Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI BITEKO ATAMANI MADINI YACHANGIE ZAIDI PATO LA TAIFA

$
0
0
 Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma leo, Januari 15 2018.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akifurahia jambo na Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto kwa Waziri) alipofika ofisini kwake kumsalimu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati. 
 Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko, akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati (hawapo pichani), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akizungumza, wakati wa hafla fupi ya kumpokea Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (katikati) Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. 
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, wakimsikiliza Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma Januari 15 mwaka huu.


Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko ameeleza kuwa anatamani kuiona sekta ya madini ikichangia zaidi ya ilivyo sasa katika Pato la Taifa.
Ameyasema hayo mapema leo, Januari 15 mjini Dodoma, alipowasili rasmi katika Ofisi yake ya Makao Makuu na kupokelewa na viongozi mbalimbali pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini na wa Wizara ya Nishati.

Amesema kuwa, sekta ya madini inaweza kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa kutoka asilimia Nne ya sasa na kuweza kufikia asilimia 10 au zaidi ikiwa kutakuwa na ushirikiano baina ya wafanyakazi wote na viongozi wa Wizara huku kila mmoja akijituma kutimiza wajibu wake ipasavyo.
“Tujiulize hivi ni kwanini hadi leo sekta hii inachangia asilimia Nne tu katika Pato la Taifa badala ya kupanda hadi asilimia 10 au zaidi. Tubainishe ni madini yapi yanayotupatia fedha nyingi zaidi na ni mbinu gani tutumie ili tuweze kupanda zaidi,” amesisitiza.

Hata hivyo, Naibu Waziri Biteko alibainisha kuwa ujio wake wizarani haulengi kubadili au kugeuza mambo bali ni kuongeza nguvu zaidi kwa watangulizi wake katika kutekeleza yale ambayo yameagizwa na Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa niaba ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Tuombeane kwa Mungu atupe kibali, hekima na uwezo wa kuyaona matatizo lakini zaidi sana atupe uwezo wa kutekeleza majukumu yetu ili sekta hii ya madini iwe sekta ambayo ina mchango mkubwa kwa Taifa letu.”
Aidha, amesema kuwa falsafa yake ya utendaji kazi ni kwa kila mmoja kuheshimu nafasi ya mwenzake bila kujali nafasi aliyonayo. 

“Binafsi ninaamini hakuna mkubwa kwenye kufanya kazi. Ukubwa wako unaonekana kwenye matokeo ya kazi unayofanya. Kwa hiyo tushirikiane wote. Mimi ninaamini katika nguvu ya ushirikiano,” amesisitiza.

Viongozi mbalimbali waliompokea Naibu Waziri Biteko akiwemo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Madini Profesa Simon Msanjila, wamemwahidi ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga amempongeza Naibu Waziri kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kueleza kwamba wafanyakazi wanayo imani kubwa kuwa atasimamia vema utekelezaji wa majukumu katika sekta husika.

“Hii ni kwa sababu tunaamini unaifahamu vema sekta ya madini kutokana na kuwa umekuwepo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa muda mrefu na umeweza kuisimamia vizuri.”

Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati wana uhusiano wa karibu kikazi kutokana na kufanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu katika iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kabla ya kutenganishwa na kuwa Wizara mbili tofauti. Hii ndiyo sababu wangali wanashirikiana katika mambo mbalimbali kama hafla hii ya kumpokea Naibu Waziri.

Naibu Waziri Biteko aliteuliwa katika nafasi hiyo Januari 6 mwaka huu na kuapishwa tarehe 8 Januari na Rais John Magufuli.

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA KHERI AWASILI RASMI OFISINI.

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kheri D James akisalimiana na Mtumishi wa Makao Makuu ya Umoja wa Vijana  wa CCM Bi.Sheila Alipowasili katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Umoja wa Vijana Wa CCM Upanga Leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shaka (kwanza kushoto)akimtambulisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James kwa Makatibu wasaidizi wakuu alipowasili ofisi ndogo za UVCCM Upanga leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Ndg.Shaka Hamdu Shaka akimuonyesha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James moja ya Ofisi ya Makao makuu.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James akisaini kitabu Rasmi Kuingia Ofisini Leo Makao makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM Upanga.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Bi Thabia Mwita akisaini kitabu,.
 Viongozi wakuu wakiwa katika Ofisi ya Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Ndg. Kheri D James akizungumza na Watumishi wa Makao Makuu ya UVCCM Upanga leo.(PICHA NA FAHADI SIRAJI)

MBUNGE RITTA KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi box la mafuta hayo katibu wa Tas mkoa wa Iringa bwana Leo Sambala katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa  
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi  la mafuta hayo katibu wa Mufindi bwana Andrea Kihwelo
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi  mafuta hayo moja ya walemavu wa ngozi
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi la mafuta hayo mwenyekiti wa wilaya ya Kilolo ndugu Anna Masasi 


Na Fredy Mgunda,Iringa

JAMII imetakiwa kuwalea, kuwatunza na kuwajali watu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuhakikisha kwamba wanaishi katika mazingira mazuri, yenye usalama na sio kuwanyanyapaa pale wanapohitaji mahitaji yao ya msingi.

Aidha Chama cha walemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Iringa kimeshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali, ili walemavu hao pia waweze kupata elimu juu ya afya ya usalama wa ngozi pamoja na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao.


Hayo yalisemwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati wakati alipokuwa akitoa msaada wa mafuta maalum ya kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi albino katika hafla fupi iliyohudhuriwa na walemavu hao ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa

“Nampongeza Mwenyekiti wa TAS mkao wa Iringa kwa jitihada zake alizozifanya juu ya namna ya kupata mafuta haya, kama chama endeleeni kuwa wabunifu namna ya kulisaidia kundi hili tete la walemavu kwa kuwalea na kuwatunza katika mazingira mazuri”, alisisitiza mbunge Kabati 

Vilevile Kabati  aliongeza kwa kuwataka viongozi wa chama hicho kutumia fursa waliyopewa na wanachama wao, kuhakikisha kwamba wana ainisha matatizo waliyonayo walemavu wa mkoa wa Iringa na kuyafikisha katika ofisi za serikali ili yaweze kufanyiwa kazi.

Kabati alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inahakikisha kuwa inafakiwa kutatua matatizo ya wananchi wa ikisha maisha yao yanaboreshwa.

“Hata haya mafuta yamenunuliwa na serikali kupitia wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto na yanasambazwa nchi nzima hivyo sisi viongozi kazi yetu ni kwasaidia usafiri walememavu hawa” alisema Kabati

Awali akitoa maelezo mafupi juu ya changamoto zinazowakabili albino katika mkoa wa Iringa huo, Mwenyekiti wao Hellen Machibya  alisema kuwa wanashindwa kuwafikia wanachama wake kwa urahisi kutokana na kukosa usafiri na rasilimali fedha, kwa ajili ya kuwatimizia mahitaji yao ya msingi. 

Machibya alifafanua kuwa kukosekana kwa fedha kunakwamisha utendaji kazi na uendeshaji wa shughuli husika, hivyo wanaiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kutatua kero zinazowakabili ili kundi hilo tete liweze kusonga mbele kimaendeleo.

Machibya alisema kuwa kazi aliyoifanya mbunge huyo ni kuokoa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwa watakuwa wanajikinga na mionzi ya jua.Machibya alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwaathirika wakubwa wa ugonjwa wa kasa kutokana na ngozi zao kushambuliwa na jua na kusababisha kuiathiri ngozi hivyo msaada uliotolewa na serikali umeokoa sana maisha.

“Jamani sisi watu wenye ulemavu tunapenda sana kufanya kazi tatizo mionzi ya jua inatuathiri sana na kusababisha kushindwa kufanya kazi zetu kwa uwezo wetu hivyo tunaomba serikali na wadau kama mbunge Ritta Kabati waendelee kutusaidia maana mafuta haya dukani ni gharama sana hivyo watu wenye ulemavu wa ngozi hatuzimudu” Machibya

Lakini Chama cha walemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati kwa kuwasidia kuwafikishia mafuta ya kujipaka mwilini kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua ambayo imekuwa ikiwasababishia kupata ugonjwa wa kansa.

MNEC SALIM ASAS AMWAGA MAMILIONI YA FEDHA KATA YA KIHESA KWA AJILI YA MAENDELEO

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa wakifurahia kukabidhiwa kwa hati kwa diwani wa chama hicho tukio hilo lilifanyika katika ofisi ya kata ya kihesa likihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani wakizungumza na wananchi waliohudhulia tukio hilo
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani wakiwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa kata ya kihesa 
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiongea na wananchi walijitokeza kushudia tukia na kupewa cheti diwani wa kata hiyo Jully Sawani

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KATA ya kihesa manispaa ya Iringa imeanza kupata neema ya mamilioni ya fedha za kimaendeleo mara baada ya kumpata diwani mpya kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya kupita bila kupigwa kutoka na vyama vingine vya siasa kutoweka wagombea.

Akikabidhiwa hati ya utambulisho wa kuwa ndio diwani halali wa kata ya kihesa,Jully Sawani alielezea mikakati ya kimaendeleo ya kata hiyo ambayo ataanza nayo ni kukarabati miundombinu ya barabara kwenye baadhi ya mitaa ya kata hiyo.

“Ukipita kwenye mitaa yetu utagundua kuwa mtaa kama mtaa wa mafifi miundombinu ya barabara sio nzuri kabisho akahidi kuwa ndani ya wiki hii atapeleka kata pila lianze kazi ya kuzikarabati bara bara hizo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wake kwa kuwa wamemtuma kufanya kazi” alisema Sawani

Sawani aliongeza kwa kusema kuwa amejianda kuhakikisha anatatua kero za wananchi kwa kushirikiana na serikali ya manispaa ya Iringa ambayo inatekeleza sera za chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 huku ikiwa na kauli mbiu inayosema kuwa hapa kazi tu.

“Naomba niseme ukweli wananchi wangu wote wa kata ya Kihesa sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio mchezo mchezo mliokuwa mnaufanya nimeomba kuwa diwani kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi wa kata hii anafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa familia yake haiwi masikini,ninasema kuwa kila ukilala hakikisha unaukataa umasikini kwa kuutamka wakati unalala tena kwa zaidi ya mara tisa hapo ndio utafanya kazi” alisema Sawani

Aidha Sawani alitoa kilio chake cha kwa kuomba msaada wa kimaendeleo kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ambapo alimwambia kuwa wananshida ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na kusaidiwa kumalizia ujenzi wa jingo la kibiashara ambalo lipo jirani na ofisi za kata ya hiyo.

“Mheshimiwa MNEC Salim Asas nipo hapa naomba utusidie msaada wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na jingo hili ambalo lipo mbele yetu unaliona linahitaji kumaliziwa ili kuweza kuongeza ajira kwa wananchi wa kata yangu hivyo naomba sana msaada wako kukamilisha hivi vyote kwa awamu hii ya kwanza” alisema Sawani

Akihutubia mamia ya wananchi walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa kata hiyo Jully Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya saruji kwa ajili ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto nyingine.

“Leo naanza kwa kutoa mifuko miambili ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za shule hiyo ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa uhuru kwa lengo la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa katika kuleta maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo hivyo nitasaidia sana kwenye elimu” alisema Asas

Asas aliwakata viongozi wa kata hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na kuacha kuishi kimazoea.

“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas


Asas alisema vijembe na malumbano ya kisiasa katika kata hiyo yanatosha na akawataka vijana hao kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakavyowawezesha kufikiwa kirahisi na mipango mbalimbali ya maendeleo

Waziri wa Kilimo Dkt.Tizeba atembelea Taasis ya Naliendele.

$
0
0
 Waziri wa Kilimo Dr.Charles Tizeba akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa wadudu na Magonjwa wa Zao la Korosho Taasisi ya NALIENDELE Dr.Wilson Nene aliyevalia Tishet Nyeupe wakati waziri wa Kilimo Dr.Tizeba alipofanya Ziara katika Taasis Hiyo.
 Kaim Mkurugenzi wa Taasisi yaUtafiti wa Kilimo NALIENDELE Iliyopo Mkoani Mtwara Dkt Omar Mponda akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba kuhusiana na Mbegu za Muhogo ambazo zinazalishwa na Taasisi ya Hiyo.

Jumla ya miche ya Mikorosho Million10 imezalishwa na  Taasisi ya utafiti wa Kilimo NALIENDELE Iliyopo mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania CBT kwa ajili ya kusambaza katika mikoa yote inayozalisha Zao la korosho.
 Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba akioneshwa Shamba la Mfano la  Karanga lililopo Taasisi ya Utafiti ya Kilimo NALIENDELE Iliyopo Mkoani Mtwara.
Waziri wa Kilimo Dr.Charles Tizeba akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa wadudu na Magonjwa wa Zao la Korosho Taasisi ya NALIENDELE Dr.Wilson Nene aliyevalia Tishet Nyeupe wakati waziri wa Kilimo Dr.Tizeba alipofanya Ziara katika Taasis Hiyo.

Article 10

SERIKALI KUPITIA DAWASA KUJENGA MITAMBO MITATU YA KISASA YA KUCHAKATA MAJI TAKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, (DAWASA), Bi. Modester Mushi(kushoto), akifafanua jambo leo Januari 15, 2018 kwa kutumia ramani ya mradi wa ujenzi wa mitambo mitatu ya kuchakata maji taka jijini Dar es Salaam, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, jijini, Mhe. Ali Hapi, wakati alipotembelea eneo la Kilongawima, Mbezi Beach jijini ambako patajengwa moja kati ya mitambo hiyo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa DAWASA, Bi. Neli Msuya.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WIZARA ya Maji na Umwagiliaji, kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASA), inajiandaa kujenga mitambo mitatu ya kisasa ya kuchakata maji taka, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha hali ya mazingira jijini.

Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa DAWASA, Bi. Modester Mushi wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa mitambo hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinodnoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Ali Hapi, wakati alipotembelea moja ya maeneo ya mradi huo huko Kilongawima, Mbezi Beach.
“Ujenzi wa mitambo hii utakwenda sambamba na ujenzi wa mfumo wa ukusanyaji maji taka katika jiji la Dar es Salaam ambapo lengo ni kulaza jumla ya kilomita 563 za mabomba ya ukubwa mbalimbali ya ukusanyaji na usafirisha maji taka kutoka sehemu mbalimbali za jiji na kuyamwaga kwenye mitambo mikubwa mitatu itakayojengwa hapa Kilongawima,(Mbezi Beach), Jangwani na Kurasini.” Kaimu Mkurugenzi huyo amemueleza Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi.
Kuhusu ukubwa wa mitambo hiyo, Bi. Modester alisema, Mtambo wa Kilongawima (Mbezi Beach) utakapokamilika, utakuwa na uwezo wa kuchakata maji taka yenye mita za ujazo 16,000 kwa siku, wakati ule wa Jangwani utakuwa na uwezo wa kusafisha (kuchakata) maji taka yenye lita za ujazo 200,000 kwa siku na ule wa Kurasini utakuwa na uwezo wa kuchakata maji taka yenye lita za ujazo 11,000 kwa siku.
“Ujenzi wa mitambo hii utaanza muda wowote mwaka huu wa 2018 na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Milioini 65.” Alisema.
Akifafanua zaidi jinsi mitambo hiyo ya kisasa itakavyofanya kazi, Bi.Modester Mushi alisema, mitambo hiyo pia itazalisha gesi asilia na umeme kwa ajili ya kujiendesha, na hivyo kupunguza matumizi na gharama za umeme.
“Lakini pia maji yatakayokuwa yamesafishwa yatauzwa na kutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kupoozea mitambo na umwagiliaji wa bustani wakati tope litakalobaki baada ya mchakato huo wa usafishaji maji taka litaweza kutumika kama mbolea kwa ajili ya kilimo lakini pia kuendesha bustani za miti ya kivuli na hivyo kulipendezesha jiji.” Alifafanua Bi. Modester na kuongeza,
Katika eneo la Jangwani , bustani ya kisasa itakayokuwa na miti ya kivuli, maua  na viti vya kupumzikia itajengwa ili kuboresha taswira ya eneo hilo la Jangwani na hiyo itakuwa ni mchango wa DAWASA katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuboresha usafi wa mazingira.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi, aliwapongeza DAWASA kwa hatua wanazochukua hususan kazi ya kuanza mradi huo na kuwataka waharakishe utekelezaji wa mradi. “Changamoto kubwa ambayo tubnakabiliana nayo sisi viongozi wa serikali hatuelewi sana ni ucheleweshwaji wa mradi,tunatamani kuona vitu vinatokea na hasa mnapotuhakikishia kuwa fedha zipo, kama mnachangamoto zozote ni vizuri kuzifikisha kwenye mamlaka zinazohusika ili ziwasaidie kutatua changamoto hizo ili kwa pamoja tuweze kuwaletea wananchi maendeleo.” Alisema Mhe. Hapi.
Mheshimiwa Hapi pia alitembelea kituo cha kusukuma maji taka cha Shoppers Plaza, Mikocheni pamoja na kutembeelea maeneo korofi yanayovuja maji taka kwenye eneo la Mikocheni na Mwenge na kuitaka Kampuni inayosimamia uendeshaji wa kuondoa maji taka DAWASCO kuhakikisha wahandisi wake wanatoka maofisini na kukagua maeneo korofi ili kuchukua hatua za kuyarekebisha.
“Nasisitiza tena Wahandisi watembelee maeneo ambayo kazi zao zipo, watembelee barabara zetu, Halmashauri zinatumia fedha nyingi kurekebiusha barabara zetu, zikirekebisha baada ya mwezi mmoja chemba zinapasuka na kuharibu barabara, hatuwezi kuendelea na utaratibu huu, ni lazima tutafute suluhu.” Alisema. 
 Mhe. Hapi akizungumza kwenye moja ya maeneo korofi ya chemba ya maji taka Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara hiyo.
 Mhe. Hapi akizunghumza kwenye eneo korofi la chemba ya maji Taka Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara hiyo.
 Mhe. Hapi (kushoto), akitazama ramani hiyo.

 Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi, (kulia), akifafanua jambo wakati alipotembelea eneo lililopangwa kujengwa mtambo wa kuchakata maji taka huko Kilongawima, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, leo Januari 15, 2018. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa DAWASA, Bi. Neli Msuya.
 Bi. Modester akimsikilkiza kwa makini Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi (hayupo pichani).
 Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, (kulia), akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa DAWASA, Bi. Modester Mushi, (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Umma, Bi., Neli Msuya.
 Mhe. Hapi akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwenge jijini Dar es Salaam, Bw.Bashiri Hoza, (kulia) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwenge, alipotembelea kuona maeneo korofi ambayo chemba za mitaro ya maji taka hufumuka mara kwa mara kwenye eneo hilo jirani na soko la Mwenge.
 Mhe. Hapi akizungumza mbele ya wananchi alipotembelea maeneo korofi ambayo chemba za maji taka hufumuka mara kwa mara eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Hapi, akitoa maelekezo alipotembelea eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuona miundombinu ya maji taka.

TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA

$
0
0
  Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua Ujenzi wa jengo la maabara lililojengwa katika  kituo cha afya cha Nyangamara Mkoani Lindi.
Mwonekano wa Nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo katika Kata ya Nyamara, wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi.

Angela Msimbira- OR-TAMISEMI LINDI.

Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Lindi Bw. Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya usimamizi wa huduma ya afya Wilaya ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia  ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya  cha  Nyangamara kilichopo kata ya Nyangamara, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.

Bw. Makenge amesema Kamati ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalojukumu kubwa la kusimamia shughuli zote za afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana budi kuhakikisha Miradi inayotekelezwa na Serikali inasimamiwa kikamilifu ikiwepo Ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.

Amesema kuwa Kamati hiyo inahitajika kusimamia wahudumu wa afya katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyopo  katika sekta ya afya.

Ameiagiza kamati hiyo kusimamia utendaji bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa kuwahimiza wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuondoa kero mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya nchini.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Bikilo Zuberi amesema kuwa mpaka sasa tayari serikali imeshatoa shilingi milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi, Ujenzi wa Maabara, Chumba cha Upasuaji, wodi ya wazazi na chumba cha kuifadhia maiti jambo ambalo litapunguza kero kwa wananchi na kuongeza huduma za afya nchini.

Ameishukuru serikali kwa kuweza kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Lindi kwa kutoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha afya cha Nyangamara kwa kuwa awali kituo kilikuwa na changamato ya kutokuwa na majengo ya kutosha ya kutolea huduma kwa wananchi ikiwemo ukosefu wa jengo la maabara, wodi ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara na chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake,Diwani wa Kata ya Nyangamara Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi Mhe. Ramadhani Malingumu ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kushirikisha wananchi kwenye ujenzi wa vituo vya afya nchini jambo ambalo litasaidia katika kutunza na kusimamia vituo vya afya vilivyojengwa.

Aidha amesema wananchi wa kata hiyo wameshirikishwa katika ujenzi wa kituo hicho kwa asilimia mia jambo ambalo linaimarisha ushirikiano kati ya wananchi na serikali katika kuleta maendeleo katika jamii.

WANANCHI WA MBAMBA BAY WATAKA BARABARA YA LAMI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (mbele), akishuka ngazi wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa unaojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Edwin Nunduma, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu hatua na changamoto wanazozipata katika miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Miradi hiyo inajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Muonekano wa hatua ya awali ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Mradi huo unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Eng. Lazeck Alinanuswe (kulia), wakati akikagua barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa tarehe 11 mwezi Disemba mwaka jana.





Wananchi wa Mbamba Bay wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay (km 67), kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mizigo wanazozipata hususan katika kipindi cha masika.

Wananchi hao wametoa kero hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, alipofika wilayani hapo kukagua barabara hiyo ambapo wamefafanua kuwa licha ya wilaya hiyo kuwa na maliasili nyingi, wawekezaji na wafanyabiashara hushindwa kufika kutokana na changamoto ya barabara, hivyo kupelekea uchelewaji wa maendeleo katika wilaya yao.

"Uduni wa barabara hii unapelekea kutopata maendeleo ya haraka, pia usafiri kutoka hapa kwenda maeneo mengine ya jirani huwa mgumu hususan katika kipindi cha mvua kwani madereva wengi hupandisha nauli", amesema mmoja wa wakazi wa Mbamba Bay, Bw. Bahati Ndege.

Aidha, wananchi hao wameipongeza Serikali kwa hatua zinazofanya katika utatuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo wamefafanua kuwa Serikali kuamua kujenga barabara ya lami kutaboresha uchumi katika wilaya yao na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri Elias Kwandikwa, amesema kuwa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo umesainiwa tangu Mwezi Desemba mwaka jana na kufafanua kuwa kinachosubiriwa sasa ni kwa mkandarasi kufika eneo la mradi na kuleta mitambo yake.

"Kila kitu kipo tayari, Wananchi wasubiri kwa hamu ujenzi wa barabara hii ambao unatarajiwa kujengwa kwa shilingi bilioni 129 na mkandarasi CHICO kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Amepongeza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa kuweka changarawe katika barabara hiyo ambapo kwa namna moja inasaidia kurahisisha usafiri kwa kipindi hiki ambacho mkandarasi anasubiriwa kufika eneo la kazi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amekagua mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba ya Makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

Naye, Meneja wa TBA mkoani humo, Mhandisi Edwin Nunduma, amesema kuwa TBA katika wilaya hiyo ina jumla ya miradi minne inayoendelea kwa sasa ikiwemo mradi wa ujenzi wa zahanati, nyumba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo amemhakikishia Waziri huyo kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Naibu Waziri Kwandikwa ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo leo amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake ili kujionea maendeleo yake.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

POLISI ARUSHA YADHIBITI UVUNJAJI MARA DUFU, YAKUSANYA 3.8 BILIONI MAKOSA BARABARANI

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeweza kudhibiti matukio ya uhalifu kwa 17.9% mwaka jana 2017 tofauti na mwaka 2016 ambapo kulikuwa na matukio 2,817 wakati  mwaka 2017 kulikuwa na matukio 1,963 pungufu ya matukio 854, huku matukio ya uvunjaji yakipungua toka 604 hadi 294 ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya mwaka 2016.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda Polisi wa mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, matukio hayo ya uhalifu yamezidi kupungua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2016 matukio yalipungua kwa 6.8% ikilinganishwa na mwaka juzi 2015, na kuongeza kwamba hayo yote yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na Jeshi hilo.

Makosa mengine ambayo yamepungua ni pamoja na Unyang’anyi wa kutumia nguvu ambayo mwaka 2016 yalikuwa 86 na mwaka jana 2017 yameshuka hadi 40 huku makosa ya kutupa watoto yalikuwa 38 lakini mwaka 2017 yameshuka hadi kufikia 13.

“Matukio ya Mauaji nayo yalipungua kutoka 65 hadi 58 kwa mwaka 2017, wizi wa Watoto yalikuwa 20 na yamepungua hadi matukio mawili, na yalioongezeka ni Ubakaji na Ulawiti ambapo mwaka 2016 matukio ya Ubakaji yalikuwa 144 na mwaka jana yameongezeka matukio matano wakati makosa ya Kulawiti yalikuwa 58 yameongeza kufikia 62”. Alisema Kamanda Mkumbo.

Aidha katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Jeshi hilo liliweza kukamata Cocaine gramu 480, Bhangi kilogramu 211 na gramu 760 na Mirungi  kilogramu 317 na gramu 710 pamoja na watuhumiwa 554.

Kwa upande wa Usalama Barabarani Jeshi hilo limeweza kukusanya jumla ya shilingi 3,825,180,000 kutokana na makosa mbalimbali ambapo kwa mwaka 2016 Jeshi hilo lilikusanya jumla ya shilingi 4,708,680,000 kutokana na makosa hayo.

Hata hivyo Kamanda Mkumbo alisema kwamba kushuka kwa makosa ya Usalama Barabrani  kumetokana na watumiaji wengi wa barabara hususani madereva wa vyombo vya usafiri kufuata vyema sheria za Usalama Barabarani hali hiyo imetokana na elimu iliyokuwa inatolewa na Jeshi hilo kitengo Usalama Barabarani kupitia Radio mbalimbali za hapa jijini Arusha, elimu kwa wanafunzi lakini pia elimu ya kituo hadi kituo kwa wadereva wa Pikipiki za abiria.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza uhalifu, Kamanda Mkumbo ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa za uhalifu na wao kuzifanyia kazi mara moja lakini pia ametoa onyo kwa yoyote atakayedhubutu kushiriki kutenda uhalifu, atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

ATAKAYEBAINIKA KUTAFUNA SH. MILIONI 320 ZA IMARA SACCOS ACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Musoma Bibi Yunia Wiga kufuatilia upotevu wa sh. milioni 320 za Imara SACCOS na atakayebainika kuhusika ashughulikiwe.

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Januari 15, 2018) alipopokea malalamiko ya wanachama wa SACCOS hiyo kupitia mabango waliyoyawasilisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku sita, alimuagiza ofisa huyo kukutana na uongozi na wanachama wa SACCOS hiyo leo mchana na kisha kumpa majibu juu ya upotevu wa fedha hizo pamoja na sh. milioni 40 za hisa ifikapo Januari 20, 2018.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Bibi Fidelica Myovella kuhakikisha anatenga fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi mbalimbali waliopisha miradi ya maendeo katika Manispaa hiyo.

Waziri Mkuu alisema siyo vizuri kwa halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama barabara, standi na kisha kukaa muda mrefu bila ya kuwalipa fidia zao.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha daladala cha Bweri ambao hawajalipwa fidia zao tangu mwaka 2013. Mkurugenzi huyo aliahidi kuanza kulipa madeni hayo kuanzia mwezi Januari, 2018.

Awali, Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini, Bw Vedastus Mathayo aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza baadhi ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Bw. Mathayo alisema wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa utekelezaji wa ahadi hiyo.

Mbali na mradi wa maji pia Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwemo ya ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami pamoja na ukarabati wa kiwanja cha ndege unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Waziri Mkuu alisema ahadi zote zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 na zile zilizotolewa na Rais Dkt. Magufuli zitatekelezwa, hivyo wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 16, 2017.

MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI,MAGEREZA,JWTZ

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya  pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Dar es salaam


Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umetakiwa kutoa maelezo kwa serikali katika kipindi cha muda mfupi kueleza sababu za kuendelea kusalia kuwepo kwa shirika hilo kutokana na kukosa umakini katika utendaji.


Kauli ya kuchukizwa na utendaji wa Shirika hilo imetolewa Leo 16 Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko Wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika hilo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam.


Mhe Biteko alisema kuwa serikali ilikuwa na makusudi mazuri kufuatia mabadiliko ya Sera za kiuchumi katika miaka ya 1980 kwa STAMICO kuwekwa kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa na hatimaye kubinafsishwa rasmi mwaka 1996 lakini katika kipindi chote cha utendaji hakuna msaada wowote ambao Shirika hilo limeipatia serikali zaidi ya kuingiza hasara maradufu.


Alisema kuwa pamoja na STAMICO kuwa na jukumu la kuendeleza migodi ya Madini na kufanya biashara za Madini ikiwemo mradi wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo Biharamlo Mkoani Kagera na Mgodi wa Makaa ya Mawe KABULO uliopo Mkoani Ruvuma lakini Taasisi hiyo imeshindwa kuendeleza migodi kwa ufanisi huku wachimbaji wadogo wakisalia kuwa katika uduni wa mbinu rafiki na tija katika utendaji kazi wao.


Alisema kuwa Shirika hilo linapaswa kutafakari kwa umakini utendaji wake kwani limeongeza hasara kwa serikali ya deni la shilingi Bilioni 1.77 hivyo serikali haiwezi kuendelea kusalia kuwa na Shirika linalozalisha madeni kuliko matokeo makubwa na faida.


Aliongeza kuwa wataalamu wote katika sekta ya Madini wanapaswa kutambua kuwa biashara ya Madini ni zaidi ya kutoa leseni hivyo watambue kuwa kuna kila sababu ya kuwa na matumizi bora ya mapato na kutazama namna bora ya kuifanya sekta ya Madini kuchangia asilimia 10% ya pato la Taifa.


Mhe Biteko alisema kuwa imani bila matendo ni uduni wa fikra hivyo kuwa na cheo kikubwa serikalini halafu uzalishaji ni mdogo ni kipimo halisi cha utendaji wa mazoea walionao watumishi wengi ambao wamekosa uzalendo na bidii katika utendaji kazi.


Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kusimamia vyema rasilimali za wananchi hivyo watendaji katika sekta mbalimbali wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Rais Magufuli katika kuteleleza adhma ya serikali.

MAKONDA APONGEZA KASI YA MATENGENEZO MAGARI YA POLISI,MAGEREZA,JWTZ

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y'all kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Kati ya magari hayo magari matano yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu na mengine sita yatakabidhiwa. 

Makonda amesema mmiliki wa kampuni hiyo amethibitisha uzalendo wake na mchango wake katika kusaidia Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam  inayotaka kuona vyombo vya ulinzi na usalama wanakuwa na usafiri wa kisasa na uhakika ili kutekeleza majukumu yao. 

Jumla ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati magari yote 11ambapo baadhi yamenfenezewa mabodi mapya kwani yalikuwa yameharibika sana. 

Akizungumza leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema wakati matengenezo ya magari hayo unaendelea wapo watu kwenye mitandao ya kijamii wanalalamika kwanini yasinunuliwe magari mapya kwa madai gharama kubwa. "Wanaosema gharama ya kutengeneza magari ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni kubwa wafahamu tu gharama za kutengeneza magari haya amejitolea mmiliki wa Kampuni ya Dar Coach Ltd,

"Ameamua kutoa mchango wake kupitia utalaam alionao wa kutengeneza mabodi ya magari ya majeshi yetu ambayo tumemletea. Ni mlipa kodi mzuri na kazi anayofanya ipo katika ubora unaokubalika. 

"Hao wanaolalamikia ukubwa wa gharama pengine  hawalipi hata kodi zaidi ya maneno tu.  Huyu ametusaidia na tunathamin mchango wake kwetu,"amesema. 

Ameomba kampuni nyingine kujenga utamaduni wa kujitolea kuisaidia Serikali na hakuna sababu ya kushurutishwa bali ni kuonesha uzalendo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya kushughulikia kero za watanzania.

Makonda amesema ametoa ombi kwa kampuni hiyo kuhakikisha wanaweka na sehemu za kuchajia simu katika magari haul ili kuhakikisha mawasiliano ya simu yanakuwa muda wote kwa watakaoyatumia. "Lazima vyombo vya ulinzi na usalama wawe na magari mazuri. Kila mmoja akifanya kile ambacho anaweza kukifanya tutapiga hatua kubwa,"amesema Malinda. 

Ameomba wananchi ambao wanataka kufanya matengenezo ya magari yao wapeleke katika kampuni hiyo kwani inatengeneza magari kwa kiwango cha juu cha ubora. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Manmeet Lal(Sunny)amesema gharama ya kutengeneza gari zote 11 ni Sh. milioni 830 na ndio mchango wao kwa Serikali na wataendelea kujitolea kadri watakavyoweza. 

"Kampuni yetu iliona umuhimu wa kusaidia kufanya matengenezo ya magari haya na kwa gharama zetu wenyewe na tumeamua kusaidia kama sehemu ya kutoa mchango wetu kwa Serikali,"amesema Lal.

 Akizungumzia ukarabati wa magari hayo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema amefurahishwa na hatua anazochukua Mkuu wa mkoa Makonda za kuhakikisha vyomvo vya usafiri vilivyokuwa chakavu vinatengenezwa na kuwa imara.

Wakati huohuo Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje amesema matengeneza ya magari hayo kwa upande wao yatasaidia kuondoa changamoto ya usafiri hasa katika kusafirisha mahabusu.
 Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya  Dar Coach. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la Magereza leo inayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd

NEC yawakumbusha wasimamizi wa Uchaguzi kuzingtia Sheria

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Februari.
 Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo.
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge, akiwasilisha Mada ya Maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kwa wasiamamizi wa Kinondoni.Picha na Hussein Makame-NEC

Na Hussein Makame -NEC.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi ili kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.

Hayo yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo la jiji la Dar es Salaam.

Alisema wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni mchakato unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.

“Hivyo mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria...,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza” alisema Elisante.

Aliwakumbusha wasimamizi hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekuwa ikisisitiza kwamba Sheria za Uchaguzi hazikuacha ombwe katika kueleza jinsi gani masuala ya Uchaguzi yanatakiwa yatatuliwe.

Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge akiwasilisha mada ya Maelekezo kwa wasimamizi hao, aliwataka kutoruhusu matumizi ya utambulisho mwingine mbadala tofauti na ule ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeruhusu kutumika.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 61 (3) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, kimeipa mamlaka Tume kuidhinisha matumizi ya utambulisho mwingine tofauti iwapo mpiga atakosa kadi ya kupigia kura” alisema Victoria na kusisitiza kuwa:

“Vitambulisho vilivyoruhusiwa na Tume ni vitatu, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria kwa maana ya Passport na Leseni ya Udereva, hivyo mtu akikosa kadi ya kupigia kura au vitambulisho hivyo hakuna utambulisho wowote utakaoruhusiwa ili mtu aweze kupiga kura”

Mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kwa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na kata zilizoko kwenye jimbo hilo, yalijumuisha viapo kwa wasiamamizi hao walioapa kutunza sira na kujivua au kukiri kuwa si mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kinondoni pamoja na Jimbo la Siha na Udiwani katika kata 10 za Tanzania, unatarajiwa kufanyika tarehe 17 Februari mwaka 2018.

KOKA ATOA MILIONI MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGU ASHULE YA MSINGI KONGOWE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.

Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi, shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme .

Koka alitoa mchango huo, wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ,Miembesaba 'A'kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.

Aliomba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi lengwa.

Akizungumzia changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni .

"Kulikuwa na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi""Lakini tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa awamu" alifafanua Koka.

Koka aliwaasa wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na darasa la kwanza kuwapeleka shule .Alisema elimu ndio nguzo na hazina ya watoto ,hivyo ni jukumu la wazazi kuona umuhimu wa kuwapa haki hiyo watoto hao.

Kuhusu tatizo la kutumia maji ya visima badala ya maji safi na salama kutoka Dawasco huko eneo la Ngungwa kata ya Kongowe ,alisema linashughulikiwa .Alisema tatizo la maji lililokuwepo awali Kibaha ,sivyo ilivyo sasa kwani wamepiga hatua ,mradi wa Ruvu Juu na Ruvu Chini imekamilika hivyo kazi iliyobakia ni kusambaza .

Katika afya ,Koka alielezea anaendelea kusimamia changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi,vifaa tiba na madawa.
Alisema kutokana na hilo ,mwezi June mwaka jana ,alileta kontena la vifaa tiba mbalimbali lililogharimu mil.400 na vifaa hivyo vilisambazwa kituo cha afya mkoani na zahanati zilizopo jimboni hapo. 

Alieleza ataendelea kusimamia asilimia 10 ya vijana ,wazee,wanawake,walemavu kwenye mapato ya ndani ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,ili inufaishe makundi hayo.Koka alisema kwasasa ,asilimia 10 inatakiwa igawanywe asilimia 4 akinamama,asilimia 4 vijana,wazee na walemavu asilimia moja ,moja.

Nae afisa elimu kata ya Kongowe,Aziza Matekenya alisema wakati baadhi ya majengo ya shule ya msingi Kongowe yakiungua shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 1,840.Alisema halmashauri ilitoa milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo na imeahidi kuongeza milioni 20 kwa ajili ya umaliziaji.

Aziza alieleza,kwasasa shule ina jumla ya vyumba 12 vya madarasa vinavyotumika ,vitatu vichakavu ambapo inahitaji vyumba vya madarasa 40 ili kukidhi mahitaji.Shule hiyo ilijengwa miaka ya 70 ,kwasasa ina wanafunzi 2,820 na walimu 35 .


NAIBU WAZIRI BITEKO ATOA CHANGAMOTO CHUO CHA MADINI

$
0
0
Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Madini kilichopo Dodoma, (hawapo pichani) alipowatembelea Januari 15 mwaka huu.
Mkutubi Msaidizi wa Chuo cha Madini (MRI), Rachel Lugoye (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko na Ujumbe wake (kulia) utendaji kazi wa Maabara katika Chuo hicho, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Januari 15 mwaka huu.
Mhandisi Mchenjuaji wa Chuo cha Madini (MRI), Dkt. Abdulrahman Mwanga, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Ujumbe wake kuhusu mitambo mbalimbali iliyo katika maabara za Chuo inavyofanya kazi, wakati wa ziara ya Naibu Waziri kujionea utendaji kazi wao, Januari 15 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Madini (MRI) kilichopo Dodoma, alipowatembelea hivi karibuni.

Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko ametembelea Chuo cha Madini (MRI) na kutoa changamoto kadhaa kwa Menejimenti na wafanyakazi wote, ili kiwe na tija stahiki kwa Taifa.
Akizungumza baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Chuo hicho kilichopo Dodoma, Januari 15 mwaka huu, Naibu Waziri alieleza kutokuridhishwa kwake na utekelezaji hafifu wa masuala kadhaa muhimu na hivyo kutoa changamoto kwa uongozi wa Chuo kuyafanyia kazi mapema.
Moja ya mambo muhimu aliyoelekeza yatekelezwe ni pamoja na matumizi mazuri ya rasilimali za Serikali kwa manufaa ya Taifa. Aliwataka kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais John Magufuli anayetaka rasilimali kidogo inayopatikana nchini itumike vizuri na kuleta matokeo.
“Mathalani, viko vifaa vya mamilioni ya shilingi katika baadhi ya maabara zenu na havijawahi kufanya kazi kwa muda wa miezi Sita sasa. Vinachakaa na kuharibika tu. Akija aliyetufadhili kununua vile vifaa, atatushangaa. Tutaonekana wote hatuna uwezo wa kufikiri kumbe ni watu wachache tu wanaosababisha,”alisema.
Kufuatia suala hilo, Naibu Waziri aliagiza maabara zote zenye vifaa ambavyo havifanyi kazi zirekebishwe na zianze kufanya kazi kufikia mwisho wa mwezi huu wa kwanza.
Changamoto nyingine aliyoitoa Naibu Waziri ni kwa Chuo kufanya tafiti ili kuisaidia Serikali kujua mahitaji halisi ya rasilimali watu kwenye sekta ya madini.
“Ninyi ni tofauti kabisa na taasisi nyingine zinazofanya biashara. Mkifanya vizuri, maafisa wetu wa madini kule mikoani na kwingineko kwenye kanda watafanya kazi rahisi sana. Kwa sababu ninyi mtakuwa mmeshafanya utafiti kwa niaba ya Wizara kugundua mahitaji ya rasilimali watu kwenye sekta ya madini.”
Akifafanua zaidi, alisema kwamba Wizara inategemea kupata chemchemi ya fikra kutoka kwenye taasisi hiyo ya Chuo. Alisema, Chuo kinatarajiwa kuzalisha wataalam wazuri ambao watakwenda kufanya kazi sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenda kufundisha wachimbaji wadogowadogo namna nzuri ya kuchenjua madini kwa kuzingatia usalama wa mazingira na kupata tija ili kupandisha hadhi ya mavuno ya rasilimali wanayopata.
Aidha, aliongeza kuwa haipendezi kuona Chuo kikifundisha vijana wengi wa kitanzania lakini kwenye migodi kunakuwa na wafanyakazi wa kigeni wakifanya kazi ambazo watanzania wanaweza kufanya.
“Changamoto kwenu kama Chuo, je, vijana wetu mnawanoa kiasi cha kutosha kushindana katika soko la ajira? Ninyi ni taasisi ya kitaaluma, mnatakiwa kuyaona mambo ya kesho leo. Na mambo ya jana yawasaidie kuboresha kesho ya nchi hii.”
Vilevile, aliwataka kuachana na utamaduni wa kulalamika kwa masuala mbalimbali badala yake wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo na matokeo ya kazi yao yaonekane. Alisema, matokeo mazuri ya kazi ndiyo yatakayoihamasisha Serikali kuona umuhimu wa kuboresha yale wanayoyalalamikia ikiwemo suala la maslahi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Naibu Waziri Biteko katika Chuo cha Madini tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na kuapishwa na Rais John Magufuli Januari 8 mwaka huu, Ikulu jijini Dar es Salaam.

BEI ELEKEZI MPYA KUWAFAIDISHA WAUZA MBOLEA RUKWA

$
0
0
Wauzaji wadogo wa mbole Mkoani Rukwa wamesifu juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wakulima wanapatiwa mbolea kwa wakati na kwa bei elekezi inayoendana na maeneo husika ambayo mbolea hiyo inasambazwa kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata hadi Vitongoji.

“Tunashkuru kwamba zile bei elekezi za mara ya kwanza nina imani hawakujua Jiografia ya Mkoa wetu, lakini kwa sasa hivi hizi bei ambazo wametuelekeza zitawasaidia wananchi na sisi tupo tayari kupelekea sehemu yoyote na faida tutaipata, serikali imetutendea haki,” Damas Kofiambili mmoja wa wafanyabiashara wadogo wa mbolea alisema.

Sifa hizo zimeibuka baada ya Uongozi wa Serikali ya mkoa wa Rukwa kutangaza bei elekezi mpya zilizopitishwa na kamati za pembejeo za wilaya kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mh. Charles Tizeba wakati akikagua maghala ya mbolea Jijini Dar es Salaam ambapo alizitaka kamati hizo kufanya marekebisho ya bei hizo ili kuendana na gharama halisi za usafirishaji ili mbolea iweze kumfikia Mkulima hadi ngazi ya Kijiji.

Akisoma bei hizo mpya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya amesema kuwa bei hizo zilizopangwa zimezingatia maoni ya wafanyabiashara na wadau wa kilimo pamoja na kuandaa fomu maalum zitakazotumika katika ngazi ya kata ili kuweza kujua kiasi cha mbolea kilichoingia kila siku katika ngazi ya kata na kumfikia mkulima kwa bei hiyo elekezi.

“Kwa makao makuu ya Wilaya ya Kalambo Bei ya DAP imepanda kutoka 57,165 hadi 58,022 na maeneo ya kata na vijiji ni 62,522 na UREA imepanda kutoka 44,711 hadi 45,443 na maeneo ya vijiji ni 49,943. Kwa makao makuu ya Wilaya ya Nkasi Bei ya DAP imepanda kutoka 56,018 hadi 57,000 na maeneo ya kata na vijiji ni 60,000 na UREA imepanda kutoka 43,565 hadi 44,000 na maeneo ya vijiji ni 47,000. 

Kwa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Bei ya DAP imebaki vile vile, maeneo ya kata na vijiji ni 62,000 na UREA imepanda kutoka 44,480 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 49,500. Kwa makao makuu ya Manispaa ya Sumbawanga  Bei ya DAP imepanda kutoka 55,442 hadi 56,000 na maeneo ya kata na vijiji ni 57,000 na UREA imepanda kutoka 42,989 hadi 45,000 na maeneo ya vijiji ni 46,000,” Alimalizia.

Marekebisho hayo yamefanywa kwa mujibu wa kanuni ya 56 (4) kwa Mamlaka ya Mbolea nchini (TFRA) kupewa jukumu la kupitia na kurekebisha bei za mbolea kulingana na sababu maalum. Hivyo wadau na wafanyabiashara wote wa mbolea Mkoani Rukwa wametakiwa kutumia bei hizi mpya zilizopitishwa na kamati za pembejeo za Wilaya.

Hayo yote yamejiri baada ya Rais John Pombe Magufuli kutoa agizo la kusambaza mbolea kwa mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji nchini baada ya kusikia mikoa hiyo bado inasuasua katika upatikanaji wa mbolea hasa katika msimu huu wa kilimo.  Hivyo hadi sasa Mkoa unahitaji tani 2618 za mbolea ya kupandia (DAP) na tani 6958.6 za mbolea ya kukuzia (UREA).

DK. KIGWANGALLA APONGEZA USHIRIKIANO WA FINLAND KATIKA UHIFADHI WA MISITU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini. 

Na Hamza Temba - Dodoma
.............................................................. 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla ameipongeza Serikali ya Finland kwa ushirikiano na misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa kuunga mkono juhudi za Serikali katika uhifadhi wa maliasili na uendelezaji wa misitu nchini.

Dk. Kigwangalla ametoa pongezi hizo leo Januari 16, 2018 kwa Balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Mhe. Peka Huka ambaye amemtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na maendeleo ya misitu nchini.

“Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Serikali ya Finland,  mmekuwa washirika wetu wakubwa wa maendeleo kwa muda mrefu ambao mmetusaidia mambo mbalimbali ikiwemo kuendeleza misitu nchini, kuendeleza Chuo cha Mafunzo ya Misitu Olmotonyi na hata mapitio ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, ni matumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha ushirikiano huu”, alisema Dk. Kigwangalla.

Alimueleza balozi huyo kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika uhifadhi wa misitu nchini ikiwemo uhaba wa rasilimali fedha na teknolojia kwa ajili ya kuwezesha uhifadhi endelevu. Alisema changamoto nyingine ni uvunaji haramu wa mazao ya misitu ambayo husababisha eneo la hekta 372,000 za misitu kupotea kila mwaka.

Alisema mbali na nguvu kubwa inayotumiwa na Serikali katika udhibiti wa uvunaji holela wa mazao ya misitu Wizara yake kwa kushirikiana na taasisi zilizoko chini yake inaendelea kuweka mikakati thabiti kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kiserikali kwa ajili ya kutafuta nishati mbadala pamoja na kuanzisha mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa miti ya mkaa kwa njia endelevu.

Akizungumzia umuhimu wa misitu nchini, Dk. Kigwangalla alisema takribani kila kitu hapa nchini kinategemea uwepo wa misitu. Alisema zaidi ya asilimia 80 ya chanzo cha nishati ya umeme nchini ni maji ambayo hutegemea uwepo wa misitu, alitaja pia kilimo na ufugaji ambao pia hutegemea mvua na maji ambayo hutegemea pia uwepo wa misitu.

Kutokana na umuhimu huo, Dk. Kigwangalla amemuomba Balozi huyo kuhamasisha wawekezaji wa Finland  kuja kuwekeza Tanzania katika uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu nchini na kuahidi kuwapa ushirikiano.

Kwa upande wake Balozi Huka, alimueleza Dk. Kigwangalla kuwa nchi yake imekua ikifadhili miradi mbali mbali ya uendelezaji wa misitu katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mikoa ya nyanda za juu kusini na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Alimueleza Waziri Kigwangalla kuwa changamoto iliyopo ya uharibifu wa misitu nchini inahitaji uwepo wa nishati mbadala ambayo mchakato wa upatikanaji wake unatakiwa kushirikisha wadau na Mamlaka nyingine za Kiserikali ikiwemo Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimkaribisha Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo.
 Balozi Peka Huka akimsikiliza Waziri Kigwangalla katika kikao hicho.
 Waziri Kigwangalla akifafanua jambo kwa Balozi Peka Huka (hayuko pichani) katika kikao hicho mapema leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimuaga Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka baada ya mazungumzo ofisini kwake leo mjini Dodoma .

TAGCO kukutana machi 12-16 katika mkutano wa 13 jijini Arusha

$
0
0
 Mweyekiti wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarjiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 Machi Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mwenezi wa TAGCO Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus na Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi.
TG2
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi na Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete
TG3
Kaimu Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akisistiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO, Abdul Njaidi, Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus
TG4
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa viongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na MELEZO
..............................................................................
Na Florah Raphael-Fullshangwe-Dar es Salaam 
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo , unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12-16 Machi mwaka huu mkoani Arusha ambapo jumla ya maofisa 300 wanatarajiwa kishiriki katika mkutano huo.
Akiongea Na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama hicho Paschal Shelutete amesema kuwa lengo kuu kuelekea mkutano huo ni kukumbushana wajibu na majukumu yao serikalini.
Aidha amesema kuwa kikao hicho kina kazi ya kuwajengea washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za serikali na kuhakikisha idara ya mawasikiano na uhusiano serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Pia ameongeza na kusema kuwa katika mkutano huo jumla ya mada 14 zitaongelewa ambazo zitajikita zaidi kwenye masuala mbalimbali yahusuyo habari, mawasiliano na itifaki.Pia amesema kuwa mada hizo zitawasilishwa na wataalam watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano na kuongeza kuwa kutakuwepo mijadala na fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya maaafisa mawasiliano na wadau wengine wa habari.
Mwisho kabisa amewaasa Maafisa Uabari, mawasiliano, uhusiano na Itifaki kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 7 machi mwaka huu.

RAIS DKT JOHN MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABOLOZI SITA IKULU DSM

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images