Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1505 | 1506 | (Page 1507) | 1508 | 1509 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa TBL - Afrika Mashariki, Thomas Kemphuis akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati akitolea ufafanuzi juu ya taarifa za kudukuliwa kwa mfumo wa mtandao wao wa kuhifadhi taarifa na kusisitiza kuwa mfumo wa taarifa zao zipo salama. Kushoto ni Meneja Masoko, Udhamini, Habari na Promosheni za Wateja - Afrika Mashariki, George Kavishe na Kulia ni Meneja Mawasiliano ya Nje wa TBL, Zena Tenga.
   


  TBL yatoa ufafanuzi juu ya madai kudukuliwa mfumo wake wa taarifa
  Yatangaza punguzo la bei ya rejareja kwa bia ya Castle Lite Premium Lager  Dar es Salaam, Ijumaa Februari 01, 2018: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), leo imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za kudukuliwa kwa mfumo wake wa kuhifadhi taarifa na kusisitiza kuwa mfumo wako na taarifa zake zipo salama.

  Kwa siku kadhaa, kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuwa, mfumo wa kuhifadhi taarifa wa TBL umedukuliwa na watu wasiojulikana na hivyo kuhatarisha kuvuja kwa taarifa zake muhimu.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Murugenzi wa Masoko wa TBL, (Afrika Mashariki), Thomas Kemphuis alisema, baada ya uchunguzi wa kina kampuni hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa hakuna tukio la aina hiyo lililotokea na kusisitiza taarifa zake zipo salama huku ikiwataka wanahisa wake, wadau pamoja na umma kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi.

  “Baada ya uchunguzi wa kina wa wataalamu wetu wa ndani na nje, TBL inapenda kuuthibitishia umma kuwa mfumo wetu wa kuhifadhi taarifa haujadukuliwa wala kuguswa kwa namna yoyote ile. Tunapenda kuwaambia wanahisa wetu, wadau na umma kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwa kuwa hakuna tukio la aina hii,” alisema Kemphuis.

  Akisisitiza nia ya TBL kuendelea kutoa huduma bora, Kemphuis alisema kampuni hiyo inachukulia kwa uzito mkubwa suala la usalama wa mifumo yake na ndiyo sababu ya kufanya uchunguzi wa haraka na wakina mara baada ya kupata taarifa za uvumi juu ya udukuzi.

  “Usalama ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwenye utendajii wa TBL. Tunafurahi kujivunia historia nzuri ya usalama ambayo tumekuwa nayo kwa miaka mingi,” alisema.

  Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa TBL itaendelea kutengeneza mifumo imara ya ulinzi wa taarifa zake ili kuepuka matukio yasiyotarajiwa kama udukuzi.

  Wakati huo huo, TBL imetangaza habari njema kwa wateja wake baada ya kutoa punguzo la bei kwa bia yake pendwa ya Castle Lite Premium Lager kutoka bei ya sasa ya shilingi elfu 2,500 hadi shilingi 2,000.

  Kwa mujibu wa Kemphuis, punguzo hilo la bei ni zawadi kwa wateja wa bia hiyo kwa kuwa wateja waaminifu na zaidi kwa kuiunga mkono kampuni ya TBL kupitia bidhaa zake.

  “Kupunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager kunadhihirisha shukrani zetu kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa kipindi kirefu. TBL siku zote ipo tayari kuwasikiliza wateja wake na kuwapa kile wanachokitaka,” alibainisha.

  Kemphuis pia aliongeza kwamba wanaelewa kuhusiana na kushindwa kuleta tamasha hilo nchini ila akaeleza kuhusu utaratibu wa kuhakikisha Wanzania wanashiriki tamasha hilo.

  “Tunajiandaa kuwapeleka watanzania 12 nchini Afrika ya kusini kuhudhuria tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi wan ne, utaratibu zaidi utatolewa,” alisema Kemphuis.

  0 0
  0 0


  0 0  0 0

  Makasha yakiwa na tikei za bahati kutoka kwa Mawakala wa Bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers cha mjini ,kinachoendesha Bahati nasibu kwa wateja wake wakubwa wajulikanao kama V.I.P Club .
  Mwandishi wa Habari wa kituo cha radio cha Kili Fm ,Mwanahamisi Jingu akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
  Mwandishi wa Habari Robert Minja akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
  Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite  Bottlers Ltd ya mjini Moshi Christopher Loiruk ,akitaja majina ya washindi katika Droo ya kupata washindi wa Bahati nasibu kwa Wateja wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.
  Zawadi za Pikipiki 25 zilizotolewa kwa washind wa Bahati Nasibu kwa wateja wakubwa wa bidhaa za Cocacola zinazozalishwa na Kampuni ya Bonite Bottlers ya Mjini Moshi.
  Sanduku 100 na Sanduku 50 pia zilikuwa ni miongoni mwa zawadi ambazo washindi 43 walijinyakulia baada ya kushiriki bahati Nasibu hiyo.
  Washiriki wa Bahati Nasibu kwa Wateja wakubwa wa Bidhaa jami ya Cocacola wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya baadhi yao kutangazwa washindi wa Droo iliyofanyika kiwandani hapo.
  Washiriki hao walipata pia fursa ya kutembelea maene mbalimbali ya kiwanda hicho kujionea hatua mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa Jamii ya Cocacola.
  Uzalishaji wa Cocacola ukiendelea katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers cha mjini Moshi .
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda a Kaskazini .

  WASHINDI wa bahati nasibu kwa wateja wakubwa wa Vinywaji baridi vya jamii ya CocaCola wamepatikana baada ya Kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mkoani Kilimanjaro kuchezesha droo ya kwanza ambapo jumla ya washindi 43 wamejinyakulia zawadi.
  Miongoni mwa zawadi kubwa ambazo washindi hao wamejinyakulia ni pamoja na Pikipiki 25 ,sanduku 100 na sanduku 50 kwa washindi watatu wa mikoa ya mauzo ya bidhaa za CocaCola ya Arusha,Kilimanjaro ,Manyara na Singida .
  Christopher Loiruk ni Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ameeleza namna ambavyo washindi hao wamepatikana kuwa ni kwa kununua sanduku tano za Soda zinazozalishwa na kiwanda hicho kasha unajipatia tiketi inayokuingiza katika Droo maalum..
  Nao baadhi ya wateja wa vinywaji baridi jamii ya Cocacola vinavyozalishwa na Bonite waliofanikiwa kushinda katika Droo hiyo wameonesha furaha yao huku wakitoa wito kwa wateja wengine kuendelea kushiriki katika bahati nasibu hizo.
  Kabla ya kuchezeshwa kwa Dro hiyo iliyosimamiwa na Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Humud AbdulHussein wateja wa vinywaji baridi jami ya Cocacola walipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha Bonite na kujionea na kupata maelezo namna ambavyo bidhaa za soda na maji zinavyozalishwa katika kiwanda hicho.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo.

  Ujenzi wa jengo hilo la kisasa ni jitiada za RC Makonda kuthamini na !kuwapa heshima Viongozi wa Dini kwa kuhakikisha wanafanyakazi katika mazingira mazuri na yenye hadhi kutokana na thamani na mchango wao mkubwa katika jamii. 

  Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Nne pamoja na Ground floor lina Ofisi ya Mufti wa Tanzania, Ofisi ya katibu, VIP room, kumbi za mikutano, Ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri,Jiko,Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua pamoja sehemu ya Mapokezi. 

  RC Makonda amesema kazi wanayofanya Viongozi wa Dini ni kubwa hivyo tunapaswa kuthamini kwa kuwaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi. Aidha RC Makonda amesema shauku yake ni kuona hadi mwezi wa Ramadhani jengo linakuwa limekamilika na kuanza kutumika. Aidha RC Makonda amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Amani Taifa na viongozi wake.
  Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber amemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika Miaka 50 BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na lakisasa Kama hilo hivyo RC Makonda anaweka historia ya kwanza.

  Mufti amesema jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya kuona hata haibu hata kupokea ugeni wa viongozi wa kislamu ulimwenguni.Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja wamemuombea Dua RC Makonda pamoja na Rais Dr. John Magufuli kwa kuwezesha kujengwa kwa msikiti wa Mfalme wa Morocco wenye uwezo wa kuchukuwa watu 8,000 ampapo ujenzi unaendelea. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana. Wa pili kushoto ni Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe akiteta jambo na Naibu Meya Jumanne Ngede. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi.

  Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.

  Sehemu ya Wakuu wa Idara na Wageni waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana.

  Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi

  UJENZI wa stendi ya mabasi kubwa na ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma unatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi mwaka huu katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

  Jumla ekari 50 zimetengwa katika eneo hilo lililopo mashariki mwa Mji barabra ya Dodoma-Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamilika baada ya kipindi cha miei 24.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Mjini hapa kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali za kimaendeleo zilizotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 kinachoanzia Mwezi Septemba hadi Desemba 2018.

  Kunambi aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa, stendi hiyo ni kubwa na ya kisasa yenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi, na kwamba itakuwa ya mfano kwa Nchi zote za ukanda wa afrika Mashariki.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

  Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.

  Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

  Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo yaliyokusudiwa.

  “Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha yenu”,alieleza Matiro.

  Aidha aliiagiza Idara ya Maendeleo na Vijana ya halmashauri hiyo kuhakikisha inatembelea vikundi vya wajasiriamali na kufuatilia kikamilifu kama fedha zilizotolewa na serikali zinatumika kama inavyotakiwa.

  Matiro alitumia fursa hiyo kuwashauri vijana na wanawake kuunda vikundi vya ujasirimali watakavyovitumia kupata mikopo huku akisisitiza kuwa serikali haiwezi kutoa pesa kwa mtu mmoja mmoja.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Bakari Kasinyo Mohammed alisema kutolewa kwa mikopo hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayotaka vijana na wanawake wapewe asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ndani ya halmashauri.

  Alisema pia Mwezi Julai 2017, halmashauri hiyo ilitoa shilingi milioni 3 kwa vikundi viwili vya vijana na kimoja cha wanawake hivyo jumla ya fedha zote zilizotolewa kwa kipindi cha Mwezi Julai,2017 hadi Disemba, 2017 ni shilingi milioni 28.

  Wakizungumza baada ya kupokea hundi hizo za mikopo,wawakilishi wa vikundi hivyo waliishukuru serikali kwa kuwapatia mikopo wakidai kuwa hawakuwa na mitaji hivyo watatumia fedha walizopata kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo.

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa kukabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zilizotolewa na halmashauri hiyo.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza vijana na wanawake waliopata mikopo kutumia fedha walizopata kwa malengo waliyokusudia. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Bakari Kasinyo Mohammed. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira.
  Wawakilishi wa vikundi vya vijana na wanawake waliopata mkopo pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.

  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Bakari Kasinyo Mohammed akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi hundi za shilingi milioni 25 kwa ajili ya vikundi vya wanawake na vijana ambapo aliwataka kurejesha mikopo kwa wakati. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Vijana halmashauri hiyo, Deus Muhoja.

  Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 5,000,000/= kwa Joyce Charles aliyewakilisha Kikundi cha Wanawake na Maendeleo kilichopo katika kata Didia chenye wanufaika watano kinachojihusisha na utengenezaji wa sabuni.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 6,800,000/= kwa Majaliwa Kihangaji aliyewakilisha kikundi cha Umoja wa Bodaboda kinachojihusisha na ubebaji wa abiria kwa pikipiki kilichopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia chenye wanufaika 60.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 10,250,000/= kwa Methusela Jackson kutoka kikundi cha Jikwamue kilichopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia chenye wanufaika 20 kinachojihusha na ufyatuaji wa matofali ya saruji.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi hundi ya shilingi 2,290,000/= kwa Sham Moses kutoka kikundi cha Shukrani Group kilichopo katika kijiji cha Didia kata ya Didia chenye wanufaika 6 kinachojihusisha na uchomeleaji,uunganishaji vyuma na utengenezaji masofa.
  Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Vijana halmashauri ya wilaya ya Shinyanga , Deus Muhoja akiwaonesha vijana fomu ya kujaza taarifa za mikopo waliyopata.

  Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Vijana halmashauri hiyo, Deus Muhoja akiwasisitiza vijana waliokabidhiwa hundi za mikopo kuhakikisha wanatumia fedha walizopata kufanya maendeleo ili wajikwamue kimaisha.

  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.

  Zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la Steigler's Gorge katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji zimefunguliwa  leo tarehe 02 Februari, 2018.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zabuni hizo kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo amesema zabuni hizo ni za Awamu ya Pili kutokana na kukosekana kwa mshindi katika Awamu ya Kwanza iliyotangazwa mapema mwaka jana.

  Alisema kuwa, katika awamu ya kwanza jumla ya kampuni 81 zilinunua nyaraka za zabuni ambapo nakala moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 200,000 lakini ni kampuni nne tu zilifanikiwa kurejesha maombi na kuongeza kuwa kampuni zote nne hazikuwa na  vigezo vinavyohitajika hali iliyopelekea kutangazwa upya kwa zabuni tarehe 19 Desemba, 2017 katika vyombo vya habari  vya ndani na nje ya nchi.

  MacAchayo aliongeza kuwa, katika awamu ya pili kampuni 17 zilijitokeza katika ununuzi wa nyaraka kwa gharama ya shilingi 500,000 kwa kila moja ambapo mpaka siku zinafunguliwa ni kampuni tano tu zimerejesha nyaraka zenye maombi ya zabuni.

  Alisema hatua inayofanyika kwa sasa ni ufanyaji wa tathmini ya zabuni hizo na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa tathmini ya zabuni hizo waombaji wote watajulishwa mshindi na baada ya hapo zitafuata taratibu za mazungumzo, barua na kuandaa mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi mara moja.Aliwataka kampuni zilizowasilisha maombi kuwa watulivu wakati zoezi la tathmini likiendelea.
   Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo (mbele) akizungumza na wawakilishi wa kampuni mbalimbali zilizoomba zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji kwenye ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 02 Februari, 2018
   Mtaalam wa Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Jackson William (kulia) akieleza jambo kwenye ufunguzi huo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi kutoka Wizara ya Nishati, Amon MacAchayo na aliyekaa kushoto ni mwakilishi wa kampuni zilizoomba zabuni,  Khaled Makkawy kutoka kampuni ya  The  Arab Contractors
   Sehemu ya wajumbe wakifuatilia zoezi la ufunguaji wa zabuni kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji katika kikao hicho.
  Wataalam kutoka Idara ya Manunuzi, Wizara ya Nishati wakifungua nyaraka mbalimbali za zabuni katika kikao hicho.

  0 0

   
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa wakimwongoza mlemavu wa maungo Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga kwenye Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi mlemavu wa maungo Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. Kulia ni ke w Bw. Ndemanga, Bi. Hawa Mohamed.
  mlemavu wa maungo Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga na mkewe Hawa Mohamed Wakiondoka na Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Abdulrahman Ndemanga ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam Agosti 25, mwaka jana. Bw. Ndemanga alimuomba Rais msada wa kupatiwa Bajaji ili ajimudu kiusafiri na kiuchumi.

  Picha na IKULU

  0 0

  Na Mary Gwera
  Katika mwendelezo wa Utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) (2015/2016-2019/2020), Mahakama ya Tanzania inaendelea na jitihada za kupata uzoefu na ujuzi kutoka katika Mahakama mbalimbali duniani zilizopiga hatua katika maboresho ya huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

  Haya yamejidhihirisha kufuatia ugeni wa Maafisa wa Mahakama waliowasili kutoka nchini Guatemala kwa mualiko wa Mahakama ya Tanzania kushiriki katika Hafla ya Siku ya Sheria nchini, iliyofanyika Februari 01, 2018 vilevile Mahakama ya Tanzania kupata maoni na ushauri zaidi wa jinsi ya kuendelea kuiboresha Mahakama nchini kwa manufaa ya wananchi ambao ndio walengwa Wakuu.

  Akiwatambulisha wageni hao kwa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Februari 1 katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu, Mahakama ya Rufani Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga alisema kuwa takribani miaka mitatu sasa baadhi ya Maafisa wa Mahakama nchini walifanya ziara nchini Guatemala kwa lengo la kujifunza ni kwa namna gani Mahakama nchini Guatemala imefanikiwa katika utoaji wa huduma zake.

  “Mhe. Jaji Mkuu, tulichojifunza na tukaona ni vyema kuiga kutoka Guatemala ni pamoja na huduma ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’, ufanyaji kazi wa Mahakama kwa masaa 24, kuweka mbele matumizi ya teknolojia katika shughuli zake  n.k, hivyo tumeona ni vyema pia kwa Mahakama nchini kupata utaalamu/uzoefu kutoka kwa wenzetu jinsi ya kuweza kutekeleza haya,” alisema Bw. Kattanga.

  Mahakama ya Tanzania imeonyesha nia ya dhati katika suala zima la maboresho, hivyo basi ujio wa Wageni hawa ambao watakuwepo nchini kwa takribani siku 5, utawezesha Wataalamu wa Mahakama kupata uzoefu na ujuzi zaidi wa namna gani Mahakama zinazotembea zinavyofanya kazi n.k.
  Aidha; kwa upande wake, Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake wa Mahakama nchini Guatemala, Mhe. Osvaldo Mendez alisema kuwa Mahakama nchini humo amepiga hatua kubwa katika suala zima la Matumizi ya TEHAMA hali ambayo imesaidia kurahisisha utendaji na kutoa haki kwa wakati.

  “Mahakama yetu pia inafanya kazi masaa 24, na tunatoa huduma hii katika Miji mikubwa mitano nchini Guatemala na tunafanya kwa ushirikiano na Wadau wetu wa Mahakama kama Waendesha Mashitaka ‘Prosecutors’ n.k ili kufanikisha kumaliza mashauri hayo kwa muda muafaka,” alieleza Mhe. Mendez.

  Mpango Mkakati unaotekelezwa na Mahakama umegawanyika  katika nguzo kuu tatu ambazo ni Utawala na Menejimenti bora ya Rasilimali, Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati na kuimarisha imani ya Jamii na Ushirikishaji wa wadau katika shughuli za Mahakama; nguzo zote zikilenga katika uboreshaji wa huduma za Mahakama.
    Jaji Mkuu wa Tanzania (pichani) akiwa katika mazungumzo na Wageni hao (hawapo pichani), katika mazungumzo yao Mhe. Jaji Mkuu amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na Mahakama nchini Guatemala.
   Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akiongea jambo na Wageni hao, Mhe. Wambali aliwaelezea Wageni hao juu ya Mfumo wa Mahakama nchini.
    Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi mbele) akiwa pamoja na baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Kiongozi, Mtendaji Mkuu na Ugeni kutoka Mahakama nchini Guatemala pindi Wageni hao walipomtembelea Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akizungumza jambo katika kikao hicho.
   Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake wa Mahakama nchini Guatemala, Mhe. Osvaldo Mendez akizungumza jambo.
   Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik akiongea jambo katika kikao hicho.
  Picha ya pamoja baada ya mazungumzo.
  (Picha na Mary Gwera, Mahakama)


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa salamu zake za maadhimisho ya Wiki ya Sheria. P_20180201_120651_1_vHDR_OnMkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo  (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga John Mgeta (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu  wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga  Dk. Adam Mambi  (wa pili kutoka kulia) na Mwanasheria wa Serikali mkoa wa Rukwa Prosper Regerera. P_20180201_120710_vHDR_On  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo  akisalimiana na  Jaji Mkuu   wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga  Dk. Adam Mambi. 
  ………………….
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema maboresho ya TEHAMA yanayofanywa na mhimili wa mahakama nchini utasaidia kupunguza foleni za wananchi wanaofika ofisi za Wakuu wa Wilaya na kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta haki zao.
  Amesema kuwa kitendo cha mwaanchi kuweza kujua mwenendo wa kesi bila ya kufika mahakamani ni maendeleo makubwa yanayofikiwa na mhimili huo na kuwaasa kuanza kufanya kazi baada ya kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.
  Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo hufanyika tarehe 1, Februari ya kila mwaka katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi.
  “Mwaka 2018 na jitihada zilizofanyika na mahakama umekuwa mwanzo mzuri, wananchi watajitokeza kutafuta elimu hii ya sheria na wanapoipata itatupunguzia msongamano kwenye ofisi zetu za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ili tufanye kazi za maendeleo sio kusuluhisha migogo ya ndoa, mirathi na ardhi ambayo yote imekaa katika misingi ya kisheria,” Alieleza.
  Na kuongeza kuwa elimu hii ya sheria iendelee kutolewa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati huku wakizingatia kaulimbiu ya maadhimisho hayo inayosema “Matumizi ya TEHAMA kwa kutoa haki kwa wakati na kuzingatia maadili.”
  Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga John Mgeta ametahadahrisha matumizi mabaya ya Teknolojia katika kuvunja maadili na misingi ya mahakama na utu kwani watu hutumia teknolojia hiyo kuendeleza rushwa kupitia namba za simu za mahakama.
  “Mtumishi wa mahakama anaweza kutumia simu kuwasiliana na mtu akimuomba rushwa au kufanya miamala ya pesa, vyombo vya habari na wananchi ambao wanakiuka maadili kwa kutumia simu na TEHAMA, sisi tunasisitiza matumizi haya yazingatie maadili,” Alibainisha.
  Awali akitoa taarifa ya chama cha wanasheria Tanzania Wakili Baltazar Chambi amesema kuwa mahakama ya Tanzania kwa kutumia TEHAMA itafikia suluhu mojawapo ya uhakika wa utoaji wa haki kwa wakati kwa kulitambua hilo wadau wa haki ni vyema wakajua matumizi ya TEHAMA ili kuleta ufanisi katika kazi zao.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria msiba wa Rubani wa Ndege za Serikali, Marehemu Kapteni Dominic Bomani aliyefariki jana kwa ajali ya ndege kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Rosemary Bomani mjane wa aliyekuwa Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rosemary Bomani mjane wa aliyekuwa Rubani wa Ndege za Serikali Marehemu Kapteni Dominic Bomani, wengine pichani ni mtoto wa marehemu Joanitha Bomani (kulia) na Dada wa marehemu Stella Bomani(kushoto) wakati alipoenda kuwapa pole nyumbani kwa marehemu Kinyerezi Kanisani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Mamlaka ya mapato mkoani Mtwara (TRA) imezifungia hotel tatu mkoani humo pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa kodi ya malimbukizo ya madeni.

  Hotel zilizofungiwa ni Naff Beach, Naf blue, BNN pamoja na kituo cha Mnarani Petrol Station ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya Shilingi bilioni moja ,ambazo ni malimbukizo ya madeni ya nyuma kwa kipindi cha miaka mitatu.

  Afisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.

  “Ni madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma,kikubwa walipe kodi,tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbikizo ya madeni ya muda mrefu,matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii sheria za kodi kama kutunza kumbukumbu,”amesema Byabato

  Byabato amesema endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao watachukua hatua nyigine kama kukamata mali au kuwapeleka mahakamani,kama hawatajitokeza kuomba na kuahidi ni lini watalipa madeni kwani hakuna aliyejitokeza kufanya hivyo.

  Aidha amesema pia yapo maduka madogo ambayo yamefungiwa na kwa sasa wako wilayani Masasi wanaendelea na ukaguzi.

  Pichani hoteli ya Naff Beach ikiwa imezungushiwa utepe na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  0 0

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza katika  hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika  hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akigawa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde  na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Wanafunzi wakiwa katika hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.

  Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma akiwa na vion.ozi mbalimbali.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akikabidhi kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma akiwa na vion.ozi mbalimbali.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) kwa kazi kubwa anayofanya ya kuwaletea wananchi maendeleo hasa katika kuboresha sekta ya Elimu jimboni humo.


  Ulega ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya ugawaji wa kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari 22 leo katika Viwanja vya Nyerere Square-Dodoma.


  Kompyuta hizo 22 zenye thamani ya Sh. Milioni 44 na zimetolewa na Mbunge Mavunde pamoja na wadau wa maendeleo katika kusaidia kuboresha sekta ya Elimu jimboni hapo.


  Naibu Waziri Ulega amesema kwa sasa Dodoma ni Makao Makuu hivyo Mavunde  anapaswa kupongezwa kwa jitihada zake katika sekta ya elimu.

  Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga amesema   kuna baadhi ya wazazi hawajawahamisha watoto wao Mkoani humo kutokana na uhaba wa shule  hivyo kupitia jitihada za Mbunge huyo shule zitaongezeka na idadi ya wanafunzi itakuwa kubwa.
  Akizungumza katika hafla hiyo, Mavunde ameahidi kuzipatia kompyuta shule zote 130 na kuahidi kuboresha miundombinu ya nishati katika shule zote ili wanafunzi wengi zaidi wapate nafasi ya kujifunza kwa kutumia teknolojia ikiwa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kieletroniki katika mashule ambao ulitanguliwa na ugawaji wa vishkwambi (tablets)500 zenye thamani ya Sh.Bilioni 1.


  Amesema Jimbo lake lina upungufu wa madarasa 1038 hivyo  kwa  kupitia mfuko wa Jimbo atatoa sh.milioni 55 ambazo zitatumika kufyatua matofali ili kupunguza upungufu huo.


  Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi ameahidi kushirikiana na Mbunge kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.


  0 0

  Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi.
  Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imetoa sh. milioni 208.5 kwa ajili ya kuwezesha kaya maskini katika kipindi cha Januari hadi Februari.
  Mratibu wa TASAF wilaya hiyo, Sospeter Nyamuhanga amebainisha hayo jana ambapo amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kaya 5959 katika vijiji 78 vilivyopo wilaya humo.Alisema kuwa zoezi hilo limeendelea kupata mafanikio kutokana na walengwa wengi kufanyia kazi elimu wanayopewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha hizo wanazowezeshwa.
  Nyamuhanga aliongeza kuwa kutokana na ufuatiliaji unaofanyika nyakati tofauti baadhi ya kaya zimeonesha mabadiliko kimaisha ambapo zimetumia fedha hizo kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.
  Alifafanua kuwa katika kaya hizo imebainika kuwa wanufaikaji wameweza kununua mifugo ikiwemo mbuzi, kondoo  na kuku huku wengine wakifanya biashara ndogondogo.Aidha, alisema baadhi ya walengwa tayari wamebadilisha aina za makazi yao kutoka nyumba za tembe na nyasi za awali na kuanza kujenga nyumba za kisasa za bati hali inayoleta matumaini katika miradi kama hii.
  “Lengo la mpango wa TASAF siku zote ni kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi na ndiyo maana mara kwa mara katika mazoezi haya tunatoa elimu ili kuwaelekeza namna bora kutumia fedha wanazowezeshwa,” alisema.
  Mratibu huyo alisema pamoja na mambo mengine pia walengwa wanapopata fedha hizi wanawajibika kuwapeleka watoto wao shule na kliniki kama ambavyo masharti yanavyoelekeza.Alisisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto wa walengwa kwani wanavyoelimika ndivyo wanaondosha umaskini na kuchangia kujikwamua katika umaskini kwa kaya zao.
  Pia aliendelea kuwataka walengwa wanaonufaika na fedha hizo za mpango huo wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kupata matibabu wakati wowote wanapohitaji.   TASAF imekuwa ikitoa ruzuku ya msingi kwa kaya zote maskini zilizoandikishwa kwenye mpango na nyingine ya utimizaji masharti ambayo hutolewa kwa kaya zenye watoto wanaotakiwa kwenda shule na vituo vya kutolea huduma za afya.
  Kishapu ni miongoni mwa halmashauri za wilaya 161 za Tanzania Bara, Unguja na Pemba zinazotekeleza Mpango wa TASAF III ili kuongeza kipato na fursa za kuboresha upatikanaji wa mahitaji muhimu.
   Zoezi la uwezeshaji Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) likiendelea katika kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo ambapo mmoja wa walengwa akiwawezeshwa ruzuku.
   Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamuhanga (wa pili kulia waliosimama) akipata maelezo kuhusu zoezi hilo alipofika kufanya ufuatiliaji kijiji cha Wela kata ya Uchunga.
   Sehemu ya walengwa wa TASAF wakiwa katika zoezi la uwezeshaji kwenye kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
  Zoezi likiendelea katika kijiji cha kijiji cha Wela kata ya Uchunga.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Rayal Village Dodoma Februari 01, 2018.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Dodoma.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akionesha ishara ya umoja na mshikamano wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) uliofanyika Dodoma.
   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) aliowasilisha katika mkutano huo.
   Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Bw. Suleiman Kikingo akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho uliofanyika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa uliofanyika Dodoma.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kupitishwa kwa muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii utasaidia kuwanufaisha watumishi wa umma kwa kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakati na wenye tija.

  Amebainisha hayo wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) walipokutana Mjini Dodoma katika warsha ya siku tano kuanzia Januari 29 hadi Februari 02, 2018 kujadili masuala ya wafanyakazi nchini.

  Waziri Mhagama alieleza kuwa, kupitiswa kwa muswada ni moja ya utekelezaji wa takwa la Ibara ya 11 kifungu kidogo cha kwanza cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulipoona umuhimu wa kuweka mifumo ya hifadhi ili Watanzania wapate manufaa hasa siku za uzeeni.

  “Maamuzi ya kuwa na Muswada huu umezingatia taratibu zote za kisheria ikiwemo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sera ya Hifadhi ya Jamii, Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani unaoongoza katika maswala ya Hifadhi ya Jamii”.Alisisitiza Mhagama
  Muswada huu umelenga kuunganisha mifuko ya Pensheni ambayo ni PSPF, LAPF, GEPF NA PPF ili kukidhi kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi cha kuunganisha mifuko hiyo ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuwa na mfumo madhubuti utakaohakikisha mwanachama anapata mafao kwa wakati.

  “Muswada umebainisha kuwa jumla ya mafao 7 yatakayolipwa na mfuko huo itakuwa:  Fao la Pensheni, Warithi, Ulemavu, Uzazi, Ukosefu wa Ajira, Ugongwa na Fao la kufiwa.” alifafanua Waziri Mhagama.

  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TALGWU Bw. Tumaini Nyamhokya aliipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kueleza kuwa ni wakati mwafaka kwa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kuunga mkono juhudi za Serikali ikiwemo kuunganishwa kwa mifuko hii kwa manufaa ya wafanyakazi wote wa umma.

  “Niwaombe watumishi wa umma wote kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha maslahi ya watumishi na kwa asilimia 98 muswada huu umeyapitisha mapendekezo na ushauri uliotolewa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na kuwekwa kwenye utekelezaji.”Alisema Nyamhokya.

  Naye, Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Suleiman Kikingo alisema kuwa kuunganishwa kwa mifuko hiyo na kuwekwa kwa tozo ya asilimia tano kwa mfuko utakao bainika kushelewesha mafao ya mwanachama itasaidia kupunguza changamoto ya ucheleweshwaji wa mafao kwa wanachama.


  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akijibu maswali bungeni Mjini Dodoma, Leo 2 Februari 2018

  Na Mathias Canal, Dodoma


  Serikali imesema kuwa Zoezi la upokeaji na usambazaji wa viuwadudu linaendelea na hadi kufikia tarehe 24 Januari, 2018 jumla ya chupa 1,733,139 za viuwadudu zimekwisha kusambazwa kwa wakulima na chupa nyingine 7,287,216 zitaendelea kusambazwa kati ya sasa na  mwezi Machi, 2018 ili kukidhi mahitaji katika msimu huu wa kilimo.


  Hayo yamebainishwa leo 8 Februari 2108 na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akijibu Swali la Mhe Khadija Hassan Aboud Mbunge wa Viti Maalumu Zanzibar aliyetaka kufahamu namna ambavyo serikali imejipanga kukidhi mahitaji ya viuwadudu kwa wakulima wa Pamba nchini.


  Alisema kuwa Katika Msimu wa Kilimo 2017/2018 wakulima wameitikia kwa vitendo azma ya Serikali ya kuimarisha kilimo cha pamba nchini kwa kuongeza eneo linalolimwa pamba kutoka wastani wa ekari 1,000,000 hadi wastani wa ekari 3,000,000, Kutokana na mwitikio huo, hadi tarehe 22 Desemba, 2017 jumla ya ekari 1,500,000 zilikuwa zimelimwa na kupandwa zao la Pamba na kuhitaji chupa (acrepacks) 4,500,000 za viuwadudu.


  Alisema, kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha wakulima wameendelea kupanda pamba ambapo hadi tarehe 24 Januari 2018 taarifa zinaonyesha kuwa jumla ekari 3,006,785 zimelimwa pamba ambapo Kutokana na eneo hilo kulimwa pamba, makisio ya chini ya uzalishaji wa pamba ni kilo milioni 600 sawa na tani 600,000 za pamba.


  Eneo lote lililo limwa pamba linahitaji jumla ya chupa 9,020,355 za viuwadudu zenye thamani ya shilingi bilioni 36 ambapo Serikali kupitia Bodi ya Pamba Tanzania imenunua jumla ya chupa 5,300,000 na Kampuni binafsi zimenunua chupa 450,000. 


  Aidha, jumla ya vinyunyizi vipya 16,500 vimenunuliwa ambapo kati ya vinyunyizi hivyo 10,157 vimekwisha kusambazwa kwa wakulima na usambazaji unaendelea huku vinyunyizi 6,000 vikiwa vimekarabatiwa ili kutosheleza mahitaji ya wakulima.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kushoto) akimkabidhi Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof Ratlan Pardede Mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Simiyu.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akifurahia jambo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akisalimiana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ofisini kwake Jijini Dar es salaam.  Na Mathias Canal

  Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa simiyu Mhe Antony Mtaka kuendeleza ushirikiano na Mkoa wa Simiyu ili kuboresha sekta ya Afya kupitia Irish Aid.

  Balozi huyo ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya pamoja na Mhe Mtaka ambapo tayari kwa pamoja wamekubaliana kuanza kutekelezwa wa kusudio hilo tarehe 6 Februari 2018 kwa kuanza na timu ya wataalamu kufika Mkoani humo ili kuanza haraka shughuli hiyo.

  Balozi H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi Mhe Mtaka kuwa tayari nchi yake ya Ireland imekusudia kwa dhati kushirikiana vyema na Mkoa huo huku akisisitiza kuendelea kushirikiana zaidi pia katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwenye sekta ya Mifugo, Kilimo na Utalii.

  Balozi wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ametoa kauli hiyo ya kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka za kutoka kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji wakati alipokutana na kufanya mazungumzo leo 2 Februari 2018 katika.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amemshukuru Balozi Sherlock kwa ubalozi wa Ireland kukubali kuwezesha safari ya mafunzo kwa wataalamu wawili kutoka Mkoani Simiyu kwenda nchini Ireland kuanzia Februari 12 mpaka 16 Machi 2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hasa kwenye upande wa uhifadhi wa Data za Mkoa. 

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Mhe Mtaka alikutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon ambapo pamoja na mambo mengine Shirika hilo limetoa zaidi Bilioni 3 kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya na upasuaji ndani ya Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu.

  Pia UNFPA imeahidi kutoa magari kwa Halmashauri 6 za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, ambapo tayari UNFPA wameamua kujenga ofisi yao ndogo ndani ya Mkoa wa Simiyu itakayoratibu shughuli mbalimbali za shirika hilo kwa mikoa yote ya kanda ya ziwa.

  Wakati huo huo Mhe Mtaka amekutana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof Ratlan Pardede ambaye pamoja na mambo mengine amekubali kutembelea Mkoa wa Simiyu mwezi Macih mwaka huu 2018 huku akiwaalika wataalamu wa Mkoa wa Simiyu nchini Indonesia mwezi Aprili mwaka huu.

  Aidha, Balozi huyo Prof Pardede alisema kuwa pia sekta rasmi ya Indonesia itazuru Mkoani Simiyu ili kuona uwezekano wa kujenga kiwanda kitakachosaidia kuongeza thamani ya zao la pamba, kuboresha mkoa dada wa Indonesia na Simiyu katika mazao ya Mpunga na pamba pamoja na kualika wawekezaji wa Indonesia kuwekeza Mkoani Simiyu kwa kuzingatia Mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Mkoa huo (Simiyu Investment Guide) ambao ameusifia kwamba ni wa kipekee na alipouona mwongozo huo kupitia mtandao wa Youtube aliona ukiwa umeitangaza sana Tanzania na wafanyabiashara wa Indonesia walihamasika sana kuuona na kuusoma katika Tovuti hiyo.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwa ameongozana na baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri ya mji wa Geita pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya ya Geita kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo magogo .
  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipokewa na katibu tawala wa wilaya ya Geita,Thomas Dimme wakati alipowasili kwenye mradi wa vijana na wanawake wa magogo.
  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akipokea taarifa ya uchunguzi ambao umefanyika juu ya mradi wa vijana na wanawake kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly.

  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua baadhi ya vifaa ambavyo vilikuwa kwenye sehemu ya chakula(Kantine).
  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akiwa kwenye kalakana ya uchomeleaji wakati alipofika kujionea vifaa vilivyopo kwenye mradi huo.
  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipokea maelezo ya mashine ya kuchomelea kutoka kwa mmoja kati ya wahusika kwenye kamati ya uchunguzi.
  Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua mashine ya kufyatulia matofali ya kisasa.
  Na Joel Maduka,Geita

  Serikali Mkoani Geita imeeleza kusikitishwa na uendeshwaji wa miradi ya mgodi wa dhahabu wa Geita, (GGM) kwa kutozingatia sheria ya ushirikishaji kwa Halmashauri zilizopo mkoani humo na kushindwa kujulikana kwa gharama za miradi ya jamii inayotekelezwa na mgodi huo.

  Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kukabidhi mradi wa Maendeleo ya uchumi kwa Vijana na Wanawake ulipo Mtaa wa Magogo Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.

  Hali hiyo ilimlazimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi kuzulu kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo kata ya Bomba mbili ,mtaa wa magogo kwa lengo la kujiridhisha baadhi ya vifaa ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo na hata hivyo amebaini kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye vifaa ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo.

  Luhumbi alisema baadhi ya watumishi kutoka serikalini na baadhi yao kutoka GGM wameendelea kushirikiana kwa pamoja kuhujumu miradi mingi ambayo imekuwa ikilenga kuleta chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Geita ambao wamezungukwa na Mgodi huo na kufuatia hatua hiyo ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili kuwabaini wale wote ambao wameshiriki kuchakachua fedha za miradi hiyo.

  “Sasa katika miradi yote ishirini na sita (26) ambayo imekwenda yote ina matatizo na ajabu mwaka huu niliambiwa kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya CSR ya mwaka huu nilikagua baadhi ya miradi kuna mradi mmoja nilikuta ni wa bilioni moja nukta sita lakini mimi siwezi kuficha hata tukitumia fedha vibaya kidogo tunaweza kutumia milioni mia tatu (300) lakini bilioni moja nukta tatu inapotea na watu kutoka ofisi zetu walikwenda mgodini wakaa na kuweka mkataba wakurugenzi hawakuwepo mkuu wa wilaya afahamu baadae tunaambiwa fedha ipo tayari kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo nimesema sisi kama mkoa hatubariki miradi hiyo kabisa”Alisema Luhumbi.

  Hata hivyo kutokana na kuonekana upungufu kwenye miradi ya jamii Mhandisi Luhumbi amewakataa maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM kutokana na kushindwa kufanya shughuli zao kwa weledi kwenye maeneo waliyopangiwa na mgodi huo.

  Na pia ameviagiza vyombo vyote vya sheria kuhakikisha wanaingia kwa undani zaidi na kufanya uchunguzi wa kutosha na ndani ya wiki moja endapo kuna mtumishi wa serikali atakayebainika kuhujumu basi sheria ichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha.

  Afisa sheria wa Mkoa huo Bi Sarah Mwangole alisema mradi wa Magogo ambao umekabidhiwa hivi karibuni umefanyika bila ya makubaliano baina ya Halmashauri na mgodi wa GGM hivyo pia wameshauri vyombo vya sheria kuingilia na kufanya uchunguzi na kwamba hadi sasa ofisini kwao hawajapata nyaraka zozote za mradi huo licha ya kuzihitaji.

  Mtandao huu umezungumza na Msimamizi wa kitengo cha mahusiano kwenye mgodi wa GGM Bw Joseph Mangilima ambaye alisema mengi ya mambo yaliyozungumziwa hawezi kuyazungumzia yeye kwa kuwa hayahusiani na kitengo chake moja kwa moja na kwamba kazi iliyompeleka kwenye mradi huo ni kupeleka funguo za majengo baada ya kusikia mkuu wa mkoa anautembelea mradi huo.

older | 1 | .... | 1505 | 1506 | (Page 1507) | 1508 | 1509 | .... | 1898 | newer