Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

Rc wangabo atoa mwezi mmoja kuzuia uvuvi haramu ziwa tanganyika

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kalambo pamoja na kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kukaa pamoja na kuandaa mkakati wa kuzui uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao wa ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao huo.

Amesema kuwa uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao huo unahatarisha maendeleo ya viwanda vya samaki vilivyopo na hatimae kudhoofisha ajira za wananchi waliopo karibu na viwanda hivyo na hatimae kurudisha nyuma juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuibua na kuimarisha viwanda vilivyopo.

“Mwisho wa mwezi huu nataka taarifa ya namna mlivyojipanga kupiga marufuku uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuwakamata wale wanaokaidi na kuendesha uvuvi haramu, uvuvi haramu ukiendelea hiki kiwanda hakitakuwepo, kwasababu ya kuua samaki na watoto wake, achene uvuvi haramu, mnamaliza samaki katika ziwaletu hili,” RC Wangabo Alisisitiza

Ameongeza kuwa samaki ndio rasilimali pekee inayowaajiri pamoja na kuendesha kiwanda na kuwataka wananchi kuungana pamoja kuhakikisha wanatunza rasilimali hiyo, na kupiga marufuku aina zote za uvuvi haramu na kuonya kutosikia kiwanda kimefungwa kutokana na kukosa samaki amabao wamekwisha kwasababu ya uvuvi haramu.

Ameyasema hayo alipotembelea viwanda viwili vya samaki vya Mikebuka Fisheris Tanzania Limited pamoja na Akwa Fisheries Tanzania Limited vilivyopo katika kata ya Kasanga ambapo kiwanda pekee kinachojikongoja ni Mikebuka fisheries huku AkwaFisheries kikiwa kimesimamisha uzalishaji.

Awali alipokuwa akisoma taarifa ya Kiwanda cha Mikebuka Fisheries Tanzania Limited Mtendaji wa Kijiji cha Muzi Gasper Kateka amesema kuwa mbali na ukosefu wa samaki ametaja kuwa changamoto nyingine ni Umeme na barabara jambo linalowafanya kutumia gharama kubwa kendesha kiwanda hicho kwa majenereta na kupakia samaki kwenye boti hadi bandari ya kasanga ili kuweza kuwasafirisha kwenda Sumbawanga kukwepa kipande cha barabara cha Km 1.2 kilichojaa mawe.

“Mikebuka Fisheries in maeneo mawili ya kuchakata samaki ikiwa Sumbawanga yenye uwezo wa kilo 8000 kwa siku na kasanga yenye uwezo wa kilo 15000 kwa siku lakini kutokana na uhaba wa samaki uwezo umeshuka na kuchakata kilo 3000 hadi 4000 kwa siku na kuajiri watu 30 na vibarua 55,” Kateka alieleza.

Kwa upande wake Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Godfrey Makoki alitoa ufafanuzi wa makubaliano ya matumizi ya ziwa Tanganyika yaliyofanya na nchi nne (Zambia, Burundi, Tanzania na DR Congo) katika kikao kilichofanyika 18/10/2012 Mjini Bujumbura katika kanuni ya nne ya makubaliano hayo imekataza uvuvi wa dagaa mchana katika ziwa Tanganyika.

“jambo linalotupa shida ni uvuvi wa kuvua dagaa mchana, kitaalamu dagaa huwa wanakuja kutaga mchana hivyo wanakuwa wakubwa kwasababu wana mayai na usiku huwaoni, sasa huwa tunawaambia kuwa huo ni uvuvi haramu hapo inakuwa ni tatizo,” Makoki Alibainisha.

Katika Kutatua tatizo la Umeme na Barabara Mh. Wangabo amemuagiza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Rukwa kuhakikisha umeme wa REA awamu ya tatu unawafika haraka katika Kijiji hicho kwani kipo kwenye mkakati na kuwaagiza TARURA na TANROAD kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha ndani ya miezi mitatu wanairekebisha barabara ya Km 1.2 ili iweze kupitika.

Mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa Mkoa wa Rukwa una Viwanda Vinne vya Samaki, Viwili vipo Kata ya Kipili, Wilaya ya Nkasi na Viwili vipo Kata ya Kasanga, Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Mikebuka Fisheries Tanzania Ltd Azim Premji (wa pili kutoka kulia) katika kiwanda cha Mikebuka Fesheries Tanzania Ltd.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akipiga marufuku uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao wa Ziwa hilo, (kushoto aliyekaa) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura.  
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (Katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Rukwa Mhandisi, Herini Mhina (Kulia) na (Kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Juleth Binyura. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mhandisi Mshauri, Martin Hossey (wa pili kushoto) kuotoka Kampuni ya Nicholas O'Dwyer inayosimamia ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga yenye urefu wa Km 112 ya thamani ya Bilioni 133 iliyomalizika kwa kiwango cha Km 71.5. 
Mwonekano wa Kiwanda cha Akwa Fisheries Tanzania Ltd kilichosimamisha uzalishaji. 

Jalada kesi ya Malinzi larudi Takukuru.

$
0
0
Jalada la kesi ya  utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake limerudishwa Takukuru  kwa maagizo ya kurekebisha vitu vichache ili kukamilisha iuchunguzi.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga. Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai amedai hayo leo mbele ya Hakimu  Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, pindi shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai alidai jalada la kesi hiyo limesharudishwa Takukuru likitokea kwa mkurugenzi wa mashtaka  DPP na kudai wamepewa maelekezo ya kukamilisha baadhi ya uchunguzi.Hata hivyo, wakili wa Utetezi Nehemia Nkonko aliomba upelelezi dhidi ya kesi hiyo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri amahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, yakiwemo ya kughushi na utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

TAN COMMUNICATION MEDIA WAMLILIA ZUBERI MSABAHA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATANGAZA RASMI VIWANGO VIPYA VYA ADA KWA MAWAKALA WA KUSAFIRISHA WATALII NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto).

Na Hamza Temba-WMU-Dar es Salaam
.......................................................................

Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza rasmi viwango vipya vya malipo ya ada kwa Mawakala wa kusafirisha watalii nchini baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni ya ada na tozo za biashara ya utalii yaliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana, 2017.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, imeeleza kuwa baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ya kanuni, Tangazo la Serikali namba 506 la tarehe 29 Desemba, 2017, limeweka viwango vipya vya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters).

Taarifa hiyo imeeleza viwango hivyo kuwa ni shilingi sawa na dola za Kimarekani 500 kwa kampuni za wazawa zenye umiliki mkubwa wa raia wa Tanzania na zinazomiliki gari 1 hadi 3.

"Shilingi sawa na dola za Kimarekani 2,000 kwa kampuni zenye gari 4 hadi 10, shilingi sawa na dola za Kimarekani 3,000 kwa kampuni zenye gari 11 hadi 50 na shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000 kwa kampuni zenye kumiliki gari 51 na kuendelea", imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa kampuni za kigeni zenye umiliki mkubwa wa raia wa kigeni na zinazomiliki gari 10 hadi 30 zitalipa ada ya shilingi sawa na dola za Kimarekani 5,000, kampuni zenye gari 31 hadi 50 zitalipa shilingi sawa na dola za kimarekani 7,500 na na kampuni zenye gari 51 na kuendelea zitalipa shilingi sawa na dola  za Kimarekani 10,000.

Kufuatia marekebisho hayo, muda wa kutumika kwa leseni za mwaka 2017 za Wakala wa kusafirisha watalii (Tour Operators na Safari Outfitters) umesogezwa mbele hadi tarehe 31 Januari, 2018 ili kuwezesha maandalizi ya kuingia kwenye mabadiliko ya viwango hivyo vipya.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa  maombi ya usajili na leseni za biashara ya utalii na leseni za waongoza watalii kwa mwaka 2018  kwa wafanyabiashara wapya na wanaoendelea na biashara yanaendelea kupokelewa.

Waombaji wote wametakiwa kufuata masharti ya uombaji wa leseni hizo ikiwemo kuwasilisha nakala za hati za usajili wa magari zilizothibitishwa kisheria kwa Wakala wa kusafirisha watalii (wapya na wanaoendelea na biashara) na kivuli cha leseni ya mwaka 2017 kwa wafanyabiasbara wote. 

"Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Desemba 10 na 11 mwaka 2017, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alikutana na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha kwa lengo la kuwashirikisha katika mapendekezo ya viwango vipya vya ada kwa Wakala wa kusafirisha watalii ambavyo vilivyotolewa na Wizara yake.  Mapendekezo ya viwango hivyo yalilenga kuongeza mapato na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wenye gari kuanzia moja kuingia katika biashara hiyo.

RAIS MAGUFULI AMEAMUA KUSAFISHA NYUMBA HAKUNA MENDE ATAKAYEBAKI: KHERI JAMES

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akionyesha fimbo ya kimasai baada ya kupewa cheo cha kiongozi wa kimila Olaigwanani rika ya Korianga akizungumza na wakazi wa akiwa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akisalimiana na wananchi wakati akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akiwasili Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.

Na Mathias Canal, Arusha 


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesifu utendaji wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na uwajibikaji wake katika kuimarisha chama pamoja na serikali kwa maslahi ya watanzania.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mndarara kilichopo Kata ya Ngaranaibor akiwa ziarani Wilayani Longido Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kampeni za Ubunge katika Jimbo la Longido.


Kheri alisema kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameamua kusafisha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania hivyo hakutegemewi mtu yeyote kusalia kama mende wa kumkwamisha katika umaridadi wa usafi huo wa maslahi ya Taifa.


Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CCM Taifa aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 13 Januari 2018 kupiga kura kwa wingi zitakazompa ushindi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa ili kutekeleza ilani ya ushindi wa chama hicho ya Mwaka 2015-2020 ambayo ni mkataba muhimu kati ya wananchi na CCM.


Alisema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua Kali za kisheria dhidi ya yeyote atakayetaka kuvuruga ama kuleta uvunjifu wa amani Siku ya uchaguzi.


"Ndugu zangu wana Mrandarara nataka niwasihi na kuwahakikishia kuwa MTU yeyote atakayeleta masihara na mchezo mchezo Siku ya uchaguzi anapaswa kuchezewa yeye mchezo mpaka ashike adabu" Alikaririwa Kheri


Alisema kuwa Mara baada ya Mbunge kuchaguliwa tu anapaswa kusimamia vyema asilimia 5% za fedha za mfuko wa vijana zinazotolewa na Halmashauri sambamba na asilimia 5% kwa ajili ya wanawake ili kuendeleza chachu na imani ya vijana na wananchi kwa ujumla dhidi ya serikali yao.


Aliongeza kuwa kumchagua mbunge wa CCM itampendeza zaidi Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Magufuli kwani atakuwa amepata msaidizi kwa ngazi ya Jimbo atakayetekeleza vyema ilani ya CCM ambayo imeainisha mambo mengi muhimu na msingi kwa maslahi ya watanzania wote hasa wananchi wa Longido.


Uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Longido na majimbo mengine matatu likiwemo Jimbo la Singida Kaskazini na Songea Mjini utafanyika tarehe 13 Januari 2018.


Wakati huo huo akiwa Kijijini Mairowa Kata ya Ngarenaibor Mwenyekiti Kheri amewataka mawakala wa CCM kote nchini kuwa waaminifu katika kusimamia vyema chaguzi mbalimbali kote nchini kwani wameaminiwa na Chama hivyo kutojihusisha na viashiria vya aina yoyote ya rushwa.


VIONGOZI MBALIMBALI WAWAONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MAMA PERAS NGOMBALE MWIRU, MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR LEO

Uzalendo wa Kweli ni Kupenda vya Kwetu

SHIRIKA LA NDEGE LA (ATCL) LAKABIDHI MSAADA WA VYAKULA KITUO CHA YATIMA MWANDALIWA MBWENI

$
0
0
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa Bi. Halima Ramadhani Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipotembelea na kuwafariji watoto Yatima katika kituo hicho leo, Msaada uliotolewa una thamani ya shilingi milioni tano

Lilian Kingamkono Afisa Masoko ATCL kushoto na Mtendaji wa Masoko Grace Magubo kulia wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Mwandaliwa wakati wafanyakazi hao walipokabidhi misaada katika kituo hicho.



Lilian Kingamkono Afisa Masoko ATCL pamoja na watoto hao wakifurahia jambo



Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akishiriki kuimba wimbo na watoto wa kituo hicho pamoja na wafanyakazi wenzake.



Bi. Halima Ramadhani Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam akiishukuru kampuni ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL mara baada ya kupokea msaada huo.



Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada kwa watoto wa kituo hicho akiwa pamoja na wafanyakazi wenzake.



Wafanyakazi wa ATCL wakipata vinywaji laini pamoja na watoto wa kituo hicho.



Bi Grace Magubo mmoja wa wafanyakazi wa ATCL akibadilishana mawazo na baadhi ya watoto wanafunzi kutoka katika kituo hicho.



Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akiwagawia watoto pipi na biskuti mara baada ya kukabidhi msaada kwa watoto wa kituo hicho



Vyakula mbalimbali vilivyokabidhiwa katika kituo hicho.

…………………………………………………………………..
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limetoa msaada wa vyakula , mafuta , sabuni, nguo,sukari na madaftari kwa Kituo cha Mwandaliwa ambacho kinaelea watoto yatima.

Akizungumza Dar es Salaam leo,Meneja Masoko wa ATCL, Christina Tungaraza amesema thamani ya msaada huo umegharimu sh.milioni tano ikiwa ni kutambua umuhimu wa jamii kusaidia wasiojiweza na hasa watoto yatima.

“Tumeanza mwaka mpya kwa kusaidia watoto walioko kwenye kituo hiki na mbali ya kuleta msaada huu, tunataka kuzungumza na uongozi kuona ni maeneo gani tunaweza kuendelea kusaidia,”amesema Tungaraza.
Amefafanua msaada ambao wameutoa kwa watoto hao ni ule ambao unatumika na kwisha na sasa wanachotaka ni kutoa msaada ambao utadumu zaidi.

Tungaraza amesema shirika lolote la biashara mteja lazima awe namba moja kwao na wanatoa kipaumbele kwa mteja na kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi.

Akiuzungumzia msaada huo Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kituo hicho, Halima Mpeta ametoa shukrani kwa msaada huo wa ATCL na kuiomba jamii kuiga mfano huo kwa kusaidia watoto walioko hapo.Amesema kuna vitu ambavyo si lazima kuvifanya lakini la kusaidia watoto yatima lina umuhimu wake na ndio maana tunaomba wenye uwezo wasaidie.

“Tunawashukuru ATCL kwa msaada wao, tunauthamini sana na tunathamini wafanyakazi wote na walichotoa Mungu atakirejesha na kulifanya shirika hilo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha,”amesema Mpeta.

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MSIBA WA SAID NATEPE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Mama Siti Mwinyi mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili (kushoto) pamoja na Huda Karume mke wa Balozi Ali Karume kwenye msiba wa Bw. Said Abdallah Natepe aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Utawala Bora.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Idd akiwasili Mazizini kuhudhuria msiba wa Said Abdallah Natepe.
  
Mwili wa marehemu Said Natepe ukibebwa tayari kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Mwache

…………………
Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo alijumuika na Viongozi pamoja na wananchi Mazizini kwenye msiba wa Marehemu Said Abdallah Natepe .

KWANDIKWA AWATAKA ‘TAA NA TPDC’ KUHAMISHA BOMBA LA GESI UWANJA WA NDEGE MTWARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ( TAA), mkoa wa Mtwara, wakati alipokuwa akikagua uwanja wa huo. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mkoa wa Mtwara, Daimon Mwakosya, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kuhusu uwanja huo kuvamiwa na wananchi kutokana na kukosa uzio, alipofika uwanjani hapo kujionea maendeleo yake.

Muonekano wa eneo ambapo bomba la gesi limepita ikiwa ni ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

Muonekano wa nyumba 5 kati ya 55 zilizovamia eneo la Uwanja wa Ndege wa Mtwara. Uwanja huo ni moja ya viwanja vya ndege 11 ambavyo Serikali imepanga kuvifanyia maboresho.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoka kukagua kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma kati ya kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara na Namoto, Msumbiji.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akikagua moja ya maboya kwa ajili ya usalama kwa watumiaji wa kivuko cha MV. Kilambo, kinachotoa huduma kati ya kijiji cha Kilambo na Namoto – Msumbiji. wakati alipofanya ziara yake mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akishiriki katika zoezi la uchanganyaji wa zege katika ujenzi wa barabara ya Tangazo-Kilambo yenye urefu wa KM 9.3, Mkoani Mtwara.


…………………


Naibu Waziri wa ujenzi, Elias Kwandikwa, ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kulihamisha bomba la gesi lililopitishwa katika maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla ya bomba hilo halijaleta madhara kwa watumiaji wa Uwanja huo.

Akizungumza mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua uwanja huo, ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa tukio la ajali ya bomba la gesi katika maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani mkoani Dar es salaam na kusababisha madhara kwa wananchi, Naibu Waziri huyo amesema kuwa uwepo wa bomba hilo katika uwanja huo si salama na huenda ikapelekea watoaji huduma za usafiri wa anga kusitisha au kutokuleta kabisa huduma zao kutokana na hofu, hali itakayopelekea Serikali kukosa mapato.

“TAA, TPDC na wataalam wa Wizara hakikisheni mnafanya kikao kuona namna ya kulihamisha bomba hili kwani jambo hili si salama na pia baadhi ya mashirika ya ndege ya kimataifa yakibaini kama kuna uwepo wa bomba la gesi katika uwanja huu wanaweza kusitisha huduma zao”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Ametoa rai kwa watendaji wa Taasisi mbalimbali za Serikali kutochukua maamuzi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kabla ya kushirikisha uongozi wa wilaya au mkoa kwa pamoja ili kupata ushauri wa maeneo ambayo yanafaa kwa ujenzi wa miundombinu hiyo.

Aidha, Naibu Waziri huyo amewaagiza wamiliki wa nyumba takriban 60 waliojenga katika eneo la uwanja huo kuondoka mara moja kabla Serikali haijawachukulia sheria kwa kosa la kuvamia uwanja huo.

Amewaonya wataalam waliopo kwenye Halmashauri hapa nchini upande wa ardhi kutokugawa viwanja kwa wananchi hususan katika maeneo ambayo si sahihi kama vile ya uwanja wa ndege kwani hali hii hupelekea ucheleweshaji wa maendeleo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kivuko cha MV Kilambo kinachotoa huduma zake katika mto Ruvuma kati ya Tanzania na Msumbiji pamoja na kivuko cha MV Mafanikio kinachotoa huduma zake kati ya Msemo na Msanga Mkuu na kuwataka wasimamizi wa vivuko hivyo kuhakikisha wanaboresha huduma pamoja na usalama wa vivuko hivyo kwa kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya kutosha vya uokoaji.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Uwanja huo, Bw. Daimon Mwakosya, ametaja changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya uwanja wa ndege na kijiji jirani cha Mangamba na uwanja kukosa uzio wa usalama.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw. Evod Mmanda, ameipongeza Serikali kwa kuchukua jitihada za dhati kwa kutatua kero mbalimbali za wananchi na hivyo kumuomba Naibu Waziri huyo kuliangalia suala la upitishwaji wa bomba la gesi katika uwanja huo kwa jicho la pekee.

Naibu Waziri Kwandikwa ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na wizara yake kujionea maendeleo yake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

DKT. NDUGULILE AING’ARISHA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI KATAVI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia moja ya bidhaa ya mvinyo inayotengenezwa na Kikundi cha Wanawake wajasiriamali cha Humbaji kilichopo katika Manispaa ya Mpanda alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsaha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo ili kuchangia azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akishona sweta kwa kutumia mashine maalum wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kuanzisha shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia sweta lililotengenezwa na moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika ziara yake ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na vikundi vya wanawake wajasilimali wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akiwahamasisha wanawake wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kuunganisha nguvu ya kufanya biashara zao wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb.) ya kuamsaha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.

Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga akielezea umuhimu wa Maafisa maendeleo ya Jamii katika kuwakusanya na kuwaunganisha wananwake katika vikundi vya wajasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb.) akitoa motisha kwa mwakilishi wa kikundi kitakaocholelewa na Kikundi kingine ikiwa ni utekelezaji wa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali kuwezeshana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya kibiashara.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali kilichopo katika Manispaa ya Mpanda mara baada ya kuhitimisha ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW




Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) ameing’arisha programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara zao.

Dkt. Ndugulile ameitambulisha programu hiyo wakati alipofanya ziara ya siku mbili katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kuibua miradi na kuanzisha shughiuli za uzalishaji kawa kuzingatia fursa, mazingira na soko.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasirimali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia uelewa wa soko, mbinu za biashara, upatikanaji wa mikopo na mahitaji ya kiufundi.

“Niseme programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amesema kuwa program ya ‘Kikundi Mlezi’ itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Wilayani Mpanda Bi.Nuru Saimon ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kusaidiana katika kuanzisha na kuinuka katika biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara ya siku mbili mkoani Katavi na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kufikia lengo la kuwa na Tanzania ya Viwanda. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda bidhaa zetu kwa kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI APOKEA KWA NIABA YA RAIS KANUNI ZA SHERIA YA MADINI NAMBA 7 YA MWAKA 2017

$
0
0
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimpa muhtasari Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kabla ya kumkabidhi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi baada ya ya kumkabidhi vitabu vya  Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018

Kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017


Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 ambaye anapokea kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyeagiza kuandaliwa kwa kanuni hizo ndani haraka ili sheria iweze kufanya kazi. Hafla hiyo ndogo, iliyohudhuriwa pia na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, wakiwa na vitabu vya Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kitabu cha Kanuni za sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 baada ya Balozi Kijazi kuvipokea kwa niaba ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 11, 2018. Wengine ni Manaibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo na Mhe. Doto Biteko, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila.

PICHA NA IKULU

HALMASHAURI YA MJI WA BABATI YAJIZATITI KUKAMILISHA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Wananchi wa Kata ya Babati mkoani Manyara wakiwa wamepanga foleni ya kuingia katika chumba cha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akielezea umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa kwa wananchi ikiwa ni kutambulika na kupata huduma za kijamii kirahisi pamoja na kuwezesha Halmashauri yake kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kupanga maendeleo kwa wanannchi wao kwa urahisi alipohojiwa na waandishi wa Radio Manyara. 
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akifanya mazungumzo juu ya maendeleo ya zoezi wakati Afisa Msajili Mkoa wa Manyara kutoka NIDA alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo hayo.

………………..

Halmashauri ya Mji wa Babati inaendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea; ambapo wananchi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kusajiliwa.

Akizungumzia zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Ndg. Fortunatus Fwema amesema kiujumla zoezi la Usajili katika Halmashauri yake linaendelea vema isipokuwa changamoto za hapa na pale.

Amezitaja baadhi ya changamoto ni ushiriki hafifu wa wananchi kutokana na msimu wa kilimo asilimia kubwa ya wananchi kuwepo mashambani, mvua na uelewa mdogo wa wananchi katika masuala yanayohusu umuhimu wa Vitambulisho.

Amewataka Wananchi kugawa muda wa kilimo na wa kujiandikisha ili waweze kutumia fursa hii kujisajili na kuagiza watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili.

Article 4

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA MAFURIKO CHEMBA DODOMA

$
0
0

Askari wa zimamoto wakiendelea na zoezi la kuokoa watu waliozingirwa na maji.

Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza na maafisa wa jeshi la zimamoto katika zoezi la kuhamisha wananchi waliozingirwa na maji.

Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.

Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.



Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.

Athari za mvua hizo zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti Abdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960

Amiry Issa ni Mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka wananchi kutosogelea maeneo hatarishi

Akizungumzia hilo,Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.

WAZIRI KIGWANGALLA ASISITIZA UZALENDO KAMATI YA UTAMBULISHO WA UTALII TANZANIA

MWENYEKITI WA CUF TAIFA PROF.LIPUMBA AHIMIZA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU

$
0
0
Mwenyekitti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Delphina Mngazija kwenye mkutano wa kampeni uliofanyia katika Kijiji cha Ughandi,Singida vijijini.
Mgombea ubunge wa CUF,Delphina Mngazija alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla na kuwaahidi kwamba endapo wataampaa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao atakwenda kupigania hadi kuondoa kero zinazowakabili wanawake wajawazito za kununua beseni,ndoo na mipira ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma vuilivyopo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ughandi wakimsikiliza mwenyekiti wa taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba alipokuwa nakiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ughandi kumuombea kura mgombea wa ubunge wa chama hicho ili aweze kuchagulia ifikapo jan,13,2018.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
 
Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasilimia wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini alikwenda kumnadi mgombea ubunge wa chama hicha,Delphine Mngazija.
Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasisitiza wananchi wa vyama vyote vya siasa kumpigia kura mgombea wa chama hicho,Delphina Mngazija kwa kuwaonyesha mfano wa karatasi la kupigia kura
 
Na Jumbe Ismailly SINGIDA Jan,11,2018 Kuwekeza 


CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufuta ada katika shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini sekta ya elimu bado haijawekeza ipasavyo kwenye sekta hiyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kuikabili sekta hiyo mpaka sasa.

Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,Delphina Mngazija uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini.

Alifafanua kiongozi huyo wa kitaifa kwamba serikali inapowekeza kwenye sekta ya elimu kwa sasa ni lazima pia iwekeze kwenye matumizi ya kompyuta kwenye shule zilizopo na kuongeza kuwa elimu ya siku hizi inakwenda sambamba na mitandao ya kompyuta.

Kwa mujibu wa Prof.Lipumba nchi nyingi pamoja na nchi maskini zimewekeza mara tu watoto wanapoanza hujifunza pia kutumia kompyuta na kwamba matumizi ya kompyuta ni sawa kama vile kujifunza lugha.
“Mtoto mdogo ni mwepesi kujifunza lugha kuliko mtu mzima,hata mtu mzima ukiwa na simu mwanao anaweza kujua kuitumia ile simu kuliko wewe mtu mzima.

Na kuongeza pia kuwa wataalamu wa mambo ya watoto wanasema kuwa mtoto anapokuwa ndani ya tumbo la mama yake na kwa miaka miwili ya kwanza ndizo zinazompa mtoto fursa ya kujenga maungo yake,ya kujenga ubongo wake,ya kujenga kinga ya mwili.”alisisitiza Prof.Lipumba.
Prof.Lipumba hata hivyo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa vituo vya afya vilivyopo kuwa na virutubisho muhimu na kwamba kutokana na taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha.

“Kwa mujibu wa taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha,hawana madini ya chuma ndani ya damu yao hii inasababisha watoto wasipate lishe bora na watoto wa Tanzania wamedumaa.”alibainisha Mwenyekiti huyo.

Naye Katibu wa CUF Mkoa wa Singida,Selemani Ntandu aliwatahadharisha wanachama wa CUF pamoja na wale wa CCM waishio katika Kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla kwamba endapo watamchagua mgombea wa CCM,Justine Monko wakae wakijua kwamba makao makuu ya wilaya hiyo yatahamishwa kwenda Kijiji cha Sagarumba badala ya Ilongero.

Aidha katibu huyo alisisitiza kwamba wananchi wa jimbo la Singida kaskazini wanahitaji huduma bora za kijamii zinaboreshwa na kuonyesha masikitiko yake kwamba hivi sasa miundombinu ya barabara kwenye maeneo mengi hairidhishi kabisa jambo ambalo halishughulikiwi na watu waliokabidhiwa dhamana ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
 

WAZIRI JAFO-WATAALAMU WA MAJI ZAIDI YA ELFU NNE WANAHITAJIKA TAMISEMI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati) akiwasili kwenye Chuo cha Maji tayari kwa kutunuku Shahada na Stashahada katika mahafali ya Tisa ya Chuo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati) akishiriki kwenye maandamano ya Kitaaluma kuelekea uwanja wa Sherehe Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Maji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Maji, Wakufunzi na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akitoa Cheti kwa mwanafunzi wa kike aliyefanya vizuri Kitaaluma katika ngazi ya Astashahada.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati) katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Chuo cha maji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo(Katikati aliyekaa) katika Picha ya Pamoja na wanafunzi waliohitimu Shaada ya Uhandisi na Rasilimali za Maji na Umwagiliaji katika Chuo cha Maji.



Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema mahitaji ya wataalam wa Maji kwa sasa katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini ni kati ya elf nne – hadi elfu saba.

Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Mji yaliyofanyika Tar 11/01/2018 katika chuo hicho kilichopo Jijini Dar es salaam.

“Taalum hii ni muhimu sana katika ustawi na Afya ya wananchi wetu kote Nchini, uhakika wa kupata maji salama bado ni changamoto kubwa kutokana kutokuwa na miundombinu ya Uhakika na zaidi ni wataalamu wachache waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa Nipongeze chuo hiki cha maji kwa kutoa Shahada kwa mara ya kwanza katika Historia ya Chuo hiki, hapo awali hapakuwa na Ngazi ya Shahada hivyo wataalamu wengi waliishia ngazi ya Stashahada ambapo mara nyingine ilihitajika Utaalamu zaidi kutokana na changamoto za kiutendaji katika maeneo mbali.

“Kwa sasa mmejibu changamoto hii katika Sekta ya Maji kwa kufanikisha kutoa wahitimu wa Ngazi ya Shahada haya ni mafanikio kwa Chuo, kwa Wahitimu na Taifa kwa Ujumla nawapongeza sana na nawakaribishe katika Kulitumikia Taifa hili kwa sababu ujuzi mlioupata unahitajika sana” Alisema Jafo.

Akizungumza na Wahitimu, Wakufunzi na wageni waalikwa Waziri Jafo alisema Kuhitimu ni jambo moja lakini jinsi gani mnaenda kutumia Taaluma yenu ni jambo lingine, mnatakiwa mkafanye kazi kwa weledi wa hali ya Juu huku, muwe waadilifu na mtumie vuzuri rasmilimali za Umma.

“Nyie sasa mtakwenda kuwa wajumbe kwenda bodi za Zabuni katika maeneo mtakayofanyia kazi mkapambane na rushwa katika miradi ya maji, ili miradi iweze kutekelezwa kwa kiwango na thamani ya Fedha ikaonekane misende kuwa sehemu ya ubadhirifu wa mali za Umma, Rushwa hupofusha maji na huondoa weledi wako mkajihadhari sana na Rushwa alimalizia Waziri Jafo.

Akizungumza katika Mahafali hayo Mkuu wa Chuo cha Maji Shija Kazumba alisema jumla ya wanafunzi 248 wamefuzu Stashahada-Uhandisi wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira wakati wahitimu 127 wamehitimu hyrolojia na Uchimbaji wa visima, wahitimu 23 wamehitimu haidrolojia na Mateorolojia, wahitimu 12 wamehitimu Stashahda ya Teknolijia ya Maabara na ubora wa maji na wahitumu 50 ni wa Stashahada, Uhandisi Umwagiliaji

Katika Ngazi ya Shahada waliofuzu na kustahili kupata shahada ya Uhandishi WA Rasilimali maji na Umwagiliaji ya Chuo cha Maji kwa mara ya kwanza ni wanafunzi 54.

KAMPUNI YA PREMIUM AGRO CHEM LTD YASAMBAZA MBOLEA MASAA 24 KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

$
0
0
 Meneja Biashara na Masoko wa  Kampuni ya Premium Agro Chem Ltd, Brijesh Barot (kulia), akiangalia upakiaji mbolea uliofanyika katika maghala ya kampuni hiyo, Vingunguti jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mbolea ikipakiwa katika malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Premium Agro Chem Ltd imeendelea kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli kwa kusambaza mbolea kwenda mikoani kwa masaa yote bila ya kujali mapumziko ya Sikukuu ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar inayofanyika leo nchini kote.

Akizungumza na waandishiwa habari wakati akisimamia upakiaji wa mbolea hiyo kwenye maghala ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo, Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Brijesh Barot, alisema kwamba kwa jana wamesambaza mifuko 20,563,000 sawa na tani 1,028 na kuwa mbolea hiyo inasambazwa   kupitia kwa mawakala wao.

"Tunaendelea kusambaza mbolea kwa mikoa yote, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe na Katavi, kupitia kwa mawakala pamoja na kuwatumia maafisa wetu walio katika vituo vya matawi yetu huko kwa ajili ya kuharakisha upatikanaji wa mbolea kwa wakulima vijijini," alisema Barot.

Barot alisema kuwa kwa leo watasambaza mifuko 1,200 sawa na tani 600 na hiyo ni kwa mbolea aina ya Urea ambapo alisema usambazaji unaendelea vizuri.

Alisema kampuni yao inafanyakazi kazi hizo kizalendo ndiyo maana wamekubali kuuza kwa bei elekezi mbolea ambayo wao walikuwa wameinunua muda mrefu kabla ya kutolewa kwa maagizo ya kununua kwa mfumo maalum wa serikali, na hili linafanywa kwa kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama  wakati gwaride la heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
 Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.
  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA wakipita mbele ya jukwaa kuu katika maandamano ya sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika  sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa Amani mara baada ya kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wanachi mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
PICHA NA IKULU
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images