Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1486 | 1487 | (Page 1488) | 1489 | 1490 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Leo Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria amemuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga, Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong’ole.

  Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano, Shinyanga na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa George Huruma Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Viongozi wa Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Mheshimiwa Josephine Matiro, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Shinyanga na Waumini wa Dayosisi hiyo

  Pamoja na kumpongeza kwa kuwekwa Wakfu, Mhe. Prof. Kabudi amemuomba Askofu Chinyong’ole awe kiungo thabiti baina ya waumini na kati ya waumini na Maaskofu katika kuzitatua changamoto zilizopo katika Kanisa na kwamba utumie vipawa na karama alizopewa na mwenyezi Mungu kuwaunganisha viongozi na waumini ili waweke mipango madhubuti ya kulijenga Kanisa na kuijenga Dayosisi ya Shinyanga.

  Prof. Kabudi amemuhakikishia Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Kanisa la Anglikana Tanzania katika ustawi wa Taifa kiroho, kisiasa, kiuchumi na kijamii na kwamba mchango huo umeiwezesha nchi yetu kupiga hatua katika nyanja zote; Kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu yote nchini katika kuweka misingi ya kila raia kuabudu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.

  Kabla ya kuchaguliwa Mwezi Oktoba, 2017 Askofu Chinyong’ole alikuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kwa miaka mitatu. Askofu Chinyong’ole anakuwa Askofu wa Pili kuiongoza Dayosisi ya Shinyanga iliyoanzishwa Novemba, 2005 baada ya Dayosisi ya Victoria Nyanza kugawanywa.

  Mhe. Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba wakati akimuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
  Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania mara baada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
  Pro. Kabudi akimpongeza Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole mara baada ya kuwekwa wakfu.


  0 0


  0 0

  Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MAWAZIRI wa wizara nne tofauti wameamua kufanya jitihada za kuondoa changamoto ya utoaji huduma kwa muda mrefu na kusababisha msongamano wa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijijini Dar es Salaam.

  Pia kuondoa changamoto ya joto katika eneo la kuchukulia mizigo pamoja na kushughukikia hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia nchini pamoja na changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma uwanjani hapo.

  Mawaziri hao ambao wamekutana leo katika uwanja huo na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala,

  Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye. Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo,Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk.Nchemba amesema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa kutatua changamoto hizo.

  Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki. Pia wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa muda mfupi.

  “Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa utoaji huduma umeshuka hadi saa moja.Lengo letu ni kushuka zaidi

  “Mbali ya kuboresha huduma tutahakikisha pia tunaongeza ulinzi na usalama katika viwanja vyetu vyote nchini ili kudhibiti wageni wenye nia ovu na nchi yetu. “Tunafahamu mataifa mengi yameitikia mwito wa uwekezaji nchini hasa katika mikakati ya kufikia Serikali ya Viwanda na uchumi wa kati”.

  “Hivyo wageni wanakuja kwa nia njema ya kuwekeza lakini hatutaki wale wenye nia mbaya kutumia mwanya huo.Hivyo tutaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika viwanja vyetu,”amesema.

  DK. KIGWANGALA ATAJA KIINI CHA ZIARA

  Akizungumza uwanjani hapo,Dk.Kigwangala amesema wamefikia hatua ya kukutana mawaziri hao baada ya wageni na hasa watalii wanaiongia nchini kulalamika kwake kuwa wanatumia muda mwingi kuhudumiwa katika eneo la uwanja huo kiasi cha kuwapotezea muda.

  Dk.Kigwangala amesema kutokana na malalamiko hayo ya muda na mengine kadhaa hatua mbalimbali zimechukuliwa na kueleza Agosti 8 mwaka 2017 manaibu waziri wa wizara hizo nne walikutana kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi na kukutana kwao leo ni muelendezo wa kushughulikia kero hizo na kuna mafanikio yameanza kuonekana.

  Dk.Kigwangala amesema ipo haja ya kuweka mikakati ya kuboresha huduma katika viwanja vya ndege nchini ukiwamo JNIA huku akisisitiza umuhimu wa watendaji na watoa huduma kwa nafasi mbalimbali kuwa wakarimu kwa wageni.

  Amesema ni vema hata Polisi walioko uwanjani hapo wakimkamata mgeni basi badala ya kutumia nguvu wawe na ukarimu kwani muhimu ni kumdhibiti mgeni bila kutumia nguvu ili ikibainika hana kosa aachiwe na asiwe na malalamiko ya kunyanyaswa. Dk.Kigwangala amesema kuna haja kwa wageni wanapokuja Tanzania wakirudi makwao wasimulie ukarimu na uzuri wa nchini yetu.

  Ameongeza anatamani kuona kuanzia uwanjani hapo hadi hotelini ambako mgeni anakwenda anatumia muda mchache, anapata nafasi ya kuona pcha za viongozi mbalimbali ambazo zitakuwa uwanjani , picha za wanyama na video ambazo zinaonesha utalii wa Tanzania.

  Amesema kumpokea mgeni jambo moja lakini namna ya kumhudumia ni jambo jingine na ndilo muhimu zaidi na akafafanua hata teksi ambayo mgeni ataitumia kusafiri dereva awe na ukarimu hata wa kumsalimia na wakati mwingine kutabasamu.

  MAMBO YA NJE WAANZA KURIDHIKA

  Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Susan Kolimba amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto zinazoelezwa kuwapo uwanjani hapo.

  Amesema wizara yao inatamani kuona idadi ya wageni inaongezeka zaidi na wakati huo huo wakifurahia huduma ambazo wanazipata wakifika nchini kwetu. “Tumefanya ziara na binafsi niseme tu nimeridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto hizo,”amesema Dk.Kolimba.


  WIZARA YA UJENZI YACHUKUA HATUA

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Nditiye amesema wizara yao tayari imechukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zilizopo ikiwamo ya kufunga viyoyozi(AC) kwa ajili ya kuondoa hali ya joto.

  “AC zilizopo ni za muda mrefu kwani ziliwekwa tangu majengo ya uwanja huo yalipojengwa.Hivyo tayari zimeanza kufungwa AC mpya na ndio maana joto limepungua” amesema.

  Pia amesema wamepata kampuni ambayo itakayofanya ukarabati kwa kuongeza eneo la kukaa wageni wanaosubiri huduma mbalimbali kabla ya kutoka uwanjani.

  Amesema kuna jitihada mbalimbali Serikali inafanya jitihada za kuondoa msongamano wa wageni ikiwamo ya kuharakisha ujenzi wa jengo jipya la kusafiria wageni la Terminal III ambalo litahudumia watu milioni sita badala ya jengo la sasa ambalo wakati linajengwa lengo lake lilikuwa kuhudumia watu milioni moja.

  “Ujenzi wa jengo jipya umekamilika kwa asilimia 70 na litakapokuwa tayari kwa asilimia 100 litaanza kutumika kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda vizuri,’amesema.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) wakati walipofanya ziara ya kukagua Changamoto mbalimbali zilizopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katika) na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba wakisikiliza.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba akizunumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba (kushoto) na, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) 
  Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Richard Mayongela wakitafakari jambo wakati wa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba.

  0 0

  MAAFISA Ugani wa Kata na Vijiji wilayani Lushoto mkoani Tanga wametakiwa kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake wahakikisha wanakwenda kwa wakulima ili kuwapa elimu ya namna ya kulima kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao. 

  Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wakati wa ziara yake wa kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji na kusikiliza kero zinazowakabili.
  Akiwa kwenye kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola, Mbunge huyo alisema wapo baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kwenda wa wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ili waweze kuwapa elimu ya namna ya kulima kisasa jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha maendeleo yao nyuma. 

  “Ndugu zangu maafisa ugani tambueni kuwa mnajukumu kubwa la kuhakisha mnakwenda kwa wananchi kuwaelimisha juu ya kulima kilimo chenye tija kwao kwani hiyo itawasaidia kuweza kupata mafanikio kuliko wanavyofanya sasa lakini pia acheni kukaa ofisini “Alisema.
  “Kwani elimu ambayo mnaweza kuitoa inaweza kuwa chachu ya wakulima kuweza kulima mazao mazuri yatakayokuwa ya ushindani na soko la kisasa hivyo jambo hilo ni muhimu sana “Alisema. 

  Alisema iwapo wakulima wataweza kufikiwa kwa wakati wataweza kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kuweza kujiandaa vema na ujio ya fursa mbalimbali za miradi mikubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga. 

  “Niwaambie ndugu zangu hii ni fursa muhimu kwa mkoa wa Tanga na wakulima ambao walikuwa wanazalisha mazao yao na kupeleka Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa laki nane hadi tisa lakini sasa mtakuwa mkitumia hata laki nne mpaka Tanga mjini kwani mradi ukianza kutakuwa na soko la uhakika”Alisema. 

  Aidha pia mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima
  kubadilika kwa kuongeza uzalishaji kutokana na uwepo wa soko la uhakika kwenye mazao yao katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa kwa lengo la kuinua vipato vyao. 

  Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani humo,Juma Khamisi alimuhaidi mbunge huyo kuwa watashirikiana na maafisa ugani waliopo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya kulima kilimo chenye tija ili waweze kunufaika. 

  “Mh Mbunge tumepokea kauli yako kwa mikono miwili na sisi kama viongozi wa kijiji hiki tutahakikisha tunashirikiana na maafisa ugani,wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji ambao utakuwa chachu ya kuweza kuwainua kiuchumi kwa kuchochoea kasi ya maendeleo kwao “Alisema.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.
  Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya nyumba 76 mkoani humo.
  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.

  ……………………

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.

  Agizo hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo hayo ili kuvutia wapangaji wao.

  “Wasimamizi wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa zimetelekezwa muda mrefu”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara, kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali.

  Amekemea tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.

  Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TBA mkoani hapo, Edward Mwangasa, amekiri kutokuwa na hati kwa baadhi ya nyumba na viwanja wanavyovimiliki na hivyo amemuahidi Naibu Waziri huyo kuhakikisha anasimamia suala la utafutaji wa hati kwa nyumba hizo na viwanja vyote 128 walivyonavyo sasa.

  “Mheshimiwa Naibu Waziri nakuhakikishia kulifanyia kazi suala la ufuatiliaji wa hati za nyumba na viwanja ili kuweza kuepuka migogoro na wananchi wanaovamia viwanja vyetu”, amesitiza Kaimu Meneja.

  Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amewataka wananchi kufuata sheria na kwamba hairuhusiwi kuvamia maeneo ya Serikali kwani maeneo hayo huwa yanatengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali.

  Wakala wa Majengo Mkoani Mtwara una jumla ya nyumba 76 ambapo Manispaa ya mji wa Mtwara ina nyumba 64, Masasi 4, Nanyumbu 5 na Tandahimba 3 ambapo baadhi ya nyumba hizo zina hati na nyingine hazina.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Wananchi wa Kata ya Itaka Kijiji cha Itaka wengi wao wakiwa ni akina Mama, wakijificha Mvua nje ya moja ya Kituo cha Usajili wakati wakishiriki zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea kwenye Kata hiyo


  Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambilsho vya Taifa akichukua alama za Vidole vya mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mbonji waliofika Katika moja ya Vituo vya Usajili ili kupatiwa huduma ya usajili na Utambuzi.


  Wananchi wa Kijiji cha Mbonji kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi wakiwa katika foleni kuelekea kupata huduma ya Usajili na Utambuzi wa watu yenye lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa, zoezi linaloendela katika kata nzima ya Itaka.
  Wananchi wa Kijiji cha Nsani wakiwa nje ya Kituo cha Usajili wakisubiri kupata huduma ya Usajili na Utambuzi.
  Wananchi wakiendelea na zoezi la kuchambua fomu nje ya Kituo cha Usajili katika kijiji cha Nsani Kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi kabla ya kwenda kupatiwa huduma ya Usajili na Utambuzi uliohusisha uchukuaji wa alama za kibaiologia, saini ya kielektroniki pamoja na Picha.
  Wananchi wa Kijiji cha Mbonji kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi wakiwa katika foleni kuelekea kupata huduma ya usajili na utambuzi zoezi linaloendela katika kata nzima ya Itaka.


  Pamoja na zoezi la Usajili linalohusisha ujazwaji wa fomu za maombi pamoja na kuchukuliwa alama za Kibaiologia pamoja na Picha, Mkoa wa Songwe umeanza zoezi msingi la Mapingamizi ambapo wananchi wanapata fursa ya kuhakiki taarifa zao pamoja na kuweka mapingamizi kwa mtu yoyote wanayehisi si raia au si Mkazi wa eneo husika na amefanya udsajili wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, ambapo Bi. Coletha amewasihi Wananchi wa katanganyifu kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.

  Zoezi hili lililoanza sambamba na kuendelea kwa usajili kwa Kata ambazo hazijakamilisha linahusisha Kata za ichenjezya, vwawa na mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe baada ya kukamilisha hatua ya awali ya usajili.

  Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Bi. Bi. Coletha Peter amesema zoezi hilo litahusisha wananchi wote wa mkoa wa Songwe na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye mbao za matangazo ambako picha zote za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa zimebandikwa pamoja na majina yao.

  Amesema kama Mamlaka wamejipanga kuhakikisha wanapokea mapingamizi ya watu wote watakao bainishwa kwa njia ya wazi na siri na kuhakikisha Mamlaka inayafanyia kazi majina hayo mapema sambamba na kuanza uchakataji wa taarifa za waombaji wote waliokamilisha taratibu za Usajili ili vitambulisho vianze kutolewa kwa wakati.

  “ Tumepanga siku 7 za mapingamizi ambazo ni fursa pia kwa wananchi kurekebisha taarifa zao iwapo watabaini kuna mapungufu yoyote na baada ya hapo hatutatoa nafasi tena ya mtu kurekebisha taarifa. Mbali na kurekebisha taarifa tunawaomba wananchi kuweka mapingamizi kwa wale wote ambao watakuwa wamesajiliwa na hawana sifa za kupewa vitambulisho vya Raia ili tuwaengue mapema kwenye mfumo” alisisitiza

  Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikao 16 ya Tanzania Bara inayoendelea na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa na kwa Wilaya ya Mbozi mbali na kuanza mapingamizi Kata za Isandula, Itumpi, Kilimampimbi, ipunga na kata ya Itaka ndiyo zinaendelea na zoezi la Usajili kwa sasa.

  Amesema baada ya kukamilika Kata hizo awamu ijayo itahusisha Kata za Nambizo, Magamba, Nanyala na Ruanda na kuwasititiza Wananchi ambao hawajafikiwa na zoezi kuvuta subira na kuendeela kujiandaa kwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa Viambatanisho msingi vinavyotakiwa katika zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu.

  Mikoa mingine inayoendelea na zoezi la Usajili ni Mara, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya.

  0 0


  Na Afisa Habari Mufindi

  Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Kampuni ya Siha Enterprises Limited, kutekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Sawala, wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, utakao wanufaisha wananchi wa Vijiji vine vya Kata ya Mtwango baada ya kuikosa huduma ya Maji safi na salama kwa miaka mingi.

  Hafla ya kihistoria ya kusaini kandarasi hiyo ya miezi 12, imefanyika katika kijiji cha Sawala mbele ya viongozi wa Vijiji vinne vya Sawala, Mtwango, Lufuna na kibao vinavyotarajiwa kunufaika na huduma hii muhimu kwa uhai wa binadamu.

  Akizungunza mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amemtaka Mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa ubora, kukamilisha kwa wakati kadri ya mkataba aliosaini bila kuongeza gharama na ameahidi kuufuatilia mradi huo kwa kila hatua ya ujenzi.

  Mh. Jamhuri pia, amewataka wananchi wa kata ya Mtwango kumpa shirikiano Mkandarasi katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi, huku akikemea tabia ya uwizi kwa Vijana watakaopata ajira kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata ya Mtwango.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina, amesema Ofisi yake inaimani kubwa na Mkandarasi huyo na akamtaka aanze kutekeleza ujenzi wa mradi kwa wakati kwani shauku pekee ya watu wa Kata ya Mtwango, ni kupata huduma ya Maji baada ya Mkandarasi wa awali kushindwa kukukidhi shauku yao.

  Ujenzi wa mradi wa Maji Sawala, utakelezwa na kampuni wa Siha Enterprises Limited na utasimamiwa na Ofisi ya Maji Mjini Iringa (Iruwasa), Ofisi ya Maji ya Katibu tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa muda usizidi miezi 12. Aidha, baadhi ya shughuli kubwa zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Matenki manne ya ujazo wa lita 450,000, kusambaza mabomba kwenye Vijiji husika pamoja na kujenga vituo 122 vya kukinga Maji.
   Afisa mipango wa Halmashauri isaya Mbenje, akimwonesha Mkandarasi Maeneo mbalimbali  ya kuyafanyia kazi katika chanzo cha Maji cha Sawala.
   Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.8
  Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina, kushoto wakimkabidhi Mkataba Mkandarasi Siha Enterprises kulia mara baada ya kusainiwa.

  0 0

  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka wa 2017 imeona jumla ya wagonjwa 64,093 kati ya hawa wagonjwa wa nje ni 60,796 na waliolazwa 3297. Wagonjwa waliolazwa 3010 waliruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri na wagonjwa 287 walipoteza maisha hii ikiwa ni sawa na asilimia 8.7.

  Wagonjwa 225 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua ambapo wagonjwa 200 waliruhusiwa na wagonjwa 25 walifariki Dunia hii ikiwa ni sawa na asilimia 11 (wastani wa kimataifa ni asilimia 13). Kati ya wagonjwa 225 waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 60 na watu wazima 45.

  Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 800 kati ya hao 798 wanaendelea vizuri na wagonjwa wawili (2)walifariki hii ikiwa ni chini ya asilimia 1.6. Kati ya wagonjwa 800 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 631 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.

  Tulikuwa na jumla ya kambi za matibabu 15. Tumefanya matibabu ya pamoja na washirika wetu kutoka mabara ya Asia, Australia, Ulaya na Amerika. Katika kambi zote hizo kambi za watoto ni tano na kambi za watu wazima 10. Jumla ya wagonjwa 120 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 80 na watu wazima ni 40. Wagonjwa 169 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 92 na watu wazima 77.

  Kwa wagonjwa wote hao 1025 kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua hapa nchini Taasisi imeweza kuokoa zaidi ya bilioni 29 (Tshs. 29,725,000,000/=) ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi. Gharama za mgonjwa mmoja anayetibiwa nje ya nchi ugonjwa wa moyo ni zaidi ya milioni 29.

  Tulifanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 52.

  Wakati huo huo Taasisi ilishiriki katika utoaji wa huduma ya upimaji afya bila malipo na kutoa elimu ya afya bora ya moyo kwa wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Lindi na Katavi. Katika mikoa hiyo tuliweza kuwaona na kuwapatia huduma wananchi 8000. 

  Malengo tuliyokuwa nayo kwa mwaka huu wa 2018 ni kuona wagonjwa wengi zaidi ya hawa tuliowaona mwaka 2017 katika kliniki zetu za kila siku na kufanya upasuaji. Taasisi imejipanga kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 400 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 1000.Tunatarajia kuwa na kambi maalum za upasuaji wa moyo zisizozidi 15.

  Aidha tunawaahidi wananchi kwa mwaka 2018 tutaendelea kutoa huduma katika kiwango cha kimataifa, kuendelea kupunguza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba katika Taasisi yetu, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi zaidi katika Hospitali yetu na kuzidi kushirikiana na Serikali na wananchi.

  Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika kazi zetu za kila siku ni ufinyu wa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa wagonjwa wanaotoka katika chumba cha upasuaji. Hii inatokea wakati ambao tunafanya upasuaji kwa wagonjwa wengi kwa wakati mmoja hasa kipindi cha kambi za matibabu. Pamoja na ufinyu wa wodi ya watoto. Asilimia 70 ya wagonjwa tunaowafanyia upasuaji wa kufungua kifua ni watoto, tunajumla ya vitanda 123 kati ya hivi vitanda vya watoto ni 24 tu.

  Wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hii ni changamoto nyingine tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu.

  Kwa upande wa wazazi na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo.

  Tunawashauri watu wazima kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.

  Katika Bara la Afrika Taasisi yetu iko katika nafasi ya tatu katika utoaji wa huduma bora za magonjwa ya moyo hasa katika upasuaji wa moyo kwa watoto.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Uhusiano
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

  15/01/2018

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.
   Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea katika Kituo cha Afya cha Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya Mkoani Rukwa.
   Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akikagua Idadi ya watu waliohudhuria Kituoni hapo kupitia mfumo wa Kompyuta katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.

  Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa wa Rukwa.

   Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye tisheti ya mistari) akipokea maelekezo ya ramani ya jingo jipya la Mama na Mtoto katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu na wa mwisho ni Mhandisi Mwakyembe.
  Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na ziara yake katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuata ni Mhandisi Mwakyembe na Mbunge wa Nkasi kaskazini Mh.Kessy Ally.  Na WAMJWW. RUKWA-NKASI

  Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

  “Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.

  Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.

  “Dawa zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ” aliendelea Dkt. Ndugulile.

  Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta, Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya wananchi (fixed akaunti).

  Akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.

  Dkt. Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223 vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.

  Kwa upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.

  0 0
 • 01/15/18--02:42: AJALI YAUA 11 KAGERA
 • Na Ripota wa Globu ya Jamii Kagera.

  WATU 11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.

  Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

  Dr Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

  Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki

  Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi

  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

  KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imesema imeamua kuhamishia huduma ya usafiri wa treni kutokea Dodoma kuanzia kesho.Uamuzi huo unakuja kipindi ambacho TRL imesitisha huduma za usafiri huo kutokea Dar es Salaam baada ya miundombinu ya reli kuharibika kati ya stesheni za Kilosa na Gulwe kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha maeneo hayo kuharibu miundombinu. 

  Akizungunza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (uendeshaji) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuuu wa kampuni hiyo, Focus Sahani amesema wakati wanaendelea na matengenezo ya miundombinu iliyohariviwa na mafuriko eneo hilo wameona ni vema usafiri huo ukaendelea kwa kuanzia Mkoa wa Dodoma. 

  Amesema uongozi baada ya kutathimini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yaliyo salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri huo wa treni kutokea Dodoma. Sahani amesema ratiba ya huduma ya muda wa kuanzia Dodoma ni kwamba treni ya abiria itaondoka saa moja usiku kesho Jumanne na Ijumaa kwenda Kigoma, Mwanza Name Mpanda ambako inatarajiwa kuwasili Mwanza saa 12 jioni siku ya Jumatano na Mpanda saa 12 jioni na Kigoma saa 12 jioni. 

  "Treni kutoka Mpanda, Mwanza na Kigoma zitatoka huko siku za Jumapili na Alhamis tu. Mpanda inatoka saa moja asubuhi, Mwanza inatoka saa mbili asubuhi na Kigoma inatoka saa1:30 asubuhi.Treni hizo zinafika Dodoma siku ya Jumatatu na Ijumaa saa 1:00 asubuhi, "amesema. 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Focus Sahani akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa kampuni hiyo kutangaza ratiba ya usafiri wa treni kuanzia Mkoa wa Dodoma kwenda mikoa mingine baada ya huduma ya usafiri huo kusitishwa kwa stesheni ya Dar es Salaam.Pichani kushoto ni wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro  mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini  kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro  mara baada ya kufanya mazungumzoleo ofisini  kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) baada ya kuwasili kwenye kambi ya Uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila leo na kuongea na wavuvi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a (mwenye kofia) na kulia zaidi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe Frank Bahati leo. Mhe. Mpina alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiwahutubia wavuvi kwenye kambi ya wavuvi katika kisiwa cha Galinzila Wilayani Ukerewe ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji Kakukuru.
  Umati wa wavuvi kwenye kambi ya wavuvi ya Kisiwa cha Galinzila wilayani Ukerewe wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) ambapo baadaye alichoma moto nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni mbili katika kijiji cha Kakukuru zilizokamatwa katika operesheni maalum ya siku tano ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Ukerewe leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi kilichofanya operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu katika Wilaya ya Magu na Busega mara baada ya kuteketeza kwa kuchoma moto zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Tsh 457,075,000/= katika kijiji cha Kageye wilayani Magu leo. 


  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina ametaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2 zilizokamatwa wakati zikitumika kwa shughuli za uvuvi katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza huku Shilingi milioni 120 zikikusanywa kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji samaki na mazao yake nje ya nchi.

  Waziri Mpina aliwaonya watu wanaotumia majina ya wavuvi kutishia kufanya migomo isiyoisha na kuandamana baada ya uamuzi wa Serikali kuanza kuchukua hatua stahiki za kudhibiti uvuvi haramu, na kwamba msimamo uliowekwa na Serikali ni thabiti na usiyoyumba hivyo migomo na maandamano ya watu wenye lengo la kukwamisha vita dhidi ya uvuvi haramu haitasaidia chochote na badala yake operesheni kali isiyo na mwisho itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma ndani ya Ziwa Victoria.

  “Rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi sisi viongozi mliotupa dhamana ya kuongoza kazi yetu ni ulinzi tu na endapo tutakomesha uvuvi haramu nyie ndio mtakaonufaika hivyo ni itashangaza tajiri aliyempa kibarua cha ulinzi, na mlinzi huyo akafanya kazi vizuri ya kulinda mali za bosi wake alafu tajiri akamlalamikia kibarua wake sisi na watendaji wa Serikali ni vibarua tu wenye mali ni ninyi hatua tunazochukua zitaleta manufaa makubwa kwenu”alisema.

  Pamoja na kuteketeza zana haramu, Waziri Mpina alieleza hali ya upatikanaji wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia 96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.

  “Tafsiri yake ni kwamba ziwa halina samaki wanaostahili kuvuliwa kulingana na kasi ya uvuvi na pia samaki wazazi ni kidogo ambapo inatishia kumalizika kwa samaki na shughuli za uvuvi kukoma katika Ziwa Victoria’alisema . 

  Akizungumza kwa nyakati tofauti na maelfu ya wavuvi katika Visiwa vya Gagalini na Kakukuru wilayani Ukerewe Waziri Mpina amesema hatua kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi kuwaonea wananchi wanyonge bali kuwatengenezea maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali zilizoko ziwani.

  Akiwa katika eneo la Kakukuru Waziri Mpina alishiriki kuteketeza zana haramu zikiwemo vyavu za Makila 14,103, Kokoro 188 , Nyavu za dagaa 211, Nyavu za timba 450, Kamba za Kokoro 10,700 na ndoano 18,450 na Mitumbwi 109 zenye thamani ya sh. Bilioni 2.

  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwaidi Mlolwa amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 26 (i) (ii) kinamtaka kila mtanzania kulinda rasilimali za nchi yetu ikiwemo samaki na mazao yake huku Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zikikataza vitendo vya kutumia zana zisizoruhisiwa kwa mujibu wa sheria.

  Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomihn Chang'a alisema Serikali ya wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe , Frank Bahati alisema halmashauri imewasimamisha kazi watumishi watatu kwa tuhuma za kujihusisha na uvuvi haramu.Kwa upande wao baadhi ya wavuvi walimuomba Waziri Mpina kuwasiliana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa kutengenezwa na kisha kuuziwa wavuvi.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

  Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.

  Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed Mgoyi,Amina Karuma na Sarah Tchao.

  Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.

  Kuteuliwa kwa viongozi hao wa TFF ni muendelezo CAF kuteua viongozi wa TFF kwenye kamati mbalimbali itakumbukwa hivi karibuni Rais wa TFF aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN inayoendelea nchini Morocco lakini pia akiteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.

  Atoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.Waziri Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu, ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.

  Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza tena 2010.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kuanza ziara mkoani humo Januari 15, 2017. Kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima,   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  majengo ya Shule ya  Secondari ya Ufundi Musoma akiwa  katika  ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017.Serikali imetoa shillingi bilioni 1.28 kwa ajilli ya ukarabati huo.  Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Mutta Venance. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitoka ndani ya bweni la Shaban Robert wakati  alipokagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma  akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara  Januari 15, 2017. Serikali imetoa zaidi ya shilling bilion 1.28 ili kugharimia ukarabati hou. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya  Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa mjini Musoma  akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 15, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.


  0 0  0 0

    MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Inaya Zanzibar Limited Cheherazade Cheikh akitoa maelezo ya bidhaa za kampuni yake katika Maonesho ya Tamasha la Nne la Biashara Zanzibar linalofanyika katika viwanja vya mpira maisara.(Picha na Ikulu)
   MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitembelea maonesho Tamasha la nne la Biashara katika viwanja vya mpira vya maisara Zanzibar akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZAIDAT cha Chukwani Tatu Suleiman, wakati akitembelea maonesho hayo.
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha ZANAP Nassor Hamad Omar, akitowa maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi chao wakati wa maoenesho ya Biashara katika viwanja vyaa maisara Zanzibar.
   WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amani Salum Ali akizungumza wakati wa Kongamano la Afya na Maisha Bora, wakati wa Tamasha la Nne la Maenesho ya Biashara katika viwanja vya maisara Zanzibar.
   MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Afya na Maisha Bora kwa Washiriki wa Tamasha la Nne la Maonesho ya Biashara katika viwanja vya Maisara Zanzibar.lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanja na Masoko Zanzibar.
   BAADHI ya Washiriki wa Kongamano la Afya na Maisha Bora lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko kwa Wajasiriamali katika viwanja vya maisara Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwaamwema Shein, akifungua Kongamano hilo la Siku moja.(Picha na Ikulu) 
   MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Waziri wa  Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali alipowasili katika viwanja vya maisara Zanzibar kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Afya na Maisha Bora. lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko.(Picha na Ikulu)


  0 0


  Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo Tukutane Januari Akaunti, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla. 

  Akizungumzia Kuhusu akaunti hii mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka. 

  Vilevile inamuwezesha mteja wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake. 

  Akaunti hii ya akiba itamuwezesha mteja kujiondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule na vyuo na manunuzi mengine ya vifaa vya shule, pia kodi za nyumba hivyo kuondokana na dhana ya Januari kuwa ni mwezi mgumu. 

  Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia sana kutatua matatizo mengi yanayoikabili familia na jamii kwa ujumla. “Mara nyingi watu wamejikuta wakiingia katika madeni makubwa na fedheha pale wanaposhindwa kulipa madeni hayo”, alisema Ndugu Manongi. 

  Akiendelea Ndg Manongi alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imebuni mkakati huu kuisaidia jamii kuazimia kupunguza na/ama kuondokana na fedheha, adha na madhara yanayotokana na kuwa na majukumu mazito mwezi huo wa kwanza wa mwaka”. 

  Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko aliongeza kwa kusema “Uzinduzi wa huduma hii mwanzoni mwa mwaka 2018 ni moja ya ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Hivyo tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Commercial Plc,  (MCB) Ronald Manongi (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa ujiwekea akiba kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka.  
   Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa kujiwekea akiba kwa wateja wake na kwa watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka.  
  Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tuki la uzinduzi wa akaunti mpya ya Tukutane Januari ya Benki ya Mwalimu Commercial Plc jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kulia), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma leo, Januari 15 2018.
   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akifurahia jambo na Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko (kushoto kwa Waziri) alipofika ofisini kwake kumsalimu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati. 
   Naibu Waziri mpya wa Madini Dotto Biteko, akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati (hawapo pichani), alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akizungumza, wakati wa hafla fupi ya kumpokea Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (katikati) Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Januari 15 mwaka huu. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. 
  Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, wakimsikiliza Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma Januari 15 mwaka huu.


  Na Veronica Simba – Dodoma
  Naibu Waziri mpya wa Madini, Dotto Biteko ameeleza kuwa anatamani kuiona sekta ya madini ikichangia zaidi ya ilivyo sasa katika Pato la Taifa.
  Ameyasema hayo mapema leo, Januari 15 mjini Dodoma, alipowasili rasmi katika Ofisi yake ya Makao Makuu na kupokelewa na viongozi mbalimbali pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini na wa Wizara ya Nishati.

  Amesema kuwa, sekta ya madini inaweza kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa kutoka asilimia Nne ya sasa na kuweza kufikia asilimia 10 au zaidi ikiwa kutakuwa na ushirikiano baina ya wafanyakazi wote na viongozi wa Wizara huku kila mmoja akijituma kutimiza wajibu wake ipasavyo.
  “Tujiulize hivi ni kwanini hadi leo sekta hii inachangia asilimia Nne tu katika Pato la Taifa badala ya kupanda hadi asilimia 10 au zaidi. Tubainishe ni madini yapi yanayotupatia fedha nyingi zaidi na ni mbinu gani tutumie ili tuweze kupanda zaidi,” amesisitiza.

  Hata hivyo, Naibu Waziri Biteko alibainisha kuwa ujio wake wizarani haulengi kubadili au kugeuza mambo bali ni kuongeza nguvu zaidi kwa watangulizi wake katika kutekeleza yale ambayo yameagizwa na Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa niaba ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  “Tuombeane kwa Mungu atupe kibali, hekima na uwezo wa kuyaona matatizo lakini zaidi sana atupe uwezo wa kutekeleza majukumu yetu ili sekta hii ya madini iwe sekta ambayo ina mchango mkubwa kwa Taifa letu.”
  Aidha, amesema kuwa falsafa yake ya utendaji kazi ni kwa kila mmoja kuheshimu nafasi ya mwenzake bila kujali nafasi aliyonayo. 

  “Binafsi ninaamini hakuna mkubwa kwenye kufanya kazi. Ukubwa wako unaonekana kwenye matokeo ya kazi unayofanya. Kwa hiyo tushirikiane wote. Mimi ninaamini katika nguvu ya ushirikiano,” amesisitiza.

  Viongozi mbalimbali waliompokea Naibu Waziri Biteko akiwemo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Madini Profesa Simon Msanjila, wamemwahidi ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

  Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga amempongeza Naibu Waziri kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kueleza kwamba wafanyakazi wanayo imani kubwa kuwa atasimamia vema utekelezaji wa majukumu katika sekta husika.

  “Hii ni kwa sababu tunaamini unaifahamu vema sekta ya madini kutokana na kuwa umekuwepo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa muda mrefu na umeweza kuisimamia vizuri.”

  Wafanyakazi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati wana uhusiano wa karibu kikazi kutokana na kufanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu katika iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kabla ya kutenganishwa na kuwa Wizara mbili tofauti. Hii ndiyo sababu wangali wanashirikiana katika mambo mbalimbali kama hafla hii ya kumpokea Naibu Waziri.

  Naibu Waziri Biteko aliteuliwa katika nafasi hiyo Januari 6 mwaka huu na kuapishwa tarehe 8 Januari na Rais John Magufuli.

older | 1 | .... | 1486 | 1487 | (Page 1488) | 1489 | 1490 | .... | 1897 | newer