Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1498 | 1499 | (Page 1500) | 1501 | 1502 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Sophia Mjema amefanya ziara ya kukagua ukarabati wa majengo unaofanyika kwenye Sekondari ya Wasichana Jangwani na Sekondari ya Wavulana Azania ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 3.

  Amefafanua kiasi hicho cha fedha pia kinahusisha ukarabati wa sekodari ya Pugu na unafanywa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania(TBA).

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, akiwa Jangwani ambayo alisoma kidato cha tano na sita, Mjema amesema amefanya ziara hiyo kuangalia maendeleo ya ukarabati huo."Nitumie nafasi hii kuwapongeza Wakala wa Majengo kwa kazi nzuri wanayoifanya.Pia naomba ukarabati huu uende kwa haraka kama ambavyo imeagizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,"amesema.

  Amefafanua ukarabati huo umeleta mabadiliko makubwa katika shule hiyo hasa walipokarabati vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu  ambavyo hapo awali havikuwepo Jangwani.

  "Kwa ukarabati huu hata wanafunzi wenye uhitaji maalumu wanaweza kuendana na mazingira ya shule kwani yatakuwa rafiki kwao,"amesema.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua Milango ya Choo cha Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani ambayo inakarabatiwa katika mpango maalum wa ulitolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk John Magufuli ya ukarabati wa shule kongwe ambapo ukarabati huo  umegharimu Shilingi Bilioni 3 za kitanzania.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akikagua Mabweni  ya Shule Sekondari ya Wavulana ya Azania ambayo inakarabatiwa na Wakala wa Majengo TBA
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akizungumza na Wasichana  wa shule ya Sekondari ya jangwani juu ya kujiepusha ngono wakiwa shuleni ili wasipate Mimba.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Azania Sekondari Goodlove Kapufi kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa ukarabati wa shule hiyo.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema  akikagua mazingira ya shule ya sekondari ya Jangwani,Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo
   Wanafunzi wa Sekondari ya wavulana Azania wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema  akiwa ameketi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani

  0 0

   Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora akifungua rasmi kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Khatib Mohamed akifafanua jambo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara Kuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Light Chobya akielezea majukumu ya idara hiyo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia mjadala kuhusu uboreshaji wa sekta hiyo jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Msajili wa Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB), Eng. Patrick Barozi akiwasilisha mada kuhusu utendaji wa Bodi hiyo katika kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo jijini Dar es Salaam. 
  Wajumbe wa kikao cha ushirikiano na uboreshaji masuala ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma
  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma.
  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi akipanda mti katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.
  wananchi wakishiriki upandaji miti Kongwa.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratious Ndejembi wakifurahi katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde akiwa ameshika miche kwa ajili ya kupanda.
  Miti inayopandwa katika wilaya ya Kongwa

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Anthony Mavunde leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA DODOMA iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

  Waziri Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa.


  Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.
  Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mhe. Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki.

  Na Hamza Temba - Dodoma

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Januari 25, 2018 mjini Dodoma ametaja majina ya watuhumiwa wa ujangili ambao wengi wao ni wamiliki na washirika wa Kampuni za uwindaji wa kitalii na kuwapa siku saba wawe wamefika kwa hiari yao wenyewe katika ofisi za Wizara hiyo Mjini Dodoma, Swagaswaga House kwa ajili kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kujibu tuhuma hiyo na nyingine nyingi zinazowakabili mbele ya kamati atakayoiunda.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangalla ametaja baadhi ya tuhuma hizo ambazo ziko kinyume cha sheria na taratibu za uwindaji wa kitalii kuwa ni uwindaji haramu, uhawilishaji wa umiliki wa vitalu vya uwindaji pasipo kufuata sheria, udanganyifu kwenye kujaza fomu za uangalizi,  rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na uhujumu uchumi.

  Alitaja tuhuma zingine kuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uwindaji (kupiga wanyama usiku, kuwinda wanyama bila kujali umri, kupiga wanyama nje ya maeneo waliyopewa), kukutolipa tozo mbalimbali za maendeleo za jamii kwenye vijiji jirani na maeneo wanaoendesha biashara ya uwindaji, kushindwa kuendesha ipasavyo shughuli za kuzuia ujangili.

  Dk. Kigwangalla aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ndugu Pasanis na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Berlette Safari Corporation Ltd na Ngugu Shein Ralgi na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania Ltd.

  Wengine ni Ndugu Howel na wakurugenzi wenzake wa kampuni ya Mkwawa Hunting Safaris Tanzania Ltd, Ndugu Thomas Fredikin na wenzake wa Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, Wengert Windrose Safaris Tanzania  Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, na Ndugu Awadh na wenzake ambao wanamiliki kampuni ya Uwindaji wa Greenmiles Safaris Ltd.

  Aliwataja washirika wengine kuwa ni Ndugu ni Kwizema, Ndugu Robert, Ndugu Solomon Makulu, Ndugu Siasa Shaban, Ndugu Hamis Abdul Ligagabile na mtumishi wa Wizara Wizara ya Maliasili na Utalii, Alex Aguma.

  Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla ametoa Ilani ya siku 30 kwa watu mbalimbali ikiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu waliovamia kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha wafike kwa Kamishna Mkuu wa Ardhi waweze kuhakikiwa na kuthibitisha umiliki wao halali ama sivyo wavirejeshe Serikalini viweze kumilikishwa kwa mmiliki wake halali.

  “Natoa ilani ya siku 30 kwa mtu yeyote ambaye anajua alivamia kiwanja katika eneo hili ambalo lina hati namba 4091 kilichopo Njiro, Arusha, haraka sana ajipange kupeleka taarifa zake mbele ya Kamishna wa Ardhi kabla hatujachukua hatua nyingine za kisheria, hati iliyoko pale ipo katika jina la Bodi ya Utalii Tanzania japo wao wanadai wana hati nyingine.

  “Wengi wao wamejenga nyumba za kudumu katika eneo lile, na wengine ni viongozi waliokuwa mawaziri wakuu wastaafu nao wana viwanja katika eneo hilo na wamejenga nyumba zao katika eneo hilo,” alisema Dk. Kigwangalla.

  Alisema kiwanja hicho kilichokuwa na ekari zaidi ya 40 kilikuwa kinamilikiwa na taasisi ya Serikali ambayo ni kampuni tanzu ya Bodi ya Utalii Tanzania iliyokuwa inajulikana kama Serengeti Safari Lodges na baadae kikauzwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

  Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wanne wanaojihusisha na mtandao wa ujangili pamoja na kupanga njama zilizopelekea mauaji ya Mhifadhi wa Wanyamapori Ndugu Wayne Lotter, raia wa Afrika ya Kusini ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni Pams Foundation, aliyeuawawa eneo la Chole Masaki Jijini Dar es Salaam mwezi Agosti mwaka jana.

  “Natoa siku saba kwa wenzetu wa jeshi la Polisi wachukue hatua dhidi ya watu wanne, ambao mimi majina yao ninayafahamu ambao miongoni mwao watatu wanahusika na kuendesha biashara ya ujangili, na ni watu wakubwa, ni matajiri wakubwa na wana mitandao mikubwa ya ujangili.

  “Ninafahamu taarifa hizi polisi wanazo lakini hawajachukua hatua za kuwakamata watu hawa na kuwafikisha kwenye macho ya sheria, muda ni mrefu  na sisi wenye taarifa hizi sasa tumeanza kuchoka kusubiri.

  “Hawa watu wanne walihusika kupanga njama ambazo zilipelekea kusababisha mauaji ya kikatili ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Palm Foundation, Ndugu Wayle Lotter mwezi Agosti mwaka jana eneo la Chole Masaki mwezi Agosti mwaka jana.

  “Nataka ndani ya siku hizi saba wawe wamechukua hatua na kama hawatochukua hatua manaake tutajua wana vested interest (maslahi) kwahivo tutaenda kuripoti kwa Amiri Jeshi mkuu ambaye ni Mhe. Rais aliyetutuma kazi ya kusimamia sekta hii,”. Alisema Dk. Kigwangalla.
   Dk. Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo leo mjini Dodoma.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume, inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation  inayotoa elimu ya kuwakinga watoto wa kiume wasikumbwe na majanga mbalimbali.
    Mkuu wa Wilaya Ilala,Sophia Mjema, akicheza na wanafunzi wa  Kiume wa shule ya msingi Muhimbili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakiwa katika Maandamano yenye mabango ambao walipita mbele ya mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema Kuonesha hisia zao.
   Mkurugenzi wa Dahuu Foundation, Husna Abdul akizungumza kabla ya kumkaribisha mkuu wa Wilaya kufanya uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation
   Mwanasheria na Mwanaharakati wa haki za Watoto Gebra Kambole akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Tumkumbuke Mtoto wa kiume inayoendeshwa na Tasisi ya Dahuu Foundation
   Mtangazaji wa kipindi cha Leo tena Gear Habibu akizungumza na Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimbili umuhimu wa kuwatunza watoto wa kiume.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema Akiwaaga wanafunzi hao

  0 0

  JOPO la maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), limefanya utambuzi wa nyumba 59 zilizopo eneo la Kipunguni A, jijini Dar es Salaam na kutoa notisi ya siku saba kwa wakazi wake kuhama.Nyumba hizo ni zile ambazo serikali tayari ililipa wakazi wake stahiki zao mwaka 2014 kufuatia uthamini uliofanyika mwaka 1997, lakini bado wanachi hao waliendelea kuishi eneo hilo linalohitajika na Serikali kwa ajili ya matumizi ya shughuli za Mamlaka ya Viwanja vya N dege.

  Akizungumza baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya utambuzi iliyofanyika leo Januari 25, Ofisa Ardhi mkuu wa TAA, Cecilia Mwing'uri amesema jopo hilo lilijumuisha watumishi kutoka TANESCO,  Polisi, TAA kitengo cha sharia na Mahusiano,  na wajumbe wa eneo hilo waliowawakilisha wananchi.

  "Tulizitambua nyumba husika na kuziwekea alama ya X na kutoa notisi ili wakazi ambao bado wapo eneo hilo la Kipunguni wahame ndani ya siku saba kuanzia leo."Kwa bahati nzuri kuna ambao wamehama na wengine wanaendelea na ubomoaji wa kistaarabu wa nyumba zao isipokuwa wachache ambao waliuziwa nyumba  na maeneo huku wamiliki wa kwanza wakijua fika, eneo hilo ni mali ya serikali na walishalipwa fedha zao," amesema.

  Kwenye zoezi hilo Bi  Cecilia alisema watumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO), kutoka mkoa wa kihuduma wa Gongo la Mboto walitoa siku tatu kuanzia kesho na kwamba baada ya hapo wataanza zoezi la kuondoa miundombinu ya umeme kwenye nyumba husika ili kurahisisha zoezi la ubomoaji.

  Mwishoni mwa mwaka jana, wakati wa ziara ya Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye kwenye makao makuu ya TAA, alikutana na hoja hiyo na kuagiza Mamlaka hiyo ya Viwanja vya Ndege kuhakikisha waliolipwa fidia na bado wapo Kipunguni A wanaondoka ndani ya siku 30.

  Amesema kwa kuwa serikali tayari imekamilisha jukumu lake kwa nafasi yake, hakuna budi watu hao wakahama ili nia ya serikali kwenye eneo hilo kama ni upanuzi wa kiwanja cha ndege au shughuli nyingine itekelezwe kwa nafasi.

  Katika mazungumzo yake na watumishi wa TAA akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Richard Mayongela, Mhandisi Nditiye aliahidiwa kuwa mamlaka hiyo itahakikisha wakazi ambao tayari wamelipwa fidia katika awamu iliyohusisha nyumba 59 inatekelezwa, kama ambavyo TAA imeanza kufanya leo.
   Mhandisi Astelius John kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania akitoka kuweka alama ya kuondolewa kwa moja ya nyumba zilizolipwa fidia eneo la Kipunguni A.
   Moja ya  Nyumba zilizoanza kubomolewa na mwananchi mwenyewe katika eneo la Kipunguni A.
  Afisa ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya viwanja Vya Ndege Bi Cecilia Mwing’uri  akisaidia  zoezi la kuweka alama ya kuondoa nyumba hiyo  kati ya nyumba 59  zinazotakiwa kubomolewa.  

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times FM, Rehule Nyaulawa(aliyesimama)akizungumza leo akiwa katika Ofisi za Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kabla ya kukabidhi tuzo maalum ambayo inalenga kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao. 
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionesha tuzo maalum ambayo wamepewa na Radio Times FM.Tuzo hiyo ni kutambua mchango wa Polisi katika kulinda usalama wa wananchi wa Dar es Salaam kwa mwaka 2017
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa(aliyesimama) akizungumza leo kabla ya kupokea tuzo maalum ya kutambua mchango wao katika suala la ulinzi na usalama iliyotolewa na uongozi wa Radio Times FM wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Rehule Nyaula(aliyekaa kushoto) .
  *Asema wamedhibiti uhalifu, azungumzia Panya road 

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema iwapo kuna mhalifu yoyote na wa kutoka sehemu yoyote anaweza kuingia Dar es Salaam salama lakini ajue hatatoka salama.

  Amefafanua kutoka na kujipanga vema kulinda usalama wa raia na mali zao kwa Jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kukomesha uhalifu na hata waliokuwa wanajiita Panya Road na makundi mengine ya kihalifu sasa imebaki historia huku akifafanua jeshi hilo halipo tayari kuchezewa.

  Mambosasa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea tuzo maalumu iliyotolewa na uongozi wa Redio Times Fm na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kama sehemu ya kutambua mchango wanaoutoa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote.Tuzo hiyo ilitolewa na Mkurugenzi .

  Mtendaji wa redio hiyo Rehule Nyaula.Amesema tuzo hiyo imewatia moyo polisi Kanda Maalumu kwani imekuwa ni kawaida kusikia tu wakilaumiwa lakini Redio Times wanatambua kazi ambayo wanafanya na kuomba wengine kuiga mfano huo wa kuthamini kazi zinazofanywa na taasisi mbalimbali nchini.

  MHALIFU HATATOKA SALAMA DAR

  Akizungumzia namna ambavyo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu la Dar es Salaam limejipanga kukabiliana na uhalifu, Kamanda Mambosasa amesema wanao mfumo mzuri wa mawasiliano ambao unasaidia kukabiliana na wahalifu kwa haraka zaidi.

  Amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na makanda wa polisi Wilaya ya Temeke, Kinondoni na Ilala, maofisa wengine wa jeshi hilo kwa ngazi mbalimbali wamekuwa wakihakikisha usalama unakuwepo kwenye kila eneo na kwa sehemu kubwa wamefanikiwa.

  Ameongeza wamefanikiwa kudhibiti wahalifu na anatambua wapo ambao wanaweza kutaka kuendelea kuingia Dar es Salaam kutoka eneo lolote lile kwa lengo la kufanya uhalifu lakini watambue wahalifu wanaweza kuingia lakini hawatatoka salama kwani polisi wako imara.

  "Tumejipanga vizuri, kupitia maelekezo na maagizo ambayo tunapokea kutoka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Simon Sirro hakika yametuweza kuifanya kazi yetu katika mfumo ambao mhalifu hana nafasi ya kufanya chochote, anaweza kuingia Dar es Salaam akiwa salama lakini hana ujanja wa kutoka akiwa salama,"amesema Kamanda Mambosasa.

  AWAZUNGUMZIA PANYA ROAD

  Kuhusu makundi ya kihalifu ambayo siku za nyuma yalitikisa Jiji la Dar es Salaam likiwamo la Panya Road na lile la Kumi ndani Kumi nje ,Kamanda Mambosasa amesema wamedhibi makundi hayo na ndio manaa hivi sasa kumekuwa kimya na wananchi wako salama wao na mali zao."Dhima yetu ni kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam wanakuwa salama pamoja na mali zao.Tutaendelea kufuatilia hatua kwa hatua ili mhalifu wa aina yoyote ashughulikiwe mapema.

  "Makanda wa polisi Mkoa wa Ilala, Temeke na Kinondoni wamejipanga vema na kila mmoja anahakikisha kipande cha ardhi anachokisimamia kinakuwa salama wakati wote na ikitokea kuna mhalifu amefanya tukio na kukimbilia mkoa mwingine wa kipolisi tunao mfumo mzuri wa kukabiliana na wahalifu,"amesema Mambosasa.

  AOMBA USHIRIKIANO.

  Wakati huohuo,amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Polisi pamoja na wadau wengine wakiwamo wananchi wa Dar es Salaam."Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tumekuwa tukipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi na wadau wengine.Ushirikiano huo ni msaada mkubwa kwetu,"amesema Kamanda Mambosasa.

  AONESHA ULIKO UHALIFU

  Kamanda Mambosasa pia ametoa mwito kwa Kampuni binafsi za ulinzi kabla ya kutoa ajira kwa hao ambao wanataka kuwa nao ni vema wakatoa taarifa Polisi ili waweze kuwasaidia katika kuwapa taarifa sahihi iwapo wamewahi kuhusika kwenye matukio ya uhalifu au la.Amefafanua wamebaini kuna baadhi ya walinzi waliko kwenye kampuni binafsi za ulinzi ambao wanashirikiana na wahalifu kufanya uhalifu kwenye maeneo ambayo wafanya ulinzi.

  "Tumebaini kuna baadhi ya walinzi wa kampuni binafsi ambao wanatoa taarifa kwa wezi na kisha wanashirikiana kufanya uhalifu.Hivyo nitoe mwito kampuni za ulinzi wawe wanawasiliana na Polisi kwani tutabaini wanayetaka kumuajiri ni raia mwema au ni mhalifu.Tunaweza kuchukua alama za vidole na kubaini kama amewahi kuhusika na uhalifu au laa,"amesema Mambosasa.

  MKURUGENZI NYAULAWA AZUNGUMZA

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Redio Times, Rehule Nyaulawa amesema kuwa wameamua kutoa tuzo hiyo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutokana na kutambua mchango wao katika suala la ulinzi na usalama.Amesema kuwa kwa mwaka 2017, jeshi hilo limefanya kazi nzuri ya kulinda usalama wa raia na mali zao na kwamba wananchi wa Dar es Salaam wamekuwa wakifurahia hali hiyo na kufanya wawe huru kufanya shughuli zao kwa usalama.

  "Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wanafanya kazi kubwa ya kutufanya tuwe salama.Hivyo tumeona ni vema tukatambua mchango wao na ndio maana tumeamua kutoa tuzo hii kwa Kamanda Mambosasa kwa niaba ya polisi wengine wa kanda maalumu,"amesema.

  0 0


  0 0

  Na Baltazar Mashaka, Mwanza.

  WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.

  Pia wamezuiwa kujenga nyumba zingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.

  Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.

   Alisema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.

  “Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.

  Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.

  Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari na  gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za ovyo ovyo.

  “Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?

  Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.

  Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.

  Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe. 
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza jambo amlipozuru kwenye eneo la Kigoto lenye mgogoro kati ya wananchi na polisi. 
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akimfafanulia jambo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipozuru eneo la Kigoto Ilemela ambalo lina mgogoro baina ya wananchi na jeshi la polisi. Kushoro wa kwanza ni Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
  Waziri wa  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimuuliza Meneja majengo na Mkaguzi wa polisi, Daud Mwakalobo (kulia) kama eneo wanalotaka kujenga gati la boti na nyumba za askari polisi liko kwenye ramani. PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA


  0 0

  Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018. 
  Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.
  Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga
  Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo 
  Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo
  Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo baada ya mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi yanayofanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza, Profesa Lema pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana, wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu  wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba 
  kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani 
  pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.

  0 0

  Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea Tsh 281,500,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga. Fedha hizi ni sehemu ya Zaidi ya Tsh 17 Bilioni zilizotolewa na Serikali kwa baadhi ya Halmashauri nchini kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari!

  Ni lengo la Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dr. John Pombe Magufuli kuondoa kero katika sekta ya elimu nchini. Tumeshaanza maandalizi ya ujenzi na kukamilisha kwa wakati ufanisi wa hali ya juu katika shule hizo
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Diwani kata ya Yaeda Chini (CCM) Bryson, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu ,Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Faustine Safari kushoto, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu  Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Bw. Faustine Safari kushoto wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Wilaya ya Mbulu wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akishiriki katika ujenzi wa Msingi wa shule wakati alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga

  0 0


  IMG-20180125-WA0078
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda jana  amezindua Jengo la Upasuaji katika Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala yenye thamani ya zaidi ya Million 420, inayoenda kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

  Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE kama sehemu ya kuenzi jitihada za RC Makonda kuboresha Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.

  RC Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March 13 ,siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.

  RC Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto, lakini kupitia jengo hilo vifo vinaenda kupungua.

  Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya Upasuaji.

  RC Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua salama ndani ya jengo hilo na linaendelea kupokea kinamama Wajawazito kila kukicha. 

  Baadhi ya Kinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru RC Makonda kuwajengea jengo zuri la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya kazi yao pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji zinaenda vizuri. 

  Viongozi waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Mstahiki Meya wa Kinondoni, watendaji wa Afya na wananchi wamempongeza RC Makonda kwa jitiada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya Afya Dar es salaam.

  0 0

  Umoja wa Mataifa Tanzania wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New York Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masulu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York. 

  Wawili hao walichaguliwa kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia mitandao ya kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya dakika moja wakieleza kwanini wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la ECOSOC. 
  Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akiongea na vijana Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masul waliochaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York kabla ya kuwakabidhi bendera ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.

   Baraza hilo linakutanisha vijana viongozi kutoka ulimwenguni kwote kujiunga na waunda sera kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika nchi wanazotoka na jinsi ya kuzitatua. Pia Mkutano huo unatoa fursa kwa vijana kutoka nchi balimbali kubadilishana ujuzi wa namna ya kutatua changamoto za vijana katika nchi zao. Mkutano huo utafanyika kuanzia Jumatatu ya Januari 30 hadi 31 na unaweza kupata tarifa za safari ya Rahman na Paschal kwa kufuatilia akaunti za Umoja wa Mataifa katika Twitter @UnitedNationsTZ na Instagram @unitednationstz  Bw. Rodrguez akiwakabidhi vijana mfano wa hundi kama mchango wa Umoja wa Mataifa Tanzania ili kuwawezesha vijana hao kuhudhiria Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC). Bw. Rodrigues akiwakabidhi Rahma na Paschal bendera za Tanzania na Umoja wa Mataifa kama utambulisho wao kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC). Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha na Rahma pamoja na Paschal wakiwa wameshika bendera ya Umoja wa Mataifa Tayari kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).

  0 0


  Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kushoto akimkabidhi unga nahodha wa timu ya African Sports ambapo kiongozi huyo alitoa mchele kg100,unga wa sembe kg 100,Ngano kg 50,maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi ,sabuni na dawa za meno

  Sehemu ya vitu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

  Katibu wa Klabu ya African Sports,Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi
  Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga aliyevaa kofia kushoto akiteta jambo na viongozi wa klabu ya African Sports mara baada ya kukabidhi msaada huo
  Katibu wa Klabu ya African Sports Ismail Mosoud kulia akimshukuru Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kwa msaada waliotoa
  Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi salehe mara baada ta kukabidhi msaada huo


  MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.

  Msaada huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika ndani ya wiki mbili.Miongoni mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg 50,Unga wa sembe kg 100,Maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy ,Kilenga aliwaambia wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .Naye kwa upande wake,Katibu wa timu ya African Sports,Ismail Masoud alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.

  Alisema mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu hiyo kwani ni ya wananchi."Tanga ina enye ,na enye ni sisi,Shime wana Tanga'Tanga Kwanza.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  NA TIGANYA VINCENTRS-TABORA

  JUMLA ya shilingi milioni 20 zimetuma katika kampeni ya upandaji miti katika maeneo mbalimbali wilayani Igunga.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Revocatus Kuuli wakati wa uzinduzi wa upandaji miti kwa wanachuo wa Chuo cha Sayansi za Afya Nkinga uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

  Alisema kuwa fedha hizo zimetumika katika ununuzi wa miche ya miti, uoteshaji wa miche na zoezi zima la upandaji katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kurudisha uoto wa asili.

  Kuuli alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kutumia fedha za Halmashauri hiyo zinazotokana na vyanzo vyake wataendelea kupambana na watu wote wanaoenesha uharibifu katika mistu, vyanzo vya maji na wanachunga mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria ili kuhakikisha matunda ya fedha hizo yanaonekana.

  Akiongea katika nyakati tofauti na Wanachuo wa Ndala, Nkinga na Kitongo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa kundi hilo la wasomi ni kundi muhimu sana katika kampeni zinazoendelea Mkoani humo.

  Alisema kuwa kundi hilo haliwezi kubaki kuwa watazamaji katika zoezi la upandaji miti linapaswa kuwa sehemu ya mradi huo unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo ili nao wabakize alama kama waliwahi kukaa na kupata elimu na hatimaye kushirikia katika utunzaji mazingira.

  Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itabaki katika kumbukumbu zao binafisi na za Mkoa wa Tabora.Alisema kuwa ni jukumu la Wakufunzi kuhakikisha kila mwanachuo kama ilivyo katika Shule za Msingi na Sekondari anakuwa na mti mmoja ambao atautunza katika siku zote ambazo yuko masomoni.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Dkt. Yohana Masonda akisoma taarifa ya Chuo cha sayansi za Afya Nkinga alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa uamuzi wake wa kutumia wanachu mbalimbali kupanda miti katika maeneo yao nay ale ya jamii.

  Alisema kuwa wao katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuu ya ile ya Mkoa katika suala la uhifadhi wa mazingira tayari wameshapanda miti maji 200 na wanatarajia kuongeza mingine 600 ili kuifanya Igunga kuwa ya kijani.

  0 0


  (From left) Acting Assistant Commissioner (New & Renewable Energy) Ministry of Energy, Eng. Styden Rwebangila, the EU Head of Cooperation, Mr. Jose Correia Nunes and the EU Head of Natural Resources, Ms. Jenny Correia Nunes attending the workshop.
  Workshop participants' in a group photo. (Prepared by Robert Okanda).


  0 0

  Kufuatia mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu wilayani Kilosa  na kusababisha athari kwa nyumba 384 kubomoka, nyumba 2,216 kuingiliwa na maji, Kaya 2,542 zenye watu 9,479 kuathirika. Baraza la maafa la wilaya  hiyo limebainisha moja ya sababu kubwa ya mafuriko hayo ni uharibifu wa Mazingira.

  Akiongea mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko wilayani Kilosa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora, alibainisha kuwa baada  ya  kujionea athari hizo na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maafa wilayani humo ambayo ilibainisha sababu tano  za kutokea  mafuriko wilayani humo, sababu hizo zote zimeonekana  msingi wake  ni uharibifu wa Mazingira.

  “Nimeelezwa hapa Shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na makazi, Kilimo kando kando ya mto mkondoa zimechangia mafuriko, pia mto Mkondoa  kubadilisha uelekeo na kubomoa tuta, lakini pia kujaa mchanga katika mto na kupunguza kina cha maji pamoja na bwawa la Kidete lilokuwa likitumika kuhifadhi na kupunguza kasi ya maji ya mto mkondoa kuharibika, niwasihi wanakilosa wahifadhi mazingira kuepuka haya” Alisema Kamuzora.

  Kamuzora aliongeza kuwa Halmashauri hiyo haina budi kuzingatia sheria za maafa na mazingira  kwa kuwaelimisha wanakilosa umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Aidha aliishauri halmashauri hiyo  kuandaa mfumo wa tahadhari za awali utakao wawezesha wananchi hao kuweza kupata taarifa za awali za mvua kunyesha kutoka katika maeneo ya jirani ili waweze kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko.

  “Kama ilivyoelezwa mvua kubwa zilizonyesha kuanzia tarehe 10 hadi 14 Januari mwaka huu, katika wilaya jirani za Mpwapwa, Kongwa na Kiteto  zilipelekea kujaa maji mengi katika mito hususan mto Mkondoa na Mkundi  inayoleta maji Wilayani hapa na hatimaye mafuriko. Hivyo mkiwa na mfumo wa kutoa tahadhari za awali  ya mvua hizo zinazo nyesha wilaya hizo wananchi wa kilosa wataweza kukabili maafa ” alisisitiza Kamuzora

  Naye Mkuu wa wilaya hiyo Adamu Mgoyi alibainisha kuwa tayari suala la kuhifadhi Mazingira  wamelipa kipaumbele kwani tayari kwa mamlaka aliyonayo baada ya  Kuwatambua wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 au 100 ametoa, Amri halali Na KLS/03/208   kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa kuzuia, kuondoa na kuondoka katika eneo la hifadhi ya mto Mkondoa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kessy Mkambala alibainisha kuwa wamejipanga katika kuhifadhi mazingira kwa kufanya mapitio ya sheria ndogo zitakazosaidia kulinda mazingira ili mkakati walionao wa Kurejesha uoto kando ya mto mkondoa kwa kupanda miti au matete uweze kufanikiwa, kwa kupanda miti ndani ya mita 60 nje ya mji wa Kilosa na mita 100 ndani ya mji wa Kilosa, utekelezaji unatarijiwa kuanza  mwezi Februari 2018 mwaka huu.

  Aidha  alifafanua kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa Kuwahamisha waathirika wa mafuriko kwenye makazi mapya na salama ambapo jumla ya viwanja 1204 vimegawiwa kwa waathirika wa mafuriko ambayo ni Malui, Mambegwa na Tindiga ambapo Malui viwanja 308, Tindiga 94 na Mambegwa 802.

  Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro, yenye  Tarafa 07  kata 40 na vijiji 139. Tarafa ya Masanze , Kimamba , Kilosa na Magole ndizo zilizoathirika na mafuriko yaliyotokea tarehe 11 – 19 Januari 2018, ambapo kata 11 zimeathirika kwa viwango tofauti.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifafanua kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la maafa wilayani Kilosa, umuhimu wa kuhifadhi mazingira kama njia ya kuepuka maafa,  wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika  na  maafa ya mafuriko wilayani humo yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi  kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo  wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208   ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.
  Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa   ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa  kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. Dkt. QU DONGYU walipokutana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijijni Dar es Salaam tarehe 26 Januari, 2018 kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikino katika sekta ya kilimo na uvuvi kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na China. Mhe. Dkt. QU DONGYU yupo nchini kwa ziara ya kikazi. 
  Mazungumzo kati ya Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Dkt. QU DONGYU yakiendelea huku wajumbe wa China na Tanzania wakifuatilia. 
  Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU kwa pamoja wakipitia baadhi ya nyaraka za ushirikiano 
  Picha ya pamoja kati ya Mhe. Hamad Rashid na Dkt. QU DONGYU pamoja na wajumbe wengine walioshiriki kikao hicho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki 
  Mhe. Hamad Rashid akiagana na Dkt. QU DONGYU mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1498 | 1499 | (Page 1500) | 1501 | 1502 | .... | 1897 | newer