Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1535 | 1536 | (Page 1537) | 1538 | 1539 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na WAMJW. Songwe

  Halmashauri  ya Mbozi imekubaliwa kupatiwa mkopo wa shilingi bilioni 1.2 toka Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma yapatayo 49 ya huduma za wagonjwa wa nje(OPD) pamoja na nyumba za watumishi.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya kikazi  kwenye halmashauri hiyo .Waziri Ummy alisema bado kuna changamoto ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini hivyo ameridhia kuwalete  mkopo huo ili kuweza kukamilisha majengo hayo na kuweza kutumika kutoa hudma za afya kwa wananchi.

  “Hatuwezi kujenga vituo vya afya kila kata zote 29, muhimu ni kuangalia jiografia ya eneo husika,idadi ya watu pamoja na changamoto za magonjwa,kwahiyo tunataka uhalisia ili kuona wapi tunataka kuweka kituo cha afya na tujenge pale palipo na mahitaji makubwa”Alisema Waziri Ummy.

  Kwa upande mwingine waziri huyo aliwapongeza Viongozi wa Wilaya hiyo kwa ongezeko la wanawake wanaojifungua katika vituo vya tiba kwa kufukia asilimia 89 ambapo ni kiwango cha juu kwa takwimu za Taifa katika kuendeleza afya ya mama na mtoto ambapo Kitaifa inatakiwa kufikia asilimia 80 mwaka 2020 ya wanawake wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya tiba.

  Aidha,amewapongeza kwa ushiriki wa wanaume katika masuala ya  afya ya mama na mtoto,”hili niwapongeze sana kwani nimelipenda jambo hili kwani ushiriki wa wanaume lazima uwepo kama kunata kufikia kuboresha afya ya mama na mtoto lazima tuwashirikishe wanaume”.

  Hata hivyo amewataka kuendelea kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora kwenye kayapamoja na taasisi zilizopo wilayani hapo” nimeona ni asilimia 37 hivyo muendelee kuhimiza wananchi kuboreshe vyoo vyao kwa sababu tumekua taifa la kulilia dawa dawa na sio kuwekeza kwenye kinga .

  Naye Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mhe.Pascal haonga alitaja changamoto inayowakabili wilaya hiyo ni ukosefu wa watumishi,gari ya kubebea wagonjwa pamoja na kukosekana kwa kitengo cha watoto njiti kwa Mkoa huo ambapo hivi sasa watoto wanaozaliwa  kabla ya muda wao mara nyingi hukazimishwa kupelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya hivyo wakati mwingine hufariki njiani. 

  Akisoma taarifa ya Wilaya hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dkt. Abdul Msuya Alisema  wamefanikiwa kufunga mfumo wa kielectroniki wa kukusanya mapato na taarifa za magonjwa  katika hospitali ya wilaya  na tangu kuanza kutumika februari 2017 wastani wa mapato umeongezeka kutoka shilingi 55,000,000 hadi 75,000,000 .
   Msafara ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Chiku Galawa(wakwanza) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (watatu) wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika chuo cha Uuguzi wa Afya ngazi ya jamii Mbozi.katikati ni Mkuu wa chuo hicho.
   Wanafunzi wa chuo cha Uuguzi wa Afya ngazi ya jamii Mbozi, wakifuatilia kwa makini ujumbe na maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  wakati alipofanya ziara ya kukagua chuo hicho.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akiwajulia hali wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi. Pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akisisitiza jambo mbele ya wanafunzi wa chuo cha Uuguzi wa Afya ngazi ya jamii Mbozi Mkoani Songwe na watumishi wa chuo hicho pindi alipofanya ziara ya kukagua chuo hicho.


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkoa huo, akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Narakauwo, Saruni Ole Sanjiro kadi ya CCM kati ya wananchi 3,500 wa Chadema waliojiunga na CCM jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza na wananchi wa kijiji cha Narakauwo Wilayani Simanjiro juu ya mgogoro wa uongozi na kumuagiza mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula aitishe kikao cha wanakijiji hao ili kujadili tatizo lao.

  WANACHAMA  3,500 wa Chadema katika Kijiji cha Narakauwo, Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Alexander Mnyeti. 

  Wananchi hao ambao awali walikuwa CCM, waliondoka kwenye chama hicho na kujiunga na Chadema, baada ya kigogo mmoja kukata majina ya baadhi ya wagombea waliokuwa wanawaunga mkono kwenye Kijiji hicho na kata hiyo mwaka 2015. 

  Akizungumza jana wakati akiwapokea wanachama hao wapya kwenye mkutano uliofanyika kijiji cha Narakauwo, Mnyeti ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Mkoani Manyara, alitoa onyo kwa wanasiasa wanaowayumbisha wananchi wa eneo hilo. 

  Mnyeti alisema kuna baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo bado wamelala kwani wanadhani huu ni wakati wa kufanya siasa ili hali ilishakwisha mwaka 2015 na huu ni wakati wa kufanya kazi. 

  "Kuna baadhi ya viongozi walikaa vikao usiku ili kukwamisha suala hili, nawapa onyo la mwisho, kama kuna mtu anataka ubunge asubiri mwaka 2020 siyo leo," alisema Mnyeti. 

  Hata hivyo, Mnyeti alimuagiza mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula kuhakikisha anamaliza mgogoro wa uongozi wa kijiji hicho. 

  "Mkuu wa wilaya baada ya siku nne rudi hapa ufanye mkutano wa kijiji kama hawa wajumbe wa serikali ya kijiji ndiyo tatizo fuateni taratibu zote waondoke uchaguzi ufanyike upya," alisema Mnyeti. 

  Alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Yefred Myenzi kuhakikisha uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi za uenyekiti unaofanyia Machi 25, ujumuishe na kijiji hicho.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Ally Kidunda alisema eneo hilo halina upinzani ila wanachama hao waliondoka kwa sababu ya hasira. 

  Kidunda aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa wanachama hao wapya ili kutimiza dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya. 

  Mmoja kati ya wanachama hao wapya, Mathayo Lesenga alisema awali waliondoka CCM baada ya wagombea waliokuwa wanawaunga mkono kukatwa majina yao. 

  Lesenga alisema wananchi wa eneo hilo walikuwa na imani na CCM lakini baada ya kuona kunafanyika ukiritimba walijitoa na kuhamia Chadema ila sasa hivi wamerudi ili kumuunga mkono Rais Magufuli na Mnyeti. 


  0 0

   Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiapa mbele ya Jaji Kiongozi Ferdinand Wambari kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Polisi na Magereza. Tukio hilo limefanyika leo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Polisi
   Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (kulia),  akipokea hati ya kiapo kutoka kwa  Jaji Kiongozi Ferdinand Wambari, ambayo inamuwezesha  kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Polisi na Magereza. Tukio hilo limefanyika leo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Polisi
   Kamishna wa Uhamiaji, Edward Chogero (kulia),  akipokea hati ya kiapo kutoka kwa  Jaji Kiongozi Ferdinand Wambari, ambayo inamuwezesha  kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Polisi na Magereza. Tukio hilo limefanyika leo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Polisi
   Jaji Kiongozi Ferdinand Wambari,akizungumza na Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro(kulia) na Kamishna wa Uhamiaji,Edward Chogero (kulia), baada ya kuwaapisha kuwa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Polisi na Magereza.Tukio hilo limefanyika leo Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Polisi

  0 0

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo ameongoza maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani huku akiziomba asasi za kiraia, na watu binafsi kushirikiana na serikali kuwapatia kinamama mbinu mbalimbali, mafunzo, mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

  Mama Magufuli pia ameupongeza mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzisha vikundi zaidi ya 400 vya wanawake vinavyojishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo usindikaji mazao, ushonaji, uchoraji na kadhalika, pamoja na kuwa na vikundi vya kukopeshana (VICOBA) vipatavyo 2,748 ambavyo kwa pamoja vina mtaji wa jumla ya shilingi bilioni 10.78.

  "Ni imani yangu kuwa kama mikoa yote na taasisi nyingine za kiserikali na kiraia zitaiga mfano wa Dar es salaam katika kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuwashirikisha kwenye shughuli za ujenzi wa viwanda basi tutawawezesha wanawake kiuchumi ikiwemo kushiriki kwenye shughuli za ujenzi wa viwanda", alisema Mama Magufuli amesema kwenye sherehe hizo zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City.
  Huku akishangiliwa kwa nguvu, Mama Magufuli amesema japokuwa serikali inajitahidi sana kuweka usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake kisiasa, kiuchumi, elimu na afya, serikali peke yake haiwezi kuzimaliza changamoto zote, hivyo ni lazima wananchi wenyewe washiriki katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

  Mama Magufuli amewapongeza viongozi wa awamu zote za nchi, ikiwa ni pamoja na kinamama shupavu wa TANU na ASP na baadaye CCM ambao kwa namna moja ama nyingine wameshiriki katika harakati za kumkomboa mwanamke nchini.

  "Kutokana na umuhimu wa siku ya leo naomba nitambue mchango wa Mama Maria Nyerere, Mama Fatma Karume, Bibi Titi Mohamed, Mama Sophia Kawawa, Bi. Hadija Jabir, Bi Johari Yusuf Akida, Mwajuma Koja, Bi. Mtumwa Fikirini na wengineo wengi. Hatuna budi kuwapongeza sana akinamama hawa kwa kupigania haki za wanawake nchini" alisema.

  Mama Magufuli ametanabahisha kwamba japokuwa vitendo vya unyanyasaji, dhuluma na ukatili dhidi ya wanawake bado vinaendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini, Tanzania  imepiga hatua kubwa na ni  miongoni mwa nchi zinazosifika duniani kwa kulinda na kusimamia haki na maslahi ya wanawake.
  "Hivyo basi hatuna budi kuwapongeza wote walioshiriki katika kulinda na kutetea haki na maslahi ya wanawake nchini", alisema, kabla ya kutembelea maonesho ya wajasiriamali kinamama waliopanga bidhaa zao katika kila pembe ya ukumbi huo.
  Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda pamoja na wakuu wa Wilaya za Kinodnoni na Ilala, Mhe. Kisare Makori na Bi. Sophia Mjema. 

  Wengine ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila pamoja na maafisa  watendaji wa wilaya ya Ubungo.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na  maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018.
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea tuzo maalumu kutoka kwa  wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kwa mchango wake wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika kucheza na kuimba nyimbo za hamasa na wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018  
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubua maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori baada ya kuhutubua wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018. Katikati ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala .
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine  katika picha ya pamoja na wawakilisji wa wajasiriamali wanawake wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali  wanawake wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Machi 8, 2018.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Yusuph Mussa, Korogwe

  MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri,  kutafuta fedha haraka ili kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi.

  Amesema hayo baada ya kufanya  ziara kwenye shule hiyo leo Machi 8, 2018 na kukuta baadhi ya madarasa ya shule hiyo ni tishio kwa usalama wa wanafunzi, kwani kuta na madirisha vinataka kuanguka, hivyo kufungwa kamba ili kuzuia mabati yasiezuliwe na upepo, huku  mabati hayo yakiwa yametoboka.

  Chatanda alisema wasisubiri watoto hao kupata madhara, bali wachukue hatua kwa kumaliza ujenzi wa maboma hayo ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi, Serikali na wahisani.

  "Ofisa Ellimu Msingi (Elias Mavoa) naomba umfikishie salamu Mkurugenzi wa Halmashauri (Shauri). Atafute fedha za haraka tumalize madarasa haya, kwani madarasa haya ya sasa ni machakavu na mimi mwenyewe nimeyaona... haiwezekani dirisha na mbao za bati ziwe zimeshikiliwa na kamba.

  "Lakini kama alivyosema Mwalimu Mkuu (Zena Machite) wakati anatoa taarifa yake, ndani ya madarasa hayo mvua ikinyesha kunavuja na inabidi kuhamisha wanafunzi kwenye madarasa hayo wakati wa mvua" alisema Chatanda.

  Mkuu wa Shule Machite, alisema moja ya changamoto kwenye shule hiyo ni uchakavu wa madarasa matatu na ofisi mbili, ile ya Mwalimu Mkuu na Ofisi ya Walimu.

  Machite alisema mpaka sasa ujenzi wa madarasa hayo matatu na ofisi mbili za walimu umegharimu sh 12,898,000 na hadi kukamilika utagharimu sh. milioni 44.1. Na baadhi ya wadau waliochangia ni jamii sh. milioni 1.9, Mfuko wa Jimbo sh. 575,000, harambee ya wadau wengine sh. 423,000 na fedha kutoka halmashauri sh. milioni 10.

  Machite alisema wanajenga choo kipya chenye matundu 10 kutokana na choo kilichopo kuwa chakavu na kuhatarisha afya na usalama wa wanafunzi, kwani wakati wowote kinaweza kuanguka.

  Alisema hadi sasa ujenzi umebakia umaliziaji ambapo ni milango na madirisha ya vyoo na rangi kwenye baadhi ya maeneo, ambapo hadi sasa ujenzi wa choo hicho umetumia sh. milioni 9.8, na ili kukamilisha kunahitajika sh. milioni 1.5.

  Hata hivyo Chatanda ameahidi kumalizia ujenzi wa choo hicho kwa kutoa sh. milioni 1.5 kupitia Mfuko wa Jimbo,  huku Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Mavoa akimshukuru Chatanda kwa kutoa sh. milioni 1.5 kumalizia ujenzi wa choo.
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda leo Machi 8, 2018 amefika Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga katika Halmashauri ya Mji Korogwe ili kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu. Pichani Chatanda akiangalia choo kipya kwenye shule hiyo, ambapo ili kukamilisha ujenzi wa choo hicho, ametoa sh. milioni 1.5 kupitia Mfuko wa Jimbo.
   Madarasa haya ndiyo yanatumika kwa sasa Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga, Halmashauri ya Mji Korogwe. Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda ambaye amefika  shuleni hapo leo Machi 8, 2018, kukagua ujenzi wa madarasa mapya matatu na ofisi mbili za walimu kwenye shule hiyo, ameitaka Halmashauri ya  Mji Korogwe kutafuta fedha kumalizia ujenzi wa madarasa hayo ili kuwaondolea adha wanafunzi wanaosoma kwenye madarasa haya, ambayo mabati yake pia yanavuja ikinyesha mvua.
  Madarasa matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga, Halmashauri ya Mji Korogwe. Hadi sasa ujenzi huo umegharimu sh. milioni 12 na hadi kukamilika itakuwa sh. milioni 44. 

  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda (kulia) akikagua majengo ya madarasa mapya matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga katika Halmashauri ya Mji Korogwe. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Zena Machita. (Picha na Yusuph Mussa).

  0 0

  Na Ismail Ngayonga. 
  WAWEKEZAJI wa ndani na nje ya Tanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika miradi mikubwa ya ujenzi wa viwanda nchini kwani kwa sasa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi II unaotarajia kuzalisha megawati 240 umekamilika kwa asilimia 90.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Stephen Manda wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Bodi hiyo nchini.

  Alisema kuwa hadi sasa jumla ya mitambo minne kati ya mitambo nane ya mradi huo tayari imeanza kufanya kazi, ambapo katika gridi ya taifa mitambo hiyo inapekeka megawati, hivyo TANESCO imejipanga kuhakikisha kuwa ifikapo Septemba mwaka huu mitambo yote ya mradi huo imeanza kufanya kazi ili kuyafikia mahitaji yote ya umeme nchini.

  Manda alisema kukamilika kwa mradi wa umeme wa kinyerezi II ni moja ya mipango na mikakati ya TANESCO ya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa nishati ya umeme nchini, hatua inayolenga kujenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda nchini.

  Mhandisi Manda alisema kukamilika kwa mradi wa umeme wa kinyerezi II ule wa kinyerezi I wenye umwezo wa kuzalisha megawati 150, na kufanya miradi hiyo kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 390  na hivyo kutasaidia kurahisisha upatikanaji wa sekta ya nishati ambayo kwa sasa mahitaji yake ni megawati 1100 nchini kote.

  "Tukikamilisha miradi yote hii, kutawezesha Tanzania kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1500 ikilinganisha na mahitaji yetu halisi ya megawati 1100, hivyo tuwaomba wawekezaji waje kujenga viwanda kwani kwa sasa tuna umeme wa kutosha kupitia vyanzo vyetu mbalimbali ikiwemo makaa ya mawe, gesi na upepo" alisema Mhandisi Manda.

  Kwa mujibu wa Manda alisema malengo ya Serikali kwa sasa ni kuzalisha kiwango cha megawati 4000 za umeme kupitia vyanzo mbalimbali pindi miradi mbalimbali ya umeme itapokamilika ikiwemo mradi wa stiegler's gorge unaotarajia kuzalisha megawati 2100 za umeme.

  Aidha aliongeza kuwa sasa matumizi ya makubwa ya umeme yapo katika Mkoa wa Dar es Salaam unaotumia kiasi cha Megawati 600 za umeme sawa na asilimia 60% ya umeme wote unaozalishwa nchini kutokana na Mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya viwanda.

  "Mkoa wa Dar es Salaam ndio kinara wa matumizi ya umeme nchini, lakini mikoa kama ya Arusha, Mwanza, na mingineyo hutumia asilimia 50-55 ya umeme wote nchini, hivyo tumejipanga katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na nishati ya uhakika katika kufanikisha dhana ya uchumi wa Viwanda" alisema Barozi.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya ERB, Prof. Ninatubu Lema alisema ERB imeridhishwa na maendeleo ya mradi pamoja na juhudi zilizofanywa na TANESCO katika kuhakikisha kunakuwepo na Wataalamu wengi wazalendo katika mradi huo.

  Aliongeza kuwa mradi wa kinyerezi II ni miongoni mwa miradi mikubwa ya sekta ya nishati inayosimamiwa na Serikali, hivyo ni wajibu wa TANESCO kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa yanasimamiwa na kuzingatiwa ikiwemo shughuli za kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani katika kuendesha mfumo wa mitambo mbalimbali ya mradi huo.

  Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya Wahindisi Nchini (ERB), Mhandisi Patrick Barozi alisema Mradi wa Kinyerezi II ni miongoni mwa miradi mikubwa ya maendeleo ya sekta ya nishati iliyopewa kipaumbele na  Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza dhana ya uchumi wa viwanda.

  Mhandisi Barozi aliwataka wataalamu wa ndani ikiwemo Wahandisi kusimamia kwa kikamilifu viwango vya utekelezaji kwa kuzingatia kuwa mradi huo unatumia vifaa na teknolojia ya kisasa ambayo uchafuzi wa mazingira na hivyo kuongeza ufanisi.
   Wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB), wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ninatubu Lema (mwenye miwani kushoto) wakifuatilia maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Mitambo ya Umeme wa Kinyerezi II,240 MW kutoka kwa Meneja Miradi wa Tanesco Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara yao katika mradi huo leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda(watatu kutoka kushoto) akiwapa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II,wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema (mwenye miwani) wakati wa ziara yao katika mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Msajili wa Bodi ya hiyo Mhandisi Patrick Barozi. Mradi huu utazalisha umeme megawati 240 pindi utakapokamilika.
   Mmoja wa Wahandisi wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (Tanesco) akionyesha namna wanavyosimamia uongozaji wa mitambo ya kuzalisha umeme katika mradi wa Kinyerezi II walipotembelewa na wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema (mwenye miwani) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Msajili wa Bodi ya hiyo Mhandisi Patrick Barozi. Mradi huu utazalisha umeme megawati 240 pindi utakapokamilika.
  Picha ikionyesha baadhi ya mitambo iliyopo katika mradi wa kuzalisha umeme kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II utakaozalisha jumla ya megawati 240 pindi utakapokamilika. (Picha na: Frank Shija).


  0 0

  Mkaguzi wa magari Sagenti, Jackson Mafuru akikagua gari la Afisa Masoko wa Kampuni ya Airtel Prosper Mwanda wakati wa ukaguzi katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Dar es Salaam jana.
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza juhudi zake za kushirikiana na jeshi la Polisi Tanzania ambapo kwa sasa wameshirikiana na polisi kikosi cha barabarani kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Kikosi cha Polisi Trafiki kuhahakisha kuwa magari yote yanakanguliwa na kuwekewa stika za usalama barabarani.

  Kwenye zoezi hilo ambalo limefanyika kwenye makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, maofisa wa kukangua magari kutoka Kikosi cha barabarani walishirikiana na Kampuni ya Airtel kwenye kukagua magari ya kampuni hiyo pamoja na ya wafanyakazi.

  Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Afisa Uhusiano na Matukio Airtel Tanzania Dagio Kaniki alisema kuwa usalama wa barabarani ni la kila mtu na ndio sababu kampuni ya Airtel imeendeleza ushirikiano wake na Polisi Kikosi cha barabarani kwenye kutimiza wito wa Kamishna wa Trafiki Tanzania la kuhakikisha kila chombo cha moto yakiwemo magari ya biashara, magari binafsi, bajaj pamoja na pikipiki zinakanguliwa na kubandikwa stika za usalama barabarani.
  Kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na Polisi kikosi cha barabarani kwenye matukio mengi. Ushirikiano huu umekuwa ni muhimu ili kupunguza ajali. Usalama wa barabarani ni jukumu la kila mtu na ndio sababu Airtel imekuwa mbele kuhakikisha hilo linafanyika, alisema Dagio.

  Leo wakaguzi wa magari wameshiriki pamoja na wafanyakazi kukangua magari yao. Natoa shukrani kwa jeshi la polisi kitengo cha trafiki kwani kufika kwao hapa kumeweza kuokoa muda wa wafanyakazi wetu kwenda kufanya ukaguzi. Sisi Airtel tutaendelea kushirikiana na Polisi kuhakikisha elimu ya usalama barabarani linafikia kila mlengwa, aliongeza Dagio.

  Dagio alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Airtel ya kuitikia wito wa ukaguzi wa magari ili kutimiza wajibu wa kila mtu. ‘Natoa rai pia kwa kile dereva ambaye kwa namna moja au nyingine anakuwa anaandikiwa faini za barabarani. Airtel Money ni suluhisho kwani ni rahisi kutumia kwa ajili ya kulipia gharama hizo.

  0 0

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imeazimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuendesha mafunzo ya kilimo kwa wanawake wakulima wa Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU) ili kuwajengea uwezo ili Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  Akizungumza na wanawake hao, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa moja ya malengo ya kimkakati ya TADB ni kuhamasisha kilimo cha kisasa na cha kibiashara kwa wakulima wadogo wadogo hasa wanawake na vijana nchini.

  Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo ina mikakati ya dhati katika kuwasaidia wakulima wanawake nchini ili hasa katika kutekeleza kwa vitendo Kauli mbiu ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu 2018 isemayo ”Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini.’’ 

  “Katika hili TADB inatambua mchango wa wanawake katika sekta ya kilimo ambao wengi wao wako vijijini na ndio wazalishaji wakubwa wa chakula katika taifa letu,” alisema.  

  Bibi Kurwijila alisema kuwa kulingana na takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu asilimia 69 ya wanawake nchini wanajishughulisha na shughuli za kilimo hivyo kiwango hiki kinazidi kiasi cha wanaume wanaojishughulisha na kilimo ambao ni asilimia 64 tu.   

  Kuhusu changamoto zinazowakabili wakulima nchini, Bibi Kurwijila alisema kuwa mwaka 2017 TADB iliunda sera rasmi inayotoa mwongozo wa namna ya kuwafikia wanawake katika utoaji mikopo ya kilimo na huduma nyingine za kibenki ikiwemo utoaji mafunzo.

  “Kwa mujibu wa sera hii angalau asilimia 20 ya mikopo na huduma za kibenki zinazotolewa kwa wakulima zinatakiwa kuwanufaisha wakulima wanawake,” alisema.

  TADB ilitumia nafasi hiyo kwa kuwapatia hundi ya shilingi milioni nne kwa ajili ya ununuzi mashine ya kusukuma maji ili kutatua changamoto za maji ya umwagiliaji mboga mboga iliyokuwa inawakabili wakulima hao. 

  Katika wiki muhimu tunayoelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na kama mdau mkubwa wa kilimo, TADB iliandaa mafunzo kwa wakulima wanawake walio chini ya mwavuli wa CHAURU na Faraja Women’s Group kwa ajili ya kutambua mchango wa wanawake katika kilimo nchini.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Rosebud Kurwijila akizungumza na wanawake wanaojishughurisha kilimo walio chini ya mwavuli wa CHAURU na Faraja Women’s Group (hawapo pichani).
   Afisa Biashara Mwandamizi wa TADB, Eunice Mbando akizungumza na wanawake kuhusu fursa za mikopo nafuu kwa wakulima itolewayo na Benki ya Kilimo nchini.
   Baadhi ya wanawake wanaojishughurisha kilimo walio chini ya mwavuli wa CHAURU na Faraja Women’s Group  wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyotolewa na Benki ya Kilimo nchini.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (aliyekaa kwenye kiti) akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wanaojishughurisha kilimo walio chini ya mwavuli wa CHAURU na Faraja Women’s Group.
  Wanawake wanaojishughurisha kilimo walio chini ya mwavuli wa CHAURU na Faraja Women’s Group wakionesha mfano wa hundi waliyoabidhiwa kwa ajili ya kununulia mashine ya maji.

  0 0

   Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akifurahia mtoto wa kike, alipotembelea wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Mbaala Rangi tatu, wilayani Temeke Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani, leo Machi 8, 2018. Mapema Mama Kabaka akiambatana na kina mama mbalimbali wakiwemo viongozi wa UWT kutoka maeneo mbalimbali, alishiriki kufanya usafi na baadaye kutoa zawadi mbalimbali kwa uongozi na waonjwa kwenye Hospitali hiyo. Kulia ni Mariam Salum, mzazi wa mtoto huyo. 
   "Haya Mama chukua kichana chetu.." akasema Mama Kabaka wakati akirejesha mtoto kwa Mariamu Salum baada ya kumkabidhi zawadi ya kanga.
   Mama Gaudentia Kabaka akitoa zawadi za juisi kwa kina mama waliojifungua katika hospitali hiyo ya Mbagala Ranitatu
   Baadhi ya Kinamama wakaiwa na zawadi za kanga na sabuni ambazo Mama Kabaka aliawa kwa kina amama waliojifunua katika hospitali hiyo.
   "Hebu chukua kanga hii kutoka kwa kina mama wenzako.." akasema Mama Kabaka wakati akimkabidhi Mwajuma Ally aliyejfungua mtoto katika hospitali ya Mbagala Rangitatu
   "Loooh mtoto umejifunugua mtoto mzuri sana..." akasema Mama Kabaka 
   Kisha akampatia zawadi ya mche wa sabuni
   Diwani wa Viti Maalum CCM, Mariam Mtemvu na wenzake wakimsalimia mmoja wa Kina mama aliyekuwa katika Wodi ya Wazazi baada ya kujifungua katika hospitali ya Mbagala Ranitatu, leo
   Ofisa wa Makao Makuu ya UWT Ndugu Kisa wapili kulia, akiwa na kina mama weningine.
   Ofisa wa Makao Makuu ya UWT Ndugu Kisa (kushoto), akiwa na wauguzi na kina mama weningine kwenye hospitali hiyo ya Mbagala Ranitatu leo. 
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akimpa zawadi ya kanga mmoja wa wauuzi katika hospitali ya Mbagala Rangitatu wakati wa ziara hiyo
   "Wauuzi na Madaktari honereni kwa kazi nzuri na hasa kwa kujali afya za kina mama na watoto...endeleni kuchapa kazi tupo pamoja nanyi", alisema Mama Kabaka wakati akizunumza na baadhi ya wauguzi na madaktari wa hospitali ya Mbagala Ranitatu wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Matroni wa wodi ya Wazazi Maria Lumambo
   Mama Kabaka akiendelea kuzunumza nao
   Mweneyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka akifuatana na Matroni wa Wodi ya Wazazi Maria Lumambo, baada ya kutoka wodini kuwaona na kuwapa zawadi wazazi
   Mweneyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka akizungumza baada ya kutoka wodini kuwaona na kuwapa zawadi wazazi
   Picha ya kumbukumbu
  Mweneyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka akiwa tayari kuondoka kwenye Hospitali ya Mbagala Rani tatu baada ya ziara yake leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akimpongeza Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe baada ya kupokea kiasi cha shilingi milioni moja kwaajili ya TIKA huku Mbunge huyo Munde Tambwe akiahidi mbele Mama Salma Kikwete kuchangia jumla ya mifuko Miambili ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Mabweni katika Shule za Sekondari za kata manispaa ya Tabora na ujenzi wa uzio Kliniki ya Tabora mjini maarufu Town Clinic. 
  Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alisema kuna haja ya kuleta mabadiliko ya kisekta yatakayoharakisha maendeleo kwa Wanawake kupitia kujenga misingi imara ya kupata elimu bora itakayotoa fursa kwa Wanawake kuajiriwa na hata kujiajiri wenyewe. 
  Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe akizungumza katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake zilizofanyika kimkoa mkoani Tabora,katika maadhimisho hayo Munde aliwalipia Kadi za matibabu maarufu TIKA Wanawake wasio na uwezo Miamoja wanaoishi manispaa ya Tabora akiwa anakamilisha idadi kama hiyo kwa Wanawake wengine mia moja kwa kila Wilaya za mkoa wa Tabora ambazo ni wilaya saba. 
  Munde akikabidhi jumla ya shilingi milioni moja kwa Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kulipia Kadi hizo miamoja za matibabu kwa Wanawake wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu Manispaa ya Tabora. 
  Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani mkoani Tabora ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi iliyofanyika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora. 
  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry akiungana na Wanawake mkoani Tabora kuadhimisha siku hiyo ya Wanawake duniani 
  Gwiji na Msanii mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Malkia Khadija Kopa akitumbuiza katika maadhimisho hayo mjini Tabora katika viwanja vya Chipukizi. 
  Wanawake wajasiliamali wakiadhimisha siku yao wakati muziiki wa taarabu ukitumbuizwa na Malkia Khadija Kopa.

  0 0


  Rais na Muasisi wa TWA Irene Kiwia akizungumza kwenye kongamano la siku ya wanawake Duniani lililoandaliwa na taasisi ya TWA leo jijini Dar Es Salaam

  Mtoa mada, Anna Chonjo Mariki kutoka Rex & Regina Attorneys akifafanua jambo kwa watoa mada wenzake kwenye kongamano la siku ya wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dar Es Salaam

  Mama Zakia Meghji akizungumza jambo kwa wageni waalikwa
  Judy Dlamini Mwenyekiti wa Mbekani Investment akizungumza kwa wageni waalikwa
  Muongoza mjadala wa kongamano la TWA Lulu Ng’wanakilala (kulia) akielezea jambo kwa wazungumzaji wa la siku ya wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dar Es Salaam , wanaofuata kutoka kulia ni Rebecca Gyumi, Mama Zakia Meghji, Irene Kiwia, Scholastica Kimaro na Mary Rusumbi
  Mshindi wa Tuzo za jumla za TWAA(Woman of Year 2018), Sister Flora Ndwata akipokea Tuzo toka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa Trade Mark Tanzania, John Ulanga kwenye hafla iliyofanyika leo Serena Hotel, Dar Es Salaam

  Judy Dlamini Mwenyekiti wa Mbekani Investment (katikati)akimkabidhi Irene Kiwia kitabu alichozindua cha “ Equal But Different” wanaoshudia Jacquiline Maleko, Zakia Meghji na Sadaka Gandi
  Dkt. Hawa Kawawa (kulia)kwa niaba ya marehemu mama yake Sophia Kawawa akipokea Tuzo ya Maisha (Life Time Achievement) toka kwa Mwenyekiti wa TWA, Sadaka Gandi

  wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini utoaji wa Tuzo
  Washindi wote wakiwa kwenye picha ya pamoja

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. Picha Zote Na MathiasCanal-Wazo Huru Blog
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini (Kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. 
  Maandamano ya wanawake wakielekea katika dhifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. 
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.

  Na Mathias Canal, Bukombe-Geita


  Mwanamke si mtu wa kubezwa kama ilivyo desturi na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke hawezi kufanya jambo lolote kama hatawezeshwa, Hii ni dhana mfu tena iliyopitwa na wakati tumejionea wanawake wangapi ambao wanawawezesha wanaume tena bila hata wao kuwezeshwa.


  Hayo yamesemwa  Leo 7 Machi 2018 na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe na kusisitiza kuwa watanazania hawapaswi Kuishi kwa kukariri ni hatari kwa ustawi wa maisha yetu hivyo ni vyema kama tutaishi kwa kujifunza maana hata tafsiri ya maisha nyepesi ni ile ya kuishi na kujifunza.


  Alisema kuwa Katika Jamii mara kadhaa yameripotiwa matukio mbalimbali ikiwemo yale ya kuwanyanyapaa wanawake, kuwapiga lakini yapo pia matukio ovu kabisa ya kuwabaka wanawake jambo ambalo Serikali inaendelea na juhudi za makusudi kukomesha madhila hayo.


  "Mwanamke ana heshima kubwa ya Jinsia yake lakini pia Wanawake ni mama zetu, dada zetu, wake zetu, wadogo zetu, shemeji zetu, shangazi zetu lakini pia ni Nyanya (bibi) zetu" Alikaririwa Mhe Biteko na kuongeza kuwa


  Kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka 2018 isemayo “Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na uwazeshaji wa wanawake vijijini” inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, Kibiashara, Upatikanaji wa mitaji, Masoko na Mikopo ili waweze kushiriki kwa usawa na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji tu.


  Maadhimisho ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, ambapo inaelezwa kuwa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Duniani kwa mara ya kwanza yalifanyika Februari 28, 1909 huko Marekani.


  Umoja wa Mataifa wenyewe umesema siku hii ni ya kutafakari juu ya hatua za kimaendeleo ambazo wanawake wamepiga, kupongeza juhudiza wanawake wa kawaida kutokana na mchango wao katika historia ya maendeleo ya nchi na jamii zao.


  Mbunge huyo wa Bukombe Mhe Biteko alisisitiza kuwa maadhimisho hayo yaifanya kuwa siku ambayo wanawake hutambuliwa kwa mchango na mafanikio yao bila kujali mipaka ya kitaifa, rangi, lugha, utamaduni, uchumu wala siasa.

  0 0


  Katika jitihada za kuongeza ufanisi wa huduma, benki ya Akiba imezindua akaunti iliyoboreshwa na programme maalum kwa ajili ya vikundi vya kuweka na kukopa (Vicoba). Akaunti hiyo iliyoboreshwa pamoja na programu maalum inayozinduliwa leo vitawawezesha wateja wa vikundi vya kuweka na kukopa kupata huduma za kibenki kwenye simu za mikononi. Kwa mujibu wa kaimu Mkurugenzi wa ACB Juliana Swai, huduma hiyo ambayo haina gharama ni rahisi na itawawezesha wanakikundi kuongeza usalama wa fedha zao, pamoja na uwazi.
   
   “ACB imezindua akaunti ya Vicoba iliyoboreshwa kwa ajili ya vikundi vya kuweka na kukopa ikiwa ni jitihada za kuongeza huduma za fedha shirikishi nchini Tanzania,” alisema. Alisema akaunti hiyo iliyoboreshwa imeunganishwa kwenye programu maalum ambayo itawawezesha wateja kupata huduma popote walipo, bila hata ya kufika kwenye tawi la benki. Faida za kutumia huduma hii ni kutotozwa gharama yoyote, kuuliza salio bila gharama na kuwawezesha wateja kupata huduma za ATM kwenye mfumo wa Umoja Switch.
   
   “wateja wataweza kuweka na kutoa fedha za kikundi kwa uwazi kwani kila muamala unaofanyika kwenye akaunti hufuatiwa na ujumbe kwa kila mwanakikundi kupitia simu zao za mkononi,” alisema. Benki ya ACB imesema ikiwa inaadhimisha siku ya wanawake duniani, hatua hii pia inachangia katika kuongeza uwezeshaji wa wanawake, kwani vikundi vingi vina wanachama wanawake. “Wakati tunasherehekea siku ya wanawake duniani ambayo kauli mbiu yake ni #Weka Msukumo katika maendeleo ya Wanawake Duniani yaani Press For Progress Now, napenda kuwahakikishia wateja wa ACB kuwa tunaweka msukumo huo kwa kuzindua akaunti na programu mpya ya Vicoba,” alisema.
  WAKINA wa VUMWE wakisema kauli mbiu' Press for Progress Now' wakati wa maadhinisho ya sikukuu ya wanawake duniani, jijini Dar es Salaam leo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Bank (ACB), Dora Saria akiwakaribisha wageni katika hafla maalumu ya uzinduzi wa akaunti ya VIKOBA App jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja Fedha wa ACB, Bertha Simon akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo.

  0 0


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel akisisitiza umuhimu wa kuheshimu wanawake wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe Mkoani humo, Jana 8 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
  Baadhi ya wanawake Wilayani Bukombe wakifatilia maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya hiyo Mkoani humo, Jana 8 Machi 2018.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel akiongoza zoezi la ukataji keki kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe Mkoni humo, Jana 8 Machi 2018.
  Mbnge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akichangia shilingi 500,000 kuunga mkono harambee iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel ambaye naye alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya jukwaa la wanawake Jimbo la Bukombe

  Na Mathias Canal, Geita


  Wakurugenzi wa Halamshauri za Wilaya katika Mkoa wa Geita wamekumbushwa kutekeleza wajibu wao kwa kutenga fedha asilimia 4 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake, asilimia 4 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya vijana na asilimia 2 kwa ajili ya watu kwenye ulemavu.


  Wakurugenzi hao wametakiwa kuongeza kasi katika kuendelea kuchambua na kutambua vikundi vya wanawake na vijana vyenye mwelekeo wa kuzalisha Mali ghafi kwa ajili ya kulisha viwanda vidogo na vya kati ili kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.


  Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe.


  Alisisitiza kuwa vikundi hivyo vinapaswa kujengewa uwezo wa kifedha, mafunzo pamoja na vifaa na hatimaye viweze kuchangia katika azma ya Serikali ya Tanzania ya uchumi wa viwanda kwani kupitia fursa hizo wanawake wengi watajiajiri na kuajiri watu wengine katika sekta isiyo rasmi.


  Alisema kuwa sambamba na kuwajengea uwezo wanawake lipo jukumu la kuwalinda wanawake hao pamoja na wasichana dhidi ya vitendo vya ukatili kimwili kama vipigo, ubakwaji, ndoa za utotoni na kuwarubuni kimapanzi wabinti wadogo.


  Aidha, amezitaka mamlaka zote ndani ya Mkoa wa Geita kuhakikisha zinatoa ushirikiano kwa wajumbe wa kamati zinazoundwa katika ngazi zote ili kwa pamoja kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinatokomezwa.


  Katika hatua nyingine Mhe Gabriel amezitaka Halmashauri za Wilaya kushirikiana na wadau mbalimbali kutenga bajeti na kuendelea kuweka mipango shirikishi ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu na usalama wa mtoto wa kike na kulinda mustakabali wake kwa kumuwezesha kiuchumi, kielimu, kiafya na kumlinda dhidi ya vitendo vya ukatili kimwili.


  Alisema kuwa kauli mbiu ya Kitaifa kwa mwaka huu ni "KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI" imeakisi dira ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa muktadha wa kuhakikisha Tanzania inakuwa ni nchi ya uchumi wa viwanda.


  Alisema Serikali inatambua nguvu na ufanisi wa wanawake kwani kupitia vikundi vya kiuchumi, VICOBA, SACCOS na vikundi vya kijamii wamekuwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi; Uchakataji wa malighafi ili kuongeza thamani, biashara ndogondogo, ufugaji ushonaji nguo, kilimo cha mazao, bustani za mbogamboga na matunda na nyinginezo.


  Katika maadhimisho hayo Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko amewapongeza wanawake Duniani kote kwa maadhimisho hayo ya siku muhimu kwao huku akiahidi kuongeza ushirikiano kupitia vikundi vya mbalimbali ambavyo ni msingi wa ustawi na uimara wa Jumbo hilo na Taifa kwa ujumla wake.


  Sambamba na hayo pia Mhe Biteko amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa kuunga mkono harambee iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel ambaye naye alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya jukwaa la wanawake Jimbo la Bukombe.

  0 0

    NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mkuranga
  NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, ameendelea kuwabana waajiri wanaokiuka sheria za nchi ambapo leo Machi 8, 2018 amehamia wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani na kuvitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 32, viwanda vitatu kwa  ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Kazi na Uhusiano Mahala pa Kazi.

  Viwanda vilivyoadhibiwa ni pamoja na kiwanda cha kutengeenza yeboyebo cha Dorin Investment Company Limited, (milioni 14), LM Furniture, (milioni 7), na Tingtang, (milioni 14), adhabu hizo zimetangazwa leo Machi 8, 2018 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde wakati wa ziara yake ya kushtukiza ili kubaini waajiri ambao wanakiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini, na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

  Kwa mujibu wa Naibu Waziri, viwanda hivyo vimekiuka sheria kwa kuhatarisha maisha na afya za wafanyakazi kutokana na mzingira hatarishi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi kutokuwa na vifaa vya kujihami (protective gears), kufanya kazi masaa mengi bila ya kulipwa malipo ya muda wa ziada ambao uko nje ya muda wa kisheria wa mfanyakazi kufanya kazi.

  Aidha Naibu Waziri ameagiza uongozi wa viwanda hivyo kuwasilisha nyaraka  muhimu kwa Kamishna wa Kazi, Jumatatu ijayo kwani nyaraka nyingi walizotakiwa kuzionyesha hawakuwa nazo, ikiwa ni pamoja na mikataba ya kazi, salary sleeps za wafanyakazi wao.

  Sambamba na hilo Mheshimiwa Mavunde ameuagiza Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), kumfikisha mahakamani mara moja mwajiri wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya plastiki, cha Tisino kwa kutojisajili na WCF kama sheria inavyotaka.

  Naibu Waziri Mvunde yuko katika ziara ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini, na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na kuonya kuwa waajiri wote ambao bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili WCF watapelekwa mahakamani na serikali haitabadili msimamo huo hadi hapo matakwa ya kisheria yatakapotekelezwa na waajiri wote nchini.

  Naibu Waziri Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeenza fanicha cha LM Furniture, ambapo aliwakuta wakifanya kazi katika mazingira hatarishi, wakiwa hawana vifaa vya kujihami, (protective gears).
   
   Naibu Waziri Mavunde akitoa maagizo kwa viongozi wa kiwanda cha kutengeenza viatu vya plastiki (yeboyebo), cha Dorin.
  Naibu Waziri Mavunde, akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha  LM Furniture ambaye licha ya kufanya kazi ya kuhamisha vitu vyenye ncha kali, kama vyuma na mabati hakuwa amevaa gloves, wala viatu vigumu (gumboots). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Mhe. Filberto Hassan Sanga (katikati), akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano -WCF, Bi. Laura Kunenge.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Mhe. Filberto Hassan Sanga (katikati), akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, (wapili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (wakwanza kushoto) na Meneja wa kiwanda cha Tingtang, Bw. Lee.
   Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
    Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
    Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
   Mhe. Mavunde akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha Tingtang, Bw. Lee.
   Wafanyakazi wa kiwanda cha Dorin, wakimsikilkzia Mhe. Mavunde, alipozungumza nao

   Maafisa wa juu waliofuatana na Mhe. Mavudne wakiwa pamoja na maafisa wa Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Mkuranga.
  Bw. Lee akijieleza mbele ya Mhe. Mavunde, na Kamishna wa Kazi, Bi. Hilda Kabisa,

  0 0


   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima akizungumza na Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD) waliofika Hospitalini hapo Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia na vitu vingine mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake MSD, Neema Mosha, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela na Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Deodata Msoma.
   Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima,  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack)
   Wanawake wa MSD wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima baada ya kupokea msaada huo.
   Kutoka kushoto ni  Florence, Agatha na Naomi wakifurahia jambo wakati wakiwa nje ya wodi ya wazazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakisubiri kutoa msaada huo.
   Wanawake wa MSD, wakiwa nje ya wodi ya wazazi wakisubiri kutoa msaada.
   Hapa wakiwa na Mifuko yenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) tayari kwa kwenda kukabidhi wodini.
   Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Deodata Msoma akiwaekeza jambo Wanawake wa MSD wakati akiwakaribisha wodini kwenda kutoa msaada huo.
   Wakina mama na baba wakiwa nje ya wodi ya wazazi na watoto wao katika hospitali hiyo.
   Vifaa vikiwa vimebebwa tayari kwa kutolewa kwa wajawazito.
   Maboksi yenye vifaa hivyo yakishushwa kwenye gari.
   Safari ya kwenda wodini kutoa msaada huo.
   Hapa wakiserebuka Makao ya Taifa ya Kurasini ya Kulelea Watoto Yatima na Wenye Shida.
   Wakijumuika na watoto wanaoishi kwenye makao hayo.
   Baadhi ya mifuko yenye chakula vilivyo tolewa.
   Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange akizungumza na wanawake wa MSD.
    Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi msaada wa vyakula na vitu vingine Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha.
   Msaada huo ukitolewa
  Picha ya pamoja.

  Na Dotto Mwaibale

  WANAWAKE Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke pamoja na chakula kwa watoto wanaolelewa Makao ya Taifa Kurasini ya Watoto Yatima na Wenye Shida jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD,  Neema Mwela alisema kwao ni faraja kubwa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wanawake wenzao katika hospitali hiyo pamoja na watoto hao.

  "Sisi wanawake wa MSD tuliona ni vizuri tukasherehekea siku yetu pamoja na wakina mama waliopo katika hospitali hii pamoja na watoto wanaolelewa katika makao ya taifa ya Kurasini kwa ajili kula nao chakula cha mchana pamoja na kuwapa msaada wa chakula na vitu mbalimbali" alisema Mwela.

  Mwela alisema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke waliweza kutoa Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000 na vifaa vingine vinavyohitajika kama sabuni na miswaki.

  Akizungumzia watoto Yatima na wenye shida wanaolelewa katika makao ya Kurasini alisema ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia watoto hao badala ya kuiachia serikali pekee.

  Alisema kazi ya malezi ya watoto hao ni kubwa mno hivyo kila mtu anapaswa kuwa na majukumu ya kuwalea kwani kumlea mtoto tangu akiwa mdogo hadi kufikia miaka 18 ni kazi kubwa.

  Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange alisema katika makao hayo kuna watoto wanaosoma shule mbalimbali za msingi, sekondari na shule za awali na kuwa kama kuna mtu anayehitaji kumchukua mtoto wa kwenda kuishi naye taratibu zote zinaanzia ofisi za ustawi wa jamii zilizopo kwenye manispaa husika.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha alisema waliguswa sherehe za siku ya wanawake duniani mwaka huu kuwatembelea wanawake wenzao waliopo wodi ya wazazi kwa ajili ya kujifungua pamoja na kula chakula na watoto Yatima na wale wenye shida waliopo Kurasini na kuwapa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya matumizi ya shule.

  Alisema fedha za kununulia mahitaji hayo zilichangwa na wao pamoja na wafanyakazi wanaume wa MSD na kuwa thamani ya fedha kwa ajili ya kununulia vitu hivyo ilikuwa ni shilingi milioni 3.5 wakati vifaa vya hospitalini viligharimu shilingi milioni 7.

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima alishukuru kwa msaada huo nakuleza kuwa changamoto kubwa walionayo ni majengo ya hospitali hiyo kuwa machache kutokana na ongezeko la wagonjwa na uboreshaji wa miundombinu.


  0 0

   Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi akitoa zawadi kwa Mmoja ya Wanawake waliolazw aktika wodi ya wamama katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo UWT Kinondoni walifika katika Hospitali hiyo kutoa Msaada katika kuadhimisha  siku ya Wanawake Dunia
   Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Kinondoni, Nuru Mwaibako, akiwa na Diwani Viti maalum CCM  Kinondoni  Frolenece Masunga wakikabidhi zawadi kwa Wanawake waliofka katika Clinic ya Hospitali ya Mwananyamala na watoto wao, UWT Kinondoni wamefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wamama waliopo katika Hospitali ya Mwananyamala.
  Diwani Viti maalum CCM  Kinondoni  Frolenece Masunga akiwa amemshika mmoja ya Watoto waliofika kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
  Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni kwa Pamoja wakimkabidhi zawadi Mganga wa Hospitlai hiyo kwa ajili ya Wanawake wa Hospitali hiyo.
  Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ukiwasili katika Hospitali ya Mwananyamala ukiongozwa na Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi

  0 0  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  SERIKALI imesema inaendelea na utaratibu wa ukarabati wa shule kongwe nchini ikiwemo za sekondari na ufundi ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali ya ubunifu kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kisasa kulingana na mazingira yanavyobadilika .

  Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk.Avemaria Semakafu wakati alipokuwa akizungumzia kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  Ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF).

  Dk.Semakafu amesema ni vyema wakajirudisha kwenye mazingira yetu ya kitanzania kwa kuwafanya wasichana kuwa wabunifu kuanzia ngazi ya familia na shuleni ili kupata wasichana viongozi.

  Amefafanua Shule za Sekondari Ifunda, Tanga, Mtwara na Moshi ambazo tangu awali zilikuwa zikitoa mafunzo ya ufundi, zinaendelea na ukarabati na wanatarajia mwaka wa masomo 2018,19 kuanza kidato cha kwanza.

  Amesema ni kosa kubwa lililofanyika la kufuta shule za sekondari za ufundi kwani mwanafunzi anapomaliza anakuwa hana elimu yoyote kuhusu masuala ya ubunifu.Ameongeza masuala ya ubunifu yamewekewa mkazo katika elimu ya juu pekee, hivyo inawaacha wanafunzi wengi wa elimu za chini.

  "Elimu ni haki ya msingi kwa kila mtanzania na elimu bure imesaidia watoto wengi kuandikishwa elimu ya msingi.Kurudisha shule za sekondari za ufundi kutasaidia uwiano kati ya wanawake na wanaume wanaofanya masuala ya ubunifu," amesema Dk.Semakafu.

  Amesema Tanzania ya viwanda itawaacha wengi chini na wengine wenye elimu ya watakaochujwa endapo hawajifunza masuala ya sayansi na teknolojia mapema.

  ‘’Shule za ufundi zinasaidia watu wengi waliopata elimu hii mapema zaidi na humpa mtoto kuchagua kama anapenda masuala ya ufundi au la. Kuboresha shule hizi kutasaidia sera ya muelekeo wa Tanzania ya viwanda na si kubaki pale ilipo,’’ amesema.Aidha, amesema udahili shule za msingi wasichana ni wengi kuliko shule za sekondari na vyuo vikuu, hivyo wanapaswa kuweka mikakati kwa kuangalia ni changamoto gani zinazowakabili wanafunzi hao.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Kimataifa (DFID), Jane Miller amesema Serikali ya uingereza imesaidia wasichana milioni 5.3 wa shule za sekondari na msingi na kuokoa maisha ya wajawazito na watoto 103,000.

  Miller amesema Serikali hiyo imesaidia kuwapatia mtaji wanawake milioni 36 kwa ajili ya kujiinua kiuchumi kwa kutumia ubunifu mbalimbali."Serikali ya Uingereza kupitia Mfuko wa Maendeleo ya watu (HDIF) umewekeza hapa nchini zaidi ya Euro milioni 39 kwa ajili ya kusaidia masuala ya ubunifu yanayoleta matokeo chanya katika elimu, afya, maji na usafi wa mazingira,"amesema Miller.

  Naye, Naibu Mkurugenzi wa HDIF, Joseph Manirakiza amesema wameandaa kongamano hilo ili kutoa fursa kwa watu kujifunza namna wanawake walivyofanikiwa katika masuala ya ubunifu."Tunayo miradi mbalimbali inayowasaidia wanawake kujiinua kiuchumi na lengo ni kuwafikia wanawake wote wa mijini na vijijini ili kuleta usawa wa kijinsia na kushiriki katika maendeleo,"amesema.
   Naibu Kiongozi  Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumza juu ya  kongamano hilo ili kutoa fursa kwa watu kujifunza namna wanawake wamefanikiwa katika masuala ya ubunifu na kuleta maendeleo katika jamii inayoiwazunguka.
   Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk Avemaria Semakafu  akizungumza katika kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)

   Mmoja wa watu waliokuwa katika uchangiaji mada aliekuwa mrembo wa Miss Tanzania na kutwa taji la urembo wa Afrika Nancy Sumari akizungumza jambo wakati wa kongamano la Wanawake lililoandaliwa na mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
   Wadau mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
   Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka shirika la Dot Tanzania, Ndimbuni Msongole akizungumza jambo juu ya ubunifu kaytika nyanja ya mawasiliano wakati wa Kongamano la Wanawake na ubunifu lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
   Mkurugenzi wa tasisi ya Empower, Miranda Naiman akizungumzia namna walivyoweza kuwawezesha wanawake na vijana katika kujikwamua wakati wa kongamano lililoanadaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
   MWanawake kutoka tasisi ya Pink Ijabu walioshiriki katika kongamano hilo lililoandaliwa na mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
  washiriki wa kongamano la siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na  mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay mara baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa Elimu wa mkoa wa Geita kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi hilo la Benki.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kupiga makofi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati msanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Chato alipokuwa akitoa burudani ya ngoma hiyo.
   Mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akimwagiwa Rangi kabla ya kuonesha umahiri wake wa kucheza ngoma hiyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard Jensen wakati akielekea kwenda kufungua Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara baada ya kutoka kwenye ufunguzi wa tawi hilo la benki ya CRDB lilopo Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


older | 1 | .... | 1535 | 1536 | (Page 1537) | 1538 | 1539 | .... | 1898 | newer