakazi wa Kanda ya Ziwa wajitokeze kupata burudani ya kutosha ya kukata na shoka. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakkitambulisha mbele ya waandishi wa habari (hawapo picha) Mwimbaji huyo amesema kwa sasa amejipanga vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wakitokeze kwa wingi.

"Sina cha kusema zaidi ya kuwaambia wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa wingi maana nimejipanga kuwapa burudani ya kutosha ikiwa ni pamoja na kumshukuru bwana kwa matendo yake makuu aliyonitendea," amesema Nkone.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE RUKWA YAONGOZWA NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu akicheza muziki wa kwaya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kizwite wakati wa Maadhisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa.


Na Mwandishi wetu Sumbawanga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya Wakurugenzi wote wa Halmashauri watakaokaidi agizo la Serikali la kutenga asilimia 4 kwa  ajili ya wanawake na vijana pamoja na asilimia 2 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Rukwa ambapo amepokea changamoto kutoka kwa wanawake wengi  kuhusu utoaji mdogo wa mikopo na wengine kutopata kabisa mikopo kutoka Halmashauri zao.

Ummy amewaagiza Wakurugenzi wa  Halmashuri zote nchini kutenga asimilia 4 kwa ajili ya wanawake na kutoa mikopo yenye tija itaakayoweza kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na sio kurudi nyuma kiuchumi.

“Mikopo ya laki tatu haina tija toeni mikopo yenye tija itakayoendana na kauli mbiu ya kuelekea uchumi wa viwanda” alisema  Ummy. Ummy ameongeza kuwa ili kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda basi Halmashauri hazina budi kujiwekea mikakati ya kutoa mikopo mikubwa itakayowezesha wanawake na wananchi kwa ujumla kufikia dhana hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula ameiomba Serikali kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwapa elimu ya jinsi ya kutumia fedha na kuendesha miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Khalfan Haule amesisitiza wadau kushirikiana na Serikali pale ambapo wanaweza kuwawezesha wanawake sehemu walipo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchango katika kuchangia kujiletea maendeleo jumuishi.

Siku ya Wanawake Duniani 2018 kilele chake ni siku ya tarehe 8 Machi, 2018 na  Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni ‘‘KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI”. Dhamira ya Wizara nikuona kila mdau mmoja mmoja anaelewa madhumuni ya kaulimbiu na kuchukua hatua kuchangia utekelezaji wa ujumbe mahususi wa kuwajumuisha wanawake wa vijijini katika maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.
 Mwakilishi wa  Ubalozi wa Canada Susan akitoa salamu za wadau wa maendeleo na wanawake kwa niaba ya wadau wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa darasa la Nne katika mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula akitoa salamu kwa niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Rukwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa.
 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu  akitoa zawadi ya Cheti kwa Kikundi bora cha wajasiliamali cha mfano katika mkoa wa Rukwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani hapo.
 
Maandamano ya wanawake yakiingia uwanja wa  Mandela Mkoani Rukwa katika kusherekea Siku ya Wanawake Duniani Mkoani hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Jukwaa la kuwezesha Wanawake Kiuchumi mkoani Rukwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Hapo.

KLNT holds 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting in Dodoma

$
0
0


Former Prime Minister, Mizengo Peter Pinda addresses participants during the 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting organized by Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) in Dodoma on Thursday.
Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) CEO and Founder, Isaac Mpatwa giving his welcoming remarks.
KLNT General Secretary, Dr. Charles Sokile delivers his speech during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma.
Former Vice President World Bank - Africa Region, Dr. Oby Ezekwesili delivers her speech during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma.
Dodoma RC, Hon. Dr. Binilith Mahenge speaking to participants during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma.
A cross section of participants during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma.
Former Prime Minister, Mizengo Peter Pinda (centre) poses for a souvenir picture with KLNT officials after the 3rd Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma on Thursday.


KLNT holds 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting in Dodoma

Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) in partnership with the Committee of Union of Churches Dar es Salaam, hosted its 3rd annual National Prayer Breakfast at the Morena Hotel -Dodoma. The event was held on Thursday 8th March 2018 with the theme “Integrity in Leadership”

The 3rd National Prayer Breakfast was attended by 200 government, business, religious and community leaders. The event was graced by Hon Mizengo P Pinda the former Prime Minister of The United Republic of Tanzania as the Guest of Honor.

In welcoming participants at the event Mr. Isaac Mpatwa, the Founder and CEO of KLNT introduced Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) as a non-governmental, non-partisan and non-denominational organization that exists to identify, develop, mentor, deploy and support Ethical Value-based leaders for Tanzania and Africa at large. He said, “At Kingdom Leadership Network Tanzania we are passionate to see transformation in leadership across all sectors and levels of leadership in our country Tanzania. KLNT is made up of people with a common desire to answer their call into leadership and become custodians of the Nation’s wealth”

He further added, “This year we deliberately organized for the event to be held in Dodoma, in recognition of Dodoma being the heart and official capital of our Nation and to bring this unifying event closer to our leaders and policy makers.”

He further Also commenting during the event, the chairman of KLNT board of trustees, Hon Ibrahim Kaduma, pointed out that similar to other nations that host the same event, the Tanzania National Prayer Breakfast is held with the intention of bringing together the nation's top leadership with a two fold purpose; first, it is coming together in prayer and thanksgiving for our Nation; and second, to sensitize and raise National Leaders into God fearing, impeccably ethical and committed patriots.

In a powerful charge and address, the key note speaker, Dr. Oby Ezekwesili (Nigeria) - the former Vice-President of the World Bank’s Africa Region and coordinator of “Bring back our Girls” campaign, stressed the link between

'WANAOTAKA KUUZA FIGO ILI WAPATE FEDHA SASA WAPIGWA MARUFUKU'

$
0
0
*Rais Chama cha Madaktari bingwa wa figo atoa sababu, atoa ushauri kwa Watanzania

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

CHAMA cha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya figo Tanzania kimepiga marufuku biashara  ya uuzaji figo nchini na kueleza kuwa huo si utaratibu mzuri kwa madhara yake ni makubwa.

Pia kimeelezea hali ya ugonjwa wa figo nchini na kwamba kwa mwaka huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa 50 huku kikielezea jitihada za Serikali katika kuhamasisha wananchi kuzuia ugonjwa figo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Rais wa Chama cha Madaktari bingwa ya figo Tanzania Dk.Onesmo Kisanga wakati anazungumza na Michuzi Blogu,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila Alhamis ya pili ya kila Machi.Siku hiyo hutumika kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa figo na hatua ambazo wanataalamu wanachukua ili kukabiliana nao.

Akizungumzia kuhusu tabia ya watu kuuza figo ili kupata fedha,Dk.Kisanga ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa kwa sasa wamepiga marufuku biashara ya watu kuuza figo kwani ina madhara makubwa.

“Nikiri tunapokea maombi mengi pale Muhimbili kutoka kwa watu ambao wanataka kuuza figo ili wapate fedha.Nieleze tu hii biashara ya kuuza figo haitakiwi kabisa nchini Tanzania.Hata Chama cha madaktari bingwa duniani nacho kimepiga marufuku biashara ya figo,"amesema Dk.Kisanga.

Amesema kikubwa ambacho wanakifanya ni kuendelea kutoa elimu kwa wale ambao wanataka kuuza figo kuwa hairuhusiwi na kubwa zaidi ikifanywa ni biashara maana yake wale wasiokuwa na uwezo watashindwa kununua matokeo yake watokosa matibabu.


WATU 50 KUPANDAKIZWA FIGO MWAKA HUU

Wakati huo huo Dk.Kisanga amesema mwaka huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa 50 na huo ndio mkakati wao na kufafanua kuwa mwezi huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa watano na mwezi unaokuna watapandikiza kwa wagonjwa saba.Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kutoa kipaumbele kwenye sekta ya afya na hivyo kufanya idadi ya madaktari bingwa katika kutibu magonjwa ya figo kuongezeka.

"Kwa mara ya kwanza Tanzania tulipandikiza figo mwaka 2017 na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Aliyepandikizwa figo yupo salama na aliyetoa figo naye yupo salama,"amesema Dk.Kisanga.


DALILI KWA MGONJWA WA FIGO

Dk.Kisanga amesema ni ngumu kubaini dalili za mgonjwa wa figo kwa haraka na wakati mwingine hadi unapoanza kuona dalili maana yake figo itakuwa imeharibika kwa asilimia 70 hadi 90.Ndio maana wanashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara.Hiyo itasaidia madaktari bingwa wa magonjwa ya figo kubaini mapema na kuzuia ugonjwa.
Ametaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo ni mwili kuchoka sana, kuvimba miguu, mikono, sura na tumbo na wakati mwingine kupata shida wakati wa kujisaidia haja ndogo.

AZUNGUMZIA ULAJI VYAKULA

Dk.Kisanga amesema kuna baadhi ya vyakula ambavyo mlaji anatakiwa kuwa makini navyo na kufafanua kuwa vyakula vyenye mafuta mengi vinaweza kusababisha matatizo ya figo.Hivyo chakula lazima kiwe bora na mlaji ale kwa kiasia.Kula kupita kiasi kuna madhara yake yakiwamo ya kuongezeka uzito, kupata shinikizo la damu na sukari na ugonjwa wa figo.

Pia amesema chakula kisiwe na chumvi nyingi kwani nayo huchangia ugonjwa figo na kufafanua wanapopima ili kubaini kama kuna ugonjwa wa figo pia wanapima na mkojo kwani hautakiwi kuwa na protini ambayo nayo ni hatari na si dalili nzuri kwani inaashiria ugonjwa wa figo.Amehimiza watu kufanya mazoezi ili kuweka miili yao katika afya njema.
Pia ameomba watu kutokuwa na tabia ya kupenda kula dawa aina ya Dicropa mara kwa mara kwani moja ya madhara yake ni kusababisha ugonjwa figo.

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI YA KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO

$
0
0


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku Alliance One Mkoani Morogopro leo Machi 9, 2018. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri 242 Mkoani Morogoro ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kufikishwa mahakamani mara moja.

NA K-VIS BLOG, Morogoro

OPERESHENI ya nchi nzima kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), inayoongozwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, imeingia Mkoani Morogoro leo Machi 9, 2018, ambapo waajiri wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.

Operesheni hiyo iliyoanzia jijini Mwanza Februari 26, 2018 inafuatia agizo alilolitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana ambapo aliagiza waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo, wafikishwe mahakamani.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, ambaye anafuatana na Mhe. Mavunde kwenye ziara hiyo ya kushtukiza, kuna jumla ya waajiri 536, na kati ya hao ni waajiri 294 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku wengine 242 bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na Mfuko.

“Naagiza waajiri hawa ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, wanaofikia 242 wafikishwe mahakamani mara moja ili wakajibu mashtaka kwanini hawajatimiza wajibu wao wa kisheria.” Aliagiza Mhe. Mavunde.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, mjini Morogoro, Mhe. Mavunde ameiagiza WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri wa kampuni ya Sengo 2000 Tanzania Limited, na Midland Inn Lodge kutojisajili na Mfuko.

Huku kampuni za Hood Transport Company Limited na Alliance One, wao wamekiuka sheria ya kazi na mahusiano kazini. “Lakini pia naagiza waajiri hawa 242 ambao bado hawajajisajili na Mfuko nao wafikishwe mahakamani mara moja ili wakajibu mashtaka kwanini hawajatimiza wajibu wao wa kisheria.” Aliagiza Mhe. Mavunde.

Mhe. Mavunde pia ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.

“Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekeleza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.­­

Aidha Mhe. Mavunde amerejea kauli yake kuwa nia ya serikali sio kuwanyanyasa waajiri au kuwapeleka mahakamani.

“Serikali inataka ninyi waajiri mfanye shughhuli zenu za biashara na uwekezaji na kazi ya kuwahudumia wafanyakazi wenu wanapopatwa na madhara wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi, jukumu hilo lisimamiwe na Serikali kupitia Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

Naibu Waziri pia amebaini kuwa waajiri katika viwanda hivyo hawatekelezi sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo ukiukwaji mkubwa wa sheria hiyo umedhihirika ambapo amewakuta wafanyakazi wakifanya kazi bila ya vifaa vya kujihami, (protective gears), kufanya kazi kwa masaa mengi kupitia kiasi, lakini pia wengi wao hawana mikataba ya kazi.

“Tumebaini kuna mapungufu makubwa sana ya sheria za kazi hasa sheria namba 6 ya mwaka 2004, sheria hii inaelekeza mwajiri azingatie muda wa masaa ya kazi, atoe mikataba kwa wafanyakazi wote,” alisema Mheshimiwa Mavunde.

Aidha Kamishna wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa, amesema, Waajiri ni sharti watoe mikataba kwa wafanyakazi inayoonyesha ni muda gani wa kufanya kazi, likizo kwa mfanyakazi, na hata kama mfanyakazi analipwa kwea siku ni sharti mambo hayo yazingatiwe.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, amesema Mfuko umjiandaa kabisa, na maagizo ya Mheshimiwa Naibu Waziri yatatekelezwa haraka na tayari baadhi ya maeneo hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi ya waajiri ambao wameshindwa kutekeelza takwa la kisheria.

“Operesheni hii ni endelevu tutahakikisha waajiri wote tunawafikia na nitoe rai tu kwa wale ambao bado hawajajisajili, wasisubiri kupelekewa hati za mashtaka, kwani lengo la Mfuko ni kuwasidia waajiri kuondokana na jukumu la kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara mahala pa kazi kwani jukumu hilo kwa sasa kwa mujibu wa sheria ni la Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi WCF na si mahala pengine popote.” Alifafanua Bi. Rehema.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi, kiwanda cha Tumbaku Mkoani Morogoro, Ujaicy Kayera leo Machi 9, 2018 wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na wale ambao hawatekelezi Sheria ya Kazi na Mabhusiano Kazini. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri 242 ambao hawajajisajili na Mfuko kufikishwa mahakamani mara moja.
Naibu Waziri Antoni Mavundeakizungumza na Meneja wa Kampuni ya Hood, Faisal Hood. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi.Rehema Kabongo
Naibu Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji kwa muajili.
Naibu Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji kwa muajili.
Naibu Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji kwa muajili.

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu, Blasius Lupenza akielezea baadhi ya mikataba ya wafanyakazi wake kwa Mhe Naibu Waziri katika Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingulwira.

Naibu Waziri akiangalia Salary slip ya mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tumbaku.

BRIGEDIA JENERELI MSTAAFU AONGOZA MAZISHI YA KABURU KIGOMA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewaongoza mamia ya wakazi wa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa katika mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini na Mwenyekiti msaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Kigoma, Amani Kaburu.

Akizungumza katika msiba huo Brigedia Jenerali Maganga amesema Kaburu ni mwanasiasa aliyejikita kutetea haki za wananchi wa Kigoma na alikuwa wa kwanza kupigania maendeleo ya mkoa huo.Mwili wa Kaburu umepumzishwa jana kwenye nyumba yake ya milele.

Amesema Serikali na CCM itamkumbuka Kaburu kwa mchango mkubwa ambao ameufanya katika mkoa huo na amekuwa mfano wa kuigwa na wengine na licha kutangulia mbele ya haki ameacha alama.

"Marehemu Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake na alipokuwa kiongozi wa vyama mbalimbali na hata katika Bunge la Afrika Mashariki.Hakika ameondoka lakini wana Kigoma tutamkumbuka daima na kwa wanasiasa wengi wanafahamu kuwa vijana wengi mkoani hapa wamejifunza siasa kutoka kwake,"amesema na kuongeza kifo cha Kaburu kimeacha pigo kubwa kwa Serikali, CCM, wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Amandusi Nzamba amesema CCM imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama hicho katika kufikia malengo yao.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema kama mtoto na mwanafunzi wa Kaburu pamoja na tofauti za kisiasa ndiye aliyekuwa mwalimu wao na aliwazibua masikio wanasiasa wengi wa Mkoa huo.

"Kaburu enzi za uhai wake ametufundisha wengi na hasa kuhusu siasa za Tanzania na kubwa zaidi alihimiza umoja na mshikamano mbele ya maendeleo ya Kigoma.Huyu ni kiongozi wa kwanza kupitia mfumo wa vyama vingi na ndio mwalimu wetu katika siasa za vyama vingi.Alijitoa na kupambana na kupigania siasa za Mkoa wetu wa Kigoma na amefanya kazi kubwa,"amesema Zitto.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) Mkoa wa Kigoma Salim Kangeta amesema Kaburu ni kiongozi aliyeshirikiana na kila mtu na hata viongozi wa dini na kubwa zaidi alikuwa anasikiliza ushauri kwa lengo la mkoa huo kusonga mbele kimaendeleo.


HISTORIA YA KABURU

Kaburu alizaliwa mwaka 1949 mkoani Kigoma na alisoma elimu yake ya msingi
Shule ya Msingi Kipampa na elimu ya sekondari katika Shule ya Living Stone Kigoma.

Baada ya hapo aliondoka na kwenda kuendelea na masomo yake nchini Marekani ambapo baada ya hapo alirejea nchini na kuanza harakati za siasa. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Kigoma kwa kipindi cha miaka tisa, pia amewahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki , Katibu Mkuu wa Chadema na amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Katika msiba huo CCM imetoa Sh.900,000 kwa ajili ya rambirambi na CCM Makao Mkuu imetoa Sh.milioni moja wakati Serikali ya Mkoa wa Kigoma nayo imetoa Sh.milioni moja kwa niaba ya Serikali Kuu.Chama cha ACT-Wazalendo kimeshiriki kusafirisha mwili.
 Baadhi ya Ndugu,Jamaa na Marafiki wakiwa kwenye mazishi ya Dkt Kaborou hapo jana.

TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MAJI ZATANGAZWA TENA

$
0
0


Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini na ne ya Tanzania kupitia programu yake ya Uhakika wa Maji, imetangaza kuongezwa muda wa uwasilishwaji wa machapisho na programu za redio na runinga kutoka kwa waandishi na vyombo vya habari ili kuwania tuzo za uandishi wa habari za maji.

Tuzo hizi, zilizinduliwa  na Shahidi wa Maji pamoja na washirika wake kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka 2017, na kupewa jina la ‘Tuzo za Habari za Maji. Ili kushiriki katika tuzo hizi, waandishi watapaswa kuwasilisha kazi zao walizochapisha au walizorusha katika vyombo mbalimbali vya habari zinazohusu masuala mtambuka ya maji kama vile; usimamizi na utawala wa rasilimali maji, ukame, mafuriko, usambazaji maji, uchafuzi wa mito na vyanzo vya maji na kadhalika.

Vyombo vya habari pamoja na waandishi watakaoshinda tuzo hizi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, vifaa vya kuboresha ufanisi wa kazi kama vile kamera na kompyuta mpakato, kombe la tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki, hii ikiwa na lengo la kuboresha uwajibikaji miongoni wa wadau wa sekta ya habari katika kuchapa na kusambaza habari zihusuzo maji ili kuleta mabadiliko chanya, endelevu na ya kudumu katika sekta ya maji na kuleta hali ya usalama na uhakika wa maji kwa watanzania wote.

Pia, makala/kazi a za washindi   zitapata fursa ya kurushwa kwenyetovuti zetu na kusambazwa katika vyomba mbalimbali vya habari na mitandao ya kimataifa kama vile: BBC, UK Guardian, Circle of Blue and Ooska News ambayo ni nafasi na fursa ya kipekee kwa waandishi na vyombo vya habari kusomwa zaidi na kutambuliwa kwa mchango wao katika kusaidia kuboresha sekta ya maji nchini.
Tuzo hizi zimeandaliwa mahsusi kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinatoa taarifa za masuala ya maji, kuchochea mabadiliko chanya katika uwajibikaji wa wadau wa sekta ya maji.  Shahidi wa Maji na washirika wake imejikita katika kufanya kazi kubadilisha namna ambavyo rasilimali maji inasimamiwa kwa manufaa ya wananchi wote, mazingira na uchumi wa nchi. Aidha, ili kufanikisha hayo shirika hilo na washirika wake wanafanya kazi kwa namna mbalimbali kama vile; Kusaidia jamii zenye uhitaji kuweza kutambua haki na wajibu walionao katika kuwezesha utekelezaji wa sheria zilizopo na kuwezesha jamii kufuatilia utatuzi wa matatizo ya usalama wa maji katika maeneo yao kwa watoa huduma ikiwemo serikali na sekta binafsi.

Mwisho wa uwasilishaji wa kazi za waandishi na vyombo vya habari umetajwa kuwa tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2018. Kufahamu zaidi kuhusu namna ya ushiriki na kupakua chapisho la maelekezo, vigezo na masharti tafadhali tembelea http://www.shahidiwamaji.org au tuma baruapepe kwenda kennedymmari@shahidiwamaji.org


Tigo Yawakabidhi simu washindi 84 wa Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

$
0
0

Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Michael Peter Ngwashi, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.
Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbagala, Grace Gastory Mandai, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.
Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Mohammed Omar Sabuni, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.

Balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali (kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara wa Vingunguti, Jasper Michael Kimei, zawadi ya simu ya 4G aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni hiyo. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#


Wateja 84 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure baada ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#

Zaidi ya simu 840 pamoja na bonasi za uhakika za intaneti bado zinashindaniwa!

Dar es Salaam, Machi 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 84 wapya wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.

Akikabidhi zawadi hizo kwa baadhi ya washindi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Mtaalam wa usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kufikia sasa promosheni hiyo imeibua washindi wa simu 240 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

‘Kila anayenunua bando la intaneti kuanzia TZS 1,000 kupita *147*00# anapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pia anaingizwa kwenye droo ya kushinda mojawapo ya simu zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zinazoshindaniwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus.’

‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa kasi ya juu ya 4G,’ Jasper Dethuel Kimei, mfanyabiashara na mkaazi wa Vingunguti Dar es Salaam alisema baada ya kupokea zawadi yake ya simu.

“Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwani baio tuna simu 840 zinazozubiri kunyakuliwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus,’ alisema balozi wa promosheni hiyo, Meena Ali.

Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

H.E SHEIKHA LUBNA AL QASIMI VISITS ETIHAD AVIATION GROUP TO CELEBRATE INTERNATIONAL WOMEN’S DAY

$
0
0

Etihad Aviation Group Panel Discussion - H.E Mrs Rachel Ruto EGH, the Wife of the Deputy President of Kenya William Ruto H.E Sheikha Lubna Al Qasimi, President of Zayed University, and Etihad Aviation Group CEO Tony Douglas.
 Sheikha Al Suwaidi, the UAE’s first female Emirati photographer.
Etihad Aviation Group celebrates International Women's Day in a networking event.

Abu Dhabi, United Arab Emirates - Etihad Aviation Group has marked the 2018 International Women’s Day with a week of engaging activities featuring a number of leading women from across the UAE.

The highlight of the activities was a panel discussion with HE Sheikha Lubna Al Qasimi, President of Zayed University, and HE Mrs Rachel Ruto EGH, the Wife of the Deputy President of Kenya William Ruto.

HE Sheikha Lubna Al Qasimi highlighted the need for women and men to work alongside one another: “At work, you have female and male colleagues and just the same in school. Take it as a partnership, take it as that everybody has a role to play in society and in life. Respect the man as they contribute a lot and support us women.”

HE Mrs Rachel Ruto, also founder of the Joyful Women Organization, said: “I advise every woman to go for their dream. I advise you to be whatever you have desired to be, to be whom you dreamt to be. Just know that you can attain that potential and that nothing should be able to prevent you from getting whatever you want in life.”

Amina Taher, Vice President of Corporate Affairs at Etihad Aviation Group, added: “We are very grateful to HE Sheikha Lubna Al Qasimi and HE Mrs Rachel Ruto for taking the time to join us at Etihad’s headquarters, and sharing their remarkable stories with us.

“At Etihad Aviation Group, we are privileged to have many inspiring women working here, and we are delighted to have hosted these activities to spotlight their extraordinary stories, as well as the impressive achievements of women from across the UAE.”

Etihad Aviation Group also invited Sheikha Al Suwaidi, the UAE’s first female Emirati photographer, to host a lecture at Etihad’s headquarters. Mrs Al Suwaidi, known as the Mother of All Photographers, encouraged everyone to pursue their dreams.

In addition, Etihad hosted an internal programme under the theme of “Press for Progress,” which consisted of networking among female Etihad employees to discuss progress in the workplace, life and health.

There was also a flower wall which allowed staff members to place a flower in return for making a donation to the NAMA Women Advancement Establishment.

WALENGWA WA TASAF WILAYANI CHATO MKOANI GEITA WACHANGAMKIA HUDUMA ZA MFUKO WA BIMA YA AFYA YA JAMII.

$
0
0
Takribani kiasi cha Shilingi Milioni 140 zimepatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya Wananchi wanaopata huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii-CHF.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Bw.Shaaban Ntarambe amewambia Wandishi wa Habari wanaotembelea Mkoani Geita kuona namna Wananchi wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanaovyotumia fursa hiyo kuwa pamoja na kuanzisha shughuli za kiuchumi ,walengwa hao pia wamehamasishwa kujiunga na CHF kwa kuchangia kiasi cha shilingi 10,000 kwa mwaka na kupata huduma za matibabu kwa kipindi chote cha mwaka.

Amesema kumekuwa na mwitikio mzuri kwa Walengwa hao wa TASAF kujiunga na huduma za CHF kwa kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha na hivyo kuboresha afya zao na kupunguzia mzigo wa serikali kuwahudumia hususani pale wanapohitaji huduma ya matibabu.

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato Dr Athanus Ngambakubi amesema katika vijiji ambavyo TASAF inatoa huduma kwa Kaya Maskini ambazo zimejiunga na CHF,Wataalam wa Afya hawalazimiki kutumia nguvu kubwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kupata huduma za matibabu hospitalini kinyume na ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango huo.

“Tunaishauri Serikali kupitia TASAF kusambaza huduma za Mpango huo katika vijiji vyote ili wananchi waweze kunufaika nayo kwa pamoja” amesisitiza Dr Ngambakubi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chato Bw,Bathlomeo Manunga amesema tangu kuanza kwa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halamshauri hiyo kumekuwa na mabadiliko chanya hususani kwa kaya zilizokuwa zinaishi katika hali ya umaskini mkubwa wa kipato.

Amesema Walengwa wengi kwa sasa wameanza kujiwekea rasilimali hususani mifugo wakiwemo mbuzi,ng’ombe na kuku huku wengine wakiboresha makazi yao kwa kutumia sehemu ya mapato kupitia utaratibu wa Uhawilishaji fedha unaotekelezwa na TASAF.

Naye Afisa Elimu wa Wilaya ya Chato, Bw. Angaselina Kweka amesema tangu kuanza kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo ,kumekuwa na ongezeko la mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka kwenye kaya za Walengwa kutoka wastani wa asilimia 79 mwaka 2015 hadi asilimia 91 mwaka 2018.

Amesema ongezeko hilo limetokana na hali ya ulinganifu wa haiba kwa wanafunzi ambao kabla ya kuanza kwa shughuli za Mpango walishindwa kuhudhuria masomo kwa kukosa sare za shule,viatu,madaftari na hata lishe mambo ambayo kwa sasa yamepatiwa ufumbuzi kwani suala la mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka kwenye kaya za Walengwa ni mojawapo ya masharti ya kuendelea kupata ruzuku inayotolewa kupitia TASAF.

“ Kwa sasa huwezi kutofautisha mtoto anayetoka katika kaya maskini na ile yenye kipato wawapo darasani kwani wote wanakuwa nadhifu hali inayoleta usikivu kwao na kufanya vizuri katika masomo yao ” Amesisitiza Afisa Elimu huyo.

Afisa elimu huyo pia amesema Wazazi wa watoto wanaotoka kwenye kaya za walengwa wanalazimika kwenda shuleni kufuatilia mahudhurio ya watoto wao ili kuepuka kukatwa ruzuku pale inapobainika kuwa mahudhurio ya watoto wao ni hafifu jambo lililosaidia kuboresha taaluma katika wilaya hiyo ambayo ni miongoni mwa wilaya 10 bora kitaifa katika kufaulisha wanafunzi.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF ,Esther Seleman mkazi wa kijiji cha Mabalasana katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) shamba la Mpunga ambalo amelima kwa kutumia sehemu ya ruzuku aliyoipata kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Isamilo katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwa katika shughuli ya kushona nguo kwa kutumia cherahani alichokinunua baada ya kudunduliza fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kama njia ya kujiongezea kipato.
Mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mabalasana katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwa mbele ya nyumba na matofari aliyopata kwa kutumia fedha za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini katika jitihada za kuboresha makazi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Geita.Ali Kidwaka akizungumza na Wandishi wa Habari juu ya utekelezaji wa Shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF hususani Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri yake ambapo amesema Mpango huo umekuwa chachu ya kaya za Walengwa kupiga vita umaskini kwa mafanikio makubwa na kutoa wito wa kutekeleza Mpango huo katika vijiji vyote.
Mmoja wa Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ,BI. Sabina Mtangwa (aliyevaa gauni jekundu ) mkazi wa kijiji cha Isamilo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ,akimwonyesha Afisa Mawasiliano wa TASAF Estom Sanga mbuzi na ng’ombe waliozaliana baada ya kununua mbuzi na kuwauza aliowapata kwa kutumia fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

WANANCHI TABORA WAJITOKEZA KWA WINGI USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Tabora, ambapo Wilaya zote zinaendelea na zoezi hilo.

Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Tabora Bi Grace Msaky, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa na kwamba wananchi wameelewa umuhimu wa Vitambulisho.

Amesema; kuhakikisha wananchi wanapata huduma na wanafikiwa mahali walipo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa sasa zoezi wanaendesha kwenye Vijiji na Mitaa wanakokaa wananchi na kwamba wananchi wanajulishwa muda na wakati wa kufika kwenye vituo kupata huduma hiyo.

“ kwa sasa wananchi wanaelewa utaratibu; ila changamoto ni baadhi ya wananchi kufika siku za mwisho wa zoezi na kufanya zoezi kuchukua muda mrefu kwenye baadhi ya Kata kinyume na ratiba iliyopangwa” alisisitiza.Mbali na Tobora mikoa mingine 19 inaendelea na zoezi kwa Tanzania Bara huku Tanzania Zanzibar zoezi hilo likiwa limekamilika kwa asilimia 99%.

Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye mashine maalumu za uchukuaji taarifa muhimu za Usajili zikiwemo upigaji picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki.
Mkazi wa Mtaa wa Ipuli Bi Halima Abed akiwa kwenye zoezi la kupigwa pichwa ili
kukamilisha Usajili

Bi Maimuna Shabani Bundala Mkazi wa mtaa wa Ipuli akiweka saini ya kielektroniki kwenye mashiya ya Usajili wakati zoezi hilo likiendelea kwenye mtaa wake.
Bw. Shaban Yasin wa Kata ya Ipuli Mtaa wa Nane Nane akichukuliwa alama za Vidole kwenye zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

$
0
0
 Kamishna Msaidizi wa Zimamoto, Hamis Telemkeni (mbele) akitoa maelezo kwa  washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto yaliyofanyika kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.
 Mkaguzi Zimamoto Theresia Tengia  (kushoto) na Sajini Maria Gulam (kulia) wakionesha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zinazoendesha shughuli zake kwenye Kuiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), moja ya kifaa aina ya blanketi linalosaidia kuzima na kufunika  moto endapo utatokea bila kumuathiri kwa kuungua.
 Sajini Maria Gulam (mbele) akionesha namna ya kutumia mtungi wa kuzimia moto kwa washiriki wa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto kilichopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
 Bi. Julieth Fonga (kushoto) wa Kampuni ya General Aviation Services iliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekezwa na Afisa Usalama wa Zimamoto na Uokoaji, Leonard Chami namna ya kuzima moto kwa kutumia mtungi, wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo kwenye kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha JNIA.
 Afisa TEHAMA, Bw. Geofrey Youze akifanya zoezi la kuzima moto katika mafunzo yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Sajini Maria Gulam leo katika mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika katika Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akionesha namba ya kupiga endapo Mwananchi atakuwa amepata tatizo la moto, ili apate msaada wa haraka.   

TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA KUWEZESHA WANAWAKE VIJIJINI-DC MCHEMBE

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akimtambulisha kwa wananchi Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi Gairo, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hope Kimaro wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.
Mgeni rasmi Mhe. Mchembe akipokea taarifa ya Wanawake Gairo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Gairo, Agnes Mkandya.
Uongozi wote wa Wilaya ya Gairo, upande wa Chama na Serikali ukielekea kwenye kupanda miti kuashiria alama ya uhai mpya kwa wanawake waliokata tamaa.

Viongozi wakiwa fuatilia.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya akitoa salamu.
Mkurugenzi wa Halmashauri, Mhe. Rahel Nyangasi akitoa salamu.
Viongozi Wanawake wa Wilaya ya Gairo wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Nyangasi (watatu kushoto) na Agnes Mkandya wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku ya Wanawake Duniani. Wilaya ya Gairo inaendeshwa na wanawake kwa asilimia zaidi ya 95 (tisini na tano).
Wanawake wakipima VVU wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.

Akinababa nao walijitokeza kuomba msaada wa kisheria. 

Wilaya ya Gairo imefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8 kupanda miti ili kuashiria uhai kwa wanawake waliokata tamaa. Zoezi hilo liliongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe na wanasheria wanawake sita akiwemo Mwanasheria wa Manispaa Mvomerowaliweza kusikiliza kero za muda mrefu za wanawake. 
 
Masuala yaliyoangaliwa katika maadhimisho hayo ni migogoro ya ardhi, mirathi, unyanyasaji kijinsia, ukeketaji na kesi za mimba za utotoni ambapo zaidi Wanawake zaidi ya 65 waliweza kuhudumiwa. Kauli mbiu katika maadhimisho hayo wakati wakiendelea katika Uchumi wa Viwanda, "Tuimarishe usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake vijijini", ambapo ulipokelewa kwa shangwe na wanawake kijiji cha Kisitwi jambo lililomvutia Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya na kugawa miche ya korosho zaidi ya elfu 40, mbegu za pamba na kahawa. 
 
Mhe. Mchembe alisisitiza wanawake kulima Kilimo cha Kibiashara ili kuinua kipato na uchumi wao waondokane na utegemezi. Mkuu wa Wilaya huyo ameziomba Taasisi za kifedha NMB na CRDB kutoa mikopo kwa wanawake yenye riba nafuu, aidha kabla ya mkopo wanawake wapewe Elimu ya fedha, masoko, vifungashio, Sheria mbambali na ujasiriamali katika mapana yake.

TATU MZUKA YAKABIDHTI KALENDA 500 KWA JESHI LA POLISI,IGP SIRRO ATOA NENO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikabidhiwa moja ya Kalenda kati ya 500 zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha Tatu Mzuka,kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano kampuni hiyo Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya faluna ya Tatu Mzuka kutoka kwa  Mratibu wa Mawasiliano  Tatu Mzuka, Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.

Kampuni ya Bahati Nasibu Tatu Mzuka imekabidhi kalenda 500 kwa Jeshi la Polisi nchini,kama mwanzo wa uhusiano mwema utakaozaa matunda kati ya Tatu Mzuka na Jeshi la Polisi. 

Akizungumza na waandishi habari wakati makabidhiano ya kalenda kwa Jeshi la Polisi mapema jana , Msemaji wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga amesema wameamua kutengeneza kalenda 500 za Jeshi la Polisi kama sehemu ya kujenga uhusiano bora, lakini pia kuendeleza kauli mbiu ya Tatu Mzuka ya ukishinda Tanzania inashinda pia. 

Maganga amesema wao ni raia wema wa Tanzania hivyo ni nafasi ya pekee kuwa mbele kutokana na kazi ambayo inafanya jeshi la Polisi katika kulinda watu na mali zao chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro,na kwamba Kauli mbiu ya Tatu Mzuka “Ukishinda Tanzania inashinda”, 

“Mchezo wa bahati nasibu wameweza kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Temeke katika kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kuwasaidia wananchi wa Mbande baada ya mapolisi kuuliwa kwa kutokuwa na kituo maeneo ya karibu. 

" Tumefanya kitu hiki kwa niaba ya washindi wa mchezo wetu wa bahati nasibu,ambao mpaka sasa wamefikia idadi ya milioni 6 ambao wote wamehakikishiwa usalama wao na jeshi la polisi.Mkuu wa jeshi la Polisi ( IGP ) Simon Sirro ameeleza kuukubali mchezo wa kubahatisha nchini wa Tatu Mzuka unaoshika kasi kwa kubadilisha maisha ya Watanzania wengi. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akipokea kalenda za jeshi hilo zilizokabidhiwa na viongozi wa Tatu Mzuka kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi, Posta jijini Dar es Salaam juzi."Mmefanya jambo jema lakini pia mmeonyesha mfano kwa wengine, binafsi nimeguswa na mwamko wenu, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi," alisema IGP Sirro.

SDA YATOA MAFUNZO KWA SANAA YA MAIGIZO YA JUKWAANI

$
0
0
Ili kupunguza Changamoto zinazomkabili Mwanafunzi hasa wa KikeShirika la Sports Development Aid SDA Limefundisha Sanaa ya Jukwaani walimu wa shule kumi za Mkoa wa Mtwara Manispaa na Mtwara Vijijini kwa lengo la Kuwafundisha wanafunzi Madhara ya Mimba za Utotoni.

Shirika Hilo ambalo Linawatumia wakufunzi waliobobea katika sanaa za Jukwaa kutoka Nchini Finland tayari limenza kuzunguka mashulni na kukagua kwa jinsi Gani Mafunzo waliyoyatoa yameweza kuwafikia wanafunzi kupitia walim wa Michezo waliokwisha kupewa Mafunzo.

Katika mafunzo hayo Walimu walipewa Fursa ya kuandaa mada ya Igizo Kuhusiana na Changamoto za Mimba mashuleni zinazowakabili na baadaye Kuonesha Igizo kwa njia ya Sanaa za majukwaani kwa lengo la Kutatuz Changamoto zinazotokana na Mila na Desturi za Jamii Husika.

Thea Swai ni Meneja Mradi wa SDA anasema Muda wa Kufanya Mafunzo kwa Njia ya Vitendo ni mdogo kwa wanafunzi kutokana na Baadhi ya shule Kushindwa kutenga Ratiba maalum kwa ajiili ya wanafunzi kuweza Kufanyia mazoezi na Kufikisha Ujumbe.
 Msanii wa Maigizo Yvone Sherry maarufu Monalisa Akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele Mkoani Mtwara Katika Moja ya Onesho la sanaa za Maigizo ya Jukwaani  Kuhusiana na Changamoto zinazowakumba Wanafunzi wa Kike.
 Wakufunzi wa Sanaa ya Maigizo ya Jukwaani  Pinja Hanton na Niina Sillanpaa kutoka nchini Finlanda Finland Wakiongea na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya naliendele Kuhusiana na Sanaa Hiyo
 Ari Koivo Mkurugenzi wa shirika la LiiKery-Sports& Development la Finland akiongea na wanafunzi wa Sekondari ya Naliendele kuhusiana na majukumu yanayofanywa na shirika lake.
 Mwenyekiti wa Waigizaji Tanzania BONGO MOVIE Elia Mjatta  akitoa mafunzo ya Jinsi ya Ushirikishwa katika sanaa ya maigizo ya Jukwaani.

CRDB TAWI LA VIVA WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAHAMASISHA WANAWAKE KUFUNGUA AKAUNTI YA MALKIA

$
0
0
 Mgeni rasmi GeminaLukuvi akizungumza wakati wa benki ya CRDB tawi la VIVA wakisheherekea siku ya wanawake dunia pamoja na kuwashawishi  jinsi ya kuhifadhi pesa zao za akiba kwa kila mwezi kwa mwaka mmoja.

WAFANYAKAZI benki ya CRDB tawi la VIVA jijini Dar es Salaam washeherekea siku ya mwanamke duniani kwa kuwahamasisha akina mama na wanawake kwa ujumla kufungua akaundi ya Malkia kwaajili ya kujiwekea akiba zao.

Hii ni sawa na kibubu cha wanawake ambapo kila mmoja anaweza kuweka akiba yake ndani ya mwaka mmoja pamoja na kupata faida.
Hii inaleta amani ya moyo kwakuwa akiba inakuwa salama pamoja na kuwa na kinga yake ni imara.

Pia tujifunze kwa baadhi ya wanawake waliofanikiwa ili kila mwanamke afanikiwe kwa kufanyka kazi kwa bidii zaidi na kutumia utashi katika kufanya shughuli zetu mbalumbali.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawila Viva waiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Naomi Mwamfupe akizungumza na wanawake wa Benki hiyo jijin Dar es Salaam jana wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Baadhi ya wanawake wakiungana na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la VIVA jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanawake wakiwa katika benki ya CRDB tawi la Viva jijini Dar es Salaam wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 kila mwaka kwaajili ya kujua mchango wa mwanamke katika nafasi mbalimbali za ajira pamoja na kujua dhamani ya Mwanamke katika jamii.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB  tawi la VIVA jijii Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Ester Kitoka akizungumza na wanawake wakati wakisheherekea siku ya mwanamke duniani iliyofanyika katika tawi la VIVA.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Ester Kitoka akizungumza na wanawake waliungana pamoja na kuzungumza namna mwanamke anaweza kuhifadhi pesa zao kwa kufunguua akaunti ya Malkia.
Injinia wamajengo na barabara na Mjasiliamali na Maida waziri akizungumza wakati wa kusheherekea siku ya wanawake duniani ambay hufanyika kila Machi 8 kila mwaka . pia amewahamasisha vijama pamoja na kinamama kujiamini wakati wakifanya shughuli zao za maendeleo.

ASASI YA KIRAIA YA FEDHA KUJA NA MRADI WA “VIJANA NA ELIMU YA PESA” (VIEPE)

$
0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kutambulisha mradi wa "Viepe" kwa kutoa elimu kwa vijana wa sekondari kakika mkoa wa Dar es Salaam na baadae Tanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa FEDHA, Mohamed Mchoro na kushoto ni  Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei. 

ASASI ya kiraia ya Financial Education for Development and human Achievement (FEDHA) Machi 28 mwaka huu kuzindua mradi wake juu ya kuelimisha vijana kuhusu udhibiti sahihi wa pesa binafsi katika nyanja za utafutaji na utumiaji pesa, uwekaji akiba, uandaaji wa bajeti na uwekezaji wa pesa ili kuwawezesha kukuza ustawi wao wa kipesa na kufikia uhuru wa kifedha.

Hayo ameyasema Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa 

Akizungumza kuhusu asasi ya FEDHA, Bw. Jafari Selemani – Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo amesema “Asasi ya kiraia ya FEDHA ni asasi pekee ambayo imejikita katika utoaji wa elimu ya udhibiti pesa binafsi ili 
kukuza uelewa wa masuala ya kifedha kwa umma wa watanzania kuanzia ngazi ya chini yaani wakiwemo watoto, vijana hadi watu wazima, dhima yetu ni kuwafanya watanzania wapate ujuzi,weledi na taarifa sahihi 
juu ya masuala ya kifedha ambapo itawasaidi kufanya maamuzi ya kujiamini yenye manuufaa kwao binafsi na kwa nchi katika kuhakikisha tunapata sekta ya fedha na uchumi imara na endelevu”

“Malengo ya FEDHA ni, kukuza ustawi wa 
kipesa kwa kutoa elimu; kuwezesha watanzania kutambua wajibu na haki zao kama watumia wa bidhaa na huduma za kifedha; kushiriki kuleta ujumuishi wa uchumi na kifedha Tanzania; na Kushirikiana na wadau 
mbalimbali katika kupambana na Umasikini pamoja na udhibiti finyu wa rasilimali fedha.” amesema Selemani.

Kwaupande wake Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei amesema  kuwa,”Mradi wa Vijana na Elimu ya Pesa ni mradi ambao unalenga kuongeza weledi, ujuzi na uwezo wa vijana juu ya udhibiti na matumizi 
mazuri ya pesa, mradi umelenga vijana hasa wa Elimu ya sekondari.

Vijana ndio muhimili,injini na nguvu kazi ya kuleta maegeuzi ya kiuchumi na hususani tukiwa katika kufanikisha sera ya Tanzania ya viwanda, kwahiyo elimu ya pesa binafsi ni msingi madhubuti kwa uchumi wetu.

Ametoa rai kwa wadau mbalimbali wakiwemo, Serikali kupitia wizara na taasisi zake kama wizara ya fedha na uchumi, wizara ya ajira vijana na kazi, wizara ya elimu, DSE, TIRA, TIC, TIB na  SSRA kuwaunga mkono na 
kuwapa ushirikiano ili waweze kuwafikia vijana na watanzania wengi.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
 
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi (aliekaa kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi wakizungumza kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.

$
0
0
Na WAMJW. Dar Es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeongeza wigo wa kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo nchini kwa kuongeza vituo vya usafishaji damu hadi kufikia vituo zaidi ya 17, na kufanya mafunzo kwa madaktari bingwa ili kuongezea nguvu madaktari bingwa 13 waliopo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika mapema leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.

“Wataalamu tunao 13 kwa upande wa madaktari, tumeiona hiyo changamoto kama Serikali, tumeongeza wigo wakufanya mafunzo kwa madaktari bingwa, na hivi karibuni tutatangaza ufadhili kupitia Serikali, vile vile tumetenga fedha kwaajili ya kuwafundisha madaktari ili kuweza kufanya matibabu ya figo” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kwamba Serikali imeongeza wigo wa usafishaji damu kwa kuongeza vituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo katika hospitali binafsi na Hospitali za Serikali.

“Tumeongeza wigo wa usafishaji damu hadi tunavyoongea, tunavituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu katika hospitali binafsi pamoja na hospitali zetu za Serikali , Muhimbili kuna vitanda 42, Mloganzira kuna vitanda 12, Bugando vitanda 6, KCMC vitanda 6, Mbeya vitanda 6, bila kusahau Regency, TMJ, Agakhan, Hindumandal, na tunaendelea kuimarisha huduma”. Alisema Dkt. Ndugulile.

Vile vile Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imeanza upandikizaji wa Figo na imeshafanikisha kwa mgonjwa mmoja mpaka sasa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na matarajio ni kufanya upasuaji kwa mgonjwa mmoja kila mwezi mmoja.

Aliendelea kusema mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi milioni 37 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama ya kusafisha damu. Aidha, anahitaji kusafiri na kufika kwenye huduma kwa wastani wa safari 126 kwa mwaka sawa na wastani wa safari 3 hadi 4 kwa wiki.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliendelea kuwa kukumbusha kuwa Serikali ya awamu ya tano imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 ilipokuwa ikiingia madarakani hadi sasa ni Bilioni 270 kwaajili ya Dawa, vifaa na vifaa tiba kwaajili ya magonjwa yakiwemo magonjwa ya Figo.

“Tumeongeza bajeti kwaajili ya Vifaa, Dawa na Vifaa Tiba kutoka Bilioni 30 wakati Serikali hii inaingia madarakani mbaka Bilioni 270, yaani mara tisa Zaidi, kwahiyo Dawa na Vifaa Tiba kwaajili ya matibabu ya Figo tunazo” alisema Dkt. Ndugulile.

Mwisho Dkt.Ndugulile alitoa wito kwa wananchi kubadili jinsi ya kuandaa vyakula nyumbani, mfano kwa kupunguza kiasi cha chumvi kwenye chakula na kiasi cha mafuta kutasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza magonjwa shinikizo la damu (hypertension), kisukari na unene wa kupindukia, vile vile kuhamasisha familia kufanya mazoezi.

“Watanzania hatujui kula, tunakula bora chakula kuliko chakula bora, Matumizi ya vyakula vya mafuta, matumizi ya chumvi nyingi, matumizi ya vilevi, matumizi ya sigara kama hayana ulazima basi tupunguze, tutumie vyakula vilivyochemshwa na vilivyochomwa, bila kusahau kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara 3 kwa wiki kwa lisaa limoja inatosha” alisema Dkt. Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria ufunguzi wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo huazimishwa kila machi 8, ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile katika matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.
Kiongozi wa Lions International Club Sayed Rizwan Qadri akikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.4 kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile ikiwa moja ya juhudi za kuunga mkono kupambana dhidi ya magonjwa ya Figo. Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akifanya mazoezi ya viungo wakati wa kujiandaa kuanza kwa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images