Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1484 | 1485 | (Page 1486) | 1487 | 1488 | .... | 1896 | newer

  0 0

   
  Leo January 12, 2018 ni siku ya kuzaliwa kwa Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko. Wote kwa pamoja tunapenda kukutakia heri na fanaka. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

  Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James (Kulia) akieleza umuhimu wa wakazi wa Kata ya Kimandolu kumchagua Ndg Gaudence Limona kuwa diwani wao wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
   Kikao kikiendelea
  Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 

  Na Mathias Canal, Arusha


  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.


  Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.


  Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.


  Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.


  Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.


  Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.


  Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.


  Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.


  “Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.

  JUMUIYA ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjini Kibaha mkoani Pwani imesema Taifa linawategemea vijana katika dhana nzima itakayothibitisha wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yanayolikabili Taifa hili.

  Aidha imekemea tabia ya kujigawa na kuweka makundi baina yao kwani kwa kufanya hivyo ni kudidimiza harakati na juhudi za kuimarisha jumuiya na kupambana kimaendeleo .

  Mwenyekiti wa UVCCM Mji wa Kibaha, Azilongwa Bohari aliyasema hayo, mara baada ya jumuiya hiyo kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi pamoja na kuchangia damu units 22 hospitalini hapo katika kuadhimisha miaka 54 ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Hata hivyo ,alisisitiza umoja na mshikamano kwa kundi la vijana.

  Azilongwa alisema, serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ,zinatakiwa kuona vijana wake wanachemchem ya maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.

  Aliwaasa vijana kwa umoja wao kujishughulisha na kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kujiinua kimaisha .

  "Tukielekea kwenye uchumi wa kati kuna kila sababu ya kupambana na umasikini,tukiwa kama vijana ,tuondokane kuwa matatizo kwenye jamii bali tuwe wapiganaji katika maendeleo na maisha yetu " alisema.

  Pamoja na hayo ,Azilongwa aliwaomba wanachama na viongozi wa jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya chini kushikamana ili kujidhatiti kwa lengo la kujenga ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

  Aliwataka viongozi wa chama na jumuiya kuendelea kuongeza wanachama wapya ambao ndio mtaji kwao na wapiga kura halali kwenye uchaguzi mkuu ujao.

  Azilongwa hakusita kusisitiza vikao vya mara kwa mara na kuwataka viongozi wa UVCCM wilayani hapo kushiriki katika vikao muhimu ili kujadili na kubuni njia mbadala za kuongeza wanachama na kuinua maendeleo ya jumuiya.

  Akielezea zoezi la kuchangia damu, alishukuru wanachama waliojitokeza kuchangia na kuwezesha units 22 ambazo kwa hakika zitasaidia kuongeza mahitaji yanayotakiwa.

  Alisema wamelenga kuchangia damu hospitalini hapo, kutokana na mahitaji makubwa na hospitali hiyo kupokea majeruhi wa ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara kwenye barabara kuu ya Morogoro.
  Nae katibu wa mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini,Method Mselewa,alisema mbali ya hayo wanatembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mkuza na kutoa misaada iliyotokana na ushirikiano wao na hisani kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na mkewe Selina Koka.
  Mselewa alimshukuru mbunge huyo na familia yake kwa ushirikiano wao .
  Baadhi ya viongozi na wanachama wa jumuiya ya vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kibaha Mjini, Pwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya usafi ,na kujitolea kuchangia damu units 22, katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi ikiwa ni sehemu yao ya kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(picha na Mwamvua Mwinyi).

  0 0


  0 0  Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
  Watanzania washauriwa kusajili na kutumia kikoa cha dot tz (.tz) na dot Africa (.africa) katika matumizi ya intanenti kwa ajili ya kutoa utambulisho wa kitaifa, ki-bara na kukuza uchumi wa Taifa na Bara la Afrika.

   Akizungumza leo Mjini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Registry.Afrika Lucky Masilela amesema kuwa vikoa hivyo vinafaida mbalimbali ikiwemo kupunguza gharama za mawasiliano na pia kukuza uchumi wa nchi na bara zima la Afrika kutokana na fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi na bara husika.

  “Nitoe ombi kwa wale wote wanaotumia mtandao watumie mtandao wa dot tz au dot Afrika kwa sababu vikoa vingine haviwezi kusaidia Afrika, kutokana na fedha zinazotumika kusajili vikoa hivyo hubaki katika nchi husika” ameongeza Masilela.

  Aidha, Masilela amefafanua kuwa Umoja wa Afrika (AU) uliridhia maombi ya rajisi ya dot africa kufanya kampeni ya matumizi ya kikoa cha dot Africa, ambapo Rajisi ya dot africa iliainisha maeneo matano (5) ya kufanya kampeni hiyo kwa niaba ya bara lote la Afrika. Maeneo hayo ni Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kaskazini, Afrika ya kati, Afrika Magharibi na Afrika ya kusini.

  “Lengo kuu la kampeni hii ni kuwahamasisha waafrika wote watumie kikoa cha dot africa na pia kujenga hamasa ya waafrika kujivunia uafrika wao na kujenga uchumi unaotegemea rasilimali ya kikoa hiki pekee kinacho watambulisha na kuwaunganisha waafrika wote” ameongeza Masilela.

  Vile vile amesema kuwa kampeni hiyo inaudhihirishia ulimwengu kuwa ucheleweshwaji wa rasilimali pekee ya kuwatambulisha waafrika wote  kwenye mtandao wa Intaneti umefikia hatima yake hivyo Waafrika sasa, kwa kutumia kikoa cha dot africa  wanauwezo wa  kuwasiliana, kutoa huduma, kufanya biashara (taasisi za umma na binafsi) bila bugudha yoyote katika mtandao wa Intaneti.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu Ntahigiye amesema kuwa rajisi ya dot africa (ZACR) ilipewa mamlaka ya kuendesha rajisi ya dot africa mwezi Februari 2017 ikiwa ni baada ya miaka mitano (5) ya juhudi za kutafuta uhalali wa kufanya hivyo.

  “Kufuatia mafanikio hayo, timu ya dot africa ilipewa jukumu na Umoja wa Africa (Africa Union - AU) kuendesha kampeni za kuhamasisha matumizi ya kikoa cha dot africa barani kote kwa kipindi cha miezi sita (6) kuanzia Agosti 2017 mpaka Januari 2018” ameongeza.

  Naye Mwanasheria wa Rajisi ya Tanzania (.tz) Sarah Mhamilawa amesema matumizi ya dot tz ni rahisi na panapotokea tatizo la kiufundi muhusika anapiga simu .tz na tatizo hutatuliwa papohapo tofauti na vikoa vingine ambavyo huhitaji kufuata mlolongo uliowekwa kwa ajili ya utatuzi wa tatizo husika ambao huchukua muda kutatuliwa.

  Kampeni ya matumizi ya  dot africa imeambatana na kuendesha magari (roadshow) wakiwa na Bendera ya  dot africa kutoka Afrika Kusini ambapo safari ilianza Januari 1, 2017 kuelekea Addis ababa, Ethiopia kupitia Botswana, Zimbabwe, Zambia, Tanzania na Kenya.

  Aidha timu hiyo ikiwa Tanzania imeanzia kampeni hiyo Tunduma kupitia Iringa, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro ambapo wakiwa Kilimanjaro watapandisha bendera ya dot Africa na dot tz kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Kulia kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela.
    Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela(wakwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye na mmoja wa wajumbe wa msafara huo Ndg. Ronald Schwaerzler
   Mmoja wa wajumbe wa msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi za mitandao ya intaneti za Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao kwa Afrika Ndg. Ronald Schwaerzler (wapili kulia) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ratiba ya kupanda mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kampeni hiyo leo mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela na wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dododma Ndg. Jabera Matogolo(wakwanza kulia) akielezea namna ambavyo mtandao wa intaneti unavyosaidia kukuza kiswahili wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma.

   ashiriki wa kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma walipokutana na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma.

  0 0

   Wananchi pamoja na wanachama wa CUF wa Kijiji cha Ughandi wakimsubiri kwa hamu Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof.Ibrahimu Lipumba kumsikiliza sera za chama na kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Delphina Mngazija.
  Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof.Ibrahimu Lipumba (wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa wanawake wa chama hicho, Salama Masudi kwenye viwanja vya mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida Vijijini kabla ya kuongea na wananchi hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

  Na,Jumbe Ismailly,  SINGIDA   
    
  MKURUGENZI wa wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Salama Masudi amesema kuwa sera ya viwanda nchini haiwezi kufanikiwa iwapo hatutaendana na mabadiliko makubwa ya soko la wakulima na ikiwezekana katika mpango mzima wa mapinduzi ya kilimo wenye lengo la kuwawezesha wakulima wa chini kuelekea soko kuu la dunia kuweza kuinua kipato kutoka kwa wananchi maskini kabisa.

  Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida Kaskazini uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida vijijini.

  Alifafanua Salama kwamba baada ya wakulima kuwa wamewezeshwa hususani katika maeneo hayo wanayotoka ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo,basi kuwezeshwa kwa viwanda hivyo kunawezekana kabisa kutoka maeneo muhimu kulingana na mazao yanayotokana na uwezeshwaji wa viwanda hivyo.

  Hata hivyo Salama alisisitiza pia kwamba katika miaka yote wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakipelekewa wagombea wanaume ambao wameshindwa kukidhi haja zao kwa kuwa wanaguswa na matatizo yanayowashika wanawake wenyewe,lakini mwaka huu CUF imewaletea mwanamama huyo mahiri na ambaye wanaamini ndiye suluhisho pekee la matatizo ya wananwake.

  “Tunaomba kwa namna ya pekee na utulivu mkubwa tunaomba kura kwa akina mama mtusaidie kuweza kumsaidia mama Delphina Mngazija kwa kuwa ninyi ndio wengi kabisa katika upigaji wa kura na mnatumiwa kuwa chambo cha kuwakandamiza wananchi”alisisitiza Salama.

  “Tumewaletea  mama huyo anaguswa na changamoto zinazotukbili sisi wanawake,wengi wetu hapa tunaumizwa na sera mbovu,tumekuja na kampeni pekee  kupitia mgombea wa chama chetu ‘Mwanamke tua ndoo maana yake akiwa sauti ya Bunge kupitia Singida kaskazini anaweza kuongea na serikali kupitia mifuko ya jimbo ili aweze kuleta visima vitakavyosaidia akina mama  kupunguza adha ya maji katika maeneo mnayoishi”alifafanua

  Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa wanawake Taifa alionyesha pia kukerwa na baadhi ya watu au vyama vinavyosusia chaguzi,na kwamba vitendo vya aina hiyo ni kinyume na demokrasia pamoja na upatikanaji wa maendeleo ya nchi.

  Hivyo Salama alitumia wasaa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wa jimbo la Singida kaskazini kutosusia chaguzi kwani kwa kufanya hivyo wanapoteza haki zao za msingi za kikatiba.

  “Niwaombe wananchi wa kata hii,hususani katika kata hii ya Ughandi hususani wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mtupigie kura chama cha wananchi CUF,siyo dhambi kabisa iwapo wananchi wenyewe kwa mapenzi mliyonayo mmemchagua mtu ambaye ni chaguo lenu na anayewahurumia,lakini badala yake ameletwa mtu kupitia kwenye njia zisizoeleweka”alibainisha Mkurugenzi.

  Hata hivyo mkurugenzi huyo alitumia mkutano huo kuwashawishi wananchi wa kata ya Ughandi kutokichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kile alichokiita ni nyimbo zilizokosa utekelezaji wake.

  Akizungumzia CUF kiongozi huyo wa chama alibainisha kuwa katika kipindi cha takribani miaka ishirini tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikitetea maslahi ya watanzania wote na kutoa mfano kwamba chama hicho kinachoongozwa na Prof.Ibrahimu Lipumba amekuwa akiandaa mijadala mbali mbali iliyochangia kuleta maendeleo.

  Naye mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini kupitia Chama Cha Wananchi  (CUF),Delphine Mngazija akiomba kura kwa wananchi wa Kijiji cha Ughandi aliahidi kwamba endapo watampa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao ataenda Bungeni kutetea akina mama waondokane na adha ya kutembea na mabeseni,ndoo pamoja na mipira ya kujifungulia.

  Alifafanua mgombea huyo kwamba maana mama mjamzito akishakuwa na ujauzito hupatwa na mawazo ya kuondoka kwenda kujifungua kwa kuanza kufikiria ni namna gani atakavyonunua ndoo,beseni na mipira.

  “Ninawaomba ridhaa yenu akina mama mambo ya kwenda hospitali na kwenda kubeba mabeseni niende kuwatetea nipigane na hilo kwa akina mama kwa sababu taasisi ya afya ina mambo mengi kwani mama akijifungulia nyumbani akimchukua mtoto wake kumpeleka hospitali hatapokelewa”alisisitiza mgombea huyo.


  0 0

  Na Tiganya Vincent
  SERIKALI Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja wazazi au walezi ambao hadi kufikia Jumatatu ijayo (15, January 2018) watakuwa wameshindwa kuhakikisha kuwa watoto wao waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka huu watakuwa hajaripoti katika Shule walizopangiwa.

  Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa iliyoakuwa ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado wengi wao hawajaripoti katika Shule walizopangiwa.

  Alisema kuwa kufikia Jumatatu ijayo anataka kupata taarifa na majina ya wanafunzi wote waliochangiwa ambao hawako shuleni ikiwa  na majina ya wazazi wao ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa la kumkoshesha watoto haki ya kupata elimu.

  Mwanri aliongeza kuwa viongozi wa kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na Wilaya ni vema wahakikishe wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao hawako shuleni ili kujua walipo na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana wapo ambao tayari wameshaozeshwa.

  Alisisitiza kuwa wakikuta mtoto yupo nyumbani na mzazi wake hataki kumpeleka Shule wamukamate mzazi wake ili hawawezi kuwajibika kwa uzembe wake.

  “Hapa tutakwenda kwa Sera ya mbanano…kama kiongozi lazima umbane mzazi ambaye hadi hivi sasa hajampeleka mtoto shule wakati wenzake wameshaanza masomo na ikibidi mfikisheni katika vyombo vya Sheria ili ajibu mashitaka yake ya kunyima mtoto haki yake ya elima”alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora

  Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya kukagua zoezi la upandaji miti kwa ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari ,Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) Suzan Nussu alisema kuwa hali ya watoto kuripoti katika Shule za Sekondari kwa wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka huu bado sio nzuri kwa baadhi yao hawajafika shuleni hadi hivi sasa.

  Alisema kuwa katika Shule ya Sekondari ya Ngulu iliyopo Sikonge walichaguliwa watoto 130 lakini hadi hivi sasa wamejiunga 44, Shule ya Sekondari Usisya iliyopo Urambo wamechaguliwa 130 lakini waliripoti ni 54 na Shule ya Sekondari Nanga Sekondari iliyopo Igunga waliochaguliwa ni 160 lakini walioripoti ni 7 hadi kufikia sasa.

  Nussu alisema kuwa kuchelewa kuripoti kwa wanafunzi hao sio tu kunarudisha nyuma maendeleo ya watoto hao kwa sababu ya kuachwa na wenzao bali pia kunasababisha usumbufu kwa walimu kuanza upya kuwafundisha wanafunzi waliochelewa ili waweze kwenda na kasi ya wenzao.

  Alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha ifikapo mapema wiki ijayo watoto wote wawe wamefika Shule kwani tayari Serikali ilishafuta ada na hivyo hakuna kisingizio ambacho kinaweza kumsababisha mtoto kushindwa kuanza masomo yake kwa ajili ya faida yake na Taifa kwa ujumla.

  Nussu alisema kuwa michango mingine inapangwa na wazazi wa watoto wa Shule husika kwa kukubaliana na Kamati za Shule na hivyo hakiwezi kuwa kikwazo kwa watoto kushindwa kuhudhuria masomo yao.

  Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ngulu  Israel Mwambikwa alisema kuwa amekuwa akipata tatizo kutoka kwa baadhi ya wazazi kushindwa kutoa hata michango waliokubaliana katika vikao vyao ya kutoa kilo 10 za mahindi ,kilo mbili za maharage na shilingi 17,000/- ambazo wazazi walikubaliana kama mahitaji ya chakula cha kila mtoto kwa mwezi.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine aliporejea kutoka Zanzibar alikohudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi leo January 12, 2018.Picha na IKULU
   


  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole akizungumza mara bada ya kikao chake na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


   Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji  Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Dk. Assimwe Rwiguza akipigaji chapa ng’ombe katika Kijiji cha Idodoma Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 wa mifugo walioko katika mikoa 26 kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa linalotarajiwa kukamilika January 31 mwaka huu.
   Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi wa mahali sahihi panapotakiwa kupiga chapa kwa ng'ombe kwa wafugaji wa Kijiji cha Idodomya wilayani Shinyanga. kushoto ni Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Dk. Clement Batisiliko
  Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk.  Asimwe  Rwiguza akitoa ufafanuzi kwa wafugaji wa Kijiji cha Idomya umuhimu wa kupiga chapa mifugo yao kabla ya muda wa nyongeza uliowekwa na Serikali kumalizika wa Januari 31 mwaka huu ambapo Dk. Assimwe ni miongoni mwa timu ya wataalamu 15 wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioko kwenye mikoa 26 ya Tanzania bara kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa.

  0 0

  Baadhi ya Watanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mgaza katikati mwenye suti.

  Watanzania wanaoishi Saudi Arabia washerehekea Sikukuu ya Mapinduzi Riyadh Palace Hotel na Balozi Mgaza

  Na mwandishi maalum, Riyadh - Saudi Arabia
  Wanadiaspora na Watanzania waishio Riyadh nchini Saudi Arabia walisherehekea na kuandhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar siku ya ijumaa tarehe 12 Januari, 2018 katika ukumbi wa Riyadh Palace Hotel.

  Sherehe hizo zilindaliwa na jumuiya ya Watanzania 'Tanzania Walfare Society' ambapo waalikwa mbalimbali kutoka miji ya Riyadh, Qasim na maeneo ya karibu walihudhuria. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe.

  Hemedi Mgaza. Miongoni mwa walihudhuria sherehe hizo pia walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi wapya wa kampuni ya ufugaji ng'ombe wa Maziwa ya Al Marai na wengine kutoka kampuni ya ufugaji kuku ya Al Watania. Kwa picha na habari zaidi angalia kupitia you tube 'Prince eddycool'

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Riyadh, Bw. Fuad Mabruk akitoa hotuba mbele ya Watanzania na wanadiaspora wa mji wa Riyadh huku nyuma yake walioketi kwenye meza kuu kuanzia kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya Dkt. Mahmoud Tuli, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Afisa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Saeed Al Jabry na wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Jumuiya Bw. Mohamed Saeed.

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, akizungumza na Watanzania.
  Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na baadaye walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.


  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Januari 12 ya mwaka huu wa 2018 Wazanzibari pamoja na Watanzania kwa ujumla watakuwa wakiadhimisha miaka 54 tangu kutokea kwa mapinduzi Visiwani Zanzibar mnamo Januari 12, 1964. Mapinduzi ambayo yaliyofanywa na wanamapinduzi wa kiafrika na kupelekea kuung’oa utawala wa kisultani na kiarabu visiwani humo na kuwa na utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Pamoja na siku hii kuadhimishwa kila mwaka, bado kuna watu wengi hawafahamu mambo muhimu kuhusu historia ya Zanzibar na yaliyopelekea mpaka mapinduzi kutokea. Kutokana na umuhimu wa siku hii kwa vizazi vilivyopita, vya sasa na vijavyo, Jumia Travel imekukusanyia mambo muhimu ambayo huna budi kuyafahamu.

  Ikiwa na historia ndefu ya utawala wa Kiarabu tangu mwaka 1698, Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya nchi ya ng’ambo ya Oman mpaka ilipojitwalia uhuru wake mnamo mwaka 1858 na kuwa chini ya utawala wake wenyewe wa Kisultani.
  Wakati wa utawala wa Sultani Ali Ibn Said mnamo mwaka 1890, Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza mpaka mwaka 1963 ilipowapatia wanzibar uhuru wao, ingawa haikuwahi kuwa chini ya utawala rasmi wa moja kwa moja wa dola ya Kiingereza.

  Wananchi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa walikuwa ni mchanganyiko kutoka mataifa mbalimbali kama vile Waarabu, Wahindi, Waajemi, Washirazi na Waafrika, ambapo waarabu na wahindi ndio kwa kiasi kikubwa walikuwa wamehodhi ardhi na shughuli kuu na njia za biashara. Kadri muda ulivyozidi kwenda maingiliano baina ya watu wa mataifa hayo yalizidi kuongezeka kitu kilichopelekea utofauti baina yao kuanza kufifia.
  Hata hivyo, walowezi wa Kiarabu kama wamiliki wa sehemu kubwa ya ardhi ya visiwani humo ndio walikuwa ni matajiri kuliko waafrika. Suala hilo pamoja na mambo mengine mengi ni miongoni mwa sababu zilizopelekea waafrika kuona sababu ya kufanya mapinduzi ili kuwa na utawala wa haki na usawa visiwani humo.

  Kwa upande wa kisiasa, vyama vikuu visiwani Zanzibar vilikuwa vikiendeshwa na kuungwa mkono kulingana na utaifa (ukabila), kama vile Waarabu walikuwa wakitawala kwa sehemu kubwa ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) huku Waafrika ilikuwa ni Afro-Shirazi Party (ASP).
  Baada ya Zanzibar kutwaliwa na utawala wa Kisultani wa Oman mnamo mwaka 1698, sehemu ya ardhi yote visiwani humo iligawiwa kwa wanafamilia wa Kifalme wa Oman, ambapo vizazi vyao viliendelea kuimiliki mpaka mwaka 1964.

  Ingawa sio Waarabu wote walikuwa ni matajiri kama familia ambazo zilikuwa zikimiliki mashamba ya karafuu na minazi, hasira ambayo waliyokuwa nayo waafrika ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye mashamba hayo ilipelekea kujisikia hali ya kubaguliwa kwenye ardhi yao wenyewe. Hususani kwa kisiwa kidogo kama cha Zanzibar ambapo ilikuwa ni rahisi kuona pengo na utofauti mkubwa kati ya familia tajiri za kiarabu zilizokuwa zinamiliki ardhi na vijakazi wao masikini wa kiafrika.
  Harakati za kutaka uhuru Visiwani Zanzibar zilianza kutokana na vuguvugu za shughuli za kisiasa ambapo kwa kiasi kikubwa waafrika hawakuwa wanapata uwakilishi sawa na nafasi bungeni. Kuanzia mwaka 1961 na kuendelea kulianza kufanyika kwa chaguzi za kisiasa za kidemokrasia ambapo vyama vikuu vya ASP na ZNP vilikuwa vikichuana vikali.

  Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na waafrika wengi cha ASP kilikuwa kikiendelea kuungwa mkono na kukubalika miongoni mwa waafrika wengi. Katika maeneo mengi kulipokuwa kunafanyika chaguzi kilionekana kuungwa mkono ingawa matokeo ya uchaguzi yalipotoka yalikuwa yanaonyesha kushinda sehemu chache.

  Sababu hiyo ambayo ilikuwa ikijirudia mara kwa mara kwenye kila chaguzi ndiyo iliyopelekea waafrika kuona haja ya kufanya mapinduzi. Mnamo Januari 12, 9164 mapinduzi yalifanyika visiwani Zanzibar na kumfanya kiongozi wa chama cha ASP, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais mpya na kiongozi wa nchi.  Mapinduzi hayo yalipelekea ukomo wa utawala wa kiarabu visiwani Zanzibar wa takribani miaka 200, hivyo kuifanya siku hiyo kusherehekewa kwa maadhimisho maalum na kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa.  

  0 0


   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
    NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.

  Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji  wa mabomba ya kusafirisha maji.

  Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani,  Dar es Salaam, sehemu ya mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016.

  “Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” Alisema

  Hata hivyo Mheshimiwa Hapi amepongeza usimamizi na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na mamlaka husika zinzosim amia mradi huo. “Niwapongeze DAWASA na DAWASCO kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Mhe. Hapi.

  Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huu kuwa ni pamoja na wakazi wa Makongo, Changanyikeni, Salasala, Bunju, Mabwepande na Wazo.

  “Mradi ukikamilika utaondoa kero ya maji katika wilaya yetu  kwa asilimia 95, kwa hivyo, hii nifaraja kubwa kwa wananchi wa Kinondonbi hususan katika maeneo nilkiyoyataja.” Alifafanua.

   Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.

   Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
   Mhe. Hapi na msafara wake wakipanda juu ya tanki linalojengwa.
   Mafundi wakiwa kazini huko Salasala.
   Mhe. Hapi akipokelewa na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. NMelly Msuya, wakati akiwasili huko Makongo Juu, kuanza ziara ya kukagua miradi hiyo.
   Meneja Uhusiano wa Jamii, Bi. Nelly Msuya, (wapilia kushoto) na Afisa Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Mecky Mdakju, wakimsubiri Mkuu wa wilaya Mhe. Hapi, alipozuru eneo la Makongo Juu kukagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
   Mhe. Hapi, (kulia), akifurahia jambo na afisa kutoka DAWASCO, Bi.Judith Singinika(katikati), baada ya kutembelea eneo la ujenzi Bunju.
   Tenki kubwa likifunikwa huko Salasala.
   Mhe. Hapi, (kushoto), akiwa na Bi.Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA, (kulia) na Bi. Nelly Msuya, Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, walipotembelea ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Bunju.
   Mkuu wa wilaya akizungumza na vibarua.

   Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara hiyo, huko Mabwepande.
  Bi.Mecky Mdaku, Afisa Uhusiano wa Jamii, DAWASA, akipanda juu ya tenki la Makongo Juu lililofikia asilimia 80 kukamilika

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo baina ya Coastal Union na Kurugenzi ya Mufundi akifuatilia mchezo huo katikati akiwa na Jezi ya Coastal Union kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Kulia ni Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga(TRFA) Beatrice Mgaya (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
   Sehemu ya mashabiki wa soka mkoa wa Tanga wakiojitokeza kufuatilia mchezo huo
   Wachezaji wa timu ya Coastal Union wakishangilia moja ya bao nne ambazo walifunga wakati wa kipindi cha dakika 45 za kwanza kabla ya kuanza kipindi cha piliambapo Coastal Union ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0
   Mchezaji wa timu ya Coastal Union Raizani Hafidhi kushoto akijaribu kumtoka wa timu ya Kurugenzi FC ya Mufindi Nickraus Mwansumbule wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la kwanza uliochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo mpaka dakika 45 Coastal Union walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta kwa ajili ya ofisi za jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akikabidhi vifaa hivyo kwa Wakuu wa Polisi wa wilaya mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akiumuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipowasili katika uwanja wa mazoezi wa kikosi cha Kutuliza Ghasia kwa ajili ya sughuli ya kukabidhi maada wa vifaa vya mawasiliano ya Kmpyuta kwa jeshi hilo.
  Gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipowasili katika viwanja hivyo kutoa msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaroo,Anna Mghwira akipokea Salamu ya Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Kilimanjaro,Edson Mwalutende kukagua Gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira mara baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi .kulia ni Afisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi daraja la kwanza ,Kamishna Mwandamizi Msaidizi ,Koka Moita.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akisalimiana na Maofisa wa Jeshi la Polisi wa ngazi mbalimbali za vyeo kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
  Afisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi daraja la kwanza ,Kamishna Mwandamizi Msaidizi ,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika uwanja 
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah akitoa neno la shukrani la utangulizi kwa msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta ambazo zitagawiwa katika vituo vya Polisi vya wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Kilimanjaro ikiongozwa na Mwenyekiti IVAN SAMSON MOSHI leo tarehe 12/01/2018 imefanya uhakiki wa mali za UVCCM KILIMANJARO .

  Kamati imebaini mambo mengi ambayo yalitokea kipindi kilichopita na Mwkt ameagiza mikataba yote ipitiwe upya haraka ili kuwezesha UVCCM kunufaika na miradi ya Vijana tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo mambo mengi hayakuwa sawa kwa Vijana! 

  Baada ya uhakiki ambapo kikao kimechukuwa kutwa nzima wapo wapangaji ambao wameonekana kuwa na mapungufu makubwa katika mikataba yao Mwkt ameunda Kamati ya wajumbe wanne ambao wanafuatilia uhalali wa wao kuwa eneo la Vijana bila taarifa rasmi 

  Walioteuliwa katika kamati hiyo ni ABDULRAHIM HAMADI Katibu wa Vijana Mkoa Kilimanjaro, YONA MAKWAIA mjumbe kamati ya utekelezaji Mkoa, NICE MUNICY Mjumbe Baraza Kuu Taifa, DICKSON JONATHAN TARIMO Katibu wa UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA WA 
  KILIMANJARO, Aidha kamati hiyo ndogo imepewa muda wa siku Tatu kumaliza uchunguzi huo na kuleta taarifa mbele ya Kamati Utekelezaji Mkoa!

  IMETOLEWA NA DICKSON TARIMO KATIBU UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA KILIMANJARO

  #KAZIINAENDELEA

  0 0

  Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wananchi hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.  NA WAMJW-DAR ES SALAAM

  ASILIMIA 80 ya wanaohitaji damu nchini ni wanawake kwa sababu mbalimbali ikiwemo uzazi salama wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida na njia ya upasuaji. 

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inafanywa na Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam. 

  “Napenda kusisitiza Damu haiuzwi na kwa mgonjwa yeyote atakayeuziwa damu kwenye kituo chochote cha afya cha Serikali atoe taarifa kwenye idara husika na atachukuliwa hatua” alisisitiza Waziri Ummy Mwalimu. 

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Uongozi wa Hospitali au kituo cha Afya cha Serikali wahakikishe kuwa wanaweka matangazo yanayoelimisha wananchi kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bila ya malipo na matangazo yaelekeze wananchi sehemu ya kutoa malalamiko. 

  Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa wananchi hasa wanaume wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili kuweka akiba ya kutosha katika benki ya damu hatimae kupunguza uhaba wa damu katika benki ya damu na kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini Vanita Omary amesema lengo la kampeni hiyo ni kufikisha chupa 300 za damu katika uzinduzi hyo na tayari washapata chupa 288 mpaka sasa. 

  “Tumeanza kampeni hii tangu jumatatu wiki hii na mpaka kufikia leo siku ya uzinduzi tumefanikiwa kupata chupa 288 tunatumaini tutavuka lengo mpaka mwisho wa kampeni hii, alisema Bi Vanita. 

  Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo na Waziri Ummy imeandaliwa na Chama Cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini kwa kushikiana na Mpango wa damu salama nchini.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama kushoto akimsalimia mwananchi anayepata huduma katika moja ya banda lililokuwa likitoa huduma za afya katika viwanja vya Biafra wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

  Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa kike wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasnia ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wasanii wakiwa wanasubiri huduma ya kuchangia damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chama cha wanawake cha Tasania ya Filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu  akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Sharifu maarufu Casilasi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo kulia ni Mwandishi wa TBC Tanga Bertha Mwambela akishuhudia
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Sharifu maarufu Casilasi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Kurugenzi ya Mufindi uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wawili hao walifanya mazungumzo jijini Dar Es Salaam leo ambapo Bw. Titov aliahidi kuwa Timu yake itaifanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kubaini chanzo cha mauaji na kutoa mapendekezo ya kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayatokei tena katika siku zijazo.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC.

  Mjumbe kutoka Tanzania wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga

  Mjumbe pekee wa kike wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

  Mjumbe mwingine wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

  Mjumbe kutoka Nigeria wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

  Wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakiendelea kusalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRCwakifuatilia mazungumzo.
  Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga.

  Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo.

  Wajumbe wa pande mbili wakiwa katika mazungumzo.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga mstari wa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. WANG Ke kabla ya kwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

  Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. WANG Ke akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga jijini Dar Es Salaam leo.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. WANG Ke mara baada ya zoezi la kwasilisha Nakala za Hati za Utambulishokukamilika.
  Mazungumzo yanaendelea.

older | 1 | .... | 1484 | 1485 | (Page 1486) | 1487 | 1488 | .... | 1896 | newer