Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1489 | 1490 | (Page 1491) | 1492 | 1493 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka  Watanzania kuchana na  vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa lengo la kujiepusha  na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mama Samia amesema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya ujenzi wa kuta za kingo katika Bahari ya Hindi eneo la Ocean Road na Kigamboni.

  Amesema kuwa Tanzania imeharibu mazingira yake kwa kiasi kikubwa hali inayofanya sehemu kubwa ya maeneo yote kuwa na hali tofauti na tulivyotegemea.Ametoa mfano Mji wa Dodoma ambao watu wamekata miti yote na hivyo kusababisha eneo hilo kuwa jangwa kiasi cha kusababisha maafa pindi mvua zinaponyesha.

  Ametaja kuwa  mikoa mingi ambayo iliyokuwa na baridi sasa hivi imekuwa ikiongoza kwa joto sawasawa na mikoa iliyopo Pwani kwa mfano mikoa ya Kilimanjaro kila ukiangalia utabiri wa hali ya hewa unaambiwa ina nyuzi joto 32 hadi 33, kiasi ambacho awali haikuwahi kufikia hapo. Amesema adhabu yote hiyo na  athari zinazoonekana sasa inatokana na uharibifu huo mkubwa wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wanachi kwenye maeneo mbalimbali nchini .

  “Napenda kutumia mfano anaotumia Papa Francis kuwa ukimkosea mwanadamu utakwenda kulia kanisani au Msikitini utasamehewa lakini ukiyakosea mazingira hayana Msikiti wala Kanisa yatakuadhibu mpaka utakaporudi kuwa rafiki tena,"amesema Makamu wa Rais .

  Ameongeza kuwa "Nasi tumeharibu mazingira kwa kukata miti, kuchimba mchanga katika fukwe na matokeo yake bahari imepata nguvu ya kula ardhi yetu,hivyo turekebishe tulipoharibu ili kurudisha urafiki huu".Amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakazi wake wamekuwa wakitupa taka katika mitaro na ikiziba inaleta madhara ya mafuriko, hivyo hiyo ni hasara kwa Taifa kwa kuwa tunatumia muda mwingi kutoa pole na anayepewa pole hutegemea uende na chochote umsaidie kama mahindi na fedha. 

  Amefafanua baada ya kutembelea miradi mbalimbali keshokutwa atakutana na wadau wa mazingira wa Dar es Salaam kupanga mikakati ya kuokoa mazingira.Kwa upande wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba amesema pamoja na kuwa Tanzania haichangii kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira lakini ni wahanga wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

  “Athari hizi zinaathiri moja kwa moja uchumi wa nchi kutokana na kuathirika kwa kilimo, utalii na uvuvi, hivyo tunaendelea na miradi mbalimbali ya kukabiliana na hali hiyo ikiwamo ujenzi wa kingo za bahari maeneo mbalimbali,” amesema.Wakati huohuo  Mtaalamu wa miradi kutoka wizara hiyo,Fred Manyika amesema miradi hiyo inayofadhiliwa na mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi(Adoptation Fund) inagharimu dola za Marekani Milioni 5.8.

  “Fedha hizi zimefanya ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari katika eneo la kigamboni na ule wa jirani na Ocean Road jijini hapa,” amesema Manyika.Ameongeza kuwa miradi mingine inajengwa katika Manispaa za Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam inayogharimu dola za Marekani 900,000.

  “Miradi hii inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya kuzuia bahari kubomoa ardhi, kupanda mikoko na kurudishia matumbawe chini ya bahari na kutoa elimu kwa wananchi,” alisema Manyika.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema pamoja na kuwa Serikali Kuu inamipango yake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi mkoa huo pia unapanda Mikoko iliyoharibiwa.

  “Tunapanda mikoko eneo la Mbweni katika Manispaa ya Kinondoni ambapo ekari tano tayari zimepandwa na Tundwi Songani ekari 40,” amesma Makonda.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Mradi na Miundo Mbinu wa UNOPS Bw. Bernard Odhuno wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameketi kwenye moja ya sehemu za kupumzikia pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Ocean Road. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Ujenzi wa Ukuta wa bahari katika eneo la umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwa na Kiongozi wa Operesheni ya maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa Ziwa Victoria, Shafii Ramadhani Kiteri wakikagua shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu zenye thamani ya shilingi milioni mia tano inayomilikiwa na Meshaki Chacha jijini Mwanza leo. Nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na mmliki akitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni hamsini ndani ya masaa 24.

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani na kofia )akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati (kushoto) wakiwa kwenye boti ya doria kutoka katika kijiji Kakukuru wakielekea kwenye kambi ya uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila ambapo Mhe.Waziri alifanya mkutano na wavuvi . Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a. (Na John Mapepele)
  Mmliki wa ghala lenye shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa kisheria zenye thamani ya shilingi milioni mia tano, Meshaki Chacha akihojiwa na Mwandishi wa Habari wa ITV baada kikosi kazi kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) kuvamia ghala lake lililopo jijini Mwanza leo. Ametakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 ndani ya masaa 24 leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani)akikagua nyavu haramu za kuvulia samaki katika kijiji cha Kakukuru wilayani Ukerewe ambapo alichoma moto nyavu haramu za zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. Kulia ni Lameki Mongo, Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kushoto ni Abbakary Murshidi, Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Ukerewe (Na John Mapepele) Aapa kutokomeza uvuvi haramu nchini
  Asema imebaki 3% tu ya Sangara wanaokubalika kuvuliwa katika ziwa Victoria

  Na John Mapepele

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Joelson Mpina amekamata marobota 1152 ya aina mbalimbali za nyavu haramu zisizoruhusiwa kisheria kutumika kuvulia samaki zenye thamani ya shilingi milioni 894 jijini Mwanza na Singida ambapo baadhi ya nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na wamiliki wakitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 120 ndani ya masaa 24 kwa makosa ya kufanya biashara ya nyavu hizo kinyume cha sheria.

  Akiongea na Vyombo vya Habari jijini Mwanza katika ghala la nyavu la Meshack Chacha mara baada ya kukamata shehena ya marobota 600 ya nyavu haramu kwenye ghala lake, Mhe. Mpina alisema nyavu haramu 294 kati ya 894 zilikamatwa na kikosi kazi maalum cha kudhibiti uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni wakati mmoja wa wafanyabiashara hao Masagati Majani alijaribu kutorosha vyavu hizo kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.452 BBS kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

  Gari hilo lipo katika kituo cha polisi cha Singida kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo kulingana na sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii)

  Aliwataja wamiliki wengine ambao walikamatwa kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya uagizaji na uuzaji wa vyavu zisizoruhusiwa kisheria kuwa ni Josia Jonam Obielo, Jeremiah Asam na Dastun Venant ambapo alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wote wanao agiza na kuuza zana haramu za uvuvi wanakamatwa na sheria kali zinachukuliwa ili kudhibiti uvuvi haramu nchini.

  “Niliapa kusimamia ulinzi wa raslimali za uvuvi nchini hivyo nitahakikisha operesheni hii inakuwa ya kudumu katika kupambana na uvuvi haramu hadi uvuvi haramu utakapokwisha” alisisitiza Mpina

  Katika hatua nyingine Waziri Mpina amelaani kitendo Kiwanda cha Sunflag cha mkoani Arusha kwa kuendelea kufadhili uvuvi haramu nchini kutengeneza na kuuza vyavu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa kisheria wakati Serikali imekuwa ikisisitiza viwanda vyote nchini kuacha tabia ya kufadhili uvuvi haramu kwa kutengeneza zana haramu za uvuvi.

  Waziri Mpina ameagiza watalam kwenda mara moja katika kiwanda hicho kuchunguza ukweli wa jambo hilo ili sheria zichukue mkondo wake.Hivi karibuni Waziri Mpina aliunda Kikosi maalum cha kupambana na uvuvi haramu ambapo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne zaidi ya zana haramu za uvuvi ikiwa ni pamoja na nyavu zenye jumla ya bilioni tatu zimeteketezwa katika kanda ya ziwa Victoria peke yake huku viwanda vitano vya kusindika samaki vilivyopo jijini Mwanza vikitakiwa kulipa jumla ya shilingi milioni 180 ndani ya masaa 24.

  Viwanda hivyo vilitozwa faini hiyo kutokana na kuendelea kuwa wafadhili wakuu wa uvuvi haramu kwa kununua na kuchakata samaki aina Sangara wachanga na wazazi kinyume cha Sheria ya Uvuvi.

  Waziri Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama kwa mlaji na kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.

  Waziri Mpina alisema samaki aina ya Sangara kwenye Ziwa Victoria wapo katika hatari ya kutoweka kabisa katika kipindi cha miaka miwili endapo hali ya uvuvi haramu ukiachwa uendelee bila kuchukua hatua za haraka na madhubuti kudhibiti janga hili.

  Alisema kulingana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017 unaonesha kuwa samaki wachanga waliochini ya sentimita 50 wasioruhusiwa kuvuliwa ni asilimia 96.6 , samaki wazazi walio zaidi ya sentimita 85 ambao pia hawarusiwi kuvuliwa ni asilimia 0.4 na samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu hivyo juhudi za pamoja za wadau wote wa sekta ya uvuvi zinahitajika ili kurejesha raslimali ya uvuvi katika Ziwa Victoria kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

  0 0

  ​Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

  Mkurugenzi wa Idara Habari( MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya Serikali kuhamia Dodoma.

  Akiwa katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Abbasi amevitaka vyombo vya habari vya Dodoma kuwa tayari na ujio wa Serikali kuhamia Dodona kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani humo.

  "Kwa baadhi ya matukio yaliyofanyika hapa Dodoma nimeona uzubaifu kwa baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahabari wenzangu tuchangamke kwani matukio mengi ya Serikali yatafanyika hapa" amefafanua Dkt. Abbasi.Aidha, Dkt. Abbasi ameutaka uongozi wa TSN kufuata maadili katika utendaji kazi kwani wananchi hutazama kampuni hiyo kwa jicho la utofauti kama chombo cha Serikali.

  “Mkiwa kama Kampuni ya Magazeti ya Serikali mnatakiwa kuibeba agenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda" ameongeza Dkt.Abbasi.

  Akiwa katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd mkoani humo, Dkt Abbasi amesema kuwa asilimia 99 ya waandishi wamejikita katika masuala ya kisiasa kuliko masuala ya maendeleo ya nchi au bajeti mbalimbali zinazohusu serikali hivyo ameshauri vyombo vya habari kujikita katika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya jamii.

  Aidha, Dkt. Abbasi amesisitiza umuhimu wa wanataaluma ya habari kujiendeleza kitaaluma ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, mwandishi wa habari atatakiwa kuwa na  atashahada ya taaluma ya uandishi wa habari.

  Akizungumzia kuhusu upatkanaji wa habari, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imewekeka mfumo wa kisheria kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara na Taasisi zake.

  Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesisitiza waandishi wa habari kujisajili ili wapatiwe vitambulisho (Press Card) kwani kuanzia mwezi Machi mwaka huu katika matukio yote ya viongozi wakuu wa Kitaifa,  kila mwanahabari atatakiwa kuwa na kitambulisho hicho.
    Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaeleza watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) umuhimu wa kubeba  ajenda ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda wakati wa ziara yakutembelea vyombo vya habari Mkoani Dodoma  iliyoanza mapema leo.
   Muwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali Mkoani Dodoma Bw.Felix Mushi akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika Ofisi za Kampuni hiyo Mkoani Dodoma.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutembelea Ofisi hizo mapema leo ili kujionea utendaji wa Kampuni hiyo na Kusisitiza uzingatiaji wa maadili ya uandishi  wa habari.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiagana na watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Mkoani Dodoma mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Kampuni hiyo mapema leo.
   Watumishi wa Gazeti la Mwananchi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma iliyoanza Januari 17, 2017.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  akiagana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Mkoani Dodoma mara baada  ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo  na kuzungumza na wafanyakazi, kushoto ni Mkuu wa Kanda wa Gazeti la Mwananchi.(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)


  0 0  Na Mwandishi wa Globu, Simiyu.


  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga ameshiriki ibaada katika kanisa la SDA liliopo Kijiji cha Itubilo na kufanya harambee ya uchangiaji wa ujenzi ya shule ya  Itubilo Pre & Primary Medium School  na kuhamasisha wananchi kujitokeza na kusaidia kwenye ujenzi huo.

  Njalu ambaye alikuwa mgeni ramsi kwenye harambee hiyo, aliweza kuzungumza na wanakijiji wa Itubilo na kuwataka wafahamu kuwa msingi mkubwa wa urithi kwa mtoto ni elimu na zaidi wanakijiji washirikiane kwa pamoja kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa shule hiyo itakayokuja kuwa na manufaa kwa vizazi vya baadae.

  Wakati wa uendeshaji wa jarambee hiyo, Njalu aliweza kuchangia kiasi cha fedha shilling laki tano (500,000) pamoja na mifuko ya saruji 170 ili kuongeza nguvu ya ujenzi wa kanisa hilo.

  Wazee wa Kanisa kwa pamoja waliweza kumshukuru Mbunge wao Njalu kwa hatua kubwa aliyofanya ya kuwapatia mifuko ya saruji ambapo wanaamini kuwa wataitumia kuendeleza ujenzi wa shule hiyo itakayokuwa ni kuanzia elimu ya  awali na Msingi. 
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya ITUBILO PRE &APRIMARY MEDIUM SCHOOL lililojengwa kwa mfuko wa kanisa mmara baada ya kumaliza ibda ya pamoja na waumini wa kanisa hilo, Pembeni ni Mchungaji wa kanisa la SDA Itubilo Michael Phabian.
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akizungumza na waumini wa Kanisa la SDA Itubilo pamoja na wanakijiji baada ya kumaliza ibada ya pamoja na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Itubilo Pre & Primary Medium School na kuchangia kiasi cha shillingi laki tano (500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akivalishwa skafu na Vijana wa pathfinder mara baada ya kuwasili katika kanisa ;a SDA lililopo Kijiji cha Itubilo kata ya Lugulu tarafa ya Kinamweli.
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akiwa anapokea mkono wa shukrani kutoka kwa Mzee wa kanisa Enock Maduhu mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha shillingi laki tano (500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akiwa anajadiliana jambo na Mwalimu Abel Pondela wakati wa harambee ya uchangiaji hela ya ujenzi wa shule ya Itubilo Pre & Primary Medium School na kuchangia kiasi cha shillingi laki tano (500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.
  Mbunge wa jimbo la Itilima Mkoani Simiyu Njalu Daudi Silanga akifuatilia jambo sambamba na wanakijiji wa Itubilo wakati wa harambee ya uchangiaji ya ujenzi wa shule ya Itubilo Pre & Primary Medium School na kuchangia kiasi cha shillingi laki tano (500,000) na mifuko ya saruji 170 kwa ajili ya ujenzi wa shule.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

  Kufuatia hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo hicho.“Serikali haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”

  Ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.Waziri Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.

  Waziri Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa zimebanduka.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara za magendo.

  Waziri Mkuu amesema magendo yanaikosesha Serikali mapato, hivyo bidhaa yoyote itakayokamatwa ikiingizwa nchini kwa njia za magendo itataifishwa pamoja na chombo cha usafiri kilichotumika. Pia Waziri Mkuu ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega, ambapo amewasisiza wananchi wasimamie elimu ya watoto wa kike ili wafikie malengo yao.

  Amesema Serikali imeweka sheria kali kwa yeyote atakayekatisha masomo kwa watoto wa kike iwe kwa kumpa ujauzito au kumoa, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kamwe wasijihusishe katika mambo ambayo hayahusiani na masomo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATANO, JANUARI 17, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wagonjwa wakati alipotembela  hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 17, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adm Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Naomi Ogaja (3) aliyelazwa katika hospitali ya walaya ya arime kwa matibabu wakati alipotembelea hospitali hiyo Januari 17, 2017. Kshoto ni baba mzazi wa mtoto huyo Ogaja Wajangwa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima. (Picha na Ofisi  Waziri Mkuu) 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Sirari wilayani Tarime Januari 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Boreha wilayani Tarime, Januari 17, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  maeneo na majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega wilayani Tarime baada ya kuifungua akiwa katika  ziara ya mkoa wa Mara Januari 17, 2018.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo akiwaonyesha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ya Ubungo inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Ndg. Lucas Mgonja.

  Mkurugenzi Kayombo kwa kushirikiana na watumishi wa Manispaa hiyo ameweza kujenga ukuta (fensi), vyoo na vyumba nane vya madarasa katika shule ya msingi Ubungo Plaza.

  Kabla ya hapo shule hiyo ilikuwa haina uzio,hali ambayo ilikuwa ni hatarishi kwa wanafunzi wa jinsia zote.

  Pia kulikuwa na uhaba wa vyoo, ambapo kilikuwa ni chanzo kikubwa cha magonjwa.Sambamba na hilo wanafunzi walikuwa wanasoma katika majengo chakavu hali iliyokuwa ikihatarisha maisha yao.

  Habari njema ni kuwa Mkurugenzi Kayombo ameahidi kujenga shule ya Sekondari ya A - level katika eneo hilo.Jambo ambalo litakuwa ni Mara ya kwa Manispaa hiyo tangu ianzishwe.

  Hongera Mkurugenzi Kayombo kwa kuendelea kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 kwa vitendo.
  vyumba nane vya madarasa vikiwa katika hatua ya mwisho kabisa,katika shule ya msingi Ubungo Plaza.
   Ukuta wa shule hiyo 
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo akiwaonyesha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ya Ubungo inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Ndg. Lucas Mgonja.
   Vyoo vya shule hiyo vikiwa tayari kuanza kutumika.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) jana amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.

  Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti amesisitiza kuwa  nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.  ''Suala la ushindi wa CCM katika uchaguzi huu wa marudio halina mjadala tutashinda kwa heshima, Amani na  demokrasia vijana wa CCM tumejipanga vyema kufanikisha hilo ngazi zote" Alisisitiza  Mwenyekiti Kheri

  Wakati huo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam. ''Tunatambua na kuthamini mchango wa Vijana wenzetu wote katika jamii mkiwemo ninyi wa Vyuo na Vyuo Vikuu tunawategemea sana hivyo tutaendelea kufanya kazi nanyi katika maeneo yote katika kutimiza wajibu wetu wa msingi” Alibainisha Mwenyekiti Kheir.
  Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Dar es Salaam Asha Feruzi pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Alex Gwantwa.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
  Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
   Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia kwa Umakini kikao hicho.
  kikao kikiendelea.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao cha Viongozi wa Seneti  Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam , kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
   Sehemu ya Wajumbe wa Vyuo na Vyuo Vikuu wakifurahia jambo(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI).

  0 0

   

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Simon Msanjila akikabidhi zawadi kwa Prosper Gasper na Erick Simon kutoka Shule ya Sekondari St. Jude's jijini Arusha baada ya kuibuka washindi wa jumla wa Mashindano ya Wanasayansi Chipukizi (YST) yaliyofanyika leo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

  Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
  SHULE za Sekondari nchini Tanzania zimetakiwa kuanza kutuma maombi sasa ili kupata fursa ya kushiriki katika Maonyesho ya 8 ya Sayansi kwa wanafunzi yanayoandaliwa na Shirika la Young Scientists Tanzania (YST) kila mwaka.
  Taarifa kutoka YST zimeeleza kwamba, maonyesho hayo ni kwa wanafunzi wa kuanzia kidato za kwanza hadi cha sita kwa shule zote za sekondari – za umma na binafsi – zilizoko nchini.


  “Mwisho wa kutuma maombi ni Machi 31, 2018 na maonyesho hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam mwezi Agosti,” imesema taarifa hiyo.
  Taarifa hiyo imeeleza kwamba, kutuma mapema maombi kutasaidia hata zoezi la mchujo ili kuwapata washiriki wenye mawazo yatakayoleta ushindani pamoja na ubunifu kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini Tanzania.
  Jumla ya mawazo 100 yanatarajiwa kushindanishwa mwaka huu ambapo washindi katika vitengo mbalimbali watapatiwa zawadi za fedha pamoja na ufadhili wa masomo ya chuo kikuu.

  MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, wanafunzi Prosper Gasper na Erick Simon wa shule ya Sekondari ya St. Jude’s kutoka Arusha, ndio walioibuka mabingwa wa jumla wa sayansi katika Maonyesho ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania 2017 kutokana na wazo lao la “Kutumia Simu za Mkononi kama Mfumo wa Kubaini Ajali za Moto” (The Use of Mobile Network as a Fire Alert System).
  Kwa ushindi huo, mbali ya kutunukiwa medali na tuzo, pia walipata kitita cha Shs. 1,800,000 pamoja na udhamini wa masomo yao hadi elimu ya juu.
  Aidha, walipata nafasi kwa mara ya kwanza ya kushiriki mashindano ya ubunifu wa sayansi na teknolojia yaliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini mwezi Oktoba 2017 na mwaka huu 2018 watashiriki maonyesho ya kimataifa ya sayansi na teknolojia jijini Dublin, Ireland.
  Kumekuwepo na ongezeko kubwa la ushiriki wa shule za sekondari kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi 100, hatua ambayo imetokana na hamasa ya kuendeleza masomo ya sayansi kwa shule mbalimbali za sekondari nchini.
  MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, uwepo wa maonyesho hayo ya sayansi kwa wanafunzi usaidia ufaulu wa masomo ya sayansi kwa shule nyingi za sekondari nchini, mfano mmojawapo ukiwa ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara.
  Katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017, kwa mara ya kwanza shule hiyo ilipata daraja kwa kwanza (Division One) kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi, jambo ambalo lilikuwa adimu.
  Uchunguzi wa MaendeleoVijijini umebaini kwamba, kwa miaka takriban 10 mchepuo wa masomo ya sayansi, Kemia, Baolojia na Jiografia (CBG), haujawahi kutoa hata mwanafunzi mmoja aliyepata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha sita.
  MaendeleoVijijini imegundua kwamba, miaka yote ufaulu mkubwa wa masomo ya sayansi shuleni hapo umekuwa daraja la pili (division two) ambao nao haukuwa wa kuridhisha ikilinganishwa na masomo ya sanaa na uchumi, huku wanaochukua mchepuo wa sayansi ‘wakiongoza’ kwa kupata daraja la nne pamoja na kupata sufuri.
  Kati ya wanafunzi nane waliopata Daraja la Kwanza mwaka 2017 shuleni hapo, wawili walikuwa wanachukua mchepuo wa sayansi na kati ya wanafunzi 57 waliopata daraja la pili, 17 wanatoka mchepuo wa sayansi pia.
  Wanafunzi wawili waliopata daraja la pili shuleni hapo Diana Sosoka na Nadhra Mresa, ambao walikuwa washindi wa jumla mwaka 2016 katika maonyesho hayo ya sayansi ya YST nao walionyesha kushangazwa na matokeo hayo.
  “Kweli ni maajabu kwa mara ya kwanza kuna Division One kwenye CBG pale shuleni kwetu, ni mafanikio ambayo yametokana na hamasa ya kuwepo kwa mashindano haya ya sayansi na sisi tunashukuru kuwa sehemu ya mafanikio,” anasema Diana.
  Diana na Nadhra ambao walipata ushindi kwa kubuni mashine ya kienyeji ya kutotoresha mayai, pia walipata udhamini wa masomo ya chuo kikuu kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
  Wote kwa pamoja walikuwa wanachukua mchepuo wa Kemia, Baolojia na Jiographia (CBG) na kwa bahati nzuri, wote wawili wamepata Division Two ya alama 12.


  0 0

  Imeandaliwa na ​ Geofrey Chambua ​kutoka vyanzo mbalimbali

  Huenda umewahi kuliona na kulipita tu ama kutovutiwa na ladha yake ama kukereka na utomvu wake baada ya kula

  Habari mbaya kwako ni kwamba umekosa kitu adimu na maridhawa sana......Hili ni moja ya matunda yanayochukuliwa kama MFALME WA MATUNDA (The King of Fruits) kwa kuwa na karibu vitamin vyote muhimu yaani A, B1, B2 na C..

  Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.........na nakusihi sana kuanzia leo ujitahidi kula walau punje tatu tu na ukiweza hata mbegu zake kwa kadri ya mada hii

  Leo nimejikuta tu nafukunyua tunda hili baada ya kulikuta mahali fulani na jinsi watu walivyokuwa wanatua kilich cha thamani ndipo nilipoanza kugoogle nikakuta faida na hata hilo jina la lugha ya malkia huitwa Jackfruit

  Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.
  Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats). Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania, Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.

  Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuz (fiber) ambazo husaidia kwenye mfumo wa mmeng'enyo na kuchagiza tatizo la kupata haja (constipation) na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa.

  Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu (cholesterol). Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha,

  Sukari ya Fenesi ni dawa ya sukari sumu mwilini kwa kuwa linasharabiwa taratibu mwilini na kufyonza sukari sumu na hii husaidia pia katika kuhibiti shinikizo la damu mwilini ( Jackfruit is more slowly absorbed into the bloodstream, which prevents sugar crashes, sugar cravings, and mood swings, They are well known because of its high potassium content. This helps the blood vessels relax and maintains proper blood pressure.)

  Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

  Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

  Kinga: Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

  Nishati: Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

  Wingi wa Vitamin A kwenye Fenesi husaidi kusharabu kwa nywele (jackfruit contains vitamin A to keep the hair moisturized through increased sebum production)

  Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

  Asthma: Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.

  Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini na pia kusaidia kukupa usingizi mwanana na kukuepusha na mauzauza (Jackfruit has a high content of magnesium, a mineral that is directly linked to improving the quality, duration, and tranquility of sleep. Jackfruit also helps regulate the metabolism, to help reduce sleep disorders and the occurrence of insomnia)

  MENGINE ZAIDI AMBAYO HAYASEMWI SANA KUHUSU FENESI

  Kuna faida lukuki kwenye MBEGU ZA FENESI (6-remarkable-benefits-of-jackfruit-seeds)

  kiboko zaidi ni ukizichoma hizo mbegu. Ni tamu sana na laini kama kiazi ila kuwa mwangalifu wakati wa kuchoma zikiiva wakati mwingine hupasuka na kutoa sauti kama ya mlipuko, sasa kama ulikuwa unasonga ugali kwenye jiko la kuni ukaweka mbegu mbili tatu kwenye moto ili uendee kugonga mdogomdogo ikipasuka hata moja ugali wote lazima ujae majivu na michanga na kama mwoga unaweza toka nduki vilevile....Ladha yake huwa inashahabiana na kiazi kitamu kilichochomwa na unachofanya ni kubandua gandale na kutafuna kokwale lililokwiva kwa moto...kuna jamii zinginea zinakula mbegu za fenesi na kuna jamii nyingine hawajui hata kama zinaliwa. Kuna some factors zinazofanya kitofautiana kwa resource kati ya jamii moja hadi nyingine......Tanga wanazichanganya na mihogo (muhogo wa aina ya kibanda meno au kitingisha ndevu maeneo ya Muheza) zinaungwa na nazi. Halafu ili ufaidi zaidi Mihogo iwe inawahi kuiva ile ya unga unga achana na ile chelema, mchanganyiko wake ni hatari sana (njoo chemba)

  Utomvu wa fenesi ni dawa ya ngiri...ichukue hiyo kama ulikuwa hujui na pia husaidia kulainisha uso japo unahangaika na SCRUB za MJINI

  Majani ya Mfenesi hutibu homa magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari

  Mibamiba ya fenesi wengine hugeuza chanuo panapo dharura na ikibidi

  Faida nyingine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.

  TANBIHI

  kuna mada ambayo inaongelewa sana, nayo ni "kula fenesi na baadaye kunywa pombe kunaweza kukupelekea mauti."
  Mtaalam wa masuala ya afya wa hospitali ya Puren ya Wuhan ameonya pia kuwa hoja hiyo ina uhalali kisayansi.

  Wakati nikibarizi kwenye mitandao mbali mbali ya habari niliweza kukutana na habari hii ambayo imekuwa kichwa cha habari nchini hapa "Wataalam wa Chuo cha Tsukuba, nchini japan wamegundua kuwa ukila fenesi na kunywa bia inaweza kuhatarisha maisha yako na kupelekea kufa.

  Ndani ya fenesi kuna chembechembe za sulphur kwa wingi ambazo hupunguza mfumo wa Alidehaidi dehydrogenase kwa asilimia sabini. enzyme hii ni muhimu katika kusafisha sumu ya pombe, kwa wenye ugonjwa wa kisukari hali hii huweza kusababisha mishipa ya damu kuziba au kupasuka, na pengine kusababisha kiharusi."  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa boma la madarasa ya shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akipiga plasta kwenye chumba cha madarasa katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitunukiwa uchifu kutoka kwa Machifu wa Kabila la Wasafwa kama shukurani kwa jitihada za kuamsha ari ya wananchi kujitolea kuchangia shughuli za maendeleo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo jiji la Mbeya Mkoani Mbeya wakati wa ziara ya yake ya kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya kazi za maendeleo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akiwa na vazi la kichifu la kabila la Wasafwa pamoja na machifu wengine wa Kabila la Wasafwa wakati alipotunukiwa uchifu wa kabila hilo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi wakishiriki kutekeleza utoaji wa haki ya kumwendeleza Mtoto kwa kumpa elimu.
  \
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akikabidhi moja ya mbati 49 kwa uongozi wa Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya jamii kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao ili kutoa haki ya Mtoto kuendelezwa.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwasanga na maeneo ya jirani katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya na kuhamasisha harambee ya kumalizia ujenzi wa madarasa matatu ya Shule ya Sekondari ya kata iliyozaa kiasi cha shilling laki nane katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo.
  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwasanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya kushiriki kazi yakuchanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitoa mchango wake kwa wazee wa Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kwa ajili kuwawezesha kupata Kadi ya Bima ya Afya kwa Jamii (CHF) katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika ngazi mbalimbali.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW  Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la Wasafwa linalopatikana katika mkoa wa Mbeya .

  Dkt. Ndugulile amesimikwa uchifu huo wakati wa ziara yake mkoani Mbeya yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

  Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, kilimo, barabara, viwanda na maji, nk.

  Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zahanati na Maghala kwa kutumia rasilimali zilizopo.

  “Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya na hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii inayotoa matokeo yenye mashiko na tija katika jamii. Tumieni stadi na mbinu shirikishi kuwezesha maendeleo jumuishi ambapo makundi yote katika jamii yanashiriki katika maendeleo yao” alisistiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

  Dkt. Ndugulile pamoja na kupewa uchifu, kushiriki katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Mwasanga pia aliendesha harambee ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo na kuwalipia wazee watano wa Kata hiyo kadi ya kupata huduma za Afya bure kupitia Huduma ya Afya kwa Jamii (CHF).

  Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Bw. Hassan Mkwawa amempongeza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) kwa kuamua kushirikiana na wananchi na viongozi kufanya kazi ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kushiriki ujenzi wa shule ya Sekondari ambayo itasaidia watoto kupata haki yao ya kuendelezwa.r

  Mmoja ya wananchi wa Kata ya Mwasanga Bw. Fredy Mwaikese ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada zao na kuwashauri wananchi wenzake kuendelea kujitolea kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo na kuchangia shughuli nyingine za maendeleo.

  “Ushiriki wa jamii katika kutekeleza kazi na miradi ya maendeleo huharakisha kufikiwa kwa malengo muhimu ambyo ni kipaumbele cha wananchi katika ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla” alisema Bw. Mwaikese.

  Wote kwa pamoja tuendelee kushirikiana pamoja kuibua miradi inayozingatia mahitaji ya wananchi kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya watoto, wanawake na wanaume kwa kuzingatia uzalendo kwanza na kuchapa kazi kwa bidii na kwa kuunga mkono kazi za maendeleo zinazofanya wananchi wa Kata ya Mwasanga kushiriki kwa hali na mali kukamilisha madarasa ya watoto wao kosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari kwa mwaka 2018. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alichangia mifuko 49 ya saruji na kuendesha harambee kiasi cha shilingi 728,050/= tasilimu kusaidia kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

  0 0


  Shirika lisilo la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) limetoa mafunzo ya Hisa kwa vijana 15 kutoka katika kata za Mwamalili,Didia na Masekelo zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 

  Pamoja na kuwapatia vyeti vya ushiriki wa mafunzo,shirika la AGAPE pia limekabidhi baiskeli 15 kwa vijana 15 walioshiriki mafunzo hayo ambazo zitawamsaidia kurahisisha kusafiri wanapotoa elimu ya hisa katika jamii. 

  Mafunzo hayo ya uwezeshaji wa vikundi vya hisa ngazi ya jamii yalianza Januari 11,2018 na kufungwa leo Januari 17,2018 katika darasa la AGAPE AIDS Control Programme lililopo katika kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga. 

  Mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo leo,yaliyohudhuriwa pia na maafisa maendeleo kutoka kata hizo tatu,alikuwa Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

  Meneja Miradi wa Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda alisema mafunzo yametolewa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuzuia ndoa na mimba za utotoni unaofanywa na shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la Firelight. 

  “Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha vijana ili wawe wawezeshaji wa vikundi vya kijamii vilivyopo katika maeneo yao ambapo watakuwa wanavipatia ujuzi juu ya faida ya kuweka akiba hasa kupitia mfumo wa Hisa ili kujikwamua kiuchumi”,alieleza Isabuda. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE,John Myola alisema kutokana tafiti mbalimbali kubainisha kuwa umaskini wa kipato ngazi ya kaya huchangia kushamiri kwa matukio ya ndoa na mimba za utotoni,shirika hilo limeamua kuwajengea uwezo vijana ili waweze kujiajiri. 

  “Tumetoa elimu ya hisa,ujasiriamali,mpango wa kukopeshana ili wakawaelimishe vijana wenzao na makundi mengine katika jamii kuhusu namna ya kupata mikopo ili kujikwamua kimaisha”,alieleza Myola. 

  “Serikali yetu inataka watu wafanye kazi,nasi tunaendelea kushirikiana na serikali,tunataka mabadiliko yapatikane katika jamii,tunahitaji vijana hawa wafanye kazi kwa kujituma kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato”,aliongeza. 
  Aidha aliwataka vijana kutumia akili na nguvu zao vizuri kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo ili kutokomeza umaskini unaochangia kwa kiasi kikubwa ndoa na mimba za utotoni. 

  Kwa upande wake mgeni rasmi,Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga,aliwataka vijana hao waliopata mafunzo kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao na kuhakikisha wanaunda vikundi watakavyovitumia kuomba mikopo katika halmashauri za wilaya. 

  “Naomba vijana mjiajiri wenyewe ili mpate pesa kwa ajili ya hisa,elimu hii mliyopewa mkaitumie vizuri pia mtunze baiskeli mlizopatiwa kwa ajili kurahisisha usafiri katika maeneo mtakayoyafikia”,alisema. 

  “Nitumie fursa hii pia kulipongeza shirika la AGAPE kwa jitihada linazozifanya katika kupambana na ndoa na mimba za utotoni,linafanya kazi kweli kweli bila ubabaishaji,kazi zake zinaonekana na zinapimika”aliongeza. 

  Nao washiriki wa mafunzo hayo walilishukuru shirika hilo kwa kuwapatia mafunzo ya hisa na kwamba wataenda kutoa elimu hiyo kwa jamii kama walivyofundishwa kwa kipindi cha wiki moja.
  Mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya hisa kwa vijana 15 na kutoka kata za Mwamalili,Didia na Masekelo zilizopo katika wilaya ya Shinyanga.Aliwasisitiza vijana kufanya kazi kwa kujituma ili kuleta mabadiliko katika jamii.-Picha zote Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Meneja Miradi wa Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda akielezea lengo la mafunzo hayo.Kushoto ni washiriki wa mafunzo hayo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.Kushoto ni Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Aisha Mwinshali.Kushoto ni mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 
  Mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula akishikana mkono na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya hisa kwa vijana 15 wakati wa kukabidhi vyeti vya ushiriki
  Mshiriki wa mafunzo hayo akipokea cheti cha ushiriki
  Baiskeli 15 zilizotolewa na shirika la AGAPE kwa ajili ya vijana 15 walioshiriki mafunzo ya hisa.Baiskeli hizo watazitumia wakati wa kutoa elimu katika jamii
  Mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula akishikana mkono na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,wakati akimkabidhi baiskeli atakayoitumia kusafiri akitoa elimu ya hisa kwa jamii
  Vijana wakipokea baiskeli
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa aevaa koti lililotengenezwa na wajasiliamali wadogo wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tea Masala wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tomato Sauce wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
   
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na wanawake wajasiliamali walioshiriki kikao cha siku moja katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya huku akiwa ameshika moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali hao wakati wa ziara yake iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa motisha kwa Vikundi ‘walelewa’ chenye mtaji mdogo na kuwaunganisha kwa ‘Vikundi Mlezi’ ambacho mtaji wake umeimarika ili waweze kusaidia katika kukuza biashara zao wakati wa ziara yake Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanyakazi za maendeleo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa mkopo wa Shillingi Million 1 kwa mmoja wa mwananchama wa Saccoss ya wanawake Mbeya wakati wa Uzunduzi wa Saccoss hiyo wakati wa ziara yake ya Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW  Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amezidua Saccoss ya Wanawake katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo ili kuweza kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupa mbinu mbalimbali za kufanikisha matarajio yao na kupata maendeleo.

  Ameizindua Saccoss hiyo Mkoani Mbeya wakati akiitambulisha Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya ya Jiji la Mbeya yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana kati yao wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

  Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo linaenda sambamba na uwezeshwaji wa wanawake katika kuwashirikisha wanawake wenyewe katika kuibua miradi na kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya fursa na weledi wa wananchi wenyewe. 

  Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake kuwaweza kuanzisha vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na kuzalisha bidhaa zitakazo uzwa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya na hivyo kuutangaza mkoa kupitia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia ubunifu na rasilimali zilizopo.

  Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saxccoss ya Wanawake ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi na kuwashirikisha wajasiliamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na vifaa.

  “Niseme uzinduzi wa Saccoss hii kwa ajili ya wajasiriamali ni muhimu kwenu wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na mitaji ya kufanya shughuli zao pamoja na kuwawezesha kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

  Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara na kusaidia kuhamasisha Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa wanawake na vijana ambazo zitatumika kama mtaji wenye masharti nafuu wa kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

  Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw. amesema kuwa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saccoss ya wanawake itasaidia kuwainua wanawake ikiwa halmashauri zitashirikiana na wadau wa maendeleo kuwawezesha wanawake kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kumwahakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa wa Mbeya.

  Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Manispaa ya Jiji la Mbeya Bi. ameishukuru Serikali kwa kuzindua Progarmu ya kikundi Mlezi na kuanzishwa kwa Saccoss hiyo utakaowawezesha wanawake kusaidiana katika kuanzisha na kuboresha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) anafanya ziara mkoani Mbeya kwa kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kuchangia lengo la kuanzisha biashara ndogo na za kati kwa manufaa ya Taifa. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

  0 0

  Shule ya sekondari ya Lupalilo inakabiliwa na ukosefu wa nishati ya umeme kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa, baada ya Transfoma iliyokuwepo kuungua na kusababisha kukwama kwa shughuli mbalimbali shuleni hapo ikiwemo wanafunzi kushindwa kujisomea usiku pamoja na kuhatarisha usalama wa wanafunzi baada ya kukosekana kwa nishati hiyo hasa nyakati za usiku

  Akizungumzia Hali hiyo makamu mkuu wa shule Mwalimu LUNANILO KILATU amesema ni zaidi ya mwezi mmoja sasa wamekosa nishati hiyo baada ya transfoma kuungua na kupelekea baadhi ya shughuli kukwama shuleni hapo ikiwemo wanafunzi kushindwa kujisomea nyakati za usiku hivyo shule kulazimika kutumia jenereta ambalo amedai linawaongezea gharama zaidi.

  Amesema wamesharipoti suala hilo kwa shirika la umeme TANESCO wilaya ya Makete tangu lilipotokea lakini hadi sasa ufumbuzi haujapatikana ingawa anaimani kuwa wanashughulikia.Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi shuleni hapo waliozungumza na mwandishi wetu wamesema wanakumbana na changamoto nyingi baada ya kukosekana nishati hiyo ikiwemo kushindwa kujisomea nyakati za usiku huku wakihofia juu ya usalama wao hususani wanafunzi wa kike

  Hata hivyo Tumemtafuta Meneja wa Tanesco wilaya ya Makete Ndugu HENRIKO RENATUS kupata ufafanuzi ambapo amesema mpaka sasa wanasubiri Transfoma nyingine kwani wameshatuma maombi ya kuomba transfoma na pindi zitakapowasili wataipa kipaumbele shule hiyo kutokana na uhitaji

  Ni zaidi ya mwezi sasa shule hiyo ikabiliwa na tatizo hilo la ukosefu wa umeme na kukwamisha mambo mengi pamoja na usalama wa wanafunzi kuwa mdogo na kupunguza uwezekano wa wanafunzi kujisomea nyakati za usiku kama ilivyokuwa awali.Habari/picha na Edwin Moshi.


  Makamu Mkuu wa shule akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake

  Mwanafunzi wa Lupalilo Sekondari akizungumza na mwandishi wetu
  Muonekano wa shule ya Lupalilo Sekondari

  Transfoma iliyopata tatizo
   

  0 0

  *Asema suala la ndoa kwa sasa kwake bado analitafakari...

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  UNAPOAMUA kuzungumzia au kutaja majina ya wasanii wa kike ambao wanajihusisha na muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva basi lazima utakutana na jina la Nuru The Light.

  Jina halisi la mwadada huyo ni Nuru Magram lakini kwenye muziki basi kama ambavyo wanafanya wasanii wengi tu wa ndani na nje ya Tanzania akaamua kuwa na a.k.a yake.

  Nuru The Right ni moja kati ya wasanii ambao wanaheshima kutokana na kazi zao za muziki wa kizazi kipya.Moja ya wimbo alioutoa kwa mashabiki wake na kumfanya atambulike na kuwa maarufu zaidi ni wimbo wake wa Walimwengu, licha ya kwamba ni juzi tu ameipua wimbo mpya unaojulikana kwa jina la Nimeachwa.

  Mbali ya muziki amekuwa akifanya mambo mengine mbalimbali na kwa sehemu kubwa anaishi nchini Swedeen, lakini kwa sasa amerejea nchini kusalimia ndugu, jamaa na marafiki.

  Sifa kubwa ya Nuru The Right ni msanii wa kike ambaye anafahamu nini ambacho anakifanya katika muziki.Anajua wakati gani wa kutoa wimbo mpya na wakati gani wa kusoma soko la muziki linakwendaje.

  Michuzi Blogu imepata nafasi ya kutembelewa na msanii huyo ambaye hana makuu, hana sifa za kijinga na siku zote amekuwa mnyenyekevu, mpole , mcheshi na mwenye kuheshimu kila mtu na kubwa zaidi ni msanii ambaye sauti yake inaweza kumtoa nyoka pangoni.Hakika ni msanii anayejali mashabiki wake.

  Akiwa katika ofisi za Michuzi Blog ameulizwa maswali mengi na kwa sehemu kubwa ameyajibu kadri ya uwezo wake.Hata hivyo moja ya swali ambalo ameulizwa lilikuwa linataka kufahamu kama ameolewa au la,Nuru The Light akatabasamu na kutoa sauti ya kicheko na kujibu kuwa kwa sasa hana mume, kwani wakati wa kuolewa na kuwa mke wa mtu bado hajafikira kwa sasa.

  Licha ya kwamba bado hajaolewa lakini anasema wakati ukifika kama mwanamke atahitaji kuwa na mume lakini si tu ilimradi mume, bali awe anasifa ambazo anahitaji kutoka kwa huyo ambaye atataka kumuoa.Kwanini hajafikiria kuolewa amejibu kuwa wakati haujafika bado kwani haipo kwenye mipango yake kwa sasa.

  Nuru The Right hakusita kuelezea baadhi ya sifa ambazo anataka kuwa nazo mtu ambaye atataka kumuoa.Moja ya sifa ambazo anataka awe nazo mwanaume atakayetaka kumuoa ni mwanaume ambaye anajitambua, anajali na kubwa zaidi awe mwenye imani ya dini na kumjua Mungu.

  "Zipo sifa nyingi za aina ya mume ambaye nataka awe nazo , lazima niwe na mwanaume ambaye anajitambua na anaelewa anachokifanya.Pia awe mwanaume mwenye imani ya dini,"amesema Nuru The Right huku akionesha kuwa zipo sifa nyingine nyingi ambazo anatamani mume atakeyemuoa awe nazo.

  Alipoulizwa kama anazungumzia vipi aina ya maisha ya baadhi ya wasanii ambayo yanaonesha kutotulia kwenye mahusiano yao ya kimapenzi, amejibu kuwa binafsi hafurahishwi na tabia hiyo kwani anapofanya msanii mmoja inaonekana ndio tabia ya wasanii wote wakati si kweli.

  "Binafsi najiheshimu na wakati mwingine ninaposikia habari za wasanii na mambo ambayo wanayafanya huwa inaniumiza sana moyo.Ni vema wasanii tukawa makini na aina ya staili ya maisha yetu.

  "Hata hivyo kuna mambo ambayo wakati mwingine yanakera.Unaweza kukuta msanii fulani anafanya mambo ambayo yanavunja heshima yake lakini hakuna ambaye anamsema wala kumwambia

  "Ila akitokea msanii mwingine akafanya hivyo hivyo watu wanakuja juu na kuanza kutoa maneno ya kila aina.Ni kama vile kuna wasanii wakifanya sawa na wengine wakifanya wanakosea,"amesema Nuru The Right.

  Baada ya kukuleza sehemu ndogo tu kati ya mengi ambayo msanii huyo ameyazungumza kuhusu maisha yake ya muziki na nini ambacho amepanga kukifanya, usikose kufuatilia hatua moja baada ya nyingine ya maswali na majibu ya msanii huyo kupitia Michuzi TV ....

  0 0

  Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba ametembelea kiwanda cha kubangua Korosho cha Micronix System Limited kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara na kuzungumza na Viongozi wa kiwanda hicho juu ya kupandisha malipo kwa Vibarua wanaofanya kazi Kiwandani hapo.

  Kwa Sasa mfanyakazi analipwa Kati ya Shilingi elfu 7 mpaka elfu 8 kwa siku ambapo wanafanya kazi Kwa Siku 5 kwa Wiki.

  Tayari uongozi wa kiwanda hicho kwa  kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo wameahidi kulifanyia kazi Suala hilo.
   Waziri wa Kilimo Dr.Tizeba akiongea na Baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha kubangua Korosho cha  Micronix System ltd kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ambacho Kimeajiri wafanyakazi 350.
   Waziri wa Kilimo Dr.Tizeba akioneshwa aina za Korosho ambazo Tayari zimebanguliwa na kuwekwa kwenye vibakuli ili kupima Ubora Tayari kwa Kupakia, Kushoto kwake ni mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo pamoja na Meneja Uzalishaji wa ETG Ltd Sunir Mizar.
   Waziri kilimo Dr.Charles Tizeba Akipanda Mche wa Mkorosho katika Kijiji cha Machombe,Kata Ya Marika kama Moja ya kuhamasisha upandaji wa Miche Mipya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

  0 0

  Na Shani Amanzi,

  Uzinduzi wa kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, utafanyika Marchi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.

  Katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga.

  Ndugu. Nyakia amesema, Jamii inatakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti, sambamba na kutunza mazingira ya asili ya Wanyama Pori. Aliongeza kwa kusema zoezi la upandaji miti ni endelevu katika Wilaya ya Chemba na jumla ya miti elfu 2000 imepandwa katika kijiji cha Kelema Kuu kata ya Paranga, maeneo ya Taasisi na Makazi ya watu.

  Wilaya ya Chemba imefanya shughuli ya upandaji miti katika Kijiji hicho kama sehemu ya kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani, sambamba na uhamasishaji wa utunzaji wa Wanyama pori kwa kuwa kijiji cha Kelema Kuu kinapakana na pori la akiba la Swagaswaga .

  Pori la akiba Swaga swaga linatumika katika shughuli za Uwindaji wa Kitalii ambapo jamii inayozunguka pori hilo inanufaika kwa kupata mgao wa ruzuku unaotokana na shughuli za utalii.

  Maadhimisho ya Uzinduzi wa siku ya Wanyama Pori Duniani umeshirikisha Katibu Tawala Wilaya ya Chemba Ndg. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus H. Mashimba, Mkurugenzi wa Taasisi ya Rafiki Wild Life Foundation, Wakuu wa Idara/Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Viongozi wa Ngazi ya Kata, Kijiji na Wananchi. 
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza mbele ya Wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Uzinduzi wa kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, ambao unatarajiwa kufanyika Marchi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma,huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,katika shughuli hiyo Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akishiriki upandaji miti kuelekea Uzinduzi wa siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, ambao unatarajiwa kufanyika Machi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma,huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.katika shughuli hiyo Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.


  0 0

  Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK-47 iliyotupwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanataka kuvamia kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

  Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema walikamata silaha hiyo usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano eneo la Tinde wakati majambazi hao wanafuatiliwa na polisi ndipo wakaamua kutupa bunduki hiyo.

  “Silaha hii aina ya AK-47 yenye namba 18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na risasi 25 ndani ya magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa kwenye mfuko mdogo wa nailoni”,alieleza Kamanda Haule.

  “Majambazi wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi mbili na koti zito”,aliongeza.

  Alisema jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018 kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa Kahama na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha silaha aina ya AK-47 yenye namba 18116428 na mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong 

  Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyotelekezwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Wachina mjini Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  Silaha na vifaa vilivyotelekezwa na majambazi
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule


  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha skafu iliyotumika kufunga bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha risasi zilizotelekezwa na majambazi

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF iliyotelekezwa na majambazi

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha koti zito lililotelekezwa na majambazi

  Jengo la ofisi za kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

  Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),bwana Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi

  Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd ,bwana Liu Buhua akilishukuru na kulipongeza jeshi la polisi kuzuia uhalifu katika kiwanda hicho

  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

older | 1 | .... | 1489 | 1490 | (Page 1491) | 1492 | 1493 | .... | 1903 | newer