Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

PIGO KUBWA CHADEMA IRINGA MJINI WAANZA MADIWANI WAKE WAWILI KATA YA KWAKILOSA NA RUAHA WAJIUZULU

0
0

Aliyekuwa  diwani  wa  kata ya  Kwakilosa  kupitia  Chadema Joseph Lyata akionyesha  barua  ya  kujiuzulu nafasi ya  udiwani  leo mbele ya  wanahabari  mjini  Iringa
Lyata  akionyesha  barua  ya  kujiuzulu kwake  Udiwani
Aliyekuwa   diwani wa kata ya  Kwakilosa  mjini  Iringa Joseph Lyata  akieleza  sababu za  kujiuzulu  kwake udiwani  leo  kulia  ni aliyekuwa  diwani wa Kihesa  Edga  Mgimwa aliyejiuzulu mwaka jana na  kushoto kada wa Chadema  Bw  Kimata  ambae  pia  alijiuzulu
Na MatukiodaimaBlog

KASI  ya  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia na  maendeleo  (chadema)  jimbo la  Iringa  mjini  kujiuzulu  imezidi  kuongezeka   na  kufikia madiwani sita   sasa  baada ya  aliyekuwa  diwani wa Kwakilosa  Joseph Lyata  na  aliyekuwa  diwani wa kata ya  Ruaha Tandesy Sanga kutangaza  kujiuzulu  nafasi hiyo  leo .

Wakati  Lyata  akizungumza na  wanahabari  mkoa  wa Iringa  kujiuzulu kwake Tandesy Sanga  amezungumza  na  wanahabari  mkoani  Dar es Salaam  juu ya  kujiuzulu  kwake leo .

Akitangaza  azma  ya  kujiuzulu kwake  nafasi hiyo   mbele ya waandishi  wa  habari Lyata  amesema  kuwa  kujiuzulu  kwake  kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.

Lyata  alisema  kuwa  mara kwa mara  amekuwa  akiandika  barua  kwa  uongozi wa  juu wa Chadema  Taifa   kuelezea  malalamiko yake ya  mahusiano mabaya kati yake na  mbunge wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Msigwa  ila wamekuwa  wakipuuza na  kuwa hajaona  sababu ya  kuendelea  kubaki ndani ya  chama  hicho  japo  safari yake ya  siasa  itaendelea  kupitia  chama  chochote ikiwezekana  hata  CCM .

"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "

Alisema  kuwa figisu  figisu kati  yake  na  mbunge  Mchungaji Msigwa  zilianza toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

"  Mbunge alikwenda katika  chombo kimoja wapo  cha  utangazaji mjini  Iringa (Radio jina limehifadhiwa ) na  kutangaza  kuwa Lyata  anautafuta  ubunge kwa  nguvu na hata  wezi  ila  niwa  wazi  sioni  kosa la  kuzuiwa  kugombea  ubunge  nikitaka na muda  ukifika  nitagombea   ila  namhakikishia  kuwa sijaondoka  katika  Chadema kutokana na kununuliwa nimeondoka  kutokana na mahusiano mabaya  kati yangu na mbunge Mchungaji Msigwa na  wapo  wengi  wanataraji  kuondoka na kujiuzulu nafasi zao  za  udiwani " alisema  Lyata

Kuwa  mchakato  wa  kumpata  naibu  meya  Manispaa ya  Iringa nafasi  ambayo  alikuwa  akiwania  mbunge aliweza  kuingilia mchakato   huo  na  kupanga  mtu  ambae  alimtaka  na  malalamiko  yake  alifikisha  ngazi  za  juu  ila  walikaa  kimya  huku  uongozi wa kanda  kuptia  katibu   wake ulimpuuza kabisa na  kuishia  kusema kuwa ni msaliti .

" Uchaguzi   mdogo wa udiwani Kimala Kilolo na  Kitwiru  mimi na Frank  Nyalusi  hatukupangwa  kushiriki kampeni Kitwiru  kwa  hofu ya  kutujenga  kisiasa  katika mbio za ubunge  tulipangwa Kilolo ila  kata  yangu  imepata maafa  ya nyumba  kuezuliwa  mbunge  hadi  sasa pamoja na kuwa na taarifa  hakuweza  kufika  aliyefika ni mkuu wa mkoa na mkuu wa  wilaya  ambao  waliweza  kunisaidia hadi  kuezeka nyumba   za  wananchi wangu ila mbunge badala ya  kushukuru  ameishia  kunilaumu  kuwa  kwanini nimeezeka nyumba na pesa nimepata wapi "

Hata   hivyo  Lyata  alisema  kwa  ajili ya kuonyesha ana  nguvu ya  kisiasa  kuliko  mbunge Mchungaji Msigwa ataendelea kufanya  siasa  na  kuwa suala la ubunge 2020 asubiri  muda  ufike  ila nyuma  yake  kuna  kundi  kubwa ya madiwani  na  viongozi wa chadema  watakaomfuata bila  kutaja majina  na  idadi yao  alisema  anaungwa mkono  na  madiwani  hao kwa uamuzi  wake .

Kuhusu  tuhuma  za  kununuliwa na  CCM kwa  zaidi ya  milioni 200 Lyata  alisema hajanunuliwa na kama amenunuliwa basi ni  mmoja  mwa  viongozi  wenye  sifa  kuzidi  ya  hao  wanaoeneza uvumi huu maana anayenunuliwa ni  yule anayekubalika na  aliyejiweka  jikoni kama  mmoja kati ya madiwani wa Chadema  ambae amekuwa  akieneza  uvumi ila huku  akitafuta  kununuliwa na  wana CCM

Kwa  upande  wake  Edga  Mgimwa  aliyekuwa  diwani wa  Kihesa  alisema  kuwa amevutiwa na kujiuzulu kwa Lyata  na  kuwa katika mkakati  wake  wa   kufanya kazi kama  kada wa CCM  jimbo la  Iringa ni madiwani  wengi  watajiuzulu .

Mbali ya Lyata na  Mgimwa  madiwani  wengine  waliojiuzulu kwa mwaka  jana na  sasa ni aliyekuwa diwani wa kata ya  Kitwiru  kupitia  Chadema  Baraka  Kimata  ambae  ni diwani  tena wa kata  hiyo  kupitia  CCM , pia  wapo madiwani  wa  viti maalum  wawili Husuna  Ngasi na Leah  Mleleu .

Mapema  mwaka jana akizungumza na  wanahabari mjini hapa  juu ya kujiuzulu kwa madiwani  wanne mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji Msigwa  ambae ni  mbunge  wa  jimbo  hilo  alisema  kuwa kuna  mkakati wa CCM kuendelea  kununua madiwani na  kukanusha malalamiko ya madiwani hao  kuwa yeye  ni  chanzo cha  wao kujiuzulu kwao .

Huku naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Dady  Igogo  alisema  kuwa chama  kimewanunulia  vifaa maalum   kwa  ajili ya madiwani wa Chadema wanaonunuliwa  kurekodi mazungumzo  ya  kununuliwa  kwao .




IGP SIRRO AFANYA ZIARA BANDARI YA DAR ES SALAAM

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akiwa ameongozana na baadhi ya maofisa wa Jeshi hilo alipofanya ziara katika bandari ya Dar es salaam, leo kwa lengo la kukagua magari 119 ya Jeshi hilo ambayo yameshawasili bandarini hapo, magari hayo ni miongoni mwa magari 777 yaliyoagizwa na Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua baadhi ya magari 119 ya Jeshi hilo ambayo yameshawasili bandari ya Dar es salaam, yakiwa ni miongoni mwa magari 777 yaliyoagizwa na Jeshi hilo kwa ajili ya shughuli mbalimbali. 
Picha na Jeshi la Polisi.

WANANCHI WAFURIKA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOANI RUVUMA

0
0
Wananchi wakazi wa Kata ya Ndilima Mtaa wa Makambi Ndilima Wilaya ya Songea, wakikagua fomu zao kabla ya kwenda kwenye maalumu cha uchukuaji taarifa kwa maana ya kupigwa picha, uchuaji alama za kibaiolojia na saini ya Kielekrtoniki. Waliopo pichani ni Bi. Hadija Yahaya (mwenye gauni la Pinki kushoto) na Bwana Hussein Nyoni (Mwenye kofia kichwani) wote wakazi wa Mtaa wa Makambi Songea.
Hawa ni baadhi tu ya wakazi wa Kata ya Ndilima Wilaya ya Songea wakisubiri huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye shule ya msingi ya Matogo na kuhusisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Kwa Wilaya ya Songea Kata zilizoanza zoezi ni Kata ya Ndilima na Seed-farm zoezi ambalo litafanyika wa siku saba tu kabla ya kuhamia Kata zingine za Wilaya hiyio.

Akionekana mwenye furaha ni Bi Haruna Thabiti Majwila wa Mtaa wa Makambi Ndilima mara baada ya kukamilisha hatua za usajili kwa maana kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia. Na hapa ya akiangalia muonekano wa Kitambulisho chake utakavyokua na kukagua picha yake kujiridhisha endapo picha yake imetoka vizuri. Kulia ni Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bwana Agaton Magnus Komba.
Pichani ni Bwana Hausi Rashid Mamba akiweka saini yake ya Kielektroniki kwenye mashine maalumu ya uchukuaji alama za kibaiolojia( alama za vidole), picha na saini ya kielektroniki wakati wa zoezi la Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Kata ya Ndilima wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Bwana Michael Komba akikagua kwa makini (aliyevaa jezi) akikagua kwa makini taarifa zake zilizojazwa kwenye fomu ya maombi ya usajili kabda la kuingia kwenye chumba cha Usajili Vitambulisho vya Taifa. Zoezi la Usajili Mkoa wa Ruvuma limeanza rasmi tangu tarehe 02/02/2018 na linahusisha wananchi wote wa mkoa huo wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.


Mamia ya Wananchi wa Wilaya za mkoa wa Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya Usajili zoezi la Vitambulisho vya Taifa huku baadhi wakiwataka viongozi kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la usajili Vitambulisho vya Taifa kuwa ni bure.

Wito huo umetolewa na wananchi wa Wilaya ya Songea wakidai kutozwa kiasi cha shs.2000/ za picha za kubandika kwenye kwenye fomu za utambulisho za Serikali za Mitaa wanakoishi na kudai gharama hizo ni kubwa kulinganisha na hali halisi ya maisha.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Makambi Bwana Anuari Methodi Nyoni ametolea ufafanuzi suala hilo na kueleza wananchi wanaoagizwa kuleta picha picha ndogo za passport size ni wale ambao wamekosa viambatisho muhimu vya kuwatambulisha na hivyo ili kujiridhisha kuwa mwananchi wanayemthibitisha kuwa ni mkazi wa eneo lao basi ni vema kuwa na picha yenye taswira yake ili kuepuka matumizi mabaya ya fomu za kuwatambulisha zinazotolewa na Serikali ya Mtaa.

Aidha amesisitiza Serikali yake ya Mtaa kusimamia na kutekeleza agizo la Serikali la kwamba zoezi la Vitambulisho vya Taifa ni bure na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuelewa Serikali inaposema zoezi ni bure haina maana kwamba Serikali itafanya kila kitu; ikutolee copy viambatisho vyako au kukulipia gharama za picha hilo haliwezekani. Amesema wao kama wasimamizi wa zoezi hilo wanasisitiza mwananchi kufika kwenye kituo na picha yake au nakala ya viambatisho vyake na huduma nyingine zote mwananchi atazifuata mtaani zinazkotolewa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph amesema Mamlaka ina mashine zake za kuwapiga picha wananchi na kwamba mwananchi anayefika kusajiliwa hapaswi kuja na picha ya passport size kama inavyoelezwa; ila changamoto kubwa ni kwa wale wananchi ambao hawana viambatisho vyovyote vya kuwatambulisha na wanahitaji kupata barua ya utambulisho wa Serikali za Mitaa wanakoishi. Hawa sasa kwa utaratibu waliojiwekea wenyewe barua za utambulisho zinazotoka kwenye Serikali za Mitaa na kugongwa muhuri wa Mtendaji au Mwenyekiti wa Mtaa wamekuwa na utaratibu wa kuweka picha ya mwananchi ili kujiridhisha na yule wanayemtambulisha kwetu.

Bi Rose amewasisitiza wananchi kujitahidi kuwa na viambatisho muhimu vinavyowatambulisha kuepukana na gharama zizisokuwa za lazima kwani mwananchi anayekuja kusajiliwa akiwa na cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule, Kadi ya kupigia kura, TIN namba, Leseni ya Udereva, Pasi ya kusafiria(Passport), Kadi ya Bima ya AFYA, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii au Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi; vichache kati ya hivyo huyu mtu hahitaji barua ya utambulisho ya Serikali ya Mtaa kwani viambatisho vyake vinatosha kumtambulisha” alisisitiza

Amesema ni vema wafanyabiashara kutotumia Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kama sehemu ya kujinufaisha na badala yake kutambua si wananchi wote wenye uwezo wa kulipa gharama za huduma wanazotoa na kuomba Mamlaka mbalimbali za Serikali kuangalia namna zinavyoweza kudhibiti changamoto hiyo ili wananchi wengi wajitokeze kwenye zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwani zoezi hilo ni bure nala muhimu kwa kila mwananchi kushiriki.

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeanza mkoani Ruvuma kwa Wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru na linatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu.

KIPINDI MAALUM.MHE.RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA MAGAVANA WA BOT IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 3,2018.

0
0

JAFO AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA TWANGOMA

0
0

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na mmoja wa mafundi kwenye ukikagua wa ujenzi wa daraja la Twangoma
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na msimamizi wa ujenzi wa daraja la Twangoma

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Twangoma
Eneo la ujenzi wa daraja ukiendelea

     .........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe.  Selemani Jafo, leo amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika daraja la Twangoma ili kujionea uhalisia wa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa Mbagala na maeneo ya Twangoma jijini Dar as salaam.

Waziri Jafo amefanya ziara hiyo kwa lengo la kupata ukweli wa utendaji kazi katika ujenzi wa daraja hilo ambao unafanywa  chini ya Ofisi yake ya TAMISEMI kupitia mradi wa DMDP.

Katika ziara yake, Jafo amefika  eneo la mradi asubuhi na mapema na kuwakuta Vijana wakiwa kazini huku ujenzi huo ukienda kwa kasi kubwa.

Waziri Jafo amewataka wakandarasi wengine kuiga mfano huo wa uchapaji kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

WAZIRI MWIJAGE: NJIA NZURI YA KUFIKIA UCHUMI WA KATI NI UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe..Charles Mwijage akizungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Ziara yake Mkoani humo .
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage(kulia) akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kufika hapo wakati wa ziara yake Mkoani humo (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akizungumza na wadau mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa Ofisi Mpya ya SIDO Isanga Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akifungua Ofisi ya Muda ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) iliyoko Mtaa wa Malambo mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage (wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa viwanda Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo.




Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema njia nzuri ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 ni kupitia Uchumi wa Viwanda jumuishi.

Waziri Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani humo, ambapo alisisitiza juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ulio imara, shindani na endelevu, utakayozingatia mambo muhimu matatu ambayo ni soko, malighafi na teknolojia.

Amesema lengo la Serikali ni kuhamasisha ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia viwanda vidogo na vya kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo mkoa wa Simiyu ambao umeonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.

“Safari ya Simiyu imeanza vizuri na lengo la safari ni kuhamasisha Watanzania kujenga uchumi wa viwanda jumuishi, viwanda ambayo malighafi yake inazalishwa na wananchi wenyewe, vitatoa ajira kwa wananchi walio wengi, vitatumia malighafi asilia na kutoa mazao yenye matumizi makubwa” alisema Mwijage.

Waziri Mwijage amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” ambapo sasa umejipanga kuelekea kwenye “Kijiji Kimoja Bidhaa Moja”.

Ameongeza kuwa mwaka 2018/2019 Serikali kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) litawasaidia wananchi kupata mafunzo ya ujasiriamali, uzalishaji na uchakataji, ambapo ameuhakikishia Viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa Ujenzi wa Ofisi ya SIDO ya Mkoa huo eneo la Isanga Mjini Bariadi utakamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti mwaka 2018, kwa kuwa fedha za ujenzi zipo.

Sanjali na hilo Waziri Mwijage amewataka Maafisa Ushirika kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshwa mitaji ya kuanzisha viwanda vidogo na Serikali pamoja na Taasisi nyingine za Kifedha kwa kuwa ni rahisi zaidi vikudi kufikiwa kuliko mtu mmoja mmoja.

Wakati huo huo Mwijage amewataka watendaji wote wa Serikali kuondoa vikwazo na kuacha urasimu unaoweza kuwakwamisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuweza kuufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Akiwasilisha tarifa ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema ili kuandaa mazingira mazuri yatakayowawezesha wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza mkoani humo, wametenga maeneo ya uwekezaji na madawati ya uwekezaji kwa kila Halmashauri na timu mahsusi ya Mkoa ya kuanzisha na kuendeleza dhana ya Simiyu ya Viwanda inayoongozwa na Katibu Tawala Mkoa.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga amesema wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo katika Ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati na akaomba Meneja wa SIDO Mkoa atembelee viwanda vilivyopo ili aweze kutoa ushauri juu kuboresha uendeshaji wa viwanda hivyo katika tija.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kupitia SIDO mkoa huo unaweza kufikia Uchumi wa Kati. “Tungehitaji kuwa ni Mkoa ambao value addition(kuongeza thamani) itafanyika kupitia SIDO, mahali ambapo mtu mwenye milioni tatu wakiungana kikundi cha walima alizeti wanaprocess(wanachaka) wenyewe mafuta” alisema Mtaka.

Pamoja na kuzungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu, Waziri Mwijage alifungua Jengo la muda la Ofisi ya SIDO Mkoa wa Simiyu lililopo Mtaa wa Malambo Mjini Bariadi na kukagua eneo la ujenzi wa Ofisi mpya ya SIDO itakayojengwa na SUMA JKT, ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti mwaka 2018.

DKT. MWAKYEMBE AUNDA KAMATI YA NGUMI

0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) leo tarehe 3 Januari, 2018 amekutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Mhe. Waziri na Wadau hao ili kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo huo wa masumbwi ya kulipwa, vikao hivyo vilianza mwishoni mwa mwaka 2017. 

Katika kikao kilichofanyika leo, Mhe. Waziri aliwaagiza wadau hao kufanya kazi kwa pamoja katika kuunda mfumo mpya utakaolinda maslahi ya mabondia na wahusika wengine wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kuliletea Taifa letu heshima kwa kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Ili kupiga hatua, Waziri Mwakyembe ameunda kamati ya watu kumi na moja (11) itakayokusanya maoni ya wadau na kupitia upya katiba ya kuunda Chombo kitakachosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini. Kamati hiyo imeanza kufanya kazi leo  tarehe  03 Januari, 2018 na itakamilisha kazi yake tarehe 31 Januari, 2018. Kamati itasimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na itakuwa na wajumbe wafuatao:-:
  1. Ndg. Emmanueli Salehe         –     Mwenyekiti
  2. Ndg. Joe Enea                      –     Makamu Mwenyekiti
  3. Ndg. Yahya Pori                    –     Katibu
  4. Ndg. Habibu A. Nyogoli         –     Mjumbe
  5. Ndg. Shomari Kimbau           –     Mjumbe
  6. Ndg. Fike Wilson                  –     Mjumbe
  7. Ndg. Anthony Ruta               –     Mjumbe
  8. Dkt. Killaga M.Killaga           –     Mjumbe
  9. Ndg. Ally B. Champion         –     Mjumbe
  10. Ndg. Rashidi Matumla          –     Mjumbe
  11. Ndg. Karama Nyilawila         –    Mjumbe
Aidha, Waziri Mwakyembe ameeleza kwamba katika kipindi cha mpito shughuli za kutoa vibali kwa mapambano ya ndani na kwa mabondia wanaosafiri nje ya nchi zitaendelea kutekelezwa na BMT. “BMT endeleeni kusimamia vibali vya mapambano ya ndani na vibali vya safari za nje ya nchi za mabondia kwa kuzingatia uzalendo, weledi, kanuni na sheria za nchi bila kumwangalia mtu usoni wala kumuonea aya”, amesisitiza Waziri Mwakyembe.

Imetolewa na
Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
03/01/2018

Kampeni ya Uzalendo yapata Mapokeo Chanya

0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza wajumbe wa kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kwa ubunifu waliyofanya katika siku ya uzinduzi uliyofanywa hivi karibuni na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, katika Kikao cha Tathimini  ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo  kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sanaa kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.Shani Kitogo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Leah Kihimbi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Sanaa  kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akieleza mafanikio ya uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) ikiwemo kupokea maombi kutoka taasisi mbalimbali kuomba wanakamati kwenda kutoa mafunzo kuhusu suala la uzalendo kwa watumishi wa ofisi zao,katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Joyce Fissoo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini akitoa mapendekezo katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu Makala ya viongozi na wadau waliyozungumzia suala la uzalendo kwa taifa itakapo kamilika iweze kusambazwa nchini nzima katika Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kuwapa fursa watoto hao kujifunza kuhusu uzalendo.
Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bw.Mrisho Mpoto akitoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoweza kufanikisha kampeni hiyo kuwa endelevu ikiwemo wajumbe kufanya tafiti kwa nchi zenye uzalendo kama China kwa lengo la kuhakikisha taifa linaelewa umuhimu wa uzalendo na manufaa yake katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

TANZIA

0
0

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI, WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA SAM KUTESA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ujumbe Maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiufungua na kuusoma Ujumbe huo maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje kwa upande wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MATUKIO MAKUBWA NA MADOGO YA JINAI KATIKA MKOA WA MBEYA

0
0


 Ifuatayo ni taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2017. Taarifa hii inaonesha matukio makubwa na madogo ya uhalifu, matukio ya usalama barabarani, matukio yaliyovuta hisia kwa jamii,  hali ya ulinzi na usalama kipindi cha sikukuu ya Kristmasi na mwaka mpya 2018, mpango mkakati wa Jeshi la Polisi Mbeya na mafanikio yaliyopatikana kutokana na operesheni, misako na doria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu kwa mwaka huu 2017.
  1. MATUKIO MAKUBWA NA MADOGO YA JINAI.
Jumla ya makosa ya jinai 26,009 yaliripotiwa kutokea mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka 2017 ikilinganishwa na matukio 32,943 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho  Mwaka 2016. [-21].
Makosa makubwa yaliyoripotiwa mwaka 2017 yalikuwa ni 2,234 ikilinganishwa na matukio 2,071  yaliyoripotiwa mwaka 2016. [+8] Makosa madogo 23,775 yaliripotiwa  mwaka 2017,  ikilinganishwa na makosa 30,872 yaliyoripotiwa mwaka 2016. [-23].
Aidha jumla ya makosa 734 yaliripotiwa mwaka 2017 kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kupitia misako, doria na operesheni mbalimbali ikilinganishwa na matukio 565 yaliyoripotiwa mwaka 2016. [+30].
  1. MATUKIO YA USALAMA BARABARANI.
Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa yote ya ajali pamoja na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani kwa kipindi cha mwaka 2017 yalikuwa 82,211   wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 yalikuwa 66,172. [+24]
Matukio ya ajali kwa mwaka 2017 yalikuwa 244 ikilinganishwa na matukio 393 yaliyoripotiwa mwaka 2016.[-38].  Ajali zilizosababisha vifo mwaka 2017 zilikuwa 141, wakati  mwaka  2016 zilikuwa 182.[-22.5]. Watu waliokufa mwaka 2017 walikuwa 170, wakati mwaka 2016 walikuwa 286. [- 40.5].
Ajali za majeruhi mwaka 2017 zilikuwa 103 wakati mwaka 2016 zilikuwa 211.[-51]  Watu waliojeruhiwa mwaka 2017 walikuwa 268  wakati mwaka 2016 walikuwa 482. [-44]
Pesa zilizokusanywa kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani [notification] mwaka 2017 zilikuwa Tshs 2,380,050,000/=,  wakati kipindi cha mwaka 2016 zilikusanywa  Tshs 1,920,900,000/= [+24]
Aidha baadhi ya sababu za kutokea kwa matukio ya ajali ni kuongezeka kwa vyombo vya usafiri mkoani Mbeya hasa magari na pikipiki, baadhi ya madereva kutozingatia sheria za usalama ikiwa ni pamoja na mwendo kasi hasa usiku na ulevi licha ya jitihada za Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na baadhi ya wadau kutoa elimu hiyo mara kwa mara. Hali ya hewa hususani ukungu na utelezi katika baadhi ya maeneo ya barabara ya Mbeya / Rungwe / Kyela.
  1. MATUKIO YALIYOVUTA HISIA KWA JAMII.
Jumla ya matukio matatu makubwa yaliyovuta hisia kwa kamii yaliripotiwa kama ifuatavyo : –
  1. JALADA LA UCHUNGUZI:
Tarehe 16.01.2017 saa 12:30hrs mtaa wa Igoma [A] kata Isanga, tarafa Sisimba jiji na mkoa wa Mbeya kulitokea tukio la waombolezaji kuzika jeneza tupu na mwili wa marehemu mtoto  HARUN JAILO KYANDO [9] Mkazi wa mtaa wa Igoma [A] kusahaulika nyumbani. Hata hivyo mwili huo baadae ulizikwa upya kwa kufuata taratibu.
  1. JALADA LA UCHUNGUZI:
Tarehe 15.02.2017 BARAKA S/O MWAFUNGO, miaka 22, msafwa, mkulima, mkazi wa Pipeline alifariki dunia kwa maradhi ya kisukari. Tarehe 18.02.2017 RUTH SEGETI [57] Mkazi wa Pipeline mama mzazi wa marehemu  akiwa na vijana wawili walifukua kaburi la mtoto wake na kutoa mwili huo kisha kuupeleka nyumbani kwake na kuuhifadhi kwa  imani kuwa atafufuka.  Hata hivyo mwili wa marehemu baadae ulizikwa upya tarehe 20.02.2017 kwa usimamizi wa Halmashauri ya wilaya Mbeya Vijijini.
  1. AJALI YA MOTO KUSABABISHA UHARIBIFU.
Tarehe 15.08.2017 saa 21:30hrs eneo la SIDO Mwanjelwa katika soko la Sido, lililopo Sido, kata ya Iyela, tarafa Iyunga jiji na mkoa wa Mbeya kulitokea ajali ya moto ambapo baadhi ya maduka / vibanda  vya soko hilo liliteketea kwa moto. Hakuna madhara kwa binadamu.  Thamani ya mali iliyoteketea inakadiliwa ni zaidi ya Tshs 500,000, 000/=.
  
  1. HALI YA ULINZI NA USALAMA KIPINDI CHA SIKUKUU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA – 2018.
Katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya 2018 kwa ujumla hali ilikuwa ni shwari, ulinzi uliimarishwa maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za ibada, kumbi za starehe, barabara kuu na maeneo yenye mikusanyiko ya watu.
Hata hivyo kuna matukio kadhaa ya uvunjifu wa amani yaliripotiwa kutokea kama kawaida kama ifuatavyo:-
  • Mauaji   – 1
  • Kujeruhi – 1
  • Ajali ya kifo – 1
Upande wa misako ni kama ifuatavyo:-
  • Bhangi gram 35
  • Pombe haramu ya moshi [gongo] lita 124
  • Silaha 3 aina tofauti Riffle 1, Shortgun 1 na Gobole 1 pamoja na risasi 8 za Shortgun na 2 za Riffle.
  • Wahamiaji haramu 17 wote raia wa Ethiopia
  • Risasi 81 za aina ya Riffle / Marv IV ziliokotwa na Polisi
  • Gari 2 aina ya Fuso zenye namba T. 394 BCL na T. 399 DCC na watuhumiwa 5 wakisafirisha milipuko  bila kibali aina ya Magzan – Kubella tani 20 kutoka [W] Chunya kuelekea mkoa wa Geita.
  • Upande wa Usalama barabarani tozo Tshs 47,160,000/= zilipatikana.
  1. MKAKATI  NA  MPANGO KAZI WA KUZUIA UHALIFU
Miongoni mwa mikakati/mpango kazi wa kuzuia uhalifu Mkoani Mbeya ni pamoja na :-
  • Kufanya tathmini ili kuyatambua matishio   katika maeneo yetu na mikakati ya kupunguza uhalifu ulioongezeka zaidi mwaka 2017.  
  • Kubaini muelekeo wa uhalifu na maeneo tete uhalifu ili kuelekeza nguvu za ziada katika  maeneo hayo [Crime threat analysis].
  • Kuchukua hatua za haraka pale tukio linapotokea na kulitolea taarifa.
  • Kuendelea na jitihada za kushawishi Halmashauri za Jiji/Miji/Wilaya katika kupambana na uhalifu. Hata hivyo changamoto iliyopo ni kwa Halmashauri hizo kutotambua kuwa jukumu la kuihakikishia jamii usalama wa maisha, mali, amani na  utulivu ni moja ya majukumu yake ya msingi kwa mujibu wa sheria namba 7 ya  mwaka 1982 ya sheria za Serikali za Mitaa [Serikali za Wilaya] pamoja na sheria namba 8 ya mwaka 1982 , sheria ya Serikali za Mitaa [Mamlaka za  Miji].
  • Kuongeza jitihada kwenye doria na misako yenye tija na ufanisi
  • Kuongeza kasi ya kueneza falsafa ya ulinzi shirikishi
  • Kuendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na taasisi za Serikali na vyombo vya udhibiti kama vile JWTZ, JKT,Magereza, Uhamiaji,Usalama wa Taifa,  Zima Moto na Uokoaji Takukuru, Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, TRA, TFDA n.k.
  • Kudumisha ushirikiano na vyombo vya habari vilivyopo Mkoa wa Mbeya.
  • Ushirikiano na Mikoa jirani [INTER-REGION CO-OPERATION] katika kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu.
  • Ushirikiano na madhehebu ya dini, wazee wa mila, viongozi wa Serikali za Mitaa, Kata, Tarafa na viongozi wa Vyama vya Siasa katika kupambana na uhalifu na wahalifu.
  • Kuimarisha utendaji wa weledi
  • Kujenga na kuimarisha uaminifu na uadilifu wa askari wetu.
  • Kuimarisha utoaji huduma bora kwa wananchi [Customer Care].
  1. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KUTOKANA NA MISAKO, DORIA NA OPERESHENI.
Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine ni :-
  • Bhangi uzito wa kilo 403 na gram 394 ilikamatwa ikiwa ni pamoja na mashamba makubwa 6  tofauti yenye ukubwa wa ekari 13 ½   ilivunwa na kuharibiwa kwa kuchomwa moto.
  • Mirungi kilo 4 pamoja na shamba moja lenye ukubwa wa nusu ekari ilivunwa na kuharibiwa kwa kuchomwa moto.
  • Dawa za kulevya aina ya heroine gram 196 ilikamatwa
  • Dawa ya kulevya aina ya amphetermine gram 20 ilikamatwa.
  •    Bidhaa za magendo zenye thamani ya Tshs 81,930,000/= ikiwemo bidhaa za magendo vipodozi vya aina mbalimbali vilivyopigwa marufuku na serikali vyenye viambata vya sumu, pombe kali na mahindi tani 60 na magunia 223 yaliyokuwa yakiingizwa nchini kutoka malawi yalikamatwa.
  • Nyara za Serikali zenye thamani Tshs 379,604,000/= na USD 300 zilikamatwa.
  • Wahamiaji haramu 344 walikamatwa wakiwemo Ethiopia 240, Malawi 48, Somalia 37, Burundi 17, Botswana 1 na Zambia 1.   Pia magari 3 yalikamatwa yakisafirisha wahamiaji haramu hao ambayo ni T. 347 DAJ toyota haice, T. 917 AWM aina ya fuso na T.155 AZU aina ya isuzu canter pamoja na wasafirishaji 7 watanzania wamefikishwa mahakamani pamoja na magari hayo
  • Pombe haramu ya moshi gongo ujazo wa lita 3,719 pamoja na mitambo 33 ilikamatwa.
  • Jumla ya silaha 28 zilikamatwa ikiwemo shortgun 17, risasi 202, Riffle 2 na risasi 47, gobole 8 na bastola 1.  
  • Sare za JWTZ “kombati” suruali 2, mashati 2, kofia 2 na viatu / mabuti jozi mbili zilikamatwa.
  • Pombe kali zilizopigwa marufuku na serikali zenye vifungashio vya plastiki  zenye thamani ya zaidi ya Tshs 1,023,508, 750/= zilikamatwa maeneo mbalimbali mkoani Mbeya na kuzuiliwa kusubiri maelekezo toka serikalini.
  • Noti bandia Tshs 1,245,000/= na USD 1,199 zilikamatwa.
  • Tozo [Notification] Tshs 2,380,050,000/=   zilipatikana.
WITO WA KAMANDA:
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa pongezi kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano wao wa dhati kwa Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na Polisi jamii katika kipindi chote cha Januari  hadi Desemba – 2017,  aidha anatoa rai kwa jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kipindi chote ili kuhakikisha mkoa wetu wa Mbeya unakuwa salama.
Pia natoa shukrani zangu za dhati kwa waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari kwa ushirikiano wetu kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kipindi cha mwaka 2017, kwa nafasi hii ninaomba ushirikiano huu uendelee katika kipindi cha mwaka 2018.
Aidha anatoa wito kwa wazazi/walezi kuzingatia utoaji wa malezi bora kwa watoto/vijana ili wakue katika misingi mizuri ya maadili mema katika jamii na kujiepusha na matukio ya kihalifu na kukataa uhalifu wangali wadogo ikiwa ni pamoja na kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya, kucheza kamari na ulevi uliopitiliza.
Kwa kutambua kuwa suala la ulinzi na usalama unaanzia ngazi ya familia, mtaa, kitongoji,  kijiji, kata, tarafa, wilaya hadi ngazi ya mkoa, ni vema kila mmoja wetu kutambua na kuamini usalama wa mali na maisha yetu unaanzia na mimi, wewe na sisi sote. Kwa kuimarisha ulinzi na usalama wetu na mali zetu inatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza katika mkoa wetu, wananchi kujiajiri na kuajiriwa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii bila kuathiri amani na utulivu.
Aidha Kamanda MPINGA anatoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi  vilivyopo katika maeneo yao.  Pia kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuheshimu sheria na alama za usalama barabarani, watembea kwa miguu kuzingatia alama za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
                 Imesainiwa na:
    [MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TAARIFA RASMI YA MAZISHI YA MPIGANAJI MWENZETU ATHUMANI HAMISI

0
0
TAARIFA RASMI
 
Mwili wa Mpendwa wetu Athumani Hamisi Msengi unataraji kuzikwa hapo kesho Januari 5, 2018 baada ya Swala ya Ijumaa na Maziko yatafanyika katika Makaburi ya KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM.

Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Sinza Madukani  Mtaa wa Weruweru (Njia ya Namnani Hotel Nyumba na 26). 

Marehemu Athumani Hamisi amefariki asubuhi ya leo Januari 4,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake. 

TUNATOA POLE KWA WOTE MLIOFIKWA NA MSIBA HUU.


TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI

0
0
Na: Veronica Kazimoto, 04 Januari, 2018,
Dar es Salaam.

Mwaka huu wa fedha wa 2017/18, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imedhamiria kuongeza idadi ya walipakodi kwa ajili ya kuisaidia nchi yetu kupunguza kutegemea misaada kutoka kwa wahisani.

Lengo kuu la kuongeza walipakodi ni kupanua wigo na kuongeza makusanyo ambayo hutumika katika kuleta maendeleo na kujenga uchumi wa nchi.

TRA ina mikakati mbalimbali ambayo imechukuliwa na inaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa, walipakodi wanaongezeka na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali.

Mikakati hiyo ni pamoja na kusajili walipakodi ambapo Mamlaka imezindua kampeni ya usajili wa walipakodi nchi nzima ili kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara anasajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa urahisi na haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania alisema, usajili wa walipakodi ni chanzo cha kuongeza idadi ya walipakodi na mapato kwa ujumla.

"Moja ya majukumu ya msingi ya TRA ni Usajili wa Walipakodi ambao huongeza idadi ya walipakodi, wigo wa ulipaji kodi, makusanyo pamoja na kutoa taarifa sahihi za walipakodi wanaostahili kukadiriwa na kutozwa kodi ili kuchangia Pato la Taifa", Alisema Mwandumbya.

Mwandumbya alisisitiza kuwa, walipakodi wadogo wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani ya siku tisini (90) kuanzia waliposajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo kwa kulipa kodi hiyo hata kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika.

"Wananchi wanaostahili kusajiliwa kama walipakodi ni watu wote wanaotarajia kuanzisha biashara, kumiliki vyombo vya usafiri kama vile gari na pikipiki, wanaostahili kulipa kodi ya majengo, wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na wanaotarajia kupata leseni za udereva", alifafanua Mwandumbya.

Aidha, Mwandumbya aliyataja mahitaji ya usajili kuwa ni Mkataba wa pango au uthibitisho wa umiliki wa mahali pa biashara, barua ya mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ikiwa na muhuri na namba ya simu ya mwenyekiti wa mtaa husika, kitambulisho cha mhusika kama vile hati ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha uraia au cha mpiga kura na mhusika ni lazima aende mwenyewe kwenye ofisi za TRA kwa ajili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole.

Kamishna Mwandumbya, amewatahadharisha wananchi kuwa makini na vishoka kwa kuwa usajili huo hufanyika bila malipo na hufanyika katika ofisi za TRA na katika vituo maalum ambapo wananchi watatangaziwa kupitia vyombo vya habari na kwenye maeneo husika.

"Napenda kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi wote wanaostahili kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi kuwa makini na vishoka wanaoweza kutumia mwanya huo na kuharibu nia njema ya kampeni hii kwasababu hakuna wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili au hata kutoa fomu ya usajili", ametahadharisha Mwandumbya.

Elijah Mwandumbya amesema endapo mtu atapata changamoto yoyote katika kusajili na kupata namba ya mlipakodi anashauriwa kuwasiliana na Ofisi ya TRA iliyopo karibu au kupiga simu bure katika Kituo cha Huduma kwa namba 0800 750075 au 0800 780078 au kutuma barua pepe huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz.

Hatua nyingine ni uwepo wa mifumo mbalimbali ya kielektroniki ya kusajili walipakodi ambayo imerahisisha ulipaji kodi na hivyo kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.

Mifumo hii imepunguza muda wa usajili ambapo kabla ya kutumia mifumo hii ya kielektroniki kazi ya kusajili walipakodi mpaka kukamilika ilikuwa inachukua takribani siku 7 lakini baada ya kuanza kutumia mifumo hii, usajili hufanyika ndani ya dakika 30 tu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Richard Kayombo akizungumza ofisini kwake alisema TRA imejiwekea lengo la kusajili walipakodi wakubwa, wa kati na wadogo wapatao milioni moja (1,000,000) kwa mwaka huu wa fedha 2017/18. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya walipakodi na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali.

Kayombo alisema kuwa, mamlaka ina mpango wa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanakuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na kuongeza ufanisi wa zoezi la usajili kwa kutumia Mfumo wa Vitalu - Block Management System ambao utawezesha kutambua walipakodi wanaostahili kusajiliwa na kulipa kodi.

Aidha, ameongeza kwamba, mamlaka ina mkakati wa kuongeza idadi ya walipakodi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Halmashauri au Manispaa mbalimbali ili kuhakikisha kila mfanyabiashara katika maeneo hayo anakuwa na namba ya TIN. Namba hii husaidia kumtambua kila mfanyabiashara mahali anapofanyia biashara yake na kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa.

"Kama mamlaka, tuna mpango wa kuwarahisishia wafanyabiashara muda wa kufanya usajili kwa kupeleka vifaa vya usajili karibu na mahali wanapofanyia biashara kwa ajili ya kuokoa muda wanaoutumia kwenda kwenye ofisi zetu kufanya usajili", amesema Kayombo.

Kupitia mkakati huu, Mamlaka ya Mapato ya Tanzania itaweza kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kwa kuwapatia Kadi ya Utambulisho. Wafanyabiashara hao ni kama vile wenye maduka ya reja reja hasa wenye ma fremu, wamachinga, washereheshaji, wachimbaji wadogo wa madini n.k.

Uwepo wa idara cha Huduma na Elimu kwa Walipakodi kilichopo ndani ya Mamlaka, ni hatua nyingine ya kuongeza idadi ya walipakodi ambapo idara hi inajishughulisha na kutoa elimu kwa Umma juu ya umuhimu wa kulipa kodi, kujibu hoja mbalimbali pamoja na kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati muafaka kupitia ujumbe mfupi wa maneno.

Mikakati na hatua zote zilizobainishwa hapo juu zitaongeza idadi ya walipakodi, uhiari wa kulipa kodi na mapato ya Serikali kwa ujumla.

WAZIRI JAFO AKWAZWA NA UBOVU WA BARABARA YA MNYAMANI -BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua barabara na Mnyamani-Vingunguti wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Ilala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Manispaa ya Ilala wakati wa ukaguzi wa barabara ya Mnyamani-Vingunguti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mbunge wa Segerea Mhe.Bonna Kaluwa wakati wa ukaguzi wa barabara ya Mnyamani-Kaluwa.

…………………

Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo amekerwa na ubovu wa miundombinu ya barabara ya Mnyamani-buguruni inayosababisha adha kwa wananchi wa maeneo hayo na kukwamisha shughuli zao za maendeleo za wananchi hao.

Waziri Jafo ameonyesha hali hiyo wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kukagua barabara ya Mnyamani na Kituo cha Afya Buguruni kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi wa maeneo hayo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

“Haiwezekani barabaraba hii iharibike kwa kiasi hiki lakini Viongozi wa Manispaa hii mpo na mnaendelea na kazi Ofisini, wananchi wanateseka, magari yao yanaharibika, vyombo vingine haviwezi kupita katika barabara kutokana na ubovu wa barabara hii ila nyie hamuoni matatizo haya ya wananchi, mmekaa tu Ofisini wala hamtafuti suluhisho la haraka la kutatua Changamoto hii” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa ninatoa wiki moja kwa Uongozi wa Manispaa ya Ilala, Tatura Wilaya na Mkoa pamoja na Shirika la Maji linalotoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam(Dawasco) kukutana na kukubaliana kwa haraka Suluhisho la kudumu na kuanza kuitekeleza na ili kumaliza changamoto hii kwa wananchi wa Buguruni.

“Kwa ubovu ninaoushuhudia katika barabara hii sitapenda muanze kujivuta sijui vikao visivyoisha, majadiliano ya muda mrefu mimi ninatoa Wiki moja tu kazi iwe imeanza na Tar 12/01/2017 nitakuja tena kukagua na kuona maendeleo ya ukarabati wa barabara hii na endapo kazi itakua haijaanza ntashughulika na Viongozi wa Ilala” Alimalizia Waziri Jafo.

Akiwasilisha kero za wananchi wake mbele ya Waziri Jafo Mbunge wa Segerea Mhe.Bonna Kaluwa amesema Maeneo ya Mnyamani na Vingunguti yana wakazi wengi sana ambao wengi wao hujishughulisha na biashara katika maeneo hayo.

Mhe.Bona aliongeza kuwa ubovu wa barabara ya kwa Mnyamani imesabisha wananchi wa maeneo hayo kufunga biashara zao kwa sababu wakati wa mvua hakuna mteja anayeweza kufika kwenye biashara, wengine wamehama makazi yao kwa sababu ya maji yaliyojaa kwenye mashimo makubwa yaliyopo kwenye barabara hiyo hii ni adha kubwa kwetu tunaomba Serikali itusaide.

Akitoa maelezo ya ubovu wa barabara hiyo Meneja wa Tarura Wilaya ya Ilala amesema ubovu wa barabara hiyo unachangiwa na ubovu wa miundombinu ya Maji iliyoko chini ya Dawasco ambayo kila mara bomba linalopita katika eneo hilo hupasuka na kumwaga maji mengi yanayopelekea kubomoka kwa Lami iliyowekwa na kwa sababu barabara hiyo inatumiwa na magari mengi hupelekea kuwa na mashimo makubwa kama haya yanayoonekana hivi sasa.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI RUVUMA KWA ZIARA.

0
0
Waziri mkuu Kassim Kajaliwa amewasili mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku sita ambapo katika ziara hii waziri mkuu atatembelea halimashauri ya MBINGA,na NYASA na kuhitimisha katika Manispaa ya SONGEA ,nakuzungumza na wananchi katika uwanja wa majimaji,huku miradi mbalimbali anatarajia kutembelea ikiwemo kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la TANESCO.

WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO

0
0
Na Shani Amanzi, 

Wananchi wa Wilaya ya Chemba wamehamasishwa kutumia fursa ya mifugo waliyonayo katika kuwapatia kipato na siyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wingi wa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo. 

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi aliyazungumza hayo mapema leo 04/1/2018 alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kueleza changamoto waliyokuwa nayo ni upungufu wa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k ) 

Bw. Simon alisema “kumekuwepo na mwitikio mdogo wa Wafugaji katika uchanjaji wa Mifugo yao hasa Mbwa (kichaa cha Mbwa) na Kuku dhidi ya Kideri ,Ukosefu wa Malisho na Maji katika maeneo mbalimbali”. 

“Lakini katika maboresho ya mikakati endelevu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa Wananchi tumepiga hatua kwa kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Kichaa cha Mbwa (Rabies) na Kideri kwa Kuku (Newscastle desease) kwa kuwachanja ili kupunguza vifo toka 20% mpaka 10% , kutibu Mifugo na kutoa tiba kwa Mifugo dhidi ya Magonjwa mbalimbali kama FMD, Minyoo na Magonjwa ya Ngozi”. 

Kumekuwepo na migogoro baina ya Wakulima na Wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi hasa maeneo ya malisho na kilimo. Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Mifugo,Viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wananchi, imekuwa katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kutenga maeneo ya malisho ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji. 

Wito kwa wafugaji wa Wilaya ya Chemba ni kuhakikisha wanajitokeza kupiga chapa kwa maendeleo ya sekta na pia wanafuga mifugo michache yenye tija na inayoendana na rasilimali zilizopo. 

Zoezi la Upigaji Chapa ni endelevu na tayari kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumefanya zoezi kwa zaidi ya 103% ya lengo, kuelimisha wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Mondo ,Hamai na Songolo ili kuongeza kipato chao na kuboresha lishe zao huku mbinu shirikishi (PPP) ikitumika kati ya Halmashauri na Kanisa la KKKT- Arusha kwenye mradi wa Mbuzi wa Maziwa. 

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi akizungumza mapema leo Ofisi kwake,kwa lengo la kuwahamasisha Wananchi wa Wilaya ya Chemba kutumia fursa ya kujipatia kipato kwa kutumia mifugo waliyonayo,mbali ya fursa zilizopo kwa Wananchi hao pia alibanisha baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya Idara yake kwa mwaka jana ( 2017)  kuwa ni upungufu wa rasilimali watu pamoja upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo (Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUZI JENGO LA MTAKIMWI MKUU WA SEREKALI MAZIZINI ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akikunjuwa kitambaa kuashiria Uzinduzi wa Jengo jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0133
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akifukia mche wa Mnazi baada ya kuupanda katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

DSC_0235
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohammed Shein akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja  .Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. kulia yake ni Makamo wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idi
DSC_0156
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0177
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi,Mayasa Mahfoudh Mwinyi akisoma Risala  katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0186
Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia  Ms,Bella Bird akitoa maelezo mafupi katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0213
Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt,Khalid Salum Mohammed akitoa maelezo kuhusiana na utekelezaji wa maazimio yaliotolewa wakati wasemina ya watendaji wakuu kuhusu umuhimu wa Takwimu  katika Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. .PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

BOT YAPIGA STOP BENKI TANO KUJISHUGHULISHA NA MASUALA YA KIBENKI

0
0

DC MVOMERO ATOA SIKU NN4 KWA WAFUGAJI KUONDOKA MAENEO YALIYOTENGWA KWA SHUGHULI ZA KILIMO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh muhamed Utaly ametoa siku kumi na nne kwa wafugaji waliovamia maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za kilimo katika kata ya Melela,kuondoka mara moja katika maeneo hayo na kupisha shughuli zilizo kusudiwa .

Tamko hilo la mkuu wa Wilaya linafuatia hivi karibuni baada ya ofisi yake kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa wafugaji, wakiilalamikia serikali ya kijiji cha melela kuwa wamevamia katika eneo lao wanaloishi na sasa wanataka kuligawa kwa wakulima kwa shughuli za kilimo ,jambo ambalo lilimlazimu mkuu huyo wa Wilaya kwenda kukutana na pande hizo mbili ili kupata muafaka.

Awali akitoa maelezo kwa niaba ya serikali ya kijiji mwenyekiti wa kijiji hicho Said Membe amesema kuwa eneo hilo linalolalamikiwa na  wafugaji lilitengwa maalum  kwa shughuli za kilimo na kufuata taratibu zote za kisheria .

Bw membe amesema wao kama serikali ya kijiji wapo kwaajili ya kufuata na kusimamia taratibu za kisheria na kwakutambua hilo ofisi yake imeanzisha mchakato wa kukusanya maombi kutoka kwa wananchi wanaohitiji maeneo ya kulima na mchakato utakapo kamilika basi watayarudisha kwa wananchi wenyewe ilizoezi lakugawa mashamba hayo ufanyike kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Naye bwana wecha kwaniaba ya wafugaji waliopeleka malalamiko hayo kwa Mkuu wa Wilaya amethibitisha kuwa nikweli wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila kuwa na utamburisho rasmi  wa kisheria unaowapa uhalali wa kumiliki maeneo hayo ukiacha mfugaji mmoja ambaye ndiye anayetambulika kisheria na serikali ya kijiji

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AMLILIA MAREHEMU ATHUMAN HAMISI,KUZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU

0
0
1
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt . Ibrahim Msengi Ndugu wa Marehemu Athman Khamis Nyumbani kwake Sinza kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba, Marehemu amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua ghafla na kulazwa hospitalini hapo kwa matibabu.Marehemu Athuman Hamisi alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN,anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kisutu .
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN Dkt. Jimmy Yonaz nyumbani kwa Marehemu Athuman Hamisi  Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
3
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah Naibu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN Nyumbani kwa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
4
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watoto wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
5
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watoto wa Marehemu Athuman Hamisi, Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
6
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na na Dkt.. Jimmy Yonaz Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSN na ndugu wa marehemu Dkt Ibrahim Msengi Nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi, Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
7
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Ankal  Issa Michuzi nyumbani kwa Marehemu Athuman Hamisi,Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
8
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na ndugu , na jamaa na marehemu wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
9
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiafamilia ndugu , na jamaa na marehemu wa Marehemu Athman Khamis Sinza Kijiweni jijini Dar es salaam alipokwenda kuhani msiba.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images