Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO.

$
0
0
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo. 
aimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.
engo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA
Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara na CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya leo mkoani Humo.
NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.

“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja” alisema Bw. Simba.

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.

Kwa upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joachim Catherine amesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi Wa mabweni matatu yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo cha maafisa tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara.

Aidha Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati na upanuzi Wa madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw. Frolian Mbungu amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya apokee majengo kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha.

Aidha wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.

DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.

Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

SERIKALI YAIPATIA TAASISI YA MOI BILIONI 16 ILI KUIMARAISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA JAMII

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti cha mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu katika Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza) akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface.
.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.



Na WAMJWW. DSM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi,

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.

“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za Afya kwa wananchi hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu ya mifupa.

“Niupongeze uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika magonjwa yanayohusiana na mifupa jambo lililosaidia kupunguza wagonjwa wengi sana kupata huduma nje ya nchi” alisema Dkt. Ndugulile.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani Zaidi ya Asilimia 95 ya maradhi ya mifupa hutibiwa katika Hospitali hiyo na asilimia zilizobaki huwapeleka nje ya nchi.

Dkt. Respicious Boniface aliendelea kuishukuru Serikali kwa Msaada huo wa Fedha kwaajili ya kununua Vifaa vya MRI na CT-Scan na kuahidi vifaa hivyo vitafika mapema ndani ya mwezi wa Nne, hivyo kazi ya kuwaudumia wananchi itaanza mapema.

“Sababu kubwa ilikuwa ni vifaa, sasa tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imekwisha toa fedha kwaajili ya vifaa hivyo hivyo ndani ya mwezi wa nne vitakuwa vimekwishafika”, alisema Dkt. Dkt. Respicious Boniface

WAVUVI WAASWA KUZINGATIA SHERIA,TARATIBU ZA UVUVI KUZILINDA RASILIMALI ZIWA VICTORIA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayni Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo, Ulega aliwapongeza wavuvi hao kwa hatua hiyo walioichukua huku akikazia msimamo wa serikali wa kupambana na uvuvi halamu. Pamoja na kuwapongeza huko,Ulega aliwasisitiza wavuvi hao kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi ili kuzilinda rasilimali hiyo, ambayo ilikuwa inaelekea kutoweka.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa samaki, wazazi walikuwa wamebaki asilimia nne, wenye hadhi ya kuvuliwa kwa maana ya sentimita 50 hadi 85 wamebaki asilimia tatu na wachanga wamebaki asilimia 93, na kama uvuvi huu ungeendelea maana yake ziwa lingebaki jangwa," alisema Ulega

Waziri Ulega aliwataka wavuvi hao kununua nyavu zinazokubalika kwenye viwanda ambavyo vinauza nyavu hizo,  badala ya kuendelea kutumia nyavu zisizoruhusiwa kwani watapata hasara kwa kuteketezewa na wengine kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu, baadhi ya wavuvi waliamua kuzisalimisha nyavu hizo wenyewe bila shuruti. 


kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu baadhi us wavuvi waliamua kusalimisha nyavu  hizo wenyewe bila shuruti.

Alisema nyavu zinazokubalika kwa mujibu wa sheria, nyavu za dagaa zinatakiwa ziwe na milimita 8, nyavu za sangara inchi 6 hadi tisa na ndoano za sato inatakiwa zenyewe ziwe namba 4, hadi 12, hizi ndio zana sahihi zinazotakiwa kuonekana ziwani," alisema Lwekaza

Naye Benzi Nestory ambaye nimmoja wa wavuvi aliomba kupata muongozo wa sehemu sahihi ya kupata zana hizo haramu kwa haraka badala ya kuambiwa kwa mdomo kuwa nyavu hizo zinapatikana ili kuondokana na hasara wanazopata.

Kwa upande wake Joel Lusigwa alilalamikia upande wa faini Sh700000 kuwa kubwa wanayotozwa pindi wanapokutwa na kosa hivyo kuomba wapunguziwe ikilinganishwa na maeneo mengine ambayo wanatozwa faini kidogo. Hata hivyo waziri Ulega alisema licha ya kuwapo sheria nyingine zinazowakandamiza wavuvi lakini alisema faini hiyo ya Sh700000 ni pamoja faini ya kutokuwa na leseni na usajili ambayo ni Sh .200000 huku faini ya kuharibu mazingira ndani yaziwa ikiwa ni Sh .500000 ambazo hazitabadilishwa lengo ni kumtia uchungu mtuhumiwa.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akiongoza shughuli za kuteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 .Wavuvi wakisogeza  Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  eneo la kuchomea  baada ya kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi  katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

WAKAZI MULEBA WAIOMBA SERIKALI KUONGEZEA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Na Emanuel Massaka-Globu ya jamii

WAKAZI wa Kisiwa cha Kerebe wilayani Muleba mkoani Kagera wameomba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais,Dk. John Maguli kuwapelekea rasilimali watu hasa upande wa afya  na elimu.

Wamesema kwa sasa wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali za kijamii kutokana na uhaba uliopo wa watumishi wa umma. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi blog juzi na jana, wakazi hao wamesema  huduma za kijamii ni changamoto kwao.

" Zimekuwa zinawaumiza hivyo wamezitaka Wizara husika kusikia kilio chao na tunaomba tujengewa hospitali na shule ili watoto na wakina mama wajazito wapate hudumu muhimu,"wamesema wakazi hao.

Pia wameomba Serikali kuwatengenezea huduma bora katika usafiri wa majini kwa kuwapatia boti kwani wamekuwa wakitumia boti za mtu binafsi ambazo si salama kwao.Hivyo wanaomba upatikane usafiri ulio bora na wa uhakika katika kulinda maisha yao.

Hata hivyo Wakazi hao Kisiwa hicho asilimia 93 wanatengemea uvuvi wa Samaki na asilimia 7 wanajishughulisha na kilimo na ufungaji, hivyo basi wameitaka Serikali kuboresha katika sekta ya uvuvi pamoja na ufungaji ili waweze kuendana na mabadiliko ya nchi kwa kupata kipato kikubwa zaidi.

Kisiwa cha Kerebe kwa sensa ya 2012 kina jumla ya wakazi  3100 lakini  idadi hiyo hupungua na kuongezeka kulingana na kilimo na upatikanaji wa samaki kwa wingi ziwani humo.

Hivyo basi kutokana na Serikali ya awamu ya tano inayosema 'Hapa kazi to' itasikiliza kilio chao na kuwapelekea huduma muhimu kwani kila Wizara itakuwa ipo tayari kushirikiana na wanakijiji hao kwa kupitia Wilaya ya Muleba

Na kuongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa wataimarisha ushirikiano wao kwa Serikali

WADAU WA MITINDO, UREMBO MSIWABAGUE WENYE ULEMAVU WA NGOZI-BRIGITA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .

MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2012 Brigita Alfred ameweataka wadau wa masuala ya urembo na mitindo kuacha kubagua watu kutokana na mapungufu yao ya kimaumbile katika tasnia hiyo.

Brigita amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wadau wa mitindo na urembo waliofika katika onesho lake Maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi lililofanyika nyumbani kwa Balozi wa Uturuki lililokwenda kwa jina la 'My Skin My Pride' na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

" Unaweza ukaona ukadhani labda nimefanya haya maonesho kwa ajili ya tasisi yangu lakini ukweli unabaki palepale kuwa katika tasnia ya mitindo sasa tunapaswa kuwapa nafasi watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi kuonesha vipaji vyao na uzuri wa ngozi yao kuliko kuwaacha wenyewe jambo linalo wafanya wajisikie tofauti"amesema Brigita.

Amesema ni jambo zuri sasa kwa waandaaji wa mashindano ya urembo na mitindo kuwajumuisha wadau hao hili nao waonekane katika majukwaa ya kimataifa.

Mkurugenzi wa Tasisi ya Brigita Foundation, Brigita Alfred akizungumza kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofika wakati wa Fashion Show ya watu ya wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uturuki Masaki jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wana Mitindo mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anapita jukwaani akionyesha mavazi yaliyobuniwa na wanamitindo mbalimbali
Warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania nchini Nancy Sumari na Jackline Mengi wakishuhudia onesho hilo la mitindo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Baadhi ya wadau wa mitindo waliofika katika Onesho la Mavazi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini lililofanyika Nyumbani kwa Balozi wa Uturuki nchini.
Mwanamitindo Nemalisa akiwa na Mmoja wa warembo wenye ulamavu wa ngozi akionyesha Vazi la nguo za jioni lililoandaliwa na kampuni ya Jackies Collection.

NAIBU MEYA ILALA AWAKUMBUSHA MADIWANI KUSIMAMIA USAFI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amewataka viongozi na madiwani wa Manispaa hiyo kuwahimiza waanchi wao kufanya usafi katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Kumbilamoto amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Michuzi blog kuhusu nini kifanyike kupunguza magonjwa ya mlipuko katika baadhi ya maeneo katika Manispaa ya Ilala na Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla.

"Viongozi tunatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na kuhimiza watu kufanya usafi kwani Rais wetu, Dk.John Magufuli alianza kwa kutuonesha kwa mfano nasi tunapawa kumuunga mkono kwa hali na mali ili tutokomeza magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi hutokana na uchafu," amesema Kumbilamoto.

Ameongeza tangu mchakato huo wa usafi mazingira uanze kwa takribani zaidi ya mwaka sasa katika kata ya Vingunguti hakujaripotiwa kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu hali ambayo tofauti na awali.Amefafanua kata hiyo ilikuwa sugu kwa ugonjwa huo kiasi cha kuwekwa kambi maalum ya wagonjwa muda wote .

Amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja wetu lakini kama viongozi inatakiwa kuacha siasa za maneno na kufanya mambo hayo kwa vitendo ili tuwe mfano bora kwa wapigakura wetu. 



 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisukuma Toroli lenye taka kwenda kumwaga Dampo wakati wa zoezi la usafi la kila mwisho wa Mwezi lililofanyika katika Kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam kama agizo la Rais  Dkt John Magufuli la kuhakikisha kila mmoja anafanya usafi katika eneo lake kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, akishiriki kusafisha Mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika Barabara ya Vingunguti Kembembuzi .
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Sharif Mbulu, akichimba mchanga na kutoa taka katika mtaro wa kutiririsha maji barabara ya Vingunguti Kembembuzi.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto ,akihamasisha zoezi la usafai kwa wakazi wa Vingunguti.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto  akikabidhi Pikipiki kwa kundi la Wajasiliamali la Watoto Pori ambao aliungana nao pamoja mapema leo katika shughuli ya Usafi.

WAZIRI UMMY AENDELEA NA ZIARA KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Waziri ummy Mwalimu akiangalia ramani ya kituo hicho cha afya ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza.
.Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo.
Waziri Ummy Mwalimu na Naibu Waziri Dkt.Angela Mabula wakikagua ujenzi wa jengo la dharura la uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wialayani Ilemela,akiyevaa koti la bluu ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Florian Tinuga.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni asilimia 80.
Jengo la Maabara lililojengwa kwenye kituo hicho cha afya katika mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za dharura za uzazi kwenye vituo vya afya nchini.(Picha zote na Wizara ya Afya)
Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua huduma za afya kwenye kituo cha afya cha kamanga kilichopo Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya mkoani hapo.

DK SHEIN AREJEA NCHINI AKITOKEA NCHI ZA FALME ZA KIARABU UAE

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE, akivishwa shada la maua na Mtoto aliyeandaliwa.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akivishwa shada la maua na mtoto aliyeandaliwa wakati wa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea katika ziara yake ya wiki moja katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mke Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za UAE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mke Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za UAE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa CCM alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kumaliza ziaya yake katika Nche za Falme za Kiarabu UAE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kuwasili Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kushoto Mama Mwanamwema, Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
WAANDISHI wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar wakiwa na Baadhi ya Mawaziri waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakifuatilia Mkutano huo na waandi katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Vyombo vya Habari mbalimbali vilioko Zanzibar akizungumzia mafanikio ya ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu, baada ya kuwasili Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Vyombo vya Habari mbalimbali vilioko Zanzibar akizungumzia mafanikio ya ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu, baada ya kuwasili Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumaliza mazungumzo na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar mafanikio ya ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu UAE.

RC MAKONDA ATOKWA NA CHOZI, NI BAADA YA KUJIONEA MAISHA YA WASTAAFU WALIODHULUMIWA NYUMBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.
RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote. 

Habari ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea mtu anamdhulumu Mali yake.
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.

Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha. 
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge. 

HAKIMU WA KWELI NI MUNGU

Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali

$
0
0
Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Chumba cha kurushia matangazo wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.


Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Vyombo vya Habari nchini vimeaswa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza Wakati wa ziara yake yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi ya Taifa letu imejengwa katika uchumi jumuishi.
“ Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kueleza faida za miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) kwa wananchi ili nao washiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ambapo ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo” Alisisitza Dkt. AbbasiMkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.- Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) toleo Maalum la Jarida la Nchi Yetu kuhusu mafaniko ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma

Akifafanua amesema kuwa dhamira yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea kutekelezwa kupitia mfumo wa elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha, Ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli na upatikanaji wa huduma muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ili kuhakiksha kuwa kila mwananchi anapata huduma muhimu na za msingi katika ubora unaotakiwa.

Aliongeza kuwa Serikali kwa sasa imeweka msukumo na kipaumbele katika kutoa huduma bora kwa wananchi wote hali inayotoa changamoto kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu katika kusaidia juhudi hizo ili malengo yake yafikiwe kwa wakati.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa na Mkurugenzi wa RASI FM Bw. Ramadhani Mkosola (kushoto) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini DodomaMkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha RASI FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.

Katika kutekeleza majukumu yake Dkt. Abbasi amepongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mageuzi ya kweli.Aidha Dkt. Abbasi aliviasa vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Tanzania mpya kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali katika vyombo vya Habari Mkoani Dodoma ni sehemu ya utaratbu wakutembelea wadau wa sekta ya Habari ili kuimarisha utendaji kazi, ambapo Leo ametembelea vituo vya redio vya ABM fm na RAS fm.

POWER ON FITNESS GYM YAUKARIBISHA MWAKA 2018 KWA MBWEMBWE

$
0
0
Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, kinondoni, Jijini Dar es salaam imeukaribisha mwaka 2018 kwa style ya kipekee ambapo wadau mbalimbali wamejumuika kufanya mazoezi pamoja na kuburudika kwa chakula, Vinywaji na muziki kabambe wa Skylight Band.

Shughuli hiyo imefanyika Jumamosi January 27,2018 katika viwanja vya posta vilivyopo Sayansi, Kijitonyama. Shughuli hiyo ilianza saa 12 asb na inatarajia kumalizika usiku mnene.

Siku hiyo imepambwa na mazoezi ya kukimbia(Jogging) ambayo yameanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, Steps, Zumba, Mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku nk.

Baada ya mazoezi kukamilika wadau wa Power on Fitness Gym wamejumuika katika burudani kabambe ya muziki iliyoporomoshwa na bendi ya Skylight na Ma DJ wakali wa hapa nchini.

Siku hiyo pia kutakuwa na Nyama choma itakayoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina.

Shughuli hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

MASAUNI AKAGUA MAKAZI YA ASKARI MAENEO YA POLISI WALIYOUZIWA WANANCHI KINYUME NA UTARATIBU MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA (kushoto), alipotembelea eneo la Tunguu lililovamiwa na wananchi, ambalo mmiliki halali ni jeshi la Polisi. Wakwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan.Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyeshwa na Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA, ramani ya moja ya maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara ya naibu waziri kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi mkoani hapo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,Hassan Khatib Hassan. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo yalipojengwa maduka ya biashara ambayo wamiliki wamenunua viwanja hivyo vya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAKAZI WA KINONDONI WAJITOKEZA KWA WINGI UZINDUZI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE BIAFRA

$
0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.

Tanzania Kinara Ukuaji wa Uchumi Jumuishi

$
0
0
Usimamizi mzuri na utekelezaji wa Sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi, kumeifanya Tanzania kuibuka kinara miongoni mwa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na Uchumi Jumuishi (Inclusive Economy) unaokua duniani.

Taarifa iliyotolewa na Word Economic Forum kupitia mradi wake wa  ‘The Inclusive Development Index’, imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya 48 kati ya nchi 103 zilizofanyiwa tathmini ya nchi zenye Uchumi Jumuishi duniani,

Katika orodha ya kumi bora, nchi zilizofuatia na nafasi ziliyoshika kidunia ni pamoja na Ghana (52), Cameron (53), Burundi (55), Namibia (56), Rwanda (57), Uganda (59), Mali (60), Senegal (61) na Nigeria (63).

Takwimu za ukuaji huu zinaakisi moja kwa moja kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akielezea kutaka uchumi wa Tanzania umilikiwe na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda ambapo watanzania wengi hivi sasa wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo.

Mtaalamu Mbobevu wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi ameeleza kuwa takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo zinatafsiri kuwa uchumi wa Tanzania unaelekea kumilikiwa na watu wengi zaidi jambo ambalo litasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya walionacho na wasionacho.

Profesa Ngowi ameeleza kuwa uchumi wa aina hiyo unawashirikisha wananchi kumiliki uchumi na kuwafanya watu wengi kufaidi matunda ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Taarifa hizi ni njema kwani kitaalam tunaita broad based economy ambapo watu wengi wanashirikishwa kumiliki uchumi na wengi wanafaidi,” alieleza Profesa Ngowi na kuongeza kuwa kuna nchi zingine zinauchumi mzuri lakini unamilikiwa na watu wachache na kufanya kuwa na pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.

Katika siku za hivi karibuni, Taasisi mbalimbali duniani zimekuwa zikitoa ripoti zikiielezea Tanzania kupaa kiuchumi ambapo ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani hivi karibuni zilitabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumwakilisha Rais Dkt Magufuli kongamano la Viongozi Wakuu Umoja wa Nchi za Afrika

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu cha kumbukumbu, cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi huyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Addis Ababa, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia. Januari 28, 2018.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa kusali pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada ya wote kwa pamoja kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli. Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wanakwaya kutoka Chuo cha Ardhi jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta akihubiri katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli mara baada ya Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Nakala za CD ya kwaya kutoka Chuo cha Ardhi mara baada ya Ibada. Kushoto ni Mke wake Mama Janeth Magufuli akifurahia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda mara baada ya kupewa na moja ya Waumini wa Kanisa hilo mara baada ya Ibada ya jumapili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini wengine mara baada ya ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA GHALA LA KUHIFADHI VIFAA VYA MAAFA DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu alipotembelea Moja ya Ghala la kuhifadhi Vifaa vya Maafa lililopo Dodoma Januari 26, 2018.
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akitoa maelezo kuhusu ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea kuangalia hali ya ghala hilo.Afisa Ugavi Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Bw. James Mashaka akionesha moja ya kifaa cha kuhifadhi maji wakati wa maafa (Collapse can jelly) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea Ghala la kuhifadhi vifaa vya Maafa.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akifuatilia maelezo ya ghala la kuhifadhia vifaa vya maafa kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Bw. Bashiru Taratibu alipotembelea kukagua hali ya ghala hilo.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akifuatilia baadhi ya taarifa zinazohusu ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa lililopo Dodoma.Muonekano wa moja ya Ghala la kuhifadhi Vifaa vinavyotumika wakati wa Maafa lililopo Dodoma.

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA,SERIKALI ZA MITAA YAPONGEZA UJENZI HOSPITALI WILAYA YA KILOLO

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imepongeza ujenzi wa majengo mbalimbali ya kutolea huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

Kamati hiyo imetoa Pongezi hizo wakati walipotembelea Kilolo na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo.Wabunge wamepongeza kazi inayofanywa na wakandarasi kwani ipo katika ubora mzuri na kiwango cha kuridhisha.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Mwanne Mchemba aliyeongoza Waheshimiwa hao amesema “naipongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, uongozi na watumishi kwa ujumla kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi ni wa kiwango cha juu na thamani ya fedha inaonekana”.

Kamati imeagiza Halmashauri kuhakikisha inakamilisha majengo yote kwa wakati ili huduma ianze kutolewa mara moja.Ameongeza kuwa ni vizuri kipindi hiki ambacho ujenzi unaendelea Halmashauri ijipange kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba, vitendanishi na dawa pamoja na kuajiri watumishi.

Naye Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege ameziagiza Halmashauri zote nchini ambazo hazina Hospitali za Wilaya zianze taratibu za ujenzi mara moja ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.

Hadi sasa ujenzi uliofanyika ni wa majengo matano ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje; jengo la maabara; jengo la huduma ya mionzi; jengo la huduma ya afya ya uzazi na mtoto; na jengo la wagonjwa wa ndani. Ujenzi wa majengo haya hadi kukamilika unatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi bilioni 4.4.

Aidha, mradi mzima wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo utagharimu Tsh. Bil 12.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ikiwasili katika Hospital ya Kilolo kukagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ikipokea Taarifa ya Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kilolo ilipofanya ziara ya Ukaguzi wa Katika Mradi huo.
Huu ndio muonekano wa Sehemu ya Jengo la Hospital ya Wilaya ya Kilolo inayoendelea kujengwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kakunda(Pili Kushoto) akijadili jambo na Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikalinza Mitaa wakati wa Ziara katika Mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Kilolo.

WAZIRI MKUCHIKA AVUTIWA NA MIRADI YA TASAF

$
0
0

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akitoka katika jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.
Mwonekano wa jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuboresha huduma za Afya kwa walengwa wake na wananchi wa eneo hilo.
Waziri Mkuchika akipanda mche wa mti katika eneo la Zahanati ya kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida iliyojengwa na TASAF na wananchi .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (aliyesimama mbele ya kamera) akiwahutubia baadhi ya watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Singida wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mwahango katika wilaya ya Singida jengo lililojengwa na TASAF ikiwa ni mkakati wa kuwasogezea huduma ya Afya wananchi na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


Estom Sanga-Singida

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mhe. George Mkuchika amepongeza hatua ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kubuni utaratibu mzuri wa kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Mhe. Mkuchika amesema utaratibu huo siyo tu kwamba unapunguza gharama bali unawafanya wananchi kuithamini miradi hiyo na kuitunza kutokana na kutumia nguvu na jasho lao katika kuitekeleza.

Waziri huyo ameyasema hayo mwishoni mwa juma baada ya kutembelea kijiji cha Mwahango katika halmashauri ya wilaya ya Singida ambako alikagua jengo la zahanati lililojengwa na TASAF kwa kuwashirikisha wananchi kijijini hapo.

Aidha Mhe. Mkuchika ameupongeza mkoa wa Singida kwa kusimamia zoezi la uandikishaji Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa uaminifu na hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya Watu wasiostahili kujumuishwa kwenye Mpango huo kinyume cha utaratibu.

Akiwa kijijini hapo Waziri Mkuchika alipata ushuhuda wa mafanikio waliyoyapata baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ambao wameweza kuboresha maisha yao katika nyanja za makazi, lishe,uanzishaji wa miradi ya kiuchumi ,kusomesha watoto na kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii na hivyo kupata huduma ya matibabu katika kipindi chote cha mwaka.

Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF mkoani Singida imeonyesha kuwa, mafanikio makubwa yamepatikana tangu kuanza utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini mkoani humo hususani katika kuamsha ari ya wananchi kuuchukia umaskini kwa vitendo.

Hata hivyo taarifa hiyo imeiomba serikali kupitia TASAF kukamilisha zoezi la kuvijumuisha vijiji vingine ambavyo wananchi wao hawakupata fursa ya kunufaika na huduma za Mpango katika awamu ya kwanza ya utambuzi iliyofanyika mkoani humo mwaka 2014.

Waziri Mkuchika amesema serikali inalifanyia kazi suala hilo kwa juhudi zaidi kwani utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini umefanyika kwa asilimia 70 tu kutokana na ufinyu wa fedha ,hata hivyo kutokana na Mpango huo kuwagusa wananchi wanaokabiliwa na umaskini moja kwa moja, utaratibu mzuri unaaandaliwa ili wananchi wote wanaostahili kujumuishwa kwenye Mpango waweze kutambuliwa hususani katika vijiji ambavyo havinufaiki na Mpango huo kwa sasa.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images