Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AIAGIZA WCF KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAAJIRI 6,907 AMBAO WAMESHINDWA KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0





NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekelkeza takwa hilo la Kisheria ikiwa ni pamoja na wale ambao hawateketekelezi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini.Akiwa kwenye kiwanda cha kugandisha barafu cha Boghal kilichoko Chamazi, Naibu Waziri pia aliahgiza kukamatwa mara moja wafanyakazi watatu raia wa kigeni ambao walikutwa hawana vibali vya kufanyia kazi.

“Dar es Salaam kuna jumla ya waajiri 14,484, na kati ya hao, 6,907, tumebaini bado hawajajisajili na nimewaagiza maafisa wa WCF kuwafikisha mahakamani mara moja kuanzia kesho mashtaka dhidi yao yaandaliwe, (leo).” Aliagiza Naibu Waziri Mavudne ambaye alifuatana na Kamaishna wa Kazi Bi. Hilda Kabisa, na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.

Aidha Naibu Waziri Mavunde, aliagiza wafanyakazi watatu wa kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, kilichoko Chamazi nje kidogo ya jiji kukamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.“Nitoe wito kwa waajiri nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha uratibu ajira za wageni, kinaelekeza kuwa hataruhusiwa mgeni yoyote kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali, na hawa tumewauliza vibali vyao hawakuwa navyo kwa hivyo nimeagiza wakamatwe na wapelekwe polisi na kasha wafikishe mahakamani.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mavunde.

Ziara ya naibu waziri ni muendelezo wa operesheni inayoendelea nchini kote kuwabaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bi. Rehema Kabongo, alisema Mfuko umeanza kutekeleza maagizo ya serikali kwa kuwafikisha mahakamani wale wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko ambao wanakabiliwa na adhabu ya kulipa faini isiyopungua shuklingi Milioni 50, (Milioni Hamsini) au kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

“Nitoe wito kwa wafanyakazi, operesheni hii ndio imeanza na kama bado kuna mwajiri ambaye bado hajatekeleza wajibu wake asisubiri kufikishwa mahakamani.” Alisema.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akizu nguzma jambo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), jijini Dar es Salaam Machi 6, 2018. Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bi. Rehema Kabongo.
Mhe. Mavunde, na Bi. Rehema wakipitia nyaraka
Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akizungumza jambo na Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Bi.Hilda Kabisama.
Afisa Mwajiri kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani akijieleza kwa Naibu Waziri Mavunde baada ya kubainika kiwanda hicho kinakiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini. kwa kutowalinda wafanyakazi kwa kuwapatia vifaa vya kujihami.Kiwanda hicho kimetozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa kosa hilo na mengineyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, (mwenye suti), akizunhumza jambo wakati alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam jana (Machi 6, 2018), ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Jumla ya waajiri 6,907 jijini Dar es Salaam, hawajajisajili na Mfuko na watapelekwa mahakamani.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Carmel akilalamika mbele ya Naibu Waziri Mavunde, kuhusu mazingira mabovu ya kufanyia kazi na mishahara midogo kinyume na maelekezo ya serikali



Naibu Waziri akiumuuliza mfanyakazi huyo wa kiwanda cha kugandisha barafu, ambacho pia kimebainika kufanya shughuli za kuchomelea vyuma, baada ya kumkuta hana viatu vigumu (gumboots)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, akizunguzma mbele ya Meneja wa kiwanda cha Carmel Concrete, Nabil Kassim, (kushoto), kuhusu kutowalinda wafanyakazi wake.

Naibu Waziri akiongozana na Kmaishana wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa na maafisa wengine wakati wakiwasili kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, huko Mbagala Chamazi nje kidogo ya jiji.

MWILI WA DK. AMANI KABURU KUSAFIRISHWA KESHO KIGOMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

MWILI wa aliyekuwa Mbunge  wa  Kigoma  Mjini, Mbunge  wa  Bunge la  Afrika  Mashariki na Mwenyekiti mstaafu  wa  Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Kigoma Dk.Amani Walid Kaburu ambaye amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili unatarajiwa kusafirishwa kesho.

Taarifa zilizotufikia zinaeleza mwili wa Dk.Kaburu utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Dk.Kaburu kabla ya kufikwa na umauti alikuwa Hospitali ya Muhimbili ambapo alifikishwa kwa ajili ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili(kiharusi).

Kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea kabla ya kuelekea Kigoma.Michuzi Blogu itaendelea kutoa taarifa za msiba huo kadri zinavyotufikia.

HISTORIA FUPI YA DK.KABURU

Dk. Kaburu alizaliwa 23 Mei mwaka 1949 na enzi za uhai wake amefanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa nchi na amekuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kwenye vyama vya siasa nchini.

Enzi za uhai wake Dk. Kaburu amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na akiwa kwenye nafasi hiyo alifanya kazi kubwa ya kuuimarisha upinzani na hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Ambapo uongozi wake kwenye nafasi hiyo alifanikiwa kushawishi wananchi wengi wa Mkoa wa Kigoma kujiunga Chadema.Hata hivyo Septemba mwaka 2006 alijiunga na CCM na Oktoba mwaka 2012 akawa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Pia Dk. Kaburu enzi za uhai wake amewahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia Juni 5 mwaka 2007 hadi Juni 4 mwaka 2012.

Mshindi wa Kampeni ya Malengo ya NBC wa Dar aondoka na kirikuu yake.

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kabla hajakabidhi zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ yenye thamani za zaidia ya shs miliono 30 kwa mshindi wa kampeni ya Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani (kulia). Alisema moja na malengo la kapeni hiyo ni kuhamasisha wateja na wasio wateja kujiwekea akiba katika benki hiyo ili kutimiza malengo. 
 Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni ya Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani akihojiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akikabidhi  kadi ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’  kwa Fatuma Saidi Ramadhani,  mmoja wa  washindi  sita wa kampeni ya  Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Anayeangalia ni Mkurugemnzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Filbert Mponzi. Kampeni hiyo ilidumu wa muda wa miezi mitatu.
Mshindi wa zawadi ya gari ya kampeni yas Malengo ya NBC, Fatuma Saidi Ramadhani (katikati), akionyesha kadi ya gari lake baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto).  Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Filbert Mponzi na baadhi ya familia ya mshindi huyo.  

DED Kishapu asisitiza uwajibikaji kwa walimu

$
0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga amesisitiza uwajibikaji kwa walimu ili kuleta ufanisi mkubwa katika sekta ya elimu.

Magoiga alitoa msisitizo huo wakati akikabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa shule ya sekondari Maganzo wilayani humo vilivyokamilika vyenye thamani ya sh. milioni 19.4.Vyumba hivyo ni sehemu ya mradi uliotekelezwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na fedha ambazo zilitolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Alisema kuwa endapo walimu hao watawajibika ipasavyo wanafunzi watafanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuleta sifa nzuri katika shule pamoja na wilaya nzima kwa ujumla.Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kwa kusema kuwa kampeni ya kufuta ziro yaani sifuri inayoendelea itaweza kupata mafanikio makubwa kama walimu watajituma katika kufundisha vizuri.

Aidha aliwataka wanafunzi kujituma na kutumia fursa ya kuwepo shuleni kwa ajili ya kusoma kwa bidii na kufaulu masomo yao hivyo kuweza kuwa watalaamu wa baadaye kwa manufaa ya jamii.

Itakumbukwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ilipata ufadhili wa fedha TEA jumla ya sh. milioni 70.5 kati y ash. milioni 141 kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa miundombinu katika shule hiyo.
Kwa kutumia fedha hizo pamoja na kushirikisha nguvu za wananchi inaendelea na ujenzi wa nyumba ya walimu sita, choo cha matundu 2 cha walimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Maganzo wakati alipozindua vyumba vya madarasa vilivyokamilika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifungua moja ya vyumba vya madarasa vilivyomalika ujenzi wake wakati akivikabidhi kwenye shule ya sekondari Maganzo.
 Walimu, wajumbe wa bodi ya shule na wanafunzi (hawapo pichani) wa shule ya sekondari  Maganzo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (aliyesimama) wakati alipozungumza alipowakabidhi vyumba vya madarasa.
 Sehemu ya jengo lenye chumba cha darasa la shule ya sekondari Maganzo lililokamilika ujenzi wake na kukabidhiwa.

SERIKALI YATENGA BILIONI TATU UJENZI WA BARABARA YA MUHEZA-AMANNI MKOAN TANGA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Tanga

SERIKALI imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 39 kutoka mjini Muheza hadi Amani wilayani humo, kwa kiwango cha lami. 

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbalo alisema fedha hizo zimetengwa kama utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka jana kwamba barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami. 

Ndumbalo alisema nia ya serikali ni kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na fedha zilizotengwa zinatokana na bajeti ya Mwaka huu."Tayari serikali imetenga fedha hizo na wiki iliyopita Naibu Waziri wa Ujenzi (Elias Kuandika) tulimpeleka Muheza na pia amewahakikishia wananchi kwamba barabara hiyo tayari imetengewa fedha hizo," alisema Ndumbalo. 

Meneja huyo alisema kuwa wanachosubiri kwa sasa ni kupewa maagizo na wizara kuhusu ama kutangaza zabuni ili ujenzi uanze au vinginevyo kwa kuwa tayari wamemaliza kazi ya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa barabara hiyo tangu mwaka jana. 

Ndumbalo alisema kwamba mkoa wa Tanga una kilomita zipatazo 327 za barabara kuu na kilomita 171 za barabara za vijijini zilizojengwa kwa kiwango cha lami, hivyo kujengwa kwa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa Kwa wananchi hasa wanaoishi tarafa ya Amani ambayo jiografia yake ni ya milima.

Barabara hiyo ambayo ilikuwa haipitiki kwa uraisi Mwaka 2011 Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi aliipatia fedha ambazo zilitumika kujenga zege Kwenye maeneo yenye kona kali na hatarishi, kiasi ilipunguza adha ya magari kukwama na sasa ikijengwa lami itasaidia wananchi wa tarafa hiyo ambao ni wakulima wa viungo vya chai na Chakula na wauzaji wakubwa wa vipepeo nje.

Meneja wa Wakala wa barabara mkoa wa Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbalo

UWT YACHARUKA, YAUNGA MKONO UAMUZI WA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) KUWACHUKULIA HATUA WALIOSHINDWA KUREJESHA MIKOPO

$
0
0


Mwenyekiti wa UWT Kabaka akizungumza leo
Na Bashir Nkoromo Dar es Salaam
 
Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) imetaka wateja sugu wanaodaiwa na Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kuhakikisha wanalipa marejesho ya mikopo yao mara moja vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Akizungumza katika Makao Makuu ya UWT  Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Gaudensia Kabaka amesema UWT inaunga mkono Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya wanawake  Tanzania (TWB) Beng'i Issa ya kutaka wadaiwa sugu wa benki hiyo walipe marejesho ya mikopo ndani ya siku saba.

" Sisi Umoja wa Wanawake Tanzania na wanawake wote wa Tanzania kwa ujumla wetu hatutakubali na hatuko tayari kabisa kuona watu wachache wakiwemo hata wanawake wenzetu wakitumia benki hii kwa kujinufaisha wao wenyewe". alisema.

Ameongeza kwamba UWT wanapenda kuona mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati ili wengine pia waendelee kukopa bila matatizo akisisitiza kuwa TWB ndiyo benki pekee inayoweza kunmkopesha mamam mjasiriamali mdogo na pia ni miongoni mwa benki tatu tu zilozopo duniani ambazo ni maalum kwa wajili ya wanawake tu benki hizo zipo Pakistan, India na Tanzania.

"UWT tunatoa rai kwa wakopaji wote na tunatoa tamko kwamba hao ambao wamekopeshwa na hawajarudisha mikopo kwa wakati wachukuliwe hatua za haraka na stahiki ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha wanalipa mikopo yao yote kwa manufaa na uhai wa benki yetu na kwa manufaa ya wanawake wote nchini.

Wadaiwa sugu ni 7065 ambao ni wengi sana hasa kutokana na fedha wanayoihodhi ambazo ni kiasi cha Sh. Bilioni 6.79. Tungependa kuona mikopo hii inarejeshwa kwa wakati" Alisema.

Alisema kuwepo kwa benki ya wanawake nchini ni maombi na kilio cha mda mrefu cha wanawake nchini tangu uhuru kupitia Jumuiya ya CCM kuzaliwa. ni kilio cha Kina bibi Titi Mohammed na mama Sophia Kawawa wakati wa uhao wao wakiwa wenyeviti wa UWT kwa nyakati  tofauti na kilio cha wenyeviti wengine waliofuata hadi sasa.

"Napenda kuwaambia kuwa jambo hili  Kama Mwenyekiti wa UWT nalifuatilia kwa karibu sana kwa kuwa ni miongoni mwa maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wetu, Rais Dk John Magufuli wakati wa Mkutano wetu Mkuu uliofanyika Desemba 8, 2017 mjini Dodoma", alisema

Alisema Uongozi mpya wa UWT umekaa na benki ya wanawake kuangalia namna gani benki itaweza kufikia wananwake wengi na kwa riba nafuu zaidi.
HABARI KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akifafanua zaidi kwa nini UWT ipo bega kwa bega na beki ya Wanawake Tanzania, wakat akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Makao Makuu ya UWT mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Amina Makilagi na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Bara Eva Kihwelo Mwingizi
Baadhi ya maofisa wa UWT wakiwa kwenye kikao hicho
Waandishi wa habari wakimsikiliza Gaudensia Kabaka
Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi akifunga Mkutano huo na Waandishi wa Habari baada ya Mwenyekiti wake Gaudensia Kabaka (katikati) kumaliza kutoa taarifa nzito ya UWT. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara Eva Kihwelo Mwingizi.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

Kauli Mbiu: Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini. 

Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini. 

· Serikali inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi. 

· Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni. 

· Kuboreshwa kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo. 

· Usambazaji umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato. 

· Uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato . 

· Serikali kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo. 

· Kurasimisha vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo. 

WAZIRI UMMY AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI ILEJE AFUNGUA KITUO CHA AFYA NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

$
0
0

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akitoa udongo wakati wa  uchimbaji wa msingi katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mtura kilicho katika kata ya Lubanda Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akielekea eneo la gari lililokwama kutokana na changamoto ya Barabara, wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Kheri Kagya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje na watumishi wa Serikali (hawapo kwenye picha) wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Wananchi wa kata ya Lubanda katika kijiji cha Mtura wilaya ya Ileje wakimsalimia Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu


WAZIRI UMMY ASHIRIKI UJENZI NA KUFUNGUA KITUO CHA AFYA WILAYA YA ILEJE

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akielekea eneo la gari lililokwama kutokana na changamoto ya Barabara, wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Kheri Kagya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje na watumishi wa Serikali (hawapo kwenye picha) wakati akiwa katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Wananchi wa kata ya Lubanda katika kijiji cha Mtura wilaya ya Ileje wakimsalimia Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akitoa udongo wakati wa  uchimbaji wa msingi katika ziara yake ya ufunguzi wa kituo cha Afya cha Mtura kata ya Lubanda wilaya ya Ileje.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mtura kilicho katika kata ya Lubanda Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe

UVCCM KIGOMA WAMLILIA KABOROU

$
0
0
Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoani Kigoma umepokea kwa masikitiko na huzuni taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa Kigoma Dk Walid Amani Kaborou aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Katika salamu za rambirambi toka Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Kigoma Sylivia Sigula kwenda kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa kigoma Ammandus Nzamba , UVCCM wameelezea kusikitishwa kwao na kifo cha kiongozi huyo mkoani humo.

Sylivia amemuomba Mwenyekiti wa ccm mkoa kigoma awafikishie salamu zao za zarambirambi na mkono wa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu na jamaa na kuwataka wawe na moyo wa subira na ustahamilivi kwa wakati huu

Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemtaja marehemu Dk kabourou katika maisha yake amekuwa kiongozi aliyetawaliwa na busara, hekima, maarifa mapana na mwenye upeo mkubwa katika medani za siasa na historia ambapo mara zote amekuwa zaidi ya mwalimu kwa vijana.

"Chama chetu kimepoteza kiongozi wake bora, msikivu na mjuzi katika masuala ya siasa na maendeleo ya demokrasia .Tunamuomba mungu mtukufu ampokee, amsaheme dhambi zake na amuweka mahali pema peponi"Alieleza Sylivia kwenye tanzia yake kwenda kwa Mwenyeliti wa CCM Mkoa Kigoma .

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amesema jumuia yake mkoani humo itaendelea kujifunza mambo yote mema na mazuri yaliokuwa yakifanywa na Dk Kabourou wakati wa uhai wake na jinsi alivyokuwa mahiri katika kujenga hoja na kujibu mapigo ya kisiasa .

Sylivia ameeleza mwili wa marehemu Dr. Walid Kabourou utasafirishwa kutoka dar es salaam kuelekea kigoma kesho saa nne asubuhi. Mazishi yamategemewa kufanyika Tarehe 9 Machi 2018, siku ya Ijumaa, katika msafa wa makaburi ya Kipampa shule ya ujiji. Mwenyekiti anawaomba wanakigoma na wanaccm kwa ujumla tushiriki kwa pamoja katika kumpumzisha mzee wetu katika nyumba yake ya milele. Msiba utakua nyumbani kwa marehemu huko Bagwe, Kigoma Mjini.

Inna lilahi wa Inna Ileiyhi Rajiun .
Imetolewa na,
Mwenyekit wa vijana mkoa wa kigoma.

MBUNGE AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI MBEGU ZA VIAZI LISHE

$
0
0

Na Allan Ntana, Urambo

MBUNGE wa jimbo la Urambo Mkoani Tabora Magreth Sitta amezindua mradi wa ugawaji na usambazaji mbegu za zao la viazi lishe linalosimamiwa na Mradi wa ‘Sambaza Marando Fasta’ wilayani humo.

Akikabidhi mbegu hizo jana Sitta alisema mradi huo unaoratibiwa na Shirika la ANSAF la jijini Dar es salaam ni muhimu sana kwa sababu ya urahisi wake na manufaa makubwa watakayopata wananchi kwa kuzalisha zao la viazi lishe.

Alisema semina iliyotolewa na Shirika hilo bungeni mjini Dodoma ilimhamasisha kuleta mradi huo kwa wananchi wake jimboni na mwezi Desemba mwaka jana alianzisha shamba la zao hilo lenye ukubwa wa ekari 2 ili kuzalisha mbegu hizo.

‘Nawashukuru sana ANSAF na Kituo cha Utafiti wa Mazao Ukiriguru kwa kufanikisha mradi huu hapa Urambo, sasa mbegu zipo tayari na leo tunazigawa bure kwa vikundi vya wakulima wa kata zote 18 jimboni kwangu’, alisema.

Alisema atahakikisha mbegu hizo zinazalishwa kwa wingi na kusambazwa katika vijiji vyote jimboni kwake na wilayani nyingine za mkoa huo ili zao la viazi lizalishwa kwa wingi sana katika mkoa huo ili kumwinua kiuchumi mwananchi.

Afisa Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru cha jijini Mwanza Rahila Amour aliwataka wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani kuchangamkia mradi huo kwa kuwa una faida nyingi na mbegu zinapatikana kwa urahisi mno, alibainisha mbegu zilizopo kuwa ni Kabode, Kakamega na Mataya.

Alisema Mradi huo unafadhiriwa na Shirika la Bill and Melinda Gates Foundation la nchini Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya ANSAF ya jijini DSM, Wizara ya Kilimo na Chakula na Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Ukiriguru-Mwanza.

Mtafiti Mwenza kutoka Kituo cha Ukiriguru Eric Chang’a alisema zao la viazi ni muhimu sana kwa sababu ni lishe nzuri (chakula), linaongeza mapato na ni kinga dhidi ya upofu, hivyo akawataka wananchi wengi zaidi kuchukua mbegu hizo.

Alisema mbegu hiyo imefanyiwa utafiti wa kina na Wataalamu wa Ukiriguru na kujiridhisha kuwa ni mbegu bora inayopaswa kulimwa na wakulima wote hapa nchini kwa kuwa inachukua muda mfupi sana takribani miezi 3-4kutoa viazi.

Baadhi ya Madiwani waliokuwepo katika tukio hilo Elizabet Mkwenda na Blandina Magupa walimpongeza mbunge wao kwa kuleta mradi huo na kuamua kuzalisha mbegu na kuzigawa bure kwa wananchi wake.

Shughuli ya uzinduzi wa Mradi huo ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Kanda wa Kituo cha Utafiti Ukirigiru Dr Everine Lukonge, Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora, Wataalamu Watafiti kutoka Ukiriguru, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa na mwenzake wa wilaya na viongozi wa UWT wilaya.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vikundi wa Wakulima kutoka kata 18 za wilaya hiyo baada ya kuwakabidhi mbegu za viazi ili wakazismabaze. Picha na Allan K

WAZIRI UMMY MWALIMU ARIDHISHWA NA UTENGAJI KAZI WA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA ILEJE

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi pamoja na mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkudew wakielekea eneo ambalo kituo cha afya kinajengwa kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi na kupokea maelezo ya ujenzi huo na namna pesa za serikali katika sekta ya afya zinavyotumika. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwa kwenye eneo ambalo kituo hicho kinajengwa.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitenda wakati wa ziara ya waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje



Na Fredy Mgunda,Ileje 

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Akiwa katika zira hiyo,Waziri Mwalimu alifanikiwa kukagua kituo cha afya cha Lubanda ambacho kilipewa kiasi cha shilingi milioni mia tano(500) kutoka serikalini kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

“Mimi nimekuja kuangalia utekelezaji wa pesa ambazo serikali tunazileta huku kwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya,maana kumekuwa na watendaji ambao wamekuwa wakizitumia vibaya pesa ambazo tumekuwa tukizileta huku” alisema Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alisema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa kituo cha afya cha Lubada unaoendelea kwa kasi nzuri na kwa viwango ambavyo serikali inavitaka na kuahidi kuwa ukimalika ujenzi huo utawaletea gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania.

“Kwa hapa mlipofikia nawapongeza sana kwa kuwa kazi nimeiona kwa macho yangu mwenyewe hivyo mkimaliza ujenzi nitakikisha kila kitu kinachotakiwa hapa kitakuwepo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa wilaya ya Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Hata Waziri Mwalimu aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Ileje kwa kufikisha asilimia tisini na moja (91) ya wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambao unarahisisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wanaotumia mfuko huo.

“Niwapongeze tena kwa kazi kubwa mliyofika ya wananchi wengi kukubali kujiunga kwenye mfuko huo,maana kuna halmashauri nyingine zijafgika hata robo yenu hiyo naona utendaji wenu uliotukuka katika kuwatumikia wananchi wa Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alizitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa halmashauri ya ileje kwa namna wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa baina ya mkurungezi mtendaji na mkuu wa wilaya hiyo ndio maana kuna matokeo chanya.

“Nichuke nafasi hii kukupongeza sana mkurugezi wangu Haji Mnasi na mkuu wa wilaya Joseph Mkude kwa ushirikiano mnaoushesha katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Ileje,napenda kama halmashauri zote hapa nchini zingekuwa kama halmashauri yetu tungekuwa tumefika mbali kimaendeleo” alisema Waziri Mwalimu

Awali akisoma hotuba kwa waziri, mkurugenzi wa halmashuri hiyo Haji Mnasi alisema kuwa halmashauri imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa afya ya jamii kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye mfuko huo.

“Tunasheria ya mwaka 2004 ambayo inawataka wananchi wote wajiunge kwenye mfuko huo hivyo tutaitumia vizuri sheria hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajiunga kwenye mfuko huo akiwa tayari amepatiwa elimu ya kutosha na kumfanya ajiunge mwenyewe bila kulazimishwa” alisema Mnasi

Mnasi alisema kuwa huduma za matibabu kwa wazee zinatolewa katika vituo vyote 33 vya huduma za afya na jumla ya wazee 11463 waliotambuliwa na walipewa vitambulisho ni 8954 sawa na asilimia 78 ambapo jumla ya shilingi 7,196,000 zilitumika mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wazee.

“Lakini ukiangalia mwaka 2017/2018 tumetenga kiasi cha shilingi 28,000,000/= ambapo kwa kila zahanati tunapeleka kiasi cha shilingi 1,000,000 na kwenye vituo vya afya tunapeleka 2,000,000 kwa ajili ya huduma ya wazee na kazi ya kuendelea kuwatambua ni endelevu” alisema Mnasi

Mnasi alimuahidi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuwa pesa zote zinazoletwa kutoka kwenye wizara yake zitatumika kama zilivyopangwa na kuhakikisha zinasimamiwa vizuri kama ambavyo wamekuwa wakisimamia pesa zote za serikali zitumike kwa malengo yanayokusudiwa.

BOHARI YA DAWA (MSD) YAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE YATAMBULIKA KIMATAIFA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana walipotembelea Bohari ya Dawa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula, akitoa maelezo kwa wanahabari jinsi vifaa tiba na dawa zinavyohifadhiwa katika bohari hiyo.
 Muonekano wa maboksi ya dawa jinsi yalivyopangwa ndani ya bohari iliyopo Makao Makuu ya MSD Keko jijini Dar es Salaam.
 Dawa na vifaa tiba zikipelekwa kuhifadhiwa ndani ya bohari.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akiwaonesha waandishi wa habari vifaa  mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi, Byekwaso Tabula na Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia.
  Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Salome Malamia, akiwaonesha wabahabari vifaa vilivyopo kwenye mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Hilda Mhagama kutoka  gazeti la Daily News.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi mfuko wenye vifaa hivyo mwandishi wa habari, Saum Juma kutoka Kituo cha Televisheni cha TV One.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imezidi kuboresha huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hata kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa na kupata ithibati ya ISO 9001:2015.         

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED ilifanya ukaguzi Makao makuu ya MSD pamoja na Kanda zake nane mwezi Agosti 2017 na MSD ilionekana kufuata miongozo ya juu ya kimataifa na matakwa ya mamlaka za udhibiti ubora nchini.             

Katika mkutano huo, Bwanakunu pia alieleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu(135)  MSD imeimarika  na kufikia asilimia 90,huku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini hali ya upatikanaji wa dawa ni kati ya asilimia 85 na 98.              

Mkurugenzi Mkuu wa MSD pia aliwaonyesha waandishi wa habari  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000.

Amesihi taasisi, asasi, jumuiya na wananchi kununua mifuko hiyo ya vifaa vya kujifungulia na kutoa msaada kwenye vituo vya afya na hospitali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya nchini .      
                              
Katika mkutano huo Bwanakunu aliwazawadia waandishi wa habari wawili ambao ni wajawazito mfuko huo wa vifaa vya kujifungulia  kwa ajili ya kujiandaa kwenda kujifungua.

SERIKALI YAFUNGA KIWANDA KWA SIKU 14 NA KUVITOZA FAINI YA JUMLA YA SH. MILIONI 40.8 VINGINE VITATU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited leo Machi 7, 2018, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


SERIKALI imesitisha shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba), cha TASIPA kilichoko jijini Dar es Salaam kwa siku 14 kuanzia leo Machi 7, 2018 baada ya kubainika kuwa kiwanda hicho kinahatarisha maisha ya wafanyakazi wake.


Sambamba na hilo, kiwanda hicho pia kimetozwa faini ya shilingi milioni 18 kwa kukiuka sheria ya usalama na afya mahala pa kazi.


Aidha Mhe. Mavunde pia amevitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 22.8 viwanda vya Hengji Investment, ambacho pia kinatengeenza viroba (mifuko ya nailoni), na kiwanda kingine cha kutengeneneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited kwa makosa mbalimbali ya kukiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.


“Katika kukagua Sheria za usalama na afya mahala pa kazi, tumebaini kuwa mazingira ya kiwanda hiki cha TASIPA ni hatarishi mno kwa mfanyakazi kufanya kazi na tayari watu wa OSHA walikwishafika hapa na kutoa maelekezo, lakini hakuna kilichofanyika.” Alisema Mhe. Mavunde.


Naibu Waziri pia aliagiza kuwa muajiri huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wote kwa mujibu wa sheria namba 6 ya mwaka 2004 na mikataba iwe imekamilika n dani ya siku 14 na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ili aipitie.


Awali Mheshimiwa Mavunde alitembelea kiwanda  cha kutrengeenza nywele na kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mikataba ya kazi, kufanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa malipo ya muda wa ziada na kufanya kazi kwenye mazingira ambayo yanahatarisha afya za wafanyakazi.


Kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 8 na kutakiwa kurekebisha kasoro zote zilkizojitokeza ndani ya kipindi kifupi.


Naibu Waziri pia alikitoza faini kiwanda cha Hengji Investment Limited kinachojishughulisha na utengenezaji mifuko ya viroba kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kazi na usalama mahala pa kazi.


Ziara ya Naibu Waziri ambayo imeianza wiki iliyopita jijini Mwanza, inalenga kufuatilia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziriu Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama aliyoyatoa Mwishoni mwa mwaka jana, kuwataka waajiri wote ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), watekeleze wajibu huo wa kisheria vinginevyo wafikishwe mahakamani.


Tayari waajiri kadhaa wameanza kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo na operesheni hiyo kwa mujibu wa Naibu Waziri ni endelevu na itafanyika nchi nzima.


 Kwa mujibu wa sharia ya usalama mahala pa kazi mfanyakazi huyu alipaswa kuvaa mask na gloves. hapa ni kiwanda cha TASUPA kinachotengeneza mifuko ya nailoni (viroba)
 Naibu Waziri Mvunde akishuhudia ukiukwaji wa sharia ya usalama mahala pa kazi kiwanda cha TASUPA
 Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
 Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH Afrique Tanzania Limited, wakimsikiliza Naibu Waziri Mabunde(hayupo pichani) alipozunhgumza nao.
 Naibu Waziri Mvunde, alipotembelea kiwanda cha SH Afrique
 Kamishna wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa, (kushoto) akizunhguzma jambo.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bi. Rehema Kabongo.
 Msaidizi wa Meneja Mwajiri kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited, Bi.Domina Domisium, (kulia), akitoa maelezo ya uendeshaji wa kiwanda hicho, mbele ya Naibu Waziri Mhe. Mavunde
 Bi. Kabisa akimuhoji Bi.Domina
 Naibu Waziri Mvunde, akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji kiwanda cha SH. Afrique Tanzania Limited, Bi.Kim Minju, (kulia). Katikati ni Bi. Rehema Kabongo.
 Mhe. Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa SH. Afrique Tanzania Limited.
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba) cha TASUPA.
 Naibu Waziri akitoa maagizo kiwanda cha TASUPA.
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha TASUPA, kwa niaba ya wenzake akizungumza mbele ya Naibu Waziri, ambapo alieleza ukiukwaji mkubwa wa haki za wafanyakazi kiwandani hapo.

NIDA KUZINDUA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KIGOMA, RUKWA NA KATAVI

$
0
0
Kaimu Ofisa Uhusiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Rose Joseph akielezea mikakati ya kuzindua usajili wa vitambulisho Kigoma, Rukwa na Katavi sambamba na ndani ya mgodi wa Tanzanite.

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  inatarajia kuzindua usajili na utoaji wa  vitambulisho hivyo katika mikoa mitatu ya Katavi, Kigoma na Rukwa.
Pia  NIDA  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini , imeanza  kuwasajili watu wote watakaoishi, kufanya kazi au biashara ndani ya eneo lililozungushiwa ukuta lenye madini ya TANZANITE huko Mererani mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo, Kaimu Ofisa Uhusiano  wa NIDA,  Rose Joseph, alisema   mpaka sasa mamlaka hiyo imaendelea  na  usajili na utoaji vitambulisho vya  uraia  katika mikoa 20.

“Hivi karibuni tutafanya uzinduzi katika mikoa mitatu iliyobaki ambayo ni Kigoma,  Rukwa na Katavi . Wananchi katika mikoa hii watakuwa na muda wa miezi mitatu wa kujisajili,  na hivyo  tutakuwa  tumeifikia nchi nzima,”alisema Rose.

Ofisa huyo alisema  pia NIDA taangu Novemba   mwaka uliopita  ilianza  usajili wa mkupuo katika mikoa mbalimbali   na muda ulikuwa ukiongezwa  kadri ilivyokuwa uinaruhusu.

“Tayari baadhi ya mikoa imemaliza kazi ya kusajili  kwa mkupuo ikiwemo mikoa ya Mara na Iringa,”.alieleza  Rose
Alisema  katika kazi hiyo ya usajili NIDA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji  wanapeleka  maofisa hadi  ngazi ya kata na vijiji,  ili  kuhakikisha  kazi hiyo inakwenda kwa mchujo sahihi na wale wote wanaosajiliwa wawe na sifa  na vigezo kuwa raia  wa Tanzania.

 “Tunasajili  vitambulisho vya aina tatu ambavyo ni vya uraia, mkimbizi na mgeni na kumekuwa na ufanisi mkubwa,”alifafanua ofisa  uhusiano huyo.

Alisema, pia NIDA kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini, imeanza usajili na kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara, wakazi na watu wote watakao kuwa wakiendesha shughuli zao ndani ya ukuta wa madini ya TANZANITE huko Mererani.

“Kila mtu atasajiliwa na kupewa kitambulisho  cha taifa. Hakuta kuwa na ruhusa ya mtu kuingia na kufanya  shughuli yoyote  ndani ya ukuta huo  bila kuwa na kitambulisho hiki,”alibainisha Rose.

Alisema lengo ni  kuona kuna kuwa na utaratibu maalumu wa kulitumia eneo hilo pamoja na kuwatambua wachimbaji wote wadogo na wakubwa na wafanyabishara wa madini katika eneo hilo.

“Lengo ni kutambua watu wanaonufaika na shughuli zozote katika eneo hilo la madini. Tunataka kuona vijana wa Tanzania ndiyo wanufaika wakubwa , hivyo kutoa vitambulisho kutadhibiti wageni kuvamia eneo hilo,”alisema Rose.

Pamoja na hayo, Rose libainisha kuwa NIDA,  kwa kushirikiana na  wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) kwa sasa wanaendelea na usajili na kuwapa vitambulisho vya uraia  watu wote waliofungua makampuni kupitia wakala huo.

“Utaratibu uliopo hivi sasa ni kwamba mtu yoyote ambaye hana kitambulisho taifa hawezi kupata usajili wa kampuni BRELA. Ni marufuku na wale ambao tayari walifungua wanatakiwa kufika BRELA kuchukua vitambulisho hivyo katika madawati yetu,”alifafanua ofisa huyo.

Aliongeza; “Changamoto  kubwa tuliyonayo watanzania  tunapenda njia za mkato, lakini katika kazi hii  ni lazima tuwe wakweli , kwani kuwa na kitambulisho cha taifa  kunakupa hadhi ya utanzania,”

Alisema  watu wengi wanataka  kusajili kampuni kwa haraka hivyo kupita nijia za mkato  kisha kukwama katika hatua za mwisho.

“Zoezi lingine  ambalo NIDA tunalitekeleza ni la kuwasiliji wananchi wanaotaka  Paspoti  na hati za kusafiria za kielektroniki.Kwa sasa hupati hati hizo bila kuwa na kitambulisho cha taifa,”alisema Rose.

Alisema kuna huduma za haraka zinazowawezesha wananchi wasio na vitambulisho hivyo wanaohitaji hati za kusafiria.

“Pia  tunaendelea  na usajili wa wanachama wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii Tanzania ambapo kwa kushirikiana na  Mamlaka  Udhibitiwa Mifuko  hiyo (SSRA), kusajili wanachama wote wa mifuko hiyo ambao hawana  vitambulisho,’ alisema.

MIRADI YA AJIRA YA MUDA INAYOTEKELEZWA NA TASAF KATIKA WILAYA YA BUKOMBE MKOANI GEITA YAWANUFAISHA WANANCH KICHUMI.

$
0
0
NA ESTOM SANGA-GEITA.

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wameipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu wa miradi ya Ajira ya Muda huo ambao wamesema licha ya kuinua kipato chao lakini pia unawaongezea hamasa ya kushiriki katika kazi za maendeleo kwenye maeneo yao.

Chini ya Utaratibu huo wa Ajira ya Muda,Walengwa wanaotoka katika Kaya Maskini huibua miradi,kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya Serikali kupitia TASAF kuongeza kipato na ujuzi cha Kaya za Walengwa.

Kupitia utaratibu huu wa ajira ya muda,walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya ya Bukombe wametekeleza miradi kadhaa ikiwemo kilimo bora cha pamba, uchimbaji wa malambo ya maji na upandaji wa miti.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Malighasi katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe ,Samweli Nyelu amewaambia Waandishi wa habari wanaotembelea mkoa wa Geita kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusu Kaya Maskini kuwa wananchi wananufaika na huduma ya malambo ya maji yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda na kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la uhaba wa maji kwao na mifugo yao lililokuwa linawakabili kabla ya kuanza kwa Mpango hu.

Aidha Walengwa wa TASAF kupitia utekelezaji wa Ajira ya Muda wamejikita katika kilimo cha pamba ambapo hupewa pembejeo, na utalaam na kisha kulipwa ujira kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato hususani katika kipindi cha hari.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe,Eliasi Kayandamila, amesema kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda, walengwa wa TASAF wilayani humo wamelima hekta 140 za zao la pamba na kupanda mbegu bora kulingana na maelekezo ya wataalam wa kilimo.

Amesema jitihada za halmashauri yake ni kuhakikisha kuwa walengwa na wananchi wengine wanafikiwa na wataalamu wa ugani mara kwa mara na kuwafikishia huduma ya madawa na mbolea kwa wakati kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa pamba katika msimu ujao wa mavuno.

Zifuatazo ni picha walengwa na baadhi ya kazi wanazozifanya wilayani Bukombe kupitia miradi ya Ajira ya Muda.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Malighasi katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe wakiwa katika shamba la Pamba walilolilima kwa utaratibu wa Ajira ya Muda kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakitoa maelezo kwa Waandishi wa habari namna walivyoshiriki kazi ya ajira ya muda kwa kulima hekari tatu za pamba.
Mojawapo ya malambo yaliyochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Waandishi wa habari wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Malighasi halmashauri ya wilaya ya Bukombe ,Samweli Nyeli kazi ya uchimbaji wa lambo ilivyofanywa na Walengwa wa TASAF na jinsi inavyowanufaisha wananchi wote kijijini hapo.
Ng’ombe wakinywa maji kwenye lambo lililochimbwa na Walengwa wa TASAF kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda katika moja ya vijiji vya halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

GGM NA SERIKALI GEITA YATILIANA SAINI MAKUBALIANO FEDHA HUDUMA ZA JAMII.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakikabiana hati ya makubaliano ya miradi ya jamii na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso baada ya zoezi la Saini ya Makubaliano. 
Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri mbili ya mji na wilaya ya Geita wakisaini makubaliano.(katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi aweka saini kwenye hati ya makubaliano ya miradi kwenye halmashauri mbili ya mji na wilaya. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. 
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga.



NA JOEL MADUKA-GEITA.

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGM) pamoja na Halmashauri mbili za Wilaya na Mji wa Geita zimetia saini ya Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja kuhusu Matumizi ya fedha za Huduma za Jamii zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa mwaka 2018.

Saini ya Makubaliano hayo inafuatia kutokana na marekebisho ya Sheria Mpya ya Madini iliyopitishwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kufanya mageuzi kwenye utekelezaji wa Fedha za Miradi ya Huduma za Jamii baina ya Kampuni za Uchimbaji Madini na Jamii kwenye eneo husika. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema Serikali mkoani humo imekusudia kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na mapato yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.

Aliongeza kuwa fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni Bilioni tisa pointi mbili (B 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, ikiwemo kiwanda cha sukari ,afya elimu na mazingira.

“Kifungu cha 105 (01) cha Sheria Mpya ya Madini kinazielekeza Kampuni zote za Uchimbaji Madini kuandaa Mpango wa matumizi ya Fedha za Huduma ya Jamii kwa kushirikiana na Halmashauri husika kabla ya kuanzisha Miradi yoyote ya Maendeleo,na hiyo ndiyo sababu leo hii makubaliano hayo ya nafanywa,” alisema Luhumbi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso alisema kuwa wanajivunia mafanikio hayo na kwamba wanaamini kufanya kazi na jamii inayowazunguka ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo kwenye jamii inayouzunguka mgodi huo.

Makubaliano ambayo yamefikiwa yatafanikisha kutekeleza miradi mipya ya maendeleo kwa mwaka 2018 katika sekta ya afya ,miundo mbinu,mjai,elimu,sanaa na utamaduni pamoja na kuwajenhea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati.

SHUWASA YATOA ELIMU YA MAJI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imeendesha semina kwa wanawake wa manispaa ya Shinyanga kuwapa elimu kuhusu utoaji huduma ya maji safi na usafi wa mazingira.

Mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika leo Jumatano Machi 7,2018 katika ukumbi wa Shinyanga Vijana Centre Mjini Shinyanga alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.

Akifungua semina hiyo,Matiro aliushukuru uongozi wa SHUWASA kwa kuthamini umuhimu wa akina mama katika jamii akieleza kuwa akina mama ni muhimili mkubwa katika malezi ya familia na jamii lakini pia ndiyo walengwa wakubwa wa huduma ya maji katika maisha ya kila siku.

"Kwa kuzingatia kauli mbiu ya kitaifa ya mwaka huu inayosema 'Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuimarishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vijijini',ni dhahiri kuwa taifa limetambua nafasi ya mwanamke katika jamii,SHUWASA nawashukuru kwa kuwapa kipaumbele akinamama katika uendelezaji na usimamizi wa mipango na mikakati ya huduma ya maji safi",alisema.

"Akina mama ni nguzo muhimu sana katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za maji kwani huduma ikiwa dhaifu,waathirika wakubwa wa hali hiyo ni akina mama na watoto hivyo ni vyema wadau wote tukashirikiana kutatua changamoto zinazojitokeza",aliongeza Matiro.

Naye Mkurugenzi wa SHUWASA, Injinia Sylivester Mahole alisema SHUWASA inatambua umuhimu wa akina mama katika huduma zake za kusambaza maji safi katika manispaa ya Shinyanga na inaunga mkono kauli mbiu ya kisekta ya “Kumtua Mwanamke ndoo kichwani”.

“Katika kuadhimisha siku wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 Machi,SHUWASA imeona umuhimu wa kukutana na wadau wetu wakubwa,sote tunafahamu kuwa akina mama ndiyo watumiaji wakubwa wa maji katika jamii”,alisema Injinia Mahole.

"Tumewaiteni hapa ili kuwapa elimu kuhusu huduma zetu kwa lengo la kuimarisha uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya SHUWASA kwa kutambua umuhimu wa akina mama katika kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Shinyanga ",aliongeza Mahole.

Wakizungumza katika semina hiyo, akina mama waliipongeza SHUWASA kwa kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa njia ya simu pindi ankara za maji zinapotoka lakini pia kuwakumbusha wateja kulipa ankara zao wanapojisahau. 

"Hivi sasa hatusumbuki wala kupoteza muda kwenda kulipia bill 'ankara' dirishani,sasa tunalipa kwa njia ya simu au benki,tunaomba SHUWASA ifikishe huduma kwenye maeneo ambayo hajafikiwa ili kuwatua ndoo kichwani wanawake ambao hawajafikiwa na huduma ya maji",alisema Happiness Mwaja na Elizabeth Ndagwa.

Kwa upande wake Marietha Mwakisu aliishauri SHUWASA kuweka utaratibu wa kufuatilia mitandao ya maji kwenye barabara kwani mabomba yamekuwa yakipasuka na kusababisha upotevu maji.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua semina ya wanawake wa Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA kama moja ya matukio ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Akina mama wa Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA), Injinia Sylivester Mahole akiwasisitiza akina mama kuendelea kushirikiana na SHUWASA katika kutatua changamoto zinazojitokeza katika utoaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Joyce Egina akizungumza wakati wa semina hiyo.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa ukumbini: Wa kwanza kushoto ni Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard ,katikati ni Afisa TEHAMA SHUWASA,Amosi Stephen akifuatiwa na Meneja Utawala na Rasilimali Watu SHUWASA, Flaviana Kifizi.
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akitoa mada kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja. Aliwataka wateja kutoruhusu vitendo vya rushwa katika huduma za maji na kuwataka wateja kutunza mita za maji na kuhakikisha wanalipa ankara za maji kwa wakati.
Afisa TEHAMA wa SHUWASA, Amosi Stephen akielezea jinsi walivyoboresha huduma za ulipaji wa ankara za maji ambapo hivi wateja sasa wanafurahia huduma na kutumia simu na benki kulipa ankara za maji.
Mwenyekiti wa semina hiyo, Ziphora Pangani (Mkuu wa wilaya mstaafu) akiongoza kipindi cha majadiliano wakati wa semina.
Mwinjilisti Esther Emmanuel akichangia hoja ukumbini.
Bora Yusuph akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo,Diana Ezekiel
Joyce Masunga (mbunge mstaafu) akichangia hoja wakati wa semina hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na akina mama wakicheza muziki/wimbo wa Wanawake na Maendeleo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SPORTPESA KUWAFUTA MACHOZI WASHINDI WA TIKETI

$
0
0
Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa imekabidhi kiasi cha TZS 12,000,000/= kwa washindi 12 wa promosheni za Zali la Mwanaspoti na Shinda na SportPesa. Washindi hawa 12 walijishindia tiketi za kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Ligi Kuu nchini humo kupitia promosheni za Zali la Mwanaspoti na Shinda na SportPesa lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kusafiri hivyo kila mmoja wao kukabidhiwa TZS 1,000,000/= kama fidia ya safari hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti, SportPesa Tanzania Ndugu Tarimba Abbas alisema “Kampuni yetu ina ushirika na klabu mbalimbali ambapo endapo mshindi atapata nafasi ya kwenda kushuhudia mechi atapata nafasi ya kutembelea makao makuu ya klabu hizo ikiwemo Arsenal na Everton.
Kutokana na vigezo na masharti vya promosheni hizi mbili, hatutawaacha washindi wetu mikono mitupu bali kila mmoja wao ataondoka na kiasi cha shilingi milioni moja ambazo watazitumia wapendavyo, na hii ni kwa mujibu wa masharti ya promotion hizo.” Nae Ndugu Musa Yohana Tupa kwa niaba ya washindi wengine alisema
Kwanza kabisa napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa, Mimi ni mshindi niliyepatikana kupitia promosheni ya Shinda na SportPesa. “Kutokana na shughuli zangu binafsi niliomba kutosafiri hivyo kuitaka kampuni inilipe fedha badala ya safari kama kanuni na masharti ya promosheni yanavyoelekeza.
Naye Meneja Masoko wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited Bi. Sarah Munema kupitia promosheni yao ya Zali la Mwanaspoti alisema “Napenda kushukuru SportPesa wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kujitolea na kuunga mkono promosheni yetu mpaka ilipofikia ukingoni na mpaka hatua hii amabapo tunaenda kuwakabidhi washindi hundi ya shilingi milioni 12.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA UNIDO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto)  akishuhudia madilishano ya makubaliano ya uendelezaji wa viwanda hapa nchini kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Bw. Li Yong pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage  leo.
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images