Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1507 | 1508 | (Page 1509) | 1510 | 1511 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0


  Na Said Mwishehe

  KWA heshima na taadhima, naomba nitumie nafasi hii kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Natoa salamu zangu kwenu nikitambua kuwa pamoja na shughuli nyingine za ujenzi wa nchi yetu , pia mpo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.Sababu za kufanyika za uchaguzi huo unatokana na uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Maulid Mtulia kuamua kujiuzulu ubunge.Baada ya kujiuzulu akaondoka CUF na kujiunga CCM.

  Sioni umuhimu wa kurudia sababu ambazo amezitoa Mtulia wakati anatangaza kujiondoa CUF.Hata hivyo moja ya sababu amedai alipokuwa CUF alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu kutokana na mpasuko uliopo.Tunafahamu ndani ya CUF hakuko sawa kutokana na tofauti ya misimamo na mitazamo baina ya vingozi wa juu wa chama hicho.Hivyo Mtulia akaona bora ajiweke kando.Ndio sababu ambayo ameitoa.

  Pia akasema juhudi za Rais ,Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo zimemfanya aone haja ya kuunga mkono kwa kujiunga na CCM.Najua kila mtu anayo nafasi ya kuchambua na kupima anachosema Mtulia.Kwa sasa Mtulia anagombea tena ubunge wa Kinondoni kwa tiketi yaCCM.Kampeni zinaendelea Kinondoni na Mtulia ni miongoni mwa wanaomba kura kwa wananchi.
   
  Katika uchaguzi huo ushindani upo kati ya Mtulia na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Salimu Mwalimu.Ni ushindani haswa na kila chama kilipozindua kampeni rasmi walitoa tambo nyingi.Tunasubiri mwisho wa tambo hizo utakuaje.

  Kila mmoja anaamini ataibuka na ushindi.Chadema wanaamini Kinondoni ni ya Salumu Mwalimu na hivyo hivyo CCM nao wanaamini Kinondoni ni ya Mtulia.Sawa yupo mgombea wa TLP ,Dk.Godfrey Malisa ambaye naye anawania jimbo hilo.Najua wapiga kura ndio wenye kuamua nani awe mbunge wao baada ya kila mmoja kupita na kutoa sera za chama chake kuhusu nini watafanya kwenye jimbo hilo.

  Pamoja na kwamba wananchi wa Kinondoni ndio wa kuamua bado ukweli uko pale pale wenye ushindani zaidi upo kwa Mtulia na Salum Mwalimu.Nikiri na kusisitiza wananchi wa Kinondoni wao ndio waaamuzi wa mwisho.Yangu macho tu na kueleza ninachoona kwa sasa.

  Nikumbushe kidogo tu.Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,Mtulia aligombea Kinondoni na akashinda.Alishinda kwa sababu wananchi waliamini ni mtu sahihi kwao.Mtulia alipambana na Idd Azan (CCM) lakini akambwaga kwa wingi wa kura.Salum Mwalimu wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliamua kwenda kugombea jimbo la Kikwajuni visiwani Zanzibar.Hakushinda uchaguzi huo.

  Hivyo tukiangalia uchaguzi mkuu uliopita utaona Mtulia alipewa imani na wananchi wa Kinondoni.Mwalimu hakuwa ameshinda kwa kule Kikwajuni.Sina maana atashindwa na uchaguzi huu maana mazingira ni tofauti na uchaguzi mkuu, lolote linaweza kutokea.

  Hata hivyo kwa Salum Mwalimu yeye kugombea jimbo la Kinondoni, ndio mara yake ya kwanza.Sote tunafahamu kura ni siri ya mpiga kura hivyo anaweza kushinda Mwalimu au Mtulia ama Dk.Malisa.Kwa yoyote atakayeshinda hakuna dhambi, kikubwa inategemea wanachanga vipi karata zao katika kipindi hiki cha kampeni.Yangu macho.Wananchi wa Kinondoni ndio wataamua nani awe mbunge wao.Kupitia kampeni zinazoendelea watawafahamu wagombea wao vizuri na vyama vyao.

  Sijui nikoje? Yaani kila nikiwaza uchaguzi huo naona ni vema nikatoa ushauri wangu kwa wananchi wa Kinondoni.Naamini ushauri wangu mtaukubali..Ila hata mkiukataa hakuna tatizo lakini nimeshauri tayari.Ni hivi naomba muwasikilize wagombea wote tena kwa umakini mkubwa.Wasikilizeni kila wanachosema na  kila wanachowaaahidi.Mwisho mtakuwa na nafasi ya kuamua nani atakuwa sahihi kwenu.

  Huu si wakati wa kuchagua mbunge kama vile mpo kwenye ushindani wa Simba na Yanga.Uchaguzi mdogo unamaana kubwa licha ya kuitwa ni uchaguzi mdogo.Ni uchaguzi unaotokana na jimbo
  kuwa wazi baada ya aliyekuwepo kuamua kujiuzulu kwa sababu ambazo amekuwa akizielezea.Hivyo kwa mujibu wa Katiba yetu lazima uchaguzi ufanyike.

  Tayari Serikali iko madarakani na kila mwananchi anajua hilo.Hivyo kinachobaki ni kupata mbunge ambaye atakuwa mwakilishi wawananchi bungeni.Wanachagua mbunge atakayechukua changamoto za wananchi na kisha kuzipeleka kwenye vyombo vya mamlaka zipatiwe ufumbuzi wake.

  Mnachagua mbunge ambaye atapinga kwa hoja na si kupinga hoja kwa vioja na vituko.Ni jukumu la wananchi wa Kinondoni kuamua kati ya Salumu Mwalim,Maulid Mtulia na Dk.Malisa nani mnaona mkimpa nafasi itakuwa rahisi kumtuma.

  Wapo wanaosema fedha nyingi zinatumika kwenye uchaguzi huomdogo.Fedha ambazo zingeweza kutumika kwenye mambo mengine yakimaendelea.Wanaweza kuwa na hoja lakini ifahamike demokrasia nigharama  na haziepukiki.Zipo tu.Kama una bisha shauri yako.Ndio maana kote ambako wabunge walitangaza kuachia majimbo uchaguzi umefanyika tena.Si jambo jipya hata huko nyuma kumeshafanyika chaguzi ndogo mara nyingi tu.Unabisha nini?Huenda umesahau acha nikukumbushe uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga baada ya Rostam Aziz kuamua kujiuzulu.Ni moja tu ya mfano kati ya mingi.Fedha zilitumika kama ambavyo zinatumika sasa.

  Hata ikitokea mbunge aliyepo amefariki lazima Tume ya Taifa Uchaguzi(NEC)itangaze kufanyika kwa uchaguzi mdogo.Huo ndio utaratibu iwe ni gharama kubwa au ndogo.Kwa wananchi wa Kinondoni kikubwa kwenu ni kuchekeka na kuwapima wagombea waliopo mbele yenu na kisha kupata mtu sahihi ambaye mtashirikisha naye kutatua kero zenu.

  Tunafahamu uchaguzi huo wa Kinondoni kwa vyama vya upinzani ni kipimo cha wao kama bado wanaendelea kuaminika kwa wananchi au la.Na kwa CCM nao ni uchaguzi ambao wanautazama kwa jicho la aina yake.Ni uchaguzi ambao unatoa picha ya namna ambavyo wananchi wanawaamini kwa kiwango gani.

  Kimsingi uchaguzi wa Kinondoni ni uchaguzi mdogo kama ambavyo tunaelezwa lakini umebeba sura ya kitaifa kutokana na mazingira yaliyopo.Nimalize tu kura zitakazopigwa siku ya uchaguzi zitatoa majibu ya nani anatakiwa na wananchi wa Kinondoni.Yangu macho maana huku namuona Mtulia na kule namuona Mwalimu.

  TUWASILIANE 
  0713833822

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwasalimia wakazi wa Mji wa Pongwe mara baada ya kuwasilia na timu ya Coastal Union ikitokea mkoani Morogoro ambapo iliweza kupanda daraja baada ya kuifunga Mawenzi ya Morogoro mabao 2-0 kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akizungumza wakati alipoipokea timu ya Coastal Union mara baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao mapokezi hayo yalifanyika kwenye eneo la Pongwe Jijini Tanga kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo
   Wapenzi wa soka mkoani Tanga pamoja na wananchi wakiwa wamezingira barabara ya Tanga kwenye mikoani eneo la Pongwe wakiilaki timu ya Coastal Union leo.
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo akizungumza katikani ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella
   Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union,Steven Mguto katikati akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa kamati ya usaji wa klabu hiyo Ahmed Aurora kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga(TRFA) Saidi Soud
  Mfungaji wa moja ya mabao yaliyoipandisha timu ya Coastal Union Athumani Iddi Chuji akizungumza kwenye mapokezi hayo leo (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, DODOMA
  KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.
  Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria  kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo.
  Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba.
  Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo  kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno.
  “Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
  Alisema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, mafanikio mbalimbali yamefikiwa ikiwa  ni pamoja na kupata hati safi kwa hesabu za mwaka 2015/2016 na 2016/2017 zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), usajili wa waajiri 12,546 hadi kufikia Januari 31, 2018, na kulipa Fidia kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa wafanyakazi 1,144.
  "Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambavyo vinatekelezwa kwa kasi kubwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinalenga kukuza uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya Watanzania na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025." Alisema Mhe. Waziri.
  "Katika kuhakikisha Mfuko unaendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha wadau wanapata huduma kwa urahisi zaidi na katika ufanisi wa hali ya juu, Mfuko utafungua ofisi mikoani kwa awamu." alisema.
  Kwa sasa Mfuko unatekeleza majukumu yake mikoani kwa kutumia Maafisa Kazi wa Mikoa.  
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema, katika mazingira yab sasa ambapo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda, jukumu la Mfuko halitakuwa kulipa Fidia pekee bali pia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza ama kuzuia kabisa ajali katika maeneo ya kazi.
  “Ili kuwezesha kufanikisha hilo, Waheshimiwa wabunge mnao umuhimu wa kipekee katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni, majukumu na uendeshaji wa Mfuko.”
  Matarajio ya Mfuko ni kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau wote, (Waajiri, wafanyakazi, Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, hospitali na vyombo vya habari, alifafanua  Bw. Mshomba.
  Akizungumzia majukumu muhimu ya Mfuko, Bw. Mshomba alitaja kuwa ni pamoja na kusajili waajiri na wafanyaakzi, kukusanya michango kutoka kwa waajiri, kulipa fidia stahiki kwa mfanyakazi na wategemezi na kuwekeza ili kujenga uwezo wa kulipa fidia.
  Katika warsha hiyo ya siku moja, waheshimiwa wabunge walipata fursa ya kuelimishwa juu ya utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba ili hatimaye Mfuko utoe Fidia stahiki.
  Lakini pai wabunge walielezwa muundo wa Mfuko huo ambapo umezingatia mfumo jumuishi, kwa maana ya kuwa na bodi ya uwakilishi wa makundi mbalimbali ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko.

    Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
   Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
   Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya  uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.

   Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Mhe.Mama Salma Kikwete, akisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba wakati wa warsha hiyo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter akitoa mada juu ya muundo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na uongozi na bodi ya wadhamini ambayo ni shirikishi.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar, akitoa mada kuhusu utaratibu unaotumika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza wajibu wake wa kazi aliyoajiriwa kwa mujibu wa mkataba kabla ya Mfuko kutoa Fidia.
  Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, akizungumza.

  Baadhi ya waheshimiwa wabunge kwa shauku kubwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa WCF.

  Kutpka kushoto, Mhe. Jenista Mhagama, Mhe. Andrew Chenge na Mhe. Najma Giga, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
  Timu ya wataalamu wa WCF, kutoka kushoto ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba,  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter,Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala,Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar na Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Mhe. William Lukuvi, (katikati), akibadilishana mawazo na  Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (kushoto na Meneja Matekelezo, (Compliance), Bw.Bw.Victor Luvena mwishomi mwa warsha hiyo.
  Wabunge juu na chini wakipitia vipeperushi vyenye maswali na majibu kuhusu shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, 9WCF), wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa kuhusu Mfuko huo.

  Mbunge wa Nkasi, Mhe. Ali Kesy(kulia) na mbunge mwenzake wakiwa kwenye warshan hiyo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Fedha na Utawala, Bw.Bezil Kwala, akizungumza mbele ya waheshimiwa wabunge.
  Meneja Madai (Claims), wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, akizunguzma kwenye warsha hiyo ya wabunge.

  Mbunge  wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe.Ndugu Cosato David Chumi, akizungumza kwenye warsha hiyo.

  Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, (Kusbhoto), akiteta jambo na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, (katkati) na Mhe. Mbunge ambaye jina lake halikupatikana wakati wa warsha hiyo.
  Mhe. Waziri na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, wakiwa katika picvha ya pamoja na uongozi wa WCF.
  Mhe. Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula, (wapili kulia), Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wabunge na viongozi wengine wa Mfuko, wakiwa katika picha ya pamoja
  Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akipeana mikono na Mkuu wa Mkuu wa Huduma za Sheria Bw. Abraham Siyovelwa. 

  Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Mshomba na viongozi wengine wa Mfuko huo. 

  0 0


  0 0

   Mkuu wa MKoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika Baraza la Biashara la Mkoa akiwa na katibu Tawala wa Mkoa Benard Makali (wa kwanza kushoto) pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri za Kalambo na Nkasi (Kulia)

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim wangabo amesikitishwa na kitendo cha wafanyabiashara kutumia mbinu mbalimbali za kukwepa kulipa kodi serikalini jambo linalorudisha nyuma maendeleo, hivyo kutoa siku saba za kujirekebisha kabla ya Mamlaka ya mapato kuanza msako mkali na kuwatia nguvuni.

  Amesema kuwa katika kipindi cha mitatu kuanzia Oktoba hadi Disemba, 2017 Mamlaka ya Mapato Rukwa imekusanya shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho hakiendani na uhalisia na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi endapo itapambana na vipingamizi vilivyopo.

  “Kuna vipingamizi kadhaa moja ni wafanyabiashara kutokuwa na EFD, pili, baadhi ya wafanyabiashara kutotoa risiti, kuna wenye EFD mbili, iliyosajiliwa na isiyosajiliwa, na wao hutumia isiyosajiliwa na wengine kuwa na vitabu viwili vya stakabadhi na kutumia kile chenye mapato madogo kupiga mahesabu ya serikali, yote hii ni mianya ya kukwepa kodi ya serikali,na wengine kuuza kwenye magari bila ya risiti,” Alisisitiza.

  Pia amebainisha kuwa kuna wafanyabiashara 316 ambao wamelipia mashine za EFD lakini hadi leo hawajapewa mashine hizo na kusababisha kuvuja kwa mapato ya serikali, ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Biashara la Mkoa.

  Katika kubainisha changamoto za wafanyabiashara mkoani humo Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Rukwa Sadrick Malila amesema kuwa wafanayabiashara mkoani humo wamekuwa na wakati mgumu kutokana na utitiri wa kodi na kutokuwa na mahusiano mazuri na Mamlaka ya mapato Tanzania na kushauri kurudishwa kwa Jukwaa la walipa Kodi kwani lilikuwa na manufaa.

  “Tulikuwa na jukwaa la walipa kodi, amabapo tulikuwa tunakaa na kujadili, lakini hili jukwaa limefutwa na kutoka pale imekuwa ubabe na wakati ule TRA walikuwa wanavuka malengo kuliko hali ilivyo hivi sasa,ambapo hawavuki malengo”Alisema

  Tuhuma hizo zilikanushwa na Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani Rukwa Fredrick Nyariri nae kutoa takwimu zilizobainisha kuvuka kwa malengo kulingana na viwango walivyopangiwa.

  “Si kweli kwamba hatuvuki malengo kwa mfano mwezi Novembea tulipangiwa Shilingi Milioni 801 tukapata Milioni 928 na Mwezi Disemba tulipangiwa kukusanya Shilingi Milioni 908 na tukapata Milioni 996, nasikitika kusema kwamba taarifa ya mwenyekiti TCCIA imejaa upotoshaji,” Alimalizia. Na kuongeza kuwa Mamlaka ya Mapato imejipanga kuuza mashine za EFD na kuepukana na kuwa na wakala mmoja wa kusambaza mashine hizo ndani ya Mkoa wa Rukwa.

  0 0

  Jumapili tarehe 4/2/2018

  - Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street, Dar es salaam. 
  -Saa 11:00 Jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)
  ******************************
  Jumatatu tarehe 5/2/2018
  - Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
  - Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
  - Saa  4:00  Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
  - Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa
  - Saa 6:00 Mchana  9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu
  - Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni
  - Saa 9:30  Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko
  - Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote
  1:30 mpaka  2:45  Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote
  3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

  Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.
  Bwana ametoa, na bwana ametwaa.
  Jina lake na lihimidiwe - AMINA

  Imetolewa na:
  Omary A. Kimbau
  Mwenyekiti wa kamati ya mazishi

  0 0

  Jeffrey Jessey anaishi ndoto ambayo kila kijana wakitanzania angependa kuishi hivyo. Akiwa na ari ya kuja kuwa na mafanikio Jeffrey alianza shule hadi kufika Chuo kikuu cha Dar es salam ambako alisoma masomo ya biashara huku akisaidia wanafunzi wenzake kupunguza nguo kubwa na kuzifanya kuwa “modo“.Jeffrey ambaye maisha yake ya nyuma yalikuwa na changamoto nyingi ambazo zilipelekea kuuza maji ili kuifanya familia ijikimu. Kwa uhakika mafanikio yake ya leo yanachangiwa sana na makuzi yake yaliyomtayarisha kupambana na kufanikiwa
  Baada ya kumaliza shahada yake ya chuo kikuu, Jeffey hakutaka kuajiriwa bali kujiajiri kama mshonaji wa nguo kupitia chapa yake ya Speshoz. Hadi sasa ameajiri watu wengi na kufanikiwa kutengeneza jezi za Yanga, kuwavesha Diamond Platnumz, Mfanya biashara maarufu Bakhresa, Wabunge , Mawaziri na Maharusi wengi.
  Simulizi ya Jeffrey imo kwenye kipindi maalum cha kukuza Ujasiriamali chenye kulenga zaidi vijana kiitwacho Extra Mile Show ambacho kimezinduliwa leo jijini Dar es salaam.
  Wakieleza mkakati wao Extra Mile Show walisema vipindi hivi vinavyopatikana kwenye mitandao na youtube, facebook, instagram na twitter kinalenga kuwawezesha vijana kutambua fursa na kubadilishana uzoefu.

  0 0


  Kampuni ya Umoja switch imewazawadia washindi wake zawadi walizoshinda kwenye droo ya Shinda na Umoja Switch iliyochezeshwa January 16 mwaka huuKatika droo hiyo ya kwanza ilitoa washindi katika vipengele vinne ambavyo ni, Mshindi wa fedha taslimu Milioni moja, washindi wa fedha taslim mara mbili ya muamala aliyofanya kwenye ATMs za UmojaSwitch, washindi watano wa Simu za mkononi (Smart phones) na washindi zaidi ya 20 wa T-shirt za UmojaSwitch.

  Akiwakabidhi zawadi hizo za afisa masoko wa Umoja Switch Umoja Beatrice Emmanuel amesema anawashukuru wateja wa Umoja Switch kwa kuendelea kutumia kadi za Umoja Switch na amewataka wale ambao hawajabadili kadi zao wafike kwenye Benki zao ili kubadilisha kadi zao na waingie kwenye droo ya Pili ya Promosheni hii ya Shinda na Umoja Switch.Akizungumza na waandishi wa habari bi Paulina Cosmas Kigolo ambae ni mjasiriamali na mmiliki wa Boda boda amesema hakutegema kama angekuwa mshindi wa fedha hizo kwani kwa mara kadhaa amekua akitumia kadi kadi yake ya umoja Switch kufanya miamala na hakuwa akijua kama kuna zawadi zinatolewa kwa watumiaji wa kadi za Umoja Switch hivyo kwake lilikuani jambo la kushangaza .“Kiukweli mara ya kwanza napigiwa Simu sikuamini kabisa kwa sababu sikuwa nikijua kama kuna promosheni inachezeshwa, kwa hiyo siku napigiwa kwakweli sikuamini kabisa, mi nawashauri wateja wazidi kutumia kadi za UmojaSwitch ili nao washinde kama mimi” alisema bi Kigolo
  Kwa upande wa mshindi wa pili wa fedha taslimu mara mbili bi, Catherin Mbogela amewashukuru sana Umoja Switch kwa kuanzisha promosheni kwa sababu inaonyesha kuwajali wateja wake

  Umoja Switch leo imechezesha droo yake mwisho ambayo washindi wake watatangazwa hivi karibuni.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa agizo la kukamatwa kwa waliokiuka amri ya mahakama na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye msitu wa Malangali Mjini Sumbawanga
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa agizo la kukamatwa kwa waliokiuka amri ya mahakama na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye msitu wa Malangali Mjini Sumbawanga katika Mkutano wa hadhara.


  Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu akiwasilisha taarifa ya msitu wa Malangali uliopo Sumbawanga Mjini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.


  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameagiza kuwasaka na kuwakamata wananchi wote waliokiuka amri ya mahakama ya kutoutumia msitu wa hifadhi ya Malangali kwaajili ya matumizi ya kibinadamu.

  Amesema kuwa pamoja na kukamtwa, wananchi hao wasimamiwe kuhakikisha kuwa wanapanda miti maeneo ambayo wameyaharibu na kusisitiza kusakwa kwa wale wote waaofanya shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo vya maji huku akitaja bonde la mto lwiche.

  “Mpite shamba kwa shamba, kamateni watu wote ambao wamevamia kule, ule msitu uache kama ulivyo, vyanzo vyetu vya maji vitakauka, Mkurugenzi fanya msako wa bonde lote hilo kwa wale wote ambao wameanza kufyeka na kulima, kamata. DC simamia hili, tunataka kukomesha uharibifu wa mazingira wa aina yoyote ile,” Alisisitiza.

  Ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara alioufanya baada ya kutembelea msitu huo wa malangali uliopo kata ya Malangali, Wlayani Sumbawanga na kujione namna wananchi hao walivyoharibu msitu huo uliojaa miti ya miombo ambayo inakatwa na kugeuzwa mkaa.

  Msitu huo wa Malangali ulianzishwa rasmi mwaka 1986 na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa huo Mh. Tumainieli Kihwelu wenye eneo la ekari 278 kwa lengo la kupunguza mmomonyoko na vimbunga.

  Wakati akisoma taarifa ya Msitu huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbwanga Hamid Njovu amesema kuwa baada ya miaka 29 wananchi waliwasilisha malalamiko ya kupokonywa ardhi na kufanywa msitu shauri lililofikishwa mahakamani na kuamuliwa wananchi hao kulipwa fidia huku hukumu ya kesi hiyo ikisitisha shughuli zote za kibinadamu kutofanyika katika msitu huo.

  “Tarehe 28/4/2016 hukumu ilitolea na kuamuliwa Manispaa ya Sumbawanga kulipa fidia huku Hukumu hiyo ikisitisha shughuli zote za kibinadamu ndani ya msitu lakini bado wananchi hao walirudi kufyeka miti na kulima na tarehe 13/11/2017 Manispaa ilitoa maelekezo kwa wananchi kutoutumia msitu kwa shughuli za kibinadamu,”Alimalizia. Mmoja wa wadau wa Mazingira Mzee Zeno Nkoswe amesema kuwa usalama wa mji wa Malangali unatokana na msitu huo na kwamba endapo utaendelea kuharibiwa mji huo utafunikwa na mmomonyoko wa udongo.

  0 0
  NA FREDY MGUNDA, IRINGA

  MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itamshughulikia mtendaji yeyote wa Serikali atakayeonyesha dalili ya kukwamisha juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

  Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ,alisema Mtu yeyote ndani ya serikali ya mkoa wa Iringa atakayeonyesha dalili za kuhujumu au kwa makusudi, serikali ya chama cha mapinduzi haita muacha na lazima itamshughulikia.

  “Nasema hatuta kubali kuona mtu yeyote atakaye onyesha kukwamisha juhudi wakati rais na mwenyekiti wetu wa Taifa tutapambana nae,Rais amejitoa kwa wananchi wake alafu mtu atokee tu na kuvuruga utaratibu lazima haiwezekani na tutapambana nae”alisema MNEC

  Alisema Wakuu wa Wilaya wanapaswa kuwaambia viongozi wao wa serikali kuwa kofia na nguo za kijani ndiyo wanaosimama kwenye majukwaa kuwatete wao,hivyo si haki CCM tubebe lawama kwa ajili ya hao watendaji wazembe wenye nia ovu kwa serikali ya kukwamisha maendeleo ili wengine wapande jukwaani wakitukane chama Tawala.

  hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho kujua majukumu yao ya kuhakikisha CCM inasimammia Serikali na si wengine wanasimama kutetea uozo wa watendaji hao ambao nia yako ni mbaya lakini kama watendaji wangejua thamani ya CCM basi ingekuwa vigumu kuwepo mtendaji wa serikali ambae ni mpinzani.

  Abri ( ASAS ) aliongeza kuwa Ilani inataka yaale mambo yaliyaidiwa kwa wananchi yanatekelezwa kwakuwa wakati wa kuomba kura ni wanaCCM ndiyo waliosimama kuomba kura na si taasisi za serikali au Mkurugenzi wa Halmashauri,hivyo hatuna budi kuhakikisha Ciongozi wa CCM wanafuatilia utekelezaji wa Ilani kwani hata pale yasipotekelezwa wananchi halaumu chama tawala na si watendaji wa serikali.

  “Sisi viongozi wa mkoa hapa wa CCM ndiyo wawakilishi wa mwenyekiti wetu na madhumuni ya ccm ni kuisimamia serikali ,haiwezekani CCM tunatukanwa ovyo kwa ajili ya wazembe,wakati serikali inasema hakuna michango mashuleni lakini mwalimu mwenye itikadi ya kipinzani anafukuza mwanafunzi eti bila michango hakuna kuingia”.

  Alisema MNEC “Haiwezekani Rais afanye kila juhudi alafu watokee watu wengine wajinga tu hivi waanze kukamisha ,sisi hapa wajumbe wa Halmashauri kuu,mwenyeviti na na viongozi wengine ndani ya chama kazi yetu nini, yaani rais atoke ikulu aje Iringa kushughulikia watu hao ”.

  Aliongeza kwakusema “haiwezekani wananchi maskini watekeseke kwa ajili ya wapuuzi puuzi wajanja ,rais kila siku anapiga kelele muwe kwenyenupande wa wanyonge au upande wa maskini ,lakini kuna watu ambao kazi yao ni kikwamisha juhudi na kubeza kazi inayofanya Rais Magufuli tunasema hatuta kubali “

  Au mtu yeyote wa serikali atakaye taka kukwamisha juhudi za Rais na Mwenyekiti wetu wa Taifa lazima tutamshughulikia na wanaCCM wawashughulikie kwa sababu wanaotukwanwa ni chama cha mapinduzi na ni kwa ajili ya uzembe wa watendaji wa serikali wasiokipenda chama

  “Kwa sababu CCM ndiyo chama kilichopo madarakani na hata kwenye kuomba kura wao hawakuwepo lakini Mkurugenzi au mwandisi amepewa fedha ya kutengeneza barabara alafu akala hela nawauliza lawama itaenda kwa nani kwa kawaida itaenda kwa chama tawala ambacho ndiyo CCM basi na sisi tusikubali”alisema,

  Pia aliwataka wanaCCM wa mkoa wa Iringa kuwapuuza wale watendaji wa serikali wanaosema hali ngumu kwani hao ndiyo watumishi waliozoea kula rushwa,mafisadi na watendaji wasiokuwa na maadili ya kazi.

  “Alafu wapuuzeni wale na watumishi wa serikali na viongozi wanaokasikiri na kulalamika kuwa hali ngumu,vyuma vimaekaza sasa mimi namuuliza mshahala wako huupati anaupata katika tarehe zilezile na je mshahara umepunguzwa hapana ni uleule sasa ugumu unatoka wapi ,nikagundua kuwa hao ndiyo wanaotupa tabu serikalini”alisema Abri .

  Aidha amewashukuru wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Iringa wa CCM kwa kuwafuta machozi wanaManispaa ya Iringa ,hawa wamekuwa mstali wa mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Manispaa hii lakini si kama wahawajali wa mufindi,kilolo wa Iringa Vijijini ni kutokana majimbo hao kuwa na wabunge wa ccm lakini Manispaa ni yatima.

  “Katika miaka miwili na nusu Manispaa ya Iringa imeonza zahama kubwa kwani hakukuwa na lolote lililofanyika katika jimbo hili zaidi ya maneno tu”alisema

  Alisema anashangazwa na Ofisi ya Meya ambayo ni ya serikali kugeuzwa ndiyo ofisi ya kutolea matamko ya chama chao “kila mara inawaita waandishi wa habari kutoa matamko ya kisiasa ya chama chao na si kuwaita kuwaeleza wamefanya nini lakini katika Manispaa ya Iringa lakini hutaona CCM inatumis majengo ya Serikali kutolea matamako kwa sababu CCM inaofisi zao”.

  Pia MNEC aliwata WanaCCM wa Manispaa ya Iringa kuhakikisha hawafanyi makosa kama waliofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 inatakiwa waseme sasa basi.

  “unajua kweli wanasiasa tunacheza siasa lakini tusicheze kwenye maisha ya watu sanjali na hali za watu ,tusiweke utani wa siasa kwenye maisha ya watu kwani siasa si kama ushabiki wa mpira,tunajenga maisha ya watu ,manispaa yetu inakuwa kila kukicha kwa kuwa watuwanaongezeka”alisema MNEC .

  Awali akimkaribisha Mgeni RAsmi ambaye ni MNEC wa Iringa ,Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magalla aliwata aliwata watendaji wa serikali na taasisi zake kuwa watekerezaji wa sera na maamuzi ya chama tawala kwani ndiyo chama kilichochaguliwa na wananchi.

  Kwa hiyo asitokee mtendaji yeyote wa serikali au kiongozi anayetaka kukwamisha sera na maamuzi ya CCM bali wawe mstali wa mbele katika kutatua kero za watu na si wao kuwa sehemu ya kero kwa wananchi wao wanaowategemea .

  Magalla alisema watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanangaile na shida za wananchi kwani hivi sasa kumekuwa viongozi wa serikali ndiyo wamekuwa kero kwa wananchi kwa kuwasumbuasumbua mara kwa mara bila hata kuwapa elimu kwanza wananchi kabla ya kuwavunjia au kukamata vifaa vyao aambavyo ndiyo vinawaingizia kipato.

  0 0  Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele

  Shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto,Picha na John Mapepele
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba akishuhudia,Picha na John Mapepele
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba wa kwanza kulia aliyevaa suti akishirikiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mary Tesha zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara ,Picha na John Mapepele


  Na John Mapepele, Mwanza.

  Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara .

  Mbali na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki na mazao yake nje ya nchi.

  Akizungumza na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.Aidha Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.

  Pia aliwaonya wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni zote za biashara zao. Alisema rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.

  Pamoja na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini.

  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.

  Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara, ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.

  Hivi karibuni watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wameweza kukamata nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa operesheni hizo zitakuwa za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.

  0 0


  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ukumbi wa mkutano baada ya kuwasili na kupokelewa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kulia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.(Picha na Ikulu)
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati Maalum ya CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar, baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa CCM uliofanyika mwaka jana Dodoma.(Picha na Ikulu).

  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.(Picha na Ikulu)

  WAJUMBE wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo wa kwanza wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  WAJUMBE wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa wamesimama wakimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyakiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiingia katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  WAJUMBE wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo wa kwanza wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu)


  WAJUMBE wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo wa kwanza wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na NaibuKatibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar.

  0 0

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyekaa mbele) akiongea na kutoa maagizo kwa Meneja wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsisitizia jambo Mfanyabiashara wa duka la nguo Wilayani Bunda Mkoani Mara kuhusu suala la umuhimu wa kutumia mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akikagua taarifa ya mauzo ya siku ya Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) toka kwa Wafanyabiashara wa duka la vifaa vya nyumbani Wilayani Bunda Mkoani Mara mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).  Na: Veronica Kazimoto-Bunda, 

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Ndg. Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara wa mkoani kwake. 

  Uamuzi huo umetokana na ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa TRA kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema Meneja huyo ameonyesha uzembe wa hali ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani kwake ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo. 

  "Katika ziara yangu nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," alisema Kichere. 

  Kutokana na uzembe huo, Kamishna Mkuu Kichere amewaagiza Mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha Meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 

  Ziara hiyo ya kushtukiza imewawezesha wafanyabiashara waliokuwa wamelipia mashine za EFD miaka ya nyuma, kupata mashine hizo na kufundishwa jinsi ya kuzitumia ambapo wengine wamejitokeza kununua mashine hizo kwa ajili ya biashara zao. Kamishna Mkuu aliongeza kuwa, mashine za EFD zina umuhimu sio tu kwa Serikali kupata mapato bali kwa wafanyabiashara husika kwani huwawezesha kutunza kumbukumbu, kujua mwenendo halisi wa biashara zao na hatimaye kulipa kodi stahiki. 

  Sambamba na hayo, Kichere amewataka wananchi wasiishie tu kudai risiti bali wakishachukua risiti hizo wazikague ili kuthibitisha uhalali wake na usahihi wa kiasi cha pesa walicholipa. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku 5 ambapo amepata nafasi ya kutembelea Vituo vya Forodha mipakani na ofisi mbalimbali za mamlaka hiyo pamoja na baadhi ya wafanyabiashara akikagua matumizi ya mashine za EFD.

  0 0


  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akitoa elimu ya mpango wa Toto Afya kadi kupitia kipeperusi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa wakihamasisha mpango wa Toto Afya kadi

  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akitoa elimu ya mpango wa Toto Afya kadi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa waki hamasisha mpango wa Toto Afya kadi
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Tangamano ambapo walikuwa wakihamasisha mpango wa Toto Afya kadi

  Mmoja kati ya wakazi wa Jiji la Tanga katikati akimsikiliza kwa umakini afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga kuhusu umuhimu wa mpango wa Toto Afya kadi
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia Shabani kulia akitoa elimu ya namna ya kujiunga na mpango wa Toto Afya kadi kwa watoto mkazi mmoja wa Jiji la Tanga ambaye aliwatembelea kwenye banda lao eneo la Tangamano
  Sehemu ya wananchi wa Jiji la Tanga wakiingia kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati mfuko huo ulipokuwa ukihamasisha umuhimu wa wazazi na walezi kuwaingiza watoto wao kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na matibabu zoezi hilo lilifanyika kwenye viwanja vya Tangamano(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0


  Na Anitha Jonas – WHUSM 

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuongeza usikivu katika maeneo mbalimbali ya mipakani mwa nchi. 

  Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya bajeti na mwenendo wa shirika hilo. 

  “Ninafuraha kubwa kupata taarifa ya kuimarika kwa usikivu katika maeneo ya mipakani yaliyokuwa na yanasumbua kwa muda mrefu kama maeneo ya Tarakea,Kibondo,Longido,Tarime na Mbababey na pamoja na maeneo ya Mtwara na Nachingwea,”Dkt.Mwakyembe. 

  Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Waziri Mwakyembe aliendelea kupongeza uongozi wa TBC kwa kufanya maamuzi ya kutumia mafundi mitambo wa ofisi yao kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo pamoja na kufanya matengenezo pia aliwapongeza mafundi mitambo waliofanya kazi hiyo kwa uaminifu na uzalendo huku akiomba uongozi wa shirika hilo kuwapeleka bungeni mafundi hao wakati wa bunge la bajeti. 

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba alieleza kuwa mpaka sasa Wilaya ya Geita tayari kumeshafungwa mitambo mipya inayosaidia kuboresha usikivu kwa uhakika na kazi hiyo imefanywa na mafundi wazalendo wa shirika hilo. 

  Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC Bw. Joseph Kambanga alieleza kuwa mpaka sasa kazi ya kububoresha usikivu inaendelea na baadhi ya mafundi walikuwa Tarime wakiendelea na kazi hiyo na kwa mwezi ujao wanategemea kuongeza usikivu kwa Mkoa wa Mtwara na Nachingwea . 

  Pamoja na hayo Waziri Mwakyembe ameuagiza uongozi wa TBC pia kufichua uovu uliyoko katika jamii kwani serikali ya awamu ya tano inapiga vita ufisadi na matendo maovu katika jamii hivyo wasibaki nyuma katika kuyaangazia hayo pale wanapohabarisha umma. 

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akiwapongeza viongozi na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa kuongeza usikivu kwa maeneo ya mipakani  (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba.

  Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa taarifa ya upanuzi wa usikivu   wa matangazo ya Shirika  hilo nchini kwa  Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mafundi mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu kutokana na kufurahiswa na kazi waliyoifanya  ya kupanua usikivu kwa maeneo mbalimbali nchini,aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba na wapili kutoka kulia aliyeketi ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi TBC Bw.Joseph Kambanga.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia)  mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo jana jijini Dar es Salaam aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba

  0 0

  Hapa nchini, tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka kila mwaka. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa, kila mwaka wagonjwa wapya wapatao 50,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali Tanzania. Na kati ya hao ni *wagonjwa 13,000 tu, sawa na 26% ndio wanaofanikiwa kufika katika Hospitali zetu kuweza kupata matibabu*. 

  Aidha, *wagonjwa walio wengi (takribani asilimia 70) hufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (hatua ya 3 na ya 4)*, hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.

  Takwimu za mwaka 2016/2017 kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kwamba Saratani zinaoongoza nchini ni: 
  1. Saratani ya Kizazi ​(32.8%)
  2. Matiti ​(12.9%)
  3. Ngozi (Kaposis Sarcoma)  ​(11.7%)
  4. Kichwa na Shingo ​(7.6%)
  5. Matezi ​(5.5%)
  6. Damu ​(4.3%)
  7. Kibofu cha Mkojo ​(3.2%)
  8. Ngozi (Skin)  ​(2.8%)
  9. Macho ​(2.4%)
  10. Tezi Dume ​(2.3%)

  Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani *ninatoa wito na kuhimiza kila mmoja wetu kupima ugonjwa wa Saratani. *Saratani inatibika endapo itagunduliwa mapema*. 

  Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea na jitihada za kuongeza uelewa  wa wananchi juu ya vyanzo mbalimbali vinavyosababisha saratani ili kila mmoja wetu aweze kujikinga. Vyanzo hivi ni pamoja na *Mtindo wa kimaisha (Life Style) kama vile Uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa (kula vyakula vyenye mafuta mengi, kutokula matunda na mboga mboga za kutosha), matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kutofanya mazoezi*.

  Aidha, Tutaongeza jitihada katika kuamsha ari na hamasa ya wananchi kupima Saratani ili kujua hali zao sambamba na kusogeza huduma za uchunguzi na matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani katika maeneo mbalimbali nchini hasa vijijini. 

  Kwa mwaka 2017, Serikali imeongeza Vituo 100 kutoka vituo 343 vilivyopo awali kwa ajili ya huduma za kupima na matibabu ikiwa ni sehemu ya jitihada zetu za kupambana na ugonjwa huu. vituo hivi (Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali) tumevipatia vifaa Tiba na utaalamu ili kuwezesha wanawake wengi kupima saratani ya Kizazi na Matiti pamoja na kupata matibabu ya mabadiliko ya awali ya saratani ya kizazi papo hapo. Tumelenga kuwafikia wanawake milioni 3 nchi nzima ifikapo Desemba 2018. 

  Vilevile, Serikali inaendelea na jitihada za kusogeza huduma za matibabu ya Saratani (matibabu kwa njia ya Dawa (Chemotherapy) na matibabu kwa njia ya mionzi (Radiotherapy)  katika Hospitali zetu za Rufaa za Kanda (Mbeya, Bugando na KCMC). Pia tunaendelea kuimarisha huduma za matibabu ya Saratani katika Hospitali ya Ocean Road kwa kuweka mashine mbili mpya za kisasa (Linear accerelators), ambazo zitasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa wagonjwa kupata  huduma za tiba ya mionzi sambamba na kuhakikisha upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100. 

  Kuanzia mwezi April 2018, Serikali itaanza kutoa *chanjo ya kuwakinga wasichana kupata ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi  (HPV vaccine)*. Chanjo hii itatolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 - 14. Niwaombe wazazi na walezi wenzangu tuwe tayari kuhakikisha binti zetu wanapata chanjo hii.

  "Tunaweza, Ninaweza. Kwa Pamoja Tuwajibike Kupunguza Janga la Saratani Tanzania".!

  Ummy Mwalimu, Mb
  WAMJW
  4 Februari 2018

  0 0

  Arusha, 4 February, 2018-Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) inaendelea kuimarisha juhudi zake za kuitangaza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika(AU) pamoja na wadau mbalimbali ili waweze kuitumia kikamilifu kupeleka mashauri yaliyotimiza vigezo katika Mahakama hiyo.

  Katika kufanikisha juhudi hizo, AfCHPR inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi (SADR) ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali.

  Katika ziara hiyo inayofanyika kuanzia Februari 05 hadi 07 mwaka huu,wajumbe wa Mahakama hiyo wakiwemo majaji 3 wataendesha semina kwa wadau husika na pia watakutana na Rais wa nchi hiyo pamoja na Spika wa bunge la SADR.

  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,Jaji Sylvain Ore’,amesema semina hiyo inalenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama hiyo hivyo, kuleta hamasa kwa nchi nyingi za Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s).

  “Ili Mahakama iweze kufanikisha malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)” alisema Rais huyo wa AfCHPR.

  Tangu mwaka 2010,Mahakama hiyo ya Afrika imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo wa Mahakama hiyo pamoja na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Chad,Ethiopia,Afrika ya Kusini,Ghana,Malawi,Kenya,Uganda,Zambia na Ivory Coast.

  Mahakama ya Afrika ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 1 cha itifaki ya mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo ambapo Itifaki hiyo ilikubaliwa Juni 09,1998 nchini Burkina Faso na ikaanza kutumika Januari 25,2004 na ilianza shughuli zake rasmi Novemba 2006.

  Aidha hadi Desemba mwaka jana,jumla ya maombi 155 ya mashauri yalipokelewa na Mahakama hiyo na kesi 32 zimekamilishwa.

  0 0

    Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo leo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018

   Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Mteule Mch. Can. Jackson Sosthenes Jackson akiweka wakfu na kusimikwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Dkt Jacob Chimeledya  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018.
   Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Willim Mkapa akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu Mhe Augustino Ramadhani akipiga kinanda kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli wakikomunika kwenye sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   na mkewe Mama janeth Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   akiongea machache baada ya kushiriki  katika Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimpongeza  Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimsihi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya kuketi kwenya kiti alichoandaliwa yeye wakati wa kupiga  picha za pamoja wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Nchini Dkt. Jacob  Chimeledya na viongozi wengine  wakati wa sherehe za  kuwekwa wakfu na kusimikwa  kwa Askofu wa Tano wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam  Jackson Sosthenes Jackson  katika Kanisa Kuu la Anglikana St. Albano Upanga jijini Dar es salaam leo February 4, 2018 

  Picha na IKULU

  0 0

  Hussein Makame, NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema uamuzi wa kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika jimbo la Kinondoni umezingatia matakwa ya kanuni za Uchaguzi kwa kuvishirikisha vyama vyote vya siasa ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani jijini Dar es Salaam, kufuatia taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya magazeti zinazodai kuwa Chadema hakikushirikishwa katika uamuzi wa kuhamisha vituo hivyo.

  Alisema kabla ya uamuzi wa kubadilisha vituo hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni iliitisha mkutano na vyama vya siasa tarehe 30 Januari, 2018 na wawakilishi 26 walishiriki kwenye mkutano huo wakiwemo wawakilishi wa Chadema.

  “Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na vyama vya siasa katika kikao kilichofanyika tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu walikubaliana kuhamisha vituo 46 na katika vituo hivyo vituo 16 viko kata ya Kigogo, vituo 8 viko kwenye kata ya Mwananyamala na vituo 22 viko kwenye kata ya Kijitonyama” alisema Kailima.

  Alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifunga cha 21 (1) cha kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vituo vya kupigia kura havitakiwa kuwa kwenye maeneo ya watu binafsi, nyumba za mashabiki wa vyama vya siasa au maeneo ya majeshi na ibada.

  “Nimesikitishwa na kauli ya Chadema eti hawakushirikishwa, nimesikitishwa kwa sababu kumbukumbu za mikutano zilizopo tarehe 30 Januari mwaka huu, chama cha Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Wilaya Bw. Mustafa Muro pamoja na Katibu wa Wilaya Bw. Shabani Kirita” alibainisha Kailima.

  Alifafanua kuwa wawakilishi hao walihudhuria mkutano wa msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kinondoni na vyama vya siasa na katika mkutano huo kulikuwa na ajenda moja tu kuhusu kuhamisha vituo vya kupigia kura na vyama vyote kwa pamoja vilikubaliana kikiwemo Chadema.

  “Unaposema chama cha Chadema hakikuhusishwa ninapata masikitiko makubwa sana.Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi kuingilia mawasiliana ya ndani ya chama husika, kwa hiyo kama hakuna mawasiliano kati ya makao makuu na ngazi ya Wilaya hilo sio tatizo la Tume” alisema Kailima.

  Alifafanua kuwa katika kata ya Kigogo kuna baadhi ya vituo vya kupigia kura vilikuwa ndani ya msikiti wa Kigogo na vingine vilikuwa ndani ya eneo la Zahanati eneo ambalo lilikuwa dogo kutosha kwa ajili vituo vya kupigia kura.

  Kailima aliongeza kuwa, vituo 8 vya Mwananyamala vilikuwa kwenye eneo ambalo wananchi walikuwa wanalilalamikia, vyama vya siasa vikaridhia kwamba vituo hivyo vihamishwe na vituo 6 vikapelekwa kwenye kata inayohusika na vituo 2 vikapelekwa uwanja wa Kopa.

  Akizungumzia vituo 22 kwenye kata ya Kijitonyama, Kailima alisema vyama vyote vilikubaliana kuvihamisha, hivyo Chadema kikisema havikukubaliana ndipo inapoleta shida.

  Alisema Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kipengele cha 9 (2) (C) kinasema kabla vituo vya kupigia kura havijahamishwa ni lazima Tume ishirikiane na vyama vya siasa na Tume imetimiza takwa hilo la kikanuni na vyama viliitwa vikakubali.

  “Ukisema huwezi kuhamisha vituo kabla hujafanya Uboreshaji, huwezi kuacha makosa yakaendelea kuwa makosa.Hatujahamisha kutoa mkoa mmoja kwenda mwingine, bali tumehamisha kwa ridhaa na vyama vikaridhia.

  “Kwa hiyo niwasihi chama cha Chadema kabla hakijaanza kulaumu wawasiliane na wenzao kwenye ngazi husika.” Alisema Kailima.

  Katika hatua nyingine, Kailima amelisihi gazeti la Mwananchi, litoe habari sahihi kuhusu Tume na kuacha kuandika habari zinazoihusu Tume bila ya kuwasiliana nayo ‘kubalance’ kuhusu habari husika.

  “Nalisihi gazeti la Mwananchi, tunaliheshimi ni gazeti bora na gazeti linaloheshimika, lakini nilisihi kabla halijatoa habari lazima lifanye balance ya habari” alisema Kailima na kuongeza kuwa:

  “Wenyewe walipowauliza Chadema wakasema hawakushirikishwa walitatakiwa kuchukua fursa ya kuwauliza Tume kama hawakushirikishwa.

  “Kwa hiyo nilisihi kwa sababu si mara moja wala mara mbili wamekuwa wakitoa taarifa ambazo si sahihi kuhusu Tume, tunawasihi na kuwaomba wanapotaka kutoa habari za Tume watoe habari za Tume zikiwa sahihi”

  Alifafanua kuwa kulitaka gazeti hilo kwamba hata linapotaka kukosoa ni lazima likosoe kwa habari sahihi na sio kwa habari za upotoshaji na za upande mmoja.

older | 1 | .... | 1507 | 1508 | (Page 1509) | 1510 | 1511 | .... | 1898 | newer