Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Binti mwenye umri chini yaa miaka 18 akiwa amembeba motto wake mdogo baada ya kukatishwa ndoto zake za kupata masomo na kijana.
baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida. 
baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida. 
Meneja wa World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja Kulangwa akiwasilisha mada juu ya madhumuni ya semina hiyo kwa wananchi waliohudhuria kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alipokuwa akizindua mpango wa mapambano dhidi ya ndoa za utotoni kwenye ukumbi wa Kanis Katoliki,mjini Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).


Na,Jumbe Ismailly SINGIDA 

TATIZO la ndoa za utotoni katika Tanzania na nchi za Afrika Mashariki limeonekana ni tatizo kubwa sana katika maeneo hayo ambapo kitakwimu inaonyesha kuwa kati ya mikoa kumi bora Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na asilimia 59 na Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya nane kwa kuwa na asilimia 42.

Meneja wa Shirika la kidini lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja kulanga aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa mpango wa kutokomeza mimba za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.

Alifafanua kwamba kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tanzania Demokratic Health Survey ya mwaka 2010 inaonyesha kitakwimu kwamba tatizo la ndoa za utotoni,Mkoa unaoongoza ni Mkoa wa Shinyanga wenye asilimia 59 huku Mkoa wa Singida ukiwa na assilimia 42 na hivyo kushika nafasi ya nane katika mikoa hiyo kumi bora.

“Kwa maana kwamba ule utafiti huwa unakwenda kuuliza kila nyumba na wakiuliza katika kila nyumba mama alipata ujauzito katika umri gani,wale waliopata mimba katika umri chini ya miaka 18 ilikuwa ni asilimia 59.”alifafanua Kulanga.

Kwa mujibu wa Meneja huyo katika asilimia 42 ya familia zilizoulizwa kina mama kwamba alipata ujauzito akiwa na umri chini ya miaka 18,asilimia 42 wakaonekana ilikuwepo na kwamba shirika hilo lilifanya utafiti katika Kanda saba kwenye maeneo wanayofanya kazi.

Aidha Meneja huyo aliweka bayana kwamba kanda hiyo ina jumla ya kanda saba ambazo ni pamoja na Kanda ya Pwani ambayo ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na kanda ya kati ambayo ni pamoja na Mkoa wa Singida ambapo kitakwimu inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la ndoa za utotoni.

Kwa upande wake Afisa wa dawati la jinsia na Watoto kutoka jeshi la polisi wilaya ya Singida,Amina Fakih Abdallah alibainisha kuwa kinachochangia kwa namna moja au nyingine kuwepo kwa ongezeko la mimba za utotoni ni ukinzani wa sheria zinazosimamia mimba za utotoni.

Hata hivyo afisa huyo wa dawati la jinsia na watoto alisisitiza pia kwamba katika sheria zinazosimamia ndoa hizo za utotoni,hakuna sheria iliyosimama na inayolinda mimba za utotoni kutokana na moja ya sheria hizo kuruhusu mtoto aolewe akiwa na umri wa miaka 14 huku sheria ya jinai inakataza motto mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.

“Sasa kama inalinda mimba za utotoni kuna sheria inaruhusu mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka 14,sasa hii sheria inaporuhusu mtoto aolewe akiwa na umri wa miaka 14,we huku kwenye sheria ya jinai unasema kwamba huyu mtoto aliye chini ya miaka 18 haruhusiwi kuolewa”alifafanua.

Naye Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo akizindua Mpango wa mapambano dhidi ya kutokomeza ndoa za utotoni za mradi wa Mtinko ADP uliopo wilaya ya Singida alisisitiza pia juu ya kuondoa mapungufu yaliyopo katika sheria zinazosimamia mimba za utotoni ili ziweze kufanana badala ya kuendelea kukinzani.

Kwa mujibu wa Tarimo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo sheria zote hizo hazina budi kutamka bayana kwamba umri wa motto usizidi miaka 18,ikiwemo sheria ya ndoa,sheria ya motto mwenyewe na kipengere kinachotamka kuwa motto anaweza kuolewa kwa kibali cha wazazi.

SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI

$
0
0
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Umma kupima maeneo yao na kuyawekea alama za mipaka ili kuepusha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi.

Waziri Lukuvi amesema hayo mara baada ya kukagua maeneo yaliyo na migogoro ya ardhi katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Aidha Mheshimiwa Lukuvi akiambata na Naibu wake ambaye ni mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza walitembelea maeneo yaliyovamiwa na wananchi ya Polisi Kigoto-Kirumba lililovamiwa na wananchi, Uwanja wa Ndege wa Mwanza na eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Nyamirolerwa katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kutokana na kujionea uvamizi huo wa maeneo hayo, Waziri Lukuvi amezitaka taazizi zote za serikali kupima maeneo yao ili wananchi waweze kutambua maeneo ya Serikali wasiweze kuyavamia jambo ambalo huzaa migogoro.

Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi waliojenga ndani ya hifadhi ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuondoa maendelezo yao ndani ya siku saba kabla kuchukuliwa hatua kwakuwa ni wavamizi na hawaruhusiwi kukaa karibu na eneo linalorusha na kutua vyombo vya anga jambo ambalo ni hatari kwao na usalama wa vyombo hivyo.

"Hawa waliojenga ni wavamizi na watambue hivyo majibu tutatoa badaye nini tutafanya lakini wajue maisha yao siyo ya hapo ndani ya uwanja," alisema lukuvi.Na katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amezitaka halmashauri zote nchini kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.

Aliyasema hayo baada ya kukutana na watumishi na wakuu wa idara wa Manispaa ya Ilemela na wa jiji la Mwanza wakati wa ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi na maendeleo ya zoezi la urasimishaji makazi moani Mwanza.

"Kazi ya ulipaji kodi sio jambo la hiari ni lazima, kila Mkurugenzi katika wilaya yake ifikapo Aprili 30, mwaka huu awe ameshja kusanya kodi na baada ya hapo watakaoshindwa kutekeleza nitatangaza majina yao katika magazeti ya umma na wataenda kulipia mahakamani, ili malengo yetu yatimie," amesema Lukuvi

Aidha Lukuvi amezitaka halmashauri zote kupima viwanja vyote na kuwaagiza maafisa ardhi kutoa hati kwa wananchi kulingana na majina yao halisia kama yalivyo katika vitambulisho vya taifa vilivyosajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuepusha usumbufu wakati wa uingizwaji katika mfumo.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa zoezi la urasimishaji makazi na makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi, Mkuu wa Idara ya mipango miji na ardhi Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando, alisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni wananchi kuvamia maeneo yaliyopimwa na kutengewa Kwa ajili ya matumizi ya umma .

"Kwa mwaka huu wa fedha hadi kufikia sasa tumekusanya Sh bilioni 1.8 sawa na asilimia 72 ya lengo la makusanyo ya Sh bilioni 2.5, na jumla ya hati 5,277 Kati ya hati 16,141 zimeandaliwa katika maeneo yaliyorasimishwa Huku jumla ya viwanja 35,336 tayari vimeingizwa katika mfumo, " alisema.

RAIS DKT MAGUFULI ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU ROBERT KISANGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na mtoto wa marehemu Amani Kisanga alipowasili na Mama Janeth Magufuli kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na mtoto wa marehemu Amani Kisanga alipowasili na Mama Janeth Magufuli kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwafariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga na mtoto wa marehemu Amani Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya maombi pamoja na mjane wa marehemu Mama Maria Kisangana mtoto wa marehemu Amani Kisanga na waombolezaji wengine baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa waombolezaji baada ya kutoa  heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa waombolezaji baada ya kutoa  heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa waombolezaji baada ya kutoa  heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Mama Janeth Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mtoto wa marehemu, Amani Kisanga, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. Pamoja nao kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma na kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mtoto wa marehemu, Amani Kisanga, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. Pamoja nao kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma na kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.  

 Waheshimiwa Majaji na waombolezaji wengine wakiwa kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  
 Waheshimiwa Majaji na waombolezaji wengine wakiwa kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph sinde Warioba akiwa na waombolezaji wengine kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  
 Majaji Wastaafu na waombolezaji wengine kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Kiongozi  Jaji Ferdinand Wambali baada ya kutoa  heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  baada ya kutoa  heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Joseph sinde Warioba  baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018. 
 Kikosi cha Skauti kikiwa chini  Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania MheshimiwaAbdulkarim Shah kikiwa tayari kuhudumia kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 28, 2018.  Picha na IKULU

CHUO CHA KODI KUWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA FORODHA ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar (ZFB) Omar Hussein Mussa wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano katika kuwajengea uwezo wanachama wa ZFB.

Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar Omar Hussein Mussa wakizungumza na wajumbe wa Kamati ya Makubaliano kutoka Chuo cha Kodi (Kulia) na Zanzibar (kushoto) kabla ya kusaini hati za makubaliano katika chumba cha mikutano ITA.


Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar (ZFB) Omar Hussein Mussa (wa pili Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA) Stephen Ngatunga (wa kwanza kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ushirikiano mara baada ya kusaini makubaliano ya kuwajengea uwezo mawakala wa Forodha Zanzibar. (PICHA ZOTE NA OLIVER NJUNWA).

…………………………………………………………………………………..

Na Oliver Njunwa- Dar es Salaam

Chuo cha Kodi (ITA) pamoja na Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar (ZFB), vimeingia katika makubaliano ya kushirikiana katika kuwajengea uwezo Mawakala wa Forodha Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano hayo, iliyofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Kodi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo amesema kwamba, makubaliano hayo ni muhimu kwani kila upande una watalaam wa kutosha kuwasaidia Mawakala wa Forodha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“ITA inajivunia utaalam wake wa kufundisha na ZFB ina utaalamu katika masuala ya kiforodha. Kwa hiyo wote kwa pamoja tutashirikiana ili malengo ya makubaliano haya yaweze kufikiwa”, alisema Prof. Jairo.

Prof. Jairo aliongeza kuwa, katika makubaliano hayo, Chuo cha Kodi kitatoa mafunzo ya muda mfupi na utaalamu wa masuala ya forodha kwa ZFB ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na Mawakala wa Forodha wanaofanya kazi kwa weledi.

Mkuu wa Chuo cha Kodi pia amesema kwamba lengo la vyuo sio kupata fedha bali kutoa wataalamu wa kutosha ambapo uwezo wa Chuo hupimwa kwa idadi ya wanafunzi wanaohitimu na aina ya sifa walizonazo.

Aidha, Prof. Jairo ameiomba ZFB kulinda hadhi ya jina la Chuo cha Kodi kwani kina jina zuri kutokana na uzoefu wake wa kutekeleza makubaliano ya ushirikiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“ITA ina makubaliano na Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) pamoja na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) na kwa nchi za nje ina makubaliano na Malawi, Zambia, Botswana na iliisadia Sudan Kusini kuanzisha Mamlaka ya Mapato nchini humo”, alisema Prof. Jairo.

Makubaliano hayo yamefanyika katika Chuo cha Kodi Dar es salaam Ijumaa tarehe 26 Januari 2017 na kutiwa saini kati ya Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar Omar Hussein Mussa na kushuhudiwa na Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) Stephen Ngatunga.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar ZFB, Omar Hussein Mussa amesema kwamba makubaliano hayo ni msingi mzuri wa kupata Mawakala wa Forodha wenye weledi na hivyo kupunguza changamoto zinazojitokeza katika tasnia ya uwakala wa forodha.

“Makubaliano haya ni jambo jema na yatakuwa endelevu kwa kuwa sisi tuko tayari kuhakikisha yanaleta mabadiliko katika utendaji wa mawakala wetu wa Forodha”, alisema Bw. Mussa.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania Stephen Ngatunga ambaye alihudhuria hafla hiyo, amekipongeza Chuo cha Kodi pamoja na ZFB kwa makubaliano hayo muhimu na kusema kwamba anafarijika kuona jitihada zake zimefanikiwa kwani yeye alichangia kufanikisha suala hilo.

Katika makubaliano hayo, Chuo cha Kodi kitasimamia kiwango cha taaluma itakayotolewa kwa kuzingatia vigezo vya Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU). Aidha, Chuo hicho pia kitasimamia udahili, mitihani, kutoa walimu na vyeti baada ya kuhitimu wakati Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar kitapokea ada, kutoa wanafunzi, madarasa pamoja na vitendea kazi.

Chuo cha Kodi ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ambacho kilipata ithbati kutoka Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa watumishi wa TRA pamoja na wadau mbalimbali katika fani za Kodi na Forodha.

WACHEZAJI 12 GOLF LUGALO WAAANZA VYEMA MWAKA 2018

$
0
0
Wapiga golf 12 akiwemo aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi jenerali Mstaafu George Waitara wameanza vyema mwaka kwa kuibuka washindi katika michuano ya Golf inayofanyika kila baadaya Miezi Mitatu ambapo kwa mwaka 2018 ndio ya kwanza.

Katika mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko na kushirikisha wacheza golf 73 kutoka katika makundi matano ambayo ni Watoto(Juniors), Seniors, Wanawake Divisheni A, B na C huku idadi kubwa ya wanawake wakiendelea kujitokeza.

Katika kundi la Divisheni A Mshindi aliiibuka Seif Mcharo ambaye ni miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Golf baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 71 akifuatiwa na Kapteni Kibuna Shaabani aliyepata Mikwaju ya Jumla 74 huku Divisheni B Mshindi akiibuka Likuli Juma Baada ya Kupata mikwaju ya Jumla 70 akifuatiwa na Michael Lotich aliyepiga 74.

Kwa Upande wa Kundi C Sajini Taji John Msey aliibuka mshindi baada ya kupata Mikwaju ya Jumla 76 akifiuatiwa na Balozi Sai Kapale aliyepiga mikwaju ya Jumla 81 wakati katika kundi la wanawake Habiba Juma aliibuka Mshindi na kueneleza historia ya yake ya kufanya vyema baada ya kupiga mikwaju ya jumla 76 na kumshinda Mwenzie Lilian Mwaulambo kwa Count Back baada ya kufungana kwa Mikwaju 76.

Katika kundi la Senior Jenerali Mstaafu George Waitara alibuka mshindi Baada ya kupata net ya 72 akifuatiwa na Brigedia Jenerali Mstaafu Julius Mbilinyi aliyepata Net ya 76 huku katika kundi la Watoto Zabron Hamis aliibuka mshindi kwa mikwaju ya jumla 70 na kufuatiwa na Karimu Ismail aliyepiga 74.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema ni mashindano ya kwanza kwa mwaka 2018 lakini yameweza kuitoa Dira ya mwelekeo wa Wachezaji.

Pia aliahidi kuendelea kuwekeza katika kuibua Wachezaji wapya na kuendeleza waliopo ikiwemo kuhakikisha wanashiriki Michuano mbalimbali ya Kimataifa na Kitaifa na kiletea heshma nchi na klabu ya jeshi ya Lugalo.

Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuwa wanachama wenye nidhamu kama ilivyo ada ili kufanikiwa kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.

KAMISHNA JENERALI MAGEREZA, DKT. JUMA MALEWA ATETA NA MAHABUSU GEREZA KEKO MAADHIMISHO WIKI YA SHERIA NCHINI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika sekta ya Sheria hapa nchini.Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko(hawapo pichani).Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu ambaye ni raia wa kigeni mara baada ya kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akikagua jiko la gesi katika Gereza la Mahabusu Keko. Jeshi la Magereza tayari limeanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuachana na matumizi ya kuni kwa kutumia nishati ya gesi katika baadhi ya magereza nchini hivyo kutunza mazingira.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza Keko ambapo chumba hicho kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli mbalimbali kwa kutumia njia ya TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia gharama Jeshi la Magereza katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na kuwarejesha magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika Chumba Maalum ambacho kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa kutumia njia ya TEHAMA(wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Noel James(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

WAKULIMA SKIMU YA UMWAGILIAJI MPUNGA NYAMAGOGO MANYONI WALALAMIKIA HALMASHAURI KUTELEKEZA KATAPILA

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly,Manyoni Jan,28,2018 Skimu

WAKULIMA wa skimu ya umwagiliaji mpunga ya Nyamagogo,iliyopo katika Kijiji cha Chikuyu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuitengeneza katapila lililokuwa likisaidia kusafisha mifereji ya kuoitisha maji kwenye mashamba hayo ili waweze kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambao kwa sasa umepungua.

Mwenyekiti wa skimu hiyo ya umwagiliaji Nyamagogo,Abdallah Rajabu Maganga alisema katapila hilo ambalo limetelekezwa tangu mwaka 2012 kutokana na kukosekana kwa vipuli vinavyohitajika kulifufua kwa sababu kifaa hicho ni aina ya kizamani na hivyo matengenezo yake siyo rahisi na badala yake lingefaa kuuzwa kwa njia yam nada.

“Tatizo wanavyosema sema ni greda la kizamani unaona bwana spea zake hazipatikani sasa tunajiuliza wanaproses kwamba wanataka kuliuza unaona bwana sasa huyo unayemuuzia atalifanyia nini kama kweli ni greda la zamani ambapo hakauna spea”alifafanua Maganga.

Alifafanua mwenyekiti huyo wa (WAUWA) kwamba ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo na kwa sababu sasa hivi dunia ni ya utandawazi spea zinapatikana sehemu yeyote pale hata kama Marekani wanaweza kwenda au kuagiza ili liweze kutengenezwa kwa manufaa ya wakulima hao wa skimu ya umwagiliaji.

Mwenyekiti huyo hata hivyo aliyataja baadhi ya athari wanazopata wakulima hao kuwa ni pamoja na kujaa kwa maji ambayo hupeleka na mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,lakini endapo wangelipata greda hilo lingeweza kuwasaidia kutoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikipotea.

Naye diwani wa kata ya Chikuyu,Benjameni Kamoga alisema kuwa kwa taarifa za awali kutoka Halmashauri zilisema kinachosumbua katapila hilo ni kukosekana kwa cheni ambayo inahitaji nguvu katika matengenezo ili wakulima waweze kunufaika na kuwepo kwa miundombinu hiyo ya kilimo.

“Kwa mfano kuna mikato ambayo imesababishwa na maji kujaa pamoja na ujenzi wa nguzo za umeme,Tanesco walikuja wakatuzibiazibia lakini hawakujua ukubwa, kwa maana hiyo kama lingekuwa zima hili lingetufanyiakazi nzuri”.alibainisha diwani Kamoga.

baadhi ya Skimu za umwagiliaji mashamba ya mpunga Nyamagogo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida yaliyoathirika kutokana na kujaa kwa maji ambayo hupeleka na mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,kwa sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikishuka. 
baadhi ya mitaro iliyojaa mchanga pamoja na takataka na hivyo kusababisha maji kukosa mwelekeo na hivyo kusambaa ovyo kwenye maeneo mengine.
Katapila lililokuwa likiwasaidia wakulima wa skimu ya umwagiliaji mpanga Nyamagogo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida kutojaa kwa maji ambayo hupeleka mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,kwa sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku kipato chao kikishuka.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

NG'OMBE 341,098 WAPIGWA CHAPA SIMANJIRO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (wapili kulia) baada ya kupewa zawadi ya nguo ya jadi na wafugaji wa kata ya Naisinyai kwenye ziara yake Wilayani Simanjiro, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Jackson Leskar Sipitieck na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Arnold Msuya. 


Ng'ombe 341,098 wamepigwa chapa Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ili kutekeleza agizo la Serikali la upigaji chapa mifugo kwa ajili ya utambuzi na kuepuka migogoro ya mara kwa mara. 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary, aliyasema hayo juzi wakati akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti. Omary alisema lengo la wilaya hiyo ni kupiga chapa ng'ombe 437,925 hivyo wamefikia asilimia 79 hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana. 

Alisema zoezi hilo lilitarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka jana ila baada ya serikali kuongeza muda hadi Januari 31 mwaka huu, watakuwa wamefanikiwa kukamilisha. Alisema wilaya hiyo ina mabwawa mawili ya Nyumba ya Mungu na Kidapash, ambayo shughuli za uvuvi zinafanyika na jitihada za kudhibiti uvuvi haramu zimefanyika. 

Kwenye sekta ya kilimo, umwagiliaji na ushirika alisema kuna ekari 346,000 zinazofaa kwa kilimo ambapo takribani ekari 144,00 hutumika kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara. "Mahitaji ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wote ni tani 42,000 za nafaka na hali ya chakula ni ya kuridhisha kwenye maeneo mengi kwani wananchi wanatumia chakula kilichovunwa msimu wa Kilimo wa 2016/2017. 

Alisema kwa upande wa mradi wa maji kutoka mto Ruvu hadi mji mdogo wa Orkesumet, serikali itautekeleza kupitia sh40 bilioni, za fedha za ndani na ufadhili wa benki ya maendeleo ya watu wa uarabuni. Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti aliagiza kila wilaya ya mkoa huo kuhakikisha inakuwa na viwanda 15 ili kutekeleza agizo la serikali la kila mkoa uwe na viwanda 100.

Mnyeti alisema wilaya ya Simanjiro iwe na viwanda 15 na nyingine zitekeleze hilo ili kuhakikisha uzalishaji wa ajira unafanyika na kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati.

Mkazi maili 35 amuomba waziri wa afya msaada aokoe maisha ya mwanae

$
0
0
Bi Flora Liberia (33) akiwa yupo na mwanae Samweli Amos miaka (2)akiwa nyumbani kwake Maili 35 kata ya Visiga Halmashauri ya mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.Picha na Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus Pwani.

MKAAZI wa eneo la Maili 35 Kata ya Visiga katika Halmashauri ya Kibaha Mjini Bi Flora Liberia (30) ameelezea masikitiko yake kutokana na kutaabika na ulezi wa mtoto wake Amos Samwel mwenye umri wa miaka miwili na nusu ambaye tangu alipozaliwa viungo vyake havijakaza, hali iliyosababisha kukumbana na muuguzi aliyedai kuwa ni mfanyakazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye amekuwa akimlaghai na kutumia fedha zake kwa madai kuwa atamsaidia kumpatia matibabu mtoto huyo.

Ameongeza kwa kusema yeye hana ajira hivyo hulima vibarua vinavyomuwezesha kupata ujira mdogo ambao hujichangisha ili aweze kumpatia matibabu mtoto wake, ambaye tangu alipomzaa viungo vyake havijawahi kuwa imara kama ilivyo kwa watoto wengine anazungumza hayo  kwa masikitiko .

Bi Flora ameomba msaada kutoka kwa Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Ummy Mwalimu ili kuweza kuokoa maisha ya mtoto wake.
Mtoto Samweli Amos miaka( 2) alizaliwa 2015 1/3 Zahanati ya mlandizi iliyopo Kibaha mkoa wa Pwani,akiwa ameketishwa katika kiti walichotengeneza wazazi kwa ajili ya kumketisha mtoto huyo kama inavyoonekana hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wa kwanza kushoto ni baba mzazi wa mtoto samweli ,Amos Hussein (39 mwenyeji wa Morogoro katikati ni Samwel Amos (2) wa kwanza kulia ni mama yake Flora Liberia (33 ) mwenyeji wa Kigoma,ila kwa sasa wanaishi mtaa mail 35 kata ya Visiga Halmashauri ya mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.Picha na Vero Ignatus Blog.

Rais Shein Ahudhuria Chakula cha Mchana na Vijana wa Halaiki

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakijumuika na Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kilichofanyika katika viwanja vya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar
BAADHI ya Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar
BAADHI ya Viongozi wa Halaiki wakiwa katika viwanja vya Vikosi SMZ wakishiriki katika hafla ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishiriki katika hafla ya chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi na Afisi ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa neno la shukrani wakatika kumalizika kwa Hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzinar kwa ajili yao kilichofanyika katika Kambi ya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine wa Serikali wakiitikia dua baada ya kumalizika hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika katika Viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakizungumza baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha mchana a Vijana hao, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamen Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana walioshiriki Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan 12-1-2018.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamen Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana walioshiriki Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan 12-1-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika hafla hiyo ya kachula maalum kilichoandaliwa kwa ajali yao katika Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.








RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kumaliza hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana hao katika Viwanja vya KVZ Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu wa Halaiki Zanzibar Ali Mohammed Bakari, alipowasili katika viwanja vya Kikosi cha KVZ Mtoni kuhudhuria hafla hiyo.

VIJANA wa Bendi ya Chipukizi wakitoa burudani wakati wahafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar
BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishiriki katika hafla ya chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.

Picha na Ikulu

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA WATANZANIA UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchi Ubelgiji Mh:Edward Joseph Sokoine katikati akiwa na baadhi ya watanzania waliofika jana kwenye kikao cha kusikiliza na kutafutia ufumbuzi kero za watanzania wanaishi mbali na Tanzania. {Picha zote na Maganga One Blog}
Kiongozi wa Watanzani kitongoji cha Antwerpen nchini Ubelgiji ndugu Joseph Makani akimkaribisha Mh;Balozi na maafisa Ubalozi alioambana nao hapa jana,kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi ndugu Shoo na upande wa kulia ni afisa ubalozi ndugu Juma Salum.Kikao kilikwenda vizuri kwani kila mmoja alipewa fursa ya kuuliza maswali. {picha zote na Maganga One Blog}
Afisa Ubalozi ndugu Juma Salum{kulia}akitoa ufafanuzi wa swali aliloulizwa kuhusu maswala ya hati za kusafiria pindi mtu anapotaka kurudi nyumbani,alielezea kwa kirefu taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili mtu kuepuka usumbufu.
Mh:Balozi akimsikiliza mmoja wa watanzania ndugu Omari Songambele {hayupo pichani}aliyetaka ufafanuzi kuhusu Uraia Pacha.
Baadhi ya kina mama wa Kitanzania na nchi jirani walihudhuria mkutano uliowakutanisha na Balozi Sokoine
Na kwa upande wa kina baba nao walijumuika kwa wingi hapo jana kusikiliza na kutoa maoni kuhusu nchi yao
Mwenyekiti wa Watanzania nchini Ubelgiji ndugu Mwasha akijitambulisha kwa Mh:Balozi kabla ya kikao hakijaanza rasmi.
Afisa ubalozi wa Tanzania ndugu Juma Salum,jana alipata nafasi nzuri ya kuyajibu vizuri maswali ya watanzania. Pichani akiendelea kufafanua jinsi ofisi ya balozi inavyofanya kazi zake vyema na kuwasaidia watanzania kwa hali na mali pindi wanapohitaji msaada kwenye ofisi za ubalozi.
Mmoja wa Watanzania ambaye anaishi nje ya nchi na amefaikiwa kuzaa na mzungu,Pichani wakimsikiliza Mh:Balozi
Pichani baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Mh:Balozi
Pichani baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Mh:Balozi
Mh:Balozi Sokoine akiwasisitiza Watanzania kuwekeza na kupeleka wawekezaji nyumbani
Afisa balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ndugu Shoo akiwaeleza watanzania Fursa za Hisa zitokanazo na mabenki makubwa nchini Tanzania na jinsi ya kujiunga nazo
Afisa Ubalozi wa Tanzania nduguKabakati nae aliongea na watanzania kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali,pichani alitoa ufafanuzi wa maswala ya umiliki wa ardhi na mashamba
Afisa ubalozi na Kanali mstaafu akiwashauri Watanzania kutokusahau walikotoka na kuwasisitiza kuwekeza nyumbani,kutovunja sheria za nchi wanazoishi
Afisa ubalozi na Kanali mstaafu akiwashauri Watanzania kutokusahau walikotoka na kuwasisitiza kuwekeza nyumbani,kutovunja sheria za nchi wanazoishi
Watanzania,Wasomali,Warundi , Wacongo na nchi nyingine za jirani kuizunguka Tanzania walihudhuria mkutano wa Balozi wa Tanzania Mh:Balozi Sokoine hapo jana. 
Maganga One Blogger akiwa na maafisa ubalozi wa Tanzania wakibadilishana mawazo
Maganga One Blogger alipata fursa ya kuongea na Mh:Balozi na kumueleza changamoto za Watanzania ughaibuni,Mh:Balozi Sokoine aliahidi kuwasaidia Watanzania kadri atakavyoweza na kutatua kero zao.
Mh:Balozi Sokoine akiagana na Omary Songambele mara baada ya kikao kumalizika hapa jana.pembeni mwa balozi ni Dulla Criss Cross mmoja wa viongozi wa Antwerpen
Shabiki namba moja wa Simba ughaibuni ndugu Nyambi kushoto akiwa na dada wa Kitanzania wakipata picha ya kumbukumbu
Kutoka kushoto ni Afisa Balozi na kanali mstaafu,ndugu Omary Songambele,Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Kassim Manara,Afisa ubalozi ndugu Kabakati na Mh:Balozi Edward Sokoine hapo jana jijini Antwerpen katika kikao cha kuzungumzia maendeleo ya nchi ya Tanzania. {Picha zote na Maganga One Blog}

VIGEZO VILIVYOIFANYA TANZANIA KUWA KINARA UKUAJI WA UCHUMI JUMUISHI

$
0
0

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bibi. Bengi’i Issa akizungumza kuhusu katika mahojiano maalumu kuhusu kungara kwa Tanzania katika ukuaji wa uchumi jumuishi miongni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara leo jijini Dar es Salaam. (Picha na: MAELEZO)

JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA IMANI YA MAHAKAMA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akijiandaa kuanza Matembezi ya uzinduzi wa wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni mkewe akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglican Nchini.
Gari linaloonesha Mfano wa Mahakama inayotembea. Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania itaanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.
Jaji Mkuu akiwa ndani ya gari hilo 

………………….

Na Lydia Churi-Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Watumishi wa Mahakama nchini kutoa huduma kwa kuzingatia Maadili, kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati pamoja na kuacha vitendo vya rushwa ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Akizindua wiki ya Sheria na Maonesho ya Elimu ya Sheria leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu alisema kuwa nguvu ya Mahakama ni imani ya wananchi na imani hiyo itaongezeka ikiwa hakuna rushwa, kuna maadili mema na kesi zitamalizika kwa wakati.

Jaji Mkuu pia amewataka wananchi kuacha kuilalamikia Mahakama na badala yake wachukue hatua kwa kuwataja watumishi wasiozingatia maadili kwa uongozi wa Mahakama.Aidha, amewashauri wananchi kujifunza na kuelewa taratibu za mashauri Mahakamani ili kurahisisha upatikanaji wa haki zao wanapozitafuta kwenye Mahakama mbalimbali nchini.

“Wananchi wengi wanakwenda kutafuta haki sehemu isiyohusika hivyo wanatakiwa kujifunza taratibu za Mahakama ili waweze kupata haki kwa wakati kwa kuwamuda mwingi unapotea kwa kutafuta haki mahali pasipostahili”, alisema Prof. Juma.Alisema hivi sasa Mahakama inaingia kwenye matumizi ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano- TEHAMA hivyo matumizi haya yatamsaidia mwananchi kuweza kufahamu hatua zote za shauri lake lililopo Mahakamani.

Jaji Mkuu ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupata elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Mahakama na sekta ya sheria kwa ujumla.

Alisema, katika maonesho hayo, wananchi watapata nafasi ya kujifunza juu ya usuluhishi nje ya Mahakama, Mahakama inayotembea (Mobile Courts) pamoja na changamoto za upatikanaji wa haki zikiwemo upungufu wa Watumishi, Miundombinu, pamoja na vifaa.Akizungumzia taratibu wa usuluhishi wa kesi nje ya Mahakama (Mediation), Jaji Mkuu amesema wakati sasa umefika kwa wananchi kutumia utaratibu huo unaorahisisha upatikanaji wa haki na kuongeza kuwa Haki bora hupatikana kwa usuluhishi majumbani.

Aidha, kabla ya kuzindua wiki ya Sheria, Jaji Mkuu aliongoza Matembezi waliyowashirikisha watumishi wa Mahakama, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla yaliyoanzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mpaka viwanja vya Mnazi Mmoja.

Matembezi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa wakati katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju.

5 YEARS DEATH ANNIVERSARY In loving memory of our loved one

$
0
0




Moses Tito Kachima

BORN:27th January 1945                  DIED: 29th January 2013

Gone but not forgotten. Your presence lingers in our life. God blessed us with your presence and now you’re not here with us but we have an angel to watch over us and heaven has also gained an angel. Years have passed but you’ll always be missed.
May your soul rest in eternal peace, Amen.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA AU NCHINI ETHIOPIA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amehudhuria katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli. Januari 29, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa (katikati) nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa (katikati) nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahi jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mjumbe Maalum na Mwenyekiti wa Umoja wa Africa Nchini Sudan, Prof. Joram Biswaro, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018.

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akishiriki shughuli ya kuteketeza zana haramu za uvuvvi zilizokamatwa hivi karibuni katika wilaya za Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya za Busega,Tano Seif Mwera akishiriki shughuli  la kutekeza  zana haramu za  uvuvvi zilizomakatwa hivi karibuni katika wilaya za Busega mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdullah Ulega akizungumzana na wavuvi juu ya kiongozi au mtu mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu zana zake zitateketezwa na yeye atachukuliwa hatua za kisheria.Picha na Emmanuel Massaka.
 

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli imeapa kutowafumbia macho viongozi au watu wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wa kutumia zana haramu zilizopigwa marufuku.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipokuwa akiteketeza zana za uvuvvi haramu zilizomakatwa hivi karibuni katika Wilaya za Busega mkoani Simiyu na Magu mkoani Mwanza.

Amesema kuwa hakuna atakayesalimika katika sakata hilo endapo tu akibainika kutumia zana haramu za uvuvi.Ameongeza kuwa Serikali ina dhamira kubwa na wavuvi katka ufanyaji wa shughuli zao na ndio maana imeamua kupiga marufuku zana zote haramu kwa lengo la kusaidia kizazi kijacho ili nacho kije kinufaike na raslimali za Taifa hili.

,"Hivyo idara ya uvuvi kamwe hautomfumbia macho kiongozi yeyote yule ambaye anajishughulisha na biashara hiyo kwa kigezo cha kuwa yeye ni kiongozi.“Kwa yule atakayebainika kuwa ni kiongozi au mtu mwenye fedha zake anajihusisha na uvuvi haramu ambao Serikali inatumia fedha nyingi kukabiliana nao basi cha mtema kunde atakiona juu yake kwani zana zake zitachomwa,faini na yeye kuchukuliwa hatua za kisheria,” amesema. 

Aidha Ulega amewataka wavuvi kuendelea kusalimisha zana haramu kabla ya kukumbwa na dhahma kubwa itakayowapeleka mahali pabaya zaidi ya hali ya sasa jinsi ilivyo.Pia amewahakikishia upatikanaji wa zana zinazohitajika mapema kwani tayari wamesha anza kupokea maombi mengi ya mashirika yanayohitaji kusambaza zana halali katika nchi yetu kwa madhumuni ya kuokoa rasilimali za majini zilizokuwa zikipatwa na shinda nyingi kutoka kwa wavuvui wasiokuwa waaminifu.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kamati Maalumu ya kuthibiti na kupambana na uvuvi haramu Kanda ya Simiyu na Mwanza, Nchama Marwa amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa hakuna uonevu wa aina yeyote ile unaofanywa na kikosi hicho kuhusu kuwawajibisha wale wanaoendelea na shughuli hiyo kwa kujifisha .Ameongeza kuwa kuna wavuvi ambao wanasalimisha na wengine bado wanaendelea kuvua kwa kujifisha laniki ni lazima tu watawakamata na sheria ya uvuvi itafuata mkondo wake bila kinyongo wala uonevu wa aina yeyote ile.

Aidha kiongozi huyo wa kikosi maalumu aliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa kazi zao kwa Naibu Waziri na kumweleza kuwa kuwa mpaka sasa wamekamata nyavu haramu za makila 33121,nyavu za dagaa175,makokoro ya sangara119.Pia nyavu za timba 3,sangara wabichi kilo 1071,sangara kayabo3463, watu hao waliokamatwa na kikosi kazi wametozwa faini kulingana na kile walichokamatwa nacho na kufikia kiasi cha Sh.milioni 767.

Naye Boniface Mkama Mkazi wa Nyamikoma wilayani Busega ameipongeza Serikali kwa kuwasaidia na vitendo vya kinyama vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wavuvi wenzao.Hivyo ameiomba kuwawaishia tu zana sahihi ili waendelea na shughuli zao za kila siku za uvuvi.

MKAZI WA JIJI LA MWANZA AJISHINDIA MILIONI 40 ZA TATUMZUKA

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akimkabidhi mfano wa hundi  mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili).
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akiwa katika picha ya pamoja na Mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili),sambamba na baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Wilaya na pamoja na ndugu wa mshindi huyo.

MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA VIANZE KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele) 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika Wilaya ya Butiama leo. 
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu Kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akisoma majina ya Wavuvi Haramu 



Na John Mapepele, Mara


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata samaki na mazao yake vilivyofungwa katika Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua kabla ya  kufikia mwezi Machi mwaka wizarani kwake.

Alivitaja viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited vilivyopo Mwanza na Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited katika mkoa wa Mara.Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba ulinzi wa raslimali hizi ni wa kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha hapa nchini” alisisitiza Mpina 

Waziri Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.

Kamanda anayeongoza kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alimweleza Waziri Mpina kuwa operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma, Butiama, Rorya na Bunda na kufanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya sh. bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya sh. milioni 189.

Waziri Mpina aliziagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua Maafisa Uvuvi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vincent Anney amesema kwamba hayuko tayari kuona Wilaya yake inaendelea kuishi na watumishi wanaojihusisha na uvuvi haramu na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika wilaya hiyo.

Aidha Waziri Mpina ameiagiza Wizara yake kuandaa bei elekezi ya kununua samaki itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha hovyo bei pindi samaki wanapoongezeka na hivyo kuwadhulumu wavuvi kupata malipo stahili yanayotokana na kazi yao.Waziri Mpina alisema Ziwa Victoria ni hazina na raslimali kubwa kwa Tanzania ambapo inaaminika kuwa ni la kwanza kwa ukubwa katika bara la Afrika kwa kuwa na eneo la 68,000Km2 na la pili duniani. 

Alisema pamoja na umuhimu wa ziwa hili katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania bado linakabiliwa na shughuli za uvuvi haramu uliokithiri ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kama hakutakuwa na jitihada za haraka za kutokomeza uvuvi haramu, ziwa hilo hali halitakuwa na raslimali za uvuvi ikiwa ni pamoja na samaki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Alitaja uvuvi haramu unaofanywa kuwa ni pamoja na kuvua katika maeneo yasiyoruhusiwa, kutumia valiyombo visivyosajiliwa, kuvua bila leseni,kutumia sumu, kutumia nyavu za utali na kuvua samaki wachanga ama wazazi wasioruhusiwa.

Uvuvi haramu mwingini nikuvua kwa kokoro na nyavu zenye macho madogo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria, katuli, kumbakumba na gizagiza ambapo alisema Serikali imedhamilia kutokomeza uvuvi huo haramu.

Aidha alisema operesheni hiyo katika kanda ya Ziwa Victoria dhidi ya uvuvi haramu ni ya kudumu na inafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na.22 yaMwaka 2003 na Kanuni 58(1) ya Uvuvi ya Mwaka 2009 na Sheria ya Mazingira Na 20 ya Mwaka 2004 kifungu Na(1), 65(1)a pia Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na 29 ya Mwaka 1994 ili kudhibiti uvuvi haramu ulioshamiri kiasi cha kutoweka kwa raslimali ya samaki katika ziwa hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Waziri Mpina alisema Tanzania inamiliki 51% ya Ziwa hili ikifuatiwa na Uganda 43% na nchi ya Kenya inamiliki 6%. Ziwa hili ni moja ya maziwa yanayozalisha samaki kwa wingi duniani kwa makadirio ya takribani tani 1,000,000 kwa mwaka ambapo asilimia 60 ya uzalishaji wa samaki wake unatoka Tanzania hivyo juhudi za pamoja za kutokomeza uvuvi haramu zinahitajika.

SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZAATHIRI UZALISHAJI UMEME NYUMBA YA MUNGU

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu kilichopo Mkoani Kilimanjaro. Anayeshuhudia ni Mtumishi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Kaimu Meneja wa Kituo cha Nyumba ya Mungu TANESCO, Clarance Mahunda akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kituo hicho kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia). Wengine katika picha ni Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati Makao Makuu na wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Nyumba ya Mungu TANESCO, Clarance Mahunda akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati). Wengine katika picha ni Watumishi wa Wizara ya Nishati na kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Nyumba ya Mungu TANESCO, Clarance Mahunda (katikati) akitoa maelezo kuhusu Bwawa la maji linalotumika kuhifadhia maji katika Kituo cha Nyumba ya Mungu. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, Ngerenja Mgejwa.




Na Rhoda James, Kilimanjaro

Imeelezwa kuwa, shughuli za Kibinadamu zinazofanywa kuzunguka Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Nyumba ya Mungu zimeendelea kuathiri uzalishaji wa nishati hiyo kutokana na kukosekana maji ya kutosha.

Hayo yalielezwa na Kaimu Meneja wa Kituo Clarance Mahunda wakati Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipofanya ziara Kituoni hapo mwishoni mwa wiki na kueleza kuwa, hivi sasa kituo hicho kinazalisha megawati 3.5 hadi 4 tofauti na uwezo wake wa kuzalisha megawati 8 kwa saa 24.“Shughuli za binadamu zikiwemo kulima, kuchunga ngo’mbe na uvuvi kumepelekea uzalishaji wa umeme katika kituo hiki kuwa hafifu, kitu ambacho kinasababisha ukosefu wa maji ya kutosha hivyo kuzalisha umeme pungufu,” alisema Mahunda.

Pia, Mahunda alimweleza Naibu Waziri wa Nishati kuwa, japokuwa zipo juhudi mbalimbali zambazo zimefanyika kuzuia athari hizo ikiwemo kushirikisha wadau mbalimbali kama Pangani Water Basin pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali, lakini baado kituo hicho kinazalisha megawati 3.5 hadi 4. 

Aidha, Mahunda alieleza kuhusu utendaji wa Kituo hicho na kusema kuwa ni mzuri kutokana na kufanyika ukarabati mkubwa uliofanyika mwezi Oktoba na Novemba,2017 na hivyo kupelekea mashine zote kufanya kazi ipasavyo.Pia aliongeza kuwa, kwa sasa kituo hicho kinasafirisha umeme kwa njia mbili za Msongo wa Kilovoti 66 kuelekea Kiungi na njia nyingine ni Umeme kusafirishwa kwa Msongo wa Kilovoti 33 kupitia Mwanga na Mkuyuni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati alizitaka Mamlaka kuanzia Serikali za Mtaa hadi Mkoa na wananchi wanaozunguka maeneo ya kituo hicho kuhakikisha wanatunza mazingira yanayozunguka kituo hicho kwa kulinda vyazo vya maji ili kupata maji ya kutosha wakizingatia umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya watu na Taifa.

“Nimeelezwa kuwa kina cha maji hakiruhusu mashine zote kuzalisha umeme, na hii ni kwa sababu ya shughuli za binadamu ambazo zinaendelea pembezoni mwa Bwawa la maji yanayotumika kuzalisha umeme huo,”aliongeza Mgalu.Mgalu aliongeza tatizo la shughuli za kibinadamu limeviathiri pia vituo vingine za kuzalishia umeme vya Hale na Pangani na hivyo kupelekea upungufu katika kuzalisha umeme kutokana na kina cha maji kupungua.

Aidha, Mgalu aliitaka TANESCO pamoja na Serikali za Mitaa kuendelea kuwaelimisha wananchi wanaozunguka maeneo hayo ili kuwezesha kituo husika kuzalisha umeme kwa viwango vinavyo takiwa.

MADARASA YA NYASI, TEMBE, UDONGO YASITUMIKE KATIKA SHULE ZOTE NCHINI, WAZIRI JAFO

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akifungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakugenzi wa Halmashauri yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi yanayofanyika kwa siku Tano Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kufungua mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja akiwasilisha taarifa ya Utangulizi wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti akitoa neno la Shukrani wakati  baada ya Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Jafo kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa Mbele) katika Picha ya Pamoja na viongozi wengine walioshiriki kwenye Ufunguzi wa mafunzo hayo na Wah.Wakuu wa Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Londido Mhe. Daniel Chongolo (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe wakati wa mafunzo ya Uongozi.


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.

“Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari kusoma”Alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi  kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini.

Niwapongeze baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.

Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya kuheshimu  mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini, kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.

Awali akizungumza katika Ufunguzi wa  Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa mafunzo haya yanakamilisha mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia   Viongozi 324.

Prof.Semboja aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati  kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade ya Jamii Tunayoihudumia.

Sambamba na hilo Mkutano huu pia unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi wetu katika kuongoza watu na rasillimali zingine zilizoko kwenye maeneo yetu ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya pamoja.

Alisisitiza kuwa Mafunzo haya yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa Binafsi za Viongozi  kwa sababu Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi katika kiLA Eneo hivyo ni lazima kila kiongozi aweze kujitenegenezea Sifa binafsi ili akubalike na kuhesimika katika Jamii husika.

“Sifa hizi binafsi tunazozizungumzia ni Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu, Mtenda Haki, Muumini wa Utawala bora na Utawala wa Sheria na zaidi kuwa mchahapa kazi na awe na weledi wa hali ya juu sasa haya yote yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya namna gani Kiongozi anaweza Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii tunazoziongoza.

Akitoa Neno la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI na Taasisi ya Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi ameahidi Umakini wa washiriki kwa siku zote za mafunzo.

Mafunzo haya ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa imegususa Viongozi kutoka katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images