Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

DKT. MAHIGA AKUTANA NA TIMU YA KUCHUNGUZA MAUAJI YA ASKARI NCHINI DRC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wawili hao walifanya mazungumzo jijini Dar Es Salaam leo ambapo Bw. Titov aliahidi kuwa Timu yake itaifanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kubaini chanzo cha mauaji na kutoa mapendekezo ya kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayatokei tena katika siku zijazo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC.

Mjumbe kutoka Tanzania wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Mjumbe pekee wa kike wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe mwingine wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe kutoka Nigeria wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakiendelea kusalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRCwakifuatilia mazungumzo.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo.

Wajumbe wa pande mbili wakiwa katika mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga mstari wa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


WAZIRI WA MAJI AWAAGIZA WAKANDARASI WA MAJI KUMALIZA MAPEMA MIRADI HIYO

$
0
0
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro pamoja na Buseresere wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi kwenye Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. 
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. 



Na,Joel Maduka,Geita.

Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji maji ambayo imeendelea kuwakabili kwa muda mrefu .

Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.

Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza wakandarasi wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.Katika Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata maji safi na salama ni ni asilimia 41.

TANGAZO KWA ABIRIA WA TRENI ZA KWENDA BARA.

$
0
0
KAMPUNI YA RELI TANZANIA

TANGAZO KWA ABIRIA WA TRENI ZA KWENDA BARA.

KAMPUNI YA RELI TANZANIA INASIKITIKA KUTANGAZA KWAMBA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI  MIUNDOMBINU YA RELI YETU KATI YA KILOSA NA GULWE IMEHARIBIKA. 

KUTOKANA NA UHARIBIFU HUO UMESABABISHA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI KUSITISHWA KWA MUDA KUTOKEA DAR ES SALAAM KWENDA DODOMA ILI KUWEZESHA UKARABATI WA MIUNDOMBINU HIYO KUFANYIKA KWA HARAKA.

KAMPUNI INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA KATIKA KIPINDI AMBACHO HUDUMA HII YA USAFIRI HAITAKUWEPO MPAKA HAPO  ITAKAPO REJESHWA TENA NA WANANCHI WATAFAHAMISHWA  RASMI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.

HATA HIVYO HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI YA ABIRIA NA MIZIGO KWA TRENI YA KUTOKA DODOMA KWENDA TABORA - MWANZA - KIGOMA NA MPANDA ITAENDELEA KAMA KAWAIDA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO KWA NIABA YA
MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL 
ND MASANJA KADOGOSA
MAKAO MAKUU YA TRL
DAR ES SALAAM
JANUARI 13, 2018

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.

………………

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.

Akihutubia katika mkutano wake kwa wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.

Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa maendeleo ya Tanzania.

Kwa upande wao wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.

Article 0

$
0
0
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka  akiwa na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo katika ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kurui.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka  akivishwa skafu wakati alipofika katika kata ya Kurui kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka  akimnadi mgombea wa udiwani wa kata ya Kurui Mussa Kunikuni

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka  akipokea mmoja wa wanachama kutoka vyama vya upinzani

 Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akizungumza katika ufungaji wa kampeni za udiwani kata ya Kurui
..................................................................................................
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka  amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Selemani Jafo kwa uchapakazi wake uliotukuka na hivyo amewataka wananchi wa kata ya Kurui wilayani Kisarawe wasifanye makosa kabisa wahakikishe wanamchagua Mussa Kunikuni kuwa diwani wa kata hiyo katika uchaguzi utakaofanyika kesho Januari 13, mwaka huu.


Akifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kurui Shaka amesema wananchi watakapomchagua Mussa Kunikuni hapo kesho itasaidia kuleta maendeleo makubwa katika kata hiyo kwa kuwa atakuwa anaunganisha juhudi kubwa inayofanywa na Rais John Pombe Magufuli pamoja na Mbunge Jafo katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya kata hiyo na wilaya nzima kwa ujumla.


Naye,Mwenyeki wa mkoa wa Pwani ndugu Ramadhani Maneno amewataka wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa katika uchaguzi wa kesho kwani mkoa mzima wa Pwani umeelekeza jicho lake katika kata hiyo ile kuleta heshima kwa mkoa wa Pwani.

ALICHOKIZUNGUMZA NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YAJAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. DKT. NDUGULILE KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Attachments area Preview YouTube video ALICHOKIZUNGUMZA DKT. NDUGULILE KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI WA MKOA WA RUKWA.

VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA WAAGIZWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI.

$
0
0

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafala wa ukaguzi wa jingo jipya  katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa katika Kituo cha Afya Mazwi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface Kasululu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiwa ndani ya jengo jipya la wodi ya kina mama wajawazito, katika ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika kituo hicho.
 

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akipitia ramani ya jengo jipya la mama na mtoto linaloendelea kujengwa katika hatua ya kuboresha huduma katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali katika moja ya jengo jipya linalojengwa katika kuboresha kituo cha Afya cha Mazwi.
 
 
Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu wa Lishe bora.

Ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya, na uhamasishaji wa vikundi vidogo vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.

”Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo, asilimia 60 ya udumavu ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao una chakula na ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo hili”, Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kwa kusema kuwa, Siku 100 za mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na nyeti sana katika kuhakikisha anapata maziwa ndani ya miezi sita, na anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue vizuri.

Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa sekretarieti ya Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya kuhusiana na masuala ya Lishe bora ili kutokomeza janga hili linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa huu.

Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly amemshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakumbuka katika mgao wa fedha za kuboresha Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza sauti juu ya ombi la gari la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha kubwa wanayokumbana nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa unaendelea kupambana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu ya Afya na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha magonjwa haya yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.

Aidha, Dkt. Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha ya upungufu wa madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya madaktari 24 wanaohitajika.
 
 

RAIS DKT MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA RWANDA MH.PAUL KAGAME LEO JIJINI DAR

$
0
0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpogea mgeni wake Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame mara baada ya kuwasili mapema leo nchini kwa ziara ya siku moja.  .Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame akisalimiana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili mapema leo nchini kwa ziara ya siku moja. Pichani kulia ni Rais Dkt John Pombe Magufuli na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga .Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame aliyewasili mapema leo katika uwanja wa ndege wa Kimaifa wa Julius Nyerere (JNI),akiwa katika ziara yake ya siku moja nchini
Burudani pia ilitolewa wakati wa makokezi ya Rais wa Rwanda.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa  pichani kulia akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh.Kisare Makori (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Alli Hapi wakati wa mapokezi ya Rais wa Rwanda Mh Paul Kagame aliyewasili mapema leo asubuhi nchini kwa ziara ya siku moja

SERIKALI YAMCHARUKIA MKANDARASI DOTT

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Dott Service na Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Kyongdong Engineering wanaojenga barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo haraka.
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara, Mheshimiwa Abdallah Chikota (Wa kwanza kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, (Wa pili kulia) sehemu yenye mteremko mkali katika mlima wa Nameleche uliopo katika barabara ya Mtwara-Mnivata-Tandahimba-Newala hadi Masasi yenye urefu wa KM 210 ambapo magari husumbuka katika kipindi cha mvua kutokana na mteremko huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnivata mkoani Mtwara alipofika hapo kukagua barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa Barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi Dott Service, anayejenga barabara hiyo kukamilisha ujenzi wake haraka.


Serikali imemtaka Mkandarasi Dott Services anayejenga barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami kuongeza vifaa na kasi katika ujenzi wa barabara hiyo ili kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao na abiria kwa wananchi wa mkoa huo.

Akitoa agizo hilo mkoani Mtwara, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kusisitiza kuwa mkandarasi huyo anatakiwa kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unaendana sawia na thamani ya fedha zilizotolewa na ubora kwa kiwango cha kisasa.

“Hakikisha unaongeza vifaa na kasi ya ujenzi wa barabara hii, la sivyo tutakutoa na hutapata kazi nyingine ya ujenzi wa barabara hapa nchini”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.Ametoa rai kwa Makandarasi wote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, weledi na kuhakikisha kazi wanazopewa zinakamilika kwa wakati na ikiwezekana hata kabla ya muda wa mkataba ili kuweza kuokoa fedha za Serikali.

Aidha ameutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani hapo pamoja na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Kyongdong Engineering, kuusimamia madhubuti mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na viwango vinavyostahili na hivyo kuweza kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa huo haraka iwezekanavyo.

Naibu Waziri huyo amesema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na ya uhakika kupitia miundombinu bora ya barabara vipindi vyote vya mwaka hivyo fedha za kuwalipa makandarasi zipo tayari ni jukumu lao kuikamilisha mapema.

Naye Meneja wa TANROADS mkoani hapo, Mhandisi Dotto Chacha amemhakikishia Naibu Waziri huyo kumsimamia mkandarasi huyo na kuhakikisha anamaliza ujenzi wa barabara hiyo kama ilivyopangwa katika mkataba.Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga barabara hiyo Mhandisi Michael Mudanye, ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwalipa fedha za awali ambazo zimewasaidia kuleta vifaa eneo la kazi.Ameongeza kuwa wamejipanga kukamilisha barabara hiyo kwa wakati kwani watafanya kazi usiku na mchana.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba mkoani humo, Mhe. Abdallah Chikota, amesema kuwa wananchi wanaisubiri barabara hiyo ikamilike kwa lami kwa kipindi kirefu kwani wamekuwa wakiteseka kutokana na vumbi pamoja na mashimo yaliyopo katika barabara hiyo.Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 89 na unatarajiwa kukamilika mwezi January mwakani. Barabara hiyo ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Newala-Masasi KM 210 kwa kiwango cha lami.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye Gadi ya Jeshi ya heshma pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili (hazionekani pichani ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia frame ya Picha ya Kiasili aliyokabidhiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumpokea mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WATILIANA SAINI MKATABA MPYA WA USHIRIKIANO NA CHUO CHA UKAMANDA DULUTI

$
0
0
Kushoto ni mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akitiliana saini na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi mkataba mpya wa ushirikiano (MoU) kati ya chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha  unadhimu Duluti .Anayeshuhudiana wa kwanza kulia kwa upande wa chuo cha uhasibu Arusha ni Denson Ndiyemalila,upande wa kushoto ni shuhuda ni Emmanuel Nyivambe kutoka chuo cha Unadhimu Duluti.zoezi hilo lilifanyika katika chuo cha Uhasibu juzi jijini Arusha.(Habari Picha na Pamela Mollel)
Kushoto ni Mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akikabidhiana mkataba mpya wa ushirikiano(MoU) na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi mara baada ya kutiliana saini kati ya chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha  unadhimu Duluti .
Kushoto ni mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Meja Jenerali H.Masebu akizungumza mara baada ya kutiliana saini  mkataba mpya wa ushirikiano(MoU) kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi .
Picha ya pamoja ya kumbukumbu mara  baada utilianaji saini huo.

MIGODI YA WACHIMBAJI WADOGO BUHEMBA YAFUNGULIWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini, Stansalus Nyongo (kulia) akijiandaa kufungua rasmi Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo wa Buhemba, Wilayani Butiama Mkoani Mara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) wakati wa kufungua migodi ya wachimbaji wadogo ya Buhemba. Wa pili kutoka kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akijiandaa kufungua rasmi migodi hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akifungua rasmi migodi ya Buhemba ya wachimbaji wadogo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa migodi ya wachimbaji wadogo ya Buhemba, Mkoani Mara.


Hatimaye Serikali imefungua Migodi ya Dhahabu ya Wachimbaji Wadogo iliyopo katika eneo la Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara baada ya kujiridhisha hali ya usalama katika migodi hiyo.

Migodi hiyo imefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo Januari 13, 2018 na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.Akizungumza katika tukio hilo, Nyongo alisema jumla ya migodi 10 imefunguliwa kati ya 16 baada ya kujiridhisha usalama wake.

Alifafanua kwamba eneo la Buhemba lina jumla ya Migodi ya Dhahabu 16 ambayo inamilikiwa na Wachimbaji Wadogo hata hivyo iliyokidhi vigezo vya kiusalama ni Migodi 10 pekee ambayo imeruhusiwa kuendeleza shughuli za uchimbaji.

Alisema Serikali ilisitisha shughuli za uchimbaji Madini kwenye eneo hilo la Buhemba Februari 2017 baada ya kutokea vifo vya Wachimbaji Saba na wengine wapatao 15 kujeruhiwa kutokana na kufanya shughuli zao bila kuzingatia taratibu na kanuni za uchimbaji salama.

Alibainisha kuwa Mwezi Desemba mwaka jana alifanya ziara kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao ambapo aliagiza shughuli za ukaguzi zikamilike ifikapo Mwezi huu wa Januari ili migodi ifunguliwe.

“Kama mtakumbuka nilifanya ziara hapa na niliagiza kufikia Januari 10, 2018 Ukaguzi wa Usalama kwenye eneo la Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba uwe umekamilika ili shughuli za uchimbaji zilizokuwa zimesimamishwa ziruhusiwe; tumejiridhisha mashimo kumi ni salama na sasa tunafungua rasmi,” alisema Naibu Waziri Nyongo.Alisema shughuli hiyo ya Ukaguzi kama alivyokua ameagiza ilifanyika kwa umakini na kwamba maduara Kumi (Migodi Kumi) yameruhusiwa na mengine Sita hayatoruhusiwa kuendeleza shughuli za uchimbaji.

Aliongeza kuwa baada ya kufika kwenye eneo hilo kwa mara ya kwanza alisikitishwa kuona wananchi wengi wakiwa wamekosa shughuli za kufanya kutokana na migodi hiyo kufungwa na ndiyo sababu ya kuagiza ukaguzi wake ukamilike haraka.“Nilivyotembelea hapa Mwezi Desemba mwaka jana nilisikitishwa kuona shughuli za uchumi kwenye eneo hili la Buhemba zimesimama kutokana na shughuli za uchimbaji kusimamishwa baada ya kutokea ajali,” alisema.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo aliwaagiza Wakaguzi wa Migodi kuhakikisha wanatembelea mara kwa mara maeneo ya migodi ili kukagua hali ya usalama pamoja na kutoa mafunzo ya uchimbaji salama kwa wachimbaji hususan wadogo lengo likiwa ni kuepusha ajali.“Ninawaagiza kwa mara nyingine Wakaguzi wa Migodi kuhakikisha mnatembelea maeneo ya migodi mara kwa mara ili kuepusha ajali,” aliagiza Naibu Waziri.

Naibu Waziri Nyongo vilevile aliwaagiza wachimbaji madini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji ili kuepusha ajali migodini na wakati huohuo kunufaika ipasavyo na shughuli zao bila kupata usumbufu.Aidha, Naibu Waziri alizungumzia ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali ambapo aliwaagiza wachimbaji hao kuhakikisha wanalipa kwa mujibu wa sheria na alionya kwamba mgodi utakaoshindwa kulipa inavyostahili, utafungiwa.

“Tumewafungulieni migodi yenu tukiamini kwamba nanyi mtatimiza wajibu wenu wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria. Mkishindwa kulipa, hatutosita kuifungia,” alibainisha Nyongo.Naibu Waziri Nyongo yupo Mkoani Mara kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi na kuzungumza na wachimbaji wadogo.

NAIBU WAZIRI KIJAJI AFANYA UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

$
0
0

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)amabye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la Wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha,alisema madhumuni ya baraza hilo ni kuwapa fursa watumishi kupitia wawakilishi wao pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali.(Habari Picha na Pamela Mollel)
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Makamu Mweneyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Bw.Juma Kaniki akisoma risala katika uzinduzi huo
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)katikati akinyoosha juu mkataba wa kuunda baraza ambao umehakikiwa na kusainiwa na Kamishna wa kazi,wa pili kulia niKaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi,na wakwanza kushoto ni Didas Malekia Mwenyekiti wa tawi la IAA chama kilichounda baraza la wafanyakazi(THTU)
Sehemu ya Baraza la Wafanyakazi Chuo cha Uhasibu Arusha

Baadhi ya wanafunzi chuo cha Uhsibu Arusha wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa umakini ambapo pamoja na mambo mengi Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji aliwasisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa mshiriki mkubwa wa kupambana na rushwa ambayo inajikita katika kupotosha na kumomonyoa maadili.

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha Tarehe 10 Januari 2018

RC MNYETI KUWACHUKULIA HATUA WANASIASA WACHOCHEZI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa wa Wilaya ya Kiteto kuwa atawachukulia hatua kali wote watakaosababisha migogoro ya ardhi kwa wananchi. 

Akizungumza kwenye kata ya Njoro, Mnyeti alisema atawachukulia hatua kali wanasiasa hao kwani yeye siyo mkuu wa mkoa wa maboksi anayeogopa kulowanishwa na mvua. Alisema alipata taarifa ya baadhi ya wanasiasa wanaotumia migogoro ya ardhi kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa, ila hatawafumbia macho wanasiasa wa aina hiyo waliopo wilayani Kiteto. 

"Tumekuwa na migogoro isiyokwisha, wewe una shamba lako kwenye kijiji cha Bwawani kuna mtu anakuzuia kulima hapa Njoro? au ukiishi hapa Njoro kuna mtu amekunyima kununua nyumba kule Kibaya makao makuu ya wilaya?" alihoji Mnyeti. Alisema atawashughulikia wanasiasa hao wanachochea migogoro ya ardhi baina ya watu na watu na kijiji na kijiji ili iwe funzo kwao na hawatasahau kitendo hicho. 

"Wanasiasa hao wababaishaji, wanaojaribu kuishika serikali sharubu nitakula nao sahani moja, kwani hatuwezi kukubali hali hiyo ijitokeze na kuacha kuchukua hatua kwao bila kuangalia vyeo vyao," alisema Mnyeti. Hata hivyo, alimuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto, mhandisi Tumaini Magessa kuhakikisha vijiji vyote vinawekewa alama za mipaka ili kuondokana na migogoro ya ardhi. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel ambaye ni diwani wa kata ya Chapakazi ni mmoja kati ya viongozi wanaotajwa kusababisha migogoro hiyo wilayani Kiteto alikana kujihusisha nayo. "Mheshimiwa mkuu wa mkoa afanye uchunguzi wake na atabaini kuwa mimi sihusiki na uchochezi wa migogoro hiyo ya ardhi zaidi ya kuongoza halmashauri yangu ya wilaya kupitia nafasi hii," alisema Mollel. 

Pia, mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian ambaye naye anatajwa kuhusika na uchochezi wa migogoro alisema wapinzani wake wa kisiasa ndiyo wanasambaza habari hizo potofu kwani yeye hausiki. Awali, mmoja kati ya wakazi wa Njoro Amina Omary alisema wanasiasa hao wamekuwa mwiba mkali kwao kwani wamekuwa wachonganishi kwa wakulima na wafugaji kwa lengo la kujipatia kura pindi kipindi cha uchaguzi kitakapofika. 

Omary alisema wanasiasa hao wamekuwa wanawaunga mkono wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima badala ya kuwakataza ili kuepusha migogoro isiyo kuwa na tija. 

Ramadhan Juma alimuomba mkuu huyo wa mkoa kuwachukulia hatua kali wanasiasa hao wababaishaji ili kuepuka kutokea kwa mapigano kama ya miaka iliyopita ambayo ilichochewa nao na kusababisha mauaji. 
 Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza kwenye Kata ya Njoro Wilayani Kiteto juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi, kushoto ni mbunge wa jimbo hilo Emmanuel Papian na Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Tumaini Magessa.
Wananchi wa Kata ya Njoro Wilayani Kiteto, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza nao,  juu ya kuwachukulia hatua kali wanasiasa wanaosababisha migogoro ya ardhi.

NAIBU WAZIRI WA MADINI BITEKO ,AMEWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI.

$
0
0
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,akisaini kwenye kitabu cha wageni wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita. 
Afisa madini wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akitoa taarifa ya shughuli za madini mbele ya Naibu waziri wa madini Doto Biteko . 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko Akizungumza na Viongozi na Watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea 
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akitoa mkono wa pole kwa familia ambayo imekumbwa na msiba wa kuondokewa na kijana wao ambaye alifukiwa na kifusi wakati akiwa kwenye kazi ya uchimbaji. 
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akisalimiana na kutoa pole kwa kaka yake na marehemu wakati alipofika nyumbani kwao na marehemu.(PICHA NA JOEL MADUKA)
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akifurahia na wananchi wa kijiji cha Ikalanga wakati alipokwenda kuzungumza nao juu ya mikakati ya maendeleo. 


Na,Joel Maduka,Geita.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwenye maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.

Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye mgodi mdogokijiji cha Buntubili eneo ambalo hivi karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye mazingira hayo.

“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja anakufa katika mazingira ya uzembe tunatamani tuone watanzania wote wanachimba wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili ,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.

Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini amewataka wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza kujisabasha hatari ya kupoteza maisha kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali nzuri ya uchimbaji.

Akisoma taarifa kwa Naibu waziri wa madini,mlinzi wa eneo hilo la mgodi ,Bw Christopha Mazige .amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na ubishi wa vijana watatu ambao walivamia mgodini hapo kwa lengo la kutafuta mali lakini ghafla wakiwa kwenye mabishano sehemu moja ya ardhi alipokuwa amesimama kijana ambaye alifukiwa na kifusi ilikatika na kushuka naye kwenye shimo kutokana na hali hiyo wenzake walikimbia.

Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Mhandisi Ally Maganga amesema bado kuna changamoto zinazoikabili Sekta ya madini kama baadhi ya Wachimbaji wadogo kushindwa kulipa kwa wakati tozo stahiki za madini kama vile ada za mwaka za leseni na Mrabaha wa madini.

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOKUTANA NA RAIS PAUL KAGAME,IKULU JIJINI DSM JANUARI 14,2018

RAIS DKT MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS KAGAME WA RWANDA BAADA YA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018


 Rais Paul Kagame wa Rwanda akiongea na vyombo vya habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akiongea na vyombo vya habari baada ya mazungumzo yake  rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018

Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018.PICHA NA IKULU

Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

$
0
0
Na. Judith Mhina 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuunganisha Reli ya Kisasa (Standard Gauge) kutoka Isaka mkoani Shinyanga mpaka Kigali nchini Rwanda, ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizi mbili.

Rais Magufuli ameeleza hayo leo Ikulu Jijini Daar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame aliyekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.“Mimi na Rais Kagame kumeongea mambo mengi ya ushirikiano na kwa pamoja tumekubaliana kuanza ujenzi wa Reli ya Standard Gauge kutoka Isaka mpaka Kigali,” ameeleza Rais Magufuli.

Ameeleza kuwa ili kuharakisha ujenzi wa reli hiyo, kwa pamoja wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na sekta ya ujenzi na wale wale wa Mambo ya Nje wa nchi hizi mbili kukutana haraka wiki ijayo kusughulikia masuala kadhaa yanayohusu ujenzi wa reli hiyo ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya upatikanaji wa fedha za ujenzi.

Akielezea umuhimu wa kukuza uchumi na biashara baina nchi hizi mbili, Rais Magufuli amesema mpaka sasa mwenendo wa biashara kati ya nchi hizi umekuwa wa kusuasua na kwamba reli hiyo itasaidia kuimarisha biashara na ushirikiano wa Tanzania na Rwanda.

“Tunataka ikifika mwezi Desemba mwaka huu, mimi na Rais Kagame tuwe tayari tumeweka mawe ya msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hii,” alisisitiza Rais Magufuli.

Amesisitiza kuwa mbali na kuimarisha uchumi, ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa takribani kilometa 400 pia utatoa ajira kwa vijana wengi na kusaidia usafirishaji wa madini ya Nickel kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Tanzania ambapo madini hayo yanashindwa kuchimbwa kutokana na kukosekana usafiri madhubuti wa reli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kwamba Tanzania inamuunga mkono Rais Kagame kwa asilimia mia moja katika kuchukua Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba itafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi marafiki pia zimuunge mkono Rais huyo wa Rwanda.

Kwa upande wake, Rais Paul Kagame amemshukuru Rais Magufuli na Watanzania kwa kumuunga mkono katika nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba atafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi za Afrika kuongeza uwekezaji na kila nchi kuweka kikakati ya kuongeza ajira ili kuwafanya vijana waachane na dhana ya kukimbili nchi za Ulaya kutafuta maisha bora.

“Tatizo la vijaqna kukimbilia nchi za Ulaya linaweza kumalizika iwapo sisi Waafrika kwa umoja wetu tutashirikiana na kutafuta ufumbuzi, ikiwa ni pamoja na nchi moja moja kuweka mikakati madhubuti ya kuwapa elimu na ujuzi sahihi ili vijana hawa waweze kumudu mazingira yao na kujiendeleza.” Ameeleza Rais Kagame.

Aidha, Rais Kagame amesifu utendaji kazi wa Rais Magufuli na kuahidi kuja mara kwa mara nchini Tanzania kwa ajili ya ushauri na kujifunza zaidi. “Naahidi kuwa nitakuwa nakujamara kwa mara kuomba ushauri kutoka kwa Rais Magufuli ili kuweza kusaidia nchi zetu na Bara la Afrika kwa ujumla. Alimalizia Kagame

Hii ni ziara ya tatu kwa Rais Kagame kuzuru Tanzania tangu Rais Magufuli aingie Madarakani mwaka 2015. Mara ya kwanza alikuja kuhudhuria sherehe za kuapishwa John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).“Wakati Serikali inapambana kupunguza makato ya hovyo kwa wakulima, kumbe huku kuna chombo cha kuwachukulia fedha wakulima hii haikubaliki.”
Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa  majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo yanaingiliana na yale ya Bodi ya Kahawa, ambayo ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya zao hilo, hivyo hakuna haja ya kuwa vyombo viwili vinavyofanya kazi moja.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”
Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie uuzwaji wa zao hilo na kuwachukulia hatua wote watakaokutwa wananunua kahawa kwa wakulima. “Anayetaka kahawa akanunue mnadani na si kwa wanavijiji lengo ni kuhakikisha mkulima anapata tija.”
Pia ameziagiza halmashauri zote zinazolima kahawa nchini kuanzisha vitalu vya miche ya kahawa na kisha kuigawa bure kwa wakulima, pia Maofiza Kilimo wawaelimishe walkulima wote wenye miti mikongwe waanzisha mashamba mapya.
Kuhusu suala la utafiti wa zao hilo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itumie vyuo vyake vya kilimo ianzishe vituo vyake vya utafiti vitakavyofanya kazi ya utafiti wa zao hilo.

WANANCHI MKOANI MARA WAITIKIA WITO WA MKUU WA MKOA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
 Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.
 Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.
 Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Bukima Ndg. Murungu Murungu akiwasaidia wananchi kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la Usajili likiendelea kwenye ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.
 Afisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Ohana Gerald akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa wakati wa zoezi la usajili  wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara.
 Bw. Shukrani Kwikalya Mgane mkazi wa kata ya Bukima, akikamilisha hatua ya upigaji wa picha wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni afisa Usajili wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Jackson Paulo.
  Bw. Shukrani Kwikalya Mgane mkazi wa kata ya Bukima, akikamilisha hatua ya upigaji wa picha wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni afisa Usajili wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Jackson Paulo.
Baadhi ya Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la kuwasajili wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini wakati wa zoezi la undikishaji Vitambulisho vya Taifa katika kituo cha ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images