Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO

$
0
0
Na Ripota Wetu, Arusha

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amepata ajali ya gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara.

Taarifa kuhusu tukio hilo zinadai kuwa Kamanda Mkumbo amepata ajali leo, baada ya gari aliyokuwa akiitumia kupasuka gurudumu la nyuma.

Baada ya kupasuka kwa gurudumu hilo, gari ilipoteza muelekeo na kisha kupinduka.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ambapo amesema ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu watatu akiwamo Msaidizi wa Kamanda Mkumbo pamoja na dereva wake na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.

Ilembo amesema ajali hiyo imetokea leo saa saa nane mchana wakati Kamanda Mkumbuko akiwa njiani kutokea mkoani Singida kwenda Arusha na alipofika eneo la katikati ya Mdori na Minjingu ndipo guruduma la nyuma upande wa kushoto la gari hiyo lilipasuka na kusababisha ajali hiyo.

Amesema Kamanda Mkumbo ameumia kidole chake cha shahada na baada ya ajali hiyo amepelekwa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha ambako anaendelea na matibabu wakati dereva wake naye analalamika maumivu kwenye paja la upande wa kushoto na msaidizi wake anasema hajaumia kwani hasikii maumivu mahali popote.

Amewataka wananchi wa Arusha kutokuwa na hofu kwani Kamanda Mkumbo hali yake inaendelea vema na kubwa ni kumuombea ili arudi kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea na majukumu mengine ya kulitumikia Taifa.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio a ajali hiyo.

MAVUNDE AAGIZA WAKURUGENZI KUPANDISHWA KIZIMBANI JIJINI MWANZA, NI KWA KUTOJISAJILI NA WCF

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, (pichani juu), ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.

Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo Jumatatu Februari 26, 2018 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jijini Mwanza, kubaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter, jiji la Mwanza pekee lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri 482 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya Mhe. Naibu Waziri kufanya ziara hiyo ya ghafla.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Mhe. Mavunde pia ameiagiza WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, (Mkurugenzi Mtendaji Bw.Karan Bachu), 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airco Holdings inayotoa huduma za kusogeza vifurushi na mizigo uwanja wa ndege wa Mwanza na hoteli ya Belmonte ya jijini humo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo, Bw. Philemon Tei, amejikuta matatani.

"Naagiza waajiri hao kulipa michango yote ya nyuma (tangu tarehe 1 Julai 2015 tangu Mfuko ulipoanza kutekeelza majukumu yake au siku mwajiri aliyoanza kazi zake iwapo ni baada ya tarehe 1 Julai 2015). 

Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko. “Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.

"Tutatekelza agizo la Mhe. Waziri kama alivyolitoa, na nitoe rai tu kwa waajiri kote nchini (Tanzania Bara), kutekeleza takwa hilo la kisheria, kwani hakuna kichaka cha kujificha tutawafikia." Alisisitiza Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter katika taarifa yake kwa waandishi wa habari. 
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde(kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bw. Anslem Peter, akitoa maagizo ya kufikishwa mahakamani mara moja mkurugenzi mtendaji wa Belmonte Hotel ya jijini Mwanza leo Februari 26, 2018 kwa kushindwa kutekeleza takwa la kisheria linalomtaka kujisajili na Mfuko huo. Naibu waziri ameonya waajiri wote nchini kuttekeleza wajibu wao kwani hakuna mahala pa kujificha na operesheni hiyo inaendelea mikoa mingine. 
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, (wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Uenmdeshaji (Director of Operations), Anslem Peter, Afisa Kazi Mfawidi Mkoa wa Mwanza, Khadija Hersi, wakipitia nyaraka za Hoteli ya Belmonte ya jijini Mwanza kuona jinsi uongozi wa hoteli hiyo unavyotekeleza Sheria ya Fidia Kwa wafanyakazi, kwa kujisajili na Mfuko huo. Naibu Waziri alifanya ziara ya kushtuikiza kwenye kampuni kadhaa jijini Mwanza ambapo hoteli hiyo ilibainika kutojisajili na aliamuru Mkurugenzi wake kupelekewa mahakamani mara moja. Wakwanza kulia aliyesimama ni Mkuu wa KItengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge.
Naibu waziri akiongozana na Bw. Anslem Peter na afisa mwingine kutoka jijini Mwanza mara baada ya kukagua ofisi za huduma za vifuriushi na mizigo uwanja wa ndege wa Mwanza, Airco Holdings.
Mkurugenzi wa Belmonet Hotel ya jijini Mwanza, Bw.Philemon Tei 
Naibu Waziri Mvunde, akizungumza na wafanyakazi wa Airco Holdings ya uwanja wa ndege wa Mwanza. Kushoto ni Bw. Anslem Peter 
Naibu Waziri akiwa kwenye ofisi za Airco Holdings uwanja wa ndege wa jijini Mwanza
Naibu Waziri akitoa maelekezo kwa uongozi wa Belmonte Hotel
Maafisa wa WCF, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anslem Peter, (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, wakitoka kwenye kiwanda cha kuchakata samaki jijini humo baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza.
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu, akijieleza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, (hayupo pichani)
Mhe. Mavunde, (kushoto), akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu
Mhe. Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO ya jijini Mwanza baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza leo Februari 26, 2018.
Mhe. Mavunde na maafisa wa WCF wakiwa ofisi za kampuni ya kuchataka samaki jijini Mwnaza
Mhe. Naibu Waziri akipitia nayaraka za kampuni ya kuchakata samaki ya jijini Mwnaza wakati wa ukaguzi wake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter akimuonyesha nyaraka za kampuni ya uchakataji samaki jijini Mwanza, ambayo imeanza kuwasilisha michango, lakini bado haijajisajili na Mfuko, ambapo aliagiza watekeeleze takwa hilo haraka.

MBUNGE MGIMWA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU,AFYA JIMBONI KWAKE

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi sim tanki ya lita 500 kwa viongozi 
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa bati na rangi kwa baadhi ya viongozi waliojitokeza kuja kuchukua masaada huo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi diwandi makopo ya rangi 


Na Fredy Mgunda,Mufindi.

MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo Mgimwa alisema kuwa ametoa mabati 280, mifuko 310 ya saruji, rangi za maji na mafuta na sim tenki la lita mia tano (500) za kuhifadhia maji.

“Nilifanya ziara katika vijiji vya kata hizo nikaona wananchi wanavyojitoa kuboresha sekta ya elimu na mimi kama mbunge wao nikaamua kuwaunga mkono kwa kuchangia vifaa hivyo” alisema Mgimwa

Mgimwa alizitaja kata zinazonufaika na msaada huo ni kata ya Mapanda, Kibengu, Ihanu na Sadani na akavitaja vijiji vinavyonufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na Ihimbo, Ukami na Chogo katika kata ya Mapanda; na Kipanga, Igeleke, Kibengu, Usokami na Igomtwa katika kata ya Kibengu.

Vingine ni kijiji cha Lulanda katika kata ya Ihanu na katika kata ya Sadani Mgimwa sehemu ya msaada huo inakwenda kusaidia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mgalo.Aidha Mgimwa alisema kuwa ataendelea kusaidia maendeleo kwenye vijiji ambavyo vinafanya maendeleo katika jimbo lake

Akiongea kwa niamba ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi na vijiji vyote vilivyonufaika na msaada huo, Makamu Mwenyekiti Asheri Mtono alisema kuwa jimbo la Mufindi Kaskazini linakabiliwa na changamoto nyingi za ujenzi wa majengo mbalimbali hivyo msaada alitoa utapunguza changamoto zilizopo kwa kiasi Fulani 

“halmashauri hii ina changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu ya shule na kwa msaada huu wa mbunge mazingira hayo yatakwenda kuboreshwa” alisema Mtono.Mtono ambaye pia ni diwani wa kata ya sadani alisema pamoja na mchango wa mbunge huo na wadau wao wengine, wananchi wa vijiji hivyo na vingine vyote katika halmashauri hiyo wanahitajika kuendelea kuchangia shughuli zao za maendeleo.

Nao baadhi ya viongozi wa vijiji wamempongeza mbunge Mgimwa kuwa kutoa vifaa vya ujenzi kwenye vijiji vyake vyote vya jimbo la Mufindi Kaskazini ambavyo vitachochoe kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Isupilo, Onorata Mwanuke alisema kwa msaada waliopatapata wanakwenda kukamilisha ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu.

“Mahitaji ya nyumba za walimu ni tisa zilizopo ni tatu na mbunge ametoa msaada wa mifuko 30 ya saruji kusaidia kukamilisha nyumba ya nne ya mwalimu. Tunategemea mbunge ataendelea kutuunga mkono”alisema Mwanuke

Kabla ya jana mbunge mgimwa alishakuwa ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Na alifanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

MNEC SALIM ASAS ATOA MSAADA WA MILIONI TANO KWA JUMUIYA YA WAZAZI KILOLO

$
0
0

Na Fredy Mgunda,Kilolo

MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa Salim Asas ameichangia jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi ( UWT) wilaya ya Kilolo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano ya hadhara.

Asas ametoa ahadi hiyo Leo wakati akifungua kikao cha baraza kuu la UWT Wilaya ya kilolo. Alisema kuwa lengo la kusaidia jumuiya hiyo ni kuitaka ijitegemee pia kuwa na miradi yake.

Kwani alisema ameona ni vema kuiwezesha jumuiya hiyo kupata ndoano kuliko kuipa samaki na kuwa kwa kipindi chake chote cha miaka mitano atakayokuwepo madarakani ataichangia jumuiya hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi huo."Ahadi yangu nitapaswa kuiweka katika maandishi ili familia yangu ijue pale nitakapo tangulia mbele za Haki ahadi hii iweze kutekelezwa na familia maana hatujui la kesho"

Hata hivyo alipongeza jitihada za UWT wilaya ya Kilolo kwa kuwa na mipango ya kimaendeleo kwa jamii tofauti na vyama vya upinzani ambavyo mipango yao ni maandamano na vurugu.
Usikose kusoma gazeti la RAI undani wa habari hii au tembelea Chanel yetu ya YouTube: matukiodaima .
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa,ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa wa Iiringa Salim Asas akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo, kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT wilayani humo.




Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga ( NEC)Salim Asas akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 5 mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT
Asas akipongezwa kwa mchango wake 

SPORTPESA KUKARABATI NYUMBA YA MADAKTARI ZANZIBAR

$
0
0

Picha ya pamoja kati ya (Baadhi ya wawakilishi/Uongozi wa SportPesa Tanzania) na uongozi wa Kizimkazi mkunguni mara baada ya kuzindua na kukabidhiwa mradi wa kujenga nyumba ya madaktari pichani, Kizimkazi Mkunguni, mkoa wa kusini, Zanzibar. Nyumba hizo zinatarajiwa kuchukua takribani miezi sita mpaka kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa uongozi wa Kizimkazi.

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri nchini ya SportPesa Limited, imekubali kufanya ukarabati wa nyumba kwa ajili ya madaktari wawili wa Kituo cha Afya, Mkunguni eneo la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema: 
“Ikiwa bado tuko mwanzoni mwa mwaka 2018, kampuni yetu tumeamua kutoa mchango wetu kwa jamii ya Zanzibar kwa kumalizia ujenzi wa nyumba ya madaktari ambayo ujenzi wa awali ulifanyika miaka 30 iliyopita, ujenzi mpya ni pamoja na kuongeza vyumba ili nyumba hiyo iweze kukaliwa na madaktari wengi zaidi.
Kwa Wanazanzibari wote, sisi kama SportPesa tupo kwa ajili yenu na si kwa upande wa Bara tu na ndiyo maana tumeamua kukarabati makazi ya madaktari kwani wapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu na ya watu wanaotuzunguka.Ujenzi wa nyumba hizi itaanza haraka iwezekanavyo na itachukua si zaidi ya kipindi cha miezi sita hadi kukamilika.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hiyo, Diwani wa Wadiyamuyuni, Mustafa Mohammed Haji alianza kwa kuwakaribisha wawakilishi kutoka SportPesa kwenye wilaya yake na Zanzibar.

“Napenda kuipongeza kampuni yenu kwa kazi nzuri mnayoifanya ikiwa pamoja na mambo mbalimbali mnayofanya ili kuendeleza na kukuza sekta ya michezo nchini
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas akiweka saini kwenye kitambu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kizimkazi, Mkunguni.

“Nilipopata taarifa juu ya ujio wenu kiukweli nilifarijika sana maana nawaamini na nategemea mambo mazuri kutoka kwenu kwani kwa maraya kwanza kusikia SportPesa ni kipindi kile mlivyoichukua timu yetu ya Jang’ombe kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup mwakaj ana.”

Huu utakuwa ni muendelezo wa huduma za kijamii ambazo kampuni ya SportPesa imeendelea kuchangia ili kubadili maisha ya Watanzania katika Nyanja mbalimbali za kimaisha.

AWESO AHIDI NEEMA KWA WAKANDARASI WA MAJI WAAMINIFU

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu. Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na Miradi ya DAWASCO na DAWASA. 

"Wizara ya Maji inajitahidi kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati"alisema Aweso Katika ziara yake hiyo, Mheshimiwa Aweso alitembela miradi ya Maji ya Hondogo, Kibamba, Kingazi A pamoja na Mburahati.
Naibu Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akiangalia bomba lililopasuka.

KIGWANGALLA ATEMA CHECHE KWA WAFUGAJI MANYARA

MILIONI 64/-ZAHITAJIKA WAZEE WOTE MKURANGA WAPATE VITAMBULISHO VYA MATIBABU-ULEGA

$
0
0
Na Emmanul,Globu ya jamii

SHILINGI milioni 64 zinahitajika ili wazee wote wilayani Mkuranga mkoani Pwani wapatiwe vitambulisho kwaajili ya matibabu.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kilimahewa Kaskazini wilayani mkuranga.

Amesema mchakato huo umekwishaanza kwa majaribio katika kata tatu ambazo ni Kisiju,Beta na Mkuranga.Ameongeza kuwa majaribio yaliyofanywa yameonesha mafanikio na tayari vitambulisho 300 vimeshatolewa.

Aidha Ulega ameongeza kuwa nchakato huo kwasasa unaendeshwa kwa awamu mbili ambapo kata 13 zitahudumiwa katika awamu ya kwanza na awamu ya pili wanatarajia kuhudumia kata 12.Amesema awamu ya kwanza Sh.milioni 6 zinatarajiwa kutumika bila kutumia mzabuni.

Amezitaja kata zitakazoanza awamu ya kwanza kuwa ni Tambani,Tengelea,Mipeko,Mkuranga,Mwandege,Vikindu,Kimanzichana,Vianzi,Beta,Kisiju,Mbezi,Shungubweni,na Kiparang'anda.
 Wananchi wa kijiji cha Kilimahewa Kaskazini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akisalimiana mara baada ya kuwasiri katika kijiji cha  Kimanzichana Kaskazini  leo mkoani Pwani.

MO Dewji aahidi kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata ufadhili wa taasisi yake

$
0
0
Taasisi ya Mo Dewji imetangaza orodha ya wanafunzi 22 wa elimu ya juu waliopata ufadhili kutoka katika taasisi hiyo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kupitia mpango wa Mo Scholars. Wanafunzi hao ni Neema Charles, Winfrida Mrope, Henritha Rwegasira, Monica Ubushimbali, Suzana Mkindi, Hamisa Selemani, Beatrice Shupa, Phoebe Mwankemwa, Amon Abraham, Venance Makambe na Amos Ntandu. 

Wengine ni Benjamin Mkondya, Ally Mashaka, Amuniri Sebarua, Iddi Mbilinyi, Samwel Ponda, Eram Temu, Busumilo Tumaini, Cosmadeus Mayunga, Amos Kashinje, Kelvin Ernest na Barnaba Barnaba ambao wote ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Akizungumza kuhusu ufadhili huo, Mwanzilishi wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji aliwapongeza washindi kwa kufanikiwa kupata ufadhili huo, lakini akiwataka kujituma ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea katika maisha yao.
Mohammed Dewji akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Mo Dewji (hawapo kwenye picha) katika hafla ya kutangaza washindi wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu (Mo Scholars). Picha zote na Rabi Hume.

“Mmepata ufadhili huu muutumie vizuri, wapo wengi ambao walituma maombi lakini nyie mmefanikiwa kupata ufadhili. Msome kwa bidii na baadae mpate kazi nzuri ambazo zitawasaidia kupata kipato na kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema Dewji. Dewji alisema aliamua kuanza kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.
Mohammed Dewji akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Mo Dewji katika hafla ya kutangaza washindi wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu (Mo Scholars).

Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuona Watanzania wengi wananufaika na mpango huo na amejipanga kuhakikisha kuwa idadi ya wanufaika wa mpango wa ufadhili unaotolewa na taasisi yake unaongezeka kila mwaka.

“Kasi yetu bado ni ndogo sana kulinganisha na ninavyotaka. Wakati tunaanza kutoa ufadhili tuliamua kuanza na wanafunzi 10 lakini mimi nataka tuwape ufadhili Watanzania wengi ikiwezekana tufike hata 100. Kwangu ni jambo jema sana kusaidia Watanzania wenzangu kwa sababu nimezaliwa hapa na nitazikwa hapa sina pengine pa kwenda,” alisema Dewji. 
Mmoja wa wanafunzi ambaye kabla ya kupata ufadhili aliweka tangazo kwenye mtandao wa kijamii kwamba anauza figo yake, Amos Ntandu akielezea histori ya maisha yake hadi alilopata ufadhili wa Taasisi ya Mo Dewji.

Nae mmoja wa wanafunzi ambaye kabla ya kupata ufadhili aliweka tangazo kwenye mtandao wa kijamii kwamba anauza figo yake, Amos Ntandu aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa ufadhili ambao imewapatia kwani baadhi yao waliokuwa wamepoteza matumaini ya kuendelea na masomo, lakini pia kuomba uongozi wa taasisi kuendelea kutoa ufadhili kwa Watanzania ili wapate elimu.

“Mimi nilikuwa tayari kuweka maisha yangu hatarini kwa kutangaza kuuza figo langu, lakini ufadhili huu mliotupatia umebadili maisha yetu. Idadi ya wanafunzi wanaokosa mkopo ni kubwa hivyo nawaomba muwe na moyo wa kuendelea kuwasaidia ili na wao wafikie ndoto zao,” alisema Ntandu.
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza kuhusu mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu (Mo Scholars).
Pamoja na kutangaza washindi hao, pia taasisi hiyo ilitoa zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo 2016/2017 ambao inawafadhili waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka wa kwanza chuoni. Kwa sasa idadi ya wanafunzi ambao wanapata ufadhili kutoka Taasisi ya Mo Dewji imefikia 30, ambapo kati yao wanafunzi 7 ni wa mwaka wa masomo 2016/2017 na wanafunzi 22 mwaka wa masomo 2017/2018.
 Baadhi ya wanufaika wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu (Mo Scholars).
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu waliopata ufadhili kutoka katika taasisi hiyo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kupitia mpango wa Mo Scholars.
 
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji akikabidhi zawadi ya laptop kwa baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu waliopata ufadhili kutoka katika taasisi hiyo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kupitia mpango wa Mo Scholars.

WAHUDUMIENI WANANCHI BILA YA UBAGUZI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati tofauti.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.Alisema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“Watumishi wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”Waziri Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa wananchi.

Pia aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika kama zilivyoelekezwa.Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi. 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa Kata ya Chiungutwa, Wilayani Masasi, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara  Februari 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


NDITIYE: WAISHIO MWAMBAO WA ZIWA KUPATA MAWASILIANO YA UHAKIKA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akizungumza na Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Msese wakisafiri kwa boti ndani ya ziwa hilo kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi kwenye mwambao wa ziwa hilo. Aliyevaa miwani ni Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard  
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akikagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi mkoani Rukwa katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Aliyeshika simu ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo Bwana Reina Lukala
 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mwalimu Julieth Binyula akimuonesha Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard maeneo ambayo hayana mawasiliano wakiwa kwenye bandari ya Kasanga wilayani humo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi mkoani Rukwa 
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akipata taarifa ya mkoa wa Rukwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Joachim L. Wangapo wakati wa ziara ya yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi mkoani humo
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) mkoa wa Rukwa Bwana Peter Kuguru alipowasili wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi mkoani humo
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (akiwa ndani ya gari la kwanza) akitoka kwenye bandari ya Kasanga iliyopo ziwa Tanganyika wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi mkoani Rukwa. Pembeni ni muonekano wa ziwa Tanganyika

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kikazi ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa na Tanganyika katika maeneo ya vijiji mbalimbali viliyopo kwenye mkoa wa Njombe, Mbeya na Rukwa.

Mhandisi Nditiye amefanya ziara hiyo ili kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio kwenye mwambao huo ili kujiridhisha kuhusu uwepo wa huduma hizo ambapo Serikali kupitia Wizara hiyo inaipatia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ruzuku inayoziwezesha kampuni za simu za mkononi kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Nditiye amebaini uwepo wa mawasiliano hafifu kwenye baadhi ya maeneo na mahali pengine hamna mawasiliano yoyote kwa wananchi waishio mwambao wa ziwa Nyasa na Tanganyika. “Nimesafiri kwa boti ndani ya ziwa Nyasa kutoka eneo la Lupingu, Ludewa mkoani Nyasa hadi matema mkoani Mbeya na sasa kwenye bandari hii ya Kabwe mkoani Rukwa, nimeshuhudia mwenyewe ukosefu wa mawasiliano ya uhakika kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa ziwa ambapo lolote likitokea ukiwa ndani ya ziwa huwezi kabisa kuwasiliana,” amesema Mhandisi Nditiye.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua unuhimu wa wananchi kuwasiliana kwa kuwa mawasiliano yanachangia ukuaji wa pato la wananchi na taifa kwa ujumla, yanawezesha na kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa eneo husika. Amesema kuwa tayari Wizara kupitia UCSAF imefanya tathmini ya kufikisha huduma za mawasiliano kwa kuzipatia ruzuku kampuni za simu za mkononi ili ziweze kujenga minara ya simu za mkononi.

Mhandisi Nditiye amefafanua kuwa ukosefu wa mawasiliano haimaanishi uwepo wa minara michache ya simu za mkononi ya kampuni fulani na ukosefu wa mnara wa kampuni mojawapo ya mawasiliano ya simu za mkononi, bali eneo ambapo hamna mnara wa simu za mkononi wa kampuni yoyote ile.

Ameongeza kuwa hadi hivi sasa Serikali imefikisha huduma za mawasiliano vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kiwango cha asilimia 94, na ni maeneo machache tu ambayo yamebaki hayajafikiwa na huduma za mawasiliano.

 “Serikali imejipanga na kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi waliosalia ifikapo mwaka 2020 ambapo wananchi waishio kwenye mwambao wa ziwa Nyasa na Tanganyika wamepewa kipaumbele hicho”, amesema Mhandisi Nditiye. 

Akitoa maelezo yake kwa Mhandisi Nditiye kuhusu mpango huo wa Serikali wa kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio kwenye mwambao, Meneja wa Uendeshaji wa UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa, tayari Mfuko umeyabaini maeneo hayo, kufanya tathmini ya mahitaji ya minara na fedha husika ili kuweza kufikisha huduma za mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo ya wananchi waishio kwenye mwambao wa maziwa hayo. 

“Tumetembea Ludewa kwenye Tarafa ya Mwambao yenye kata nne za Kilondo, Lumbila, Lupingu na Makonde zilizopo mwambao wa ziwa Nyasa na kubaini uwepo wa mawasiliano hafifu na mahali engine hakuna mawasiliano kabisa ambapo Serikali imetenga kiasi cha dola za marekani 252,500 ambazo zitatumika kufikisha mawasiliano”. Amesema Mhandisi Richard.

 Akizungumza na Mhandisi Nditiye kuhusu hali ya mawasiliano na miundombinu mengine kwenye mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere amesema kuwa tayari Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) inaendelea na kazi ya kupita kwenye eneo la mwambao wa ziwa Nyasa ili kuweza kujenga barabara kwa kuwa wananchi waishio eneo hili hawana barabara ya uhakika. 

Pia, amemshukuru Mhandisi Nditiye kwa kufanya ziara hiyo na kuzungumza na wananchi ambapo amewahakikishia kuwa Serikali inakamilisha ujenzi wa meli mpya kwa ajili ya eneo hilo na itajenga minara ya mawasiliano ili kutimiza ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inaayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwatumikia wananchi.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Nditiye akiwa mkoani Rukwa kwenye bandari ya Kabwe na Kasanga na bandari ya Itungi, iliyopo Kyela mkoani Mbeya, amelielekeza Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kufunga mitambo ya mawasiliano kwenye meli mpya ili abiria waweze kuwasiliana wakiwa ndani ya meli kwa kuwa wengine ni wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo ndani na nje ya nchi kupitia maziwa hayo. 

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Bwana Godfrey Kawache amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa kuna ukosefu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo ya kata ya Nguna, Ngonga, Busele, Kajungumele na maeneo ya Kandete na Ibada.

Mhandisi Nditiye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mwalimu Julieth Binyula  na wa Nkasi Bwana Said Mohamed Mtanda wa Mkoa wa Rukwa akiwa katika ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uchukuzi katika maeneo ya mkoani Rukwa. Bwana Mtanda amemuomba Mhandisi Nditiye kuwaelekeza wataalamu wake kushirikiana na Ofisi za Wakuu wa Wilaya kutekeleza majukumu ya Serikali kwa manufaa ya wananchi. 

RC MTAKA: FEDHA ZA WADAU WA AFYA ZILENGE KUJIBU MAHITAJI YA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watendaji katika Sekta ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa Afya mkoani humo katika kikao maalum kilichofanyika kwa lengo la kutathmini mchango wa wadau wa Afya(mashirika mbalimbali yanayofanya kazi na mkoa huo) ambacho kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa na Wilaya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti UKIMWI Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamisi Kulemba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani humo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa na Wilaya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao cha tathmini ya mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), Bi. Christine Mwanukuzi Kwayu akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirikala Cuso International Tanzania, Ndg.Romanus Mtung’e akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao cha tathmini ya mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Mkoa wa Simiyu (CCT), Mchungaji Martine Samson Nketo akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau (mashirika) mbalimbali wa Sekta ya Afya wanaofanya kazi na Mkoa huo mara baada ya kufungua kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.

………………

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wadau na mashirika mbalimbali wanaofanya kazi na Mkoa huo katika sekta ya Afya kuelekeza fedha zao zaidi katika masuala yanayojibu mahitaji ya wananchi wa Mkoa huo kwenye Afya badala ya kujikita zaidi katika kugharamia mafunzo na semina kwa watumishi.

Mtaka ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika Februari 26, Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa fedha za wahisani na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya mkoani Simiyu na matokeo yake katika mahitaji halisi ya Kiafya kwa wananchi.

Mtaka amesema mkoa huo una wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali katika sekta Afya na wanatoa fedha nyingi ambazo zikiwekwa pamoja na fedha zinazotengwa na Serikali kupitia bajeti za Halmashauri zinaweza kujibu mahitaji ya mkoa huo ambayo ni pamoja na upungufu wa zahanati na vituo vya Afya

“ Msingi mkubwa wa kikao hiki ni kutaka tufanye tathmini ya fedha zinazotolewa na wadau ndani ya mkoa wetu, kwa mwaka huu kwenye Halmashauri zetu tumetenga Bilioni 33.4 na tuna shilingi bilioni 11 kutoka kwa wadau kwa ajili ya sekta ya afya, hivi ‘impact’(matokeo) ya hizi bilioni 11 iko wapi? Natamani hapa kila mwenye fedha yake atuambie mwaka huu atafanya nini” alisema Mtaka.

“Nashukuru TAMISEMI mko hapa hili ni la kuliangalia , kama tunaingia mikataba ya shilingi bilioni 11 kwa mwaka na mashirika yanayofanya kazi za Afya ndani ya Mkoa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi, uhamasishaji na semina, wakati tukiwa kwenye mazingira ambayo hatuna hata nusu ya idadi ya zahanati na vituo vya afya vinavyohitajika ni lazima tutafakari wote” alisisitiza Mtaka.

Wakati huo huo Mtaka ametoa wito kwa wataalam wa Afya kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kuzingatia uzazi wa mpango na akasisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wazazi watarajiwa (vijana) ili waanze kufanya maandalizi mapema juu ya maamuzi ya idadi ya watoto watakaoweza kuwahudumia baadaye.

Naye Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema malengo waliyojiwekea katika kikao hicho ni pamoja na kuhakikisha kazi zinazofanywa na wadau wa Afya mkoani humo zinajibu matatizo ya Wanasimiyu na namna ya kuwa na uratibu mzuri wa shughuli zao, mambo ambayo yamepokelewa na wadau hao na kuahidi kuweka uratibu mzuri ili kuimariasha afya za wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirikala Cuso International Tanzania, Ndg.Romanus Mtung’e amesema wadau wa Afya Mkoani humo watashirikiana na Viongozi na Wataalam wa Afya katika kuweka mipango ya baadaye na watazingatia vipaumbele ambavyo vitaleta matokeo chanya yanayoonekana kwa wananchi mkoani humo.

Kikao cha wadau wa Afya na Viongozi Mkoa Simiyu kimewahusisha Viongozi na Wataalam wa Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa Dini pamoja na wadau(mashirika) wa Afya wanaofanya kazi na mkoa wa Simiyu wakiwemo AMREF, AGPAHI, CUAMM, UNFPA, Mkapa Foundation, AMERICARE, PSI,Red Cross, ICAP, TAMA, INTRAHELTH, WORD VISION, BORESHA AFYA, CHAI, MARIESTOPES na BRIDGE2 AID.

MAKAMU WA RAIS AMSAIDIA MKAZI WA SALASALA KITI CHA MAGURUDUMU

$
0
0
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nehemia Mandia (kulia)akizungumza na Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Machimbo ya Zamani Salasala kabla ya kumkabidhi Kiti cha Magurudumu kilichotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Livingstone , Machimbo ya Zamani akikabidhiwa kiti cha magurudumu alichosaidiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Bi. Sidonia Ntibashigwa ambaye pia anafahamika kama Mama Sophia mkazi wa Machimbo ya Zamani, Sala Sala Mbuyuni amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kiti cha magurudumu (wheel chair).Mama Sophia ambaye alipata ya ajali ya kugongwa na roli tarehe 28 Mei, 2016 Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais Siasa Ndugu Nehemia Mandia alisema “Mheshimiwa Makamu wa Rais aliguswa na suala lako ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na ajali kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa ajili ya wewe kufanya shughuli ndogo ndogo unazoweza kufanya”.

Kwa upande wake Mama Sophia alishukuru sana kwa msaada huo wa Kiti na kumuomba Makamu wa Rais aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wake .Alisema kwa sasa bado anaendelea na matibabu kwa sababu mguu wake mmoja bado haujawa na nguvu hivyo hawezi kusimama.

Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne alisema pia bado anahitaji msaada ili aweze kupata matibabu zaidi.

WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO

$
0
0
Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maslahi ya pande zote za Muungano. 

Hayo yameelezwa  na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph Meza.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja,  Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika Muungano.

"Tumejadiliana kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.

"Tumekubaliana pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu," alisema Maj. Gen. Milanzi. 

Alisema katika mkutano huo wa siku moja wataalamu kutoka pande zote za Muungano waliagizwa kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendesha biashara ya mazao ya misitu na kupendekeza utaratibu wa kufanya biashara kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.

Alisema kupitia mkutano huo Wizara hizo zimeunda kamati maalum ya kuratibu utekelezaji wa maazimio ya pamoja ya kuimarisha usimamizi bora wa sekta hizo na utatuzi wa changamoto zilizopo kwa kuandaa mapendekezo ya kimkakati ya muda mfupi na mrefu.

"Kamati hiyo itaongozwa na Afisa Mipango Mkuu Msaidizi kutoka Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka (DFNR), Saleh Kombo Khiari na Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii, Mugure Wambura," alisema Milanzi.

Mbali na hayo alisema kutakuwepo na vikao mbalimbali vya kuimarisha Muungano kupitia Wizara hizo katika ngazi ya wataalamu, Makatibu Wakuu na Mawaziri ambapo kikao kingine kinatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe 30 Machi, 2018.

TIGO NA MILVIK TANZANIA ZACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA GSMA ZA UVUMBUZI WA SIMU ZA MKONONI KATIKA SOKO LINALOCHIPUKIA

$
0
0
Milvik Tanzania na Tigo wamechaguliwa katika tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia katika kundi la Ubora kwa jamii (Social good) katika Tuzo za Simu za Mkononi za GSMA. Tuzo hizi za heshima zinalenga kutambua na kusherehekea mchango uliotolewa katika sekta ya simu za mkononi inayoendelea kubadilika duniani kote.

Tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia zinatambua uvumbuzi halisi katika jitihada za simu za mkononi ambazo zinalenga kutambua mchango unaotolewa na makampuni katika ushirikishaji, upatikanaji na uhai wa masoko yanayochipukia. Uteuzi huo unalenga kutambua juhudi za Milvik na Tigo kwa jamii kwa kuwapatia wateja ambao mwanzo walikuwa wamesahaulika katika huduma za bima ya afya kwa gharama nafuu.

Milvik imeleta gharama ndogo za upatikanaji wa huduma ya bima Afrika kwa masoko yanayochipukia (3% tu) kwa kuunganisha pamoja nguvu ya teknolojia ya simu za mkononi na makampuni ya simu kufungua upatikanaji mpya wa huduma nafuu za mawasiliano, na kuunganisha jamii za pembezoni zilizokuwa zimesahaulika katika huduma muhimu za bima kwa lengo la kuleta ushirikishwaji jumuishi wa kifedha.

Milvik na Tigo wameanzisha mfumo wa kwanza wa kidigitali wa bima katika simu za mkononi kwa kuunganisha mfumo wake wa bima katika simu za mkononi na miundombinu ya teknolojia ya makampuni ya simu, jambo ambalo linawawezesha wateja kujiunga na kulipia bima kupitia simu zao za mkononi.

Nchini Tanzania, Milvik inashirikiana na Tigo kuleta huduma za bei nafuu za bima kwa wateja wa Tigo ambapo wataweza kulipia bima zao kwa kutumia fedha zilizoko katika simu. Ushirika huu wa Tigo/Milvik kwa sasa unatoa moja kati ya huduma kubwa zaidi ya bima ya kulipia kupitia simu za mkononi duniani.

Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, amesema: “ninafuraha kwamba kazi ambayo Tigo na Milvik wamefanya katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha kupitia uvumbuzi huu unaanza kutambulika.
 
 Kwa kuwezesha upatikanaji wa bima kupitia simu za mkononi, wateja ambao kwa kawaida wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kupata huduma za kifedha kupitia taasisi zingine, kwa sasa wataweza kupata ulinzi wa kifedha, wao na familia zao. Tunajisikia furaha kushirikiana na Milvik kutoa bidhaa zenye thamani kubwa za bima kwa wateja wetu pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.”

Tom Chaplin, Meneja wa Milvik Tanzania, kwa upande wake alisema: “Kupitia mfumo wetu wa bima kwa simu za mkononi na ushirika wetu na Tigo, tumeweza kusambaza huduma rahisi ya bima na yenye bei nafuu kwa watu wengi na kuwezesha upatikanaji wa bidhaa za msingi za kifedha.
 
 Kadri ambavyo huduma za simu zinavyozidi kujipenyeza katika masoko yanayochipukia, tunaona fursa nyingi katika kushirikiana na makampuni ya simu na kuwapatia watu zana za kifedha wanazohitaji kuhakikisha mafanikio yajayo ya kiuchumi na familia zao.”

Mshindi wa Tuzo hizo atatangazwa katika Kongamano la Simu za Mkononi Duniani (Mobile World Congress) Barcelona, litakalofanyika kuanzia tarehe 26 Februari mpaka tarehe 1 Machi mwaka huu.

MAAFISA ELIMU KUWENI WABUNIFU NA KUONGEZA WELEDI KAZINI-JAFO

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao kazicha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma leo
 Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula akieleza na kufafanua masuala ya Lishe, Uwajibikaji katika kazi na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala kwamba kila mmoja ana jukumu la msingi katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora kwa Watanzania, kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma leo
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Rais TAMISEMI, pia baadhi ya washiriki wa kikao kazicha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara (waliosimama).
 Pichani Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu,
Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara na Wakurugenzi wa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kinachofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 27 hadi
28 Februari, 2018.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe (kulia) akisikiliza jambo toka kwa Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI (ELIMU), Tixon Nzunda wakati
wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango wa Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara mjini Dodoma.
...........................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amewataka Maofisa Elimu nchini kote kuwa wabunifu kwa kuwapa motisha walimu katika maeneo yao ili wafanye kazi kwa weledi.


Jafo aliyasema hayo alipokua akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi Elimu, Makatibu Tawala wasaidizi wa Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa Hesabu,na Maafisa Elimu Wilaya kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara.


Alisema kila Afisa Elimu aoneshe uthubutu na ajipime utendaji kazi wake hali wakiangalia changamoto katika maeneo yao na kutoa taarifa mapema ili ziweze kutatuliwa.


Alisema kwa mfano mkoa wa Dodoma bado una shida ya elimu kwani bado haufanyi vizuri, hivyo Maafisa Elimu wachunguze na kujua tatizo ni nini.


Aidha, alisema Maafisa Elimu wafanye utafiti kubaini changamoto na kutafutia majibu na Ofisi yake ipo tayari kushirikiaana nao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya vibaya katika sekta hiyo nuhimu.


“Tamisemi ipo tayari kuwasaidi, ila hatutavumilia kama mtafanya vibaya, jukumu lenu kubwa ni kufuata miongozo na kutoa taarifa kwa Viongozi kwani bila kufanya hivyo mtaleta mikanganyiko katika jamii,”alisema


Pia Mhe. Jafo, aliongelea suala la michezo kuwa serikali imeamua kuimarisha michezo katika ngazi zote, kwani michezo na elimu vinaenda sambamba. Watoto wasioshiriki michezo mienendo yao inakua ipo chini hivyo amewaagiza ushiriki wa michezo mashuleni.


Amewaagiza maafisa elimu wasichague wanafunzi ambao sio wawakilishi sahihi wafuate utaratibu wa kuchagua wachezaji kutoka shule zote.


Aliwaagiza Maafisa Elimu wajenge utaratibu wa kujenga uzalendo kwa wanafunzi, wasisitize kuimba nyimbo za kitaifa ili kujenga uzalendo katika nchini.


Katika hatua nyingine, Jafo amewataka Maafisa Elimu kusimamia suala la mazingira mashuleni ili kuunga mkono Kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais ya upandaji miti na kusaidia suala zima la kutunza mazingira.


Amewaasa Washiriki hao kubadili Sekta ya Elimu kwa kuboresha ufaulu hadi kufikia asilimia 80 kama sehemu ya majukumu yao.


Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe aliwataka maofisa hao kuanzia ngazi ya kata hadi mikoa kuacha kuwatesa walimu kwa kuwa wanasababisha wajazane kwenye wizara hiyo kuonana na viongozi.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro aliwasisitiza Maafisa Elimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma pamoja na maadili ya taaaluma zao kwani kumekua na malalamiko mengi juu ya ukandamizwaji wa waalimu nchini.


Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu, amesema kuwabaadhi ya Maafisa Elimu wanashirikiana na baadhi ya walimu kuhujumu vifaa vya maabara mashuleni na kuvipeleka kwenye mashule yao binafsi na kwamba waache tabia hiyo kwani Serikali haitowavumilia.


Dkt. Semakafu amesema Maafisa Elimu waache uonezi kwa walimu pindi wanapotaka kujiendeleza kielimu kwa kuwanyima fursa hiyo kwa kuwasimamishia mishahara yao bila sababu za msingi.


Awali kabla ya ufunguzi wa kikao kazi hicho, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula alielezea na kufafanua namna ya kuboresha masuala ya Lishe katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Uwajibikaji katika kazi kwa washiriki na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala (CCM) kwamba kila mmoja ana jukumu la msingi kwa mujibu wa Ilani hiyo, katika kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora kwa Watanzania na hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na uadilifu kwa maendeleo ya Watanzania.

WASHIRIKA WA MAENDELEO WAAHIDI KUSHIRIKIANA KWA KARIBU ZAIDI NA TANZANIA KULETA MAENDELEO

$
0
0
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa tatu kulia), kushoto kwake ni Mwenyekiti Mwenza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika hao wa Maendeleo Bw. Alvaro Rodriguez, mjini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Bi. Doroth Mwanyika (kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Dkt. Khatibu Kazungu, wakifuatilia kwa makini mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania katika mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, Bw. Dickson Lema (kushoto) akifuatilia mjadala kati ya pande hizo mbili uliolenga kuimarisha zaidi ushirikiano, uliofanyika mjini Dodoma.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika wa Maendeleo nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez, akihutubia mkutano wa kimkakati wa maendeleo kati ya Serikali ya Tanzania na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akihutubia washiriki wa mkutano wa kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika mjini Dodoma ukilenga kuimarisha mahusiano kati ya pande hizo mbili ili kuiwezesha nchi kufikia malengo yake ya maendeleo.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga na Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo wa Canada Bi. Susan Steffen, wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo ili kufanikisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanzibar (MKUZA III)), uliofanyika mjini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi na Somalia, Bi. Bella Bird, nje ya ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna pande hizo mbili zinavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani- USAID Bw. Andy Karas, nje ya ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna Serikali na Washirika wa Maendeleo wanavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuiwezesha nchi kuharakisha maendeleo yake kwa manufaa ya wananchi wake.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango



……………………

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) imekubaliana na Washirika wa Maendeleo kurejesha uhusiano wa karibu na wenye tija ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka Mitano pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanziba (MKUZA III).

Hayo yamebainishwa mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati akifungua mkutano wa Mazungumzo ya kimkakati kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo.

Bw. James amesema kuwa Mwongozo huo wa miaka 7, kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2014/2025, umelenga kuipa Serikali nafasi ya kuongoza mchakato wa maendeleo na kuijengea Serikali uwezo wa kukusanya mapato yake ya ndani, kuchambua fursa muhimu za uwekezaji na kutumia masoko ya kikanda na kimataifa kupata faida.

“Tumekubaliana kwamba tutasimamia mchakato mzima wa maendeleo sisi wenyewe kama nchi, matumizi mazuri ya rasilimali, kuimarisha uwajibikaji, kukuza biashara na uwekezaji wa ndani na nje” alifafanua Bw. James

Amesema kuwa nchi inajivunia hatua kubwa iliyofikiwa kiuchumi na kijamii ambayo Tanzania imefikia, ikiwemo kutambuliwa kimataifa kuwa kinara wa masuala ya ukuaji wa uchumi wa Taifa na uchumi jumuishi, ambapo imekuwa ikifanya vizuri kimataifa, kikanda na katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha Washirika wa Maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani, Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika hao Bw. Alvaro Rodriguez, ameahidi kuwa watashirikiana na Tanzania ili malengo yake ya maendeleo yaweze kufikiwa kwa kuboresha zaidi ushirikiano ambao hapo awali ulianza kulegalega.

Ameelezea kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali zote mbili-Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar katika kufanikisha malengo yake ya kukuza uchumi kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo (FYDPII) na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanzibar (MKUZA III).

Amesema ili mipango hiyo iweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kuishirikisha kikamilifu Sekta Binafsi pamoja na washirika wa maendeleo kwa kuweka mazingira ya kuongeza uzalishaji, kukuza ajira kwa vijana wa kike na wa kiume na hatimaye kufanya mapinduzi ya kiuchumi.

“Vijana takribani milioni moja wanaingia katika soko la ajira kila mwaka, hivyo ni muhimu kuweka mazingira ya upatikanaji wa ajira tena zenye staha katika kipindi hiki ambacho nchi inafanya mapinduzi makubwa ya viwanda na uchumi” alisisitiza Bw. Rodriguez.

Amesema kuwa uwekezaji katika masuala ya elimu, afya, hifadhi ya jamii, kutoa fursa sawa kwa wote (wanaume na wanawake) ni muhimu kwa kuwa jamii yenye afya itashiriki vizuri katika masuala ya uzalishaji.

Ameahidi kuwa Wadau wa Maendeleo wako tayari kusaidia jitihada hizo ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo hayo kwa kuwezesha miundombinu ya ukusanyaji mapato yake ya ndani, usimamizi na matumizi mazuri ya fedha za umma, kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika miradi ya kielelezo pamoja na kusaidia kuibua sera bora na kufadhili miradi yake ya maendeleo.

Serikali na Washirika wa Maendeleo wamekubalina kukutana mara mbili kwa mwaka ambapo kikao kingine kinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2018.

DK. MWANJELWA AMSIFU BINTI MKULIMA WA KITANZANIA ALIYEAJIRI WAFANYAKAZI 26 SHAMBANI

$
0
0
 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Business Company Solutions Ltd, Hadija Jabiri alipotembelea sehemu ya shamba lenye hekari 30 analomiki mkulima huyo linalozalisha Mbogamboga na matunda kwa ajili ya biashara ndani na nje ya Nchi katika kijiji cha Kiwele Mkoani Iringa hivi karibuni.  (Na Robert Okanda Blogs)
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 30 la GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri akiwa na mwenyeji wake mmiliki wake, Hadija Jabiri (wa pili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ukanda wa Kusini wa kukuza Kilimo (SAGCOT), Geoffrey Kirenga na Afisa kilimo wa mkoa wa Iringa Lucy Nyalu.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na Mmiliki wa GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri alipotembelea shamba kitalu cha kampuni hiyo. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto) akishiriki upangaji wa bidhaa za mbogamboga kwenye madajara alipotembelea sehemu ya kufungashia mazao ya GBRI Business Solutions Company Limited. Kushoto ni Mmiliki wa kampuni hiyo, Hadija Jabiri na sehemu ya wafanyakazi. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akimsikiliza mmoja wa wananchi akitoa maoni yake kuhusiana na miundombinu ya jirani na shamba la bidhaa za mbogamboga la kampuni ya 'GBRI Business Solutions Company Limited'.
Wageni na baadhi ya maofisa wa Serikali na SAGCOT wakimsikiliza Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa alipotembelea shamba la GBRI Business Company Solutions Ltd kwenye kijiji cha Kiwele linalomilikiwa na Hadija Jabiri.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akizungumza na wageni na baadhi ya maofisa wa Serikali na SAGCOT alipotembelea shamba la GBRI Business Company Solutions Ltd kwenye kijiji cha Kiwele linalomilikiwa na Hadija Jabiri (kushoto kwake). Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akikagua shamba la mbombamboga la Kampuni hiyo. 
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akikagua mazao ya mbombamboga yakifungashwa.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akikagua mazao ya mbombamboga yaliokwisha fungashwa yakiwa kwenye chumba baridi tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kulia ni Mmiliki wa GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri. 
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akijionea mazao ya mbombamboga yaliokwisha fungashwa yakiwa kwenye chumba baridi tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Pamoja naye (kulia) ni Mmiliki wa GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ukanda wa Kusini wa kukuza Kilimo (SAGCOT), Geoffrey Kirenga ambao ni washauri wakuu wa maswala ya kilimo wa kampuni hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje yaahidi kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akitoa taarifa ya ufunguzi katika kikao cha Wizara na wadau kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Februari 2016.

Lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi ya maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayotarajia kufanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 ambayo yanatarajiwa kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Tanzania (Tanzania day) ambayo husherehekewa tarehe 26 Aprili 2018 siku ya Muungano. Maonesho hayo ni njia mojawapo za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi inayosisitiza katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji. 
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akizungumza. Balozi Chana alieleza kuwa Ofisi za Ubalozi zimejidhatiti kuhakikisha zinasimamia fursa zote za Watanzania hususan masuala ya biashara ili kuweza kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla. 
Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi kuhusiana na maonyesho iliyokuwa ikiwasilishwa na Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Juma Ali Juma, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka. 
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi Mtendaji-Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye na Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Godfrid Muganda. 
Wajumbe kutoka Serikalini na sekta binafsi wakifuatilia kikao. Waliokaa mstari wa kwanza ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na nyuma yake ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia kikao. 

SERIKALI YAOMBWA KUENDELEA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA WANAWAKE NCHINI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu, akihutubia wakati akifungua akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Mtandao, Vicensia Shule akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akihutubia.
 Profesa Bernadeta Killian akitoa mada kuhusu hali halisi ya wanawake na uongozi hapa nchini.
 Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anna Makinda na Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Taswira ya ukumbi kwenye kongamano hilo.


Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya akizungumza na wanahabari

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga bajeti kubwa katika bajeti zake kwa ajili ya kumuendeleza mwanamke wa Tanzania.

Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu wakati akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 jijini Dar es Salaam jana.

"Tunaomba bajeti ya serikali ibadilike kwa kuangalia ajenda ya jinsia ukizingatia changamoto mbalimbali walizonazo wanawake" alisema Dk.Nagu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.Dk. Nagu aliwataka wanawake wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuzijua changamoto walizonazo na kuzitatua kwa msaada wa viongozi wanawake wastaafu.

Aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa na ndio wazalishaji wakubwa wa mali lakini kwa namna moja hama nyingine wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya mali zinazotokana na uzalishaji wao kutumiwa na wanaume wao.

Katika hatua nyingine Dk.Nagu aliomba wake wa maraisi wawe mbele kuwaendeleza wanawake wenzao kama ilivyokuwa kwa Mama Anna Mkapa kupitia taasisi yake ya Wote Sawa na Mama Salma Kikwete kupitia WAMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema wameamua kuandaa kongamano hilo kama sehemu ya kutoa fursa kwa wanawake na wadau wengine kutafakari wapi wamefanikiwa, wapi bado kama kunachangamoto na kupanga mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi pamoja na uongozi.

Alisema kongamano hilo pia litatoa fursa ya kutafakari suala la ushauri, ulezi au ukungwi katika kuimarisha uongozi.Alisema tafiti zinaonesha kuwa nchi za Afrika zinapoteza takribani dola za kimarekani 105 milioni kwa mwaka kwa kutowaingiza wanawake katika uchumi, pia takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni zaidi ya asilimia 70 ya wakulima wadogo ambao ndio wanalisha nchi yetu.

Alisema wanawake walioko katika sekta isiyo rasmi ni asilimia 51.1. ambapo wanaume ni 48.9 na kuwa ni asilimia 20 tu ya wanawake ndio wanamiliki ardhi.Katika kongamano hilo walihudhuria viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wengine ambapo kauli mbiu ilikuwa ni "kusherehekea na kutambua Mchango wa Uongozi wa Wanawake Jukwaani na Nyuma ya Pazia".

Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya amewata wanawake kuwa na moyo wa kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanauwezo wa kuongoza.

Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images