Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1497 | 1498 | (Page 1499) | 1500 | 1501 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Afisa Muelimishaji Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rose Mahendeka akiwaelimisha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2017/18 katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
   Msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi ya Majengo, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
  Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Valentine Baltazar akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Taratibu za Kiforodha, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)

  Na: Veronica Kazimoto
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa ofisi za Serikali na Asasi za Kiraia kwa ajili ya kuongeza ufahamu na kuwa mabalozi wa masuala yanayohusu kodi.
  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu ya kodi kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) yaliyofanyika leo ofisini hapo,  Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Edwin Rutageruka amesema TRA inastahili kupongezwa kwa kazi inayoifanya ambayo imepelekea kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
  "Ni dhahiri kwamba, sasa hivi  TRA inafanya kazi kubwa ya ukusanyaji wa mapato na kutoa elimu ya kodi kwa vikundi na taasisi mbalimbali, hivyo, fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili kuongeza uelewa wa kutosha kuhusu kodi ili tuwe  mabalozi wazuri kwa wengine", amesema Rutageruka.
  Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  Bi. Rose Mahendeka, akiwasilisha mada ya Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 amesema,  kila mwananchi anajukumu la kudai risiti kila anaponunua bidhaa na kila mfanyabiashara anatakiwa kutoa risti kila anapofanya mauzo.
  "Suala la kulipa kodi lipo kwa mujibu wa sheria hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kudai risiti wakati wote anaponunua bidhaa na vivyo hivyo kwa upande wa wafanyabiashara wanapaswa kutoa risiti kila wanapofanya mauzo", amesisitiza Mahendeka.
  Muelimishaji mwingine kutoka TRA aliyewasilisha mada kuhusu Kodi ya Majengo Bw. Chama Siriwa amewahimiza wafanyakazi hao wa TANTRADE kuwahi kulipa kodi ya majengo ya mwaka huu wa fedha 2017/18 ili kuepuka usumbufu usio wa lazima na msongamano wa watu ambao mara nyingi hujitokeza kulipa mwishoni.

  "Watu wengi wana tabia ya kusubiri tarehe za mwisho kulipia kodi ya majengo suala ambalo linasababisha msongamano usio wa lazima na hivyo kuchelewa kupata huduma kwa wakati", amefafanua Bw. Siriwa.
  Siriwa ameongeza kuwa, Kodi ya Majengo hulipwa kuanzia mwezi Julai Mosi ya mwaka wa fedha husika hadi Juni 30 ya mwaka unaofuatia na kusisitiza kuwa muda huu ni muafaka kabisa wa wananchi kuanza kulipia kodi ya majengo mpaka ifikapo tarehe 30 Juni, 2018.
  Mamlaka ya Mapato Tanzania, katika kipindi cha miezi 6 iliyopita imefanya jumla ya semina 137 kwa wafanyakazi wa Serikali, Asasi za Kiraia, wafanyabiashara na vikundi mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu na kuongeza uhiari katika ulipaji wa kodi.

  0 0

    Afisa Uhamiaji Ndg. Ali S. Nasor Mkuu wa Utawala na Fedha (DCI) Makao Makuu ya Ofisi ya Uhamiji ZanzIbar akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) viwanja vya Maisara -  Unguja.
  Wananchi waliotembelea Banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakifuatilia Vitambulisho vyao kutoka Shehia mbali mbali za Mjini Unguja, wakati zoezi la Ugawaji Vitambulisho likiendelea. 

  Mamia ya wananchi wa Tanzania Zanzibar wameendelea kufurika katika viwanja vya Maisara Zanzibar kunakofanyika Tamasha la Nne la Maonyesho ya Biashara la Zanzibar; yakiwa ni sehemuu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

  Katika maonyesho hayo pamoja na mambo Mengine Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inatoa huduma ya ugawaji Vitambulisho vya Taifa, kusajiliwa kwa wale ambao hawakuwahi kusajiliwa pamoja na kupatiwa maelezo yanayohusu huduma zinazotolewa na Mamlaka.

  Miongoni mwa Shehia ambazo Vitambulisho vinatolewa ni Mkunazini, Kiponda, Shangani,Kikwajuni juu, Kikwajuni Bondeni,Kisima Majongoo,Kiswandui, Malindi, Mchangani,Mwembe Tanga, Kilimani, Urusi, na Jang’ombe,.

  Akizungummzia huduma zinazotolewa kwenye Banda hilo Meneja wa Mifumo wa Komputa ndugu Abdallah Mmanga amesema Wananchi waliofika kwenye Banda la NIDA kusajiliwa wanatakiwa kufika na nakala ya Cheti cha kuzaliwa, Vyeti  vya shule kuanzia na  Cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi, Pasi ya kusafiria (Pasport),Kadi ya Kupigia kura, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya mfuko wa Jamii (NSSF,ZSSF,PPF,GEPF nk)

  Pindi maonyesho hayo yatakapomalizika; wananchi ambao watakosa fursa wameshauriwa kufika kwenye ofisi za NIDA zilizopo kwenye kila Wilaya kwa Unguja na Pemba; ili kusajiliwa pamoja na kuendelea kuchukua Vitambulisho vyao kwa wale ambao wamekamilisha taratibu za Usajili.

  Kwasasa Zanzibar imekamilisha Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa kwa asilimia 99 na mipango ya kuanza rasmi kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa inaendelea kupitia wadau mbalimbali ili wananchi kuanza kunufaika.


  0 0

  Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
  Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
  Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
  Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

  Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.

  Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

  Makabidhiano haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.Katika uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.

  Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.

  Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.

  0 0

  Dk. Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Nzega Vijijini alipoteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii tarehe 7 Oktoba 2017 kutoka kuwa Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, wachambuzi wengi wa mambo ya siasa na wa sekta ya maliasili waliona ametwikwa mzigo mzito katika kipindi muhimu ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imejizatiti kupambana na ufisadi na ubadhirifu. 

  Sekta ya Maliasili ina mambo mengi na changamoto zake nyingi zinajulikana. 

  Hakika Dk. Kigwangalla mwenyewe alionesha kutambua hilo alipowataka watanzania kuendelea kumuombea dua mara tu baada ya kupata taarifa za uteuzi wake kutekeleza majukumu yake mapya.Lakini katika utendaji wake miezi hii michache ya wadhifa wake huu mpya, wachambuzi hawana budi kujiuliza kama dua tu za watanzania zinatosha na kama kweli Dk. Kigwangalla ametambua nini kiini halisi cha changamoto za Sekta ya Maliasili hadi kuifanya Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa kaa la moto hadi kufikia kuongozwa na mawaziri 13 ndani ya miaka 29. 

  Labda anafahamu kuwa sekta hii ina mapato makubwa sana kutoka rasilimali za maliasili na utalii hivyo kuwa na maslahi kwa watu wengi hasa wafanyabiashara na wanasiasa na hivyo kusababisha tuhuma zisizoisha kuhusu rushwa na ufisadi. Kashfa za uuzwaji wa pori la Loliondo, kuuzwa kwa hoteli za serikali kwa bei ya kutupa, uuzwaji wa vitalu na biashara haramu ya pembe za ndovu ni baadhi tu kwenye orodha ndefu ya yanayozungumziwa vibaya juu ya sekta hii. 

   Pia labda atakumbuka kashfa kubwa iliyotokana na Operesheni Uhai lililokuwa na lengo la kutukomeza vitendo vya ujangili na pia atakumbuka Anthony Diallo, aliyeshikilia wizara hiyo hapo awali aliwahi kusema kuwa hizara hiyo “imezungukwa na watu ambao wana mambo yao wanafanya” ikiwemo watendaji kumtengenezea majungu baada ya yeye kama waziri kuwabana kwenye biashara yao ya magogo.  

  Pia hapo awali tembo wengi sana waliuawa na uwindaji haramu ulishamiri huku watendaji wakionekana kutofanya yanayohitajika ili kukabiliana na tatizo. Kwa maani hiyo, waziri yeyote aingiapo Wizara ya Maliasili na Utalii akithubutu kupambana na rushwa na ufisadi, basi ajue anatengeneza maadui wa ndani wakishirikiana na wenye maslahi binafsi huko nje ya wizara.Lakini kama kweli anayatambua haya na mengine mengi, mbona utendaji wake Dk. Kigwangalla unaonekana kama anataka kuingia kwenye mtego ambao waliomtangulia walifanya? 

  Je, waziri huyu anategemea kupita njia ile ile waliyopita wenzake na kupata matokeo tofauti? Mara tu alipoanza majukumu yake mapya, alikutana na kazi ya wanamtandao wanaolinda maslahi ya wachache kwenye sekta ya maliasili iliyosambazwa mitandao ya kijamii:"BREAKING NEWSMkakati mkali umeandaliwa na Waziri Kigwangalla, na timu yake ili kuzififisha taarifa zote za magazeti na televisheni juu ya kuwapo kwa makundi makubwa ya mifugo Loliondo.Taarifa za uhakika ni kuwa Waziri ameshauriwa afike Loliondo haraka iwezekanavyo ili apate picha za kuonyesha hakuna mifugo.

   Yote hii ni katika kusafisha hali ya hewa kutokana na agizo lake batili la kuruhusu mifugo kuivuruga Loliondo na pia Hifadhi ya Taifa Serengeti.Waziri atakuwapo huko kwa siri kubwa, akiwa na timu ya waandishi hasa wapigapicha wa televisheni. Ziara hii atatumia magari mawili hivi. Zitapigwa picha mahali kusikokuwa na mifugo na kuwaaminisha wananchi kuwa Loliondo na Serengeti hakuna mifugo.

   Atataka kuonyesha kuwa waandishi ni waongo!Usiku huu alitarajiwa kulala hoteli ya Acacia, Karatu, tayari kwa safari ya kesho Loliondo. Naambiwa tayari maandalizi yote yamekamilika hapo hotelini. Huu ndio ushauri aliopewa na washauri wake, Gambo, Nasha na wengine wa aina yao. Simameni imara kutetea uhifadhi.Usiku mwema.”Dk. Kigwangalla inambidi afikirie ‘nje ya boksi’ kama anataka kufanikiwa kuijenga Wizara hii kama dhamana aliyopewa na Mh. Rais. 

  Alipopokea uteuzi huu alikuwa ana kati ya mawili: aidha ajiunge na mtandao wa ufisadi kwenye sekta ya maliasili au apambane na rushwa. Inavyoonekana, ameamua na kuchagua kupambana na vitendo viovu. Hivyo basi, hana budi kufanya tofauti na haya ni baadhi ya mikakati ambayo anaweza kuitumia:1. 

  La kwanza, afahamu fika hawa wanamtandao wabadhirifu katika sekta ya maliasili hawataacha kupambana naye eti kisa tu anakwenda na kasi ya mheshimiwa Rais ya kupambana na ufisadi na rushwa. Mtu akiwa anakula chake, ukitaka kumpokonya atapambana na yeye akishikilie kwa nguvu zote! 

  Ndivyo wafanyavyo hawa ndugu zetu walio ndani ya wizara wakishirikiana na wafanyabiashara katika sekta hii. Hivyo basi, lazima awaoneshe hawa kuwa vita hii ni endelevu na amewatambua kuwa wao ni vikwazo. Morali yake ndiyo itashusha morali ya wasiotakia sekta hii mema maana wao watafahamu fika kuwa si tu Mheshimiwa Rais yuko nyuma yake, bali taifa nzima.2. Kuna haja ya kuonge faragha na Mheshimiwa Rais juu ya vikwazo hivi apewe rungu zaidi kusafisha hii wizara. 

  Malengo yake, ya wizara yanaendana na yake ya Rais na agenda ya serikali ya awamu ya tano. Sababu moja kwa nini kuna watendaji wenye viburi ni kwa sababu kama wengi wao husema “sisi siku zote tupo Mawaziri huja na hutuacha hapa!” Muda umefika kuonesha kuwa sasa upo uwezekano mkubwa waziri akabaki n awatendaji wakaondolewa kama si waaminifu! Mtandao wa kifisadi kamwe hauwezi kuvunjwa kwa kuwepo na uwoga kuwa watendaji hawawezi kubadilishwa.3. 

  Kama ‘mashine ya mawasiliano’ ndani ya Wizara nayo imetekwa na wanamtandao hawa na ndiyo wanashirikiana na waandishi wa habari wasio wazalendo kutendeneza mizengwe na kupika majungu ili waziri aondolewe? Basi hakuna budi waziri huyu kuhakikisha ana kuwa na mbinu mbadala za kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi hadi pale watendaji wanaomuhujumu watakapobainika na kushughulikiwa. 

  4. Waziri akaribishe maoni kutoka kwa walio chini ya utawala wa juu wa wizara ya jinsi waonavyo kinatakiwa kifanyike kurudisha siyo tu heshima ya wizara bali pia kuiweka sekta nzima ya maliasili na utalii katika hali ya kuaminika na kuwa shirikishi kama vili ilivyolengwa kwenye dira na dhima ya wizara. 

    Sambamba na haya, kuwe na mpango maalum wa kutambua kazi nzuri zinazofanywa na watendaji wa serikali ambao ni wachapakazi na waadilifu. Muda umefika sasa kurudisha utamaduni wa wale wanaofanya mema kuthaminiwa na wabadhirifu kuaddibiwa.Kuna mengi zaidi Waziri anaweza kufanya ila kwa muda huu, haya ndiyo ya msingi. Akichelewa, yatamkuta ya mawaziri waliyopita.
  Baadhi ya kurasa za mbele za magazeti zilizochapishwa juu ya Waziri Dk.Kigwangalla

  0 0

  *Yaelezwa saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza 
  *Wanafunzi wa kike kuanzia darasa la nne kupewa chanjo

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  TAASISI ya Saratani ya Ocean Road imesema imekuwa ikipokea wagonjwa wapya wa saratani 50,000 kila mwaka huku ikielezwa saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoonekana kuongeza.

  Pamoja na hali hiyo, imeelezwa jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali kwa kushirikiana na taasisi hiyo ambapo wameweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wa kike waliopo kuanzia dasara la nne nchi kote watapatiwa chanjo itayakayosaidia kuwakinga na aina hiyo ya saratani.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Chrispin Kahesa wakati wa semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

  Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa satarani, hali ilivyo kwa sasa nchini, sababu zinazosababisha ugonjwa huo na pamoja na jitihada zinazochukuliwa kupunguza kasi ya saratani nchini.

  WATANZANIA 50,000 KILA MWAKA HUPATA SARATANI

  Akizungumzia ugonjwa huo ,Dk.Kahesa amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(HWO), Tanzania kila mwaka kunakuwa na wagonjwa wapya 50,000 wa saratani na hivyo unaweza kuona ukubwa wa ugonjwa huo nchini kwetu.

  "Kila mwaka Tanzani wagonjwa wapya wa saratani ni 50,000.Ni idadi kubwa ambayo lazima tuweke mikakati ya pamoja kuhakiksha tunapunguza idadi hiyo na ukweli tunaweza.

  "Ni suala la kuamua tu kuanzia mtu mmoja mmoja, familia na Watanzania kwa ujumla kwani baadhi ya sababu zinazosababisha ugonjwa huu tunaweza kuzikwepa.

  "Baadhi ya sababu zinazosababisha saratani ni uvutaji sigara, pombe, vyakula vyenye mafuta mengi, kutofanya mazoezi ya mwili,unene na  taka sumu.Hivyo ukiangalia hizo sababu unaweza kuziepuka na ukishindwa zote basi chagua hata sababu mbili zieupuke,"amesema.

  Amefafanua zipo saratani ambayo hutokana na kirusi ambacho hubebwa na mwanaume na kisha kukiacha kwa mwanamke kupita tendo la ndoa na aina hiyo ya kirusi ndicho kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi.

  WANAFUNZI WA KIKE KUPEWA CHANJO

  Wakati huohuo Dk.Kahesa amesema ili kukabiliana na saratani hiyo, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na taasisi hiyo wameandaa mkakati utakawezesha wanafunzi wa kike kuanzia dasara la nne wote nchini wapate chanjo ya saratani ili kuwakinga.

  "Watoto wa kike ambao wapo dasara la nne tunaamini hawajaanza kujihusisha na tendo la ndoa kwani kirusi ambacho kinasababisha saratani ya shingo ya kizazi inatokana na tendo hilo,"amesema.

  WATU WAPIME SARATANI MAPEMA

  Dk. Kahesa ameeleza umuhimu wa watanzania kuwa na uratatibu wa kuangalia mapema kama wana dalili za saratani kwani hiyo itasaidia kujitambua mapema na hivyo kupata ushauri wa kitaalamu pamoja na tiba.

  Amesema changamoto kubwa wagonjwa wengi wa saratani ambao wanafika kwenye taasisi hiyo na Hospitali za Rufaa ambazo zinatoa huduma za ugonjwa wanafika wakiwa wako katika hatua za mwisho.

  "Ni muhimu kuangalia afya yako mara kwa mara kwani hii itasaidia kubaini  ugonjwa mapema.Ukiwahi kupima na ukabainika kuwa na saratani upo uwezekano wa kuishi muda mrefu tu.

  "Wapo wanaoamini saratani ni ugonjwa wa ajabu, hapana bali ni ugonjwa kama magonjwa mengine na ndio maana tupo kwa ajili ya kuwahudumia,"amesema Dk.Kahesa.

  SARATANI NI UGONJWA WA PILI KWA KUUA 

  Akizungumza kwenye semina hiyo Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dk.Mariam Kalola pamoja na kueleza mambo mbalimbali amesema pia magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiwasumbua watanzania walio wengi ni saratani, kisukari ,shinikizo la damu na moyo.

  Pia kwa sasa kuna tatizo la ugonjwa wa figo ambalo nalo limekuwa liigharimu Serikali fedha nyingi kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wa figo.

  "Magonjwa ambayo si ya kuambukiza yamekuwa yakichangia vifo vya Watanzania kwa asilimia 31 na huo ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015.Saratani inashika nafasi ya pili ukiondoa ya magonjwa ya moyo na ajali za barabarani kwa kusababisha vifo,"amesema.

  Ameeleza Februari 4 mwaka huu itakuwa siku ya magonjwa ambayo si ya kuambukiza ukiwamo ugonjwa wa saratani, hivyo akashauri vyombo vya habari vikaendelea kutoa elimu kuhusu magonjwa hayo ili kuisaidia jamii kuwa na uelewa mpana.

  Pia amesema Serikal inajitahidi kuhakikisha wagonjwa wanaostahili kupata huduma ya tiba na dawa wanaipata kwa wakati na ndio maana bajeti ya Wizara ya Afya mwaka jana imeongezeka.

  0 0

  Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mara wamelipongeza Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kutekeleza kikamilifu mradi wa “Boresha” unaotoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi mkoani humo.

  Pongezi hizo zimetolewa Januari 23,2018 na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mara, Charles Kitamuru Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya wakati akifunga mafunzo kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili ‘Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC)’.

  Mafunzo hayo ya siku mbili kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili yaliyoanza Januari 22,2018 hadi Januari 23,2018 yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwembeni na kuhudhuriwa na wakurugenzi na viongozi wa timu za afya za mikoa na wilaya.

  Mwenyekiti huyo wa wakurugenzi alisema shirika la AGPAHI limekuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya kwenye halmashauri za wilaya mkoani humo hususani katika miradi yake ya Ukimwi na kusisitiza kuwa halmashauri zote zitaendelea kuunga mkono shughuli zinazofanywa na AGPAHI.

  “Kwa niaba ya wakurugenzi wenzangu nikiwa kama mwenyekiti wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoani hapa, natoa shukrani za pekee kwa wadau wetu AGPAHI na Watu wa Marekani kupitia CDC kwa shughuli mnazofanya kufanikisha huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na Ukimwi”, alieleza Chacha.

  “Shirika hili limekuwa la mfano katika masuala ya Ukimwi na kila mtu mkoani hapa amekuwa na mtazamo chanya na AGPAHI, ndiyo maana tumekuwa tukiwashirikisha hata kwenye vikao vyetu vya mkoa ikiwemo Baraza la Ushauri la mkoa (RCC) na kuwapa nafasi ya kueleza mambo wanayofanya”,aliongeza Chacha.

  Aidha alitumia fursa hiyo kuziomba halmashauri za wilaya kutumia vizuri fedha za wafadhili shilingi bilioni 7.2 zilizotolewa na AGPAHI mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Boresha mkoani Mara huku akisisitiza uwasilishwaji wa taarifa za mradi kwa wakati.

  Naye Meneja wa Shirika la AGPAHI Kanda ya Ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele alizishukuru halmashauri za wilaya na serikali ya mkoa wa Mara kwa ushirikiano wanaotoa katika kuhakikisha kuwa malengo ya shirika hilo kutekeleza miradi ya Ukimwi yanafanikiwa.

  Kwa upande wake, Afisa Ruzuku Mwandamizi wa shirika la AGPAHI, Leticia Gilba alisema mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakurugenzi wa halmashauri na timu za afya za mkoa na wilaya kuhusu namna ya kutumia fedha za mfadhili sawa sawa na matakwa na makubaliano kati ya AGPAHI na serikali ya Marekani.

  Alisema miongoni mwa mada zilizotolewa wakati wa mafunzo hayo kuwa ni vigezo na masharti ya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Boresha, taratibu za matumizi ya fedha za wafadhili, uandaaji wa ripoti na viambatanisho sahihi vya malipo pamoja na utunzaji wa rasilimali. 

  Washiriki wa mafunzo hayo walikuwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya Mji wa Bunda na Tarime Mji, Manispaa ya Musoma, Bunda Vijijini, Butiama, Musoma Vijijini, Rorya,Tarime Vijijini na Serengeti na timu za afya za mkoa na wilaya.
  Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 9 za mkoa wa Mara, Charles Kitamuru Chacha akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kuhusu taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za wafadhili "Watu wa Marekani kupitia CDC" katika ukumbi wa Mwembeni uliopo katika manispaa ya Musoma.
  Chacha akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mambo waliyojifunza ili kuboresha utendaji kazi kwenye maeneo yao. 
  Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mara, Dk. Oning'o Felix akilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuboresha huduma katika vituo vya afya.
  Meneja wa Shirika la AGPAHI Kanda ya Ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele akizishukuru halmashauri za wilaya na uongozi wa mkoa wa Mara kwa kuendelea kushirikiana na AGPAHI kutekeleza miradi ya Ukimwi mkoani humo.
  Afisa Ruzuku Mwandamizi wa shirika la AGPAHI, Leticia Gilba akiwapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kuwa wasikivu katika mada zote zilizotolewa kwa muda wa siku mbili.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
  Mratibu wa AGPAHI mkoa wa Mara, Alio Hussein akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga mafunzo hayo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  TAASISI ya Msichana Initiative imezindua kitabu kidogo kinachozungumzia haki mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike.

  Uzinduzi wa kitabu hicho umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa tasisi hiyo Rebeca Gyumi amesema ni vema watanzania wakakitumia kitabu hicho kilichoandaliwa na timu ya mawakili kwani kimeandikwa kwa lugha rahisi zaidi kuhusu maamuzi  yote yanayotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Julai 8 mwaka 2016.

  “Mahakama Kuu, kupitia Majaji wake katika kesi hii waliona kuwa vifungu hivi haviendani na Katiba ya nchi.Pia vinabagua haki za watoto wa kike ukilinganisha na haki za watoto wa kiume.

  "Vifungu hivyo vinaruhusu mtoto wa kiume kuoa katika umri wa miaka 18 na mtoto wa kike kuoelewa katika umri wa miaka 14 na 15 kwa ruhusa ya Mahakama na wazazi,"amesema Gyumi.

  Amesema vifungu hivyo vinachochea kwa kiasi kikubwa suala la ndoa za utotoni hasa kwa watoto wa kike na kutaja Tanzania ni moja ya nchi yenye asilimia kubwa ya tatizo la ndoa za utotoni ikilinganishwa na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki ukiacha Uganda.

  Ameongeza wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na wasichana hao hukumbwa na changamoto nyingi wanapoingia katika ndoa.

  "Wanaolewa wakiwa na mri mdogo wanapopata mimba wakati wa kujifungua wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa sababu via vyao vya uzazi bado ni vichanga.Pia huwanyima haki yao ya kupata elimu,"amesema.

  Gymi amesema kupitia kitabu hiki chenye maamuzi ya Mahakama Kuu, jamii itaelewa na kutambua zaidi namna ambavyo vifungu hivyo kandamizi kwa watoto wa kike na kuona haki ambazo zimetambuliwa kisheria kupitia hukumu hiyo,  pia madhara ya ndoa za utotoni .

  Amefafanua Msichana Initiative pamoja na wadau wengine wanaamini suala la ndoa za utotoni litakoma endapo jamii itakuwa tayari kuwashika mkono watoto wa kike kwa kuwalinda na kutetea haki zao msingi.


  Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya pamoja wageni waalikwa wakiwa wameshika kitabu kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali ya haki za watoto.

  Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali y watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
  Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Tamwa, Valerie Msoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika Protea Jijini Dar es Salaam.
  Mwanasheria aliyoongoza jopo la Mawakili kupinga sheria ya ndoa za Utotoni katika Mahakama kuu ya Tanzania.
  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Msichana Initiative,Benedict Kikove akitoa neno la shukrani kwa wadau waliofika katika uzinduzi wa kijitabu cha sheria ya kupinga ndoa za utotoni.
  Baadhi ya wadau waliofika kushuhudia uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
  Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.

  0 0


  ·         Merged entity to have largest customer base of 5.9 million subscribers
  ·         Merger to result in the only negative ebitda OpCo joining other 13 positive ebitda OpCos in Africa
  ·         Merged entity to have Rwanda’s largest sales and distribution network
  Bharti Airtel Limited (“Airtel”) a leading global telecommunications services provider with operations in 16 countries across Asia and Africa, today announced that it has received an approval for the acquisition of Tigo Rwanda Limited (“Tigo Rwanda”), a subsidiary of Millicom International Cellular S.A. ("Millicom") from the Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA).
  The merged entity will have the largest customer base in Rwanda with 5.9 million subscribers. The combined networks of the two companies will serve customers with voice/ data services, global roaming and mobile banking services. It will also have Rwanda’s largest sales and distribution network.
  The merger will result in the only negative ebitda OpCo joining other 13 positive ebitda OpCos in Africa.
  On completion, the acquisition will undergo seamless integration, both on the customer as well as the network side and further strengthen Airtel’s market position in Rwanda. 
  Airtel thanked the Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA) for their support during the merger process.

  With a presence in 14 countries across Africa, Airtel is one of the largest telecom service providers on the continent in terms of geographical reach, and had close to 84 million customers at the end of quarter ended December 30, 2017. Globally, Airtel is ranked as the third largest mobile services provider in terms of customer base.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizunguma na Mtukufu Dk. Sheikh Sultan Bin Mohammed Al Qasimi alipofika katika makaazi yake kwa mazungumzo akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.

  ZANZIBAR na Sharjah zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wao uliopo katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo zikiwemo elimu na biashara,  

  Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makaazi ya Mtukufu Dk. Sheikh Sultan Mohammed Al Qasimi mjini Sharja, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kiongozi huyo wote kwa pamoja walisisitiza haja ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kwa lengo la kuimarisha sekta hizo muhimu za maendeleo.

  Rais Dk. Shein kwa upande wake alimpongeza Dk. Sultan kwa hatua zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji.
  Pamoja na hayo, viongozi hao walizungumza jinsi ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kuimarisha sekta ya elimu hasa ikizingatiwa kuwa Sharjah imeweza  kupata mafanikio katika sekta hiyo kutokana na kuwa na miundombinu mizuri ya elimu vikiwemo vyo vikuu.

  Aidha, Dk. Shein alieleza haja kwa Sharjah kutoa ushirikiano wake kwa Zanzibar katika sekta ya elimu kupitia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), jambo ambalo Dk. Sheikh Sultan Mohammed Al Qasimi ameliunga mkono.

  Pia, viongozi hao kwa pamoja, wameeleza namna ya pande mbili hizo kushirikiana katika sekta ya biashara hasa ikizingatiwa kuwa kuna bidhaa ambazo ziko Zanzibar na zinatumika sana nchini Sharjah vikiwemo viungo ambapo nchi hiyo wamekuwa wakinunua kutoka nchi za mbali ikilinganishwa na masafa kati ya Zanzibar na Sharjah.

  Dk. Shein, pia alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Sultan hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii zikiwemo uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar ambapo tayari serikali imejenga ukuta wa kuzuia athari za maji ya bahari katika eneo la Mizingani kuelekea katika bustani ya Forodhani.

  Kwa upande wake Dk. Sheikh Sultan nae alimueleza namna Sharjah ilivyokuwa na uhusiano na ushirikiano na Zanzibar kwa muda mrefu jambo ambalo amehakikisha ataliendeleza na kuliimarisha kwa lengo na manufaa ya pande zote mbili.

  Pia, Dk. Sheikh Sultan alimuleza Rais Dk. Shein namna Sharjah ilivyopiga hatua katika sekta ya elimu sambamba na inavyotoa fursa za ufadhili wa masomo na kusisitiza kuwa kuna kila  sababu na Zanzibar nayo ikafaidika na fursa hizo.

  Aidha, Dk. Sultan alimueleza Dk. Shein fursa mbali mbali za kibiashara zilizopo Sharjah na kusisitiza haja ya kuwepo mashirikiano kati ya pande mbili hizo ili sekta hiyo ilete manufaa kwa pande zote mbili hizo.

  Katika kuendeleza na kukuza sekta ya biashara na utalii kati nchi mbili hizo, Dk. Sultan alimueleza Rais Dk. Shein umuhimu wa kuwepo usafiri wa ndege wa moja kwa moja kati ya Zanzibar na Sharja na kusisitiza kupitia Shirika la ndege la Sharjah hilo atahakikisha analiweka katika vipaumbele vyake katika kukuza uhusiano na ushirikiano uliopo.

  Katika ziara yake mjini Sharja Dk. Shein alipata fursa ya kutembelea eneo la shughuli za uvuvi la ‘East Fishing Processing LLC”, lililoko Al Jurf  katika eneo la Ajman  na kupata maelezo juu ya namna ya eneo hilo lenye kiwanda kikubwa cha kisasa cha samaki jinsi kinavyosarifu  na kuhifadhi samaki pamoja na kuwaweka katika mfumo maalum wa kwa ajili ya kuuzwa.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo inayolishirikisha kundi la Kampuni ya THOMSUN, K.V. Thomas alimueleza Rais Dk. Shein namna na kiwanda hicho kinavyosarifu samaki wa aina mbali mnali wakiwemo kamba kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.

  Dk. Shein kwa upande wake alipendezewa na namna kiwandaa hicho kinavyofanya kazi na kutokana na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya uvuvi na viwanda vya samaki pamoja na azma ya kuanzisha Kampuni ya Uvuvi, 

  Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja ili Zanzibar ipate kupanua wigo katika sekta hiyo.

  Kutokana na kiwanda hicho kutumia teknolojia ya kisasa katika kusarifu samaki wa aina mbali mbali pia, soko la ajira limeonekana kuchukua fursa yake kutokana na kuajiri vijana wengine hatua ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika kupambana na changamoto iliyopo katika suala zima la ajira.

  Wakati huo huo, Dk. Shein na ujumbe wake akiwemo Mama Mwanamwema Shein walitembelea katika  shamba la ngombe wa maziwa la Al Rawabi, ambapo pia eneo hilo lina viwanda vya vinywaji vya matunda pamoja na bidhaa nyengine zinazotokana na maziwa.  

  Akiwa katika eneo hilo la Al Rawabi, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa uongozi wake ambapo Mkuu wa Kampuni inayosimamia Shamba hilo Abdalla Eleweis alimkaribisha Dk. Shein na ujumbe wake na kumueleza namna eneo hilo linavyofanya shughuli zake za ufugaji wa ngombe pamoja na uendelezaji wa viwanda vya matunda.

  Nae Meneja Mkuu wa Shamba hilo Dk. Ahmed Eltigani Al Mansour alimueleza Rais Dk. Shein na ujumbe wake jinsi ya shamba hilo linavyofuga ngombe kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwemo kuwawekea viyoyozi na mafeni maalum kutokana na mazingira ya hali ya hewa ya ukanda huo.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Ahmed shamba hilo lina ngombe 12,500 ambapo kwa kila ngombe mmoja kwa siku hutoa lita 60 za maziwa na kutoa lita 250,000 kwa siku huku akitumia fursa hiyo kueleza siri ya mafanikio hayo ikiwa ni pamoja na utafiti mkubwa walioufanya kabla ya kuazisha ufugaji huo.

  Dk. Ahmeda alieleza kuwa ufugaji wanaoufanya ni ufugaji bora duniani na pia ni eneo lililopata mafanikio makubwa ikifananishwa na ufugaji unaofanyika katika maeneo mbali mbali zikiwemo nchi za Afrika na hata nchi zilizoendelea ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa wingi.

  Akimaliza ziara yake katika eneo hilo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi wa Al Rawabi kuwa Zanzibar itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo katika sekta hiyo ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kupanua wigo na kujifunza jinsi ya mafanikio hayo yalivyopatikana.

   Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

  0 0

  Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo MCB Salary Advance, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla. 

  Akizungumzia Kuhusu bidhaa hii mpya ya mkopo wa ‘MCB Salary Advance’, Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko, Bwana Valence Luteganya alisema, mteja ataweza kuchukua mkopo huu pale anapouhitaji, Nia ni kuwezesha mteja wetu kuyakabili mahitaji ya dharura yanayojitokeza wakati wowote. 

  Alisema, bidhaa ya salary advance inayowalenga wateja wafanyakazi wanaopitishia mishahara yao katika Benki ya Mwalimu, “Mkopo huu unariba nafuu na unapatikana kwa urahisi na haraka, Lengo ni kutoa mkopo wa bei nafuu utakao wasaidia wateja wetu kupunguza ukali wa Maisha”. 

  Aliongeza “Kupitia huduma ya Salary advance mfanyakazi anayepitisha mshahara MCB, ataweza kupata hadi asilimia 50 ya mshahara wake kwa riba nafuu. Kupata huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi la benki au kutuma meseji kupitia whatsapp kwa kuandika neno ‘mshahara wangu’ kwenda namba 0629331755. 

  Akiendelea Ndg Luteganya alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imekuja na mikakati ya kutoa bidhaa nzuri zinazokidhi matakwa ya watanzania ili kuisaidia jamii kupunguza na/ama kuondokana na shida ambazo zinaweza kutatuliwa kwa urahisi. 

  Naye Mkuu wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Ndg. John Mhina aliongeza kwa kusema “Huu ni mwendelezo wa mchakato maalum kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya wateja wetu mwaka 2018, na ni ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa njia ya Mitandao wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa. 
  Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa njia ya Mitandao, John Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa. 
  Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tukio la uzinduzi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura jana katika ukumbi wa tawi la benki hiyo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiongoza shughuli ya kuteketeza nyavu haramu zenye thamani ya zaidi shilling milioni 100,a zilizo salimishwa na zilizokamatwa katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera jana.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi  wanaoishi katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera, juu ya kutumia zana  sahihi za uvuvi na kuacha kutumia zana haramu.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye boti huku akiwa ameambatana na viongozi wa kikosi maalum cha kupambana na uvuvi haramu wakiwasiri katika kisiwa cha Kerebe mkoa wa Kagera kwa usafiri wa boti.Picha na Emmanuel Massaka.


  0 0

  Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga alisema kuwa wanayo furaha kubwa ya kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana tarehe 21 Januari 2018, jumapili iliyopita kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.

  Maganga aliwataja washindi hao kuwa ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27,Mshindi mwingine alikuwa ni Britony Mtalemwa ambaye ametokea Songea,ambaye alijishindia milioni 40.

  "Washiriki wa wiki hii walichukua jumla ya milioni 134 kwa pamoja. Washindi wengine wa wiki hii walikuwa ni Gibson Erasmas kutoka Mwanza aliyeondoka na milioni 40 na Andrew Kagoma kutoka Arusha aliyejinyakulia milioni 27'alisema Maganga..

  Amesema Tatu Mzuka inawawezesha Watanzania wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali na mikoa tofauti kuliko mchezo mwingine wowote. Kama Tatu Mzuka, amini kwamba tunatafuta njia zaidi kukupa fursa ya kuwa milionea kwa kiwango cha chini kabisa cha shilingi 500.Kila saa ndani ya siku, Tatu Mzuka inakupa fursa ya kushinda hadi milioni 6.Kila siku, siku sita za wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi tuna droo ya milioni 10 inayoitwa ‘Mzuka Deile’.

  "Na Jumapili ya wiki hii, tuna milioni 60 ambayo inatafutiwa mshindi,Nafasi hizi zote zinapatikana kwako kwa kiasi cha shilingi 500 tu''alimaliza kusema Maganga.  Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani,mapema jana jijini Dar wakati wa kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana mwishoni mwa wiki Jumapili Januari 21 2018, kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.Pichani kulia ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27. na kushoto ni Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.
  Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Ndugu Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.
  Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundiMzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed, akiendelea na ziara yake katika Nchini za Umoja wa Falme za Nchi Kiarabu UAE, akitembelea Kiwanda cha Samaki Sharjah East Fishing Prosessing, kujionea utaalamu wa kuhifadhi samaki na kusafirishwa nje 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo K.V.Thomas jinsi ya kuhifadhi samaki na ufanyaji wa peki kwa ajili ya kusafirisha
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya utayarishaji wa Kambo hadi kupekiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya Nchi na katika Soko la ndani akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya picha katika gazeti la kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas , akiwa katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya picha katika gazeti la kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas , akiwa katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya picha katika gazeti la kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas , akiwa katika ziara ya Kiserikali katika Nchi za Umoja wa Nchi za Kiarabu UAE 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas, bada ya kumaliza ziara yake kutembelea kiwanda hicho
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa mfano Jahazi na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sharjah East Fishing Processing K.V.Thomas, baada ya kumaliza ziara yake kutembelea kiwanda hicho.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa),Allan Kijazi akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira iliyofanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Millanzi akizungumza kwenye kikao na kamati hiyo,kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kemilembe Lwota akifatilia kwa makini. 
  Mbunge wa jimbo la Sumve mkoa wa Mwanza,Richard Ndassa(kushoto),Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga(katikati) na Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakiwa ndani ya Hifadhi hiyo. 
  Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa,Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani. 
  Mbunge wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani. 
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kemilembe Lwota akitembea juu ya daraja hilo. 
  Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete naye hakua nyuma kutembea juu ya daraja hilo ambalo limeongeza shughuli za utalii kwenye hifadhi hiyo. 
  Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira wakiwa juu ya daraja maalumu lililojengwa kuwawezesha watalii kuwaona wanyama aina ya Viboko na aina mbalimbali za ndege. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga akifurahia mandhari ya daraja linalomwezesha mtalii kuona vizuri eneo la Ziwa Manyara. 


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa),Allan Kijazi akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira iliyofanya ziara ya kikazi kwenye Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Millanzi akizungumza kwenye kikao na kamati hiyo,kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kemilembe Lwota akifatilia kwa makini. 
  Mbunge wa jimbo la Sumve mkoa wa Mwanza,Richard Ndassa(kushoto),Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga(katikati) na Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakiwa ndani ya Hifadhi hiyo. 
  Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa,Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani. 
  Mbunge wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani. 
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kemilembe Lwota akitembea juu ya daraja hilo. 
  Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete naye hakua nyuma kutembea juu ya daraja hilo ambalo limeongeza shughuli za utalii kwenye hifadhi hiyo. 
  Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira wakiwa juu ya daraja maalumu lililojengwa kuwawezesha watalii kuwaona wanyama aina ya Viboko na aina mbalimbali za ndege. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga akifurahia mandhari ya daraja linalomwezesha mtalii kuona vizuri eneo la Ziwa Manyara. 


  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Chisichili Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme.
  Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (aliyesimama), akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (wa pili kutoka kulia), kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
  Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) akibadilishana mawazo na wananchi wa Mtaa wa Chisichili, Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme. Kulia kwake ni Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde.
  Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
  Wananchi wakiuliza maswali na kutoa maoni mbele ya Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.  Na Veronica Simba – Dodoma

  Serikali imebainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 499 zimeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme nchini kote katika mwaka huu wa fedha unaoendelea.

  Hayo yalisemwa jana, Januari 24 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa katika ziara katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini kwa ajili ya kujionea hali ya upatikanaji wa nishati hiyo muhimu pamoja na kuzungumza na wananchi.

  Naibu Waziri Mgalu, ambaye aliambatana na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde aliwaambia wananchi wa maeneo aliyotembelea kuwa, kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na kitawezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme katika vijiji vyote 7873 vilivyosalia nchi nzima.

  “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli pamoja na Bunge la Jamhuri kutuidhinishia kiasi hicho cha fedha. Kazi yetu sisi wasaidizi wake katika Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunatekeleza jukumu alilotutuma la kuwapelekea wananchi kote nchini nishati ya umeme wa uhakika. Tunaahidi hilo litafanyika kwa ukamilifu.”

  Akizungumzia umuhimu wa nishati ya umeme, Naibu Waziri alisema kuwa, sekta zote zinategemea umeme ili zifanye kazi kwa ubora. Alitoa mfano wa sekta ya afya ambayo pasipo umeme wa uhakika haiwezi kutoa huduma bora. “Vivyo hivyo kwa sekta ya elimu, kilimo, viwanda na nyinginezo,” alisisitiza.

  Aidha, Naibu Waziri Mgalu alitoa maagizo kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha Wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo wanatoa kipaumbele kwa taasisi za kijamii kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za ibada, miradi ya maji na nyinginezo. Hata hivyo alisema Wakandarasi lazima wahakikishe hakuna mtu au eneo linalorukwa wakati wa kutekeleza mradi huo.

  Vilevile aliwataka wananchi kufanya maandalizi ya kuunganishiwa umeme katika makazi yao na katika miradi na taasisi mbalimbali. “Tunataka zoezi la kupitisha umeme katika maeneo yenu likikamilika tu nanyi bila kuchelewa mnaunganishiwa katika nyumba zenu, hivyo anzeni kufanya maandalizi sasa.”

  Awali, akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, alisema kuwa wananchi wa Dodoma ni wakulima wazuri wa zabibu na mazao mengine mbalimbali, hivyo wanahitaji huduma ya umeme wa uhakika ili kuboresha kazi zao za kilimo kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani.

  Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu alisema zoezi la kufanya tathmini ya awali kwa ajili ya kutekeleza Mradi huo katika maeneo yaliyosalia litaanza mapema mwezi Februari mwaka huu.

  Ziara ya Naibu Waziri Mgalu ilihusisha Kata za Mpunguzi, Matumbulu, Mkonze, Nala na Ipagala zilizopo Dodoma Mjini.

  0 0

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Omar Kinana amfikishie Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kifo cha Mtumishi wake Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla aliyefariki leo Januari 25,2018.

  Bi. Nakia amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

  Katika Salamu zake Dk. Mabodi amesema CCM Zanzibar imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo kwa Mshutuko, Majonzi na Simanzi kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii na ubunifu wa hali ya juu katika utumishi wake.

  Pamoja na hayo alitoa pole kwa familia Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM, Marafiki pamoja na Jamaa wa karibu walioguswa na msiba huo, na kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huo.

  “ Marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa enzi za uhai wake hasa kwa kujitolea na kukipigania Chama cha Mapinduzi muda wote wa uhai wake, hivyo tumepoteza mtu muhimu sana ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.

  Pia nawaomba watumishi na wanachama na Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huo, na tuendelee kumuombea dua mwenzetu ili Mwenyezi Mungu amuweke pahala pema peponi Amin.”, alieleza Dk. Mabodi.

  Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla amefariki leo Tarehe 25/1/2018 Nyumbani kwake Mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, amezaliwa Januari 6,1965 katika Kijiji cha Ndagaa Wilaya ya Kati Unguja.

  Alipata elimu yake ya Sekondari ya Kidato cha Tatu katika Shule ya Ben-Bella Mjini Zanzibar.Enzi za uhai wake Marehemu Bi. Nakia amehudumu katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwa nafasi mbali mbali zikiwemo Ukarani wa Simu (Telephone Operator), Ulinzi pamoja na nyinginezo.

  Marehemu ameolewa na ameacha Mume na Watoto Wawili. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.

  Imetolewa na:-

  “KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI’’
  Mohamed Sijaamini Mohamed
  Kny: Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.

  ZANZIBAR.
  25 Januari, 2018.

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Dkt Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame (kushoto kwa Rais),  katika mazungumzo yaliyohudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Dkt. Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Dkt. Donald Kaberula, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame  na ujumbe wake pamoja na  na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Dkt. Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, huku Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akishuhudia baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika na kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 25, 2018.

  PICHA NA IKULU

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Moja ya jengo la Makazi ya Askari Magereza likionekana hatua iliyofikia. Nyumba hizo zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, zinajengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA-B) na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B).  Kushoto (meza kuu) ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe, anaefuata ni Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba hizo, Mhandisi Khadija Salum, na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo, Peter Kikwati. Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Cosmas Mtambala. Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B), pamoja na wasimamizi wa mradi huo ambao ni Maafisa wa Jeshi la Magereza.  Kushoto (meza kuu) ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe. Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akimsalimia Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakala wa Majengo nchini (TBA-B), Manasseh Slekelaghe (Kushoto), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari Magereza, zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Katibu Mkuu Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) Khamis Mwinyi Mohammed (aliesimama) akitoa maelezo juu ya mchakato na ufanikishaji wa Madhimisho ya Mei mosi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba.
  Afisa kutoka Wizara ya Kazi Zanzibar Amin Ali Amin akichangia kitu katika Mkutano huo uliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba.

  Katibu Tawala Mkoa Kaskazini Pemba Ahmed Khalid Abdalla akiwakaribisha wageni katika Mkutano wa kujadili madhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yanayotarajiwa kufanyika katika Mkoa huo.
  Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akifungua Mkutano wa kujadili madhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yanayotarajiwa kufanyika katika Mkoa wake.
  Picha na Makame Mshenga Pemba.

older | 1 | .... | 1497 | 1498 | (Page 1499) | 1500 | 1501 | .... | 1897 | newer