Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 149 | 150 | (Page 151) | 152 | 153 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
  Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
  Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na kulia kwa Mengi ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto) akiwatambulisha baadhi ya maofisa katika kitengo hicho katika hafla hiyo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akishikana mikono na Meneja Uhusiano wa NBC, Makyalen Marealle katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi wa kitengo hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.

  0 0


  DEFENDING FREEDOM OF EXPRESSION AND INFORMATION

  One year on, still no Justice for Daudi Mwangosi

  By Paul Kimumwe

  Today (2nd September 2013,) marks exactly one year since journalist Daudi Mwangosi was brutally murdered at the hands of the Tanzania Police. His only crime was being a journalist. As the sole breadwinner, his demise meant a new life of suffering for his dependants.

  The widow, Mrs. Itika Mwangosi is yet to cope with the loss, having to look after their four children. For Bethseba (10) and Herzegovina (13); they still ask the mother when Dad will be back. It is only Nehemia (17) who come to the rescue and try to explain the Dad is in heaven with the angels. At two, Mworia is just too young to understand anything.


  To the media fraternity, the late Mwangosi was to become only the first. Their honeymoon had officially ended. Many more journalists were soon to be consistently attacked. A community radio journalist Issa Ngumba was found dead in a forest in Kakonko, in the northwestern region of Kigoma, on 8 January, three days after he went missing.

  It was clear from the injuries on his body that he was murdered. A reporter for Radio Kwizera, the 45-year-old Ngumba left his home on the evening of 5 January to look for medical plants for his second job as a traditional healer. After he was reported missing, police and civilian volunteers searched intensively until his body was found in nearby Kajuluheta Forest.

  A month earlier, on the night of Tuesday 4th December 2012, Shaaban Matutu, a journalist with Free Media Limited - publishers of the Tanzania Daima newspaper – had been shot by police. This happened at Matutu’s home in Kunduchi Machimbo after an alleged altercation with police officers, one of them firing and hitting Matutu in his left shoulder.

  It was however the attack on Absalom Kibanda, the Chairman of the Tanzania Editors’ Forum in March 2013 that sent a strong message of intent and put the recent crackdown against the media and freedom of expression into context. The June 2012 indefinite ban on Mwanahalisi and brutal attack against Dr. Stephen Uliomboka, had seemed like isolated incidents.

  With the last 12 months, Tanzania has gone from the beacon of hope in the region, which registers some of the worst attacks and violations against freedom of expression, to become one of the worst to be a human rights defender. After the tramped charges curtsey of the draconian laws failed to bully critical voices into submission, it seems the attention was to employ physical attacks and assaults.

  For a country going through a constitutional review process, these attacks on the media and other critical voices are counterproductive as they have a chilling effect on any meaningful debate of the issues raised by the draft constitution and active involvement of the citizens in the subsequent democratic processes, including elections.

  For all these attacks, no one has been held accountable, despite the various promises by the state, including the personal pledge by president after the attack Mr. Kibanda. The journalists, like all citizens have a right to protection from, and prevention of these attacks, and the state has a duty to thoroughly investigate the reported cases of abuse and violations of these rights to their logical conclusions and bring the culprits to book.

  The right to freedom of expression is not a preserve of the media alone. Any violations and attacks on the media have far reaching consequences on the enjoyment of all other rights by the citizens. The government of Tanzania must demonstrate its commitments to the protection of freedom of expression as proposed in the draft constitution by first; ensuring that journalist are safe from all kinds of attacks; apprehend and hold all those implicated in these attacks, including its own officers accountable; as well as allowing for meaningful dialogue.

  The time for political rhetoric is over. For Mrs. Itika Mwangosi and children, the wait to see justice for those responsible for killing her husband should not be a lifelong experience. The same applies for Dr. Uliomboka, Kibanda, Matutu and others who have been brutally attacked in the recent past.

  Mr. Kimumwe works with ARTICLE 19 Eastern Africa, a Human Rights Organisation

  0 0

   Mdau Fredy Anthony ambaye ni Head of Group Research and Product Development wa Tone Multimedia Group , akiwa Nje ya ukumbi wa Dewan Tun Canselor   Mara baada kupata shahada yake ya pili  (Master of Business administration - Multimedia Marketing)   katika Chuo kikuu cha Multimedia kilichopo Malaysia.
  Mdau Fredy Anthony akiwa katika Picha ya Pamoja na Marafiki walio msindikiza katika Mahafali hayo.

  0 0

  Airtel Yatosha inazidi kupamba moto. Zimebaki siku CHACHE SANA kwa wewe MTEJA wa Airtel kuibuka mshindi wa Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha iliyojengwa na Shirika la nyumba la taifa (NHC) iliyopo maeneo ya kigamboni jijini Dar es saalam.

  Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando amesema “Siku ya Alhamisi tarehe 5 mwezi wa 9 ndio siku inayosubiriwa kwa hamu; ambapo tutapata mshindi wa nyumba ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha”

  Wewe mteja wa Airtel Yatosha bado una nafasi ya kuibuka mshindi! Ni rahisi. Piga *149*99# sasa na ujiunge na kifurushi chochote cha SIKU, WIKI AU MWEZI cha Airtel Yatosha na moja kwa moja utaingia kwenye droo ya kushinda. Kumbuka, pia kuna Tsh milioni 1 kushindaniwa kila siku. Usilaze damu! Jiunge zaidid na Airtel Yatosha, uongeze nafasi zako zakushinda! Alidokeza bw, Mmbando

  Airtel Yatosha. Na BADO!!
  Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari.

  0 0

   Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold akimkabizi helmet na pikipiki Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya kwa ajili ya Afisa Wilaya wafuatiliaji wagonjwa wa Malaria, katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar. 
   Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akimkabizi funguo ya pikipiki mmoja wa Afisa Wilaya wa ufuatiliaji wagonjwa wa Malaria, huko  katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanziba  
  (Picha zote na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
    Mwakilishi wa Shirika la Misaada la  Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold, akielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinazochukuliwa juu ya kutokomeza Malaria Zanzibar (kulia) Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, Afisa wa RTI kanda ya Afrika Mashariki Volkan Cakir kabla yakukabidhi pikipiki 10, huko katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya maafisa mbalimbali wa Wizara ya Afya wakimskiliza Mwakilishi wa Shirika la Misaada laMarekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold (hayupo pichani) katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar.
   
  ========  =======  =========
  USAID yakabidhi pikipiki 10 kufuatilia malaria Zanzibar

  Na Salum Vuai, Maelezo.

  MFUKO wa Rais wa Marekani unaoshughulikia mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria katika nchi mbalimbali za Afrika (PMI), umekabidhi pikipiki kumi kwa Wizara ya Afya Zanzibar, zitakazotumika kufuatilia kesi za malaria katika wilaya zote Unguja na Pemba.

  Hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo zenye thamani ya shilingi milioni 63 amabzo ni maalumu kwa ajili ya Kitengo cha Kupambana na Malaria Zanzibar, ilifanyika jana huko Wizara ya Afya Mnazimmoja na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa wizara hiyo.

  Mwakilishi wa Shirika la Misaada la  Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold, alisema pikipiki hizo zitasaidia kazi za kufuatilia kesi za malaria majumbani, ambako familia zitapimwa ugonjwa huo na kupatiwa tiba inapobidi.

  “Hii ina maana kuwa, maofisa wenu wa malaria mawilayani, wataongeza uwezo wao katika kufuatilia, kuchunguza, kutibu pamoja na kukinga ugonjwa huo kwa kuhakikisha kwamba wananchi wanaogundulika nao wanatibiwa haraka iwezekanavyo, na kusaidia kuvifanya visiwa vya Zanzibar kutokuwa na malaria”, alisema.

  Rebold alieleza kuwa, tangu PMI ilipoanzishwa mwaka 2006, pamoja na washirika wake wengine ikiwemo RTI, wmaefanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya Zanzibar na Tanzania Bara kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa malaria.

  Alifahamisha kuwa, misaada ya kitaalamu na ya kifefha kutoka mfuko huo wa Rais wa Marekani, imeisaidia Zanzibar kupunguza ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 25 mwaka 2006 hadi kufikia chini ya asilimia moja mwaka 2009, na kwamba mafanikio hayo yamekuwa endelevu.

  “Mafanikio haya ni kielelezo cha uhusiano na ushirikiano madhubuti kati ya PMI na Serikali ya Zanzibar, sambamba na uongozi imara wa serikali yenu”, alieleza Rebold.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, alisema kwa kuwa kazi ya kupambana na malaria inahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara, pikipiki hizo zitawarahisishia maofisa wa kitengo cha malaria mawilayani kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na wepesi.

  Alisema msaada huo ni faraja kwani utatia fursa kwa watu wanaogua malaria hasa walioko vijijini, kupatiwa tiba kwa wakati pamoja na watu wanaoishi nao kuchunguzwa ili kubaini kama wameathirika na kuwezesha kutibiwa kwa wakati.

  Kwa niaba ya serikali, Dk. Sira alishukuru kwa msaada huo na mingine inayotolewa na PMI, RTI na USAID, ambayo alisema imeifanya Zanzibar kupunguza malaria kwa kiasi kuwa na kuwa mfano kwa nchi nyengine.

  Mapema Afisa wa RTI kanda ya Afrika Mashariki Volkan Cakir, aliipongeza Zanzibar kwa hatua kubwa iliyopiga na kupunguza malaria kwa kiwango cha chini ya asilimia moja, na kusema taasisi yao inaona fahari kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO
  29 AGOSTI 2013 

  0 0
 • 08/30/13--07:47: CCM :TUTAWASAIDIA WAZEE
 •  Baadhi ya wawakilishi wa Mtandao wa Wazee wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma leo tarehe 30 Agosti 2013.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mmoja wa wawakilishi wa Mtandao wa Wazee Bibi Koku , Wazee hao walifika Makao Makuu ya CCM kuja kuzungumza madai ya mafao yao ambayo waliahidiwa na serikali.

  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete attends the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013. Left are members of his delegation, Professor Rwekaza Mukandala, Vice Chancellor of the University of Dar es salaam and Profesor Joseph Semboja, Principal Uongozi Institute.
  President Jakaya Mrisho Kikwete attends the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013. Right is the host and Co-Chairman of the Retreat, Mr Manuel Jose Barroso, President of the European Commission, followed by Ms Valerie Amos, UN Under-Secretary-General of for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator.
  President Jakaya Mrisho Kikwete walks with Ms Kristalina Georgieva, the European Commissioner for International Cooperation and Humanitarian Aid, shortly before the start of the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.
  President Jakaya Mrisho Kikwete with Mr Manuel Jose Barroso, President of the European Commission, at the start of the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.
  President Jakaya Mrisho Kikwete walks with Dr Jeffrey Sachs, Director of Earth Institute at the Columbia University, as they head to the meeting hall to attend the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.STATE HOUSE PHOTOS.

  0 0


  Na Ali Issa –Maelezo Zanzibar.30/8/2013.


  Wakulima wa Bonde la Bubwisudi Wilaya ya Magharibi Unguja wame iomba   Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa utaratibu wa kununua Mpunga  wa wakulima wa Bonde hilo ili wakulima waweza kufaidika na matunda ya 
  kilimo hicho kwa kupata pesa zitakazo wasaidia katika mahitaji yao 
  ya kila siku.  Hayo yamesemwa huko Bumbisudi na Diwani wa wadi hiyo Masuod Abrahaman   
  Masuod wakati wa uzinduzi wa Maazimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya    
  Zanzibar yalio fanyika  katika wadi ya Bubwisudi Wilayani humo.  Wamesema kumekuwa na mpunga wakutosha katika baadhi ya majumba ya
  wakulima ambao walilima kwa kujituma katika msimu uliopita  na hatimae
  kufanikiwa kupata mavuno mazuri, hivyo baadhi ya  wananchi wanahitaji
  kuuza mpunga kupata pesa ili ziwasaidie katika maisha yao  lakini
  hawajui nani wa muuzie bidhaa hiyo.  Wamesema bidha wanayo ya kutosha hivyo,iwapo Serikali itaweza kuandaa
  mpango huoitawasaidia wakulima hao kuweza kupata pesa za matumizi na
  kujikwamuwa katika mahitaji yao.  “Natoa wito kwa seriakali waweke utaratibu wa kununua mpunga kwa
  wananchi, kwani huu mpunga upo kwa baadhi ya wakulima wanataka kuuza  lakini hawamjuwi nani wamuuzie”,alisema Diwani huyo.
  Aidha diwani huyo alisema kua hali ya uchumi katika shehia hiyo ni
  nzuri kwani wananchi wa  Bubwisudi wote  ni wakulima na wanajituma
  ipasavyo kwa vile kilimo ni ajira wanayo itegemea.  Akielezea changamoto zinazo wakabili wakulima hao walisema kua
  kumekuwa na ada kubwa ya malipo ya umeme katika mashamba ya mpunga ya  umwagiliaji maji haliambayo hushindwa kulipa umeme huo ipasavyo.
  “Tunalipa elfu 30 kwa mwezi ploti moja ya mpunga wa umwagiliaji hiki
  ni kiwango kikubwa, tunaomba tusaidiwe ili kukidha mahitaji yetu”,
  alisema Bi Fatuma Daud Katibu wa Sheha Shehia ya Bubwisudi.  Wakulima hao walimueleza Diwani kua, wana kabiliwa na tatizo la wizi
  wa mazao, na wana nchi wahapo hadi sasa bado hawajaweza kuazisha
  Polisi jamii suala ambalo lingeweza kusaidia kupambana na vitendo
  vibaya vya wizi na uhalifu.  Mapena diwani katika shamra shamra hizo alifungua kituo cha Taarifa na
  maarifa za Ukatili wa Kijisia na unyanyasaji ili kukuza usawa wajinsia
  kwa watoto na kinamama, jambo linaloonekana kuenea kila pembe ya
  Zanzibar.

  0 0

  Tiketi za uzinduzi wa LULU Bado zinapatikana na Zitauzwa Mlangoni Kwa Gharama za shilingi Elfu 30 tu. UZINDUZI UNAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY KUANZIA SAA MOJA JIONI.

  usikose wahi sasa na tiketi ni chache.Njoo Uone mapinduzi ya kweli kwenye tasnia ya filamu.Mzigo mzma unasimamiwa na Proin Promotions Limited.

  0 0


  0 0

  Mashine maalum ya kufulia nguo aina ya HITACHI iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda kwa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa na kukabidhiwa kituoni hapo na Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda leo tarehe 30, Agosti 2013. Msaada huo wenye thamani ya Tshs. Milioni moja na nusu (1.5) ni ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa alipotembelea kituoni hapo mapema mwaka huu.
  Ndudu Charles Kanyanda Katibu wa Jimbo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi akimkabidhi Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala mashine maalum ya kufulia nguo iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa kituo hicho leo tarehe 30, Agosti 2013. 
  Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika wamiliki wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa akitoa shukrani zake za dhati kwa Waziri Mkuu kupitia kwa Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda kwa msaada huo wa mashine ya kufulia. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

   Kaimu Mhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bruno Kawasange akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji na mafanikio mbalimbali waliyoyapata tangu kuundwa kwake mwaka 1959 chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari  leo Jijini Dar es Salaam na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.

  Kaimu Mhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bruno Kawasange akiwaonesha waandishi wa habari jarida linaloeleza mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro


  Picha na Frank Mvungi-MAELEZO


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini(GEPF)Bw. Festo Fute akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni(VSRS)kwa watu wote ili kupambana na majanga mbalimbali, Katika mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.


  Picha na Frank Mvungi-MAELEZO.  ==========   ========  =========
  MFUKO WA AKIBA YA WAFANYAKAZI SERIKALINI (GEPF)


  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUKO WA AKIBA GEPF


  1.0         UTANGULIZI

  Mfuko wa Akiba GEPF ulianzishwa chini ya sheria Namba 51 ya mwaka 1942 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 (Re 2002). Madhumuni ya Mfuko hapo awali ilikuwa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikali kuu ambao utumishi wao  ilikuwa si wa masharti ya kudumu na malipo ya pensheni. Mfuko huu toka kuanzishwa mwaka 1942 ulifanya kazi zake chini ya Wizara ya Fedha mpaka kufikia mwaka 2004 ambapo Mfuko ulipata Bodi yake na Menejimenti na kuanza kufanya kazi kama taasisi ya umma inayojitegemea.


  2.0         MAGEUZI KATIKA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII

  Sekta ya hifadhi ya jamii imepitia mageuzi mbalimbali katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mageuzi hayo yamechochewa na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya jamii ya mwaka 2003. Sera hiyo imeainisha changamoto mbalimbali za sekta. Matokeo ya sera hiyo ni kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kusimamia na Kuratibu Sekta ya Hifadhi ya Jamii  kwa sheria Na. 8 ya mwaka 2008. Sheria hiyo imekuja na mageuzi makubwa katika sekta ya hifadhi ya jamii ambapo pamoja na mambo mengine imefungua milango kwa Mifuko iliyopo nchini kusajili wanachama bila mipaka kama ilivyokuwa hapo awali. Lakini pia sheria hiyo inaruhusu kuwafikia  watu wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato bila kujali aina ya ajira.


  3.0         WANACHAMA WA MFUKO

  GEPF ni Mfuko unaoendeshwa kwa mfumo wa akiba tofauti na Mifuko mingine inayoendeshwa kwa mfumo wa bima. Hivyo wanachama wa GEPF wanatokana na waajiriwa wote wanaofanya kazi kwa mikataba na wale wote ambao ajira zao hazikidhi kulipwa pensheni. Mageuzi ya sekta yametoa fursa ya kusajili watumishi bila mipaka, hivyo waajiriwa wote walio katika masharti ya mikataba wanaweza kujiunga na Mfuko huu, Lakini pia wale wote waliojiajiri wenyewe wanaweza kujiunga na GEPF chini ya mpango maalum ujulikanao kama Mpango wa Hiari wa Kujiwekea Akiba ya Uzeeni maarufu kama VSRS.

  Idadi ya wanachama imeongezeka kutoka wanachama 30,227 mwaka 2008/09 hadi kufikia wanachama 60,030 mwezi Juni, 2013 hii ni kutokana na  jitihada za Mfuko kuhakikisha watu wote wenye uwezo wa kuweka akiba wanafanya hivyo.

  Jedwali Na. 1: Ongezeko la idadi ya wanachama kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita

  Mwaka

  2008/09

  2009/10

  2010/11


  2011/12

  2012/13

  Wanachama

  30,227

  35,279

  41,879


  52,670

  60,030


                        Chati Na. 1: Ongezeko la wanachama katika kipindi hicho

                           4.0         MAENDELEO YA MFUKO


  Maendeleo ya Mfuko hupimwa kwa kuangalia ongezeko la thamani ya Mfuko. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita Mfuko umeweza kukua kwa kasi kubwa, hii inatokana na ongezeko la michango ya wanachama na kufanya uwekezaji wenye tija. Thamani ya Mfuko imeongezeka kutoka Sh. 72.55 bilioni mwaka 2008/09 hadi kufikia kiasi cha Sh. 198.30 bilioni mwezi Juni, 2013.


  4.1       Jedwali Na. 2: Ongezeko la thamani ya Mfuko kwa kipindi cha  miaka mitano


  Mwaka

  2008/09

  2009/10

  2010/11


  2011/12

  2012/13

  Thamani (Bilioni)

  72.55

  91.28

  119.40

  154.50

  198.30                        Chati Na. 2: Ongezeko la thamani ya Mfuko

                       
  4.2    Uwekezaji wa fedha za wanachama


  Ili kulinda thamani ya michango ya wanachama Mfuko hufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali yaliyo salama na yanayotoa faida kubwa. Mfuko huwekeza  kwenye Amana za Serikali, Makampuni yaliyo orodheshwa kwenye soko la mitaji (DSE),  Uwekezaji wa muda maalum kwenye mabenki ya biashara, Mikopo, Hati fungani na Majengo. Vitegauchumi vya Mfuko viliongezeka kutoka Sh. 64.94 bilioni mwezi Juni, 2009 hadi kufikia Sh. 179.68 bilioni mwezi Juni, 2013. Vilevile mapato yaliongezeka kutoka Sh. 5.48 bilioni mwezi Juni, 2009 hadi kufikia Sh. 18.25 bilioni mwezi Juni, 2013.


  Jedwali Na. 3: Ongezeko la mapato ya uwekezaji kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita


  Mwaka

  2008/09

  2009/10

  2010/11


  2011/12

  2012/13

  Vitegauchumi (Bilioni)

  64.94

  82.47

  101.29

  137.75

  179.68

  Mapato (Bilioni)

  5.48

  7.69

  9.81

  11.54

  18.25  Chati Na. 3: Ongezeko la mapato ya uwekezaji katika asilimia (%)

                         4.3   Ongezeko la michango ya wanachama


  Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita michango ya wanachama imekuwa inaongezeka kwa kasi. Hii inasaidia katika ukuaji wa Mfuko moja kwa moja lakini pia kuongeza mapato yatokanayo na uwezekezaji.


  Jedwali Na. 4: Ongezeko la michango ya wanachama  kwa kipindi cha miaka mitano


  Mwaka

  2008/09

  2009/10

  2010/11


  2011/12

  2012/13

  Mapato (Bilioni)

  13.79

  16.32

  25.71

  30.15

  37.29

                                                                                                                                                       


  Chati Na. 4: ongezeko la michango  ya wanachama katika asilimia (%)
  5.0         ULIPAJI WA MAFAO KWA WANACHAMA


  Mfuko wa GEPF hulipa mafao ya mkupuo (lump-sum) kwa wanachama wake kulingana na aina ya ajira zao. Wengi wa wanachama wa mfuko huu ni wafanyakazi wa mikataba, hivyo pindi wamalizapo mikataba yao hulipwa mara moja. Ulipaji wa mafao huzingatia michango kutoka kwa mwanachama na mwajiri pamoja na faida anayopewa mwanachama kila mwaka kutokana na mapato ya uwekezaji. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13 jumla ya kiasi cha TZS. 5.25 Bilioni kililipwa kwa wanachama ikiwa ni mafao yao.  6.0         MPANGO WA HIARI WA KUJIWEKEA AKIBA YA UZEENI (VSRS)


  Hii ni Skimu maalum ambayo imebuniwa mwaka 2009 ili kutoa fursa kwa watu wote kuweka akiba ambayo itawasaidia kupambana na majanga mbalimbali ikiwemo uzee. Mpango huu ni matokeo ya mageuzi katika sekta ambayo yanamtaka kila mtu mwenye uwezo wa kuzalisha kipato anaweza kujiunga na Hifadhi ya Jamii. Kupitia Skimu hii kila mtu anaweza kujiunga, awe mkulima, mjasiliamali, sekta ya usafiri na makundi mengine.


  GEPF ulikuwa Mfuko wa kwanza kuanzisha Skimu ya aina hii hivyo mafanikio yaliyofikiwa kwenye Skimu hii ni makubwa sana ukilinganisha na Mifuko mingine. Skimu hii imeundwa kwa kuzingatia mazingira rafiki ya makundi yote ya uzalishaji. Kwa mfano uchangiaji wa michango haujali kiwango maalum wala muda maalum, ni moja ya muundo unaomwezesha kila mtu kwa kipato chake kuweza kujiwekea akiba. Wanachama wanawekewa faida kila baada ya miezi sita pia wana fursa ya kutumia mpaka 50% ya akiba yao pindi wanapopata dharura.  6.1                Mafanikio katika Skimu ya Hiari (VSRS)


  Toka kuanzishwa kwake Novemba, 2009 Skimu hii imefanikiwa kusajili wanachama 18,700 kufikia Juni, 2013.  Jumla  ya akiba za  wanachama  zilifikia kiasi  cha  TZS. 3.05Bilioni katika kipindi hicho.


  Jewali Na. 5: Mchanganuo wa usajili wa wanachama wa VSRS hadi Juni, 2013;

                       

  Mwaka

  Nov. 09 – Jun. 10

  2010 - 2011

  2011-2012

  2012-2013

  JUMLA

  Usajili

  1,644

  4,911

  6,688

  5,457

  18,700  Chati Na. 5: Usajili wa wanachama wa VSRS  Jedwali Na. 6: Mchanganuo wa michango ya wanachama wa VSRS hadi Juni, 2013


  Mwaka

  Nov. 09 – Jun. 10

  2010 - 2011

  2011-2012

  2012-2013

  JUMLA

  Michango (Milioni)

  59.48

  311.44

  840.76

  1,839.12

  3,050.80  Chati Na. 6:  Mchanganuo wa michango wa wanachama wa VSRS;  6.2                Mgawanyiko wa wanachama kisekta


  Katika jumla ya wanachama 18,700 walisajiliwa mpaka kufikia June, 2013 mgawanyiko wao kisekta ni kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 7.


   Jedwali Na. 7: Mgawanyiko wa wanachama wa VSRS kisekta


  Sekta

  Biashara

  Kilimo na ufugaji

  Usafirishaji

  Waajiriwa

  JUMLA

  Wanachama

  7,480

  6,545

  1,683

  2,992

  18,700  Chati Na. 7:  Mgawanyiko wa wanachama wa VSRS kisekta
  7.0         CHANGAMOTO


  Pamoja na mafanikio yaliyoainishwa hapo juu, Mfuko umekuwa unakabiliana na changamoto mbalimbali ambazo ni;


  i)             Kupitwa na wakati kwa sheria inayoongoza Mfuko ambayo inafanyiwa mapitio hivi sasa


  ii)            Ufahamu mdogo wa watu kuhusu Mfuko


  0 0  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji Ujangili kutoka Mfuko wa Kuhifadhi Wanyama Pori Bw. Paul Sarakikya akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mipango ya serikali katika kupambana na ujangili na mikakati ya kulinda hifadhi za wanyama pori nchini, Katika mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. Picha na Frank Mvungi-MAELEZO.
  ========  =========  ==========


  MUHTASARI KUHUSU SHUGHULI ZA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMAPORI TANZANIA


  1.0               UTANGULIZI

  Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Protection Fund, TWPF) ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1978 baada ya kukifanyia marekebisho kifungu cha 69 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori (Wildlife Conservation Act) Na. 12 ya mwaka 1974. Marekebisho hayo yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 21 la tarehe 22 Mei, 1981.


  Baada ya kufanyika mapitio ya Sheria ya Wanyamapori Na. 12 ya mwaka 1974, sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya sasa Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura ya 283) inabainisha uwepo wa Mfuko kisheria katika kifungu cha 91(1). Lengo la kuwa na Mfuko ni kuiongezea Idara ya Wanyamapori uwezo wa kifedha za kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa wanyamapori. Serikali inatambua kuwa ulinzi wa wanyamapori unahitaji fedha nyingi na fedha kutoka Hazina hazikidhi mahitaji yaliyopo.


  2.0               MAJUKUMU YA MFUKO

  Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(2) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009, malengo ya Mfuko (TWPF) ni kuwezesha na kusaidia shughuli wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa hususani katika maeneo yafuatayo:-

  (i)      Uzuiaji ujangili na usimamizi wa sheria;

  (ii)    Uendeshaji wa Kikosi cha Ulinzi wa Wanyamapori;

  (iii)   Uhifadhi wa wanyamapori;

  (iv)   Kusaidia maendeleo ya jamii zinazozunguka maeneo yaliyohifadhiwa;

  (v)    Utoaji wa elimu, mafunzo na uhamasishaji kuhusu masuala ya wanyamapori;


  3.0               USIMAMIZI WA MFUKO

  3.1    Bodi ya Wadhamini ya Mfuko

  Mfuko unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini (Board of Trustees) kwa mujibu wa kifungu cha 92 cha Sheria tajwa. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko anateuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Wajumbe wengine wa Bodi ambao huingia kutokana na nyadhifa zao ni Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka za Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ambaye ni Katibu wa Bodi. Aidha, Wajumbe wengine wawili wa Bodi huteuliwa na Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii. Bodi husimamia Mfuko katika vipindi vya miaka mitatu. Bodi iliyoko sasa ilianza kufanya kazi Juni 2011 na inatazamiwa kumaliza kipindi chake ifikapo Juni 2014.  4.0                 PROGRAMU ZILIZO CHINI YA MFUKO

  Mfuko unagharamia uendeshaji wa program mbili zinazohusika na utoaji wa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kwa jamii ndani na nje ya nchi. Programu hizo ni “Malihai Clubs of Tanzania” na Majarida ya Kakakuona na “Tanzania Wildlife”


  4.1                                 Malihai Clubs of Tanzania (MCT)

  “Malihai Clubs of Tanzania” ni Programu ya Serikali chini ya Idara ya Wanyamapori inayoshughulika na utoaji wa elimu ya Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira katika Taasisi za Elimu (Shule za Msingi, Kondari, Vyuo). Pia kwa mwanachama mmoja mmoja na makundi ya jamii hasa wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa mapori yaliyohifadhiwa. Kwa kupitia program hii elimu ya uhifadhi kwa umma kwa vitendo katika Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo na Vijiji hususan vile vinavyopakana na maeneo yenye wanyamapori huenezwa.

  Kwa sasa, MCT inaendesha shughuli zake katika Kanda tatu ambazo ni:

  a.    Kanda ya Kaskazini – yenye makao yake makuu katika Jiji la Arusha

  b.    Kanda ya Ziwa – yenye makao yake makuu katika Jiji la Mwanza

  c.    Kanda ya Nyanda za Juu Kusini – yenye makao yake makuu Mbarali Mkoani Mbeya.


  4.2                                 Majarida ya kutoa elimu ya uhifadhi na kukuza Utalii

  Mfuko unachapisha majarida mawili: Kakakuonaambalo ni la Kiswahili na Tanzania Wildlife (la Kiingereza). Majarida haya ni nyenzo muhimu kwa kueneza elimu ya uhifadhi kwa umma wa Tanzania na kutangaza utalii ndani na nje ya nchi. Pia, ni jukwaa la wataalam mbalimbali wa uhifadhi wa Maliasili, mazingira, utalii wa ndani na nje ya nchi. Pia, ni jukwaa la wataalam mbalimbali wa uhifadhi wa Maliasili, mazingira, Utalii na utamaduni kubadilishana mawazo, kuelezea uzoefu na utalaam wao. Majarida yote mawili huchapishwa mara nne kwa mwaka. Nakala 6,000 (nakala 3,000 za jarida la Kiswahili la Kakakuona na nakala 3,000 za jarida la Kiingereza la Tanzania Wildlife) huchapishwa kila robo ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2012-2013, jumla ya nakala 24,000 za majarida zilizochapishwa na kusambazwa katika vituo vya uuzaji ambavyo viko sehemu mbalimbali nchini katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, mahotelini, kwenye baadhi ya vituo vya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.


  5.0                  VYANZO VYA MAPATO YA MFUKO

  Kifungu Na. 91(3) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, kimeainisha vyanzo vya mapato ya Mfuko kama ifuatavyo:-

  a.    Mapato mbalimbali kama yatakavyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnamo mwaka 1983, Serikali kupitia Hazina ilitoa ruzuku ya Shilingi 2,500,000/= kama kianzio (seed money) cha Mfuko;

  b.    Asilimia 25 ya mapato yatokanayo na mauzo ya wanyamapori na nyara au silaha, magari, vyombo, ndege, mahema au kitu chochote kilichohusika katika kutenda kosa la ujangili kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 111 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009. Hiki ndicho chanzo kikuu cha mapato ya Mfuko;

  c.    Zawadi na michango mbalimbali ndani na nje ya nchi itakayotolewa na wahisani, taasisi, Serikali, au mashirika ya kimataifa; na

  d.    Kiasi chochote au mali yoyote itakayotolewa kwa Mfuko kutokana na vyanzo vingine ambavyo vitabuniwa na Mfuko.


  6.0                 MIRADI/VITEGA UCHUMI VYA KUIMARISHA MFUKO

  Ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya uhifadhi endapo vyanzo vya sasa vya mapato vitayumba, Mfuko umebuni miradi mbalimbali kama vyanzo vya kuongeza na/au mbadala vya mapato (complimentary and/or alternative sources of income). Miradi hiyo ni Jengo la Kakakuona (Kakakuona House), Pori la Akiba Pande, Bustani ya Wanyamapori Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila (Songea) na Kambi ya kitalii katika Pori la Akiba Selous.


  7.0                 CHANGAMOTO ZA MFUKO

  Katika kutekeleza majukumu yake, Mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali. Changamoto kubwa ni mbili kama ifuatavyo:


  7.1       Kutokana na mabadiliko ya hali ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la ujangili nchini na makubwa ukilinganisha na miaka ya 80 na 90. Kutokana na hali hiyo Mfuko hauna uwezo wa kukidhi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kuzuia ujangili hususan fedha za kununua vifaa vya doria (magari, radiocalls, mahema, sare), mafuta ya magari na ndege pamoja na malipo ya posho ya kujikimu ya wahifadhi wanyamapori.

  7.2       Chanzo kikuu cha mapato cha Mfuko ni 25% ya mapato yatokanayo na biashara ya uwindaji wa kitalii. Biashara ya uwindaji wa kitalii hutegemea wateja ambao ni matajiri kutoka nchi za Ulaya na Marekani. Mtikisiko wowote wa kisiasa, kiamani au kiuchumi unapotokea katika nchi ambazo watalii hao wanatoka huathiri hali ya uwindaji nchini na hivyo mapato ya Mfuko huporomoka.


  8.0                 MIPANGO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

  Hatua mbalimbali zinachukuliwa ili kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na;


  8.1         Kutafuta vyanzo vingine vya mapato zaidi ya biashara ya uwindaji wa kitalii. Miradi ya maendeleo ya Mfuko imebuniwa ili kuiendeleza na kuwa vyanzo vya mapato ya Mfuko. Miradi hiyo ni Ujenzi wa Jengo la Kakakuona, Pori la Akiba Pande, Bustani ya Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila (Songea) na Kambi ya Utalii katika Pori la Akiba Selous Miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali za kuiendeleza.


  8.2         Kuandaa maandiko ya miradi kwa wahisani ili kupata fedha za kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori nchini.  0 0


  0 0

   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
   
  Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
   
  Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
   
  Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
   
  WAKATI HUO HUO,KOCHA KIM AONGEZA MMOJA TAIFA STARS
  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
   
  Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd, Shomari Kapombe na John Bocco.
   
  Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.
   
  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai  pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa  cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni  shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
   Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe,  Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.

  0 0

   
  Picha mbalimbali za maonesho ya mavazi katika uzinduzi wa maonesho ya mavazi ya NECHA yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Ltd (SBL), kupitia kinywaji chake cha BAILEYS yaliyofanyika katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam. Kinywaji cha baileys kikionekana kutawala ukumbini pamoja na vinywaji vingine vinavyotengenezwa na SBL katika hafla hiyo. 
  Meneja wa Kinywaji cha Baileys ambacho kilidhamini maonesho hayo, Bi. Azda kutoka kampuni ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) akizungumza kuwakaribisha wageni waalikwa katika maonesho hayo ya mavazi kabla ya kuanza kwa hafla nzima 
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiburudika na kinywaji cha Baileys huku wakishuhudia maonesho hayo ya mavazi [ 
  Baadhi ya wageni waalikwa wakipiga picha za kumbukumbu katika eneo maalumu la kupigia picha katika hafla ya maonesho ya mavazi iliyodhaminiwa na kinywaji cha Baileys. Baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo baada ya maonesho huku wakiburudika kwa vinywaji vya wadhamini wa hafla hiyo (SBL)

older | 1 | .... | 149 | 150 | (Page 151) | 152 | 153 | .... | 1897 | newer