Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR NA BOHARI YA DAWA (MSD) WASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ally Abdullah wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano mjini Zanzibar leo. Wengine wanaoshuhudia ni wanasheria wa taasisi hizo mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu, akielezea namna MSD ilivyojipanga kwenye majukumu yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu, akimkabidhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Asha Ally Abdullah , mpango mkakati wa MSD, 2017-2020, ripoti ya maboresho ya MSD na kitini cha bei za bidhaa za MSD (MSD price catalogue)
Kabla ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia) na timu yake walitembelea ghala la kuhifadhi dawa la Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS)


WIZARA ya Afya ya Zanzibar na Bohari ya Dawa (MSD) wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa MSD kuipatia wizara hiyo huduma ya kuwasambazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kupitia Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS)

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuhakikisha wananchi wake wanapata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.Akizungumza wakati wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Abdulla amesema changamoto ya upatikanaji wa dawa ilikuwa kubwa, zikipatikana kwa gharama ya juu na kiwango kidogo walichohitaji ilikuwa inaleta shida wanapoagiza wenyewe.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muungano shairi,na kuipongeza Bohari ya Dawa (MSD) na Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMS) kwa kutekeleza taratibu zote kwa haraka hadi kufika kusaini makubaliano hayo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu amewahakikishia kuwa watawapa huduma nzuri,zenye viwango na kwa wakati na bei nafuu kutokana na kushuka kwa bei ya dawa kwani wananunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.

Ameongeza kuwa pamoja na maboresho ya kiutendaji yanayoendelea kufanyika MSD,taasisi hiyo pia imeteuliwa kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa Jumuiya ya nchi za Ukanda wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hivyo huduma zake zinakubalika kimataifa,hasa katika mnyororo mzima wa ugavi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMS Zanzibar , Zahran Ali amesema licha ya makubaliano yaliyofikiwa na kusainiwa, wamekuwa wakishirikiana na MSD kwa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutoa watalaam wa kuwasaidia kuboresha mnyororo wa ugavi na masuala ya maoteo sahihi ya mahitaji ya wateja.

STEVE NYERERE AMSHUKURU RAIS MAGUFULI

DC SHINYANGA AUNGANA NA WANANCHI KUZUIA MAJI BWAWA LA MWALUKWA YASITOROKE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Ijumaa Januari 26,2018 ameungana na wananchi wa kijiji na kata ya Mwalukwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kuziba ukingo wa bwawa la Mwalukwa ambao umebomoka na kusababisha maji yatoroke.

Matiro aliyekuwa ameambatana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bahati Kasinyo Mohammed pamoja na baadhi watendaji wa halmashauri akiwemo Injinia wa maji Silvester Mpemba aliungana na wananchi kuziba sehemu ya ukuta/ukingo wa bwawa iliyobomoka na kusababisha maji yavuje/yatoroke.
Bwawa hilo lililojengwa kwa nguvu ya wananchi kati ya mwaka 1941- 1951 linahudumia wananchi wa kata ya Mwalukwa yenye vijiji vinne ambavyo ni Ng’hama,Bulambila,Mwalukwa na Kadoto B lakini pia kijiji cha Mwamadilanha kilichopo katika kata ya Pandagichiza.

Akizungumza wa zoezi hilo la kuziba sehemu ya bwawa inayovuja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro aliwataka wananchi kutunza bwawa hilo wakati serikali inaendelea na utaratibu wa kufikisha huduma ya maji ya mradi wa Ziwa Victoria katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mradi huo.

“Nimekuja hapa kuungana nanyi kuongeza nguvu ya kuzuia maji yasitoke,niwapongeze pia kwa kuja,naomba mtunze bwawa hili kwani kuna maeneo mengine wanatamani kuwa na bwawa kama hili,maafisa watendaji ,viongozi wa sungusungu na viongozi ngazi za vijiji na kata wekeni utaratibu wa kutunza hili bwawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo yenu”,alisema Matiro.

Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Bahati Mosinyo Mohamed alisema pesa zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo bado hazijafika hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na hofu kuwa huenda pesa zimeliwa na baadhi ya watu.

Nao Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela na katibu wake Jumanne Katundu walioshiriki katika zoezi hilo,waliwaomba viongozi wa vijiji na kata kuunda sheria na kanuni kwa ajili ya kutunza bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiangalia maji yaliyoroka katika bwawa la Mwalukwa lililopo katika kata ya Mwalukwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kulia ni wananchi wa kijiji cha Mwalukwa wakiweka mchanga kwenye mifuko ili kuzuia maji yasitoroke katika bwawa hilo.
Sehemu ya bwawa la Mwalukwa.
Kulia ni diwani wa kata ya Mwalukwa Ngassa Mboje akionesha sehemu ambayo bwawa limemong'onyoka ukuta na kusababisha maji yavuje/yatoroke.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifukia sehemu ya ukingo wa bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mwalukwa kuchimba udongo kwa ajili kuziba sehemu ya ukuta/ukingo uliobomoka katika bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akiwa amebeba karai la udongo aliouchimba kwa ajili ya kuziba ukingo/ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishirikiana na mwananchi kubeba mfuko wa udongo kwa ajili ya kuziba ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasititiza wananchi kulinda bwawa hilo.

WANANCHI WAPEWA MIEZI SITA KUTOA MAZAO NDANI YA HIFADHI YA RELI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda kiberenge kwenda kukagua ukarabati wa reli iliyoharibika kwa mvua katika eneo la umbali wa kilomita mia moja lililopo kati ya Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Bwana Masanja Kaodogosa (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) kazi ya kukarabati reli ikiendelea unaofanywa na wafanyakazi wa Shirika hilo baada ya kuharibika kwa mvua wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati huo katika kijiji cha Mkadage kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akishuka kwenye tingatinga inayojaza udongo kwenye eneo lililopo katika kijiji cha Munisagala kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kukagua kazi inayoendelea ya kujenga na kurejesha miundombinu ya reli iliyoharibika na mvua wakati wa ziara yake kwenye eneo hilo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa.
 Kazi ya kujaza udongo kwenye eneo la ukubwa wa mita 170 lililopo katika kijiji cha Munisagala kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro ikiendelea kwa ajili ya kujenga na kurejesha miundombinu ya reli iliyoharibika na mvua.
Mhandisi Mkuu Ujenzi wa TRL Mhandisi Nelson Ntejo akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano (kulia) uharibifu wa miundombinu ya reli uliotokea kutokana na mvua wakati wa ziara yake ya kukagua uharibifu huo na ukarabati unaoendelea kati ya Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa.


Serikali imetoa miezi sita kwa wananchi wanaolima ndani ya eneo la hifadhi ya reli inayopita Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kuhama eneo hilo baada ya kuvuna mazao yao ili kuhifadhi miundombinu ya reli na kupunguza uharibifu wa miundombinu hiyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ua Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake alipotembelea kukagua ukarabati wa reli iliyopo eneo la Kilosa, Morogoro na Gulwe, Dodoma lenye umbali wa kilomita mia moja baada ya kuharibika kwa mvua na Serikali kusitisha usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbali mbali na nchi za jirani.

Nditiye amesema kuwa uharibifu wa eneo hilo ni wa kiwango kikubwa kwa kuwa katika kipande cha umbali wa kilomita mia moja zilizoharibika kwa mvua baadhi ya maeneo reli imebomoka, kuhama kwenye njia yake na ardhi husika kuliwa na maji ya mvua yaliyojaa kwenye mto Mkondoa ambao unapita pembezoni mwa reli hiyo. 

Ameongeza kuwa uharibifu huo unasababishwa na shughuli za kibinadamu ambapo wananchi wanaishi na kulima ndani ya mita thelathini upande wa kulia na kushoto mwa reli ambapo ni hifadhi ya miundombinu ya reli na wananchi hawaruhusiwi kutumia eneo hilo kwa shughuli yeyote. “Nakuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa ushirikiane na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kuwahamisha wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi hii wakishavuna mazao yao kwa kuwa kilimo kinasababisha mmomonyoko wa udongo hivyo kuharibu miundombinu ya reli”, amesisitiza Mhandisi Nditiye.

Amesema kuwa Wizara yake itawasiliana na kushirikiana na Wizara ya Maji, Kilimo na Umwagiliaji ili waweze kukarabati mabwawa makubwa matatu ya Hombolo, Kidete na Manyara ili yaweze kuhifadhi maji na kuyadhibiti kama ilivyokuwa hapo awali ili yasipitilize kuingia kwenye mto huo bila kufunguliwa kwa utaratibu  na kuharibu miundombinu ya reli.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bwana Masanja Kadogosa amesema kuwa tayari Shirika lake limeleta vifaa na wafanyakazi katika eneo hilo ambapo wanafanyakazi kazi mchana na usiku ili kuhakikisha kuwa reli hiyo inaanza kutumika tena kwa shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo.

 Ameongeza kuwa kwa siku Shirika lake linapoteza takribani shilingi milioni mia mbili ambazo ni chanzo cha mapato kwa Shirika hilo na Serikali kwa ujumla. Amesema kuwa Shirika lake limefanya tathmini na kubaini kuwa kiwango cha uharibifu wa reli hiyo ni kikubwa na tayari ameiomba Serikali impatie jumla ya shilingi million 994 za kukarabati eneo hilo.

Aidha, Bwana Kadogosa amewashukuru wakandarasi wanaojenga reli mpya ya kisasa ya SGR kwa kuwa wazalendo na kuwapatia vifaa ambavyo wanavitumia kukarabati eneo hilo. Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika hilo akiwa katika moja ya eneo la tukio lililopo katika kijiji cha Mkadage wilayani Kilosa mkoani Morogoro, akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, Bwana Jumanne Kinyasi ameiomba Serikali kumpatia Bwana Kadogosa fedha hizo na kuwaongeza vifaa ili waweze kukarabati reli hiyo ili waweze kurejesha huduma kwa wananchi. 

Bwana Kadogosa amemweleza Mhandisi Nditiye kuwa ukarabati huo utakamalika mapema wiki ya pili ya mwezi Januari mwaka huu. Bwana Kadogosa alifafanua kuwa reli hiyo imekuwa ikikumbwa na changamoto ya kuharibika kila baada ya kipindi cha miaka kumi ambapo iliwahi kuharibika tena mwaka 1998, 2007 na sasa mwaka huu 2018 kutokana na mabadiliko ya majira ya mvua, tabia nchi na hali ya hewa. 

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili wa kutoka Japan na mkandarasi anayejenga reli ya kisasa ili kuweza kupata mwarobaini wa kudumu wa kudhibiti na kuondoa kabisa uharibifu wa miundombinu ya reli hiyo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RPC TABORA AWAOMBA WADAU KUSAIDIA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA POLISI.

$
0
0
Na Tiganya Vincent

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi Askari wake jambo linalowafanya wengi kupanga uraini ambapo sio salama kulingana na shughuli zao.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Wilbroad Mtafungwa wakati wa hafla fupi ya sifa na zawadi kwa askari Polisi vyeo mbalimbali mkoani humo waliotumia Jeshi hilo kwa weledi na nidhamu.

Alisema kuwa ambazo wanaishi Maaskari ni kongwe na chakavu ambapo zinahitaji ukarabati mkubwa na kujengwa mpya ambazo zitasaidia Askari waliopanga uraiani kuondoka huko na kuisha katika nyumba hizo.

SACP Mtafungwa alisema kuwa Askari wanaoishi kambini hivi sasa ni 327 na waliopo uraiani ni 853 na hivyo kufanya Askari wengi kuwa uraiani.Kufuatia hali Kamanda huyo wa Mkoa aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia Jeshi la Polisi ili liweze kupata makazi katika maeneo yao maalum ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi.

Alisema kuwa kama wanavyochangia katika Ujenzi wa Vituo mbalimbali vya Polisi ni vema wakachangia pia ujenzi wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Polisi ili kuondoa tatizo la ukosefu wa nyumba kwao.

Akizungumza mara baada ya kuwapa tuzo Askari wa vyeo mbalimbali waliofanya vizuri,Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilipongeza Jeshi hilo mkoani katika jitihada inazoendelea nazo katika kupambana na uhalifu ikiwemo mauji ya vikongwe kwa imani za kishirikina.

Alilitaka Jeshi hilo kuendelea na kazi yao waliyoanza ya kupambana na vitendo vya uhalifu kwa ajili kuifanya Tabora kuwa mahali salama na safi pa watu kuishi na kwenda kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kukabiliana na uhalifu mkoani humo.

Mwanri alisema kuwa ni vema namba za kutoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi zikaendelea kuwa wazi ili wananchi wenye taarifa ambazo ni sahihi waweze kujulisha Jeshi hilo ili liweze kuzuia.

Alisema kuwa lengo ni kutaka kuufanya Mkoa wa Tabora uwe kimbilia la wawekezaji kwa kuwa sehemu ambayo haina usalama hakuna mtu anayetaka kuwekeza fedha zake.“Endeleeni kupambana na wahalifu wa aina zote mpaka hapo tutakapoona kuwa Mkoa wetu umekuwa na amani kama zilivyo nyumba za Ibada…na ambapo wahalifu wataogopa kuingia mkoani kwetu” alisema Mwanri.

Katika sherehe hizo jumla ya Askari 27 na raia 1 walipatiwa tuzo kwa ajili ya utumishi wao ulitukaka, unaozingatia weledi na nidhamu na hivyo kulijengea heshima Jeshi hilo.

HAKIKISHENI WALIMU WANAPANDA MADARAJA - WAZIRI JAFO

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu(TCC) kusimamia na kuhakikisha Walimu wote wanapanda madaraja kwa wakati na kwa mujibu wa Elimu zao ili kupunguza Malalamiko ya Walimu wetu Nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Tume za Utumishi wa Walimu za Wilaya kwa Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo Mkoani Dodoma mapema leo Tarehe 26/01/2017.

Waziri Jafo alisema kuwa kumekuwa na malalamiko, manunguniko na masononeko ya muda mrefu toka kwa Walimu kuhusu suala hili ya Upandaji wa madaraja halifuati taratibu aliyeajiriwa mwaka 2000 na anaweza kuwa sawa na yule aliyeajiriwa mwaka 2008 na wengine wamejiendeleza Kielimi lakin hakuna mabadiliko yoyote madaraja yao.

‘Tume hii ifanye kazi ya kurudisha hadhi ya Walimu, iwajengee heshima na thamani yao katika Jamii, shughulikieni malalamiko yao ya Msingi madaraja yao yapande kwa kuzingatia muda waliokaa kazini, elimu yao na Utendaji wao wa kazi; Hilo lisitegemee “favour” ya Katibu wa Watumishi wa Tume waliopo katika eneo husika’

Wakato huo huo Waziro Jafo alisisitiza  wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu kuwa Mkutano huu utumike kupeana maarifa ya kazi, jinsi gani mnaweza kufanya kazi kwa Usahihi zaidi kwa kuzingatia Sheria iliyounda TUME YA UTUMISHI WA WALIMU ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2016.

‘Tume hii Ndio iwe Kimbilio la Walimu, iwe tegemeo la Utatuzi wa matatizo yote ya Walimu kwa sababu Tume ya Walimu ndio muajiri wa Walimu, Inasimamia Nidhamu za Walimu na mchakato mzima unaohusi Ajira za Mwalimu awapo kazini hivyo mfanye kazi kwa Haki, mkaepuke rushwa, Mkawe na busara na Hekima katika kutatua changamoto za Walimu’ 

Aidha Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha wajumbe wa Tume ya Utumishi wa walimu kuhusu mgawanyo wa Walimu katika halmashauri kwa kuzingatia vipindi wanavyotakiwa kufundisha na uwekaji wa takwimu sahihi za Walimu waliopo sasa, wanaotarajiwa kustaafu kwa mwaka huu na kuweka maoteo ya ajira mpya zitakazohitajika kutokana na nafasi zitakazoachwa na wale wanaostaafu hivi karibuni.

“Takwimu zisiwe za kubahatisha tena kupitia Tume hii mhakikishe mnakuwa na Takwimu sahihi kwanza za mgawanyo wa Walimu katika kila Halmashauri je mgawanyo wa walimu waliopo Malinyi ni sawa na mgawanyo wa Walimu waliopo Manispaa sio Mwalimu wa Manispaa anafundisha vipindi viwili kwa wiki wakati anatakiwa kufundisha 20 na pia mahitaji ya walimu kulingana na masomo wanayofundisha maoteo kwa kuzingatia idadi ya wale wanaostaafu” Alisema Jafo.

 Waziri Jafo alimalizia hotuba yake kwa Tume hiyo kufanya tadhimini  ya kina  kuhusu maadili ya waalimu  na wanafunzi na kwa waalimu wanaovunja Sheria, Kanuni na maadili  ya kazi ya waalimu  ikiwemo uzembe , utoro kazini, rushwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya  Utumishi wa Walimu Ndg.Oliva Mhaiki alisema wajumbe wa kamati za TSC Wilaya waliteuliwa rasmi na Tume katika mkutano wa Tar 20-25/02/2017 na tangu walipoteuliwa na kuanza kutekeleza majukumu yao hawakuwahi kupewa mafunzo yeyeote hivyo Sekretariet imeona upo umuhimu wa kufanya mkutano wa kazi kwa lengo la kuelekezana wajibu na majukumu yao kama kamati.
 Waziri WA Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akifungua Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Katibu wa Tume ya Walimu (kushoto aliyesimama) Mwl. Winifrida G. Rutaindurwa  akiwasilisha taarifa ya Tume katika Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw.Oliva Paul Mhaiki akitoa neon la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
Waziri WA Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa katikati) katika Picha ya Pamoja na Sekretariet ya Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA BOHARI YA DAWA TANZANIA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo  .

WIZARA  ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja na hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla Juma alitia saini kwa upande wa Wizara hiyo na Mkurugenzi  Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu aliiwakilishi Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Zanzibari Mnazimmoja.

Akizungumza baada ya kutiliana sani Bi. Asha Abdalla alisema ushirikiano huo utaisaidi Serikali na wananchi kwa jumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha  dawa zote zinapatikana  bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya afya na kufanikisha  malengo yake ya kuwapatia wananchi  huduma bora za afya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya ameshauri mashirikiano yaliyoanzishwa baina ya Bohari  Kuu ya Dawa Zanzibar na Bohari Kuu ya Tanzania yawe endelevu na kuwa mfano kwa Taasisi nyengine za pande mbili za Muungano na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Rugambwa Bwanakunu ameihakikishia Wizara ya Afya kwamba watatoa huduma bora kwani dawa wanazoagiza ni za uhakika  na zenye ubora .

Alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa dawa na vifaa tiba na hivi sasa wameingia mikataba na viwanda vikubwa  vya kuzalisha dawa vya  ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amewapongeza maafisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  waliosimamia na kufanikisha mpango huo kwa muda mfupi bila ya kuwa na urasimu katika utekelezaji wake.

Ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuwaamini na kukubali kushirikiana nao katika kazi ya uagizaiaji wa dawa na vifaa Tiba na amewahakikishia kwamba kazi hiyo wataifanya kwa pamoja katika viwanda vya kuzalisha dawa.    

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania amewashauri wawekezaji wa Zanzibar kuwekeza viwanda vya dawa kwa lengo la kupunguza kuagiza bidhaa hiyo kutoka viwanda vya nje.

Alisema kati ya viwanda vitano vya dawa walivyoingia mkataba wa kununua dawa hakuna hata kiwanda kimoja kutoka Zanzibar wakati wafanyabiashara wenye  uwezo wa  kuwekeza katika sekta hiyo wapo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa  Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakitia saina makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya  Zanzibar na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Asha Abdalla Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu wakibadilisha hati za makubaliano baada ya kutiliana saini makubaliano hy katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Laurean Lugambwa Bwanakunu akizungumza  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Abdalla Juma akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa Bohari ya Dawa Tanzania  baada ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati yao. Picha na Abdalla Omara Maelezo - Zanzibar

DKT TULIA ACKSON APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE YA WALEMAVU KATUMBA MKOANI MBEYA

$
0
0

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea Msaada wa Vifaa kwa ajili ya shule ya Walemavu ya Katumba iliyopo Mkoani Mbeya Wilaya ya Rungwe .
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akipokea Msaada wa kofia kwa ajili ya Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule ya Walemavu Katumba kutoka kwa Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery.
 Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery akizungumza kabla ya kukabidhi Msaada  wa Vifaa kwa ajili ya shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Katumba.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akipokea Msaada wa Karatasi kwa ajili ya watu wasioona kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Quintex International Shafiq Dhalla ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya ya Human Relief Foundation .
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, akipokea Baiskeli ya Walemavu kutoka kwa Meneja wa Miradi wa Human Relief Fondation Mustafa Bunamay  wakati tasisi hiyo ilipokuwa ikikabidhi msaada kwa ajili ya shule ya Maalum Katumba.
  Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery, akimkabidhi alama ya tasisi hiyo Mjumbe wa bodo wa Human Relief Tanzania Mohamed Bahaswan(Big Bon).
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akipokea alama ya Tasisi ya Human Relief Foundation kutoka kwa  Mkurugenzi wa Human Relief Foundation  Sheikh Khalid Butchery
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tasisi ya Human Relief  Tanzania

RAIS DKT MAGUFULI NA MAMA JANETH MAGUFULI WACHANGIA SH. MILIONI 15 KWA AJILI YA MATIBABU YA MWIGIZAJI WASTARA JUMA

$
0
0


  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwasilli kumkabidhi mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya Sifael nchini India, kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.     
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizochangwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya sifael nchini India, kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo. 
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na waendesha kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU wakimsikiliza mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma  akishukuru kwa kupokea shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu yake nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike pia alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya sifael nchini India kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.  
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na ujumbe alioongozana nao pamoja na  waendesha kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mwigizaji wa filamu za Bongo movie Wastara Juma  baada ya kumkabidhi  shilingi milioni 15 zilizotolewa na Rais John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 26, 2018. Bw. Samike pia alimkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizocahngwa na wasaidizi wa Rais. Msanii huyo maarufu, ambaye alionekana na Rais kupitia kipindi cha Clouds TV cha SHILAWADU akiomba msaada wa pesa ili kurudi hospitali ya Sifael nchini India kwa  matibabu chini ya uangilizi wa hospital hiyo, amemshukuru Rais kwa kuwajali wananchi wake.  

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH WATOA MSAADA KWA MSANII WASTARA JUMA ISSA

SERIKALI YAWATOA HOFU WAKULIMA MKOANI RUVUMA UHABA WA MBOLEA

$
0
0
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania TFRA imewatoa hofu wa kulima wa mkoa wa ruvuma, baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika maghala ya kuhifadhia mbolea SONAMCU ,na kukuta shehena ya mbolea ikiwa ya kuridhisha kama anavyobainisha Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mbolea Lazaro Kitunda.  

Ujenzi wa ofisi za walimu yaanza kutimia-Makonda

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa fikira ya kutaka kuwa na ofisi bora za walimu katika mkoa wa Dar es Salaam imeanza kutimia kwa baadhi ofisi kufikia hatua ya upauaji.

Akizungumza leo katika uzinduzi ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi, Makonda amesema sasa anapata usingizi kuona ndoto yake inanitimia ya kuwapa ofisi nzuri za wanafunzi.

Makonda amesema kuwa wakati alipikuja na wazo hilo alijua hali ni kazi ngumu lakini kutokana na msukumo wa sasa chini ya Serikali ya Dk. John Pombe Magufuli ya elimu bure inatimia.Amesema maendeleo yeyote kwa watoto wa kitanzania yanaanza kwa walimu ambao ndio wataweza kuzalishwa watoto hao kupata elimu na kuinuka kiuchumi.

“Mtu mwenye umasikini hana nyumba ambayo haina bati kamwe hawezi mtu kuwa na nyumba ya bati ili aweze kuwa na nyumba hiyo lazima apate elimu”amesema.Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa huyo amesema wanaonunua maeneo ya shule ni kukamatwa pamoja na wanaonunua wakamatwe ambapo mtu mmoja Ajay Shohan amekamatwa kwa kununua eneo la shule ya msingi Mapinduzi.

Katika hafla ya uzinduzi wa upauji wa shule msingi Mapinduzi kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali na ofisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mchango huo kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Halotel, Le Van Dai amesema mchango huo ni sehemu tu ya jitihada kubwa zinazofanywa na kampuni hiyo katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu nchini ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha maendeleo ya nchi hasa kupitia sekta ya elimu ambayo ni muhimili wa maendeleo ya kila nchi duniani.

“Tunatambua kuwa, huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na waalimu ni moja ya msingi imara katika kukuza sekta ya elimu nchini, kwa kuzingatia hili tumeamua kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa mchango wetu wa kifedha ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za waalimu ikiwa ni sambamba na kuboresha mazingira utendaji kazi kwa waalimu ya kazi na kurahishisha ufanisi wao katika kuwafunza wanafunzi ambao ni taifa la leo na kesho” alisema Dai.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea Hundi ya Milioni 50 kutoka kampuni ya Hallotel kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu 402 Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kukamalika kwa ujenzi wa ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi, leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akitoa taarifa ya hatua za mbalimbali za ujenzi wa ofisi za walimu leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa upauaji wa ofisi ya walimu shule ya msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjemini Sitta akizungumza juu hatua ujenzi wa ofisi katika manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipaua jengo la ofisi ya walimu katika shule msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitoa Cha Polisi Magomeni, Morcase akipata maelezo kwa Ajay Shohan aliyenunua eneo la shule ambapo Mkuu wa Mkoa aliamuru akamatwe,leo jijini Dar es Salaam.

WATU WASIYOJULIKANA WACHOMA MOTO BANDA LA VIJANA WA KIKUNDI CHA KUJIKOMBO GROUP WILAYA YA WETE PEMBA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba Abeid Juma Ali akikagua banda la vijana wa kikundi cha Kujikomboa Group kiliopo shehia ya Gando Ziwengi Wilaya ya Wete lililoteketezwa kwa moto na watu wasiyojuilikana usiku wakuamkia leo Januari 26, 2018
 Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali akizungumza na vijana wa kikundi cha Kujikomboa Group cha shehia ya Gando Ziwengi alipofika kuwafariji.
Eneo la shamba la matunda na alizeti linaloshughulikiwa na kikundi cha Kujikomboa Group cha Gando Ziwengi.Picha na Makame Mshenga Pemba.

TAA YARUDISHIWA KIWANJA CHA NDEGE KAHAMA

$
0
0
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (wanne kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack (Mwenye ushungi) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), jana wakikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama kabla ya makabidhiano ya kurudishwa serikalini na Kampuni ya Madini ya ACACIA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainabu Telack akihutubia wananchi waliofika kushughudia makabidhiano ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama yaliyofanyika jana baina ya Kampuni ya Madini ya ACACIA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), akisaini nyaraka za makubaliano ya kurudishwa Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa serikali kutoka kwa Kampuni ya Madini ya ACACIA, ambapo wa pili kulia ni Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu na wakwanza kulia ni Mwanasheria wa ACACIA, Bi Diana Wamuza, huku Naibu Waziri Sekta ya Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (mwenye miwani) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack wakishughudia
Mwanasheria wa ACACIA, Bi. Diana Wamuza (wa kwanza kulia) akishuhudia makabidhiano ya nyaraka za kurudishwa kwa Kiwanja cha ndege cha Kahama uliofanywa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu.
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akizungumza mara baada ya makabidhiano ya kurudishwa serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kutoka kwa Kampuni ya Migodi ya ACACIA, uliofanyika jana mkoani Shinyanga. Mwenye ushungi ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela



KAMPUNI ya madini ya ACACIA yenye kumiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu imekirudisha serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa ujumla.

Awali mwaka 2005 kiwanja hicho kilikabidhiwa kwa makabidhiano maalum kati ya serikali na iliyokuwa kampuni ya madini ya Barrick walioomba ili kurahisisha shughuli zao za migodini ikiwemo ya kutumia ndege kusafirisha wafanyakazi wao na vifaa. 

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela aliiomba serikali kusaidia kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kutoka Km. 1.5 hadi kufikia Km 2, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa ikiwemo ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400. 

“Tunashukuru wenzetu wa ACACIA kwa kurudisha tena serikalini kiwanja hiki, lakini bado tunaimani tutaendeleza ushirikiano baina yetu, lakini ombi langu kwa serikali ni kuongeza urefu wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ili ndege kubwa zaidi ziweze kutua ninaimani zitachochea shughuli za kilimo, biashara na madini na uchumi wananchi utaimarika zaidi,” alisema Bw. Mayongela. 

Pia alisema kutua kwa ndege nyingi kutatoa fursa za ajira kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani, ambapo pia TAA itaweza kusogeza huduma zaidi ikiwemo ya maduka, hoteli na mafuta ya ndege, ambapo sasa ndege hazitalazimika tena kujaza mafuta Tabora au Mwanza, kwa safari zake mbalimbali. Naye Naibu Waziri, Mhe. Kwandikwa alisema serikali itahakikisha inasaidiana na wadau mbalimbali ili waweze kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa za abiria na mizigo, ambazo zitachochea maendeleo ya Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla. 

Hatahivyo, Mhe. Kwandikwa aliwataka ACACIA kuweka katika mipango yao ya kusaidia ujenzi wa upanuzi na urefushaji wa Kiwanja cha ndege cha Kahama, ili kiweze kutumika kwa lengo la kutua kwa ndege kubwa, ambapo itachochea sera ya kukuza viwanda. 

“Tunamaeneo mengi sana hapa Shinyanga, tunawaita wawekezaji waje kuwekeza kwa wingi katika ujenzi wa viwanda, kilimo, madini na biashara nyingine, sasa usafiri wa uhakika upo ukizingatia tunaviwanja viwili vya ndege kikiwemo hiki cha Kahama na kile cha Shinyanga, na malighafi, umeme na maji vipo vya kutosha hivyo waje tu kuwekeza,” alisisitiza Mhe. Kwandikwa. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Bi. Telack alisema sasa mkoa wake utainuka kwa kuwa umepata fursa ya kuongezewa kiwanja cha pili cha ndege cha Kahama, ambapo sasa wananchi wataweza kusafirisha mazao ya kilimo na kufanya biashara na mikoa mingine kutokana na usafiri wa ndege ni wa haraka na uhakika. 

“Ninakuomba Naibu Waziri najua hili lipo kwenye wizara yako, utusaidie kuharakisha kumalizika kwa kiwanja cha ndege cha Shinyanga, maana hiki hapa tayari kipo ili na sisi tuweze kupata wawekezaji katika viwanda mfano Wachina wasiende kuwekeza mkoani Pwani pekee bali waje na huku, tunaimani tutachochea maendeleo sio ya mkoa wetu tu ila kwa Taifa kwa ujumla,” alisema Bi. Telack. 

Kwa upande wa Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu alisema wanajivunia tukio la kurudisha kiwanja cha ndege cha Kahama kwa serikali, ili sasa kiweze kutumika na Watanzania wote katika kuchochea ukuaji wa viwanda. Hata hivyo, Bw. Busuzu ameahidi wataendelea kutoa huduma mbalimbali kwenye kiwanja hicho kama ilivyokuwa awali, na wataendeleza ushirikiano mzuri ulipo kati yao na TAA.

Waziri Ummy Mwalimu afungua CT-Scan hospitali ya Bugando

$
0
0
Na WAMJWW.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB)  ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akifungua mashine ya  CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vya hospitali hiyo.
Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kupata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya  JKCI ya jijini Dar es Salaam.
 Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa  CT-Scan kwenye hospitali ya Bugando,kulia ni Baba Askofu wa Kanisa katoriki jimbo la Geita Flavian Kasala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
.
Mashine ya CT-scan iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6
 Waziri Ummy mwalimu akiongea na watumishinwa hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya bugando wakati wa uzinduzi wa mashine ya CT-scan.
 Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya bugando dkt.Abel Makubi akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.
 Mtaalamu wa Mionzi wa hospitali ya Bugando akimpatia maelezo Waziri wa Afya mara baada ya ufunguzi wa mashine hiyo
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu.
 Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa Hospitali hiyo kwenye kitengo cha Saratani hospitalini hapo.
 Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mzee Juma Salumu kutoka tabora aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya masikio.Waziri amewahakikishia serikali ipo mbioni kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali ya mkoa ya Tabora ili kupunguza gharama kwa wananchi

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA SHUGHULI ZA UPANDAJI MITI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akihutubia wakati zoezi la upandaji miti kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani  iliyofanyika mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akipanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani  iliyofanyika mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Kangi Lugola akishiriki katika zoezi la upandaji miti katika kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akifurahia jambo na Wajumbe wa kamati ya bunge ya viwanda , biashara na Mazingira katika siku ya zoezi la programu ya  upandaji wa miti na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliohudhuria katika zoezi hilo wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani)
Pichani Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakitumbuiza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti.

Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla

$
0
0
Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla (MB) mapema leo Januari 26,2018,amefanya ziara maalum katika Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Namba 62, ambayo aliishi hapo miaka ya 1950's Dk. Kigwangalla ameweza kujionea mambo mbalimbali ndani ya makumbusho hayo huku pia akipokea maoni ya namna ya kufanyiwa maboresho ya kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi na maegesho ya wageni wanaotembelea hapo.

"Nimefika hapa leo kujionea Kituo hichi ambacho ni kielelezo kikubwa cha Mwasisi wa Taifa letu. Hapa pana hazina kubwa na kituo hiki kina mambo mengi sana ya kumuenzi Baba wa Taifa. Kwa hali tuliookuta kwa kweli tutakaa na timu yangu kuona tunafanya maboresho makubwa kabisa ili kiwe kama maeneo mengine yenye Wahasisi wa Mataifa yao, tumeona kama eneo alilozaliwa Mzee Mandela kule Afrika Kusini, nyumba yake imehifadhiwa vizuri na imekuwa na wageni wengi. Kwa hapa kwetu na sisi tutakaa na wenzetu kutatua changamoto hizi. 

Hapa tutajenga Maktaba ambapo watu watakuja kusoma vitabu vya Mwasisi wetu na kuona mambo aliyokuwa akifanya. Lakini pia tutaonana na Viongozi wa Halmashau ri ya Kinondoni kuona namna ya kupaboresha mahala hapa ikiwemo miundombinu ya Barabara ya kuingia na kutoka eneo ili" alieleza Dk. Kigwangalla.

Pia aliongeza kuwa, kituo hicho kipo katika hali mbaya kikikabiriwa na changamoto licha ya kuwa ni kituo muhimu sana hapa nchini. hivyo amewahakikishia wahifadhi wa Makumbusho hayo mipango iliyopo ni pamoja na kukifanyia marekebisho kutengeneza choo, kupaka rangi pamoja na kufanyia ukarabati mkubwa vionyeshi vya kumbukumbu nzima ya Baba wa Taifa.

Aidha, amesema kuwa, lengo kwa sasa ni kuifanya nyumba hiyo iwe kama nyumba halisi ailivyokuwa akiishi mwenyewe Baba wa Taifa kwani ndani bado kuna vitu halisi alivyokuwa akivitumia Mwasisi mwenyewe huku pia mikakati ni pamoja na kununua hata nyumba za jirani ili kuongeza eneo na kuongezwa baadhi ya ofisi na pawe na hadhi kama Mwasisi mwenyewe" alieleza Dk.Kigwangalla. 

  "Kiukweli nimefika hapa kushuhudia makumbusho haya ambayo kiuhalisia hapa ni hazina kubwa sana ya kumbukumbu ya Taifa letu hasa katika harakati za kupigania Uhuru pia zilianzia hapa katika nyumba hii. Pia tutaboresha zaidi kwa kuweka studio maalumu ambayo pia tutaboresha CD zote za Baba wa Taifa zitakuwa zikioneshwa humo ikiwemo zile za Hotuba.Awali Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho hayo, Bi. Neema Mbwana alieleza changamoto zinazoikabili kituo hicho pamoja na kuomba kuboreshwa kwa vitu muhimu ikiwemo Ukarabati wa nyumba nzima, ikiwemo, paa na kupaka rangi. 

  Aidha, waliomba kuboreshewa vionyeshwa ikiwemo kujengea vioo katika kuta za vionyeshwa, kuzitengeneza picha katika fremu kitalaamu. Mhifadhi huyo aliendelea kusema kuwa, kwa umuhimu wa vitabu ambavyo hakuna nakala zake halisi ambavyo ni mali za Baba wa Taifa, walimuomba Waziri awachapishie tena nakaza zaidi ili ziweze kutumika kwa miaka mingi zaidi kwani vilivyopo vimezidi kuchakaa. 

  Mbali na kutembelea Makumbusho hayo ya Nyumba ya Baba wa Taifa hiyo ya Magomeni, Dk. Kigwangalla pia aliweza kutembelea soko kubwa la Vinyago lililopo Mwenge na kujionea wachngaji vinyago hao ambao ni kiungo muhimu cha Utalii hapa nchini hata hivyo alikutana na kero juu ya Watalii kusumbuliwa Viwanja vya ndege kwa bidhaa zao hizo za vinyago.
Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho nyumba ya Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam,Bi. Neema Mbwana akisoma taarifa za kituo hicho kwa Waziri Dk Kigwangalla alipotembelea kituoni hapo mapema leo Januari 26,2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha Wageni alipowasili kituoni hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akitambulishwa wafanyakazi wa kituo hicho
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya vitabu vya Mwalimu Nyerere ambavyo vimehifadhiwa nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya picha mbalimbali za Baba wa Taifa ambazo zipo nyumbani hapo
Mhifadhi Mkuu Neema Mbwana akimuonesha Dk. Kigwangalla moja ya makochi aliyokuwa akiyatumia Baba wa Taifa wakati akiishi hapo
Dk. Kigwanglla akiangalia moja ya chungu cha shaba alichokuwa akitumia Mwalimu Nyerere katika nyumba yake hiyo ya Magomeni
Dk. kigwangalla akiangalia moja ya pasi ya mkaa aliyokuwa akitumia Baba wa Taifa wakati akiishi nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na watoto wa Baba wa Taifa wakati akikaa hapo. (Chumba cha watoto wa Baba wa Taifa walitumia)
Dk. Kigwangalla akiangalia kitanda alichokuwa akikitumia Baba wa Taifa wakati akiishi kwenye nyumba hiyo
Mhifadhi Neema Mbwana akimuonesha Waziri Dk. Kigwangalla nyuma ya nyumba hiyo na eneo lilivyo
Eneo la nyuma ya nyumba hiyo kama linavyoonekana
Akiwa katika Eneo la Vinyago Mwenge, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kushuhudia baadhi ya bidhaa hizo ambazo pia zimekuwa ni kielelezo kikubwa cha watalii
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago cha Umoja abacho kinaelezea taswira mbalimbali ikiwemo hali ya uhifadhi wa hifhadhi za Taifa katika nyanja za Ulinzi wa wanyama
 
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vinyao vyenye umbo tofauti ambavyo vimekuwa vikitumika sana katika maofisi za Serikali na mashirika ikiwemo Balozi
Dk.Kigwangalla akiwa anatembelea baadhi ya mabanda ya wachongaji vinyago hao
Dk.Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago kikubwa chenye taswira ya Kimbunga
 
Mkurugenzi wa Mipango na matumizi endelevu ya misitu na nyuki nchini, Mohamed Kilongo (kulia) akimwelezea jambo Waziri Dk.Kigwangalla namna wanavyoshughulikia suala la Wachongaji vinyago hao haswa katika vibali vya miti
Dk.Kigwangalla akimsikiliza kwa makini mmoja wa wachonga vinyago ambao walilalamikia hali ya kutozwa kwa gharama kubwa katika viwanja vya ndege hasa kwa wageni ambao asilimia kubwa ni watalii
 
Dk.Kigwangalla akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wachonga Vinyago Mwenge kukaa pamoja ili kuona watakavyoelewana namna ya kumiliki eneo hilo huku akiahidi kushughulikia suala la bidhaa zao zinazotozwa ushuru mkubwa viwanja vya ndege vya hapa nchini
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
 
Dk. Kigwangalla akiangalia moja wachoraji wakongwe wa Umoja wa michoro ya Tingatinga alipotembelea kujionea michoro hiyo eneo la Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE

RAIS MSTAAFU KIKWETE AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

$
0
0
 Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam NGAMANGE




Na Richard Mwaikenda, Msoga.

.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)


Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani  kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu  Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.



Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.



Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.



Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.



Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.



Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging) bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.



Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.Ezra alizidi kumfurahisha, Dk. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi sh. mil. 80,000,000 kwa mchanganuo ufuatao; 



Heka moja inaweza kupandwa mipapai 1000 hadi 1200 na kwamba mpapai mmoja unaweza kuzaa papai 100 hadi 1300 na endapo kila papai lenye uzito wa kilo 2 likiuzwa kwa bei ya jumla sh. 800 ukizidisha na wastani wa papai 100 kila mche halafu zidisha kwa miche 1000 tu unapata kiasi hicho cha fedha kwa msimu wa kwanza.



Pia alimueleza kuwa uzuri wa miche ya papai huishi miaka mitatu ambapo kila wiki utakuwa unavuna na kuuza, hivyo kukupatia faida kubwa tofauti na mazao mengine ambayo ukivuna mara moja tu.



"Laiti kama ungekuwa mchungaji, padri au sheikh anayehubiri kutafuta waumini, basi bila shaka mimi mmenipata nimekuwa muumini wenu." Alisema Dk. Kikwete huku akicheka kwa furaha."Kubwa mlilonifurahisha ni jinsi mlivyopunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kuzalisha papai 

na faida kubwa nitakayoipata, nipo tayari kutoa heka 10 za kuanzia."Aliahidi Dk. Kikwete ambaye alisema kazi ya kilimo anaipenda na kwamba iko kwenye damu yake. 


Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita Adam Ngamange, ambaye akabla y yote alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuwaalika na kumuomba ajiunge na mtandao, jambo ambalo alilikubali.



Ujumbe alioongozana nao ni Ezra Machogu, Martine  Wamaya wa Kampuni ya Awino Farm, Khalid Tamim, Hassan Tamim na Ali Said ambao ni Wawekezaji wa zao la muhogo,  Mkurugenzi  Betl Worldwide Ltd, Murtaza Bharmal ambaye ni mtaalamu wa masoko na uongezaji thamani mazao na Richard Mwaikenda ambaye ni Mshauri wa Habari wa mtandao huo.

 Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita
 Dk. Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Awino Farm, Wamaya.
 Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra
 Dk. Kikwete akisalimiana na wanachama wa Mkikita wawekezaji katika shamba la Muhogo. Kushoto ni Khalid Tamim na Hassan Tamim.
 Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga
 Ngamange akielezea mbele ya Dk Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
 Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu
 Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai
 Dk. JK akinusa mafuta hayo ya mchaichai


 Dk. Kikwete akifungua kasha la mchaichai

 Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
 J akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
 Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
 JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika
JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor

maonesho ya kitalii kufikia kilele jumapili jijini new york

$
0
0
Mkurugenzi wa East point hotel, ndugu Rashid Adam, na Pia ni Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya ZARA TOURS akiwa kwenye maonesho ya kitalii nchini marekani New York times travel show. Watu ni wengi na maonesho ni makubwa New York times travel Sambamba na Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Wilson Masilingi, wapo pia Tanzania Tourist Board ngorongoro crater pamoja na Tanapa. Maonesho hayo yanatarajiwa kufikia kilele siku ya Jumapili

RAIS WA FIFA KUSHUHUDIA FAINAL YA NDONDO SUPER CUP

$
0
0

 Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika mapema jana jijini Mbeya.
Baada ya kufanyika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup kwa mafanikio katika mikoa ya Mwanza na Mbeya sasa yaongeza wigo kwa mabingwa wa mikoa.

jana jijini Mbeya kamati ya mashindano hayo imetangaza rasmi uwepo wa mashindano ya Ndondo Super Cup itakayofanyika jijini Dar es salaam mwezi februari kwa kushirikisha mabingwa wa mikoa ilipofanyika Sports Xtra Ndondo Cup.

Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amewaambia waandishi wa habari kuwa uwepo wa mashindano hayo ni hitimisho la msimu wa Ndondo Cup 2017 kabla ya kuzinduliwa msimu mpya mwezi wa tatu.

"Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakua na michezo minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, na 21 mwezi februari jiji Dar es salaam" amesema Dauda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Super Cup Gipson George amesema hili ni jambo lingine kubwa kutoka Clouds Media kama support ya wanamichezo wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla hususani ujio wa viongozi wa FIFA nchini.

"Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima kubwa tuliyopewa Duniani lazima na sisi tuwaoneshe kuthamini ujio wao"

"Shaffih Dauda amewasiliana na TFF kuona namna ya kushirikiana kutusaidia kuwezesha kumpata rais wa FIFA kuja kwenye fainali ya Ndondo Super Cup ndio maana tumepanga iwe tarehe 21" amesema Gipson.

Gipson ameongeza kuwa mashindano hayo yanaendana na agenda ya Rais wa sasa wa FIFA ya kurudi chini kabisa (grassroot) mpira unapochezwa na watu wa kawaida wenye vipaji vya hali ya juu.

Msafara wa FIFA ukiongozwa na Rais Infantino unatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 na siku inayofuata watakua katika mkutano utakaofanyika hapa nchini.

Kutangazwa kwa michuano hiyo mikubwa kwa timu za mtaani jijini Mbeya ni heshima kwa chama cha soka cha mkoa huo MREFA ambapo mwenyekiti wake Elias Mwanjala amesema hiyo ni bahati ya kipekee waliyopata kwenda kukutana na Rais wa FIFA.

"Ndondo imefanyika miaka minne lakini sisi tumepata nafasi ya kukutana na rais wa FIFA ni bahati iliyoje, lakini kikubwa ni wana mbeya kuungana kufanikisha jambo hili kwani sio la chama cha soka bali ni jambo la mkoa na nyie Clouds mtusaidie kupata wadhamini" amesema Mwanjala.

Timu zitakazoshiriki Ndondo Super Cup ni mabingwa wa Mwanza timu ya Mnadani Fc, Mabingwa wa Mbeya Itezi United na mabingwa wa Dar es salaam timu ya Misosi Fc huku Goms United iliyocheza fainal msimu uliopita na misosi imeongezwa kama heshima ya mkoa wa Dar es salaam kuwa mwasisi wa mashindano hayo.

Mbali na kutangazwa kwa mashindano hayo Clouds Media imetoa zawadi ya fedha kwa washindi wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup Mbeya yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Mabingwa Itezi Fc wamepata milion tatu, washindi wa pili Terminal fc milion mbili, na washindi wa tatu Tukuyu Star milion moja.

Gasper Samwel Mwaipasi wa Tukuyu Star ameibuka mfungaji bora kwa kufunga goli tano, Frank Anthonwa Itezi United amechaguliwa kuwa kipa bora na beki wa kushoto wa Itezi United Salum Idrisa Chau ametajwa kuwa mchezaji bora


Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images