Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1518 | 1519 | (Page 1520) | 1521 | 1522 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Dk. Ali Mohamed Shein pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo hicho yaliofanyika katika ukumbi mpya wa SUZA wa Dk Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu).

  BAADHI ya Wakufunzi na Wahitimu wa Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) (Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili Salma Omar Hamad, wakati wa hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA) jumla ya wahitimu watano wametunukiwa Shadaha hiyo.
  WAHITIMU wa Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakati akihutubia na kutowa nasaha zake kwa wahitimu wa mahafali ya 13 ya SUZA.
  WAHITAJI wa Stashahada ya Utibabu wakila kiapo baada ya kutunukiwa stashahada katika hafla ya Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,Tunguu yaliofanyika katika ukumbi mpya wa Dk. Ali Mohamed Shein,Tunguu Zanzibar.
  WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Kiswahili wakitunukiwa shahada yao wakati wa mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA, wakati wa mahafali hayo yaliofanyika katika ukumbi mpya wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu Zanzibar.
  BAADHI ya Waalikwa katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA ) wakiwa katika ukumbi wa mahafali hayo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)

  0 0

   
  Pichani ni muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Robanda lililopo Serengeti wilayani Mugumu, jengo hili lilijengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na Mahakama ya Tanzania lilikabidhiwa rasmi tayari kwa matumizi Januari 26, 2018, uwepo wa jengo hili utasaidia kuwapunguzia wananchi aza ya kusafiri kilomita zipatazo 40 kwenda Mahakama ya Mwanzo Serengeti kutafuta haki zao.
  Maafisa Tawala wa Mahakama mkoani Mara wakionyesha baadhi ya ofisi za jengo hilo; hapo ni sehemu ya ukumbi wa Mahakama hiyo ‘court room’ ambayo ina ukubwa wa kutosha wa kuwawezesha wananchi wenye kesi kusikiliza kesi zao bila usumbufu.
  Muonekano wa Ukumbi wa Mahakama ‘court room’

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema Februari 15, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Watatu kushoto ni Waziri wa Kilimo , Dkt. Charles Tizeba na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Anthony Diallo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua darasa wakati alipozindua madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema, Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Dkt. Flavian Kassala baada ya kuweka jiwe la msing la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitanda wakati alipokagua Bweni lililopewa jina la Dkt.John Pombe Magufuli katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Wafanyakazi wa TBL wakipata mafunzo sambamba na burudani za vinywaji baada ya saa za kazi. Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakifuatilia mafunzo ya mahusiano na afya.
  Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifutilia mafunzo. TBL Moshi hawakubaki nyuma katika mafunzo hayo.
  TBL Mbeya nao walishiriki mafunzo na mijadala ya mahusiano Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev, imeitumia Siku ya Wapendanao kuandaa semina za wafanyakazi wake kuhusiana na masuala ya mahusiano katika familia, zilizoendeshwa na wataalamu wa masuala ya Saikolojia na ushauri nasaha kutoka taasisi mbalimbali za mafunzo nchini. Semina hizo zilifanyika katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha. 

   Kwa kutumia kauli mbiu ya ‘Nogesha Upendo Valentine hii’ wafanyakazi walipata fursa ya kupata mafunzo,na kushiriki mijadala kuhusiana na mahusiano bora katika ndoa na familia sambamba na changamoto mbalimbali zilizopo, pia waliweza kupata majibu na ushauri wa changamoto hizo waliokuwa wakiendesha mafunzo.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ambapo awali alikuwa na cheo cha Meja Jenerali kabla hajamuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati Maafisa Mbalimbali wastaafu wa (JWTZ) walipokuwa wakizungumza mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi ambao wamepandhishwa vyeo kutoka Cheo cha Brigedia Jenerali na kupewa cheo kipya cha Meja Jenerali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

   Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.

    Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.
     Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma hasa ukizingatia anatumia mkono mmoja zaidi.

  Ombi langu kwenu.
   
  Tumkopeshe mungu kupitia kijana huyu tukiamini ni jukumu letu kama jamii kumsaidia. Namba yake ni +255768924516 inapokea M-pesa na jina la YUKI HAMISI. Pia mnaweza kumpigia kumsikiliza zaidi.🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha inafunga kamera katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi ili kudhibiti vitendo vya hujuma katika mifumo ya kampuni hiyo hususani kwenye Mapato. 

  Ametoa rai hiyo jijini Mwanza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV Clarias na kusisitiza kuwa matumizi ya mfumo huo mpya yaende sambamba na elimu stahiki kwa watumishi wanaoutumia mfumo huo katika kukatisha tiketi. 

  “Niwapongeze sana kwa hatua hii ya kuingia kwenye mfumo wa kielektroniki katika utoaji huduma lakini niwatake sasa kuongeza kamera kwenye maeneo yote unapofanyika ukaguzi ili kudhibiti mianya yote inayoweza kujitokeza ya kuhujumu mapato ya kampuni” amesema Prof. Mbarawa. 

  Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye shirika hilo ili liweze kupata faida na liweze kujitegemea na kuagiza kuwa kwa sasa kila fedha inayopatikana itumike vizuri sababu Shirika limeanza kupata faida. 

  Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), kutengeneza mfumo kama huo kwa ajili ya Shirika la Reli Nchini (TRL), ili kudhibiti uvujaji wa mapato. 

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Kuwe, amesema mfumo huo umetengenezwa na Wakala ili kuiwezesha taasisi hiyo kuthibiti mapato kwani mfumo huo utarahisisha Huduma kwani abiria ataweza kukata tiketi akiwa sehemu yoyote nchini. 

  Naye Kaimu Meneja Mkuu wa MSCL, Bw. Erick Hamis, amesema mfumo wa kielektroniki umeanza kwa meli moja ya MV Clarias inayofanya Safari zake kutoka Mwanza kuelekea kisiwa cha Ukerewe ambapo katika mpango wa baadae Kampuni inategemea kutumia mfumo huo kwenye meli zote za kampuni hiyo. 

  “Toka tuanze kutumia mfumo kumekuwa na ongezeko la mapato kwa zaidi ya asilimia 20, pia na kwenye matumizi ya mafuta hii inatupa ishara kuwa mfumo huu utatusaidia kidhibiti mapato mengi yaliyokuwa yakipotea kwenye tiketi”amesema Hamissi. 

  Ameongeza kuwa kampuni imejiwekea mpango wa miaka miwili wa kukarabati meli Tisa za kampuni hiyo ambapo mpaka sasa meli Tatu zimeshakarabatiwa na kuanza kazi wakati hatua ya kuanza ukarabati kwa meli zilizobaki uko kwenye hatua mbalimbali za manunuzi. 

  Mfumo huo mpya wa kielektroniki wa ukatishaji tiketi katika kampuni hiyo umegharimu kiasi cha shilingi takriban milioni 50.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV. Clarias inayotoa huduma kati ya Mwanza na Ukerewe.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata tiketi ya kieletroniki mara baada ya kuzindua mfumo wa tiketi hizo katika Meli ya MV Clarias, mkoani Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamis, wakati akikagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias, mkoani Mwanza.

  0 0


  0 0


  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wauguzi wa zamu wa Wadi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine’s Day) ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. Taasisi ya Doris Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha, wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo, lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid (Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo.
   Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
   Muwakiliwa wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
   Wakinamama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.

  0 0

  Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 14 Februari, 2018 ameshiriki makabidhiano ya Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda lililojengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya Dola za Marekani 148,146. Aidha, Waziri Kalemani ameshiriki utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Japan na Tanzania kwa ajili ya ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita moja ya Muganza kwa gharama ya Dola za Marekani 90,645.
  Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida (kulia) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Joel Hari (kushoto) mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Japan kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Muganza kwenye uzinduzi huo. Katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
  Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida akisoma hotuba katika uzinduzi huo.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akielezea mafanikio ya mkoa wake katika uzinduzi huo.
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kushoto, waliosimama mbele) Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida ( wa n ne kushoto, waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita mara baada ya uzinduzi wa Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda.
  Sehemu ya wananchi wa Kitongoji cha Kasenda kilichopo wilayani Chato mkoani Geita wakisikiliza hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele) akicheza pamoja na kikundi cha Mwagazege katika uzinduzi huo.

  0 0

   Kaimu Balozi wa Kuwait nchini,  Mohamed Al-Amiri akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuikabidhi Shule ya Msingi ya Jeshi la uokovu vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi pembeni yake mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma, Mwalimu wa shule Bi. Flourina Milinga na Afisa elimu taaluma Mkoa Bw. Fortunatus Kagoro
   Mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation, Suleiman Magoma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi vyenye thamani ya shilingi milioni 30 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya nchi ya Kuwait,pembeni yake aliyevaa kanzu ni Kaimu Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Mohamed Al-Amiri
  Kaimu Balozi wa Kuwait nchini, Mohamed Al-Amiri awakabidhi wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi ya Wokovu viti vya matairi,pembeni yake mwasisi wa Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma na Mkurugenzi qa shule Thomas Sinana.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Mwanza Februari 15, 2018 .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kulia ni Mbunge wa Buchosa na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WADIWANI BUCHOSA WAMKATAA MKURUGENZI  MADIWANI wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.  Wametoa ombi hilo leo (Alhamisi, Februari 15, 2018) katika kikao cha Waziri Mkuu na watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.  Waziri Mkuu baada ya kupokea ombi hilo alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.  Awali, Waziri Mkuu  aliweka jiwe la msingi la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55.  Pia Waziri Mkuu amezindua madarasa manne ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na kuwata wanafunzi wasome kwa bidii.  Waziri Mkuu amesema wanafunzi hao wanatakiwa wasome sana kwa sababu Rais Dkt. John Magufuli amewaondolea wazazi michango  ya hovyo ili wao wapate fursa ya kusoma.  Pia amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango ili wajikite na masuala ya taaluma. Kama kuna michango kutoka mtu mmoja mmoja, vikundi au Taasisi yote sasa itafikishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.  Amesema awali wanafunzi walikuwa wanatumika kama njia ya kutengeneza fedha, ambapo wazazi au walezi wanaposhindwa kutoa michango hiyo watoto wao walikuwa wanarudishwa nyumbani. Waziri Mkuu amesema kila mwezi Serikali inapeleka moja kwa moja shuleni sh. bilioni 20.8 kwa ajili ya kugharamia Elimumsingi bila malipo.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  ALHAMISI, FEBRUARI 15, 2018.

  0 0


  0 0


  0 0


  Raia wawili wa Tanzania, Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa walikamatwa nchini China Jan. 19 mwaka huu kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82.

  Watuhumiwa hao walikatwa wakiwa wameandama na mtoto wao mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo alitarajiwa kuingia nchini leo saa saba mchana akiwa ameambatana na Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda.

  Serikali kupitia Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu na jamaa wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwao kwa jaili ya malezi na matunzo.

  Taarifa Na: Rogers W. Siyanga
  Kamishna Jenerali:
  Mamlaka Ya Kudhibiti Na Kupambana Na Dawa Za Kulevya Nchini.

  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya
  Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza Faiswary.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya

  ………………….

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi bandari ya Itungi iliyopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.

  Katik ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitolea maeneo yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

  Naye Mkuu wa Wilaya wa Ludewa Bwana Andrea Tsere amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa tayari wamekamilisha kazi ya kuhakiki malipo ya fidia za wananchi waliotoa ardhi zao eneo la Manda na Lupingu. “Wanachi wa eneo la Manda watalipwa shilingi milioni 192 ambapo wametoa eneo la ukubwa wa hekari 24 na wa Lupingu wametoa eneo ukubwa wa hekari 10.6 na watafidiwa shilingi milioni 166, amesema Tsere”.

  Bwana Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania inakamilisha ujenzi wa meli ya mizigo na abiria na itaanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo ndani bandari za Ziwa Nyasa mwezi Agosti mwaka huu ambapo meli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria mia mbili na mizigo tani mia mbili kwenye jumla ya bandari kumi na tano zilizopo ndani ya mwambao wa ziwa Nyasa.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa amemshukuru Mhe. Mhandisi Nditiye kwa niaba ya wananchi wake kwa kufika kwenye makazi ya wananchi hao waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa na kukagua mahitaji ya usafiri wa majini wa abiria na mizigo wa Ziwa hilo ambapo Serikali tayari imetenga fedha kulipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi na upanuzi wa bandari za Ziwa hilo.

  Ujenzi wa bandari hizo na utoaji wa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo ni ukamilishaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambao wanategema Ziwa hio kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kiuchumi, biashara na kijamii ambazo zitachangia ukuaji wa uchumi wa wananchi hao na taifa kwa ujumla.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano

  0 0

  Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita na Mahakama ya Wilaya Geita likiwa katika hatua za awali za ujenzi IMG_7739
  Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe likiwa katika hatua za awali za ujenzi wake katika mji mdogo wa Ushirombo wilayani Bukombe
  IMG_7742
  Jengo la Mahakama ya wilaya ya Chato likiwa katika hatua ya Msingi. Majengo haya yote yanajengwa kwa Teknolojia ya Gharama nafuu na ya muda mfupi iitwayo Moladi na yanajengwa na Kampuni ya Moladi Tanzania. Ujenzi wake unatarajiwa kutumia muda wa miezi sita.
   ……………………
  Na Lydia Churi-Geita
  Katika kutekeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za Mahakama na kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza rasmi ujenzi wa majengo matatu ya Mahakama katika mkoa wa Geita pamoja na wilaya zake za Bukombe na Chato.
  Ujenzi wa Mahakama hizi ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2015. Miradi hii kwa pamoja inalenga kuboresha huduma na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
  Mahakama imeanza ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mkoa wa Geita ambalo  litajumuisha pia na Mahakama ya wilaya ya Geita. Majengo mengine yanayojengwa ni ya Mahakama za wilaya za Bukombe na Chato.
  Majengo haya yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita kutoka sasa na yanajengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu na ya muda mfupi iitwayo Moladi ambapo kampuni ya Moladi Tanzania ndiyo imepewa dhamana ya kujenga majengo hayo. Jumla ya majengo ya Mahakama za Mkoa, wilaya na Mwanzo sita tayari yameshajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi katika jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.
  Majengo haya ni yale ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo, Kigamboni, Mkuranga pamoja na jengo la Mahakama ya wilaya ya Kigamboni na Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar es salaam.
  Mhandisi wa Kampuni ya Moladi Tanzania anayesimamia ujenzi wa Mahakama za Geita, Bukombe na Chato, Camilius Mihambo akielezea ujenzi wa Mahakama hizo alisema ujenzi huo unaendelea vizuri na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita kilichopangwa . Mhandisi Mihambo amesema hatua ya ujenzi iliyofikiwa sasa ni hatua ya awali ya kujenga msingi katika majengo yote matatu.
  “Kazi kubwa na inayochukua muda mrefu kwa sasa ni ya kujenga msingi, hatua inayofuata ya kuweka ukuta ni ya muda mfupi kwa kuwa tunatumia teknolojia ya Moladi ambayo kuta zinaweza kusimama ndani ya siku tatu na kuendelea, alisema Mhandisi huyo.
  Akizungumzia hatua ya Mahakama ya Tanzania kuanza ujenzi katika Mkoa wa Geita, Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Geita, Lothan Simkoko anaelezea kufurahishwa kwake kwa uamuzi wa Mahakama kujenga Majengo ya Mahakama za wilaya na Mkoa katika mkoa wa Geita. Anasema ujenzi huo utasaidia upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wananchi wanaofika Mahakamani kutafuta haki zao pia kumaliza changamoto ya ufinyu wa ofisi. Alisema, jengo la Mahakama ya Mkoa litakapomalizika litatoa nafasi zaidi na kuboresha huduma. Mahakama ya Mkoa wa Geita ina upungufu wa chumba cha Mahabusu, chumba cha kuhifadhi ushahidi pamoja na ofisi kwa ajili ya watumishi wake.
  Mtendaji huyo alisema Mahakama Mkoani Geita haina jengo la Mahakama ya wilaya na badala yake jengo linalotumika sasa kwa Mahakama ya wilaya na Mwanzo ni la kuazima na pia haliko katika hali nzuri. Alisema kukamilika kwa jingo jipya la Mahakama mkoani humo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za Mahakama.
  Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliohojiwa juu ya ujenzi wa Mahakama hizo walionyesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Mahakama kujenga majengo yake mapya. Bwana Mika Jonathan Shija ambaye ni Mkazi wa Geita anaelezea kufurahishwa kwake na ujenzi wa Mahakama ya Mkoa na ya Wilaya ya Geita na kusema kuwa ujenzi huo utakapokamilika utawarahisishia wananchi kupata huduma. “kama tulivyoambiwa kuwa Mahakama ya Mkoa na wilaya zitakuwa kwenye jengo moja hivyo kwetu sisi ni rahisi kwa kuwa itakuwa ni rahisi kutoka  sehemu moja kwenda nyingine”, alisema.
  Naye Pili Malongo Mkazi wa Bukombe yeye alisema amefurahishwa na ujenzi wa Mahakama wilayani humo kwa kuwa anaamini jengo jipya la Mahakama litakuwa na sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wananchi kupumzika wakati wakisubiri kupatiwa huduma mahakamani hapo.
  Pamoja na ujenzi wa Mahakama hizo tatu katika Mkoa wa Geita, Mahakama ya Tanzania tayari imeanza kutekeleza program ya ujenzi wa majengo 18 ya Mahakama katika mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 anabainisha Mkuu wa  Kitengo cha Majengo (Estate Management) wa Mahakama ya Tanzania Mhandisi Khamadu Kitunzi.
  Kwa mujibu wa Mhandisi Kitunzi, kati ya majengo 18 yaliyoanza kujengwa nchini,  majengo mawili ni ya Mahakama Kuu yanayojengwa kwenye Mikoa ya Mara na Kigoma, matano ni ya Mahakama za Hakimu Mkazi yanayojengwa katika mikoa ya Geita, Njombe, Lindi, Simiyu, na Katavi. Aidha jumla ya majengo 11 ya Mahakama za Wilaya yanajengwa katika wilaya za Kasulu, Rungwe, Ruangwa, Kilwa Masoko, Kilindi, Sikonge, Kondoa, Bunda na Longido.
  Aidha, Mahakama pia imefanikiwa kujenga Mahakama za Mwanzo na pia kumalizia baadhi ya Mahakama zilizoanza kujengwa kwa nguvu ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini kama vile Itinje-Meatu, Robanda-Serengeti, Wasso-Loliondo, na Karatu Arusha. Maeneo mengine ni Beleko-Kondoa, Mahakama ya Old Korogwe-Korogwe, Mvomero Morogoro, Mahakama ya Mwanzo Totoe iliyopo Mkoani Songwe na Mahakama ya Mwanzo Iguguno mkoani Singida.
  Akifafanua zaidi kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama, Mhandisi Kitunzi anaeleza kuwa hivi sasa zipo Mahakama Kuu 14 na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama kuu katika mikoa ya Mara na Kigoma kutakuwa na jumla ya Mahakama kuu 16 nchini na kubaki na uhitaji wa Mahakama Kuu 10 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Mahakama ya Tanzania inalenga kujenga majengo ya Mahakama kuu ambayo yatatumika kama Kituo Jumuishi cha kutoa huduma za kimahakama yaani Intergrated Justice Centre. Mahakama tayari ilifanya ukarabati mkubwa wa jengo la Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ambapo hivi sasa Mahakama hiyo inafanya kazi kama kituo Jumuishi cha huduma za Kimahakama.
  Mhandishi Kitunzi anasema Mahakama inao mpango wa kujenga Majengo ya Mahakama Kuu ambayo yatatoa huduma kama kituo Jumuishi cha kutoa Huduma za Kimahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia katika mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Mwanza na Arusha.

  0 0


  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 15.02.2018

  Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umekabidhiwa rasmi Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015.

  Cheti hicho cha ubora ni kielelezo cha taasisi ya ZFDA juu ya kusimamia misingi imara ya kuhakiki ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya hususan upatikanaji chakula, dawa na Vifaa tiba.

  Amesema kunahitajika ubunifu na jitihada za makusudi za kila mfanyakazi wa ZFDA kuhakikisha Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba ni bora na salama kwa afya za wananchi.Amefahamisha kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana yawe chachu ya kuongeza ufanisi kiutendaji ili kufikia dira iliyowekwa.

  “Mkifikia dira dira hiyo itakuwa mmetekeleza kikamilifu jukumu mllopewa na Serikali la kulinda afya ya jamii.Serikali inaaamini mnao uwezo wa kuwa taasisi bora ya udhibiti Afrika na Duniani kwani hakuna kizuizi cha kufikia dira hiyo” Alisema Waziri Kombo.Aliitaka menejimenti ya ZFDA kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa Chakula, Dawa na Vipodozi nchini kiholela ili kulinda afya za Wazanzibari.

  “Ndugu wafanyakazi mna jukumu kubwa sana kwa Wananchi wetu na mbele ya Mungu maana mtakaporuhusu uingizwaji wa bidhaa duni zenye madhara mtahatarisha afya za Wananchi na kesho mbele ya haki Mungu mutaulizwa” aliwanasihi Waziri Kombo.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya ACM Ltd iliyokabidhi cheti hicho Nyasha Mupukuta alisema haikuwa kazi rahisi kwa Taasisi hiyo kupatiwa Cheti hicho cha ubora.Alisema kulipita ukaguzi wa kutosha na wa muda mrefu kabla ya Cheti hicho kutolewa na hivyo kuendelea kuipongeza ZFDA kwa kazi kubwa waliyoionesha.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Burhani Othman Simai wakati akielezea sababu zilizopeleka kupatiwa ZFDA kupatiwa Cheti hicho ni pamoja na kuwepo kwa sera na miongozo ya ubora, mkataba huduma kwa wateja, kanuni za maadili za wafanyakazi (code of Conduct), wafanyakazi kusaini fomu za conflict of interest or competing interest na taratibu sanifu za utendaji kazi (SOP).

  Sababu nyingine ni ufanyaji wa tathmini ya mteja kuridhika huduma zinazotolewa (customer satisfication survey) na kuainisha majukumu ya kazi kwa kila mfanyakazi (Job Description).

  Hafla ya kupokea cheti hicho cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 zilifanyika katika Ofisi ya ZFDA Mombasa mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Wakurugenzi mbalimbali na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Andy Michel.


  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR


   Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katikati akizungumza mara baada ya kupokea Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 katika hafla iliyofanyika Ofisi za ZFDA Mombasa mjini Zanzibar

  0 0

  Mtaalamu wa Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Liqui Moly Tanzania,Nyanzige Nyabero akizungumza mapema jana mbele ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa bidhaa zao za Liqui Moly nchini Tanzania.
  Baadhi ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakifautilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni hiyo ya Liqui Moly nchini Tanzania.
  MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Liqui Moil Tanzania, Faraja Mkinga  akizungumza Mbele ya Wanahabari kuhusiana na Uzinduzi wa bidhaa zao nchini Tanzania,mapema jana jijini Dar Es Salaam.Mkinga alisema kuwa kampuni yao inajisikia fahari kubwa kuwapatia Watanzania bidhaa zenye ubora wakati Taifa likijipanga kuelekea katika uchumi wa kati. 

  ''Tanzania imeingia katika mapinduzi makubwa kwenye sekta ya magari na mitambo kwa kuanza  kutumia Oili na vilainishi bora na halisi vya kampuni ya Liqui Moly yenye makao yake makuu nchini Ujerumani'',alisema Mkinga. 

  Kuhusu kampuni hiyo, Mkinga amesema ilianzishwa mwaka 1957 nchini Ujerumani na inatengeneza bidhaa zaidi ya 4,000 ambazo zinazosambazwa katika nchi zaidi ya 130 duniani na kwa mara ya kwanza sasa zimeanza kupatikana nchini Tanzania kupitia mawakala wao.Pichani kulia ni Mtaalamu wa Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Liqui Moly Tanzania,Nyanzige Nyabero na kushoto ni Mtaalamu kitengo cha Ufundi Harry Hartkorn
  MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Liqui Moil Tanzania, Faraja Mkinga  akiwaonesha Waandishi wa habari moja ya bidhaa yao mara baada ya kuzindua bidhaa zao mbalimbali nchini Tanzania,mapema jana jijini Dar Es Salaam.MKinga alisema kuwa “Kuna vilainishi vya magari madogo, magari ya usafirishaaji, meli, majenereta, pikipiki, ndege na mashine mbalimbali za viwandani''. Pia tuna mpango wa kuhakikisha tunakuwa na mawakala kwa ajili ya bidhaa zetu maeneo mbalimbali nchini  Tanzania,” alisema Mkinga. Amewataja baadhi ya mawakala hao ni Jaffary  Car Wash( Mikocheni), Fishcrab Auto Care (Kinondoni) , Top Gear (Kinondoni) , 0-60 (Kinondoni)  na TFL Garage (Mikocheni) na wote wapo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakifautilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni hiyo ya Liqui Moly nchini Tanzania.
  Sehemu ya meza kuu wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo mara baada ya bidhaa za kampuni hiyo kuzinduliwa rasmi nchini Tanzania


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya, wilaya ya Bunda alipokutana nao baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Mara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 54. Barabara hiyo inajengwa na wakandarasi wazawa M/S Mbutu JV.

  …………………

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

  Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya na kusema kuwa usanifu wa barabara na madaraja katika barabara hiyo umewasilishwa sasa ni jukumu la mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kasi na kwa viwango vya ubora.

  “Serikali ina nia njema kwa wananchi wa wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara sasa tunaijenga barabara hii na mwishon mwa mwaka mtaanza kunufaika nayo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo utarahisisha mawasiliano na kupunguza gharama za shughuli za usafirishaji wa samaki, mazao na abiria, uboreshaji makazi na kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya barabara.

  Kuhusu suala la fidia, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali italipa fidia kwa mwananchi ambaye barabara imemfuata kama anavyostahili.

  “Serikali haina nia ya kumuonea mtu yeyote bali inachofanya inalipa kulingana na sheria inavyoelekeza”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Sanzale KM 50 na kumwagiza mkandarasi wa M/S Mbutu JV Contractor (T) kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

  “Mradi huu ni wa muda mrefu sana na wananchi wameusubiri kwa muda kama hamtamaliza mradi huu mpaka mwezi juni, hii itakuwa kazi yenu ya mwisho, maana ninategemea nyinyi kama wazawa mngekuwa wa mfano” amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema kwa sasa mkoa umeamua kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya barabara kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara, Mhandisi Mlima Ngaile amesema Wakala utasimamia mradi wa ujenzi wa barabara hizo na kuhakikisha mradi unazingatia viwango kulingana na mkataba.

  Waziri Prof. Mbarawa yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

older | 1 | .... | 1518 | 1519 | (Page 1520) | 1521 | 1522 | .... | 1897 | newer