Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MPINA ATOA MAAGIZO YANAYOTAKIWA KUTEKELEZWA NDANI YA WIKI MBILI

0
0
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake akiwa akiwa katika ziara katika kituo cha Taifa cha uzalishaji Mbegu bora za Mifugo kwa njia ya chupa, (NAIC) kilichopo Mjini Arusha.
Katikati Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo akisoma Hotuba katika zoezi la uzinduzi wa madume ya kisasa ya mbegu bora za Ng’ombe katika kituo cha taifa cha uzalishaji mbegu bora kilichopo mjini Arusha, Kushoto ni waziri wa Mfugo na Uvuvu Mhe. Luhaga Mpina, na kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara hiyo, Dkt.Lowlence Asiimwe.
Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia dume bora la kisasa kutoka nchi ya New Zealand katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha (NAIC) Arusha jana alipokuwa katika ziara maalum ya uzinduzi wa Madume hayo.kulia ni Dkt Paul Mollel, Mkurugenzi wa Kituo hicho.
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madume bora ya kisasa kutoka nchi ya South Africa na New Zealand yaliyoletwa nchini kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora za mifugo. Pembeni yake ni katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo na ujumbe wake.


Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepewa wiki mbili kufanya tathmini kuona kama kuna haja ya kuagiza maziwa na mazao yake kutoka nje ya nchi na kama waagizaji wanafuata taratibu na masharti ya kisheria yaliyowekwa na Serikali.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara ya kutembelea kituo cha Taifa za uzalishaji wa mbegu Bora za Mifugo kwa njia ya chupa kilichopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Waziri Mpina pia aliitaka Wizara yake kuandaa mpango kazi utakao wezesha kuzalisha Ng’ombe milioni moja kwa mwaka kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza kusaidia kujenga viwanda vya maziwa na kuweza kumudu soko la ndani na hata kuhudumia bara zima la Afrika na kusaidia kuongeza pato la Taifa.

“Kuna makampuni 43 nchini yanayoingiza maziwa toka nje ya nchi,na makampuni 81 yanayojishughulisha na maziwa na mazao yake,Wizara ifanye tathmini kama kweli tunahitaji kuingiza maziwa hayo. Alisisitiza Mpina.” 

Aliongeza kuwa maziwa mengi yanaingia ndani ya nchi kwa kupitia njia za panya, na kusema kuwa wale wote wanaojishughulisha na biashara hizo wapo hatarini kukamatwa na sheria itachukua mkondo wake. “Mimi na Wizara na yangu tumejipanga kimwili kiroho na kiakili tutawashughulikia wote wanaofanya biashara hizi kimagendo hakuna suluhu kwa yeyote atakaye kamwatwa. Alisisitiza.” 

Sambamba na hilo, Waziri Mpina pia alimpongeza katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo kwa kazi kubwa ya kuhakikisha kuna kuwepo na mbegu za kutosha kwa kuwepo kwa madume bora 26 hadi sasa yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya dozi 3,120,000 kwa mwaka.

Kwa upande wake, Dkt. Mashingo alimshukuru Waziri kwa kutoa maelekezo ambayo yanalenga kuleta mapinduzi ya mifugo na kwamba ameyapokea na yatatekelezwa mara moja kama alivyoagiza.

DC SHINYANGA AFANYA OPARESHENI YA USAFI NA MAZINGIRA,AKAMATA NA KUTOZA FAINI WENYE MITI ILIYOKUFA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendesha oparesheni ya usafi na Mazingira kukagua usafi na miti iliyotelekezwa na kuwawajibisha wananchi ambao miti yao imekufa kwa kulipa faini ya shilingi 50,000/= kwa kila mti na kuwataka wapande miti mingine. 

Mkuu huyo wa wilaya amefanya oparesheni hiyo Februari 24,2018 katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga ambapo kila mwananchi ambaye miti iliyopandwa kwenye eneo lake imekufa aliwajibishwa kwa kufanya uzembe na kusababisha miti ife. 

Katika opareshini hiyo kila mwananchi aliyepigwa faini alikuwa anapatiwa risiti ya malipo na aliyeshindwa kulipa alikuwa anapandishwa kwenye gari la polisi kwa hatua zaidi za kisheria. Akizungumza wakati wa oparesheni hiyo Matiro ambaye alikuwa ameambatana na maafisa mbalimbali na askari polisi alisema hataki kuona miti iliyopandwa kupitia kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa Septemba 23,2017 yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ inakufa kwa uzembe kwani walikubaliana kila mwananchi atunze miti hiyo. 

“Miezi mitano iliyopita tulianzisha kampeni ya upandaji miti wilayani hapa ili kuboresha mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa,tukapanda miti na kumtaka kila mwananchi atunze iliyopo kwenye eneo lake”,alieleza Matiro. “Nimeanza kukagua miti hii ili nione imefikia hatua gani,kama mti uliopo kwenye eneo lako lazima tukuwajibishe,wote tuliokuta miti imekauka tumewapiga faini ya shilingi 50,000/=”,aliongeza. 

Matiro alisema wilaya hiyo imepiga marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=. Afisa Misitu wa Manispaa ya Shinyanga,Emmanuel Nyamwihura alisema wanatoza faini hizo kwa mujibu wa sheria ya Usafi na Mazingira ya Mwaka 2014. 
Mmoja wa wananchi katika kata ya Ibinzamata akijitetea kwa kuonesha dumu la maji alilokuwa analitumia kumwagilia maji mti wake uliokufa.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. Kushoto ni Afisa Misitu wa Manispaa ya Shinyanga,Emmanuel Nyamwihura - Picha zote na Kadama Malunde1 blog 
Wananchi ambao miti iliyopandwa mbele ya makazi au biashara zao imekufa wakipanda kwenye gari la polisi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza mwananchi ambaye miti yake imekua vizuri. 
Mwananchi akionesha mti wake uliokufa kabla ya kulipa faini ya shilingi 50,000/=. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahoji wananchi ambao miti yao imekufa. 
Maafisa walioambatana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakizungumza na mmiliki wa Nyumba ya Kulala wageni ya Masanja Safari Logde ambaye miti iliyokuwa imepandwa mbele ya nyumba hiyo imekufa. 
Kulia ni Mwananchi akitetea kwanini miti aliyopanda imekufa. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwataka wafanyabiashara waliopo karibu na Benki ya NMB Manonga kupanda miti katika eneo lao la biashara. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia sehemu ambayo imepandwa mawe badala ya mti katika eneo la Mnara wa Voda mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiipongeza ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa kukuza miti vizuri mbele ya ofisi hiyo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia mwananchi anavyotoa vijiti vilivyowekwa kwenye mti ambao tayari umestawi vizuri. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi waendesha bodaboda katika eneo la Kambarage wanavyoondoa maganda ya miwa yaliyotapakaa katika eneo hilo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa maagizo kwa mama lishe katika eneo la Kambarage kuondoa uchafu na kuzuia maji machafu katika eneo lake la biashara. 
Wananchi ambao miti yao imekufa wakiwa katika gari la polisi. 
Katikati ni Afisa Misitu wa Manispaa ya Shinyanga,Emmanuel Nyamwihura akiangalia Nyanya iliyopandwa badala ya mti. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwataka wananchi waliokamatwa kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Soma Uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji Miti Shinyanga

MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAJITOKEZA KUJISAJILI KUSHIRIKI Tigo Kili Half Marathon 2018

0
0

Msajili wa mbio za Tigo Kili Half Marathon, Celina Charles (kulia), akimuandikisha, Nicholas Njanga, kutoka nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Machi 4 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kushiriki kupitia namba *149*20#.






Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio za Km 21 za Tigo Kili Half Marathon katika zoezi la usajili linaloendelea siku ya leo na kesho katika  eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.  Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu. 



Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio za Km 21 za Tigo Kili Half Marathon katika zoezi la usajili linaloendelea siku ya leo na kesho katika  eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.  Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu. 

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio za Km 21 za Tigo Kili Half Marathon katika zoezi la usajili linaloendelea siku ya leo na kesho katika  eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.  Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu. 

Add capBaadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio za Km 21 za Tigo Kili Half Marathon katika zoezi la usajili linaloendelea siku ya leo na kesho katika  eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.  Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu. 

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usajili wa Tigo kili half Marathon unaondelea siku ya leo na kesho katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wateja wa Tigo wanaweza kujisajili kupitia namba *149*20# ili kushiriki mbio hizo zitakazofanyika katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi tarehe kupitia 8 Machi mwaka huu. 



Usajili na kuchukua namba za ushiriki wa Tigo Kili Half Marathon 2018 umeanza leo katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Watu wengi wa rika zote wamejitokeza leo kukamilisha usajili wao ili kukimbia mbio hizo za KM 5, Km 21 na KM 42 ambazo zitafanyika katika viwanja vya ushirika Moshi tarehe 8 Machi, 2018. 
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambapo usajili ulikuwa unaendelea, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa wateja wa Tigo wanaweza pia kujisajili kupitia namba *149*20#
 'Kujisajili, piga namba *149*20#   kisha fuata maelekezo rahisi ili ukamilishe usajili na kufanya malipo. Utapata ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaothibitisha muamala wako. Tunza ujumbe huo mfupi na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika vituo vilivyotajwa  ili kuchukua namba yako  ya ushiriki' alisema Woinde.
Vituo, tarehe na maeneo ambapo zoezi la kukamilisha usajili na kupokea namba ya ushiriki ni kama ifuatavyo; 

Dar es Salaam
TAREHE : 24 & 25 Februari - Jumamosi Na Jumapili.
MUDA: Saa Sita mchana hadi saa Kumi na Moja jioni
MAHALI: Mlimani City Mall karibu na Mgahawa wa Grano


Arusha:
TAREHE: 27 & 28 February – Jumanne na Jumatano 
MUDA: Kuanzia saa Nane Mchana hadi saa Mbili usiku.
MAHALI: Kibo Palace Hotel (Mlango wa Nyuma Parking )

Moshi
Tarehe: 01 March -  Alhamisi Saa Sita Mchana hadi saa Moja Usiku
Tarehe 02 March – Ijumaa Saa Nne Asubuhi Hadi saa Moja Usiku
Tarehe 3 March– Jumamosi Saa Tatu asubuhi hadi saa Sita Mchana
Mahali: Keys Hotel. Uru Road

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI,MASONGA WAHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KOSA LA UCHOCHEZI

0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Hukumu hiyo imetolewa leo Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite baada ya kuridhika ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Pia mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miezi sita katibu wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga kwa kosa hilo.

Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha rais Disemba 31, 2017 katika viwanja vya Luanda Nzovwe wakati wakizungumza na wananchi.

MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA

0
0
Miongoni mwa maeneo ya kitalii ambayo hayapewi kipaumbele au kutokuwa maarufu ni pamoja na Kusini mwa Tanzania. Tofauti na vivutio vya kitalii vya kanda ya Kaskazini kuwa maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro, kuna uwezekano mkubwa kwamba Kusini mwa Tanzania kuna hazina kubwa ya vivutio kwa watalii ambavyo havitangazwi au kuvumbuliwa na wengi.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za kitalii kwa ukanda wa Kusini ni pamoja na miundominu hafifu kama vile barabara, viwanja vya ndege ambavyo hupelekea maeneo hayo kufikika kwa ugumu pamoja na upungufu wa malazi kama vile hoteli za kisasa na zinazokidhi vigezo.

Kwa kutambua umuhimu wa ukanda huu, serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya jitihada za makusudi ambazo zitakuwa ni chachu katika kukuza utalii. Jitihada hizo ni pamoja na kuzinduliwa kwa mpango wa uwekezaji katika miundombinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa Kusini mwa Tanzania (REGROW) eneo la Kihesa, Kilolo mkoani Iringa. Mradi huo ulizinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Bi. Samia Suluhu na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala. 
Pamoja na jitihada hizo watalii na watanzania kwa ujumla wanahitaji kujua vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo. Kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu juu ya vivutio mbalimbali nchini Tanzania, Jumia Travel imekukusanyia vivutio na shughuli zifuatazo za kitalii pindi utembeleapo eneo la Kusini mwa Tanzania.
Iringa. Mkoa wa Iringa ni kivutio tosha kutokana na historia yake ndefu tangu enzi za utawala wa kikoloni wa Wajerumani. Ni eneo ambalo Wajerumani walijenga ngome yao kwa ajili ya kupambana na vuguvugu za harakati za kukataa kutawaliwa kutoka kwa kabila la Wahehe ambazo ziliongozwa na Chifu Mkwawa. Mji huu ambao ulijengwa tangu karne ya 19 una mambo mengi ya kujifunza na kujionea pindi utembeleapo ambayo hayapatikani sehemu yoyote nchini. 
Isimila. Mbali na harakati za wazi za kupinga ukoloni wa Wajerumani, eneo la Kusini linasifika kwa kupatikana kwa mabaki ya historia za kale. Eneo hili limegundulika kuwa na masalia ya kutosha ya zana za kale za Zama za Chuma kuliko eneo lolote duniani, ambapo inasemekana ni maeneo ya mwanzo kabisa kuzalisha zana za viwandani na vichwa vya mishale.
Bonde la Kilombero. Ukubwa wa bonde hili ambalo hujaa maji kwa msimu umelifanya kuwa ndilo kubwa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kuna shughuli nyingi za kufanya kama mtalii na mambo kadhaa ya kujifunza pindi utembeleapo eneo hili linalopatikana mkoani Morogoro. Miongoni mwa shughuli za kufurahia ni pamoja na kujionea ndege wa aina mbalimbali wa kuvutia pamoja na shughuli za kijadi za wakazi wa eneo hilo kama vile uvuvi.
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Kama unaishi Dar es Salaam itakuchukua mwendo wa nusu siku kwa gari ili kufika kwenye mbuga hiyo. Ikiwa imezungukwa na safu ya milima, hifadhi hiyo ya taifa inatoa mandhari nzuri ya mawio na machweo. Mikumi ni mahali pazuri kwa kujionea wanyama wa aina mbalimbali wanaoonekana kwa urahisi na ndani ya muda mfupi. Lakini pia ni sehemu ambayo unaweza kuvinjari aina tofauti za ndege.  

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Mbuga hii ni maarufu kwa kujionea wanyama mbalimbali ambao watalii wengi hupendelea kuwaona. Ukiwa kwenye hifadhi hii wanyama kama vile chui, duma, simba na mbwa mwitu ni jambo la kawaida kuwaona. 
Selous. Hii ndiyo hifadhi inayoshikilia rekodi ya ukubwa duniani kama ulikuwa haufahamu. Kutokana na ukubwa huo hutoa fursa ya kuwatazama wanyama kwa utulivu zaidi kwani watalii sio wengi tofauti na ukanda wa Kaskazini. Hifadhi ya mbuga ya Selous ni nyumbani kwa wanyama wakubwa kama vile simba, chui, mbwa mwitu, viboko na makumi ya maelfu ya tembo. 


Milima ya Udzungwa. Hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa ni hifadhi ya misitu ambapo hurusiwa kutembea pekee. Miongoni mwa vivutio ukiwa hapa ni pamoja na kuvinjari matembezi katikati ya msitu wenye miti mirefu yenye urefu wa takribani mita 60 na kujionea maporomoko marefu ya maji yanayotiririka kutoka milimani. Safu ya milima ya Udzungwa ina utajiri wa takribani 40% ya misitu na wanyama wa aina mbalimbali. 


Milima ya Uluguru. Badala ya kufunga safari kwenda mikoa ya Kaskazini unaweza kutembelea safu ya milima ya Uluguru ambayo ipo umbali mchache kutokea mji wa Morogoro. Ikiwa na urefu wa takribani mita 2300, milima hii itakupatia wasaa mzuri wa kuepuka pilikapilika za jiji la Dar es Salaam. Kama kupanda milima hiyo haitoshi, eneo hili pia limepakana na Hifadhi za Taifa za Selous na Mikumi.  
Zipo shughuli nyingi za kufanya na mambo ya kuvutia pindi utembeleapo vivutio vilivyopo eneo la mikoa ya Kusini. Lakini ni karibu zaidi na hivyo kuokoa gharama za usafiri kwani hakuna umbali mrefu. Faida nyingine ni kwamba kutokana na watalii wengi kumininika ukanda wa Kaskazini, maeneo ya Kusini hutoa fursa ya kujionea vivutio vingi zaidi kwa utulivu bila ya kuwa na msongamano mkubwa.

WATUMISHI WA UMMA MSINYANYASE WACHIMBAJI WADOGO – BITEKO

0
0
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na wachimbaji.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri wakiwa kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa machimbo ya dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Katavi.
Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli wanazofanya pamona na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) alipofika kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli wanazofanya pamona na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akiwasilikiza baadhi ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge wakiuliza maswali na kuelezea changamoto mbalimbali ziazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mwenye kipaza sauti) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye machimbo ya Kitunda ya Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora. Biteko alifanya ziara kwenye machimbo hayo ili kujionea shughuli zinazoendelea sambamba na kuzungumza na wachimbaji.

……………….

Serikali imesema itawachukulia hatua za kinidhamu watendaji wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kujipatia kipato kinyume na taratibu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Dhahabu ya Kitunda yaliyopo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora.

Wakielezea changamoto zinazowakabili, wachimbaji wa machimbo hayo kwa nyakati tofauti walimueleza Biteko masikitiko yao juu ya unanyasaji wanayofanyiwa na baadhi ya Maafisa wa Serikali wasiowaaminifu wakiwemo Askari Polisi na Maafisa Madini.

Wachimbaji hao walisema kumekuwepo na tabia ya kushinikizwa kutoa rushwa ama kugawana faida kwa vitisho kuwa watazuiwa kuendelea kufanya shughuli zao kwenye maeneo husika.

“Kuna baadhi ya Maafisa Madini na Askari Polisi wamekuwa wakitulazimisha nao tuwape mgawo wa mawe tunayochimba vinginevyo watafukia maduara yetu,” alisema Alfred Kulwa mmoja wa wachimbaji kwenye machimbo hayo.

Kufuatia malalamiko hayo, Naibu Waziri Biteko alitoa onyo kwa watendaji wenye tabia hiyo kuacha mara moja na alimuagiza Afisa Madini kushirikiana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya husika kuhakikisha wanafuatilia suala hilo na watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“OCD, tendeni haki, hawa wawe salama. Askari atakayebainika ananyanyasa mchimbaji madini achukuliwe hatua za kinidhamu haraka bila kuchelewa,” aliagiza Naibu Waziri Biteko.

Biteko alisema Afisa yeyote anayehitaji kujishughulisha na biashara ya madini aache kazi ili ajikite katika biashara hiyo na sio kutumia cheo chake kuwanyanyasa wachimbaji.

Aliongeza kuwa hairuhusiwi Mtumishi wa Umma kutumia cheo kujinufaisha. “Marufuku watendaji wa Serikali ama wamiliki wa leseni za uchimbaji madini kutumia madaraka yao vibaya. Kama unataka ingia uchimbe mwenyewe. Serikali hii ya Awamu ya Tano inatutaka tuondoe manyanyaso,” alisema Biteko.

Biteko alisema mchimbaji atakayenyanyaswa atoe taarifa Polisi na pia amfahamishe kwa njia ya simu kuhusiana na manyanyaso hayo ambapo alitaja namba zake za simu ili kukitokea hali ya sintofahamu wasisite kumfahamisha.

Hata hivyo, Biteko aliwataka wachimbaji hao kuacha kuwasilisha taarifa za uwongo ikiwemo kusingiziana na mara zote wasimamie haki ili kuepusha migogoro baina yao na Serikali.

MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA MBALI MBALI VYA WALEMAVU KUTOKA SERIKALI YA KUWAIT

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Vifaa vya Walemavu vilivyotolewa na Serikali ya Kuwait ,pichani ni Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al Najem (katikati) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa .
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya vifaa vya walemavu vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem, wengine pichani ni Msaidizi wa Balozi wa Kuwait Bi. Zainab Ally (kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijaribu kusukuma kiti maalum cha magurudumu kwa ajili ya walemavu mara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem (kulia), wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa na Msaidizi wa Balozi wa Kuwait nchini Bi. Zainab Ally.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI NCHINI

0
0
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo .

Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na pia kamati maalum ya wataalam hao imeundwa iili kuufatilia na kusimamia mpango huo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye dhamana ya kuratibu maafa kama ya magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali za kuwakutanisha wataalam hawa ili ni kuweza kuijenga jamii salama ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.

Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa kati ya binadam na. wanyama.

Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.
Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi mjini Morogoro, tarehe 2 Februari, 2018.
Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi.

DK.SHEIN AZUNGUNGUMZA NA MABALOZI WAPYA (WILBROAD SLAA NA ALLY MBOWETO) LEO

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha pia na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa (katikati) na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe.Wilbroad Peter Slaa (katikati) wakati wa mazungumzo yao na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe.Muhidin Ally Mboweto (kushoto) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha na kumuaga Rais baada ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Picha na Ikulu

PLAN INTERNATIONAL,UMOJA WA ULAYA YAWAWEZESHA KIUCHUMI VIJANA 592 WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU KIBAHA

0
0
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Sememani Jafo Kulia wa Meneja wa mradi wa Yee kutoka Shirika lisolokuwa la kiserikali la Plan international Simon Ndembeche wa kushoto wakikagua vifaa mbavyo vimetolewa kwa vijana wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kisrawe katika halfa fupi ya kukabishi vitendea kazi
Diwani wa kata ya Kiluvya Aidan Kitare akizungumza jambo wakati wa sherehe ya kukabiddhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, ambapo wamesomeshwa na kupatiwa vitendea kazi na shirika la Plan International kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na janga la umasikini.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza katika halfa ya kukabidhi vifaa kwa vijana wa kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu, na wengine yatima.
Baadhi ya vijana wanaoishi katika mazingiza magumu katika kata ya Kiluvya Wilayani Kibaha ambao wamewezeshwa kiuchumi na shirika la Plan Innternationala ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasisiki.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU


VICTOR MASANGU, KISARAWE

JUMLA ya vijana wapatao 592 wanaoishi katika mazingira magumu,yatima,na wasichana waliopata mimba katika umri mdogo kutoka katika Wilaya ya Kisarawe Kibaha Mkoani Pwani wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ya ufundi stadi wa aina mbali mbali pamoja na kukabidhiwa vifaa vya kazi kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini ambalo limekuwa likiwakabili.

Vijana hao wamepatiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kuendeshea shughuli za ujarisiamali kupitia mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi ujulikanao kwa jina (YEE) ambao unasimamiwa na Shilika lisilokuwa la kiserikali la Plan Internationala kwa ufadhili wa jumuiya ya umoja wa Ulaya.

Wakizungumza katika halfa fupi ya makabidhiano hayo baadhi ya vijana hao walionufaika na mradi huo akiwemo Magnalena Mwendo na Piusi Charles walisema kwamba msaada huo na mafunzo na vifaa walivyopatiwa vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini ambapo pia wameiomba serikali kuwasaidia kupata mikopo ya fedha mfumo wa maendeleo ya vijana.

“Sisi vijana tumefarijika sana kwa kupata vifaa hivi ambavyo kwa kweli vitaweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondoka na janga la umasikini kwani hapa awali tulikuwa tunaishi katika mazingira magumu hivyo kwa upande wetu tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa shirika la Plan international pamoja na Umoja wa ulaya amnbao ndio wamefadhuli mradi huu wa kuwawezesha vijana kiuchumi hasa sisi tuliokuwa katika hali dumu,”walisema.

Pia vijana hao walisema katika kufanikisha malengo ambayo wamejiwekea katika kufanya shighuli zao za ujasiriamali waliiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kwamba inawasaidia katika kuwapatia mikopo na mitaji ambayo itaweza kuwaletea tija zaidi katika kukuza biashara zao na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Kwa upande wake Meneja ya mradi (YEE) wa kuwawezesha vijana kutoka Plan International Simon Ndembeche alisema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu una lengaa kuwasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweza kupata mafunzo ya kujifunza stadi mbali mbali ambazo zitawasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo aliagiza halmashauri kuhakikisha fedha zote ambazo zinapatikana kupitia mapato ya ndani ziweze kuwanufaisha makundi ya vijana na wakinamama kwa lengo kuweza kuwasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali ili kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi.

Jafo alisema kwamba mikakati ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawawezesha vijana na wakinamama katika suala zima la kiuchumi hivyo ili kuweza kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na wimbi la umasiniki.

MRADI huo ambao wa miaka mitatu umeanza kutekelezwa manamo mwaka 2015-2018 unasimamiwa na Shilika la Plan International kwa udadhili wa Umoja wa Ulaya umeweza kuwanufaisha vijana hao 592 ambao wameweza kupata fursa ya kufundishwa fani mbali mbali kutoka VETA, ikiwemo mapishi,mapambo, ushonaji, umeme wa majumbani,ufundi magari, pamoja na uchomeleaji vyuma,iseremala, pamoja na uedreva wa magari

Tigo Yamwaga Smatifoni Kwa Washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

0
0
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Rajabu Saidi Yote (kulia), ambaye ni mkaazi wa Tandika Dar es Salaam,  akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo.
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Tinna Sharon Masatu (kulia), ambaye ni mkaazi wa Mbezi Beach akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo. 


Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Margareth Martin Hiza (kulia), ambaye ni mkaazi wa Ubungo, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. 



Add caMshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea  Nyaka Nyaka Bonus, Daniel Joseph Swai  (kulia), ambaye ni mkaazi wa Iala, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo.  



Baadhi ya washindi zaidi ya 84 waliojinyakulia simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kati) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi. Jumla ya washindi 156 wa simu tayari wamepatikana katika promosheni hiyo ambapo zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa.  


  • Wateja 156 wa Tigo wajinyakulia smartphone za TECNO R6 4G

  • Zaidi ya simu 900 na bonasi za internet bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Februari 26, 2018 –‘Kwa sasa mama yangu anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi kuwasiliana kikamilifu kwa njia ya mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia picha za wajukuu wake. Ndio maana  nitampa zawadi ya simu hii mpya niliyoshinda kutoka Tigo leo ili iturahisishie mawasiliano yetu na kumfanya awe sehemu ya ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni maneno ya Margareth Martin Hiza, mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka moja wa washindi wa simu mpya za kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 4G katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo Tanzania.

Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwaya *147*00#.

Akikabidhi zawadi kwa washindi wa wiki hii, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna zaidi ya simu 900 aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G ambazo zinashindaniwa na wateja watakaonunua vifurushi vya intaneti vya kuanzia TSH 1,000 kupiita menu *147*00#.

‘Washindi wetu wote 156 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi ya 900 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Woinde alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.




MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifukuzia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk.William Morris raia wa Marekani dhidi ya mke wake Dk.Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira kwa garama.

Dk.William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo, akiomba, mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.Katika Maombi hayo Dk. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba Mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA.

Lengo ni kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.Katika madai yake, Dkt. Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).

Mapema mahakamani hapo,akisoma hukumu hiyo leo February 26 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk.Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Dk. Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.Hivyo mahakama imeifukuzia mbali kesi hiyo ya madai na kueleza mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

"Si tu ameshindwa moja kwa moja lakini ameshindwa kiasi ambacho Mahakama hii inalazimika kutoa amri kuwa alipe garama walizotumia wadaiwa kwenye shauri hili" amesoma Hakimu Simba.Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili wa mdai, Respicius Ishengoma amesema hawajaridhika na uamuzi huo na watakata rufaa.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini imesomwa leo nyakati za saa 8 mchana.Awali kwenye utetezi wa Dk.Phills Nyimbi aliieleza Mahakama hiyo hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.

Akiongozwa na Wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk. William Morris, Dk.Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh.bilioni 7.5 anazodai kwa sababu yeye hakuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira.

Dk.Nyimbi kupitia Wakili wake Swai aliomba Dk.Morris asilipwe kiasi hicho cha fedha kwa sababu yeye hajawahi kuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira na kwamba hicho anachokidai si madai halali.

Wakili Swai alimuuliza Dk.Nyimbi anasemaje kuhusu madai ya mumewe Dk.Morris, kuwa wewe na yeye mkapimwe HIV.Dk Nyimbi alidai yeye mwenyewe huwa ana utaratibu wa kupima na kwa bahati nzuri sheria za Tanzania zinaruhusu.

Swai alimueleza Dk.Phillips kuwa mumewe Dk.Morris anataka mtoto wake akapime vinasaba (DNA).Dk Phillips alidai mtoto huyo ni wa kwake yeye, Dk.Phillis na hajasema ni wa Dk.Morris wala wa Mchungaji Mwingira.Pia ameiomba Mahakama iamiru gharama za kesi zilipwe na Dk Morris.

Dk Nyimbi alisisitiza kukana kuzaa na Mchungaji Mwingira na kwamba Mchungaji huyo wala hajawahi kuujua mwili wake.Dk.Nyimbi alitoa utetezi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhini.

Alidai kuwa alifunga ndoa na Dk.Morris mwaka 2001 katika Kanisa la Mtakatifu Albano.Alieleza baada ya ndoa walikaa mapumziko kwa siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili ambako alikuwa anaishi katika chumba kimoja akiwa katika mafunzo ya vitendo.

Alidai kuwa baada ya miezi mitatu Dk.Morris alikwenda Marekani na mawasiliano kati yao yalikuwa ya shida shida.Alidai kutokana na hali hiyo alichanganyikiwa kwa kuwa madaktari wenzake walikuwa wakimuuliza anaondoka lini na kwamba alikuwa akilia tu.

Alidai alijaribu kwenda katika Ubalozi wa Marekani mara mbili kutafuta hati ya kusafiria lakini ilishindikana, hivyo akaamua kuendelea kusoma ili asije akakosa vyote.Alidai Dk.Morris baada ya miaka minane alikuja Tanzania Aprili 25, mwaka 2009 baada ya kupata taarifa anakuja alikwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa KIA.

Alidai baada ya kumpokea walilala katika hoteli iliyopo Moshi ambapo usiku huo alimuelezea historia ya maisha yake, kwa muda mrefu, aliomuacha.Alimueleza kuwa anamaisha yake na amezaa mtoto ambaye ana umri wa mwaka mmoja. Alimueleza alimuoa akiwa na miaka 30 hivyo amezaa akiwa na miaka 38.

Alidai alimueleza alimsukuma kitandani. Alieleza Dk Nyimbi.Dk Nyimbi alidai waliporudi nyumbani kwao Kibaha mkoani Pwani alimwambia kwamba mtoto huyo wa kiume kazaa na mfanyabiashara ambaye yuko nje ya nchi anaitwa Baraka.

Alidai Dk.Morris alisema ana kuna ili mtoto huyo atakuwa wake kwa sababu anampenda mkewe lakini siku zilivyokuwa zikienda mumewe alimwambia kwamba mtoto huyo kazaa na Nabii Mwingira."Aliniambia naitwa Polisi Kibaha nikatoe maelezo kuhusiana na mtoto, nilikataa, nikapigiwa simu na Polisi Kibaha ndipo nilipoamua kwenda, niliambiwa kwamba mu

mewe wangu kalalamika kuwa nimebakwa na Nabii Mwingira na nimezaa naye mtoto." Alieleza Dk. Nyimbi.Alidai alipoulizwa na Polisi alikataa hakuna jambo kama hilo na hajawahi kubakwa wala kuzaa na Mchungaji Mwingira.

Kwa upande wa Mchungaji Mwingira naye alikana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Dk.Phills.Katika kesi hiyo, Dk.Morris ambaye ni raia wa Marekani pamoja na mambo mengine anaiomba Mahakama hiyo imuamuru Mwingira kulipa Sh 7.5 bilioni kama fidia ya kuzini na kuwa na mahusiano na mke wake huyo.

Pia anaomba itoe amari ya kwenda kupima Ukimwi kwa yeye, Mchungaji Mwingira na mkewe Phillis na ifanyike kipimo cha DNA kati ya mtoto na walalamikiwa hao.Inadaiwa Mwingira na Phillis waliingia katika mahusiano muda usiojulikana bila ya kujali kuwa Phills alikuwa ni mke wa Morris na kwamba mara baada ya Morris kufanya uchunguzi juu ya mahusiano hayo mke wake alidai kwamba yeye alibakwa na Mchungaji Mwingira.

Iliendelea kudaiwa kuwa kubakwa huko kulipelekea siyo tu mke wake kuwa na ujauzito pia kulisababisha kuwa na matatizo ya afya.Desemba 28,mwaka 2011 Morris na Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati wa mahusiano yao, Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.

Na kubahatika kupata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 9.Mlalamikaji huyo anadai alitoa taarifa katika kituo cha polisi Kibamba ambapo walimueleza suala hilo ni la uzinzi ama udhalilishaji na haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa kufungua kesi ya madai.

Kitendo cha mke wake kuwa na mahusiano na Mwingira ni kwenda kinyume na ndoa yao halali na kwamba kitendo hicho kimeharibu mipango yake ya mbele kiasi cha kumfanya apoteze hata matumaini ya kuendelea kuishi.

Pia kimemuaibisha na kushusha hadi yake siyo tu Tanzania na Duniani hivyo  kumsababisha ateseke kiakili na kiuchumi.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MTWARA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo la wazazi katika kituo cha afya Chiwale, Wilayani Masasi, akiwa ameanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wodi ya wazazi katika kituo cha afya Chiwale, mara baada ya kuweka jiwe la msingi kituoni hapo, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa Chiwale, Wilayani Masasi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wazazi katika kituo cha afya Chiwale. Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR NA BAADAYE AKUTANA NA MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan alipofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika yeye na Mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria walipofika kuaga rasmi. Kati kati yao ni Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria Muhidin Ali Mboweto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ali Mboweto Kushoto na Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Dr. SlaaKulia na Balozi Seif Kulia wakifanyiana mzaha walipokuwa wakikumbushana utumishi wao wakati walipokuwa Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya M,uungano wa Tanzania mara baada ya mazungumzo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kulipa ushirikiano wa kina Jeshi la Polisi Nchini katika kuona Amani ya Taifa pamona na Raia wake inaendelea kudumu muda wote.

Alisema Zanzibar ina changamoto nyingi zikiwemo za Kisiasa, Dawa za Kulevya na ukosefu wa Maadili unaopelekea kuibuka kwa kasi zaidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia ambazo zinahitaji kushughulikiwa ipasavyo ili kuleta ustawi na Utulivu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan aliyefika kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli hivi karibuni.

Balozi Seif alisema masuala ya udhalilishaji pamoja na Dawa za kulevya hivi sasa yamekithiri na kuleta sura mbaya ndani ya Jamii kiasi cha kulazimika kutungwa sheria ili kujaribu kupambana na kadhia hiyo inayotoa picha mbaya katika uso wa Dunia.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliviagiza vyombo vya Dola kuwasaka na baadae kuwashughulikia ipasavyo wale wote wanaohusika na uingizaji wa Dawa za Kulevya Nchini kwa vile wao ndio chanzo cha balaa zote zinazotokea katika Mitaa mbali mbali Nchini.

Hata hivyo Balozi Seif alikemea tabia ya baadhi ya Maofisa wa Vyombo vya Dola kujaribu kufifilisha kesi za Dawa za kulevya kwa kuwapa afuweni Watuhumiwa huku wakizingatia zaidi kupokea Rushwa badala ya kuwaonea huruma wale wanaoathirika kutokana na wimbi la Dawa hizo.

Alifahamisha kwamba tabia hii hupelekea mwenye hatia kuachwa huru na hatimae kuonekana kudunda Mitaani kifua mbele huku akianza majisifu na kutia hofu Wananchi wanaomuelewa madhambi yake.

Akigusia suala la Kisiasa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Kamishna Mpya huyo wa Polisi Zanzibar kwamba ni vyema vyombo vya Dola kwa kushirikiana na Wananchi wema wakaelewa kwamba vurugu na Fujo si jambo la kupewa nafasi.

Balozi Seif alisema Zanzibar licha ya kipindi cha Kampeni za Uchaguzi inahitaji kuendelea kubakia kuwa ya amani muda wote ili Raia wake wafanye shughuli zao za kujitafutia riziki bila ya vikwazo vyovyote.

Alimpongeza Kamishna wa Polisi wa Zanzibar kwa wadhifa aliopewa na Taifa ambao anastahiki kuusimamia katika misingi ya Maadili na nidhamu ili lengo la kupewa nafasi hiyo likamilike ipasavyo.

Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan alisema suala la Amani ndio kazi kubwa na ya msingi atakayohakikisha anaisimamia kwa nguvu zake zote kwa kushirikiana na Viongozi na askari wenzake ili kutoa fursa kwa Wananchi waendeshe maisha yao kama kawaida.

Kamishna Mohamed alisema changamoto zilizopo pamoja na udhaifu wa baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi hilo unaweza kuondoka au kupungua kwa kiasi kikubwa kama nguvu za ushirikiano zitapewa nafasi pana zaidi kwa pande zote husika.

Aliiomba Serikali licha ya uchumi duni lakini bado upo umuhimu wa kufikiria kununua mashine za kisasa za uchunguzi wa Dawa za Kuelevya hasa katika maeneo ya Uwanja wa Ndege na Bandarini.

Kamishna Mohamed alisisitiza kwamba katika jitihada za kukabiliana na wimbi la uingizaji, uuzaji na utumiaji wa Dawa za kulevya ipo haja ya Wananchi kuendelea kulipa ushirikiano wa karibu zaidi Jeshi la Polisi katika mbinu za kuvurugu soko la uuzaji wa Bidhaa hiyo haramu.

Hata hivyo Kamishna Mohamed Haji Hassan alieleza kwamba Viongozi wa Dini bado wana nafasi ya kuwaelimisha Waumini wao hasa Vijana kujiepusha na wimbi hilo la Dawa za Kulevya kwa kutumia Kongamano, semina pamoja na Hotuba.

Alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba makosa mengi yanatokea na kuripotiwa lakini ikichunguza kwa undani inatokana na Watu kukosa Doria za Kiimani.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo na Mabalozi Muhidin Ali Mboweto anayeiwakilisha Tanzania Nchini Nigeria na Dr. Wilbrod Slaa anayekwenda Nchini Sweeden walipofika Ofisini kwake kumuaga rasmi wakielekea katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa.

Katika mazungumzo yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mabalozi hao kwamba nafasi ya Ubalozi ni fursa nzito ya Uwakilishi wa Nchi inayopaswa kutumikiwa kwa uzalendo wa hali ya juu.

Balozi Seif aliwaeleza Mabalozi hao wa Tanzania kwamba Nigeria na Sweeden ni Nchi zenye Historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania inayopaswa wasimamizi hao wa Diplomasia kuangalia maeneo ambayo yanaweza kuendelea kudumisha Uhusiano huo.

Alisema zipo sekta ambazo Nigeria na Sweeden zinaweza kuisaidia Zanzibar Kitaaluma akitolea Mfano eneo la Utalii, Umeme Mbadala na hata masuala ya Uhifadhi wa Nyaraka kwa vile Mataifa hayo tayari yameshapiga hatua kubwa Kitaaluma.

Mapema Balozi wa Tananzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa kwa niaba ya mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria alisema wanajitambua kwamba wao ni Wawakilishi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dr. Slaa alimueleza Balozi Seif kwamba utumishi wao wa Kidiplomasia watauelekeza zaidi katika Diplomasia ya Kiuchumi kama Dunia ilivyobadilika kujikiota zaidi katika eneo hilo.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/2/2018.

ALIYEKUWA MGOMBEA UDIWANI KATA YA MPINGA AHAMIA CCM

0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno akizungumza alipotembelea kata ya Mapinga ,wilaya ya Bagamoyo wakati wa muendelezo wa ziara yake anayoendelea nayo mkoani hapo kushukuru kuchaguliwa nafasi hiyo.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,(hayupo pichani) wakati alipokuwa amefanya ziara yake ya kushukuru wilayani humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Mapinga kupitia ACT Wazalendo uchaguzi mkuu uliopita ,Tabia Juma akiongea baada ya kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno aliyoifanya wilayani Bagamoyo,pamoja na hilo uongozi mzima wa ACT kwenye kata hiyo ulihamia CCM.

IGP SIRRO AWATAKA ASKARI KUTENDA HAKI KWA WANANCHI WANAOWAHUDUMIA BARIADI, SIMIYU

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (wapili kushoto), akikagua baadhi ya vielelezo katika kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari mkoani humo, IGP Sirro amewataka askari kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima kutoka kwa askari wa kikosi maalum cha Jeshi hilo wakati alipowasili Bariadi mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi IGP Sirro pia aliwataka askari kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuzungumza na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo (hawapo pichani), kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Antony Mtaka. Picha na Jeshi la Polisi.

MAVUNDE AAGIZA WAAJIRI MWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF)

0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameagiza Wakurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya JASCO LTD,AIRCO na JB BELLMONT HOTEL kufikishwa Mahakamani kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jennister Mhagama ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo 30.09.2017.

Katika Mkoa wa Mwanza, Mavunde amesema jumla ya waajiri takribani 700 hawajajisajili katika mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi ambapo zoezi la msako wa waajiri hao litaendelea kwa wiki nzima na kuwachukulia hatua stahiki wale waajiri wote wataokuwa hawatii matakwa ya sheria ya Fidia ya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) Mwajiri yoyote atakayeshindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh.50,000,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Pamoja na hayo, Mavunde amemuagiza Afisa Kazi Mfawidhi wa Mwanza kuwapa waajiri hao Amri tekelezi ya siku 30 kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 kwa kuwapa Wafanyakazi wao mikataba,malipo ya mshahara kwa kima cha chini cha sekta husika na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi wa viwango vya kazi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika ukaguzi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye ziara yake mkoani Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la Mhe.Waziri Jenister Mhagama.
 

KUTOKA JESHI LA POLISI DAR: MWANAUME NA MWANAMKE WASHIKILIWA TUHUMA YA MAUAJI KADA WA CHADEMA DAR

0
0

*Polisi yaendelea kuchunguza kifo cha Akwilina,waua majambazi  Dar

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mwanamke mmoja na mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya kada wa Chadema  Daniel John  aliyekutwa amekufa maeneo ya Coco Beach jijini.

Akizungumza leo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kutokana na uchunguzi unaendelea kuhusu mauaji hayo huko maeneo ya Hananasifu Kinondoni wamefanikiwa kuwakamata  watu wawili.

Amesema majina ya watu hao yamehifadhiwa kwa lengo la kutoharibu uchunguzi unaoendelea kuhusu tukio hilo la mauaji ya kada huyo wa Chadema.

UCHUNGUZI KIFO CHA AKWILINA WAENDELEA

Wakati huohuo, Kamanda Mambosasa amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usafirishaji Akwilina Akwiline aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

Mambosasa amesema bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo ambalo limegusa hisia za watu wengi na baada ya kukamilisha uchunguzi wao watatoa taarifa kwa umma ili ujue.

WAKAMATA SILAHA TANO, RISASI 35

Pia Mambosasa amesema Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa takriban wiki mbili sasa wamekuwa wakifanya operesheni ya kukamata wahalifu wanaojihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini.

Amesema maeneo ya Pugu  alikamatwa mtu mmoja aitwaye Peter Kwema a.k.a Babu na alipohojiwa alikiri kujihusisha na matukio ya ujambazi katika mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Arusha,Tanga na Kilimanjaro.Pia ametaja baadhi ya wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao.

"Baada ya kumhoji alikubali kwenda kutuonesha ambako wenzake wapo lakini baadae aliamua kupiga kelele kuwashutua kwa lengo la polisi washambuliwe ili yeye atoroke.

"Majambazi hao walianza kurushia risasi askari na ndipo yakaanza majibizano na hatimaye Polisi kufanikiwa kuua majambazi wawili.Pia tumekamata silaha  mbili ambazo ni SMG moja iliyokuwa na risasi saba na bastola mbili aina ya Saurus mmoja iliyokuwa na risasi tatu,"amesema Mambosasa.

Amesema jambazi Kweka yeye alipigwa risasi ambazo zilimjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake wakati akijaribu kutoroka chini ya ulinzi wa Polisi na hatimaye akafariki dunia.

Pia Februari 16 mwaka huu,Polisi walipata taarifa za kiitelejensia huko maeneo ya Chanika kuna kundi la wahalifu limepanga kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha. Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji.

Amesema saa tano usiku wakiwa njiani kuelekea maeneo ya Chanika Homboza kuelekea eneo la kufuatilia wahalifu hao walikutana na kundi la watu sita na waliposimamishwa walikaidi amri  na kuanza kufyatua risasi kwa askari.

Amesema askari walijibu mashambulizi  na hatimaye kuwazidi nguvu  na kusababisha majeraha kwa majambazi huku wengine wakikimbia.

Majambazi hao walipopekuliwa mmoja alikutwa na SMG iliyofutwa namba ikiwa na risasi 28 ndani ya magazini na mwingine akiwa na Bastola aina ya Browning yenye namba Tz Car 103143 ikiwa na risasi 9 ndani ya magazini.

DK. KIGWANGALLA ATOA MIEZI TISA KWA WANANCHI KULIPWA FIDIA WAPISHE HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE NA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO

0
0

Na Hamza Temba-WMU-Manyara

........................................................................

Serikali italipa fidia na vifuta jasho kwa vitongoji ambavyo vipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero ili viweze kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.


Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Kimotorok katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambao ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Simanjiro, Kiteto na Kondoa.


Alisema fidia hiyo italipwa kwa vitongoji viwili vya kijiji cha Irkishbo vya Maasasi na Lumbenek  vilivyopo katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ambavyo vilikutwa ndani ya Pori la Akiba Mkungunero wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 1996 kwa Tangazo la Serikali Na. 307.


"Tutafanya tathmini, tutawaomba wananchi mshirikiane na Serikali ili muweze kulipwa fidia mpelekwe maeneo mengine, jukumu letu sisi ni kugharamia zoezi la tathmini na kulipwa fidia ili muweze kuondoka katika maeneo haya ya hifadhi," alisema Dk. Kigwangalla.


Alisema kwa upande wa baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kimotorok ambao wameanzisha makazi kimakosa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero hawatalipwa fidia na badala yake watafanyiwa tathmini na kulipwa kifuta jasho na kupelekwa maeneo mengine.


"Kimsingi ukimkuta mtu yupo katika eneo lako hupaswi kulipa fidia, hapa tumekuwa waungwana na kutumia roho ya kibinadamu, vinginevyo tungeweza kusema leo hapa tusione mtu na tungevunja kwa sababu ni eneo halali la hifadhi na hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria mtu kuishi ndani ya hifadhi.


"Kwa sasa hatutatumia nguvu, lakini tukikamilisha zoezi la tathmini tukalipa watu fidia yao, tutatoa muda maalum wa watu kuondoka na watu watapaswa kuondoka, ilimradi tutajiridhisha kwamba tulimtendea haki kila mwananchi anayeishi katika eneo hili," alisema Dk. Kigwangalla.


Akizungumzia moja ya zahanati iliyojengwa ndani ya kitongoji hicho cha Kimotorok ambayo nayo itabomolewa baada ya zoezi la kulipa vifuta jasho, aliiagiza TANAPA kujenga zahanati nyingine katika eneo jipya litakalopangwa Halmashauri husika kwa ajili ya wananchi hao kuhamia.


Alisema zoezi la tathmini pamoja na wananchi kulipwa fidia na vifuta jasho linatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi tisa ijayo kuanzia mwezi Machi, 2018. 


Akizungumzia hatma ya makazi mapya kwa wananchi watakaondolewa kwenye maeneo hayo ya hifadhi, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmashauri husika za Kiteto, Kondoa na Simanjiro kupanga maeneo mengine mbadala ya kuwahamishia wananchi hao punde baada ya kulipwa fidia zao.


Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa linalosimamia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori inayosimamia Pori la Akiba Mkungunero kusaidia jamii jirani na maeneo hayo ya hifadhi kwa kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi, kuendeleza eneo la malisho na kuchimba mabwawa ya maji ya kunywesha mifugo ili kujenga misingi ya urafiki na ujirani mwema.


Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla amefuta mipaka ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makame ambayo imeingia kimakosa ndani ya Pori la Akiba Mkungunero na kumuagiza Meneja wa Pori hilo, Emmanuel Bilaso kuweka ulinzi mkali katika eneo hilo.


Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula alisema watasimamia utekelezaji wa maagizo hayo ya Serikali ili kuhakikisha mgogoro huo wa muda mrefu unapatiwa ufumbuzi. 


Katika ziara hiyo ya siku moja Mkoani Manyara, Waziri Kigwangalla alitembelea na kukagua eneo la Ranchi ya Manyara ambayo pia ni sehemu ya mapito ya wanyamapori,  eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge, Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Pori la Akiba Mkungunero ambapo alitoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha maeneo hayo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara. 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na viongozi wa hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho kukakua maeneo ya mapito ya wanayamapori na mipaka ya hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi mkoani Manyara jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makuta wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua changamoto za uhifadhi katika Kijiji cha Kimotorok mkoani Manyara jana. Wanaoshuhudia kushoto Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa.

WATANZANIA KUPENYA SOKO LA KENYA

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akifafanua jambo kwa washiriki wa kikao cha kujadili maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kuia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dk. Pindi Chana na katikati ni Mtendaji Mkuu wa TANTRADE Edwin Rutageruka.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kujadili maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa - MAELEZO

Jonas Kamaleki- MAELEZO.

Serikali imetoa wito kwa  wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa zao katika soko la Kenya ili kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda wakati wa kikao cha Maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya.

Prof. Mkenda alisema kuwa ni nia ya Serikali kuhakikisha watanzania wanapenya katika masoko ya kimataifa ili kuongeza pato la mtu binafsi na la Taifa kwa ujumla.“Hali ya biashara kwa sasa ni nzuri sana, hivyo vikwazo visiwepo kabisa kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”, alsiema Prof. Mwaikenda.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kuwa watanzania inabidi wathubutu na kuingia katika soko la Afrika Mashariki hususan soko la Kenya.Amesema kuwa wafanyabiashara wa Kitanzania wasiogope kuingia katika masoko ya nje ya nchi, wajitahidi ili waweze kuongeza vipato kutokana na ukubwa wa soko lililopo nchini na Kenya kwa ujumla.

“Mkifanya biashara Kenya mtaongeza mitaji, ajira na kipato kwa ujumla kwani nchi hizi mbili zina zaidi ya watu milioni 90”, na hii inaendana na falsafa ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya Uchumi wa Viwanda, hivyo hatuna budi kufuata maono ya Kiongozi wetu na kutengeneza na kuuza bidhaa za viwandani nje ya nchi”, alisema Balozi Pindi Chana.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Juma Ali Juma amesema wazo la kufungua soko la Kenya ni zuri na kumpongeza Balozi Pindi Chana kwa ubunifu huo.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa zipo changamoto ndogo ndogo katika masoko lakini zinafanyiwa kazi ili kuhakikisha biashara kati ya Tanzania na Kenya inaenda vizuri.Bwana Juma alisisitza kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini inabidi ziwe na ubora na kuwa na vifungashio bora ili kumvutia mteja kununua.

Naye  Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE), Edwin Rutageruka amesema watanzania waende Kenya wakijiamini kwani bidhaa zao zinahitajika sana.Aliwataka wafanyabiashara kujenga maghala mipakani ili kutunza bidhaa zao humo na kuziuza kwa bei nzuri wakati muafaka.

Akichangia mada katika kikao cha maandalizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye aliwaomba seka binafsi wajitokeze ili kupeleka bidhaa zao nchini Kenya na kuitumia hiyo fursa katika kukuza biashara zao.

Simbeye aliiomba Serikali kuwapeleka waambata wa kibiashara kwenye balozi za Tanzania Duniani ili washughulikie suala la masoko na fursa nyingine za kibiashara.Kikao hiki cha maandalizi kimetokana na maono ya Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana ambaye amebuni wazo la kufanya wiki ya Tanzania nchini Kenya kwa ajili ya kutafuta soko la bidhaa za Tanzania ambayo itafanyika 26 Aprili, 2018 na itadumu kwa wiki moja.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images