Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Watendaji Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Wapewa Mafunzo ya Bajeti Kijinsia

$
0
0

 Meza kuu ikiwasilisha hotuba zake kwa washiriki wa mafunzo.


Mkurugenzi wa Mashirika yasio ya Kiserikali toka wizara hiyo, Marcel Katemba akisoma hotuba ya Katibu Mkuu


Mkurugenzi wa Mashirika yasio ya Kiserikali toka wizara hiyo, Marcel Katemba akizungumza kabla ya kufungua mafunzo.

 Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo ya kijinsia
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada anuai.

 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada anuai.
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo

===========  ==========  ============
Watendaji Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Wapewa Mafunzo ya Bajeti Kijinsia .

Na Mwandishi wa Thehabari.com

VIONGOZI wakuu na watendaji wa idara mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini leo wamepewa mafunzo ya namna ya kuandaa bajeti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mafunzo hayo ya siku nne yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yameandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia taasisi yao ya Chuo cha Jinsia (GTI), ambapo washiriki hao kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wanawezeshwa kuandaa bajeti kwa mtanzamo wa kijinsia.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanasaidia kujenga stadi na maarifa kwa viongozi na watendaji wakuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuzingatia masuala ya jinsia kwenye bajeti ya Wizara hiyo.

Alisema ni mafunzo yanayounganisha utashi wa kisiasa kwa kuzingatia masuala ya jinsia na usawa serikalini, ili kupunguza mapengo yaliyopo inabidi kuwekeza fedha na rasilimali anuai.

alisema nadharia iliyopo kwenye sera inaweza kutekelezeka endapo kutakuwa na uwezeshaji wa rasilimali na fedha ili kuhakikisha huduma za kijamii zinatekelezwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi yote yaani wanawake na wanaume. 

Aidha aliongeza kuwa mara nyingi mahitaji ya kundi la wanawake yamekuwa yakisahaulika jambo ambalo lina onesha kuna kila sababu ya kuwawezesha watendaji wizara husika kiuchambuizi wa sera na bajeti kwa mlengo wa kijinsia na kuainisha mapungufu kama hayo ili yaweze kufanyiwa kazi.

Alisema kundi la wanawake bado limekuwa na changamoto hasa katika huduma za afya, elimu na yinginezo ambazo zinaongeza mzigo kwa wanawake. Ameitaka Serikali kuongeza uwekezaji katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, na kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo vya uamuzi ili kuleta usawa wa kijinsia.

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ndiyo wizara yenye dhamana katika usimamizi wa masuala ya kijinsia nchini Tanzania na usimamizi wa sera ya jinsia na uratibu wa vitengo vyote vya jinsia...hivyo ni muhimu kwa watendaji wake kuwa na uelewa kwa kutosha, uwezo wa kirasilimali na rasilimali watu ili watendaji hao waweza kufanya ufuatiliaji wa kutosha katika utekelezaji wa masuala anuai kwenye bajeti.

Alisema wakati TGNP ikijiandaa kuadhimisha miaka 20 ya utendaji wake licha ya uwepo wa changamoto kadhaa, yapo mafanikio ambayo yanaonekana katika juhudi za mapambano ya harakati za kijinsia kupitia taasisi hiyo.

"Mabadiliko yoyote ya kijamii ni mchakato na miaka 20 ni mingi, tungetarajia tuwe tumepiga hatua kubwa zaidi, lakini kwanza ni vizuri kutambua juhudi zilizofanywa zimeanza kuzaa matunda kwenye maeneo mengi, miaka 20 iliyopita hata dhana ya jinsia haikuwepo kwenye mazungumzo yetu hata dhana ya mfumo dume ilikuwa haipo lakini kwa sasa wanawake na wanaume wanakaa pamoja na kuzungumzia masuala hayo," alisema Bi. Mallya.

Naye Mkurugenzi wa Mashirika yasio ya Kiserikali toka wizara hiyo, Marcel Katemba akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu alisema serikali inajitahidi katika upangaji na utekelezaji wa bajeti maeneo anuai ili kuhakikisha makundi yote yananufaika na rasilimali za taifa.

Akifafanua juu ya kuendelea kwa hali ya unyanyasaji wa kijinsia katika baadhi ya maeneo licha ya juhudi za kupambana na vitendo hivyo alisema serikali inaendelea na utoaji wa elimu ya uelewa juu ya masuala ya haki, kwani jamii ikielewa vitendo kama hivyo vitakoma mara moja. 

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

KOCHA SUPER D ,YASSIN ABDALA WAMPOKEA FRANCOIS BOTHA LEO PAMOJA NA RAIS WA WBF

$
0
0

Mgeni rasmi katika mpambano wa Kimataifa wa Ubingwa wa WBF Bondia bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu Zamani, Francois Botha 'Wwite Buffalo' katikati baada ya kupokelewa alipowasili katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam leo.Wengine kushoto ni Raisi wa TPBO Yassini Abdalla na Rais wa World Boxing Federation ,Howard Goldbeg pamoja na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  Mpambano wa ubingwa wa Dunia wa chama hicho unafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuwakutanisha Mabondia Fransic Cheka na Phil Williams wa Marekani siku ya August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya ijumaa hii -

BONDIA WA DUNIA FRANCOIS BOTHA WA PILI KUSHOTO AKIWA NA JAY MSANGI RAISI WA WBF ,HOWARD GOLDBEG,YASSINI ABDALL, NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila wa pili kutoka kulia akifuraia jambo na Francois Botha pamoja na yassini Abdalla kulia

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwafikisha wageni katika hotel ya Southern sun wa pili ni Rais wa WBF, Howard Goldbeg, Rais wa TPBO, Yassini Abdallah na mmoja wa Majaji wa mpambano huo pamoja na Bondia bingwa wa Uzito wa Juu Duniani Francois Botha Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BONDIA WA DUNIA FRANCOIS BOTHA WA PILI KUSHOTO AKIWA NA JAY MSANGI RAISI WA WBF ,HOWARD GOLDBEG,YASSINI ABDALL, NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'

vyoo vya shule ya msingi Ukange makete ni majanga

$
0
0
Muonekano wa choo hicho kwa mbele kutokana na kukosa milango wamelazimika kutengeneza uzio wa nyasi.
Kushoto ndiyo tundu halisi la choo, na tundu la kulia limetokana na choo hicho kubomoka chenyewe.

 Nyufa zilizomo kwenye kuta za choo hicho.

=============================
Na Edwin Moshi, Makete.

Wanafunzi wa shule ya msingi Uganga kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani Njombe wapo hatarini kupoteza maisha yao kutokana na vyoo wanavyovitumia kubomoka na kuweka nyufa na matundu makubwa kutokana na uchakavu.

Mtandao huu umebisha hodi shuleni hapo hivi karibuni ka kukuta vyoo hivyo vinavyotumiwa na wanafunzi vikiwa katika hali mbaya huku wanafunzi hao wakiendelea kuvitumia bila wasiwasi.

Mwanafunzi mmoja anayesoma darasa la tano katika shule hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni amesema haoni shida kutumia vyoo hivyo kwa kuwa hakuna sehemu nyingine ya kujisaidia na kuongeza kuwa licha ya hatari ya kupoteza maisha waliyonayo wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo lakini bado wataendelea kuvitumia.

Akizungumzia suala hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Danie Kyando amekiri kuwepo kwa vyoo hivyo chakavu na kusema kuwa ameshapeleka kwenye ngazi husika suala hilo ambapo amejibiwa kuwa litafanyiwa kazi.

Amesema kwa hivi sasa wanamuomba Mungu isitokee hatari yoyote kwenye vyoo hivyo katika kipindi hiki wanaposubiri wakubwa kulishughulikia suala hilo kama walivyomuahidi ingawa ni muda mrefu umepita.

"Mimi katika taarifa zangu wakati mwingine huwa naandika kuwa shule haina vyoo vya wanafunzi kutokana na uchakavu hebu ona mwenyewe vyoo gani hivi, hii si hatari tupu, matundu mengine tumeziba na magogo ili wanafunzi wasiingie" alisema.

Shule hiyo ambayo inadhaniwa kuanza miaka ya 1970 inakabiliwa na changamoto lukuki ikwemo majengo kwa kuwa mengi yamechakaa.

KITENGO CHA KUDHIBITI UGONJWA WA MALARIA ZANZIBAR CHAFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI JUU YA MIKAKATI YA KUMALIZA MALARIA ZANZIBAR

$
0
0
Kaimu Meneja wa Kitengo cha kudhibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Mwinyi Issa Mselem akifafanu kitu juu ya mikakati ya kumaliza Malaria Zanzibar katika mkutano na Waandishi wa Habari, huko katika ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar.
Mtaalamu wa mbu waenezao Malaria katika Kitengo cha kudhibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Khamis Ameir, akionyesha moja mbu waenezao Malaria katika mkutano na Waandishi wa Habari huko katika ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliokuwepo katika ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar, wakifuatilia kwa makini taarifa ya Kaimu Meneja wa Kitengo cha kuzibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Mwinyi Issa Mselem hayupo pichani.
Mwandishi wa Habari Juma Abdallah wa Zenji Fm Radio akiuliza suali kwa Mtaalamu wa mbu waenezao Malaria katika Kitengo cha kuzibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) Khamis Ameir (hayupo pichani) juu ya mikakati ya upigaji dawa huko katika ukumbi wa kitengo cha kuzibiti Malaria mwanakwerekwe Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanziabr).

MDAU BOKHE ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWAKE

$
0
0
2
Bokhe akikata keki kama ishara ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake katika hafla fupi ya chakula cha jioni iliyofanyika Kebbys Hotel Mwenge jijini Dar es salaam jana ambapo alijumuika na marafiki zake pamoja na baadhi ya ndugu zake.5Hapa akimlisha keki rafiki yake Sinta.
4Hapa akimlisha keki ndugu yake Getu.3Akimlisha keki ndugu yake Winnie.
10Bokhe akiwa na Winnie kushoto na Sauda katika picha15Akimlisha keki rafiki yake Sauda wa Nguvu13Story kidogo kabla ya kukata keki .9Bokhe kulia Winnie Kushoto na Getu wakipozi kwa picha6Bokhe akifurahi na marafiki zake

J'mosi Hii @ Grooveback-Arcade!

POLISI MAKETE LAWAMANI

$
0
0
Na Edwin Moshi, Makete
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani Makete mkoani Njombe limeingia lawamani kufuatia kutwishwa tuhuma nzito za kutoza faini kwa madereva pikipiki bila kuwapa risiti ya fedha hizo

Baadhi ya madereva bodaboda waliozungumza na mtandao huu wamesema wamekuwa wakikamatwa na askari hao wa usalama barabarani huku akimtaja kwa jina askari ambaye amekuwa kinara wa kuwatoza faini bila kuwapa risiti (jina tunalihifadhi kwa sasa)

Tuhuma hizi zimetolewa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM kwenye kijiji cha Ndapo na Kinyika wilaya ya Makete ulioongozwa na mwenyekiti wake Bw. Francis Chaula uliofanyika katika kata ya Matamba wilayani hapo ambapo pamoja na mambo mengine aliruhusu wananchi kutoa kero zao ndipo lilipoibuka suala hilo

Wamesema wamekuwa wakitozwa faini ya zaidi ya shilingi laki tatu pasipo kupewa risiti na pindi wanapohoji huambulia kipigo kutoka kwa askari hao

Akizungumza wakati wa kujibu suala hilo mwenyekiti wa CCm wilayani hapo Bw Francis Chaula amesema askari hao hawana haki ya kuwapiga madereva hao na pia kitendo wanachokifanya cha kutoza faini bila risiti ni kinyume na utaratibu wa serikali hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja

Amesema kufuatia tuhuma hizo viongozi wa jeshi la polisi wilayani hapo wanatakiwa kuchukua hatua haraka na endapo askari hao watabainika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria

Jeshi la polisi kupitia kwa afisa upelelezi wake Bw. Gosbert Komba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya amesema vitendo hivyo havikubaliki kisheria huku akiongeza endapo suala hilo likichunguzwa na kubainika lina ukweli sheria itachukua mkondo wake kwa askari hao

Bw Komba amesema madereva nao wana wajibu wa kuelewa sheria inasema nini hasa pale wanapokamatwa na makosa na kusema kuwa faini hulipwa kwenye kituo cha polisi na risiti ya malipo hayo hutolewa na kutaka kushirikiana na jeshi hilo kufichua wale wanaokiuka utaratibu huo ili wachukuliwe hatua

Amesema kwa kufanya hivyo kutaepusha usumbufu usio wa lazima ikiwemo lawama zisizo za msingi ambazo zinaelekezwa kwa jeshi hilo

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KAMATI YA MJI MPYA WA MABWE PANDE

$
0
0
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akimkabidhi Pikipiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, aliyeikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande, Abdallah Kunja.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, akizungumza na wananchi wa Mji mpya wa Mabwe Pande, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wananchi wa mji huo mpya, ambapo Mkuu wa Wilaya, alikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais.
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo baada ya makabidhiano.
Sehemu ya wakazi wa Mji Mpya wa Mabwe Pande waliohudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.Picha na OMR

RADIO IMAAN NA KWANEEMA FM ZAACHIWA HURU

Walimu wawili na wakulima wawili waibuka Washindi wa Promosheni ya Airtel Yatosha

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wakati Airtel ilipochezesha droo ya saba ya washindi wa shilingi milioni moja kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi million 44 zimeshatolewa. Akishuhudia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Bahati nasibu.
Washindi wa siku wa shilingi milioni moja wa promosheni ya Airtel yatosha bwana Thomasi Joackim Chali na Abdallah Omari Muhomba kwa pamoja wakionyesha furaha mara baada ya kukabithiwa zawadi za pesa taslimu baada ya kuibuka washindi wa siku wa promosheni ya Airtel yatosha.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetangaza washindi wake saba wa wiki ya saba ya Airtel Yatosha promosheni na kukabidhi zawadi za washindi wa wiki ya sita wa promosheni ya Airtel Yatosha.

Airtel imechezesha droo ya wiki ya saba ya promosheni ya Airtel yatosha Jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco jijini Dar es saalam ambapo wateja saba wameibuka washindi wa kitita cha shilingi million 1 kila mmoja.

Washindi hao ni pamoja na Theresia Martine Komba wa Morogoro -Mkulima, John Kimoro wa kondo Dodoma -Mwalimu, Yohanna Masunga Zengo wa Maswa Shinyanga -Mkulima, Isabellah Joseph wa Chamwino Dodoma -Mwalimu, Nassor Mohammed Nassor wa Kariakoo DSM -Mfanyabiashara, Modest Laurian Mussa wa Bukoba Kagera -Mfanyabiashara na Masanja Mwanamenda wa Nkyala Singida -Mfanyabiashara.

Wakati huo huo Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Airtel Yatosha ambapo washindi wa wiki ya sita nao walikabidhiwa zawadi zao ambapo kila mmoja aliondoka na shillingi milioni moja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika ofisi za makao makuu ya Airtel bwana Abdallah Omari Muhomba mmoja wa washindi wa million 1 alisema, "nashindwa jinsi ya kuongea lakini nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 1 ambazo kwangu nikama ndoto.

Nategemea kutumia pesa hizi kujiendeleza kiuchumi na maaendeleo ya familia yangu. Binafsi nachukua fursa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama mimi hivi leo".

Kwa upande wake bwana Thomas Joachim Chali ambaye pia ni Mshindi wa wiki ya sita alisema, "anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni yaAirtel Yatosha , na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya".

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema, "leo tunao washindi saba waliojishindia shilingi milioni 1 kila moja katika droo ya wiki. Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Airtel Yatosha.

Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi vya maongezi bila kulipia gharama ya ziada". Aliongeza Mmbando.

Promosheni ya Airtel Yatosha bado inaendelea na wateja wetu wa Airtel Yatosha bado wananafasi ya kuendelea kujishindia pesa taslim na Nyumba mbili za kifahari zilizopo Kigamboni bado kushindaniwa.

Droo itakayomchagua mshindi wa nyumba kwa mwezi huu inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 5/9/2013 saa tano asubuhi. hii itachagua mshindi mmoja kati ya wateja wote waliotumia huduma ya Airtel yatosha kwa mwezi huu.

Ili mteja wa Airtel aweze kushiriki anatakiwa kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha kwa kupiga *149*99# na kujiunga na vivurushi vya Airtel Yatosha. Kila unapojiunga na kifurushi unaingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda.

BONDIA MMAREKANI PHIL WILLIAMS ATUA KUMKABILI CHEKA IJUMAA HII

$
0
0
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na bondia Phil Williams wa marekani baada ya kutua nchini kwa ajili ya mpambano wake na Francis Cheka utakaofanyika August 30 siku ya ijumaa hii  katika ukumbi wa Diamon Jubilee jijini Dar es salaam /
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mchezo huo kushoto ni promota Jay Msangi kulia ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D wengine ni wadau waliokuja kulaki uwanja wa ndege baada ya kutua usiku huu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mdau wa michezo nchini Saidi kindeka kushoto akiwa na Bondia Phil Williams wa marekani
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mchezo huo kushoto ni promota Jay Msangi kulia ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D wengine ni wadau waliokuja kulaki uwanja wa ndege baada ya kutua usiku huu.
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa WBU
Bondia Phil Williams wa marekani akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa WBU
Bondia Phil Williams wa marekani

MH Waziri Mkuu alipokutana na Watanzania Uingereza Part 2

$
0
0
Urban Pulse Creative Media wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wanakuletea Sehemu ya pili katika ziara fupi ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na Watanzania waishio Nchini Uingereza mapema Agosti 2013
Asanteni,
Urban Pulse Creative

WAZIRI ABOUD AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUJADILI SHEREHEA ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohd akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar juu ya suala zima la uboreshaji Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.
 Viongozi  wa vyama vya siasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Mohd alipokutana nao Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa Chama cha Wananchi CUF Salum Bimani akitoa mchango wake katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kufanikisha Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
=======  =======  =======

Khadija Khamis na Amina Shaibu 
wa Habari Maelezo, Zanzibar .


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka viongozi wa vyama vya siasa kushirikiana na kutoa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar . Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Abuod Muhammed alipokutana na wawakilishi wa vyama vya siasa ofisini kwa ke Vuga. 

 Alisema kuwa Serikali imeamua kuzifanya sherehe hizo kuwa za aina yake na zinahitaji mchango wa kila mtu bila ya kuangalia itikadi ya vyama vya siasa ili kuonyesha uelewa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini.

 “Mapinduzi yetu yanafikia nusu karne, tutafanya sherehe kubwa na tumeamua kuyashirikisha makundi yote kuanzia hatua za awali wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wafanya biasha, 
makampuni, taasisi binafsi, waandishi wa habari na makundi mengine ili kufanikisha sherehe hizo,” alisema Waziri Aboud Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa pili wa Rais Alidokeza kuwa mgeni Rasmi katika Sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China na wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki, nchi wanachama wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ulaya pia wamealikwa kushiriki.
 Aidha alisema katika shamrashara za sherehe hizo kutakuwa na ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo, uwekaji wa mawe ya msingi, makongamano na utajengwa mnara maalumu wa miaka 50 ya Mapinduzi ya  Zanzibar . 

 Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Dkt Khalid Salum Muhammed alisema kuwa katika kufanikisha sherehe hizo kumeandaliwa vazi rasmi siku ya kilele cha sherehe hizo yenye rangi za bendera ya Zanzibar. 

 Aliongeza kuwa vipindi maalum na picha za mafanikio ya Mapinduzi katika kipindi cha miaka 50 vitaendelea kuonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vya Serikali na binafsi na changamoto zilizojitokeza ili kuweza kukabiliana nazo katika kipindi chengine cha miaka 50 . 

 Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoongozwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume yatatimiza miaka 50 tarehe 12 Januari 2014 na kilele chake kitachokuwa katika uwanja wa Amaan

TAARIFA MSIBA KUTOKA KWA ANGELLA MSANGI

$
0
0

Angella Michael  Msangi anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Easter Michael Singoye kilichotokea alfajiri ya tar 28.08.2013! Msiba uko kimara bonyokwa -kituo cha kindole! Kwa mawasiliano 0713297408,0782297408 ,mipango ya mazishi inaendelea

TASWIRA KUTOKA UVINZA- KIGOMA KUELEKEA URAMBO-TABORA

$
0
0
 Sehemu ya barabara ikiendelea kujengwa kuanzaia maeneo ya Uvinza mkoani Kigoma kuelekea mkoa wa Tabora na kwingineyo.
 Sehemu ya daraja la mto Malagaras likionekana kwa mbali,ambapo ujenzi wake kwa asilimia kubwa umekwishakamilika. 
 Sehemu ya machimbo ya Chumvi Uvinza mkoani Kigoma kama yaonekanavyo kwa mbaali.
 Mchuma ukipogoma kutoka Tabora kwenda Kigoma
 Sehemu ya ujenzi wa barabara ya Urambo Tabora ikiendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
 Kokoto zikiandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara
 sehemu ya barabara iliyowekwa lami maeneo ya Urambo mkoani Tabora


WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO WAJIVUNIA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo Bw. Philemon Kawamala akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mchango wa wakala huo katika uzalishaji wa mbegu bora za kilimo kwa kipindi cha misimu sita tangu kuanzishwa,wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.

 3149  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji kutoka Wakala wa Mbeg u za Kilimo Bw. Philemon Kawamala(hayupo pichani). PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-MAELEZO.



TAARIFA YA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA) KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa ya wakala wa mbegu za kilimo wa Taifa (ASA) itazungumzia mambo makuu matatu

·         Mchango wa ASA katika uzalishaji wa mbegu bora kwa kipindi cha misimu sita tangu ianzishwe

·         Aina tano za mpunga aina ya AMMKA (Aina Mpya ya Mpunga kwa Africa) zinazopandwa kwenye maeneo ya nchi kavu (Upland rice)

·         Mfumo mpya  wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”

1.     Mchango wa ASA katika kuzalisha mbegu bora kitaifa

Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) ulianzishwa tarehe 23 Juni, 2006 chini ya sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997. Pamoja na majukumu mengine jukukumu kubwa la wakala ni kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora nchini. Msimu wa kwanza  wa 2006/2007 wakala ulizalisha tani za mazao mbali mbali 429  ambapo ilikuwa ni sawa na asilimia 2.6 ya soko la mbegu nchini na hadi kufikia 2011/2012 uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 5,542 sawa na asilimia 19.79 ya soko la mbegu nchini (angalia jedwali na.1)

 Jedwali namba 1: Uzalishaji wa mbegu wa ASA kuanzia 2006/07 hadi 2011/12.

Msimu

Kiasi cha uzalishaji kwa kilo

Kiasi kilichozalishwa na sekta binafsi kwa kilo

Jumla ya kilo zilizozalishwa kitaifa

Asilimia ya mchango wa ASA kitaifa

2006/07

429,000

16,097,000

16,526,000

2.6

2007/08

637,000

16,174,000

16,811,000

3.79

2008/09

918,000

10,511,000

11,429,000

8.03

2009/10

1,882,000

14,633,000

16,515,000

11.4

2010/11

3,092,000

23,462,000

26,554,000

11.64

2011/12

5,542,000

28,000,000

28,000,000

19.79

2.     Aina Mpya ya Mpunga kwa Afrika (NERICA-series)

Kamati ya mbegu ya taifa imepitisha aina tano za mpunga wa nchi kavu aina ya AMMKA au NERICA. Kirefu cha AMMKA ni Aina mpya ya mpunga kwa Africa au kwa kiingereza NERICA”New Rice for Africa” AMMKA  ni jina linalounganisha aina nyingi za mpunga kwenye kundi moja. Aina hizi ni NERICA -1, NERICA-2, NERICA-4, NERICA-5 na WAB450. Kutokana na hali ya mabadiriko ya tabia nchi na hasa ukame, aina hizi zinavumulia sana ukame na zinapandwa kwenye maeneo yanayotegemea mvua kama mahindi. Aina hii itachangia sana katika kuongeza uzalishaji wa mpunga hapa nchini kwani maeneo kama haya ni mengi ikilinganishwa na mabonde ya umwagiliaji au mabonde yanayotegemea mvua. Natumia fursa hii kuwaambia wakulima wa Tanzania kulima aina hizi mpya za mpunga. Kwa wakulima wanaopata mvua za muda mrefu wana nafasi ya kupanda na kuvuna mara mbili kwa mwaka kwani zinakomaa kwa muda mfupi kwa kutumia siku 90 hadi siku 100 shambani.


3.                 Mfumo mpya  wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”


Mnyororo wa thamani wa zao husika huanzia upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji, kuvuna, kuongeza thamani na kuuza kwenye masoko yaliyokusudiwa. Mfumo wa zamani katika kuandaa teknolojia hadi kuifikisha kwa walengwa haukuwa ukiangalia sana mahitaji ya soko. Katika mfumo huu wa ASA  wakulima na wasindikaji wanapewa aina 13 za mbegu ya mpunga na kuzitathimini kuanzia upandaji, utunzaji wa shamba, uvunaji na usindikaji na mwisho wakulima kwa kushirikiana na wafanya biashara huchagua mbegu ambayo wanajua itatoa ushindani kwenye soko na mbegu hiyo huzalishwa kwa wingi ili kukidhi mahitaji yao. Mfumo huu tulianza kuujaribu kwenye zao la mpunga na kuongeza matumizi ya mbegu kutoka tani 60 mwaka 2007 na kufikia tani 1500 mwaka 2012. Katika msimu wa 2012/13 ASA imefanyakazi na vijiji 120 katika kanda ya kati kwenye zao la alizeti ambapo tayari mwitikio kwenye matumizi ya mbegu ya alizeti unaaza kuwa mzuri ikilinganishwa na hapo awali.



SHIMIWI KUFANYA MKUTANO MAALUM WA KUPANGA RATIBA JUMAMOSI HII.

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw.Moshi Makuka akisisitiza umuhimu wa vilabu kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za mashindani ya SHIMIWI leo ofisini kwake.

========  =====   =====
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linatarajia kufanya mkutano maalum wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu utakaofanyika kesho kutwa jumamosi ya agosti 31 majira ya saa 4 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.


Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka alisema mkutano huo  utawahusisha wenyeviti na makatibu wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI kutoka katika Wizara,Idara Zinazojitegemea,Sekretarieti za Mikoa na Wakala za Serikali. “Wenyeviti na Makatibu wa Vilabu vinavyoshiriki michezo ya SHIMIWI mnatakiwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa ili kufanikisha mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza hivi karibuni” alisema Bw.Makuka.

Aidha,Bw.Makuka aliwataka wenyeviti na makatibu wa vilabu vyote kuja na viambatanisho muhimu kama vile barua za kuthibitisha kushiriki,fomu za usajili wa wachezaji watakaoshiriki na vikombe (kwa vilabu vilivyopata vikombe katika mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika mjini Morogoro).


Mashindano ya michezo ya SHIMIWI kwa mwaka huu yamepangwa kufanyika mjini Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi oktoba 5 ambapo yatahusisha michezo ya mpira wa miguu,netiboli,kuvuta kamba,riadha,baiskeli,karata,bao na drafti.



miss tanzania aagwa leo jijini dar

$
0
0
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara  (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL 28 ZA KISIMA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA NA BIASHARA MOSHI

$
0
0
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Kilimanjaro, Leiya Hermenegild (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.mil.28 Mkandarasi wa Kampuni ya uchimbaji visima ya Aqwe Drilling and Construction ya Mjini Moshi, Rishi Shah kwa ajili ya kuchimba kisima katika Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara cha Mjini Moshi (MUCCoBS) chuoni hapo mwishoni mwa wiki.Aliyevaa tai ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu (wa tatu kulia)akielekezwa jambo na Rishi Shah  wa Kampuni ya Ukandarasi wa Uchimbaji Visima ya Aqwe Drilling and Construction ya Mjini Moshi  liyokabidhiwa hundi ya sh. mil. 28 za kuchimbia kisima cha maji katika Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara cha Mjini Moshi (MUCCoBS). TBL  iliyokabidhi hundi hiyo hivi karibuni chuoni hapo, imefadhili uchimbaji wa kisima hicho.

KITAMBI SASA BASI

$
0
0

ONDOA  KITAMBI  KWA  SIKU  KUMI  NA  NNE

NEEMA   HERBALIST   &  NUTRTITIONAL  FOODS  CLINIC
  
Ni  wauzaji  wa  dawa  mbalimbali  za  asili. Tunayo  dawa mpya ya   asili   iitwayo " KITAMBI  SASA  BASI "   inayo  ONDOA  KITAMBI  NDANI  YA MUDA  MFUPI.  Dawa  hii  ni  ya  asili kabisa  “ pure  herbal “, haijachanganywa  na  kemikali   yoyote, haina  side  effect  kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne  tu.  Bei  yake  ni Shilingi  Elfu  Hamsini   Tu ( Tsh.50,000/=) 

Tunapatikana   jijini  Dar  Es  salaam, katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.  Vile vile  tunafanya   ‘delivery’ kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, na  kwa  wateja  wa  mikoani  tunawatumia   kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar  tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya   meli  na  kwa  wateja  waliopo  nje  ya  nchi  tunawatumia  kwa  , DHL, ama posta.

PIA  tunayo  dawa  ya  asili  iitwayo  JIKO  ambayo  hutibu  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.
Kwa  maelezo  zaidi wasiliana    Nasi  kwa  Simu :  0767010756   au  0766538384.

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images