Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe.Sahabu Isah Gada Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe. Mhe.Sahabu Isah Gada  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe. Mhe.Sahabu Isah Gada Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 16, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Poland nchini Mhe. Krysztof Buzalski Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Poland nchini Mhe. Krysztof Buzalski Ikulu jijini Dar es Salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 16, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa mwambata wa kijeshi wa Ubalozi wa Uturuki nchini Navy Commander Murat Ozen  baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa  Uturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto)   Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 16, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na balozi mpya wa  Uturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu akiwa na Mwambata wa Kijeshi Navy Commander Murat Ozen na Katibu wa pili ubalozini Nihat Kumhur baada ya kupokea hati ya yake ya utambulisho. Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Ufaransa mchini Mhe. Frederic Clavier  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na balozi mpya wa Ufaransa nchini nchini Mhe. Frederick Clavier Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Israel hap  nchini Mhe. Noah Gal Gendler  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Israel  Mhe. Noah Gal Gendler Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Australia nchini Mhe. Alison Chartres Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bw.  Robert Sirotka, mume wa balozi mpya wa Australia nchini, Mhe. Alison Chartres  (katikati) baada ya kupokea hati  za  utambulisho toka kwa balozi huyo mpya  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018. Kulia ni Katibu wa Pili Ubalozini Deanna.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na  Bw.  Robert Sirotka, mume wa balozi mpya wa Australia nchini, Mhe. Alison Chartres  (katikati) baada ya kupokea hati  za  utambulisho toka kwa balozi huyo mpya Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA WILAYANI RORYA MKOANI MARA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Nati Hassan mmoja wa wazazi waliojifungua wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua Kituo cha Afya cha Kinesi wilayani Rorya Januari 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Nyamungo wilayani Rorya, Juma Wilfred baada ya kuzungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinesi Januari 16, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Kituo cha wilaya cha Kipolisi cha Kinesi wilayani Rorya, SSP Juma Wilfred Majula (wapili kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho na kuvutiwa na juhudi ziizofanywa na Mkuu huyo wa Polisi za kujenga kituo hicho bila kusubiri fedha za serikali Januari 16, 201.. Waziri Mkuu aliendesha harambee ya papo kwa papo na kufanikiwa kupata shilingi milioni 20 za kumalizia jengo jipya la kituo hicho. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Tarime na Rorya, David Mwaibambe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Utegi wilayani Rorya wakati alipolazimika kuasimama baada ya kuona umati mkubwa watu waliokuwa na shauku ya kumuona na kuksikiliza Januari 16, 2018.

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Azungumza na Wenyeviti wa Jumuiya za Chama Ikulu

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumza na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuchukua nafasi hiyo kuiongoza kwa kipindi cha miaka mitano.(Picha Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzu Dk. Ali Mohamed akiwa na mgeni wake Mwnyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund, akimshindikiza baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar alipofika kujitambulisha.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, akitowa maelezo na kumtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James walipifika kwa mazungumzo na kujitambulisha Ikulu Zanzibar leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao na kujitambulisha Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania (UWT) Thuwaiba Editon Kisasi alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar walipofika kujitambulisha.(Picha Ikulu) 

MKAZI WA DAR NA KIGOMA WAJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 10 KILA MMOJA

$
0
0


.Akizungumza na waandishi habari wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao , mapema leo mbelee ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Mmoja wa Maofisa Habari wa Tatu Mzuka, Millard Ayo alisema droo hiyo inachezwa kila siku,huku wenye bahati zao wakiendelea kujinyakulia vitita vyao vya Tatumzuka.Milard amewaasa Watanzania waendelee kucheza kwa wingi na mara kwa mara mchezo huo,kwani ukiibuka mshindi maisha yake huinuka na kuwa bora zaidi tofauti na alivyokuwa hapo awali.Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umetoa washindi wawili wa sh. Milioni 10 katika droo inayochezwa kila siku,mmoja akitokea jijini Dar na mwingine akitokea mkoani Kigoma
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka,Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka inayofanyika kila siku ,Harieth Steven (21) mkazi wa Kigoma ambaye anajishugulisha na kazi za ndani (housegirl),mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .
Harieth Mwenye mtoto mmoja alifurahia kujishindia donge hilo kupitia mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka,kwani baada ya kutaarifiwa kuwa amejishindia kiasi hicho cha fedha,akajipa matumaini ya kuwa ndoto yake ya kufanya biashara ya vitenge sasa inakwenda kutimia rasmi,na kuacha kufanya kazi za ndani.
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka,Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka ,Ally Rashid (26) mkazi wa Yombo Buza ambaye anajishugulisha na biashara ya kuuza Mboga mboga jijini Dar,mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .

BASHE AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe mapema leo amekagua mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika jimbo la Nzega Mjini.

Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa ya maji nchini huku ukitarajiwa kutumia zaidi ya Bilioni Mia Sita ambazo zilitiliwa saini baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya India mwezi Mei mwaka 2017.
Tayari mkandarasi ameanza ujenzi wa matanki makubwa ya maji na njia za kupitisha mabomba makubwa ambayo yataifanya Nzega Mjini kuwa kitovu kikuu cha Usambazaji wa Maji haya ya Ziwa Victoria.
Katika kuhakikisha mradi huu unanufaisha wananchi wote wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Bashe aliwasilisha maombi binafsi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli fedha kwa ajili ya kupanua mtandao wa Maji Nzega na tayari Rais amekwisha kutoa fedha hizo ili kuboresha upatikanaji wa Maji ya uhakika katika Mji wa Nzega ambao kwa miaka mingi umekua na kilio kikubwa.
Kwa upande mwingine Mhe. Bashe ametembelea eneo la Sagara ambapo kwa pamoja na Halmashauri ya Mji wa Nzega wamekusudia kujenga kisima kikubwa chenye uwezo wa kusambaza maji kwenye maeneo jirani. Upanuzi wa kisima hiki ni katika juhudi mahsusi za kuhakikisha hakuna tena tatizo la maji Nzega.
Aidha, kuhusiana na ajira zitakazotokana na mradi huu Mhe. Bashe amesema "Kipaumbele kwa ajira ambazo zitatokana na mradi huu watapewa watanzania ambao wanaoishi katika maeneo ambayo mradi unapita ili kuhakikisha mzunguko wa fedha na ajira zinakuwepo kwa vijana na wananchi ndani ya Mji wa Nzega"

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU NA TAMISEMI, APIGA MARUFUKU MICHANGO MASHULENI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. Taarifa kamili inakuja.Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifafanua jambo kwa msisitizo  mara baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo (kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako (kulia) Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo (kushoto) na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako (kulia) Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. .Picha na IKULU 

WAZIRI KAMWELWE AZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 2.76 MTWARA

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja. 
 
Na Athumani Shariff- MoWI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja.

Mradi wa maji wa Mayaya katika Halmashauri ya Mtwara uligharimu shilingi 973,022,925 una vituo 37 vya kuchotea maji na unanufaisha wananchi wapatao 4,997.

Katika Halmashauri ya Masasi Waziri Kamwelwe alizindua mradi wa maji wa Shaurimoyo– Mpindimbi wenye thamani ya shilingi 1,791,353,368.19 ambao utanufaisha wakati wapatao 8,400 washio katika vijiji vya Shaurimoyo, Kachepa, Mpindimbi na Kanyimbi.

Wakati wa uzinduzi wa Miradi hiyo, wananchi walishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwani walikuwa na adha kubwa ya maji ambapo kabla ya mradi walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi elfu moja na baada ya mradi wananunua ndoo moja kwa shilingi hamsini tu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi amemshukuru Wazira wa Maji na Umwagiliaji na serikali ya awamu ya tano kwa kukamilisha ahadi zao, na ana furaha isiyo na kifani kwa kukamilika miradi hiyo ambayo imeondoa kero kubwa ya maji kwa wananchi.

Waziri Kamwelwe kesho ataendelea na ziara ya kikazi Mkoani Lindi ambapo atakagua mradi wa maji wa Ng’apa kisha ataelekea Wilayani Newala Mkoani Mtwara kwa ajili ya uzinduzi mradi wa maji wa Mapili uliojengwa kwa thamani ya shilingi 1,668,826,940.

Baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Mhandisi Kamwelwe atarudi Dodoma alhamisi kuendelea na shughuli za bunge.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR ATILIANA SAINI NA BALOZI MDOGO WA CHINA XIE XIAO WU ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed kushoto akitiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed kushoto wakibadilishana hati na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt, Khalid Salum Mohammed kushoto wakipea na Mikono na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu kulia baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt, Khalid Salum Mohammed kulia akizungumza machache baada ya kutiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
 aziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed akisisitiza jambo alipozungumza machache baada ya kutiliana saini na Balozi mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiao Wu Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed wapili kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mdogo alioko Zanzibar Xie Xiao Wu baada ya kutiliana saini Msaada wa Fedha za Kitanzania  Shilingi  Bilioni 34.9 ambazo zitasaidia miradi mbalimbali ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye.  Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo. 
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.

 Katika kujali makundi yenye changamoto za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha. Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. 

Mchembe amesema kuwa huo ni utamaduni aliojiwekea kila mwanzo wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima na wale waishi katika mazingira magumu. "Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 

Mhe. Mchembe aliwakumbusha watoto hao kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma. Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi. Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike kuwaepusha na mimba za utotoni.

WCF YAWANOA WAAMUZI, WASULUHISHI NA MAKATIBU MUHTASI KUTOKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

$
0
0
 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.

Hayo yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.

“Katika jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda,  makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la utoaji huduma za Mfuko kwa wadau  litaongezeka na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba  alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.

“Jambo hili si rahisi kwa sababu ndio linaanza kwa hivyo tunahitaji ushirikiano wa karibu sana kutoka kwa wadau mbalimbali mkiwemo ninyi CMA, na katika hilo ushirikiano tu hautoshi Mfuko umekuwa ukitoa elimu ili kuwawezesha watu  wajue Mfuko umeanzishwa kwa sababu gani, kazi zake, lakini pia kujua taratibu za kudai fidia pale mfanyakazi anapopatwa na majanga ya kuumia au kuugua wakati akitekeleza wajibu wake wa kikazi.” Aliongeza Bw. Mshomba.

“Ndio maana leo hii tunao wataalamu wetu watakaotoa mada mbalimbali zikiwemo, Sheria za Fidia, Namna Fidia inavyolipwa lakini shughuli za Mfuko.” Alibainisha Mkurugenzi Mkuu Bw. Mshomba.

Aidha aliishukuru Tume kwa kuwashirikisha WCF ili kuwaelimisha wafanyakazi wake kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

“Ni muhimu kwetu sisi kuwaelimisha wadau kuhusu shughulim zetu na ndio maana huwa tuko tayari wadau wetu wanapotualika ili kutoa elimu hiyo.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ……..kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Bw. Eric F. Shitindi amewahimiza washiriki wa kuzingatia elimu watakayoipata kwenye mafunzo hayo ili hatimaye watekeleze ipasavyo malengo ya serikali ya awamu ya nne ya kujenga uchumi wa kati ifikapo mwak 2025.

“Ni matarajio yetu kwamba Tume na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, mnao wajibu mkubwa sana katika kufanikisha azma hiyo ya serikali kama nyinyi mtatekeleza wajibu wenu.” Alisema.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Edrisa Mavura, akitoa hotuba yake.
Maafisa wa CMA wakiteta jambo.
Bw. Mshomba, (kulia), na Bw.Nungu, wakijadili jambo.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akikaribishwa na Wakurugenzi wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia) na wa CMA, Bw.Shanes Nungu, alipofika kufungua mafunzo hayo
 Bw. Mshomba akijibu baadhi ya maswali ya washiriki kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya washirtiki wakifuatilia mafunzo.
Kamishna wa Tume, Bi.Suzanne Ndomba, (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo. Wengine ni Makamishna wenzake, kutoka kushoto, Bw.Kibwana Njaa, Bw.Jones Majura na Bw.Jaffary Ally Omar.
Picha ya pamoja.
Bw. Mashomba akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar.
Washiriki wakipitia vipeperushi vya WCF.

KATIBU UVCCM IRINGA MJINI ANUSURIKA KUFA BAADA KITU CHENYE MLIPUKA KURUSHWA KITANDANI KWAKE

$
0
0
Aelezea hatua kwa hatua namna nyumba yote ilivyoteketea kwa moto.


Na Said Mwishehe-Globu

KATIBU wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Alophance Myunga amenusurika kifo baada ya kitu chenye mlipuko kurushwa dirishani kwake na kufikia kitandani huku yeye akiwa amelela na kisha kusababisha moto ulioteketeza nyumba anayoishi yote.

Amesema kutokana na kurushwa kwa kitu hicho ambacho kilisababisha mlipuko mkubwa chumbani kwake na kisha moto kuanza kuwaka alichofanikiwa ni kuchukua simu yake ya mkononi tu huku vitu vingine vyote vikiteketea kwa moto.

Akizungumza na Michuzi Blogu kwa njia ya simu leo , Myunga amesema yeye ni moja kati ya wapangaji saba wanaoishi kwenye nyumba ambayo wanaishi na chumba ambacho kilianza kuwaka moto ni cha kwake.


ASIMULIA MOTO ULIVYOANZA CHUMBANI KWAKE

Katibu huyo wa UVCCM Wilaya ya Iringa amesema kuwa kwenye mida ya saa saba usiku akiwa amelala chumbani kwake alisikia dirisha lililopo chumbani kwake likivunjwa.Hata hivyo aliogopa kuchungulia kwani hakujua wanaofanya hivy wanalengo gani dhidi yake.

Ameongeza wakati anaendelea kutafakari huku akiwa bado yupo kwenye itanda chake alishangaa kuona amerushiwa kitu ambacho hawezi kukielezea ni cha aina gani lakini ghafla kikaangukia chini na kusababisha kulipuka na moto kuanza kuwaka.

"Naogopa kusema ni kitu aina ya bomu au laa.Maana si mtaalamu wa kutambua aina ya kitu ambacho kimerushwa chumbani.Niseme tu baada ya kitu hicho kurushwa kitandani na kudondokea chini, moto ukaanza kufuka na kisha kulipuka.Nilichofanikiwa ni kuchukua simu na Kompyuta mpakato na kisha kukimbilia nje.

"Nilipotoka nje na wapangaji wenzangu nao wakatoka na kuanza kuulizana nani amefanya tukio hilo.Tayari tumetoa taarifa Polisi jana usiku baada ya nyumba kuungua na hivyo tunasubiri watakachobaini kilichosababisha nyumba kuchomwa na waliohusika kufanya tukio hilo,"amesema.

ANAHISI NINI BAADA YA TUKIO HILO?

Kuhusu swali hilo, amejibu kuwa anachoamini sababu kubwa itakuwa ni mambo ya siasa kwani yeye si mfanyabashara na hana kazi nyingine zaidi ya siasa na siku za karibuni kuna moja ya kiongozi wa kisiasa wa upande wa upinzani alimtishia kwa bastola.

"Mbali ya kunitisha kwa bastola aliniambia kuwa nitakiona na lazima atanihamisha Iringa kwani najifanya mjanja kwa kuwa nimetoa Dar es salaam.Huyu kiongozi(jina tunalo) ndio atakuwa adui yangu namba moja na ndio namhisi atakuwa kafanya tukio hilo.

"Inaonesha kabisa walikuwa wamedhamiria kuniuua mimi na ndio maana walvunja dirisha la chumbani kwangu na kurusha kitu hicho ambacho kilisaabisha mlipuko uliofanya moto kuanza kuwaka.Hata hivyo acha Jeshi la Polisi Iringa nalo lifanye kazi yake ya kuchunguza na ukweli utapatikana,"amesema.
 Baadhi ya vitu vilivyoteketea kufuatia mlipuko huo.
 Hivi ndivyo huo mlipuko ulivyoteketeza vitu hivyo



Baadhi ya ndugu jamaa na majirani wakishuhudia tukio hilo

DK.MABODI AIPONGEZA SMZ

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema mafanikio yliyofikiwa na Serikali ya awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ni kielelezo tosha cha kuenzi kwa vitendo Mapinduzi hayo ya Januari 12, mwaka 1964.

Udhibitisho huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ wakati akitoa tathimini yake juu ya hotuba ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein aliyoitoa katika kilele cha wamaadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi zilizofanyika Uwanja wa Amaan Mjini hapa.

Dk. Mabodi alisema mambo yaliyotajwa katika hotuba hiyo ni sehemu ya mafanikio ambayo kila mwananchi anatakiwa kujivunia kwani ni hatua ya maendeleo yanayotokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote.

Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza mambo mbali mbali ya kimaendeleo bila kujali changamoto na vikwazo vya kisiasa kwa lengo la kurahisisha upatanaji wa huduma za msingi kwa wananchi waliopo mijini na vijijini.

Alieleza kuwa mambo yaliyotolewa ufafanuzi wa kina ndani ya hotuba hiyo ya Dk.Shein ni pamoja na kuimarika kwa sekta ya uchumi ambapo makusanyo ya mapato yamefikia shilingi bilioni 548.571 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na shilingi bilioni 487.474 zilizokusanywa katika mwaka 2016.

Alisema kwa mujibu wa hotuba hiyo imetaja kasi ya ukuaji wa uchumi kwa bei halisi imekua kwa asilimia 7.0 kwa mwaka 2017, ikilinganishwa na asilimia 6.8 kwa mwaka 2016, hatua inayopongezwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar.

Naibu Katibu mkuu huo anaendelea kueleza kuwa kutokana na juhudi za serikali chini ya usimamizi wa CCM pato la mtu mmoja limetajwa kufikia shilingi 1,806,000 ikilinganishwa na shilingi 1,632,000 kwa mwaka 2015.

Pia alieleza kuwa kasi ya mfumuko wa bei imefikia asilimia 5.6 katika mwaka 2017 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2016.

“Mafanikio yote hayo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi tulizotoa kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu wa dola uliopita kwa hiyo tunaendelea kutekeleza kwa kasi kubwa ili ikifikia uchaguzi mkuu ujao tuwe tupo katika kiwango cha kuridhisha katika utatuzi wa kero za wananchi.”, alisema Dk.Mabodi.

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha ni kuimarisha uchumi,kupunguza umasikini na kuifanya Zanzibar kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kiwango cha kati ifikapo mwaka 2020 huku ikijipanga kufikia kiwango cha nchi za visiwa zilizoendelea duniani.

Dk.Mabodi aliisifia serikali kwa hatua zake za miradi mikubwa 25 ambayo ikikamilika itatoa ajira 915 kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar.

Akizungumzia sekta mama ya Utalii nchini alisema katika hotuba ya Dk.Shein imeweka wazi kuimarika kwa Nyanja hiyo ambayo imeingiza jumla ya watalii 433,116 nchini katika kipindi cha mwaka 2017,ikilinganishwa na idadi ya watalii 379,242 walioingia nchini katika mwaka 2016 ambalo ni ongezeko la asilimia 14.2.

“Sina shaka na ahadi ya Rais wetu mpendwa Dk.Shein ya Serikali kufikia idadi ya watalii 500,000 ifikapo mwaka 2020”,, Dk.Mabodi alipongeza juhudi hizo na kutoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha dhana ya utalii kwa wote.

Pamoja na hayo Dk.Mabodi alisema serikali chini ya usimamizi wa CCM imekuwa mstari wa mbele kuimarisha sekta ya Elimu ambayo ni chimbuko na uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi yoyote duniani kwa kuzalisha wataalam wa fani mbali mbali wanaosaidia kutekeleza sera za kisiasa ili ziendane na mahitaji halisi ya wananchi.

Kupitia tathimini ya hotuba hiyo Dk.Mabodi alisifia tamko la Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein la kuwatangazia wananchi kuwa kuanzia mwezi wa Julai 2018, serikali itaanza kutekeleza azma ya kurudisha utaratibu wa elimu bure kwa ngazi za msingi na sekondari ili kutekeleza shabaha ya Mapinduzi.

Mbali na tamko hilo pia Dk.Mabodi alisema CCM inaunga mkono msimamo wa Serikali kutoa pencheni jamii kwa wazee wote waliofikia umri wa miaka 70 , bila kuzingatia kazi walizokuwa wakifanya ambapo jumla ya wazee 27,627 wamelipwa jumla ya shilingi bilioni 10.175 tangu utaratibu huo umeasisiwa mwezi April 2016, kwa kila Mzee kupewa sh.20,000 kwa mwezi.

Naibu Katibu Mkuu huyo Dk.Mabodi alifafanua kuwa suala la maendeleo halitakiwi kuchanganywa na tofauti za kisiasa, kidini na kikabila kwani linawahusu wananchi wote hivyo wasikubali baadhi ya wanasiasa waliofilisika kwa hoja wawagawe kupitia kivuli cha siasa zilizopitwa na wakati.

Mahakama kwenda Kidijitali

$
0
0
 Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bi. Penina Henjewele akitoa Mada ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) kwa Washiriki wa Mafunzo hayo (hawapo pichani) 
 Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiongea jambo na Washiriki katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Sehemu ya Wahasibu na Makarani wa Mahakama wakiwa katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja

Na Mary Gwera, Mahakama

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya malipo yote ya huduma zake na ukusanyaji wa mapato kielektroniki ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na vilevile kuboresha huduma kwa manufaa ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso Januari 16, alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Mahakama kama ilivyo kwa Taasisi nyingine za Serikali imejiunga katika Mfumo huu ili kufanya ukusanyaji wa Mapato na malipo yote ya Huduma za Mahakama kufanywa kwa njia ya Kieletroniki, kwa hiyo ili kuwezesha matumizi ya mfumo huu yameandaliwa mafunzo haya maalum kwa Watumiaji katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi hii,” alifafanua Bw. Uisso.

Alitaja kuwa kwa kuanzia mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yameshirikisha jumla ya Watumishi 35 wa Mahakama kwa Mkoa wa Dar es Salaam, akitaja watumishi hao kuwa ni pamoja na Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Makarani kutoka Makao Makuu na ngazi zote za Mahakama kwa mkoa huu.

“Tunatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine kwa awamu, ili kuiwezesha Mahakama nchi nzima kutumia mfumo huu,” aliongeza Bw. Uisso.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo Msaidizi anasema kuwa Mfumo wa sasa unaotumika na Mahakama una changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na baadhi ya Mahakama kutowasilisha ‘bank slip’ kwa wakati, fedha kuingizwa kwenye akaunti ambazo sio za Mahakama n.k 

Bw. Uisso anaongeza kuwa Mfumo huu umekuja wakati muafaka kwa Mahakama ambapo kwa sasa ipo katika maboresho ikiwa ni pamoja na kuwa na mpango wa kuanzisha ‘e-Judiciary’ ili kuboresha mfumo wa usimamizi wa mashauri na ukusanyaji wa takwimu.

Kwa upande wake Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bi. Penina Henjewele aliwatoa hofu Washiriki wa Mafunzo hayo kuwa mfumo huo ni rafiki kutumia hivyo wasiwe na wasiwasi katika utekelezaji.

“Mfumo huu ni rafiki sana kutumia, vilevile unaokoa muda, hivyo basi msiwe na wasiwasi mtaelewa na kufanya vizuri cha msingi ni kufuata taratibu na maelekezo yanayokuwa yakitolewa,” alisema Bi. Henjewele.

Mafunzo hayo ya siku tano (5) yanaendeshwa na Wawezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mfumo huu wa ‘GEPG’ uliandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wadau wengine.
Tayari Mfumo huo umeshaanza kutumiwa na baadhi ya Taasisi za Serikali kama Wizara ya Ardhi, Wakala wa Misitu, Jeshi la Polisi-Kitengo cha Usalama Barabarani ‘Traffic’ na baadhi ya Halmashauri za Serikali za Mitaa.

Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifanya upasuaji kwa wagonjwa

$
0
0
  Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa ambaye mshipa mkubwa unaosambaza damu upande wa kushoto  wa moyo umeziba upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting). 
 Madaktari  Bingwa wa Usingizi na wagonjwa mahututi  wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia jinsi moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi (mapigo ya moyo)  kwa kutumia mashine maalum wakati mgonjwa huyo akifanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).
Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Benjamin Bierbach wa nchini Ujerumani wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu ya moyo mtoto mwenye  umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT. ... N MAGUFULI KUHUSU ELIMU BURE


SALAAM ZA MWENYEKITI WA BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA SIKU YA POSTA AFRIKA 2018

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa salamu zake katika kuadhimisha Siku ya Posta Afrika kesho, Januari 9, 2018. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya viongozi wa vitengo vya Shirika la Posta wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitoa salamu zake katika kuadhimisha Siku ya Posta Afrika kesho Januari 9, 2018. 
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, jijini leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitoa salamu zake katika kuaadhimisha Siku ya Posta Afrika kesho.
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakiwa katika mkutano huo jijini leo.
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakisikiliza, salamu zilizokuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, mbele ya waandishi wa habari, katika kuaadhimisha Siku ya Posta Afrika jijini Dar es Salaam kesho.
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo akitoa salamu zake katika za maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika, mbele ya waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha TPC, Elia Madulesi (kulia) na Meneja Msaidizi wa Huduma za Barua, Jasson Kalile, wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa mbele ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari, mara baada ya kutoa salamu zake za  maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika.
Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang'ombe, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa wafanyakazi na wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia mkutano huo.


KESHO tarehe 18/01/2018, Shirika letu la Posta litaungana na Mashirika mengine Afrika kuadhimisha kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) mnamo mwaka 1980.


Umoja huu makao makuu yake yapo Arusha Tanzania. Lengo la kuanzishwa Umoja huu ni kusimamia maendeleo ya Posta Afrika.


Pamoja na salaam zangu kwa Katibu Mkuu wa Umoja huu Bwana Younouss Djibrine na watendaji wenzake, napenda kuwapongeza wanaposherehekea miaka 38 ya Umoja huu.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “POSTA: Muundombinu muafaka kwa Serikali katika kufikia Malengo yake ya Maendeleo”.


Kutokana na Posta kuwa na matawi mengi yaliyosambaa katika nchi kuliko watoa huduma wengine hapa nchini, tunapongeza kauli mbiu hii na kwa kweli Shirika limejipanga katika kuhudumia wananchi katika kuwezesha mafanikio yao kibiashara, kama mnavyofahamu mwaka jana 2017 Shirika letu liliibuka kidedea katika kundi la watoa huduma (Trade Facilitation) na kukabidhiwa ngao ya ushindi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli..


Shirika letu limeanza mikakati ya kufungua vituo “Huduma Express” hapa Posta Mpya Dar es salaam na vingine vitaanza Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya na Zanzibar. Katika vituo hivi tunaweza kutoa huduma mbalimbali mahali pamoja “One-Stop-Centre” na hii itasaidia sana Serikali kutoa huduma zake kwa wananchi kwa urahisi zaidi. Hii inaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu. “POSTA kama Muundo Mbinu muafaka kwa Serikali katika kufikia malengo yake ya maendeleo”.


Pia Dk. Kondo alitumia fursa hiyo kuelezea kwa muhtasari mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo Shirika lilikabiliana nazo mwaka jana 2017.

Alielezea kuwa Shirika kwa ujumla lilipata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuzindua nembo mpya mwezi Desemba 2017 na sasa liko kwenye maandalizi ya kuboresha muonekano wa Shirika katika ofisi zake nchini kote.


Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya wenye fanaka 2018.


Lt. Col. Mstaafu. Dr. Haruni Kondo

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA 

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO WA GYPSUM KUWA NA UMOJA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwasili kijiji cha Hoteli Tatu, Kata ya Mandawa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kwa ajili ya kuembelea kampuni ya Universal Mining Ltd kujionea hali ya uzalishaji wa jasi (Gypsum) unavyoendelea wakati wa ziara ya Siku tatu katika Mkoa wa Lindi na Mtwara, Leo 17 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko  akikagua uzalishaji wa madini aina ya Jasi (Gypusm) katika kijiji cha Hoteli Tatu, Kata ya Mandawa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, Leo 17 Januari 2018.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko  akizungumzia umuhimu wa wachimbaji wadogo kuwa na umoja ili kukuza ufanisi na tija katika kupanga bei ya rasilimali wanazozalisha wakati alipozuru kijiji cha Hoteli Tatu, Kata ya Mandawa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, Leo 17 Januari 2018.


Na Mathias Canal, Lindi


Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko Leo 17 Januari 2018 amewataka wachimbaji wadogo wa madini Jasi(Gypsum) kuwa na umoja na mshikamano katika uuzaji madini hayo na kuwa na kauli moja katika ushiriki wa soko la bidhaa hiyo.


Mhe Biteko ameyasema hayo alipotembelea katika kijiji cha Hoteli Tatu, Kata ya Mandawa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Siku tatu katika Mkoa wa Lindi na Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na makundi ya wachimbaji wadogo ili kubaini changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.


Alisema kuwa kila mchimbaji anajipangia gharama aitakayo yeye pasina kushirikiana na wachimbaji wengine ili kuwa na bei moja ambayo itakuwa na tija na manufaa kwa kila mmoja hivyo kupitia umoja wao watakuwa na kauli na maamuzi ya pamoja yenye tija na faida kwao.


Mhe Biteko aliwashauri wachimbaji hao kuwa na umoja utakaokuwa na uwezo wa kudai bei itakayofanana kwa wote pia kuwa na uwezo wa kutengeneza sheria ndogondogo ambazo zitatumika kujisimamia wao wenyewe.


Aidha, amezitaja Changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi sambamba na wachimbaji wadogo hususani ubovu wa barabara ambapo ameishauri Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kusaidia utengenezaji wa Barabara itakayorahisisha usafirishaji wa jasi (Gypusm) na kurahisisha huduma za wananchi ili kufika kwa urahisi katika Barabara kuu.


Mhe Biteko alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli itaendelea na juhudi zake za kuweka miundombinu rafiki kwa ajili ya wananchi, wawekezaji, na wachimbaji (wakubwa na wadogo) hivyo ili kufikia adhma ya mafanikio hayo ni lazima kusema na kutekeleza maelekezo yote ili kupiga hatua za maendeleo.


Alibainisha kuwa nia ya sekta ya madini ni kufanya mchakato wa kuongeza pato la Taifa kufikia asilimia 10% tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo sekta ya madini inachangia kiasi kidogo kwenye pato la Taifa.

KAMATI YA RAIS YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE YAANZA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA TANZANITE ONE

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi   akisalimiana  jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018   na wawakilishi wa kampuni ya Tanzanite One kabla ya kuanza na mazungumzo ambayo yanalenga kuhakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini hayo ambayo yanachimbwa nchini Tanzania pekee. Picha na IKULU

SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo kutoka kwa Kapteni Desiderius Chuwa wa Meli ya MV. Clarias kuhusu usalama wa chombo hicho na abiria wake kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani Mwanza.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kuhusu usalama wa abiria na matumizi ya vifaa vya uokoaji majini kwa watendaji na abiria wa meli ya MV. Clarias kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akipatiwa maelezo kuhusu matengenezo ya yaliyofanyika ya mfumo wa mafuta wa meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akikagua meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi (kushoto) akitoa maelezo kuhusu meli hiyo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) alipokagua meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) ikiwa tayari kusafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Kampuni ya Huduma za Meli kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusu ujenzi na ukarabati wa meli katika maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa wakati wa kikao na Kamati hiyo kilichofanyika bungeni mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa wa Bodi wa Kampuni hiyo Bi. Rose Lugembe.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi bilioni 24.496 kwa ajili ya kujenga meli mpya mbili na kukarabati meli tano ili ziweze kutoa huduma ya uchukuzi wa kusafirisha abiria na mizigo katika maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ujenzi wa meli katika maziwa makuu kwenye kikao kilichofanyika bungeni mjini Dodoma. Mhe. Nditiye aliongeza kuwa fedha hizo tayari zimeshatolewa na Serikali na kupatiwa Kampuni ya MSCL kwa ajili ya kuanza ujenzi wa meli 2 mpya za kubeba abiria na mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria na kukarabati meli 5 ambazo ni MV. Victoria, MV. Butiama, MV. Liemba, MV. Umoja na MV. Serengeti.  
Mhandisi Nditiye aliongeza kuwa lengo la Serikali la kutoa fedha hizo ni kuboresha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu ili wananchi waweze kupata huduma za usafiri wa uhakika; kwa wakati na zinazozingatia usalama wa abiria na mizigo yao; kuiwezesha Serikali kupata mapato na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla; na kwa kutambua fursa ya biashara iliyopo kwenye maziwa hayo kwa kuzingatia kuwa meli hizo ni kiungo kikubwa baina ya nchi yetu na nchi za jirani za Uganda, Kenya, Zambia, Malawi na DRC Congo kwa kuwa zinatumia meli zetu kusafirisha abiria na mizigo yao kupitia maziwa hayo.
Aidha, Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya MSCL Bwana Eric Hamissi alifafanua kuwa tayari Kampuni yake kwa kushirikiana na wataalamu wa Kampuni hiyo na wengine kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) na Jeshi la Wananchi Kitengo cha Wanamaji (TPDF Navy Command) wamekamilisha taratibu za kumpata mkandarasi wa kujenga meli mpya ya Ziwa Victoria ambaye ni mkandarasi wa Kampuni ya STX Engine Co. Ltd na STX Offshore & Shipbuilding Co. Ltd Joint Venture; na mkandarasi wa Kampuni ya KTMI kwa kushirikiana na Kampuni ya Yuko’s Enterprises Co. Ltd  kwa ajili ya kukabarati meli za MV. Victoria na Butiama ambapo kampuni zote ni za kutoka nchi ya Korea ya Kusini. Bwana Eric alisema kuwa Kampuni hizo zimekidhi vigezo vya mahitaji ya meli ya kubeba abiria na mizigo na zina teknolojia ya kisasa ya ujenzi na ukarabati wa meli ili kufikia azma ya Serikali ya kutoa huduma nzuri kwa abiria na wananchi wake. Mkataba wa ujenzi wa meli mpya unatarajiwa kusainiwa mwezi Februari, 2018 na wa ukarabati utasainiwa mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla King ameiipongeza Serikali kwa kutoa fedha za kujenga na kukarabati meli za maziwa makuu ya Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa. Aidha, Prof. Norman Sigalla King ameishauri Serikali iajiri wafanyakazi wa meli wenye vigezo vya kimataifa kwa kuwa wengi waliopo wanakaribia kustaafu na ameitaka MSCL kutumia fedha hizo kama zilivyopangwa na kwa wakati ili wananchi wapate huduma za usafiri bora zaidi kwenye maziwa makuu.
Mhandisi Nditiye alifafanua kuwa Serikali inakabiliana na changamoto ya upungufu wa manahodha wa meli kwa kuzalisha wataalamu hao wenye weledi wa kisasa kutoka kwenye Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI na Jeshi la Wananchi Kitengo cha Wanamaji (TPDF Navy Command). Katika hatua nyingine, Mhandisi Nditiye aliwataarifu wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Mwezi Januari mwaka huu alifanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo alitembelea na kukagua utendaji kazi wa Kampuni ya MSCL ikiwa ni pamoja na kukagua meli ya MV. Clarias ambayo imeanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Nansio-Ukerewe baada ya kufanyiwa ukarabati wa mfumo wa mafuta, injini na sehemu za kukaa abiria ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa meli hiyo wazingatie usalama wa abiria na mizigo na kuwapatia elimu ya vifaa vya uokoaji majini wanapokuwa safarini ili waweze kujiokoa na kujinga na ajali wakiwa safarini pindi itakapotokea.
Bwana Eric Hamissi alifafanua kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetoa shilingi milioni 300 ambazo zimetumika kukarabati meli nne za Kampuni ya MSCL za kubeba mizigo na abiria ambazo ni MT. Sangara, MV. Clarias, ML. Wimbi na MV. Umoja ambazo zimeanza kazi na zitaiwezesha Kampuni ya MSCL kujiendesha, kufanya kibiashara na kuongeza mapato ya Serikali kwa kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye mwambao wa maziwa makuu na nchi za jirani.
Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ina jukumu la kutoa huduma za usafiri wa majini kwa kutumia meli zake katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa na kujiendesha kibiashara kupitia huduma zake. Kampuni hii inasafirisha abiria na mizigo kwa safari za ndani na nje ya nchi zilizoko katika mwambao wa maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

ZANTEL YAZINDUA KAMPENI YA ‘JERO YAKO TU' KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

$
0
0








Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary na kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi.




Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi (kushoto) na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) (kulia).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary akijaribu moja ya Pikipiki ambazo zitakazoshindaniwa kila wiki kwenye Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkuu wa Zantel, Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha).
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images