Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1509 | 1510 | (Page 1511) | 1512 | 1513 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

  Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi vya Watu wenye Ulemavu ili kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri na kupata ujuzi mbadala wa kumudu maisha yao.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa lililohusu umuhimu wa kuwatazama vijana wenye ulemavu mbalimbali kwa namna ya kipekee.

  Mhe. Ikupa amesema kuwa Serikali inatambua Vijana wenye ulemavu kuwa ni kundi mojawapo miongoni mwa watanzania wenye ulemavu ambalo linakabiliwa na changamoto mbalimbali.

  “Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la watu wenye ulemavu wakiwemo vijana, Serikali iliunda Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu ambalo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri kwa Serikali na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya watu wenye ulemavu juu ya namna bora ya kushughulika na changamoto zao zikihusisha zile za kundi la vijana wenye ulemavu,” amefafanua Naibu Waziri Ikupa.

  Aidha, Mhe. ikupa amesema kuwa Serikali imeendelea kuunda kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Wilaya, Kata na Mtaa kwa lengo la kuhakikisha masuala ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa ili kuondokana na kero mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu Elimu, Afya, Ajira na Mikopo ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  Hata hivyo, Naibu Waziri Stella Ikupa amewahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia ipasavyo utekelezaji wa suala hilo ambalo liko kisheria na pia ametoa wito kwa Wakurugenzi hao kuhamasisha walemavu kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ikiwemo vikundi vya vijana.

  0 0


  WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa, ameitisha kikao cha wadau wa pamba nchini, ili kujadili namna bora ya kuongeza tija ya zao hilo.

  Kikao hicho kitakachofanyika jijini Mwanza Februari 15 hadi 16, 2018, kinatarajiwa kuondoa sintofahamu iliyogubika sekta ya pamba, kuhusu mustakabari wa kilimo cha mkataba kutokana na kusudio la Serikali kuanzisha ununuzi wa pamba kwa njia ya mnada kupitia vyama vya ushirika.  

  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuonesha kusudio la kusitisha kilimo cha mkataba, na uwezekano wa pamba kuuzwa kwa njia ya mnada.Kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, kikao hicho muhimu kimelenga kuondoa hali ya sintofahamu, juu ya kilimo cha mkataba na uuzwaji wa zao hilo kwa njia ya mnada.  Kusudio hilo la Serikali la kuuzwa pamba kwa njia yamnada, limeonekana kuleta wasiwasi kwa makampuni yaliyowekeza kwenye sekta hiyo muhimu katika uchumi wa nchi. 
  Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo Charles Tizeba kabla ya kuanza ziara ya kuona utekelezaji wa kilimo cha Pamba na uzalishaji wa mbegu bora za pamba za UKM08 Msimu 2017/2018 uliofanyika jana tarehe 04 feb 2018.
  Afisa Kilimo wilaya ya Igunga Erasto Konga akiwasilisha taarifa ya wilaya kwa Waziri wa Kilimo.
  Akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa mkoa huo Agrey Mwanri, Waziri Tizeba pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakulima na kugundua kuwa bado elimu ya unyunyiziaji dawa haijakaa sawa.
  Na hapa ikawa nafasi ya kutoa darasa upya kwa mkulima huyu.
  "Tunakwenda kujadiliana nao wanunuzi hawa wa pamba, hususani walioingia kilimo cha mkataba. Asilimia 40 ya Watanzania wote wanategemea uchumi wao kupitia pamba," alisema Waziri Tizeba.Alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwa ziara ya kukagua mafanikio ya zao la pamba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
  Waziri Tizeba akitizama namna mkulima wa pamba ambaye ni Mwalimu wa Shule ya msingi , Bw. Faustine Francis anavyo nyunyizia dawa. 
  Afisa ugani Kata ya Mbutu Iddi Uledi akitoa maelezo kwa Waziri Tizeba.
  Shamba la zao la Pamba wilayani Igunga.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Gaki Investment inayojihusisha na ununuzi wa pamba, Gasper Gaki, alisema: “Tunakingoja kwa hamu sana kikao hiki na Waziri Mkuu, naamini kitakuwa na mafanikio.”

  Katika hatua nyingine, Waziri huyo mwenye dhamana ya Kilimo alisifu juhudi za kilimo cha pamba, ambapo Mkoa wa Tabora umevuka lengo lake la uzalishaji zao hilo.

  Zaidi ya kilo milioni 187 zinatarajiwa kuvunwa mwaka huu mkoani hapa, kwamba kasi ya kilimo hicho inaleta tija kiuchumi na pato la taifa.

  Idadi hiyo ni kiwango cha juu, kuliko matarajio ya awali ya kuvuna zaidi ya kilo milioni 136 za pamba, msimu huu.

  Waziri Tizeba alisema kuwa, takribani sh. Bilioni 50 zinahitajika kwa ajili ya manunuzi ya dawa za kuuwa vijidudu vya mazao.

  "Haijawahi kutokea. Tumepata mafanikio makubwa sana ya kilimo cha pamba mwaka huu. Viongozi na wananchi hongereni sana, mtauza kwa bei nzuri.

  Waziri huyo aliagiza maofisa kilimo 30 waliopo wizarani kwake, na wengine 30 kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru kuanzia wiki ijayo, kusambazwa Mikoa ya Tabora, Simiyu, Shinyanga na Mwanza.

  Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga, alisisitiza wakulima wa zao hilo kupulizia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.

  "Ukipuliza dawa mchana hautauwa hawa wadudu. Muda wa kupuliza ni asubuhi, mwisho saa 3:00 asubuhi, baadaye tena jioni," alisema Mtunga.
  Awali, Ofisa Kilimo Mkoa wa Tabora alizitaja wilaya nyingine za mkoa huo na idadi ya uzalishaji kilo kwenye mabano kuwa ni Kaliua (kilo 11,554,000).

  Nzega (kilo 16,300,000), Urambo (4,307,000) na Uyui inayotarajia kuzalisha zaidi ya kilo milioni 6.81.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye katika picha ya pamoja na Kikosi cha Maokozi cha Jeshi hilo, wakati alipotembelea Kikosi hicho kilipokuwa kikionesha zoezi la maokozi, kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Bashiri Madhehebi ambaye ni Mkuu wa kikosi hicho.
  Wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo pichani), jinsi wanavyoweza kufanya maokozi katika maji alipotembelea eneo la daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni walipokuwa wakifanya zoezi hilo, mapema leo asubuhi (kushoto) ni Sajini wa Zimamoto Salehe Salla na aliyevaa boya maalum kwa ajili ya maokozi ni Koplo wa Zimamoto Omary Katonga.
  Mzamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini wa Zimamoto Saidi Sekibojo akiwa katika mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.
  Sehemu ya Askari wazamiaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Koplo Omary Katonga (kulia) wakionesha utimamu mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo (hayupo picha) mara baada ya kufanikiwa kumuokoa mhanga aliyekuwa kazama katika kina kirefu cha maji, wakati wa mazoezi ya uzamiaji katika eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere mapema leo asubuhi, lengo ni kujiweka tayari kwa ajili ya Maokozi majini pindi ajali zinapotokea.
  Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo kwa wataalamu wa sekta ya afya wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba mtandao nchini kwa wataalamu wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
  Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Peter Phillip Mwasalyanda (aliyeketi katikati), akisikiliza kwa makini kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma
  Wataalamu wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (hayupo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma


  Serikali imejipanga kutumia tiba mtandao kuboresha huduma za afya nchini kwenye hospitali zote za ngazi ya taifa, rufaa na wilaya ili kuwawezesha wagonjwa waishio sehemu mbali mbali nchini kupata huduma za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

  Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF, Dodoma.

  Dkt. Ulisubisya amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watendaji wakuu wa hospitali za taifa nchini, madaktari bingwa wa sekta ya Afya, wakuu wa taasisi zinazoshughulika na sekta ya Afya, Wizara ya TAMISEMI, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; taasisi nyingine za Serikali; sekta binafsi na wabia wa maendeleo ili kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja wa kufanikisha utekelezaji wa huduma za tiba mtandao ili kuboresha huduma za afya nchini.

  Amesema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na madawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayotokana na ajali za barabarani. “Hadi hivi sasa ni asilimia 37 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ndio wanaotambulika na kupatiwa huduma na Wizara ya Afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo, tiba mtandao itawezesha upatikanaji wa wagonjwa na ufikishaji wa huduma kwao kwa wagonjwa wengine asilimia 63”, amefafanua Dkt. Ulisubisya.

  Ameongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri kufuata madaktari. Aidha, amewataka wakuu hao wa taasisi kuwaruhusu wataalamu wao, wa Wizara ya TAMISEMI na wa Wizara ya Afya, kushiriki mafunzo ya tiba mtandao ili kuongeza ufanisi wao katika kuhudumia wagonjwa.

  Amewataka wataalamu wa afya na wakuu wa taasisi zinazohusika na masuala ya afya kununua vifaa tiba vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) vyenye viwango na ubora unaohitajika ili kuwezesha tiba mtandao na manunuzi hayo yazingatie na kufuata ununuzi wa pamoja wa huduma na bidhaa za Serikali. 

  Vifaa vya kisasa vya TEHAMA vinavyohusika na tiba mtandao vitawawezesha wataalamu kufanya uchunguzi kwa mgonjwa, kupata majibu ya uhakika na kumpatia mgonjwa tiba inayostahili na ya uhakika. Aidha, amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Ulanga, ambao ndio waanadaji na waratibu wa kongamano hilo, kushirikiana na TTCL kuhakikisha kuwa tiba mtandao inapatikana katika hospitali zote za rufaa na hospitali ambazo zina changamoto ya kijiografia ya kufikika kwa urahisi. Aidha, hadi hivi sasa huduma ya tiba mtandao inapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bagamoyo, KCMC-Moshi, Bugando-Mwanza na Benjamin Mkapa, Dodoma. 

  Naye Eng. Ulanga amesema kuwa UCSAF imeanzisha huduma ya tiba mtandao kwenye vituo 14 vya majaribio. Aidha, imeainisha orodha ya vituo 279 ikiwa ni pamoja na hospitali za taifa, rufaa na wilaya ambazo zitaunganishwa na kuwezeshwa kutoa huduma ya tiba mtandao nchini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam Dkt. Julius Mwaiselage, akiwa mmoja wa washiriki wa kongamano hilo amesema kuwa, tayari tulikuwa tunatumia huduma ya tiba mtandao kwa wagonjwa wetu kwa kushirikiana na hospitali nyingine zilizopo nchini India kwa kuwafanyia wagonjwa uchunguzi na kuona kama kweli mgonjwa husika anahitaji kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi. 

  “Uwepo wa huduma ya tiba mtandao kwenye hospitali zetu nchini, itatuwezesha kufanya uchunguzi na kutoa tiba kwa wagonjwa waliopo mikoani hivyo kuwapunguzia gharama wagonjwa za kuja Dar es Salaam na endapo watalazimika kuja basi watakaa kwa muda mfupi ukilinganisha na hapo awali”, amesema Dkt. Mwaiselage. Washiriki wengine wa kongamano hilo ni kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bugando, MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kiwete, Mloganzila, Aga Khan, Hospitali ya Rufaa Mbeya, NHIF, PATH na Shirika la Afya Duniani.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki akishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe.
  Wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katiia kijiji cha Wishiteleja kata ya Mondo.
  Moja wa ng’ombe akiwa tayari amepigwa chapa katika sehemu ya mguu.


  Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi 

  Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imeweza kupiga chapa jumla ya ng’ombe 225,131 katika zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo linalofanyika katika kata zote zenye wafugaji wilayani humo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na limeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa.

  Alisema zoezi hilo ni agizo kutoka serikalini na kinachofanyika ni kulitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa na kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo mbalimbali katika kata za wilaya hiyo.

  “Zoezi la upigaji chapa ng’ombe tulilipokea na tumeweza kulitekeleza ingawa zipo changamoto mbalimbali zikiwemo baadhi ya maeneo kutokuwepo kwa wafugaji tumefanikiwa kuifikia mifugo hiyo,” alisema.

  Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dk. Alphonce Bagambabyaki alisema Wilaya imeweza kufikia lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 75 ya lengo ambalo ni ng’ombe laki tatu.

  Alisema vijiji lengwa vyote 125 vimeweza kufikiwa na ingawa zipo baadhi ya changamoto kama imani potofu kwa baadhi wafugaji kuwa huenda wakachukuliwa mifugo yao pindi wanapoifikisha vituo vya zoezi la upigaji chapa.

  Zoezi hilo lilianza rasmi Oktoba 20 mwaka jana ambapo lilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba linataka mifugo yote nchini kutambuliwa kwa kutumia chapa chini ya sheria ya utambuzi namba 12 ya mwaka 2010.

  Aidha, zoezi hilo limekuwa likitekelezwa na wataalamu wa mifugo kutoka wilayani makao makuu wakishirikiana na wataalamu wa kata na vijiji mbalimbali ili kuhakikisha limekwenda kwa ufanisi.

  Wakati akizindua zoezi hilo Mh. Taraba alibainisha kuwa zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa ng’ombe kwa kutumia chapa litapunguza changamoto zinazowakabili wafugaji.

  Alibainisha kuwa Kishapu ni miongoni mwa wilaya ambazo baadhi ya wafugaji wake wanakabiliwa na matatizo yakiwemo wizi wa mifugo katika unaoweza kutokea katika maeneo mbalimbali nchini.

  Pia linasaidia kupunguza migogoro migogoro baina ya wakulima na wafugaji wanaokuwa wanahama hama bila kufuata utaratibu maalumu kwa lengo la kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
   Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi  la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
   Wajukuu wa marehemu pamoja na wafiwa wengine wakiwa katika hali ya majonzi makaburini hapo. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Mkuu wa mkoa Geita ,mhandisi Robert Luhumbi kushoto akiwa na Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafisi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18. 
  Katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Celestine Gesimba akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi. 
  Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja  akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Mkoani humo. 

  Na,Consolata Evarist,Geita

  Wananchi Mkoa wa Geita wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye zoezi la utafiti wa mapato na matumizi kwenye Kaya binafsi ili kutoa takwimu za hali ya umasikini zitakazosaidia serikali na wadau wengine kutathimini hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. 

  Miongoni mwa Malengo hayo ni pamoja na yale yaliyoainishwa katika mpango wa pili wa maendeleo ya miaka mitano pamoja na maendeleo endelevu.

  Kata, Vijiji, Mitaa na vitongoji 34 mkoani humo vinatarajia kufanyiwa utafiti huo ili kupata taarifa zinazohusu Kaya na wanakaya, Uzazi na unyonyeshaji, elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, bima, hali ya ajira, biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya.

  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi alisema utafiti huo utasaidia kuweka misingi katika kutambua viashiria vya kiuchumi, ajira na ustawi wa jamii vitakavyofuatiliwa kwa kipindi husika na kupata makadirio ya jumla ya mwenendo wa matumzi ya kaya ili kuandaa fahirisi za bei.

  “Napende kuwahakkisa wananchi wa mkoa wetu kuwa katika kutekeleza maagizo ya serikali ,uongozi wa mkoa umeendelea kuhimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”Alisema Luhumbi.

  Amendelea kusema madhumuni ya utafiti huu wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara wa mwaka 2017/18 ni kutoa takwimu za hali ya umasikini na takwimu nyingine ili kusaidia serikali na wadau wengine kutathmini hatua zilizofikiwa katika kutimiza malengo mbali mbali ya kitaifa na kimataifa yakiwemo yale yaliyoanishwa katika mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) na malengo wa maendeleo endelevu.

  Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Douglas Masanja alisema azma ya serikali ni taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo kutokana na misingi hiyo zinatakiwa ziwepo taarirfa sahihi kutoka kwa wananchi.

  Zoezi la utafiti ambalo linafanyika nchi nzima limeanza Desemba Mosi mwaka jana na linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kushoto) akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) ameongoza ujumbe huo uliokuja kwa ziara ya mafunzo nchini Tanzania. 
  Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini wakiwa kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. 
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akielezea namna TANROADS inavyotekeleza kazi zake kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu na wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele (kushoto) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano za jijini Dar es Salaam katika ziara ya mafunzo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa nchi ya Lesotho, Mathabathe Hlalele (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania. 
  Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Lesotho wakiwa katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania. 
  Baadhi ya maofisa watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wakieleza namna ya utekelezaji miradi mbalimbali iliyo chini ya wakala hiyo.
  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akiwa katika mazungumzo hayo.
  Kikao cha wajumbe hao katika ofisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kikiendelea.

  0 0

  Mwakilishi wa kampuni ya TatuMzuka,Milard Ayo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,alipokuwa akiwatambulisha washindi wa TatuMzuka Daily,waliojinyakulia Milioni 10 wakiwemo wapenzi walioingia kwenye kampeni ya Valentine iliobeba kauli mbiu ya ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’.Pichani kulia ni washindi wa kampeni ya Valentine Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja walijishindia milioni 10 na kushoto ni Nicolaus Chilipweli aliyejishindia milioni 10.
  Pichani kushoto ni Mshindi wa TatuMzuka Daily,Nicolaus Chilipweli mkazi wa Bagamoyo akielezea namna alivyojishindia Kitita cha Milioni 10 kupitia mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka na namna atakavyozitumia fedha hizo.
  Pichani ni washindi wa kampeni ya Valentine waliotimiza kauli mbiu ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’  Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja walijishindia milioni 10

  Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka ilizindua kampeni mpya ya Valentine, ambayo ilianza rasmi hivi karibuni mpaka Februari 18,2018.Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao pia kupata fursa ya kushinda.

  0 0

  1
   Meneja Usimamizi wa Mabenki (BOT), Eliamringi Mandari akiwasilisha mada ya Usimamizi wa shughuli za Mabenki na Taasisi za Fedha katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali inayofanyika kwenye ukumbi wa (BoT) mkoani Mtwara, ambapo wanahabari wamepata ufafanuzi mbalimbali katika masuala ya ya shughuli zinazofanywa na mabenki katika biashara ya kifedha nchini Tanzania kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
  2
  3
  Eliamringi Mandari Meneja Usimamizi wa Mabenki (BoT) akifafanua mambo kadhaa wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Usimamizi wa shughuli za Mabenki.
  4
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo inayoendelea kwa siku ya pili leo mjini Mtwara
  5
  Kushoto ni Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki na Sadiki Nyanzowa Afisa Benki Mwandamizi Idara ya Udhamini wa Mikopo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
  6
  Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akitoa mchango wake katika semina hiyo kuhusu mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
  7
  Jonson Myella Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BoT) akichangia mada kuhusu Mabadiliko ya Mfumo mpya wa Kuandaa sera ya Fedha, Mapitio ya Maendeleo ya Uchumi nchini, Kikanda na Kimataifa Duniani iliyotolewa katika semina hiyo.
  8
  Meneja Msaidizi Idara ya Utafiti Dkt Suleiman Missango  akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa habari wakati wa semina hiyo
  9
  Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa.
  10
  Bi. Fatma Kimario Meneja Msaidizi Idara ya Udhamini na Mikopo akitoa mada kuhusu Mifuko ya Dhamana kwa Wajasiriamali na Dhamana za Serikali
  11
  Jonson Myella Mkurugenzi Tafiti za Uchumi (BOT), Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) na Eliamringi Mandari Meneja Usimamizi wa Mabenki (BOT) wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa semina hiyo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph kakunda kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikati
  Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (kushoto) ofisis kwa mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuanza kwa ziara iliyofanyika jana ya kutembelea eneo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo.
  Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikatiNaibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakiangalia nyaraka feki iliyowasilishwa na miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali katiaka eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakatia wa ziara iliyofanyika jana ikiwa na Manaibu wa wawili wa Maliasili na Utalii pamoja na wa TAMISEMI.Mkuu wa wilaya ya Morogoro akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara akiwa ameongozana na Manaibu wawili wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda wakati walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .


  Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakimsikiliza miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali katika eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakati wa ziara iliyofanyika jana kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Baadhi wananchi wakiwasilikiliza Manaibu Waziri katika mkutano uliofanyiak jana katika eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati wakati wa ziara kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU, Shaban Kolahili akisalimia na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati Naibu Waziri huyo alipowasili katika kijiji cha Mbwade akiwa ameongozana naNaibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda.
  ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT


  Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na wa TAMISEMI imetoa siku saba kwa wananchi waliovamia kwa kuendesha maisha yao na kufanya shughuli za kilimo pamoja na kulisha mifugo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo katika Halmashuri ya Morogoro vijijini kuondoka katika hifadhi hiyo.

  Hali hiyo inafuatia baada ya wananchi hao kwenda mjini Dodoma kuonana na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na kumuelezea malalamiko yao kuwa wao ni wakazi halali katika eneo hilo lakini hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Regina Chonjo amekuwa akiwalazimisha kuondoka.

  Kufuatia hali hiyo , Waziri Mkuu K Majaliwa alimuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa TAMISEMI kwenda huko kwa ajili ya kushughulikia tatizo hilo ambapo Mawaziri hao kutokana na kubwana na majukumu mengine waliwaagiza Manaibu Waziri wao kutembelea eneo. .

  Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda jana walitembelea eneo hilo na kujionea uharibifu unaoendelea.Katika ziarz hiyo Manaibu Waziri hao walizungumza na wananchi hao kwa kumtaka mwananchi yeyote mwenye nyaraka halali za kuishi katika eneo hilo aziwasilishe katika mkutano huo lakini hata hivyo hakuna mwananchi yeyote aliyeziwasilisha

  Kutokana na wananchi hao kukiri kuishi kinyume na sheria katika eneo hilo la Hifadhi, Wananchi hao waliowaomba viongozi hao wapewe muda ili waweze kutafuta sehemu ya kuhamia kwa vile hawana sehemu ya kwenda,Kulingana uharibifu mkubwa waliojionea katika eneo hilo hali ya mazingira, Mnaaibu Waziri hao waliweza kuagiza mambo yafuatayo huyo. Kama.

  Manaibu Waziri hao waliagiza kuwa materekta yote yatakayoonekana katika eneo hilo la hifadhi baada ya siku saba kupita yataifishwe.Pia, Waliagiza kuwa yakamatwe na hatimaye kupigwa mnada kwa mujibu wa sheria kwa mifugo yote itakayooneka katika eneo hilo la hifadhi.Aidha, Waliagiza kuwa mwananchi yeyote atakayekutwa ndani ya hifadhi hiyo baada ya siku saba kuwa atakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuvamia hifadhi.

  Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo aliwaeleza Manaibu Waziri hao kuwa wananchi hao wamekuwa wakilima na kuchunga mifugo katika maeneo hayo hali iliyopelekea wanyamapori katika maeneo hayo kuhama.Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya JUKUMU, Shaban Kolahili ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii iwasaidie kuhakikisha kuwa hifadhi hhiyo inalindwa ili kuzuia vitendo vya ujangili na uvamizi unaoendelea ili kuwavutia wawekezaji ili hatimaye iweze kujitegemea.

  Wananchi wa eneo hilo mnamo mwaka 2010 walituma maombi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba wasaidiwe katika kulihifadhi eneo hilo ambalo hutumiwa na wanyapori kupimzika na kuzaliana

  0 0

  Na,Jumbe Ismailly ITIGI 

  SHEHENA nyingine ya magogo 297 yenye thamani ya shilingi milioni 26,370,000/= yaliyokuwa yakimilikiwa na Kampuni ya ARIZONA ENTERPRISES iliyopo katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida yametaifishwa na serikali wilayani Manyoni na hivyo kufanya jumla ya magogo 720 yaliyotaifishwa na serikali baada ya kubainika kwamba mmiliki wa kampuni hiyo alikiuka taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu.

  Mapema mwezi Oktoba,2017 serikali wilayani Manyoni ilitaifisha shehena ya magogo 423 yenye thamani ya shilingi milioni 283,022,000/= yaliyokuwa yamefichwa kwenye mashamba ya Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi,Yahaya Masare katika Kijiji cha Damwelu,kata ya Ipande,wilayani Manyoni,baada ya mmiliki wa mashamba hayo kuyakana kuwa siyo mali yake,licha ya kwamba mmoja wa watu waliokuwa wakishikiliwa na polisi wilayani Manyoni,Hassani Masare ni ndugu yake.

  Akithibitisha shehena hiyo ya mazao ya misitu kutaifishwa,Afisa Ardhi na Maliasili Halmashauri ya Itigi,Rodney Ngalamba alisema baada ya kukamilisha taratibu za kisheria,mtuhumiwa au mshukiwa wa magogo hayo aliweza kulipa serikalini faini ya shilingi milioni 46.

  Kwa mujibu wa afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya ardhi na Maliasili aliweka bayana pia kwamba katika upekuzi iligundulika kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kwa maana baadhi ya shehena katika kiwanda ARIZONA ENTERPRISES kilichopo mjini Itigi kulikuwa na mzigo zidifu wa magogo 297.

  “Kwa hiyo baada ya hapo mzigo huu wa magogo 297 pamoja na mzigo ule uliokamatwa awali shambani vimewekwa chini ya uangalizi wa serikali kwa ajili ya kupigwa mnada hapo baadaye kama taratibu za sheria za misitu namba 14 ya mwaka 2002 inavyoeleza.”alisisitiza Ngalamba.
  Hata hivyo Ngalamba alithibitisha pia kwamba kimsingi magogo hayo yanaonekana ni ya HARIMU ENTERPRISES ambaye ni mshirika mkubwa wa kiwanda cha ARIZONA ENTERPRISES kinachomilikiwa na Yahaya Omari Masare kilichopo Itigi mjini.

  Akizungumzia kuhusu hatua itakayofuata baada ya mtuhumiwa kutozwa adhabau ya faini,Ngalamba aliweka bayana kuwa shehena hiyo ambayo imetaifishwa na serikali itauzwa kwa njia ya mnada na baada ya kupatikana kwa nyaraka zinazohalalisha mzigo uliopo kiwandani,mmiliki wa Arzona Enterprises ataweza kurudishiwa ili aweze kuendelea na shughui zake za uchakataji wa magogo hayo.

  Kuhusu shehena nyingine ya magogo iliyogundulika kwenye kituo cha reli Itigi,afisa huyo alibainisha kuwa magogo hayo bado yapo kituoni hapo na kwamba baada ya kupatiwa nyaraka halali ikiwemo TP,ndipo ataendelea na utaratibu wake ikiwepo kupeleka kwenye soko la kuuzia mazao hayo.

  Kwa upande wake Mwanasheria wa Halmashauri hiyo,Gilbert Modesti Kalanda aliyekuwa mmoja wa wajumbe sita wa tume iliyokwenda Kaliua,alisema akiwa mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo walikwenda Mkoani Tabora,na wilayani Kaliua kwenye eneo ulikotoka mzigo huo la Mpandaline mpakani mwa Kaliua na Katavi.

  Kwa mujibu wa Kalanda baadhi ya mapendekezo ya tume hiyo yalikuwa ni pamoja na kuainisha makosa ya kukutwa na mazao ya misitu bila kufuata sheria na walimtaka mtuhumiwa kulipa shilingi milioni 26,370,000/= ambazo ni gharama za mzigo wote

  “Lakini sheria inaenda mbali zaidi kwamba baada ya kulipa hizo gharama tajwa faini tajwa nini kinatakiwa kifanyike kwenye mzigo ambao unahusika kwenye ufanyikaji wa makosa hayo ya kisheria,tunaelekezwa pia na kifungu namba 95 kinachohusiana na masuala ya Compound tunatakiwa kutaifisha mzigo husika wa mazao ya misitu na kuwa mali ya serikali ambao utauzwa kwa taratibu za kimnada”alisisitiza.
   Mwanasheria wa Halmashauri ya Itigi,Gilbert Modesti Kalanda akitoa maelezo ya sababu zilizofanya magogo 297 kutaifishwa na kusubiri kuuzwa kwa njia ya mnada na serikali ya wilaya ya Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly) 
  baadhi ya magogo yaliyotaifishwa na serikali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 26.3 kutokana na kukiuka taratibu za kisheria zinazosimamia misitu.

  0 0

   Katika kusherehekea miaka 41 ya CCM , Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu ameongozana na wanachama wa CCM wengine kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Irente na kuwakabidhi misaada  ya vitu mbalimbali.
   Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu akiwa ameongozana na baadhi ya wanachama wakikabidhi sehemu ya msaada huo kwa mmoja wa wawakilishi wa kituo hicho kulelea watoto yatima cha Irente ,wilayani Lushoto.
  Baadhi ya Wanachama wa CCM wakiwa sambamba na  Katibu wa CCM  wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu wakiwafariji baadhi ya watoto waliopo kituoni hapo,aidha Muwakilishi wa kituo hicho cha Irente alieleza moja ya changamoto inayokikabili kituo hicho ni chakula,hivyo amewaomba Watanzania kusaidia chochote kile walichonacho kuhakikisha kituo hicho kinaendelea na kutoa huduma ya kuwatunza watoto hao walipo kituoni hapo.

  0 0

  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na  Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili)  wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar es Salaam. 
  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG

  Serikali imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. 

  Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. "Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange. Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
  Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.
  Wageni waliohudhuriwa sherehe hiyo.
  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange akipatiwa huduma za afya wakati aliposhiriki kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
  Huduma za afya zikitolewa bure kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
  Mpiga picha wa Gazeti la Nipashe, Mpochi akipatiwa huduma. Mwandishi na mpiga picha wa Kajunason/MMG akipatiwa huduma.

  0 0

  Katika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo hususani kilimo mashindano ya mpira wa mguu na mpira wa pete UCHUMI CUP yamefunguliwa rasmi kwa ngazi ya robo fainali na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mapema mwishoni mwa wiki.

  Akifungua mashindano hayo kwenye viwanja vya Kigoda Stadium Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi.Upendo Magashi alisema kuwa michezo ni furaha na amani hivyo fursa hiyo itumike kukuza vipaji lakini pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji hususani kilimo ukizingatia Handeni shughuli kuu ni kilimo.

  Aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha vijana wanatumia vipaji walivyonavyo katika kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuendana na falsafa ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU!.

  Kwa upande wake mratibu wa mashindano Bw. Baraka Nkatura alisema kuwa Mashindano yalianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe na kuamua kuyatumia kwenye msimu huu wa kilimo ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiinua kiuchumi.

  “Tunaamini mbali ya kukuza mahusiano baina yetu, tutaweza kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kukuza vipaji vyetu na kujiinua kiuchumi” alisema Mratibu.

  Upatikanaji wa timu zilizoshiriki Robo fainali ulianzia ngazi ya Tarafa tarehe 20/11/2017 ambapo, Tarafa 7 zilishiriki kutoa timu mbilimbili zilizoingia kwenye robo fainali na timu 2 alikwa moja kutoka jamii ya wamasai na ya pili kutoka Kabuku. Jumla ya timu 18 zimeingia ngazi ya mashindano ya robo fainali.

  Aidha, baada ya kupatikana timu 18 kutoka kila Tarafa iliundwa mechi ya makundi kwa timu za ( Mjini Chanika kundi A, Misima B, Mkata C na Kabuku D). washindi wawili waliopatikana katika kila kundi waliingia robo fainali na kufanya timu shiriki 8.

  Mpaka tarehe 4/2/2018 timu 4 zimecheza robo fainali , mchezo kati ya kurugenzi Fc na Nyikani walitoana 2-1, Ambapo Kurugenzi FC iliwafunga Nyikani FC bao 2 kwa mojo. Dakika ya 5 mchezaji John kutoka Nyikani FC alifunga goli la kuongoza na baadae mchezaji Nguruko kutoka Kurugenzi FC alisawazisha goli dakika ya 30 kabla ya mapumziko. Mchezaji Peter aliifungia Kurugenzi FC kwa shuti nje ya 18 Dakika ya 70 na kufanya bao la pili.

  Mechi zinazocheza Robo fainali kwa lengo la kupata washiriki wa nusu fainali na fainali ni Kurugenzi FC vs Nyikani FC, Vibaoni United vs Kwamkono FC, Mtazamo United vs Ndolwa United na Umoja FC Vs Kwapara FC ambapo mwisho wa mashindano ya robo fainali ni 6/2/2018. Nusu fainali itachezwa tarehe 8-9/2/2018 na Finali itachezwa tarehe 11/2/2017.

  Mashindano haya yamebeba kauli mbiu ya “Kipaji changu mtaji wangu” mbapo Mshindi wa kwanza atapa zawadi ya Kombe, pesa taslimu Tsh.500,000/=,medali za dhahabu, jezi seti moja na mipira mitatu. Mshindi wa pili atapata pesa taslimu Tsh.300,000/=, medali za fedha(Silva), jezi seti moja, mpira mmoja. Na mshindi wa tatu pesa taslimu Tsh.200,000/=,medali za shaba (Brons), jezi seti moja na mpira mmoja.

  Washindi wa mpira wa Pete , mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu Tsh.500,000/=, mshindi wa pili Tsh.300,000/= na mashindi wa tatu Tsh.200,000/=.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
   Wachezaji wa Kurugenzi FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano dhidi ya Nyika FC
   Timu ya mpira ya Nyika FC wakiwa tayari kuikabili timu ya Kurugenzi FC
   Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi wa kwanza kushoto, waratibu wa michezo wawili upande wa kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wachezeshaji wa mpira kabla ya mechi kuanza
   Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifuatiwa na waratibu WA michezo wakisalimiana  na Timu na uongozi wao kabla ya mechi kuanza
   Mechi Kati ya Kwamkono United na Vibaoni united ikiendelea
   Timu Ya Kwamkono FC wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa michezo
   Wachezaji wa timu ya Vibaoni United wakiwa tayari kukabiliana na Vibaoni
   Mratibu WA michezo Bw Baraka Nkatula akizungumza na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ngazi ya Robo fainali
  Kaimu katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifungua mashindano kwa kuzungumza na wachezaji

  0 0

    Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto anayepiga makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Husein Mwinyi wakati alipokuwa akiandika jambo katika hotuba yake.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mara baada ya kufungua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.

   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mapinga(hawaonekani pichani) waliokuwa wakiwasilisha kero mbalimbali za ardhi wakati alipokuwa akirejea jijini jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani.
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makomandoo wa JWTZ ambao walishiriki katika mazoezi ya Kijeshi kabla ya ufunguzi wa kituo hicho.
   Kikundi cha Ngoma za asili cha Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Mafunzo maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Ratlan Pardede, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Balozi Ratlan Pardede, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Balozi Ratlan Pardede na Viongozi wa Serikali baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0


  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Hanang, Sarah Msafiri  akikagua gwaride wakati  alipofunga Mafunzo ya Mgambo katika tarafa ya Bassotu wilayani humo mwishoni mwa wiki. (Picha kwa Hisan ya New Hanang Photo Studio)

  0 0

  MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,(kulia)akielekeza jambo baada ya kuonyeshwa ramani ya ghala la korosho ambapo linatarajia kujengwa huko Mkuranga, wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa ghala hilo .(Picha na Mwamvua Mwinyi)   Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

  MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha inamlipa ,malipo ya awali kiasi cha sh.bilioni 1.6, mkandarasi wa ghala la kuhifadhia korosho wilayani Mkuranga.

  Alitoa agizo hilo ,wilayani Mkuranga alipotembelea ujenzi wa ghala hilo linalojengwa na kampuni ya BQ Contractors Ltd .Alieleza kabla ya ujenzi waliingia mkataba wa kulipa asilimia 30 ya malipo ya awali ya ujenzi wa ghala hilo la kisasa ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.5 hadi kukamilika kwake.

  Aidha Ndikilo alisema, kampuni hiyo ilitoa malalamiko kuwa zimepita siku 52 wakiwa hawajapewa hata shilingi moja kwa ajili ya ujenzi huo hali ambayo inasababisha ujenzi huo kuwa mashakani kukamilika kwa wakati.

  “CBT ihakikishe inatoa fedha hizo ndani ya wiki hii, bodi ya korosho ambao ndiyo wamiliki wa ghala hilo na endapo watashindwa kufanya hivyo atawapeleka kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya hatua zaidi";

  "Mkurugenzi wa bodi hiyo itabidi wakutane Dodoma kwa ajili ya kueleza ni sababu gani inawafanya washindwe kumlipa mkandarasi huyo,” alisema Ndikilo.Alisema serikali kwa kushirikiana na bodi ya korosho walikubaliana kujenga ghala hilo ili kuwe na ghala moja kwa kila wilaya tatu za Mkuranga, Kibaha na Rufiji ambako ndiko zinalimwa korosho nyingi.

  Ndikilo alieleza lengo la kuwa na ghala la uhakika ni kufanikisha mfumo wa stakabadhi ghalani.“Kuanzia msimu ujao korosho zote zitauzwa kwenye ghala moja kubwa badala ya kutumia maghala ya watu binafsi ama ya vyama vya msingi vya ushirika ambao wanaonekana kufanya hujuma kwa kuweka korosho ambazo hazina viwango ,:;ambapo kwa msimu huu tatizo lilikuwa kubwa sana,” alifafanua Ndikilo.

  Hata hivyo ,alieleza kutotolewa fedha hizo kutasababisha ujenzi huo kutokamilika kwa wakati kutokana na hali ya mvua za masika unaokuja ambazo zitasababisha ujenzi huo kushindwa kufanyika katika kipindi lengwa.Nae mwakilishi wa bodi ya korosho Japhari Matata alikiri kucheleweshwa kwa fedha hizo .Alisema kwasasa taratibu za kuzipata fedha hizo zinaendelea ili kumpatia mkandarasi huyo.

  Matata alisema atalifikisha suala hilo kwa wahusika kwa ajili ya kuhakikisha linafanikiwa ili ujenzi huo ukamilike mwezi wa nane kipindi ambacho ndicho ilipangwa ukamilike.Awali akitoa taarifa kuhusu ujenzi huo, meneja wa maendeleo ya biashara wa kampuni hiyo Hilu Bura, alisema changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya ujenzi huo ambao ulianza Oktoba mwaka jana.

  Alitaja changamoto nyingine ni eneo hilo kuwa na maji kwa wingi hivyo endapo fedha zitachelewa kutasababisha kujenga kipindi cha mvua za masika ambacho kinakaribia kuanza.Bura alimuomba mkuu wa mkoa huyo wa Pwani kuwasaidia ili waweze kupatiwa fedha za awali.

older | 1 | .... | 1509 | 1510 | (Page 1511) | 1512 | 1513 | .... | 1898 | newer