Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1528 | 1529 | (Page 1530) | 1531 | 1532 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
  Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
  Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
  Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
  Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
  Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo nchini.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

  “Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

  Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti.

  Aidhe, Serikali imepanga kuanza na wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini, huku ikitegemea kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika jitihada za kutokomeza kabisa tatizo hili la Saratani ya mlango wa kizazi nchini,

  Mhe Ummy alisisitiza kuwa Chanjo hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya nchini vya Serikali, vya watu binafsi na vikundi mkoba bure, na kuwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii ili kujikinga na ugonjwa huo.

  Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya duniani na mamlaka ya chakula na viodozi nchini (TFDA).

  0 0


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko, leo Jumanne Februari 27,2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi wa almasi wa El – Hilal Minerals Limited uliopo katika kijiji cha Maganzo kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

  Manaibu Waziri hao walikuwa wameambatana na maafisa kutoka WCF na Ofisi ya Kazi ,lengo la ziara hiyo ikiwa ni kubaini kama wamiliki wa mgodi huo wanatekeleza sheria za uendeshaji.

  Wakati Mheshimiwa Mavunde alikuwa akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund -WCF), Mhe. Biteko alikuwa akifuatilia kwa nini mgodi huo haujawasilisha wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).

  Akiwa katika mgodi huo Mhe. Mavunde alibaini kuwa Mgodi huo bado ulikuwa haujajisajili na Mfuko wa WCF na badala yake uongozi ulipeleka michango siku moja kabla ya ziara ya Naibu waziri huyo kufika katika mgodi huo.

  “Serikali inataka waajiri wazingatie sheria, na ninyi mmevunja sheria kwa kutojisajili, ingawa mmelipa michango yenu jana, ninachoweza kusema, agizo la serikali la kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawajajisajili nchi nzima liko pale pale, ni juu yenu kutekeleza hilo kabla hamjapelekwa mahakamani”, alisema Mhe. Mavunde.

  Mh. Mavunde pia alibaini kuwa mgodi huo hautoi mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi,wafanyakazi kufanyishwa kazi zaidi ya muda wa kazi bila malipo,wafanyakazi kutopewa vifaa kinga na mishahara kutolipwa kwa wakati na kuwaagiza kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye mgodi huo ndani ya siku 30.

  “Nawapa siku 14 za kujisajili WCF na kurekebisha mapungufu yaliyopo hapa ndani ya siku 30,ni lazima tutii na kuziheshimu sheria zetu wanaokiuka sheria tunawafikisha mahamani”,alisema Mhe. Mavunde.

  Ziara ya Naibu Waziri Mavunde ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 26, 2018 jijini Mwanza ambapo aliagiza kufikishwa mahakamani waajiri watatu jijini Mwanza ambao hawajajisajili katika mfuko wa WCF.

  Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.

  “Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja,Nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria­”,alisema.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde akizungumza katika mgodi wa almasi wa El - Hilal Minerals Ltd leo Februari 27,2018 akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi -WCF. Kulia ni Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko. Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi huo,Gofrey Leshange. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
  Kulia ni Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akielezea namna mgodi huo unavyokiuka sheria na kuwataka kuwasilisha wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).
  Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde akiangalia mikataba ya wafanyakazi katika mgodi huo ambapo alibaini kuwa mgodi huo hautoi mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi na kuwataka kurekebisha mapungufu hayo ndani ya siku 30.
  Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF ,Laura Kunenge na Kamishna wa Kazi Msaidizi nchini Rehema Moyo wakiangalia mikataba ya wafanyakazi katika mgodi huo na kubaini kuwa kuna ukiukwaji wa sheria.
  Wa pili kushoto ni Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi huo,Gofrey Leshange akijitetea kwanini hawatoi mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi wao na badala yake wanatoa mikataba ya miezi sita hadi mwaka mmoja.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde akiusisitiza uongozi wa mgodi huo kuzingatia sheria za nchi la sivyo watawafikisha makahamani.
  Mazungumza yakiendelea katika mgodi huo.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakielekea katika eneo la uzalishaji wa almasi katika mgodi wa El - Hilal uliopo Kishapu mkoani Shinyanga
  Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi huo,Gofrey Leshange akielezea namna uzalishaji wa almasi unavyofanyika katika mgodi huo

  Mfanyakazi wa mgodi huo "Plant Manager",Peter Mayeka akielezea jambo

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakitoka katika chumba cha kuhifadhi almasi katika mgodi wa El - Hilal

  Mwenyekiti wa wafanyakazi katika mgodi wa almasi wa El - Hilal Evarist Seleman akielezea changamoto zilizopo katika mgodi huo.
  Kushoto ni Mhasibu katika mgodi wa El- Hilal Amour Nassor akijitetea baada ya wafanyakazi wa mgodi huo kuwaeleza manaibu Waziri hao kuwa mgodi huwa haulipi Overtime na mishahara kucheleweshwa.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko wakisaini vitabu vya wageni katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kueleza lengo la ziara yao. Katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwamba

  Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akizungumza katika ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga walipowasili mkoani Shinyanga kuueleza uongozi wa mkoa lengo la ziara yao.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde akielezea zaidi kuhusu ziara yake na mwenzake mkoani Shinyanga.
  Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume akisoma taarifa ya mkoa kwa manaibu waziri hao.
  Afisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Shinyanga,Revocatus Mabula akizungumza.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde akimweleza mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro (kulia) lengo la ziara yao.
  Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko akizungumza katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga (Josephine Matiro - kulia).Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo Jengo la Extelecoms Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam kulia ni Bw.Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION)kin2
  Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akimzikiliza Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION) wakati alipokuwa akijibu moja ya swali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.
  kin3
  Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akijibu maswali katika mkutano huo pamoja na  Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION) na maafisa wengine wa shirika hilo.
  ……………………………………………………………………………..
  Waziri Waziri Kindamba  Mkurugenzi Mkuu wa (TTCL CORPORATION)  leo amezindua  huduma  mpya  ya kampuni hilyo iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle, Amesema huu ni mwendelezo wa ubunifu wa Kampuni yenu ya kizalendo katika kuwapatia huduma za kipekee kabisa.
  Kindamba amesema TTCL Corporation imechukua hatua ya kuwafuata nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano. Kupitia huduma hii mpya ya Fiber Connect Bundle, ambapo mteja  atapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu.
  Amesema kwa kuanzia, mradi unatarajiwa kufikisha huduma katika nyumba zipatazo 500 katika eneo la Mikocheni,   Nyumba 500 zingine katika eneo la Mbezi Beach na nyumba zaidi ya 200 katika eneo la Medeli Mkoani DODOMA.
  Ameongeza kwamba Kupitia kifurushi cha Fiber Connect, Mteja ataweza kufaidika na huduma zifuatazo; Kwanza, Mteja atapata Intaneti yenye kasi isiyo na kikomo( Unlimited). Pili, Mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na (Sim Card) ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intaneti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani.
  Akizungumzia  mwelekeo wa utendaji wa Shirika  amesema unaonesha ukuaji mzuri licha ya changamoto zilizopo. Mapato yameendelea kuongezeka na hasara kupungua kwa kiasi kikubwa, jambo linalotupa uhakika wa kutimiza ahadi yetu ya kutoa gawio Serikalini katika mwaka huu wa fedha 2017/2018.
  “Mtakumbuka kuwa, kwa zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita, TTCL haikuawahi kutoa gawio. Tumedhamiria kuvunja mwiko huu kwa kutimiza ahadi yetu kwa Umma ya kutoa gawio la shilingi Bilioni moja katika mwaka huu wa fedha” Aemesema Kindamba.
  Menejimenti itaendelea kuweka mkazo katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu, kuongeza Wateja wapya, kusambaza huduma za 4G LTE katika Makao Makuu ya Mikoa yote Nchini ifikapo Juni 2018.
  Aidha, tutaendelea kuongeza uwekezaji katika Teknolojia na Miundo mbinu yetu kote nchini, kuboresha mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi na Vitendea kazi, kukusanya Madeni ya Shirika, kuongeza Wateja na ufanisi katika huduma za fedha Mtandao (TTCL PESA) na kuongeza ufanisi katika Miundombinu ya Kimkakati ya Serikali inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania na hapa ninazungumzia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo Mahiri cha kuhifadhia Kumbukumbu(National Data Centre).
  Huduma ya tatu , Mteja atapata huduma za wireless service (WiFi) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia Teknolojia ya Intaneti vitaunganishwa na kuweza kutumia huduma hii. Mfano wa vifaa husika ni Smart Tv, Tablets, Laptops na kadhalika
  Nne, Mteja atapatiwa vifaa  vyote bure pamoja na uhakika wa huduma za baada (After Sells Services) endapo itahitajika
  Mchanganuo wa gharama na mgawanyiko wa kifurushi hiki ni kama ifuatavyo
  Jina la Kifurushi                   Muunganiko wa Huduma  
  Gharama
   
  Matumizi
  Kasi ya Intaneti (Mbps) Dakika za maongezi Mitandao yote
  Fiber Connect Lite 10 50 100,000.00  
  Siku 30
  Fiber Connect Basic 30 100 150,000.00
  Fiber Connect Preffered 50 300 200,000.00
  Ili kupata huduma ya kifurushi hiki maalumu cha FTTH, Mteja unapaswa kufanya yafuatayo; Piga namba 100/ 022214100100 kuongea na Wahudumu wetu au
  Tembelea kituo  chetu cha Huduma kwa Wateja kilicho karibu nawe.
  Huduma hii inazilenga:  Taasisi zote za Serikali, Wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na Ofisi mbalimbali.

  0 0
 • 02/27/18--22:49: TAA,JNIA WAMLILIA SWAI
 • Marehemu Jerome Swai
  Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (kulia), akimpa pole Bi. Honoratha Emmilian aliyefiwa na mume wake marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba (JNIA), alifariki tarehe 26 Februari, 2018 kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian, akitoa pole kwa Bi. Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa fundi bomba.
  Waombolezaji kwenye msiba wa marehemu Jerome Swai (kushoto), wakipokea pole kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian. Marehemu Swai alikuwa Fundi Bomba JNIA na alifariki tarehe 26 Februari 2018
  Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (mwenye tai) alipofika kuwafariji, ambapo marehemu alikuwa Fundi Bomba JNIA.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), wakiwa kwenye msiba wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba. Swai alifariki rarehe 26 Februari 2018 katika hospitali ya Amana.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Juluius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka aliyeinama (kushoto) akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa JNIA waliofika kwenye msiba wa aliyekuwa fundi Bomba, Bw. Jerome Swai.


  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wamesikitishwa na kifo cha Bw. Jerome Swai (58) aliyekuwa fundi bomba mahiri kilichotokea  tarehe 26 , 2018 kwenye hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda Mfupi.

  Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.

  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi. Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
  Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na hakukubali kushindwa.

  “Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift (zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi yake,” alisema Bw. Mwakosya.

  Bi. Fatma Matimba, Kaimu Meneja Utawala JNIA, alisema marehemu Swai alikuwa mchapakazi, ambapo mwaka jana alichaguliwa kuwa mfanyakazi hodari. Pia aliwahi kupewa cheti cha ufanyakazi hodari mwaka 2001 kinachotolewa TUGHE.

  Marehemu Swai alizaliwa mwaka 1960 wilaya ya Rombo, na kupata elimu katika shule ya msingi Kilesi mwaka 1976, na baadaye kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Makalema akisomea fani ya ufundi bomba daraja la tatu, na baadaye kujiendeleza katika Chuo cha Ufundi cha Chang’ombe mwaka 1988 na VETA mwaka 2007.

  Marehemu aliajiriwa na TAA mwaka 1984 akiwa kama fundi bomba daraja la tatu na baadaye alijiendeleza na kufanikiwa kusoma hadi kufikia daraja la kwanza. Marehemu ameacha mjane Bi. Honoratha Emmilian ambaye naye ni mfanyakazi wa TAA katika Idara ya Utawala akiwa kama mhudumu.

  Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahala pema peponi.


  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akielekea kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa TRA aliyeko katika kituo cha Huduma za  Pamoja Mipakani (OSBC) Paul Kamkulu  kuhusu huduma zinazotolewa katika kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mpaka wa Tanzania na Kenya.
   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi msaidizi Upimaji vijijini wa wizara Huruma Lugalla (wa pili kulia) wakati akikagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa ujumbe alioambatana nao wakati wa  kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na ujumbe wake wakitembea eneo la ardhi huru kuelekea ilipo alama ya mpaka baina ya Tanzania na Kenya Namanga mkoani Arusha.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula  akiwa amemshika Ngamia aliyemkuta eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wakati alipokuenda kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa wakiwasalimia wananchi, wakati wakiwasili katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya bakora, kutoka kwa mzee Mohammed Abeid Liyanga, anaye wawakilisha wazee wa Newala, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala Mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala Mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi mashine ya kubangulia korosho, Aziza Juma, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi mashine ya kubangulia korosho, Halima Maulid, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.

  0 0

  *Serikali yapiga marufuku mashirika kutoa takwimu ambazo hazina uthibitisho wa ofisi ya Takwimu

  Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

  WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 huku asilimia 50 wakiwa ni wa umri chini ya miaka 18.

  Pia Dk.Mpango amewakumbusha wadau wote was ndani na nje ya nchi kuwa takwimu za idadi ya watu kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza leo na si vinginevyo.
  .
  Hivyo amepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi ya Taiga ya Takwimu na atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za kisheria.

  Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazondua taarifa ya makisio ya idadi ya watu Tanzania amvapo amesema kwa makadirio yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

  Na kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu Tanzania sasa ni milioni 52.6 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni 52.6 na Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.Dk.Mpango amesema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.

  Amefafanua kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao milioni 1.6 hapa nchini.Dk.Mpango amesema ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani 400,000 kwa mwaka.

  "Utafiti wa mama na mtoto wa mwaka 2015/16 unaonesha kwamba mwanamke wa kitanzania atazaa watoto watano katika maisha yake yote ya uzazi .

  " Hata hivyo kiwango cha uzazi kilipungua kutoka wastani wa watoto 7 mwaka 1978 had I wastani wa watoto watano mwaka 2016.Baadhi ya sababu za juu cha uzazi ni kiwango kikubwa cha vifo vya watoto,familia kupendelea kuwa na watoto wengi,umasikini,mila,imani za kidini na matumizi madogo ya uzazi wa Mpango,"amesema.

  Ameongeza matokeo yake ni kuwa na idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.

  Amesema kwa mtazamo wake wingi au au uchache wa idadi ya watu sio tatizo bali tatizo ni pale ambapo kasi ya ongezeko la idadi hiyo inazidi kasi ya ukuaji wa uchumi na hivyo kulifanya Taifa kushindwa kumudu ipasavyo mahitaji ya wananchi.

  Dk.Mpango amesema kasi ya ongezeko la idadi ya watu pia inaleta changamoto ya idadi kubwa ya watoto na vijana ."Kwa mfano takwimu nilizozizindua leo zinaonesha asilimia 50 ya watu wote nchini ni watoto wenye umri chini ya miaka 18.

  "Asilimia hii kubwa ya watoto katika nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko ya kidemografia kutoka viwango vya juu vya vifo lakini wakati huo viwango vya uzazi vibaki juu," amesema.

  Ameongeza asilimia kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani kwa vile kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima yatimizwe na Serikali na jamii kwa ujumla wake.Dk.Mpango amesema mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na idadi kubwa ya watoto.

  Amesema kwa mfano kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi kiumri ni asilimia 92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 40 kwa nchi zinazoendelea.Hiyo ikiwa na maana kuwa kwa Tanzania kila watu 100 wenye umri wa miaka 15 hadi 64 wanategemewa na watu 92 wenye umri chini ya miaka 15 wenye umri zaidi ya miaka 65.

  Dk.Mpango amesema ili kukabiliana na changamoto hizo za ongezeko la idadi ya watu ,Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa pamoja na kutunga na kutekeleza sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992 na ilifanyiwa marekebisho mwaka 2006.

  Amesema lengo la Sera hiyo ni kutoa ni kutoa miongozo ya kushughulikia masuala ya idadi ya watu.Kwa kutambua kuwa kuna mahusiano baina ya mwenendo wa idadi na ubora wa maisha ya wananchi kwa upande mmoja na ulinzi wa mazingira.

  0 0


  Na Leandra Gabriel , Globu ya Jamii

  MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga ametangaza rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu.

  Hivyo kuanzia sasa mashindano ya Miss Tanzania nchini yataendeshwa na The Look Company Limited, chini ya Mkurugenzi Basila Mwanukuzi aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga amesema uamuzi huo umetokana na malengo yao ya kutaka mashindino hayo kusimamiwa na damu changa kwa lengo la kuleta chachu katika tasnia ya urembo nchini.

  “Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona kampuni yetu tayari imejijengea sifa na heshima nchini.Hata hivyo tunaamini The Look Company Limited chini ya Mkurugenzi Mwanukuzi watasimamia taratibu, kanuni, sheria na miiko ya uongozi na hatimaye kumpeleka mrembo katika mashindano ya dunia kama ilivyo kawaida,”amesema. Amewataka waandaaji wapya wa mashindano ya urembo wasisite kuomba ushauri au mawazo ya kujenga kutoka kwao pale watakapohitaji.

  Lundenga ambaye ni maarufu kama Uncle Hashim amewashukuru Baraza za sanaa la Taifa (BASATA), na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa ushirikiano mkubwa kwa muda wote tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 1994.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Look Limited, Mwanukuzi amesema wamejiwekea mikakati kuendeleza fani ya ulimbwende pale ambapo kampuni ya Lino imeishia. Amesema kuwa pale penye changamoto katika kuandaa masuala ya warembo watakuwa karibu na Kampuni ya Lino pamoja na BASATA ili kufanikisha na kuleta tija katika Taifa.
   MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga akitangaza uamuzi wake rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu,pichani kati ni Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi pamoja na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.
   Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati akikabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli za shindalo la Miss Tanzania

  0 0  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

  WAFUASI watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) 
  leo, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa 
  tuhuma za kufanya mkusanyiko isivyo halali.

  Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amewataja washtakiwa hao watatu 
  kuwa ni, Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi ambao wanadaiwa 
  kupigwa risasi na jeshi la polisi waliofikishwa kizimbani kwa Hakimu 
  Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wakiwa na majeraha katika sehemu za miguu na mapaja yakiwa yamefungwa bandeji.

  Washitakiwa hao Machi 8, mwaka huu wataunganishwa na wenzao 
  28, wanaodaiwa kutenda kosa pamoja.Kwa pamoja wanadaiwa, 
  Februari 16, mwaka huu, huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni 
  lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko 
  usio wa halali kinyume cha sheria kwa nia ya kufanya uvunjifu wa 
  amani na kusababisha taharuki kwa wananchi.

  Wametajwa baadhi ya washitakiwa hao 28 ni Thabita Mkude, Haji 
  Lukwambe, Emmanuel Kimoi,Mohammed Juma, Hussein Mrombo, 
  Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein 
  Nguli na Edna Kimoro.

  Wengine ni Jonathan Lema,Salha Ngondo, Ramadhan Mombo, 
  Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda,Omary Hamad, Fatima 
  Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa,Dickson Kerefu, 
  Raphael Mwaipopo, At human Mkawa, Mussa Kusigila, OMARY Danga, 
  Jackson Masilingi,Asha Kileta na Ally Rajabu.

  Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana.
  Baada ya kuachiwa kwa washtakiwa hao watatu ndugu zao waliwakumbatia na kuangua vilio mahakamani hapo.Kwa upande wake Wakili wa washtakiwa Alex Masaba alisema wamemaliza suala la msingi la wafuasi hao waliokamatwa Mkwajuni,ambao mwanzo hawakuletwa mahakamani lakini wenzao 28 waliletwa mahakamani na walipata dhamana

  Alisema walifuatilia katika vituo vya polisi kwa siku 12 ambapo 
  walishindwana na polisi ambapo Februari, 26,mwaka 2018 
  walipeleka maombi Mahakama Kuu na juzi walipangiwa tarehe ya 
  kusikilizwa maombi yao ambayo ni jana.

  0 0

  Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) and National Development Corporation (NDC) signed a Memorandum of Understanding of cooperation in resource mobilization, lending, distribution, and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania.

  Speaking on the objective of cooperation, the acting managing director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha said that the signed MOU will facilitate establishment of country-wide demand for tractors and farm implements as well as to facilitate mobilization of sustainable financial resources for provision of loans, procurement, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania and to facilitate the application of sound lending principles in the provision of loans for purchase of tractors and farm implements, including loan monitoring and evaluation.

  Other benefits will include facilitating establishment of more efficient means of procurement, distribution, and delivery of tractors and farm implements; and providing a framework for establishing effective and continuing collaboration between the Bank and the Corporation.

  “This MoU between the Bank and the Corporation will draw mutual benefits from cooperation between the two organizations in resource mobilization, lending, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania,” he said.

  Mr. Chacha added that the Bank and the Corporation are desirous to establish cooperation in resource mobilization, lending, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers.

  Adding that based on the mandate of the Bank, TADB is ready to facilitate increased access to finance through provision of short, medium and long-term credit facilities at affordable rates and terms across agricultural value chains of focus, including provision of loans for purchase of tractors and farm implements.

  According to the signed document TADB will be mandated among others to manage financial resources for financing procurement of tractors and implements through extension of loans to farmers in Tanzania and design innovative financing products and services with favorable conditions for financing agricultural mechanization by farmers in Tanzania.

  Other activities include conduct credit appraisal of identified agricultural projects earmarked for tractor and farm implement loans as well as managing the overall lending activities related to financing purchase of tractors and farm implements by farmers including loan monitoring and evaluation; and provide trade finance services to the Corporation as it relates to procurement of tractors and farm implements from source manufacturers.

  On his part, NDC’s Boss, Eng. Ramson Mwilangali said one of the major focuses of the Corporation includes promotion of agricultural mechanization in Tanzania; hence the signed cooperation will assist in improving agriculture production for both domestic consumption in Tanzania.

  He added that through the proposed cooperation NDC and TADB will facilitate the industrial feedstock through establishment of Tractor Assembly Plant at Kibaha for assembling semi knocked down (SKD) and completely knocked down (CKD) tractors along with farm implements for selling to individuals/groups of farmers.

  “This collaboration between the Bank and the Corporation among others may entail any of the subject matters covered by their mandates,” he said.

  He mentioned specific areas of collaboration that will include, but will not be limited to establishing country-wide demand for tractors and farm implements and costs thereof, formulating resources mobilization strategies for financing procurement Semi Knocked Down (SKD) and Completely Knocked Down (CKD) tractors for assembly alongside associated implements, provision of loans, distribution and servicing of agricultural inputs to farmers for the second phase II of the NDC Tractor Assembly Project as well as designing innovative financing products and services for loan financing and adoption of appropriate technologies by farmers in the country.

  Others according to Eng. Mwilangali will include identifying and appraising loan applications for tractors and farm implements by farmers; and conducting needs assessment, preparing and implementing capacity-building programs related to the application of modern technologies in agriculture in Tanzania.

  In order to facilitate implementation of the signed MoU, NDC is required to ensure timely procurement of Semi Knocked Down (SKD) and Completely Knocked Down (CKD) tractors and farm implements from abroad for assembly in Tanzania, ensure availability of tractors ready for sale to farmers at Tractor Assembly Plant in Kibaha and other designated sales centres and ensure timely delivery of tractors to farmers for which the payment and release order have been received.

  Other responsibilities include providing after sale technical service of tractors and farm implements lent to farmers at the designated service centers countrywide as well as ensure adequate stocks of tractor spares are available at the designated service centers at all times; and providing and manage two years warranty for the sold tractors.

  TADB and NDC are public owned institutions that aim at facilitate development in the country where the former is mandated to promote and support transformation of agriculture from subsistence to commercial undertaking to effectively and sustainable contribute to economic growth and poverty reduction while the latter is bestowed with a broad mandate as a development and promotion institution to stimulate industrialization in partnership with private sector.
   Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) speaks on the role of the Bank in implementing Government’s Industrialization Strategy during MoU signing in ceremony between TADB and NDC held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam. Centre is NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali who is flanked by NDC’s Director of Heavy Industry, Mr. Abdalllah Mandwanga.
   NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali (right) stresses on position of NDC in supporting Government’s Industrialization Strategy during MoU signing in ceremony between TADB and NDC held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam. Centre is TADB’s Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha and left is TADB’s Head of Legal Service, Ms. Neema Christina John.
   Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) together with NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali (right) sign MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania. The signing in ceremony held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam.
   Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) and his NDC’s counterpart, Eng. Ramson Mwilangali (right) display signed MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.
  TADB’s management together with NDC’s counterpart in the Memoir Group Photo after signing the MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.

  0 0


  Na Agness Francis, Globu ya jamii

  KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania, imeendelea kutoa zawadi kwa wateja wake kupitia promosheni ya SMATIKA yatosha na Intanenti Bando inayoendelea kufanyika nchini.

  Ambapo wateja wa Airtel hujishindia GB na zawadi zingine ikiwa ni simu za mkononi aina ya Smartphone na Modern ya Maajabu. Pia leo kampuni hiyo imemkabidhi mshindi wa simu aina ya Smartphone Mussa Ngai ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam. 

  Akizungumza leo jijini, Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando baada ya makabidhiano hayo akiwa kwenye duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dar es salaam kuwa sasa wamefikia droo ya 10 kufanyika katika promosheni hiyo ambayo bado inaendelea kwa siku 30 zaidi. 

  "Tumetimiza wateja 21,000 waliojishindia GB za bure na 30 waliojishindia simu na Modern ya maajabu kwa wateja wetu endeleeni kununua bando ili muweze kujishindia zawadi mbalimbali kutoka kwetu,"amesema Mmbando. 

  Aidha Msimamizi wa duka la Airtel money Ukonga Mzambarauni Dorice Opiyo amewakaribisha wateja ambao ni wakazi wa maeneo hayo kupata huduma za kurejesha laini na kujipatia salio kwa wale wanatoa huduma za mawaka

  Mshindi wa simu aina ya Smartphone, Mussa Ngai mkazi ambaye ni mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, akizungumzia kushinda promosheni hiyo amesema amefurahi kushinda kwani hakutegemea na alikuwa akinunua bando na kujiunga mpaka siku alipopigiwa simu kutoka Airtel ya kuambiwa ameshinda simu aina ya Smartphone.
   Mshindi wa Smartphone Mussa Ngai akikabidhiwa zawadi leo na  Dorice Opiyo Msimamizi wa Brunch ya Airtel Money Ya Ukonga Mzambarauni Jijini  Dar es salaam.
  Mshindi wa simu ya Smartphone   Mussa Ngai  akikagua simu yake mara baada ya zoezi la makabidhiano kumalizika leo katika  tawi la Airtel Money Ukonga Mzambarauni Jijini  Dar es Salaam.
   Mshindi wa simu ya Smartphone  Mussa Ngai akipiga picha na wasimamizi wa Brunch ya Airtel money Ukonga Mzambarauni Jijini Dar es Salaam mara baada ga kukagua zawadi yake aliyoshinda kupitia promosheni ya SMATIKA na yatosha Intanenti bando.


  0 0

  Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

  Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.

  Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

  Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Bw. Doto James amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia  kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  "Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini" Alisema Bw. Doto James.

  Ameishukuru Japan kwa msaada mwingine uliotolewa mwezi Septemba, 2017 wa kiasi cha fedha za Japan (Yen) milioni 69 sawa na shilingi bilioni 1.4 ambazo zimetumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hiyo itakayoanza kujengwa

  Bw. James ameeleza kuwa  awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge pamoja na kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Mlalakuwa, Lugalo na Tegeta.

  “Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza Bw. Doto James.

  Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kutolewa kwa msada huo ili kuwezesha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara kuanza kutayafanya matokeo ya kujenga barabara hiyo kuanza kuonekana dhahiri ikiwemo kupunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa ili kuokoa fedha nyingi zinazotokana na changamoto za msongamano huo.

  "Ili kukamilisha usanifu wa kina wa mradi huu, nilisaini mkataba wa usanifu wa kina wa mradi wa upanuzi wa barabara ya new Bagamoyo  (Awamu ya Pili) miezi mitano iliyopita, hatimaye sasa ninasaini mkataba wa sehemu kuu ambayo ni ujenzi wenyewe" Alisema Balozi Yoshida.

  Balozi huyo wa Japan hapa nchini, amesema mradi huo utasaidia kuboresha ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini na kwamba msaada huo ni mwendelezo wa kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania.

  Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari  yanayokadiriwa 52,000 yanayopita kila siku katika barabara hiyo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale. baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida, baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya Mradi wa upanuzi wa  Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili yaMradi wa upanuzi wa Barabara ya njia nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam. Anayeangalia makaratasi nyuma ni Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kuhakikisha inadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule.

  Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba. Waziri Mkuu amesema ni lazima viongozi hao wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike katika wilaya hiyo wasipate mimba ili waendelee na masomo. 

  “Kwa nini kila mwaka mimba Tandahimba zinaongezeka, viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukua hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.” Amesema lazima wahusika wote wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwa sababu wanaharibu elimu ya motto wa kike jambo ambalo si zuri. 

  Waziri Mkuu ametolea mfano mwaka 2015 wafunzi 10 walipata mimba, mwaka 2016 waliopata mimba walikuwa 20, mwaka 2018 waliongeza na kufikia 57.Amesema takwimu hizo haziridhishi, hatua kali zichukuliwe kudhibiti vitendo hivyo na Serikali haitaki kusikia mwanafunzi ameacha shule kwa sababu ya kupata mimba.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu na wafuate sheria. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi amewasisitiza watumishi wa umma wawafuate wananchi vijijini na wawahudumie ipasavyo.

  Amesema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.“Serikali inataka kila mtumishi atimize wajibu wake na haina muda wa kuwalea watumishi wazembe, wala rushwa na wasiowajibika, hivyo watambue wajibu wao.” 

  Pia amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo wahakikishe wanakwenda kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao. 

  IMETOLEWA NA: 
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMATANO, FEBRUARI 28, 2018.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kushoto akiwakabidhi wafanyabiashara soko kuu TV na king'amuzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyomshinda mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) miaka 10 toka ahahidi 
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ,katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wakiwa na wafanyabiashara baada ya kutekeleza ahadi iliyomshinda mbunge Msigwa 


  Na MatukiodaimaBlog 

  CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimetekeleza ahadi ya TV iliyoahidiwa wakati wa kampeni za ubunge mwaka 2015 na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika soko kuu la Manispaa ya Iringa .

  Akizungumza leo mara baada ya kukabidhi TV hiyo na king'amuzi chake kwa uongozi wa soko kuu mjini Iringa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa CCM imelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya TV nchi 58 baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kuomba kusaidiwa TV hiyo kwa ajili ya kufuatilia habari mbali mbali zinazojiri nchini wakiwa katika sokoni hapo .

  Alisema pamoja na kuwanunulia TV hiyo aina ya Sumsung wamepata kuwanunulia king'amuzi pamoja na kuwalipia malipo ya mwezi mmoja kuwa lengo la CCM kufanya hivyo ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbali mbali za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao .

  " CCM tumeendelea kutekeleza ahadi mbali mbali ila kama mtakumbuka kata ya Kihesa kulikuwa na jengo ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka 10 ila baada ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kihesa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri aliahidi na tayari ametekeleza hivyo CCM tukiahidi tunatekeleza wenzetu wakiahidi wanatelekeza ahadi zao "

  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Magufuli aliwaagiza viongozi wa CCM kwenda kutatua kero za wananchi na ndivyo ambavyo CCM Iringa mjini imekuwa ikifanya hasa ukizingatia kuwa chama kinachotawala ni CCM hivyo lazima CCM kutatua kero za wananchi bila kujali zilitolewa na upinzani ama CCM .

  " Hatupendi kuona wananchi wanasikitika ama wanapoteza haki zao hivyo tutawasikiliza na kutatua kero zao wenzetu wanaahidi bila kutekeleza ila sisi kama CCM tutahakikisha ilani yetu inatekelezwa kwa nguvu zote na tutakwenda tena kuwasikiliza wanahitaji nini "

  Katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga alisema kuwa kuwa pamoja na CCM kutekeleza ahadi ya mbunge Msigwa wa Chadema ila imeendelea kusaidia jamii katika shughuli za maendeleo kama kutoa bati 300 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na kutoa elimu kwa wanawake juu ya ujasiliamali .

  Alisema kuwa kutoka na wapinzani kufanya kazi ya kwenye mitandao ya kutukana na kubeza CCM ila wao CCM kazi yao ni kuwakomboa wananchi na kuona wanatatuliwa kero walizo nazo na kudai kuwa kwa kazi zinazofanywa na CCM Iringa mjini ndizo zinapelekea madiwani zaidi ya Chadema kujiuzulu na kujiunga na CCM .

  " Hadi hivi sasa CCM toka madiwani wa kata watatu sasa ina madiwani 9 waliohamia CCM hivyo ndio maana tunasema madiwani waliobaki nje ya CCM wajiunge na CCM timu ya maendeleo maana shabaha kubwa ni kuwatumikia wananchi "

  Katibu huyo wa CCM Iringa mjini alisema kumekuwepo na maneno mengi yasiyo ya kweli juu ya CCM kununua madiwani wa Chadema na kuwa suala hilo halipo kwani CCM haina pesa za kununua diwani ina pesa za kuwaletea wananchi maendeleo .

  Mwenyekiti wa soko kuu la Iringa Sturmi Fussy akishukuru kwa msaada huo alisema kuwa TV hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wafanyabiashara sokoni hapo kwani itawapunguzia muda wa kutoka katika eneo lao la kazi kwenda kutazama TV nje ya soko hilo hata hivyo aliomba CCM kusaidia daladala kufika eneo hilo la soko ili kuongeza wateja zaidi katika soko hilo 

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Baadhi ya Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipotoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar .
  Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Balozi Seif alipokuwa akisoma Hotuba ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.
  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar M,h. Zubeir Ali Maulid akiongozwa na Askari wa Baraza hilo wakitoa nje ya Ukumbi baada kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi huko Chukwani.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.

  Picha na – OMPR – ZNZ.
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano yake dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia vilivyokithiri katika maeneo mbali mbali Nchini, kamwe haitamvumilia, kumuonea aibu, wala muhali Mtu yeyote wa cheo chochote na ngazi yeyote pindi atakapobainika kuhusika na vitendo hivyo.

  Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukifanyika katika Majengo ya Baraza hilo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya na kutahadharisha wazi kwamba Viongozi na Wananchi wanapaswa kutambua kuwa Sheria ni Msumeno.

  Balozi Seif alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kushiriki katika kadhia hiyo ikiwemo wafanyaji na wale wote wanaoshiriki katika kuwalinda na kuwakingia kifua wahalifu wote wa masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.

  Alivinasihi vyombo vya ulinzi na usalama kupambana zaidi dhidi ya vitendo hivyo vinavyolitia aibu Taifa sambamba na kuharibu maisha ya Wananchi, huku Jamii ikipaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo hivyo katika Mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo baya Kijamii na hata Kidini.

  Balozi Seif alisema tabia ya baadhi ya Watu hasa Familia kuzimaliza kesi za Udhalilishaji Majumbani itakupunguza kasi ya Serikali kuwashughulikia wahalifu hao na kuwanasihi Wananchi wahusika kufika Mahakamani kwa kutoa ushahidi utakaotoa nguvu ya sheria kuchukuwa mkondo wake na haki kupatikana ili hatimae kuvimaliza vitendo hivyo katika Taifa hili.

  Alieleza kwamba Baraza la Wawakilishi tayari limeshapitisha Sheria ya adhabu kwa wahusika wa vitendo vya udhalilishaji, ambapo imeweka bayana kuwa Mtuhumiwa ye yote wa kosa la udhalilishaji hatopaswa kupewa dhamana.

  Balozi Seif alifahamisha kwamba Sheria hiyo sasa inangojea kuwekwa saini na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili iwe Sheria ambapo Mheshimiwa Rais anatarajiwa kuifanya kazi hiyo muda sio mrefu kuanzia hivi sasa.

  Akizungumzia suala la ulipaji umeme kwa Deni ya Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} kwa upande wa Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ililiamuru Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO}kulilipa deni hilo kwa Tanesco kwa kiwango cha Shilingi Bilioni Mbili kwa Mwezi.

  Alisema malipo hayo yamepangwa kwenda sambamba na Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar pia kuagizwa kupunguza Deni hilo kwa kiwango cha Shilingi Bilioni Moja kwa Mwezi malipo ambayo yalianza utekelezaji wake.

  Hata hivyo Balozi Seif alieleza kwamba utekelezaji huo ulikumbwa na changamoto zilizojitokeza kwa upande wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} kwa kutoendelea kulipa kwa ukamilifu kiwango kilichowekwa na Serikali na badala yake Shirika lililipa kwa Miezi Minne tu kuanzia Mwezi Juni, 2017 hadi Oktoba, 2017.

  Alisema Miezi iliyofuata ZECO ililipa Deni hilo chini ya kiwango kilichoagizwa kutokana na ukusanyaji mdogo wa mapato yanayotokana na ankara za matumizi ya umeme kutoka kwa baadhi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na zile za Muungano wa Tanzania zilizopo Zanzibar.

  Balozi Seif alisema hali hiyo imepelekea Shirika la Umeme Zanzibar kutokuwa na mapato ya kutosha kulipa deni hilo kila Mwezi badala ya kukidhi mahitaji mengine ya msingi na ya lazima ya kuliendesha Shirika hilo.

  Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma za Maji safi ya salama Mjini na Vijijini, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali Kuu kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imejipanga kutekeleza miradi Minne mikubwa ya huduma hiyo Nchini.

  Aliutaja ule Mradi wa Uimarishaji wa Miundombinu katika kubadilisha Mabomba yaliyochakaa wenye urefu wa Kilomita 68 katika Maeneo ya Bumbwisudi, Kinumoshi, Kianga, Welezo, Muembe Mchomeke, Amani pamoja na Kiponda Mji Mkongwe.

  Alisema utekelezaji wa Mradi huu unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Afrika wa Awamu ya 12 {ADF 12} unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni 48 hadi kukamilika kwake.

  Balozi Seif aliutaja mradi mwengine wa Uimarishaji wa miundombinu ya Maji Mjini unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 225 za Kitanzania utahusisha ujenzi wa Matangi ya kuhifadhia Maji katika maeneo ya Welezo juu pamoja na Welezo Magharibi.

  Alieleza Mradi huo utakwenda sambamba na ulazaji wa Mabomba yenye urefu wa Kilomita 120 katika Zoni ya Migombani pamoja na uwekaji wa huduma za Umeme katika maeneo husika.

  Balozi Seif alisema upo mradi mpya wa uimarishaji miundombinu ya Maji Mjini utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni Mia 207 utakaohusisha ulazaji wa Mabomba katika maeneo ya Zoni ya Mfenesini, Kizimbani, Tunguu na Fumba.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekubali kufadhili mradi wa uchimbaji Visima 11 pamoja na ulazaji wa Mabomba ndani ya Mkoa Kaskazini Unguja na baadhi ya Wilaya ya Kati na Magharibi “A” unaotarajiwa kugharimu shilingi Bilioni 12 za Kitanzania.

  Alisema ili miradi yote iendelee kudumu kwa kipindi kirefu katika utoaji wa huduma zake Wananchi watawajibika kuchangia gharama za uendeshaji wa huduma hiyo kwa wale watakaopata badala ya kubakia na dhana ya uchangiaji wa huduma ya Maji safi ni jukumu la Serikali pekee.

  Mkutano wa Baraza la Wawakilishi ulipokea na kujadili Ripoti za Kamati za kudumu Saba za Baraza hilo ambapo pia Wajumbe wa Baraza hilo walijadili na kuipitisha Miswada Mitatu ya Sheria.

  Miswada hiyo ni ule wa kufuta Sheria ya kusimamia mwenendo wa Biashara na kumlinda mtumiaji ya Zanzibar Nambari 2 ya Mwaka 1995 na kutunga Sheria Mpya ya Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji, Kuweka Masharti Bora zaidi pamoja na Mambo Mengine yanayohusiana na hayo.

  Mwengine ni Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Adhabu na kutunga Sheria Mpya ya Adhabu, Kuweka Masharti Bora zaidi pamoja na Mambo Mengine yanayohusiana na hayo.

  Mswada wa Tatu ni ule wa Sheria ya kufuta Sgeria ya Mwenendo wa Jinai Nambari 7 ya Mwaka 2004 na kutunga Sheria Mpya ya Mwenendo wa Jinai na kujweka utaratibu Bora wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Usikilizaji wa Kesi za Jinai na Mambo Mengione yanayohusiana na hayo.

  Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi Jumatano ya Tarehe 9 Mwezi Mei Mwaka 2018.

  Othman Khamis Ame

  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  27/2/2018.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri.

  Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

  Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

  1.    OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

  i.    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu

  2.    OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

  i.    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman

  ii.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim

  3.    OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

  i.    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri

  ii.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis


  4.    OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

  i.    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed

  ii.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga

  5.    WIZARA YA AFYA

  i.    Waziri wa Afya- Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed

  ii.    Naibu Waziri wa Afya – Mheshimiwa Harusi Said Suleiman

  6.    WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

  i.    Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Salama Aboud Talib

  ii.    Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Juma Makungu Juma  7.    WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

  i.    Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Balozi Amina Salim Ali

  ii.    Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh

  8.    WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

  i.    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma

  ii.    Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri

  9.    WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

  i.    Waziri wa Fedha na Mipango – Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum Mohamed

  10.    WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE

  i.    Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale  - Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo

  ii.    Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Choum Kombo Khamis


  11.    WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO

  i.    Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico

  ii.    Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Shadia Mohamed Suleiman

  12.    WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

  i.    Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Rashid Ali Juma

  ii.    Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Dkt. Makame Ali Ussi

  13.    WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI

  i.    Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya

  ii.    Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Mohamed Ahmada Salum

  14.    WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

  i.    Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo - Mheshimiwa Balozi Ali Abeid Karume

  ii.    Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo - Mheshimiwa Lulu Msham Abdulla  Aidha, Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib wanaendelea kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum.


  WAKATI HUO HUO Rais wa Zanzibar naMwenyekitiwaBaraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi katikaTaasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

  1.    UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA

  i.    Bwana Issa Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba.

  ii.    Bwana Rajab Ali Rajab ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.

  2.    UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WILAYA

  i.    Bwana Bakari Ali Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kaskazini, Pemba.

  ii.    Bibi Fatma Mohamed Juma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Kusini, Unguja.

  iii.    Bwana Juma Abdulla Hamad ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mjini.

  iv.    Bwana Hamza Mahmoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Magharibi B.

  v.    Bwana Makame Machano Haji ameteuliwa kuwa Katibu Tawalawa Kaskazini B.


  3.    UTEUZI WA OFISA MDHAMINI WA WIZARA YA AFYA - PEMBA

  i.    Bibi Shadya Shaaban Seif ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhaminiwa Wizara ya Afya – Pemba.

  4.    UTEUZI WA MWENYEKITI NA MKURUGENZI MKUU WA WAKALA  WA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO NA VYA KATI

  i.    Bwana Mussa Ame Silima ameteuliwa kuwa Mweyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.

  ii.    Bwana AbdulhamidIdrisa Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati.

  5.    UTEUZI WA MKURUGENZI WA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

  Dr. Mustafa Ali Garu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.

  6.    UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAJI (ZAWA)

  Bwana Mussa Ramadhani Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Kuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).

  7.    UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI NA WATENDAJI WA WAKALA WA MATUKIO YA KIJAMII

  i.    Bwana Haji Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekitiwa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

  ii.    Dkt. Hussein Khamis Shaaban ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

  iii.    Bwana Idrisa Shaaban Zaharan ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaehusika na Usajili wa Mzanzibari Mkaazi na Wageni Wakaazi katika Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii.

  iv.    Bwana Shaaban Ramadhan Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anaeshughulikia Usajili wa Vizazi, Vifo, NdoanaTalaka.

  8.    UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PBZ

  Bibi Kidawa Hamid Saleh ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi ya PBZ.

  Uteuzi huo unaanza tarehe 1Machi, 2018.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
  nembo%20ya%20NEC

                       Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikia malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo aliyawasilisha jana kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
  Malalamiko yaliyotolewa na Mhe. Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani aliongea na Mhe. Mbowe kwa njia ya simu. Madai kwamba tume haikuwajibu malalamiko yao sio kweli. Ni upotoshaji wa hali ya juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.
  Tume ya taifa ya uchaguzi haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa, bali inajibu hoja kwa mujibu matakwa ya katiba, sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi na maelekezo yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa  kwa matakwa ya sheria na katiba na sio matakwa ya mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa.
  Kanuni, sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utararatibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.  Utaratibu uko wazi kwa changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, wakati wa kampeni ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.
  Kwa masikitiko CHADEMA walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea, walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa tume ya uchaguzi na Tume ilipitia na ikawarudisha wagombea wao kwenda kugombea.
  CHADEMA walitaka wakati wa kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa uchaguzi na wajumbe ni kutoka vyama vyote vilivyosimamaisha wagombea na ndio wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa Tume badala ya kuwasilsiha malalamiko kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote.
  Sio sahihi kusema Tume hatukujibu malalamiko yao. Mfano tarehe 15 Chadema waliwasilsiha barua mbili Tume ya Uchaguzi, waliwasilisha barua moja asubuhi na saa 1.30 jioni waliwasilisha barua nyingine, jumla barua hizo zikiwa na hoja tano na Tume ikawaandikia barua zenye ufafanuzi wa hoja hizo.
  Hoja ya kwanza, CHADEMA walitaka kuapishwa mawakala wao mbadala asilimia 15. Tuliwajibu kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachokipa fursa chama chochote cha siasa kuapishiwa mawakala mbadala asilimia 15. Kifungu 57 (3) kinafafanua vizuri namna ya mawakala wanavyotakiwa kuwepo na kuapishwa
  Lakini pia hata kama kifungu hicho kingekuwa kinatoa fursa hiyo, Chadema walileta malalamiko yao  tarehe 15 Februari 2018 wakati uteuzi wa mawakala ulikuwa tarehe 10 Februari 2018, hivyo hakukuwa na muda wa kuwaapisha mawakala wengine kwa mujibu wa sheria kwa kuwa hawakuwemo kwenye orodha.

  Hoja nyingine ya CHADEMA ni msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni alikataa kuwapa mawakala barua na fomu za viapo. Tulifanya hesabu tukaona kwamba msimamizi alitakiwa kusaini barua 22,000 na fomu za viapo 14,000. Tukasema kwamba kutakuwa na utaratibu wa mawakala kupewa fomu na viapo vyao kupitia kwa wawakilishi wao na walipewa kwa njia hiyo. Hili tuliwajibu hivyo katika barua yetu.
  Hoja nyingine mawakala wa CHADEMA waliambiwa kwenda na vitambulisho kwenye vituo vya kupigia kura. Katika hoja hii tuliwajibu kwamba wakala chama cha siasa ni mpiga kura kama walivyo wapiga kura wengine. Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi kifungu namba 61 na namba  62 cha sheria za Serikali za mitaa, Tume ilitoa ridhaa kwa wapiga kura kutumia vitambulisho mbadala ili nao waweze kupiga kura ndio maana wakaelekezwa kwenda navyo.

  Hoja nyingine ni kwamba msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni, hajatoa maelekzo ni wapi pa kuhesabia kura. Tukawajibu kwamba Tume ina barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi akiwajulisha vyama vya siasa kwamba sehemu ya kujumlishia kura itakuwa ni sehemu ya Biafra. Kanuni inasema wangejulishwa eneo hilo la kujumlishia baada ya kura kupokelewa, lakini msimamizi wa uchaguzi alijiongeza akawajulisha mapema eneo la kujumlishia kura.
  Hoja nyingine ni wasimamizi wa vituo hawakuteuliwa kwa utaratibu. Majibu ya hoja hii ni kwamba sheria ya uchaguzi imeweka utaratiibu wa namna wasimamizi hao wanavyopatikana. Lakini kanuni za uchaguzi wa Rais namba 15 na kanuni 11 za Serikali za Mitaa zinaeleza namna msimamizi wa kituo anavyopatikana.

  Kanuni hiyo inasisitiza kuwa msimamizi wa uchaguzi atatoa tangazo, Kwa jimbo la Kinondoni msimizi alitoa tangazo, watu waliomba, walifanya usahili na kabla ya uteuzi mkurugenzi wa uchaguzi alitoa matangazo ya majina katika mbao zote za kata 10 za jimbo la Kinondoni.
  Msimamizi wa uchaguzi aliwaandikia barua vyama vyote kama vina pingamizi vijitokeze. Kama kulikuwa na tatizo vyama vilikuwa na fursa ya kuweka pingamizi, lakini hawakufanya hivyo na Tume tuliwajibu hivyo. Unaposema tume haikuwajibu sio kweli, labda CHADEMA waseme tuliwajibu nje ya matakwa yao waliyotaka na sio kwa mujibu wa sheria.

  Hoja nyingine ni kwamba kuna wizi wa kura. Katika kituo cha kupigia kura kuna msimamizi wa kituo, msimamizi msaidizi na wakala wa chama cha siasa na kuna waandishi wa habari. Utaratibu ulikuwa wazi. Pia kuna utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha malalamiko kama mtu haridhiki kabla wakati na baada ya kupiga kura, wakati wa kuhesabu na baada ya kuhesabu kura.
  Mtu au chama kisipofuata uratibu huo, lazima utalalamika tu na utaona tume ni korofi. Hii ni kwa sababu mtu akija Tume kulalamika, ataelekezwa kufuata utaratibu huo. Mgombea akikataa kufuata utaratibu huo hata akija Tume kulalamika,ataelekezwa na Tume atumie wakala wake kujaza fomu zote namba 14 na 16 zinazohusika kisheria kuwasilisha malalamiko.

  Tunamsihi Mbowe na chama chake, wasome sheria za uchaguzi na kuzielewa. Tume iko tayari kumpa elimu ya mpiga kura kuzifahamu sheria hizi kwa mapana yake.
  Pia tunamwomba Mhe. Mbowe kama hakuridhika na taratibu za uchaguzi, ana fursa ndani ya siku 30 za kuwasilisha malalamiko yake mahakamani ndicho chombo pekee cha kutoa haki. Aende mahakamani kwa kutumia ushahidi ambao mawakala wake walijaza kwenye fomu namba 14 na 16 kwa sababu Tume ya Uchaguzi haina tena fursa ya kupokea malalamiko kisheria baada ya uchaguzi kupita.
  Kailima, R.K
  MKURUGENZI WA UCHAGUZI

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (katikati) wakiangalia mashine ya kubangulia korosho katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah, katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kukaushia korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa, wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 1528 | 1529 | (Page 1530) | 1531 | 1532 | .... | 1897 | newer